Sözler

The Twenty-Fourth Word

Source: risaleinur multilingual dataset, risale.site source · Risale-Nur multilingual research corpus
Risale reading plan
§1

Kwa kutazama kiasi cha ugumu unaofunika kufahamu sehemu ya Hadithi tukufu ambazo zinazungumzia (Alama za kiama na matukio yake) na katika (Fadhila za amali na thawabu zake) idadi katika wenye elimu wenye kuzithamini akili zao wamezidhoofisha, na baadhi yake wameziweka katika hesabu ya (Maudhuati) na wakapitiliza wengine katika dhaifu wa Imani wenye kudanganywa na akili zao wakashika mrengo wa kuzikanusha. Nasi hapa hatutaki kuwajadili kwa upambanuzi, bali tutatanabahisha (Misingi kumi na mbili) katika misingi na nguzo za jumla ambazo yawezekana kuzifuata katika kufahamu Hadithi hizi tukufu za maudhui ya somo. Msingi wa Kwanza (Dini ni Mtihani) Na hili ni suala ambalo tumelibainisha katika kujibu swali lililokuja mwishoni mwa (Neno la Ishirini) na muhtasari wake: Kwamba Dini ni mtihani na jaribio, inabainisha roho za juu na roho za chini, kwa hiyo inaelezea matukio ambayo watu watayashuhudia katika mustakabali kwa tamko lisilojulikana na kufichikana kwa kiwango cha kuwa gumu kulifahamu, na sio wazi uwazi mno ambao hakuna namna kulisadikisha, bali inalionesha kwa namna iliyofunguka kwa akili, haifanyi zishindwe, wala hainyang’anyi uwezo wa kuchagua. Alama katika alama za kiama ingedhihiri kwa uwazi wa vilivyo wazi kabisa, na watu wangelazimika kusadiki, hapo ingekuwa sawa utayari wa kimaumbile kama mkaa katika uduni wake na utayari wa kimaumbile kama almasi katika thamani yake, na ingepotea siri ya kukalifisha na matokeo ya mtihani yangepotea bure. Basi kwa ajili hii imedhihiri hitilafu nyingi katika masuala mengi, kama masuala ya Al-Mahdy As-Sufyaany na zimetoka hukumu zenye kugongana kwa wingi wa hitilafu katika mapokeo. Msingi wa Pili (Tabaka za Masuala ya Kiislamu) Masuala ya Kiislamu yana tabaka na ngazi, wakati ambapo moja wapo linahitaji hoja ya kukinaisha, kama katika masuala ya itikadi, na mengine yanatosheleza kuzidia kwa dhana, na mengine kuyapokea tu na kuyakubali na kutoyakataa. Kwa ajili hii haitakiwi hoja na kukiri kwa yakini katika kila suala katika masuala ya kimatawi au matukio ya kinyakati ambayo sio katika misingi ya kiimani, bali inatosha kuyapokea na kutokataa. Msingi wa Tatu (Maarifa ya Watu wa Kitabu) Wengi katika wanazuoni wa Wana wa Israeli na Wakristo wamesilimu katika enzi za sahaba wema (r.a), na wakachukua pamoja nao katika Uislamu maarifa yao ya awali, kuchukua kwao sio kuchache kutoka maarifa hayo yaliyotangulia yenye kuhitilafiana na hali halisi kana kwamba ni katika elimu za Kiislamu. Msingi wa Nne (Idraju) Imeingizwa kiasi katika kauli za wapokezi, au maana walizozitoa ndani ya matini ya Hadithi, zikachukuliwa na illa zake. Na kwa kuwa mwanadamu hasalimiki kukosea, imedhihiri kiasi katika kauli hizo na istinbati zikihitilafiana na uhalisia, yaliyosababisha udhaifu wa Hadithi. Msingi wa Tano (Ilhamu) Yamezingatiwa baadhi ya maana yatokanayo na mawalii na watu wa kufunuliwa miongoni mwa Muhadithina kwamba hayo ni Hadithi, juu ya kuwa katika umma wapo wahadithina , yaani wenye kupewa Ilhamu. Na katika yanayojulikana hakika ilhamu ya mawalii zinaweza kuwa za makosa katika baadhi ya hali, basi inayumkinika kudhihiri kinachoenda kinyume na hakika katika mifano ya aina hii ya mapokezi. Msingi wa sita (Methali) Baadhi ya hekaya zinakuwa mashuhuri baina ya watu, basi hikaya hizo zinapita mapito ya methali, na methali hazitazamwi katika maana yake ya kihakika, bali inatazamwa katika lengo linaloelekezewa hiyo methali, na kwa ajili hii ilikuwa katika baadhi ya Hadithi kutaja baadhi ya yale ambayo watu wamezoeana nayo katika visa na hekaya ikiwa ni fumbo na kumithilisha kwa njia ya maelekezo. Ikiwa kuna upungufu na dosari katika maana ya hakika katika mfano wa masuala haya, yanarudi katika kawaida za watu na inarejea katika waliyosikia kati yao na kuzoeana nayo miongoni mwa hekaya. Msingi wa Saba (Tashbiha za Kibalagha) Kuna nyingi ya tashbiha na mifananisho ya kibalagha inachukuliwa kama hakika za kimaada, ima kwa kupita kwa zama au kwa kugura kwake kutoka kwenye mkono wa ujuzi kwenda katika mkono wa ujinga, hapo watu wanaingia katika kosa la kudhania tashbiha hizo ni hakika halisi. Basi mathalani: Hakika ya malaika wawili wenye kuitwa kuwa ni ng’ombe na samaki, na wenye kushika sura zao katika ulimwengu wa mfano, nao ni katika malaika wa Allah (s.w) wenye kusimamia wanyama wa nchi kavu na baharini, wamegeuka kuwa ni ng’ombe mkubwa na samaki mkubwa mwenye kupewa mwili katika dhana ya watu na taswira yao ya makosa, jambo ambalo limepelekea kuipinga Hadithi hiyo. Na mathalani: Ilisikika sauti katika baraza la Mtume (s.a.w), akasema: Hii ni sauti ya jiwe linaporomoka kwenye jahanamu tangu miaka sabini na sasa ndio wakati lilipokoma katika kina chake basi ambaye anaisikia Hadithi hii na hakubainikiwa hakika ataikanusha, na anapotoka, lakini akijua kilichokuwa ni thabiti kabisa, kwamba baada ya kitambo kifupi alikuja mmoja wao akampa habari Mtume (s.a.w) kwamba mnafiki fulani mashuhuri amekufa kabla ya punde, wakati huo atakuwa na yakini hakika Mtume (s.a.w) ameweka picha kwa balagha yake ya kiunabii ya hali ya juu yule mnafiki ambaye ameingia miaka sabini katika umri wake kama jiwe linaloviringika kuelekea jahanamu, ambapo uhai wake wote ni kudondoka kuenda katika ukafiri na kuporomoka kuenda chini ya walio chini, na hakika Allah (s.w) ameisikilizisha sauti ile katika punde ya kifo cha Mnafiki huyo na akaifanya ni alama juu yake. Msingi wa Nane (Hekima ya Kuficha) Mwenye hekima zote mjuzi wa kila kitu anaficha katika makazi haya ya mtihani na medani ya majaribio, mambo muhimu mno kati ya wingi wa mambo. Na inafungamana na kuficha huku hekima nyingi na manufaa mbali mbali. Basi mathalani: Ameficha (s.w) (Usiku wa cheo) ndani ya mwezi wa Ramadhani, na (Saa ya kujibiwa dua) katika siku ya Ijumaa, na (Mawalii wema) kati ya mijumuiko ya wanadamu, na (Saa ya kifo) katika umri, na (Kusimama kwa kiama) katika umri wa dunia, na kama hivi, lau ingekuwa saa ya mauti ya mwanadamu ni maalum na inajulikana wakati wake, mwanadamu huyu masikini angemaliza nusu ya umri wake katika kughafilika kabisa, na nusu yake nyingine akiwa mwenye hofu na mshangao kama mwenye kupelekwa hatua kwa hatua kwenda kwenye kamba ya kitanzi. Wakati ambapo inahitajia kuhifadhi uwiano utakiwao kati ya Dunia na Akhera na masilahi ya kubaki kwa mwanadamu ni yenye kuangikwa moyo wake baina ya matumaini na hofu, iwe kila dakika inayompitia mwanadamu ni yamkini kwa kutokea mauti au kuendelea uhai. Na kwa hivi kunafanywa ni bora miaka ishirini ya umri usiojulikana saa ya kifo juu ya miaka elfu ya umri unaojulikana saa ya kifo. Na kama hivi basi kusimama kwa kiama, ndiyo saa ya kifo ya hii dunia, ambayo ni kama mwanadamu mkubwa, ingekuwa wakati wake ni maalum na umetangazwa zingepita karne za awali na za kati zimegubikwa katika usingizi wa kughafilika, wakati ambapo karne za mwisho katika hofu na mshangao, hiyo ni kwa sababu mwanadamu ni mwenye mahusiano madhubuti na uhai wa makazi yake makubwa na mji wake mkubwa, dunia, kwa hukumu ya maisha yake ya kijamii na kibinadamu kama anavyofungamana na nyumba yake na mji wake kwa hukumu ya maisha yake ya kila siku na ya kibinafsi. Kutokana na hili tunafahamu kwamba ukaribu unaoelezwa katika Qur’an: اقْتَرَبَتِ السَّاعَةُ haupingwi na kupitwa na miaka elfu na ziada, kwa kuwa kiama ni saa ya kifo cha Dunia. Na uwiano wa miaka elfu au alfu mbili katika miaka kwa umri wa Dunia sio isipokuwa kama uwiano wa siku moja au mbili au dakika au mbili kwa miaka ya umri. Na kadhalika haitakikani kupotea kwenye fahamu zetu kwamba siku ya kiama sio saa ya kifo cha wanadamu tu, hata ipimwe ukaribu wake na umbali wake kwa kipimo cha umri wao, bali hiyo ni saa ya kifo cha viumbe wote na mbingu na ardhi vyenye umri wa kutisha usiopimika wala kuhesabika. Na kwa ajili hii Mwingi wa hekima Mjuzi wa kila kitu ameficha muda wa kusimama kiama katika ujuzi wake kati ya mambo matano yaliyokuwa ghaibu, na imekuwa katika hekima za kuficha huku watu katika enzi zote waogope kusimama kiama, hata sahaba wema (r.a) walikuwa wenye kuogopa sana kusimama kwa kiama katika wakati wao kuliko wengineo, pamoja na kuwa wao walikuwa wanaishi katika bora ya karne, na hiyo ni karne ya furaha na kudhihiri kwa hakika, bali baadhi yao wamesema: Hakika ishara za kiama na alama zake zimeshathibiti. Basi ambao hawajui hekima za kuficha na hakika yake katika wakati wa sasa wanasema kwa dhulma: Vipi sahaba watukufu (r.a) walidhani kukaribia kwa kutokea hakika muhimu na nyeti itakayokuja baada ya miaka elfu moja na mia nne, wameidhania ipo karibu katika enzi zao. Kwa kujua kwamba wao walikuwa ni Waislamu wenye uwezo zaidi na bora wao zaidi katika kutambua maana ya akhera, na wakali zaidi wa waumini kwa busara na wakali wa hisia kwa ishara za yatakayoletwa na zama? Kana kwamba fikira yao imekengeuka hakika kwa miaka elfu! Jibu: Kwa kuwa sahaba wema - (r.a) - walikuwa ni wenye kutafakari sana fikira ya akhera kuliko watu wote, na wenye yakini iliyojikita kuliko wao kwa kutoweka kwa Dunia, na wenye ujuzi mpana kuliko wao wa hekima ya Allah (s.w) kuficha wakati wa kiama, na hii ni kwa fadhila ya nuru ya usuhuba wa Mtume (s.a.w) kwao, kwa ajili hiyo walikuwa wenye kungojea muda wa dunia, wakiwa tayari kwa kufa kwake kama anayengojea muda wake binafsi, wakajitahidi kwa ajili ya Akhera yao jitihada ya pupa. Kisha hakika kukariri kwa Mtume (s.a.w) (Basi ngojeni Kiama) kunatokana na hekima hii hekima ya kuficha na kutobainisha na humo kuna maelekezo ya Mtume (s.a.w) fasaha, na sio kuainisha muda wa kiama kwa wahyi, hata idhaniwe umbali wake na hakika, kwani hekima ni kitu kinachotofautiana na sababu. Na kama hivi basi Hadithi tukufu ambazo ziko katika aina hii zinatokana na hekima ya kuficha na kutobainisha. Na kwa msingi wa hekima hii yenyewe, watu wamengojea tangu muda mrefu, bali tangu zama za wafuasi wa sahaba, kudhihiri kwa Al-Mahdy na Dajjali na As-Sufyany, kwa matarajio ya kukutana nao, hata baadhi ya mawalii na wema wamesema kuwa wakati wao umepita. Basi hekima katika kutokubainisha nyakati za kudhihiri kwao ni hekima ile ile ya kutokuainisha siku ya kiama. Na kwa ufupi ni hivi ifuatavyo: Hakika kila wakati na kila enzi ina haja ya “Maana” ya Al-Mahdy ambaye anakuwa ni msingi wa nguvu ya kimaanawy, na ukombozi wa kukata tamaa. Basi inalazimu kila enzi kuwa na sehemu ya maana hii. Na vivyo hivyo inapasa watu katika kila enzi kuwa macho na wenye tahadhari kutokana na watu wa shari wanakuwa katika uongozi wa unafiki na wanaoongoza mrengo mkubwa wa shari, na hiyo ili nafsi isijiachilie moja kwa moja kwa kujiachia na kutojali. Ingekuwa nyakati za kudhihiri kwa Al-Mahdy na Dajjali na mfano wa wawili hao katika watu maalum yangepotea masilahi ya mwongozo na maelekezo. Ama siri ya kutofautiana kwa mapokezi yaliyopatikana kuwahusu wawili hao: Hakika ya ambao wamezifasiri Hadithi hizo tukufu wamechanganya na istinbati zao na jitihada zao binafsi pamoja na matini ya Hadithi. Kama kutafsiri kwao kwamba matukio ya Al-Mahdy na Matukio ya Dajjali yatatokea kuzunguka Shamu, Basra na Kufa kulingana na mawazo yao, ambapo miji hiyo ilikuwa katika eneo linalozunguka makao makuu ya ukhalifa wakati huo ndani ya Madina Munawwara na Shamu. Au wao wamezifasiri Hadithi hizo tukufu kwamba athari kubwa ambazo zinashika nafasi ya haiba ya kimaanawy ya watu hao au zinazofanya hayo makundi yao, wameyafikiria yanatokana na haiba zao binafsi za mmoja mmoja, katika yaliyopelekea kufahamika kwamba watu hawa watadhihiri kwa namna ya kufurutu ada, basi watu wote watawajua, na hali – kama tulivyosema – kwamba dunia ni medani ya majaribio na mtihani, na hakika Allah (s.w) anapomjaribu mwanadamu hamnyang’anyi hiari bali anafungua mlango mbele ya akili yake, kwa hiyo watu hawa - yaani Dajjali na Al-Mahdy - hawatajulikana kwa watu wengi wakati wa kudhihiri kwao, bali hajitambui huyo Dajjali wa kuogofya nafsi yake mwanzoni mwa jambo, bali atawajua hao anayewatazama kwa nuru kali ya imani inayopenya katika mikondo. Na Dajjali ambaye ni katika alama za kiama Mtume (s.a.w) amesema kumhusu yeye kwamba siku katika siku zake ni kama mwaka na siku kama mwezi na siku kama Ijumaa na baki ya siku zake kama siku zenu. Na kwamba dunia itasikia sauti yake na atatembea Ardhini katika siku arubaini. Basi ambao hawakufuata insafu wamesema: Mapokezi haya ni aina ya mihali, na wameyakanusha. Hashalillahi, bali hakika yake - ujuzi uko kwa Allah - ni ifuatavyo: Hakika katika Hadithi tukufu kuna ishara ya kutokea mtu kwa upande wa kaskazini, eneo lenye wingi mno kwa ulimwengu wa ukafiri, anaongoza mrengo mkubwa unaotokana na itikadi ya kimaada ya kukana Mungu, na kulingania ukanaji Mungu na kumkanusha Muumba. Basi maana ya Hadithi ndani yake kuna ishara ya kudhihiri kwa mtu huyu kutokea kaskazini mwa ulimwengu. Ishara hii inajumuisha nembo yenye hekima nayo ni: Kwamba duara lililo karibu na mhimili wa kaskazini huko mwaka unakuwa ni mchana na usiku, ambapo miezi sita katika mwaka huo ni usiku na miezi sita mingine ni mchana. yaani siku ya Dajjali huyu ni mwaka mmoja kama ilivyokuja “Siku kama mwaka”. Basi hii ni ishara ya kudhihiri kwake karibu na duara hilo. Na muradi wa “Siku kama mwezi” ni kuwa kila tunapokwenda mbele kutokea kaskazini upande wa maeneo yetu wakati mwingine mchana unakuwa mwezi kamili, ambapo jua halizami mwezi wakati wa majira ya joto. Na hii ni ishara vilevile ya kuvuka kwa Dajjali katika ulimwengu wa hadhiri baada ya kudhihiri kwake kaskazini. Na ishara hii inakuja kutokana na kuegemeza siku kwa Dajjali. Na kama hivi kila tunapokaribia kuteremka kutoka kaskazini kuelekea kusini tunaona jua halizami kwa muda wa wiki moja, hadi inakuwa tofauti katika mawio na machweo saa tatu, yaani kama siku zetu za kawaida. Hakika nilikuwa katika mahali kama hapa nilipokuwa mateka huko Urusi, ikawa jua halizami kwa wiki katika mahali karibu nasi, hata ilikuwa watu wanatoka kuja kushuhudia mandhari mageni ya kuzama jua. Ama kufika kwa sauti ya Dajjali hadi pande za ulimwengu, na kwamba anazunguka ardhi katika siku arobaini, hakika kumetatuliwa na vyombo vya redio na kupashana habari na njia za usafiri za sasa kama treni na ndege. Basi wale ambao waliokanusha hali hizi mbili katika wakana mungu jana na wakazihesabu hizo katika mihali leo wanaziona ni katika mambo ya kawaida. Ama Yaajuj na Maajuj na ukuta ambazo ni katika alama za kiama, nimeshaandika kuhusu hayo kwa ufafanuzi katika risala nyingine, naelekeza huko, ama hapa ninasema: Kama makabila mawili ya Mangor na Maghuli yalivyoangamiza jana jamii za kibinadamu na ikawa ni sababu ya kujenga ukuta wa China, kuna mapokezi yanayoashiria kwamba pamoja na kukaribia kusimama kwa kiama ustaarabu mpya pia utaanguka pia na kuteketea chini ya mapigo ya nyayo za fikira zao za kigaidi na fujo za kutisha. Na hapa wanauliza idadi ya wakanaji mungu: Liko wapi kundi hili la wanadamu, na ambao wamefanya na watafanya mfano wa matendo haya? Jibu: Kama ilivyo nzige ni maafa ya kilimo yanakumba eneo maalumu katika msimu maalum, kisha yanajificha kufuatia kubadilika kwa msimu. Hakika sifa za jinsi hizo ambazo zimeteketeza eneo hilo zimejificha katika makunjo ya baadhi ya watu wachache kati yao, basi yanadhihiri maafa hayo hayo, kwa amri ya Kiungu, katika msimu maalum, na kwa wingi mkubwa, yaani hakika ya jinsi zake hupotea na sio kwisha, ili ipate kudhihiri upya katika msimu maalum. Basi kama jambo lilivyo hivyo katika nzige, hakika ya watu ambao wameeneza ufisadi katika ulimwengu katika wakati fulani, watadhihiri katika wakati waliopangiwa kuwaangamiza wanadamu kwa amri ya kiungu na kwa kutaka kwake (s.w), hivyo wanateketeza ustaarabu wa wanadamu mara nyingine, kuchochea kwao na kutikisa kwao kutakuwa kwa mtindo mwingine, wala hajui ghaibu isipokuwa Allah (s.w). Msingi wa Tisa (Mwelekeo wa Masuala ya Kiimani) Hakika ya mkusanyiko wa sehemu ya masuala ya kiimani yanaelekea katika mambo yanayoambatana na huu ulimwengu finyu uliofungika, na sehemu nyingine kati ya hizo inaelekea katika ulimwengu wa kiakhera mkunjufu uliofunguliwa. Na kwa kuwa sehemu ya Hadithi za mtume zilizokuja kuhusu fadhila za amali hakika amezielezea Mtume mtukufu (s.a.w) kwa njia ya kibalagha inayowiana na kuraghibisha na kuhofisha, basi wasiotazama kwa makini wamedhani kwamba Hadithi hizo Tukufu zinabeba Chuku!. Kamwe, hakika hizo zote ni dhati ya haki na hakika tupu na hakuna humo chuku katu. Mfano: Hakika kinachozindua akili za wenye kuingia gizani na kuziamsha ni Hadithi ifuatayo: “Dunia ingekuwa inalingana mbele ya Allah japo na ubawa wa mbu, Kafiri asingekunywa humo funda la maji . Au kama alivyosema. Na hakika yake ni: Hakika neno (Mbele ya Allah) linaeleza ulimwengu wa kubaki, basi nuru inayochomoza kutoka katika ulimwengu wa kubakia, japo kiasi cha ubawa wa mbu ni kunjufu na jumuishi zaidi, kwa sababu ni ya milele, kuliko nuru ya muda maalum japo iwe inajaza Ardhi. Yaani Hadithi haifungamanishi mlinganisho ubawa wa mbu na ulimwengu mkubwa, bali mlinganisho kati ya dunia ya kila mmoja wapo, umedhibitika katika umri wake mfupi, na baina ya nuru ya kudumu yenye kuangaza, japo kwa kiasi cha ubawa wa mbu kutoka katika neema ya kiungu na hisani yake enevu. Kisha hakika dunia ina pande mbili bali pande tatu. Kwanza: Upande mmoja kama kioo unaakisi madhihirisho ya majina mazuri. Pili: Upande unaangalia Akhera, yaani dunia ni shamba la Akhera. Ama tatu: Ni upande ambao unaangalia katika kukosekana na kutoweka, basi upande huu mwingine ni Dunia isiyoridhiwa, inajulikana kuwa dunia ya watu wa upotevu. Kwa hiyo Dunia iliyoelezwa katika Hadithi tukufu sio dunia kubwa ambayo ni kama vioo vya majina mazuri na barua za kiungu Mtegemewa kwa haja zote, wala sio dunia ambayo ni shamba la Akhera. Bali hiyo ni dunia ambayo ni kinzani ya Akhera na chimbuko la makosa yote na dhambi na chanzo cha mabalaa yote na masaibu, ni dunia ya wenye kuabudu dunia, ambayo hailingani na Atomu moja katika ulimwengu wa Akhera ya milele iliyotunukiwa kwa waja wa Allah waumini. Basi iko wapi hakika hii ya kweli yenye kusibu na ufahamu wa watu wa ukanaji mungu madhalimu kwa walichokidhania wao kuwa ni chuku?. Mfano mwingine: Ni mrengo walioshika wapinga mungu na wamepitiliza huko kwa kuingia kwao gizani walipodhani kwamba yaliyopatikana katika Hadithi tukufu kuhusu thawabu za amali na fadhila za baadhi ya sura katika Qur’an tukufu kuwa ni chuku isiyoingia akilini, bali hata wamesema kwamba hizo ni muhali! Imekuja - mathalani - kwamba Surat “Al-Faatiha” ina thawabu ya Qur’an, na surat “Al-Ikhlasi” inalingana na theluthi ya Qur’an, na surat Az-“Zilzala” robo ya Qur’an, na surat “Al-Kaafirun” robo ya Qur’an , na surat “Yasini” ina thawabu ya mifano kumi ya Qur’an. Basi ambao hawatazami kwa makini na hawana insafu na umakini wanadai kuwa aya hizi ni muhali! Ambapo wanasema: Vipi itakuwa surat “Yasini” na fadhila hii nayo ni sura katika Qur’an Tukufu? Na kuna sura nyingine zilizo bora?! Hakika za mapokezi haya: Hakika kila herufi katika herufi za Qur’an Tukufu ina thawabu, nalo ni jema moja, lakini kwa fadhila za Allah (s.w) na ukarimu wake thawabu za herufi hizi zinaongezeka maradufu na zinazaa wakati mwingine mema kumi na wakati mwingine sabini, na nyingine mara mia saba (Kama katika herufi za Ayatul Kursy) na mara ya nne: Elfu na mia tano (Kama katika herufi za surat Al-Ikhlasi) na ya tano: Mema elfu kumi (Kama kusoma aya katika nyakati bora na usiku wa nusu ya Shaabani) na ya sita: Thelathini elfu katika mema (Kama katika kusoma aya katika Lailatul Qadri) basi huongezeka mema haya maradufu kama zinavyoongezeka mbegu za nyasi. Na inayumkinika kuongezeka kwa thawabu hadi thelathini elfu kutokana na aya tukufu: خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍ Na kama hivyo haiwezekani kupimisha wala kulinganisha Qur’an tukufu pamoja na kuwepo kwa mwongezeko huu wa kiidadi wenye kupanda wa thawabu iliyoelezwa, lakini inayumkinika hivyo pamoja na asili ya thawabu ya baadhi ya sura. Na tufafanue hilo kwa mfano: Tukadirie kwamba shamba ndani yake kuna punje elfu moja za mahindi, zingemea baadhi ya punje zake mashuke saba katika kila shuke moja katika kila shuke moja kuna punje mia moja, hakika punje moja ya Atomu wakati huo inalingana na theluthi mbili za zilizomo shambani. Mathalani tungekadiria kwamba, punje nyingine imemea mashuke kumi katika kila shuke moja kuna punje mia moja, basi hakika punje moja wakati huo itakuwa ni sawa na maradufu ya punje zilizopandwa kwa asili ( hapo awali ), na kama hivi pima katika mwanga wa mwelekeo wa mfano huu. Basi sasa tunaleta picha Qur’an tukufu ni shamba la kimbinguni la kinuru takatifu, kila herufi humo pamoja na thawabu zake za kiasili ni sawa na punje moja, bila kutazama mashuke yake, ukitumia mfano huu juu ya mfano uliopita unaweza kutambua fadhila za sura ambazo zimekuja Hadithi tukufu kuzielezea sura hizo, kwa kuzilinganisha na asili ya herufi za Qur’an. Mfano wa hilo: Hakika herufi za Qur’an mia tatu elfu na mia situ na herufi ishirini, herufi za surat Al-Ikhlasi pamoja na Bismillahi ni herufi sitini na tisa, Basi kuzidisha mara tatu ya sitini na tisa sawasawa na herufi mia mbili na saba. Yaani mema ya kila herufi katika herufi za surat Al-Ikhlasu yanakaribia mema elfu moja na mia tano. Na kadhalika ukihesabu herufi za surat “Yasini” na ukachukua uwiano kati yake na kati ya jumla ya herufi za Qur’an, na tukachukua kuongezeka hadi mara kumi mfano wake kwa jicho la mazingatio, tutakuta hakika kila herufi humo ina kiasi kinachokaribia zaidi ya mema mia tano. Basi ukipima kwa namna hii baki ya yaliyokuja katika fadhila za sura katika Hadithi basi utatambua kiasi cha kuwa kwake ni hakika yenye kusibu njema, na kiasi cha umbali wake na kila kinachoashiria kuwa ni chuku na israfu katika maneno. Msingi wa Kumi (Ufasaha wa Maelekezo) Huenda wakadhihiri katika watu wenye mambo yenye kufurutu ada katika amali na matendo, kama inavyotokea katika mengi ya makundi ya viumbe. Basi ikiwa mtu wa kipekee huyu amewashinda wengine na kuwavuka kwa fora katika heri na wema, basi atakuwa sababu ya kupelekea fahari ya wana wa jinsi yake na uwanja wa kujivunia kwao, na kama si hivyo basi yeye ni onyo la sudi mbaya na balaa juu yao. Basi wote katika hawa watu wa pekee hujitokeza kama haiba ya kimaanawy kila mahali katika jamii, na wengine wanajitahidi kumuiga katika matendo yake na wanajitahidi katika kufika kilele chake, na huenda mmoja wao anafikia ngazi yake katika tendo hili au lile. Basi kadhia kwa hiyo kwa upande wa mantiki ni kadhia (Yamkini), kwa yamkini ya kuwepo kwa huyo mtu mwenye kufurutu ada, kila mahali uwepo wenye kujificha na wa hali zote. Yaani amekuwa ni mtu wa kiujumla kwa tendo lake hili, yaani katika yamkini kuzaliwa aina hii ya amali ikiwa ni matokeo kama haya. Basi angalia kwa mwanga wa mfano huu Hadithi tukufu za Mtume (s.a.w) zilizokuja kwa maana haya: Mwenye kuswali rakaa mbili kadha basi ana ujira wa Hija. Yaani thawabu ya rakaa mbili katika nyakati maalum inakuwa sawa na Hija, hii ni hakika thabiti. Kwa hiyo inajuzu kila rakaa mbili za swala kubeba maana hii kwa ujumla, lakini kutokea kimatendo kwa aina hii ya mapokezi sio daima wala kwa jumla, kwani kukubalika kuna masharti maalum. Kwa hiyo mfano wa mapokezi kama haya yanakosa sifa ya ujumla na kudumu, hayo ima ni ya muda maalum kwa hali zote; au ni kadhia yamkini, ya jumla. Na ujumla katika mifano ya Hadithi hizi ni katika upande wa yamkini ya kuzingatiwa, kama ilivyo katika: (Kusengenya ni kama kuua). Yaani mtu anakuwa kwa kusengenya ni sumu hatari yenye kuua. Na kama ilivyo katika: (Neno zuri ni sadaka kama kuacha huru mtumwa). Na hekima katika kuleta Hadithi kwa tamko hili ni: Kudhihirisha yamkini ya kutokea kwa sifa hii ya kimaanawy iliyo kamili katika kila mahali na katika picha yake ya hali zote, kwa sababu ni ya balagha zaidi katika kuhofisha na yenye kuhimiza zaidi nafsi kufanya heri na yenye kuepusha zaidi kutenda shari. Kisha hakika mambo ya ulimwengu wa kimilele hayapimwi kwa vipimo vya ulimwengu wetu wa sasa, kwani hakika kikubwa zaidi ya tulivyonavyo chaweza kikawa ni kitu kidogo zaidi huko wala hakiendi sambamba nacho. Basi thawabu za amali kwa kutazama kuwa kwake zinaangalia katika ulimwengu huo wa milele basi hakika ya mtazamo wetu wa kidunia ulio finyu unakuwa ni mfupi kwake, tunashindwa kuufahamu vema kwa akili zetu ndogo. Basi kwa mfano: Kuna mapokezi yanayogeuza macho ya ambao hawatazami kwa makini wala hawafanyi insafu katika hoja zao. Ni: (Mwenye kusoma hii atapewa mfano wa thawabu za Musa na Harun), yaani: الحَمْدُ للهِ رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَرَبِّ الأَرَضِيْنَ رَبِّ العَالَمِيْنَ وَلَهُ الكِبرِيَاءُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ وَهُوَ العَزِيْزُ الحَكِيْم. الحَمْدُ للهِ رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَرَبِّ الأَرَضِيْنَ رَبِّ العَالَمِيْنَ وَلَهُ العَظَمَةُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ وَهُوَ العَزِيْزُ الحَكِيْم. وَلَهُ الملْكُ رَبّ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ وَهُوَ العَزِيْزُ الحَكِيْم. Basi hakika ya mifano ya Hadithi hizi ambazo zinachokoza akili ni: Hakika sisi hatutambui kiasi cha thawabu ambazo wanazipata manabii wawili wakubwa ambao ni Musa na Harun (a.s) isipokuwa kulingana na mawazo yetu na ndani ya eneo la fikira yetu finyu na ndani ya mipaka ya mtazamo wetu mfupi wa kidunia; kwa hiyo hakika ya thawabu ambayo anaipata mja mwenye kushindwa kwa hali zote kwa kusoma kwake uradi huo, kutoka kwa Bwana Mlezi Mrehemevu mkunjufu wa rehema, katika uhai wa kudumu wa milele, yamkini ikawa yenye kufanana na thawabu ambayo tuliyoiwaza kwa akili zetu zenye kasoro kwa manabii wawili wakubwa, na hii kulingana na duara la ujuzi wetu na kimo cha fikira zetu. Mfano wetu katika hili ni kama mfano wa Bedui hajawahi kumuona Mfalme wala hatambui ukubwa wake na hadhi yake, na katika mtazamo wake mdogo na fikira yake finyu, kwamba mfalme ni Sheikh kama sheikh wa kijiji au mkubwa zaidi kuliko yeye kwa kidogo. Hata pembezoni mwetu - katika mashariki ya Anatolia - kulikuwa na wanakijiji wa kawaida wanasema: Hakika Mfalme anakaa karibu na jiko na anasimamia upishi. Kwa maana anachokiwaza Bedui kwa ukubwa wa Mfalme hata hakipandi hadi katika ngazi ya mwamrishaji wa kundi la baadhi ya askari jeshi. Ingesemwa kwa mmoja wa hawa: Ukinitimizia mimi kazi hii nitakulipa cheo cha Mfalme (Yaani nafasi ya Mwenye kuamrisha jeshi) basi kauli hii ni hakika na yenye kusibu, hakika ukubwa wa mfalme katika akili ya msikilizaji na katika fikira yake ndogo ni kwa kiasi cha ukubwa wa kiongozi wa kikundi cha jeshi na sio vingine. Na kama hivi hakika sisi hatukaribii mfano wa Bedui huyu kufahamu hakika zilizopo katika thawabu za amali zinazoelekea Akhera kwa akili zetu finyu na fikira zetu pungufu na kwa mtazamo wetu wa kidunia, ambapo yaliyomo katika Hadithi tukufu sio kufunga mlinganisho baina ya thawabu ya hakika ambayo anaipata Musa na Harun (a.s) ambayo haijulikani kwetu, na thawabu ambayo anaipata Mja mwenye kutaja uradi; kwa sababu msingi wa Tash’biha ni kupima kisichojulikana kwa kinachojulikana, yaani kutambua hukumu ya kisichojulikana kutoka katika hukumu ya kinachojulikana. Yaani hakika ya mlinganisho ni baina ya thawabu zao wawili hao (zinazojulikana) kwetu kulingana na mawazo yetu na thawabu ya hakika ya mja mwenye kudhikiri (isiyojulikana) kwetu. Kisha hakika ya picha ya jua yenye kuakisi kutoka katika uso wa bahari na kutoka katika tone la maji ni picha ileile, tofauti ni katika aina tu. Kwani zote hizo mbili zinaakisi picha ya jua na mwanga wake, kwa hiyo roho ya wote Musa na Harun (a.s) ambayo ni kioo safi kama bahari inaakisi juu yake katika ainisho la thawabu yanayoakisi juu ya roho ya mja mwenye kudhikiri ambayo ni kama tone la maji. Basi zote ni thawabu moja kwa upande wa ainisho na kiasi isipokuwa aina ni tofauti, kwa sababu inafuata ukubalifu. Kisha kukariri dhikiri na tasbihi maalum, au kusoma aya moja inaweza kufungua katika milango ya rehema na furaha kiasi kisichoifungua ibada ya miaka sitini, yaani zipo hali aya moja inatoa humo faida kiasi cha Qur’an tukufu yote. Kisha hakika ya nuru za kiungu zenye kudhihiri kwa Mtume Mtukufu (s.a.w) kwa kusoma kwake aya moja huweza ikawa ni sawa na nuru ya kiungu kamili kwa Mtume mwingine; kwani yeye (s.a.w) ni mahali pa udhihirisho wa jina tukufu. Ikisemwa hakika ya mja mwenye kudhikiri amekutana na neema kutoka katika kivuli cha jina tukufu kwa fadhila ya urithi wa Unabii na amepata thawabu kwa hilo kwa kiasi cha ukubalifu wake, kwa kiasi cha nuru ya kiungu juu ya Nabii mwingine, basi hakuna kwenye kauli yake tofauti na hakika katu. Kisha hakika thawabu na ujira kutoka katika ulimwengu wa nuru wenye kudumu, ambao yamkini ukadhibitika ulimwengu unaotokana nao ndani ya atomu moja, kwa mfano wa kudhibitika kwa picha ya mbingu pamoja na nyota zake ndani ya kipande kidogo cha kioo na kuziona humo. Kwa hiyo kusoma aya moja au dhikiri maalum kwa nia ya ikhlasi yamkini ikazalisha uangavu katika roho – kama chupa – yaweza kuchukua thawabu za kinuru kama mbingu pana. Matokeo: Ewe mwenye kutazama kila kitu kwa jicho la kukosoa na kutia dosari na bila ya kuchunguza vema, na ewe mwenye imani ya chini na fikira iliyojaa falsafa ya kimaada! Fanya insafu japo kwa uchache! Dumisha kutazama katika misingi hii kumi, na ole wako unyooshe kidole cha kupinga kwako katika Hadithi tukufu na kwa duru yake katika yanayonyongesha cheo cha kuhifadhiwa Mtume Mtukufu (s.a.w) kwa hoja ya unayoona katika mapokezi katika tofauti kabisa na uhalisia na kukinzana na hakika. Basi hii misingi kumi, na medani za utekelezaji wake, inakufanya uachane na ukanushaji na kukuzuia na kukataa kwanza. Kisha inakusemesha: Ikiwa kuna upungufu wa hakika, basi hii inarejea kwetu (Yaani katika misingi) na sio katu katika Hadithi tukufu. Na kama hakuna upungufu wa kweli inarudi katika ubaya wa ufahamu wako wewe! Hitimisho: Hakika anayejiachia katika kukanusha na kukataa ni juu yake kuvunja misingi kumi iliyoelezwa na kama si hivyo hawezi kukanusha. Ukiwa kweli mwenye insafu basi zingatia vema hii misingi kumi, na kutokea hapo baadaye usiinuke kwa ajili ya kukanusha Hadithi ya Mtume (s.a.w) ambayo akili yako inaiona kuwa ni yenye kutofautiana na hakika, bali sema: Huenda kuna tafsiri yake, taawili au maelezo na acha kupinga! Msingi wa Kumi na Moja (Mutashabihati) Kama ilivyo katika Qur’an kuna aya Mutashabihati zinahitaji taawili au zinataka kuzipokea kwa hali zote, Na kadhalika katika Hadithi tukufu kuna wakati mwingine kuna mishkeli inahitaji tafsiri au maelezo ya umakini. Na yamkini kwako kutosheka na mifano iliyotajwa. Naam, hakika aliye macho anaweza kuelezea njozi ya mwenye kulala, Wakati ambapo mwenye kulala ambaye anasikia pembezoni mwake katika walio macho anaweza kuyachukua maneno yao kwa namna ilivyo katika usingizi wake. basi analielezea kwa namna inavyowiana naye katika usingizi. Basi ewe mwenye kulazwa usingizi kwa kughafilika na falsafa za kimaada, na ewe usiyekuwa na insafu! hakika ambaye Allah (s.w) anasema kumhusu: na ambaye anasema kuhusu nafsi yake: مَا زَاغَ الْبَصَرُ وَمَا طَغَى تَنَامُ عَيْنَايَ وَلَا يَنَامُ قَلْبِي yeye ni aliye macho wa hakika, basi usikanushe anayoyaona yeye, bali yaelezee na ujitahidi katika kuyaelezea katika njozi yako, na utafute tafsiri kwa ajili yake. Kwani ikiwa mbu atamng’ata mtu aliyelala, hakika ya athari ya hilo zitadhihiri kwake kana kwamba amejeruhiwa vitani. Na anapoulizwa baada ya kuamka kwake atasema: Naam nilikuwa katika vita vya kumwaga damu nyingi na mizinga imeelekezwa upande wangu! Wakati ambao walio macho ambao wanaomzunguka wanachukua kubabaika kwake huku namna ya istihizai. Basi mtazamo wa kughafilika wenye kulaza na fikira ya falsafa ya kimaada haviwezi kuwa kabisa kithibitisho cha hakika za unabii. Msingi wa Kumi na Mbili (Kutofautiana Pembe ya Kutazama) Hakika mtazamo wa unabii, Tawhidi na Imani unaona hakika katika nuru ya kiungu na akhera na umoja wa ulimwengu, kwa kuwa ni yenye kuelekea huko. Ama elimu ya kimajaribio na falsafa ya kisasa hakika inaona mambo kutokea katika pembe ya sababu za kimaada nyingi na Asili, kwa sababu imeelekea huko. Kwa hiyo basi masafa kati ya pembe mbili za kutazama ni mbali sana. Basi huenda lengo kubwa tukufu mbele ya watu wa falsafa ni duni na dogo halikaribii kuonekana kati ya makusudio ya wanazuoni wa Usuli El-Dini na Ilmul Kalam. Na kwa ajili hii hakika wameendelea watu wa elimu ya majaribio sana katika kujua sifa maalum za vilivyomo na pambanuzi zake na sifa zake nyeti, wakati ambapo wamechelewa sana hata kuliko waumini wa kawaida kabisa na wachache wao kwa elimu katika nyanja za elimu ya hakika nazo ni elimu za kiungu za hadhi ya juu na maarifa ya kiakhera. Basi ambao hawatambui siri hii, wanadhani kwamba wanazuoni wa Uislamu, wamechelewa mbali na wanazuoni wa Asili na wana Falsafa. Na hali ya kuwa ambao akili zao zimeteremka katika macho yao na wakawa hawafikiri isipokuwa kwa wanavyoviona, na wamezama katika wingi wa viumbe, wapi kwao ujasiri hata wakutane na warithi wa Mtume (a.s) ambao wameyafikia makusudio ya kiungu ya hadhi ya juu na shabaha yake iliyonyanyuka na kuwa juu. Kisha hakika ya mtazamo ikiwa kutokea pembe mbili tofauti, basi hapana shaka kutokea kwa hakika mbili zenye kupishana, na yaweza zikawa zote hizo ni hakika. Na kwa vyovyote vile haigongani hakika ya kielimu ya kukinaisha pamoja na hakika ya maelezo ya Qur’an matakatifu, ambapo mkono mfupi wa elimu ya majaribio pungufu ni mpungufu kuweza kufikia nyusi za ncha katika hakika za Qur’an zilizonyanyuka zilizotakasika. Na tutaleta mfano mmoja tu juu ya hili: Hakika ya tufe la Ardhi katika mtazamo wa watu wa sayansi ni kwamba: Ni moja ya sayari yenye ukubwa wa kati na kati, inazunguka jua, nalo ni umbo dogo kulinganisha na Sayari na nyota ambazo hazihesabiki wala hazidhibitiki. Ama tukiangalia katika tufe la Ardhi kwa mtazamo wa watu wa Qur’an, basi hakika yake ni kama lilivyobainisha (Neno la kumi na tano): Hakika mwanadamu ambaye ndiye tunda jema zaidi la ulimwengu, na muujiza jumuishi katika miujiza ya Mweza Mwenye hekima zote, na kiumbe wa ajabu zaidi na mtukufu zaidi na mzuri zaidi, pamoja na kuwa yeye ni mwenye kushindwa na dhaifu mno kuliko viumbe wote, mwanadamu huyu anaishi katika Ardhi hii, basi Ardhi kwa hiyo ni tandiko kwa ajili ya huyu mwanadamu, basi hiyo Ardhi pamoja na udogo wake na uduni wake kwa kulinganisha na mbingu basi hiyo ni kubwa na tukufu kwa upande wa maana, yaliyomo na ajabu, hata ikawa kwa mtazamo wa Qur’an: Ni moyo wa ulimwengu na kituo chake kikuu kwa upande wa maana na maonesho ya bidhaa zote zilizotengenezwa za muujiza. Na mahali pa kudhihiri kwa majina mazuri yote, hata kana kwamba ni lenzi yenye kukusanya nuru hizo. Na mkusanyiko wa matendo ya Kiungu bwana Mlezi ya hali zote na kioo chake. Na soko pana la kudhihirisha uumbaji wa kiungu wa hali zote, Na hasa kupatisha kwake wingi wa kutisha katika mimea na wanyama nyeti kwa wema wote na ukarimu. Na kielezo kidogo cha bidhaa zilizotengenezwa kwa ulimwengu wa Akhera mkunjufu mpana. Na ni kiwanda kinafanya kwa kasi ya mbali kwa ajili ya kuzalisha bidhaa za kufumwa za kudumu milele. Na mahali pa maonesho ya vielelezo vya mandhari ya kudumu vyenye kubadilika kwa kasi ya juu. Na shamba finyu la muda maalum ili kuzalisha mbegu ndogo ndogo zinalelewa kwa kasi kwa ajili ya bustani za kudumu za kupendeza. Kwa ajili hii yote Qur’an tukufu inaifanya ardhi kuwa ni mwenza wa mbingu, kwa upande wa ukubwa wake kwa maana na ya muhimu zaidi kwa kutengenezwa. Na kana kwamba ni tunda dogo la mti mkubwa, na kana kwamba ni moyo mdogo wa mwili mkubwa. Basi Qur’an tukufu inaitaja ikiilinganisha na mbingu, hiyo iko katika kitanga na mbingu zote ziko kwenye kitanga, basi aya tukufu inakaririwa. رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ Na kama hivi basi pima masuala mengine kwa uelekea huu, na ufahamu: Kwamba hakika mfu zenye kufifia za falsafa, haziwezi kugongana na hakika za Qur’an zilizo hai na zenye kutiwa nuru. Basi zote hizo ni hakika, isipokuwa hitilafu iko katika pembe ya kutazama, basi hakika hudhihiri zikiwa tofauti.

Private reading note

This note stays on this device and is never uploaded to a server.

Up to 1,200 characters