Mektubat

The Twentieth Letter

Source: risaleinur multilingual dataset, risale.site source · Risale-Nur multilingual research corpus
Risale reading plan
§1

بِاس۟مِهٖ سُب۟حَانَهُ وَ اِن۟ مِن۟ شَى۟ءٍ اِلَّا يُسَبِّحُ بِحَم۟دِهٖ لَٓا اِلٰهَ اِلَّا اللّٰهُ وَح۟دَهُ لَا شَرٖيكَ لَهُ لَهُ ال۟مُل۟كُ وَ لَهُ ال۟حَم۟دُ يُح۟يٖى وَ يُمٖيتُ وَ هُوَ حَىٌّ لَا يَمُوتُ بِيَدِهِ ال۟خَي۟رُ وَ هُوَ عَلٰى كُلِّ شَى۟ءٍ قَدٖيرٌ وَ اِلَي۟هِ ال۟مَصٖيرُ Hakika sentensi hii ambayo inafupisha Tawhid, ni ibara ya maneno kumi na moja na kwa kuyasoma baada ya swala za alfajiri na magharibi kuna fadhila kubwa, hata imepokewa katika moja ya mapokezi sahihi kwamba inabeba daraja la (Al-Ismi Al-Aadham). Hakuna shaka kwa hiyo kuvuja kila neno katika maneno yake matumaini yenye kuponya na bishara yenye kufurahisha, na kubeba daraja tukufu katika daraja za Tawhid ya Rububiyya (kumpwekesha Bwana Mlezi) na inabainisha kutokea pembe ya Al-Ismi Al-Aadham ukuu wa umoja na ukamilifu wa Tawhid. Na ilivyokuwa kwamba hakika hizi zilizonyanyuka zimefafanuliwa kwa ufasaha katika (Maneno) mengine basi tunaelekeza huko. Na hapa tunatosheka kwa kuweka fahirisi yake, kwa msingi wa ahadi iliyotangulia kwa sura ya muhtasari mfupi mno. Inaundika kutokana na ‘vituo viwili’, na ‘utangulizi’.

§2

Jua kwa yakini kwamba lengo kuu kabisa la uumbaji na matokeo makuu ya maumbile ya kibinadamu ni (Imani ya Allah (s.w)) na ujue kwamba ngazi ya juu kabisa ya ubinadamu, na makamo bora kabisa ya utu ni (kumjua Allah) kuliomo katika imani hiyo. Na jua kwamba furaha yenye kuchanua mno kwa watu na majini na neema tamu mno ni (kumpenda Allah (s.w)) inayotokana na ujuzi huo. Na jua kwamba furaha safi mno kwa roho ya mwanadamu na sherehe nadhifu mno kwa moyo wake ni ‘ladha ya kiroho’ inayotona kutoka katika mahaba hayo. Ndio, hakika aina zote za furaha ya kweli, furaha ya dhati, neema ambayo hakuna baada yake neema na ladha ambayo haipitwi na ladha, hakika imo katika kumjua Allah (s.w), katika kumpenda Allah (s.w), basi hakuna furaha wala neema ya kweli ya haki bila hiyo. Basi kila aliyemjua Allah (s.w) haki ya kumjua na akaujaza moyo wake nuru ya mahaba yake, atakuwa mwenye kustahiki furaha isiyokoma na neema isiyotindika na kwa nuru na siri zisizokwisha, na atazipata hizo ima kiuhalisia au kwa utayari na ukubalifu. Wakati ambapo ambaye hamjui Muumba wake haki ya kumjua, na wala hamwelekezei kiasi kinachostahiki cha mapenzi atasibiwa na taabu za kimaada na kimaanawy mawili haya ya kudumu, na atabaki akisumbuka na machungu na dhana kiasi kisichohesabika. Naam, hakika ya mtu huyu mwovu ambaye anataabika na maumivu kwa kumkosa Mola wake na mhami wake na anababaika kutokana na uduni wa uhai wake na kutokufaa kwake, naye ni mwenye kushindwa na dhaifu kati ya mikusanyiko ya watu wenye taabu, kitu gani kitamtosheleza kunako hayo anayotaabika nayo hata akiwa ni Mfalme wa dunia yote! Basi ubaya ulioje wa mtu huyu mwenye kubabaika katika msiba wa maisha ya kutoweka yenye kuondoka na baina ya mikusanyiko huria ya wanadamu ikiwa hakumkuta Mola wake wa haki na hakumjua mmiliki wake na Bwana Mlezi wake haki ya kumjua! lakini angemkuta bwana Mlezi wake na akamjua Mola wake na mmiliki wake angekimbilia katika hifadhi ya Rehema zake kunjufu na angeegemea katika utukufu wa uweza wake wa hali zote na dunia yenye kutisha ingemgeukia na kuwa ni bustani lenye kuliwaza na soko la biashara yenye faida.

§3

Kila neno miongoni mwa maneno haya ya Kitawhid yenye kupendeza yanapeleka bishara yenye kufurahisha na kueneza matumaini yenye vuguvugu. Na katika kila bishara kuna ponya na katika kila ponya kuna ladha ya kimaanawy na ukunjufu wa kiroho.

§4

(لاَ إِلهَ إِلاَّ الله) Neno Hili Linavuja Bishara Adhimu Na Matumaini Yenye Kufurahisha Kama Ifuatavyo: Hakika roho ya mwanadamu yenye pupa na mahitaji yasiyokuwa na mpaka, na mwenye kulengwa kutoka upande wa maadui wasiohesabika, roho hii yenye kupewa mtihani kati ya mahitaji yasiyo koma na maadui wasiojulikana kwa hesabu, inapata katika neno hili adhimu chemchem tajiri ya msaada, kwa namna inayoifungulia milango ya hazina za rehema kunjufu hupata kutokana na neema hiyo kinachotuliza haja zote na kudhamini mahitaji yote, na humo pia inakuta kituo ngome yenye nguvu na maegemeo ya kuridhisha inayoikinga na shari zote, na kumwondolea madhara yote, na hii ni kwa yale inayomwonesha mwanadamu katika nguvu ya Mola wake wa haki, na kumwongoza kwa mmiliki wake mzuri, na kumjulisha kwa Muumba wake na Mwabudiwa wake, na kwa uoni huu ulionyooka na kumtambua Allah (s.w) mmoja wa pekee, huokoa – neno hili –moyo wa mwanadamu kutoka katika giza la upweke na dhana, na kuiokoa roho yake kutokana na machungu ya huzuni na majonzi. Bali inamdhaminia furaha ya milele na kudumu.

§5

وَح۟دَهُ Neno hili linachanua matumaini na kupeleka bishara yenye kufurahisha kama ifuatavyo: Hakika roho ya mwanadamu na moyo wake ambavyo vimechoka bali vimezama hadi kuziba pumzi chini ya mibinyo ya mafungamano makali na mahusiano madhubuti pamoja na walio wengi wa sampuli ya viumbe, vinapata katika neno hili kimbilio salama, linaviokoa kutokana na maangamizo na misiba hiyo. Yaani hakika neno (وَحْدَه) linasema kimaana: Hakika ya Allah ni mmoja wa pekee, basi usiitaabishe nafsi yako ewe mwanadamu kwa kuwarejea wengine, wala usijidhalilishe kwao ukawa chini ya wema na maudhi yao. Wala usiinamishe kichwa chako mbele yao na kufanya unafiki. Wala usiichoshe nafsi yako ukaenda mbio nyuma yao. Wala usiwahofu na kutetemeka mbele yao. Kwa sababu mfalme wa ulimwengu ni mmoja, na yeye ana funguo za kila kitu. Mkononi mwake kuna hatamu ya kila kitu, hufunguka mafundo ya kila kitu kwa amri yake, na kila shida hupata faraja kwa idhini yake. Ukimpata yeye umemiliki kila kitu, umefuzu unachokitafuta na umeokoka kutokana na mazito ya masimulizi na udhia na kutoka katika mateka ya hofu na dhana.

§6

لَا شَرٖيكَ لَهُ Yaani kama asivyokuwa na mwenza wala dhidi yake katika Uungu wake kwa sababu Allah ni mmoja, hakika kuwa kwake ni Mlezi na utendaji wake na kupatisha kwake viumbe ni vyenye kutakasika vilevile na ushirika. Tofauti na wafalme wa Ardhini, kwani hutokea kuwa mfalme ni mmoja pekee katika ufalme wake isipokuwa si wa pekee katika utendaji wake, ambapo wafanya kazi wake na watumishi wake wanahesabiwa kuwa ni washirika katika kurahisisha mambo na kutekeleza utendaji na yamkini wakawazuia kuhudhuria wote mbele yake, na kuwataka kupitia kwao kwanza! lakini Allah (s.w) naye ni mfalme wa Azali na milele ni mmoja hana mshirika katika ufalme wake. Basi katu hana haja katika utendaji wake wa kiungu – Ubwana Mlezi vilevile washirika na wasaidizi wa kutekeleza kwa sababu kitu chochote hakiathiri katika kitu kingine isipokuwa kwa amri hila na nguvu yake, basi inayumkinika kwa wote kumrejea yeye bila ya mkaa kati, kwa kutokuwa na mshirika au msaidizi na haisemwi wakati huo kwa mwenye kurejea: Haijuzu kwako kuingia katika hadhara ya kiungu. Na kama hivi neno hili linabeba ndani yake furaha yenye kuleta tabasamu na bishara yenye kuleta sherehe. Ukasema: Hakika mwanadamu ambaye roho yake imechukua nuru ya Imani hakika anaweza kuonesha haja zake zote bila ya kizuizi mbele ya huyo Mzuri Mwenye utukufu, huyo Mweza Mwenye ukamilifu, na kutafuta yanayohakikisha matashi yake, popote alipo mwanadamu huyo anatandaza haja zake zote mbele ya huyo Mwenye kurehemu ambaye anamiliki hazina za rehema kunjufu kwa kuegemea nguvu yake ya hali zote. Wakati huo basi anajawa na furaha kamili na yenye kumwenea.

§7

لَهُ ال۟مُل۟كُ Yaani hakika ufalme wote ni wake bila ya kuvua, na wewe pia ni milki yake, kama ulivyokuwa ni mja wake na mmiliki wake, wewe pia ni mfanya kazi katika ufalme wake. Basi neno hili linanukia matumaini na kuvuja bishara yenye kuponya na kusema: Ewe mwanadamu! Usidhani kuwa wewe ni mwenye kumiliki nafsi yako, hapana. Kwa sababu wewe huwezi kuendesha mambo ya nafsi yako, na huo ni mzigo mzito na jukumu kubwa na huwezi kulihifadhi, kuiokoa na balaa na mabaya, na kuitimizia mahitaji ya uhai wako. Kwa hiyo usiipe nafsi yako machungu bure bure, ukaitupa kwenye kifua cha wasiwasi na babaiko bila ya manufaa. Kwani ufalme sio wako. Bali hakika ni wa mwingine asiye kuwa wewe, na huyu Mmiliki ni Mweza, naye ni mwenye kurehemu, basi egemea katika uweza wake, wala usiituhumu rehema yake, acha yaliyochafuka na uchukue yaliyo safi. Tupa magumu na shida na ushushe pumzi na fuzu kwa starehe na furaha, na chukua raha na furaha. Na unasema vilevile: Hakika ya huu uwepo ambao unautamani kimaana na kuambatana nao, unaumia kwa taabu zake na migongano yake, na unahisi kushindwa kwako kuutengeneza, uwepo huu wote ni mali ya Mweza Mwenye kurehemu. Basi salimisha ufalme kwa Mola wake, na uache yeye anaitawalia, na ufurahi kwa mambo yake yenye kufurahisha, bila ya kukuchafua taabu zake na shida zake, basi Mola ni Mwingi wa hekima na mwenye kurehemu, anasarifu katika ufalme wake namna atakavyo kulingana na hekima yake na rehema yake. Ikiwa itakuchukua woga na mshangao, basi chungulia kutoka kwenye madirisha wala usiyavamie na useme kama alivyosema mshairi Ibrahim Haki: Tuone Mola anafanya nini Na anachokifanya ndiyo kizuri zaidi.

§8

وَ لَهُ ال۟حَم۟دُ Yaani hakika sifa zote njema na kunata na madihi na wema ni mahususi kwake yeye peke yake, na yenye kufaa kwake yeye peke yake, kwa sababu neema zote ni kutoka kwake peke yake, na inamimina kutoka katika hazina zake pana, na hazina ni za kudumu hazikomi. Na kama hivi neno hili linatoa bishara nyororo, na linasema: Ewe mwanadamu ! Usitaabike na maumivu kwa kuondoka kwa neema, kwa sababu hazina za rehema haimaliziki. Wala usipige kelele kwa kuondoka kwa ladha, kwa sababu neema hiyo si chochote isipokuwa ni tunda la rehema kunjufu isiyo na ukomo, basi matunda hufuatana maadamu mti ni wenye kubaki. Na jua ewe mwanadamu kwamba unaweza kuifanya neema kuwa ni nzuri zaidi na kubwa kuliko ilivyo mara mia moja na hiyo ni kwa kuona kwako kugeuka neema upande wako, na ukarimu wake kwako na hii ni kwa shukurani na kuhimidi, kwani kama ilivyo kama mfalme mkubwa na mtawala mwenye hadhi ikiwa amekutumia zawadi, na iwe ni Tufaha mathalan, hakika zawadi hii inabeba ladha inayozidi ladha ya tufaha la kimaada kwa maradufu ya maradufu. Hiyo ni ladha ya umuhimu wa kiufalme na uelekea wa kiufalme uliovikwa taji kwa kuhusishwa na hisani. Kadhalika neno (lahulhamdu) linafungua mlango mpana mbele yako kutoka katika mlango huo inabubujika ladha ya kimaanawy iliyo safi ni tamu kuliko hizo neema zenyewe kwa maradufu ya maradufu elfu moja, na hii ni kwa himidi na shukurani. Yaani kwa kuhisi uneemeshaji kupitia neema, yaani kwa kumtambua mneemeshaji kwa kutafakari katika uneemeshaji wenyewe, yaani kwa kutafakari na kuangalia kwa busara katika kugeukia neema zake (s.w) na kuelekea kwake kwako na huruma yake kwako na uneemeshaji wake kwako.

§9

يُح۟يٖى Yaani yeye ndiye anayetoa uhai na yeye ndiye anayeudumisha kwa kutoa riziki, na yeye ndiye anayedhamini kwa mambo yake ya lazima na haja zake, na yeye ndiye anayeandaa mahitaji yao ya lazima, basi shabaha za hadhi ya juu ya maisha humrejea yeye, na matokeo yake muhimu yanaelekea kwake na tisini na tisa katika mia ya matunda na matokeo yake yanamkusudia na kumrejea yeye. Na kama hivi basi neno hili linamuita mwanadamu huyu mwenye kutoweka mwenye kushindwa, na kumsogezea bishara inayomulizia kwake roho ya matumaini, na kusema: Ewe mwanadamu! Usiichoshe nafsi yako kwa kujibebesha mizigo mizito ya maisha juu ya mgongo wako dhaifu, wala usiitaabishe nafsi yako kwa majuto juu ya kumalizika kwa uhai na kutoweka kwake, wala usioneshe majuto na majonzi kutokana na kuja kwako katika uhai kila uonapo kutoweka kwa neema zake na uduni wa matunda yake, na ujue kwamba uhai wako ambao unaimarisha uwepo wako hakika unarejea kwa (الحَيُّ القَيُّوْمُ) kwani yeye ndiye mdhamini wa mahitaji yako yote. Basi uhai huu unarudi kwake peke yake kwa shabaha zake chungu tele na matokeo yake mengi, na wewe si lolote isipokuwa ni mfanya kazi rahisi sana katika jahazi la uhai, basi tekeleza wajibu wako kwa namna iliyo bora. Kisha pokea ujira wako na ustarehe nao, na ukumbuke daima: Kiasi cha utukufu wa uhai huu ambao unapasua mawimbi ya uwepo, na kiasi cha utukufu wa faida zake na matunda yake, na kiasi cha ukarimu na upana wa rehema ya Mola wake. Chunguza hilo na uogelee katika anga la furaha, na pokea habari njema na utimize shukurani iliyo juu yako upande wa Mola wako, na ujue kwamba wewe ukiwa mnyoofu katika matendo yako husajiliwa katika kurasa zake mwanzoni matokeo ya jahazi hili la maisha, na hapo hukupa wewe uhai wenye kubakia na kuishi maisha ya milele.

§10

وَ يُمٖيتُ Yaani hakika yeye ndiye anayetunuku umauti, yaani yeye ndiye ambaye anakuruhusu kutoka katika jukumu la uhai na anabadili mahali pako duniani yenye kutoweka, na kukuokoa kutoka katika jukumu la huduma na kukukomboa kutoka katika masuulia ya jukumu. Yaani anakuchukua kutoka katika uhai huu wenye kutoweka kwenda uhai wenye kubakia. Na kama hivi basi neno hili linapiga kelele katika sikio la wanadamu na majini wenye kutoweka na kusema: Bishara yenu. Umauti sio kinyongo. Wala si mchezo wala sio bure bure, na kuteketea. Wala kuzimika wala kufariki kwa milele. Kamwe sivyo hivyo, umauti sio kukosekana, wala jambo la sadifu wala kukosekana kidhati bila ya mtendaji. Bali ni ruhusa kutoka kwa ambaye ni mtendaji mwingi wa hekima mwenye kurehemu, kubadili mahali, na kugeuza kituo, na kupelekwa kuelekea kwenye furaha ya kudumu. Mahali pa mji wa asili. Yaani ni mlango wa mawasiliano na ulimwengu wa Barzakh, ulimwengu unaojumuisha asilimia tisini na tisa ya wapenzi.

§11

وَ هُوَ حَىٌّ لَا يَمُوتُ Yaani hakika ya ukamilifu na uzuri na hisani ya dhahiri katika vilivyokuwepo ni njia ya mapenzi, inadhihiri kwa namna ambayo haiyumkiniki kuielezea na kwa namna isiyozuiliwa na mipaka na juu ya ngazi za juu kutoka kwa mmiliki wa uzuri na ukamilifu na hisani basi mwanga kutoka katika midhihirisho ya uzuri wake (s.w) unalingana na wapendwa wote wa dunia kwa ujumla wao. Mola huyu mpendwa Mwabudiwa ana uhai wa milele wa kudumu wenye kutakasika na madoa ya kutoweka na vivuli vya kutoweka upo mbali na sifa za upungufu na kasoro. Kwa hiyo neno hili linatangaza kwa kaumu zote wakiwemo majini na watu na watu wenye hisia na utambuzi na watu wa ashiki na mahaba na kusema: Bishara ni kwenu. Ishara ya matumaini na kheri, hakika mna mpendwa wa azali mwenye kubakia. Anaagua majeraha yatokanayo na maumivu ya kutengana kwa milele kwa mpendwa wenu wa kidunia na kuyagusa kwa dawa yenye kuponya kwa mafuta ya rehema. Basi maadamu yeye yupo na maadamu yeye ni mwenye kubaki basi kila kitu kinakua rahisi. Msiwe na wasiwasi wala msikate tamaa. Hakika ya uzuri na hisani na ukamilifu ambaye amekujalieni wenye shauku kwa wapendwa wenu sio isipokuwa ni pepeso la kivuli dhaifu kimepasuka kutoka katika vivuli vya pazia na sitara nyingi mno za mdhihirisho mmoja katika midhihirisho ya uzuri wa huyo mpendwa mwenye kubakia. Kusikuadhibuni kutoweka kwa hao na kufarikiana nao, kwani wote hao sio isipokuwa ni sampuli ya vioo vyenye kuakisi. Na kubadilisha vioo na kuvigeuza hufanywa upya na kuweka vizuri akisi za dhihirisho la uzuri na mimuliko yake angavu. Basi maadamu yeye yupo, kwa hiyo basi kila kitu kipo.

§12

بِيَدِهِ ال۟خَي۟رُ Hakika kheri yote iko mkononi mwake, na matendo yenu ya kheri yote yanasajiliwa katika faili lake, na mnayoyatanguliza katika amali njema yote huwekwa kwake. Basi neno hili linawanadia majini na watu, na kuwapelekea bishara na kuwatunukia matumaini na shauku linasema: Enyi masikini! Msiseme mnapoondoka duniani kuelekea makaburini (Oh!.. Ee! majuto yalioje, Ee! huzuni ilioje, hakika mali zetu zimepotea kama vumbi lililopepeswa na upepo, na jitihada zetu zimepotea bure, basi tumeingia katika ufinyu wa kaburi baada ya nafasi ya dunia). Hapana, msipige kelele kwa kukata tamaa, kwa sababu vyote mlivyo navyo vimehifadhiwa kwake (s.w), na kila mlichokitanguliza katika amali na juhudi kimesajiliwa na kuwekwa kwenye diwani kwake. Basi hakuna kitu kinachopotea wala hakuna juhudi inayosahaulika, kwa sababu mwenye utukufu ambaye mkononi mwake kuna kheri zote atakulipeni kwa amali zenu, na atawaiteni kuhudhuria mbele yake baada ya kuwawekeni kwenye mchanga, mafikio yenu ya muda maalum. Basi wenye furaha kiasi gani nyinyi, na mmekwishakutimiza huduma zenu, na mmemaliza majukumu yenu, uwanja wenu umetakasika, na siku za kutaabika zimekwisha na mizigo mizito. Basi nyinyi hivi sasa mnakwenda kukabidhiwa malipo na kupokea faida. Naam, hakika Mweza Mtukufu ambaye amehifadhi mbegu na kokwa ambazo ni nyaraka za matendo ya majira ya machipuo yaliyopita na daftari za huduma zake na vyumba vya majukumu yake na kuzitawanya katika majira ya machipuo yenye kupendeza na katika pambo la kuvutia mno, na katika upeo wa kung’ara, na katika wingi wa baraka, na katika sura ya kuvutia mno, hakika ya huyu Mweza mtukufu hapana shaka vilevile atahifadhi matokeo ya uhai wenu na vyanzo vya amali zenu, na atakulipeni kwayo malipo bora zaidi na thawabu nyingi mno.

§13

وَ هُوَ عَلٰى كُلِّ شَى۟ءٍ قَدٖيرٌ Kwamba yeye ni mmoja wa pekee, hakimsumbui kitu, wala hakimpotei kitu, wala hakiwi kigumu kwake kitu chochote. Basi kuumba majira kamili ya machipuo - mathalani – ni rahisi na wepesi kwake kama kuumba ua moja, na kuumba pepo kwake kama kuumba hayo majira ya machipuo na kwa urahisi na wepesi vilivyo kamili. Basi viumbe visivyokuwa na mpaka ambavyo anavipatisha na kuvifanya upya kila siku, kila mwaka, kila enzi, vyote vinashuhudia kwa ndimi zisizokuwa na mpaka juu ya uweza wake usio na mpaka. Basi neno hili vilevile linatunuku matumaini na bishara njema na kusema: Ewe mwanadamu hakika amali zako ambazo umezitekeleza na uja wako uliosimamia kuutimiza, haviendi kama vumbi lenye kupepeswa, kuna makao ya malipo ya kudumu, na mahali pa furaha ya kustarehesha vimeandaliwa kwa ajili yako. Basi mbele yako kuna pepo ya kudumu yenye shauku ya kufika kwako. Basi kuwa na hakika ya ahadi ya Muumba wako mwenye utukufu ambaye unaporomoka kwa ajili yake ukiwa mwenye kusujudu na kuabudu, mwamini yeye na kuwa na matumaini naye, kwani ni muhali yeye kuhalifu ahadi aliyoiweka juu ya nafsi yake, kwani uweza wake hauingii doa au upungufu. Matendo yake hayaingiliani na kushindwa au udhaifu. Basi kama alivyokuumbia bustani yako ndogo na anaihuisha, basi yeye ni Mweza kukuumbia pepo kunjufu. Bali ameiumba kwa hakika, na amekuahidi kuingia humo. Na kwa kuwa yeye ameahidi basi kwa vyovyote atatimiza ahadi yake, na atakuchukua kwenda katika pepo hiyo. Na maadamu tunaona kwamba yeye anakusanya na kutawanya kila mwaka katika uso wa hili tandiko zaidi kuliko sampuli mia tatu elfu katika sampuli za mimea na jamii ya wanyama na kwa mpangilio kamili na kwa mizani nyeti, na katika kasi ya haki ya juu na urahisi kamili basi hapana budi kwamba huyu Mweza mtukufu ni Mweza vilevile kuweka ahadi yake mweko wa kutekeleza. Na maadamu Mweza wa hali zote kila mwaka anapatisha maelfu ya vielelezo vya ufufuo na pepo na kwa mitindo na maumbo mbalimbali, na maadamu yeye anabashiria pepo iliyoahidiwa, na anaahidi furaha ya milele katika amri zake za mbinguni zote, na maadamu hatua zake zote na mambo yake ni haki na hakika na kweli na yenye kusibu, na maadamu athari zake zote zinashuhudia kwamba makamilifu yote hakika hayo ni dalili kuwa yeye ni mwenye kutakasika na upungufu na kasoro, na maadamu kuvunja ahadi na kuhalifu ahadi na uongo na kuchelewesha ni katika sifa mbaya mno ukiachilia mbali huo ni upungufu na kasoro, basi hapana budi hakika huyo Mweza mwenye utukufu, na huyo mwingi wa hekima mwenye ukamilifu, na huyo mwenye kurehemu mwenye uzuri, atatimiza ahadi yake kwa vyovyote itakamilishwa atafungua milango ya furaha ya milele, na atawaingizeni nyinyi peponi enyi waumini, makazi ya baba yenu Adamu.

§14

وَ اِلَي۟هِ ال۟مَصٖيرُ Hakika ya ambao wanapelekwa katika makao ya duniani, makao ya mtihani na uchaguzi, kwa ajili ya biashara na kutimiza majukumu, kwa mara nyingine watarejea kwa mpelekaji wao Muumba Mwenye utukufu. Baada ya kuwa wametimiza majukumu yao na wametimiza biashara yao, na kufikia ukomo wa huduma zao, na watamkuta Mola wao mkarimu ambaye amewatuma, yaani wao watapata utukufu wa kuhudhuria mbele ya Bwana wao Mlezi Mwenye kurehemu, katika kikazi cha ukweli mbele ya mfalme wao Mwenye uweza, hapana kati yake nayo kizuizi chochote, na hakika wamekombolewa na machungu ya sababu na giza la vizuizi na wakaa kati. Na kila mmoja kati yao atapata na atatambua kwa utambuzi safi mkamilifu kumtambua Muumba wake na Mlezi wake na Bwana wake na Mfalme wake. Basi neno hili linaangaza matumaini na kung’ara bishara njema inayovuka matumaini yote hayo na bishara zenye ladha. Linasema: Ewe mwanadamu! Je, unajua kuwa unakwenda wapi? Na wapi unakopelekwa? Hakika imetajwa katika neno la thelathini na mbili, kuishi miaka elfu katika maisha ya dunia na katika furaha ya kustarehesha hailingani sawa na saa moja katika maisha ya peponi. Na kwamba kuishi maisha ya miaka elfu na moja kwa furaha kamili katika neema za peponi hakulingani sawa na saa moja ya furaha ya kuona uzuri wa mzuri subuhana. Basi wewe kwa hiyo ewe mwanadamu ni mwenye kurejea katika medani ya rehema yake, mwenye kuwa katika vizingiti vya diwani ya hadhara yake, uzuri na jamala unaouona kwa wapenzi wako wa majazi (sio hakika) unakuwa na shauku nao na kufitinika nao, bali si uzuri na jamala ambao unauona katika vyote vilivyomo duniani isipokuwa ni aina ya kivuli katika kudhihiri kwa jamala (s.w) na uzuri wa majina yake (s.w) na aina zote za shauku na mahaba kwa vilaini vyake na matamu yake. Na Huri wake na kasri zake si chochote hivyo isipokuwa ni udhihiri katika midhihirisho ya rehema zake (s.w) na aina zote za shauku na mahaba na kuvutika. Na vyenye kuvutia si chochote isipokuwa ni mwale katika mahaba ya huyo mwenye kuabudiwa mwenye kubakia na huyo mwenye kupendwa Msimaizi wa kila kitu.! Basi nyinyi ni wenye kwenda katika duru ya hadhi yake na makamo ya hadhara yake tukufu, nanyi kwa hiyo ni wenye kuitwa katika makao ya dhifa yake ya milele kwenda katika pepo ya kudumu milele. Basi msihuzunike, wala msilie wakati wa kuingia kwenu kaburini. Bali furahieni kheri na muipokee kwa tabasamu na furaha. Na neno hili linafuatilia jukumu lake katika kuzagaza nuru ya matumaini na bishara na linasema: Ewe mwanadamu! Usituhumu kuwa wewe unakwenda kwenye kutoweka, kukosekana, mchezo, giza kusahaulika, kufumuka, kuvunjika, kupasukapasuka, kuzama katika wingi na kukosekana. Bali wewe ni mwenye kwenda katika kubaki na sio katika kutoweka, na wewe unapelekwa katika uwepo wa kudumu na sio katika kukosekana, nawe unakwenda katika ulimwengu wa nuru na si katika giza, na wewe unakwenda kwa Mola wako na Mmiliki wa haki, na wewe unarudi katika makao makuu ya Mfalme wa ulimwengu, Mfalme wa uwepo. Utastarehe na kukunjuka katika medani ya Tawhidi kinyume na kughariki katika wingi milele, basi wewe ni mwenye kuelekea katika kukutana na kuungana na sio kuwa mbali na kutengana!

Private reading note

This note stays on this device and is never uploaded to a server.

Up to 1,200 characters