Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.
Source text is preserved. When a suitable model is available, translation is displayed separately.
Sikke-i Tasdik-i Gaybî
DONDOO YA PILI
Source: quranrisale.com international high-fidelity editions · Risale-Nur official authorized multilingual publication
Sikuwaumba majini na watu ila wapate kuniabudu. *Sitaki kwao riziki, wala sihitaji wanilishe. *Hakika Mwenyezi Mungu ndiye anaye kuruzuku, Mola Mlezi Mwenye nguvu, Mwenye kudumu. (51:56-8)
Kwa muda mrefu aya hizi ziliisumbua akili yangu, kwani kwa mujibu wa tafsiri nyingi za Qur’ani maana yake ya wazi haikuakisi muujiza wa hali ya juu wa Qur’ani. Sasa nitaeleza kwa ufupi vipengele vitatu vya maana zake nzuri sana na zilizotukuka, vinavyotokana na mng'aro wa Qur'an.

