Watu wengi wataingia katika dini ya kweli baada ya Issa (a.s) kumuua Dajjali zama za mwisho, wakati imekuja katika mapokeo mengine: “Hakitasimama kiama mpaka pasisemwe ardhini: Allah... Allah...” Vipi watu wadondoke kwa wingi huu katika ukafiri baada ya kuingia kwa wingi kwenye Imani? Jibu: Kuwa wenye udhaifu wa Imani wanakanusha kilichokuja katika Hadithi sahihi kuhusu kushuka kwa Isa (a.s) na kumuua Dajjali na kuifanyia kazi sharia ya Kiislamu. Lakini kama ukweli wa mapokeo ukibainika haitabaki nafasi ya kukanusha kamwe. Na hiyo: Hakika maana ambayo Hadithi hiyo inajulisha na mapokeo yanayosimulia kuhusu Mahdi na Sufyani ni kama ifuatavyo: Kwamba makundi mawili ya wakana Mungu yatapata nguvu katika zama za mwisho: Kwanza: Mtu wa kutisha aitwaye “Sufyani” atakana utume wa Muhammad akijificha kwa unafiki, na kushika hatamu ya wanafiki, na atafanya juhudi kuangamiza sharia ya Kiislamu, na atakutana na mtu wa kinuru kutoka katika jamaa wa nyumba ya Mtume anayeitwa Muhammad Mahdi atashika hatamu ya watu wa uwalii na watu wa ukamilifu waliyofungamana na kizazi cha kinuru cha jamaa wa nyumba ya Mtume, na atawaua kundi la unafiki ambalo linamwakilisha Sufyani wa kimaana na kuliangamiza kabisa. Ama Kundi la Pili: Ni kundi lililovuka mpaka katika uasi, lililotokana na falsafa ya Wana-asili na Wana-maada, kundi hili litasambaa na kupata nguvu hatua kwa hatua kupitia falsafa ya kimaada katika zama za mwishoni mpaka itafikia kuukana Uungu. Watu wa kundi hili wenye kumkana Allah (s.w) watazipa nafsi zao aina ya uungu wa bwana mlezi kana kwamba ni Manamrudi wadogo, kama vile Mjinga asiyemtambua Mfalme wala jeshi na askari wake anavyompa kila askari aina ya utawala na uongozi. Ama Dajjali ambaye ni kiongozi anayewatawala atapewa mambo ya ajabu yanayofanana na matendo ya kichawi na kiini macho, na anazama sana mpaka anaongeza kwenye serikali yake yenye nguvu kidhahiri aina ya uungu wa Mola Mlezi, na kutangaza uungu wake. Na hapana shaka kuwa madai ya uungu kwa mwanadamu mwenye kushindwa, ambaye anashindwa kuumba nzi na hata ubawa wake, ni wazimu juu ya wazimu, unastahiki kudhihakiwa. Na namna kama hii, katika kipindi kama hiki, na kundi hilo linapoonekana lenye nguvu sana itadhihiri dini ya kweli aliyokuja nayo Isa (a.s), na ambaye ni haiba ya kimaanawi ya bwana wetu Isa (a.s), yaani anashuka kutoka mbingu ya rehema ya kiungu, Ukristo wa sasa utasafika mbele ya ukweli huo na kuondokana na uongo na uzushi na hivyo kuungana na kweli za Kiislamu. Yaani Ukristo utabadilika kimaana na kuwa ni aina ya Uislamu. Mtu huyo wa kimaanawi wa Kikristo atakuwa ni mfuasi, kwa kufuata Qur’an tukufu na Uislamu utabaki kwenye makamo ya imamu mwenye kufuatwa, na matokeo ya muungano huu ni dini ya haki kupata nguvu kubwa, kwani wakati dini ya Kiislamu na ya Kikristo zilipokuwa kila moja peke yake hazina uwezo wa kuzuia kundi la Wakanaji Mungu, zitakuwa kwa fadhila ya kuungana baina yao tayari kuangamiza kikamilifu kundi la Wakanaji. Katika kipindi hiki haiba ya Isa (a.s) iliyopo kwa mwili wake wa kibinaadamu katika ulimwengu wa mbinguni itashika hatamu ya kundi la dini hiyo ya kweli. Ameeleza hili mtoa habari wa kweli kwa kuegemea ahadi kutoka kwa Mweza wa kila kitu, na kwa vile ameeleza, basi jambo hilo ni kweli halina shaka ndani yake. Na Mweza wa kila kitu anapoahidi hapana shaka kuwa atatimiza ahadi yake. Naam, hakika anayewatuma Malaika kwa mkururo kutoka mbinguni kuja ardhini na baadhi ya nyakati kuwafanya katika sura ya binaadamu (kama alivyomfanya Jibril (a.s) katika sura ya sahaba Dahyatu Al-Kalbiy) na kuwatuma viumbe wa kiroho kutoka ulimwengu wa kiroho, na kuwafanya kufanana na sura za kibinaadamu, bali huzituma hata roho za wengi katika mawalii waliofariki kwenye miili yao bora kuja duniani... haikanushwi kutoka kwa hekima ya Mwenye hekima na utukufu kumtuma Isa (a.s) aliye hai kwa mwili wake kwenye mbingu ya dunia kuja duniani, bali hata angelikuwa ameenda pande za mbali za ulimwengu wa Akhera, na akawa ni maiti kweli kwani yeye (s.w) ni Mweza na hekima yake inalazimu kumvisha mwili upya, na kumtuma duniani kwa ajili ya matokeo haya matukufu na makubwa, na ili iwe mwisho mwema kwa dini aliyokuja nayo Isa (a.s). Na ameahidi hili (s.w) kwa mujibu wa hekima yake tukufu. Na kwa kuwa ameahidi basi bila ya shaka atamtuma. Na hailazimu kila mmoja kumjua kuwa yeye ni Isa mwenyewe wakati wa kushuka kwake duniani, bali watu wake mahususi na wa karibu ndio watakaomjua kwa nuru ya Imani, kwani si watu wote watakaomjua kwa uwazi kabisa. Sual: Rivayetlerde gelmiş ki: “Deccal’ın bir yalancı cenneti var, kendine tabi olanları ona atar. Hem yalancı bir cehennemi var, tabi olmayanları ona atar. Hattâ o, kendi merkebinin de bir kulağını cennet gibi bir kulağını da cehennem gibi yapmış. Azamet-i bedeniyesi bu kadardır, şu kadardır…” diye tarifat var? Elcevap: Deccal’ın şahs-ı surîsi insan gibidir. Mağrur, firavunlaşmış, Allah’ı unutmuş olduğundan surî, cebbarane olan hâkimiyetine, uluhiyet namını vermiş bir şeytan-ı ahmaktır ve bir insan-ı dessastır. Fakat şahs-ı manevîsi olan dinsizlik cereyan-ı azîmi, pek cesîmdir. Rivayetlerde Deccal’a ait tavsifat-ı müthişe ona işaret eder. Bir vakit Japonya’nın Başkumandanının resmi, bir ayağı Bahr-i Muhit’te, diğer ayağı on günlük mesafedeki Port Artur Kalesinde tasvir edilmiş. O küçük Japon Kumandanının bu surette tasviriyle, ordusunun şahs-ı manevîsi gösterilmiş. Amma Deccal’ın yalancı cenneti ise medeniyetin cazibedar lehviyatı ve fanteziyeleridir. Merkebi ise şimendifer gibi bir vasıtadır ki bir başında ateş ocağı bulunur, kendine tabi olmayanları bazen ateşe atar. O merkebin bir kulağı yani diğer başı cennet gibi tefriş edilmiş, tabi olanları oraya oturtur. Zaten sefih ve gaddar medeniyetin mühim bir merkebi olan şimendifer, ehl-i sefahet ve dünya için yalancı bir cennet getirir. Bîçare ehl-i diyanet ve ehl-i İslâm için medeniyet elinde cehennem zebanisi gibi tehlike getirir, esaret ve sefalet altına atar. İşte İsevîliğin din-i hakikisi zuhur ile ve İslâmiyet’e inkılab etmesiyle, çendan âlemde ekseriyet-i mutlakaya nurunu neşreder. Fakat yine kıyamet kopmasına yakın tekrar bir dinsizlik cereyanı baş gösterir, galebe eder ve “El-hükmü li’l-ekser” kaidesince, yeryüzünde “Allah Allah” diyecek kalmayacak, yani ehemmiyetli bir cemaat, küre-i arzda mühim bir mevkiye sahip olacak bir surette “Allah Allah” denilmeyecek demektir. Yoksa ekalliyette kalan veyahut mağlup düşen ehl-i hak, kıyamete kadar bâki kalacak; yalnız, kıyametin kopacağı anında, kıyametin dehşetlerini görmemek için bir eser-i rahmet olarak ehl-i imanın ruhları daha evvel kabzedilecek, kıyamet kâfirlerin başına kopacaktır.
Source text is preserved. When a suitable model is available, translation is displayed separately.
Mektubat
The Fifteenth Letter
Source: risaleinur multilingual dataset, risale.site source · Risale-Nur multilingual research corpus

