Mektubat

The Twenty-Sixth Letter

Source: risaleinur multilingual dataset, risale.site source · Risale-Nur multilingual research corpus
Risale reading plan
§1

Swali la mfano wa tatu kutoka katika nukta ya tatu ya sababu ya tano katika sababu zenye kuzuia Ijtihad wakati wa sasa kutoka katika neno la ishirini na saba Swali muhimu: Baadhi ya watu wa Elimu na uhakiki wanasema: Ilivyokuwa lafudhi za Qur’an na dhikiri zilizopokelewa, na tasbihati zilizokuja (Katika maelekezo), zinanawirisha pande mbalimbali za vipole vya kimaanawy kwa mwanadamu na kumlisha kiroho, Je haiwi katika ubora kutamka kila watu lafudhi hizo kulingana na ulimi wao maalum ili maana yake yapate kufahamika? Kwani lafudhi peke yake hazitoshelezi shabaha inayotakiwa ambapo hizo katika hakika yake ni mavazi na vyombo vya maana? Jibu: Hakika lafudhi za maneno ya Qur’an, na tasbihati za Mtume (s.a.w), sio vazi lisilo na uhai linalokubali kubadilishwa na kugeuzwa bali hakika mfano wake ni mfano wa ngozi hai ya mwili, bali hakika imekuwa kweli ni ngozi hai kwa kupita kwa zama, na hakuna mjadala katika kuwa kubadili ngozi na kuigeuza kunadhuru mwili. Kisha hakika ya maneno hayo yenye baraka katika swala, dhikiri na adhana, yamekuwa ni jina na jina la pekee kwa maana yake ya kikawaida na kisharia na haiwezekani kubadili majina na majina ya pekee. Na nimefikia katika hakika hii, baada ya kuzingatia na kuchunguza katika hali iliyonipitia, nayo: Siku moja nilipokuwa ninasoma katika Arafat Sura Al-Ikhlas mara mia moja kwa kuirudiarudia mfululizo niliona: Hakika ya baadhi ya milango yangu ya fahamu ya kiroho pole, baada ya kuwa imechukua chakula chake kwa kurudia rudia imechoka na kusimama; na kwamba nguvu ya kutafakari ndani yangu imelekea kwenye maana, ikachukua fungu lake, kisha ikasimama na kuchoka. Na hakika moyo ambao unaonja maana ya kiroho na kuyatambua, nao pia umenyamaza, baada ya kuwa umechukua fungu lake katika kurudiarudia. Wakati ambapo kwa kuendelea na kukariri mfululizo kusoma nimeona sehemu ya vipole katika uwepo wa kibinadamu haichoki haraka, haidhuru kughafilika ambako kunadhuru nguvu ya kutafakari, bali hiyo inaendelea na kudumisha katika kuchukua fungu lake kiasi haiachi haja yoyote katika kuchunguza kwa makini na kutafakari maana, kwani inatosha maana ya kimazowea ambayo ni jina na jina la pekee, na inatosha lafudhi na maana ya kiujumla ya lafudhi hizo tajiri zilizoshibishwa. Bali huenda ikasababisha uchovu na unyong’onyo wakati inaanza kutafakari kuelekea katika maana, hiyo ni kwa kuwa vipole hivyo havihitaji kujifunza na kufahamishwa kwa kiasi cha hivyo vinavyohitaji kukumbuka na kuelekeza na kuhimiza. Kwa hiyo basi hakika lafudhi ambayo ni yenye kushabihiana sana na ngozi inatosha kwa vipole hivyo na katika kutekeleza jukumu la maana, na hasa hakika ya maneno hayo ya Kiarabu ni chanzo cha nuru ya kudumu, kwani yanakumbusha maneno ya kiungu na mazungumzo ya bwana Mlezi. Basi hali hii ambayo nimeijaribu kwenye nafsi yangu inatubainishia: Hakika ya maelezo kwa lugha yoyote iwayo isiyokuwa lugha ya Kiarabu, kuhusu hakika ya adhana na tasbihati za swala, sura Al-Ikhlas na Sura Al-Fatiha ambazo daima hukaririwa, kunadhuru mno. Na hii ni kwa sababu vipole vya kudumu vitabaki vimenyimwa fungu lake la kudumu baada ya kukosa vyanzo vya hakika vya kudumu ambavyo ni lafudhi za Kiungu na Mtume (s.a.w). Ukiachilia mbali kwamba yanapotea kwa uchache mema kumi kwa kila herufi. Na kwa sababu ya kukosekana kudumu utulivu na kuwa hadhiri kimoyo kwa kila mmoja kwenye swala, maelezo ya kibinadamu yaliyoturujumiwa wakati wa kughafilika yanapeleka giza lake kwenye roho. Na mfano wa hayo katika madhara mengine. Naam, basi kama alivyosema imamu Abu Hanifa (r.a) kuwa: ( لاإله إلا الله ) ni jina la pekee la Tawhidi. Kadhalika tunasema: Hakika wingi wa hali zote wa maneno ya Tasbihati na Dhikiri na hasa maneno ya Adhana, Swala na Dhikiri, yamekuwa ni sawa na jina na jina la pekee, basi hutazamwa maana zake za kimazowea za kisharia kuliko kutazamwa katika maana zake za kilugha, na kwa hiyo haiyumkiniki kisharia kuyabadilisha kwa hali zote. Ama maana yake ambayo kila muumini hana budi kuyafahamu, hakika mtu yeyote wa kawaida anaweza kufahamu na kujifunza jumla ya maana yake katika muda mfupi sana. Basi vipi atasamehewa Mwislamu huyo ambaye anatumia umri wake akiwa amejaza fikira yake na akili yake mambo ambayo yasiyo mhusu na wala hatumii sehemu ndogo ya wakati wake kufahamu maana hayo ambayo ni funguo za uhai wake wa milele na furaha yake ya kudumu. Bali vipi atazingatiwa kuwa katika Waislamu na vipi ataitwa kuwa yeye ni mwanadamu mwenye akili!! Je, ni katika akili hata kidogo kuharibiwa lafudhi hizo ambazo ni ghala la vyanzo vya hizo nuru kwa sababu ya kujibweteka kwa hao wavivu?! Kisha ni kwamba muumini yeyote anaposema, kwa lugha yeyote anayozungumza: (سبحان الله) hakika anajua kwamba anamtakasa Mola wake mlezi (s.w), je haitoshi kiasi hiki?! Wakati ambapo anapohusisha mkazo wake kwa maana tupu, kwa lugha yake maalum, hakika hajifunzi isipokuwa kulingana na kufikiri kwake na akili yake, ambayo inachukua fungu lake na kufahamu mara moja, na hali ya kwamba yeye anakariri neno hilo lenye baraka zaidi ya mara mia basi ukiachilia mbali ufahamu huo wa kiakili hakika maana ya kiujumla iliyopita katika lafudhi hilo na kuchanganyika nalo ni chanzo cha kupeleka nuru na neema nyingi mno, na hasa hakika ya lafudhi hizo za Kiarabu zina umuhimu wake na utakatifu wake na nuru zake na neema zake, kwa kuwa hayo ni maneno ya kiungu. Kwa ufupi: Kwamba neno lingine lolote haliyumkiniki katu kusimama mahali pa lafudhi za Qur’an ambazo ni hifadhi na vyanzo vya dharura za kidini, na wala haiyumkiniki kwa neno lingine lolote kushika mahali pake kabisa, wala kutimiza shabaha kutokana na lafudhi hiyo kwa utakatifu wake, hadhi yake ya juu, na kudumu kwake, na hata likitekeleza kwa muda mfupi sehemu kidogo katika hizo. Ama mambo ya kidini yasiyokuwa ya kidharura basi hakuna haja ya kubadili lafudhi zake vilevile kwa sababu haja hiyo inaondoka kwa kuendelea kutoa nasaha kuelekeza na mawaidha. Na matokeo: Hakika ujumuishi wa lugha ya Kiarabu fasaha na ukunjufu wake, na bayana ya kimuujiza katika lafudhi za ki Qur’an, vinazuia kufasiri lafudhi hizo, na kwa hiyo haiwezekani kuzifasiri kabisa, bali hakika hilo ni muhali. Na mwenye kuwa inamzonga shaka katika hili basi na arejee (Neno la ishirini na tano) katika miujiza ya Qur’an ili aone cheo cha aya tukufu kwa muujiza wake na kutanzuka kwake na uzuri wake na maana yake ya hali ya juu na wapi katika hayo (Tafsiri) ambayo ni maana iliyotindwa bali pungufu na yenye kasoro.

Private reading note

This note stays on this device and is never uploaded to a server.

Up to 1,200 characters