Risala hii inabainisha zaidi ya miujiza mia tatu ya Mtume mtukufu (s.a.w) yenye kujulisha ukweli wa Utume wake, nayo katika wakati ambao inaubainisha inatangaza nafsi yake kwamba ni karama katika karama za hiyo miujiza, ni kipawa katika vipawa vyake, hivyo na yenyewe imekuwa ni jambo lenye kufurutu ada la wazi kwa zaidi ya pande tatu. Kwanza: Utunzi wake ni tukio lenye kufurutu ada bila shaka, kwani imetungwa bila ya kurejea chanzo chochote, kwa kutegemea kumbukumbu tu pamoja na yaliyomo katika mapokezi ya Hadithi tukufu katika zaidi ya kurasa mia moja. Zaidi ya kuwa imeandikwa katika vilele vya milima na matumbo ya bustani, kwa muda unaokaribia siku nne na kwa kiasi cha saa tatu kwa siku, yaani katika saa kumi na mbili. Pili: Mwenye kuinakili hachoki kunakili kwa namna iwayo atakavyo inakili. Na kudumu kuisoma hakuondoi utamu wake pamoja na urefu, imeamsha hima za wavivu katika wenye kunakili, wakaandika – wakituzunguka – kiasi kinacho karibia nakala sabini - ndani ya mwaka mmoja, katika wakati huu mgumu, jambo ambalo limewapa ukinaifu kamili wenye kuziona hali zetu kwamba Risala hii ni moja katika karama za miujiza hiyo. Tatu: Hakika neno (Mtume mtukufu) (s.a.w) katika Risala yote, na neno (Qur’an tukufu) katika fungu la tano la Risala hiyo, yamewafikiana kwa waandishi wa nakala bila ya kuwa wanajua kuwepo kwa Tawafuq, na kuafikiana hukohuko kumetokea tena kwa waandishi wa nakala wanane wengine bila ya watu hawa kukutana na kabla ya kugundulika kwa kuafikiana kunako tajwa hata kwetu sisi. Basi ambaye ana chembe ya insafu hachukulii hili kuwa sadfa kabisa, bali kila aliyeona amekiri kuwa hii ni siri katika siri za ghaibu, na kwamba Risala hii ni karama katika karama za muujiza wa Muhammad (s.a.w) juu yake wingi wa rehema na amani. Hii na misingi ambayo inatangulia Risala hii ni muhimu sana, na kwamba Hadithi zilizopatikana katika Risala hiyo ukiachilia mbali kuwa kwake ni sahihi na yenye kukubalika mbele ya maimamu wa Hadithi, inabainisha mapokezi yenye uthabiti wa kukikanisha zaidi. Ikiwa tunataka kubainisha sifa pambanuzi za Risala hii tungehitaji Risala nyingine mfano wake, kwa ajili hiyo tunawatayarisha wenye kuwa na shauku ya hiyo kuisoma japo mara moja ili waguse wenyewe sifa hizo pambanuzi. Said Nursî Tanbihi Nimeleta Hadithi Sharif nyingi katika Risala hii, na sikua na chochote katika vitabu vya Hadithi, nikikosea katika tamko la Hadithi zilizopatikana isahihishwe au ichukuliwe kwa mapokezi kwa maana, kwani kauli yenye uzito: Kwamba inajuzu kusimulia Hadithi Sharif kwa maana yake, yaani msimulizi ataje maana ya Hadithi kwa tamko la kwake, makosa yoyote ya kimatamshi yatakayo kutwa katika Risala hii, basi yatazamwe kwa kuyazingatia (masimulizi kwa maana .
Source text is preserved. When a suitable model is available, translation is displayed separately.
Mektubat
The Nineteenth Letter
بِاس۟مِهٖ سُب۟حَانَهُ وَ اِن۟ مِن۟ شَى۟ءٍ اِلَّا يُسَبِّحُ بِحَم۟دِهٖ هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَكَفَى بِاللَّهِ شَهِيدًا ٭ مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّهِ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاء عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاء بَيْنَهُمْ تَرَاهُمْ رُكَّعًا سُجَّدًا يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّهِ وَرِضْوَانًا سِيمَاهُمْ فِي وُجُوهِهِم مِّنْ أَثَرِ السُّجُودِ ذَلِكَ مَثَلُهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَمَثَلُهُمْ فِي الْإِنجِيلِ كَزَرْعٍ أَخْرَجَ شَطْأَهُ فَآزَرَهُ فَاسْتَغْلَظَ فَاسْتَوَى عَلَى سُوقِهِ يُعْجِبُ الزُّرَّاعَ لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِنْهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا [Kwa kutazama kuthibitisha kwa (Neno la kumi na tisa) na la (Thelathini na moja) yanayohusu Utume wa Muhammad, Utume wa Muhammad (s.a.w) kwa dalili za kukinaisha, tunaelekeza huko suala la kuthibitisha na hapa tunabainisha - kuzikamilishia - ming’ao katika hakika hiyo kubwa ndani ya (Ishara kumi na tisa za fasaha na zenye maana)].
Hapana shaka kwamba mmiliki wa ulimwengu huu na Bwana mlezi wake anaumba anachoumba kwa ujuzi na anasarifu katika mambo yake kwa hekima, na kuendesha kila upande kwa kuona na kushuhudia, na kila kitu anakilea kwa ujuzi na busara, na anaendesha mambo akikusudia kudhihirisha, hekima, shabaha, na masilahi ambazo zinaonekana katika kila kitu. Maadamu muumbaji anajua, basi mjuzi anaongea. Na kwa kuwa yeye ataongea, basi maneno yake kwa vyovyote yatakuwa pamoja na anayeyafahamu katika wenye utambuzi, fikra na kudiriki, bali pamoja na mwanadamu ambaye ni mbora wa aina za wenye utambuzi na ufahamu na mwenye kukusanya sifa hizo zaidi. Na maadamu maongezi yake yatakuwa pamoja na aina ya mwanadamu, ataongea, kwa hiyo na watu wenye kustahiki kusemeshwa katika waliokamilika katika wanadamu ambao wana utayari wa juu na tabia za juu na wale ambao wanastahiki zaidi kuwa kigezo kwa jinsi ya mwanadamu na viongozi kwao. Basi hapana shaka kwamba atazungumza na Muhammad (s.a.w) ambaye wameshuhudia haki yake mawalii na mahasimu kuwa yeye ni mtu mwenye tabia za hadhi ya juu na maandalizi mazuri, na ambaye moja ya tano ya ulimwengu imemfuata, na wamejiunga chini ya bendera yake ya kimaanawy nusu ya Ardhi, na kuangaza mustakabali kwa nuru ambayo amepelekwa nayo ndani ya muda wa karne kumi na tatu, na ambaye watu wa Imani wanamswalia na wenye nuru katika watu daima na wanamwombea rehema, furaha, sifa na mapenzi, na wanafanya naye upya ahadi ya Utii kwake mara tano kila siku, na ameongea naye hasa. Na atamjaalia kuwa mtume wake bila ya shaka na amemjaalia hasa. Na atamjaalia kuwa ni kigezo na imamu wa watu wote na amemjaalia hivyo hasa.
Mtume Mtukufu (s.a.w) ametangaza unabii, na ametoa dalili juu ya hilo, nayo ni Qur’an tukufu. Na amedhihirisha kiasi cha miujiza elfu moja dhahiri, kama ilivyo thabiti kwa watu wa tahakiki katika wanazuoni. Miujiza hii kwa jumla yake yote ni thabiti kwa kukinaisha kama ukinaishi wa kuthibiti kwa madai ya unabii, hata kuhusisha miujiza na uchawi ambako kunaelezwa na Qur’an tukufu katika sehemu nyingi kwa ulimi wa makafiri wakubwa kunaashiria kwamba wao hawakukanusha kutokea kwa miujiza na hawakuweza hilo, lakini waliihusisha na uchawi kwa kujidanganya wao wenyewe na kuwadanganya wafuasi wao. Naam, hakika miujiza ya Muhammad (s.a.w) ni ya kukinaisha kikamilifu inafika nguvu ya tawatur mia moja, hakuna njia katu ya kuikanusha. Na miujiza kwa dhati yake ni kusadikisha kutoka kwa Mola mlezi wa viumbe wote kwa madai ya mjumbe wake mkarimu, yaani kana kwamba miujiza inasimama mahali pa kauli ya Allah (s.w): “Kasema kweli mja wangu basi mtiini”. Mfano Kwa Ajili Ya Kuweka Wazi Ukiwa kwenye hadhara ya mfalme au katika ikulu yake, na ukawaambia wanao kuzunguka: Mfalme ameniteua katika jambo fulani, na walipotaka dalili kutoka kwako juu ya madai yako mfalme yeye mwenyewe akaashiria: Kwamba naam, hakika nimemfanya kuwa mfanya kazi wangu. Je, huo haui ushahidi wa ukweli kwako? Na vipi ikiwa mfalme atavunja kawaida zake kwa ajili yako na kubadili kanuni zake kwa maombi kutoka kwako? Je, huko hakui ni kusadikisha kwenye nguvu zaidi kwa madai yako na kauli yenye uthabiti zaidi kuliko kusema: Naam? Na kadhalika madai ya Mtume (s.a.w) yalivyokuwa, wakati aliposema: Hakika mimi ni mjumbe kutoka kwa mola mlezi wa walimwengu. Ama dalili yangu ni kuwa (s.w) anabadili kanuni zake za kawaida kwa mwelekeo wangu na maombi yangu na tawasali yangu. Haya tazameni vidole vyangu, hakika anabubujiza maji kutoka kwenye vidole hivyo kama yanavyobubujika kwenye chemchem tano, na tazameni mwezi anaupasua kwa ajili yangu vipande viwili kwa ishara kutokea kwenye kidole changu, na tazameni mti ule namna unavyokuja kwangu kunisadikisha na kunishuhudia, na angalieni hili gao la chakula namna linavyoshibisha watu mia mbili au mia tatu! Na kama hivi Mtume (s.a.w) amedhihirisha mamia ya miujiza mfano kama hii. Na jua, kwamba dalili za ukweli wa Mtume (s.a.w) na hoja za unabii wake, haziishii katika miujiza yake, bali wachunguzi wanaona kuwa harakati zake, matendo yake, hali zake, kauli zake, tabia zake, hatua zake, mwenendo wake na sura yake, vyote hivyo vinathibitisha ikhlasi yake na ukweli wake. Hata wengi wakamwamini katika wanazuoni wa Bani Israil kwa kumwangalia tu mwonekano wake angavu. Mifano: Abdullah Bin Salam ambaye amesema: (Nilipobaini uso wake nikajua kwamba uso wake sio uso wa Mwongo). Na licha ya kuwa wanazuoni wahakiki wametaja kiasi kinacho karibia dalili elfu moja katika dalili za unabii wake na miujiza yake kuna maelfu ya hiyo, bali mamia ya maelfu. Wamesadikisha unabii wake mamia ya maelfu ya watu wenye kutofautiana katika fikira kwa mamia ya maelfu ya njia. Na Qur’an tukufu peke yake inadhihirisha elfu moja katika hoja juu ya unabii wake, zisizokuwa muujiza wake mkubwa kwa pande arobaini. Kwa kuwa unabii ni jambo la hakika lililothibiti katika jinsi ya wanadamu, na kwamba mamia ya maelfu ya wanadamu wamekuja na kutangaza unabii, na wameleta miujiza ushahidi na kuunga mkono kwa huo unabii, hapana shaka kwamba unabii wa nabii Muhammad (s.a.w) unakuwa thabiti zaidi na wenye mkazo zaidi kuliko wa wote, kwa kuwa eneo la unabii wa manabii na namna ya muamala wao na umati wao na dalili na sifa za kipekee na mazingira yaliyoijulisha juu ya unabii wa mitume wote kama Musa na Issa (a.s) zinapatikana kwa sura zake kamili na maana zake bora zaidi kwa Mtume mkarimu (s.a.w). Kwa kuwa hukumu ya unabii ni kamilifu na bora mno katika dhati yake (s.a.w), basi hukumu ya Utume hapana namna ni thabiti kwa ukinaifu wa wazi zaidi kuliko manabii wengine (a.s).
Hakika miujiza ya Mtume (s.a.w) ni mingi na aina mbalimbali mno, na hii ni kwa sababu ujumbe wake ni wa jumla kwa viumbe wote, kwa ajili hiyo katika aghalabu ya viumbe anayo miujiza inayomshuhudia, hebu tufafanue hilo kwa mfano: Lau balozi mtukufu angefika kutoka kwa mfalme mtukufu ili kuzuru mji wenye makazi ya watu mbali mbali, akiwa amewabebea zawadi za thamani mbali mbali, hakika kila kundi kati yao litamtuma katika hali hii mwakilishi wake kumpokea kwa niaba yake na kumkaribisha kwa ulimi wake. Kadhalika Balozi mkuu (s.a.w) wa mfalme wa azali na milele, alipoupa ulimwengu heshima, na kuunawirisha kwa kufika kwake akiwa ni mjumbe kutoka kwa Mlezi wa walimwengu kwa watu wote, akiwa amebeba pamoja naye zawadi za kimaanawy na hakika zenye nuru zinahusiana na hakika za viumbe wote, amemjia kutoka kila kundi ambaye anakaribisha ujio wake na kumpongeza kwa lugha yake mahususi, na kutanguliza mbele yake muujiza wa kundi lake kusadikisha unabii wake, na kuukaribisha, kuanzia kwenye jiwe, maji, mti na mwanadamu, na kumelea kwenye mwezi, jua na nyota, kana kwamba kila moja kati ya hivyo inakariri kwa ulimi wa hali: Karibu karibu kwa kutumwa kwako. Hakika somo la miujiza hiyo yote linahitaji vitabu vikubwa kwa wingi wake na kwa kuwa ni anuwai, wanazuoni wateule wametunga vitabu vikubwa kuhusu maelezo ya dalili za unabii na miujiza, isipokuwa sisi hapa tunatosheka na Ishara za jumla katika ambacho ni cha uthabiti wa kukinaisha na mutawatir kimaana katika aina za jumla ya miujiza hiyo. Hakika dalili za unabii wa Mtume (s.a.w) ni sehemu mbili: Kwanza: Hali ambazo zimeitwa kuwa ni Irhasati, nayo ni matukio yenye kufurutu ada ambayo yametokea kabla ya tume na wakati wa kuzaliwa. Pili: Dalili za unabii nyingine na hii inagawika katika sehemu mbili: Kwanza: Mambo yaliyofurutu ada ambayo yaliyodhihiri baada yake (s.a.w) kusadikisha Utume wake. Pili: Mambo yaliyofurutu ada ambayo yaliyodhihiri katika kipindi cha uhai wake wenye baraka (s.a.w). Na hii pia ni sehemu mbili: Kwanza: Yaliyodhihiri katika dalili za Utume katika haiba yake sira yake, sura yake, tabia zake na ukamilifu wa akili yake. Pili: Yaliyodhihiri kati ya hayo katika mambo ya nje ya dhati yake tukufu, yaani katika anga na ulimwengu. Na hii vilevile ni sehemu mbili: Sehemu ya kimaanawy na ki Qur’an. Na sehemu ya kimaada na kiulimwengu. Na hii ya mwisho ni sehemu mbili vilevile: Sehemu ya kwanza: Miujiza ambayo imedhihiri ndani ya kipindi cha Daawa ya Mtume (s.a.w), nayo ima kwa ajili ya kuvunja ukaidi wa makafiri au kutia nguvu imani ya waumini, kama kupasuka kwa mwezi, na kububujika maji kutoka katikati ya vidole vyake vitukufu, na kuwashibisha wengi kwa chakula kichache, na kuongea kwa mnyama, mti na jiwe. Na mfano wa hiyo katika miujiza ambayo inafikia aina ishirini, kila aina moja katika hizo ni kwa daraja ya Mutawatir ya kimaanawy, na kila aina kati ya hizo ina mifano mingi yenye kujirudiarudia. Sehemu ya pili: Matukio ambayo ameyaelezea (s.a.w) kabla ya kutokea kwake, kwa alivyomjulisha Allah (s.w), na yamedhihiri matukio hayo na yametokea kwa hakika kama alivyoelezea. Na sisi tunaanzia na sehemu hii ya mwisho ili kufikia katika faharisi yenye mtiririko wa ujumla.
Hakika aliyobashiri Mtume (s.a.w) katika habari za ghaibu kwa kujulishwa na Allah (s.w) mjuzi wa ghaibu ni mengi na hayahesabiki wala kudhibitika. Hakika tumeashiria aina zake katika (Neno la ishirini na tano) linalohusu muujiza wa Qur’an, na huko tumeweka hoja zake, kwa hiyo basi habari za ghaibu zinazoambatana na nyakati zilizopita, manabii waliotangulia, hakika za kiungu na hakika za ulimwengu, na hakika za akhera kuhusu hizo lirejewe neno hilo. Ama hapa tutaleta mifano michache katika habari za ghaibu za kweli zinahusu matukio ambayo yatawasibu jamaa na masahaba – (r.a) wote - baada yake na utakayoyakuta uma wake katika siku zake za usoni. Na ili kufikia katika kutambua hakika hii utambuzi kamili mbele yake tunabainisha misingi sita ikiwa ni utangulizi wake.
Hali zote za Mtume (s.a.w) na hatua zake zinaweza kuwa ni dalili juu ya ukweli wake na ushahidi juu ya unabii wake, isipokuwa hii haina maana kuwa hali zake zote na matendo yake ni yenye kufurutu ada, hii ni kwa kuwa Allah (s.w) amemtuma akiwa ni mwanadamu mtume, ili awe kwa matendo yake na harakati zake zote ni imamu na kiongozi kwa watu wote, na katika hali zao zote, ili aweze kuwapatia kwayo furaha ya dunia na akhera na ili awabainishie mambo yaliyofurutu ada ya ufundi wa mola mlezi na usarifu wa uweza wa mola mwaabudiwa wa haki katika mambo yaliyozoeleka, yale mambo ambayo yenyewe kwa dhati yake ni miujiza. Angekuwa Mtume (s.a.w) katika matendo yake yote ni mwenye kufurutu ada, nje ya hali ya kibinadamu, isingekuwapo fursa kwake kuwa ni kigezo cha kuigwa, na asingeweza kwa matendo yake, hali zake na hatua zake kuwa imamu kwa wengine. Na kwa ajili hii hakuwa akielekea katika kudhihirisha miujiza isipokuwa kati ya zama na nyingine, wakati wa haja, kuthibitisha unabii wake mbele ya wapingaji makafiri. Na ilipokuwa mtihani na majaribio ni katika yanayohitajika kwa takilifu ya kiungu, muujiza haukuwa ni wenye kulazimisha kusadiki - yaani sawa mtu ametaka au hakutaka - kwa sababu siri ya mtihani na hekima ya takilifu vyote vinahitajia kufungua uwanja wa hiari mbele ya akili bila kuipokonya utashi. Kama muujiza ungedhihiri kwa waziwazi wenye kuilazimisha akili kama ilivyo hali ya vitu vya wazi, akili isingekuwa na hiari hapo, na angesadiki Abu Jahali kama alivyosadiki Abu Bakar (r.a), na isingekuwepo faida ya takilifu na shabaha ya mtihani, na vingekuwa sawa mkaa duni na almasi ya thamani! Pamoja na kuwa kinachoamsha mshangao ni kwamba katika wakati ambao maelfu ya mataifa mbalimbali ya watu wameamini kwa muujiza wake au kwa maneno yake au kwa kutazama mwonekano wake angavu, au yanayoshabihiana na hayo katika dalili za ukweli wa unabii wake, na wamemwamini maelfu ya wanazuoni wachunguzi na wahakiki, kwa yaliyonakiliwa kwao katika ukweli wa habari zake na uzuri wa athari zake unakili sahihi wa tawatur, ninasema: Hivi haisababishi ajabu waovu wa zama hii kuona dalili zote hizi zilizo wazi kana kwamba hazitoshelezi kwao kuamini na kusadiki unawaona wanateleza katika shimo la upotevu?
Hakika Mtume mtukufu (s.a.w) ni mtu, yeye anaishi na watu kwa mujibu wa utu wake huu. Na yeye vilevile ni Mtume, na kwa muktadha wa Utume yeye ni msemaji mwaminifu kwa jina la Allah (s.w) na mfikishaji mwaminifu wa amri zake (s.w), basi ujumbe wake unaegemea katika hakika ya wahyi. Na wahyi ni mafungu mawili: Kwanza: Wahyi wa wazi kama Qur’an tukufu na baadhi ya Hadithi Qudusi. Mtume katika hili yeye ni mfikishaji tu na si vinginevyo, bila ya yeye kuwa na usarifu au kuingilia kitu katika huo. Pili: Wahyi wa kimadhumuni, ni ambao unaegemea katika muhtasari wake na ufupi wake na ujumla wake katika wahyi na ilhamu, isipokuwa katika upambanuzi wake na taswira yake unarejea kwa Mtume (s.a.w). Basi upambanuzi wa tukio lijalo kwa muhtasari kutoka katika wahyi huu na taswira yake ima anabainisha Mtume (s.a.w) wakati mwingine kwa kuegemea katika ilhamu au kwenye wahyi, au anaubainisha kwa firasa yake ya kibinafsi. Na upambanuzi huu anaoubainisha Mtume (s.a.w) kwa jitihada yake ya binafsi, ima anaubainisha kutokana na hali aliyo nayo ya nguvu ya kiutakatifu ya hali ya juu kwa mujibu wa Utume, au anaubainisha kwa sifa zake mahususi za kibinadamu na kwa kiwango cha mazoea, kawaida na fikira za watu. Na kama hivi haitazamwi katika upambanuzi wote wa kila Hadithi kwa mtazamo wa wahyi mtupu tu. Wala hazifuatiliwi athari za hadhi ya juu za Utume katika miamala yake (s.a.w) na fikira zake ambazo zinakwenda kwa miktadha ya kiutu. Na kwa kuwa baadhi ya matukio anafunuliwa wahyi kwa ujumla na kwa hali zote na yeye kwa nafasi yake anausawiri kwa firasa yake ya kibinafsi au kulingana na mtazamo wa mazoea ya jumla, kwa hiyo wakati mwingine inalazimu kutafsiri na huenda kuelezea hizi zilizoshabihiana na zenye mushkeli iliyomo katika huko kusawiri. Kwa sababu baadhi ya hakika hukaribishwa katika akili kwa kufananisha. Mfano wa hizo ni: Watu walisikia – mara moja – na hali ya kuwa wamekaa kwa Mtume (s.a.w) kishindo kikubwa, Mtume (s.a.w) akasema akifafanua Hadithi: (Hili ni jiwe limetupwa kwenye moto tangu miaka sabini linaanguka kwenye moto hivi sasa hadi limefika katika kina chake), haikupita saa hadi likaja jibu, ambapo alikuja mmoja wao akisema: Hakika mnafiki mashuhuri ambaye amefikia miaka sabini katika umri wake ameshakufa na kuelekea jahanamu na ubaya uliyoje wa mafikio, hii ikawa ni ta’wili (Tafsiri ya undani) ya tashbiha fasaha aliyoieleza Mtume (s.a.w).
Hakika athari zilizonakiliwa zikiwa ni mutawatir ni za uthabiti wa kukinaisha na zinafidisha yakini. Na tawatur ni sehemu mbili: Kwanza: Tawatur ya wazi, au tawatur ya kitamko. Pili: Tawatur ya kimaana na hii ni sehemu mbili: Kwanza: Ya kunyamaza, yaani kuonesha kuridhia kwa kunyamazia. Mfano wa hilo: Lau mtu angewaeleza jamaa zake kuhusu tukio lililotokea mbele yao na hawakumkadhibisha katika maelezo yake bali waliyakabili kwa kunyamaza, hilo lina maana ya kukubali kwao kutokea kwa jambo hilo, na hasa ikiwa tukio linalosimuliwa lina uhusiano na jamaa hao, na jamaa hao wako tayari kukosoa na kukanusha na kuonesha ila, na kutoka kwa watu ambao hawakubali makosa asilani, bali wanaona uongo ni jambo baya kabisa, kulinyamazia kwao inajulisha juu ya kutokea kwa tukio hilo kwa namna ya kukinaisha. Sehemu ya pili: Katika tawatur ya kimaanawy: Ni kuafikiana kwao kwa kiasi cha kushirikiana kati ya habari zao hata ikiwa masimulizi ni aina mbali mbali. Mfano wa hilo: Ikisema wakia moja ya chakula imewashibisha watu mia mbili. Ambao wame Hadithia hili wanasimulia katika sura anuwai na kwa ibara tofauti mbali mbali. Huyu ametaja watu mia moja na mwingine watu mia tatu na mwingine wakia mbili za chakula na kama hivi. Utaona wote wanaafikiana juu ya kutokea kwa tukio, nalo ni kuwa chakula kichache kimeshibisha watu wengi. Kwa hiyo tukio kwa namna yake kwa hali zote ni mutawatir kimaana, na hiyo inafidisha yakini, na haidhuru sura za hitilafu. Na katika baadhi ya nyakati habari ya mpokezi mmoja kwa kutegemea baadhi ya masharti inafidisha hukumu ya kukinaisha kama kukinaisha kwa mutawatir, na inaweza kufidisha kukinaisha mara nyingine chini ya alama za nje. Kama hivi sehemu kubwa mno katika yaliyonakiliwa kwetu katika dalili za unabii na miujiza ya Mtume (s.a.w) ni kwa: Tawatur ya wazi au ya kimaanawy au ya ukimya, na sehemu kati yake ni habari za Aahadi. Isipokuwa ni ndani ya masharti maalum yenye kuchujwa vyema huchukuliwa na kukubaliwa mbele ya maimamu wa Al-Jarhi wa At-Ta’diili katika wanazuoni wa Hadithi za Mtume (s.a.w), na hapo huwa dalili ya ni ya kukinaisha kama Tawatur. Hapana shaka ikwa wanazuoni wa Hadithi wahakiki katika wenye sahihi sita na wamekubali Hadithi za Aahadi na mbele yao ni (Al-Bukhary) na (Muslim) na ni mahafadhi bingwa ambao walikuwa wakihifadhi kiasi kisichopungua Hadithi mia moja elfu, na wakiridhia maelfu katika maimamu wachamungu, katika ambao wanaswali swala ya Al-Fajiri kwa udhu wa swala ya Ishaa kiasi cha miaka hamsini katika umri wao. Nasema: Ikiwa wamekubali hawa usahihi wa habari za Aahadi, basi hapana shaka kwa hiyo katika kukinaisha kwake na hukumu yake haiwi chache kulinganisha na tawatur yenyewe. Naam, hakika wanazuoni wa elimu ya Hadithi na wachambuzi wake wamebobea katika fani hii kwa kiwango cha kwamba wamepata uwezo katika kujua hadhi ya juu ya maneno ya Mtume (s.a.w) na balagha ya maelezo yake, na mtindo wa kufidisha kwake, wakawa wanaweza kuyapambanua kati yake na maneno mengine, kwa kiasi ambacho lau wangeiona Hadithi Maudhui baina ya Hadithi mia moja wangeikataa kwa kusema: Hii ni Maudhui!. Hii haiyumkiniki kuwa Hadithi Sharif! Wamekuwa kama masonara hodari wa asili wanajua johari ya Hadithi ya nabii na maneno mageni yaliyoingia ndani yake. Licha ya kuwa sehemu ya wahakiki wamepitiliza katika kukosoa Hadithi kama (Ibn Al-Jawzy) ambaye alihukumu Hadithi sahihi kuwa ni Maudhui. Hali ya kujua kwamba (Maudhui) inamaanisha: Kwamba maneno haya sio maneno ya Mtume (s.a.w), na haina maana kwamba maneno hayo ni batili na hayafai. Swali: Nini faida ya sanadi ndefu: Kutoka kwa fulani, kutoka kwa fulani, kutoka kwa fulani, ambapo hakuna faida katika kuwataja kwenye tukio linalojulikana? Jibu: Faida ni nyingi, hakika ya kutaja sanadi hii ndefu inabainisha aina katika ijmaa katika ambao wamo kwenye sanadi katika wenye kuaminika wa kweli katika wasimulizi ambao wanategemewa, inatudhihirishia aina ya kuungana na kuafikiana kwa watu wa elimu wenye kuhakiki katika sanadi, kana kwamba kila imamu na mwanazuoni anasaini katika hukumu ya Hadithi hiyo na anatia muhuri wa usahihi wake kwa kutia kwake muhuri wake. Swali: Kwa nini haikunukuliwa (Miujiza) kwa umuhimu mkubwa kama ilivyonakiliwa hukumu za kisharia za kidharura nyinginezo kwa kunukuu kwa mutawatir na kwa njia tofauti?. Jibu: Ni kwa kuwa wengi mno ya watu katika aghalabu ya nyakati wanahitajia sana hukumu za kisharia, hizo ni (kama faradhi za aina) kwao. Kwa vile yalivyo na uhusiano kwa kila mtu. Wakati miujiza haihitajii kila mtu kila wakati. Hata tungekadiria kuwepo haja yake, basi inatosha kuisikia mara moja, hiyo ni (Kama faradhi kifaya) ambayo inatosha kuijua kwa kawaida sehemu ya watu. Na kwa sababu hii inaweza kutokea kuona kutokea kwa moja ya miujiza hali ya kuthibiti kwa kukinaisha kwenye nguvu kuliko kukinaisha kwa kuthibiti kwa hukumu ya kisharia kwa maradufu ya maradufu, isipokuwa msimulizi wake ni mtu mmoja au watu wawili, wakati ambao idadi ya wasimulizi wa hukumu hiyo ya kisheria ni kumi au kumi na moja.
Hakika ya sehemu ya matukio ya mustakabali ambao ameielezea Mtume (s.a.w) ni matukio ya kiujumla, yanakariri katika nyakati tofauti, na sio tukio la kisehemu moja. Kwa hiyo Mtume (s.a.w) anaweza kuelezea tukio hilo la kiujumla kwa sura ya kisehemu akibainisha baadhi ya hali zake, ambapo mfano wa tuko hili la kiujumla lina pande nyingi, Mtume (s.a.w) anabainisha kila mara upande mmoja katika pande zake. Lakini katika kukusanya pande hizi kwa msimulizi wa Hadithi katika mahali pamoja, inaonekana kuwepo na kinachoshabihiana na tofauti na uhalisia. Mfano wa hilo: Kuna mapokezi tofauti kuhusu (Al-Mahady) yanatofautiana humo maelezo na taswira. Mtume (s.a.w) ameeleza kuhusu kudhihiri kwa Al-Mahdy kwa kuegemea wahyi, ili alinde nguvu ya watu wa Imani ya kimaanawy kila zama, na ili azuilie dhidi ya kudondoka kwao katika kukata tamaa kwa matukio ya kutisha wanayoyaona, na ili kuwafunga uma kwa mafungamano ya kimaanawy kwa mnyororo wa kinuru wa Ahlul Bayt. Tumethibitisha hilo katika moja ya matawi ya (Neno la Ishirini na Nne). Na kutokea hapa unaona kwamba kila zama katika zama amepatikana aina ya (Al-Mahdy) katika Ahlul Bayt kama ambaye atakayedhihiri mwisho wa zama, bali kina Mahdy, hata amepatikana katika Mahdy wa Al-Abbasy – ambaye anahesabiwa katika Ahlul Bayt – nyingi ya sifa za Mahdy huyo mkuu. Na kama hivi, sifa za wale wanaomtangulia Al-Mahdy mkubwa katika wanaowakilisha katika enzi zao, kama Makhalifa waongofu na Maqutub waongofu, zimechanganyika na kuingiliana na sifa za huyo Mahdy mkubwa. Ikatokea tofauti katika Riwaya.
Hakuwa Mtume mtukufu (s.a.w) anajua ghaibu ambayo Allah (s.w), hajamjulisha kwani hajui ghaibu isipokuwa Allah (s.w) yeye (s.a.w) anawafikishia watu aliyomjulisha Allah (s.w). Na kwa kuwa Allah (s.w) ni Mwingi wa hekima Mwenye kurehemu, basi hekima na rehema yake zinahitajia kusitiri mengi ya mambo ya kighaibu na kuyabakisha katika kifuniko cha kificho na kutojulikana, kwa sababu yasiyomfurahisha mwanadamu katika matukio ya hii dunia ni mengi kuliko yanayomfurahisha, kuyajua mambo hayo kabla ya kutokea kwake ni jambo la kuumiza mno. Basi kwa ajili ya hekima hii umauti na muda uliyopangwa ni vitu visivyojulikana vimesitiriwa mbali na ujuzi wa mwanadamu, na yamebaki yale yatakayomsibu mwanadamu katika masaibu na majanga yamefunikwa katikati ya ghaibu, ikawa muktadha wa hekima hii ya kiungu mola mlezi na Rehema ya kiungu Mwaabudiwa wa haki asimwoneshe Mtume wake kwa namna ya kiujumla na kwa upambanuzi watakayoyakuta ali zake na sahaba zake na umati wake baada yake katika matukio ya kuumiza na masaibu yakuhuzunisha. Bali Allah (s.w) amempa habari ya baadhi ya matukio muhimu – kwa msingi wa hekima maalum - upashaji habari usiohuzunisha, kwa kufanyia upole yale anayobeba katika rehema kubwa na huruma kubwa kwa umati wake na kwa ali zake na sahaba zake. Kama vilevile yeye (s.w) amembashiria matukio ya kufurahisha vilevile kwa bishara ya jumla kwa baadhi yake na nyingine yenye kupambanuliwa basi Mtume (s.a.w) aliwaeleza umati wake kwa aliyomjulisha mola wake mlezi na wameyanakili wanazuoni wa Hadithi wa kweli waadilifu kwa masimulizi sahihi kwetu, wale ambao walikuwa na ucha mungu mkubwa na kwa kuhofia kuwasibu mikemeo ya kutisha katika kauli yake. (s.a.w): (Mwenye kunisingizia kwa makusudi basi na aandae makalio yake motoni) na ambao walikuwa wanakimbia kwa hofu isiwapate aya tukufu: فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن كَذَبَ عَلَى اللَّهِ
Hakika hali za Mtume (s.a.w) na sifa zake zimebainishwa kwa namna ya Sira na historia, Isipokuwa aghalabu ya hali hizo na sifa zinaakisi hali yake ya kiutu tu, ambapo haiba ya kimaanawy ya hiyo dhati ya kinabii iliyobarikiwa ni ya hali ya juu sana na Ainisho lake takatifu ni la kinuru kiasi kwamba yaliyotajwa katika historia na sira katika sifa na hali hazifikii makamo ya hadhi hiyo na ngazi hiyo ya juu sana, kwa sababu yeye (s.w) kwa mwanga wa msingi wa (Sababu ni kama mtendaji) huongezwa kila siku, hadi sasa, katika daftari la makamilifu yake ibada kubwa kiasi cha ibada za umati wake kwa ukamilifu wake. Na kama anavyopata kwa maandalizi yasiyo na ukomo tunu za rehema za kiungu mola mwaabudiwa wa haki, vilevile anapata kila siku dua isiyo na mpaka kwa wasio na mpaka katika umati wake. Huyu Nabii mwenye kubarikiwa (s.a.w) ambaye ni natija bora kabisa ya viumbe na ni tunda lake lililokamilika zaidi na mfikishaji kutoka kwa Muumba wa ulimwengu, na kipenzi cha Mola mlezi wa walimwengu, hali zake na hatua zake za kiutu ambazo vitabu vya sira na historia vimeeleza hazifikii kuzungukia ainisho lake kamili na wala hazifiki katika hakika za makamilifu yake. Wapi na wapi haiba hii yenye baraka ambayo wote walikuwa kuanzia Jibrili, Mikaili ni wenye kusuhubiana naye waaminifu katika vita vya Badri idhibitike katika hali ya kidhahiri au tukio la kibinadamu liioneshe kwa dhahiri kama tukio lililotokea na mwenye farasi ambaye Mtume (s.a.w) alimnunua farasi kutoka kwake lakini alikana kuuza huko na akataka shahidi kutoka kwa Mtume (s.a.w) wa kumsadikisha akajitokeza sahaba mtukufu (Khuzaymah) kumshuhudia. Ili mtu yeyote asiingie katika kunyemelewa na kosa inalazimu kwa anaye sikia sifa zake za kiutu za kikawaida daima anyanyue macho yake juu ili aangalie ainisho lake la hakika, na haiba yake ya kimaanawy ya kinuru kubwa katika kilele cha ngazi ya Utume, na kama sio hivyo ataleta adabu mbaya, na kuingia katika utata na dhana. Na ili kufafanua suala hili zingatia mfano huu: Kokwa ya tende imewekwa chini ya mchanga ikapasua ikapasukana kutoa mtende wenye kuzaa matunda kochokocho, na unaendelea kupanuka na kukua kwa tambo, au yai la tausi limevunjwa na kutoa kifaranga cha tausi baada ya kuelekezewa joto, na kila anapokuwa huwa mzuri zaidi na kupendeza, kwa vile ambavyo kalamu ya uweza ilivyopamba pande zake zote nakshi za ajabu zenye kupendeza. Kuna sifa na hali maalum zinarejea kwa vyote katika ile kokwa na lile yai, kila moja kati ya hayo mawili yanabeba maada nyeti pole sana. Na mtende na tausi vilevile vina sifa za juu na namna na hali za juu kulinganisha na sifa za mbegu na yai. Zinapofungamanishwa sifa za kokwa na yai na sifa za mtende na ndege na kutajwa kwa pamoja, inapasa akili ya mwanadamu inyanyue jicho lake mbali ya kokwa kwenda kwenye mtende na kuutazama, na kuelekea kutoka kwenye yai hadi kwenye tausi na kuchunguza kwa makini, ili akubali hizo sifa ambazo anazozisikia. Na kinyume na hivyo atasombwa katika kukadhibisha wakati anapomsikia mmoja wao anasema: (Nimechukua tani ya tende kutokana na gao la kokwa, au hili yai ndio mfalme wa ndege). Na kama hivi ubinadamu wa Mtume Mtukufu (s.a.w) unashabihiana na hiyo kokwa au yai (katika mfano). Na Ainisho lake linalozagaza jukumu la Utume mfano wake kama mfano wa mti wa Tuba wa peponi na ndege wa peponi katika kuwa na hadhi ya juu. Kwa hiyo katika wakati ambao tunafikiri ugomvi ambao ulitokea sokoni pamoja na bedui, inapasa tuinue juu jicho la mawazo na tutasawari dhati ya kinuru yenye kupaa na kupendeza (Buraqi) na yenye kuondoka kuelekea kwenye ukaribu wa Upinde na mshale au karibu zaidi, akimwacha nyuma yake Jibrili (a.s). Na kama sio hivyo nafsi yenye kuamrisha uovu ima italeta adabu mbaya na kuanguka katika ngazi ya uchache wa heshima, au mguu wake kuteleza katika kutosadiki.
Nayo inahusu matukio yenye kuhusiana na mambo ya kighaibu, tunataja mifano michache katika hayo: Mfano wa kwanza: Amesema Mtume wa Allah (s.a.w) katika hotuba katikati ya mkusanyiko wa masahaba (r.a), na Hadithi hiyo imenakiliwa kwetu unakili sahihi na wa mutawatir: (Hakika mwanangu huyu ni Bwana na huenda Allah (s.w) akasuluhisha kwa (Mwanangu huyu) baina ya makundi mawili miongoni mwa Waislamu) na katika mapokezi mengine (Makubwa). Na baada ya kupita miaka arobaini yamekutana majeshi mawili makubwa ya Waislamu, Hasani akafanya suluhu na Muawiya (r.a), kwa suluhu hii akawa amesadikisha muujiza wa kighaibu wa Babu yake Mtukufu (s.a.w). Mfano wa pili: Imethibiti kwa unakili sahihi kwamba (s.a.w) alimwambia Ali (r.a): Utapigana na wahalifu wa ahadi waliokwenda upogo na waliotoka nje ya dini. Akaelezea kuhusu tukio la Al-Jamal, Siffain na kuhusu Al-Khawarij. Na amesema (s.a.w) kumwambia Az-Zubayr: (Kwa hakika utamuua na hali ya kuwa wewe ni dhalimu) alipomwona na Ali (r.a) wanapendana. Na amesema (s.a.w) kuwaambia wakeze Wataharifu: (Vipi ikiwa mmoja wenu wanambwekea mbwa wa Al-Hauabu) (kuliani kwake na kushotoni kwake wanauliwa watu wengi). Na baada ya miaka thelathini Hadithi hizi sahihi zimethibiti kwa hakika kimatendo kabisa, na hilo ni katika tukio la Al-Jamal ambalo lililopita baina ya Ali na aisha akiwa pamoja naye Talha na Az-Zubayr (r.a), kama lilivyotokea kwa hakika katika tukio la Siffain ambalo lilitokea kati ya Ali na Muawiya (r.a), na imetokea kwa hakika katika tukio la Haruraa na Naharwani lilikuwa kati ya Ali (r.a) na Al-Khawarij. Na Mtume (s.a.w) alimweleza Ali (r.a) kuhusu atakayemuua akasema: (Ambaye atakupiga ewe Ali kwa huu mpaka urowe kwa hii) yaani zirowe ndevu zake kwa damu ya kichwa chake na Ali alikuwa anamjua, naye ni Abdul-Rahman Ibn Muljim Al-Khawarij. Vilevile ameelezea kuhusu mwenye matiti kwa alama yenye kutenganisha kwake, kwamba atakuwa baina ya wauliwa wa Khawariji na kweli alikuwa mwenye matiti kati yao naye ni (Mwanamume mweusi moja katika mifupa panya yake miwili ni mfano wa titi la mwanamke). Ali (r.a) akamjaalia huyo kuwa ni hoja juu ya kuwa yeye ni mwenye haki, na akatangaza kuhusu muujiza wa Mtume mtukufu (s.a.w). Na ameeleza Mjumbe wa Allah (s.a.w) kwa mapokezi sahihi kutoka kwa Ummu salamat na wengine: Kwamba Husein atauawa katika mahali panapoitwa Al-Taffu yaani Karbala. Na baada ya miaka hamsini ikatokea huzuni hiyo ya kuumiza, likasadikisha maelezo hayo ya kighaibu. Na alielezea akiwa anakariri (s.a.w): (Hakika watu wa nyumbani mwangu baada yangu watapata mauaji na kutolewa kutoka kwa umati wangu), na ikawa kama alivyoeleza. Hapa Linakuja Swali muhimu Inasemwa: Kwamba Ali (r.a) alikuwa anastahiki zaidi kuwa khalifa na mbora zaidi kwa huo Ukhalifa, kwani yeye ni mwenye udugu na Mtume (s.a.w), na mwenye ushujaa wa nadra wenye kufurutu ada, na mwenye elimu nyingi. Basi kwa nini hawakumtanguliza katika Ukhalifa? na kwa nini hali za Waislamu zikawa za migogoro katika kipindi chake? Jibu: Amesema Qutbu mkubwa katika watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w): Mtume (s.a.w) alikuwa anatamani Ali awe ndiye khalifa, lakini alijulishwa kutoka kwenye ghaibu kwamba matakwa ya Allah (s.a.w) sio hivyo, akaachana na matakwa yake kwa kufuata anachotaka Allah (s.w). Na katika yafuatayo kuna hekima moja ambayo imo katika matakwa ya Allah (s.w) kwenye jambo hili: Masahaba wema (r.a) walikuwa ni wahitaji mno kuafikiana na kuungana baada ya kuwa Mtume (s.a.w) ameondoka kwa Rafiki wa hadhi ya juu, lau angekuwa Ali (r.a) ametawala Ukhalifa, kungekuwa na uwezekano wenye nguvu kuamsha mielekeo yake yenye sifa za kutoendana na wengine na kujitenga kwa rai zake pamoja na kuipa nyongo kwake dunia, na ushupavu wake wa nadra na kutowahitajia kwake watu, ukiachilia mbali ushujaa wake wa hali ya juu, – sifa hizi za pekee – zikatikisa mshipa wa ushindani kwa watu wengi na makabila mengi, na kupelekea mfarakano kati ya safu za Waislamu, kama ilivyotokea katika kipindi cha Ukhalifa wake matukio na fitina mbalimbali. Ama sababu ya kucheleweshwa Ukhalifa wa Ali (r.a) moja ya sababu zake ni hii ifuatayo: Vimbunga vya fitina vilivuma katikati ya Umati wa Uislamu ambao unakusanya watu mbalimbali katika fikira na ambao kila moja inabeba mbegu za faraka katika makundi sabini na tatu, kama alivyoelezea Mtume (s.a.w), hivyo ilikuwa inatakikana uwepo wa haiba yenye nguvu ya kipekee, yenye upande wa haiba, yenye ushujaa wa hali ya juu na firasa kali na nasaba yenye kwenda mbali na asili kubwa katika watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w) na katika Bani Hashim, ili asimame thabiti mbele ya fitina hizi. Mfano wa haiba hii ya kipekee, ilikuwa inapatikana kwa Ali (r.a), akathibiti kihakika mbele ya vimbunga hivyo vikubwa. Na Mtume (s.a.w) alimweleza hilo atapigana katika njia ya kuawili (Tafsiri ya ndani) Qur’an kama yeye (s.a.w) alivyopigana katika njia ya kuteremka kwake. Kisha isingekuwa Ali (r.a) huenda ufalme wa dunia unawasukuma bani Umayya na kuwafitini kiujumla, na kuwatelezesha na njia ya sawa, lakini kwa kuwa walikuwa wanaona mbele yao kuna Ali na watu wa nyumbani mwa Mtume (s.a.w), walijitahidi kufikia kilele chao na kulingana nao katika nafasi zao ili wasikose ngazi yao katika mtazamo wa umati, wakalazimika aghalabu ya viongozi wa dola ya bani Umayya katika kuwahimiza wafuasi wao kusimamia uhifadhi wa Imani na kuieneza na kulinda hukumu za Qur’an na Uislamu, licha ya kuwa wao hawakufanya chochote wao wenyewe, kwa ajili hiyo walichipukia katika kivuli cha dola yao mamia ya maelfu ya wanazuoni wahakiki mujitahidina na maimamu wa Hadithi na mawalii wema na wateule na watendaji, na bila ya makamilifu wanayosifika nayo Ali Bayti na wema wao na Uwalii wao kwa Allah (s.w), Bani Umayya wangeteleza na kuwa mbali kabisa na njia ya haki, kama yalivyoishia mambo yao mwishoni mwa siku zao, na kama ilivyotokea mwishoni mwa siku za Al-Abbasiyyin. Ikisemwa: Kwa nini Ukhalifa haukutulia kwa watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w), hali ya kujua kwamba wao ni wenye haki zaidi kwa ukhalifa? Jibu: Hakika ufalme wa dunia unahadaa sana, wakati ambapo watu wa nyumba ya Mtume wamekalifishwa kuhifadhi hakika za Uislamu na hukumu za Qur’an. Inatakikana kwa anayepokea hatamu ya ukhalifa wa dunia isimdanganye, kama kuwa maasumu kama Mtume (s.a.w), au kuwa mwenye uchamungu mkubwa, mwenye kuipuuza dunia sana kama makhalifa waongofu, Umar bin Abdil-Azizi na Al-Mahady wa Al-Abbasy ili asidanganyike. Kwa hiyo ufalme wa dunia haufai kwa Ahlul Bayt, kwa sababu unawasahaulisha jukumu lao la msingi, nalo ni kuihifadhi dini na kuhudumia Uislamu. Na ukhalifa wa Dola la Fatimiyya amabalo lilisimama kwa jina la Ahlul Bayt huko misri, na serikali ya Muwaheddin huko Afrika, na Dola ya As-Safawiyya Irani, kila moja kati ya hizo imekuwa hoja kwamba ufalme wa dunia haufai kwa watu wa nyumba ya Mtume. Wakati ambapo tunawaona pale ambapo wameacha ufalme, wamejitahidi kwa pupa na wamejitolea juhudi isiyo na kifani katika kuhudumia Uislamu na kuinua bendera ya Qur’an. Ukitaka zingatia Maqutubu ambao wamekuja kutokana na uzao wa Hasan (r.a), hasa Maqutubu wanne, na hasa Sheikh Al-Kaylany. Basi ukitaka zingatia pia maimamu ambao wamekuja kutoka katika Uzao wa Husein (r.a), hasa Zainul AI-Abidin na Jaafar As-Sadiq na mfano wa hao, kila mmoja kati yao amekuwa sawa na Al-Mahdy wa kimaanawy, walitokomeza dhuluma na magiza ya kimaanawy kwa kueneza kwao nuru za Qur’an na hakika za Imani, na wakathibitisha kweli kuwa wao ni warithi wa Babu yao Mtukufu sana (s.a.w). Ikisemwa: Nini hekima ya fitina ile ya damu ya kutisha ambayo imewasibu umma wa kiisalimu katika enzi za waongofu na karne bora, ambapo hailingani kwa hao wema kutumia mabavu na kuteremka kwa masaibu na wapi inapatikana sura ya Rehema ya kiungu katika hilo? Jibu: Kama zilivyo mvua nyingi zinazofuatana na vimbunga katika majira ya machipuo huamsha mazingira ya ukubalifu wa kila kundi katika makundi ya mimea na kuyabainisha na hivyo kueneza mbegu na kutupa kokwa, na kufunguka maua yake yanayohusiana nayo, kila moja kati ya hayo hupokea jukumu lake la kimaumbile, Vivyo hivyo ile fitina ambayo waliojaribiwa nayo masahaba wema na wafuasi (r.a), imeamsha mbegu za vipaji vyao mbalimbali, na kuhamasisha kokwa za ukubalifu wao aina kwa aina, kila kundi likaonya kila kundi kati yao na kuwahofisha kwamba hatari inaunyemelea Uislamu, na kwamba moto utaripuka katika safu za Waislamu, jambo lililofanya kila kundi likimbilie katika kuhifadhi dini na kukinga imani, kila mmoja akachukua katika ahadi yake jukumu moja katika majukumu ya kuhifadhi imani na kukusanya muungano wa Uislamu, kila mmoja kulingana na ukubalifu wake, akaenda kwa kila juhudi na ikhlasi katika njia hii. Kati yao wapo waliohifadhi Hadithi Sharif za Mtume (s.a.w), kati yao wapo waliohifadhi Fiqh ya Sharia angavu, na kati yao kuna aliyehifadhi itikadi na hakika za kiimani, kati yao kuna aliyehifadhi Qur’an tukufu, na kama hivi kila kundi lilijiweka chini ya jukumu na wajibu katika mambo ya wajibu ambayo yanalazimisha uhifadhi wa imani na kulinda Uislamu, na limekwenda mbio katika njia ya kutekeleza jukumu lake kwa jitihada sana, kutokana na mbegu ambazo zimeenezwa na vimbunga vinavyovuma vikali katika pande mbalimbali, maua ya kupendeza kwa rangi za kuvutia mbalimbali katika ulimwengu wa Kiislamu yakafunguka, hadi ulimwengu wa Kiislamu ukageuka kuwa ni bustani zilizostawi kwa mawaridi na mirihani. Isipokuwa – kwa masikitiko - kumedhihiri kati ya hizo bustani za kupendeza miba ya watu wa bidaa vilevile. Na kana kwamba mkono wa Uweza wa kimungu mmoja wa haki imetunuku zama hizo kwa utukufu na haiba, na kuiendesha kwa ukali na mabavu, ikachochea hima na kuwasha hisia kwa wenye hima na ghera, harakati hiyo inayotoka katikati, ikapeleka wengi katika maimamu wenye kujitahidi, watu wa Hadithi, Mahafidhi, Wateule, Maqutubu na Mawalii kwenda katika ulimwengu wa Kiislamu na kuwalazimisha kuhama. Na kuwachemsha Waislamu mashariki na magharibi na kufungua uoni wao ili wafaidike kutoka katika Qur’an na hazina zake. Na sasa turudi katika mada tuliyokuwa nayo. Hakika aliyoyaeleza Mtume (s.a.w) katika mambo ya ghaibu na yakatokea kihakika kama alivyoeleza, yanafika maelfu bali inazidi, bali hapa tutaashiria mifano tu kati ya hayo, ile ambayo wameafikiana usahihi wake watu wa vitabu sita sahihi, na katika utangulizi wao (Al-Bukhary) na (Muslim), hata mingi kati ya hiyo imenakiliwa kwa namna ya mutawatir, kwa upande wa maana. Na wanazuoni wameafikiana na watu wa tahakiki juu ya kusihi kwa baadhi yake kwamba ni sawa na tawatur sahihi. ..Watu wa sahihi na maimamu wamefanya uchunguzi wa Hadithi: Yale ambayo Mtume (s.a.w) amewajulisha sahaba zake katika aliyowaahidi katika kushinda juu ya maadui zake na kufungua Makka na Bayt Al-Maqdis, Yemen Shamu na Iraq, na itafunguliwa Khaybar na akaelezea kugawana kwao (Hazina za Kisra na Kaisari) dola kubwa kabisa Ulimwenguni katika enzi hizo. Kisha Mtume (s.a.w) wakati alipokuwa anaelezea habari hii ya kighaibu hakusema: Nadhani, nafikiri au huenda, lakini alielezea kwa ujuzi wa yakini kana kwamba inatokea anaiona, na imetokea kama alivyoeleza, kwa kujua kwamba yeye wakati alipoelezea habari hii alikuwa ameamrishwa kuhama, na sahaba zake ni wachache. Na ulimwengu wote na wanaozunguka Madina ni maadui wanaonyemelea kila upande. Na katika mapokezi sahihi, Mtume (s.a.w) alieleza mara kwa mara: (Wafuateni wawili ambao watakuja baada yangu Abubakar na Umar). Kwa kauli hii akafidisha kuwa Abubakar na Umar wataishi baada yake, na watakuwa makhalifa, na watatekeleza ukhalifa haki yake kamili kwa namna anayoridhia Allah (s.w) na Mjumbe wake (s.a.w). Kisha kwamba Abubakar atashika ukhalifa muda mfupi, wakati ambapo Umar (r.a) ataushika kwa muda mrefu, ukiachilia mbali kwamba yeye atatimiza Fat’ hu nyingi (Kufungua miji). Na amesema Mtume (s.a.w): (Hakika ya Allah (s.w) aliikunjua Ardhi kwa ajili yangu nikaona pande zote mashariki yake na magharibi zake na kwamba umati wangu utafikia ufalme wake pande zote nilizokunjuliwa kuziona kwa ajili yangu katika hiyo Ardhi). Na ikawa kama alivyosema. Na Mtume (s.a.w) alielezea kabla ya vita vya Badri - katika mapokezi sahihi - juu ya vifo vya makafiri katika Badri na akaashiria mahali pa kuuliwa kwao na vifo vya maraisi wao: Hapa ni mahali pa kufa kwa Abu Jahal, hapa mahali pa kifo cha Utba, na hapa ni mahali pa kifo cha Umayya, hapa ni mahali pa kifo cha fulani na fulani (Na akajulisha kwamba Ubayya bin Khalaf atauliwa), na ikawa kama alivyojulisha. Na imethibiti katika sahihi kwamba amesema kama anayewashuhudia sahaba zake na kuwaangalia katika vita vya Mu’tah, nayo ikiwa umbali wa mwendo wa mwezi mmoja kutokea mipaka ya Shamu: (Bendera ameichukua Zaid akasibiwa kisha akaichukua Jafar akasibiwa kisha akaichukua Ibn Rawaha akasibiwa, na macho yake yakitoa machozi, hata akaichukua bendera upanga katika panga za Allah (s.w) hata Allah (s.w) akawafungulia), na baada ya kupita wiki chache alirudi Ya’laa bin Munabbih kutoka katika uwanja wa vita, na kabla ya kuelezea yaliyotokea huko Mtume wa Allah (s.a.w) alibainisha yaliyotokea huko kwa upambanuzi. Akaapa Ya’laa, na akasema: (Naapa kwa yule ambaye amekutuma wewe kwa haki hukuacha katika Hadithi yao japo herufi moja). Na katika mapokezi sahihi kwamba Mtume (s.a.w) alieleza kwamba ukhalifa baada yake utakuwa miaka thelathini kisha utakuwa ufalme kandamizi, (Na kwamba jambo hili limeanza likiwa ni unabii na rehema, kisha litakuwa ni rehema na ukhalifa, kisha utakuwa ufalme kandamizi, kisha utakuwa ushupavu na ujabari na ufisadi katika umma), akaelezea (s.a.w) kuhusu muda wa ukhalifa wa uongofu, nayo, ni miaka thelathini, na muda huu unakamilika kwa miezi sita ya ukhalifa wa Hasan (r.a), kisha kufuatana ufalme, ujeuri na ufisadi katika umma, na kweli yamethibiti kwa hakika kama alivyosema: Na imethibiti kwa mapokezi sahihi kwamba Sayyidina Uthman (r.a) atauliwa na hali ya kuwa anasoma msahafu, na kwamba Mtume (s.a.w) alisema: (Hakika Mwenyezi Mungu huenda akamvika kanzu na wao wanataka kumvua) na ikawa kama alivyosema. Na katika mapokezi sahihi mengine kwamba: Wakati Mtume (s.a.w) alipofanya hijama Abdullah Bin Az-Zubayr alikunywa damu yake iliyo tohara kwa ajili ya kutabaruku, na hakuimwaga akamwambia: (Ole wao watu kutoka kwako na ule wako kutoka kwa watu) akawa ameeleza kwamba Abdullah ataongoza watu kwa ushujaa mkubwa, na atakuwa lengo la mashambulizi makali, na yatashuka kwa watu masaibu na majanga kwa sababu yake. Na kweli yametokea kama alivyosema, ambapo Abdullah bin Az-Zubayr alitangaza ukhalifa Makka kipindi cha banu Umayya na Al-Hajjaj bin Yusuf dhalimu alimzingira na jeshi kubwa Makka, na baada ya mapigano makali na ushupavu wa nadra na vita vyenye kumwaga damu alianguka hali ya kuwa ni shahidi. Na Mtume (s.a.w) alieleza (Ufalme wa Bani Umayyah) yaani kudhihiri kwa Dola la banu Umayya (Na utawala wa Muawiyah, na akamuusia) alipomwambia: Ukitawala pangilia au fanya wema au fanya nasaha na zitakuwa falme zake na maraisi wake ni madhalimu, na watatokea kati yao watu mfano wa Yazid na Walid. Kama alivyoeleza (s.a.w) kuhusu (Kutoka kwa mtoto wa Al-Abbas na bendera nyeusi na kumiliki kwao maradufu ya waliyomiliki) kwamba Dola ya Abbasiyya itadhihiri baada ya Bani Umayya, na watabakia kwenye ufalme muda mrefu sana. Yametokea kiuhakika yote hayo hivyo hivyo kama alivyoeleza Mtume (s.a.w). Na imethibiti katika sahihi kwamba amesema: (Ole wao waarabu kutokana na Shari iliyokaribia) akawa ameelezea shari ya Jenkizkhan na Holako, na kuteketeza kwao Dola ya Al-Abbasiyyah ya Kiarabu, na imekuwa hakika vilevile kama alivyosema. Na alimwambia Saad bin Waqqas katika mapokeo sahihi, alipokuwa katika maradhi makali: (Huwenda utabakia hata watanufaika watu, na kudhurika kwa ajili yako wengineo) akaeleza (s.a.w) kuwa yeye atakuwa kiongozi mkubwa, na Allah (s.w) atafungua miji mingi kwa mkono wake (Saad) na watanufaika naye watu wengi kwa kuingia kwao kwenye ngome ya Uislamu, na watadhurika kwa ajili yake wengineo ambapo Dola yao itaanguka. Na imekuwa kama alivyosema. Ambapo Saad amekuwa ni kiongozi wa jeshi la Kiislamu na aliteketeza Dola ya Waajemi na ikawa ni sababu ya kuingia wengi katika watu na mila kwenye hozi ya Uislamu. Na imethibiti vilevile kwamba Mtume (s.a.w) (Alimwomboleza An-Najashy katika siku ambayo alikufa), katika mwaka wa saba Hijiria, na alimswalia, na baada ya kupita wiki ilikuja habari kwamba alifishwa siku ambayo aliyoieleza Mtume (s.a.w). Na alisema Mtume (s.a.w): (Thubutu kwa hakika juu yako kuna Nabii na Rafiki na Shahidi) wakati alipokuwa Mtume (s.a.w) pamoja na wateule katika masahaba wema juu ya Mlima Uhud – au Juu ya Hiraa - na mlima ulitetemeka kwa chini yao, ikafidisha kwamba Umar na Uthman na Ali watakufa mashahidi, ikawa kama alivyoeleza. Ewe mnyonge na ewe ambaye moyo wake umekufa na ewe mwovu! Huenda unasema kwamba Muhammad (s.a.w) alikuwa bingwa, akajua kwa ubingwa wake mambo haya ya kighaibu na unafumba macho yako kuhusu hakika ya Unabii yenye kuangaza kama jua!. Ewe masikini! Ulichokisikia sio ila ni aina kumi na tano katika aina za jumla za miujiza yake Mtume (s.a.w), na umejua kwamba yote hiyo imethibiti kwa mapokezi sahihi na kwa tawatur ya kimaanawy. Nawe bado hujasikia isipokuwa ni kiasi kidogo katika yanayohusiana na mambo ya kighaibu. Je baada ya mwanadamu kusikia miujiza hii amwambie mwenye miujiza hiyo: Yeye ni bingwa anagundua mustakabali kwa firasa yake?. Jaalia kwamba sisi tumesema kama wewe: Yeye ni bingwa! Je inawezekana kuchanganyika uoni juu ya yule anayemiliki mamia ya maradufu ya busara takatifu na ubingwa wa hadhi ya juu? Na je, inayumkinika kwa mfano wa haiba hii ya hadhi ya juu ianguke kutoka katika hadhi yake ya juu ya kweli iwe inaeleza habari tupu zisizo na usahihi? Je, sio wazimu na upumbavu hakuna baada yake upumbavu wa kupinga yanayoelezwa na ubingwa huu wa kipekee juu ya furaha ya makazi mawili!?.
Imethibiti kwamba yeye (s.a.w) alimweleza Fatima: (Hakika yako wewe ni wa mwanzo wa watu wangu watakaonifuatia), yaani wa kwanza atakaye kufa baada yake (s.a.w) kwa hiyo anamfuata katika watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w). Na baada ya miezi sita likatokea alilosema. Na imethibiti kuwa hakika yake (s.a.w): (Alimweleza Abu Dharri (r.a) kufukuzwa kwake) yaani kutoka Madina Munawwara (na kuishi kwake peke yake na kufa kwake peke yake), na baada ya miaka Ishirini jambo hilo lilitokea kama alivyoeleza. Na vilevile aliamka kutoka usingizini katika nyumba ya Ummu Haram (Mama mdogo wa Anas bin Malik) akatabasamu huku akisema: (Watu katika umati wangu wameoneshwa kwangu wakiwa wapiganaji katika njia ya Allah (s.w) watapanda mgongo wa bahari hii wakiwa wafalme wakiwa juu ya viti vya heshima, akasema (Huyo mama): Omba ewe mjumbe wa Allah (s.w) niwe pamoja nao, akamwombea). Na baada ya miaka arobaini alifuatana na mumewe Ubbadatu bin As-Saamit kwa ajili ya kuifungua Kobrus na kafishwa huko. Na kaburi lake hivi sasa liko huko na linafanyiwa ziara. Imethibiti kwamba yeye (s.a.w) alisema: (Hakika katika Thaqif kuna Mwongo na dhalimu) akamwelezea Mukhtar aliye mashuhuri ambaye amedai Utume, na mmwagaji damu Al-Hajjaj dhalimu ambaye ameua nafsi mia moja elfu. Na imethibiti vilevile kwamba yeye (s.a.w) alisema: (Kostantinopole itafunguliwa, mbora wa amiri aliyoje amiri wake na bora ya jeshi lilioje jeshi lake) akafidisha kwa hili kwamba utafunguliwa mji wa Istanbul kwa mkono wa Waislamu, na Muhammad Al-Fatih atakuwa na cheo cha juu: (Mbora wa amiri aliyoje). Na ilidhihiri jambo hili kama alivyosema. Na imethibiti vilevile (s.a.w) amesema: (Hakika ya dini ingekuwa imeangikwa kwenye nyota ya thurea wangepata watu miongoni mwa wana wa Uajemi) akiashiria wale ambao nchi ya Uajemi imezalisha wakiwemo wanazuoni na mawalii mifano ya Imamu Abu Hanifa An-Nuuman. Na imethibiti vilevile (Mwanazuoni wa Makuraishi atajaza tabaka za Ardhi kwa elimu) akiashiria kwa hilo Imamu Shafii. Na ameeleza (s.a.w): (Hakika ya umma utafarikiana katika makundi sabini na tatu na hakika lenye kukoka katika hayo ni Ahli Sunnat wal jamaat). Na amesema (s.a.w): (Kundi la Al-Kadariyya ni wamajusi wa umma huu), akiashiria kwa hilo kundi la Al-Kadariyya ambao wanakanusha Qadar, na akajulisha kundi la Ar-Raafidhat na ambao limegawika katika tanzu na makundi mengi. Na vilevile ameeleza kuhusu makundi mengi, ambapo imethibiti kwamba alimwambia Ali ambayo maana yake: Hakika mfano wako ni mfano wa Issa (a.s), utakuwa sababu ya hilaki ya makundi mawili ya watu: Mojawapo kutokana na kupitiliza mahaba na lingine kutokana na kupitiliza uadui. Ambapo Wanasara wamepitiliza katika kumpenda Issa (a.s) hata wakavuka mpaka uliowekwa na sharia basi wanahiliki na wamesema: Hakika yeye ni mwana wa Allah (s.w) -hashalillah – na Mayahudi vile vile wamepitiliza katika uadui kwake wakakanusha unabii wake na cheo chake cha juu. Na kadhalika kundi katika watu watapitiliza katika mapenzi kwako na kukiuka mpaka uliowekwa na sharia basi watahiliki, ambapo (s.a.w) amesema kuwahusu wao: (Wana kundi linaitwa Ar-Raafidhat), na kundi lingine watazidisha katika uadui kwako nao ni (Al-Khawarij) na sehemu ya wenye kupitiliza mpaka katika kuwatii Banu Umayya nao ni (An-Naaswiba). Ikisemwa: Hakika Qur’an tukufu inaamrisha kuwapenda ali al-bait, na amehimiza Mtume (s.a.w) juu ya hilo, pengine mapenzi haya pengine yakatengeneza udhuru, ambapo watu wa mapenzi ni watu wa hisia na ulevi - yaani wamechukuliwa akili - basi kwa nini Mashia na hasa Ar-Raafidhat hawanufaiki na mapenzi haya na wala hayawaokoi kutokana na adhabu, bali tunaona kinyume ya hivyo wao wanakaribia kutokana na kupitiliza mapenzi kama ilivyoashiria Hadithi?!. Jibu: Mapenzi ni sehemu mbili Mojawapo: Mapenzi (Kwa maana ya neno) nayo ni mapenzi ya Ali na Hasan na Husein na watu wa nyumba ya Mtume mapenzi kwa ajili ya Allah (s.w) na kwa ajili ya Mtume (s.a.w) na katika njia ya wawili hao. Basi mapenzi haya huzidisha mapenzi ya Mtume (s.a.w) na inakuwa ni njia ya kumpenda Allah (s.w). Mapenzi haya yamo katika sharia, haidhuru kupitiliza, kwa sababu havuki mpaka na wala hayasababishi kumtukana mwingine na kumfanyia uadui. Na pili yake: Mapenzi (Kwa maana ya jina) nayo ni kuwapenda kidhati, na kwa ajili yao, yaani kumpenda Ali kwa ajili ya ushujaa wake na ukamilifu wake, na kumpenda Hasan na Husein kwa ajili ya fadhila zao na sifa zao za kipekee ziliokamilika tu, bila ya kumkumbuka Mtume (s.a.w), hata kati yao wapo wanao wapenda hata wasipomjua Allah (s.w) na mjumbe wake. Mapenzi haya hayawi njia ya kumpenda Allah (s.w) na mjumbe wake (s.a.w). Na inapokuwa katika mapenzi haya kuna kupitiliza basi hakika ya mapenzi hayo yanapelekea kuwatukana wengine na kuwafanyia uadui. Na kama hivi – kama ilivyoelezwa katika Hadithi sharifu – Wapo kati yao walivuka mpaka katika mapenzi kwa Ali na kujiweka mbali na Abu Bakar na Umar, wakaingia katika hasara kubwa. Mapenzi haya hasi yakawa – siyo chanya – ni sababu ya hasara yao. Na imenukuliwa unakili sahihi kwamba (s.a.w) aliutahadharisha umma kwamba wao (Wakitembea mwendo wa kiburi na kuhudumiwa na Mabinti wa Uajemi na Rumi, Allah (s.w) atarejesha nguvu zao kati yao na kuwasalitisha washari wao juu ya wema wao). Na baada ya miaka thelathini jambo hilo lilitokea kama alivyosema. Na imethibiti vilevile kwamba (s.a.w) aliwajulisha sahaba zake: (Kufunguliwa Khaibar kwa mkono wa Ali). Na katika kesho ya siku hiyo ulitokea muujiza wa kinabii – juu ya kilichokuwa kinatazamiwa – Ali akachukua mlango wa ngome kwa mkono wake na akaujaalia kuwa ni ngao. Na jambo la kufungua lilipotimia aliutupa Ardhini, na mlango ulikuwa ni mkubwa, hata kwamba hawakuweza watu wanane – katika mapokezi mengine wanaume arobaini- kuunyanyua kutoka Ardhini. Na alisema (s.a.w): (Kiama hakisimami mpaka makundi mawili makubwa yapigane madai yao ni mamoja) akawa ameeleza kuhusu vita ambavyo vimetokea katika Siffain baina ya Ali na Muawiyah (r.a). Na katika aliyoelezea (s.a.w): (Kwamba Ammar litamuua kundi lenye kuasi), na baada ya hapo aliuawa katika vita vya Siffain. Ali akachukua hoja kwake kwamba wanaomuunga mkono Muawiya ni kundi asi, lakini Muawiya alifanyia taawili Hadithi hii (Aliifasiri kwa maana nyingine). Na akasema Amru bin Al-As: Waasi ni wale wauaji wake tu, na wala sio sisi sote waasi. Na alisema vilevile (s.a.w): (Hakika fitina haidhihiri maadamu Umar yungali hai). Jambo likawa kama alivyoeleza. Aliposhikwa mateka Suheil Bin Amri – kabla ya kusilimu kwake – Siku ya Badr Umar alisema: Ewe mjumbe wa Allah hakika huyo ni mwanamume msemaji niache niyatoe meno yake mawili ya chini, hatasimama kuwa mzungumzaji dhidi yako baada ya leo, Mtume (s.a.w) akasema: (Na huenda atasimama kisimamo kitakachokufurahisha ewe Umar). Akawa hivyo pale wakati kilipotokea kifo cha Mtume (s.a.w), tukio hilo kubwa ambalo subira ilichoka katika tukio hilo, alisimama Abubakr (r.a) akiwapa taazia Waislamu Madina Munawwara na kuzithibitisha nyoyo za sahaba akawahutubia hotuba yenye Ufasaha. Na Suheil pia akasimama Makka mukarrama akielekea mwelekeo wa Abubakar, hata maneno ya hotuba mbili yamepatikana sawa katika maana moja. Na Mtume (s.a.w) alisema kumwambia Suraqa (Vipi itakuwa hali yako utakapovikwa mikufu ya Kisra) na katika zama za Umar (r.a) Dola la Kisra lilianguka na yakawa yamekuja mapambo ya Kisra kwa Umar akamvika Suraqa mapambo hayo na akasema: (Alhamdulillah ambaye amemnyang’anya Kisra na kumvisha Suraqa) na kusadikisha aliyoyaeleza Mtume (s.a.w). Na vilevile alisema: (Akiangamia (Akifa) Kisra hakuna Kisra Baada yake). Na jambo likawa kama alivyoeleza. Na Mtume (s.a.w) alimweleza mjumbe wa Kisra: (Hakika Allah (s.w) amemsalitisha Kisra mwanawe Shaharawayhi katika wakati kadha..). Yule mjumbe alipopata hakika ya wakati wa kuuliwa kwa Kisra, alikuwa na yakini kwamba kuuliwa kwake kulikuwa katika wakati uleule ambao aliuelezea Mtume (s.a.w) akasilimu kwa sababu hiyo. Na jina la mjumbe huyo ni (Feyruz) kama ilivyopatikana katika baadhi ya mapokezi. Na ameelezea kuhusu barua ya Haatib bin abi Balta’ah ambayo aliituma kwa siri kwenda kwa makafiri wa Makuraishi. Mtume (s.a.w) akamtuma Ali na Al-Miqdad (r.a) kwamba katika mahali fulani kuna binti anayo barua. Nileteeni, wakaenda na wakaileta barua mahali ambapo Mtume (s.a.w) aliwaelezea na akaagiza kuitwa Haatibu na akamwambia: Nini kilichokupelekea ukafanya hivi? Akadhihirisha udhuru wake akamkubalia. Na hii ni riwaya sahihi iliyothibiti. Na imethibiti vilevile kwamba (s.a.w) alisema kuhusu Utbah bin Abi Lahabi: (Watamla mbwa wa Allah) akaeleza kuhusu mwisho wake wa kuhuzunisha, na baada ya muda Utbah alikwenda akielekea Yemen akamjia mnyama mkali akamla. Akasadikisha dua yake juu yake. Na imenukuliwa kwa unakili sahihi: (Kwamba Mtume (s.a.w) alipofungua Makka alimwamuru Bilali (r.a) apande juu ya Al-Kaaba na aadhini juu ya Al-Kaaba. Na Abu Sufyan Bin Harb na Uttab bin Asad na Al-Harith Bin Hisham nao ni wakuu wa Quraysh wamekaa kwenye uwanja wa Al-Kaaba. Uttab akasema: Allah amemkirimu Usayda kwani hakuiona siku hii. Na Al-Harith akasema: Hivi Muhammad hakupata muadhini mwingine asiyekuwa huyu Kunguru Mweusi! Abu Sufyani akasema: Sisemi kitu, ningesema kitu haya majabali yangemweleza. Mtume (s.a.w) akawatokea na akasema: Nimejua mlichokisema na akaeleza maneno yao. Al-Harith na Uttab wakasema: Tunashuhudia kwamba wewe ni Mjumbe wa Allah, haya hakumjulisha yeyote aliyekuwa pamoja nasi hata tuseme amejua kwa kupitia yeye). Basi ewe usiyemwamini Nabii huyu mkarimu na ewe mkanaji! Zingatia hawa wakaidi wawili katika wakuu wa Makuraishi vipi walivyoona nafsi zao zinalazimika kuamini, kwa walichosikia katika habari moja ya kighaibu. Basi nini kilichoharibu moyo wako nawe unasikia maelfu ya miujiza mfano wa hiyo, na yote imethibiti kwa njia za tawatur za kimaanawy na pamoja na hivyo moyo wako hautulii, na turudi kwenye mazungumzo yetu. Na imethibiti vilevile, kwamba (s.a.w) (Ameelezea mali ambayo ameiacha Ammi yake Al-Abbas (r.a) kwa Ummi Al-fadhli (Mkewe) baada ya kuwa ameificha) Basi alipochukuliwa mateka katika Badri na ikatakiwa kwake kutolewa fidia akasema: Sina mali mimi. Mtume (s.a.w) akamwambia (Imefanya nini mali ambayo umeiweka kwa Ummu Fadhli). Akasema: (Hakuijua isipokuwa mimi na isipokuwa yeye. Akasilimu). Na imethibiti vilevile: Kwamba mchawi khabithi Labid Myahudi alifanya uchawi ili umuudhi Mtume (s.a.w) akafunga nywele kwenye chanuo, na akakiweka kwenye kisima, Mtume (s.a.w) akamuamuru Ali na masahaba wengine, waende kwenye kisima fulani na walete zana za uchawi, wakaenda na wakazileta. Na ilikuwa kila inapofunguka katika huo unywele fundo moja Mtume (s.a.w) anapata kiasi cha tahafifu. Na imethibiti vilevile, kwamba aliwaambia jamaa ambao ndani yao alikuwamo Abu Hurayra na Hudhayfa: (Jino la mmoja wenu motoni mfano wa mlima wa Uhudi), akawa ameelezea juu ya kuritadi kwa mmoja katika jamaa hao na kabainisha mwisho wake mbaya. Amesema Abuu Hurayra: (Watu hawa wakaondoka - yaani wakafariki – na nikabakia mimi na mwanamume mmoja (nikahofia), akauliwa akiwa ameritadi siku ya Al-Yamamah). Na ikadhihiri hakika ya maelezo ya Mtume (s.a.w). Na imethibiti vilevile (Kadhia ya Umair na Safwan wakati alipomwambia siri na kumwekea sharti kwa kumuua Mtume (s.a.w)) kwa malipo ya kiasi kikubwa cha mali (Wakati Umar alipomjia Mtume (s.a.w) akikusudia kumuua, na akamjulisha Mjumbe wa Allah (s.a.w) juu ya jambo hilo na siri hiyo - na kaweka mkono wake juu ya kifua chake – alisilimu). Hivi na hakika zimetokea nyingi katika mifano ya bashiri kama hizi za kighaibu za kweli, na imezitaja vitabu sita sahihi vilivyo maarufu pamoja na sanadi zake. Na aghalabu ya yaliyotajwa katika risala hii katika matukio hakika yako katika hukumu ya Mutawatir ya kimaanawy, nayo ni yenye kuthibiti kwa hali ya kukinaisha na ya kiyakini, na ameyanakili Al-Bukhary na Muslim katika sahihi zao mbili ambazo ni vitabu sahihi zaidi kuliko vitabu vyote baada ya Qur’an, katika waliyokuwa nayo watu wa elimu na tahakiki, kwa kujua kwamba zimebainishwa katika vitabu vingine sahihi vya sunna kama Al Tirmidhy na An-Nasaiy na Abu Dauud na Mustadrak ya al-Hakim na Musnad ya Ahmad bin Hanbal na dalili za Al-Bayhaqy pamoja na sanadi zake. Basi ewe mkanaji mwenye kughafilika! Usivurumishe maneno bure tu ukasema: Hakika Muhammad (s.a.w) ni mtu mwenye akili mwerevu! Kisha unaliacha jambo kama hivyo na unaondoka, habari hizi za kweli ambazo zinagusa mambo ya kighaibu hazikosi kuwa na mambo mawili: Ima hakika unasema: Mtu huyu ana uoni mkali na ubingwa mpana sana, yaani ana jicho linaloona muda uliopita na mustakabali kwa pamoja na ulimwengu wote, kwa jicho hilo basi anajua kila kitu na kila tukio, basi pande za Ardhi na ulimwengu wote mashariki na magharibi chini ya mtazamo wa kushuhudia kwake, na ana uhodari mkubwa unaomwezesha kugundua mambo yote ya muda uliopita na mustakabali.! Basi hali hii haiyumkiniki - kama unavyoona – kuwa kwa mtu katu. Na kama imetokea kwa yeyote kwa hiyo huyo ni mwenye kufurutu ada na atakuwa na kipaji cha hali ya juu ambacho Bwana mlezi wa walimwengu wote amemtunuku yeye. Na jambo hili lenyewe kwa dhati yake ni muujiza mkubwa. Au yatakikana kwako uamini kwamba huyo mtu mwema ni mwenye kuamuriwa na mwanafunzi na anapokea miongozo na maelekezo kutoka kwa yule ambaye anaona kila kitu na ana uweza wa kusarifu katika kila kitu katika ulimwengu wote na zama zote, basi kila kitu kimeandikwa kwenye ubao wake uliohifadhiwa, kutokana nao anamfundisha mwanafunzi wake anachokitaka na wakati wowote autakao. Kwa hiyo imethibiti kwamba Muhammad (s.a.w) anapokea darsa kutoka kwa mwalimu wake (s.w) na anafikisha vilevile. Na imethibiti vilevile kwamba Mtume (s.a.w) alipomtuma Khalid bin Al-Walid akapigane na Akydar – kiongozi wa Domat Al-Jandal, alimwambia: (Hakika utamkuta anawinda ng’ombe) - yaani ng’ombe mwitu – na akamweleza kuwa atamleta akiwa mateka pasia na upinzani kutokea kwake. Na Khalid alikwenda na akamkuta kama alivyomwelezea Mtume (s.a.w) akamchukua akiwa ni mateka na akaja naye. Na imethibiti vilevile kwamba yeye Mtume (s.a.w): alijulisha: (Quraysh mchwa kula yaliyomo katika tangazo lao walilotumia kuwashinda Bani Hashim na kukata udugu wao kwalo, na kwamba alibakisha kila jina la Allah (s.w), wakalikuta kama alivyosema), likiwa limetungikwa juu ya Al-Ka’ba. Na imethibiti kwamba (s.a.w) alielezea kuhusu kutokea kwa Tauni wakati wa kufungua nyumba takatifu. Basi katika kipindi cha Umar ilienea tauni kuenea kubaya kiasi idadi ya wale waliokufa ikiwa ni matokeo ya maradhi ilikuwa ni watu sabini elfu ndani ya siku tatu. Na imethibiti pia kwamba Mtume (s.a.w) ameelezea kuhusu kuwepo kwa Basra na Baghdad kabla ya kukaliwa, na akaelezea kuhamisha hazina za Ardhi kwenda katika mji wa Baghdad. Na Mtume (s.a.w) aliwaeleza kuhusu (Kupigana kwao na Waturuki) na mataifa ambayo yanazunguka bahari ya Al-Khizr kisha baada ya hapo wataingia wengi mno wa mataifa haya katika dini yaa Uislamu, na watawatawala Waarabu kati yao ambapo alisema: (Inakaribia kukithiri ndani yenu Waajemi (wasiokuwa Waarabu) wanakula ndani yenu na wanapiga shingo zenu). Na alisema Mtume (s.a.w): (Kuangamia kwa umma wangu ni mkononi mwa vijana wa kiquraysh) akaelezea kuhusu Yazid na Walid na mfano wao katika wakuu waovu katika bani Umayya. Na akaeleza Mtume (s.a.w) kuhusu kuritadi kwa baadhi ya maeneo kama Al-Yamamah. Na amesema katika vita vya handaki: (Hakika ya Quraysh na makundi hawatanipiga vita kamwe na mimi nitawapiga vita) na jambo likawa kama alivyoeleza. Na imethibiti vilevile kwamba (s.a.w) alieleza kabla ya kufariki kwake kwa miezi miwili: (Kwamba mja alihiarishwa akachagua yaliyoko kwa Allah). Na kasema kuhusu Zayd bin Swauhan: (Kiungo kitamtangulia peponi, ukakatwa mkono wake kwenye jihadi) na kikawa shahidi, siku ya Nahawandi, kikamtangulia kwenda peponi. Na kama hivi, yote tuliyotafiti katika mambo ya ghaibu hakika ni aina moja tu kati ya aina kumi ya miujiza yake (s.a.w), basi sisi hatujajua bado kumi ya makumi ya aina hii, na hakika tumebainisha kwa kujumlisha aina nne katika habari za ghaibu katika Neno la ishirini na tano linalohusu muujiza wa Qur’an. Basi zingatia hivi sasa aina hii, na uijumuishe katika aina nne nyingine ambazo amezielezea Mtume (s.a.w) kwa ulimi wa Qur’an, na tazama namna inavyounda dalili ya kukinaisha ya kung’aa juu ya Utume kiasi atakiri ambaye akili yake haijavurugika na moyo wake na atasadiki kwamba huyu Mtume mtukufu (s.a.w) si vingine hakika yeye ni Nabii anayeelezea kuhusu ghaibu kutoka kwa Muumba wa kila kitu na mjuzi wa ghaibu yote.
Tutaashiria mifano michache katika miujiza ya Unabii ambayo inahusu baraka ya chakula na imethibiti kwa mapokeo sahihi ya kukinaisha na kwa Tawatur ya kimaanawy. Na tunaona katika linalofaa zaidi mbele yake tuweke utangulizi.
Hakika ya mifano itakayokuja kuhusu miujiza wa baraka ya chakula kila moja kati ya hiyo imepokewa kwa njia nyingi, bali sehemu ya hizo imepokewa kwa njia kumi na sita, na imetokea sehemu kubwa ya mifano hii mbele ya mkusanyiko wa watu wengi sana miongoni mwa sahaba wema waliotakasika na uongo na ambao wana cheo cha hali ya juu katika ukweli na uaminifu. Mfano wa kuweka wazi: Na katika mapokezi ni kuwa: Wamekula wanaume sabini katika pishi moja na wote walishiba. Wanaume sabini wanasikia mapokezi haya ambayo mmoja wao anayaelezea, kisha hawamhalifu na wala hawamkanushii, yaani wao wanamsadiki kwa kunyamaza kwao kimya. Basi sahaba wema (r.a) wote walikuwa katika kilele cha ukweli na haki ambapo waliishi katika karne bora na wao wamehifadhika na kunyamazia batili. Mmoja wao angeona jambo japo kidogo la uongo katika maneno yoyote yawayo asingeweza kulinyamazia katu, bali kwa lazima angelikataa. Kwa hiyo mapokezi ambayo tunayataja ukiachilia mbali kwamba yamepokewa kwa njia nyingi, wengine wameyanyamazia kwa kuyasadiki, yaani kama vile jamaa wameyapokea kwani mwenye kunyamaza katika wao ni kama mwenye kutamka kwa hiyo hizo zinafidisha kukinaisha kama Mutawatir za kimaanawy. Na historia inashuhudia – na hasa Sira - kwamba Sahaba wema wamezitenga nafsi zao baada ya kuhifadhi Qur’an kwa kuhifadhi Hadithi tukufu, yaani kuhifadhi hali zake, matendo yake na kauli zake, sawa kati ya hizo zinazohusu hukumu za kisheria au miujiza na hawakupuuza – Allah awalipe kheri - harakati yoyote vyovyote itakavyokuwa ni ndogo katika sira yake yenye baraka, bali waliishughulikia na mapokezi yake, na waliiandika katika vitabu vyao, na hasa akina Abdallah saba na hasa mkalimani wa Qur’an Abdullah bin Abbas na Abdullah bin Amr bin Al-As. Na kama hivi zilihifadhiwa Hadithi katika kipindi cha Sahaba wema baadae wakaja wakubwa wa Taabiina baada ya miaka thelathini au arobaini wakazipokea mpya mbichi kutoka kwao na wakazihifadhi kwa uaminifu na ikhlasi, na wakaziandika na kuzipokea kutoka kwao baada ya hapo Maimamu mujtahidina na maelfu ya wahakiki na Wanazuoni wa Hadithi basi wakaziandika na kuzidawini, kisha walizipokea - baada ya kupita miaka mia mbili baada ya Hijra - watu wa vitabu Sita Sahihi maarufu na mwanzoni mwao ni Al-Bukhary na Muslim, kisha ikaja zamu ya wakosoaji na watu wa fani ya Jarh na Taadili, na wakadhihiri katika wao wenye misimamo mikali – mfano wa Ibn Al-Jawazy - wakazipambanua Hadithi maudhui ambazo wameziweka baadhi ya wakanushaji na watu wajinga juu ya Hadithi sahihi. Kisha wakawafuatia wanazuoni bora wenye ucha Mungu na woga mfano wa Jalaluddin As-Suyuuty na yeye ni Al-Allamah Imamu ambaye alipata utukufu wa kuongea na Mtume (s.a.w) akajitokeza kwake mara sabini katika hali ya kuwa macho – kama wanavyosadikisha hilo watu wa kufunuliwa katika Mawalii wema - wakazipambanua Johari za Hadithi sahihi – na baki ya maneno mengine yaliyowekwa. Na kama hivi utaona kwamba Hadithi - na miujiza ambayo tutaijadili - imefika kwetu ikiwa salama sahihi baada ya kuzipokea wasiohesabika wala kudhibitika katika mikono ya kuaminiwa. (Basi Alhamdulillah, hii ni miongoni mwa fadhila za Mola wangu mlezi) Na kwa hivyo haitakiwi kupita kwenye mawazo: Vipi tutajua kwamba matukio haya ambayo yametokea tangu muda wa kitambo kirefu mno zilibakia zikiwa zimelindwa salama kutokana na mkono wa mchezo? Mifano kuhusu miujiza ya baraka ya chakula:
Sahihi sita zimeafikiana na mwanzoni mwao Al-Bukhary na Muslim katika Hadithi ya Anas (r.a) (Amesema: Mtume (s.a.w) alikuwa ni Bwana harusi kwa Zainab, akakusudia mama yangu Ummu Sulaym tende na samli na Ukat, akatengeneza haysa akaiweka katika bakuli na akasema: Ewe Anas! peleka hiki kwa Mtume wa Allah (s.a.w) mwambie mama yangu ameagiza hiki, naye anakusalimia, na anasema: Hakika hiki kutoka kwetu kwa ajili yako ni kichache ewe Mjumbe wa Allah! Basi nikaenda na nikasema, akasema: (Kiweke) kisha akasema: (Nenda ukaniitie fulani) na fulani na fulani wanaume aliwataja (na mwite utakayekutana naye) nikawaita aliowataja majina na niliokutana nao nikarejea tahamaki nyumba imejaa watu. Anasi akaambiwa: Idadi yenu mlikuwa wangapi? Akasema: Kiasi cha mia tatu. Nikamwona Mtume (s.a.w) anaweka mkono wake katika kile chakula kidogo cha tende na akaongea alichotaka Allah (s.w) kisha akawa anawaita kumi kumi wanakula humo, na akasema kuwaambia (Tajeni jina la Mwenyezi Mungu, na kila mtu na ale kile kilicho mbele yake) akasema: Wakala mpaka wakashiba, likatoka kundi, likaingia kundi, mpaka wakala wote akanambia: (Ewe Anas! Nyanyua) nikanyanyua, basi sijui nilipoweka kilikuwa kingi zaidi au wakati nilipokinyayua).
Mtume (s.a.w) alifikia akiwa mgeni kwa Abu Ayyub Al-Answary, basi siku moja (Alitengeneza kwa ajili ya Mtume wa Allah (s.a.w) na kwa ajili ya Abubakar chakula kiasi cha kuwatosha wawili hao. Mtume (s.a.w) akamwambia waite thelathini katika watukufu wa kianswary! akawaita wakala mpaka wakaacha. Kisha akasema: Waite Sitini, ikawa mfano wa hivyo, kisha akasema: Waite sabini wakala mpaka wakaacha, na hakutoka kati yao yeyote mpaka amesilimu na kufunga Bay’ah (Ahadi ya utii), akasema Abu Ayyub: Wakala kutokana na chakula changu wanaume mia moja na themanini).
(Hadithi ya Salamata bin Al-Akwa’a, na Abu Hurayra, na Umar Bin Al-Khattab na Abu Amrat Al-Answary (r.a), wakataja njaa iliyowasibu watu pamoja na Mtume (s.a.w) katika baadhi ya vita vyake, akaagiza baki ya vyakula, mtu akaja na gao la chakula, na zaidi ya hapo, na juu yao ni yule ambaye ameleta pishi ya tende, akaikusanya juu ya busati la ngozi. Amesema Salamata: Nikavikusanya, kama mkao wa mbuzi, kisha akawaita watu na vyombo vyao, hakikubaki katika jeshi chombo ila walikijaza, ikabakia katika chakula hicho kadiri ya kilicholetwa na zaidi, (Na katika mapokezi) lau wangekila watu wa Ardhi kingewatosha).
Imethibiti katika sahihi na mwanzoni mwazo ni Al-Bukhary na Muslim kwamba Abdul Rahmani Bin Abu Bakar As-Siddiq amesema: (Tulikuwa pamoja na Mtume (s.a.w) watu mia moja na thelathini) katika safari (Na akataja katika Hadithi kwamba ilikandwa pishi ya chakula, na kutengenezwa mbuzi ukaokwa weusi wa tumbo lake) (maini), amesema: Naapa kwa Allah hakuna katika thelathini na mia isipokuwa amekata sehemu katika weusi wa tumbo lake, Kisha akajaalia katika maini hayo sahani mbili tukala sote, na yakasalia katika vyombo viwili, nikayabeba juu ya ngamia.
Imethibiti pia katika sahihi: (Hadithi ya Jabir katika kulisha kwake (s.a.w) siku ya handaki wanaume elfu kutokana na pishi ya Shairi na ndama wa mbuzi na amesema Jabir: Basi ninaapa kwa Allah (s.w) hakika wamekula hata wakakiacha na kugeuka, na hali ya kuwa chungu chetu kikichemka kama kilivyo na ngano yetu ikiokwa mikate) na alikuwa Mtume mtukufu (s.a.w) aliweka katika ngano ile na chungu katika maji ambayo ndani yake yalikuwa yenye kubarikiwa na aliyaombea baraka. Basi Jabir akawa anatangaza hali akiwa anaapa kwa Allah (s.w) muujiza wa baraka huu katika hadhira ya sahaba elfu akidhihirisha uhusiano wao na muujiza huo. Mapokezi haya ni ya kukinaisha kana kwamba wanaume elfu wameyapokea.
Na imethibiti katika sahihi kwamba Aba Talha Ami wa Mtumishi wa Mtume (s.a.w) Anas anasema: (Hakika Mtume Mtukufu alilisha katika alichokuja nacho Anas chini ya kwapa yake katika uchache wa mikate ya shairi kiasi cha wanaume themanini hata wakashiba. Na alikuwa (s.a.w) aliamrisha huo mkate ukatwe kipande kipande. Na akaomba baraka. Na kwamba nyumba ilikuwa finyu kwao wakawa wanakula kumi kumi, na walirejea wote wakiwa wameshiba).
Imethibiti katika sahihi ya Muslim na As-Shifaa na vinginevyo kwamba Jabir Al-Answary anasema: (Kwamba mwanaume alimjia Mtume (s.a.w) anamwomba ampe chakula, akampa chakula nusu ya wasaki ya shairi, hakuacha kuwa anakula katika chakula hicho yeye na mkewe na mgeni wake hadi walipokipima) ili wajue kilichopungua katika chakula hicho, wakaona kwamba baraka imeondoka kwenye chakula hicho, na kikawa kinapungua kidogo kidogo. Akaja kwa mtume (s.a.w) na akamweleza, akasema: (Lau usingekipima mungekula katika chakula hicho na kingedumu kwenu).
Zinabainisha sahihi kama At-Tirmidhy, An-Nasaiy, Al-Bayhaqy na kitabu cha As-Shifaa (Kutoka kwa Sumrata bin Jundubi: Alimjia Mtume (s.a.w) na chombo ndani yake kuna nyama, wakala kwa zamu tangu asubuhi hadi usiku wanasimama watu na wanakaa wengine). Na kwa msingi wa tuliyoyataja kwenye utangulizi, tukio hili lililopatikana katika baraka sio mapokezi ya Sumrata tu, bali kana kwamba yeye ni mwakilishi wa makundi hayo ambayo yamekula katika chakula hicho. Basi anatangaza mapokezi haya badala yao.
Wanaume wakutegemewa wanasimulia kama mwenye Al-Shifaa na Ibn Abi Shaybah na At-Tabarany kwa Sanadi nzuri na wanazuoni wahakiki: Kutoka kwa Abi Hurayra: Mtume (s.a.w) aliniamrisha nimwitie watu wa Sufa (Nao ni mafukara wa Muhajirina ambao idadi yao ilikuwa inazidi mia moja. Ambao wamejifanyia Sufa ndani ya msikiti kuwa ni makao yao. Nikawafuatilia hata nikawakusanya. Ikawekwa sahani mbele yetu, tukala tulichokitaka, na tukamaliza (Tumeshiba) na hali ya kuwa iko kama ilivyowekwa, isipokuwa ndani yake kulikuwa na athari za vidole). Basi abu Hurayra anaileta habari hii kwa jina la watu wa Sufa akiegemea kusadikisha kwao. Hiyo basi ni riwaya ya kukinaisha kana kwamba watu wote wa Sufa wameipokea. Basi je inayumkinika habari hii kuwa kinyume na haki na kusibu kisha hao wa kweli wakamilifu wasikanushe wala kuikataa?.
Imethibiti kwa mapokezi sahihi kwamba Imamu Ali (r.a) amesema: (Mtume wa Allah (s.a.w) alikusanya siku moja Bany Abdil Muttalib na walikuwa arobaini, kati yao watu wanakula Al-Jadata na wanakunywa Al-Firaq), yaani kati yao wapo wanaokula mtoto wa ngamia na kunywa wakia nne za maziwa (Akawatengenezea kibaba cha chakula wakala hata wakashiba na kikasalia kama kilivyo, kisha akaagiza chano) yaani chombo cha mbao chenye maziwa yanayotosha kwa watatu au wanne (Wakanywa mpaka wakaondoa kiu. Na yakasalia kana kwamba hayakunywewa). Basi huu ni mfano mmoja wa muujiza wa baraka ya chakula nao ni kwa ukinaifu wa ushujaa wa Ali (r.a) na ukweli wake.
Imethibiti kwa riwaya sahihi Katika kumuozesha Mtume (s.a.w) Ali (r.a) Bi Fatma alimwamrisha Bilali kuleta chombo cha vibaba vinne au vitano na kuchinja ngamia kwa ajili ya walima yake. Amesema: Nikamletea hivyo akamchoma kichwani kwake, kisha akawaingiza watu kundi baada ya kundi wanakula katika ngamia yule, mpaka wameshiba, na yakabakia katika chakula hicho masalia, akaombea baraka akaamrisha kuyabeba kwa wakeze, na akasema: (Kuleni na mlisheni anayewafunika). Kweli! Hakika ya mfano wa ndoa hii yenye kheri inastahiki mfano wa muujiza huu katika baraka.
Amepokea Jaafari As-Saadiq kutoka kwa baba yake Muhammad Al-Baqir kutoka kwa baba yake Zaynul Abidin kutoka kwa Ali (r.a): (Kwamba Fatma amepika chakula kwenye chungu kwa ajili ya mlo wao na kamwelekeza Ali kwa Mtume (s.a.w) ili ale pamoja nao, akamwamuru akachota katika chakula hicho kwa ajili ya wakeze wake sahani kwa sahani kisha yake Mtume (s.a.w) na kwa ajili ya Ali kisha chake (Fatima) kisha akanyanyua chungu hali ya kuwa kinamwagika, akasema (Fatima): Tukala katika hicho kiasi alichotaka Allah (s.w)). Basi ni ajabu ewe mwanadamu kwa nini hausadiki muujiza huu wa wazi kusadiki kwa kushuhudia baada ya uliyoyasikia kwamba wapokezi wake ni katika mnyororo tohara, hata Shetani mwenyewe hapati njia ya kukanusha!
Maimamu wamepokea mfano wa Abi Daud, Ahmad Ibn Hanbal na Al-Bayhaqy kutoka kwa Dukain Al-Ahmasy bin Said Al-Muzayyin, na kutoka kwa sahaba ambaye amepata utukufu yeye na ndugu zake sita kusuhubiana na Mtume (s.a.w) naye ni Nuuman bin Muqrin Al-Ahmasy Al-Muzayyin, na kutoka katika mapokezi ya Jariri na kutoka katika njia mabli mbali kwamba Mtume mtukufu (s.a.w): (Alimwamuru Umar bin Al-Khattab awape masurufu wapandaji mia nne kutoka Uhmus. Akasema: Ewe mjumbe wa Allah sio chochote ila pishi chache tu. Akasema: Nenda, akenda na akawapa masurufu kutokana na kiasi hicho. Na ilikuwa kiasi cha tende kama ngamia ndama aliye kaa, na kubaki katika hali yake). Na kama hivi, muujiza huu wa baraka, umetokea na hali ya kuwa unahusiana na wanaume mia nne, na hasa Umar (r.a). Basi hawa wote ni wasimuliaji kwa sababu kunyamaza kwao kwa vyovyote ni kusadikisha mapokezi hayo. Wala usiseme kwamba hiyo ni habari ya Aahadi (Yaani msimuliaji mmoja) kisha unapita katika mambo yako kwani mifano ya matukio kama haya ingawa ni habari ya Aahadi, isipokuwa hizo zinaleta utulivu katika moyo kwa sababu ni sawa na mutawatir kimaanawy.
Imethibiti katika sahihi na mwanzoni mwazo ni Al-Bukhary na Muslim Hadithi ya Jabir (r.a) Katika deni la baba yake, na alikuwa alitoa kwa wadeni wa baba yake asili ya mali yake ili waikubali na katika matunda yake miaka miwili haikuwa inatosha deni lao, Mtume (s.a.w) akaja baada ya kumwamrisha kulikata na kulijaalia muhimu katika asili yake, akaenda humo na kuomba, Jabiri akalipa kutokana na asili hiyo wadeni wa baba yake na kubaki mfano wa walivyokuwa wakikata kila mwaka, na katika mapokezi mfano wa alivyowapa, amesema: Na wadeni walikuwa Mayahudi wakastaajabu kutokana na hilo. Na kama hivi muujiza huu katika baraka ya chakula sio ni masimulizi anayosimulia Jabiri na watu wachache tu lakini masimulizi hayo ni Mutawatir kwa upande wa maana wanasimulia wapokezi wote hao wakiwakilisha kila mwenye kuhusiana na mapokezi haya.
Wanazuoni wahakiki wanasimulia mapokezi sahihi mwanzoni mwao ni Imamu At-Tirmidhy na Al-Bayhaqy, kutoka kwa Abi Hurayra (r.a) kwamba amesema: Watu iliwasibu njaa katika moja ya vita – na katika mapokezi kwenye vita vya Tabuk - Mtume wa Allah (s.a.w) akaniambia: Je kuna kitu chochote? Nikasema: Naam kiasi cha tende katika chombo cha masurufu na katika Mapokezi tende kumi na tano Akasema niletee, akaingiza mkono wake akatoa mshiko wa ganja moja akaukunjua na kuomba baraka. Kisha akasema waite kumi. Wakala mpaka wakashiba, kisha kumi vilevile, mpaka akalisha jeshi lote na wakashiba, akasema: Chukua ulichokuja nacho na uingize mkono wako na ukamate katika hicho (kilichomo) wala usikimwage, nikakamata zaidi ya nilichokuja nacho, nikala katika (chakula) hicho na nikawa ninakila uhai wa Mtume wa Allah (s.a.w) na Uhai wa Abi Bakar na Umar hadi alipouliwa Uthman nikapokonywa na kikaondoka. Na katika mapokezi nilichukua katika tende hiyo kadha wa kadha cha wasaki katika njia ya Allah (s.w). Na kama hivi, hakika muujiza wa baraka anaousimulia Abu Hurayra, na yeye ndiye ambaye amejifunza kwa mwalimu wa ulimwengu na Bwana wake Muhammad (s.a.w) na alidumu na madrasa ya Sufa na kuchomoza katika sufa kwa hifadhi kwa dua ya Mtume (s.a.w) aliyomwombea, basi sahaba huyu Mtukufu anasimulia riwaya hii katika mkusanyiko wa watu – kama vita vya Tabuk - hapana budi kuwa riwaya hii ni ya Mutawatir kwa upande wa maana, na yenye nguvu madhubuti kwa nguvu ya jeshi lote, yaani kama vile jeshi lote hili linasimulia.
Imethibiti katika sahihi ya Bukhary na sahihi nyingine: Kwamba njaa ilimsibu Abu Hurayra, (Mtume (s.a.w) akamfuatilia, akakuta maziwa kwenye kikombe ambayo alipewa zawadi, na akaamuru awaite watu wa Sufa. Akasema: Maziwa haya ni nini kwao, nilikuwa mimi mwenye haki zaidi kupata funda nipatie nguvu, nikawaita), Na walikuwa wanavuka mia, Mtume (s.a.w) akaamrisha niwanyweshe Nikawa ninampa mtu anakunywa mpaka anakata kiu. Kisha anachukua mwingine mpaka wote wakakata kiu akasema: Mtume (s.a.w) akachukua kikombe na akasema: Nimebaki mimi na wewe, kaa na unywe. Nikanywa kisha akasema: Kunywa. Hajaacha kuwa akisema hilo na ninakunywa mpaka nikasema: hapana, naapa kwa yule ambaye amekutuma kwa haki siyapatii mahali pa kuyapitisha (Yaani tumbo limejaa). Akachukua kikombe na akamshukuru Allah (s.a.w) na kusema Bismillahi na akanywa masalia. Basi pongezi kwako mara mia elfu ewe mjumbe wa Allah. Basi huu muujiza uliosalimika na mavumbi ya shaka na uliosafi nyororo kama maziwa umesimuliwa na vitabu sahihi na mwanzoni mwavyo sahihi ya Imamu Al-Bukhary ambaye alikuwa amehifadhi Hadithi mia tano elfu. Kwa hiyo hayo ni mapokezi sahihi hakuna shaka ndani yake katu na ya kweli na yenye kuthibiti kana kwamba yanashuhudiwa kwa kuona kwa macho kabisa, kama alivyosimulia mwanafunzi wa madrasa ya Kiahmadia takatifu, madrasa ya Sufa, yule mwanafunzi mwenye kuaminika Al-Haafidh Abu Hurayra, amesimulia kwa jina la watu wa Sufa wote na kuwashuhudisha juu ya hilo. Na ambaye haipokei habari hii kwa mapokeo kama vile anaishuhudia, mtu huyu ima ni fisadi wa moyo au mkosaji wa akili. Je, waonaje ni katika yanayo yumkinika kwamba sahaba mtukufu mfano wa Abu Hurayra mkweli ambaye amejitolea uhai wake katika kuhifadhi Hadithi za Mtume, aangushe thamani ya kile alichokihifadhi katika Hadithi za Mtume aeleze ambacho kinachokoza shaka na utata na aseme kinachohalifu haki na uhalisia, na yeye ndiye ambaye amesikia kauli ya Mtume (s.a.w): (Mwenye kunisingizia kwa makusudi basi na aandae makalio yake Motoni)? Hasha kwake na hilo. Basi ewe Bwana mlezi kwa utukufu wa baraka ya Mtume huyu Mkarimu (s.a.w), tupe baraka katika ulivyotupa katika riziki za kimaada na kimaanawy.
Ni wazi kila vinapokusanyika vitu vya chini dhaifu hupata nguvu. Zikichukuliwa nyuzi nyembamba na kuunganishwa pamoja hugeuka kuwa ni fundo madhubuti lisilokatika. Hapa tumetoa mifano kumi na sita ya sehemu katika sehemu kumi na tano ya aina ya muujiza wa baraka ambazo zinawakilisha aina katika aina kumi na tano ya aina za miujiza, na kila mfano tulioleta ni wenye nguvu wenyewe kwa dhati yake na peke yake unatosha kuthibitisha Utume. Na lau tungekadiria - makadirio ya muhali - kwamba baadhi yake ni dhaifu hauna nguvu wenyewe kwa dhati yake, haijuzu kuuhukumia kwamba mfano hauna nguvu ya kuwa dalili ya muujiza kwa sababu hupata nguvu kwa kuafikiana kwake na wenye nguvu. Kisha kukusanyika mifano hii kumi na sita ambayo imo katika daraja ya tawatur ya kimaanawy kunajulisha muujiza mkubwa wenye nguvu, lau ungechanganywa muujiza huu pamoja na baki ya sehemu kumi na nne katika miujiza yake (s.a.w) kuhusu baraka ambayo hapa haikutajwa, ungekuwa ni muujiza mkubwa kama kamba zilizoungana pamoja ambazo hazina kukatika. Kisha kama utaongezea muujiza huu mkubwa wenye nguvu katika miujiza mingine kumi na nne ungeona hoja yenye nguvu isiyotetereka, hoja ya wazi juu ya unabii wa kweli. Kama hivi basi nguzo ya unabii wa Muhammad ni nguzo kama mlima mkubwa unaundika kutokana na jumla ya miujiza hii. Hapana shaka kwamba umetambua sasa uduni na uzuzu wa anayeona jengo hili kubwa lenye kuimarika la unabii kisha anadhani kuwa linaporomoka kwa sababu ya dhana tata zenye kuanguka zinapita katika dhana yake katika sehemu ndogo ndogo za mifano. Naam, hakika ya miujiza hiyo ambayo inahusu baraka katika chakula inajulisha kwa namna ya kukinaisha juu ya unabii wa Muhammad (s.a.w) na kwamba yeye ni mwaamrishwa Mwenye kupendwa kwa yule Mwenye kurehemu Mwingi wa ukarimu ambaye anatunuku riziki na anaiumba. Na yeye ni mja mkarimu kwake kwa namna anamletea viongezo vilivyojaa kwa aina za riziki – kinyume na ilivyozoeleka – kutoka katika hakuna na kutoka katika hazina za ghaibu ambazo hazitindikii. Na inajulikana kwamba bara Arabu ni eneo lenye uhaba wa maji na kilimo kwa kiasi kwamba watu wake - hasa mwanzoni mwa Uislamu - walikuwa katika dhiki ya maisha na shida na uhaba wa maji na kuwa katika hatari ya kiu. Kwa msingi wa hekima hii, imedhihiri miujiza muhimu zaidi ya Muhammad ya wazi zaidi katika chakula na maji. Miujiza hii kwa hiyo ni sawa na takrima ya kiungu Mola Mlezi, na hisani ya kiungu Mola mwaabudiwa wa haki, na dhifa ya Mwingi wa Rehema kwa Mtume Mtukufu (s.a.w), anamkirimu kulingana na haja, basi hiyo takrima zaidi kuliko kuwa ni dalili ya Utume. Kwa sababu ambao wameona miujiza hii, walikuwa ni waumini imani yenye nguvu kwa Utume. Muujiza kila unapodhihiri imani inaongezeka na kupata nguvu, na kama hivyo miujiza hii inawaongezea nuru juu ya nuru ya imani yao.
Inabainisha Sehemu Ya Miujiza Ambayo Inahusiana Na Maji.
Hakika ya matukio ambayo yanatokea mbele ya macho ya watu, Ikiwa yatanukuliwa kwa njia ya Aahadi na hayakukadhibishwa ni dalili ya ukweli wa kutokea kwake, kwa sababu maumbile ya mwanadamu yameumbwa juu ya kufedhehesha uongo na kuukataa. Na hasa hao ambao hawanyamazi juu ya uongo nao ni sahaba wema. Na hasa ikiwa matukio yanaambatana na Mtume (s.a.w), na hasa zaidi kwamba wasimuliaji ni katika mashuhuri wa sahaba. Msimuliaji wa habari hiyo moja anakuwa wakati huo kana kwamba yeye ni mwakilishi wa kundi hilo ambalo limeshuhudia ushahidi wa kuona kwa macho. Kwa kujua kwamba kila mfano katika mifano ya miujiza inayoambatana na maji ambayo tutaichunguza umepokewa kwa njia nyingi, kutoka kwa wengi wa sahaba wema na kuupokea maimamu wa Taabiina na wanazuoni wao kwa kuhifadhi na kukabidhi kila riwaya kati ya hizo kwa uaminifu mkubwa kwa wale ambao wanakuja baada yao katika enzi nyinginezo. Enzi ambayo baada yao imezipokea kwa bidii na uaminifu na kwa zamu yao wakazinakili kwenda kwa wanazuoni wa enzi iliyofuatia. na kama hivyo walipokezana juu yake maelfu ya wanazuoni watukufu katika kila enzi na kila tabaka, hata ikafika katika siku zetu hizi, ukiachilia mbali kwamba vitabu vya Hadithi viliandikwa katika enzi za Utume na kukabidhiwa kutoka mkono kwenda kwenye mkono hata vikafika katika mikono ya maimamu wa Hadithi mfano wa Bukhary na Muslim wakazifahamu ufahamu kamili, na wakazipambanua riwaya hizi kulingana na ngazi zake, na walisimama kukusanya kila kilichokuwa sahihi iliyo takasika na vumbi la utata katika sahihi zao, wakatuelekeza katika yenye kusibu. Allah awalipe kheri. Mfano: Kutiririka maji kutoka kwenye vidole vya Mtume (s.a.w) na kuwanywesha watu wengi, ni tukio Mutawatir. Wamelinakilia kundi la watu wengi haiyumkiniki kuafikiana kwao katika uongo bali ni muhali wao kuongopa. Basi muujiza huu kwa hiyo ni thabiti wa kukinaisha, ukiachilia mbali kwamba umekariri mara tatu mbele ya makundi makubwa matatu. Tukio hili wamelipokea kwa mapokezi sahihi kundi la mashuhuri wa kisahaba, na mwanzoni mwao ni Anas (Mtumishi wa Mtume (s.a.w)) na Jabir na Ibn Masuud na wameinakili kwetu – kwa nyororo za njia – Maimamu wa Hadithi mifano ya Bukhary, Muslimu, Imamu Maliki, Ibn Shuaybu na Qatadah Mungu awaridhie. Na tutataja mifano tisa tu katika miujiza inayoambatana na maji.
Imethibiti katika sahihi ya Bukhary na Muslim na wengine: Kutoka kwa Anas bin Malik amesema (Nimemwona mjumbe wa Allah (s.a.w) na umefika wakati wa swala ya Alasiri watu wakatafuta udhu (Maji) hawakuupata). Akasema: Aliletewa Mtume (s.a.w) chombo naye akiwa Al-Zawraa, akaweka mkono wake kwenye chombo, maji yakawa yanabubujika kutoka baina ya vidole vyake, watu wakatawadha. Qatadah akasema: Nilimwambia Anas: Mlikuwa wangapi? Akasema: Mia tatu au zaidi ya mia tatu. Basi unaona kwamba Anas (r.a) anaelezea tukio hili kwa sifa yake kuwa ni mwakilishi wa wanaume mia tatu. Basi je inayumkinika wasishirikishwe hao watu mia tatu katika habari hii kimaana na je inayumkinika wasimkadhibishe – hasha - ikiwa tukio hili halikutokea kiukweli?
Imethibiti katika sahihi na mwanzoni mwake Bukhary na Muslim: (Kutoka kwa Salim bin Abil Ja’d kutoka kwa Jabir Ibn Abdallah Al-Answary (r.a) amesema: Watu walipata kiu siku ya hudaibiya na Mtume (s.a.w) mbele yake kulikuwa na rakwa (Chombo cha ngozi kinatumika kutawadhia), akatawadha, wakasongamana watu upande wake akasema: Mna nini? Wakasema: Hatuna maji ya kutawadha wala kunywa, ila yaliyo mbele yako. Amesema Jabir: Mtume (s.a.w) akaweka mkono wake katika rakwa yakawa maji yanafoka kutokea kati ya vidole vyake, kama mifano ya chemchem, tukanywa na tukatawadha. Amesema Salim: Nilimwambia Jabir: Mlikuwa wangapi? Akasema: Tungekuwa mia moja elfu yangetutosha, tulikuwa kumi na tano mia). Unaona kwamba wapokezi wa muujiza huu wanafikia watu elfu moja na mia tano kwa upande wa kimaana kwa kuwa mwanadamu ameumbwa kuufedhehesha uongo na kuuambia uongo: Huu ni uongo. Basi vipi sahaba hawa wema ambao wamejitolea roho zao, mali zao, baba zao, wana wao, watu wao na makabila yao katika njia ya haki na ukweli? Ukiachilia mbali kwamba ni muhali kuwa wao wanyamazie uongo baada ya kusikia kuhofisha kwa kuogofya katika Hadithi sharif: (Mwenye kunisingizia mimi kwa makusudi na ajiandae makao yake motoni). Maadamu hawakupinga habari hii bali wameikubali na wameiridhia, kwa hiyo wamekuwa ni wenye kushiriki katika mapokezi na wenye kuyasadiki kwa upande wa maana.
Vitabu sahihi vinasimulia (Na katika hivyo Al-Bukhary na Muslim) katika kutaja vita vya (Buwat) kwamba Jabir amesema: (Ameniambia Mtume wa Allah (s.a.w): Ewe Jabir ita udhu) pakasemwa hatuna maji. Akataka maji kidogo. Akaletewa Mtume (s.a.w) akaingiza mkono wake, na akaongea kitu sikijui ni nini. Na kasema: Ita chungu cha wasafiri, nikaleta nikakileta mbele yake, na akasema kwamba Mtume (s.a.w) amekunjua mkono wake kwenye chungu na katawanya vidole vyake. Na jabiri akamwagilia na akasema: Bismillah! Amesema: Nikaona maji yanabubujika kati ya vidole vyake, kisha chungu kilitoa maji na kuzunguka hadi kikajaa, na akaamrisha watu kunywa walikunywa hata wakakata kiu. Nikasema: Je amesalia mtu ambaye mwenye haja? Mtume (s.a.w) akanyanyua mkono wake kwenye chungu hali ya kuwa kimejaa. Basi muujiza huu wa dhahiri ni mutawatir kwa upande wa maana, kwa sababu Jabir alikuwa katika mwanzo wa wenye kushuhudia basi ni katika haki yake kwa hiyo yeye kuzungumzia hilo, na kulitangaza kwa ulimi wa watu hao ambapo yeye alikuwa anamhudumia Mtume (s.a.w) wakati huo. Na katika mapokezi ya Ibn Masuud katika sahihi: Na hakika nimeyaona maji yanabubujika kutoka kati kati ya vidole vya Mjumbe wa Allah (s.a.w). Je unaona ikiwa sahaba wenye kutegemewa watukufu mfano wa Anas na Jabir na Masuud wakipokea na akasema kila mmoja (Nimeona), Je ni katika yanayo yumkinika kwao kutoona? Na baada ya hayo, unganisha mifano hii pamoja, ili uone kiasi cha nguvu ya muujiza huu wa wazi, kwa sababu njia tatu zikiungana zitathibitisha mapokezi hayo uthibitisho wa kukinaisha kwa tawatur ya kimaanawy, kwamba maji yalikuwa yanafoka kutoka baina ya vidole vyake (s.a.w). Basi muujiza huu ni mkubwa na wa hadhi ya juu mno kuliko Musa (a.s) kupasua maji na kutoka chemchem kumi na mbili kutoka kwenye jiwe, kwa kuwa kuchimbuka maji kutoka katika jiwe ni kitu yamkini kina mwenza kulingana na kawaida, lakini hakuna mwenza katika kufoka maji kutoka katika nyama na mfupa kama Al-Kawthar As-Salsabil (Mito ya peponi).
Amepokea Imamu Maliki katika kitabu chake cha thamani mno (Al-Muwatta) kutoka kwa sahaba watukufu (Kutoka kwa Muadh bin Jabal katika kisa cha vita vya (Tabuk) kwamba walipita kwenye chemchem na hali ya kuwa ikiwa inatiririka kiasi cha maji mfano wa kamba ya viatu) Mtume wa Allah (s.a.w) akaamrisha kuwa: Kusanyeni kutokana na maji yake (Wakachota kutoka katika chemchem kwa mikono yao hata yakakusanyika katika kitu. Kisha Mtume (s.a.w) akaosha ndani ya maji hayo uso wake na mikono yake na akayarejesha humo yakatoka maji mengi watu wakanywa) hata amesema katika Hadithi ibn Is-haka (Ikapasuka katika maji sauti kama sauti ya vimbunga. Kisha akasema: Inakaribia ewe muadh ukiwa na uhai mrefu kuona yamejaa viunga) na ikawa kama hivyo.
Amepokea Bukhary kutoka kwa Al-Barraa, na Muslimu kutoka kwa Salamata Bin Al-Akwai, na kutoka kwenye njia nyingine katika vitabu sahihi vingine (Tulikuwa siku ya Hudaibiya mia kumi na nne, na Hudaibiya ni kisima, tukayanywa, hata hatukuacha katika hayo japo tone akakaa Mtume kwenye ukingo wa kisima akaagiza maji akasukutua na akayatema kwenye kisima tukakaa mahali sio mbali na tukanywa hata tukakata kiu na kukata kiu vipando vyetu) Amesema Al-Barraa: Mtume (s.a.w) aliamuru ndoo ya maji yake, tukayaleta, akatema mate yake kutoka kwenye kinywa chake chenye baraka na akaomba, kisha baada ya hapo akamimina ndoo katika kisima maji yakaja juu na kuinuka ujazo wa mdomo wake wakajinywesha nafsi zao na vipando vyao.
Wamesimulia maimamu wa Hadithi, mfano wa Muslim na Ibn Jariri At-Tabary na wengine wasiokuwa hao wawili kutoka kwa Abi Qatada kwamba amesema: (Hakika ya Mtume (s.a.w) aliwatokea hali ya kuwa akiwapa msaada watu wa Muutah wakati ilipomfikia kuuliwa kwa maamiri) na nilikuwa na chombo cha kutawadhia. Mtume (s.a.w) akasema: اِح۟فَظ۟ عَلَىَّ مٖيضَئَتَكَ فَسَيَكُونُ لَهَا نَبَأٌ عَظٖيمٌ (Nihifadhie chombo cha kutawadhia chako hakika kitakuwa na habari) na baada ya hapo kiu kikaanza kutuzidia na tulikuwa sabini na mbili - na katika riwaya ya At-Tabary – tulikuwa zaidi ya mia tatu - Mtume (s.a.w) akasema: (Lete chombo cha kutawadhia chako, nikakileta akakichukua na akaweka mdomo wake kwenye mdomo wake na sikujua je alipulizia humo au hapana? Kisha baada ya hapo wakaja wanaume sabini na mbili wakanywa kutokana na hicho na wakajaza vyombo vyao kisha baada ya hapo nikakichukua – yaani chombo cha kutawadhia – kikabaki mfano wa kilivyokuwa) basi zingatia katika muujiza huu wa wazi na useme: Ewe Mola mpe rehema na amani kwa idadi ya matone ya maji.
Na amesimulia Al-Bukhary na Muslim kutoka kwa Amran bin Husein wakati ambapo kiu kilimsibu Mtume (s.a.w) na sahaba zake katika baadhi ya safari zao (Tulikuwa katika safari pamoja na Mtume (s.a.w), watu wakalalamika kwake kutokana na kiu akateremka, na akamwita Ali akasema: Nendeni mkatafute maji, wakaenda wakamkuta mwanamke kati kati ya vyombo viwili, wakamleta kwa Mtume (s.a.w), Mtume (s.a.w) akaita chombo (kiletwe) akamimina ndani ya chombo hicho kutoka katika midomo ya vyombo viwili (vya yule mwanamke), na pakalinganiwa kwa watu kunyweni kunyweni, na kwa hakika yanatujia mawazo kuwa kilikuwa kimajaa zaidi kuliko ilipoanza (kujazwa) ndani yake). Na Mtume (s.a.w) amesema: Kusanyeni wakakusanya kwa ajili yake, hata wakamkusanyia chakula wakakijaalia kwenye nguo na wakakibeba juu ya ngamia wake (yule mwanamke), akasema: Unajua kuwa hatukupunguza chochote katika maji yako lakini Allah (s.w) ametunywesha. Mpaka mwisho wa Hadithi.
Amepokea ibn Khuzayma Hadithi ya (Umar (r.a) katika jeshi la Usrah, na akaeleza yaliyo wasibu katika kiu hata kwamba mtu anamchinja ngamia wake na anakamua utumbo wake na kunywa maji yake, Abubakar alimpendekeza Mtume (s.a.w) kuomba dua. Akanyanyua mikono yake hakuirejesha mpaka mbingu ikafunika na kunyesha mvua nyingi wakajaza vyombo walivyonavyo na hakurukwa askari). Basi huu ni muujiza wa Muhammad (s.a.w) msafi hakuna kuingilia kwa sadfa humo katu.
Kutoka kwa Amru bin Shuaib (Mjukuu wa Abdallah bin Amru bin Al-As) ambaye wamemkubali maimamu wanne kuwa ni wakutegemewa katika watu wa Sunna katika kutoa kwake Hadithi: (Hakika Abu Twalib alimwambia Mtume (s.a.w) na hali akiwa mwenye kufuatana naye huko Dhy al-majaz: Nimepata kiu na sina maji. Mtume (s.a.w) akashuka na akapiga Ardhi kwa mguu wake yakatoka maji, akasema kunywa). Mmoja wa wanazuoni wahakiki amesema: Tukio hili lilikuwa kabla ya Utume. Kwa hiyo hilo ni katika Irahasaat (miujiza kabla ya Utume) na kuchimbuka maji chemchem ya Arafa baada ya kupita miaka elfu moja inahesabiwa katika takrima za Allah (s.w) kwa Mtume Mkarimu (s.a.w). Na kama hivyo miujiza inayoambatana na maji, hata ikiwa haikufikia mifano tisini katika mifano ya hii tisa isipokuwa ni kwamba hiyo imepokewa kwa pande tisini. Na mifano saba ya mwanzo ni yenye nguvu, na ya kukinaisha, kama tawatur ya kimaanawy. Ama mifano miwili ya mwisho – hata kama njia zake si zenye nguvu na nyingi na wasimulizi wake ni wengi isipokuwa watu wa Hadithi kama Imamu Al-Bayhaqy na Al-Hakim wamepokea kutoka kwa Umar (r.a) muujiza wa pili kuhusu mawingu kuunga mkono muujiza katika mfano wa nane ambao ameupokea Sayyidina Umar. Na riwaya ni kwamba: (Kiu kiliwasibu watu katika baadhi ya vita vyake (s.a.w), Umar akamwomba dua, akaomba, kikaja kiwingu kikawanyeshea kiasi cha haja yao kisha kikaondoka) kana kwamba kiwingu kilikuwa kimeamrishwa kunyeshea jeshi tu - ambapo kilinyesha kulingana na haja - basi kama tukio hili linavyounga mkono mfano wa nane na kuutia nguvu, na kuubainisha kwa masimulizi thabiti ya kukinaisha, hakika Ibn Al-Jawzy - ambaye anashika msimamo mkali na kuzikataa hata Hadithi sahihi na kuzijaalia katika hesabu za Hadithi Maudhui – anasema: Hakika tukio hili limetokea katika vita vya Badr na kulihusu imeteremka aya tukufu: وَيُنَزِّلُ عَلَيْكُم مِّن السَّمَاء مَاءً لِّيُطَهِّرَكُم بِهِ basi maadamu aya hii imeteremka kuhusu vita hiyo na kuibainisha kwa uwazi, kwa hiyo basi hakuna shaka kutokea kwake. Na imekariri mara nyingi kuteremka kwa mvua kwa dua ya Mtume (s.a.w) kabla ya kushuka mikono yake miwili iliyonyanyuliwa na huo ni muujiza unaojitegemea kwa mpaka wa dhati yake. Na aliomba mvua Mtume (s.a.w) nyakati nyinginezo na hali akiwa kwenye Mimbari, na mvua ziliteremka kabla ya kushusha mkono wake na hili limethibiti kupitia njia iliyo Mutawatir.
Hakika moja ya miujiza ya Mjumbe mkarimu (s.a.w) ni miti kutekeleza amri zake kama utekelezaji wa watu, na kung’oka kwake kutoka mahali pake na kumwendea. Basi muujiza huu unaoambatana na miti ni mutawatir kwa upande wa maana kama kutoka maji (kwa kasi) kutoka katika vidole vyake vyenye baraka na una sura nyingi. Na umepokewa kwa njia nyingi. Naam, inasihi kusemwa kwamba habari ya kung’oka mti kutoka mahali pake na kuja kwake kwa kutekeleza amri ya Mtume mkarimu (s.a.w) na Mutawatir kwa namna ya usahihi, ambapo mapokezi haya yamesimuliwa kutoka kwa sahaba wema wa kweli maarufu, mifano ya: Ali, Ibn Abbas, Ibn Masud, Ibn Umar, Yaalaa bin Murrat, Jabir, Anas Bin Malik, Buraydat, Usamah bin Zayd na Ghaylan bin Salamat, na wengineo kila mmoja basi kati yao ameelezea muujiza huu unaoambatana na miti habari thabiti ya kukinaisha. Na wameyapokea kutoka kwao mamia ya maimamu wa Tabiina kwa njia tofauti, na mwanzoni mwa kila njia kuna sahaba mtukufu, yaani kana kwamba mapokezi hayo yamenakiliwa kwetu kwa unakili wa mutawatir wenye kuongezeka maradufu. Kwa hiyo shaka haingilii muujiza huu wala utata katu. Huo basi ni katika hukumu ya mutawatir ya kimaanawy uliokatiwa shauri. Basi muujiza huu inagawa umekariri mara nyingi, isipokuwa sisi tutabainisha idadi ya sura zake sahihi nyingi, na kuzileta katika mifano michache:
Amepokea bin Majah, Ad-Daramy na Al-Bayhaqy kutoka kwa Anas bin Malik na Aly, na amepokea Al-Bazzar na Al-Bayhaqy kutoka kwa Umar (r.a), kwamba watatu katika sahaba wema (r.a) wamesema: Mtume (s.a.w) alikuwa amehuzunika huzuni kubwa kutokana na makafiri kumkadhibisha yeye (Amesema: Ewe Mola! Nioneshe ishara sitojali atakayenikadhibisha baada yake). Na katika mapokezi ya Anas (Hakika Jibril (a.s) alimwambia Mtume (s.a.w) na alimwona akiwa amehuzunika: Je unapenda nikuoneshe ishara. Akasema: Naam! Mtume (s.a.w) alitazama mti nyuma ya bonde, akasema: Uite mti ule, ukaja ukitembea hadi ukasimama mbele yake, akasema: Uamrishe urejee, ukarejea mahali pake).
Amepokea kadhi Iyadh – Allama wa Moroko – katika kitabu chake (As-Shifaa) kwa sanadi ya juu sahihi kutoka kwa Abdillah Ibn Umar (r.a) amesema: Tulikuwa pamoja na Mtume wa Allah (s.a.w) kwenye safari, bedui akamkaribia, akasema: Ewe bedui: Unakusudia wapi? Akasema: Kwa jamaa zangu. Akasema: Je ungepata kheri? Akasema: Na ni ipi hiyo? akasema: Ushuhudie kuwa hakuna Mungu apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah peke yake hana mshirika na kuwa Muhammad ni mja wake na Mtume wake. Akasema: Nani atakaye kushuhudia unayoyasema? Akasema: Huu mti wa As-Samura , nao ukiwa ukingoni mwa bonde, ukaja ukipasua Ardhi, hata ukasimama mbele yake, akautaka shahada mara tatu ukashahadia kwamba ni kama alivyosema. Kisha ukarejea mahali pake. Na kutoka kwa Buraidah kupitia njia ya swahib Al-Aslamy kwa unakili sahihi: Bedui alimuuliza Mtume (s.a.w) ishara akamwambia: Uambie ule mti, Mjumbe wa Allah anakuita. Amesema: Mti ukayumba kuliani kwake na kushotoni kwake na mbele yake na nyuma yake, mizizi yake ikakatika katika, kisha ukaja hali ya kuwa unapasua Ardhi ukivuta mizizi yake kwa haraka hata ukasimama mbele ya mjumbe wa Allah (s.a.w) ukasema: Assalam Alayka ya Rasuulallah. Bedui akasema: Uamrishe urejee katika maoteo yake. Ukarejea ukashusha mizizi yake na kusimama sawa sawa. Bedui akasema: Nipe idhini nikusujudie. Akasema: Lau ningemwamrisha yeyote amsujudie yeyote ningemwamrisha mwanamke amsujudie mumewe, akasema: Basi nipe idhini nibusu mikono yako na miguu yako, akampa idhini.
Amepokea Muslim na watu wa vitabu sahihi vingine kutoka kwa Jabir (r.a): Kwamba amesema: Tulikuwa katika safari pamoja na Mtume wa Allah (s.a.w), Mtume wa Allah (s.a.w) alikwenda kukidhi haja yake, hakuona kitu cha kujisitiri nacho, ghafla miti miwili kwenye ukingo wa bonde, akaenda Mtume wa Allah (s.a.w) kwa mmoja wapo kati ya miwili hiyo, akachukua tawi katika matawi yake, akasema: اِل۟تَئِمَا عَلَىَّ بِاِذ۟نِ اللّٰهِ Nifuate kwangu kwa idhini ya Allah ukamfuata pamoja naye mfano wa ngamia mwenye kuvutwa na kamba ambaye anamtii kiongozi wake, na ametaja kwamba yeye alifanya kwa mwingine mfano wa hivyo hata ikawa mahali pa katikati kati yao, akasema: Jikusanyeni kwangu (Mnisitiri) yakajikusanya akakaa nyuma yake, na baada ya kuwa amekidhi haja yake, aliamrisha kurejea kila moja kati ya mawili hayo mahali pake. Na katika mapokezi mengine, akasema: Ewe Jabir! Uambie mti huu: يَا جَابِرُ قُل۟ لِهٰذِهِ الشَّجَرَةِ يَقُولُ لَكِ رَسُولُ اللّٰهِ: اِل۟حَقٖى بِصَاحِبَتِكِ حَتّٰى اَج۟لِسَ خَل۟فَكُمَا Mtume wa Allah (s.a.w) anakwambia kaungane na mwenzi wako hata nikae nyuma yenu. Ukatambaa hata ukaungana na mwenziwe. Akakaa nyuma ya miti hiyo miwili, nikatoka mbio, nikakaa ninaisemesha nafsi yangu, nikageuka tahamaki mjumbe wa Allah (s.a.w) akija, na miti miwili imetengana, kila mmoja kati yao ulisimama kwa mlingoti, mjumbe wa Allah (s.a.w) alisimama kisimamo akasema kwa kichwa chake kama hivi kulia na kushoto.
Usama Bin Zaid amepokea - mmoja wa viongozi wa mjumbe wa Allah (s.a.w) na mtumishi wake wa kulia - : Tulikuwa katika safari pamoja na Mtume wa Allah (s.a.w), na hakukuwa na mahali patupu kwa ajili ya kukidhi haja panapositiri mbali na macho ya watu, akasema: Je unaona Mtende wowote au mawe? Nikasema: Ninaona mitende imekaribiana, akasema: اِن۟طَلِق۟ وَقُل۟ لَهُنَّ اِنَّ رَسُولَ اللّٰهِ يَأ۟مُرُكُنَّ اَن۟ تَا۟تٖينَ لِمَخ۟رَجِ رَسُولِ اللّٰهِ وَقُل۟ لِل۟حِجَارَةِ مِث۟لَ ذٰلِكَ Nenda na ukaiambie kwamba Mjumbe wa Allah (s.a.w) anakuiteni mahali alipokwenda Mtume (s.a.w) kwa ajili ya haja na uyaambie mawe mfano wa hivyo. Nikayaambia hivyo, basi naapa kwa ambaye amemtuma kwa haki nimeiona mitende inakaribiana hadi ikakutanika na mawe yanasongana hata yakawa ni rusu nyuma yake, na alipokidhi haja yake aliniambia: Yaambie yatawanyike, naapa kwa ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake nimeiona pamoja na mawe inatawanyika hata ikarudi mahali pake. Matukio haya mawili mbayo ameyasimulia Jabir na Usama wameyapokea wote Ya’laa bin Murrat, Ghaylan bin salamat Al-Thaqafy na Ibun Masuud katika vita vya Hunayn.
Ametaja Allama wa zama zake Imamu ibn Fawrak - ambaye aliyekuwa akiitwa Shafiiy wa pili ikiwa ni fumbo la juhudi yake kamili na fadhili yake - : (Hakika yeye (s.a.w) alikwenda katika vita vya Taif wakati wa usiku hali ya kuwa anasinzia, ukampinga mkunazi, ukachanika kwa ajili yake na kuwa nusu mbili hata akavuka kati kati ya nusu mbili hizo, na ukabaki ukiwa katika milingoti miwili hata wakati wetu).
Ametaja Ya’laa Bin Siyaba: Kwamba Twalha Au Sumrata ilikuja na kumzunguka kisha ikarejea katika maoteo yake Mjumbe wa Allah (s.a.w) akasema: Hakika miti hiyo imeomba idhini kunisalimia. Yaani imetaka idhini kutoka kwa bwana mlezi wa walimwengu.
Wamepokea Masheikh wawili kutoka kwa Ibn Masuud (r.a): Kwamba amesema: (Mti ulimtangazia Mtume (s.a.w) Majini siku walipomsikiliza) na hii wakati walipokuja Majini wa Nasibain katika tumbo la Mtende kwa Mtume (s.a.w) kwa ajili ya kusilimu, mti ukatangaza habari ya kuja kwao kwa Mtume (s.a.w). (Na imepokewa kwa Mujahidi kutoka kwa Ibn Masuud katika Hadithi hii: Hakika Majini walisema nani atakayekushuhudia? Akasema: Mti huu) Akauamuru mti (Njoo ewe mti! Ukaja hali ya kuwa unakokota mizizi yake ukiwa na sauti). Na kama hivi, umetosha muujiza mmoja taifa la Majini. Je haiwi kwa anayesikia miujiza elfu moja na muujiza mmoja wa mifano yake kisha anafanya kiburi wala haamini ni mpotevu zaidi kuliko yule Sheitani ambaye Qur’an imemzungumzia kwa kauli ya Majini. يَقُولُ سَفِيهُنَا عَلَى اللَّهِ شَطَطًا
Amepokea At- Tirmidhy kutoka kwa ibn Abbas (ra), hakika (s.a.w) alimwambia Bedui: اَرَاَي۟تَ اِن۟ دَعَو۟تُ هٰذَا ال۟عِذ۟قَ مِن۟ هٰذِهِ النَّخ۟لَةِ اَتَش۟هَدُ اَنّٖى رَسُولُ اللّٰهِ؟ (Je unaonaje nikiliita hili karara la mtende kutoka katika mtende huu utashuhudia kuwa mimi ni mjumbe wa Allah? akasema: Naam! Akaliita likawa linachupa hata likamjia akasema: Rejea, likarudi mahali pake). Na kama hivi, kuna mifano mingi kama ambayo tumeitaja yote imepokewa kwa njia nyingi, na katika yanayojulikana kwamba zikiungana nyuzi kadhaa nyembamba hugeuka kuwa kamba yenye nguvu. Basi mfano wa muujiza huu unaoambatana na mti na umepokewa kwa njia nyingi, na kutoka kwa mashuhuri wa sahaba wema hapana budi kwamba huo una nguvu ya tawatur ya kimaanawy, bali ni mutawatur kwa tawatur ya kihakika. Na hakuna shaka kwamba ulipohama kwenda kwa tabiina umechukua hali ya tawatur, na hasa njia ambazo wamezipita watu wa sahihi kama Bukhary, Muslim, Ibn Hibban, At-Tirmidhy na wengine, hakika hiyo ni njia sahihi haina vumbi ndani yake. Bali kuiona Hadithi yoyote iwayo kwenye Bukhary hakika huko ni kama kuisikiliza kutoka kwa sahaba wema wenyewe kwa dhati yao. Unaona ikiwa miti inamjua Mjumbe wa Allah (s.a.w) na kumjulisha na kusadiki Utume wake na imemsalimia, na kumzuru, na imetekeleza amri yake – kama tulivyoona katika mifano iliyotajwa huko nyuma – basi vipi asimjue wala kumwamini yule mpumbavu asiye na roho ambaye anajiita nafsi yake kuwa ni Mwanadamu? Je huyu sio mtupu wa akili na moyo? Je hawi duni kuliko mti mkavu na wakupuuzwa kuliko kuni ambayo haistahiki isipokuwa kuitupia motoni?.
Hakika ya ambacho kinaunga mkono miujiza hii inayoambatana na miti ni muujiza wa kilio cha kigogo cha mtende kilichonakiliwa kwa tawatur. Naam, hakika kilio cha shina kavu lililokuwapo katika msikiti wa Mtume (s.a.w) kwa Mtume wa Allah (s.a.w) kwa ajili ya kutengana naye – kutengana kwa muda - na kunung’unika kwake mbele ya kundi la watu wengi la sahaba wema inatilia nguvu mifano ambayo tumeitoa katika miujiza inayoambatana na miti na kuitia nguvu. Kwa kuwa shina ni katika jinsi ya miti, jinsi ni moja, isipokuwa muujiza huu kwa dhati yake ni mutawatir, wakati ambapo sehemu nyingine ni mutawatir kinamna, kwani vijisehemu vyake vingi na mifano yake havipandi katika ngazi ya tawatur ya wazi. Msikiti wa Mtume (s.a.w) ulikuwa umewekwa dari kwa mashina ya mtende akawa Mtume (s.a.w) akihutubu anasimama katika moja ya mashina yake, alipotengenezewa mimbari, na akawa juu yake, ilisikika kwa kishina hicho sauti kama sauti ya ngamia mwenye mimba naye akiugua na kulia, hata akaja Mtume (s.a.w) na akaweka mkono wake juu yake, na akazungumza nacho na akakiliwaza, kishina kikanyamaza. Muujiza huu umenakiliwa kwa njia nyingi kwa kunakili kwa mutawatir. Naam, muujiza wa kilio cha kishina ni mashuhuri na umeenea, na habari yake ni katika mutawatir ya wazi, wameupokea mamia katika maimamu wa kitaabiina kwa njia kumi na tano kutoka kwa kundi katika sahaba wema (r.a), na kama hivi wameunakili kwa wanaokuja baada yao. Na kutoka kwa waliousimulia katika wanazuoni wa kisahaba: Anas bin Malik – Mtumishi wa Mtume (s.a.w) –na Jabir bin Abdallah Al-AnSwary, Abdallah ibn Umar, Abdallah Ibn Abbas, Sahal bin Saad, Abu Said Al-khudry, Ubayy Bin Kaab, Buraidat na mama wa waumini Umm Salamata (r.a) na kila mmoja kati ya hawa yuko kwenye kichwa cha njia katika njia za wapokezi wa Hadithi. Hakika amepokea Bukhary na Muslim na wengineo katika wenye Sahihi muujiza huu mkubwa wenye kuja kwa tawatur na wameunakili kwetu. Kutoka kwa Jabir anasema: (Msikiti Uliezekwa kwa vishina vya mitende Mtume (s.a.w) akawa akihutubia anasimamia kwenye kishina kimojawapo, Alipotengenezewa mimbari na akawa juu yake tukasikia kwa hicho kishina sauti kama sauti ya ngamia wenye mimba hata akaja Mtume (s.a.w) akweka mkono wake juu yake kikanyamaza). Kishina hakikustahamili kutengana naye (s.a.w). Na kutoka kwa Anas: (Mpaka msikiti ukatikisika kutokana na mngurumo wake). Na kutoka kwa Sahal bin Saad: (Na vilio vya watu vikakithiri walipo kiona kishina kikiwa na kilio na minung’uniko). Na kutoka kwa Ubayy bin Kaab: (Mpaka kikapasuka pasuka) kwa nguvu ya kulia kwake. Wamezidisha wengine: Akasema mtume (s.a.w): اِنَّ هٰذَا بَكٰى لِمَا فَقَدَ مِنَ الذِّك۟رِ (Hakika ya hiki kimelia kwa kile kilichokosa katika dhikiri) na wameongeza wengine: لَو۟ لَم۟ اَل۟تَزِم۟هُ لَم۟ يَزَل۟ هٰكَذَا اِلٰى يَو۟مِ ال۟قِيَامَةِ تَحَزُّنًا عَلٰى رَسُولِ اللّٰهِ (Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake kama nisingekinyamazisha kisinge acha kuwa hivi hadi siku ya kiama) kwa ajili ya kumhuzunikia Mtume wa Allah (s.a.w). Na katika Hadithi ya Buraidat: Kishina kilipolia Mtume (s.a.w) aliweka mkono wake mtukufu juu yake na akasema: Ukitaka nakurudisha katika bustani uliyokuwa ndani yake, mizizi yako iote na umbo lako likamilike na zifanyike upya kwa matawi na matunda. Na ukitaka nitakupandikiza peponi wale matunda yako mawalii wa Allah. Kisha Mtume (s.a.w) akakisikiliza asikie kinachosema, kikasema: اِغ۟رِس۟نٖى فِى ال۟جَنَّةِ يَأ۟كُلُ مِنّٖى اَو۟لِيَاءُ اللّٰهِ فٖى مَكَانٍ لَا يَب۟لٰى Bali unipandikize peponi wale mawalii wa Allah kutokana na mimi na niwe katika mahali ambapo sitachakaa hapo, akasikia aliyekifuatia (aliye karibu nacho), Mtume (s.a.w) akasema: Nitafanya hivyo bila shaka yoyote. Kisha akasema: Kimechagua makazi ya kubakia badala ya makazi ya kutoweka. Amesema imamu Abu Is’haka Al-Isfrainy – naye ni katika maimamu wa wanazuoni wa Al-Kalamu - hakika Mtume mtukufu (s.a.w) hakuenda kwa kishina bali (Alikiita kwake kikamjia kikipasua Ardhi akakinyamazisha, kisha akakiamrisha kikarudi mahali pake). Ubayy bin Kaab anasema: Na baada ya kudhihiri kwa muujiza huu: Mtume (s.a.w) aliamrisha kikazikwa chini ya mimbari), (Ikawa Mtume (s.a.w) akiswali huswali mbele yake. Wakati msikiti ulipovunjwa kwa ajili ya kuujenga upya alikichukua Ubayy kikawa kwake mpaka kikaliwa na Ardhi kikawa kimeoza. Na wakati Hassan Al-Basary alipokuwa anasimulia hili kwa wanafunzi wake alikuwa akilia na kusema: (Ewe mja wa Allah! Kigogo kinafanya mahaba kwa Mtume wa Allah (s.a.w) kwa kumfanyia shauku kwa nafasi yake basi nyinyi mna haki zaidi kuwa na shauku ya kukutana naye). Na sisi tunasema: Naam! Kuwa na shauku naye na kumpenda hakika ni kwa kufuata sunna yake na sharia yake angavu. Nukta Muhimu Ikisemwa: Kwa nini haikuwa mashuhuri miujiza hiyo ambayo inahusu baraka katika chakula na ambayo imewashibisha maelfu ya watu katika vita vya Handaki kwa pishi ya chakula, wala miujiza hiyo ambayo inahusu maji ambayo imekata kiu cha watu elfu wakati yalipotoka kwa kasi kutoka kwenye vidole vya Mtume vyenye baraka (s.a.w). Kwa nini haikunakiliwa kwa njia nyingi kama ilivyokuwa mashuhuri muujiza wa kishina kulia na kunakiliwa. Pamoja na kuwa kila moja kati ya makundi hayo mawili - ambayo miujiza imetokea mbele yao - ni wengi kuliko kundi la muujiza wa kilio cha kishina? Jibu: Hakika ya miujiza ambayo imedhihiri ni sehemu mbili: Ya kwanza: Inayodhihiri kwa Mtume (s.a.w) ili kusadikisha madai ya Utume, na kuwa ni hoja yake, hapo basi kuongezeka imani ya waumini na kuwapeleka watu wa unafiki kwenda katika Ikhlasi na Imani, na kuwaita watu wa ukafiri kwenye ngome ya Imani. Na muujiza wa kulia kwa kishina ni wa aina hii, na kwa ajili hiyo wameuona watu wa jumla na watu mahususi na walishughulikia kuueneza zaidi kuliko mwingine. Ama muujiza wa chakula na muujiza wa maji, ni karama zaidi kuliko kuwa kwake ni muujiza, bali ni takrima ya kiungu zaidi kuliko kuwa ni karama, bali ni dhifa ya kiungu Mwingi wa rehema – kulingana na uwepo wa haja – zaidi kuliko takrima ya kiungu. Hiyo miwili japo ikiwa ni dalili mbili za madai ya Utume na ni miujiza miwili kwa ajili yake, isipokuwa kwamba shabaha ya msingi ni kuwa kwamba jeshi ambalo linafika nguzo zake kiasi cha watu elfu moja, lilikuwa linahitaji sana chakula na kinywaji hivyo Allah (s.w) akawapa msaada kutoka katika hazina za ghaibu kiasi cha kuwa aliwashibisha kutokana na pishi moja ya chakula wanaume elfu moja kama anavyoumba Allah kutokana na kokwa moja ratili elfu moja za tende. Vivyo hivyo aliwanywesha na kukata kiu kiasi cha elfu ya wapiganaji katika njia ya Allah (s.w) wakati kilipowasibu kiu, aliwanywesha kwa maji yenye baraka kama Kauthar, kwani aliyapitisha Allah (s.w) kutoka kwenye vidole ya kiongozi wao mkuu (s.a.w). Kwa ajili hiyo daraja ya muujiza wa chakula na maji haikufikia daraja ya kilio cha kupenda cha kishina. Isipokuwa jinsi ya miujiza hiyo miwili na aina yake kulingana na hali ya ujumla ni mutawatir kama kuwa mutawatir kwa kilio cha kishina. Kisha hakika si kila mtu anaweza kuona baraka ya chakula na kububujika maji kwa kasi kutoka katika vidole kwa dhati yake bali anaona athari yake, lakini kila aliyekuwa msikitini amesikia kilio cha kishina, kwa ajili hii kilitangazika zaidi. Ikisemwa: Hakika ya sahaba wema (r.a) walitilia umuhimu mkubwa kwa kuchunguza hali zake zote (s.a.w) na harakati zake zote wakazinakili kwa uaminifu na uangalizi, basi kwa nini ilisimuliwa mifano ya miujiza hii mikubwa kwa njia ishirini tu, na haikusimuliwa – kwa uchache – kwa njia mia moja? Na kwa nini yanakuja mapokezi mengi kutoka kwa Anas, Jabir na Abi Hurayrah, na hayakuja kupitia kwa Abi Bakar na Umar isipokuwa machache yake. Jibu: Upande wa kwanza wa swali jibu lake limepita katika (Msingi wa tatu katika Ishara ya Nne). Ama jibu la upande wa pili ni kwamba mwanadamu anapohitaji dawa anamrejea Tabibu, na akihitaji jengo humrejea mhandisi, na akihitaji kujifunza sheria anamjia mufti na kumuuliza, na kama hivi hakika Jukumu la baadhi ya sahaba lilikuwa limejihusisha tu na kuchukua Hadithi na kuzinakili katika zama zingine. Wakawa wanajitahidi kwa nguvu zote alizowapa Allah (s.w) kutimiza shabaha hii. Basi Abu Hurayra aliukusanya uhai wake wote kwa ajili ya kuhifadhi Hadithi za Mtume (s.a.w). Wakati ambapo alikuwa Umar (r.a) amezama katika kubeba majukumu ya Ukhalifa na siasa ya dola. Kwa hiyo aliwategemea sahaba hawa: Abi Hurayra, Anas na Jabir na wengineo katika kunakili Hadithi tukufu kwa umma, ikawa nadira kwake kupokea Hadithi, kisha hakika msimuliaji mkweli mwenye kusadikiwa na watu wote hutosha masimulizi yake hakuna haja ya masimulizi ya mwingine, na kwa ajili hii yananakiliwa baadhi ya matukio muhimu kwa njia mbili au tatu.
Ishara hii inabainisha muujiza wa mtume unaohusu mawe na milima katika visivyokuwa na roho kama ilivyoashiria (Ishara ya kumi) muujiza wa Mtume kuhusu miti, tunataja kati ya mifano yake mingi mifano minane:
Amesimulia Bukhary na Allamat wa Moroko Al-Qadhy Iyadh kutoka kwa ibn Masuud - Mtumishi wa Mtume (s.a.w) - kwamba amesema: (Tulikuwa tukisikia tasbihi ya chakula na hali kikiliwa).
Na imethibiti vilevile kutoka kwa Anas na Abi Dharri (r.a), amesema Anas: (Mtume (s.a.w) alichukua gao la vijiwe vikafanya tasbihi katika mkono wa Mtume wa Allah (s.a.w) hata tukaisikia tasbihi, kisha akavimimina katika mkono wa Abu Bakar (r.a) vikafanya tasbihi, kisha katika mikono yetu havikufanya tasbihi). Na alisimulia Abu Dharri mfano wake na akaeleza kuwa yalifanya tasbihi katika kiganja cha Umar (r.a) kisha akaviweka juu ya Ardhi vikawa vimenyamaza, kisha akavichukua na akaviweka juu ya kiganja cha Uthumani, vikafanya tasbihi kisha akaviweka juu ya mikono yetu vikanyamaza.
Imethibiti kwa unakili sahihi kutoka kwa Ali, Jabir na Aisha (r.a) hakuwa Mtume (s.a.w) akipita kwenye mlima wala jiwe ila limesema: Assalamu alayka yaa Rasuulallah. Na katika mapokezi ya Ali (r.a) amesema: (Tulikuwa Makka - mwanzoni mwa Utume - pamoja na Mjumbe wa Allah (s.a.w) akatoka kwenda baadhi ya pande zake, basi haukumpokea mti wala mlima isipokuwa umesema: Assalaam Alayka yaa Rasulallah). Na katika mapokezi ya Jabir (r.a) amesema: (Mtume (s.a.w) hakuwa akilipitia jiwe wala mti isipokuwa vilimsujudia) yaani kila moja kati ya hivyo vina mfuata na kusema: Assalaam alayka yaa Rasulallah. Na katika mapokezi mengine Kutoka kwa Jabir bin Sumrat (r.a) kutoka kwa Mtume (s.a.w): (Hakika mimi ninajua kwa yakini jiwe lililopo Makka lilikuwa linanisalimia) yaani kabla ya kupewa Utume (Imesemwa: Hakika hiyo ni ishara ya jiwe Jeusi). Na kutoka kwa mama Aisha (r.a) amesema: Mtume (s.a.w) amesema: Wakati Jibril aliponikabidhi Utume nikawa sipitii kwenye jiwe wala mti isipokuwa vinasema: Assalam alayka yaa Rasuulallah.
(Na katika Hadithi ya Al-Abbas (r.a) wakati alipokusanyika Mtume (s.a.w) na wanawe) nao ni Abdallah, Ubaydillah, Al-Fadhl na Waqatham (kwenye shuka na akawaombea kusitiriwa (kuwekwa mbali) na moto) aliposema: Ewe Mola huyu ni Ami yangu ni mfano wa baba yangu na hawa wanawe basi wasitiri (waweke mbali) na moto kama kusitiri kwangu ninavyowasitiri kwa shuka. (Vikaitikia amin kizingiti cha mlango na kuta za nyumba: Amin Amin) na vikashiriki katika dua.
Vitabu sahihi vimepokea hali ya kuafikiana na mwanzoni mwao Al-Bukhary, Ibn Hibban, Abu Daud na At-Tirmidhy kutoka kwa Anas na Abu Hurayra na kutoka kwa Uthuman Dhy An-Nuurayn na Said bin Zaidi mmoja wa kumi waliobashiriwa pepo kwamba: (Alipanda Mtume (s.a.w) na Abubakar na Umar na Uthman Uhud, ukatetemeka nao) kutokana na haiba zao au kutokana na furaha yake, (Akasema: Uhud tulia hakika juu yako kuna Nabii na Siddiiq na Mashahidi wawili). Kwa hiyo kwa Hadithi hii Mtume (s.a.w) anabashiri kuhusu kufa shahidi kwa Umar na Uthman kuelezea kwa ghaibu. Na imenukuliwa – ukamilisho wa mfano huu – kwamba Mtume (s.a.w) alipohama kutoka Makka na wakamtaka makafiri wa kikuraishi alipanda juu ya mlima wa Thubair. (Thubair ulimwwambia: Shuka ewe mjumbe wa Allah (s.a.w) hakika mimi ninahofia wasije kukuua ukiwa juu ya mgongo wangu akaniadhibu Allah. Hiraa ukamwambia: Njoo kwangu ewe mjumbe wa Allah). Kutokana na hili watu wa moyo na kutengenea na wanahisi hofu kwa (Thubair) na amani na utulivu kwa (Hiraa). Inafahamika kutokana na jumla ya mifano hii hakika ya milima mikubwa ni yenye kuamuriwa na inafuata kama mtu katika watu. Nayo kama mja yeyote kiumbe anamsabihi Allah (s.w) na ana jukumu maalum linalomhusu. Na kwamba anamjua Mtume (s.a.w) na kumpenda, milima haikuumbwa kwa batili.
Na amepokea Ibn Umar (r.a): Hakika Mtume (s.a.w) amesoma juu ya mimbari: وَمَا قَدَرُوا اللَّهَ حَقَّ قَدْرِهِ kisha amesema: Kajitukuza Al-Jabbar nafsi yake anasema: Mimi ndiye Al-Jabbar mimi ndiye mkubwa mwenye utukufu wa juu. Mimbari ikatetemeka hata tukasema itamdondosha.
Kutoka kwa Hibr Al-Ummah na Mkalimani wa Qur’an ibn Abbas (r.a), kutoka kwa Ibn Masuud – miongoni mwa wanazuoni wa kisahaba –(r.a) kwamba amesema: (Pembezoni mwa Al-Kaaba kulikuwapo masanamu mia tatu na sitini imethibitishwa miguu yao kwa risasi kwenye mawe alipoingia mjumbe wa Allah (s.a.w) msikitini mwaka wa Fat’hu alikuwa anaashiria kwa gongo lilikuwa mkononi mwake kuyaelekea wala hayagusi. Na anasema: جَاء الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقًا basi hakuashiria sura ya sanamu yoyote isipokuwa ilianguka kwa kichogo chake na si kichogo ila ilianguka kwa uso wake hata haikubakia katika hayo masanamu yoyote).
Ni kisa mashuhuri cha Buhaira Padri nacho ni: (Kwamba Mtume (s.a.w) alitoka kabla ya kupewa Utume pamoja na ami yake Abi Talib na kundi la makuraishi kwenda pande za Shamu. Na walipofika jirani na Kanisa la padri walikaa huko) na alikuwa padri huyo hamtokei yoyote, akatoka akawa anawachanua hata akashika mkono wa Mtume wa Allah (s.a.w) akasema: (Huyu ni bwana wa walimwengu wote Allah anamtuma akiwa ni Rehema kwa walimwengu) wazee katika makuraishi wakamwambia: Umejuaje? Akasema: (Hakika haukubakia mti wala jiwe ila limeporomoka ikimsujudia na havisujudu ila kwa Nabii). (Kisha akasema na akaja Mtume (s.a.w) na hali juu yake kukiwa na kiwingu kikimpa kivuli alipokaribia watu aliwakuta wamemtangulia katika kivuli cha mti alipokaa kivuli kikamili (kikainama) kwake). Na kama hivi kuna mifano themanini kama mifano hii minane. ukiiunganisha mifano hii minane ingekuwa ina nguvu haiyumkiniki kuufikia utata wowote vyovyote iwavyo. Basi aina hii ya miujiza (Yaani kuongea kwa visivyo na roho) inaunda dalili ya kukata shauri juu ya kuthibitisha madai ya Utume, nayo iko katika hukumu ya tawatur kwa upande wa maana. Kila mfano unachukua nguvu nyingine kutoka katika nguvu ya wote inavuka nguvu yake ya pekee. Mfano wake katika hili, mfano wa mtu dhaifu amejiweka katika kundi la jeshi, anapata nguvu hata anakuwa anaweza kuwakabili watu elfu moja, au kama mlingoti dhaifu ukiwa utakusanywa pamoja na milingoti mingine yenye nguvu hupata nguvu. Basi vipi ikiwa riwaya zote ni sahihi na zinaungana imara?
Mifano mitatu muhimu inafungamana na ishara ya kumi na moja.
Aya tukufu inabainisha wazi: وَمَا رَمَيْتَ إِذْ رَمَيْتَ وَلَكِنَّ اللّهَ رَمَى kwa maelezo yake ya kukata na kwa uhakiki wa jumla ya wafasiri wanazuoni na maimamu wa Hadithi: Kwamba Mtume (s.a.w) alichukua gao la mchanga na vijiwe na akavitupa usoni mwa makafiri na akasema: (Zimeharibika nyuso). Gao lile la mchanga likaingia machoni mwa kila Mshirikina, mfano wa lilivyofika neno (Zimeharibika Nyuso) kwenda masikioni mwa kila mmoja kati yao, wakawa wanaagua macho yao kutokana na mchanga, wakakimbia wakati ambapo walikuwa katika hali ya kuwaelekea Waislamu. Na anapokea Imamu Muslim: Hakika ya makafiri katika vita vya Hunain walipokuwa wanawashambulia Waislamu, Mtume (s.a.w) alichukua gao la mchanga na akalirusha kwenye nyuso za washirikiana, na akasema: (Nyuso zimeharibika) basi hakuna hata mmoja kati yao ila macho yake yalijaa mchanga – kwa idhini ya Allah – kama sikio lake lilivyosikia neno hili wakakimbia hali ya kugeuka nyuma. Tukio hili lenye kufurutu ada limetokea katika Badri na Hunain. Ni tukio linalovuka uwezo wa wanadamu, kama lilivyo kuwa haiyumkiniki kuliegemeza kwenye sababu za kawaida, kwa ajili hii amesema Allah (s.w): وَمَا رَمَيْتَ إِذْ رَمَيْتَ وَلَكِنَّ اللّهَ رَمَى yaani ni tukio linalotokana na uweza wa kiungu mtupu.
Vitabu vya maimamu wa Hadithi vinaeleza na mwanzoni mwavyo Al-Bukhary na Muslim: Kuwa mwanamke wa kiyahudi - na jina lake ni Zainab Bint Al-Harth - alimpa zawadi Mtume (s.a.w) huko Khaybar Mbuzi aliyeokwa aliyemtia sumu, Mtume (s.a.w) akamla, na watu wakala, akasema: اِر۟فَعُوا اَي۟دِيَكُم۟ اِنَّهَا اَخ۟بَرَت۟نٖى اَنَّهَا مَس۟مُومَةٌ Inueni mikono yenu, hakika mwanamke huyo amenipa habari kuwa huyo mbuzi amewekwa sumu, wote wakanyanyua mikono yao, isipokuwa Bishr Ibn Al-Barra alikufa kutokana na athari ya sumu, Mtume (s.a.w) akamwita yule Myahudi mwanamke na akamwambia: (Nini kilichokupelekea ambacho umekitenda?) Akasema: Ikiwa ni Mtume hakitakudhuru nilichokitenda, na ukiwa ni Mfalme nimewapumzisha watu na wewe. Akaamuru kuuliwa, na katika baadhi ya mapokezi ni kwamba hakuamuru kuuliwa. Wamesema wanazuoni wahakiki: hakuamuru kuuliwa bali alimkabidhi kwa mawalii wa Bishr bin Al-Barra, wakamuua. Sasa sikiliza nukta hizi tatu ili kubainisha hali ya muujiza wa tukio hili. Nukta ya Kwanza: Imekuja katika moja ya mapokezi: Hakika ya idadi ya masahaba walisikia kauli yake alipoeleza mbuzi kuwa ametiwa sumu. Nukta ya Pili: Na katika mapokezi mengine ni kwamba baada ya Mtume kueleza kuhusu kadhia ile alisema: Semeni bismillah kisha kuleni, hakika baada yake haitadhuru sumu hiyo. Mapokezi haya ingawa Ibn Hajar Al-Asqalany hakuyakubali isipokuwa wanazuoni wengine wameyakubali. Nukta ya Tatu: Alitulia kila aliyesikia maneno yake (s.a.w): (Hakika amenieleza kuwa kwamba imewekwa sumu) kana kwamba ameyasikia yeye mwenyewe, kwani haijasikika kutoka kwake kauli yoyote inayohalifu uhalisia katu, na hii ni moja katika kauli hizo. Wakati ambapo Wayahudi wanapanga vitimbi ili wateremshe pigo lao la kumaliza kwa Mtume (s.a.w) na sahaba wake wema (r.a) tahamaki njama zinafichuka kupitia habari kutokana na ghaibu na inabatilisha njama na hila mbaya na habari inakuwa kama alivyoelezea (s.a.w).
Ni muujiza wa Mtume (s.a.w) katika matukio matatu unashabihiana na muujiza wa Nabii Musa (a.s), katika muujiza wa mkono wake mweupe na fimbo. Tukio la Kwanza: Ametoa Imamu Ahmad Hadithi sahihi, kutoka kwa Abu Said Al-Khudry (r.a): Kwamba Mtume (s.a.w) (Alimpa Qatadat bin An-Nuuman kigongo – na ameswali Al-Ishaa pamoja naye – katika usiku wenye giza wenye kunyesha. Na akasema: Nenda nayo itakuangazia mbele yako kumi na nyuma yako kumi. Ukiingia nyumbani mwako utaona weusi upige hadi utoke huyo ni shetani. Akaondoka, kile kigongo kikamwangazia (Kama mkono mweupe) hata akaingia nyumbani mwake na akakuta weusi akaupiga hata ukatoka). Tukio la Pili: Upanga wa Ukasha ibn Muhsin Al-Asady ulikatika akiwa anapigana kwa upanga huo katika vita vya Badr kuu - vita hivyo ambavyo ni chimbuko cha mageni - Mtume (s.a.w) akampa kipande cha kuni - yaani jiti zito - (Na akasema: Piga kwa mti huu ukarudi mkononi mwake ukiwa ni upanga mkali mrefu wa kimo mweupe wenye nguvu madhubuti, akapigana kwa kutumia upanga huo, kisha haukuacha kuwa pamoja naye akishuhudilia na upanga huo matukio mbali mbali mpaka alipouliwa shahidi katika mapigano ya watu wa Ridda) huko Yamamah. Tukio hili limethibiti bila shaka yoyote, na Ukasha alikuwa anajifaharisha kwa upanga huo uhai wake wote, na upanga ulikuwa unaitwa (Al-Aun), kuwa mashuhuri upanga kuwa ni (Al-Aun) na kujifaharisha Ukasha kwa upanga huo ni hoja mbili vile vile juu ya kuthibiti kwa tukio hili. Tukio la Tatu: Amesimulia Ibn abd Al-Barr na yeye ni katika wanazuoni wa zama zake kati ya wanazuoni wahakiki: Kwamba Abdallah bin Jahash mwana wa shangazi wa Mjume wa Allah (s.a.w) (Upanga wake ulishaondoka) katika vita vya Uhud naye akiwa anapigana, Mtume wa Allah (s.a.w) akampa (Karara la mtende likarejea kuwa ni upanga katika mkono wake). Anasema Ibn Sayyid An-Nas katika (Sira yake): Upanga huu ukabakia muda na haukuacha kua unahama hama hata ukauzwa kwa mtu anaye itwa Ghai Al-Turkiy kwa Dinari mia mbili. Basi panga hizi mbili ni miujiza miwili kama muujiza wa fimbo ya Musa, isipokuwa ni kwamba sura ya muujiza wa fimbo ya Musa haikubakia baada ya kufa kwake (a.s), na panga hizi mbili zilibaki kuwa ni miujiza miwili baada ya kufarikia kwake (s.a.w).
Na katika miujiza yake (s.a.w) ni : Kuponesha wagonjwa na majeruhi kwa mpulizo wake wenye baraka. Na aina hii ya miujiza ni mutawatir kimaanawy -kwa upande wa aina - ama vijisehemu vyake basi sehemu kati yake ni kwa hukumu ya mutawatir ya kimaanawy na sehemu kati yake ni Aahadi, isipokuwa zinaleta ukinaifu wa kielimu na utulivu na hii ni kwa uthibitisho wa wanazuoni kwa mapokezi hayo na kusahihisha kwa maimamu wa Hadithi. Tutaeleza katika mifano ya aina hii ya miujiza mifano michache tu kati ya mifano yake mingi.
Anasimulia Al-Qadhy Iyaadh kutoka kwa Saad ibn Waqqas naye ni katika kumi waliobashiriwa pepo na alitawalia huduma ya Mtume (s.a.w) na alikuwa mmoja wa viongozi wake, na aliongoza jeshi la Kiislamu katika kipindi cha Umar Ibn Al-Khattab (r.a) kwamba amesema: Hakika ya Mtume (s.a.w) alikuwa ananipa mshale hauna makali na anasema: Urushe, na hakika alirusha Mjumbe wa Allah (s.a.w) kutoka katika upinde wake mpaka ukakatik hii ilikuwa katika vita vya Uhudi, na ilikuwa mishale ambayo isiyokuwa na makali inapita kama yenye manyoya na kuthibiti katika mwili wa makafiri. Na amesema vilevile: Na siku hiyo lilisibiwa jicho la Qatadat (Ibn An-Nuuman) hata likatua kwenye shavu lake, Mtume (s.a.w) akalirudisha kwa mkono wake wenye baraka wenye kuponesha (Likawa bora zaidi kati ya macho yake mawili) na tukio hili lilikuwa mashuhuri hata kwamba mmoja wa wajukuu wa Qatadah alipokuja kwa Umar ibn Abdul Aziz alijitambulisha kwa kuimba beti zifuatazo: Mimi ni mwana wa yule ambaye jicho lake lilitoka na kuning’inia kwenye shavu lake. Likarejeshwa kwa kiganja cha Mustafa ubora wa kurudishwa. Likarudi kama lilivyokuwa mwanzo wa hali yake. Ee uzuri ulioje wa jicho na uzuri ulioje wa lililorudishwa! Na vilevile imethibiti: Kwamba aliweka mate yake kwenye kijeraha: (Mshale uliathiri katika uso wa Abi Qatada katika siku ya Dhii Qird amesema: Halikuuma wala kutunga usaha) ambapo alipangusa mjumbe wa Allah (s.a.w) kwa mkono wake wenye baraka.
Amesimulia Bukhary na Muslim na wengine: Kwamba Mtume (s.a.w) amempa bendera Ali siku ya Khaibar, alikuwa anaumwa macho, alipompulizia katika jicho lake ikawa ni ponya kwa jicho lake likapona kwa idhini ya Allah (s.w). Ilipokuja kesho Ali alichukua mlango wa ngome na ulikuwa wa chuma kana kwamba ni ngao mkononi mwake, na kufungua ngome. (Na alipuliza juu ya pigo kwenye muundi wa Ibn Al-Akuwai siku ya Khaibar ukapona).
Amesimulia An-Nasaaiyyu kutoka kwa Uthman bin Hunaif: Hakika ya kipofu alikuja kwa Mtume wa Allah (s.a.w) akasema: Ewe mjumbe wa Allah (s.a.w) muombe Allah anifunulie uoni wangu. Akasema: Au nikuache? Akasema: Ewe mjumbe wa Allah kuondoka kwa uoni wangu kumenipa mashaka. Akasema: Nenda katawadhe kisha swali rakaa mbili kisha sema: Ewe mola mimi ninakuomba na ninaelekea kwako kwa Nabii wangu Muhammad Nabii wa Rehema, ewe Muhammad mimi ninaelekea kwa mola wako mlezi kwako wewe, anifunulie uoni wangu, ewe Allah mshufaishe kwangu, na unishufaishe katika nafsi yangu. (Akarejea na Allah amemfunulia uoni wake).
(Abu Jahal siku ya Badr alikata mkono wa Muawwadh bin Afraa) kati ya kumi na nne waliokufa shahidi katika Badr (Akaja anabeba mkono wake, Mtume (s.a.w) akautemea na akauunga ukaunganika, ameipokea Ibn Wahab) na yeye ni katika maimamu wa Hadithi - kisha akarejea katika mapigano akapigana hata akafa shahidi. (Na katika masimulizi yake vilevile: Hakika Khubayb bin Yusaf alisibiwa siku ya Badr pamoja na Mjumbe wa Allah (s.a.w), kwa pigo juu ya bega lake hadi ubavu wake ukainama, Mtume (s.a.w) akaurudisha, na akaupulizia hadi ukapona). Basi haya matukio mawili na hata ikiwa hayo ni ya kiaahaadi isipokuwa usahihishaji wa Imamu Mtukufu Ibn Wahab mapokezi hayo, na kuwa yametoka katika chimbuko la miujiza, Badr, na kwa ajili ya kuwepo kwa shahidi nyingi kama hiyo hatilii shaka yeyote katika kutokea kwake. Na kama hivi kuna mifano elfu moja na mmoja imethibiti kwa Hadithi sahihi, kwamba mkono wa Mtume Mtukufu (s.a.w) umekuwa ni ponya na dawa kwa wenye majeraha na wagonjwa. KIFUNGU HIKI KAMA KINGEANDIKWA KWA MAJI YA DHAHABU NA KUREMBWA KWA ALMASI KINGESTAHIKI HIVYO. Ni kweli! Na kama ilivyotangulia kupita huko nyuma: Hakika ya tasbihi ya mawe na unyenyekevu wake katika kiganja cha Mtume (s.a.w) na kugeuka kwa mchanga na vijiwe katika kiganja hicho kama risasi katika nyuso za maadui hata wakageuka wakirudi nyuma kwa kauli yake (s.w): وَمَا رَمَيْتَ إِذْ رَمَيْتَ وَلَكِنَّ اللّهَ رَمَى na kupasuka mwezi vipande viwili kwa kidole cha kiganja hichohicho kama ilivyoeleza Qur’an tukufu: وَانشَقَّ الْقَمَرُ na kububujika maji kwa kasi kama chemchem yenye kutembea kutoka katikati ya vidole kumi na kunywa jeshi kutokana na maji hayo na kuwa mkono huo ni tiba ya majeruhi na ponya ya wagonjwa, yanabainisha wazi wazi kiasi cha baraka ya mkono huo mtukufu. Na kiasi cha kuwa kwake ni muujiza wa uweza wa kiungu mkuu. Kwa hakika kana kwamba kiganja cha mkono huo. Ni kituo cha dhikri cha kisubhana kidogo baina ya wapendwa, lau vijiwe vitaingia katika kituo hicho vingefanya tasbihi, na kudhikiri. Na silaha ndogo ya kiungu Bwana Mlezi mbele ya maadui, lau mchanga utaingia hapo ungeruka urukaji wa mabomu. Na inarejea famasia ndogo ya kiungu Mwingi wa Rehema kwa ajili ya wagonjwa na majeruhi. Lau ingegusana na ugonjwa ingekuwa ni ponya kwake. Na wakati mkono huo unaponyanyuka hunyanyuka kwa utukufu na kupasua mwezi vipande viwili kwa kidole chake. Na kama vitageuka ugeukaji wa uzuri na kupasua chemchem ya rehema inayobubujika kutoka chemchem kumi inayotembea kama Kauthar Salsabili. Kwa kuwa mkono wa Mtume mtukufu (s.a.w) ni mahali pa miujiza ya dhahiri kwa kiwango hiki. Je haitambuliki kwa uwazi kuwa: Nafasi yake kubwa kwa mola wake? Upeo wa ukweli wake katika madai yake na kiasi cha furaha ya wale waliofunga ahadi na mkono ule wenye baraka? Swali: Hakika wewe unasema katika mengi ya mapokezi kwamba ni mutawatir, wakati ambapo hatujayasikia isipokuwa sasa, je tawatur haijulikani kwa kiasi hiki?. Jibu: Kuna mambo mengi Mutawatir mbele ya wanazuoni wa sharia wakati ambapo hayajulikani kwa wengine. Mbele ya wanazuoni wa Hadithi katika Hadithi Mutawatir zipo zisizojulikana isipokuwa ni aahadi kwa wengineo. Na kama hivyo, yaliyo wazi na ya kinadharia ya kila elimu hakika hubainishwa kulingana na walivyokubaliana watu waliobobea elimu hiyo, ama watu wengine wao wanawategemea wao katika elimu hiyo. Basi ima wakubaliane na kauli yao, au watajizatiti katika kuidurusu elimu hiyo wayakute waliyoyakuta. Tuliyoyaeleza katika Mutawatir ya hakika na maanawy, au matukio yaliyo katika hukumu ya mutawatir, hukumu yake wameibainisha watu wa Hadithi, wanazuoni wa sharia na wanazuoni wa Usuli, na walio wengi wa wanazuoni wengine. Ikiwa watu wa kawaida walioghafilika hawazijui, au yule anaye fumba jicho lake na kujiweka mbali na elimu katika wajinga, lawama haiangukilii ila juu yao.
Imamu Al-Baghawy ametoa: (Mguu wa Ali Bin Al-Hakam ulisibiwa siku ya Handaki ukavunjika) akaupangusa Mtume wa Allah (s.a.w) (Akapona mahali pake, na hakuteremka kunako farasi wake).
Amesimulia Al-Bayhaqy na wengine: Aliugua Ali Bin Abi Talib, akawa anaomba. Mtume (s.a.w) akasema: (Ewe Mola mponeshe au mnusuru kisha akampiga kwa mguu wake, hakuugua maumivu hayo baada ya hapo).
(Katika kiganja cha Sharahabili Al-Jaafy kulikuwa na tezi iliyokuwa inamzuia kushika upanga na kamba ya mnyama akashitakia kwa Mtume (s.a.w) hali hiyo, hajaacha kuwa anaisaga kwa kiganja chake hata alipokinyanyua haikubakia athari yake yoyote).
Watoto sita wamepata – kila mmoja peke yake – muujiza katika miujiza ya Mtume mtukufu (s.a.w). Wa Kwanza: Amepokea Ibn Abi Shayba- naye ni katika maimamu wa Hadithi – kwamba: (Mwanamke wa kutoka kabila la Khathaama alimjia Mtume (s.a.w) akiwa na mtoto ana balaa haongei, yakaletwa maji, akasukutua kinywa chake na akaosha mikono yake, kisha akampa maji hayo huyo mwanamke na akamwamuru kumnywesha na kumpangusa nayo, akapona kijana yule na akapata fahamu inayozidi akili za watu). Wa Pili: (Na imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas: Alikuja mwanamke na mwanawe mwenye wazimu, Mtume (s.a.w) alipangusa kifua chake akakohoa kikohozi likatoka tumboni mwake mfano wa kaa jeusi) kitu cheusi kama tango dogo – akapona. Wa Tatu: Amesimulia Imamu Al-Bayhaqy na An-Nasaiy: (Kilipinduka chungu juu ya mkono wa Muhammad Bin Haatib, hali ya kuwa ni mdogo Mtume (s.a.w) alipangusa juu yake na kumwombea dua) na akapuliza mpulizo ndani yake kuna mate yake matukufu akapona wakati uleule. Wa Nne: (Hakika Mtume (s.a.w) ameletewa kijana amekonga) yaani amekuwa mkubwa (Hajaongea katu, akasema: Nani mimi? akasema: Mtume wa Allah) Allah (s.w) akamtamkisha. Wa Tano: Ametoa Imamu wa zama hizi Jalalu Ad-Ddin As-Suyuty - ambaye alipata utukufu wa kumwona Mtume (s.a.w) katika hali ya kuwa macho mara nyingi - kwamba: Mtu mmoja katika watu wa Yamamah alimjia Mtume (s.a.w) na kijana siku aliyozaliwa, Mtume (s.a.w) akamwambia: Ewe mtoto? Nani mimi ? Akasema: Wewe ni Mjumbe wa Allah. Akasema: Umesema kweli Allah akubariki. Kisha kijana yule hakuongea mpaka alipokuwa mkubwa akawa anaitwa (Mbarikiwa wa Yamamah) kwa dua ya nabii kwake abarikiwe. Wa Sita: (Alimwomba dhidi ya mtoto) mgumu wa tabia (Alimkatishia swala Allah amkate athari yake akakalishwa chini) na akapata malipo ya ukorofi wake. Wa Saba: (Msichana alimwomba chakula naye akiwa anakula, akampa kutoka mikononi mwake na alikuwa mchache wa haya, akasema: Hakika ninataka ambacho kinatokana na kinywa chako, akampa kilichomo kinywani mwake, alikuwa haombwi kitu akakizuia. Kilipotulia tumboni mwake akapewa kiasi cha haya ambapo hakuwapo mwanamke Madina mwenye haya zaidi kuliko yeye). Na kama hivi kuna mifano mingi inavuka mifano mia nane, kama ambayo tumeieleza, na mingi yake imebainishwa na vitabu vya Hadithi na sira. Naam, ulivyokuwa mkono wa baraka wa Mtume mtukufu (s.a.w) kama famasia ya Luqman Al-Hakiim, na mate yake kama maji ya chemchem ya uhai ya khidhr (a.s), na mpulizo wake kama mpulizo wa Isa (a.s) katika ponya, na kwamba wanadamu wanakutana na masaibu na mabalaa, hapana shaka kwamba amepewa kiasi kisicho na mpaka cha watoto na wagonjwa na wenda wazimu na hapana shaka kwamba wote walipona kutokana na maradhi na shida zao. Hata Tausi Al-Yamany naye ni katika maimamu mashuhuri wa taabiina kwa zuhudi yake (kuipa nyongo dunia) na ucha mungu wake ambapo alihiji mara arobaini na aliswali swala ya asubuhi kwa udhu wa Ishaa miaka arubaini, aliwakuta wengi katika sahaba wema, mwanazuoni huyu mtukufu anapasha habari kwa kukata shauri na kusema: (Hakuna mwenda wazimu aliyekuja kwa Mtume (s.a.w) na akaweka mkono wake Mtukufu juu ya kifua chake isipokuwa alipona wazimu wake). Akipasha habari Imamu kama At-Taawus Al-Yamany - ambaye amewakuta sahaba wema - habari hii ya kukata shauri hapana shaka kuwa wamekuja kwa Mtume (s.a.w) wengi mno katika wagonjwa, huenda wanafikia maelfu na wote walipona maradhi yao.
Na katika aina za miujiza yake (s.a.w) kuna aina kubwa, nayo ni mambo ya kufurutu ada yaliyodhihiri kwa dua yake. Aina hii hapana shaka ni mutawatir kwa namna ya kihakika, na mifano yake na vijisehemu vyake ni vingi mno havimaliziki kwa idadi, na mingi ya mifano yake imefikia daraja ya mutawatir, bali imekuwa mashuhuri na kuwa karibu ya mutawatir, na kati yake ni ile waliyonakili maimamu watukufu ambapo ukinaifu katika hiyo inafidisha kama mutawatir iliyo mashuhuri. Na sisi hapa tunaeleza kwa njia ya mifano baadhi ya mifano yake mingi mno ambayo ni karibu na mutawatir, au ambayo ni kwa daraja ya mashuhuri, kama tutakavyoeleza vijisehemu vya kila mfano:
Wamepokea maimamu wa Hadithi na mwanzoni mwao ni Al Bukhary na Muslim hakika ya dua ya Mtume (s.a.w) katika kuomba mvua ilikuwa inajibiwa papo hapo, na imetokea hivyo mara nyingi sana, hata Mtume (s.a.w) alikuwa akinyanyua mikono yake wakati mwingine akiwa juu ya mimbari, basi anajibiwa kabla ya kuteremka, na mapokeo haya yamethibiti yamefikia daraja ya tawatur. Na tumetaja huko nyuma: Kwamba watu walipatwa na kiu kwenye safari, na mawingu yalikuwa yanakusanyika katika kila mara wanapohitajia maji wananyweshwa kisha inakoma kunyesha. Bali dua yake ilikuwa (s.a.w) ikijibiwa hata kabla ya Utume, akawa Abdul Mutalib babu wa Mtume (s.a.w) akiomba mvua kwa sura ya Mkarimu (s.a.w) katika ujana wake, ikawa mvua inashuka. Na tukio hili limekuwa maarufu hata alilitaja Abdul Mutalib Katika baadhi ya mashairi yake. Na hakika Umar Ibn Al-Khattab aliomba mvua kwa (kupitia) Al-Abbas ami wa Mtume (s.a.w) baada ya kufariki kwa Mtume (s.a.w) akasema: (Ewe Mola tulikuwa tunatawasali kwako kwa kupitia Nabii wetu unatupa mvua na hakika tunatawasali kwako kwa kupitia ami wa Nabii wetu tunakuomba utupe mvua, akasema na wakapewa mvua). Na wamepokea Mashekhe wawili kwamba Mtume (s.a.w) aliombwa amwombe Allah awape mvua (Akaomba Mtume (s.a.w) dua ya kuomba mvua wakanyeshewa kisha wakamshitakia mvua akaomba wakaachwa na anga likiwa safi).
Imepokewa riwaya mashuhuri iko karibu na tawatur kwamba (s.a.w) wakati waumini walipokuwa wachache na wanaficha imani na ibada yao (Aliomba Uislamu upewe nguvu kwa Umar (r.a) au kwa Abu Jahl akajibiwa kwa Umar) aliposema: (Ewe Mola upe nguvu Uislamu kwa Abi Jahl bin Hisham au kwa Umar bin Al-Khattab, akaamka Umar akajihimu kwa Mtume (s.a.w) akasilimu) akawa sababu ya nguvu ya Uislamu na kwa ajili hii aliitwa kuwa ni Al-Faaruq (Mtenganishaji wa haki na batili).
Mtume (s.a.w) aliwaombea baadhi ya sahaba kwa makusudi mbalimbali akajibiwa kujibiwa kuliko furutu ada, hata ikafikia karama za dua hizo daraja ya miujiza. Kati ya hiyo zile alizopokea Bukhary na Muslim na wengine kwamba Alimwombea Ibn Abbas: Ewe Mola muelimishe dini na umfundishe Taawili (tafsiri ya ndani) baada ya hapo akaitwa Al-Hibr na mkalimani wa Qur’an hata Umar (r.a) alikuwa anamuidhinisha Ibn Abbas – pamoja na uchipukizi wa Umri wake – akae katika baraza la wakubwa wa kisahaba wema. Na amepokea Bukhary na wengine Kutoka kwa Anas (r.a) amesema: Amesema mama yangu: Ewe mjumbe wa Allah (s.a.w) mtumishi wako Anas mwombee Mungu. Akasema: Ewe Mola kithirisha mali yake na watoto wake na umbarikie katika uliyompa, na katika mapokezi ya Ikrima amesema Anas: Basi naapa kwa Allah hakika mali yangu ni nyingi na hakika watoto wangu na watoto wa watoto wangu hivi sasa wanahesabiwa kiasi cha mia. Na katika mapokezi, simjui yeyote amepata neema niliyoipata, na hakika nimezika kwa mikono yangu hii miwili mia moja katika wanangu sisemi njiti wala mtoto wa mtoto (Mjukuu) na yote hayo yalikuwa kwa baraka ya dua ya Mtume (s.a.w). Na amepokea Imamu Al-Bayhaqy na wengine katika maimamu wa Hadithi hakika (s.a.w) (Alimwombea baraka Abdulrahaman bin Auf) na yeye ni mmojawapo katika kumi waliobashiriwa pepo akapata mali nyingi sana kwa baraka ya dua ile hata (Mara moja alitoa sadaka msafara ndani yake wakiwemo ngamia mia saba waliokuja kwake wakiwa wamebeba kutokana na kila kitu akawatoa sadaka ngamia hao na vilivyo juu yake na ndani yake) mashallah katika baraka hii na tabarakallah. Na amepokea Al-Bukhary na wengine kwamba Mtume (s.a.w) alimwombea baraka Urwata bin Abiljaad katika biashara yake. Akasema: (Nilikuwa nikikaa Al-Kanaasat sirejei mpaka nimepata faida Arubaini elfu. Na amesema Al-Bukhary katika Hadithi yake, akawa angenunua mchanga angepata faida katika mchanga huo). (Na alimwombea Abdallah bin Jafar baraka katika mapatano ya mkono wake wa kuume basi hakununua kitu ila alipata faida katika kitu hicho hata alikuwa mashuhuri katika zama zake kwa utajiri na mali kwa mfano wa alivyo kuwa mashuhuri kwa Ukarimu). Na aina hii ina mifano mingi mno tumeileta hii minne kwa njia ya mfano. Na amepokea Imamu At-Tirmidhy: Kwamba (s.a.w) alimwombea Saad bin Abi Waqqas: Ewe Mola mjibu saad atakapo kuomba. Akawa mwenye kujibiwa dua watu wanamwogopa kuwaombea dua dhidi yao. Na alimwambia Abi Qatada: Umefaulu uso wako, ewe Mola mbarikie katika nywele zake na ngozi yake. Akafa na hali akiwa na umri wa miaka sabini kana kwamba mtoto wa miaka kumi na tano. Hakika mapokezi haya yenye kuthibiti yamekuwa mashuhuri. Na alipoimba mshairi mashuhuri An-Naabighat mbele yake (s.a.w): بَلَغ۟نَا السَّمَاءَ مَج۟دُنَا وَسَنَائُنَا وَ اِنَّا نُرٖيدُ فَو۟قَ ذٰلِكَ مَظ۟هَرًا Tumefikia mbingu katika utukufu wetu na umaarufu wetu Kwa hakika tunataka kuonekana juu zaidi ya hapo. Mtume (s.a.w) alisema: Unakwenda wapi ewe abu Layla? Akasema: Kuelekea peponi ewe mjumbe wa Allah. لَا يَف۟ضُضِ اللّٰهُ فَاكَ Kisha akaimba kasida nyingine inabeba maana matukufu Mtume (s.a.w) akasema: (Allah asibomoe kinywa chako) halikumdondoka jino, na alikuwa mzuri wa watu kwa kinywa, likimng’oka jino linamuota jino lingine. Na aliishi miaka mia na ishirini. Na inasemwa kuwa zaidi ya hivi. Na katika mapokezi sahihi kwamba (s.a.w) alimwombea Ali (r.a) akasema: اَللّٰهُمَّ اك۟فِهِ ال۟حَرَّ وَال۟قَرَّ Ewe Mola mkinge na joto na baridi, ikawa kwa baraka ya dua hii: (Anavaa wakati wa majira ya baridi mavazi ya joto, na wakati wa majira ya joto mavazi ya baridi na wala halimsibu joto wala baridi). (Na akamwombea binti yake Fatima Allah asimpe njaa. Amesema: Sikupata njaa baada ya hapo). Na akamwomba At-Tufayl bin Amr ishara kwa watu wake, akasema: (Ewe Mola Mlezi mnawirishie. Ikamchomozea nuru kati ya macho yake mawili, akasema: Ewe Mola ninahofia kuwa watasema: Kioja, ikageuka katika ncha ya mjeledi wake, akawa anaangaza kwenye usiku wenye giza, akaitwa mwenye nuru). Basi matukio haya hayana shaka katika mapokezi yake katu. (Kutoka kwa Abi Huraira amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Allah mimi ninasikia kutoka kwako Hadithi nyingi ninazisahau. Akasema: Kunjua kishari chako nikakikunjua. Akasema: akachota kwa mkono wake (Kama mwenye kuchukua kitu kutoka ghaibu), kisha akasema: Kikusanye, nikakikusanya. sikusahau kitu baada ya hapo). Basi matukio haya ni kutokana na Hadithi mashuhuri.
Tunabainisha mifano kadhaa kuhusiana na kujibiwa kwa dua alizoziomba Mtume (s.a.w) kwa baadhi ya watu. Kwanza: Imekuja habari kwa Mtume (s.a.w) ya kuchana kwa mfalme wa Uajemi aitwaye (Barweiz) barua ya Mtume (s.a.w) akasema: Akasema: Ewe Mola Mchane. Akachanika kuchanika kwa jumla. Pale ambapo mwana wa mfalme Shiraweihi alipomuua baba yake kwa Sime, Na Saad bin Abi Waqqas akauchana ufalme wake (Haukubakia masalio yake wala haukubakia kwa Uajemi uongozi wowote kwa nchi za dunia) wakati ambapo ufalme wa Kaisari ulibaki na falme nyingine kwa ajili ya kuheshimu kwao barua za Mtume (s.a.w) kwao. Pili: Imethibiti kwa Hadithi mashuhuri iliyo karibu na Mutawatir – na kwa vile ambavyo inaashiria aya tukufu – kwamba walikusanyika viongozi wa kikuraishi ndani ya msikiti mtukufu na wakamtendea Mtume muamala mbaya akawaombea dua dhidi yao, akawataja. Akasema Ibn Masuud. (Hakika niliwaona wameuliwa siku ya Badr). Tatu: Na akawaombea Mudhar nalo ni kabila kubwa, kwa vile lilivyomkadhibisha, (Wakapata janga la ukame hata Makuraishi wakawaonea huruma akawaombea wakapewa mvua) mapokezi haya ni karibu na Tawatur.
Ni kujibiwa dua la Mtume (s.a.w) alilowaombea watu maalum, tunataja kwa njia ya mfano mifano mitatu kati ya mifano yake mingi. Kwanza: Dua dhidi ya Utba bin Abi Lahab, na akasema: اَللّٰهُمَّ سَلِّط۟ عَلَي۟هِ كَل۟بًا مِن۟ كِلَابِكَ (Ewe Mola msalitishie mbwa katika mbwa wako). Utba baada ya hapo akasafiri akaja simba anamtafuta, akamchukua kutoka katikati ya msafara akamla. Tukio hili ni mashuhuri wamelinakili maimamu wa Hadithi na wamelisahihisha. Pili: Mtume (s.a.w) alipeleka doria na katika uongozi wake alikuwa Amir bin Al-Adhbut, na alikuwa Muhallim bin Juthama pamoja naye, Muhallim akamuua kwa kumvizia, habari ilipokuja kwa Mtume (s.a.w) alighadhibika na akasema: Ewe Mola usimsamehe Muhallim, akafa baada ya siku saba. Ardhi ikamtema kisha akafukiwa ikamtema mara nyingi, wakamtupa kati ya kingo mbili za bonde na wakamkusanyia mawe. Tatu: (Alisema kumwambia mtu aliyemkuta anakula kwa mkono wake wa kushoto: Kula kwa mkono wako wa kuume, akasema siwezi akasema: Hutaweza, hakuunyanyua kwenda kinywani mwake).
Tutataja mambo kadhaa yaliyofurutu ada yenye kuthibiti uthibiti wa kukinaisha katika yale yaliyodhihiri kwa dua ya Mtume (s.a.w) na kwa kugusa kwake. Kwanza: Hakika Mtume (s.a.w) alitoa nywele katika nywele zake kumpa Khalid Ibn Al-Waliid (Upanga wa Allah) na akamwombea ushindi, Khalid akaziweka kwenye kofia yake (Hakushuhudia nayo vita ila aliruzukiwa ushindi). Pili: Hakika Salman Al-Farisy alikuwa mtumwa wa Mayahudi, akaandikiana naye Wasimamizi wake juu ya mabonde mia tatu atakayoyapandikiza kwao zote zinabeba na kutoa matunda na juu ya wakia arobaini za dhahabu, Mtume (s.a.w) akafanya kazi ile na akazipandikiza kwa ajili yake kwa mkono wake isipokuwa mmoja alipandikiza mwingine asiye kuwa yeye, yote ikashika isipokuwa ule mmoja Mtume (s.a.w) akaung’oa kisha akaurudisha ukashika. Katika kitabu cha Al-Bazzar, Mitende ile ikalisha kuanzia mwaka ule isipokuwa mmoja Mtume (s.a.w) akaung’oa na akaupandikiza ukalisha kutokea mwaka wake ule. Na akampa mfano wa yai la kuku katika dhahabu baada ya kuwa ameizungusha juu ya ulimi wake, akapima dhahabu hiyo kwa ajili ya wasimamizi wake wakia arobaini na ikabaki kwake mfano wa kiasi kile alichowapa. Tukio hili ni katika mambo yaliyofurutu ada muhimu ambayo yamepita katika Uhai wa Salman Al-Farisy (r.a), wamelipokea maimamu wenye kutegemewa. Tatu: (Ummu Malik sahaba alikuwa na Ukka chombo cha ngozi cha kuwekea Samli akitoa zawadi ya samli kwa Mtume (s.a.w) katika chombo hicho Mtume (s.a.w) akamwamrisha asiikamue kisha akampa, tahamaki imejaa samli wanawe wanamjia wanamuomba chakula na hawana kitu, anaenda kwenye chomo hicho, na kukuta samli ndani yake, ikawa inadumisha mafuta yake mpaka alipokikamua) hawakukuta kitu tena baada ya hapo ndani ya chombo hicho.
Maji machungu yanageuka kuwa maji baridi matamu na kunukia riha nzuri kwa baraka ya dua ya Mtume (s.a.w) na kuyagusa kwake maji hayo. Tunaleta mifano michache tu: Kwanza: Amepokea Al-Baihaqy na maimamu wa Hadithi kwamba kisima cha (Qubaa) kilikuwa baadhi ya nyakati kinavuja (Na akamwagia kutokana na masalia ya udhu wake katika kisima cha Quba hakikuvuja baada ya hapo). Pili: Amepokea Abu Naim katika Dalailu An-Nubuwwat, na watu wa Hadithi kwamba katika nyumba ya Anas kulikuwa na kisima Mtume (s.a.w) akakitemea na akaomba (Haikuwa katika Madina maji matamu kuliko hayo). Tatu: Amepokea Ibn Majjah kwamba Mtume (s.a.w) (Aliletewa ndoo ya maji ya zamzam akayatemea ndani yake yakawa mazuri kuliko miski). Nne: Amepokea Imamu Ahmad bin Hanbali kwamba Mtume (s.a.w) aliletewa ndoo kutoka kisimani akatemea ndani yake kisha yakamiminwa maji ndani yake yakawa mazuri kuliko miski. Tano: Amepokea Hammad bin Salamat naye ni katika watu wenye kutegemewa ambao Imamu Muslim anapokea kutoka kwao, kwamba (s.a.w) alijaza (Chombo cha maji baada ya kuwa amekifunga na kuomba ndani yake) na akakitoa kwa sahaba wema na akawaamuru wasikifungue ila kwa udhu. (Ilipowahudhuria swala walishuka na wakakifungua tahamaki ndani yake kuna maziwa mazuri na mtindi kwenye mdomo wake). Mifano hii mitano ya kisehemu baadhi yake ni mashuhuri, na wanainakili Maimamu wanazuoni wakubwa. Basi hii na ambayo hatukuitaja hapa kwa ujumla wake inahakikisha kwa tawatur ya kimaanawy muujiza huu uhakikishaji mkamilifu.
Mbuzi ambao chuchu zao zilitoa maziwa mengi kwa baraka ya dua ya Mtume (s.a.w) baada ya kuwa yamekauka. Kuna mifano mingi sana ya hili isipokuwa sisi tutaeleza mitatu kati ya hiyo iliyo mashuhuri na kuthibiti. Kwanza: Vimepokea vitabu vya sira vya kutegemewa kwamba Mtume Mtukufu (s.a.w) alipohama pamoja naye akiwemo Abubakar As-Siddiq alipita katika kambi ya Atika binti Khalid Al-Khuzaiy aliyeitwa kuwa ni Umm Maabad, akashuka hapo na alikuwa na mbuzi mkondefu hana maziwa. Akamwambia: Mbuzi huyu hana maziwa? Umm Maabad akasema: Hakuna damu ndani yake maziwa yatoke wapi? Mtume (s.a.w) akagusa mgongo wake na akapangusa chuchu zake, kisha akasema: Leteni chombo na mumkame, wakamkama akanywa Mtume (s.a.w) yeye na Abubakar As-Siddiq na kukasalia masalia kwenye chombo wakanywa waliokuwa katika khabai wote hadi wakashiba. Na kama hivi yule mbuzi alibaki kuwa mwenye baraka na mwenye nguvu. Pili: Kisa cha mbuzi wa Ibn Masuud (r.a) nacho: (Kutoka kwa Ibn Masuud amesema: Nilikuwa ninachunga mbuzi wa Uqbat bin Abi Muit, wakanipitia Mjumbe wa Allah (s.a.w) na Abu Bakar, akasema: Ewe kijana kuna maziwa? Alisema: Nikasema: Ndio lakini mimi ni mwaminiwa. Akasema: Je kuna mbuzi yeyote hajapandwa na fahali?. Nikamletea mbuzi akampangusa chuchu yake, yakateremka maziwa akayakama kwenye chombo, akanywa na akamnywesha Abubakar..) na ilikuwa hii ndiyo sababu ya kusilimu kwa Ibn Masuud. Tatu: Kisa cha mbuzi wa Halima As-Saadiyya mama aliyemnyonyesha Mtume (s.a.w), na hicho ni kisa mashuhuri kwa kuwa kulikuwa na ukame mwaka huo uliosibu Ardhi ya watu wake, Mbuzi wakawa wakondefu, wakavu wa machuchu, hawakula machungani hadi wakashiba. Wakati alipopelekwa Mtume (s.a.w) kwa Halima As-Sadiyya mbuzi wake wakawa wanakuja kwenye machunga hali ya kuwa wamekula sana na maziwa yao yamejaa, na mbuzi wa watu wake kinyume na hivyo. Na hiyo sio isipokuwa kwa baraka yake (s.a.w). Na kuna mifano mingi mingine katika vitabu vya sira, na tulioueleza unatosha kwa mada tuliyokuwemo ndani yake.
Tunataja mifano michache katika mifano mingi iliyo mashuhuri ya matukio yaliyofurutu ada ambayo yamedhihiri wakati Mtume (s.a.w) alipopangusa vichwa vya baadhi yao na nyuso zao kwa mkono wake na kuwaombea. Kwanza: (Alipangusa juu ya kichwa cha Umair bin Saad na kukibariki, akafa na hali akiwa na umri wa miaka themanini wala hakukonga). Pili: Mtume (s.a.w) alipangusa kichwa cha Qaisi bin Zaid Al-Judhamy na akamwombea, akafariki naye akiwa na miaka mia moja, na kichwa chake cheupe na mahali alipoweka kiganja Mtume (s.a.w) na sehemu ambazo kimepita katika nywele zake ni nyeusi, akawa anaitwa Mwenye kung’aa. Tatu: (Na amepangusa kichwa cha Abdulrahaman bin Zaid bin Al-Khattab akiwa mdogo, na alikuwa mbaya na akamwombea baraka akawa juu ya wanaume kwa urefu na ukamilifu). Nne: (Alipangusa damu kwenye uso wa Aidh bin Amri na alikuwa amejeruhiwa siku ya Hunaini na akamwombea akawa na baka kama baka la farasi). Tano: (Alipangusa uso wa Qatadat bin Milhan ukawa uso wake una mmemetuko hata ikawa kunatazamwa katika uso wake kama inavyo tazamwa kwenye kioo). Sita: (Alinyunyiza kwenye uso wa Zainabu (akiwa mdogo) bint wa Ummu salama Mnyunyizo wa maji) aliyokuwa anatawadha kwayo (haikuwa inajulikana katika uso wa mwanamke uzuri kama ule alionao). Na kuna mifano mingi kama hivi vijisehemu ambavyo tumevieleza wameipokea maimamu wa Hadithi kwa ujumla wake inafidisha tawatur ya kimaanawy na inabainisha kutokea kwa muujiza wa Muhammad wa hali zote. Na hata tungekadiria kila moja katika mifano hii ni habari ya kiaahadi, na dhaifu, hakika jumla yake inakuwa kwa hukumu ya mutawatir ya kimaanawy, kwa sababu lau lingenakiliwa tukio fulani katika sura mbalimbali na mapokezi tofauti, basi hii inamaanisha kuwa kwamba tukio limetokea na hapana shaka ndani yake isipokuwa mapokezi yake na sura zake ni tofauti au dhaifu. Mathalan: Ikisikika kwenye baraza kishindo, baadhi yao wakasema: Nyumba ya fulani imevunjika, na wengine wakasema: Imevunjika nyumba ya mtu mwingine. Na mwingine akasema: Nyumba ya fulani na kama hivi kila mapokezi katika mapokezi hayo pamoja ya kuwa ni ya Kiaahadi na dhaifu au yenye kuhalifu uhalisia isipokuwa tukio la asili halina shaka kutokea kwake, nalo ni kuvunjika kwa nyumba. Basi mapokezi kwa ujumla wake yanafidisha kwa ukinaifu kutokea kwa tukio nayo yanaafikiana katika asili. Wakati ambapo mifano ya vijisehemu ambavyo tumevitaja ni mapokezi sahihi yote, hata kwamba baadhi yake yamefikia daraja ya umashuhuri. Lau tungekadiria kila mmoja kati ya hiyo ni dhaifu, ingekuwa kujulisha kwa jumla yake pia ni ujulishaji wa kukinaisha juu ya kuwepo kwa muujiza wa Muhammad kama yalivyojulisha mapokeo katika mfano wa juu ya kuvunjika kwa nyumba kati ya nyumba. Na kama hivi kila aina katika aina za miujiza ya dhahiri ni thabiti haina shaka ndani yake. Na vijisehemu vyake sio ila ni vielelezo vya sura mbali mbali za muujiza huo wa hali zote. Kama ulivyo mkono wake (s.a.w), vidole vyake, mate yake, pumzi zake na kauli zake – yaani dua yake – ni chanzo cha mingi katika miujiza, hakika ya vipole vyake vyote vingine na milango yake ya fahamu na viungo vyake ni eneo la kuzunguka mengi ya mambo ya kufurutu ada vilevile. Na vitabu vya sira na Historia vimebainisha matukio hayo ya kufurutu ada na vimefafanua nyingi katika dalili za utume ambazo ziko kwenye sira yake na sura yake na viungo vyake na hisia zake.
Hakika ya wanyama, wafu, Majini na Malaika wanamtambua huyo Nabii Mtukufu (s.a.w), kila kundi kati yao linadhihirisha baadhi ya miujiza yake ili kusadikisha unabii wake na kuutangaza kama vile yalivyoudhihirisha mawe, miti, mwezi na jua, na kubainisha kwamba vinamjua Mtume (s.a.w) na vinasadiki unabii wake. Ishara hii ya kumi na tano inajumuisha tanzu tatu:
Ni utambuzi wa jinsi ya wanyama kwa Mtume (s.a.w) na kudhihirisha kwake miujiza yake. Tanzu hii ina mifano mingi. Hapa tunataja baadhi iliyokuwa mashuhuri na yenye kukinaisha kwa tawatur ya kimaanawy katika matukio. Au ambayo inakubalika kwa maimamu wa elimu, au Umma umeipokea kwa kuikubali. Tukio la Kwanza: Tukio la pango mashuhuri mno kwa kiwango cha tawatur ya kimaanawy, nalo ni kuwa Mtume Mtukufu (s.a.w), alipojihifadhi kwenye pango pamoja na Abu Bakar As-Siddiq ili kuokoka na utafutaji wa Makuraishi wanaomtafuta, (Allah (s.w) ameamrisha njiwa wawili wakasimama kwenye mdomo wa pango. Na katika Hadithi nyingine, kwamba buibui alifuma kwenye mlango wa pango) hata Ubayya bin Khalaf – naye ni katika wapingaji wakubwa wa kikuraishi, Mtume Mtukufu (s.a.w) alimuua huyu siku ya Badr - walipomtaka makafiri wa kikuraishi aingie pangoni, alisema: (Nini haja yenu humo, na juu yake kuna mtando wa buibui sioni ila umefumwa kabla ya kuzawa kwa Muhammad) na walisimama njiwa wawili juu ya mdomo wa pango, Makuraishi wakasema: (Lau ingekuwa ndani yake yuko yeyote njiwa wawili wasingekuwa mlangoni pake na Mtume (s.a.w) anasikia maneno yao, wakaondoka). Na amepokea Ibn Wahab, kwamba njiwa wa Makka, walimfunika kivuli Mtume (s.a.w), siku ya kuifungua, akawaombea baraka. (Kutoka kwa mama Aisha (r.a), amesema: Tulikuwa na ndege wa nyumbani, Mtume wa Allah (s.a.w) akiwa nasi anatulia na kuthibiti mahali pake, haji wala haendi na akitoka Mtume wa Allah (s.a.w) huja na kuondoka). Yaani yule njiwa alikuwa anamheshimu Mtume (s.a.w) kwa hiyo anatulia tuli anapokuwepo Mtume (s.a.w). Tukio la Pili: (Ni kisa cha mbwa mwitu kilicho mashuhuri), na kimepokelewa kwa njia nyingi hata kimechukua hukumu ya tawatur, kisa hiki cha ajabu kimenakiliwa kwa njia nyingi kutoka kwa mashuhuri wa kisahaba wema, kati yao: Abu Said Al-Khudry, Salamata bin Al-Akuwai, Ibn Abi Wahab, Abu Hurayra na mwenye kisa: Mchungaji Uhban. Wamepokea hawa kwa njia nyingi kwamba (Wakati ambapo mchungaji mmoja anachunga mbuzi wake, akajitokeza mbwa mwitu kwa mbuzi kati yao, akamchukua (Mchungaji), mbwa mwitu akachuchumaa, na akamwambia mchungaji: Je humchi Allah, umenizuilia kati yangu na riziki yangu, mchungaji akasema: Ajabu kwa mbwa mwitu anayeongea maneno ya binadamu! akasema mbwa mwitu: Je nikujuulishe cha ajabu zaidi kuliko hicho? Mjumbe wa Allah kati ya harra mbili (Madina) anawasimulia watu habari za yaliyotangulia. Milango ya pepo imefunguliwa kwa ajili yake. Anakuiteni kuelekea huko). Na pamoja na kuwa njia zote zimeungana katika kuongea kwa mbwa mwitu, isipokuwa yenye nguvu zaidi ya hizo ni Hadithi ambayo ameipokea Abu hurayra (r.a) basi ndani yake: (Amesema Mchungaji: Ni nani wa kunusuru mbuzi wangu? Mbwa mwitu akasema: Mimi ninawachunga hadi utakaporejea, mtu yule akasalimisha mbuzi kwake kisha akaenda zake, na akaeleza kisa chake, na kusilimu kwake, na kumkuta kwake Mtume (s.a.w) akipigana) akarejea akamkuta mbwa mwitu akiwa mchungaji mwaminifu, wala hakuna upungufu katika mbuzi (Na akamchinjia yule mbwa mwitu mbuzi mmoja kati ya wale) malipo ya kumwelekeza kwake. Na katika njia nyingine (Kwamba imetokea kwa Abi Sufian bin Harb na Swafwan bin Umayya pamoja na mbwa mwitu waliyemkuta amemchukua paa, paa akaingia kwenye Haramu, mbwa mwitu akaondoka, wakashangaa kwa jambo hilo, akasema mbwa mwitu: Cha ajabu kuliko hicho ni Muhammad bin Abdullah yuko Madina anakuiteni kwenda peponi. Akasema Abu Sufian: Naapa kwa Lata na Uzza lau ukiyaeleza haya Makka utaiacha tupu). Tunapata kutokana hii: Hakika kisa cha mbwa mwitu hiki kinaleta ukinaifu na utulivu kama Mutawatir ya kimaanawy. Tukio la tatu: Ni kisa cha ngamia kilichopokelewa kwa njia tano au sita kutokana na sahaba mashuhuri: Abu Hurayra, Tha’laba bin Malik, Jabir bin Abdallah, Abdallah bin Umar, Abdallah bin Abi Awfa na mifano yao, wote ni wenye kuafikiana juu ya kwamba: Ngamia alimjia Mtume (s.a.w) na akasujudu mbele yake sijida ya taadhima na kutukuza na akaongea naye. Na wanaeleza kwa njia nyinginezo, hakika ngamia huyo alicharuka kwenye bustani (Na ilikuwa haingii yeyote kwenye bustani hiyo isipokuwa ngamia huyo humletea shida, basi Mtume (s.a.w) alipoingia kwake akamwita akaweka mdomo wake juu ya Ardhi na akapiga magoti mbele yake akamwekea hatamu). (Na katika habari katika Hadithi nyingine hakika Mtume (s.a.w) aliwauliza kuhusu ngamia huyo wakaeleza kuwa wao walitaka kumchinja). (Na katika mapokezi: Hakika yake ameshitakia kwangu kwamba nyinyi mlitaka kumchinja baada ya kumtumia katika kazi ngumu tangu utotoni kwake, wakasema: Naam). Na pia kwamba ngamia wa Mtume (s.a.w) anayeitwa Al-Adhbaa (Hakula wala hakunywa baada ya kifo chake (s.a.w) hata akafa) na ameeleza Abu Is-haqa Al-Asfarany (Kisa cha Al-Adhbaa na kuongea kwake na Mtume (s.a.w)) katika jambo muhimu. Na imethibiti katika sahihi kwamba ngamia wa Jabir bin Abdallah Al-Answary alichoka kwenye safari hakuweza kuendelea na mwendo mpaka Mtume (s.a.w) akampiga mpigo hafifu (Akachangamka hata akawa haimiliki hatamu yake) na hii ni kwa kile alichoona katika upole wa Mtume (s.a.w). Tukio la Nne: Amepokea Al-Bukhary na maimamu wa Hadithi: (Watu wa Madina usiku mmoja walifazaika, watu wakaenda upande wa sauti wakakutana na Mtume (s.a.w) akiwa anarejea na alikuwa amekwisha watangulia kwenda kwenye sauti ile. Na tayari amekwisha hakikisha habari yenyewe juu ya farasi wa Abu Twalha amechukuliwa vitu vyake na hali ya kuwa upanga ukiwa shingoni mwake naye akisema: Hamtachungwa (Yaani hakuna kitu mnacho kihofu)) na akasema kumwambia Abu Twalha: Tumemkuta farasi wako baharini na alikuwa na mazao, Yaani anatembea taratibu. Akawa baada ya usiku ule hakaribiwi. Na imethibiti kwa mapokezi sahihi kwamba (Alimwambia farasi wake - (a.s) - akisimama kwa ajili ya swala katika baadhi ya safari zake: Usiondoke Allah akubariki mpaka tumalize swala yetu. Na akamweka upande wake wa kibla. Basi hakutikisa kiungo hadi Mtume (s.a.w) aliposwali). Tukio la Tano: (Ni kumtiisha simba kwa Safina – Mtumishi wa Mtume (s.a.w) – wakati alipomwelekeza kwa Muadhi huko Yemen akamkuta simba akamtambulisha: Kuwa Yeye ni mtumishi wa Mtume (s.a.w) na barua yake akanguruma na kujiepusha na njia. Na akataja katika kuondoka kwake mfano wa hivyo) na katika mapokeo mengine kutoka kwake: Kwamba Safina alipotea njia katika kurudi akamwona Simba, akasema: (Akawa ananisogeza kwa bega lake hadi akanisimamisha juu ya njia). (Na imepokewa kutoka kwa Umar (r.a) kwamba Mtume (s.a.w) alikuwa katika sherehe baina sahaba wake tahamaki akaja bedui amewinda kenge. akasema: Nani huyu? Wakasema: Nabii wa Allah, akasema: Naapa kwa Al-Lata na Al-Uzza sitakuamini au huyu kenge akuamini akamtupa mbele ya Mtume (s.a.w) Mtume (s.a.w) akamwambia: Ewe kenge, akamjibu kwa ulimi bayana wanamsikia kaumu yote: Labeika wa sa’dayka....) Bedui yule akaamini. (Na kutoka kwa Ummu Salamat: Mtume (s.a.w) alikuwa kwenye jangwa, paa akamwita: Ewe mjumbe wa Allah) mpaka mwisho wa Hadithi Akatoka anakimbia naye akisema: (Nashuhudia hapana Mola ila Allah na wewe ni mtume wa Allah). Na kama hivi kuna mifano ya vielezo hivi mingi mno hatukubainisha isipokuwa yaliyokuwa mashuhuri katika mifano yenye kukinaisha. Basi ewe mwanadamu na ewe usiyemjua Nabii huyu Mkarimu (s.a.w) wala humtii, zingatia! Na ujitahidi ili usiporomoke katika hali ambayo ni ya chini zaidi kuliko ya mbwa mwitu na simba, kwani wanyama hawa wanamjua Mtume mtukufu (s.a.w) na wanamtii.
Ni kwa Wafu, Majini na Malaika kumtambua Mtume (s.a.w), na ina matukio mengi mno tutaeleza kati ya hayo kwa njia ya mfano mifano michache mashuhuri walioinakili maimamu wa kutegemewa. Tutaeleza kwanza mifano ya Wafu ama Majini na Malaika basi mifano yake mutawatir na mingi mno. Mfano wa Kwanza: Amepokea Imamu Al-Hasan Al-Basry, na yeye ni Imamu wa wanazuoni wa Dhahiri na Batin na katika wanafunzi wa kweli wa Imamu Ali Karramallah wajhahu katika kipindi cha Taabiina: (Mtu alimjia Nabii (s.a.w) akamweleza kwamba yeye amemweka binti yake katika bonde kadha) Mtume (s.a.w) akamuhurumia (Akaenda pamoja naye kwenye bonde na akamwita kwa jina lake: Ewe fulani jibu kwa idhini ya Allah, akatoka na huku yeye (mwanamke) akisema: Labbayka wasaadayka: Akamwambia: Wazazi wako wamesilimu – ukipenda – nikurejeshe kwao. Akasema: Sina haja nao mimi, Nimemwona Allah ni bora kwangu kuliko wao). Mfano wa Pili: Amepokea Imamu Al-Baihaqy na Imamu Ibn Ady hali ya kuwekwa sanadi (Kutoka kwa Anas kwamba kijana katika answary alifariki, naye ana mama kikongwe kipofu - naye ndiye wa pekee wake - tukamsitiri, na tukamuazz akasema: Mwanangu! Tukasema: Naam. Akasema: Ewe Mola ikiwa unajua kwamba mimi nimehama kwa ajili yako na kwa ajili ya Nabii wako kwa matarajio kuwa utanisaidia kwa kila shida, basi usinibebeshe msiba huu kamwe. Hatukuondoka ila alifunua nguo uso wake, akala na tukala). Imamu Al-Busiry ameashiria tukio hili katika kasida yake (Burdat Al-Madihi) kwa kusema: لَو۟ نَاسَبَت۟ قَد۟رَهُ اٰيَاتُهُ عِظَمًا اَح۟يَى اس۟مُهُ حٖينَ يُد۟عٰى دَارِسَ الرِّمَمِ Angenasibisha utukufu wake aya zake kwa utukufu Jina lake lingehuishwa wakati akiitwa msomaji wa waliooza. Tukio la Tatu: Amepokea Imamu Al-Baihaqy na wengine Kutoka kwa Abdillah bin Ubaidillah Al-Answary: Nilikuwa katika waliomzika Thabit Bin Qays, na alikuwa ameuliwa Yamaamah, tukamsikia wakati tulipomwingiza kaburini anasema: Muhammadun Rasulullah, Abubakr As-Siddiq, Umar As-Shahiid, Uthman Al-Barru Rahiim. Tukamtazama wakati huo alikuwa maiti Akawa ametoa habari ya kufa shahidi kwa Umar kabla ya kutawalia kwake ukhalifa. Tukio la Nne: Amepokea Imamu At-Tabarany na Abu Nuaim katika Dalailu An-Nubuwwat kutoka kwa Nuuman Bin Bashir kwamba Zaid bin Kharijah alidondoka maiti katika moja ya vijia vya Madina akainuliwa na kusitiriwa, tahamaki walimsikia kati ya waombolezaji na wanawake wakipiga kelele kumzunguka akisema: Nyamazeni, nyamazeni, akafunua uso wake, akasema: Muhammadun Rasulullah.. kisha akasema: Assalamu alaykum warahamatullah wabarakaatuhu. Kisha akarudi kuwa maiti kama alivyokuwa. Ikiwa wafu ambao hawana uhai wanasadikisha utume wake (s.a.w) vipi ikiwa hawamsadiki walio na uhai? Je hawa walio hai waovu hawawi ni wenye kukosa uhai zaidi kuliko wale wafu? Ama Malaika kumhudumia Mtume (s.a.w) na kumdhihirikia na Majini kumwamini yeye na kumtii, ni jambo lililothibiti kwa tawatur, Qur’an imeweka wazi jambo hili katika nyingi ya aya zake tukufu, na elfu tano katika Malaika walikuwa watiifu kwa amri yake - kama sahaba wema - katika vita vya Badri kama ilivyopatikana katika Qur’an tukufu, hata Malaika hao walipata – baina ya Malaika wengine – utukufu wa kushiriki katika vita kama walivyoupata watu wa Badr. Katika suala hili kuna pande mbili: Upande wa Kwanza: Kuwepo kwa Majini na Malaika na uhusiano wao na sisi. Hili limethibiti kwa namna ya kukinaisha kama kuwepo kwa mnyama na Mwanadamu hakuna yeyote anatilia shaka hilo. Na hili tumekwisha kulithibitisha kwa yakini ya kukata shauri katika (Neno la Ishirini na Tisa) basi tunaelekeza kuthibitisha kwenye neno hilo. Upande wa Pili: Ni kuona kwa watu wa umma Malaika na kuongea nao na Majini kwa vile walivyopata utukufu wa kunasibiana na Mtume Mtukufu (s.a.w) na kudhihirisha athari katika athari za miujiza yake. Hakika amepokea Al-Bukhary na Muslim na Maimamu wa Hadithi kwa Kuafikiana: (Kutoka kwa Umar (r.a) amesema: Wakati ambapo tumekaa kwa Mtume wa Allah (s.a.w) siku moja alipotuchomozea mtu mweupe sana wa nguo mweusi sana wa nywele haionekani kwake athari ya safari wala hakuna yeyote kati yetu anayemjua mtu yule hadi akakaa kwa Mtume (s.a.w)), مَا ال۟اِس۟لَامُ وَمَا ال۟اٖيمَانُ وَمَا ال۟اِح۟سَانُ akamuuliza kuhusu Uislamu, Imani na Ihsani na alimjulisha Mtume (s.a.w) mtu huyo yote aliyoyauliza. (Kisha akasema: Ewe Umar Je, unamjua ni nani muulizaji, nikasema: Allah na Mjumbe wake ni wajuzi zaidi, akasema: Hakika yule ni Jibril amekujieni kuwafundisha dini yenu). Na imethibiti kwa mapokezi sahihi yaliyokatiwa usahihi na yako katika daraja la tawatur ya kimaanawy wanaipokea watu wa Hadithi: Kwamba sahaba mara nyingi walikuwa wakimwona Jibril (a.s) kwa Mtume (s.a.w) akiwa katika sura ya Dahiyyat Al-kalby (r.a) mwenye uzuri na kupendeza, kati yao ni Umar, Ibn Abbas, Usama, Harith, Aisha As-Siddiqat na Ummu Salamat (r.a) wanasema: Hakika sisi tunamwona Jibril kwa Mtume (s.a.w) akiwa katika sura ya Dahiyyat Al-kalby mara nyingi sana. Je inayumkinika kwa hawa kusema kitu: Tunaona na hali ya kuwa hawaoni? Na imethibiti kwa isinadi sahihi kutoka kwa Sa’d bin Abi Waqqas – mmoja wa waliobashiriwa pepo na mfunguzi wa Uajemi – amesema: Hakika sisi tumeona katika vita vya Uhud kwamba Mtume (s.a.w) (Kuliani kwake na kushotoni kuna Jibril na Mikail katika sura ya wanaume wawili na juu yao (wamevaa) nguo nyeupe) nao wakiwa katika hali ya walinzi wawili wanaomlinda. Akisema bingwa katika mabingwa wa Uislamu mfano wa Saad: Tumeona, je inayumkinika kutokea kinyume?. Kisha abu Sufyan bin Harithi bin Abdil-Muttalib – Ibn ami wa Mtume (s.a.w) - aliona siku ya Badr (Wanaume weupe juu ya farasi wenye Bulqin (wenye rangi ndani yake kuna weupe na rangi nyengine) baina ya mbingu na Ardhi). (Na Mtume (s.a.w) alimwonesha Hamza Jibril katika Al-kaaba akaanguka akiwa amezimia). Basi mifano hii ya kuona Malaika ni mingi sana, na matukio yote haya yanadhihiri ikiwa ni aina ya miujiza ya Muhammad na inajulisha kwamba Malaika wanaogelea kama vipepeo katika nuru ya utume wake. Ama kukutana na Majini na kuwashuhudia, kunatokea kwa wingi sana hata kwa watu wa kawaida, basi vipi kwa sahaba wema (r.a), isipokuwa maimamu wa Hadithi wanatunakilia habari sahihi zaidi na zenye kuthibiti. (Abdullah Ibn Masuud aliona Majini usiku wa Majini – yaani kuongezeka kwao katika tumbo la mtende – na alisikia maneno yao na aliwashabihisha na watu wa Az-Zatt) nao ni watu kutoka Sudan warefu. Kisha hakika tukio mashuhuri wanalinakili na wanalitoa maimamu wa Hadithi na wanalikubali nalo: (Khalid Bin Al-Waliid – wakati alipolivunja (sanamu) Al-Uzza - kumuua mwanamke mweusi ambaye amemtokea akiwa ametawanya nywele zake akiwa uchi akamkata vipande viwili kwa upanga wake na akamjulisha Mtume (s.a.w) akasema: Huyo ni Al-Uzza), na walikuwa watu wanamwabudu naye akiwa katika sanamu la Al-Uzza. Na hatoabudiwa milele. Na kutoka kwa Umar Bin Al-Khattab (r.a), kwamba amesema: Wakati ambapo sisi tulikuwa tumekaa pamoja na Mtume (s.a.w). Ghafla alikuja Mzee mkononi mwake kuna fimbo akamsalimia Mtume (s.a.w) Mtume akumuitikia. Na akasema sauti ya jini, nani wewe? Akasema: Mimi ni Haamat. Katika Hadithi ndefu na hakika Mtume (s.a.w) alimfundisha sura za Qur’an. Tukio hili pamoja na kuwa limekosolewa kwa watu wa Hadithi isipokuwa maimamu wengine wamehukumu usahihi wake. Na kwa hali yoyote hatuoni ulazima wa kurefusha, kwani mifano katika mlango huu ni mingi sana. Na tunasema vilevile: Hakika ya wale ambao wamepata nuru ya Mtume (s.a.w) na wameleleka kwa mafunzo yake na wamefuata nyayo yake na wao wanazidi maelfu katika mifano ya Sheikh Al-Kaylani katika mawalii na Maqutubu na Wanazuoni wateule hakika wamekutana na Malaika na Majini na wameongea nao, mapokezi ni mutawatir na mengi na ya kukinaisha. Naam, kwa hakika Umma wa Muhammad kukutana na Malaika na Majini na kuongea nao hakika hiyo ni athari katika athari za malezi ya Mtume (s.a.w) na uongofu wake usio wa kawaida.
Hakika Ismat (kuepusha maasi) ya Allah (s.w) kwa Mtume (s.a.w) na kumlinda kutokana na maudhi ya watu ni muujiza dhahiri na hakika iliyo wazi ambayo Qur’an tukufu imeielezea katika kauli yake (s.w): وَاللّهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ Basi katika aya hii tukufu kuna miujiza mingi. Kwani Mtume Mtukufu (s.a.w) alipotangaza utume wake hakika hakuwa ametoa changamoto kwa kundi moja wala kaumu wala wanasiasa wala watawala maalum wala jamii yake bali aliwapa changamoto masultani wote na watu wote wa dini, aliwapa changamoto wote na hana mhifadhi isipokuwa Allah, na hata ami yake amemchangia uadui. Na kaumu yake na kabila lake walikuwa ni maadui kwake. Na pamoja na hivi alidumu kwa miaka ishirini na tatu bila ya mlinzi anayemlinda, pamoja na kukabiliana kwake na hatari na hali ya maangamizi Allah alimlinda kutokana na watu na alimhifadhi hata akagura kwenye hadhara ya juu kwa utulivu kamili. Katika yanayotujulisha ujulisho wa jua kwenye weupe wa mchana kiasi cha umadhubuti wa hakika iliyomo katika aya tukufu: وَاللّهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ na kiasi cha kuwa ni nukta ya kuegemea kwake. Na tutataja machache katika matukio ambayo yamethibiti kwa namna ya kukinaisha na tutayaeleza kwa njia ya mfano: Tukio la Kwanza: Wanasimulia watu wa Sira na Hadithi wakiafikiana juu ya kuwa: Wakati walipokutanika Makuraishi juu ya kumuua (s.a.w) aliwajia Ibilisi katika umbo la mzee na akawaelekeza wachukue kijana kutoka katika kila kabila – ili usitokee mzozo kati yao – wakaenda kiasi cha zaidi ya wanaume mia mbili wakiongozwa na Abi Jahl na Abi Lahab kuelekea katika nyumba ya Mtume (s.a.w) na Ali (r.a) alikuwa kwake akamwamrisha alale kitandani kwake na Mtume (s.a.w) aliwangojea mpaka Makuraishi walipokuja na kuzingira nyumba (Akawatokea Mtume (s.a.w) kutoka nyumbani mwake na akasimama machoni pao na Allah (s.w) alipiga juu ya uoni wao (wakawa hawaoni) na akamwaga mchanga juu ya vichwa vyao, na akakombokana nao). Na vilevile (Kumuhami kwake wasimwone pangoni kwa aliyoyaandaa Allah katika ishara na Buibui aliyefuma juu yake. Na wakasimama njiwa wawili juu ya mdomo wa Pango). Tukio la Pili: Nalo ni kisa cha Suraqa Bin Malik Wakati wa kuhama, na Makuraishi walitenga kwa ajili ya Mtume (s.a.w) na Abubakar kiasi cha mali akaonya kwa hilo, akapanda farasi wake na akamfuata hata alipomkaribia Mtume (s.a.w) alimuombea dua dhidi yake miguu ya farasi wake ikatitia akadondoka chini, kisha akapanda na akamkaribia hata akasikia kisomo cha Mtume (s.a.w) na hali ya kuwa hageuki na Abubakar (r.a) anageuka na akamwambia Mtume (s.a.w) tumefikiwa, akasema: Usihuzunike hakika ya Allah yu pamoja nasi. Kama alivyosema hilo pangoni (Akatitia tena hadi kwenye magoti yake na akadondoka akitengana naye akamkemea akasimama (farasi) kwa miguu yake kama moshi, Akawalingania kwa kuomba amani. Mtume (s.a.w) alimwandikia amani. Na Mtume (s.a.w) alimwamuru (Suraqa) asimwache yeyote kuwafuata akaondoka). (Na katika habari nyingine kwamba mchungaji mmoja alitambua habari yao, akatoka akishadidia kuwajulisha Makuraishi alipofika Makka alipigwa kwenye moyo wake, ikawa hajui akifanyacho na akasahaulishwa kile alichotoka kwa ajili yake hadi akarejea mahali pake) kisha akajua kwamba yeye amesahaulishwa. Tukio la Tatu: Na wanapokea maimamu wa Hadithi kwa njia tofauti kwamba katika vita vya (Ghatafan) na (Anmar) mkuu wa kabila lake naye ni (Ghaurith ibn Al-Harith Al-Muhariby alitaka kummaliza Mtume (s.a.w) ikiwa Mtume (s.a.w) hakujua (Kuja kwake) isipokuwa alipokuwa ghafla amesimama kichwani kwake akiwa amenyoosha upanga wake akasema: Ewe Mola nitosheleze kwa utakavyo akaangukia uso wake kutokana na machungu makali yaliyokuwa kati ya mabega yake na upanga wake ukadondoka kutoka mkononi mwake). Na imepokelewa kwamba (s.a.w) alimjia Bedui (Akanyoosha upanga wake na akasema: Nani anayekuzuia kutokana na mimi? akasema: Allah! Mkono wa yule Bedui ukatetemeka na upanga wake ukadondoka) Mtume (s.a.w) akauchukua na akasema: Na nani anayekuzuia hivi sasa? Kisha Mtume (s.a.w) akamsamehe Akarejea kwa watu wake akasema: Nimekujieni kutoka kwa mbora wa watu. Na yamesimuliwa mfano wa masimulizi haya kwamba imemtokea siku ya Badr hali ya kuwa alikwishakaa peke yake mbali na sahaba zake kwa ajili ya kukidhi haja yake, mtu mmoja katika wanafiki akamfuatilia, akaeleza mfano wake kwamba alinyanyua upanga wake ili amteremshie Mtume (s.a.w) tahamaki anamtazama basi pale Mnafiki akawa anatetemeka na upanga ukadondoka kutoka mkononi mwake. Tukio la Nne: Wamepokea maimamu wa Hadithi kwa mapokezi mashuhuri yaliyo karibu na Mutawatir, na wametaja wengi wa Wanazuoni wa tafsiri, Kwamba sababu ya kuteremka aya tukufu: إِنَّا جَعَلْنَا فِي أَعْنَاقِهِمْ أَغْلاَلاً فَهِيَ إِلَى الأَذْقَانِ فَهُم مُّقْمَحُونَ ٭ وَجَعَلْنَا مِن بَيْنِ أَيْدِيهِمْ سَدًّا وَمِنْ خَلْفِهِمْ سَدًّا فَأَغْشَينَاهُمْ فهُمْ لاَ يبْصِرُونَ kwamba Abu Jahal aliapa kwamba endapo nitamwona Muhammad akiwa anasujudu kwa hakika nitampiga kwa jiwe hili (Akamjia na jiwe na hali akiwa anasujudu na Makuraishi wanatazama, ili amtupie likanasa mkononi mwake na mikono yake ikakauka shingoni kwake) na baada ya Mtume (s.a.w) kutimiza swala yake akaondoka na ukafunguka mkono wa Abi Jahal. Ima kwa idhini yake (s.a.w) au kwa kutokuwepo kwa haja tena. Hakika Al-Walid Ibn Al-Mughira (Alimjia Mtume (s.a.w) ili amuue kwa jiwe kubwa Allah akafuta uoni wake hakumwona Mtume (s.a.w), na akasikia kauli yake akarejea kwa sahiba zake na hakuwaona hadi walipomwita) hadi Mtume (s.a.w) alipotoka msikitini uoni wake ulirejea, kwa ajili ya kutokuwepo kwa haja tena. Na imethibiti kutoka kwa Abi Bakar (r.a) kwamba: Baada ya kuteremka sura (tabbat yada Abi lahabi) alikuja Ummu Jamili, mke wa Abi Lahab aliyepewa jina kuwa Kichukuzi wa kuni (Mtume wa Allah (s.a.w) akiwa amekaa msikitini na pamoja naye alikuwa Abu Bakar na mkononi mwake kulikuwa kuna gao la mawe aliposimama kwao hakumwona isipokuwa Abu Bakar na Allah (s.w) alichukua uoni wake kumwona Mtume (s.a.w) akasema: Ewe Abu Bakar yuko wapi sahibu wako imenifikia kwamba ananisema vibaya, wallahi ningemwona hakika ningepiga mdomo wake kwa gao hili la mawe). Naam. Mchukuzi wa kuni wa jahanamu – bila ya shaka – haoni Mfalme mtukufu kama huyu ambaye amemteua Allah mahususi kwa daraja ya juu. Tukio la Tano: Imethibiti kwa unakili sahihi (Habari ya Amir bin At-Tufail na Arabid bin Qays walipokuja kwa Mtume (s.a.w), na Amir alikuwa amemwambia: Mimi nitakushughulishia uso wa Muhammad wewe mpige, ikawa hakumwona amefanya kitu, alipomsemesha katika hilo, alimwambia: Wallahi sikukusudia kumpiga ila nimekuona wewe kati yangu na kati yake, je nikupige?). Tukio la Sita: Na imethibiti kwa unakili sahihi vilevile: (Kuwa Shaybatu Ibn Uthman Al-Hajaiby imemkuta siku ya Hunain) au Uhud (Na Hamza alikuwa amemuua baba yake na ami yake, akasema: Leo ninapata (ninatimiza) kisasi changu kwa Muhammad, watu walipochanganyika alimjia kutokea kisogoni kwake na akanyanyua upanga wake ili aupige juu yake. Akasema: Mtume (s.a.w) akanihisi (Kuwa nataka kumpiga) akaniita akaweka mkono wake juu ya kifua changu na hali ya kuwa ni kiumbe anayechukiza zaidi kwangu basi hakuuinua (mkono huo) isipokuwa akiwa ni kiumbe anayependeza zaidi kwangu. Akaniambia: Sogea, na upigane, nikaenda mbele yake nikipiga kwa upanga wangu na nikimkinga kwa nafsi yangu, lau ningekutana na baba yangu saa ile ningempiga tofauti na yeye Mtume (s.a.w)). Na kutoka kwa Fudhala bin Amru amesema: Nilitaka kumuua Mtume (s.a.w), mwaka wa kufungua Makka, naye akiwa anatufu kwenye nyumba, nilipomkaribia akasema: Ni Fudhalat? Nikasema ndio! Akasema: Nini ulikuwa unaiambia nafsi yako? Nikasema: Hapana kitu. Akacheka na akanitakia msamaha na akaweka mkono wake juu ya kifua changu, moyo wangu ukatulia, Wallahi hakuunyanyua hadi ikawa Allah hakuumba kitu chenye kupendwa zaidi kwangu kuliko yeye. Tukio la Saba: Imethibiti kwa unakili sahihi: Hakika Wayahudi walikula njama juu yake wakati (Aliokaa kwenye ukuta, akachomoza mmoja wao ili amtupie jiwe Mtume (s.a.w) akasimama akaondoka) yakabatilika waliyokuwa wanayafanya kwa hifadhi ya Allah. Na kulikuwa na matukio mengi katika mifano ya tukio hili. Basi anapokea Imamu Al-Bukhary na Muslim na maimamu wa Hadithi Kutoka kwa Aisha (r.a) amesema: Mtume (s.a.w) alikuwa analindwa hadi ilipoteremka aya: وَاللّهُ يعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ Mtume (s.a.w) akatoa kichwa chake kutoka kwenye Quba: يَا اَيُّهَا النَّاسُ ان۟صَرِفُوا فَقَد۟ عَصَمَنٖى رَبّٖى عَزَّ وَجَلَّ Enyi watu ondokeni Allah (s.w) ameshanilinda. Risala hii inaweka wazi tangu mwanzo hadi hapa: Hakika kila aina katika aina za viumbe hivi, na kila ulimwengu kati hivyo, vinamtambua Mtume (s.a.w) vina mafungamano na uhusiano pamoja naye. Ambapo vinadhihirisha miujiza yake (s.a.w) kutoka katika kila aina miongoni mwa aina za viumbe, yaani huyu Mtume (s.a.w) ni Mjumbe na Mwenye kutumwa kutoka kwa Allah (s.w) kwa sifa yake kuwa ni Mola Mlezi wa walimwengu Muumba wa ulimwengu. Naam, kama ilivyo afisa mwenye cheo na Mkaguzi mwenye daraja mbele ya Sultani kila ofisi inamtambua katika ofisi za Dola, na anapoingia yeyote kati ya hizo atakua na makaribisho motomoto, kwa kuwa yeye ni mwenye kuamrishwa kutoka kwa Sultani Mkuu, kwani lau tungekadiria kwamba amekuwa Mkaguzi wa Sharia tu, basi zitamkaribisha ofisi za sheria tu, na hazimjui vyema afisi nyingine, na kama akiwa mkaguzi mkuu wa jeshi hazimjui afisi nyengine rasmi za Dola, wakati ambapo inafahamika kutoka katika mifano iliyotangulia hakika afisi zote za kiungu zinamtambua Mtume (s.a.w) sana au Mwenyezi Mungu anamtambulisha kwao kuanzia kwa Malaika hadi kwa Nzi na Buibui. Basi yeye bila shaka ni mwisho wa Manabii na Mtume wa Bwana Mlezi wa walimwengu, na kwamba Utume wake ni wa jumla kwa viumbe wote hauhusu umma maalum kama wengine katika Manabii na Mursalina.
Nazo ni ishara tangulizi: Yaani ni mambo yanayovunja ada ya ulimwengu, yaliyodhihiri kabla ya kupewa Utume, na yanahesabiwa ni katika dalili za Utume kwa Nabii Muhammad (s.a.w), kwa sababu ya kuhusiana na Utume, mambo hayo yanagawika sehemu tatu:
Yale ambayo Taurati, Injili, Zaburi na Sahifa za Manabii (a.s) vimeelezea kuhusu Utume wa Nabii Muhammad (s.a.w) na hili limethibiti kwa kauli ya Qur’an tukufu. Naam, maadamu vitabu hivyo ni vitabu vya mbinguni, na wenye vitabu hivyo ni Manabii watukufu (a.s), hapana budi kuelezea kwao nuru itakayoangazia nusu ya ulimwengu, na kufuta dini nyingine, na kubadili alama za ardhi, nasema kuwa kumtaja mtu huyu mwenye baraka tele ni jambo la hakika na linalohitajika. Hivi inawezekana kwa vitabu hivyo ambavyo havipuuzii matukio madogo madogo viache kutaja tukio kuu kabisa katika historia ya wanadamu ambalo ni tukio la Utume wa Nabii Muhammad (s.a.w)? Ikiwa hapana budi vitabu hivyo kuelezea, kwani ima vitakanusha habari hiyo ili ilinde dini yake na kitabu chake kutokana na kufutika na kuharibiwa, au vitalisadikisha, yaani kumsadikisha yule Nabii wa ukweli vipate kuhifadhi dini na kitabu chake kutokana na kupenya imani potofu na kunyemelea kwa upotoshaji. Na kwa kuwa marafiki na maadui wameafikiana juu ya kutokuwepo alama yoyote katika vitabu hivyo ya kukadhibisha kwa vyovyote iwavyo, kwa hiyo zilizopo ni alama za kusadikisha. Maadamu kusadiki kumesimama kwa namna isiyo na mipaka na kwamba kuna sababu ya wazi na sababu ya msingi inayohitajia kuwepo kwa usadikishaji huu, kwa upande wetu tutathibitisha huo usadikishaji kwa kutumia hoja tatu za wazi ambazo zinazojulisha kuwepo kwake:
Hakika mtume mtukufu (s.a.w) amewasomea aya tukufu akiwapa changamoto kwazo, ni kana kwamba anawaambia kwa lugha ya Qur’an tukufu: Hakika vitabu vyenu vinasadikisha ambayo yanahusu sifa zangu na kukubali ambayo ninayafikisha kwa walimwengu wote. قُلْ فَأْتُواْ بِالتَّوْرَاةِ فَاتْلُوهَا إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ فَقُلْ تَعَالَوْاْ نَدْعُ أَبْنَاءنَا وَأَبْنَاءكُمْ وَنِسَاءنَا وَنِسَاءكُمْ وَأَنفُسَنَا وأَنفُسَكُمْ ثُمَّ نَبْتَهِلْ فَنَجْعَل لَّعْنَةُ اللّهِ عَلَى الْكَاذِبِينَ Pamoja na changamoto hii ya waziwazi hajajitokeza mwanazuoni yeyote katika wanazuoni wa Kiyahudi, wala Kasisi katika Makasisi wa Kikristo kuweza kuonesha tofauti na asemayo Mtume wa Allah (s.a.w). Kama kungekuwa na kitu chochote hata kiwe kidogo sana cha aina hii hao makafiri na wanafiki wangetangaza hilo miongoni mwa Wayahudi wenye ukaidi na hasadi, nao ni wengi kila mahali na wakati. Changamoto ikawa, waone tofauti yoyote katika amri za Allah (s.w) ambazo mtume (s.a.w) anazifikisha, au atapambana nao mapambano yasiyo na nafuu ndani yake. Na kwa kuwa wameshindwa kuleta yaliyo tofauti na anavyofikisha wakafadhilisha vita maangamizo na kugura, yaani hawakupata jambo la kumsuta. Na kama wangepata tofauti na kauli yake basi kuonyesha hilo ingekuwa ni jepesi kwao kuliko kupoteza roho, mali, na kuharibu miji.
Aya za Taurati, Injili na Zaburi zimechanganyika na maneno mageni na vitabu hivyo, kwa kufululiza kufasiriwa kwake, na kuchanganyika maneno ya wafasiri na taawili zao za makosa na aya zake, kwa kuwa aya zake hazina muujiza sawa na uliomo katika Qur’an tukufu, ukiachilia mbali na waliyofanya majahili na wenye nia mbaya miongoni mwa upotoshaji ndani ya vitabu hivyo, upotoshaji huo na mabadilisho vilizidi hata kwamba Al-Allaamah mashuhuri Rahmatallah El-Hindy aliwapa wanazuoni wa Wayahudi na Wakristo hoja isiyojibika kwa kuonyesha maelfu ya mapotosho katika vitabu vilivyotangulia. Na pamoja na kiasi hiki cha upotoshaji, mwanazuoni mashuhuri Husein El-Jisr - (Allah amrehemu) - ametoa katika zama hizi kutoka katika vitabu hivyo dalili mia moja na kumi juu ya Utume wake (s.a.w). Kutoka katika vitabu hivyo na kuzithibitisha katika kitabu chake kinachoitwa (Ar-Risaalat Al-Hamidiyya) na marehemu Ismail Haqy Al-Munaasitry amekifasiri kitabu kwenda katika lugha ya Kituruki, basi atakaye na akirejee. Kisha walio wengi katika wanazuoni wa Kiyahudi na Wakristo wamekiri kuwa: Katika vitabu vyetu zimo sifa za Nabii Muhammad (s.a.w), kati ya hao ni: Hercules katika wafalme wa Rumi ambaye alikiri kwa kusema kuwa: (Hakika ya Issa (a.s) amebashiri ujio wa Muhammad (s.a.w)). Na kama alivyokiri mtawala wa Misri Al-Mukawakas, Ibn Suriya, Ibn Akhtab na nduguye Kaab bin Usd, Zubayr bin Baatya na wengine katika wanazuoni wa Kiyahudi na viongozi wao wakisema kuwa: (Ndio sifa zake zimo ndani ya vitabu vyetu zimetajwa humo). Na kama walio wengi kati ya watu mashuhuri wa wanazuoni wa Kiyahudi na Wakristo wametupilia mbali uhasama na ukaidi wakaamini Uislamu baada ya kuwa wameziona sifa za Mtume (s.a.w) ndani ya vitabu vyao, na kuzibainisha kwa wengine katika wanazuoni, na kuwashinda kwa hoja. Kati yao ni: Abdullah bin salaam, Wahab bin Mnabbih, Abu Yaasir na Shamuel - mtawala wa Tubbaa - na kama kabila la Tubbaa walivyoamini kabla ya kuletwa Utume, na wana wawili wa Saayat nao ni Usaid na Thaalab ambao walinadi katika kabila la Bani Nadhiir wakiwalaumu zama walipompiga vita Mtume (s.a.w) hali wakisema: (Wallah yeye ndiye ambaye Ibn Haiban amekutoleeni ahadi kumhusu yeye). Na Ibn Haiban huyu ni mtu mchamungu ambaye alifikia hapo akiwa ni Mgeni kwa Bani Nadhiri kabla ya mtume hajapewa Utume (s.a.w), na akawaambia: وَاللّٰهِ هُوَ الَّذٖى عَهَدَ اِلَي۟كُم۟ فٖيهِ اب۟نُ هَي۟بَان۟ (Umekaribia muda wa kudhihiri kwa mtume na huu ndio mji wake wa kuhamia) na akafariki huko, isipokuwa kabila la bani Nadhiir halikuwajali, basi yakawasibu yaliyowasibu. Kama walivyoamini kati ya wanazuoni wa Kiyahudi: Ibn Yaamin, Mukhayrik, Kaab Al-Ahbaar na wengine mfano wa hao wengi katika wale walioziona sifa za mtume (s.a.w) ndani ya vitabu vyao na kuwashinda kwa hoja wale wasioamini. Na katika waliosilimu miongoni mwa wanazuoni wa Kikristo ni padri Bahira - kama ilivyokwisha kutajwa huko nyuma - na hii pale ambapo Mtume (s.a.w) alipokwenda Shamu pamoja na Ami yake Abu Twalib, hali ya kuwa ni mtoto wa miaka kumi na mbili, Bahira aliandaa chakula kwa ajili ya msafara wa Makuraishi, kwa kumkirimu mtume (s.a.w) akatazama na kukuta kuwa kiwingu kilichokuwa kikifunika msafara ule kilibaki kilipo, akasema, basi ninayemtaka bado amebakia pale, akamtuma mtu atakayemleta akamwambia ami yake Abu Twalib: Mrejeshe Makka, kwani Wayahudi ni mahasidi watamfanyia vitimbi, kwani sisi tunaziona sifa zake kwenye Taurati. Waliamini wote Nestuura na mfalme wa Uhabeshi An-Najashy, walipoona sifa za mtume (s.a.w) ndani ya kitabu chao. Na mwanazuoni wa Kikristo mashuhuri Dhaghaatur alitangaza sifa zake (s.a.w) kati ya watu wa Rumi, akafa shahidi. Pia aliamini Haarith ibn Abi Shummar Al-Ghassany - mwanazuoni wa Kikristo mashuhuri - na viongozi wa kiroho huko Shamu, na wafalme wake yaani mtawala wa Eliya, Hirakalet, Ibn Naatur, Garuud na wengineo mfano wa hao, walipoziona sifa zake (s.a.w) ndani ya vitabu vyao, isipokuwa Hiraklet hakutangaza imani yake kwa ajili ya kulinda utawala wake. Na mfano wa watu hawa ni wengi kama Salman Al-Faarisy ambaye alikuwa Mkristo, na hakuona sifa za mtume (s.a.w) ila alianza kumtafuta aliko na alipomuona akasilimu. Na vilevile Tamimi na huyu ni mwanazuoni mkubwa, na An-Najaashy mfalme mashuhuri wa Uhabeshi, na Wakristo wa Uhabeshi, na Maaskofu wa Najraan, hawa wote kwa kuafikiana kauli zao wanaelezea: Hakika sisi tumeamini tulipoziona sifa zake kwenye vitabu vyetu.
Tutataja kwa namna ya mfano tu, baadhi ya aya kutoka kwenye Taurati, Injili na Zaburi ambazo zinambashiria Mtume (s.a.w). Kwanza: Kuna aya katika zaburi ambayo maana yake: (Ee Mola tuletee msimamishaji wa sunna baada ya kukatika kwa Mitume). Na msimamishaji wa sunna ni katika majina yake Mtume (s.a.w). Na aya ya Injili: قَالَ ال۟مَسٖيحُ اِنّٖى ذَاهِبٌ اِلٰى اَبٖى وَ اَبٖيكُم۟ لِيَب۟عَثَ لَكُمُ ال۟فَارَق۟لٖيطَا (Masihi alisema mimi ninakwenda kwa baba yangu na baba yenu ili akutumieni huyo Al-Farqlet) yaani akuleteeni Ahmad. Na aya nyingine kutoka katika Injili اِنّٖى اَط۟لُبُ مِن۟ رَبّٖى فَارَق۟لٖيطًا يَكُونُ مَعَكُم۟ اِلَى ال۟اَبَدِ (Nami ninaomba kwa Bwana wangu akupeni Farkalet abaki nanyi hata milele). Na Al-Farkalet: Ni anayepambanua kati ya haki na batili, na hilo ni jina la Mtume (s.a.w) katika vitabu hivyo. Na aya ya Taurati: اِنَّ اللّٰهَ قَالَ لِاِب۟رَاهٖيمَ اِنَّ هَاجَرَ تَلِدُ وَيَكُونُ مِن۟ وَلَدِهَا مَن۟ يَدُهُ فَو۟قَ ال۟جَمٖيعِ وَيَدُ ال۟جَمٖيعِ مَب۟سُوطَةٌ اِلَي۟هِ بِال۟خُشُوعِ (Hakika Mwenyezi Mungu alimwambia Ibrahim. Hajar atazaa na itakuwa katika uzao wake mtu ambaye mkono wake utakuwa juu ya wote na mikono ya wote itakuwa imekunjuliwa kwake kwa unyenyekevu). Na aya nyingine katika Taurati: وَقَالَ يَا مُوسٰى اِنّٖى مُقٖيمٌ لَهُم۟ نَبِيًّا مِن۟ بَنٖى اِخ۟وَتِهِم۟ مِث۟لَكَ وَاُج۟رٖى قَو۟لٖى فٖى فَمِهٖ وَالرَّجُلُ الَّذٖى لَايَق۟بَلُ قَو۟لَ النَّبِىِّ الَّذٖى يَتَكَلَّمُ بِاِس۟مٖى فَاَنَا اَن۟تَقِمُ مِن۟هُ (Na akasema ewe Musa hakika mimi nitawapelekea wao Nabii kutoka katika wana wa ndugu zao atakuwa mfano wako na nitapitisha maneno yangu kwenye kinywa chake na mtu ambaye hakubali maneno ya Nabii anenaye kwa jina langu basi nitamuadhibu). Na aya ya tatu imo katika Taurati: (Musa amesema: Mola hakika ninaona katika Taurati umma ambao ni bora uliko nyumati zote uliotolewa kwa watu wanaamrisha mema na kukataza mabaya na wanaamini Allah, basi jaalia umma huo uwe wangu, akasema: Huo ni Umma wa Muhammad).
Vitabu vimeelezea kuhusu Muhammad kwa majina ya Kisaryani ndani ya majina ya Kiebrania kwa mfano: (Mushaffah, Munhamna, Himyata) na mengine katika majina ambayo yanatumika kwa maana ya Muhammad katika lugha ya Kiarabu. Ama jina la wazi kabisa (Muhammad) halikuja ila kwa nadra, na hili Wayahudi wamelipotosha kwa husda yao na upinzani wao, kati ya hizo ni aya ya Zaburi: (Ewe Daudi baada yako atakuja Nabii anaitwa Ahmad na Muhammad mkweli bwana, umma wake ni wenye kurehemewa). Kuwepo kwa aya hii ifuatayo katika Taurati alitangaza kabla ya mikono ya upotoshaji haijachezea sana, kila mmoja kati ya Abdallah bin Amri bin Al-Aas naye ni mmoja kati ya kina Abdallah saba ambao wana mtalaa mpana katika vitabu vilivyotangulia, na Abdallah bin Salaam na yeye ni katika wanazuoni wa Kiyahudi mashuhuri ambaye aliwatangulia wenzake katika kusilimu, na Kaab Al-Ahbaar na yeye ni katika wanazuoni wa Kiyahudi. Aya inamsemesha Nabii Musa (a.s), kisha inaelekea kwa mtume atakayekuja: Ewe Nabii hakika tumekutuma uwe shahidi na mwenye kubashiria kheri na mwonyaji na mlinzi wa wasiojua kusoma, wewe ni mja wangu, nimekuita mwenye kutawakkal, sio mkali wala mwenye ugumu, wala si mpiga kelele masokoni, wala si mwenye kuondosha ovu kwa ovu, bali anasamehe na Allah hatomfisha mpaka ainyooshe mila iliyopinda kwaye na waseme: لا إله إلا الله Na aya nyingine kutoka kwenye Taurati: (Muhammad ni mjumbe wa Allah kuzaliwa kwake ni Makka, na kuhamia kwake ni mji wa tiba, na ufalme wake utakuwa Shamu. Na umma wake ni wasifuji mno) na tamko la (Muhammad) kwenye aya hii limekuja kwa jina la Kisaryani yaani Muhammad. Vilevile aya nyingine kutoka katika Taurati: (Wewe ni mja wangu na mjumbe wangu nimekuita mwenye kutawakali). Basi aya hii inamuelezea ambaye atatumwa baada ya Musa (a.s) kutoka kwa wana wa Israel ambao ni ndugu wa wana wa Is’haq. Na aya nyingine kutoka katika Taurati: (Mja wangu mteule si mkali wala mgumu) na mteule ni Mustafa na hili ni jina katika majina ya Mtume (s.a.w). Na kumekuja fasili mbalimbali zinamhusu (Raisi wa ulimwengu) anayebashiriwa kuja kwake baada ya Issa (a.s) ndani ya Injili, kati ya bishara hizo: (Ana fimbo ya chuma ambayo hupigana kwayo na umma wake kadhalika) Fimbo ya chuma yaani ni upanga. Yaani atakuja ambaye ni mtu wa upanga, na umma wake umeamuriwa kupigana jihadi, kama ilivyowasifu Qur’an tukufu mwishoni mwa surat Al-Fathi وَمَثَلُهُمْ فِي الْإِنجِيلِ كَزَرْعٍ أَخْرَجَ شَطْأَهُ فَآزَرَهُ فَاسْتَغْلَظَ فَاسْتَوَى عَلَى سُوقِهِ يُعْجِبُ الزُّرَّاعَ لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ Na kuna aya nyingine nyingi zenye kushabihiana na hii ndani ya Injili. Imekuja katika mlango wa thelathini na tatu kwenye kitabu cha tano cha Taurati aya hii: (Na akasema: Bwana alikuja kutokea Sinai na kutuangazia upande wa Saera utatangaza kutokea mlima wa parani na pamoja naye maelfu ya bendera za watakatifu kuumeni kwake). Aya hii kama inavyoelezea utabiri wa Musa (a.s) juu ya kuja kwa haki kutokea mlima Sinai, inaelezea pia utume wa Issa (a.s) kwa: (Ametuangazia kutokea Saera) na wakati huo huo inatoa habari kwa Utume wa Muhammad (s.a.w) kwa kudhihiri haki kutokea parani ambayo ni milima ya Hijazi kwa maafikiano, kwa hali yoyote ile aya inaelezea Utume wake (s.a.w). Ama (Na pamoja naye maelfu ya watakatifu kuumeni kwake) inasadikisha hukumu ya aya tukufu mwishoni mwa surat Al-Fathi katika ذَلِكَ مَثَلُهُمْ فِي التَّوْرَاةِ ambapo inawasifia masahaba wake (s.a.w) wataharifu watakatifu nao ni mawalii wema. Na aya hii imekuja katika mlango wa arobaini na mbili kutoka kwenye kitabu cha Nabii Isaya: (Mwenyezi Mungu (s.w) atamtuma mteule wake katika zama za mwisho na atamtumia roho mwaminifu amfundishe kisha baada ya hapo atawafundisha watu kama Jibril alivyomfundisha, na atahukumu watu kwa haki, nayo ni nuru itakayowatoa watu katika giza na kuwapeleka kwenye nuru. Mola wangu amenijulisha yatakayotokea hivyo ninawaambieni). Aya hii basi inabainisha waziwazi sifa za Mtume (s.a.w). Katika mlango wa nne kutoka katika kitabu cha Nabii Mikael kuna aya hii ifuatayo: (Mwishoni mwa zama kutakuwapo umma unamuabudu bwana na kukanyaga mlima mtukufu, na watakusanyika huko watu wengi kutoka kila kitongoji wanamuabudu Bwana wala hawamshirikishi na chochote). Aya hii inabainisha (Arafa) na watu wengi ni mahujaji wanaokusudia mlima huo mtakatifu na wanamuabudu Allah, na kwamba umma uliyorehemewa ni umma wa Muhammad, kwani wasifu huu ni alama yao. Na katika mlango wa sabini na mbili katika Zaburi kuna aya hii: (Yeye anamiliki kutoka bahari, hadi bahari na kutoka katika mito hadi upeo wa mbali wa Ardhi, na zitamjia zawadi kutoka Yemen na Algeria, na wafalme watamsujudia na kumtii na atasaliwa kila wakati na kuombewa baraka, na nuru yake itaangaza kutokea Madina, na utajo wake utadumu milele na milele, na kwamba jina lake lipo kabla ya kuumbwa kwa jua, na litabaki jina lake muda wa kubakia kwa jua). Aya hii iko wazi katika kumsifia mtume (s.a.w), na je baada ya Nabii wa Allah Daud amekuja Nabii yeyote asiyekuwa Muhammad (s.a.w) ambaye ameitangaza dini mashariki na magharibi, na wafalme akawafanya kuwa wanampa jizya yeye hali ya kutii, na wafalme masultani wamemfuata kwa mapenzi na unyenyekevu, na kuzawadia swala na dua kila siku kutoka kwa sehemu moja ya tano ya wanadamu wote, na kuchomoza nuru zake kutokea Madina? Je kuna mwingine? Na aya ya ishirini katika mlango wa kumi na nne katika Injili ya Yohana (Iliyofasiriwa kwa Kituruki) ni: (Sitasema nanyi tena sana kwani mkuu wa ulimwengu huu anakuja, na hana kwangu kitu au hana mfano kwangu). Ibara ya mkuu wa ulimwengu ni fahari ya ulimwengu, na hii ni anuani mashuhuri sana kwa bwana wetu mtume (s.a.w). Na aya ya saba katika mlango wa kumi na sita katika Injili ya Yohana: (Lakini nawaambieni kweli kuwa ni heri kwenu niondoke, kwani nisipoondoka hatawajieni msaidizi) je mwenye kusaidia yupo baada ya Issa (a.s) kama si Muhammad (s.a.w). Yeye ndiye anayeongoa watu wote kutoka katika hukumu ya kutoweka na kukosekana kwa milele na kutia furaha, yeye ni bwana wa walimwengu na fahari ya viumbe. Na aya ya nane katika mlango wa kumi na sita katika Injili ya Yohana: Na anapokuja huyo ulimwengu utawajibika juu ya makosa na wema na hukumu (atawalazimisha kuepuka makosa kutenda wema na kufuata hukumu) ambaye atabadili uharibifu wa ulimwengu na kuwa wema, na kuwaokoa watu na madhambi, makosa na shirki, na kubadili misingi ya siasa na utawala duniani, atakuwa nani asiyekuwa Muhammad (s.a.w)?. Na aya ya kumi na moja katika mlango wa kumi na sita kutoka katika injili ya Yohana: (Imefika zama za ujio wa Bwana wa ulimwengu) au (Na kwa habari ya kukaribia kwa bwana wa ulimwengu huu amekaribia) Hapana budi kuwa bwana wa ulimwengu ni bwana wa ulimwengu Muhammad (s.a.w). Na aya ya kumi na tatu kutoka katika mlango wa pili kutoka katika injili ya Yohana: (Atakapokuja huyo roho wa kweli, yeye ndiye atakaye kuongozeni katika kweli yote, kwani yeye hatamki kutokana na nafsi yake, bali anaongea yote ayasikiayo na anakujulisheni mambo yajayo). Basi aya hii iko wazi kuhusiana na Mtume mtukufu (s.a.w), basi ni nani asiyekuwa yeye (s.a.w) ambaye amewalingania watu wake katika haki? Na nani mwingine asiyetamka ila kwa wahyi, na asemaye ayasikiayo kutoka kwa Jibril (a.s)? Na nani asiyekuwa yeye anayeelezea matukio ya kiama na akhera kwa namna ya upambanuzi kabisa? Kisha katika nyaraka za mitume kuna majina ya Mtume (s.a.w) yenye maana ya: (Muhammad), (Ahmad), (Mteule) na (Mustafa), na hayo ni kwa lugha za kisariyani na kiebrania: Katika nyaraka za Shuaibu (a.s), kuna (Mushaffah) na hii ni kwa maana ya (Muhammad) kama ilivyo katika Taurati jina la (Munhamna) na hili ni kwa maana ya jina la (Muhammad). Kama ilivyokuja katika Zaburi (Himyata) na hii kwa maana ya Nabii wa Haram (Maeneo matakatifu ya Makka). Na humo pia kuna (Mteule), na katika Taurati limekuja jina la (Al-Hatim na Al-Khatam), na limekuja neno (Msimamishaji wa sunna) ndani ya vyote Taurati na Zaburi. Na katika Suhufi za Ibrahim na Taurati: (Mazmar) na katika Taurati pia kuna (Ahyad). Na hakika Mtume (s.a.w) amesema: (Jina langu kwenye Qur’an Muhammad na katika Injili Ahmad na katika Taurati ni Uhayid, na hakika nimeitwa kuwa ni Uhyid kwa sababu mimi ninawaepusha Umma wangu na moto wa jahanamu) Na katika majina ya Mtume (s.a.w) ambayo yamepatikana katika Injili (Mwenye gongo na rungu) hapana shaka kwamba yeye ni Nabii mkuu kabisa baina ya manabii kwa jihadi yake na jihadi ya umma wake. Na vile vile: (Mwenye taji) Sifa hii ni mahususi kwake (s.a.w) kwani Umma wa Kiarabu ndio maarufu kwa kilemba na agali kati ya nyumati na taji na kilemba ni kwa maana moja. Basi mwenye taji aliyetajwa katika Injili sio mwingine isipokuwa ni Mtume (s.a.w). Na ndani yake vilevile: Parakalet au Farkalet, na maana yake kama ilivyokuja katika tafsiri ya Injili: Kwamba yeye ni Mtenganishaji kati ya haki na batili, nalo ni jina la Mtume (s.a.w) ambaye anawalingania watu kwenda katika haki. Na hakika Isa (a.s) katika Injili amesema: (Nitaondoka ili aje bwana wa ulimwengu) je asiye kuwa Muhammad yupo aliyekuja baada ya Isa (a.s), na kuongoza ulimwengu na kutenganisha baina ya haki na batili, na kuwaongoza watu katika heri na kutengenea. Yaani hakika ya Isa (a.s) alikuwa anabashiri daima kuwa atakuja mmoja wao baada yangu wala haitabakia haja ya mimi kwani mimi ni kitangulizi chake. Kama inavyoweka wazi hilo Qur’an Tukufu. وَإِذْ قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ إِنِّي رَسُولُ اللَّهِ إِلَيْكُم مُّصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التوْرَاةِ وَمُبَشِّرًا بِرَسُولٍ يَأْتِي مِن بعْدِي اسْمُهُ أَحْمَدُ Naam hakika ya Isa (a.s), aliwabashiria umma wake mara nyingi kwamba atakuja Bwana wa Ulimwengu na mkuu wake na anamtaja kwa majina tofauti kwa kisariyani au kiebrania. Basi wanazuoni wahakiki wanaona kwamba majina haya yanamaanisha: Ahmad, Muhammad Mfarikishaji baina ya haki na batili. Swali: Kwa nini Isa (a.s) alibashiri ujio wa Mtume (s.a.w) mara nyingi zaidi kuliko mwingine katika manabii (a.s) wakati ambapo wengine walitosheka kwa kumwelezea tu? Jibu: Kwa sababu Mtume Mtukufu (s.a.w) alimwokoa Isa (a.s) kutokana na ukadhibishaji wa Wayahudi na kutokana na Uzushi wao mbaya, na ameikoa dini yake kutokana na upotoshaji mbaya sana, ukiachilia mbali kuwa yeye amekuja na sharia yenye msamaha badala ya sharia ile ambayo iliwabinya wana wa Israili ambao hawamwamini Isa (a.s), basi sharia hii angavu ni yenye kujumuisha hukumu ni yenye kukamilisha kilichopungua katika sharia ya Isa (a.s), kutokana na hapa inakuja bishara ya Isa (a.s) kwa Mtume Mtukufu (s.a.w) kwamba atakuja kiongozi wa ulimwengu. Na kama hivi tunaona kuwa Taurati, injili na zaburi na baki ya suhufi za Manabii vimemtilia umuhimu Nabii wa mwisho wa zama na aya nyingi zinakusanya sifa zake, kama tulivyobainisha vielelezo kadhaa katika sifa hizo. Yeye basi ametajwa kwa majina na sifa mbalimbali ndani ya vitabu hivyo. Je yaonekana ni nani atakuwa nabii wa mwisho wa zama ambaye vitabu vyote vya manabii wamemtaja utajo wa bidii kwa kiwango hiki. Katika aya zenye kukaririwa asiyekuwa Muhammad!
Katika Irhasat na dalili za Utume ni: Kuelezea kwa makuhani na mawalii watambuzi wa Allah (s.w) katika kipindi cha (fatrat) (yaani kabla ya Nabii (s.a.w) kupewa Utume) kuhusu kuja kwake (s.a.w) walitangaza kuhusu yeye mbele ya makundi ya watu, na wametuachia habari zao kwenye mashairi yao. Habari hizi ni nyingi sana, hatutaji katika hizo isipokuwa zilizoenea na mashuhuri na zenye kukubalika mbele ya watu wa sira na historia. Ya kwanza: Aliyoona mfalme wa Tubbai - katika wafalme wa Yemen - katika sifa za Mtume (s.a.w) katika vitabu vya zamani, na akaamini. Na akatangaza hilo kwa shairi: شَهِد۟تُ عَلٰى اَح۟مَدَ اَنَّهُ رَسُولٌ مِنَ اللّٰهِ بَارِى النَّسَمِ فَلَو۟ مُدَّ عُم۟رٖى اِلٰى عُم۟رِهٖ لَكُن۟تُ وَزٖيرًا لَهُ وَاب۟نَ عَمٍّ Nimeshuhudia juu ya Ahmad hakika yeye Ni Mjumbe kutoka kwa Allah (s.w) Muumba wa viumbe Ungerefushwa umri wangu hadi kufika umri wake Ningekuwa waziri wake na binamu yake Yaani ningekuwa kwake kama Ali (r.a). Pili: Kutangaza kwa Qis bin Saaidat aliye mashuhuri kwa ufasaha zaidi watoa hutuba wa Kiarabu na mwenye kupwekesha (Anaamini Mungu Mmoja), kuhusu Utume wa Muhammad alitangaza kwa mashairi kabla ya kupewa Utume kwa beti zifuatazo: Ameletwa kwetu Ahmad Nabii bora aliyeletwa. Allah amswaliye muda ambao imesongamana kwake misafara na mahimizo Tatu: Aliyoyasema Kaab Bin Luayy naye ni mmoja wa mababu wa Mtume (s.a.w). Kapewa ilhamu ya ubeti huu kuhusu Utume wa Muhammad: عَلٰى غَف۟لَةٍ يَأ۟تِى النَّبِىُّ مُحَمَّدٌ فَيُخ۟بِرُ اَخ۟بَارًا صَدُوقًا خَبٖيرُهَا Katika hali ya ghafla Nabii Muhammad atakuja Ataeleza habari zenye kusadikisha mjuzi wa habari zake Nne: Aliyoyaona Saifu Bin Dhy Yazni Mmoja wa wafalme wa Yemen katika vitabu vilivyotangulia katika sifa za Mtume (s.a.w) na akamwamini na akawa na shauku naye, na zama alipoenda Babu wa Mtume (s.a.w) huko Yemen pamoja na msafara wa Biashara wa Makuraishi mfalme Saifu Bin Mundhir Bin Dhy Yazin aliwaita na akawaambia: اِذَا وُلِدَ بِتِهَامَةَ وَلَدٌ بَي۟نَ كَت۟فَي۟هِ شَامَةٌ كَانَت۟ لَهُ ال۟اِمَامَةُ وَاِنَّكَ يَا عَب۟دَ ال۟مُطَّلِبِ لَجَدُّهُ Ikiwa atazaliwa katika Tuhama (Yaani: Hijazi) Mtoto kati ya mabega yake kuna doti zuri (Alama ya kupendeza) uongozi utakuwa wake na wewe Abdul Muttalib ni Babu yake. Tano: Ulipoteremka wahyi kwa mara ya kwanza kwa Mtume Mtukufu (s.a.w) imemchukua hofu na woga, Khadija akaenda naye hadi akafika kwa Waraqa Bin Naufal (Binamu wa Khadija) akasema (mama Khadija): Ewe mwana wa Ami sikia kutoka kwa Mwana wa Ndugu yako. Waraqa akamwambia: Ewe mwana wa ndugu yangu Unaona nini? Mtume wa Allah (s.a.w) akamweleza alichokiona. Waraqa akamwambia: Huo ni wahyi ambao Allah (s.a.w) aliuteremsha kwa Musa (a.s) natamani ningekuwa kijana katika wakati huo, laiti ningekuwa hai wakati watu wako watakapo kutoa. Na katika aliyoyasema Waraqa: بَشِّر۟ يَا مُحَمَّدُ اِنّٖى اَش۟هَدُ اَنَّكَ اَن۟تَ النَّبِىُّ ال۟مُن۟تَظَرُ وَبَشَّرَ بِكَ عٖيسٰى Furahi ewe Muhammad mimi nashuhudia kuwa wewe ni Nabii mwenye kungojewa na amekubashiria Isa. Sita: Al-Athakalani Al-Himyary mtambuzi wa Allah alipowaona Makuraishi kabla ya kupewa Utume Mtume (s.a.w) aliwaambia: Je yupo kwenu anayedai Utume? Wakamjibu: Hapana, kisha akauliza swali hilohilo zama za kupewa Utume nabii Muhammad (s.a.w), wakasema: Naam, hakika kati yetu yupo anayedai Utume akasema: Hakika Ulimwengu unamngojea. Saba: Ameeleza mmoja wa wanazuoni wa kinasara naye ni Ibn Al-Ulla kuhusu Mtume (s.a.w) kabla ya kupewa Utume, kisha akaja baada ya kupewa Utume akamwona Mtume (s.a.w) akamwambia: وَالَّذٖى بَعَثَكَ بِال۟حَقِّ لَقَد۟ وَجَد۟تُ صِفَتَكَ فِى ال۟اِن۟جٖيلِ وَبَشَّرَ بِكَ اب۟نُ ال۟بَتُولِ Naapa kwa yule ambaye amekutuma wewe kwa haki hakika nimekuta sifa yako kwenye Injili na amekubashiria wewe mwana wa Al-Batuli (Mwana wa Mariamu). Nane: Amesema A-Najjashy mfalme wa Uhabeshi ambaye yametangulia maelezo yake: لَي۟تَ لٖى خِد۟مَتَهُ بَدَلًا عَن۟ هٰذِهِ السَّل۟طَنَةِ Laiti mimi ningepata kumhudumia badala ya mamlaka haya ya kifalme. Na baada ya tuliyoyaeleza waliyotabiri hawa watambuzi kwa ilhamu kutoka kwa Allah (s.w) kuhusu ujio wa Mtume (s.a.w) tunaeleza waliyoyasema makuhani na kutabiria katika habari za ghaibu kwa kupitia roho na Majini, wameweka wazi ujio wa Mtume (s.a.w) na kutabiria unabii wake nao ni wengi, isipokuwa sisi hatutaeleza ila yale yaliyokuwa katika hukumu ya Mutawatir na yameelezwa katika vitabu vya sira na historia na tunaelekeza visa vyao virefu na kauli zao zilizorefushwa kwenda kurejea katika vitabu vya sira. Basi hapa hatuelezi ila kwa ufupi. Kwanza: Kuhani anayeitwa (Shiqqi) ambaye alikuwa ni ubavu wa mwanadamu mkono mmoja na mguu mmoja na jicho moja. Kuhani huyu ameeleza kuhusu Mtume (s.a.w) mara nyingi hata kauli zake zikafikia kiwango cha tawatur. Pili: Kuhani wa Shamu aliyeitwa (Satiih) ambaye alikuwa ni ajabu katika maajabu kwani alikuwa ni mwili usiokuwa na viungo na hakuna mfupa ndani yake isipokuwa kichwa na uso wake ulikuwa kifuani kwake, na aliishi sana, habari zake za ghaibu za kweli zilikuwa mashuhuri sana hata Kisra mfalme wa Uajemi alipoota njozi ya ajabu iliyomhofisha –zama za mazazi ya Mtume (s.a.w) – katika kupasuka kwa vigorofa kumi na nne vya baraza yake na kuporomoka chini, alimtuma mwanazuoni anayeitwa (Mwezan) akamuulize Satiih kuhusu hekima ya njozi hii, akatuma maneno kwa Kisra yenye maana hii: (Watatawala kwenu wafalme kumi na nne kisha ufalme wenu utafutwa na dola yenu itaondoshwa, na atakuja anayedhihirisha dini mpya, na atakuwa ni sababu ya kutoweka kwa dini yenu na Dola lenu). Na kama hivi alielezea Satiih habari ya wazi juu ya ujio wa Mtume wa aheri ya zama. Hakika ameeleza Sawad Bin Qaarib Al-Duusy na Khanafir na Af’aa wa Najran (Katika wafalme wake), Jadhal bin Jadhal Al-Kindy, Ibn Khulliswah Al-Dusy, Faima Bin An-Nu’man A-Nnajjariyyat na mifano ya hao katika Makuhani mashuhuri wote wameelezea kuhusu ujio wa Nabii wa aheri ya zama na kwamba huyo ni Muhammad (s.a.w) kama vilivyomwelezea vitabu vya sira na historia kwa ufafanuzi. Na kwamba Saad bin bint Kariz naye ni katika jamaa wa karibu wa Uthman (r.a) amepokea kupitia kwa makuhani habari ya Utume wa Muhammad (s.a.w) kutokea ghaibu, akaashiria kuamini kwa Uthman (r.a) mwanzoni mwa kudhihiri kwa Uislamu kwa kusema: Nenda kwa Muhammad na amini, Uthman akaamini na hili alilieleza saad kwa shairi: Allah (s.w) alimwongoza Uthman kwa kauli yangu ambayo Kwayo ni Uongofu wake na Allah anaongoza katika haki. Na Hawatifu pia zimeelezea kama walivyoelezea makuhani kuhusu ujio wa Mtume (s.a.w), na hawatifu ni sauti ya juu ambayo inasikika kutoka kwa asiyeonekana mtu wake. Kati ya hizo: Kusikia kwa Dhiyabu Bin Harith hatifu kutoka kwa jini, na ikawa ni sababu ya kusilimu kwake na kusilimu kwa wengine: We Dhiyabu we Dhiyabu Sikia ajabu ya maajabu Muhammad ametumwa na kitabu Analingania huko Makka wala hapewi jawabu Na kati ya hizo: Kusikia kwa Ibn Qurrat Al-Ghatafany hatifu ikisema: Haki imekuja ikaangaza Na batili imeteketezwa na kuzimika. Ikawa sababu ya kuamini kwa watu. Na kama hivi ubashiri wa makuhani ni mashuhuri na mwingi sana. Zimesikika kutokea matumboni mwa masanamu na machinjo ya masanamu habari ya Ujio wa Mtume (s.a.w) kama zilivyosikika hatifu katoka kwa makuhani. Kati yake: Hakika Sanamu la kabila la Maazin limeelezea kuhusu ujio wa Mtume (s.a.w) pale liliponadi likasema: هٰذَا النَّبِىُّ ال۟مُر۟سَلُ جَاءَ بِال۟حَقِّ ال۟مُن۟زَلِ diyerek risalet-i Ahmediyeyi (asm) haber vermiş. Na kama hivyo hakika sababu ya kusilimu kwa Abbas Bin Mirdasi ni tukio hili mashuhuri: Hakika yake alikuwa na sanamu lilikuwa linaitwa (Dhamar) Siku moja sanamu hilo lilisema: اَو۟دٰى ضِمَارُ وَكَانَ يُع۟بَدُ مُدَّةً قَب۟لَ ال۟بَيَانِ مِنَ النَّبِىِّ مُحَمَّدٍ Mfukie Dhimar na alikuwa akiabudiwa Kabla ya kubainika kwa Nabii Muhammad. Umar (r.a) kabla ya kusilimu kwake alisikia sauti kutoka kwa mbuzi ambaye mtu mmoja alimtoa sadaka achinjwe anasema: Enyi watu wa kichinjwa, ni jambo la kufaulu, mwanamume mwenye fasaha, anasema: لا إله إلاَّ اللهُ. Na kama hivi kuna matukio yenye kufanana na haya mengi mno mithili ya tuliyoyaeleza yamenakiliwa na vitabu vyenye kutegemewa katika sira na historia. Kama kwamba makuhani na watambuzi wa Allah na hatifu hata masanamu wanyama wa kuchinjwa wameeleza kuhusu Utume wa Muhammad (s.a.w), na ikawa kila tukio ni sababu ya kusilimu sehemu ya watu na vilevile baadhi ya mawe na shahidi za makaburi zimeonekana juu yake ibara mwandiko wa zamani (Muhammad ni mtengenezaji mwaminifu) na hakika wameamini kwa sababu hiyo baadhi ya watu. Naam, hakika ya ibara (Muhammad ni mtengenezaji mwaminifu) inamstahikia Mtume (s.a.w) kwa sababu yeye ndiye mwenye kusifika kwa mtengenezaji mwaminifu na kwa kuwa pia hakuwapo kabla ya hapo anayeitwa kwa jina la Muhammad isipokuwa wanaume na hao si wenye kustahiki jina hili.
Ni ishara na matukio ambayo yamedhihiri wakati wa mazazi yake (s.a.w), basi matukio ambayo kudhihiri kwake kunafungamana na mazazi yake na ambayo yamedhihiri kabla ya kupewa kwake Utume yote hayo yanahesabiwa kuwa ni muujiza katika miujiza yake nayo ni mengi sana, isipokuwa sisi hapa tutaeleza mifano mashuhuri waliyoikubali maimamu wa Hadithi. Na imethibiti kwao usahihi wake. Kwanza: Yale aliyoyana mama yake (s.a.w) (Katika nuru ambayo ilitoka pamoja naye wakati wa kuzaliwa kwake) na aliiona mama wa Uthman bin Al-Aas na mama wa Abdulrahman bin Auf ambao walipitisha usiku kwake (Mama Amina) usiku wa kuzaliwa. Hakika walisema: Tuliona nuru wakati wa kuzaliwa iliyotuangazia baina ya mashariki na magharibi. Pili: Kuanguka Mengi ya masanamu yaliyokuwa ndani ya Al-Ka’ba. Tatu: (Kutetemeka kwa baraza ya Kisra na kuanguka kwa vigorofa vyake) kumi na nne. Nne: (Lilididimia Ziwa la Saawah) usiku ule nalo ni lile ambalo lilikuwa likitukuzwa. (Na kuzimika kwa moto wa Uajemi na ulikuwa na miaka elfu moja haukuwa umezimika) ambapo ulikuwa unawashwa kwenye mji wa Istikhar Abadi na wa Majusi wakiuabudu. Basi matukio haya manne hakika hizo ni Ishara kwamba huyo mzaliwa mpya atazuilia ibada ya sanamu na atateketeza ufalme wa Uajemi, na ataharamisha kutukuza ambacho Allah hakukiidhinisha. Tano: Tukio la tembo: Nalo japo kuwa lenyewe sio katika matukio ya usiku ule isipokuwa ni la karibu kutokea na kuzaliwa kwake, kwa hiyo nalo ni katika irhasat vilevile, hakika Qur’an tukufu imelibainisha hilo katika kauli ya Allah (s.w). أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِأَصْحَابِ الْفِيلِ na muhtasari wa kisa chake: Kwamba Abraha mfalme wa Uhabeshi alitaka kuvunja Al-Ka’ba, akampeleka tembo mkubwa mbele ya Jeshi anaitwa tembo yule: (Mahmud). Na zama tembo alipowasili karibu na Makka alipiga magoti na hakusogea kila walivyojitahidi pamoja naye, waliposhindwa walirudi, isipokuwa ndege hawakuwaacha salama wakawarushia mawe kutokana na udongo wa moto na wakawadhakilisha na wakashindwa kushindwa kubaya kabisa. Kisa hiki ni mashuhuri katika vitabu vya historia nacho ni katika alama za Utume wake (s.a.w) ambapo kabila lake na mahali pendwa sana kwake, Al-Ka’bah, kutokana na uharibifu wa Abraha kuokoka kulikofurutu ada. Sita: Allah (s.w) kumfunika kivuli kwenye safari yake na imepokelewa kwamba Halima As-Sa’diyya aliona kiwingu kinamfunika naye akiwa kwake katika utoto wake na amekishuhudia mumewe, akawaeleza watu hilo ikawa tukio maarufu na mashuhuri. (Kama alivyoona kama Bahira alivyokiona kiwingu na akawaonesha watu aliposafiri kwenda Shamu pamoja na Ami yake naye akiwa katika umri wa miaka kumi na mbili katika umri wake). (Na katika mapokezi kwamba Khadija na wanawake wake walikiona alipokuja) (s.a.w) kutoka katika safari yake kutoka Shamu. (Na Malaika wawili wanamfunika kivuli - kama kiwingu - akaeleza hilo kwa Maysara) kijana wa Khadija (Akamweleza kwamba ameona hilo tangu alipotoka naye katika safari yake). Saba: Na imethibiti kwa unakili sahihi (Kwamba aliteremka katika baadhi ya safari zake kabla ya kupewa Utume chini ya mti mkavu pakaota majani pembezoni mwake na ukastawi na ukakuwa) yaani ulikuwa na kuendelea juu (Na yakaja chini matawi yake). Nane: (Kwamba alikuwa akila pamoja na ami yake Abi Twalib na jamaa zake wakati akiwa mdogo walishiba na kukata kiu akiwa hayupo, na wakala katika hali ya kutokuwepo kwake hawakushiba) na hili tukio mashuhuri sahihi. Na amesema Ummu Ayman Mwachwa huru wa Mtume (s.a.w) na mlezi wake: (Sikumwona (s.a.w) kuwa alishitakia njaa wala kiu alipokuwa mdogo wala mkubwa). Tisa: Baraka ambayo ilipatikana katika mbuzi na ngamia wa mnyonyeshaji wake Halima As-Sa’diyya tofauti na watu. Na hili ni tukio mashuhuri na hapana shaka katika usahihi wake. (Na kwamba nzi walikuwa hawatui juu ya mwili wake wala nguo zake) Na hawakuwa wanamuudhi. Na hakika amerithi Sheikh Abdul-Qadir Al-Kaylani (q.s) hili kutoka kwa babu yake Mtume mtukufu (s.a.w), ambapo vilevile nzi hakuwa anatua juu yake. Kumi: Kukithiri kwa kurusha vienge vya mbinguni baada ya ujio wa Mtume (s.a.w) duniani, na hasa usiku wa kuzaliwa kwake. Na hakika tumethibitisha kuteremka kwa vimondo vya mbinguni na kuwapiga Shetani katika (Neno la kumi na tano), na tumebainisha kwamba makusudio katika kuteremka vimondo vya mbinguni ni ishara katika kukata upelelezi wa shetani Majini kunako mbingu na kuwazuia kusikiliza kwa wizi. Maadamu Mtume (s.a.w) amedhihiri kwa wahyi kwa ulimwengu wote kwa hiyo imelazimika kuzuiliwa kauli za makuhani na anayeongea katika ghaibu katika kauli za Majini yenye kuchanganywa na uongo na kinyume na uhalisia ili usichanganyike wahyi na kitu kingine na kusiweko na utata wowote katika jambo la wahyi. Makuhani walikuwa wengi mno kabla ya Utume, lakini baada ya kuteremka Qur’an tukufu walizuiliwa kabisa, na hata walio wengi kati yao waliamini, kwa sababu hawakuwapata wa kuwaeleza katika Majini ili wawatabirie katika habari za ghaibu. Hivyo Qur’an tukufu ikawazuilia njia. na ilidhihiri aina ya ukuhani uliotangulia katika Ulaya wakati huu kwa wakaa kati ambao wanataka kuhudhurisha roho, na kwa hali zote. Hitimisho: Yamedhihiri matukio mengi na watu wengi kwa ajili ya kuunga mkono Utume wa Muhammad kabla ya kupewa kwake Utume. Naam, hakika ya ambaye atakuwa Bwana wa ulimwengu kimaana, na ambaye atabadilisha sura za ulimwengu za kimaanawy, na ambaye atabadilisha dunia kuwa ni shamba la Akhera, na ambaye atatangaza kuwa juu kwa cheo cha viumbe na thamani yake, na ambaye atawaongoza Majini na watu katika uongofu na njia ya furaha, na kuwaokoa - nao wametoweka - kutoka katika kukosekana kwa hali zote, na ambaye atafumbua hekima ya kuumbwa na fumbo linaloufanya ulimwengu kutahayari, na ambaye atajua na kujulisha makusudio ya Bwana Mlezi wa walimwengu, na ambaye atatambua na atatambulisha Muumba huyo Mtukufu, hakika mwanadamu kama huyu hapana budi kuwa kila kitu, kila aina, na kila kundi la viumbe, ni lenye kuwa na shauku na ujio wake na kuutazamia kwa hamu kubwa, na kujiandaa kusherehekea kwa ujio wake mtukufu, bali watawabashiria wengine kwa kuja kwake - ikiwa Muumba wake atajulisha hilo – kama tulivyoona usadikisho wa hilo katika Ishara na mifano iliyotangulia kwamba kila aina katika aina za viumbe imedhihirisha miujiza yake kwa kinachoshabihiana na kumkaribisha, na kana kwamba inasema kwa ulimi wa muujiza: Wewe ni mkweli katika madai yako.
Hakika Muujiza mkubwa kabisa wa Mtume (s.a.w) baada ya Qur’an tukufu ni dhati yake yenye baraka, yaani vilivyokusanyika kwake (s.a.w) katika tabia njema na matendo bora, hakika wameafikiana maadui na marafiki juu ya kwamba yeye ni mwenye heshima ya juu sana kuliko watu wote na mwenye nafasi tukufu sana na mkamilifu wao kwa mazuri. Hata bingwa wa ushujaa imamu Ali (r.a) anasema: (Hakika tulikuwa balaa limepamba moto – na inapokelewa kuwa kushitadi kwa balaa - na jicho kuwa jekundu tukijikinga kwa Mtume (s.a.w)). Na kama hivi Mtume (s.a.w) alikuwa katika kilele ambacho hapandi huko yeyote mwingine asiyekuwa yeye katika kila tabia njema kama ilivyo katika ushujaa. Tunaelekeza muujiza huu mkubwa katika kitabu (As-Shifaa fi Huquuq Al-Musatafa) cha Al-Qadhy Iyadh Al-Maghriby, na hakika amefanya vema katika kitabu hicho na katika kubainisha ubainifu mzuri kabisa, na kuuthibitisha kwa upambanuzi mzuri sana. Kisha hakika sharia angavu ambayo haikuja na haitakuja mithili yake ni muujiza mwingine wa Mtume Mtukufu (s.a.w) hadi wameafikiana maadui na marafiki juu ya hilo. Tunaelekeza ufafanuzi wa muujiza huu katika yote tuliyoyaandika katika (Maneno) thelathini na tatu, (Maandiko) thelathini na tatu, (Minga’o) thelathini na moja na (Miale) kumi na tatu. Kisha muujiza mkubwa, muujiza huo ni muujiza wa (kupasuka kwa Mwezi) ambao umepokewa mapokezi ya tawatur na umethibiti uthibiti wa kukinaisha utata wowote hauukaribii. Hakika imepokelewa kwa njia nyingi na kwa sura ya Mutawatir kutoka kwa: Ibn Masu’d, Ibn Abbas, Ibn Umar, Imamu Ali, Anas na Hudhayfa, na mifano ya hao ni mingi katika masahaba wengi watukufu (r.a), ukiachilia mbali kuunga mkono kwa Qur’an tukufu na kuutangaza muujiza huo. اقْتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانشَقَّ الْقَمَرُ Makafiri wa kikuraishi hawakujitahidi na hali ya kuwa wao ni watu wa upinzani na ukaidi - kukanusha muujiza huu, lakini walisema: Hakika huo ni (Uchawi). Yaani kupasuka kwa mwezi ni jambo thabiti limekatwa hakika yake hata kwa upande wa makafiri wenyewe isipokuwa wao wamelifanyia taawili tukio hilo kuwa ni uchawi. Tunaelekeza katika kupasuka mwezi ambalo ni nyongeza ya Risala ya Miiraji. Kisha hakika Mtume mkarimu (s.a.w) amedhihirisha muujiza mkubwa muujiza wa (Miiraji) kwa wakazi wa mbinguni kama alivyodhihirisha kwa wakazi wa Ardhini muujiza wa (kupasuka kwa mwezi). Basi tunaelekeza kwenye Risala ya Miiraji nayo ni neno la (Thelathini na Moja), ambalo limethibitisha ukweli wa muujiza huo na kuudhihirisha kwa uwazi, isipokuwa sisi hapa tutataja ambayo ni utangulizi wa muujiza huo nayo ni safari yake kwenda Baytul Maqdis, na Makuraishi kumtaka aelezee wasifu wa Baytul maqdis asubuhi ya Miiraji, na vilevile miujiza iliyotokea katika safari hii. Basi wakati Mtume Mtukufu alipoeleza asubuhi ya usiku wa Miiraji kuhusu safari yake, Makuraishi walimkadhibisha na walisema: Ukiwa kweli umekwenda Baytul Maqdis basi tusifie Milango yake na kuta zake na hali zake. فَكَرَب۟تُ كَر۟بًا لَم۟ اَك۟رُب۟ مِث۟لَهُ قَطُّ فَجَلَّى اللّٰهُ لٖى بَي۟تَ ال۟مَق۟دِسِ وَكَشَفَ ال۟حُجُبَ بَي۟نٖى وَبَي۟نَهُ حَتّٰى رَاَي۟تُهُ فَنَعَتُّهُ وَ اَنَا اَن۟ظُرُ اِلَي۟هِ Mtume Mtukufu (s.a.w) alisema: (Nikapata shida sijapata shida mfano wake kabla yake katu, Allah akaninyanyulia nikawa ninaitazama) yaani ilinyanyuliwa Baytul Maqdis kwa ajili yake na akaanza kuielezea huku akiiangalia, Makuraishi wakawa na yakini na habari ile (na wakasema: Lini utakuja) yaani msafara ambao aliuona Mtume (s.a.w) njiani, (Akasema: Siku ya Jumatano. Ilipokuwa siku hiyo walijitokeza Makuraishi wanangojea na mchana umeshageuka, na msafara haujafika: Mtume wa Allah (s.a.w) akaomba, akazidishiwa saa moja katika mchana na jua likazuiliwa). Basi unaona kuwa Ardhi inaacha jukumu lake kwa saa moja ya mchana ili kusadikisha habari yake (s.a.w), na jua kubwa linashuhudia ukweli wake, Je yaonekana ubaya ulioje kwa yule ambae hasadiki maneno ya Mtume huyu Mtukufu (s.a.w) ambaye Ardhi iliacha jukumu lake na jua lilijizuilia kwa ajili ya kusadiki maneno yake. Na kufaulu kulioje kwa wale ambao wamepata utukufu wa kutekeleza amri zake (s.a.w) na wakasema: Tumesikia na tumetii. Zingatia hili na useme: الحمد لله على الإيمان والإسلام
Hakika muujiza mkubwa katika miujiza ya Mtume Mtukufu (s.a.w) ni Qur’an Tukufu, ambayo inakusanya mamia ya dalili za Utume, na imethibiti kuwa kwake muujiza kwa pande arobaini kama katika (Neno la ishirini na tano), kwa hiyo tutaelekeza ufafanuzi wa hazina hii kubwa ya miujiza kwenda katika neno hilo, na hapa tunatosheka na kabainisha nukta tatu tu.
Swali: Ikisemwa hakika siri ya Qur’an tukufu kuwa ni muujiza hakika ipo katika balagha yake ya hali ya juu, wakati ambapo hawapandi isipokuwa mmoja katika elfu katika wanazuoni wakubwa wa balagha katika kutambua siri hii, pamoja na ilikuwa inatakiwa kuwa kwa kila tabaka katika matabaka ya watu kuwa na sehemu yake katika hali hii ya muujiza.? Jibu: Hakika Qur’an tukufu ina hali ya muujiza kwa kila tabaka katika matabaka ya watu, isipoukwa ni kwamba utatambulika huu muujiza wake kwa mtindo maalum. Mathalani: Inabainisha hali yake ya muujiza iliyo wazi katika balagha (kwa watu wa balagha na fasaha). Na mathalani: Kati ya mtindo wake wa hali ya juu mzuri wa kipekee (Kwa watu wa mashairi na fani ya hotuba). Mtindo huu pamoja na kuwa kila tabaka linapendezwa nao katika watu isipokuwa yeyote yule hathubutu kuuiga, hauchushi wingi wa kurudia rudia na wala haichakazi kupita kwa zama, ni njia safi mpya inahifadhi ujana wake na ustawi wake daima, ni njia inabeba kutoka katika nathari iliyotungwa na utungo uliowekwa nathari jambo linaloifanya kuwa ya hali ya juu na yenye ladha wakati huo huo. Kisha inabainisha hali yake ya muujiza katika inayoyaeleza katika habari za muujiza kuhusu ghaibu inawapa changamoto kwa habari hiyo tabaka la makuhani (Na ambao wanadai kuwa wao wanapasha habari mambo yanayohusu ghaibu). Kisha inasimulia (Watu wa historia) na ambao wanafuatilia matukio ya ulimwengu katika wanazuoni yale yanayowatambulisha muujiza wake, na hiyo ni kwa kuelezea kwake kuhusu mataifa yaliyopita zamani na hali zao, na matukio yatakayotokea katika mustakabali, sawa katika uhai wa kidunia au katika barzakh au katika akhera, inawapa changamoto kwa hii hali yake ya muujiza ya kupendeza. Na vilevile inaonesha hali yake ya muujiza inawaonesha (Wanazuoni wa mambo ya jamii siasa na utawala) na hii kwa kudhihirisha yaliyomo katika kanuni za Qur’an zilizo takatifu miongoni mwa hali ya Muujiza, naam! Hakika ya sharia angavu inayochomoza kutoka katika Qur’an tukufu inadhihirisha udhihirisho uliyotimia siri ya hali hiyo ya Muujiza. Na inabainisha vilevile kwa wale ambao wamezama katika (Maarifa ya elimu za kiungu na hakika za kiulimwengu) hali ya kimuujiza iliyo wazi katika kuelezea kwake hakika za kiungu za hadhi ya juu takatifu, au kuwatambulisha kwa kuwepo kwa hali hii ya muujiza. Na kwa wale ambao wanapita (Njia za Uwalii na tasaufi) Qur’an tukufu inabainisha hali yake ya muujiza kwa hazina za siri zilizomo kwenye bahari ya aya zake zilizosheheni. Na kama hivi mbele ya kila tabaka katika matabaka arobaini ya watu linafunguliwa dirisha lenye kuangalia katika hali ya muujiza iliyo dhahiri. Bali inabainisha hali yake ya kuwa ni muujiza hata kwa wale ambao hawamiliki isipokuwa uwezo wa kusikiliza bila ya kuweza kuzama katika ufahamu katika (Watu wa kawaida). Basi tunawaona wanasadikisha kuwa kwake ni muujiza na wanatambua kwa kusikiliza tu, wakati yule mtu wa kawaida anazungumza na nafsi yake na anasema: (Hakika mtindo wa hii Qur’an inatofautiana kabisa na mitindo ya vitabu vingine, basi ima imo katika kiwango ambacho ni cha chini kuliko vitabu hivyo na hili ni Muhali - bali hajalitamka hilo adui mkubwa na mwenye uhasama - au ni mtindo ulio juu kuliko yote, yaani hakika ni muujiza). Basi mtu wa kawaida hawezi isipokuwa kusikiliza, anafahamu hali ya muujiza kwa muundo huu, na ili tumsaidie jambo katika utambuzi wake huu tunafafanua yafuatayo: Qur’an tukufu imeamsha hisia kwa watu tangu awali ilipodhihiri katika medani ya changamoto imeamsha matakwa mawili makubwa: Kwanza: Matakwa ya kuiga kwa wapenzi wake, yaani mapenzi yao makubwa ya kujifananisha na mtindo wake wa hali ya juu, wakawa na shauku ya kufanana mitindo yao na hiyo Qur’an. Pili: Matakwa ya kupinga na kukosoa ambako kumezaliwa mbele ya maadui na mahasimu, yaani kuleta mtindo mithili yake ili kuvunja madai ya kuwa muujiza. Basi matakwa haya mawili makubwa yamesababisha kutokea kwa mamilioni ya vitabu vya Kiarabu vilivyopo mbele yetu, lakini kama tungelinganisha vya fasaha zaidi katika vitabu hivi na Qur’an tukufu, yaani kama tungevisoma kwa pamoja kila msikiaji angesema bila ya kusita, hakika ya Qur’an haifanani na mtindo wowote katika mitindo hii, hivyo hiyo Qur’an sio kiwango cha vitabu hivyo, basi ima ni yenye mtindo wa chini zaidi kuliko vyote, na hili ni muhali pasipo na chembe ya shaka, na hajalitamka hilo yeyote katu bali hata shetani anashindwa kutamka hilo, kwa hiyo ikathibiti kwamba mtindo wa Qur’an tukufu ni juu ya mitindo yote na hii ni kwa sababu ya muujiza wake wa kupendeza. Bali hakika mtu wa kawaida mjinga ambaye hafahamu kitu katika maana za Qur’an tukufu anatambua hali ya muujiza wa Qur’an kutokana na kutokuchosha kwake katika kuisoma. Anazungumza mtu huyo wa kawaida mjinga kwa kusema: Hakika kuendelea kuisoma hii Qur’an hakuzalishi uchovu katu, bali wingi wa kuisoma unazidisha utamu, wakati ambapo lau ningesikiliza kasida nzuri za kupendeza kwa mara nyingi hakika ninahisi uchovu, kwa hiyo Qur’an sio maneno ya mwanadamu bila ya shaka. Kisha hakika ya (Watoto) ambao wanataka kuhifadhi Qur’an tukufu, inadhihirisha muujiza wake katika uwezo wao katika kuhifadhi kwao katika akili zao nyororo ndogo, pamoja na kuwepo kwa maeneo yenye kurandana yanayowachanganya, utawaona wanahifadhi Qur’an kwa wepesi wote wakati ambapo wanashindwa kuhifadhi ukurasa mmoja wa kitabu kingine. Bali hata (wagonjwa na wenye kukata roho) katika sakarati al-Mauti katika wanaopata maumivu kwa maneno madogo mno, utawaona wanasikiliza Qur’an tukufu na aya zake zinateremka kwenye masikio yao kana kwamba ni maji matamu ya salsabil, na kwa hiyo wanatambua kuwa kwake ni Muujiza. Kutokana na yaliyo tangulia tunapata: Hakika Qur’an tukufu haimwachi hata mmoja akiwa amenyimwa kuonja hali ya kuwa kwake ni Muujiza, basi kila tabaka katika matabaka arobaini katika matabaka mbali mbali ya watu wana sehemu yao katika muujiza huu au Qur’an inawatambulisha hali yake ya kuwa ni muujiza, hata kwamba inabainisha aina ya muujiza wake kwa wale ambao hawana fungu katika elimu na hawamiliki (Isipokuwa kuona) bila ya uwezo wa kusikiliza au kufahamu au utambuzi wa kimoyo na hilo ni kama ifuatavyo: Hakika ya maneno ya msahafu uliochapwa kwa hati ya (Al-Hafidh Uthman) yanakabiliana na kutazamana. Mathalani: Hakika ya neno وَثَامِنهُمْ كَلْبهُمْ ambalo limo katika Surat Al-Kahf linatazama neno قِطْمِيرٍ ambalo limo katika surat Al-Fatir kama zitatobolewa kurasa kwa kuanzia katika neno la kwanza lingebainika neno la pili kwa kupinda kidogo na lingefahamika jina la mbwa. Na vivyo hivyo neno مُحْضَرُوْنَ ambalo limekaririwa mara mbili katika surat (Yasin) tunaliona moja wapo juu ya lingine. Nayo yanakabiliana na neno مُحْضَرُوْنَ ,﴿مُحْضَرُوْنَ ambalo limo katika surat As-Saaffat, basi ikitobolewa mojawapo yangedhihiri kupita kurasa neno hilo hilo pamoja na kupinda kidogo. Na vivyo hivyo neno مَثْنىَ ambalo limo katika surat As-Sabaa linaangalia neno hilo hilo ambalo limo mwanzoni mwa surat al-Fatir, basi katika Qur’an linajikariri neno مَثْنىَ mara tatu, na yanatazamana mawili kati yake sio hali ya sadifa kamwe. Na aina hii ya kutazamana na kukabiliana ina mifano mingi mno katika msahafu mtukufu hata kwamba neno moja linakariri katika sehemu zinazokaribia sita, kama zitaunganishwa kati yake kwa tundu mengine yangeonekana kwa kupinda kidogo. Hakika nimeshuhudia msahafu umeandikwa sentensi zenye kutazamana katika kurasa zake zote kwa hati nyekundu, wakati huo nikasema: (Maeneo haya hakika ni alama ya aina ya hali ya muujiza ya Qur’an), kisha baada ya hapo nikawa natazama sentensi za Qur’an tukufu nikaona kwamba nyingi kati ya hizo zinatazamana kupitia kurasa kutazamana kunakohusiana na maana madhubuti. Na ilivyokuwa mpangilio wa Qur’an iliyoenea ni yakusimamia kwa mujibu wa maelekezo kutoka kwa Mtume (s.a.w), na wameiandika waandishi wenye kupewa ilhamu, hakika katika nakshi yake ya kupendeza na katika hati yake nzuri kuna ishara ya aina ya muujiza, na hii kwa sababu hali hii haiwezekani kuwa ni sadifa wala haitokani na kufikiria kwa mwanadamu. Na kama sio kasoro za chapa maneno yenye kutazamana yangeambatana kwa kuwa katika tabaka kamili. Kisha hakika tunaona katika sura zilizoteremka Madina ndefu na za kati na kati kuna kukariri kwa ajabu katika mpangilio wa tamko tukufu (Allah), kwa ghalibu linakariri kwa idadi maalum, ima tano, sita, saba, nane, tisa au mara kumi na moja, ukiachilia mbali kwamba uwiano wa kiidadi ulio mzuri unabainisha juu ya pande mbili za karatasi ya msahafu zinazokabiliana.
Uchawi ulikuwa umeenea katika zama za nabii Musa (a.s), miujiza yake Mikubwa ikaja kwa namna inayo inayoshabihiana na uchawi, na tiba ilikuwa imeenea katika zama za nabii Isa (a.s) basi gbalibu ya miujiza yake ikaenda katika jinsi hii. Kama ilivyokuwa kuna vitu vinne vilivyoenea katika Bara Arabu zama za kupewa Utume Mtume (s.a.w): Kwanza: Balagha na fasaha. Pili: Ushairi na fani ya hotuba. Tatu: Ukuhani na kutabiri mambo ya ghaibu Nne: Utambuzi wa matukio yaliyopita na matukio ya kiulimwengu. Qur’an ikaja ikiwa inawapa changamoto mabwana wa maarifa haya manne. Wakaja watu wa balagha na wenye fasaha kwanza wakiwa wamehemewa mbele ya balagha yake ya kimuujiza wakiisikiliza kwa tahayuri na kupendezwa mno. Na wakawa washairi na wahutubu katika kuchanganyikiwa kutokana na jambo lao, hata ikawa kwamba imeshusha hadhi ya waliyokuwa wakijitukuza nayo katika (Al-Muallaqat as-Sab’u) mashairi bora ya Waarabu yaliyotundikwa juu ya Al-Kaaba ambayo yanawakilisha vielelezo bora zaidi vya ushairi wao, bali waliyaandika kwa maji ya dhahabu na kuyaangika juu ya ukuta wa Al-Ka’ba. Na ikawaondoshea Makuhani na wachawi uoni wao wa kusibu na kuwasahaulisha waliyokuwa wakiyazungumzia katika habari za ghaibu, ambapo majini wao walifukuzwa na kuteremshwa pazia juu ya makuhani na kuzuiliwa milango yao hadi milele. Na ikawaokoa wasomi wa historia ya mataifa yaliyotangulia na matukio ya ulimwengu kutokana na yaliyozuka juu yake katika upotofu usingiziaji na habari za uongo, na kuwaelekeza katika matukio ya wakati uliopita na matukio halisi ya ulimwengu ambayo yanaangaza nuru. Na kama hivi matabaka haya manne yamepiga magoti mbele ya adhama ya Qur’an tukufu, na kutahayari na kutukuza kunawafunika, wakaanza kujifunza kwake, na kupokea mwongozo na maelekezo kutoka kwake, haikutokea katu kuweza yeyote kati ya hawa kwa kuipinga Qur’an kwa hali yoyote vyovyote itakavyo kuwa, japo kwa sura moja. Na ikisemwa: Vipi tutajua kwamba hakutokea yeyote katika medani ya upingaji, na hakuweza yeyote kuleta mithili ya Qur’an, na vipi tutajua kuleta mlingano kwenyewe kwa dhati yake ni jambo la muhali? Jibu: Ingekuwa upingaji unayumkinika, basi hakuna namna wangekuwa wanajitahidi hilo. Na asingefanya ajizi yeyote katika jambo hili, kwani haja ya kupinga ilikuwa kubwa, na hii ili kuokoka na hatari ya changamoto ili kuokoa dini yao mali nafsi na watu wao, kwa hiyo ingekuwa upingaji unayumkinika asingesita yeyote kufanya hivyo abadani, na makafiri na wanafiki - nao ndiyo walio wengi - wangekuwa wanaeneza habari yake kati ya watu, bali wangeieneza katika pande zote kama walivyokuwa wakieneza yanayodhuru Uislamu, kwa uadui. Kisha wangekuwa wameeneza hayo - ambapo kupinga kungekuwa kunayumkinika - wana historia wangekuwa wanayasajili hayo katika vitabu vyao vingi. Lakini Historia hii hapa na vitabu vyake vyote viko mbele yetu, hatuoni humo chochote katika kupinga Qur’an isipokuwa vifungu alivyosingizia Musailamat al-kadh’dhaab (Musalilama jiongo). Hali ya kujua kwamba Qur’an tukufu imewapa changamoto muda wa miaka ishirini na tatu na kugonga masikio yao kwa aya zake za miujiza, na kwa mtindo huu wa kuleta changamoto: Hii hapa Qur’an tukufu mbele yenu, basi leteni mithili yake kutoka kwa (Ummiyyu) (asiyejua kusoma na kuandika) kama Muhammad Mwaminifu! Ikiwa nyinyi ni wenye kushindwa na hili basi na awe mtu huyo (Mwanazuoni) mkubwa, na sio asiyejua kusoma! Ikiwa nyinyi hamuwezi hili vilevile, basi leteni mithili yake (Mkiwa mmekusanyika) na sio kutokana na mtu mmoja! Na walikusanyikie hilo wanazuoni wenu na wanafasihi wenu, na wasaidiane wao kwa wao, bali waiteni mashahidi wenu asiyekuwa Allah, na walete mithili yake. Na mkishindwa yote haya, basi leteni (Vitabu vilivyotangulia) vyenye ufasaha vyote na mtafute msaada kwa vitabu hivyo katika kupinga, bali waiteni (Vizazi) vijavyo vilevile! Na ikiwa mmeshindwa vilevile, basi na iwe hiyo mithili ni kwa (Sura kumi) tu, na sio lazima kuwa Qur’an yote. Na mkiwa mmeshindwa vilevile basi na yawe maneno yenye balagha mfano wa balagha ya Qur’an japo ikiwa kutokana na (Hikaya za kuzuliwa). Na ikiwa mmeshindwa vilevile basi leteni sura moja na iwe sura fupi. Na ikiwa mmeshindwa vilevile: Basi dini zenu na nafsi zenu kwa hiyo zinatishiwa duniani sawa na zinavyotishiwa akhera. Na kama hivyo Qur’an imetoa changamoto nane kuzipa tabaka za watu na majini, na haikuhusisha changamoto yake ndani ya miaka Ishirini na tatu tu bali imeendelea hadi miaka elfu na mia tatu bali haijaacha kuwa inachagiza Ulimwengu na itabaki kama hivi mpaka Allah atakapo irithi Ardhi na vilivyomo. Na kwa ajili hii ingekuwa upingaji unayumkinika wale makafiri wasingechagua njia ya vita na udamiri na kuziweka nafsi zao na mali zao na watu wao katika maangamizo wakiacha njia ya kupinga iliyo fupi nyepesi. Kwa hiyo upingaji hauyumkiniki na haupo katika uwezo wa wanadamu. Kwani je inayumkinika kwa mwenye akili mtambuzi - kuiweka kwenye hatari nafsi yake mali yake na watu wake na kuchagua njia ya vita na udamiri ikiwa ni katika uwezo wake kupita njia ya upingaji japo kwa sura moja katika Qur’an kutokana na mwanafasihi miongoni mwao, akaiokoa nafsi yake na mali yake kutokana na chagizo la Qur’an, ikiwa kuleta mithili yake ni rahisi? Hitimisho: Aliyosema (Al-Jahidhu): Ilipokuwa haiyumkiniki kupinga kwa herufi wakachagua kupambana kwa panga. Ikisemwa: Hakika wamesema baadhi ya wanazuoni wahakiki: (Haiwezekani kuipinga aya yoyote katika aya za Qur’an tukufu wala kifungu katika aya wala neno katika aya, basi vipi sura? Na hakujitokeza yeyote katika medani ya kupinga. Yaani kwa hiyo Qur’an haikupingwa). Na tunaona katika maneno haya kuna kutia chuku ambako akili haikukubali, kwa sababu kuna sentensi nyingi katika maneno ya wanadamu zinashabihiana na sentensi za Qur’an na ibara zake. Kwa hiyo basi nini maana ya kauli hii, na nini hekima yake? Jibu: Kuna madhehebu mawili katika kubainisha hali ya muujiza wa Qur’an: Madhehebu ya kwanza: Ndiyo ghalibu na yenye uzito nayo ni madhehebu ya walio wengi katika wanazuoni nayo ni kwamba balagha nyororo ya Qur’an na sifa pekee za maana yake ziko juu ya uwezo wa Wanadamu. Ama madhehebu ya pili: Na ambayo imezidiwa uzito kwamba kuipinga sura moja ya Qur’an kuko ndani ya uwezo wa wanadamu, isipokuwa hakika Allah (s.w) amezuia hilo kwa viumbe, ili Qur’an ipate kuwa ni muujiza wa Mtume (s.a.w), na hili linaweza kufafanuliwa kwa mfano: Hakika kusimama kwa mwanadamu na kukaa kwake ndani ya uwezo, basi ikiwa Nabii mtukufu atamwambia Mtu: Hutaweza kusimama, ili kudhihirisha muujiza, na ikawa hakuweza yule mtu kusimama kweli, basi hapo muujiza umetokea. Madhehebu haya yaliyozidiwa uzito: Madhehebu ya kugeuza. Yaani Allah (s.w) ndiye ambaye amegeuza majini na watu wawe mbali na uwezo wa kupinga, basi kama asingewageuza Allah (s.w) na kuwaweka mbali na kuleta mithili yake majini na watu ingekuwa ni katika uwezo wao kuleta mithili yake. Na kama hivi basi wanazuoni ambao wanasema kwa mujibu wa madhehebu haya: (Haiwezekani kuipinga Qur’an hata kwa neno moja) ni maneno ya haki hayana ubishi ndani yake, kwa sababu Allah (s.w) amewazuilia hilo kwa ajili ya kudhihirisha muujiza, kwa hiyo hawataweza kutamka kitu cha kupinga, na lau watataka kusema kitu chochote cha kupinga hawataweza pasi na kutaka kwa Allah (s.w). Ama kwa mnasaba wa madhehebu ya kwanza nayo ni yenye uzito na ambayo wameridhia wengi wa wanazuoni, basi wao katika hili wana sura madhubuti: Hakika ya maneno ya Qur’an tukufu na sentensi zake zinatazamana baadhi yao kwa baadhi nyingine, kwa hiyo zinaelekeana na kutazamana maneno na sentensi, yaweza likawa neno moja linaelekea katika maeneo kumi, na hapo utakuta ndani yake kuna nukta kumi za kibalagha, na alama kumi zinazofungamanisha na maneno mengine, na hakika tumeeleza mahusiano haya katika tafsiri yetu (Isharaatul Al-I’jazi fi madhani Al-I’jaz) sawa katika surat Al-Fatiha au katika utangulizi wa Surat Al-Baqara: الم ٭ ذَلِكَ الْكِتَابُ لاَ رَيْبَ فِيهِ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ Na tufafanue hilo kwa mifano: Lau kama tutaleta taswira ya kasri kubwa, kuta zake zimetiwa nakshi wa nakshi za ajabu, zimepambwa kwa marembo ya kupendeza hakika kuweka jiwe kunachukua fundo la msingi la mapambo hayo na nakshi katika mahali pake panapostahiki - ambapo linafungamana pamoja nayo yote na kuangalia yote kwa pamoja - inahitaji maarifa kamili ya nakshi hizo zote na mapambo hayo ambayo yanajaza kuta za kasri. Na mfano mwingine, tunachukua kutoka katika mwili wa mwanadamu: Kuweka mboni ya jicho la mwanadamu mahali pake panapo faa kunategemea uhusiano wa jicho na mwili wote na kujua kiasi cha uhusiano wa mafungamano ya mboni ya jicho na kila sehemu katika sehemu za mwili na kazi yake. Basi pimia kwa mifano hii miwili ili ujue namna waliotangulia katika watu wa hakika walivyobainisha yaliyomo katika maneno ya Qur’an miongoni mwa sura nyingi na mahusiano mishikamano na mafungamano ambayo yanayafunga pamoja na sentensi zake nyingine na aya zake. Na hasa wanazuoni wa elimu ya herufi za Qur’an, hakika wamezama sana katika maudhi hii, na wamethibitisha kwa dalili: Hakika katika kila herufi katika Qur’an tukufu ina siri madhubuti zinatosha kurasa tisa kamili za kubainisha na kuweka wazi. Naam, maadam Qur’an tukufu ni maneno ya Bwana Mlezi wa walimwengu na Muumba wa kila kitu, basi kila neno katika maneno yake kwa hiyo ni sawa na kokwa, ambayo kutokana na kokwa hiyo inaweza huota mti wa kimaanawy katika siri na maana, au ni sawa na moyo ambao huuzunguka maana na siri (nyingi) zilizofanyika mwili. Kwa ajili hiyo tunasema: Naam, hakika katika maneno ya watu kuna yanayoshabihiana na maneno ya Qur’an na sentensi zake na aya zake, isipokuwa hakika ya aya hiyo tukufu au neno na sentensi ya Qur’an vimewekwa mahali pake panapofaa kwake kwa kiasi katika kuwekwa kwake yamechungwa mengi sana miongoni mwa mafungamano na mahusiano katika mambo ambayo yanalazimu ujuzi unaozungukia kiujumla kila eneo ili kuyaweka katika mahali hapo panapofaa.
Hakika ya Allah (s.w) ameneemesha juu yangu siku moja kutafakari kihakika kuhusu muhtasari wa ainisho la Qur’an yenye wingi wa hekima basi naandika tafakuri hiyo kama ilivyokuja katika moyo kwa lugha ya Kiarabu kisha nitaleta maana yake. Ametakasika ambaye imeshuhudia juu ya upweke wake na kuweka wazi kwa sifa za uzuri na ukamilifu wake Qur’an yenye wingi wa hekima ambayo pande zake sita zina nuru yenye kubeba siri ya ijmai ya vitabu vyote vya manabii na mawalii na wenye kupwekesha waliyotofautiana katika enzi, masharibu na masalaki, wenye kuafikiana kwa nyoyo zao na kauli zao juu ya kusadikisha mambo ya msingi ya Qur’an na mambo ya mikusanyiko ya hukumu zake kwa sura ya kiujumla, nayo ni wahyi mtupu kwa ijmai ya Mteremshaji, kilichoteremshwa na aliyeteremshiwa, na ni dhati ya uongozi kwa uwazi na madini ya nuru za imani kwa dharura na mkusanyiko wa hakika kwa yakini na mfikishaji katika furaha kwa kuonekana dhahiri na yenye matunda yenye kukamilika kwa kushuhudiwa na yenye kukubaliwa na Malaika, watu na majini kwa makisio ya kweli kutokana na mitengano za alama na yenye kuungwa mkono kwa dalili za kiakili kwa maafikiano ya wenye akili waliokamilika na yenye kusadikishwa kutokana na upande wa kimaumbile ulio salama kwa ushahidi wa kutulia kwa moyo wa ndani na muujiza wa milele wenye kubaki sura ya hali ya muujiza wake kwa mapito ya zama kwa kushuhudiwa na yenye kukunjuka duara la uongozi wake kutoka katika hadhara ya juu hadi katika afisi ya watoto wanafaidika kutoka katika dhati ya somo la Malaika pamoja na watoto na vivyo hivyo hiyo ni yenye jicho la hali zote linaona vitu kwa ukamilifu wa uwazi na kudhihiri na kuzungukia na kugeuza ulimwengu mkononi mwake na kuutambulisha kwetu kama anavyogeuza fundi saa kiganjani kwake na kuwajulisha watu. Basi Qur’an hii yenye utukufu wa hadhi ndiyo ambayo inasema kwa kukariri لَٓا اِلٰهَ اِلَّا هُوَ فَاع۟لَم۟ اَنَّهُ لَٓا اِلٰهَ اِلَّا اللّٰهُ Ama maana ya tafakuri hii ni kama ifuatavyo: Hakika ya pande sita za Qur’an tukufu ni zenye nuru na kuangaza mambo ya utata na dhana hayazikaribii, kwa kuwa: Nyuma yake kuna Arshi tukufu, inaiegemea, kuna nuru ya wahyi. Na mbele yake kuna furaha ya makazi mawili inayalenga, mafungamano yake yameungana na mahusiano yake yameungana na Milele na Akhera kuna nuru ya pepo na furaha. Na kutokea juu yake inametameta ishara yenye hali ya muujiza na inazagaza mionzi yake. Na chini yake kuna nguzo za hoja zilizopangika imara na dalili zenye nguvu, basi ndani yake kuna uongofu mtupu. Na kunako kulia kwake kunasimama kusemesha kwa akili na kusadikisha kwake, kwa wingi wa yaliyomo ndani yake أَفَلَا يعْقِلُوْنَ… Na kunako kushoto kwake kuna kushuhudisha moyo wa ndani hadi utamke kwa kupendezwa kwake mno kwa mshangao (Tabarakallah) katika yale inayopuliza katika hewa za kiroho kwa moyo. Basi utata na dhana zitaweza kujipenyeza kwake kutokea upande gani? Basi Qur’an tukufu ni yenye kujumuisha siri ya ijmai ya vitabu vya manabii na mawalii na wenye kupwekesha wote, licha ya kutofautiana kwa enzi zao, mashirabu zao na masilaki zao. Yaani wenye akili salama wote na nyoyo zilizotulia wanasadikisha mjumuisho wa hukumu za Qur’an tukufu na msingi wa inachokilingania, kiasi ambacho wanataja katika vitabu vyao. Kwa hiyo wao ni sawa na mashina ya mti wa Qur’an ya mbinguni. Kisha hakika Qur’an tukufu inaegemea wahyi wa kiungu, bali ni wahyi mtupu, kwa sababu Allah (s.w) ambaye ameiteremsha katika moyo wa Muhammad (s.a.w) anaibainisha kwa miujiza ya Nabii wake Mtukufu kuwa ni wahyi mtupu. Na Qur’an iliyoteremka kutoka kwa Allah inabainisha kwa hali yake ya kimuujiza ya dhahiri kwamba ni kutoka katika Arshi tukufu. Na kwamba hatua za aliyeteremshiwa juu yake naye ni Mtume Mtukufu (s.a.w) na kubabaika kwake mwanzoni mwa kuteremka kwa wahyi, na wakati ya kuteremka kwake, na anayoyaonesha katika heshima na kutukuza zaidi kuliko kingine, yanabainisha kwamba hiyo ni wahyi mtupu kwa uwazi anamteremshia mgeni kutoka kwa Mfalme wa Azali. Kisha Qur’an hiyo tukufu ni wahyi mtupu kwa uwazi, kwa sababu kinyume chake ni upotevu na kufuru. Kisha hakika kwa dharura hiyo ni madini ya nuru na Imani, na hapana kinyume cha nuru isipokuwa ni giza totoro. Na hakika tumethibitisha hakika hii katika maneno mengi. Kisha hakika ya Qur’an tukufu ni mkusanyiko wa hakika kwa yakini basi mawazo ya kufikirika na mapotosho ni mbali nayo umbali wa hali zote, kwani kile ilicho kiunda katika ulimwengu wa Kiislamu, na ilichokileta katika sharia angavu, na iliyoyabainisha katika mifano ya hadhi ya juu, bali hata wakati wa kujadili kwake kuhusu ulimwengu wa ghaibu - kama ilivyo katika kujadili kwake ulimwengu wa kushuhudiwa – ni dhati ya hakika, hakikaribii kitu chochote kinyume na hakika abadani. Kisha hakika Qur’an tukufu kama ilivyo hali halisi – inafikisha katika furaha ya makazi mawili bila shaka, na inawapeleka watu kuelekea huko, Basi inayempitia shaka basi na airejee Qur’an mara moja, na aisikilize na aone baada ya hivyo nini Qur’an inasema. Kisha hakika matunda ambayo mwanadamu anayavuna kutoka katika Qur’an tukufu hakika ni matunda pevu yaliyonona yenye uhai na uchangamfu. Hakuna shaka kwamba mashina ya mti wa Qur’an ni yenye kwenda kina katika hakika yenye kunyooka katika uhai, na kwamba uhai wa tunda unajulisha juu ya uhai wa mti. Ukitaka tazama ni kiasi gani Qur’an imewapa matunda wateule wenye nuru na mawalii wema wakamilifu katika muda wote wa zama mbali mbali. Kisha hakika Qur’an tukufu ni mahali pa maridhio ya watu majini na malaika na hii ni kwa makisio ya kweli, yanayotokana na alama nyingi, ambapo wanakusanyika kuizunguka wakati wa kuisoma kama vipepeo kuizunguka nuru Kisha hakika Qur’an pamoja na kuwa ni wahyi wa kiungu ni yenye kuungwa mkono kwa dalili za kiakili. Na ushahidi juu ya hili: Kuafikiana kwa wenye akili waliokamilika na katika utangulizi wao ni maimamu wa elimu ya Al-Kalamu na werevu wa falsafa mfano wa (Ibn Sina) na (Ibn Rushd) wote hao basi kwa kuafikiana wamethibitisha misingi ya Qur’an kwa misingi yao na dalili zao. Kisha hakika Qur’an tukufu kwa upande wa maumbile salama – kama hayakuiathiri kipingamizi au maradhi – ambapo kutulia kwa moyo wa ndani na raha ya moyo hakika yanatokana na nuru zake, yaani maumbile yaliyo salama yanaisadikisha kwa utulivu wa moyo. Naam! Hakika maumbile kwa ulimi wa hali yake yanaiambia Qur’an tukufu: (Ukamilifu wetu hautimii bila ya wewe) Na hakika tumeithibitisha hakika hii katika mahali tofauti kwenye Risale-i Nur. Kisha Qur’an ni muujiza wa kudumu wa milele kwa kushuhudia na kwa uwazi, inabainisha hali yake ya muujiza kila wakati, nuru yake haififii - kama miujiza mingine – wala wakati wake haukomi – bali muda wake unaendelea hadi milele. Kisha ngazi ya uongozi wa Qur’an tukufu ina upana na uenevu kiasi kwamba somo moja kutoka kwake analipokea Jibril (a.s) ubavu kwa ubavu na mtoto mdogo. Na wanapiga magoti mbele yake wanafalsafa werevu - mfano wa Ibn Sina - pamoja na mtu wa kawaida sana ummiyyu, wanapokea somo hilo hilo. Bali anaweza kuchota huyo mtu wa kawaida (Katika kundi la jumla) kutoka katika Qur’an kwa sababu ya kile anachokibeba katika nguvu ya Imani na sifa zake kiasi ambacho hakichoti (Ibn Sina). Kisha hakika katika Qur’an tukufu kuna jicho lenye kuona lenye kupenya kali sana kiasi linaona uwepo wote na kuuzungukia, na inaweka viliyomo vyote mbele yake, kana kwamba ni kurasa za kitabu na inafafanua tabaka zake na limwengu zake. Ni kama fundi saa anapopokea saa ndogo anaigeuza kwa mkono wake, na anaitambulisha na kuifungua, vivyo hivyo ulimwengu mbele ya Qur’an tukufu inautambulisha na kubainisha sehemu zake. Basi hii Qur’an tukufu inathibitisha upekee kwa. فَاع۟لَم۟ اَنَّهُ لَٓا اِلٰهَ اِلَّا اللّٰهُ اَللّٰهُمَّ اج۟عَلِ ال۟قُر۟اٰنَ لَنَا فِى الدُّن۟يَا قَرٖينًا وَ فِى ال۟قَب۟رِ مُونِسًا وَ فِى ال۟قِيَامَةِ شَفٖيعًا وَ عَلَى الصِّرَاطِ نُورًا وَ مِنَ النَّارِ سِت۟رًا وَ حِجَابًا وَ فِى ال۟جَنَّةِ رَفٖيقًا وَ اِلَى ال۟خَي۟رَاتِ كُلِّهَا دَلٖيلًا وَ اِمَامًا اَللّٰهُمَّ نَوِّر۟ قُلُوبَنَا وَ قُبُورَنَا بِنُورِ ال۟اٖيمَانِ وَ ال۟قُر۟اٰنِ وَ نَوِّر۟ بُر۟هَانَ ال۟قُر۟اٰنِ بِحَقِّ وَ بِحُر۟مَةِ مَن۟ اُن۟زِلَ عَلَي۟هِ ال۟قُر۟اٰنُ عَلَي۟هِ وَ عَلٰى اٰلِهِ الصَّلَاةُ وَ السَّلَامُ مِنَ الرَّح۟مٰنِ ال۟حَنَّانِ اٰمٖينَ
Hakika tumethibitisha kwa yakini kwa dalili za kukinaisha katika ishara zilizotangulia kwamba Mtume Mtukufu (s.a.w) ambaye Utume wake umethibiti kwa maelfu ya dalili za kukinaisha hakika ni hoja ya wazi ya upweke wa kiungu, na dalili yenye kuangaza ya furaha ya milele. Na tutatambulisha katika ishara hii utambulisho wa muhtasari kwa namna ya ufupi wa ufupi wa hoja hiyo ya kweli na dalili yenye kuangaza juu ya upweke, kwa sababu: Inalazimu kuijua dalili na kuzungukia kwa namna ya udalili wake maadamu yeye ni dalili kuelekea maarifa ya kiungu. Kwa ajili hiyo hapa tutabainisha kwa muhtasari sana namna ya udalili wake (s.a.w) juu ya Tawhidi na kiasi cha ukweli wake na kusibu kwake basi tunasema: Hakika Mtume Mtukufu (s.a.w) yeye mwenyewe kwa dhati yake ni dalili juu ya kuwepo kwa Muumba Mtukufu na juu ya upweke wake kama chochote kilichopo katika vilivyokuwapo vya ulimwenguni kinavyojulisha hilo. Na hakika ametangaza (s.a.w) hii namna ya udalili wake juu ya Tawhidi na uwepo pamoja na kujulisha vilivyokuwepo vyote. Na kwa kuwa yeye (s.a.w) ni dalili juu ya Tawhidi tutaashiria juu ya ukweli wa kuwa kwake ni dalili na kuwa kwake ni hoja na kusibu kwake na kuwa kwake mwenye kustahiki ndani ya misingi kumi na tano.
Hakika ya dalili hii ambayo inajulisha juu ya muumba wa ulimwengu kwa dhati yake na kwa ulimi wake na kwa kujulisha hali zake na kwa ulimi wa hatua zake, na kwa hakika ni mkweli mwenye kusadikishwa kwa upande wa hakika za ulimwengu, kwa sababu hali za dalili za viumbe vyote katika upweke hakika ni sawa na shahada za kuthibitisha kwa anayetamka upweke. Yaani anachokilingania kinasadikishwa mbele ya ulimwengu wote. Na kwa kuwa anachobainisha katika upweke, ambao ni ukamilifu wa hali zote, na anayobashiria katika furaha ya milele ambayo ndiyo kheri ya hali zote, vinaambatana kikamilifu na uzuri na ukamilifu mawili yenye kudhihiri katika hakika za ulimwengu. Hakika yeye ni mkweli katika madai yake kwa makato. Basi mjumbe mtukufu (s.a.w) kwa hiyo ni hoja ya kweli yenye kusadikishwa ya upweke wa kiungu na furaha ya milele.
Hakika ya dalili hiyo ya kweli yenye kusadikishwa ambayo inamiliki maelfu ya miujiza – zaidi kuliko iliyokuwa kwa manabii waliotangulia – na ambaye ameleta sharia yenye msamaha angavu haifutwi wala haibadilishwi, na kwa ulingano wenye kuenea kwa majini na watu, hapana shaka kwamba yeye ni Bwana wa Mitume (a.s), kwa hiyo yeye ni mwenye kukusanya hekima na siri ambazo zilizomo ndani miujiza ya manabii (a.s) na kuafikiana kwao. Yaani hakika nguvu ya ijmai ya manabii wote, na ushahidi wa miujiza yao kwa hiyo inaunda msingi wa ukweli wake na kusibu kwa ulingano wake. Kisha hakika ya wateule na mawalii na wema ambao wamefikia ukamilifu kiasi walichofikia hakika ilikuwa kwa malezi yake ya hadhi ya juu na kwa mwongozo wa sharia yake ya haki yeye basi ni mwelekezi wao na Mkuu wao, kwa ajili hiyo yeye ni mwenye kukusanya siri ya karama zao na kusadikisha kwao kwa ijmai na nguvu ya masomo yao na tahakiki zao, ambapo wao wamepita njia ambayo milango yake amefungua ustadhi wao, na akaiacha ikiwa wazi, wakaikuta hakika. Basi karama zao zote na tahakiki zao za kimatendo na ijmai zao hakika zinawakilisha msingi wa ukweli wa ustadhi wao ulio safi na kusibu kwa ulingano wake. Kisha hakika ya hoja hiyo iliyo wazi ya upweke - kama ilivyobainika katika ishara zilizotangulia - inamiliki katika miujiza ya wazi ya kukinaisha ya yakini. na irhasati za kufurutu ada, na dalili za Utume zisizo na shaka ndani yake, zote hizo zinamsadikisha usadikishaji mkubwa, kwa kiasi kama ulimwengu ungekusanyika wote ili kujeruhi usadikishaji huo ungeshindwa kutimiza hilo.
Hakika ya huyo mlinganiaji katika upweke na mbashiri wa furaha ya milele ambaye ana miujiza hii ya wazi anamiliki katika tabia za hadhi ya juu katika dhati yake yenye baraka, na katika tabia za hali ya juu katika jukumu la Utume wake, na katika sifa bora katika anayoyafikisha miongoni mwa sharia na dini, hali ambayo inalazimu kumsadiki maadui wake wakubwa hawapati njia ya kukanusha. Basi maadam anamiliki katika dhati yake na katika jukumu lake na katika dini yake tabia njema mno na nzuri, na ukamilifu wa tabia na za thamani zaidi, na sifa za hali ya juu na bora zaidi, basi hapana shaka kwamba yeye ni mfano wa ukamilifu wa vilivyomo, na mwakilishi wa tabia bora na mfano wake ulioundwa kuwa mwili, na ruwaza yao njema, na kwa ajili hii makamilifu ambayo yanamulika kama mionzi kutoka katika dhati yake na kutoka katika jukumu lake na kutoka katika dini yake kwa hakika ni nguzo yenye nguvu kubwa ya ukweli wake ambao haiyumkiniki kwa chochote kuuteteresha.
Hakika ya mlinganiaji huyo wa upweke na furaha ya milele ambaye yeye ni madini ya makamilifu na mwalimu wa tabia bora. Hatamki kuhusu nafsi yake mwenyewe na kulingana na Utashi wa nafsi yake – hasha – bali hakika anatamka kwa wahyi wa kiungu. Yeye anapokea wahyi kutoka kwa mola wake mtukufu na kuwafikishia wengine. Kwa kuwa imethibiti kwa maelfu ya dalili za Utume, kama ilivyotajwa katika misingi iliyotangulia na kufafanuliwa sehemu kati yake: Hakika Bwana Mlezi (s.w) ambaye ameumba miujiza yote hiyo na kuipitisha katika mkono wa Mtume wake (s.a.w), hakika anabainisha kuwa Mtume wake Mtukufu (s.a.w) anatamka kwa ajili yake na katika njia yake na anafikisha maneno yake yaliyo wazi. Na kwamba Qur’an tukufu ambayo imeteremka juu yake inabainisha kwa hali yake ya kimuujiza ya dhahiri na ndani kwamba yeye (s.a.w) ni mfikishaji kutoka kwa Bwana Mlezi wa walimwengu. Na kwamba dhati yake tukufu (s.a.w) na yanayodhihiri kwake katika ikhlasi kubwa na uchaji na jitihada ya upeo mkubwa katika kufikisha amri ya Allah (s.w), na uaminifu wa kweli katika hilo, yanabainisha katika hali zake na hatua zake zote kwamba yeye hazungumzi kwa jina lake binafsi, wala sio katika uzao wa fikira yake ya dhati mwenyewe lakini hakika anazungumza kwa jina la Allah Bwana Mlezi wa walimwengu. Kisha hakika ambao wamemsikiliza miongoni mwa watu wote wa hakika wamesadikisha kwa kufunuliwa na uhakiki wa kielimu, na wameamini kwa imani ya yakini kwamba yeye hatamki kwa utashi wa nafsi yake, hiyo sio kingine ila ni wahyi unaofunuliwa, basi yeye ni mfikishaji mwaminifu kutoka kwa Mola Bwana Mlezi wa walimwengu wote, anawaita watu kwenda kwenye uongofu kwa wahyi wa kiungu. Na kama hivi hakika ukweli wa dalili hii (s.a.w) na kustahiki kwake kunaegemea katika misingi hii minne thabiti imara.
Hakika ya huyo mfikishaji mwaminifu wa maneno ya Allah (s.w) ya azali anaona roho, na anazungumza pamoja na Malaika, na anawaongoza majini na watu kwa pamoja. Hapokei elimu kutoka katika limwengu za Malaika na roho ambazo ni za hadhi ya juu kuliko ulimwengu wa watu na majini bali anapokea elimu kutoka juu ya limwengu zote hizo, bali anachungulia nyuma ya limwengu hizo katika mambo ya kiungu, basi miujiza iliyotangulia kuelezwa, na sira yake tukufu ambayo imenakiliwa kwetu kwa tawatur mawili haya yanathibitisha hakika hii. Kwa ajili hii hawaingilii majini wala roho wala Malaika katika mambo anayoyafikisha bali hawakaribii katika ufikishaji wake hata waliokurubishwa miongoni mwa Malaika isipokuwa Jibril (a.s), bali wakati mwingine anamtangulia hata rafiki yake Jibril ambaye alikuwa anasuhubiana naye nyakati nyingi.
Hakika dalili hiyo ambayo ni Bwana wa Malaika na majini na watu hakika ni tunda lenye nuru zaidi kamilifu zaidi la mti wa viumbe, na mfano halisi wa rehema ya kiungu, na mfano wa mahaba ya kiungu, na hoja yenye nuru ya haki, na taa yenye kuangaza ya hakika, na ufunguo wa talasimu la viumbe, na mfumbuzi wa fumbo la uumbaji, msherehishaji wa hekima ya ulimwengu na mlinganiaji wa mamlaka ya kiungu na mwelekezi mzuri kwa mazuri ya sanaa ya kiungu Bwana Mlezi, basi zile ni Atomu zenye baraka. Kwa sifa za jumla inazomiliki kwa hakika anawakilisha kielelezo kamili zaidi cha makamilifu ya vilivyomo, kwa hiyo basi sifa hizi pambanuzi ambazo anazimiliki huyu Mtume Mtukufu na haiba ya kimaanawy anayosifika nayo vinadhihirisha viwili hivyo kwa uwazi kwamba huyu nabii Mkarimu (s.a.w) ni sababu ya ulimwengu ya kishabaha, yaani yeye ni mahali pa utazamaji wa muumba wa ulimwengu, amemtazama na akaumba ulimwengu, na inasihi kusema kuwa lau isingekuwa amemleta katika uwepo asingeuleta ulimwengu katika uwepo. Naam, hakika ya aliyokuja nayo Mtume Mtukufu (s.a.w) katika hakika za Qur’an na nuru za imani kwa watu na majini wote, na yanayoshuhudiwa katika dhati yake yenye baraka miongoni mwa tabia za hadhi ya juu na makamilifu ya kupitiliza, ni ushahidi wa kweli wenye kukinaisha juu ya hakika hii.
Hakika ya hoja ile ya haki na taa yenye kuangaza ya hakika imedhihirisha dini iliyonyooka, na kudhihirisha sharia enevu kwa kiasi kwamba inakusanya kanuni zenye kujumuisha ambazo zinahakikisha furaha ya makazi mawili, kama ambavyo kwamba inabainisha ubainifu kamili zaidi wa hakika ya ulimwengu na jukumu lake na majina ya muumba mtukufu na sifa zake. Basi ambaye anaangalia kwa makini katika huo Uislamu mnyoofu na sharia angavu enevu katika mtindo wa utambulisho wake kwa ulimwengu atatambua kwa yakini kwamba dini hiyo hakika ni mfumo wa Muumba wa Ulimwengu huu mzuri ambao unamtambulisha Muumba huyo. Ambapo kama ilivyo mjenzi stadi wa kasri yenye kupendeza anaweka utambulisho unaowiana na Kasri na anaiandika ili kubainisha umahiri wake wa hali ya juu, vivyo hivyo dini hii adhimu na sharia yenye msamaha na yaliyomo ndani yake miongoni mwa uenevu na kuzungukia na kuwa juu yanadhihirisha kwa uwazi kwamba ambaye ameiweka katika sura hii ya hali ya juu hakika yeye ni mweka wa ulimwengu na mwendeshaji wake. Naam, hakika ya mwenye kuwa mpangiliaji wa huu ulimwengu wa ajabu na kwa mpangilio huu wa kupendeza hapana budi kuwa yeye ndiye ambaye amepangilia dini hii iliyo kamilifu mno kwa mfumo huu mzuri mno.
Hakika anayesifika kwa sifa hizi nzuri zilizoelezwa, na Utume wake unaegemea katika dalili hizo na nguzo madhubuti, huyo ni Mtume mpendwa (s.a.w), anaongea kwa jina la ulimwengu wa ghaibu hali ya kuelekea katika ulimwengu wa kushuhudia, hali ya kutangaza juu ya vichwa vya wenye kushuhudia miongoni mwa majini na watu, akiwasemesha kaumu waliorundikana nyuma ya zama zijazo, basi anawanadia wote mnada wa juu wenye hadhi anawasikilizisha wote kwa jumla katika zama zote popote wapatikanapo na vyovyote walivyo. Naam, naam tunasikia!
Hakika ya hotuba yake hii ni ya juu kwa kiasi zama zote wanaisikia, naam, hakika kila zama inasikia mrejeo wa mwangwi wa maneno yake.
Hakika sisi tunaona katika hali zake na sira yake iliyotakasika hakika anaona kisha anafikisha katika mwanga wa anayoona, hakika yeye anafikisha hata wakati ambapo mawazo yanamkodolea, bila ya kusitasita wala kubabaika na kwa kujiamini kote bali peke yake anaweza kuchagiza ulimwengu wote.
Hakika amekwisha kutangaza ulingano wake kwa nguvu zote alizompa Allah (s.w), ameutangaza kwa dhahiri hadi amejaalia nusu ya Ardhi na moja ya tano ya ulimwengu wanaitikia amri zake na wanasema kwa kila neno lililotoka kwake: Tumesikia na tumetii.
Hakika analingania kwa ikhlasi kamili na kwa bidii iliyotimia basi analea malezi imara, kwa kiasi kwamba kanuni zake zinawekwa nakshi kwenye vipaji vya uso vya zama na kurasa za miji na nyuso za dahari kwa dahari nyingi.
Hakika anaongea kwa maneno yaliyojaa kujiamini na kutulia basi anafikisha hukumu hali akiwa mwenye kujiamini kwa kujiamini kote kutokana na ukweli wake na kusibu kwake, na analingania kwa ulinganiaji wa wazi hakuna kuchanganya ndani yake kwa kiasi kama ulimwengu wote utakutanika hautaugeuza mbali na Daawa yake wala mbali na hukumu miongoni mwa hukumu hizo. Na sira yake iliyotakaswa na historia ya maisha yake yaliyobarikiwa ni ushahidi wa kweli zaidi juu ya hakika hii.
Hakika analingania kwa utulivu mkubwa na kutegemea kikamilifu, kwa namna ambayo hashuki na kuacha kitu katika Daawa yake. Na hasiti mbele ya mushkeli wowote vyovyote uwavyo, haimwingii khofu na mshangao, bali analingania kwa usafi kamili na ikhlasi timamu. Na anatekeleza anacholingania katika hukumu juu ya nafsi yake kwanza na kuitii kisha wanaifundisha wengine. Na chenye kushuhudia hili ni zuhdu (kuipa nyongo dunia) kubwa na ukwasi wake mbali na watu na upaji wake nyongo mapambo ya dunia yenye kutoweka, kama lijulikanavyo hili mbele ya marafiki na maadui.
Hakika yeye alikuwa Mwenye hofu zaidi wa Allah kuliko watu wote na mnyenyekevu wao zaidi kwa amri zake (s.w) na mwabudu wao zaidi na mchaji wao zaidi wa kujiweka mbali na makatazo yake, mambo ambayo yanatujulisha kwamba yeye ni mfikishaji mwaminifu wa Sultani wa azali na milele, basi yeye ni mjumbe wake kipenzi na mwenye ikhlasi zaidi ya waja wake wote, na mfikishaji wa ujumbe wake. Tunahitimisha hii misingi kumi na mitano: Hakika ya huyu Mtume Mtukufu (s.a.w) aliyesifika kwa sifa hizo zilizotajwa hakika ametangaza upweke na akalingania kwa kila alivyompa Allah (s.w) miongoni mwa nguvu, alilingania kwa nguvu zote alizompa Allah (s.w), Na katika mzunguko wa uhai wake wote wenye baraka: لَٓا اِلٰهَ اِلَّا اللّٰهُ. اَللّٰهُمَّ صَلِّ وَ سَلِّم۟ عَلَي۟هِ وَ عَلٰى اٰلِهٖ عَدَدَ حَسَنَاتِ اُمَّتِهٖ سُب۟حَانَكَ لَا عِل۟مَ لَنَٓا اِلَّا مَا عَلَّم۟تَنَٓا اِنَّكَ اَن۟تَ ال۟عَلٖيمُ ال۟حَكٖيمُ
Kwa matarajio tupate siri ya aya tukufu: وَأَمَّا بِنِعْمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثْ tunasema: Hakika athari ya uangalizi wa kiungu Bwana Mlezi na mguso wa rehema ya kiungu umedhihiri wakati wa kuandika risala hii, nautaja kwa wasomaji wake wema ili waigeukie kwa kutilia umuhimu mkubwa: lilikuwa (Neno la thelathini na moja) na (La kumi na tisa) ambayo yanajadili kuhusu Utume wa Muhammad yamekwisha andikwa, kwa hiyo haikupita moyoni mwangu chochote kuhusu kuandika risala hii, tahamaki wazo linakuja moyoni moja kwa moja, linanisisitiza kuandika katika wakati ambao ukali wa hifadhi yangu umechoka na kufifia mwanga wake chini ya pigo la masaibu na mabalaa, ukiachilia mbali kwamba mimi katika vitabu vyangu nilivyoandika - kwa mujibu wa Mashrabu yangu - njia ya kunakili katika vitabu (Kasema fulani, imesemwa kadha), na juu ya kwamba sikuwa na chanzo chochote katika vyanzo vya Hadithi tukufu au sira iliyotakaswa. Lakini licha ya yote haya nimesema: (توكلت على الله), na nikaanza kuandika risala hii haki ya kumtegemea yeye peke yake, ikapatikana kutokana na taufiki ya kiungu kilichofanya uhifadhi wangu kuwa na nguvu kwa kiasi ulikuwa unanisaidia msaada unavuka sana uhifadhi wa (Saidi wa Zamani) hata imeandikwa kiasi cha kurasa arobaini kwa kasi ya hali ya juu ndani ya muda unaokaribia masaa manne, bali ziliandikwa kurasa kumi na tano ndani ya saa moja. Nukulu zilikuwa ghalibu ni kutoka katika vitabu vya Hadithi kama Bukhary, Muslimu, Al-Baihaqy, As-Shifaa cha Qadhi Iyadh, Abu Nuaim, At-Tabary na mifano wa hizo. Na moyo wangu unapepea na kutikisika kwa nguvu, kwani kama lingetokea kosa katika unukulu huu ingefuatia dhambi juu yake, kwa kuwa hiyo ni Hadithi sharifu. Lakini tulitambua kwa yakini hakika uangalizi wa kiungu uko pamoja nasi na kwamba haja ya risala hii ni kubwa. Hadithi zikaandikwa kwa fadhili ya Allah (s.w) zikiwa salama na sahihi. Na pamoja na hili, ikiwa itapatikana katika lafudhi za Hadithi sharifu au katika jina la Mpokezi kosa lolote basi matumaini (tuliyonayo) kutoka kwa ndugu wapenzi kulisahihisha na kusamehe kosa hilo. Said Nursî Naam! Hakika alikuwa Ustadhi anatufanyia imla nasi tunaandika muswada, na hakuwa na chanzo chochote kiwacho, na hakurejelea (kubadili) maneno yake katu. Maneno yake yalikuwa katika ukomo wa kasi, nasi tulikuwa tukiandika kiasi cha kurasa arobaini ndani ya saa mbili au tatu. Basi tukayakinisha kwamba hakika taufiki hii ya kiungu katika utunzi ni karama katika karama za muujiza wa Nabii kwa mwenyewe ziende ziada za rehema na ziada za salama. (Al-Hafidh taufik) mwandishi wa muswada (Al-Hafidh khalid) Ndugu yake Akhera na mwandishi wa Muswada (Sulayman Samy) Mhudumu wake na mwandishi wa muswada. (Abdallaha Jawuosh) Mhudumu wake Mkazi.
Kutoka Katika Risala ya (Muujiza wa Muhammad (s.a.w)) [Kwa mnasaba wa kituo hapa limekusanywa (Neno la kumi na tisa) nalo linahusu Utume wa Muhammad (s.a.w) pamoja na nyongeza yake ambayo inajadili muujiza wa kupasuka mwezi.] بِسْمِ اللهِ الرَّحْمنِ الرَّحِيمِ Neno hili (Mng’ao wa kumi na nne) linajumuisha vitone kumi na nne:
Vinavyotujulisha Mola wetu ni wajulishaji wakuu wa watatu: Kwanza: Kitabu cha ulimwengu, ambacho tumesikia kitu kutokana na ushahidi wake katika ming’ao kumi na tatu (Kutoka katika ming’ao ya mathnawy al-Araby An-Nury). Pili: Ni ishara kuu ya kitabu hiki kikubwa naye ni mwisho wa diwani ya Utume (s.a.w). Tatu: Ni Qur’an yenye hekima zote. Basi ni juu yetu hivi sasa kutambua hii hoja ya pili yenye kuzungumza, naye ni wa mwisho wa manabii na Bwana wa mitume Mursali (s.a.w). Na tumsikilize kwa hushui. Jua! Hakika ya hoja hiyo yenye kuongea ina haiba ya kimaanawy kubwa. Ukisema: Ni nini hiyo? Na nini ainisho lake? Utaambiwa: Ni yule ambaye kwa utukufu wake wa kimaanawy uso wa Ardhi umegeuka kuwa ni msikiti wake, na Makka ni mihirabu yake, na Madina ni mimbari yake, naye ni imamu wa waumini wote wanamfuata wakijipanga safu nyuma yake, na msemaji wa wanadamu wote anawabainishia kanuni za furaha yao, mkuu wa manabii wote anawatakasa na kuwasadikisha kwa ujumuishi wa dini yake kwa mambo ya msingi ya dini zao, na bwana wa mawalii wote anawaelekeza na kuwalea kwa jua la Utume wake, na ni mhimili katikati ya duara la dhikiri liliundika kutokana na manabii na wanazuoni na masiddiqina na wema wenye kuafikiana na neno lake na wenye kulitamka, na mti wa kinuru mizizi yake ya kiuhai madhubuti ni manabii kwa misingi ya mbinguni, na matawi yao ya kijani kiwiti mabichi na matunda yake nyororo yenye nuru ni mawalii kwa maarifa yao ya kiilhamu. Basi hakuna madai anayo yadai ila wanamshuhudia manabii wote wakiegemea miujiza yao, na mawalii wote wakiegemea karama zao, hivyo kana kwamba kila madai katika madai yake yana mihuri ya wakamilifu wote, ambapo tunamuona amesema: ﴾لا إله إلاَّ الله﴿ na kudai Tawhidi wakati huo tunasikia kutoka muda uliopita na mustakabali kutoka katika safu hizo mbili za nuru majua ya wanadamu na nyota zake waliokaa katika duara la dhikiri – neno hilo hilo, wanalikariri na wanaafikiana juu yake, pamoja na kuhitilafiana kwa maslaki zao na kupambanuka kwa mashrabu zao. Basi kana kwamba wao wanasema kwa ijmai: (Umesema kweli na umetamka haki tupu). Basi umbali ulioje kwa dhana kunyoosha mkono wake ili kupinga madai yaliyoungwa mkono na shahidi za wasio na mpaka ya wenye kushuhudia ambao miujiza yao na karama zao zina watakasa.
Jua! Hakika ya hoja hii ya kinuru ambayo imejulisha juu ya Tawhid na kuwaelekeza wanadamu katika hilo, kama inavyoungwa mkono na nguvu ya yaliyomo katika mbawa mbili unabii na uwalii kutokana na ijmai na tawatur. Kadhalika zinamsadikisha mamia ya ishara za vitabu vya mbinguni katika biashara za Taurati, Injili na Zaburi na vitabu vya wale wa awali, na kadhalika zinamsadikisha alama za maelfu ya irhasati nyingi zenye kushuhudiwa, na vilevile zinamsadikisha maana za dalili za miujiza yake miongoni mwa mifano ya: Kupasuka mwezi, na kutokea kwa maji kutoka katika vidole vyake kama Kauthar kuja kwa mti kwa yeye kuuita, na kuteremka kwa mvua papo hapo muda wa kuomba kwake dua, na kushiba watu wengi kutokana na chakula chake kichache, na kuongea kwa kenge, mbwa mwitu, paa, ngamia na jiwe, hadi elfu ya miujiza ya hekima walivyoibainisha wapokezi na wana Hadithi wahakiki. Na vile vile inamsadikisha sharia yenye kujumuisha furaha za makazi mawili. Na jua! Kama zinavyomsadikisha dalili hizi za kianga, vile vile yeye ni kama jua linajulisha juu ya dhati yake kwa dhati yake mwenyewe, basi zinamsadikisha dalili za kinafsi, kwa kuwa zimekutanika tabia zote njema katika dhati yake kwa kuafikiana. Na vilevile mkusanyiko wa haiba yake ya kimaanawy katika jukumu lake tabia zote bora na mambo yaliyotakasika, na vivyo hivyo nguvu ya imani yake kwa ushahidi wa zuhdu yake yenye nguvu na nguvu ya ucha mungu wake na uja wake wenye nguvu. Na kadhalika ukamilifu wa kutegemea kwake kwa ushahidi wa mwendo wake, na ukamilifu wa bidii yake na ukamilifu wa umadhubuti wake, na vilevile nguvu ya matumaini yake katika harakati zake kwa ushahidi wa nguvu ya utulivu wake, inamsadikisha kama jua lenye kuangaza katika madai ya kushikamana kwake na haki na kupita kwake kwenye hakika.
Jua! hakika mazingira ya kiwakati na mahali yana taathira kubwa katika maamuzi ya akili. Ukitaka njoo ili twende katika bora ya karne na zama za mafanikio ya furaha ya Mtume (s.a.w) ili tupate ziara yake tukufu (s.a.w) – japo kwa namna ya kimawazo – naye akiwa katika kichwa cha jukumu lake akifanya kazi. Basi fungua macho yako mawili na utazame! Hakika cha kwanza kinachodhihirika kwetu kutoka katika mamlaka haya: Ni mtu mwenye kufurutu ada, mwenye uzuri wa sura wa hali ya juu, na katika uzuri wa mwenendo wa kupendeza. Basi ni huyo anashika mkononi mwake kitabu cha muujiza kitukufu, na kwa ulimi wake mazungumzo ya muhtasari yenye hekima, anafikisha hotuba ya kiazali na anaisoma kwa wanadamu wote, bali kwa Majini na watu wote, bali kwa vilivyokuwamo vyote. Basi ee ajabu iliyoje! Nini anachokisema? Naam! Hakika anasema kuhusu jambo kubwa, na anajadili kuhusu habari kubwa, ambapo anasherehesha na anafumbua fumbo la ajabu katika umbo la ulimwengu, na anafungua na kufunua talasimu iliyofungwa katika siri ya hekima ya viumbe, na anafafanua na kujadili kuhusu maswali matatu magumu ambayo yamezishughulisha akili na kuzitupa katika tahayuri, ambapo hayo ndiyo maswali ambayo anayaulizia kila kilichomo. Nayo: Wewe ni nani? Na unatoka wapi? Na unakwenda wapi?
Tazama! Kwa huyu mtu wa kinuru vipi anaeneza mwanga wenye nuru kutoka katika hakika na kutoka katika haki nuru yenye kuangaza, hata akageuza usiku wa watu kuwa mchana na majira ya baridi kuwa majira ya machipuo, kana kwamba viumbe umbo lake limebadilika, ulimwengu ukageuka ni wenye kucheka wenye kufurahika baada ya kuwa umenuna wenye hasira, na ikiwa utavitazama viumbe nje ya nuru ya uongozi wake, unaona matanga ya jumla katika viumbe, na unaona vilivyomo kama wa kando wageni na maadui, hawajuani wenyewe kwa wenyewe, bali anamfanyia ubaya, na unaona visivyo na uhai ni majeneza yenye kushangaza, na unawaona wanyama wake na watu wake ni mayatima wenye kulia kwa mapigo ya kutoweka na utengano. Basi hili ndio ainisho la viumbe kwa yule mbaye hajaingia katika duara la nuru yake, sasa tazama kwa nuru yake, na kwa mngojeo wa dini yake, na katika duara la sharia yake kwa viumbe. Unawaonaje? Basi tazama! Umbo la ulimwengu limebadilika, nyumba ya matanga ya jumla imegeuka kuwa ni msikiti wa dhikiri na tafakuri na baraza la jadhiba na shukurani, na kugeuka kwa maadui wa kando katika vilivyomo kuwa wapenzi na ndugu, na kugeuka vyote katika vyake visivyo na roho vifu vyenye kunyamaza kuwa ni hai mwenye kuliwaza mwamuriwa mwenye kudhalilishwa hali ya kutamka kwa ulimi wa hali yake aya za muumba wake, na kubadilika kwa wenye uhai katika hivyo – mayatima wenye kulia wenye kulalamika – hali ya kukumbuka kwenye tasbihati zao, hali ya kushukuru kwa kuruhusiwa kwao kutokana na majukumu yao.
Kwa nuru hiyo zimegeuka harakati za viumbe na tofauti za aina zake na mabadiliko yake kutoka katika hali ya mchezo na uduni na kuwa mahali pa mchezo wa sadfa na kuwa maandishi ya kiungu Bwana Mlezi, na kurasa za aya za kimaumbile, na vioo vya majina ya kiungu. Hadi ulimwengu ukapanda na kugeuka kuwa ni kitabu cha hekima cha kiungu Mola mtagemewa kwa kila haja. Na mtazame mwanadamu namna gani alivyopanda kutokea nafasi ya chini ya kiuhayawani ambayo aliyoporomokea kwa kushindwa kwake na ufukara wake na kwa akili yake yenye kunakili huzuni za wakati uliopita na hofu za mustakabali, amepanda hadi katika kilele cha ukhalifa kwa kupata nuru kwa akili hiyo kushindwa na ufakiri huo. Na tazama vipi zimegeuka sababu za kudondoka kwake – kutokana na kushindwa na ufukara na akili – kuwa sababu za kupanda kwake kwa sababu ya kuchukua kwake nuru kwa nuru ya haiba hii ya kinuru. Kwa hivi, lau asingepatikana mtu huyu viumbe vingeanguka na mwanadamu, na kila kitu kwenda katika daraja la kutokuwepo, havina thamani wala umuhimu. Kwa mfano wa viumbe hivi vya ajabu vizuri inalazimu mfano wa mtu huyu mwenye kufurutu ada wa hali ya juu aliyetambulishwa na kuhakikishwa, na kama hakuwa huyu basi haviwi viumbe, kwani havina maana kwa mnasaba na sisi.
Ukisema: Nani huyu mtu ambaye tunamwona amekuwa ni jua la ulimwengu, kwa dini yake anafunua makamilifu ya viumbe? Na anasema nini?. Utaambiwa: Tazama na sikiliza anayoyasema: Huyo anapasha habari kuhusu furaha ya milele na kuibashiria, na anafunua kuhusu rehema isiyo na ukomo, na anaitangaza na kuwaita watu kuiendea. Naye ni mpiga mbiu wa mazuri ya ufalme wa kiungu na mwangalizi wake, na mfunuaji wa yaliyofichikana ya hazina za majina ya kiungu na ni mtambulishaji wake. Basi mwangalie kwa upande wa jukumu lake (Utume wake), utamwona kuwa ni hoja ya haki na taa ya hakika na jua la uongofu na njia ya furaha. Kisha mwangalie kwa upande wa haiba yake (Uja wake), utamwona kuwa ni mfano wa mahaba ya kiungu mwingi wa Rehema na mfano halisi wa Rehema ya kiungu Mola Mlezi, na utukufu wa hakika ya kibinadamu, na ua lenye nuru zaidi la matunda ya mti wa kuumbwa. Kisha tazama! Vipi nuru yake na dini yake imezunguka mashariki na magharibi katika kasi ya umeme unaochomoza, na wamekubali kwa utiifu wa moyo idadi inayokaribia nusu ya Ardhi na humusi (1/5) ya wanadamu wamekubali zawadi ya uongozi wake, kiasi inatoa roho zao fidia kwa ajili yake. Na je yawezekana kwa nafsi na shetani kujadili bila ya kufanya makosa katika madai ya mfano wa matu huyu, na hasa katika madai ambayo ndio msingi wa madai yake yote. Nalo ni ﴾لا إله إلاَّ الله﴿ kwa ngazi zake zote?
Ukitaka kujua kuwa kinachompa harakati hakika ni nguvu ya kitakatifu, basi tazama shughuli zake katika kisiwa hiki kipana! Je huoni hawa watu mbali mbali wa kiujima katika jangwa hili pana sana, wenye kushikilia tamaduni zao, wenye ukaidi katika kujinasibu na koo zao na uhasama wao, vipi mtu huyu ameondoa tabia zao zote mbaya za kiujima na kuzing’oa katika muda mchache mkupuo mmoja? Na akawaandaa kwa tabia njema za hali ya juu, akawafanya kuwa waalimu wa ulimwengu wa kiutu na maustadhi wa mataifa yaliyostaarabika. Basi tazama! Ufalme wake sio kwa nje tu, bali huyu hapa anafungua nyoyo na akili, na kuzitiisha roho na nafsi, mpaka amekuwa ni kipenzi wa nyoyo na mwalimu wa akili na mlezi wa nafsi na sultani wa roho.
Katika yanayojulikana ni kuwa tabia ndogo - kama kuvuta sigara – kutokana na taifa dogo kwa ujumla, inaweza kuwa ni jambo gumu kwa mtawala mkubwa, kwa hima kubwa, pamoja na kuwa sisi tunamwona Mtume huyu Mtukufu (s.a.w) ameondosha kwa ujumla, tabia nyingi, kutoka kwa kaumu kubwa kubwa, wenye kushikilia tabia zao, wakaidi katika hisia zao, ameziondosha kwa nguvu ndogo, na hima chache katika dhahiri ya hali, na katika muda mfupi, na amepandikiza badala yake kwa kujikita imara kikamilifu katika mwenendo wao ameweka tabia za hali ya juu, na mambo ya tabia ghali, yanaonekana kwetu basi miongoni mwa maajabu ya shughuli zake za kimsingi maelfu ya tuliyoyaona, basi asiyeona zama hizi za mafanikio tunamwingiza machoni mwake kisiwa hiki na tunampa changamoto. Basi na ajaribu nafsi yake humo. Na wachukue mia moja miongoni mwa wanafalsafa wao na waende huko na wafanye kazi miaka mia moja je itakuwa wepesi kwao kufanya sehemu ndogo katika sehemu mia moja ya yale aliyoyafanya (s.a.w) ndani ya mwaka mmoja kwa mujibu wa wakati huo?!
Jua! Ukiwa mtambuzi wa tabia za wanadamu, kwamba haiwi wepesi kwa mwenye akili kudai – katika madai ambayo ndani yake kuna ushindani – uongo ambao anahofia kudhihirika kwake, na auseme bila tabu na bila ya kusita na bila ya kubabaika kunakoashiria hila yake, na bila ya kujifanyisha na kuhemkwa viwili vinavyoonesha uongo wake, mbele ya macho ya mahasimu wake wakosoaji, japo akiwa ni mtu mdogo, japo katika jukumu dogo, japo katika nafasi duni, na japo katika kundi dogo, na japo katika suala dogo. Basi vipi itayumkinika kuingilia kwa hila na kuingia tofauti katika madai ya mfano wa mtu huyu ambaye ni afisa mkuu na katika jukumu kuu kwa mazingira makuu, pamoja na kuwa anahitaji himaya kubwa, na katika kundi kubwa, mkabala na uhasama mkubwa, na katika suala kuu, na katika madai makubwa? Na huyu hapa anasema anayosema bila ya kujali mpingaji na bila ya kusita, bila kuona tabu, bila ya kuhofia na bila ya kubabaika, kwa usafi wa umadhubuti, kwa jadhiba safi na kwa mtindo unaochokoza hasira za mahasimu wake, kwa kuzipumbaza akili zao na kudharau nafsi zao na kuvunja utukufu wao, kwa mtindo mkali wa hali ya juu. Basi je inayumkinika kuingilia kwa hila katika mfano wa madai kama haya kutoka kwa mfano wa mtu kama huyu, katika mfano wa hali hii iliyotajwa? Hapana! إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَى Naam, hakika ukweli ni mkwasi mno kufanyiwa udanganyifu, na mtazamo wa hakika ni wa juu zaidi kuliko kufanyiwa udanganyifu. Naam! Hakika maslaki yake ya haki ni makwasi na udanganyifu, na mtazamo wake mkali ni wenye kutakasika na kuchanganyika kwa mawazo ya kufikirika na hakika.
Tazama na sikiliza anayoyasema! Huyo anajadili hakika kubwa za kustaajabisha, na anajadili masuala yenye kuvuta nyoyo, yenye kuleta akili katika umakini na kutazama, kwani katika yanayojulikana kwamba shauku ya kugundua hakika za mambo imewapeleka wengi kati ya wenye kupenda kutafuta, wenye pupa na kutilia umuhimu katika kutoa fidia roho zao. Je huoni kwamba ungeambiwa: Ikiwa utatoa fidia nusu ya umri wako, au nusu ya mali yako, angeteremka kutoka mwezini au kutoka sayari ya mushtara mtu ambaye atakaye kupasha habari za mageni ya hali zake, na kukupasha habari ya hakika ya mustakabali wa siku zako? Nakudhania utaridhia kutoa fidia. Basi ajabu iliyoje? unafidia unachokipupia kwa nusu ya umri na mali, wala hutilii umuhimu anayoyasema Nabii huyu Mtukufu (s.a.w) na wanamsadikisha ijmai ya watu wa ushahidi na tawatur ya watu wa (nyanja) mahususi miongoni mwa manabii na masiddiqina na mawalii na wahakiki! Wakati ambao yeye anajadili kuhusu mambo ya Mfalme, mwezi katika ufalme wake sio chochote isipokuwa ni kama nzi anaruka pembezoni mwa kipepeo, na huyu anaogelea pembezoni mwa taa miongoni mwa maelfu ya kandili ambazo ameziwasha katika nyumba miongoni mwa maelfu ya nyumba ambazo ameziandaa kwa ajili ya wageni wake. Na vivyo hivyo anapasha habari kuhusu ulimwengu ambao ni mahali pa mambo ya kufurutu ada na maajabu na kuhusu mapinduzi makubwa, kwa kiasi ambacho Ardhi ingelipuka na kuruka milima yake kama mawingu isingekuwa sawa kwa ushuru ya sehemu kumi (1/10) ya mageni ya mapinduzi hayo. Ukitaka basi sikiliza kutoka ulimini mwake mifano ya sura tukufu: إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ na إِذَا السَّمَاء انفَطَرَتْ na الْقَارِعَةُ Na vilevile anatoa habari kwa ukweli kuhusu mustakabali, sio mustakabali wa dunia kwa mnasaba wake yeye isipokuwa kama tone la mazigazi pasipo na manufaa kulingana na bahari bila ya pwani. Na vile vile anabashiri kwa ushahidi wa furaha, furaha ya dunia sio chochote kulinganisha na hiyo isipokuwa kama umeta wenye kuondoka kulingana na jua la milele.
Hakika chini ya pazia za viumbe hivi - vyenye maajabu na siri - yanatusubiri mambo ya ajabu mno. Hapana budi kutoa habari ya maajabu hayo na mambo ya kufurutu ada kutoka kwa mtu wa ajabu mwenye kufurutu ada anatazamiwa kutokana na hali zake kwamba yeye anashuhudia kisha anatoa ushahidi, na anaona kisha anaeleza. Naam, tunashuhudia katika mambo yake na hatua zake kwamba anashuhudia kisha anatoa ushahidi basi anaonya na kubashiri. Na vilevile anaelezea kuhusu yanayomridhisha Mola Mlezi wa walimwengu - ambaye ametufunika kwa neema zake za dhahiri na ndani – na matilaba yake kwetu na kama hivi. Basi majuto yaliyoje kwa wenye kughafilika! Ee. Hasara juu ya wapotevu! Na ajabu iliyoje kutokana na upumbavu wa wengi wa watu! Vipi wamejifanya upofu na kujiweka mbali na haki hii na kujifanya viziwi kunako hakika hii? Hawatilii umuhimu maneno ya Nabii huyu mkarimu kutolewa fidia roho kwa ajili yake (s.a.w) pamoja na kuwa katika hali ya mfano wake na kuendewa kwa haraka kwa kuacha dunia na vilivyomo?
Jua hakika ya Nabii huyu Mkarimu (s.a.w) aliyeshuhudiwa kwetu kwa haiba yake ya kimaanawy, mashuhuri ulimwenguni kwa mambo yake ya hali ya juu, kama alivyo kuwa yeye ni hoja yenye kutamka ya kweli juu ya upweke, na dalili ya haki kwa daraja ya hali ya haki ya Tawhidi, vile vile yeye ni hoja yenye kukinaisha na dalili yenye kumulika juu ya furaha ya milele, bali kama yeye alivyo kwa ulingano wake na kwa mwongozo wake ni sababu ya kupata furaha ya milele na njia ya kuifikia, kadhalika kwa maombi yake na uja wake ni sababu ya kupata furaha hiyo ya milele na njia ya kuifanya iwepo. Na kwa mnasaba wa makamo (hapa) tunarejea siri hii ambayo imepatikana katika mjadala wa ufufuo. Ukitaka mtazame naye akiwa katika swala kuu, ambayo kwa adhama ya ukunjufu wake imekigeuza kisiwa hiki bali Ardhi ni vyenye kuswali swala hiyo kubwa. Kisha tazama hakika yeye anaswali swala hiyo na jamaa hii kubwa, kwa kiasi kwamba kana kwamba yeye ni Imamu katika mihirabu ya zama zake na wamejipanga safu nyuma yake, wakimfuata wote wa bora wa wanadamu, tangu Adamu (a.s) hadi zama hizi hadi mwisho wa dunia katika safu za zama wakiwa maamuma kwake na kuitikia amina kwa dua yake. Kisha sikiliza akifanyacho katika swala hiyo na jamaa hiyo. Ni huyu hapa anaomba kwa haja kali kubwa ya jumla kiasi ambacho wanashiriki pamoja naye katika dua yake Ardhi bali mbingu bali vyote vilivyomo, wanasema kwa ndimi za hali: Naam ewe Mola wetu Mlezi kubali dua yake, nasi pia bali pamoja na yote yaliyodhihiri juu yetu katika majina yako tunataka yatokee anayotaka yeye. Kisha tazama katika hatua zake katika mtindo wa unyenyekevu wake vipi anaomba kwa unyenyekevu, kwa uhitaji mkubwa, katika shauku kali, huzuni ya kina, na katika hali ya upenzi yenye huzuni, kiasi anahemua kilio cha viumbe anaviliza na vinashirikiana naye katika maombi. Kisha tazama ananyenyekea kwa makusudio na shabaha ipi? Huyu anaomba kwa makusudio bila ya kupatikana kwa makusudio hayo Mwanadamu angeanguka, bali ulimwengu, bali viumbe wote na kuwa chini ya walio chini havina thamani wala maana. Na kwa maombi yake vilivyomo vinapanda katika makamo ya makamilifu yake. Kisha tazama namna anavyonyenyekea kwa kuomba msaada mkubwa, katika usaidizi mkubwa, katika kuomba huruma kwa kujipendekeza kwa huzuni, kiasi cha kuisikilizisha Arshi na mbingu na kuamsha hisia yake ya ndani, hata kana kwamba Arshi na mbingu zinasema: Amin ewe Mola amin. Kisha tazama: Anatafuta mahitaji yake kutoka kwa nani, Naam! Anatafuta kutoka kwa Mweza wa kila kitu, mwenye kusikia kila kitu, Mkarimu, Mjuzi wa kila kitu, mwenye kuona kila kitu na Mwenye kurehemu, ambaye anasikia dua iliyojificha mno kutoka kwa hayawani aliyejificha mno katika haja iliyojificha mno, wakati ambapo anamjibu kwa kukidhi haja yake kwa kushuhudia, na vivyo hivyo anaona matarajio ya chini mno kwa wa chini mno wa mwenye uhai katika kusudi la chini mno, kwa namna asiyotazamia kwa kushuhudia, na anakirimu na kurehemu kwa sura ya hekima, na kwa mtindo uliopangika. Haibakii shaka kwamba malezi haya na uendeshaji huu ni kutoka kwa Msikivu wa kila kitu Mjuzi wa kila jambo na kutoka kwa mwenye kuona kila kitu mwingi wa hekima.
Basi ee ajabu iliyoje! Anachoomba huyu ambaye amesimama juu ya Ardhi, na amekusanya nyuma yake wa bora wote wa kibinadamu na ameinua mikono yake miwili kuelekea Arshi tukufu anaomba dua ambayo wanaitikia amina vizito viwili (majini na watu). Na inajulikana katika mambo yake kwamba yeye ni utukufu wa aina ya Mwanadamu, na mpekee wa ulimwengu na zama, na fahari ya hivi viumbe kila wakati, na anaomba shufaa kwa majina yote matakatifu ya kiungu yenye kudhihiri katika vioo vya viumbe, bali majina hayo yanaomba na kutaka hicho hicho anachokitaka yeye, basi sikia! huyu hapa anataka kubakia, kukutana, pepo na ridhaa. Zisingekuwapo kiasi kisichohesabika miongoni mwa sababu zenye kupasisha za kutoa furaha ya milele miongoni mwa rehema na uangalizi na hekima na uadilifu wenye kushuhudiwa - ambao kuwa kwake kunasimamia rehema na uangalizi na hekima na uadilifu juu ya kuwepo Akhera na vilevile majina yote matakatifu - ambazo ni sababu zinazohitajia – sababu zenye kuihitaji Akhera, dua ya mtu huyu wa kinuru ingetosha Mola wake kumjengea pepo yeye na wana wa jinsi yake, kama anavyotuanzishia katika kila majira ya machipuo bustani zenye kupambwa kwa miujiza ya vitengenezwa vyake. Basi kama ulivyokuwa Utume wake ni sababu ya kufunguliwa kwa makazi haya ya dunia kwa ajili ya mtihani na uja, vivyo hivyo maombi yake na uja wake ni sababu ya kufunguliwa mkazi ya Akhera kwa ajili ya malipo na jaza. Basi je inayumkinika mpangilio huu wa hali ya juu kukubali, katika Rehema hii kunjufu, katika ufundi huu mzuri bila ya mapungufu, katika uzuri huu bila ya ubaya - kwa daraja ya kuwa amewatamkisha watu wa tahakiki na akili kuwa (Sio katika yamkini kuwa vema zaidi kuliko ilivyokuwa) - hakika hizi zibadilike na kuwa ubaya mno, na dhuluma ya kutisha, na babaiko kubwa. Yaani kwa kutokuja kwa Akhera? Wakati ambapo kusikia sauti ya chini zaidi kutoka kwa kiumbe wa chini mno katika haja ya chini zaidi na kuikubali kwa umuhimu uliotimia, pamoja na kutokusikia sauti na dua ya juu zaidi katika haja shadidi mno, na kutokubali mwombwaji mzuri mno, katika matumaini na matarajio mazuri mno, ni ubaya hakuna ubaya mithili yake na upungufu haulingani sawa nao upungufu wowote, hasha kisha hasha na sivyo hivyo, mithili ya uzuri huu wenye kushuhudiwa bila ya upungufu haukubali mfano wa ubaya huu mtupu. Basi ewe rafiki yangu katika utalii huu wa ajabu. Je haikutoshi ulichokiona? Ukitaka kuzunguka haiyumkiniki, lau tungebaki katika kisiwa hiki miaka mia moja tusingezunguka na wala tusingechoka kutazama fungu moja katika mafungu mia moja katika maajabu ya majukumu yake, na mageni ya shughuli zake. Basi na turudi kinyumenyume, na tutazame zama kwa zama, namna gani zama hizo zilivyoshika kijani kibichi na kuchota katika neema za zama hii? Naam, unaona kila zama maua yake yamefunguka kwa jua la zama za furaha ya mafanikio, kila zama imezaa matunda mifano ya Abu Hanifa, Al-Shafii, Abu Yazidi Al-Bistwamy, Al-Junaid, Sheikh Abdul-Qadir Al-Kaylani, Al-Imamu Al-Ghazzali na As-Shah An-Naqshabandy, Imamu Ar-Rabbany na wengine kama wao maelfu ya matunda yenye nuru kutoka katika neema ya uongofu wa huyu mtu wa kinuru. Basi na tuahirishe maelezo ya ushahidi wetu katika kurejea kwetu hadi wakati mwingine. Na tunaitakia rehema na amani juu ya dhati ile ya nuru yenye kuongoza, yenye miujiza kwa swala na salamu zinazo ashiria katika sehemu miongoni mwa miujiza yake. عَلٰى مَن۟ اُن۟زِلَ عَلَي۟هِ ال۟فُر۟قَانُ ال۟حَكٖيمُ مِنَ الرَّح۟مٰنِ الرَّحٖيمِ مِنَ ال۟عَر۟شِ ال۟عَظٖيمِ سَيِّدِنَا مُحَمَّدٍ اَل۟فُ اَل۟فِ صَلَاةٍ وَ اَل۟فُ اَل۟فِ سَلَامٍ بِعَدَدِ حَسَنَاتِ اُمَّتِهٖ ٠ عَلٰى مَن۟ بَشَّرَ بِرِسَالَتِهِ التَّو۟رٰيةُ وَ ال۟اِن۟جٖيلُ وَ الزَّبُورُ ٠ وَ بَشَّرَ بِنُبُوَّتِهِ ال۟اِر۟هَاصَاتُ وَ هَوَاتِفُ ال۟جِنِّ وَ اَو۟لِيَاءُ ال۟اِن۟سِ وَ كَوَاهِنُ ال۟بَشَرِ ٠ وَ ان۟شَقَّ بِاِشَارَتِهِ ال۟قَمَرُ ٠ سَيِّدِنَا مُحَمَّدٍ اَل۟فُ اَل۟فِ صَلَاةٍ وَ سَلَامٍ بِعَدَدِ اَن۟فَاسِ اُمَّتِهٖ ٠ عَلٰى مَن۟ جَائَت۟ لِدَع۟وَتِهِ الشَّجَرُ وَ نَزَلَ سُر۟عَةً بِدُعَائِهِ ال۟مَطَرُ وَ اَظَلَّت۟هُ ال۟غَمَامَةُ مِنَ ال۟حَرِّ وَ شَبَعَ مِن۟ صَاعٍ مِن۟ طَعَامِهٖ مِأَتٌ مِنَ ال۟بَشَرِ وَ نَبَعَ ال۟مَاءُ مِن۟ بَي۟نِ اَصَابِعِهٖ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ كَال۟كَو۟ثَرِ وَ اَن۟طَقَ اللّٰهُ لَهُ الضَّبَّ وَ الظَّب۟ىَ وَ ال۟جِذ۟عَ وَ الذِّرَاعَ وَ ال۟جَمَلَ وَ ال۟جَبَلَ وَ ال۟حَجَرَ وَ ال۟مَدَرَ صَاحِبِ ال۟مِع۟رَاجِ وَ مَازَاغَ ال۟بَصَرُ ٠ سَيِّدِنَا وَ شَفٖيعِنَا مُحَمَّدٍ اَل۟فُ اَل۟فِ صَلَاةٍ وَ سَلَامٍ بِعَدَدِ كُلِّ ال۟حُرُوفِ ال۟مُتَشَكِّلَةِ فِى ال۟كَلِمَاتِ ال۟مُتَمَثِّلَةِ بِاِذ۟نِ الرَّح۟مٰنِ فٖى مَرَايَا تَمَوُّجَاتِ ال۟هَوَاءِ عِن۟دَ قِرَائَةِ كُلِّ كَلِمَةٍ مِنَ ال۟قُر۟اٰنِ مِن۟ كُلِّ قَارِءٍ مِن۟ اَوَّلِ النُّزُولِ اِلٰى اٰخِرِ الزَّمَانِ وَ اغ۟فِر۟لَنَا وَ ار۟حَم۟نَا يَا اِلٰهَنَا بِكُلِّ صَلَاةٍ مِن۟هَا اٰمٖينَ [Jua: Hakika ya dalili za Utume wa Muhammad hazihesabiki wala haziwekewi mipaka, hakika wametunga katika kuzibainisha wakubwa wa wahakiki. Nami pamoja na kushindwa kwangu na upungufu wangu nimebainisha mionzi kutoka katika jua katika Risala ya Kituruki inaitwa (Mionzi ya kumtambua Mtume (s.a.w)) na katika (Andiko la kumi na tisa). Na vilevile nimebainisha kwa muhtasari pande za hali ya muujiza wa miujiza yake mikubwa - yaani Qur’an - na nimeashiria kwa ufahamu wangu wa upungufu pande arobaini katika pande za hali ya muujiza ya Qur’an katika Risala ya (Ming’ao), na nimebainisha katika pande hizo upande mmoja nao ni balagha ya hali ya juu ya kiutungo katika kiasi cha kurasa arobaini katika tafsiri yangu ya Kiarabu iitwayo (Ishaaraat Al-Iijaz). Ukitaka basi rejea katika vitabu hivi vitatu.]
Jua! kwamba Qur’an tukufu ni bahari ya miujiza na muujiza mkuu inathibitisha Utume wa Muhammad na upweke wa kiungu kwa kuthibitisha, na inasimamisha hoja na kutoa ushahidi na kudhihirisha dalili inatosheleza kuliko hoja yoyote nyingine. Hapa sisi tutaashiria ainisho lake, kisha tutaashiria katika ming’ao kutoka katika hali yake ya muujiza ambayo imeamsha masuala kwa baadhi. Basi Qur’an ya hekima ambaye inamtambulisha Bwana wetu Mlezi kwetu: Ni ukalimani wa Azali wa viumbe hivi na mkalimani wa milele wa ndimi zake zenye kusoma aya za kimaumbile, na mfasiri wa kitabu cha ulimwengu. Na vivyo hivyo ni mmulikaji wa vilivyofichikana vya hazina za majina yaliyositirika katika kurasa za mbingu na Ardhi. Na vilevile ni ufunguo wa hakika ya mambo yaliyodhamiriwa katika mistari ya vyenye kuzuka, vilevile ni ulimi wa ghaibu katika ulimwengu wa kushuhudia, vilevile ni hazina ya maongezi ya kiazali ya kusubuhana na mikengeuko ya milele ya mwingi wa Rehema, vilevile ni misingi na uhandisi na jua la ulimwengu huu wa kimaanawy wa Kiislamu, vilevile ni ramani ya ulimwengu wa kiakhera, vilevile ni kauli ya kusherehesha na tafsiri ya wazi na hoja ya kukinaisha na mkalimani angavu wa dhati ya Allah (s.w) na sifa zake na majina yake na mambo yake, na vilevile ni mlezi wa ulimwengu wa kibinadamu. Na kama maji na kama mwanga kwa utu mkuu ambao ni Uislamu. Na vilevile ni hekima ya kihakika ya sampuli ya wanadamu, nayo ni mwelekezi mwongozi katika waliyoumbiwa wanadamu kwa ajili yake, na vilevile kwa mwanadamu hiyo ni: Kama kilivyo kuwa ni kitabu cha sharia vile vile ni kitabu cha hekima, na kama kilivyo ni kitabu cha dua na kufanya ibada na vilevile ni kitabu cha amri na daawa, na kama kilivyo ni kitabu cha dhikiri vilevile ni kitabu cha fikira, na kama kilivyo ni kitabu kimoja lakini ndani yake kuna vitabu vingi vyenye kukabiliana na haja zote za mwanadamu za kimaanawy, na vilevile ni kama nyumba takatifu iliyosheheni vitabu na barua. Hata kwamba imedhihirisha mashrabu ya kila mmoja katika watu wa mashrabu tofauti, na kwa maslaki ya kila mmoja katika watu wa maslaki mbalimbali katika mawalii na masiddiqina na katika watambuzi na wahakiki ujumbe wenye kuwiana na vionjo vya mashrabu hiyo na kuinawirisha kwake, na kwa mielekeo ya maslaki hiyo na taswira yake hata kana kwamba ni mkusanyiko wa barua. Basi tazama katika ufafanuzi wa mng’ao wa hali ya kimiujiza katika ukariri wa Qur’an ambao wapungufu huudhania ni kasoro katika balagha. Na jua hakika ya Qur’an tukufu ni kitabu cha dhikiri, kitabu cha dua, na kitabu cha daawa, kukariri kwake kunakuwa kuzuri na kwa balagha mno bali kuna hoja yenye nguvu zaidi, na sio kama walivyodhania wenye upungufu, kwa sababu dhikiri hukaririwa, na dua hurudiwa rudiwa. Na daawa hukokotezwa. Kwa sababu katika kukariri kwa dhikiri kuna kutia nuru na katika kurudia dua kuna kutuliza na katika kukariri kwa daawa kuna kukokoteza. Na jua kwamba haiyumkiniki kwa kila mmoja katika kila wakati kusoma Qur’an yote ambayo ni dawa na ponya kwa kila mmoja katika kila wakati. Basi kwa ajili hii ameingiza mwingi wa hekima mwenye kurehemu makusudio mengi ya Qur’an katika sura zake nyingi, na hasa katika sura hizo ni zile ndefu ndefu, mpaka ikawa kila sura ni Qur’an ndogo, akarahisisha njia kwa kila mmoja, bila ya kumnyima yeyote, basi akakariri Tawhidi, ufufuo na kisa cha Musa (a.s). Jua! Hakika kama ilivyo kwamba haja za kimwili ni zenye kutofautiana katika nyakati, vivyo hivyo haja za kimaanawy za kibinadamu vile vile ni zenye kutofautiana nyakati. Basi sehemu kila wakati (هُوَ اللهُ) kwa ajili ya roho - kama haja ya mwili kuhitajia hewa. Na sehemu kila saa kama (بِسْمِ اللهُ) na kama hivi basi pimia. Basi kukariri kwa aya na maneno kwa hiyo ni kwa ajili ya kujulisha kukariri kwa uhitaji, na kwa ajili ya kuashiria kushitadi kwa uhitaji wa aya hizo, na kwa ajili ya kuutanabahisha mshipa wa uhitaji na kuuamsha, na kwa ajili ya kutia shauku juu ya uhitaji, na kwa ajili ya kutikisa hamu ya uhitaji wa vyakula hivyo vya kimaanawy. Jua! Hakika Qur’an ni muasisi wa Dini hii tukufu madhubuti, na misingi ya huu Ulimwengu wa Kiislamu, na mpinduaji wa mambo ya kijamii ya wanadamu na mgeuzaji wake na mbadilishaji wake. Na jawabu la yenye kukaririwa ya maswali ya tabaka mbalimbali ya wanadamu kwa ndimi za kauli na hali. Na hapana budi kwa mwasisi kukariri ili kuweka ithibati, na kurudia rudia ili kukokoteza, na kukariri ili kutuliza na kuunga mkono. Jua! Hakika Qur’an inajadili maswala makuu na inaziita nyoyo katika kuyaamini, na kuhusu hakika nyeti na inaziita akili katika kuzitambua. Basi hapana budi kuyatuliza katika nyoyo na kuyathibitisha katika fikira za watu jumla kutokana na kukariri katika sura mbalimbali na mitindo anuwai. Jua! Hakika kila aya ina nje na ndani na mpaka na matlai, na kila kisa kina pande (mbalimbali), hukumu, faida na makusudio, basi hutajwa katika mahali upande fulani, na pengine upande mwingine, na katika sura makusudio fulani na katika nyingine makusudio mengine na kama hivi. Na kwa hivi hakuna kukariri isipokuwa katika sura (picha ya mwonekano tu). Ama kujumuisha kwa Qur’an tukufu baadhi ya maswala ya kiulimwengu na kuyaficha baadhi nyingine hakika huo ni mng’ao wa hali ya kimuujiza wenye kuangaza na sio kama walivyodhania watu wa ukanaji mungu kuwa kasoro yoyote wala sio eneo la kukosoa. Ukisema: Kwa nini Qur’an haijadili kuhusu viumbe kama inavyojadili fani ya hekima na falsafa? Hivyo inaacha baadhi ya mswali hali ya ujumla na mengine inayaeleza maelezo yanayowiana na utambuzi wa watu wa kawaida na fikira zao haiyagusi kwa udhia wala kuyachosha bali inayaeleza kwa urari rahisi katika dhahiri? Kujibu Tunasema: Kwa kuwa falsafa imeacha njia ya hakika na kupotea mbali nayo, na kwa vyovyote umekwisha kufahamu kutokana na masomo na maneno yaliyotangulia kwamba Qur’an tukufu hakika inajadili kuhusu viumbe kwa kuchuchia, ili kutoa dalili juu ya dhati ya Allah na sifa zake na majina yake mazuri, yaani inafahamisha maana ya kitabu hiki, kitabu kikubwa cha ulimwengu ili imtambulishe Muumba wake. Yaani hakika Qur’an tukufu inatumia vilivyomo kwa (Kufahamisha juu ya) muumba wake na sio kwa nafsi yake (Hivyo vitu vyenyewe) ukiachilia mbali kuwa inasemesha kundi la watu wengi. Na kwa hivi, maadamu Qur’an inatumia vyenye uwepo kuwa ni dalili na hoja, basi miongoni mwa sharti la dalili iwe dhahiri na dhahiri zaidi kuliko tija mbele ya mtazamo wa watu wengi. Kisha hakika Qur’an maadam ni mwelekezi basi katika hali ya balagha ya uelekezi ni kuendana na mtazamo wa watu wa kawaida, na kuchunga hisia za watu jumla na kuliwaza fikira ya watu, mawazo yao yasipate upweke pasipo na faida na fikira yao isiingie mshawasha pasipo faida, na hisia zao zisitangetange bila masilahi, basi maneno yaliyo ya balagha na watu hao na uelekezi yawe ya dhahiri rahisi mepesi hayawashindi, muhtasari hayawachoshi, yenye kujumuishwa katika yale yasiyolazimu maelezo kwao, na yanapiga mifano ili kuyakurubisha katika fahamu yao yale yaliyokuwa nyeti. Na kwa kuwa Qur’an ni mwelekezi wa tabaka zote za wanadamu balagha ya uelekezi inalazimu isitaje yanayowaingiza wengi katika makosa na kufanya kiburi pamoja na mambo yaliyokuwa wazi katika mtazamo wao wa dhahiri, na isigeuze kile kinachojulikana kwa watu wote na kuhisiwa kwao bila ya ulazima wowote, na kupuuza au kufupisha yasiyo lazima kwao katika jukumu lao la asili. Kwa mfano: Inajadili kuhusu jua sio kwa ajili ya jua, wala sio kuhusu ainisho lake, bali kwa yule aliyelitia nuru na kulijaalia kuwa ni taa, na kuhusu kazi yake kwa kulifanya kuwa ni mhimili wa kupangika kwa ufundi na kituo kikuu cha mfumo wa uumbaji, na kupangika na mpangilio si kingine isipokuwa ni vioo vya kumtambua mtengenezaji Mtukufu. Basi Qur’an inatujulisha kwa kuonesha mfumo wa usukaji na kupangika kwa vyenye kusukwa na makamilifu ya muumbaji wake Mwingi wa hekima na mtengenezaji wake mjuzi wa kila kitu, basi anasema: وَالشَّمْسُ تَجْرِي na inafahamisha kwalo na kutanabahisha matendo ya uweza wa kiungu mkubwa katika kuhitilafiana kwa usiku na mchana na kufuatana kwa majira ya joto na machipuo. Na katika kugeuzisha macho kulielekea ni kutanabahisha msikiaji katika adhama ya uweza wa mtengenezaji na upweke wake katika uungu wake Bwana Mlezi. Basi vyovyote iwavyo hakika ya kutembea kwa jua na kwa sura yoyote iwayo hakika hiyo haiathiri katika makusudio ya Qur’an katika kuonesha mpangilio unaoshuhudiwa na wenye kufumwa pamoja. Na vilevile anasema: وَجَعَلَ الشَّمْسَ سِرَاجًا katika ibara ya taa ni kuupa ulimwengu sura ya kasri, na kuvipa sura vitu vilivyomo ndani yake katika sura ya vyenye kulazimu kasri hiyo, mapambo yake, na vyakula vyake kwa ajili ya wakazi wa kasri na wasafiri wake, na kuleta hisia kuwa vitu hivyo umeviandaa kwa ajili ya wageni wake na wahudumu wake mkono wa Mkarimu sana mwenye kurehemu. Na jua sio chochote isipokuwa ni lenye kuamrishwa lenye kutiishwa na ni taa yenye kutiwa nuru. Basi katika ibara ya taa kuna tanbihi ya rehema ya Muumba katika adhama ya Uungu wake Bwana Mlezi, na kufahamisha hisani yake katika ukunjufu wa rehema zake, na kutia hisia ya ukarimu wake katika adhama ya ufalme wake. Basi sasa hebu sikiliza anasema nini mwanafalsafa mwenye porojo kuhusu jua. Amesema: (Ni dude kubwa kutokana na uji wa moto unaozunguka wenyewe mahali pake, kutokana na moto huo vimeruka vicheche navyo ni Ardhi yetu na sayari nyingine basi madude haya makubwa mbalimbali katika ukubwa hivi.. ainisho lake kama hivi..) Tazama suala hili limekupa faida gani isipokuwa tahayuri yenye kushangaza na mshangao wenye kuogofya, haikukupa faida ya ukamilifu wa kielimu wala kionjo cha kiroho wala lengo la kiutu wala faida ya kidini. Basi pimia jambo hili uweze kukadiria thamani ya masuala ya kifalsafa ambayo nje yake yamepambwa na ndani yake kuna ujinga mtupu. Basi kusikudanganye kumeta meta nje yake ukapuuza ubainifu wa Qur’an ya miujiza.
Hakika tumeeleza katika Al-Mathnawy Al-Araby aina kumi na tano katika aina za hali ya muujiza wa Qur’an inayofikia aina arobaini nayo ni katika matone sita katika kitone cha kumi na nne, na hasa nukta nyeti sita za tone la nne. Kwa ajili hiyo tumefupisha hapa kwa kutosheka na tuliyoyaeleza huko. Basi mwenye kutaka na ayarejelee. اَللّٰهُمَّ اج۟عَلِ ال۟قُر۟اٰنَ شِفَاءً لَنَا مِن۟ كُلِّ دَاءٍ وَ مُونِسًا لَنَا فٖى حَيَاتِنَا وَ بَع۟دَ مَمَاتِنَا وَ فِى الدُّن۟يَا قَرٖينًا وَ فِى ال۟قَب۟رِ مُونِسًا وَ فِى ال۟قِيَامَةِ شَفٖيعًا وَ عَلَى الصِّرَاطِ نُورًا وَ مِنَ النَّارِ سِت۟رًا وَ حِجَابًا وَ فِى ال۟جَنَّةِ رَفٖيقًا وَ اِلَى ال۟خَي۟رَاتِ كُلِّهَا دَلٖيلًا وَ اِمَامًا بِفَض۟لِكَ وَ جُودِكَ وَ كَرَمِكَ وَ رَح۟مَتِكَ يَا اَك۟رَمَ ال۟اَك۟رَمٖينَ وَ يَا اَر۟حَمَ الرَّاحِمٖينَ اٰمٖينَ اَللّٰهُمَّ صَلِّ وَ سَلِّم۟ عَلٰى مَن۟ اُن۟زِلَ عَلَي۟هِ ال۟فُر۟قَانُ ال۟حَكٖيمُ وَ عَلٰى اٰلِهٖ وَ صَح۟بِهٖ اَج۟مَعٖينَ اٰمٖينَ اٰمٖينَ اَل۟بَاقٖى هُوَ ال۟بَاقٖى Said Nursî
NYONGEZA Neno La Kumi Na Tisa Na Thelathini Na Moja بِسْمِ اللّٰهِ الرَّحْمٰنِ الرَّح۪يمِ اِق۟تَرَبَتِ السَّاعَةُ وَ ان۟شَقَّ ال۟قَمَرُ وَاِن۟ يَرَو۟ا اٰيَةً يُع۟رِضُوا وَ يَقُولُوا سِح۟رٌ مُس۟تَمِرٌّ Hakika ya wanafalsafa wa kimaada, na wanaowaiga uigaji wa upofu, wanataka kufuta na kuzima muujiza wa kupasuka kwa mwezi wenye kuangaza kama mwezi, basi wanaamsha dhana mbovu kuhusu suala hili, ambapo wanasema: (Kupasuka kungekuwa kumetokea kiukweli basi ulimwengu ungelijua, na vitabu vyote vya historia vingelitaja hilo!). Jibu: Hakika kupasuka kwa mwezi ni muujiza wa kuthibitisha Utume, umetokea mbele ya wale ambao wamesikia madai ya Utume na wakayakanusha, na umetokea usiku, katika wakati ambao umeenea mghafala, na umedhihirishwa kwa muda mfupi sana, ukiachilia mbali kwamba kuhitilafiana kwa matlai na kuwepo kwa mawingu na mfano wa hivyo katika vizuizi vinayozuia mwezi kuonekana. Hali ya kujua kwamba kazi za kutafuta mwezi na nyenzo za kimaendeleo wakati ule hazikuwa zimeenea, kwa hiyo hailazimu watu wote kuona kupasuka mwezi katika kila mahali, na hailazimu pia kuingia katika vitabu vya historia. Basi sasa sikiliza nukta tano tu kati ya nyingi miongoni mwake, kwa idhini ya Allah zitatokomeza mawingu ya dhana ambayo yamegubika juu ya uso wa muujiza huu wa wazi.
Hakika ukaidi wa makafiri katika zama zile unajulika na ni mashuhuri kihistoria, basi wakati Qur’an tukufu ilipotangaza: ﴾ وَانشَقَّ الْقَمَرُ ﴿ na mwangwi wake ukafika kwenye anga, hakuthubutu yeyote katika makafiri, nao wanapinga Qur’an, kukadhibisha aya hii tukufu. Yaani kukana kutokea kwa tukio. Kwani kama isingekuwa tukio hilo limetokea kiukweli katika wakati ule, na halikuwa lenye kuthibiti kwa wale makafiri, wangejitokeza kwa nguvu ili kubatilisha madai ya Utume, na wangemkadhibisha Mtume (s.a.w). Wakati ambapo vitabu vya historia na sira havikunakili chochote katika kauli za makafiri kuhusu kukanusha kwao kutokea kwa kupasuka kwa mwezi, isipokuwa yaliyobainishwa na aya tukufu: ﴾ وَيقُولُوا سِحْرٌ مُّسْتَمِرٌّ ﴿. Nayo ni kwamba wale ambao wameshuhudia muujiza ule katika makafiri wamesema: Huu ni uchawi ebu tumeni kwa watu wa anga mpaka kutazama je wameona au hapana?. Na ilipofika asubuhi misafara imefika kutokea Yemen na kwingine wakawauliza, wakawaeleza kwamba wao wameona mithili ya hivyo. Wakasema: Hakika uchawi wa yatima wa Abi Talib umefika mbinguni!
Hakika wamesema walio wengi wa maimamu wa elimu ya Al-Kalamu, katika mfano Saad At-Taftazany: (Hakika kupasuka kwa mwezi ni Mutawatir, mfano wa kutoka kwa maji kati ya vidole vyake vitukufu (s.a.w) na kunywa jeshi maji hayo, na mfano wa manung’uniko ya kishina kutokana na kutengana naye (s.a.w) alichokuwa anaegemea wakati wa hotuba, na kundi la watu wa msikitini kusikia masikitiko yake. Yaani tukio wamelinakili kundi kubwa la watu kutoka kwa kundi kubwa ni muhali kwao kuupokea uongo, kwa hiyo tukio ni mutawatir kwa kukata shauri kama kudhihiri kwa kimondo kabla ya miaka elfu moja na kama kuwepo kwa kisiwa cha Serandibu ambacho hatujakiona). Na kama hivi hakika ya kuamsha shaka kuhusu suala hili la kukinaisha na mifano yake katika masuala yenye kushuhudiwa ushahidi wa macho wazi wazi hakika ni uzuzu na upumbavu, kwa sababu yatosha katika hayo kwamba ni katika yamkini na sio muhali. Kwa kujua kwamba kupasuka kwa mwezi ni jambo la yamkini kama kupasuka kwa mlima kwa volkeno.
Hakika ya muujiza huja kwa ajili ya kuthibitisha madai ya Utume kwa njia ya kuwakinaisha wakanushaji, na sio kuwalazimisha kuamini. Kwa hiyo inalazimu kuudhihirisha kwa wale ambao waliosikia madai ya Utume, ambayo yatawafikisha katika kukinai na kutulia katika ukweli wa Utume. Ama kudhihirisha mahali pote, au kuudhihirisha kwa udhihirisho wa wazi kiasi watu walazimike kukubali na kutii hilo linapingana na hekima ya Allah (s.w), na vilevile ni lenye kuhalifu siri ya takilifu ya kiungu. Na hiyo ni kwa sababu siri ya takilifu ya kiungu inahitajia kufungua nafasi kwa akili na sio kuipokonya hiari. Ingekuwa muumba mtukufu ameacha muujiza wa kupasuka mwezi ni wenye kubaki muda wa saa mbili, na kuudhihirisha kwa ulimwengu wote na kuingia ndani ya historia kama wanavyoutaka wanafalsafa makafiri wangekuwa wanasema hakika hilo ni tukio la kifalaki la kawaida. Na isingekuwa hoja juu ya ukweli wa Utume, wala muujiza unaomhusu Mtume mtukufu (s.a.w). Au ingekuwa unageuka ni muujiza wa wazi unalazimisha akili kuamini na kuipokonya hiari, na wakati huo zitakuwa sawa roho za chini kama mkaa duni mfano wa Abi Jahl, pamoja na roho za hadhi ya juu safi kama almasi na roho za juu mfano wa Abu Bakar As-Siddiq (r.a) yaani ingekuwa inapotea siri ya takilifu ya kiungu. Na kwa ajili hii muujiza ulitokea kwa punde tu, usiku, na wakati mghafala unaenea, na kuwa tofauti za matlai na mawingu na mfano wake ni vizuizi mbele ya watu kuuona. Na haukuingia ndani ya vitabu vya historia.
Hakika ya muujiza huu ambao umetokea usiku, na punde, na katika wakati wa kughafilika, hawauoni watu wote bila shaka kila mahali. Bali hata ungedhihiri kwa baadhi yao, asingesadiki jicho lake, hata kama amesadiki, hakika tukio kama hili limepokewa kutoka kwa mtu mmoja halina thamani kwa historia. Hakika wamejibu wanazuoni wahakiki kilichozidishwa katika mapokezi ya muujiza kwamba mwezi baada ya kupasuka kwake ulishuka Ardhini! Wamesema: Huenda ziada hii wameiingiza baadhi ya wanafiki ili wayadondoshe thamani ya mapokezi na kutweza hadhi yake. Kisha katika wakati huo mawingu ya ujinga yalikuwa yamegubika anga la Uingereza, na wakati unakaribia magharibi Hispania, na Marekani katika mwanga wa mchana, na asubuhi imekwisha kupambazuka huko China na Japani. Na katika miji mingine kuna vizuizi vingine vya kuona. Muujiza huu mkubwa haushuhudiwi huko. Basi ukijua hili zingatia maneno ya ambaye anasema: (Hakika historia ya Uingereza, China, Japani, Marekani na mfano wa nchi kama hizo hazitaji tukio hili, kwa hiyo halikutokea!). Ni mzaha wa namna gani huu. Ee maangamizo kwa wale wanaokula makombo ya Ulaya.
Hakika kupasuka kwa mwezi sio tukio lililotokea lenyewe, kwa misingi ya sababu za kiasili na kwa njia ya sadfa! Bali amelitukisha Muumba mwingi wa hekima, Bwana Mlezi wa jua na mwezi, lilikuwa ni tukio lenye kufurutu kanuni za kimaumbile, kwa kusadikisha Utume wa Mtume wake kipenzi (s.a.w), na kutangaza kuhusu ukweli wa madai yake, basi Allah (s.w) akaudhihirisha kulingana na hekima yake na kwa muktadha wa siri ya uelekezi na takilifu na hekima ya kufikisha ujumbe, na ili asimamishe hoja kwa anayemtaka katika wenye kushuhudia, wakati ambapo ameuficha kulingana na hitajio la hekima yake (s.w) na matakwa yake, kwa wale ambao haikuwafikia daawa ya Mtume (s.a.w) katika wakazi wa nchi za ulimwengu, na ameuzuilia kwao kwa mawingu na kutofutiana kwa matlai na kutochomoza kwa mwezi, au kuchomoza kwa jua katika baadhi ya nchi na kudhihiri kwa mchana katika nyingine, na kuzama jua kwingine, na mfano wa hizo miongoni mwa sababu zinazopelekea kuzuilika kuona kupasuka kwa mwezi. Muujiza ungedhihirishwa kwa watu wote ulimwenguni kote, basi ungekuwa unadhihiri kwao ikiwa ni matokeo ya ishara ya Mtume (s.a.w) na kuonesha muujiza wa Mtume, na wakati huo ungefika katika hali ya uwazi, yaani watu wote wangelazimika kusadiki, yaani wangenyang’anywa hiari, basi ingepotea siri ya takilifu wakati ambao Imani inahifadhi uhuru wa akili katika kuchagua wala haiunyang’anyi. Au ingetokea kwao kama tukio tupu la mbinguni, na hapo uhusiano wake na Utume wa Muhammad ungekatika na usingebakia na sifa maalum. Muhtasari: Hakika kupasuka kwa mwezi hakuna shaka ndani yake. Kumethibitishwa uthibitisho wa kukinaisha. Na hapa tutaashiria kutokea kwake kwa hoja sita za kukinaisha kati ya nyingi, nazo: Ijmai ya sahaba wema (r.a) nao ni waadilifu. Na kuafikiana wanazuoni wahakiki katika wafasiri mbele ya tafsiri yao. ﴾ وَانشَقَّ الْقَمَرُ ﴿ Na kunakili kwa wataalamu wa Hadithi wote wa kweli katika mapokezi yao kutokea kwake kwa isinadi na njia nyingi. Na kushuhudia watu wote wa kufunuliwa na ilhamu miongoni mwa mawalii wa kweli wema. Na kusadikisha maimamu wa elimu ya Al-Kalamu waliobobea licha ya kutofautiana maslaki na mashrabu zao. Na kukubali kwa umma ambao hauungani katika upotevu kama ilivyoeleza hilo nasi ya Hadithi sharifu. Yote hayo yanabainisha kupasuka kwa mwezi na kuuthibitisha kwa uthibitisho wa kukinaisha unalingana na jua katika uwazi wake. Hitimisho: Somo hadi hapa lilikuwa kwa jina la tahakiki ya kielimu, kumlazimisha hasimu (kwa nguvu ya hoja). Ama baada ya hapa maneno yatakuwa kwa jina la hakika na kwa ajili ya Imani. Tahakiki ya kielimu imekwisha kutamka namna hii. Ama hakika inasema: Hakika mwisho wa diwani ya Utume (s.a.w) naye ni mwezi wenye nuru kwa mbingu ya Utume, na uko juu uwalii wa uja wake hadi ngazi ya hali ya kupendwa, basi amedhihirisha karama kubwa na muujiza mkuu kwa Miiraji. Yaani kwa kutembea kwa mwili wa ardhini katika anga za mbingu za juu, na kumtambulisha yeye wakazi wa Mbinguni, nimethibitisha kwa muujiza huo uwalii wake mkuu kwa Allah na U-kipenzi wake wa dhati kwake na nafasi yake ya juu ya watu wa mbingu na hadhara tukufu. Vilevile Allah (s.w) amepasua mwezi ulioangikwa mbinguni na wenye kufungana na ardhi kwa ishara kutoka kwa mja wake ardhini, basi akadhihirisha muujiza wake huu, ili kumthibitisha mja huyo kipenzi, hata akawa (s.a.w) kama vipande viwili vyenye nuru kwa mwezi, akapazwa katika vilele vya makamilifu kwa mbawa mbili za Uwalii na Utume zenye nuru. Hata akafika usawa wa pinde mbili au karibu mno akiwa ni fahari kwa wakazi wa mbinguni kama alivyo fahari kwa wakazi wa ardhi. عَلَي۟هِ وَ عَلٰى اٰلِهِ الصَّلَاةُ وَ التَّس۟لٖيمَاتُ مِل۟أَ ال۟اَر۟ضِ وَ السَّمٰوَاتِ سُب۟حَانَكَ لَا عِل۟مَ لَنَٓا اِلَّا مَا عَلَّم۟تَنَٓا اِنَّكَ اَن۟تَ ال۟عَلٖيمُ ال۟حَكٖيمُ
[Somo hili liliandikwa - ndani ya masomo ya dalili za Utume wa Muhammad - likiwa ni jibu la swali lililopatikana katika mushkeli wa kwanza kutoka katika mishkeli mitatu muhimu iliyopatikana mwishoni mwa msingi wa tatu katika Risala ya Miiraji, hiyo ni sawa na faharisi fupi.]. Swali: Kwa nini amehusishwa Muhammad (s.a.w) kwa hii Miiraji tukufu? Jibu: Hakika mushkeli wenu huu wa kwanza, umetatuliwa kwa maelezo katika maneno thelathini na tatu ndani ya kitabu cha (Maneno), isipokuwa hapa tutaashiria kiasi tu cha ishara ya jumla kwa sura ya faharisi ya muhtasari makamilifu ya Mtume (s.a.w), na dalili za Utume wake, na kwamba yeye ndiye mwenye kustahiki mno kwa Miiraji hii tukufu. Kwanza: Hakika vitabu vitakatifu, Taurati, Injili na Zaburi vinajumuisha bishara za Utume wake (s.a.w) na kumwashiria yeye, pamoja na kukutana na upotoshaji kwenye zama mbalimbali. Na katika zama zetu hizi huyu mwanazuoni mhakiki Husein Al-Jisri ametoa bishara mia moja na kumi kutoka katika vitabu hivyo, na akazithibitisha katika kitabu chake kilichoitwa (Ar-Risaalat Al-Hamiidiyyat). Pili: Hakika ni jambo lenye kuthibiti kihistoria, Na limepokewa kwa mapokezi sahihi, bishara nyingi ambazo makuhani wamezibashiri mfano wa makuhani wawili mashuhuri: Shiq na Satih, mbele punde ya kupewa kwake Utume (s.a.w) na wameeleza kwamba yeye ni nabii wa aheri ya zama. Tatu: Yaliyotokea usiku wa mazazi yake (s.a.w) ikiwemo kudondoka kwa masanamu ndani ya Al-Kaaba na kupasuka kwa vibaraza vya Kisra na mfano wake katika mamia ya Irhasaati na mambo ya kufurutu ada yaliyokuwa mashuhuri katika vitabu vya historia. Nne: Kutoka maji kati ya vidole vyake vitukufu na kulinywesha jeshi kwa maji hayo, na kulia kwa kishina cha mtende kikavu kilichokuwapo ndani ya msikiti wa Mtume (s.a.w) kwa Mtume wa Allah (s.a.w) kwa ajili ya kutengana naye na kulia kwake mbele ya kundi kubwa la sahaba wema na kupasuka mwezi kama aya tukufu ilivyoeleza hilo: ﴾ وَانشَقَّ الْقَمَرُ ﴿ na mfano wake katika miujiza iliyothibiti mbele ya wanazuoni wahakiki na ambayo inafika elfu moja vimethibitisha vitabu vya sira na historia. Tano: Wameafikiana maadui na marafiki jambo lisilo na shaka ndani yake kwamba tabia alizopambika nazo Mtume (s.a.w) katika tabia njema ni katika ngazi za juu sana, na kwamba sifa anazosifika nazo katika daawa yake ni katika ngazi za juu sana, miamala yake na watu na nyendo zake pamoja na watu zinashuhudia hayo. Na kwamba sharia yake angavu inajumuisha mazuri yaliyokamilika mno, yanashuhudia hilo matendo ya tabia njema katika dini yake nyoofu. Sita: Hakika tumeashiria katika ishara ya pili katika (Neno la kumi) kwamba Mtume Mtukufu (s.a.w) ndiye ambaye amedhihirisha ngazi ya juu kabisa ya uja katika dini yake kuitikia matakwa ya Allah katika kudhihiri uungu wake kwa muktadha wa hekima na ukweli. Na kwamba yeye vilevile - kama inavyo shuhudiwa - ni mjulishaji mkubwa juu ya ukamilifu wa ufundi katika uzuri wa hali zote wa mtengenezaji wa ulimwengu, na kwa daawa kubwa mno na sauti ya ulingano mno, akaitikia matakwa ya Allah (s.w) katika kuleta macho kuangalia ukamilifu wa ufundi wake na kuutangaza. Naye vilevile - kwa dharura - ni mkamilifu wa waliotangaza ngazi zote za Tawhidi, akaitikia matakwa ya Bwana Mlezi wa walimwengu katika kutangaza upweke katika tabaka za wingi wa viumbe. Naye vilevile kwa - dharura - ni kioo dhahiri na safi mno kwa kuakisi mazuri ya uzuri wa mmiliki wa ulimwengu na mapole ya uzuri wake uliotakasika - kama athari zake za kupendeza zinavyoashiria hilo - naye ndiye mbora wa aliyempenda na kumpendezesha - akaitikia matakwa yake (s.w) katika kuona uzuri huo mtakatifu na kuuonesha kwa muktadha wa hakika na hekima. Naye kadhalika - kwa uwazi - ni mkuu mno aliyetambulisha yaliomo kwenye hazina za ghaibu hazina hizo zilizojaa tele maajabu ya miujiza na johari za thamani mno, naye ni mbora aliyezitangaza na kuelezea wasifu wake, akaitikia matakwa yake Allah (s.w) katika kudhihirisha hazina zilizofichikana. Naye vilevile – kwa uwazi – ni mwelekezi mkuu wa Qur’an tukufu kwa majini na wanadamu bali kwa maruhani na Malaika, na mkuu aliyebainisha maana ya athari za mtengenezaji wa viumbe ambaye amevipamba kwa mapambo ya kupendeza mno na kuwawezesha wenye utambuzi katika viumbe wake ili watazame kwa makini na kutafakari na kuzingatia, akaitikia matakwa yake (s.w) katika kubainisha maana za athari hizo na kuzipa thamani yake kwa watu wa fikira na kushuhudia. Na yeye vile vile – kwa uwazi - ni mzuri mno aliyefunua hakika za Qur’an kuhusu maana zilizokusudiwa kutokana na mabadiliko ya viumbe na shabaha yake, na mkamilifu mno ambaye amefumbua fumbo lenye kutahayarisha katika vilivyomo. Nalo ni maswali matatu magumu: Wewe ni nani? Unatokea wapi? Na unakwenda wapi? Akaitikia matakwa yake (s.w) katika kufumbua fumbo hilo lililofumbwa kwa wenye utambuzi kupitia kwa mjumbe. Na kwamba yeye ndiye vilevile – kwa uwazi – ni mkamilifu mno aliyebainisha makusudio ya kiungu kwa Qur’an tukufu na mbora aliyeweka wazi snjia katika anayoyaridhia Bwana Mlezi wa walimwengu, akaitikia matakwa yake (s.w) katika kutambulisha anayoyataka kutoka kwa wenye utambuzi na anayoyaridhia kwao kwa kupitia kwa mjumbe, baada ya kuwa ametambulisha nafsi yake kwao kwa vitengenezwa vyake vyote vyenye kupendeza na kuvipendezesha kwao kwa neema ghali alizowaenezea. Naye vile vile – kwa uwazi – ni mkuu aliyetimiza jukumu la Utume kwa Qur’an tukufu na kulitekeleza kwa utekelezaji bora katika ngazi ya juu na upeo wa sura na mtindo bora, akaitikia matakwa ya Bwana Mlezi wa walimwengu, katika kugeuza uso wa mwanadamu huyu kutoka katika wingi kwenda katika umoja na kutoka katika chenye kutoweka na kwenda kwenye chenye kubaki, mwanadamu huyo ambaye Allah (s.w) amemuumba akiwa ni tunda la ulimwengu na kampa maandalizi yanayotosha ulimwengu wote na amemwandaa kwa ajili ya uja (Utumishi) wa ujumla na kumtahini kwa hisia zenye kuelekea katika wingi na dunia. Na kwa kuwa Sharifu mno kuliko vyote vilivyomo ni vyenye uhai, na vitukufu mno kuliko vilivyo hai vyote ni wenye utambuzi, na wenye utambuzi watukufu mno kuliko wote ni wanadamu wa hakika waliokamilika, basi yule ambaye ametimiza miongoni mwa wana wa Adamu aliyekirimiwa majukumu hayo yaliyotajwa huko nyuma na kuyapa haki yake katika utekelezaji katika sura bora mno na ngazi adhimu mno katika ngazi za utekelezaji, hapana shaka kwamba atapandishwa Miiraji - Miiraji adhimu – awe usawa wa pinde mbili au karibu zaidi, na atagonga mlango wa furaha ya milele na atafungua hazina za rehema kunjufu, na ataona hakika za Imani za kighaibu kuona kwa kushuhudia, na nani huyo atakuwa asiyekuwa Nabii Karimu (s.a.w)? Saba: Mwenye kuzingatia katika vitengenezwa hivi vilivyotawanywa ulimwenguni kwamba ndani yake kuna tendo la kuweka uzuri katika ukomo wa uzuri na tendo la upambaji katika ukomo wa kupendeza, basi ni jambo lililo wazi kwamba mfano wa uwekaji uzuri huu na upambaji huu vinavyojulisha juu ya uwepo wa kutaka kuweka vizuri na kukusudia kupamba kwa mtengenezaji wa vitengenezwa hivyo, matakwa hayo yenye kushitadi kwa dharura yanajulisha juu ya uwepo wa raghba yenye nguvu ya hadhi ya juu, na mahaba matakatifu kwa huyo mtengenezaji kwa utengenezaji wake. Kwa hiyo ni katika mambo yaliyo wazi kuwa kiumbe mpendwa sana mbele ya muumba mtukufu ambaye anapenda vitengenezwa vyake na mwenye kusifiwa kwa sifa hizo, na anayedhihirisha katika dhati yake vipole vya ufundi dhihirisho kamili, na ambaye anaujua na kuujulisha, na ambaye anayependezeshwa nafsi yake na kujua uzuri - kwa kupendezwa na kuthamini – uzuri wa vitengenezwa vingine. Basi ni nani ambaye amejaalia mbingu na Ardhi vinagonga sauti ya mwangwi سبحان الله... ماشاء الله ...الله أكبر katika dhikiri za kupendezwa na tasbihi na takbira mbele ya kinachopangilia vitengenezwa katika sifa za pekee za kupambika kwake na mema ya kurembeka kwake na vipole na makamilifu ya kunawirika kwake? Na ni nani ambaye ametikisa viumbe kwa naghama za Qur’an tukufu ikajadhibika bara na bahari kwake kwa shauku kubwa ya kuhisi uzuri na kuthamini katika kutafakari na kutangaza na kuifanya mashuhuri, na dhikiri na tahalili? Nani atakuwa dhati hiyo yenye baraka asiyekuwa Muhammad mwaminifu (s.a.w)?. Basi mfano wa Nabii huyu Mtukufu (s.a.w) ambaye huongezwa katika kitanga cha mema yake katika mizani mithili ya waliyofanya umma wake miongoni mwa mazuri kwa siri ya: ﴾ السبب كالفاعل ﴿ na ambayo huongezewa katika makamilifu yake ya kimaanawy swala ambazo Umma wake wote wanazitekeleza. Na anayeongezewa kutoka katika rehema ya kiungu na mahaba yake ambayo viwili hivyo haviekewi mipaka yoyote, ukiachilia mbali anayoyapata katika matunda ya aliyoyatimiza katika jukumu la Utume wake kutokana na thawabu ya kimaanawy kubwa. Naam, basi mithili ya Nabii huyu mkubwa hapana shaka kwamba kwenda kwake peponi, na katika mkunazi wa ukomo, na katika Arshi kuu, akawa usawa wa pinde mbili au karibu zaidi, hakika hiyo ni haki yenyewe, na dhati ya hakika na hekima tupu. اَل۟بَاقٖى هُوَ ال۟بَاقٖى Said Nursî Hâşiye: En mühim bir ceride-i İslâmiyede, umum âlem-i İslâm’a taalluk eden ve gayet ehemmiyetli siyasîlerden ve hayat-ı içtimaiye ile çok alâkadar olan umum hukukçulardan 1927 senesinde Avrupa’da toplanan bir kongrede mühim ecnebi feylesoflar, şeriat-ı Muhammediyeye (asm) dair bu aşağıda yazılan Arabî fıkranın aynını kendi lisanlarıyla söylemişler. O Arabî ceridenin naklettiği Arabî ifadeyi aynen yazıyoruz ve tercümesini de Arabî ifadenin altına ilâve ediyoruz. Nur Çeşmesi’nin âhirinde yazılan ecnebi feylesoflardan kırk üç tanesinin beyanatı, bu iki kahraman feylesofun beyanatıyla kırk beş tane şahid-i sadık oluyor. اَل۟فَض۟لُ مَا شَهِدَت۟ بِهِ ال۟اَع۟دَاءُ “Fazilet odur ki düşmanlar dahi onu tasdik etsin.” Arabî ceridenin beyanatı: وَقَد۟ اِع۟تَرَفَ حَتّٰى عُلَمَاءُ ال۟غَر۟بِ بِسُمُوِّ مَبَادِى ال۟اِس۟لَامِ وَصَلَاحِهَا لِل۟عَالَمِ … قَالَ عَمٖيدُ كُلِّيَّةِ ال۟حُقُوقِ بِجَامِعَةِ فِيَنَا اَل۟اُس۟تَاذُ شَبُول۟ فٖى مُؤ۟تَمَرِ ال۟حُقُوقِيّٖينَ ال۟مُن۟عَقَدِ فٖى سَنَةِ (٧٢٩١): اِنَّ ال۟بَشَرِيَّةَ لَتَف۟تَخِرُ بِاِن۟تِسَابِ رَجُلٍ كَمُحَمَّدٍ (ع ص م) اِلَي۟هَا اِذ۟ اِنَّهُ رَغ۟مَ اُمِّيَّتِهٖ اِس۟تَطَاعَ قَب۟لَ بِض۟عَةِ عَشَرَ قَر۟نًا اَن۟ يَأ۟تٖى بِتَش۟رٖيعٍ سَنَكُونُ نَح۟نُ ال۟اَو۟رُوبَائِيّٖينَ اَس۟عَدَ مَا نَكُونُ لَو۟ وَصَل۟نَا اِلٰى قِي۟مَتِهٖ بَع۟دَ اَل۟فَى۟ عَامٍ وَ قَالَ بَر۟نَار۟د شَو۟ : لَقَد۟ كَانَ دٖينُ مُحَمَّدٍ (ع ص م) مَو۟ضِعَ التَّق۟دٖيرِ السَّامٖى دَائِمًا لِمَا يَن۟طَوٖى عَلَي۟هِ مِن۟ حَيَوِيَّةٍ مُد۟هِشَةٍ لِاَنَّهُ عَلٰى مَا يَلُوحُ لٖى هُوَ الدّٖينُ ال۟وَحٖيدُ الَّذٖى لَهُ مَلَكَةُ ال۟هَض۟مِ لِاَط۟وَارِ ال۟حَيَاةِ ال۟مُخ۟تَلِفَةِ وَالَّذٖى يَس۟تَطٖيعُ لِذٰلِكَ اَن۟ يَج۟ذِبَ اِلَي۟هِ كُلَّ جَي۟لٍ مِنَ النَّاسِ وَ اَرٰى وَاجِبًا اَن۟ يُد۟عٰى مُحَمَّدٌ (ع ص م) مُن۟قِذَ ال۟اِن۟سَانِيَّةِ وَ اَع۟تَقِدُ اَنَّ رَجُلًا مِث۟لَهُ اِذَا تَوَلّٰى زَعَامَةَ ال۟عَالَمِ ال۟حَدٖيثِ نَجَحَ فٖى حَلِّ مُش۟كِلَاتِهٖ وَاَحَلَّ فِى ال۟عَالَمِ السَّلَامَةَ وَالسَّعَادَةَ ( يَع۟نِى ال۟مُسَالَمَةَ وَالصُّل۟حَ ال۟عُمُومِىَّ) وَمَا اَشَدَّ حَاجَةَ ال۟عَالَمِ اَل۟يَو۟مَ اِلَي۟هَا … Tercümesinin bir hülâsası: Evet, Garp uleması ve feylesofları itiraf ve ikrar etmişler ki: “İslâmiyet’in kanunları, yüksek bir tarzda âlemin ıslahına kâfidir.” Hem Külliyetü’l-Hukuk Kongresi’nin cemiyetinde, bütün hukukiyyunun toplandığı o kongrede 1927 senesinde onun reisi feylesof üstad Shebol demiş ki: “Muhammed’in (asm) beşeriyete intisabıyla bütün beşeriyet muhakkak iftihar eder. Çünkü o zat ümmi olmasıyla beraber, on üç asır evvel öyle bir şeriat getirmiş ki biz Avrupalılar iki bin sene sonra onun kıymetine ve hakikatine yetişsek en mesud en saadetli oluruz.” İkincisi veyahut Nur Çeşmesi’nin âhirine ilâve edilenlerle kırk beşincisi olan Bernard Shaw demiş: “Din-i Muhammedî’nin (asm) en yüksek makam-ı takdire çıkmasının sebebi, gayet acib ve sağlam bir hayatı temin etmesidir. Bana açılan budur ki o din; tek, yekta, emsalsiz bir din-i ferîd olup bütün muhtelif ayrı ayrı hayatın etvarlarını ve çeşitlerini hazmettiriyor. Yani ıslah ve istihale tarzında tasfiye ve terakki ettiriyor. Hem Muhammed’in (asm) dini öyle bir dindir ki insanın ayrı ayrı bütün milletlerini kendine celbedebilir. Ben görüyorum ve itikad ediyorum ki beşere vâcibdir ki desin: “Muhammed (asm) insaniyetin halâskârıdır. Ve halâskârlık namı, ona verilmek lâzımdır.” Hem diyor: “Ben itikad ediyorum ki Muhammed’in misli, yani sîretinde, tarzında bir adam şimdiki yeni âleme reis olsa hükmetse; bu yeni âlemin müşkülatını halledip bu yeni karmakarışık âlemde müsalemet-i umumiyeye ve saadet-i hayatın husulüne sebep olacak. Evet, bu yeni âlemin müsalemet ve saadet-i hayatiyeye ne kadar şedit ihtiyacı var olduğunu herkes anlar.”
Ambayo inajadili kuhusu (Utume wa Muhammad (s.a.w)) [Kwa mnasaba wa makamo ngazi hii imeunganishwa hapa] Kisha yule mtalii katika dunia aliisemesha akili yake akisema: Maadam ninamtafuta mmiliki wangu na Muumba wangu kwa kuvitamkisha vilivyomo vya ulimwengu huu. Basi ni bora ni mzuru ambaye ni mtu mkamilifu zaidi katika uwepo, na mtukufu zaidi anayeongoza katika kheri - hata kwa kusadikisha kwa maadui wake - na wa juu yao kwa sauti na mkweli wao kwa mazungumzo na wa juu yao kwa daraja na mwenye nuru wao zaidi kiakili, ee naye ni Muhammad (s.a.w) ambaye ameangaza kwa fadhila zake na kwa Qur’an yake muda wa karne kumi na nne. Na kwa ajili ya kuwa nipate kumzuru ziara yake tukufu, na niombe ufafanuzi kutoka kwake ninayoyatafuta, yatakikana twende kwa pamoja katika heri ya karne katika zama za furaha, (zama bora) zama za Utume, akaingia kwa akili yake katika zama hizo akaona kwamba zama hizo zimekuwa kwa sababu yake Mtume (s.a.w) ni zama za furaha kwa wanadamu kiukweli. Kwa sababu yeye Mtume (s.a.w) aligeuza katika muda mchache kwa nuru ambayo amewaletea watu waliozama katika ujinga mkubwa, na ubedui mkongwe mno na akawageuza kuwa ni maustadhi na mabwana wa ulimwengu. Na vilevile aliisemesha akili yake kwa kusema: (Ni juu yetu kabla ya kila kitu tujue kitu kuhusu adhama ya dhati hii ya muujiza, na hii ni kutokana na u-haki wa Hadithi zake, na ukweli wa habari zake, kisha tuombe tafsiri kwake kuhusu muumba wetu), akaanza kutafiti. Akaona juu ya ukweli wa Utume wake kutokana na dalili za kukinaisha zilizothibiti kiasi kisicho hesabiwa wala kumalizwa, lakini alihitimishia katika tisa kati ya hizo: Kwanza: Ni kusifika kwake Mtume (s.a.w) kwa sifa zote bora na mambo mema, hata walishuhudia hivyo maadui zake, na kudhihiri mamia ya miujiza kutoaka kwake, kama kupasuka kwa mwezi ambao ulipasuka katika vipande viwili kwa ishara kutoka kwenye kidole chake kama Qur’an ilivyoeleza juu ya hilo: ﴾ وَانشَقَّ الْقَمَرُ ﴿ na kushindwa kwa jeshi la maadui kwa mchanga mchache ulioingia machoni mwao wote ambao aliwarushia kutokana na gao alilokamata kwenye kiganja chake, kama Qur’an tukufu ilivyoeleza juu ya hili: وَمَا رَمَيْتَ إِذْ رَمَيْتَ وَلَكِنَّ اللّهَ رَمَى kukata kiu sahaba zake kutokana na maji yaliyotoka kama Kauthar kutoka katikati ya vidole vyake vitano vilivyobarikiwa wakati kilivyowazidia kiu. Na mingine katika mamia ya miujiza ambayo ilidhihiri mbele yake, na iliyonakiliwa kwetu kwa nukulu sahihi za kukinaisha na Mutawatir, mtalii yule akachungulia katika (Andiko la kumi na tisa) yaani (Risala ya muujiza wa Muhammad (s.a.w)) Risala ile ya kufurutu ada yenye karama inayojumuisha zaidi ya miujiza mia tatu katika miujiza yake (s.a.w) kwa dalili zake za kukinaisha na isinadi zake zenye kutegemewa. Kisha akaisemesha nafsi yake kwa kusema: Hakika mwenye kuwa na (tabia njema) kwa kadiri hii na (fadhila) kwa kiwango hiki, na (Miujiza) ya wazi kwa wingi huu, basi hakuna shaka kuwa yeye ni mwenye maneno ya kweli mno na kwa ajili hiyo haiyumkiniki abadani - na hasha kwake - kujishusha kwenda katika hila na uongo na udanganyifu ambavyo ni kawaida ya watu mafisadi (Waharibifu). Pili: Kuwa Qur’an ambayo imo mkononi mwake (s.a.w) ni muujiza kwa namna saba. Hiyo amri iliyotoka kwa Mmiliki wa Ulimwengu ambayo wanaitii na kuisadiki zaidi ya watu milioni mia tatu katika kila zama. Na ilipokuwa (Neno la ishirini na tano) yaani Risala ya (Miujiza ya Qur’an) nayo ni jua la (Risale-i Nur) imethibitisha kwa dalili zenye nguvu kwamba hii Qur’an tukufu ni Muujiza kwa pande arobaini, na kwamba ni maneno ya Mola Mlezi wa walimwengu, na kwa ajili hiyo ameelekea Mtalii huyo katika Risala hiyo mashuhuri kwa ajili ya maelezo yake yaliyofafanuliwa ya muujiza. Kisha amesema: Hakika mtunza amana wa maneno ya Allah, na mkalimani wa kimatendo wa maneno hayo, na mfikishaji wa habari hii kubwa kwa watu wote, ni haki yenyewe na hakika kwa dhati yake, haiyumkiniki kutokea kwake uongo katu, na wala hatakuwa mahali pa utata abadani. Tatu: Hakika (s.a.w) ameletwa na sharia iliyotakaswa, dini ya kimaumbile, uja uliotakasika, dua ya hushui, dua yenye kukusanya na kwa Imani iliyo madhubuti, hakuna mithili ya alicholetwa nacho wala haitokuwa, na hakupatikana mkamilifu zaidi yake wala hatapatikana. Kwa kuwa (Sharia) ambayo imedhihiri kutoka kwa ummy (asiyejua kusoma) na kuongoza humusi (1/5) ya wanadamu pamoja na tofauti zao tangu karne kumi na nne uongozi uliosimama juu ya haki na uadilifu kwa kanuni zake madhubuti nyingi, haukubali mithili yake abadani. Na vivyo hivyo Uislamu ambao umetokea kutokana na matendo ya mtu ambaye ni ummy na kutokana na matendo yake na hali zake, yeye ni kiongozi wa milioni mia tatu katika wanadamu na marejeo yao katika kila zama, na mwalimu wa akili zao na mwelekezi wake, na eneo la kufunuka kwa roho zao na madini ya kupanda hadhi yake haikuja na wala haitokuja mithili yake. (yaani kama dini ya Kiislamu). Na vilevile kuwa kwake Nabii Muhammad (s.a.w) ni wa juu katika aina zote za ibada ambazo zimo katika dini yake, na uchaji wake mkubwa zaidi kuliko yeyote awaye, na hofu yake kali sana kwa Allah (s.w) na jitihadi yake yenye kuendelea na uchungaji wake wa haki ya juu kwa siri nyeti mno za uja hata katika hali nzito sana na mazingira magumu, na kutimiza kwake uja huo uliotakasika, bila ya kumwiga yeyote na kwa maana yake yote akiwa mwenye kuanza, na kwa ukamilifu wa sura zake, hali ya kuunganisha mwanzo na ukomo, hapana shaka hakuonekana na hatoonekana mithili yake. Na vilevile anasifu, katika (Al-Jawshan Al-Kabiir) - ambayo ni moja katika maelfu ya dua zake na munajati yake - anamsifu Bwana Mlezi wake kwa maarifa ya kiungu ya hadhi ya juu, watambuzi na mawalii wote hawakufikia ngazi hiyo ya maarifa, wala daraja ya sifa hiyo tangu hapo tangu pamoja na kukutana kwa fikira. Katika yanayodhihirisha kwamba hana mithili yake katika (Dua). Na mwenye kutazama katika ufafanuzi wa muhtasari wa kifungu kimoja kutoka vifungu tisini na tisa vya Jawshan kubwa, nayo ni katika utangulizi wa Risala ya (Munajati) haitamtosha kusema ila kwamba hapana mithili yake kwa hii dua nzuri (Al-Jawshan) ambayo inashika nafasi ya kilele cha utambuzi wa kiungu. Na vilevile hakika kudhihirisha kwake katika (Kufikisha Ujumbe) na katika kuwalingania kwake watu katika haki katika umadhubuti, uthabiti na ushujaa ambao hakuna yeyote anaukaribia, Hakuingiwa - japo kwa kiasi cha dhara – na athari yoyote ya kusita na wala haikumuingia wasiwasi katu, wala hofu haikumpata yeye hata kidogo, pamoja na uadui wa dola kubwa na dini kuu - na hata kaumu yake, kabila lake na ami yake wamemwekea uadui mkubwa - akachagiza peke yake dunia yote, na Allah (s.w) akamnusuru na kumpa ushindi akavika kichwa cha dunia kwa taji la Uislamu, basi nani mithili ya Muhammad (s.a.w) katika kufikisha jumbe za Allah?. Na vilevile kubeba kwake (Imani yenye nguvu madhubuti, na yakini ya kukata shauri ya kufurutu ada, na kufunuliwa kwa maumbile kwa muujiza, na itikadi ya hadhi ya juu imeujaza ulimwengu kwa nuru) haikuyumkinika kumwathiri fikira zote na itikadi zote na hekima ya wenye hekima na elimu za wakuu wa kiruhani walioenea katika zama hizo, japo kwa utata, au kwa kusitasita, au kwa udhaifu, au kwa wasiwasi. Naam, haikuyumkinika kuathiri katika yakini yake, wala katika itikadi yake wala katika kumtegemea kwake Allah, wala katika kutulia kwake (kwa kumtumainia Allah), pamoja na kupingwa na kumhalifu yeye na kuikanusha juu yake. Na ongeza juu ya hili kupata ilhamu wale wote ambao waliopanda katika mambo ya kimaanawy na ngazi za kiimani katika watu wa Uwalii na wema, na katika utangulizi wao sahaba wema, na kupokea kwao daima kutoka katika ngazi yake ya kiimani na wao kumwona yeye kuwa yuko katika daraja za juu. Yote hayo yanonesha - wazi - kwamba Imani yake (s.a.w) haina mithili pia. Mtalii akafahamu, na akasadiki akili yake kwamba ambaye amekuwa ni mwenye sharia hii ya msamaha ambayo haina mithili, na Uislamu ulionyooka ambao hauna mfano, na uja uliotakata ambao hauna kifani, na dua ya ajabu ya kupendeza, na madai ya kiulimwengu yenye kuenea, na imani ya kimuujiza, uongo wowote hautakuwa kwake na hatakuwa mdanganyifu abadani. Dalili ya Nne: Ijmai ya manabii (a.s) na kuafikiana kwao juu ya hakika za kiimani hizohizo ni dalili ya kukinaisha juu ya kuwepo kwa Allah (s.w) na juu ya upweke wake, na ni ushahidi wa kweli pia juu ya ukweli wa Mtume huyu (s.a.w) na juu ya Utume wake, hiyo ni kwa sababu kila kinachojulisha ukweli wa manabii hao (a.s), na kila ambacho ni eneo la Utume wao katika sifa takatifu na miujiza, na majukumu ambayo waliyokuwa nayo yanapatikana mithili yake na kwa ukamilifu zaidi yake kwake (s.a.w), kama hili linavyosadikishwa kwa historia. Basi manabii hao (a.s) wameelezea kwa ulimi wa maneno – yaani kwa Taurati, Injili, Zaburi na Suhufi ambazo zilizomo mbele yao – kwa ujio wa hii dhati yenye kubarikiwa na wamebashiri watu kwa ujio wake (s.a.w) (hata zaidi ya Ishara Ishirini za wazi dhahiri katika ishara zenye kubashiri za vitabu hivyo vitakatifu zimebainishwa ubainifu ulio wazi na zimethibitishwa katika Risala ya Muujiza wa Muhammad) kama kwamba walivyobashiri ujio wake (s.a.w) hakika wanamsadiki (s.a.w) kwa ulimi wa hali yao - yaani kwa Unabii wao na kwa miujiza yao - na wanahitimisha kwa kuunga mkono juu ya ukweli wa daawa yake ambapo yeye ndiye mtangulizi kamili zaidi katika jukumu la Utume na daawa kwa Allah (s.w). Mtalii yule akatambua kwamba wao kama wanavyojulisha - yaani hao manabii - kwa ulimi wa maneno na ijmai juu ya upekee, hakika wanashuhudia - kwa ulimi wa hali kwa kuafikiana vilevile - juu ya ukweli wa huyu Mtume mtukufu (s.a.w). Dalili ya Tano: Hakika kufika kwa maelfu ya mawalii katika haki na hakika, na waliyoyapata katika makamilifu na karama na hali za kufunuliwa walizopata na kushuhudia sio kwa vyovyote isipokuwa ni kwa kufuata mwongozo wa kanuni za Mtume huyu (s.a.w), na kwa malezi yake, kwa kumfuata yeye na kufuata athari yake, na basi kama wanavyojulisha wote juu ya upweke wa Allah basi wanashuhudia kwa ijmai na kwa kuafikiana juu ya Mtume huyu Mtukufu (s.a.w) - ustadhi wao na Imamu wao – na juu ya kustahiki kwake Utume. Mtalii akaona kwamba watu hawa kushuhudia sehemu katika aliyoyaeleza (s.a.w) katika ulimwengu wa ghaibu kwa nuru ya Uwalii na kuitakidi kwao hilo na kusadikisha kwao yote aliyoyaelezea kwa nuru ya kumwamini yeye – Ima kwa elimu ya yakini au kwa dhati ya yakini au kwa haki ya yakini - hakika sio vingine bali inadhihirisha udhahiri kama jua: Ukweli ulioje wa mwelekezi wao mkuu na haki iliyoje kwa kiongozi wao mkuu (s.a.w). Dalili ya Sita: Hakika ya mamilioni ya wanazuoni wadadisi wateule, na wahakiki wa kweli, na mahodari wa wenye hekima waumini, katika ambao wamefikia ngazi za juu kwa fadhili ya walichokisoma na kujifunza juu ya yale aliyokuja nayo Nabii huyu Mtukufu (s.a.w) na yaliyotokana nayo miongoni mwa elimu za juu, na yaliyogunduliwa kutokana nayo katika maarifa ya kiungu, hakika hawa wote kama wanavyothibitisha upweke ambao ni msingi wa daawa yake (s.a.w) na wanaisadikisha wakiafikiana kwa hoja zao zenye kukinaisha, wao pia hakika wanaafikiana juu ya ukweli wa mwalimu huyu mkuu na kusibu kwa ustadhi huyu mkuu na juu ya kuwa maneno yake ni ya haki (s.a.w). Basi ushahidi wao huu ni hoja iliyo wazi kama mchana juu ya ukweli wake na kusibu kwa Utume wake. Na (Risale-i Nur) kwa juzu zake ambazo zinazidi mia moja mathalani sio isipokuwa hoja moja tu juu ya ukweli na kusibu kwa Nabii huyu kipenzi (s.a.w). Dalili ya Saba: Hakika ya mkusanyiko mkubwa ambao unaitwa (Jamaa na sahaba) ambao ni wanadamu mashuhuri zaidi baada ya Manabii kwa Firasa (Uoni wa ndani) na wenye utambuzi zaidi, wenye makamilifu ya hadhi ya juu zaidi, wenye daraja bora zaidi, wenye umaarufu zaidi, wenye kushikamana zaidi na dini na wenye matazamo mkali zaidi, hakika ya upekuzi wao na kuchunguza kwao vema kwa yote yaliyojificha na yaliyodhihiri katika hali za Mtume huyu (s.a.w) na fikira zake na matendo yake kutafuta kwa ukamilifu wa pupa na shauku, kwa umakini zaidi na kwa ukomo wa bidii kwa kuafikiana na ijmai kwamba yeye (s.a.w) ni mkweli zaidi ya watu waliomo dunia kwa mazungumzo, na Mwenye nafasi ya juu zaidi na mwenye kushikamana zaidi na haki na hakika. Basi kusadikisha kwao huku ambako hakutetereki pamoja na imani ya kina waliyonayo, hakika ni dalili ya wazi kama mchana kuwa dalili ya mwanga wa jua. Dalili ya Nane: Hakika ya huu ulimwengu kama unavyojulisha juu ya mtengenezaji wake, mwandishi wake na msawiri wake ambaye aliupatisha, na ambaye anauendesha na kuuratibu na anasarifu ndani yake kwa kusawiri na kukadiria na kuendesha kana kwamba ni kasri kubwa, au kana kwamba ni kitabu kikubwa, au kana kwamba ni maonesho ya ajabu, au kama ni mahala pa matangazo makubwa, basi kadhalika unahitajia pasi na namna nyingine kuwepo kwa mwenye kuelezea maana yaliyomo ndani ya kitabu hiki kikubwa, na ajue na ajulishe makusudio ya kiungu nyuma ya kuumbwa kwa ulimwengu, na afundishe hekima za kiungu Bwana Mlezi katika mabadiliko yake, kugeuka kwake na mabadiliko yake, na afundishe matokeo ya michakato yake ya kimajukumu, na atangaze thamani ya ainisho lake na makamilifu yaliyomo katika vilivyomo. Yaani inahitajia mlinganiaji mkuu, mpiga mnada wa kweli, ustadhi wa haki na mwalimu mwerevu. Basi yule mtalii akatambua: Hakika ya ulimwengu - kwa hali hii ya kuhitajia - unajulisha na kushuhudia juu ya ukweli wa Mtume Mtukufu (s.a.w) na kusibu kwake ambaye ni mtu bora aliyetimiza kazi hizi na majukumu haya, na kwa kuwa kwake ni mjumbe bora na mkweli zaidi wa Bwana Mlezi wa walimwengu. Dalili ya Tisa: Maadam nyuma ya pazia yupo anayetangaza ukamilifu wa kuwa kwake wa ajabu mwenye kutengeneza vema, kwa hivi vitengenezwa vyake, vyenye kutengenezwa vyema na hekima. Na anaitambulisha nafsi yake na kuipendezesha, kwa viumbe vyake visivyo na mpaka wenye mapambo na uzuri. Na kupasisha shukurani na sifa njema, kwa neema zake zisiyohesabika zenye ladha na thamani. Na kuwapa shauku viumbe katika ibada upande wa uungu wake kwa uja wenye kuchukua alama ya mapenzi na kupokea neema na shukurani mkabala wa malezi haya, na kupewa maisha kwa jumla, kwenye huruma na himaya (Hata kwamba hakika yake na andaa vyakula na dhifa za kiungu Bwana Mlezi kiasi kinachotuliza vionjo makini vya vinywa na aina zote za hamu ya kula) na kuwatiisha viumbe katika Imani na kusalimu amri na kufuata na kutii kwa Uungu Mola mwabudaiwa wa haki ambaye anaudhihirisha kwa kubadilisha majira, na kuzungusha usiku juu ya mchana, na kuhitilafiana viwili hivyo, na mfano wa hayo katika matendo ya usarifu mkubwa, shughuli tukufu, na utendaji kazi wa kushangaza na hali ya uumbaji wenye hekima, na anadhihirisha uadilifu wake na kushika kwake insafu kwa himaya yake daima kwa wema na walio wema na kuondosha kwake shari na walio wa sahari na kuwafuta kwake madhalimu na wakadhibishaji na kuwahilikisha kwao kwa mabalaa ya kushuka kutoka mbinguni. Basi hapana shaka, kwamba kiumbe mpendwa kabisa mbele ya yule aliyefichikana kwa ghaibu, na mja mkweli mno kwake ni yule ambaye amekuwa mtendaji kwa ikhlasi kwa makusudio yake yaliyoelezwa huko nyuma, na anayefunua siri kuu katika kuumba ulimwengu na kufumbua fumbo lake, na mwenye kujitahidi daima kwa jina la muumba wake na kuchukua nguvu na taufiki kutoka kwake (s.w), na ni nani huyu awaye asiyekuwa Muhammad Mkuraishi (s.a.w). Kisha yule mtalii aliisemesha akili yake kwa kusema: Kwa kuwa hakika hizi tisa ni shahidi za kuthibitisha juu ya ukweli wa Nabii Mtukufu (s.a.w), basi hapana shaka kwa hiyo: Kuwa yeye ni mhimili wa utukufu wa Ubinadamu, na mahali pa kuzunguka kwa fahari ya ulimwengu, na kwamba ni mwenye kustahiki mno na mwenye kufaa kuitwa kuwa ni utukufu wa binadamu, na kupewa jina la fahari ya walimwengu. Na kwamba kilichomo mkononi mwake katika amri ya mwingi wa rehema nayo ni Qur’an tukufu yenye kutamalaki utukufu wa ufalme wake wa kimaanawy juu ya nusu ya ardhi pamoja na anayomiliki katika makamilifu ya kihaiba na mambo yake ya hadhi ya juu yanadhihirisha mawili hayo kwamba mwanadamu mkuu kabisa katika uwepo ni huyu Nabii Mtukufu, basi kauli ya upambanuzi kwa hiyo kwa haki ya Muumba wetu (s.w) ni kauli yake (s.a.w). Basi njoo ewe akili yangu na uzingatie: Hakika ya msingi wa madai yote ya Mtume huyu (s.a.w), na shabaha ya maisha yake yote, hakika ni kushuhudia juu ya kuwepo kwa aliye wajibu kuwepo, na kujulisha juu ya upweke wake, na kubainisha sifa zake tukufu, na kudhihirisha majina yake mazuri, na kuthibitisha yote hayo na kuyatangaza na kuyajulisha, kwa kuegemea yaliomo katika dini yake katika maelfu ya hakika zenye msingi uliojikita na nguvu ya yale aliyoyadhihirisha Allah (s.w) mkononi mwake katika mamia ya miujiza yake ya kukata shauri iliyo wazi. Hakika ya jua la kimaanawy ambalo linaangazia ulimwengu huu na hoja yenye nuru juu ya kuwepo kwa Muumba wetu (s.w), na upekee wake hakika ni huyu Nabii Mtukufu ambaye ameitwa kuwa ni kipenzi wa Allah (s.a.w). Kuna aina tatu za ijmai kuu hazihadai wala hazihadaiki zinaiunga mkono ushahidi wake na kuusadikisha: Ijmai ya Kwanza: Ijmai ya wale ambao wamekuwa mashuhuri, na kuwa na sifa za pekee katika ulimwengu kwa jina la (Jamaa wa Muhammad (s.a.w)) ni kundi la kinuru ambalo analitangulia imamu ali (r.a) ambaye amesema: (Ingeondoshwa pazia nisingeongezeka yakini), na nyuma yake kuna maelfu ya mawalii watukufu katika wenye uono mkali na mtazamo wenye maliwazo ya ghaibu katika mifano ya shaikh Al-Kaylani (q.s) ambaye alikuwa anaangalia kwa uoni wake wenye kupenya katika Arshi tukufu na Israfil kwa utukufu wake na hali ya kuwa yungali ardhini. Ijmai ya Pili: Ni ijmai ya kundi lile linalojulikana kuwa ni sahaba watukufu walio mashuhuri ulimwenguni (r.a) na kusadiki kwao kwa kuafikiana na kwa imani iliyojikita yenye nguvu kwa huyu Nabii Mtukufu, hata hilo likawapeleka katika kujitoa fidia roho zao, mali zao, baba zao na jamaa zao, nao ni wale ambao walikuwa ni watu mabedui wanaishi katika mazingira ya kiummy yasiokuwa na hali za maisha ya kijamii na fikira za kisiasa, hawana mwongozo wala kitabu chenye nuru. Na walikuwa wamegubikwa katika giza la zama za (Fatrat) wakawa katika muda mfupi ni maustadhi waelekezi na wanasiasa na watawala waadilifu kwa mataifa ya juu kiustaarabu, elimu, jamii na siasa, wakatawala ulimwengu mashariki na magharibi na zikapeperuka bendera za uadilifu wao bara na baharini. Ijmai ya Tatu: Ni kusadikisha kundi kubwa katika wanazuoni watukufu ambao hawahesabiki wala hawadhibitiki wingi wao, waliobobea katika elimu zao na wahakiki wachunguzi ambao wametokea katika uma wake na wakapita maslaki mbali mbali, nao katika kila zama kuna maelfu ya wenye kupata kiguzo cha utangulizi – kwa umahiri wao – katika kila elimu. Kusadiki hawa wote kwa kuafikiana na kwa daraja ya elimu ya yakini ni ijmai iliyoje! Mtalii yule akaamua kwamba ushahidi wa nabii huyu Ummy (s.a.w) juu ya upweke sio ushahidi binafsi na wa sehemu ndogo, bali ni ushahidi enevu wa jumla umejikita hautetereki, na hawataweza kukabiliana nao mashetani wote katika upande wowote na hata wakijikusanya kwa hilo. Na kama hivi imeelezwa ishara ya muhtasari kwa yale aliyoyapata yule mtalii ambaye ametembea kwa akili yake katika zama za ufaulu pande za maisha kutoka katika madarasa ile ya kinuru katika (Ngazi ya kumi na sita katika makamo ya kwanza) kama ifuatavyo: لَٓا اِلٰهَ اِلَّا اللّٰهُ ال۟وَاجِبُ ال۟وُجُودِ ال۟وَاحِدُ ال۟اَحَدُ الَّذٖى دَلَّ عَلٰى وُجُوبِ وُجُودِهٖ فٖى وَح۟دَتِهٖ فَخ۟رُ ال۟عَالَمِ وَ شَرَفُ نَو۟عِ بَنٖى اٰدَمَ بِعَظَمَةِ سَل۟طَنَةِ قُر۟اٰنِهٖ وَ حِش۟مَةِ وُس۟عَةِ دٖينِهٖ وَ كَث۟رَةِ كَمَالَاتِهٖ وَ عُل۟وِيَّةِ اَخ۟لَاقِهٖ حَتّٰى بِتَص۟دٖيقِ اَع۟دَائِهٖ وَ كَذَا شَهِدَ وَ بَر۟هَنَ بِقُوَّةِ مِاٰتِ ال۟مُع۟جِزَاتِ الظَّاهِرَاتِ ال۟بَاهِرَاتِ ال۟مُصَدِّقَةِ ال۟مُصَدَّقَةِ وَ بِقُوَّةِ اٰلَافِ حَقَائِقِ دٖينِهِ السَّاطِعَةِ ال۟قَاطِعَةِ بِاِج۟مَاعِ اٰلِهٖ ذَوِى ال۟اَن۟وَارِ وَ بِاِتِّفَاقِ اَص۟حَابِهٖ ذَوِى ال۟اَب۟صَارِ وَ بِتَوَافُقِ مُحَقِّقٖى اُمَّتِهٖ ذَوِى ال۟بَرَاهٖينِ وَ ال۟بَصَائِرِ النَّوَّارَةِ اَل۟بَاقٖى هُوَ ال۟بَاقٖى Said Nursî

