Mektubat

The Twenty-First Letter

Source: risaleinur multilingual dataset, risale.site source · Risale-Nur multilingual research corpus
Risale reading plan
§1

بِاس۟مِهٖ سُب۟حَانَهُ وَ اِن۟ مِن۟ شَى۟ءٍ اِلَّا يُسَبِّحُ بِحَم۟دِهٖ بِسْمِ اللّٰهِ الرَّحْمٰنِ الرَّحِيمِ اِمَّا يَب۟لُغَنَّ عِن۟دَكَ ال۟كِبَرَ اَحَدُهُمَٓا اَو۟ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل۟ لَهُمَٓا اُفٍّ وَلَا تَن۟هَر۟هُمَا وَقُل۟ لَهُمَا قَو۟لًا كَرٖيمًا ۝ وَاخ۟فِض۟ لَهُمَا جَنَاحَ الذُّلِّ مِنَ الرَّح۟مَةِ وَقُل۟ رَبِّ ار۟حَم۟هُمَا كَمَا رَبَّيَانٖى صَغٖيرًا ۝ رَبُّكُم۟ اَع۟لَمُ بِمَا فٖى نُفُوسِكُم۟ اِن۟ تَكُونُوا صَالِحٖينَ فَاِنَّهُ كَانَ لِل۟اَوَّابٖينَ غَفُورًا Ewe uliyeghafilika, na ewe ambaye baba mzee anaishi nyumbani kwake au mama mzee au mmoja wa watu wake wa karibu, au ndugu katika dini, au mtu mgonjwa asiyejiweza.. tazama aya hii tukufu kwa umakini na mazingatio, tazama vipi aya moja inaleta aina tano za rehema kwa wazee wawili wakongwe kwa namna tofauti? Naam, hakika ukweli wa hali ya juu duniani ni huruma ya mama na baba kwa watoto wao, na kwamba haki ya juu ni haki ya kuwaheshimu kama ni malipo ya huruma na upole huo, hiyo ni kwa kuwa wanajitolea maisha yao kwa ajili ya uhai wa watoto wao kwa kila ladha na furaha. Na kwa hivyo hakika kila mtoto - kama ubinadamu wake haujaporomoka na haujabadilika kuwa unyama - hapana budi kuwahishimu kwa ikhlasi vipenzi hivyo vyenye heshima, wenye kujitoa na wa kweli na kuwahudumia huduma ya kweli, na kufanya bidii ili wapate radhi zao na kuingiza furaha nyoyoni mwao. Hakika ya baba mkubwa au mdogo na shangazi wao ni kama baba, na hakika ya mama mkubwa au mdogo na mjomba wapo katika nafasi ya mama, basi tambua kwamba ni ukosefu uliyoje wa dhamiri kutia uzito uwepo wa wazee hawa na kuwataka wafe! Bali ni ubaya uliyoje wa kuwa kwao duni na kudhalilika. Tambua hili na zinduka! Ndiyo, elewa ni ubaya uliyoje wa dhulma na ubaya uliyoje wa ukosefu wa dhamiri kwa mtu kutamani kutoweka kwa yule ambaye ameutoa muhanga uhai wake wote kwa ajili ya uhai wake yeye! Ewe mwanadamu uliyejaribiwa kwa mahangaiko ya riziki! Tambua kuwa nguzo ya baraka ya nyumba yako na njia ya rehema ndani yake na kuzuia msiba, si vinginevyo ila ni mzee huyo, au kipofu huyo katika jamaa zako wa karibu ambaye anakupa uzito. Kamwe usiseme: Hakika maisha yangu ni magumu, sijizulii uongo katika hilo! Hiyo ni kwakuwa lau kama Baraka si zenye kuja kupitia wao basi dhiki ya maisha yako ingekuwa kubwa zaidi. Basi chukua ukweli huu kutoka kwangu na uamini, kwani mimi natambua dalili nyingi madhubuti kuhusu ukweli huu, na ninaweza kukufanya uzisadiki pia. Lakini ili jambo lisiwe refu ninalifupisha. Kuwa na Imani saana na maneno yangu haya. Naapa kwa Allah kuwa ukweli huu upo katika ukomo wa uhakika, kiasi kwamba nafsi yangu na shetani wangu wamesalimu amri mbele yake. Hapana shaka kuwa ukweli uliomkasirisha na kumnyamazisha shetani wangu na kuuvunja ukaidi wa nafsi yangu yenye kuamrisha maovu hapana budi kuwa unaweza kukukinaisha wewe pia. Ndio, hakika Muumba Mwenye utukufu na ukarimu, Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu na ambaye ni Mpole na Mkarimu - kwa ushuhuda wa vyote vilivyo ulimwenguni – anapowaleta watoto duniani hutuma na riziki zao nyuma yao moja kwa moja kwa ukomo wa upole; kama kutoa kilicho katika maziwa na kububujisha kama chemchemu vinywani mwao, vile vile hakika ya riziki za wazee ambao wameingia katika kundi la watoto bali wana haki zaidi ya kuhurumiwa, Allah (s.w) hutuma riziki hizo kwa namna ya Baraka, wala hawabebeshi watu mabahili kuwapa riziki hawa wala hawaachii wao. Ukweli unaojulishwa na aya tukufu: إِنَّ اللَّهَ هُوَ الرَّزَّاقُ ذُو الْقُوَّةِ الْمَتِينُ وَكَأَيِّن مِن دَابَّةٍ لَا تَحْمِلُ رِزْقَهَا اللَّهُ يَرْزُقُهَا وَإِيَّاكُمْ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ Ni ukweli wenye ukarimu, viumbe vyote anuai miongoni mwa vyenye uhai vinautamka na kuutangaza kwa ndimi za hali zao. Na si wazee wa karibu peke yao huwajia riziki yao kwa wepesi kwa sura ya baraka, bali hata riziki ya baadhi ya viumbe waliyoletwa kuishi na mwanadamu mfano wa paka. Hakika ya riziki zao hutumwa ndani ya riziki ya mwanadamu, na inakuja kwa sura ya baraka pia. Na kinachounga mkono hili ni mfano niliyouona mwenyewe. Nao ni: Nilikuwa nina fungu la chakula kila siku - kama wapenzi wangu wa karibu wanavyotambua - kabla ya miaka miwili au mitatu nalo ni nusu ya mkate, na mkate wa kijiji hicho ulikuwa mdogo, na mara nyingi ulikuwa haunitoshi.. Kisha walinijia paka wanne kama wageni basi chakula hicho kilinitosha na kikawatosha. Bali mara nyingi kilikuwa kikibakia. Hali hii imejirejea kwangu kiasi kwamba imenikinaisha kikamilifu kwamba mimi ndiyo niliyokuwa nafaidika na Baraka za paka hao! Na mimi ninatangaza tangazo la kukata shauri sasa hivi kuwa paka wale hawakuwa mzigo kwangu wala hawakuwa chini ya neema yangu, bali mimi ndiye niliyekuwa chini neema yao. Enyi watu! Hakika mnyama mfano wa mnyama mwitu aliyekuja mgeni katika nyuma anakuwa ni sehemu ya Baraka, basi vipi akija katika nyumba mwenye kukirimiwa zaidi ambaye ni mwanadamu? Na ambaye ni mkamilifu zaidi kati ya watu naye ni muumini? Na ambaye katika wazee wagonjwa na wenye umri mrefu kati ya watu wa Imani? Na ambaye mwenye kustahiki zaidi huduma na mapenzi kati ya wagonjwa wenye umri mrefu na wenye kustahiki zaidi jamaa wa karibu? Na ambao ni marafiki wa kweli wapenzi wa kweli kati ya hawa jamaa wa karibu nao ni wazazi wawili?! Vipi wakija katika nyumba. Ni juu yako kupima ukubwa uliyoje wa njia ya baraka, na njia ya kuleta rehema na sababu ya kuzuia msiba, kama hadithi tukufu ilivyokusanya maana hiyo: (Kama si wazee wenye kurukuu mngeshushiwa balaa). Hivyo ewe mwanadamu! Zingatia na tambua kwamba usipokufa hakuna namna utakuwa mzee tu, na usipowaheshimu wazazi wako itakuja siku watoto wako hawatakuheshimu, na hiyo ni kwa alichokiweka Allah miongoni mwa siri ya (malipo huwa kwa mujibu wa matendo yenyewe). Hivyo ikiwa ni mpenzi wa Akhera yako basi mbele yako kuna hazina kubwa nayo ni: Wahudumie ili upate radhi zao. Na ikiwa unaipenda dunia basi waridhishe pia na uwashukuru. Ili maisha yako yaende kwa raha na ili riziki yako ije na Baraka nyuma yao. Kinyume na hivyo, kuwaonea uzito wao na kutamani wafe na kuzijeruhi nyoyo zao laini zenye hisia kali zitakufanya uwe miongoni mwa wale wanaotamkwa na ukweli wa Aya tukufu: خَسِرَ الدُّنْيَا وَالْآخِرَةَ Kama unataka rehema ya Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu basi warehemu waliyoletwa na Mwingi wa rehema na amana alizokupa kwenye nyumba yako. Nilikuwa nina ndugu miongoni mwa ndugu wa akhera naye ni (Mustafa Jaushi) na nilikuwa nikimwona aliyepata taufiki wa dini yake na dunia yake kwa pamoja. Na sikuwa nikielewa siri. Kisha nikaelewa sababu ya taufiki hiyo: Nayo ni kuwa mtu huyu mwema alikuwa anatambua haki za baba yake na mama yake, naye amezichunga haki hizo kwa ukamilifu. Akapata raha na rehema kwa baraka ya nyuso zao. Na ninataraji awe ameijenga akhera yake pia Insha Allah. Basi anayetaka kuwa na furaha amuige na awe kama yeye. اَللّٰهُمَّ صَلِّ وَسَلِّم۟ عَلٰى مَن۟ قَالَ «اَل۟جَنَّةُ تَح۟تَ اَق۟دَامِ ال۟اُمَّهَاتِ» وَ عَلٰى اٰلِهٖ وَصَح۟بِهٖ اَج۟مَعٖينَ سُب۟حَانَكَ لَا عِل۟مَ لَنَٓا اِلَّا مَا عَلَّم۟تَنَٓا اِنَّكَ اَن۟تَ ال۟عَلٖيمُ ال۟حَكٖيمُ

Private reading note

This note stays on this device and is never uploaded to a server.

Up to 1,200 characters