Lem'alar

The Seventeenth Gleam

Source: risaleinur multilingual dataset, risale.site source · Risale-Nur multilingual research corpus
Risale reading plan
§1

Üç meseledir. فَمَن۟ يَع۟مَل۟ مِث۟قَالَ ذَرَّةٍ خَي۟رًا يَرَهُ ۝ وَمَن۟ يَع۟مَل۟ مِث۟قَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُ Aya hii inaonesha udhihirisho kamili mno wa jina tukufu la Al-hafiidh mlinzi na muhifadhi wa kila kitu. Kama unataka uthibitisho kuhusu ukweli huu wa Quran yenye hekima zote, tazama kurasa za kitabu cha ulimwengu, ambacho ki- meandikwa katika mtindo wa kitabu kilicho wazi, utaona kiwango cha juu kabisa cha kudhihirisha jina tukufu la Al-hafiidh, na mambo mengi yenye kulingana na ukweli mkuu katika ulimwengu huu. Kwa mfano, hebu chukua mbegu za miti mbali mbali kwa ujazo wa kiganja chako, maua, na mimea, halafu zika mbegu hizo, ambazo ni kama mifano midogo midogo ya maua tofauti, mti, mimea yote, vyote hivyo ni tofauti na aina mbali mbali, ndani ya giza la ardhi tupu isiyo na uhai, halafu mwagilia rasha rasha za maji yasiyo na uzito wowote, na yasiyoweza kupambanua chochote na kwenda popote unapoyamwagilia. Sasa, hebu njoo kwenye majira ya machipuo, mandhari ya ufufuo kwa kila mwaka, tazama! Na chunguza kwa makini, wakati wa majira ya machipuo, wakati ambapo radi ambayo ni mfano wa malaika Israfiil anavyoita mvua kama vile anapuliza baragumu lake kwa sauti kubwa, akipasha habari njema ya pumzi ya maisha inayopuliziwa ndani ya mbegu zilizozikwa chini ya ardhi; utaona kwamba chini ya udhihirisho wa jina tukufu la Al-hafiidh, mbegu ambazo zinafanana na zote zikiwa zimechanganywa pamoja, zinaafikiana kikamilifu na bila makosa na amri ya uumbaji kutoka kwa Muumbaji Mwingi wa hekima, zinaafikiana sawa sawa kabisa kiasi kwamba katika kukua kwake, utambuzi wa wazi kabisa, uono wa ndani, madhumuni, utashi, ujuzi, ukamilifu, na busara vinakuwa dhahiri, kwani unaona kwamba mbegu hizo, ambazo zote zinafanana, zinajitenga na kujipambanua kutokana na wenzake. Kwa mfano mbegu hii ndogo kabisa, imekuwa mtini, imeanza kueneza neema za Mwingi wa hekima Muumba juu ya vichwa vyetu, inazigawanya, na kuzieneza kwetu kwa mikono yake na mbegu hizi mbili ambazo kwa muonekano ziko sawa zimezaa maua yaitwayo maua ya jua na pansi yamejipamba kwa ajili yetu, yanatabasamu nyusoni mwetu, yanatufanya tuyapende, na aina hii ya mbegu imezaa matunda mazuri, ilikuwa miche, kisha matunda yenye kuchochea hamu yetu ya kula kwa ladha zake tamu, kunukia, na sampuli zake, yanajitoa muhanga kwa ajili ya wateja wake kiasi kwamba yanaweza kupanda kutoka katika kiwango cha maisha ya mmea na kuwa katika kiwango cha maisha ya mnyama, na kuendelea au unaweza kuleta mifano mingine zaidi kwa maana hii, mbegu zilizoendelea kwa namna hiyo ambapo gao moja tu limekuwa kama bustani iliyojazwa miti na maua mbalimbali, hakukupatikana kosa la aina yeyote kati yake, zinabainisha maana ya aya: فَار۟جِعِ ال۟بَصَرَ هَل۟ تَرٰى مِن۟ فُطُورٍ Kupitia udhihirisho na kutangaza jina la Al-hafiidh, kila mbegu inatunza na kuonesha wasifu uliorithiwa kutokana na wazazi na asili yake, bila kuchanganya wala dosari yoyote. Kwa hiyo, hii ni ishara ya hakika kabisa kwamba Mwenye kuhifadhi anatenda kazi za maajabu kama hizi ataonesha tangazo kuu juu ya uhifadhi wake katika ufufuo wa wafu na hukumu ya mwisho. Naam, kudhihirisha uhifadhi ambao hauna makosa na kutokuwa na dosari kutokea katika kiwango kama hichi, hali ndogo mno ya mpito ya muda mfupi sana ni ushahidi wa kukinaisha, kwamba matendo, kazi, maneno, na amali njema na amali mbaya za mtu, matendo ya mshika amana na khalifa wa Allah (sw) Ardhini ambayo yana athari ya kudumu na umuhimu mkubwa yanahifadhiwa kwa muhtasari na yatakuja kuhesabiwa. Hivi mwanadamu anadhani ataachwa kufanya atakavyo? Allah (sw) Apishe mbali! mwanadamu amewekewa hatima ya milele. na kwa ajili ya furaha ya kudumu na majonzi ya kuendelea ataitwa kwenye hisabu kwa matendo yake yote aliyoyafanya, dogo au kubwa mengi au machache atapokea ima thawabu au adhabu. Kwa hiyo, ushahidi wa uhifadhi wa hali ya juu na ukweli wa aya iliyotajwa mwanzoni, ni mkubwa kuliko kiasi cha kuhesabika, hayo tuliyoyaonesha katika suala hili ni kama tone katika bahari, ni nukta moja ya vumbi katika mlima. سُب۟حَانَكَ لَا عِل۟مَ لَنَٓا اِلَّا مَا عَلَّم۟تَنَٓا اِنَّكَ اَن۟تَ ال۟عَلٖيمُ ال۟حَكٖيمُ Utakatifu ni Wako! hatuna ujuzi ila ule uliotufundisha, hakika Wewe ni Mjuzi wa kila kitu Mwingi wa hekima.

§2

Ndugu zangu mnaosikiliza kumbukumbu hizi, tambueni! Kuwa naweza kuandika dua la moyo wangu kwa Mola wangu pamoja na kuwa ilipaswa kufichwa na si kuandikwa, kwa kutaraji kutoka katika rehema yake (s.w) kukubali matamshi ya maandiko yangu badala yangu pale umauti utakapounyamazisha ulimi wangu... Ndio, toba ya ulimi wangu haitoshi kuwa kafara ya dhambi zangu nyingi katika umri wangu mfupi. Basi matamshi ya maandiko thabiti na ya kudumu ni yenye kufaa zaidi kwa dhambi hizo. Kabla ya miaka kumi na tatu katikati ya mgongano mkali wa kiroho na katika kubadilika kwa vicheko vya “Saidi wa zamani” kuwa kilio cha “Said wa sasa” nilizinduka kutoka usiku wa ujana kuingia katika asubuhi ya uzee nikaandika dua hii kwa lugha ya Kiarabu, naileta kama ilivyo: Ewe Mola wangu Mlezi Mwenye rehema na ewe Mola Mkarimu! Umri na ujana wangu umepotea kutokana na uchaguzi wangu mbaya, na hakuna kilichobaki katika matunda yake ila dhambi zenye kuumiza na kudhalilisha, maumivu yenye madhara na kupotosha, na mashaka yenye kusumbua yenye kudhoofisha, nami kwa mzigo huu mzito, moyo wenye ugonjwa na uso wenye haya najikurubisha – kwa uwazi – kwa ukamilifu wa haraka, bila ya kwenda upogo, bila uchaguzi, kama baba zangu, vipenzi vyangu, ndugu zangu, na rafiki zangu kwenye mlango wa kaburi, nyumba ya ukiwa na upweke kwenye njia ya milele, kwa kufarikiana milele na nyumba hii yenye kutoweka yenye kuangamia kwa yakini, yenye kuondoka kwa uwazi, na hasa ni yenye kutoweka na yenye vitimbi kwa mfano wangu mwenye nafsi yenye kuamrisha maovu. Ewe Mola wangu Mlezi Mwenye rehema na ewe Mola Mkarimu! Najiona kwa karibu nimevaa sanda yangu na nimepanda jeneza langu, nimeshawaaga vipenzi vyangu, na nimeshaelekea kwenye mlango wa kaburi langu, ninaita kwenye mlango wa rehema yako: Amani Amani ewe Hannani ewe Mannani, niokoe na aibu ya kukuasi. Ole wangu! sanda ipo juu ya shingo yangu, nami nimesimama kwenye kichwa cha kaburi langu, nainua kichwa changu kwenye mlango wa rehema yako nikiita: Amani Amani ewe Rahman ewe Hannan, niokoe na uzito wa mzigo wa kukuasi. Ole wangu! nimevikwa sanda yangu na nimewekwa kaburini kwangu na wenye kunisindikiza wameniacha, nami nasubiri msamaha na rehema yako... na nashuhudia kuwa hakuna kimbilio wala uokovu ila kwako, na naita: Amani Amani kutokana na ufinyu wa sehemu hii, ubaya wa kukuasi, na kutokana na ubaya wa sura ya dhambi. Ewe Rahman ewe Hannan... ewe Mannan... na ewe Dayyan niokoe na usuhuba wa dhambi na kukuasi. Ewe Mola wangu! Rehema yako ni kimbilio langu na ni njia yangu, na kwako naleta maradhi yangu, huzuni yangu na malalamiko yangu. Ewe Muumba wangu Mkarimu, ewe Mola wangu Mlezi, ewe Bwana wangu, na ewe Mola... Kiumbe chako, uliyemtengeneza, na mja wako aliyeasi dhaifu, aliyeghafilika, mjinga, mgonjwa, dhalili, mkosa, mzee, mweye huzuni, mtoro, amerejea baada ya miaka arobaini kwenye mlango wako akikimbilia kwenye rehema yako, anayekiri dhambi na makosa, aliyejaribiwa kwa dhana potovu na magonjwa, anayekuomba Wewe... Ukimkubali, kumsamehe na kumrehemu basi wewe ni mstahiki wa hilo na Wewe ni mwenye kurehemu kuliko yeyote, kama si hivyo ni mlango gani utakusudiwa usiokuwa mlango wako... Na Wewe ni Mola Mlezi Mwenye kukusudiwa na Muabudiwa wa kweli. Na hapana Mola ila Wewe peke yako huna mshirika... Maneno ya mwisho duniani na ya mwanzo Akhera na kaburini: Nashuhudia hapana Mola ila Allah na nashuhudia kuwa Muhammad ni mjumbe wa Allah (s.a.w). لَٓا اِلٰهَ اِلَّا اَن۟تَ وَح۟دَكَ لَا شَرٖيكَ لَكَ اٰخِرُ ال۟كَلَامِ فِى الدُّن۟يَا وَ اَوَّلُ ال۟كَلَامِ فِى ال۟اٰخِرَةِ وَ فِى ال۟قَب۟رِ اَش۟هَدُ اَن۟ لَٓا اِلٰهَ اِلَّا اللّٰهُ وَ اَش۟هَدُ اَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللّٰهِ صَلَّى اللّٰهُ تَعَالٰى عَلَي۟هِ وَ سَلَّمَ

§3

Kutoka kwenye Muale wa kumi na saba Ewe Mwanaadamu! Hali ya ajabu ambayo Muumba Mwingi wa hekima, ameijumuisha katika maumbile yako ni kushindwa kumaliza haja katika ulimwengu huu; kama mtu aliyezibwa pumzi kwenye gereza, unaangalia mahali pengine papana zaidi kuliko ulimwengu huu, na bado unaingia katika mambo madogo sana, kumbukumbu, punde, na kutua ndani yake. Moyo wako na akili ambavyo haviwezi kutuama katika ulimwengu mkubwa vinatulia kwenye kitu hicho kidogo. Utashangaa pamoja na mihemko yako iliyosheheni katika muda huo mfupi, kumbukumbu hiyo ndogo sana. Na amefungasha katika maumbile yako nguvu ambazo sio za kimaada na vipawa madhubutii, ambazo kama baadhi yake zingemeza ulimwengu, zisingetosheka. Na baadhi ya hizo haziwezi kuhimili hata kidogo sana ndani yake wenyewe. Kama jicho haliwezi kuhimili unywele japo kichwa kinaweza kubeba mawe mazito, vipawa hivyo haviwezi kuhimili uzito hata wa unywele, ambapo, baadhi ya hali zisizokuwa kubwa, hutokea kutokana na kughafilika na upotevu. Baadhi ya wakati huzimwa na hata kufa. Kwa kuwa ni hivyo, kuwa muangalifu, kanyaga kwa tahadhari, kuwa na hofu ya kuzama! Usizame katika ujazo wa kinywa, neno, mbegu, mwanga, ishara, busu! Usivitumbukize vipawa vyako vipana ambavyo vinaweza kumeza ulimwengu katika vitu kama hivi. Kwa sababu kuna vitu ambavyo ni vidogo sana ambavyo kwa namna moja vinaweza kumeza vitu ambavyo ni vikubwa sana. Mbingu pamoja na nyota zake vinaweza kuingia kwenye kipande kidogo sana cha kioo na kuzamishwa. Na aghlabu ya kurasa za amali zako na majani ya maisha yako huingia katika kipawa cha kumbukumbu yako, kidogo sana kama mbegu ya hardali. Kwa hiyo kuna vitu vidogo sana pia vinavyomeza vitu vya ukubwa wa namna huo na kuvihifadhi ndani yake. Dördüncü Remiz: Ey dünya-perest insan! Çok geniş tasavvur ettiğin senin dünyan, dar bir kabir hükmündedir. Fakat, o dar kabir gibi menzilin duvarları şişeden olduğu için birbiri içinde in’ikas edip göz görünceye kadar genişliyor. Kabir gibi dar iken, bir şehir kadar geniş görünür. Çünkü o dünyanın sağ duvarı olan geçmiş zaman ve sol duvarı olan gelecek zaman, ikisi ma’dum ve gayr-ı mevcud oldukları halde, birbiri içinde in’ikas edip gayet kısa ve dar olan hazır zamanın kanatlarını açarlar. Hakikat hayale karışır, ma’dum bir dünyayı mevcud zannedersin. Nasıl bir hat, sürat-i hareketle bir satıh gibi geniş görünürken, hakikat-i vücudu ince bir hat olduğu gibi; senin de dünyan hakikatçe dar fakat senin gaflet ve vehm ü hayalinle duvarları çok genişlemiş. O dar dünyada, bir musibetin tahrikiyle kımıldansan, başını çok uzak zannettiğin duvara çarparsın. Başındaki hayali uçurur, uykunu kaçırır. O vakit görürsün ki o geniş dünyan; kabirden daha dar, köprüden daha müsaadesiz. Senin zamanın ve ömrün, berkten daha çabuk geçer; hayatın, çaydan daha süratli akar. Madem dünya hayatı ve cismanî yaşayış ve hayvanî hayat böyledir; hayvaniyetten çık, cismaniyeti bırak, kalp ve ruhun derece-i hayatına gir. Tevehhüm ettiğin geniş dünyadan daha geniş bir daire-i hayat, bir âlem-i nur bulursun. İşte o âlemin anahtarı, marifetullah ve vahdaniyet sırlarını ifade eden لَٓا اِلٰهَ اِلَّا اللّٰهُ kelime-i kudsiyesiyle kalbi söylettirmek, ruhu işlettirmektir.

Private reading note

This note stays on this device and is never uploaded to a server.

Up to 1,200 characters