Mektubat

The Seventh Letter

Source: risaleinur multilingual dataset, risale.site source · Risale-Nur multilingual research corpus
Risale reading plan
§1

بِاس۟مِهٖ سُب۟حَانَهُ وَ اِن۟ مِن۟ شَى۟ءٍ اِلَّا يُسَبِّحُ بِحَم۟دِهٖ اَلسَّلَامُ عَلَي۟كُم۟ وَ رَح۟مَةُ اللّٰهِ وَ بَرَكَاتُهُ اَبَدًا دَائِمًا Dada zangu wapendwa! Mmemwambia Al-Hafidh Tawfiq Ash-Shamy aniulize masuala mawili nayo ni: Kwanza: Kwamba watu wa upotovu wa sasa wanaona kuwa Mtume (s.a.w) kumuoa Zainabu ni sehemu ya kukosoa na kupinga, kama walivyokuwa wanafiki katika zama zilizopita. Kwa kuwa wanaona ni ndoa iliyojengwa kutokana na matamanio na misukumo ya kinafsi! Jibu: Ametakasika Allah na hapana! Hapana mara elfu hapana! Hakika mkono wenye kutia shaka upo chini sana kufika katika ncha ya hadhi hiyo ya juu. Naam, anayemiliki chembe ya insafu anatambua kuwa Mtume (s.a.w) kutoka miaka kumi na tano mpaka arobaini, kipindi hicho ambacho joto la matamanio linachemka na matamanio ya kinafsi yanawaka, amejizuia kikamilifu, kwa ushuhuda wa maadui na marafiki, akatosheka na mke mmoja aliye mfano wa mzee, naye ni Khadija mkuu (r.a). Basi hapana budi kuwa wingi wa kuoa Mkarimu huyu mwenye kujizuia (s.a.w) baada ya miaka arobaini – katika kipindi cha kutulia kwa joto la matamanio - haikuwa kwa matamanio ya kinafsi, bali ni kutokana na hekima muhimu, kati ya hizo ni: Hakika kauli za Mtume, matendo, hali, ngazi, kushughulika na kutulia kwake, ni chanzo cha dini, hukumu na sharia. Na hakika Masahaba watukufu (r.a) wamepokea hukumu hizi na wakabeba jukumu la kufikisha kilichodhihiri kwao katika maisha yake (s.a.w). Ama siri za dini na hukumu za kisheria zitokanazo na hali zake zilizofichikana kwao, ndani ya mipaka ya mambo yake binafsi, hakika wapokezi wake ni wake zake wasafi, hakika wametekeleza jukumu hili ipasavyo, bali takriban nusu ya hukumu za dini na siri zake zinakuja kupitia wao. Kwa maana, wadhifa huu mtukufu unalazimu uwepo wa wake wengi, na wenye mielekeo tofauti pia. Ama ndoa yake (s.a.w) kwa Zainabu, imeelezwa katika Mwale wa Tatu katika Mwako wa Kwanza wa “Neno la Ishirini Tano”, kwa kinachohusu aya tukufu: مَا كَانَ مُحَمَّدٌ اَبَٓا اَحَدٍ مِن۟ رِجَالِكُم۟ وَلٰكِن۟ رَسُولَ اللّٰهِ وَ خَاتَمَ النَّبِيّٖنَ Kuwa aya moja ina maana nyingi, kwa sura nyingi, kwa mujibu wa ufahamu wa matabaka ya watu. Basi sehemu ya tabaka la watu ya kufahamu aya hii tukufu ni: Kuwa Zaid (r.a) aliyekuwa mtumwa wa Mtume wa Allah (s.a.w), na aliyepata kuitwa: Ewe mwanangu! Hakuiona nafsi yake ni yenye kuendana na mkewe mtukufu wa nafsi basi akamtaliki kwa sababu hiyo, kama riwaya sahihi zilivyokuja, na kutokana na kukiri kwake mwenyewe. Yaani Zainab (r.a), ameumbwa katika kiwango kingine cha tabia za hali ya juu, kwa elimu yake Zaidi akahisi kuwa ana maumbile ya hadhi ya juu inayostahiki kuwa mke wa Nabii, ambapo amejiona si mwenye kuendana naye kimaumbile, kitu kilichopelekea kukosekana muungano wa kinafsi na kiroho baina yao, akamtaliki, na Mtume (s.a.w) akamuoa kwa amri ya kiungu. Aya tukufu. (زَوَّجْنَاكَهَا) inajulisha kwa kuashiria kuwa ndoa hiyo imefungwa kwa mafungamano ya mbinguni, ni mafungamano yasiyo ya kawaida, na juu ya mazoea na miamala ya kidhahiri, kwani ni mafungamano yaliyofungwa kwa hukumu ya kudura ya kiungu kabisa, kiasi kwamba Mtume (s.a.w) akatii hukumu hiyo kwa kulazimika na si kwa matakwa ya nafsi yake. Na hukumu hii ya kikadari inakusanya hukumu muhimu ya kisheria, hekima ya jumla na maslahi ya wote. Basi kwa ishara ya aya tukufu: لِكَيْ لَا يَكُونَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ حَرَجٌ فِي أَزْوَاجِ أَدْعِيَائِهِمْ Kuwa wakubwa kuwaita wadogo kwa: Ewe mwanangu! Si haramu, kwa kuwa haibadilishi hukumu kama kauli ya Al-Mudhwahir kwa mkewe (Yaani kauli yake: Wewe kwangu ni kama mgongo wa Mama yangu). Na pia hakika Mitume na wakubwa wanapozungumza na umma wao na watu wao wanaowaongoza, na wanapowaangalia, kama baba, basi hilo ni kwa kuzingatia jukumu la utume na si kwa kuzingatia haiba ya kibinaadamu hata iwe haramu kwao kuwaoa. Na tabaka la pili la watu linafahamu kama ifuatavyo: Hakika bwana mtukufu na kiongozi mwenye kutawala anawaangalia wananchi wake kama baba. Yaani anawaonea huruma kama huruma ya baba kwa mwanawe. Basi kiongozi huyo akiwa mfalme wa kiroho, nje na ndani, basi huruma yake inaongezeka maradufu kwa maradufu kuliko ile ya baba. Na watu kwa upande wao wanamuona kama mzazi, kana kwamba ni watoto wake hasa, na kwa vile mtazamo wa ubaba ni vigumu kubadilika na kuwa mtazamo wa mume, na mtazamo wa binti pia si rahisi kugeuka kuwa mke, kwa hiyo watu wameona ni tatizo kwa Mtume kuwaoa mabinti wa waumini, na Qur’an tukufu inasahihisha uelewa wao kwa kusema: Hakika ya Mtume (s.a.w) anawahurumieni na anakutendeeni kama baba, na anawatazama kwa jina la rehema ya kiungu, basi nyinyi ni kama watoto kwa mujibu wa Utume anaoubeba. Lakini si baba yenu kwa kuzingatia haiba ya kibinaadamu, ili kupatikane tatizo katika jambo hilo: Jambo la ndoa. Na hata akikuiteni enyi wanangu na watoto wangu, nyinyi si watoto wake kwa mujibu wa hukumu za kisharia, basi hamuwi watoto wake kweli. Mwenye kubaki Yeye ni mwenye kubaki Said Nursî

Private reading note

This note stays on this device and is never uploaded to a server.

Up to 1,200 characters