Kutoka Katika Andiko la Ishirini na Nane Kujadili Hadithi Tukufu Nimeandika suala hili kwa sababu ya kutatua mishkeli na kuondosha mjadala unaoendelea kuhusu Hadithi Tukufu inaelezwa ndani yake kwamba Sayyidina Musa (a.s) alipiga kofi jicho la Sayyidina Izraili (a.s). Imegonga masikio yangu kwamba mjadala wa kielimu ulipita katika (Eğridir). Hakika ya kupitisha mjadala huo ni kosa, na hasa katika wakati huu kwa dhati yake. Na nimeulizwa mimi pia - na sijui lolote katika huo mjadala - na walinionesha Hadithi tukufu ya Mtume (s.a.w) katika kitabu chenye kuaminika kinachotegemewa, imeashiriwa humo katika Hadithi kwa alama ya (Qaf) kwa ajili ya kujulisha kwamba hiyo ni (Muttafaqun Alayhi), na wakahoji: Je, hii ni Hadithi ya Mtume (s.a.w) au siyo? Niliwaambia: Naam, ni Hadithi tukufu ya Mtume (s.a.w), yatakikana kwenu kutegemea na kuamini ambaye amehukumu kuafikiana kwa Masheikh wawili juu ya Hadithi iliyoelezwa, katika kitabu kama hiki chenye kuaminika. Lakini kama ilivyo katika Qur’an kuna aya Mutashabihati, basi Hadithi tukufu vilevile kuna Mutashabihati, maana yake ya undani hawaitambui isipokuwa wanazuoni mahususi. Na nimesema vilevile: Pengine dhahiri ya Hadithi hii inaingia ndani ya sehemu katika mishkeli ya Hadithi. Ningekuwa najua mjadala ambao umepita kuhusu Hadithi iliyotajwa, nisingekua nimefupisha jibu langu kwa nilivyosema: Bali ningekuwa ninajibu kwa yafuatayo: Kwanza: Hakika sharti la kwanza katika kujadili masuala haya na mfano wake ni: Iwe kujikumbusha katika mazingira ya insafu, na yapitishwe kwa nia ya kufikia katika haki, na kwa sura isiyo na hali ya ukaidi, na kati ya watu ambao wenye kustahiki mjadala, na bila ya kuwa ni nyenzo ya kufahamiana vibaya na kupokea vibaya. Basi ndani ya masharti haya yaweza kuwa kujadili masuala haya na mfano wake ni jambo linalojuzu. Ama dalili kwamba kujadili ni katika njia ya kufika kwenye haki ni kwamba mwenye kujadili asibebe kitu moyoni mwake, wala asione uchungu wala asihemkwe ikiwa imedhihiri haki katika ulimi wa upande tofauti na yeye, bali ni juu yake kuridhia na kutulia, kwani amejifunza alichokuwa hakijui, basi lau haki itadhihiri katika ulimi wake asingezidi elimu na pengine ingemsibu ghururi. Pili: Ikiwa maudhui ya mjadala ni Hadithi tukufu basi yatakikana kujua: Ngazi za Hadithi, na kuzungukia madaraja ya wahyi jumuishi, na vigao vya maneno ya Mtume (s.a.w). Wala haijuzu kwa yeyote kujadili Hadithi zenye mushkeli kati ya watu miongoni mwa watu wa kawaida, wala kulinda rai yake ili kuonesha kuwa juu ya wengine, wala kutafuta dalili zinazotia uzito rai yake na kukuza ghururi yake juu ya haki na insafu. Lakini kwa kuwa suala limetolewa, na imekuwa uwanja wa mjadala, itapelekea taathira yake ovu katika fahamu za watu wa kawaida ambao wanashindwa kuelewa mifano ya Hadithi hizi Mutashabihati. Lau mmojawapo akiikanusha kwa nafsi yake basi amefungua mlango wa kuangamia na hasara, ambapo kukanusha huku kunampeleka katika kukanusha Hadithi sahihi zilizothibiti. Na lau akikubali dhahiri ya maana inayofidishwa na Hadithi na akazungumza na kueneza maana hiyo kati ya watu, basi itakuwa ni sababu ya kufungua mlango wa pingamizi za watu wa upotevu juu ya Hadithi tukufu, na kufungulia ndimi zao kwa kuitendea uovu Hadithi, na kauli yao: Kwamba ni uzushi! Na ilivyokuwa macho yameelekea kwenye Hadithi hii tukufu Mutashabihi bila sababu, bali katika hali ambayo ndani yake kuna madhara. Na kwamba zipo Hadithi nyingine Mutashabihi kwa wingi; bali inalazimu kubainisha (Hakika) ili kukinga Shubuhati na kuondosha dhana, ninasema: Hakika kutaja (Hakika) hii ni jambo la dharura bila ya kutazama kunako kuthibiti kwa Hadithi. Tutaashiria hakika hiyo kwa ishara ya jumla, tukiwa tumetosheka na tuliyoyaeleza katika maelezo ndani ya Risale-i Nur (Miongoni mwa hayo ni tawi la tatu kutoka katika neno la ishirini na nne na tawi la nne kutoka neno hilo, na msingi unaohusu vigawanyo vya wahyi mwanzoni mwa utangulizi wa andiko la kumi na tisa). Na hakika ni kwamba Malaika hawajifungii katika sura moja maalum kama mwanadamu, bali wao ni katika hukumu ya jumla, pamoja na kwamba wao wana maumbo yao maalum. Basi Izrail (a.s) ni mtazamaji wa Malaika waliowakilishwa kuchukua roho na ni Raisi wao. Swali: Je Izrail (a.s) ndiye anayechukua roho hasa, au ni wasaidizi wake ndio ambao wanazichukua. Jibu: Kuna njia tatu kuhusiana na hili: Njia ya kwanza: Hakika Izrail (a.s) ndiye ambaye anachukua roho ya kila mtu. Kitendo hapa hakizuilii kitendo huko kwa sababu ni wa kinuru, na kitu cha kinuru kinayumkinika kuhudhuria na kuwepo kwa dhati yake katika mahali pasipo kuwa na mipaka, kwa kupitia vioo visivyo na mpaka. Basi kuwepo kwa hali ya kinuru kunamiliki sifa zake maalum. Na inazingatiwa ni dhati yake na si kitu kingine. Basi kuwepo kwa jua katika vioo mbali mbali kama linavyodhihirisha mwanga wa jua na joto lake, hakika ya kuwepo kwa maruhani – kama Malaika – hudhihirisha vilevile sifa zake maalum katika vioo mbalimbali katika Ulimwengu wa mfano, basi wao ni dhati ya hao maruhani na si wengineo. Basi malaika wanakuwepo katika kioo kulingana na ukubalifu wa vioo, mathalani: Zama Jibril alipokuwa mbele ya mtume (s.a.w) katika baraza ya sahaba (r.a) katika sura ya sahaba “Dahiyyatul Kalaby” na alikuwa anakuwepo katika punde hiyo hiyo katika maelfu ya mahali katika sura mbali mbali, kama ilivyokuwa anasujudu chini ya Arshi akiwa ameweka angani mbawa zake pana za kutisha mashariki na magharibi, basi yeye kwa hiyo ana uwepo kila mahali kulingana na ukubalifu wa mahali hapo, na uhudhuriaji katika wakati mmoja katika maelfu ya mahali. Na kama hivi, basi kulingana na njia hii: Sio muhali katu, wala hilo si jambo la juu ya ilivyozoeleka, wala si jambo lisiloingia akilini, kupata mfano wa malaika wa mauti kuwepo kwa mwanadamu wakati wa kuchukua roho yake – nao ni mfano wa kisehemu wa kibinadamu – kwa kofi la Sayyidina Musa (a.s) naye ni haiba kubwa yenye heshima katika ulul-azmi miongoni mwa Mitume. Kisha yeye kulipofua jicho la sura hiyo ya kimfano ya malaika wa mauti, ambaye amevaa mavazi ya sura hiyo. Njia ya pili: Kwamba Malaika watukufu katika mifano ya Sayyidina Jibril na Mikail na Izraili (a.s), kila mmoja kati yao ni sawa na mwangalizi mkuu au Raisi, wana wasaidizi wa aina yao na katika wanaoshabihiana nao, lakini kwa sampuli ndogo. Basi hawa wasaidizi wadogo ni wenye kutofautiana kulingana na kutofautiana kwa viumbe waliowakilishwa kwao. Basi ambao wanatoa roho za wema wanatofautiana na wanaochukua roho za wabaya, basi hao ni makundi tofauti ya malaika mfano wa zinavyoashiria aya tukufu: وَالنَّازِعَاتِ غَرْقًا ۞ وَالنَّاشِطَاتِ نَشْطًا Basi kwa mujibu wa njia hii: Hakika Sayyidina Musa (a.s), hakumpiga kofi Sayyidina Izraili, bali aliupiga kofi mwili wa kimfano wa mmoja wa wasaidizi wake, na hii kwa anuani ya Unabii Mtukufu na nguvu ya mwili wake na umadhubuti wa umbo lake na hadhi yake mbele ya Mola wake Bwana Mlezi Mweza, na kama hivi jambo linakuwa linaingia akilini sana. Njia ya tatu: Tumekwishabainisha katika (Msingi wa nne kutoka katika neno la ishirini na tisa), na kwa mujibu wa maana za Hadithi tukufu za Mtume (s.a.w): Kuna katika malaika wanaomiliki vichwa arobaini elfu, na katika kila kichwa kuna ndimi arubaini elfu - yaani wana macho themanini elfu vilevile - na kila ulimi unaleta tasbihi arobaini elfu. Basi kwa kuwa malaika wenye kuwakilishwa wamewakilishwa kulingana na ulimwengu wa kushuhudiwa, nao wanawakilisha tasbihi za aina hiyo katika ulimwengu wa roho, basi hapana budi wao kuwa na sura hiyo na umbo hilo. Kwa sababu ardhi - mathalani - nayo ni kiumbe mmoja, inamsabihi Allah. Nayo inamiliki aina arobaini elfu katika aina mbali mbali, bali mamia ya maelfu ya aina hizo, na ambayo kila moja kati yake ni kwa nafasi ya vichwa vyenye kuletea tasbihi, na kila aina miongoni mwa aina hizo kuna maelfu ya idadi ambayo ni sawa na ndimi. Na kama hivyo. Basi malaika mwenye kuwakilishwa juu ya tufe la Ardhi inatakikana kuwa na vichwa arobaini elfu, bali mamia ya maelfu ya vichwa, na hapana budi kuwa kila kichwa na mamia ya maelfu ya ndimi. Na kama hivyo. Basi kwa msingi wa njia hii: Hakika Izraili (a.s) ana uso unaomwelekea kila mtu, na jicho linalo mtazama kila mtu, kwa ajili hiyo kofi la Sayyidina Musa (a.s) sio kofi katika ainisho la binafsi la Sayyidina Izraili – hasha - wala katika umbo lake la hakika, na hakuna dharau ndani yake, wala sio kumrudi, bali kitendo chake hiki kinatokana na kuwa yeye ni mwenye kupenda kuzidi kudumu jukumu la utume na kuendelea kubakia kwake, na kwa ajili ya hili alimpiga kofi - na haki yake kupiga kofi – jicho lile ambalo linaangalia muda wake, na ambalo linataka kukomesha jukumu lake katika Ardhi. Na Allah ni mjuzi zaidi wa lenye kusibu na hajui ghaibu isipokuwa yeye. اَللّٰهُ اَع۟لَمُ بِالصَّوَابِ لَا يَع۟لَمُ ال۟غَي۟بَ اِلَّا اللّٰهُ قُل۟ اِنَّمَا ال۟عِل۟مُ عِن۟دَ اللّٰهِ هُوَ الَّذٖٓى اَن۟زَلَ عَلَي۟كَ ال۟كِتَابَ مِن۟هُ اٰيَاتٌ مُح۟كَمَاتٌ هُنَّ اُمُّ ال۟كِتَابِ وَاُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ فَاَمَّا الَّذٖينَ فٖى قُلُوبِهِم۟ زَي۟غٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِن۟هُ اب۟تِغَٓاءَ ال۟فِت۟نَةِ وَاب۟تِغَٓاءَ تَا۟وٖيلِهٖ وَمَا يَع۟لَمُ تَا۟وٖيلَهُٓ اِلَّا اللّٰهُ وَالرَّاسِخُونَ فِى ال۟عِل۟مِ يَقُولُونَ اٰمَنَّا بِهٖ كُلٌّ مِن۟ عِن۟دِ رَبِّنَا وَمَا يَذَّكَّرُ اِلَّٓا اُولُوا ال۟اَل۟بَابِ
Source text is preserved. When a suitable model is available, translation is displayed separately.
Mektubat
The Twenty-Eighth Letter
بِسْمِ اللّٰهِ الرَّحْمٰنِ الرَّح۪يمِ وَ اِن۟ مِن۟ شَى۟ءٍ اِلَّا يُسَبِّحُ بِحَم۟دِهٖ Imejaa Quran Tukufu kwa bayana yake ya miujiza, na inahimiza kushukuru kwenye aya nyingi kama vile; اَفَلَا يَش۟كُرُونَ اَفَلَا يَش۟كُرُونَ وَسَنَج۟زِى الشَّاكِرٖينَ لَئِن۟ شَكَر۟تُم۟ لَاَزٖيدَنَّكُم۟ بَلِ اللّٰهَ فَاع۟بُد۟ وَ كُن۟ مِنَ الشَّاكِرٖينَ Na inabainika katika aya hizi; katika amali kubwa anazozitaka Allah Muumba Mwingi wa huruma kwa waja wake ni shukurani, na anawalingania waja wake kwenye shukurani mlinganio wa wazi ulio bayana, na ameupa umuhimu maalum, kwamba kwamba kuachana na kushukuru ni kukadhibisha neema za Allah na kuzikufuru, na ameuliza dhidi ya hilo mara thelathinii na moja ndanii ya Quran, ndanii ya surat Alrahman فَبِاَىِّ اٰلَٓاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ makemeo mazito ya kutisha, na kuwahadharisha wote majini na wanadam kwamba kukosa kushukuru na kuzipinga ni kukadhibisha na kupinga kwa wazi kabisa. Kwa mfano kama huu Quran Tukufu imebainisha kwamba kushukuru ni sababu ya kuumbwa na lengo lake kuu. Ulimwengu ni mfano wa Kitabu cha Allah kilicho wazi cha kutazama,na kinamaanisha wazi kwamba lengo la kuumbwa viumbe ni kushukuru, na hakika ukizingatia sana kwenye viumbe itakubainikia yafuatayo: Hakika umbile la ulimwengu na viliomo ndani vimeumbwa katika hali ya kupelekea kushukuru, kila kitu kinaelekeza kwenye shukurani, na ndio maana utaona kuwa tunda kuu katika mti wa maumbile ni shukurani, na hakika bidhaa bora kabisa yenye thamani, yenye kuzalishwa na kiwanda cha ulimwengu ni hii shukurani na hakika tunaona kwamba; Viumbe ndani ya ulimwengu vimeumbwa katika maumbo ya duara kubwa, na maisha yakaumbwa ndio nukta ya mazingatio, ndio maana tunaona viumbe vyote vinatumikia maisha na kuyalinda na kuyaelekea, na kuyadhaminia mahitajio yake yote ya lazima, hakika Mola Muumba wa ulimwengu anayachagua maisha baina ya viumbe vyake. Tunaona pia viumbe vyengine vyenye uhai, vimeumbwa kwa njia ya duara pana na mwanadamu ndie anaechukua nafasi ya kati, na malengo makuu katika viumbe hivi yanarudia kwa mwanadam, Allah Muumba anavikusanya viumbe vyote hivyo kwa mwanadam, na akaviwepesisha kwa ajili ya huduma yake, akamfanya mwanadam kuwa ni bwana na mwenye kuviendesha, kwa maana inabainika kuwa Allah amemchagua mwanadam baina ya viumbe, bali akamjaalia kuwa ndie alieshika nafasi ya mwanzo katika matakwa yake na ubora wa uchaguzi wake. Tunaona ulimwengu wa mwanadam pamoja na ulimwengu wa wanyama, ni mfano pia wa duara, na kati kati pamewekwa riziki, na pakapambwa hamu na shauku ya kupata riziki kwa mwanadam na mnyama, tunawaona wote kwa pamoja ni watumishi wa hiyo riziki na wamewepesishiwa, riziki zinawaongoza na zinawatawala, na tunaiona riziki nayo kuwa ni hazina kubwa pana yenye utajiri wala haziwezekani kuhesabika, kama tunavyoona hisia ya kuonja kitu (ladha) imeumbiwa vipimo imara kwa mujibu wa vyakula na kuweza kupambanua baina ya aina na aina ya riziki hizo, Ukweli wa riziki ni jambo la maajabu mno kwa viumbe na ni lenye maajabu na mishangazo pia ni lenye utamu mkubwa na kamilifu. Tunaona kama vile ulivyozunguka kila kitu, kwa riziki na kusimamia na kuitunza, hivyo riziki yenyewe kwa wenyewe na aina zake zote ni zenye kusimama juu ya shukurani kwa kila hali kimaada kihali na kimaneno, na inapatikana shukurani, na inazalikana shukurani na kubainika na kuijuilisha, kwani hakika hamu na shauku ya kupataa riziki ni aina ya shukurani ya kimaumbile. Ama kupata raha na ladha zote nazo ni shukurani, kwa njia isiyo ya hisia, kama vile wanavyostarehe wanyama kwa ujumla na shukrani hii- lakini mwanadam ni kiumbe pekee mwenye kuweza kugeuza shukrani hii ya kimaumbile kwa kuelekea kwenye upotofu na kufuru, hivyo kuporomoka kutoka kwenye shukurani kwenda kwenye shirki. Yale yanayobebwa na neema yenyewe ni riziki, kwa maumbile mazuri ya kuvutia na maumbo ya kupendeza na harufu tamu na njema, na katika vyakula vitamu na vionjo vizuri, yote hayo si vyengine ila ni dalili na vivutio vya shukurani, waongozaji hao na vivutio hivyo ni wanadiaji wazuri wenye kupigia chapuo shauku kwa viumbe na kuwahimiza kuja kwao na kuwasukuma kwa shauku hii katika kufanya mema na kuheshimu, na wanaipokea shukuran kwao kimaana, pamoja na kwa kuvutia wale wenye hisia kuweza kuzingatia na kuwafanya wapendezwe nayo na kushangazwa nayo, na kuwaelekeza neema hiyo njia ya kushukuru kwa kauli na amali, na inawafanya wawe ni wenye kushukuru, na kuwapa kupitia shukrani, ladha bora na ya kipekee yenye thamani zaidi, kwa yale yenye kuwadhihirikia, kwamba hakika riziki hizi ni bora na neema nzuri, pamoja na ladha yake ya dhahiri na fupi na ya muda maalum ni yenye kukupelekea kushukuru na tafakuru katika hadhira ya Allah mwenye rehema, yenye kubeba ndani yake ladha na kionjo vyenye uhakika na vya kudumu visivyokwisha, na kwa ukumbusho huu wa riziki na kurejea kwa Allah aliye mkarimu mwenye kumiliki hazina ya rehema iliyo kubwa kabisa, ukarimu usio na mipaka wala mwisho wa utamu wake, unampa mwanadam kwa mazingatio haya ladha za kiroho za peponi zenye kudumu nae akiwa bado yupo hai duniani. Wakati ambao riziki kupitia shukuru zinakuwa na hazina pana iliyojaa na kumwagika kwa kujitosheleza na starehe, inamfanya mtu aporomoke kwa kasi kubwa kwa sababu ya huko kukosa kushukuru na kuona kama kwamba amejitosheleza. Tumebainisha katika (neno la sita), kwamba kazi kubwa ya ulimi ukiwa umeelekezwa kwenye njia ya Allah, kwa maana unapoelekea kwenye riziki ya kutekeleza wajibu wa kushukuru, na nguvu na hisia hizo za ulimi ni mfano wa, mlinzi mheshimiwa na mwenye shukurani, hivyo huwa sawa na mwenye heshima mwenye kushukuru, kwenye ukwasi wa Allah, lakini inapokuwa unafanya kazi zake kwa ajili ya matamanio ya nafsi yenye kuamrisha maovu na kushibisha shahawa yake tu, kwa maana ya kutumia neema pasina kukumbuka mneemeshaji wa riziki hizo kwake, unaporomoka ulimi kutoka kwenye daraja yake bora tukufu, ya uaminifu hadi kufika mlinzi wa kiwanda cha tumbo na mlinzi wake, na kama hivi anaporomoka mhudumu wa riziki chini kabisa na kuachana na shukurani, kama wanavyoporomoka wengine, kutoka daraja bora kuja ya chini, kufikia ya mbali baina yake na hekima za Muumbaji. Hakika kipimo sahihi cha shukurani ni ukinaifu na kuwa mchumi na kuridhia na kutoa, ama kipimo cha kukosa shukurani na kuachana nayo, ni ubakhili na israfu na kushindwa kukadiria na kuheshimu, na kupenda kukusanya kila kinachompitia bila ya kupambanua baina ya halali na haramu. Hakika licha ya pupa la ubakhili ni kwenda kinyume na kuacha kushukuru, bali ni kiongozi mkuu na njia kuu ya udhalili na kujidogosha, kama mduduchungu au siafu aliye bora mwenye kumiliki maisha ya kijamii, anakanyagwa na kupondwa chini ya miguu na kuvurugika, pengine kwa pupa lake na udhaifu wake katika kukinai, licha ya kwamba chembe chache za ngano zingalimtosha kwa mwaka mzima, lakini utamuona ni mwenye kukusanya chembechembe nyingi na kwa maelfu. Ama nyuki mbora, na kwa ukinaifu wake kamilifu ni kuruka juu ya vichwa vya watu, mpaka anakinai kwa asali yake na kutoa asali kwa ajili ya mwanadam, kwa ukarimu wake kwa amri ya Allah. Kweli hakika jina la Arrahaman ambalo ni katika majina makuu katika majina yake Allah linafuatana na jina lake Allah. Ambalo ni jina la lake lililo kubwa la dhati iliyo tukuka,na hakika jina hili la Arrahman linabeba kwa usimamizi wake riziki, hivyo tunaweza kufikia nuru ya jina hili kwa kushukuru, ambazo zimejaa kwenye riziki, tukijua kwamba maana kuu ya Arrahman imo kwenye jina lake la Arrazaq. Shukurani ziko aina tofauti, ama jumla ya aina hizo na kamilifu yake ni sala, kwenye kushukuru kunapatikana imani safi na tamu, nayo ni tawhid ya kweli, kwa mfano mwenye kula tufaha, akaanza kwa bismillah na kumalizia kwa Alhamdulillah, huwa ni mwenye kutangaza shukurani, tufaha lile huwa ni lenye kumkumbusha qudra ya Allah moja kwa moja, nayo ni zawadi kutoka kwenye hazina ya Allah (Mkwasi), kwa kauli kama hii na itikadi kama hii anakuwa anasalimisha kila kitu kwenye mikono na qudra ya Allah, na anatambua kuenea rehema za Allah katika kila kitu, na ndipo anapodhihirisha imani ya uhakika kwa kushukuru na kubainisha imani ya kweli na sahihi. Hapa tutabainisha mtazamo mmoja tu, wenye kuonyesha hasara nyingi ambazo mwanadam aliyeghafilika huporomoka kwa sababu ya kukufuru kwake neema na kukanusha. Anapotumia au kula mwanadam neema iliyo tamu, na akashukuru, hakika neema hiyo huwa kwa kupitia shukrani, mfano wa nuru yenye kumurika, na kubadilika na kuwa ni matunda ya peponi, ziada ya kuwa ni yenye kumpa ladha, hakika kuwepo fikra kwamba ni matunda miongoni mwa matunda ya kuzingatia rehema za Allah zilizo pana na ukarimu wake Allah, neema hizo zinampa ladha ya kudumu, bora za kudumu bila mipaka, hali hii inamfanya mwenye kushukuru anakuwa ni mwenye kutanguliza vitu bora na safi na vyenye maana kwenye daraja za juu - akiacha nyuma takataka na maganda yasiyo na faida, na haja tena, na kubadilika uchafu au kinyesi kinachorudi tena kwenye asili yake ya mwanzo. Lakini mwanadam aliyeneemeshwa na Mola wake anapoacha kumshukuru aliyemneemesha, hakika neema ile na ladha ile hugeuka na kuacha machungu na maumivu makali na majuto na kuwa ni uchafu na kubadilika badala ya kuwa ni almasi kuwa ni makaa yenye kuunguza. Riziki zenye kupita hugeuka kwa kushukuru kuwa ladha za kudumu, na matunda yenye kubaki, ama neema isiyo na shukurani inabadilika kutoka sura yake nzuri ya kupendeza na kuwa ni yenye sura ya kutisha na kuchukiza iliyo mbaya, kwani aliyeghafilika daima hufikiria kuwa mwisho wa ladha ni kinyesi tu. Kweli kabisa riziki ni yenye sura ya kung’ara na inastahiki mapenzi, ambayo hudhihirisha shukurani, ama kinyume chake, hakika mapenzi ya walioghafilika na kupotea kuitambua riziki na kuwa mbali nayo, huwa ni sawa na wanyama. Pima haya ili ujue kiwango cha hasara cha wale waliopotea na kughafilika na uovu wa mambo yao. Kiumbe mwenye kuhitajia zaidi riziki na aina zake ni mwanadam, Allah Mtukufu amemuumba mwanadam akiwa ni kioo cha majina yake Allah mazuri, na akampa muujiza wenye kuonyesha qudra zake pana, hakika mwanadam ni mwenye kumiliki kiungo, kinachomwezesha kujua na kutathmini hazina za Allah na rehema zake na kuzitambua. Allah amemuumba kwa umbo la khalifa wa ardhi mwenye kumiliki nyenzo nyeti na kuweza kujua ubora wa majina ya Allah kwa undani, lakini kwa yote haya Allah amempa mwanadam ufakiri usio na mipaka unaomfanya awe ni mwenye kuhitaji daima aina za riziki zisizo na mipaka ya riziki ima za kiroho au kimaada, na wasila na njia pekee ya kumpandisha daraja na kuwa ni kiumbe (ahsan taqwiim) hakuna zaidi ya shukurani. Ama ikipotea na kutoweka hakika mwanadam anaporomoka na kuwa katika wa chini kabisa, na anakuwa ni mwenye kufanya dhuluma iliyo kubwa. Kwa ufupi kabisa, hakika shukuru ni msingi mkuu katika misingi minne anayoitegemea mwenye kufuata njia tukufu nayo ni njia Al - ubudiyya walhubbu lillah taala na kupendana imetajwa misingi hiyo minne kuwa ni: Udhaifu kwa Allah, Kumuhitajia Allah, kuwa na shauku na Allah, na kumshukuru Allah. اَللّٰهُمَّ اج۟عَل۟نَا مِنَ الشَّاكِرٖينَ بِرَح۟مَتِكَ يَا اَر۟حَمَ الرَّاحِمٖينَ سُب۟حَانَكَ لَا عِل۟مَ لَنَٓا اِلَّا مَا عَلَّم۟تَنَٓا اِنَّكَ اَن۟تَ ال۟عَلٖيمُ ال۟حَكٖيمُ اَللّٰهُمَّ صَلِّ وَ سَلِّم۟ عَلٰى سَيِّدِنَا مُحَمَّدٍ سَيِّدِ الشَّاكِرٖينَ وَ ال۟حَامِدٖينَ وَ عَلٰى اٰلِهٖ وَ صَح۟بِهٖ اَج۟مَعٖينَ اٰمٖينَ وَ اٰخِرُ دَع۟وٰيهُم۟ اَنِ ال۟حَم۟دُ لِلّٰهِ رَبِّ ال۟عَالَمٖينَ

