Lem'alar

The Nineteenth Gleam

Source: risaleinur multilingual dataset, risale.site source · Risale-Nur multilingual research corpus
Risale reading plan
§1

İktisat Risalesi Risala Ya Uchumi (kufanya wepesi) Katika Ibada بِسْمِ اللّٰهِ الرَّحْمٰنِ الرَّح۪يمِ كُلُوا وَ اش۟رَبُوا وَ لَا تُس۟رِفُوا Aya hii tukufu inatupa darsa muhimu mno na inatuongoza kwenye muongozo mzuri wa hekima, kwenye umbo la amri na kufanya uchumi na kuachana na israfu, na masuala haya tuta zungumza katika vifungu saba.

§2

Hakika Allah mwingi wa rehema, amewataka wanadam washukuru kutokana na neema alizowapa, lakini israfu ni yenye kwenda kinyume na kushukuru na kufanya uchumi ni unyenyekevu wenye manufaa mbele ya neema. Hakika kufanya uchumi kama ilivyo kushukuru kiroho, ni heshima kubwa mbele ya rehema za kiungu zilizojaa ndani ya ihsani na neema. Nayo ni sababu pekee ya kupata baraka na kuongezeka, nayo ni asili ya siha ya mwili, na njia ya utukufu na kuepukana na udhalili na kupata nguvu za kiroho, pia ni njia madhubuti ya kupata hisia za yaliyomo kwenye neema na ladha zake, nayo ni sababu imara ya kupata ladha illiyofichikana ndani ya neema isiyo dhihiri utamu wake, kwa kuwa israfni yenye kwenda kinyume na hekima tulizozitaja hivyo mwisho wake unabaki kuwa ni mbaya mno.

§3

Hakika muumbaji mwenye hekima, amemuumba mwanaadam mfano wa jengo lililo kamilika, au pengine ni mfano wa mji ulio kamili mipangilio yake, akajaalia hisiya utamu iliyo midomoni ni sawa na bawabu (mlinzi) imara na mishipa ya hisia ni sawa na nyuzi za simu, zikifanya kazi nyeti na muhimu ya kufikisha habari baina ya nguvu za kupata ladha na tumbo, ambalo lipo kwenye kituo kikuu cha mwanadam, na hisia hii ya utamu kufikisha kile kilicho bora na kitamu kwenye kinywa cha mwanadam na kulizuilia tumbo, dhidi ya vile vyenye madhara, visivyohitajika ndani ya mwili, huku ikisema (si ruhusa kuingia) ikivikataa na kuvifukuza na kuvitemea mate kwa dharau mbele ya kila kisichokuwa na manufaa kwa mwili au chenye madhara na kibaya kwake. Kama ilivyokuwa kwa nguvu ya ladha kwenye kinywa ni mfano wa mlinzi, hivyo hivyo tumbo ndio mfalme wa mwili na mtawala wake katika uongozi, na kama itafikia kima cha zawadi anazopelekewa kiongozi kwenye kasri daraja mia, hakika khumsi yake tu ndiyo yenye kujuzu kupewa mlinzi na wala sio zaidi, ili asije mlinzi akapotea na kusahau wadhifa wake, na hivyo kasri kuvamiwa na waovu na kutoa rushwa kwa senti chache. Kwa mujibu wa siri hii kama tujaalie kwamba mbele yetu vyakula aina mbili, cha kwanza kimekusanya vyakula vyenye lishe bora, mfano wa jibini, mayai, n.k, na vinakadiriwa thamani yake ni shilingi mia, ama chakula cha pili halawa za kifakhari zenye kukadiriwa thamani yake kuwa ni shilingi mia tano, vyakula hivi kabla havijaingia kinywani bila shaka vyote viko sawa na havina tofauti, na viko sawa vikiingia katika kujenga siha ya mwili baada ya kuingia kinywani na kushuka kupitia kooni hadi tumboni, bali inaweza kuwa jibini iliyokuwa thamani yake rahisi shilingi mia tu ikawa bora kisiha kuliko chakula chengine, hivyo kuna tofauti isipokuwa kwa hisia ya utamu ndani ya kinywa ambayo haitumii ila muda mchache mno wa nusu dakika tu, hebu na akadirie mtu madhara ya israfu na apime kiwango cha ubaya wa kutumia shilingi mia tano badala ya kutumia mia kwa ajili ya kupata ladha isiyodumu zaidi ya nusu dakika! Mlinzi kupata malipo mara tisa zaidi ya kinachotolewa kwa kiongozi kwenye kasri katika zawadi bila shaka inaweza kumpelekea kwenye ghururi na tamaa, na kuanza kusema ‘mimi ndie mkuu hapa na atakaenipa zawadi zaidi ndie nitakaempitisha ndani’, hivyo huanza kuharibu nidhamu iliyopo hapo na kuanza kuwasha moto na kusababisha watu kuanza kupiga makelele, “Msaada haraka nipelekeni kwa tabibu anipunguzie joto na sindikizo anipungizie joto azime moto wangu” Uchumi na ukinaifu ni zenye kwenda sambamba na hekima za kiungu, kwani zinafanya kazi pamoja na hisi ya kionjo upamoja wa mlinzi, na unauweka kwenye mipaka yake na unaulipa kwa mujibu wa wadhifa wake. Ama israfu kwa kuwa unafuata njia kinyume na hekima hiyo ya kiungu, ni haraka mwenye kufanya israfu hukumbana na kipigo chenye kuletea maumivu na machungu mazito, kwani hupata mikorogo ya maumivu tumboni mwake, inayopelekea kupotea kwa hamu ya kweli ya chakula, hivyo hula kwa hamu ya uongo,akiipamba kwa aina ya vyakula vyenye kumsababishia uzito kwenye usagaji wake.

§4

Punde tu hivi tumesema kwenye zingatio la pili, kwamba nguvu za hisia ya utamu inafanya kazi ya mlinzi, na hivi pia ndivyo ilivyo kwa wale walio ghafilika, ambao hawajapanda daraja bado ya kiroho, wala hawajasonga mbele katika uwanja wa shukurani na kufikia daraja zake, hakika haipaswi mtu kukimbilia kwenye israfu kwa kutumia mara kumi ya thamani ya kitu kwa kukidhi ladha ya hisia hiyo fupi. Lakini hisia hii ya kionjo au ladha kwa wenye kushukuru na kwa watu wa kweli na wenye nyoyo safi na akili timamu ni mfano wa mlinzi na muelekezaji msimamizi wa jiko la rehema ya Allah (kama tulivyobainisha kabla), ama kinachotokea katika nguvu zile za kionjo ni kazi ya kudiriki kima cha neema za Allah na kuzitambua kwa aina mbali mbali ikiwemo vipimo madhubuti vingi kupitia vyakula tofauti, nayo ni kuufikisha mwili ujumbe na tumbo kwa kuchelewa kushukuru neema hizo za kiroho. Wadhifa wa nguvu za hisia ya kionjo haimalizikii kuwa ni mlinzi wa kimwili pekee, bali ni hakimu mzuri wa wadhifa wa tumbo na wa daraja ya juu, kwani pia ni mlinzi bora wa moyo na roho na akili, na kuvipa ulinzi vyote, tukitambua kwamba ni yenye kuweza kufikia njia ya kufikia ladha zake, kwa sharti la kutofanya israfu, kwa ajili ya kukamilisha wajibu wa shukurani za kweli zilizokadiriwa kwa ajili yake, na kwa nia ya kujua na kutambua neema za Allah kwa ladha na hisia zake, kwa sharti za uhalali na kutozifanya kuwa ni njia ya kujidhalilisha na kujikweza, kwa maana tunaweza kuufanya ulimi kuwa ni mbebaji wa nguvu hizi za kionjo katika kushukuru kwa ajili ya kutofautisha baina ya chakula tofauti. Huu hapa mfano wa tukio lenye kuashiria hakika ya haya na ni jumla ya makarama ya sheikh Al-kaylany. Kulikuwa na mtu mzima mwanamke akiwa na mtoto wa kiume mmoja pekee, mtoto huyu alikuwa akilelewa kwa sheikh, siku moja huyu mama alikwenda kumtembelea mwanawe, akamkuta anakula mkate mkavu, alikuwa amekonda kwa sababu ya riyadha za kiroho, mama akaingiwa na huruma na huzuni kwa hali ile,akatoka na kwenda kumshtakia sheikh Al-kaylany, akamkuta sheikh anakula kuku wa kuchoma, lakini kwa huruma juu mwanawe (hakunyamaza) aliendelea na akasema “Mwanangu anakaribia kufa kwa njaa na wewe unakula kuku!”, na sheikh akasema kumwambia kuku “simama kwa idhini ya Allah” alitoka yule kuku kwenye chombo baada ya kuwa keshammaliza kumla hii imepokewa na watu wa kutegemewa, kudhihirisha karama moja ya mtu mashuhuri aliyekuwa na makarama katika ulimwengu huu, nae ni sheikh Al-kaylany, na sheikh alimwambia yule mama, “akifikia mwanao daraja hizi na ale na yeye kuku“, mafunzo kwenye kauli hii kwamba, “Wakati ikifikia roho ya mwanao kuhukumia mwili wake na moyo kumiliki nafsi yake, na akili ikawa ni kiongozi wa tumbo na ladha kushikamana na kushukuru, hapo atakuwa anaweza kula anachotaka katika vyakula.

§5

Mwenye kufanya uchumi hakika haogopi ufukara wala umaskini kama inavyofahamika katika hadithi tukufu لَا يَعُولُ مَنِ اق۟تَصَدَهِ hapati ufukara asiefanya israfu, hakika kuna mifano yakutosha na isiyohesabika katika hili, yenye kuonyesha kwamba kufanya uchumi ni sababu ya kuteremka baraka, na ni msingi madhubuti wa maisha bora, nitataja hapa baadhi ya niliyoyaona ndani ya nafsi yangu na kwa ushahidi wa wengine walionisaidia katika huduma na wakanikubali kwa ikhlasi na hapa nasema: Niliwahi kupata baadhi ya wakati na walipata rafiki zangu mara kumi zaidi ya baraka kwa sababu ya uchumi, na hata kabla ya miaka, wakati waliponiomba sana viongozi wa baadhi ya makabila waliokuwa uhamishoni pamoja nami huko Burdur, nikubali zaka zao ili niondokane na hali ya idhilali na hali ya uchache wa pesa niliokuwa nao, nikasema kuwaambia wale viongozi matajiri, licha ya kuwa ni mwenye uwezo mdogo kifedha lakini namiliki uchumi na nimezoea ukinaifu, hakika mimi ni tajiri zaidi kulikoni nyie. Hivyo nikalikataa ombi lao walilokuwa wakilikariri, na kwa bahati mbaya baadhi ya waliokuwa wakinitaka suala lile walifikwa na msiba wa madeni baada ya miaka miwili, kwa kukosa kufanya uchumi katika mali zao, lakini fedha ndogo zilinitosha Allah ndie wa kushukuriwa, kwa baraka za kufanya uchumi, wala hawai kuninawishwa uso wala haikunipelekea kujitangaza haja zangu kwa watu, wala sikuharibu yale niliyoyafanya kuwa ni msingi katika maisha yangu nayo ni (Ni kutoshelezeka na kuacha kuombaomba vitu vya watu). Hakika asiefanya uchumi ni mwenye kuporomoka bila shaka kwenye idhilali, na, anakuwa ni mwenye kuteleza kuelekea kukosa heshima, hakika mali inayotumiwa kwa israfu katika zama zetu hizi ni mali nyingi sana, ambayo hutumiwa wakati mwengine hadhi na utukufu kama ni thamani ya rushwa, bali inaweza hata kupoteza utukufu wa dini, na mtu kupewa fedha chafu, na kupokea vijisenti vya pesa, juu ya hesabu ya mamia ya shilingi za kiroho, na laiti angalitoshelezeka, manadam na mahitajio ya lazima, na akafanya hima yake juu ya hayo, basi angalipata riziki kwa njia asizozitarajia kama ilivyokuja kwenye aya اِنَّ اللّٰهَ هُوَ الرَّزَّاقُ ذُو ال۟قُوَّةِ ال۟مَتٖينُ na katika aya وَمَا مِن۟ دَٓابَّةٍ فِى ال۟اَر۟ضِ اِلَّا عَلَى اللّٰهِ رِز۟قُهَا Riziki ziko aina mbili. AINA YA MWANZO Riziki ya uhakika na ukweli ambayo inasimamia maisha ya mwanadam, nayo ni chini ya ahadi ya Allah kwa mwanadam kwa hukumu ya aya hii tukufu, anaweza mtu kupata riziki za lazima kwa hali yoyote ile,ikiwa haujapita uchaguzi mbaya, bila ya kuhitajika kutoa thamani utu na utukufu wake. AINA YA PILI Hii ni riziki kimaana tu (majazi) na anaeitumia vibaya anakuwa hawezi kuachana na mambo yasiyo ya lazima, ambayo yalimpitikia kuwa ni ya lazima kutokana na matunda ya mitihani ya wigo, na thamani ya kupata rizki hizi mbaya ni kubwa mno hasa hasa katika zama hizi, ambapo udhamini wa Allah unaonekana kama uko mbali, kwani mtu anaweza kupokea mali kwa kutolea muhanga utu na utukufu wake na kuridhia udhalili, bali inawezekana hata kuporomoka katika shimo la maangamizo, nakufikia kubusu miguu ya watu dhalili, zaidi ya hayo ni kufikia hata kutolea muhanga kwa mali hiyo chafu dini yake iliyotukufu, dini ambayo ni nuru ya maisha yake ya daima, hakika machungu wanayoyapata watu wenye dhamira njema katika kufikiria maumivu wanayoyapata wenye mahitajio machafu katika zama hizi ambazo ufakiri na mahitajio, ni kutokana na ladha zao wanazozipata katika mali za haramu, na huongezeka uchungu wanapokuwa na dhamira njema. Inapaswa katika zama hizi za maajabu kutoshelezeka, na mahitajio ya lazima tu kwenye mali zenye mashaka na wasi wasi, kwa mujibu wa hukumu ya kisheria isemayo (madhara yanakadiriwa kwa kiwango chake). Kwani inawezekana kuchukua mali ya haramu kwa dharura tu na sio zaidi ya hapo. Na mwenye dharura hawezi kula maiti mpaka kushiba, bali atakula kwa kiwango cha kumuepusha na kumkinga na mauti, na kama hivyo na vile vile hakiliwi chakula kwa pupa kwa mamia ya wenye njaa. hapa tutaonyesha mfano wenye dalili ya wazi wenye kubainisha kuwa uchumi ni sababu ya utukufu na ukamilifu. Alisimama Hatim Altaiy aliyekuwa mashuhuri kwa ukarimu wake na utajiri wake siku moja, na akatoa zawadi yenye thamani kwa wageni wake, baadae akatoka na kuanza kutembea jangwani, akakutana namtu kikongwe amebeba mzigo mzito mgongoni mwake, ulikuwa ni mzigo wa kuni zenye miba miba na majani, na huku damu ikitoja toja mwilini kwa sababu ya miba, Hatim akamwambia (bila ya kumwambia yeye ni nani) “Ewe bwana leo Hatim ana ugeni mkubwa na atagawa zawadi za thamani kwa wageni wake, hebu nawe harakiza ufike pengine utapata chochote kile mara mbili zaidi ya hichi unachokipata kwenye mzigo huu”, Yule mtu akamjibu kumwambia “Nitabeba mzigo wangu huu kwa utukufu wa nafsi yangu na kwa jasho la kipaji changu cha uso wala sitaki kupata chochote kwenye utajiri wa Hatim Altaiy” Alipoulizwa Hatim Altaiy siku moja “Ni mtu gani umemkutia kuwa ni bora zaidi kuliko wewe na mkarimu? Akajibu “Ni yule niliekutana nae jangwani aliekinai mchumi, hakika naona ni mbora na mkarimu”

§6

Hakika katika ukamilfu wa ukarimu wa Allah, ni kwamba anaonjesha ladha ya ukarimu wa neema zake kwa mtu fakiri kabisa, kama vile anavyomuonjesha tajiri wao, maskini anaonja ladha neema sawa na kiongozi (rais –mfalme). Ladha anayoipata maskini kwa kula mkate mkavu kwa sababu ya njaa, bila shaka ikojuu zaidi ya ile anayoipata tajiri kwa kula vitamu (halawa) za kifakhari kwa kuchoka na hata kwa kutokuwa na hamu navyo sana na kwa israfu. Katika maajabu zaidi ni kuona baadhi ya wapenda israfu na ubadhirifu, kuwatuhumu wenye uchumi katika matumizi yao kuwa ni mabakhili, hakika sio hivyo kabisa, bali kuwa mchumi ni utukufu na ukarimu, lakini ubakhili udhalili ni sifa za wenye kufanya israfu ubadhirifu kutoka katika utajiri wa juu juu. Kuna tukio limetokea chumbani kwangu huko Isparta, mwaka nilipokua naandika risala hii, tukio lenye kuthibitisha haya. Mmoja wa wanafunzi alikuwa akinishikilia nipokee zawadi yake iliyokuwa na thamani ya waqiya mbili na nusu za asali, hii ilikuwa ni kinyume na misingi yangu ya maisha, na kila nilivyojaribu kumfahamisha hakuweza kufahamu na kukinai, ikanibidi nikubali pasina budi, lakini kwa sharti kwamba watu watatu wengine tushirikiane kula asali ile kidogo kidogo ndani ya mwezi wa shaaban na ramadhani ili alietupa apate thawabu, nao wasiwe bila ya asali, na nikawausia kukubali ile zawadi, wakati mimi nilikuwa tayari nina waqiya ya asali.. Licha ya kwamba wale rafiki zangu watatu walikuwa ni watu wa msimamo mwema na istiqama, hakika waliisahau kwa sababu ya ukarimu walio wakifanyiana baina yao na kuchunga hisia za wengine na kuwapendelea kheri, na mfano kama huo wa sifa njema, hivyo ile asali wakaimalizakwa siku tatu tu, nikawaambia, “Nilitaka kwenyenia yangu hii asali muitumie kwa siku thelathini au zaidi lakini mumeimaliza kwa siku tatu tu, hongereni!, bali mimi nimekuwa natumia asali yangu kwa kila siku na kwa miezi miwili shaaban na ramadhani, na kwamba pengine ilikuwa ni sababu ya kumshukuru Allah kwa kupata thawabu kwani nilikuwa nawapa kijiko kimoja kimoja wakati wa kufutari. Na pengine wale waliokuwa wakishuhudia huyo waliona kama kwamba ni hali ya ubakhili, lakini wakaona ile hali ya rafiki zangu ya siku tatu tu ni ubora na utukufu, lakini katika ubakhili usio wa wazi ubora mkubwa na Baraka na thawabu nyingi katika hali halisi, na katika ukarimu na israfu hasa kama hapajaachwa kuangalia na kutaka vya watu kwa tamaa kwa hali zilizo chini zaidi ya ubakhili.

§7

Hakika uwazi mkubwa na tofauti kubwa sana baina ya uchumi na ubakhili, kama ilivyokuwa unyenyekevu ni jumla ya tabia zenye kupendeza, na inakwenda kinyume na maana ya kuwa idhilali ambayo ni katika tabia yenye kuchukiza, licha ya kwamba ziko karibu ya sura, kama ilivyo sifa ya heshima kuwa ni sifa njema inakwenda kinyume na maana ya kiburi, ambayo ni sifa yenye kuchukiza licha ya kwamba zinashabihiana kisura. Na kama hivyo ndivyo ilivyo katika uchumi ambayo ni sifa ya kiutume iliyo bora, bali ni sifa ya kimsingi, kwake inazunguka nidhamu za hekima za Allah zinazoongoza ulimwengu wote, na haina mahusiano yoyote na sifa ya ubakhili ambayo ndani yake umo uchoyo tamaa na pupa la kupata, bali hakuna mafungamano yoyote isipokuwa mshabaha wa nje nje tu hili hapa tukio lenye kuthibitisha hayo. Aliingia Abdallah bin Omar mtoto kubwa wa Seyyidina Omar ibn Al-khatab Alfarouq khalifa wa Mtume na mmoja katika Abdallah saba walio mashuhuri baina ya wanazuoni masahaba watukufu, aliingia sahaba huyu mtukufu kwenye mazungumzo mazito alipokuwa sokoni akitafuta kitu kidogo cha thamani kwa ajili ya kuhifadhi uchumi na kuchunga amana na istiqama ambazo ni sifa muhimu zenye kuzunguka baina yake biashara, mara sahaba mwengine akamuona akadhinia ni aina ya ubakhili na akachukulia kuwa ni jambo zito, kuwa jambo kama hili linafanywa na mtoto wa Amir Al-muuminina, na kiongozi wa dunia akamfuata mpaka nyumbani kwake ili afahamu baadhi ya mambo yake, akamkuta anatumia baadhi ya wakati wake na mtu fakiri mlangoni pake na akawa anabadilishana nae mazungumzo nae kwa bashasha na mapenzi, baadae akatoka kwa mlango mwengine na kuzungumza na fakiri mwengine, jambo hili lilimshangaza sana na akatoka haraka na kuwafuata wale mafakiri na kutaka ubayana kwao, “Hebu niambieni amefanya nini Ibn Omar aliposimama nanyi” wakasema “kila mmoja wetu amempa kipande cha dhahabu”. Akashangazwa sana na kauli ile akasema Subhanallah, jambo la kushangaza mno, sokoni anaingia kwa mazungumzo makubwa kwa ajili ya senti moja, halafu nyumbani kwake anatoa mfano wake mara mia kwa wenye kuhitajia kwa maridhio yake, bila ya mwengine kujua; akatoka na kwenda kumuuliza Ibn Omar. Ewe imamu jee hunitatulii tatizo langu hili? Ulipokuwa sokoni ulifanya mambo kadha wa kadha, na nyumbani ulifanya mambo kadha wa kadha kwa nini?” akamjibu kwa kusema “Yaliyotokea sokoni kwa sababu ya uchumi na kuchunga amana na kuhifadhi ukweli, kwani hizo sifa za mauziano na roho yake wala sio uchoyo wala ubakhili, ama yaliyonitokea nyumbani yanatokana na mapenzi na huruma ya moyo na roho njema na ukamilifu wake wala sio ubakhili wala israfu. Kwa siri hii amesema Imam Abu Hanifa bin Nuuman (Allah awe radhi nae) “Hakuna israfu katika kheri wala hakuna kheri katika israfu”, na kama ilivyokuwa hakuna israfu katika kheri na ihsani kwa anaestahiki, hivyo hivyo hakuna kheri katika israfu.

§8

Hakika israfu ni yenye kuletea pupa la kupata na pupa linaletea mambo matatu: MWANZO: Kukosa kukinai Kukosa kukinai kunapelekea kukosekana shauku ya kuhangaika na kufanya kazi, hali inayopelekea kwa mwenye kukosa kukinai daima na malalamiko na wala sio shukurani, na kumsukuma kwenye viwanja vya uvivu, hivyo huacha mali safi inayotokana na chumo la halali, na anatafuta yale yasio na tabu wala uchovu katika mali zisizo halali kisheria, na kupoteza katika njia hiyo tukufu na hadhi yake. PILI: Kuvunjika moyo na kula hasara. Anapoteza malengo na kuwa karibu na uzito (katika masuala yake) na anakoseshwa uwepesi na msaada mpaka inamthibitikia kauli mashuhuri (Mwenye pupa ni mla hasara na kuvunjika moyo). Athari za pupa na kukosa ukinaifu ni zenye kwenda kwenye ulimwengu wa viumbe hai kwa mujibu wa sharia na mwenendo wa maisha ya kila siku, hakika mimea kupata riziki zake za lazima ni kwa sababu ya ukinaifu wake wa kimaumbile, na wanyama kutoka wenyewe kutafuta riziki kwa shida inaonyesha kiasi gani mwili unapata shida katika kufanya pupa la kupata na kwa kiwango cha manufaa makubwa yanayopatika katika ukinaifu.. Hakika kutiririka maziwa – chakula chenye lishe bora-kwenda kwenye kinywa cha mtoto mdogo dhaifu, pasina kujuwa wapi yanatokea kwa ukinaifu wao kama inavyobainika katika hali zao, au wanyama wanavyokimbilia kwa pupa na tamaa kwenye riziki zao zenye mapungufu na kuchanganyika changanyika ni ithibati ya yale tunayoyazungumza. Ama hali ya samaki wakubwa wasio na akili wasio na ukinaifu wakupata riziki zao kwa ukamilifu, na kushindwa wanyama wenye uhodari mfano wa mbweha na kima kupata mawindo yao kwa ukamilifu licha ya pupa lao la kuwinda wanabakia wembamba, ni alama nyengine ya kubainisha kuwa sababu yake ni pupa kubwa la kupata mashaka na shida, na yale ambayo sababu yake ni ukinaifu nayo ni raha na furaha. Hem Yahudi milleti hırs ile riba ile hile dolabı ile rızıklarını zilletli ve sefaletli, gayr-ı meşru ve ancak yaşayacak kadar rızıklarını bulması ve sahra-nişinlerin (yani bedevîlerin) kanaatkârane vaziyetleri, izzetle yaşaması ve kâfi rızkı bulması; yine mezkûr davamızı kat’î ispat eder. Hem çok âlimlerin (Hâşiye ) ve ediblerin (Hâşiye ) zekâvetlerinin verdiği bir hırs sebebiyle fakr-ı hale düşmeleri ve çok aptal ve iktidarsızların fıtrî, kanaatkârane vaziyetleri ile zenginleşmeleri kat’î bir surette ispat eder ki: Rızk-ı helâl, acz ve iftikara göre gelir; iktidar ve ihtiyar ile değil. Belki o rızk-ı helâl, iktidar ve ihtiyar ile makûsen mütenasiptir. Çünkü çocukların iktidar ve ihtiyarı geldikçe rızkı azalır, uzaklaşır, sakîlleşir. اَل۟قَنَاعَةُ كَن۟زٌ لَا يَف۟نٰى hadîsinin sırrıyla kanaat, bir define-i hüsn-ü maişet ve rahat-ı hayattır. Hırs ise bir maden-i hasaret ve sefalettir. Üçüncü Netice: Hırs ihlası kırar, amel-i uhreviyeyi zedeler. Çünkü bir ehl-i takvanın hırsı varsa teveccüh-ü nâsı ister. Teveccüh-ü nâsı müraat eden, ihlas-ı tammı bulamaz. Bu netice çok ehemmiyetli, çok cây-ı dikkattir. Elhasıl: İsraf, kanaatsizliği intac eder. Kanaatsizlik ise çalışmanın şevkini kırar, tembelliğe atar; hayatından şekva kapısını açar, mütemadiyen şekva ettirir. (Hâşiye ) Hem ihlası kırar, riya kapısını açar. Hem izzetini kırar, dilencilik yolunu gösterir. İktisat ise kanaati intac eder. عَزَّ مَن۟ قَنَعَ ذَلَّ مَن۟ طَمَعَ hadîsin sırrıyla kanaat, izzeti intac eder. Hem sa’ye ve çalışmaya teşci eder. Şevkini ziyadeleştirir, çalıştırır. Ama uchumi unapelekea ukinaifu na ukinaifu unazaa utukufu kwa muijibu wa hadithi (Utukufu kwa mwenye kukinai na idhilali kwa mwenye tamaa), na shauku inaongezeka kwa kuhangaika na kufanya kazi na kumpelekea katika bidii na kufanya bidii, kwani mtu anapohangaika siku moja na kupata ujira wake jioni, kama hivyo atahangaika siku ya pili kwa sababu ya siri ya kukinai, ama mwenye kufanya israfu hatohangaika siku ya pili kwa kukosa ukinaifu na hata atakapohangaika hatahangaika kwa shauku. Kama hivi ndivyo ulivyo ukinaifu uliojaa uchumi unavyofungua mlango wa shukurani na kufunga mlango wa malalamiko, na anabakia mwanadam kwenye shukurani kwa uhai wake na ukinaifu hautazami mtazamo wa watu kwani haina haja nao, hivyo inajifungulia mlango wa ikhlasi na kufunga wa riya. Nimeshuhudia madhara mengi makubwa na hasara nzito zinazotokana na israfu na kukosa uchumi, nimeziona kwa mapana sana kama hivi ifuatavyo: Nilikwenda kwenye mji fulani kabla ya miaka tisa, ulikuwa wakati huo ni msimu wa kipupwe, hivyo sikuwahi kushuhudia chemchem zake za kheri na uzalishaji, Mufti Allah amrehemu wake akaniambia, “Watu wetu ni mafakiri na masikini,” akakariri kauli yake hii mara nyingi, na iliniathiri kauli yake hii sana, ikanijaza huruma nikabaki nawaombea rehema na nikawa napata machungu kwa hali za watu wake, kwa kipindi chenye kufikia miaka sita, na baada ya miaka minane nilirejea tena kwenye mji ule na ulikuwa ni wakati wa kiangazi, na macho yangu yakavutiwa na mabustani yake, nikakumbuka kauli ya yule Mufti nikasema katika hali ya kushangazwa: “Subhanallah hakika mazao ya mabustani na mashamba haya yamezidi mahitajio ya mji kwa kiwango kikubwa, na ilitosha watu wake kuwa ni matajiri ! nikabaki kuwa ni mwenye wasiwasi na suala hili, lakini nikabaki na uhakika wala sikuhadaika na sura ya nje, nikadiriki yakini kabisa kwamba baraka ilikuwa imeondoshwa ndani ya mji huu kwa sababu ya israf na kukosa kuwa wachumi, na ndilo jambo lililompelekea yule Mufti kusema “watu wangu ni mafakiri na masikini”, licha ya kiwango hichi kikubwa cha chemchem za kheri na mali na hazina. Hakuna shaka yoyote kwamba imethibiti kwa uzoefu, kuwa kutoa zaka na kuwa mchumi katika ibada ni sababu mbili muhimu za kuzidisha na kuletea baraka, ama israfu na kuzuia zaka ni sababu mbili kuu za kuondosha baraka. Na amefasiri Ibn Sina mwanafalsafa na mwalim wa mafilosofi wa kislam, na mkuu wa matabibu amefasiri aya hii كُلُوا وَ اش۟رَبُوا وَ لَا تُس۟رِفُوا kwaa zawiya ya kitabibu kwa beti za kishairi zenye : جَمَع۟تُ الطِّبَّ فِى ال۟بَي۟تَي۟نِ جَم۟عًا وَ حُس۟نُ ال۟قَو۟لِ فٖى قَص۟رِ ال۟كَلَامِ فَقَلِّل۟ اِن۟ اَكَل۟تَ وَ بَع۟دَ اَك۟لٍ تَجَنَّب۟ وَ الشِّفَاءُ فِى ال۟اِن۟هِضَامِ وَ لَي۟سَ عَلَى النُّفُوسِ اَشَدُّ حَالًا مِن۟ اِد۟خَالِ الطَّعَامِ عَلَى الطَّعَامِ Nimekusanya tiba kwenye beti mbili pekee Na kauli bora ni kufupisha maneno Punguza chakula unapokula na baada ya Na shifaa ni katika kusaga chakula Hakuna hali ngumu kwa mtu kama Kuingiza chakula juu ya chakula Cây-ı hayret ve medar-ı ibret bir tevafuk İktisat Risalesi’ni, üçü acemi olarak beş altı ayrı ayrı müstensih ayrı ayrı yerde ayrı ayrı nüshadan yazıp birbirinden uzak, hatları birbirinden ayrı, hiç elifleri düşünmeyerek yazdıkları her bir nüshanın elifleri; duasız elli bir, dua ile beraber elli üçte tevafuk etmekle beraber; İktisat Risalesi’nin tarih-i telif ve istinsahı olan Rumîce elli bir ve Arabî elli üç tarihinde tevafuku ise şüphesiz tesadüf olamaz. İktisaddaki bereketin keramet derecesine çıktığına bir işarettir. Ve bu seneye “Sene-i İktisat” tesmiyesi lâyıktır. Evet, zaman iki sene sonra bu keramet-i iktisadiyeyi, İkinci Harb-i Umumî’de her taraftaki açlık ve tahribat ve israfatla ve nev-i beşer ve herkes iktisada mecbur olmasıyla ispat etti. سُب۟حَانَكَ لَا عِل۟مَ لَنَٓا اِلَّا مَا عَلَّم۟تَنَٓا اِنَّكَ اَن۟تَ ال۟عَلٖيمُ ال۟حَكٖيمُ

Private reading note

This note stays on this device and is never uploaded to a server.

Up to 1,200 characters