Mektubat

The Third Letter

Source: risaleinur multilingual dataset, risale.site source · Risale-Nur multilingual research corpus
Risale reading plan
§1

بِاس۟مِهٖ سُب۟حَانَهُ وَ اِن۟ مِن۟ شَى۟ءٍ اِلَّا يُسَبِّحُ بِحَم۟دِهٖ Hakuna chochote ila kinamtukuza! kwa sifa zake njema. (sehemu ya barua iliyoandikwa na Bediuzzaman kwenda kwa mmoja katika wanafunzi wake) Uliandika katika moja ya barua zako ulizonitumia kwamba ulitaka nikusimulie hisia zangu, sasa sikiliza moja ya sehemu elfu ya hisia zangu. Usiku mmoja, nikiwa juu ya jengo lenye duru mia moja kwenye nyumba yangu ya mti na kileleni mwa mti wa mwerezi nilitazama sura nzuri ya mbingu iliyojawa na nyota nikaona mwanga ulionyanyuliwa wa hali ya kimiujiza na siri ya kushangaza ya hekima katika kiapo cha Qur’an, yenye hekima zote. فَلَٓا اُق۟سِمُ بِال۟خُنَّسِ ۝ اَل۟جَوَارِ ال۟كُنَّسِ Aya hii, inayohusiana na sayari na hali za kule kufichikana kwake na kutawanyika, inaonesha katika kutazama kwa watazamaji ufundi na sanaa tele zilizopo katika kitambaa kilicho pambwa kwa ufundi mkubwa pamoja na sayari zinazojitokeza kwenye mzunguko wa jua kama kamanda wake, na kuingia katika duara la nyota zilizothibiti mahali pake, na kuonesha mapambo mazuri na mifano ya sanaa mbinguni, wakati mwingine huja bega kwa bega na nyota nyengine na kuonesha mandhari ya kupendeza na mara nyingine huingia kati ya nyota ndogo na kushika nafasi ya kamanda hasa katika majira haya baada ya jioni. Sayari ya zuhura ikiwa angani usawa wa mlalo na kabla ya mapema alfajiri moja ya wenza wake wanaong’ara huonesha mandhari ya kweli ya kuvutia na kupendeza, halafu, baada ya kutimiza majukumu yake kama wakaguzi na kutenda kama zana ya kupamba katika ufundi wa ufumaji zinarejea na kuingia katika duara linalong’ara mno la jua na kujificha, hapo zinadhihirisha ufalme mkuu katika mng’ao mfano wa jua unaoteremka kutoka kwa yule anayeizungusha hii dunia yetu na sayari ambazo zimeelezwa kwenye aya iliyopo hapo juu kwenye anga kwa mpangilio kamili angani, kila mmoja ni kama meli au ndege zake zenye kuzunguka mara elfu ilhali ni kubwa kuliko dunia, na zinazunguka katika mzunguko wa kasi mara elfu zaidi ya dunia. Unaweza kuona kutokana na haya ni kiasi kipi cha furaha, na heshima kubwa ilioje, na kule kuunganishwa na ufalme uliomo ndani ya ibada na imani ya kweli na kuwa mgeni kwake, kisha nikatizama kwenye mwezi na kuona mwanga wake wenye kung’ara kimuujiza katika aya hii: وَال۟قَمَرَ قَدَّر۟نَاهُ مَنَازِلَ حَتّٰى عَادَ كَال۟عُر۟جُونِ ال۟قَدٖيمِ Na mwezi tumeukadiria vituo vyake mpaka ukarejea kama karara la mtende la zamani” Kwa kweli, maamuzi, mzunguko, na kuweka mizani na kung’ara kwa mwezi, na kuwaka kwake kwa kuzingatia dunia na jua, na muhtasari wa kumbukumbu ni ajabu sana, la kushangaza sana kwamba hakuna chochote ambacho kingekuwa kigumu kwa Al-Qadiir Muweza wa kila kitu ambaye anaamuru na kuamua hayo, hivyo, yanawaelekeza viumbe wote wenye akili wenye kuyafahamu hayo, na kuwasilisha fikra ya kwamba yule ambaye anayefanya hayo kwa namna hiyo, kwa hakika anaweza kufanya chochote kile. Amri yake inaliamrisha jua na wala halikengeuki njia yake hata kwa sekunde, au kubaki nyuma japo kidogo katika majukumu yake, inawafanya wale wanaotazama hayo watamke: “Utukufu uwe kwa Yule ambaye ufundi wake unahemeza akili” hasa majira kama mwishoni mwa mwezi wa tano huja na muunganiko wa kilimia kwa umbo la hilali la kupendeza, ikijitokeza kama tawi la karara jeupe la mtende, na kilimia kikidhihiri kama kole la zabibu, inaleta sura katika mawazo kuwepo kwa mti mkubwa unaog’ara nyuma ya pazia ya mbingu ya kijani, kana kwamba ncha ya moja wapo ya matawi ya mti imetoboa pazia na kuungana kichwa chake na kole lake la zabibu na kwa kilimia na mwezi mchanga, na matawi mengine yamekuwa ni matunda ya mti uliojificha. Tazama werevu na ufasaha wa mfano. كَال۟عُر۟جُونِ ال۟قَدٖيمِ “kama karara la mtende la zamani” Halafu aya hii ilinitokea: سُب۟حَانَ الَّذٖى سَخَّرَ لَنَا هٰذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُق۟رِنٖينَ Utukufu ni Wake aliyemfanya huyu atutumikie, na tusingeliweza kufanya wenyewe. Ambayo inamaanisha kuwa ardhi ni jahazi linalo endeshwa au kuabiriwa, kutokana na hili niliona nafsi yangu ikiwa juu ya meli kubwa iendayo kasi angani, nikasoma aya hii: سُب۟حَانَ الَّذٖى سَخَّرَ لَنَا هٰذَا Utukufu ni Wake aliyemfanya huyu atutumikie. Ambayo ni sunna kuisoma wakati wa kuabiri chombo cha usafiri kama farasi au meli. Nimeona mwendo wa tufe la ardhi umechukua nafasi ya kikuza picha ambao unaonesha taswira kama kwenye sinema, unaleta mbingu zote kwenye mwendo na kuanza kukusanya nyota zote kama jeshi kubwa, unaonesha mandhari ya juu ambayo yanawalewesha wanayoyatafakari na kuwajaza mshangao: “Utukufu ni kwa Allah (sw)” nikapaza sauti “ni kazi nyingi, kubwa, za ajabu, utukufu kiasi gani, ambazo zinatendwa kwa gharama kidogo sana, nukta muhimu sana zinazohusu imani zilinitokezea baada ya hapa. Kwanza: Siku chache zilizopita niliulizwa swali na mgeni: Kiini cha swali hilo, ambalo lilimaanisha shaka lilikuwa hili: pepo na moto wa jahannam viko mbali sana kupitia rehema tukufu, watu wa peponi watapita katika sirat kama umeme au kwa kasi kama Buraq; na kuingia peponi lakini watu wa motoni, watakwendaje kwa miili yao mizito iliyotopewa na mizigo mizito ya dhambi zao watasafiri vipi? Kilichonitokezea ni hiki: Kama kwa mfano mataifa yote yataalikwa kwenye baraza kuu marekani, na kila mmoja akapanda mashua kubwa na kwenda huko, kwa namna hiyo hiyo, dunia, ambayo hufanya safari kwa masafa ya miaka ishirini elfu, ndani ya mwaka mmoja katika bahari kuu ya ulimwengu, itachukua kwa watu wake kusafiri kuelekea katika uwanja wa kukusanyika siku ya kiama na kuwashusha huko, zaidi ya hapo moto ulio kati ya ardhi unaashiriwa na ukweli kwamba hali ya joto ya ardhi huongezeka nyuzi joto moja kwa kila mita thelathini na tatu kwamba moto wa Jahannam utamimina moto wake kwenye Jahannam kuu. Joto hilo la nyuzi joto laki mbili ni sawa na lile lililoelezwa ndani ya hadithi na kwa mujibu wa hadithi itatimiza baadhi ya majukumu ya moto wa Jahannam kubwa hapa duniani na katika mamlaka ya mpito, halafu kwa amri tukufu ardhi itabadilishwa na kuwa katika muundo bora na wa kudumu, na itakuwa ni miji ya makao ya akhera. Nukta ya pili: Inayokuja akilini, ni kaida ya mtengenezaji Al-Qadiir Muweza wa kila kitu, Muumba ambaye ni Al-Hakiim Mwingi wa hekima ni Mmoja wa pekee, ili kuonesha ukamilifu katika uweza wake na uzuri wa hekima zake na uthibitisho wa upweke wake ni kutenda matendo mengi kwa kiasi kidogo sana na kuwa na majukumu makubwa yanayotimizwa kwa vitu vidogo kabisa kama nilivyosema katika baadhi ya maneno, kama mambo yote yangehusishwa kwa mmoja pekee, basi mambo huwa ni mepesi kama kuwa kama ya lazima, wakati ambapo kama yatahusishwa kwa wafanyaji wengi na kwa yale wanayofanyia kazi, basi ugumu mwingi utajitokeza na kuyafanya hayo kuwa ni muhali, kwa mtu mmoja pekee kama afisa au mjenzi mkuu na nafasi za askari wengi kwa kitendo kimoja pekee, mchakato mmoja, hupatikana tija ya jambo, lakini kama kwa ajili ya kupata nafasi na matokeo hayo, yanayohusishwa na askari katika jeshi au mawe katika kuba, ambayo bila msaada yanaweza kutimizwa kwa matendo mengi ya kweli, ugumu mwingi na kuchanganyikiwa kukubwa. Na kwa hiyo, kama matendo hayo katika mfano wa misokoto na mizunguko ya mahala pake na kuzunguka kitu kingine, na utukuzo wa matembezi na mtawanyiko na kuleta majira manne, mchana na usiku duniani, haya yanahusishwa na umoja na kuamuru dunia moja na kwa amri moja, mmoja anaweza kupata hali hizo tukufu na matokeo makuu, anaweza kudhihirisha maajabu katika kubadilishana misimu na maajabu ya hekima katika mizunguko ya mchana na usiku, na matukio ya neema ya kuvutia na mienendo dhahiri ya nyota, jua na mwezi. Kwani majeshi yote ya viumbe ni yake. Kama anataka anaweza kuagiza askari kama ardhi kuwa ni kamanda wa nyota zote, na kulifanya jua lenye nguvu kuwa ni taa inayotoa joto na mwanga kwa watu wake, na misimu minne ambayo ni meza ya maandishi ya uweza wake kama urembo, na usiku na mchana ni kurasa za maandiko yake ya hekima, na anaweza kuweka katika mapindo kwa kuonesha mwezi kila siku kwa umbo tofauti huufanya kuwa ni kalenda kwa ajili ya kukumbuka wakati, kama anavyozifanya nyota kuwa ni taa za kupamba, za usanifu na kung’ara mikononi mwa malaika, zikicheza kwa furaha kwa hiyo pia anaonesha mifano mingi ya hekima inayoonekana kwenye ardhi, kama hali hii haikutazamiwa kwa mmoja aliyopo, ambaye amri, sharia na kanuni zake zinawalenga viumbe wote, basi jua na nyota zote zingelazimika kwenda masafa yasiyo na ukomo kila siku kwa mwendo halisi na kasi isiyo na kikomo. Kwa sababu ya wepesi wa uso na upeo kwenye umoja na ugumu usio na upeo katika wingi, hadi wafanya biashara na wanaviwanda huweka umoja kwenye wingi na kwa hiyo kufanya vitu kuwa rahisi hii ndio maana wanaunda mashirika. Kifupi: Kuna ugumu usio na tamati katika njia ya wapotevu, na wepesi usio na tamati katika njia ya Umoja (Tauhid) Wa milele Yeye ni wa milele! Said Nursî

Private reading note

This note stays on this device and is never uploaded to a server.

Up to 1,200 characters