Lem'alar

The Thirtieth Gleam

Source: risaleinur multilingual dataset, risale.site source · Risale-Nur multilingual research corpus
Risale reading plan
§1

Inahusu Mojawapo ya Nukta za Jina la Allah Al-Adlu وَإِن مِّن شَيْءٍ إِلاَّ عِندَنَا خَزَائِنُهُ وَمَا نُنَزِّلُهُ إِلاَّ بِقَدَرٍ مَّعْلُومٍ Ilijionesha kwangu nukta nyororo katika zilizo nyororo za aya hizi, na nuru katika midhihirisho ya jina la Allah: (Al-Adlu) ambalo ni jina kuu kabisa la Allah, au ni nuru katika nuru zake sita. Imejionesha kwangu nuru hiyo kutokea mbali – kama ilivyo hali katika nukta ya kwanza – nami nikiwa mwenye kufikia jela ya (Eski Şehir) na kwa ajili ya kuiweka karibu na fahamu vilevile tutapita njia ya kupiga mifano. Basi tunasema: Huu ulimwengu ni kasri la ajabu linajumuisha mji mpana hufuatia sababu za kuharibu na kustawisha, na katika mji huu kuna ufalme mpana unaochemka mfululizo kutokana na ukali wa matukio ya vita na kuhama, kati ya pande za ufalme huo kuna ulimwengu mkubwa unaogelea kila zama katika kukusanya umauti na uhai, lakini licha ya matukio ya mkanganyiko, hakika mlinganisho wa jumla na mizani nyeti, na kazi madhubuti ya upimaji inatamalaki katika pande zote za kasri. Na pande za mji na kuenea katika maeneo yote ya ufalme na sehemu za ulimwengu, na inatamalaki, kwa namna ambayo kiasi cha kwamba inajulisha wazi juu ya: Kwamba katika mabadiliko yanayotokea ndani ya hivi vilivyomo visivyodhibitiwa na hesabu, na yanayoingia na yanayotoka haiyumkiniki kuwa isipokuwa kwa upimaji timamu, na mizani ya mwenye kuona pande za uwepo zote kwa wakati mmoja, na ambaye vyote vilivyomo vinakwenda chini ya jicho la usimamizi wake kila wakati, huyo ni yule mmoja wa pekee (s.w). Na kama sio hivyo ingekuwa sababu zinazoelekea kuvurugika kwa mizani ya sawa, ni huru au imeachiliwa kwa sadfa ya holela au nguvu pofu au asili ya giza zuzu, ingekuwa mayai ya samaki mmoja ambayo yanazidi maelfu yangevuruga mizani hiyo ya sawa, bali mbegu za ua moja – kama khash-khash (Mmea) - unaozidi ishirini elfu ungevuruga mizani hiyo ya sawa, achilia mbali kububujika kwa chembe zenye kutembea kama mto, na mabadiliko makubwa ambayo yanatokea pande za ulimwengu. Vyote hivyo kama vingekuwa huru ingekua nyenzo ya kuvuruga mizani madhubuti iliyowekwa kati ya vilivyomo, na kuharibu mizani kamili kati ya sehemu za viumbe ndani ya mwaka mmoja, bali ya siku moja. Na ungekuwa unauona ulimwengu fujo imeshika nafasi. Na ingekuwa katika hatari ya migongano na uharibifu. Basi bahari inajaa vilivyo kwisha na mizoga, na kuoza, na hewa inapata sumu kwa gesi inayodhuru na kuziba pumzi, na kuharibu. Na ardhi ingekuwa ni jalala na mahali pa kuchunia ngozi za wanyama, na ingekuwa ni kidimbwi kilichovunda maisha ndani yake hayawezekani. Ukitaka basi tazama kwa makini, vilivyo kuwamo vyote, kuanzia katika vipenyo vya mwili hadi katika seli nyekundu na nyeupe za damu, na kutoka katika mabadiliko ya Atomu mpaka katika kuwiana na kuchukuana kati ya zana za mwili, na kutoka katika bidhaa za bahari na sarifu zake na hadi katika bidhaa za maji ya Ardhini na sarifia zake, na kutoka katika kuzaana kwa wanyama na mimea na vifo vyake hadi katika uharibifu wa majira mapukutiko na ustawishaji wa majira ya machipuo, na kutokea katika kazi za chembe na nyendo za nyota hadi katika kubadilika kwa umauti na uhai, na katika kugongana kwa nuru na giza hadi katika kupingana kwa joto na baridi. Na yanayoshabihiana nayo, ili uone kwamba vyote: Vinapimwa na kukadiriwa kwa mizani nyeti kupita kiasi, na kwamba vyote vinapimwa kwa kipimo cha upeo wa unyeti, kwa namna ambayo akili ya mwanadamu inashindwa kuona israfu ya hakika mahali popote na mchezo katika sehemu yoyote, bali elimu ya mwanadamu inatambua na kushuhudia ukamilifu wa mpangilio na mzuri mno katika kila kitu na anajaribu kuuonesha, na anaona mizani ya sawa mno na ya ajabu katika kila kilichomo basi anajitahidi kuudhihirisha. Basi elimu ambazo mwanadamu amezifikia sio vingine isipokuwa ni tafsiri ya mpangilio huo wa ajabu na kuelezea mizani hiyo nzuri. Basi chunguza katika mizani nzuri kati ya jua na nyota za sayari kumi na mbili ambayo kila moja kati ya hizo ni tofauti na nyingine, je mizani hii haijulishi kwa namna ya wazi kama uwazi wa jua lenyewe juu ya Allah (s.w) naye ni (Al-Adlu Al-Qadiir)? Kisha ichunguze ardhi - nayo ni kati ya nyota – jahazi hili lenye kutembea na kuogelea angani ambalo linatembea mwaka mmoja kwa masafa yanakadiriwa urefu wake miaka ishirini na nne elfu. Na pamoja na kasi hii haiparaganyi maada yaliyomo juu yake wala haigongani navyo na wala haiviachii angani. Kingeongezwa kitu kidogo katika kasi yake au kupunguzwa katika kasi hiyo ingewatupa wakazi wake angani, lau mizani yake ingevurugika kwa dakika moja – bali sekunde moja – ingejikwaa katika kwenda kwake na kujigonga, na huenda ingegongana na sayari nyingine na kiama kingesimama. Kisha chunguza katika vizazi na vifo vya mimea na wanyama na kupewa kwao maisha na uhai wao juu ya Ardhi na ambazo sampuli zao zinazidi idadi yake zaidi ya sampuli elfu nne, unaona mizani nzuri yenye rehema, inakujulisha kwa kukinaisha kabisa kwamba Muumba mwadilifu Mwenye kurehemu (s.w), kama kujulisha kwa mwanga juu ya jua. Kisha chunguza viungo vya kiumbe hai ambavyo havihesabiwi wala kudhibitiwa hesabu yake, na chunguza katika zana zake na milango yake ya fahamu, humo utaona kuchukuana kikamilifu na kuwiana kikamilifu na mizani madhubuti ambayo inakujulisha wazi juu ya Mtengenezaji ambaye ni (Al-Adlu Al-Hakamu). Kisha chunguza katika vipenyo vya kiumbe hai na ndani ya vyombo vya damu, na katika seli zinazoogelea katika damu, na katika Atomu za seli hizo, utaona katika mizani ya ajabu kiasi kinacho kuthibitishia kwa kukinaisha kabisa kwamba mizani hii nzuri haipatikani na wala uendeshaji wake wa jumla, wala malezi yake yenye hekima zote isipokuwa kwa mizani nyeti na kwa kanuni yenye kutenda kazi na kwa mpangilio mkali wa Muumba Mmoja wa pekee (Al-Adlu Al-Hakiimu) ambaye mkononi mwake kuna utosi wa kila kitu, (Amedhibiti kila kitu) na kwake kuna funguo ya kila kitu, hakijifichi wala kumponyoka kitu chochote, na anaendesha kila kitu kwa wepesi sawa na kuendesha kitu kimoja. Hakika ambaye haitakidi kwamba amali za majini na watu siku ya mahshari kuu zinapimwa kwa mizani ya uadilifu wa kungu, na kushangaa hilo na kulikataa na wala haliamini, nasema angeweza kuchunguza katika ambalo ni dhahiri mambo yanayoonekana katika aina za mizani kubwa mbele yake ukanushaji wake lazima ungeondoka. Ewe mwanadamu mwenye kufanya fujo dhalimu mchafu! Jua, hakika (Uchumi twahara na Uadilifu) ni kanuni za kiungu zinafanya kazi ulimwenguni, na taratibu za kiungu za kiujumla gurudumu ya vilivyomo linazunguka katika kanuni hizo chochote hakitoki katika hilo isipokuwa wewe ewe mwovu, na wewe kwa kuhitilafiana kwako na vyote vilivyomo katika kwenda kwake kulingana na kanuni za jumla unapata chuki kutoka kwao na ghadhabu na wewe unaistahili. Basi unaegemea nini na kuamsha ghadhabu za vyote vilivyomo juu yako basi unavuna dhuluma na israfu na wala hujali mizani na usafi? Naam, hakika hekima ya jumla inayotamalaki kwenye ulimwengu na ambayo ni udhihirisho wa jina kuu (Al-Hakiimu) hakika inazunguka katika mhimili wa uchumi na kutofanya israfu, bali inaamrisha uchumi. Na hakika uadilifu wa jumla unaofanya kazi katika ulimwengu unaotokana na kudhihiri kukuu kwa jina (Al-Adlu) hakika unaendesha mizani ya vitu vyote, na unawaamuru wanadamu kusimamisha uadilifu. Na hakika ya kutajwa kwa mizani mara nne katika surat Ar-Rahmani ni ishara ya aina nne za mizani katika ngazi nne na kubainisha umuhimu wa mizani kwa mkazo na kwa thamani yake kubwa katika ulimwengu. Na hii ni katika kauli yake: وَالسَّمَاء رَفَعَهَا وَوَضَعَ الْمِيزَانَ ۞ أَلَّا تَطْغَوْا فِي الْمِيزَانِ ۞ وَأَقِيمُوا الْوَزْنَ بِالْقِسْطِ وَلَا تُخْسِرُوا الْمِيزَانَ Naam, kama ilivyokuwa hakuna israfu katika kitu, basi kadhalika hakuna dhulma ya hakika katika kitu, wala kupunja katika mizani katu, bali hakika ya kusafisha na usafi unaotokana na kudhihiri kukuu kwa jina (Al-Quddus) kunavihudhurisha vilivyomo katika sura yake dhahiri mno na pambo lake la ajabu, basi hakuonekani uchafu wowote katika uwepo, wala hauonekani ubaya wowote wa asili katika kitu chochote maadamu hakijaguswa na mkono mchafu wa wanadamu. Basi jua kutokana na hili kuwa (Uadilifu, uchumi na usafi) ambavyo hivyo ni katika hakika za Qur'an na taratibu za Uislamu, ni kiasi gani kuzama kwake mno katika vina vya maisha ya kijamii, na ni kiasi gani kuzidia kwa uasilia. Na najua kutokana na hili kiasi cha kufungamana sana kwa hukumu za Qur'an na ulimwengu, na namna gani kuwa zimenyoosha mashina ya kina katika mikondo ya ulimwengu ikazunguka kwa kamba imara isiyo katika. Kisha fahamu kutokana na hayo kwamba kuharibu hakika hizo ni jambo lisilokuwa kama isivyokuwa uharibifu wa mpango wa ulimwengu na kuvuruga na kuharibu sura yake. Na kama ambavyo hakika hizi zilizo zunguka ulimwengu zinavyo lazimu, na hizi nuru kuu tatu (Uadilifu, uchumi na usafi) Hashiri na Akhera, basi hakika zenye kuzunguka pamoja nazo: Kama rehema, utunzaji, uangalizi na mifano yake katika mamia ya hakika zenye kuzunguka na nuru kubwa zinalazimisha hashiri na kuhitajia maisha ya Akhera, na je inayumkinika kugeuka kwa mifano ya hakika hizi zenye kutamalaki kwa vilivyomo na zenye kuzungukia ulimwengu kuwa dhidi zake kwa kutokuja kwa ufufuo na kutokusimama kwa Akhera, yaani igeuke rehema na kuwa dhidi yake nayo ni dhulma, na kugeuka hekima au uchumi kuwa dhidi yake nayo ni mchezo na israfu, na usafi ubadilike na kuwa dhidi yake nayo ni mchezo na uharibifu. Hasha lillah.. Hakika ya rehema ya kiungu, na hekima ya kiulezi wa kiungu ambazo zinahifadhi hakika ya uhai wa mbu dhaifu uhifadhi unaotambulika kwa rehema kunjufu, haiyumkiniki kupotezwa - kwa kutokusimamisha ufufuo - haki za wote wenye utambuzi wasio kuwa na mipaka na kuzisaga haki zisizokuwa na ukomo kwa vilivyomo kwa hesabu isiyoweza kumalizwa. Na hakika ya adhama ya ulezi wa kiungu ambao unadhihirisha umadhubuti wa ukomo na unyeti wa hali ya juu – ikifaa ibara hii - katika rehema, uadilifu na hekima, na vivyo hivyo Uungu unaokunjua mamlaka yake katika uwepo wote na ambao unataka kudhihirisha ukamilifu wake na kutambulisha nafsi yake na kupendezesha viumbe kwa mapambo yake kwa maajabu ya utengenezaji wake na kwa neema alizowaenezea Je, inayumkinika kuruhusu - Ulezi huu mkuu na Uungu mtukufu - kwa kutosimamisha ufufuo jambo ambalo linasababisha kuangusha thamani ya makamilifu yake na thamani ya viumbe wake kwa ujumla?. Ameepukana Allah na hilo kuepuka kukubwa. Basi mfano wa uzuri huu wa hali zote hauridhii – kiakili - mfano wa ubaya huu wa hali zote. Basi anayetaka kukanusha Akhera ni juu yake kukanusha uwepo wa ulimwengu huu kwanza kwa hakika zake zote zilizomo ndani yake. Na kama sio hivyo basi viumbe na hakika zao zilizojikita ndani yake vinamkadhibisha kwa maelfu ya ndimi, vinamthibitishia kuwa yeye ndiye muongo mkuu. Hakika imethibitisha (Risala ya Ufufuo) kwa dalili za kukinaisha: Kwamba kuwepo kwa Akhera ni thabiti na kwenye kukinaisha hakuna shaka ndani yake kama kuwepo kwa hii dunia. Inaashiria nuru ya tatu katika nuru sita za Al-Ismi Al-A’dham.

§2

Al-Hakamu ادْعُ إِلِى سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ Hakika imejionesha kwangu nukta moja katika nukta nyeti za aya hii tukufu, na nuru katika nuru za midhihirisho ya jina la Allah (Al-Hakamu) ambalo ni jina la Allah Al-A’adham, au moja ya nuru zake ndani ya mwezi wa Ramadhani Al-Mubarak. Basi zikaandikwa nukta hizi ambazo zinakusanya nukta tano kwa haraka, na kuzithibitisha katika hali yake katika muswada bila uhariri wala kugeuza.

§3

Kama tulivyotaja katika (Neno la kumi) hakika kudhihiri kukuu kwa jina la (Al-Hakamu) kumefanya ulimwengu huu sawa na kitabu kikubwa kimeandikwa mamia ya vitabu katika kila ukurasa miongoni mwa kurasa zake, na imechorwa katika kila neno lake mamia ya misitari, na yanasomwa chini ya kila herufi ndani yake mamia ya maneno, na imehifadhiwa katika kila nukta miongoni mwa nukta zake faharisi muhtasari ndogo inafupisha yaliyomo ndani ya kitabu kizima. Basi kitabu hiki pamoja na kurasa zake na misitari yake bali pamoja na nukta zake kinajulisha kwa namna ya wazi yenye kuangaza – kwa mamia ya namna - juu ya Mwenye kukipa sura na mwandishi wake, hata hakika kushuhudia kitabu hiki kikuu cha kiulimwengu hili peke yake linatosha kujulisha juu ya kuwepo kwa mwandishi wake, bali kunatupeleka katika kutambua uwepo wake na umoja wake kiasi kilicho zaidi ya kitabu kujijulisha chenyewe maradufu ya maradufu. Kwani ambapo herufi moja inajulisha juu ya kuwepo kwake na kuelezea nafsi yake kwa kiasi cha herufi moja hakika herufi hiyo inaelezea sifa za mwandishi wake kwa kiwango cha msitari. Naam, hakika uso wa Ardhi ni (Ukurasa) katika kitabu hiki kikubwa, ukurasa huu unajumuisha vitabu kwa idadi ya jamii za mimea na wanyama, na vinaandikwa mbele ya macho yetu katika majira ya machipuo katika upeo wa ukamilifu na ufundi bila kosa, maandishi yenye kuingiliana, bega kwa bega, wakati mmoja. Na bustani (Ni mstari) katika ukurasa huu, tunashuhudia ndani yake kasida zilizotungwa na hali zikiandikwa mbele ya macho yetu kwa idadi ya maua na miti na mimea, maandishi yenye kuingiliana, bega kwa bega, bila ya kosa. Na mti wenye kumea wenye kustawi majani yake, wenye kufunguka maua yake na umekaribia kuzaa matunda yake kutoka katika vikonyo vyake, mti huu ni (Neno) katika mstari ule, basi neno hili linashika nafasi ya paragrafu kamili yenye maana inaelezea kwa namna ya fasaha juu ya sifa zake na himidi zake na kujulisha kwake kuhusu (Al-Hakamu) Mwenye uzuri, kwa idadi ya majani yake yaliyopangika na matunda yake yaliyowekwa kwa mizani, hata kana kwamba huo mti uliofunguka maua ni kasida safi inaimba madihi na sifa juu ya neema za Muumba wake mtia sura Mtukufu. Na kana kwamba (Al-Hakiimu) Mwenye utukufu anataka kuwaonesha waja wake yale aliyoyahudhurisha katika maajabu ya athari zake na maajabu ya viumbe vyake katika maonesho ya Ardhi ya ajabu kwa maelfu ya macho. Na kana kwamba hizo zawadi za thamani na nishani ghali na nembo nyororo ambazo Allah (s.w) ameutunuku ule mti ameupa katika umbo zuri lililopambwa, na hali iliyowekwa kwa mizani iliyopambika, na ubainishaji wa hekima fasaha kiasi cha kuutayarisha kwa ajili ya kuoneshwa mbele ya mtazamo wa mfalme mkuu katika siku ya sikukuu yenye furaha na kuuonesha kwa jumla kwa viumbe. Katika majira ya machipuo yenye kustawi, basi inakwenda na kushuhudia juu ya kuwepo kwa Muumba mtia sura, na kujulisha majina yake mazuri ndimi nyingi na nyuso nyingi zenye kuingiliana; kutoka katika kila ua miongoni mwa maua ya mti, na kutoka katika kila tunda miongoni mwa matunda yake. Basi mathalani: Hakika kila kilichomo katika ua na tunda kimewekwa kwa mizani madhubuti, na mizani hiyo imekadiriwa kulingana na kuchukuana kwa ajabu, na huko kuchukuana kunawiana pamoja na mpangilio na kulingana mizani kunakofanyika upya, Na mpangilio huo na uwiano wa mizani vinapita katikati ya mapambo ya kifahari na ufundi uliotendwa vema, na hayo mapambo na utendaji vema vinadhihiri kwa harufu zenye maana na kwa vionjo vyenye hekima. Na kama hivi linaashiria kila ua kwa Al-Hakamu Mwenye utukufu kwa ishara na kujulisha juu yake kwa dalili, kwa idadi ya maua ya mti huo. Na mti ambao ni sawa na neno, na matunda yake ambayo ni kwa nafasi ya herufi ya neno hilo, na mbegu za matunda kana kwamba ni nukta za hizo herufi ambazo zinajumuisha faharisi ya mti kamili na inabeba mpango wa kazi zake. Huu mti tukiuchukua kuwa ni mfano na tukaupimia kitabu cha ulimwengu kikubwa, tunaona misitari yake na kurasa zake zimegeuka kuwa kwa kudhihiri kwa jina la (Al-Hakiimu Al-Hakamu) ni muujiza dhahiri, bali kila ukurasa, kila mstari, kila neno, kila herufi na kila nukta yake ni muujiza unaofikia katika ukuu kiasi ambacho zingekusanyika sababu za kimaada zote ili ziulete mfano wa nukta hiyo - yaani mbegu - au mfano wake zisingeleta mfano wake. Bali sababu zote zinashindwa kushindwa kwa hali zote kuipinga nukta hiyo. Naam, hakika kila aya ya kiulimwengu katika aya za Qur'an kuu ya Ulimwengu yenye kuonekana inaonesha kwa ajili ya kuonekana miujiza yenye nuru kwa idadi ya nukta zake na herufi zake, basi hakuna shaka kwamba sadfa holela na nguvu pofu, na asili kiziwi zuzu ambayo haina lengo wala mizani, haiwezekani kuingilia – katika upande wowote uwao - katika mizani hii maalumu iliyoundwa vyema, na katika huu mpangilio madhubuti wa ajabu wenye kujulikana (viwili hivi) kwa hekima na busara. Lau ingekadiriwa kuingilia kwake - kwa ajili ya mjadala – ingeonekana athari ya kuingilia, wakati ambapo haishuhudiwi mahali popote tofauti yoyote wala ufa wowote katu.

§4

Nayo ni masuala mawili:

§5

Kama ilivyowekwa wazi katika (Neno la kumi) kwamba ni katika kanuni za msingi zilizo imara: Kwamba uzuri ambao umo katika upeo wa ukamilifu hapana budi ushuhudie na ushuhudishe uzuri wake. Na kwamba ukamilifu ambao uko katika ukomo wa uzuri hapana budi ushuhudiwe na ushuhudishe ukamilifu wake. Basi kwa msingi wa kanuni hii ya jumla hakika Muumba mwenye kutia sura (s.w) ambaye ameumba kwa ajabu hiki kitabu cha ulimwengu kikubwa anatambulisha uzuri wa ukamilifu wake na anaupendezesha kwa ndimi za viumbe wake – kuanzia kwa sehemu mdogo mno hadi katika jumla kubwa kabisa – basi (s.w) anajitambulisha dhati yake takatifu, na anafahamisha ukamilifu wake wa hadhi ya juu, na anadhihirisha uzuri wake wa ajabu, kwa kila ukurasa ndani yake na kwa kila mstari ndani yake, na kwa kila neno ndani yake, bali hata kwa kila herufi na kwa kila nukta ya kitabu chake hiki kikubwa. Basi ewe mwenye kughafilika! Hakika ya huyu (Al-Hakiimu Al-Hakamu Al-Haakimu) Mwenye utukufu na uzuri ambapo anaitambulisha nafsi yake kwako na kuipendezesha kwako kwa kila kiumbe katika viumbe vyake, na kwa sura hii ya kupendeza na kwa wingi huu wenye kukithiri miongoni mwa nyenzo za ajabu, ikiwa hukubadilishana na utambulisho wake huu kwa imani na hukumjua, na kama hukubadilishana na kupendezesha kwake huku kwa kumwabudu na ikiwa hukujipendekeza nafsi yako kwake, basi ukubwa ulioje wa ujinga wako, na hasara yako ni kubwa kiasi gani! Tahadhari! Tahadhari! na amka kutoka katika kughafilika kwako.

§6

Hakika katu hakuna nafasi ya ushirikina katika ulimwengu huu mpana mkubwa ambao ameuunda Fundi Mweza Mwingi wa hekima kwa uweza wake na hekima yake; kwani kuwepo ukomo wa mpangilio katika kila kitu hakutoruhusu ushirikina abadani, ingeingilia mikono mingi katika kuumba kitu fulani ingebainika tofauti na hitilafu katika kitu hicho, mfano wa mambo yanavyochanganyika iwapo wamepatikana wafalme wawili katika mji, Mas’uli wawili katika mji, na watawala wawili katika mji, na kama anavyo kataa mfanya kazi wa kawaida sana kuingilia yeyote kwenye jambo kati ya mambo yake ambayo yanahusu kazi yake. Yote hayo hakika sifa mahususi ya msingi ya kutawala hakika ni: (Uhuru) na (Kuwa pekee) basi mpangilio unahitajia umoja na kama utawala unahitajia upekee, ikiwa kivuli fifi chenye kutoweka cha utawala mbele ya huyu mwanadamu asiyejiweza fakiri unakataa kwa nguvu kuingiliwa, basi vipi utawala wa hakika ambao uko katika daraja ya ulezi wa hali zote mbele ya Mweza wa hali zote (s.w)? Je haukatai ushirikina kabisa? Ingekadiriwa kuingilia – japo kwa kiasi cha Atomu – mpangilio ungechanganyika na uratibu, na mpangilio ungevurugika na mizani!. Pamoja na kujua kwamba huu ulimwengu umeundwa kwa namna ya ajabu ya kupendeza kwa kiasi ambacho inalazimu kuumba mbegu moja uweza wenye uweza wa kuumba mti kamili, na inalazimu kwa kuumba mti mmoja uweza wa wenye kuweza kuunda ulimwengu wote. Na ikikadiriwa kuwepo kwa mshirika katika ulimwengu wote inapasa kudhihiri hisa yake katika kuingilia kwa kuumba mbegu ndogo kabisa mathalani – kwani mbegu ni kielelezo cha viumbe – na wakati huo itapasa kutulia ulezi miwili - hautoshi ulimwengu mkubwa - katika mbegu ndogo, bali katika Atomu! Na hii ni katika mihali mibaya sana na taswira za fikira batili na iko mbali mno na mantiki na akili. Basi jua kutokana na hili, uduni ulioje wa shirki na ukafiri katika uzushi! Uwongo ulioje wa neno! na ubaya ulioje wa kuzua mambo hayo mawili! Kwani yanahitajia kushindwa kwa Mweza wa hali zote ambaye anashikilia mbingu na Ardhi zisiondoke, na ambaye mikononi mwake kuna sukani za mbingu na Ardhi anaziendesha kwa mizani ya uadilifu wake na mpangilio wa hekima yake. Vinahitajia kushindwa kwake (s.w) hata katika mbegu ndogo! Na jua! Kusibu mno kwa Tawhidi katika haki na hakika! Na uadilifu wake ulioje katika ukweli na kusibu! Tambua hili na lile na useme: Alhamdulillahi kwa ajili ya Imani.

§7

Hakika mtengenezaji mweza kwa jina lake la (Al-Hakamu na Al-Hakiimu) ameingiza katika ulimwengu huu maelfu ya limwengu zilizopangika za ajabu, na akampa makao mwanadamu – ambaye ndiye mwingi zaidi anayewakilisha hekima zilizokusudiwa ulimwenguni na mbora zaidi anayezidhihirisha - mahali pa utangulizi, na amemfanya kuwa ni kati kati ya limwengu hizo na ni mhimili wake; ambapo anatazamia hekima zilizopo na masilahi kwa mwanadamu. Na ameifanya riziki ni sawa na kituo katika duara la uhai wa mwanadamu; basi unakuta kwamba sehemu kubwa ya hekima na shabaha na ghalibu ya maslahi na faida - ndani ya ulimwengu wa mwanadamu – na kuwa wazi kwa kupitia yeye; kwa hio hakika midhihirisho ya jina la (Al-Hakiimu) inaonekana wazi kwa sura zake dhahiri mno na zenye kung’ara zaidi kupitia hisia za mwanadamu, na katika kukithiri kwa vionjo vya riziki, hata imekuwa kila elimu moja - katika mamia ya elimu ambazo zinamwafikisha mwanadamu kuvumbua kwake hisia alizonazo –inajulisha udhihiri mmoja katika midhihirisho ya jina la (Al-Hakamuu) katika sampuli miongoni mwa sampuli. Basi mathalani: Ingeulizwa elimu ya tiba: Nini viumbe hivi? Ingejibu: Hakika hivyo ni famasia kubwa imeandaliwa kwa ufundi dawa zote na kuwekezwa. Na ikiulizwa elimu ya kemia: Nini hili tufe la Ardhi? Ingejibu: Kwamba ni maabara ya kikemia iliyopangika ya ajabu iliyo kamilika. Wakati ambapo elimu ya Mashine inajibu: Kwamba ni kiwanda kilichopangika kamili hauonekani upungufu ndani yake. Kama inavyojibu elimu ya kilimo: Kwamba ni bustani lenye kuimba na ni tunu ya shamba, humo kunaoteshwa aina za mazao, kila moja katika nyakati zake. Na elimu ya biashara ingejibu: Kwamba ni maonesho makubwa ya bishara, na kutangazwa katika upeo wa uzuri na mpangilio, na ni duka la biashara linakusanya bidhaa zenye thamani mno zilizotengenezwa na bora. Na elimu ya hifadhi ya uhai: Kwamba ni ghala kubwa linakusanya riziki zote kwa aina zake mbali mbali. Na ingejibu elimu ya lishe: Hakika ni jiko la kiungu humo hupikwa mamia ya maelfu katika vyakula vitamu vyenye ladha njema bega kwa bega kwa mpangilio katika upeo wa ufundi na ukamili. Lau elimu ya uaskari ingeulizwa kuhusu Ardhi!. Ingejibu: Kwamba ni kambi kubwa hupelekwa humo katika kila majira ya machipuo askari wenye kupewa silaha wapya wanaunda jamii tofauti za mimea na wanyama hesabu yake inafikia zaidi jamii mia nne elfu, basi mahema yao husimikwa pande za uso wa Ardhi. Na licha ya kuwa riziki za kila jamii inatofautiana na nyingine, na mavazi yao ni tofauti na silaha zao ni mbali mbali, na mafunzo yao yanahitilafiana, na ruhusa zao ni tofauti, isipokuwa mambo ya wote yanakwenda kwa mpangilio mzuri, na mahitaji ya wote yanatayarishwa bila ya kusahau wala kuchanganya, na hiyo ni kwa amri kutoka kwa Allah (s.w) na kwa fadhili ya rehema zake zenye kuenea zikitokea kwenye hazina yake kunjufu. Na ikiulizwa elimu ya umeme: Ingejibu: Kwamba dari ya kasri la huu ulimwengu imepambwa kwa taa zenye kumetameta hakuna mpaka wa wingi wake wala hakuna ukomo wa uzuri wake na kuratibika kwake, hata hakika ya mpangilio wa ajabu na kuratibika kuzuri vinazuia kulipuka kwa taa hizo za mbinguni zenye kuwaka daima - nazo zinaizidi Ardhi kwa ukubwa kwa mara elfu moja na mbele yake ni jua - na bila ya kupungua mizani yake au kuzuka kwa moto kati yake. Je, ni kutokea chanzo kipi kinazalisha taa hizo zisizokuwa na mpaka na matumizi yake hayaishi?. Na kwa nini haivurugiki mizani ya kuwaka? Hali ya kujua kwamba taa ndogo ya mafuta ikiwa haikuchungwa na kutiliwa umuhimu kwa mfululizo mwanga wake unazimika na kupotea. Basi utakatifu ni wake subhana Aliye Mweza wa kila kitu Mwingi wa hekima Mwenye utukufu vipi aliliwasha jua ambalo ni kubwa kuliko Ardhi kwa mara milioni na umepita katika umri wake zaidi ya miaka milioni - kwa mujibu wa yaliyofikiwa na elimu ya Falaki - bila ya kuzimika na bila ya hatabu wala mafuta. Chunguza hili na utakase jina la Mola wako Mtukufu na useme: “ ماشاءالله، تبارك الله، لا إله إلاّ الله ” yaseme hayo kwa idadi ya sekunde zilizopita katika umri wa jua. Basi hapana shaka kwamba mpangilio wa ajabu mkali ndio ambao unatamalaki juu ya taa hizi za mbinguni zenye kumeremeta na hapana budi hakika uchungaji na usimamizi wake ni madhubuti, hata kana kwamba chanzo cha joto - na jiko la gesi - la maumbo hayo ya moto ambayo yako katika ukomo wa ukubwa na katika upeo wa wingi, hakika ni jahanamu joto lake halimaliziki na inalipeleka kwa wote likiwa na giza totoro bila ya mwanga. Na kana kwamba mashine za taa hizo zenye nuru na kandili zenye mwanga ambazo hazihesabiki wala kudhibitiwa idadi yake ni pepo ya kudumu inaipelekea nuru na mwanga basi unaendelea kuwaka kwake kwa kudhihiri utukufu kwa jina la (Al-Hakamu na Al-Hakiimu). Na kama hivi kwa kupimia mifano hii, basi hakika kila elimu katika mamia ya elimu inashuhudia kwa kukinaisha: Kwamba ulimwengu huu umepambwa kwa hekima na masilahi mbali mbali ndani ya mpangilio kamili usio na kasoro ndani yake, na kwamba mifumo hiyo ya ajabu na hekima za hadhi ya juu inayotokana katika hiyo hekima ya muujiza yenye kuzunguka ulimwengu imewekwa kwa kipimo kidogo mno, hata katika kiumbe mdogo sana na katika mbegu ndogo sana. Na katika yanayojulikana wazi hakika ya kufuatilia shabaha na kuangalia hekima na faida kwa mpangilio hakupatikani isipokuwa kwa kutaka, hiari kukusudia na majaaliwa, kama si hivyo hapana. Na kama ilivyo hii kazi ya ajabu sio katika jambo la sababu na Asili - ambazo mbili hizo hazimiliki kutaka wala hiari wala kusudio wala hisia - haiwi kwa viwili hivi kuingilia katika jambo hilo vilevile, kwa hiyo ni jambo gani limewatia ujinga wasiojua wala kuamini kwa Mtendaji Mwenye kuchagua na Mtengenezaji Mwingi wa hekima ambayo inajulisha juu yake mifumo hii ya ajabu na hekima za juu zisizo na mpaka nazo zimezagaa katika vilivyomo ulimwenguni kote kwa jumla. Naam, ikiwa kuna kitu cha kukishangaa na kinaamsha ajabu kwa watu katika dunia hii hakika ni: Ni kukanusha kuwepo kwake (s.w); kwa sababu mpangilio kwa aina zake za ajabu ambazo hazihesabiki na hekima kwa namna zake za hadhi ya juu ambazo hazidhibitiki na zilizoingia katika kila kilichomo kwenye ulimwengu ni mashahidi wa kweli juu ya kupasa kuwepo kwake (s.w) na juu ya umoja wake. Basi utokomee mbali upofu ambao hakuna baada yake upofu! Na uende mbali ujinga hapana baada yake ujinga kwa asiyemuona huyu Bwana Mlezi Mwingi wa hekima (s.w)! Hata inayumkinika mimi kusema: Hakika watu wa safsata ambao wanahesabiwa kuwa ni wapumbavu kwa kukanusha kwao kuwepo kwa ulimwengu, wao ni wenye akili zaidi ya watu wa Ukafiri; kwa sababu kuitakidi kuwepo kwa ulimwengu na baada yake kukanusha Muumba wake – naye ni Allah (s.w) - haliyumkiniki kabisa, na halikubaliki asilani, kwa hiyo walianza kwa kukanusha ulimwengu na wakakanusha kuwepo kwao wao vilevile, na wamesema: Hakuna kitu kipo kabisa, wakazibatilisha akili zao, na wamejiokoa kwa kukaribia kwao kidogo katika akili kuliko upotevu wa upumbavu usio na kikomo kwa wakanushaji wakinzani wapumbavu wenye kujificha kwa pazia ya akili!

§8

Kama ninavyoashiria katika (Neno la kumi) kwamba: Ikiwa atasimika fundi mzuri wa ujenzi Mwingi wa hekima kasri refu, na akaweka katika kila jiwe miongoni mwa mawe yake mamia ya hekima na maslahi na faida, basi mwenye utambuzi hapati picha kwamba hataijengea dari kwa kuihifadhi kutokana na kuoza na kuharibika; kwa sababu hili ni kuliacha jengo katika hatari ya kutokuwepo, kuharibika na kupotea kwa faida hizo na hekima ambazo alikuwa anazichunga na kuzitawalia, na hili ni jambo ambalo mwenye utambuzi haliridhii. Au hakika Mwingi wa hekima kwa hali zote anaanzisha kutoka katika dirhamu ya mbegu mamia ya tani ya faida na hekima na shabaha, na anafuatilia na kuyaongoza, haiyumkiniki kutasawari yule ambaye anayo akili kutokea mchezo na israfu vitu viwili vyenye kupingana jumla na hekima ya hali zote kutoka kwa huyo mwingi wa hekima wa hali zote basi akauvika mti mkubwa faida ya kijisehemu, na lengo duni na matunda machache, hali akijua kuwa anagharamia kuanzisha kwake na kuweka matunda yake mengi!. Naam, basi kama ilivyo haiyumkiniki kutasawari hili kwa ambaye ana gao la akili, kutokea kwa Mtengenezaji Mwingi wa hekima mchezo na israfu kwa kutoileta Akhera na kutosimamisha kwake ufufuo na kiama baada ya kuvika kila kilichomo katika kasri la Ulimwengu hili mamia ya hekima na maslahi na kukiandaa kwa mamia ya kazi – hata kwamba ameuvika kila mti hekima kwa idadi ya matunda yake na majukumu kwa idadi ya maua yake – wala haiyumkiniki kupita katika fahamu ya mwenye akili huyu mwingi wa hekima Mtukufu kupoteza hekima zote hizi na makusudio na majukumu yote haya kwa kutokusimamisha kwake kiama na Akhera. Kwani hili linamaanisha kuegemeza kushindwa kabisa kwa uweza wa Mweza Mwenye uweza wa hali zote, na kunasibisha mchezo na upotevu kwa hekima kuu ya Mwingi wa hekima wa hali zote, na kurejesha ubaya wa hali zote kwa uzuri wa rehema ya Mwenye kurehemu wa hali zote, na kuegemeza dhulma ya hali zote kwa uadilifu uliotimia wa Mwadilifu wa hali zote, yaani kukanusha vyote ikiwemo hekima na rehema na uadilifu vyenye kudhihiri vyenye kushuhudiwa, na kuvikanusha hivyo kwa jumla katika uwepo! Na hili ni katika ajabu ya muhali na iliyo mbaya zaidi na batili zaidi!. Basi watu wa upotevu, waje na watazame upotevu wao vipi ambavyo ni wenye giza, umejaa nge na nyoka kama makaburi yao ambayo watakayofikia! Na watambue kwamba njia ya imani na Akhera ni yenye kumulikwa nuru nzuri kama pepo basi na waipite na waneemeshwe kwa Imani.

§9

Nayo ni masuala mawili:

§10

Hakika ya kufuatilia kwa Mtengenezaji Mtukufu - jina la (Al-Hakiimu) kwa sura nyororo katika kila kitu na njia fupi mno na namna bora mno, na umbo lenye manufaa zaidi, inajulisha kwa namna ya wazi hakika maumbile hakuna israfu ndani yake katu wala mchezo. Na hakuna kitu isipokuwa ndani yake kuna manufaa, na hakika israfu kama inavyopingana na jina la (Al-Hakiimu) basi uchumi ni jambo lake lenye kuilazimu na kulihitajia na kanuni yake ya msingi. Basi ewe mwenye kufanya israfu mbadhirifu: Jua kiasi cha kuepuka kwako hakika kwa kujibweteka kwako kunako njia ya kanuni kubwa mno ya ulimwengu iliyojengwa juu ya uchumi. Na kuzingatia aya tukufu: وكُلُواْ وَاشْرَبُواْ وَلاَ تُسْرِفُواْ ujue kiasi cha kujikita kwa kanuni kunjufu yenye kuenea inayoielekeza.

§11

Inasihi kusemwa: Hakika jina la Allah (Al-Hakamu na Al-Hakiimu) yanahitajia kwa dhahiri unabii wa Muhammad (s.a.w) na ujumbe wake, na yanajulisha hivyo na kulazimisha. Naam, Maadam kitabu fasaha kwa maana yake na makusudio yake, kinahitajia kwa lazima mwalimu mwema ili kukifundisha. Na uzuri wa hali ya juu unahitajia kioo ili uonekane katika kioo hicho, na uonekane uzuri wake kwa kioo hicho. Na ufundi wa ajabu unahitajia mpiga mnada mwenye kulingania hilo. Basi hapana budi kuwepo kati ya wana wa Adamu ambaye ndiye mwelekezewa mazungumzo ya kitabu cha ulimwengu mkubwa wenye kubeba mamia ya maana ya fasaha na hekima madhubuti katika kila herufi miongoni mwa herufi zake, nasema: Hapana budi kuwepo kiongozi mkamilifu, mwalimu mkubwa, ili awaongoze watu katika yaliyomo ndani ya kitabu hicho kikubwa katika hekima takatifu za hakika, na afundishe uwepo wa hekima zilizozagazwa katika pande zake na kujulisha juu yake. Na awe chanzo cha kudhihiri kwa makusudio ya kiulezi wa kiungu katika kuumba ulimwengu, bali ni sababu ya kupatikana kwake. Na ili aelekeze yale anayoyataka Muumbaji kuyadhihirisha katika ukamilifu wa ufundi wake wa ajabu, na uzuri wa majina yake mazuri, basi anakuwa kioo safi cha ukamilifu huo wa ajabu na uzuri wa hali ya juu, na ili asimame kwa ajili ya uja mkunjufu - kwa ajili ya viumbe kwa ujumla - mbele ya matukio ya kiulezi wa kiungu mkunjufu, hali ya kuamsha shauku na kueneza roho ya ndani katika maeneo bara na baharini hali ya kugeuza macho ya wote kwa Mtengenezaji Mtukufu kwa kulingania na dua, kwa tahalila, tasbihi na takdisi, inatoa sauti pande za mbingu na Ardhi, na ili igonge masikio ya wenye akili wote kwa masomo anayofundisha yenye utakatifu wa hadhi ya juu na maelekezo yenye hekima kutoka katika Qur'an yenye hekima. Na ili abainishe kwa sura nzuri mno na tukufu mno kwa Qur'an tukufu makusudio ya kiungu ya huyo Mtengenezaji Al-Hakamu Al-Hakiimu, na ili apokee kwa mapokezi makamilifu zaidi na yaliyotimia matukio ya hekima kubwa na uzuri na utukufu wenye kudhihiri katika pande mbali mbali. Basi mtu ambaye hili ni jukumu lake, ni mwanadamu ambaye kuwepo kwake ni muhimu, bali ulimwengu unalazimisha ulimwengu huu, kama dharura ya jua na ulazima wake kwa ulimwengu. Basi ambaye anatekeleza majukumu haya, na anatimiza kazi hizi katika sura yake timamu sio isipokuwa Mjumbe Mtukufu (s.a.w) kama inavyoshuhudiwa; kwa hiyo kama jua linavyolazimu mwanga, na mwanga kulazimu mchana, basi hekima zilizotawanywa katika maeneo na pande za ulimwengu zinalazimu unabii wa Muhammad (s.a.w) na utume wake. Naam, kama inavyohitajia udhihiri mkuu wa jina la (Al-Hakamu Al-Hakiimu) - katika ukunjufu wa kiasi chake - ujumbe wa Muhammad, hakika aghlabu ya majina mazuri (Allah, Ar-Rahman, Ar-Rahim, Al-Wadud, Al-Mun’im, Al-Karim, Al-Jamiil, Ar-Rabb) na mifano yake, yanalazimu utume wa Muhammad katika ukuu wa udhihiri wake na kuzunguka kwake ulimwengu wote, ulazima wa kukinaisha bila shaka yoyote. Mathalan: Hakika rehema kunjufu ambayo ni udhihiri wa jina la (Ar-Rahiim) inadhihiri kwa uwazi kwa yule ambaye ni rehema kwa walimwengu, na hakika ya kujipendezesha kwa kiungu, na kujitambulisha kwa Bwana Mlezi – ambako ni katika midhihirisho ya jina la (Al-Wadudi) - yanaangazia katika matokeo yake na yanakuta mkabala kwa kipenzi cha Bwana Mlezi wa walimwengu, hakika aina zote za uzuri: Kutokea kwenye uzuri wa dhati hadi kwenye uzuri wa majina, na uzuri wa ufundi na kutengeneza vyema, na uzuri wa vilivyotengenezwa na vilivyoumbwa, kila sampuli za uzuri - ambazo ni udhihiri miongoni mwa midhihirisho ya jina la Al-Jamiil - inashuhudiwa katika kioo hicho cha Muhammad, na kushuhudishwa kwacho, bali hata midhihirisho ya adhama ya ulezi wa kiungu, na kutamalaki kwa mamlaka ya kiungu hakika hujulikana kwa ujumbe wa mlinganiaji huyu mkuu kwa Mfalme wa ulezi wa kiungu na kubainika kwake, kufahamika, kuchukuliwa na kusadikiwa kwake, na kama hivi basi aghalabu ya majina mazuri hakika ni hoja ya dhahiri juu ya utume wa Muhammad kama ilivyopita huko nyuma. Kwa ufupi: Ni kwamba maadamu ulimwengu upo kiuhalisia na haiyumkiniki kuukanusha, vivyo hivyo haiyumkiniki kukanusha ambayo ni sawa na rangi na mapambo yake, na mwanga wake na ufundi wake, na sampuli za maisha yake, na mitindo ya mafungamano yake katika hakika zenye kushuhudiwa, kama hekima, usimamizi, rehema, uzuri, mpangilio, mizani, mapambo na mfano wa hayo katika mambo ya hakika, maadamu haiyumkiniki kukanusha sifa hizi na matendo, haiwezekani kukanusha wenye kusifiwa na sifa hizo, na haiyumkiniki kukanusha Mtendaji wa matendo hayo na nuru ya jua kwa mianga hiyo, nakusudia dhati ya Allah takatifu (s.w) ambaye ni wajibu kuwepo, ambaye ni (Al-Hakiimu, Al-Rahiim, Al-Jamiil, Al-Hakamu, Al-Adlu). Na kadhalika haiyumkiniki kukanusha ambaye ana mahali panapo zunguka kudhihiri kwa sifa na matendo hayo, bali ambaye ndiyo eneo la kuonesha makamilifu yake, bali kuthibiti kwa midhihirisho yake, huyo ni Mjumbe Mkarimu Muhammad (s.a.w), Kiongozi mkubwa, na Mwalimu mkamilifu, na Mlinganiaji mkuu, na mfumbuzi fumbo la viumbe, na kioo cha Swamadaniyya (Kiungu, mkusudiwa kwa haja zote) na kipenzi cha Al-Rahman. Basi haiyumkiniki kukanusha utume wake kabisa, kwa sababu ni nuru angavu mno katika ulimwengu huu kama kuangaza kwa mwanga wa ulimwengu wa hakika na nuru ya hakika ya viumbe. عَلَي۟هِ وَعَلٰى اٰلِهٖ وَ صَح۟بِهِ الصَّلَاةُ وَالسَّلَامُ بِعَدَدِ عَاشِرَاتِ ال۟اَيَّامِ وَذَرَّاتِ ال۟اَنَامِ سُب۟حَانَكَ لَا عِل۟مَ لَنَٓا اِلَّا مَا عَلَّم۟تَنَٓا اِنَّكَ اَن۟تَ ال۟عَلٖيمُ ال۟حَكٖيمُ

Private reading note

This note stays on this device and is never uploaded to a server.

Up to 1,200 characters