Kufunga mwezi wa Ramadhani, inakuja katika mwanzo wa nguzo tano za uislam, na saumu katika ibada tukufu za kiislam. Nyingi ya hekima zenye kumiminika tokasaumu ya mwezi wa Ramadhani, ni zenye kubainisha rububiya ya haki ya Allah aliyetukuka, vilevile kama zinavyomiminika katika maisha ya mwanadam ya kijamii na maisha ya mwanadam kipekee, na zinamiminika pia katika kuilea na kutakasa nafsi, na katika kushukuru neema za Allah. Tutataja neema moja baina ya neema nyingi sana, ambayo inasimama ndani yake utukufu na rububiya ya haki ya Allah aliyetukuka kuputia saumu, nayo ni kwamba Allah ameumba uso wa dunia mfano wa meza kubwa (ya vyakula) iliyo na neema nyingi asizoweza mtu kuzihesabu, na akaziandaa vyema hakuna awezae kufanya hivyo kwa maana hii Allah amebainisha ukamilifu wa rububiya yake na rehema zake, lakini mwanaadam hadiriki hayo kwa ukamilifu, chini ya pazia la mghafiliko, na licha ya pazia la sababu, ni ukweli usio na shaka,- ukweli unaothibiti faida zake kwenye mazingira ya kawaida, pia anaweza kusahau baadhi ya nyakati-. Ama katika wakati wa Ramadhani tukufu, waumini wanakuwa mfano wa askari kwenye amri za uongozi mkakamvu, wanafuata amri, wanakuwa wote kwa pamoja ni wenye kutekeleza amri za Mola, na wakati wa kabla ya kufutari wanakuwa tayari kufuata amri za Allah mtukufu (Karibuni kwenye meza ugeni wa ukarimu) na wanaitikia kwa hali yao hii rehema kubwa kamilifu pana na tukufu. Jee wanastahiki wale ambao hawakushiriki katika utumwa huu mtukufu (mbele ya Allah), viumbe kama hivi kuitwa wanaadam?
Source text is preserved. When a suitable model is available, translation is displayed separately.
Mektubat
The Twenty-Ninth Letter
Kuna hekima nyingi kwenye kufunga saumu ya Ramadhani, kwa kushukuru neema ambazo Allah ametupa. Kati ya hizo ni kile chakula kilichotayarishwa na mtumishi kutoka jiko la mwenye uwezo, hakika ni chenye thamani, kama tulivyotaja kwenye (zingatio la mwanzo), haitakuwa ni akili kudai kwamba chakula hicho kizuri cha thamani, kuwa hakina hadhi wala kutomjua Mneemeshaji wa kweli, wakati ambao mtumishi anahangaika anaandaa na kutoa zawadi kwa watu, Hivyo vyakula na neema zisizohesabika ambazo Allah amezileta katika ardhi, zote tunatakiwa sisi thamani yake na thamani yake ni kushukuru. Ama katika sababu za kidhahiri katika neema hizi na wale walioneemeshwa ni mfano wa watumishi ambao sisi huwa tunawalipa vya kutosha thamani ya kazi yao, na inaonekana kama kwamba wao ndio wenye fadhila nyingi zaidi ya vile wanavyostahiki, wakati ambao mneemeshaji wa uhakika ni Allah, anaestahiki kwa kuleta neema hizi kumtangulizia shukrani za dhati na kuzipokea na kuziridhia, nae ndiye anayestahiki hayo zaidi, hivyo kurejesha shukrani kwa Allah na kuonyesha kuridhia hizo neema, inatokana na kuwa na elimu ya kwamba neema hizo ni zenye kutoka kwake Allah moja kwa moja, hivyo ni dharura kuzikadiria na kuheshimu thamani yake na kuwa na hisia za kuwa na haja nazo. Hakika kufunga Ramadhani ni ufunguo bora wa shukurani ya hakika na yenye ikhlasi kwa Allah, kwani watu wengi huwa hawatambui thamani ya neema nyingi, na wanakuwa kama kwamba hawana umuhimu nazo baadhi ya wakati, mfano wa wale wasio na njaa au kujua madhara ya njaa, hawajui umuhimu wa mkate mkavu uliokauka, na hawa ni wale walio matajiri na hali nzuri, lakini muumini anayatambua haya wakati anapotaka kufutari kwamba ni neema ya kiungu iliyo kubwa, na inashuhudiwa na nguvu zake zenye utamu, kwa hivyo wanapata wenye kufunga ,kuanzia kiongozi hadi fakiri wa chini kabisa shukurani za kiroho kwa Allah alietukuka kwa kudiriki kwao ukubwa wa neema hizo, Ama mtu kujizuilia na kula mchana kutwa ni njia yenye kumpelekea kutambua uhakika wa neema hii, kwani huwa anazungumza na nafsi huku akisema “Hakika neema hizi siyo miliki yangu, nami siko huruwa kuzitumia, bali ni zenye kurudi kwa aliye Pekee Mmoja, na ni katika neema na ukarimu wake, na mimi niko nasubiri amri zake” Katika hali kama hii anakuwa ameshukuru neema hii kiroho. Kwa sura hii saumu ndivyo inapokuwa ufunguo wa kushukuru kwa njia tofauti, Shukurani ambayo ndiyo kazi kuu ya mwanadamu.
Hekima moja kati ya hekima nyingi za saumu, ni yenye kuelekeza kwenye maisha ya kijamii ya mwanaadam, nayo ni kwamba watu wameumbwa katika hali tofauti za kimaisha, na ndio maana Allah akawataka matajiri kunyoosha mikono yao ya msaada kwa ndugu zao mafakiri. Hakuna shaka kwamba matajiri hawawezi kuwa na hisia za ukweli kabisa juu ya ufukara kwa sababu ya utajiri wao, wala hawawezi kuwa na hisia za ndani kabisa mbele ya njaa, isipokuwa tu kupitia njaa itokanayo na funga, Laiti kama siyo saumu isingalikuwa rahisi kwa matajiri wenye kufuata matamanio, kuweza kudiriki, ni kiasi gani makali ya njaa yapo, na kiasi gani mafukara wanahitajia mapenzi na huruma zao,ndio maana huruma ni jumla ya ghariza muhimu ya mwanaadam, nayo ni katika msukumo muhimu na wa kimsingi unaosukuma kufikia shukurani za uhakika, na kumfanya kila mmoja kumuona yeyote aliye fakiri zaidi yake kwa njia yoyote kuwa ana wajibu wakumhurumia. Kama kusingalikuwa na dharura ya kuionjesha nafsi makali ya njaa, hakuna yeyote yule ambae angalifanya ihsani kwa wengine,jambo ambalo linahitaji nguvu za pamoja na mapenzi kwa wanaadam, na hata kama atafanya hivyo haitakuwa kwa hali ya ukamilifu kwani hatakuwa ndani ya nafasi yake na hisia kamilifu za kiimani.
Hakika saumu ya Ramadhani ni yenye kubeba upande wa malezi ya nafsi ya mwanaadam, hekima nyingi, kati ya hizo ni kwamba nafsi kwa maumbile yake, ni yenye kupenda kukata kamba na kuwa huru, hadi kufikia baadhi ya wakati kudai Ubwana na Uungu, hali kama hii ya uhuru usio wa kweli unapelekea kusahau kwamba, anakuwa na kulelewa ndani ya neema za Allah zisizo na mipaka, na hasa pale mtu anapokuwa ni mwenye kipato na uwezo katika hii dunia, mghafiliko ni wenye kumsaidia, na huwa kama vile mnyama anafanya mambo yake bila ya idhini wala ruhusa. Lakini nafsi (ya muumini) ina kutafakari na kupata akili yenyewe pale inapoanza ramadhani, kuanzia matajiri wa juu kabisa hadi kufikia fakiri wa chini kabisa, watu hudiriki kwamba sio wamilikaji wa chochote, bali wao ni wamilikiwa, wala sio huru uhuru usio na mipaka, bali ni waja (watumwa wa Allah) walioamrishwa, hawezi kufanya jambo lolote ila kwa amri, bali hata kuunyoosha mkono kuchukua maji hauwezi, na kwa hali hii ndio inapovunjikavunjika ghururi ya ubwana wa uongo, na kupokea utumwa sahihi kwa Allah, na akaingia kwenye wajibu wake wa uhakika ambao ni (shukurani).
Hakika funga ya ramadhani ni yenye hekima nyingi katika kuielekeza nafsi na kuilea dhidi ya nafsi yenye kuamrisha mabaya, kuzipima na kuzitathmini akhlaki na tabia zake na kuifanya ikomboke dhidi ya kufanya mambo bila ya nadhari na kwenda ovyo; nahapa tutataja hekima moja. Nafsi ya mwanaadam ni yenye kusahausahau uhakika wake na kughafilika, na haijitambui ilivyokuwa ni yenye ajizi isiyo na mipaka na ufakiri usio na mwisho, na mapungufu mazito, lakini haipendelei kuyaona yote haya kuwa inayo, wala haifikirii udhaifu ulionayo, na kiasi gani inaweza kuondoka mara moja, kiasi gani mitihani na majanga yanaisogelea, vilevile husahau kwamba kaumbwa kwa nyama na mifupa inayooza na kuyayuka haraka haraka, lakini bado tasarufu zake sio za busara, kama kwamba ameumbwa kwa shaba, na ameondoshewa mauti, nae ni mwenye kubaki daima, utaiona nafsi yake inavamia dunia na kufunikwa na guo lake akiwa na tamaa ya kila kitu na kuwa na mahusiano na mapenzi makubwa ya shauku, kuvamia kila chenye ladha faida (chache), katika hali kama hii humsahau Muumba wake, mwenye kumlea kwa ukamilifu wa mapenzi na huruma, na kama hivi huporomoka ndani ya shimo la matamanio na akhlaqi mbovu akisahau mwisho mbaya katika maisha ya dunia na maisha ya akhera. Lakini funga ya Ramadhani inamzindua mtu aliye ndani ya mghafiliko mkubwa kabisa na alie asi uasi mkubwa, udhaifu wake na ajizi yake na ufukara wake, Na kwa kupitia njaa (ya saumu), kila mmoja anafikiria nafsi yake na tumbo lake lililo tupu, anafikiri haja ya tumbo lake na anatafakari pia udhaifu wake, haja yake ya kupata rehema za Allah na mapenzi yake, hivyo hupata hisia ndani ya nafsi ya kugonga mlango wa maghufira ya Mola Mlezi, kwa ajizi kamili aliyonayo na ufakiri wake, huku akiachana na ufirauni wa nafsi, akiwa tayari kugonga mlango wa rehema za Allah, kwa mikono ya shukurani ndani ya nafsi yake. (maadam tu mghafiliko haujafisidi bado akili yake).
Na katika jumla ya hekima nyingi katika funga ya Ramadhani ni maelekezo katika kuteremshwa Quran tukufu, na kwamba mwezi wa Ramadhani ni wakati muhimu ulioteremka Quran, na hapa tunazungumzia hekima moja tu. Ilivyokuwa Quran tukufu imerteremka ndani ya mwezi wa Ramadhani mtukufu, ni lazima kujitakasa na mambo madogo madogo ya nafsi, na kuachilia mbali mambo yasiyo ya kimsingi, na kujitayarisha na kupokea kauli ya mbinguni, kwa matayarisho yanayolingana nayo, nayo ni kwa kuwa tayari kuipokea wakati wa kuteremshwa kwake katika mwezi huu, na kujishabihisha na hali za kiroho za kimalaika, kwa kuacha kula na kunywa, na kwa kuisoma Quran kisomo kama kwamba aya zake ni zenye kuteremka hivi sasa, na kwa kuizingatia vyema kwa hisia za unyenyekevu kamili, na kusikiliza vyema, maelekezo ya kiungu yaliyomo, ili kupanda daraja tukufu, na kuwa na hali bora ya kiroho, kama kwamba msikilizaji anaisikiza moja kwa moja kutoka kwake Mtume عَلیهِ الصَّلاةُ و السّلام, bali anasikiliza kwa makini zaidi kama kwamba anaisikia moja kwa moja kutoka kwa Jibrili عَلیهِ السّلام, bali pia kama kwamba anaisikia moja kwa moja kutoka kwake Allah. Na akasimama kwa kuifikisha na kuisoma kwa wengine, na kuwabainishia hekima katika hekima za kuteremshwa kwake. Hakika ulimwengu wa kiislam ndani ya ramadhani, unabadilika mfano wa msikiti, msikiti mtukufu ulioje uliokusanya kila pembe na zawiya zake mamilioni ya mahafidhi wa Quran, wanasoma maelekezo ya mbinguni ya kiungu kwa sauti za viumbe wa ardhini, na wanaidhihirisha kwa mtindo mwema, wakithibitisha kauli yake Allah شَه۟رُ رَمَضَانَ الَّذٖٓى اُن۟زِلَ فٖيهِ ال۟قُر۟اٰنُ . Huku wakiwa ni wenye kuthibitisha hakika mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa Quran, na huku wengine wako wanawasikilliiza kwa makini na kwa khushuu na unyenyekevu mkubwa, na wengine wakikariri aya wenyewe kwa wenyewe. Ubaya ulioje ni kule kujitoa ndani ya msikiti huu mtukufu, na kwa hali ya kutisha na kuwa nyuma ya vyakula na vinywaji tu, na kufuata matamanio ya nafsi yenye kuamrisha maovu, kiasi gani mtu kama huyu anakuwa ni mwenye kutishia wale waliomo ndani ya msikiti? Na kama hivi ndivyo inavyokuwa kwa wale wanaowapinga wenye kufunga ramadhani, wanakuwa ni wenye kudogoka na kuwa duni ndani ya nafsi zao, na kwa waislam wote wa ulimwengu wa kiislam.
Hakika saumu ya Ramadhani ni yenye kumnyanyua mwanadam, ambae ameletwa duniani kwa ajili ya, kuongoza machumo ya akhera na biashara zake, hapa ni penye hekima nyingi, lakini sisi tutaikamata moja tu katika hizo, Nayo ni kwamba thawabu za matendo ndani ya ramadhani ni zenye kuongezeka moja kwa elfu. Ni jambo lenye kueleweka wazi kwamba kila herufi moja ya Quran ni yenye thawabu kumi, zenye kupatia matunda kumi katika matunda ya peponi, kama ilivyokuja katika hadithi tukufu,na katika mwezi wa ramadhani kila herufi ni yenye kuzalisha elfu katika matunda hayo ya kiakhera, badala ya kumi, na katika kila herufi miongoni mwa jumla za aya za Quran, mfano ayatu alkursiy, ni yenye kufunua mlango mbele ya maelfu ya thawabu hivyo kuweza kupata machumo ya uhakika huko akhera, na zinaongezeka thawabu hizo, kwa kupitiwa na siku za ijumaa ndani ya Ramadhani hadi kufikia elfu thelathini kwa thawabu za usiku wa Laylat alqadr. Kweli hakika Quran yenye kutoa kwa kila herufi matunda elfu thelathini yenye kubaki, yanakuwa ni mfano wa mti wa nuru, kama vile mti wa –altuba- peponi, ambao unamtajirisha muumini ndani ya ramadhani kwa matunda ya milele na kudumu,ambayo ni kwa mahesabu ya mamilioni. Hebu zingatia biashara hii tukufu yenye faida, na tupia jicho la mazingatio, na halafu fikiria vyema kwa wale wasiofahamu kima cha herufi hizitukufu, ni hasara ilioje kwao? Kama hivi ndivyo ulivyo mwezi wa Ramadhani, mfano wa maonyesho makubwa ya biashara yenye kupendeza kwa ajili ya bidhaa za akhera, au ni kama vile soko lililojaa harakati, na faida katika biashara hii ni mfano wa ardhi yenye rutuba nyingi na uwezo wa kuzalisha kwa wingi mazao ya kiakhera, nayo ni mfano wa mvua yenye kunyesha kwenye msimu wa masika, na kuifanya mimea ikuwe na imee kwa baraka nyingi. Ni mfano wa siku ya iddi iliyojawa na furaha, kwa kuwemo mfurahiko wa waja mbele ya utukufu na ulezi wa Allah kwao uliojaa utukufu na heshima. Kwa hali kama hii mwanaadam amekuwa ni mukalafu kwa kufunga, ili aepukane na kuporomoka kwenye shahawati za kinyama, kama vile kula nakunywa dhidi ya mahitajio ya kinafsi kwa kughafilika nayo, na aepukane na kuzama kwenye matamanio na kwenye mambo yasiyomuhusu, anakuwa mja kupitia saumu ni sawa na kioo chenye kuakisi yaliyo (ndani ya nafsi) na anakuwa kwa kipindi fulani ameepukana na ulimwengu wa kinyama na kupanda kwenye ulimwengu wa kimalaika, au ni sawa kuwa amekuwa ni mtu wa kiakhera na kiroho, na dhahiri kwa mwili, kwa kuingia kwake katika biashara ya kiakhera na kuachana na matamanio ya kidunia kwa muda maalum. Hakika mwezi wa Ramadhani ni wenye kumuongezea mja katika dunia hii yenye kupita na umri huu wenye kumalizika, na katika uhai huu ulio mfupi; umri wenye kubaki na mrefu wa kudumu, inawezekana kwa mwezi mmoja tu wa ramadhani mtu kupata machumo ya umri unaofikia miaka themanini, na haya yamo ndani ya laylat alqadri kama ilivyokuja ndani ya Quran nayo ni hoja ya wazi kabisa. Ni mfano wa kiongozi wa nchi, ambae huchagua siku maalum katika uongozi wake, au kila mwaka, ima iwe ni siku ya kumbukumbu yake ya kuja kwenye kiti, au siku maalum ya kukumbuka tokeo fulani, hufanya siku hizo ni sherehe kwa raia zake, utamuona kiongozi huyo hawafanyii raia zake wakweli muamala wanaostahiki, bali hufanya kama kwamba ni mwenye kuwafanyia ihsani na kuwaneemesha na kuwapa fadhila zake. Atawaita kwenye diwani zake (ofisi) bila ya vipingamizi, kuwapa huduma maalum zisizo za kawaida, na kuwapa maelekezo yake mema, mfano wa haya yako kwa Allah mwenye uwezo, na utukufu na ukarimu na mwenye mamlaka kuu yenye zaidi ya sayari kubwa elfu kumi na nane, ameteremsha katika mwezi wa Ramadhani amri zake tukufu na Quran yake tukufu yenye kulekeza kwenye ulimwengu wote, hivyo kuingia mwezi huu wa Ramadhani katika hukumu ya iddi na mnasaba wa furaha na sherehe na vikao vya kiroho yote hayo ni katika jumla ya hekima za Allah, kwa hivyo ikiwa Ramadhani ni yenye furaha zote hizi, ndivyo inavyopaswa kuamrishwa watu kufunga, ili wapande daraja, na kuepukana na mishughuliko ya kidunia ya kuporomoka, na ukamilifu katika saumu ni kuvizuia viungo vyake mwanaadam jicho, sikio, moyo na mawazo na fikira vyote hivi vinaingia katika saumu kama vile linavyofunga tumbo, yaani kuvizuia viungo dhidi ya mambo ya haramu na mambo ya kijinga, na yasiyomuhusu, na kuiongoza kwenye utumwa wa Allah. Mfano: Mtu huuzowesha ulimi wake kufunga dhidi ya uongo, kusengenya, matusi na anauzuia dhidi ya yote hayo, na anaulainisha kwa kusoma Quran na dhikri ya Allah na kumsalia Mtume عَلیهِ السّلام. Mfano wa pili: Anafumba macho yake dhidi ya mambo ya haramu, na analizuia sikio lake kusikiliza matusi, na macho yake anayapeleka kutazama yenye mazingatio, na masikio kusikiliza maneno ya haki, na viungo vyake vyengine kuwa ni vyenye kufunga. Inajulikana kwamba tumbo ni mfano wa kiwanda kikubwa, kikisimama kiwanda kazi zake kwa sababu ya funga, hivyo husita viwanda vidogo vidogo vyengine ni jambo jepesi na rahisi.
Hekima katika hekima nyingi za funga ya Ramadhani, ni yenye kufungamana na maisha ya mtu binafsi, tutabainisha kwa muhtasari kama ifuatavyo. Katika saumu kunapatikana aina ya tiba muhimu kwa mwanaadam (himaya) iwe ni ya kiroho au ya kiwiliwili, na himaya (himya) ni tiba muhimu bila shaka, kwani mwanadam kila inapofuata nafsi yake njia huru ya kula na kunywa, inamsababishia madhara ya kimwili katika maisha yake, na kama hivi ndivyo inavyokuwa hali yake ya kiroho, kwani kila anapovamia anachokutana nacho bila ya kuzingatia kilichomuhalalikia au kumharamikia, atafika mahala itakuwa ni vigumu kwa nafsi yake kutii moyo au roho yake, hivyo uongozi utakuwa ni mikononi mwake atajikuta kuwa ni huru kabisa, hivyo itamuelekeza mwanadam kwenye matamanio pasina kuwa kwenye mamlaka yake na maelekezo yake. Ama katika mwezi wa Ramadhani nafsi inakuwa imezowea kupata himaya, kupitia saumu, na inakuwa ni yenye kujitahidi kufuata njia ya kujitakasa na kuilea nafsi na kujifunza utiifu na kufuata amri, wala haisibiwi na maradhi yanayotokana na kujaza tumbo, na kuingiza chakula baada ya chakula, na inakuwa tayari kupokea maelekezo ya akili na sheria, na kujiepusha na kuzama katika mambo ya haramu, kama ilivyopokea maelekezo ya kuachana na mambo ya haramu, na inajitahidi kuacha kuharibu maisha yake ya kiroho. Wengi ya watu wanapata mtihani wa njaa, mara nyingi watu kama hawa wanahitaji zoezi, la njaa inayomuezesha mtu kuwa na subira na kustahamili, na saumu ya Ramadhani, inatoa fursa hiyo na kumfanya mtu awe na subira, kwa kuweza kubakia muda wa saa kumi na tano au hata saa ishirini na nne kwa aliyekosa daku, hivyo saumu ni kinga muhimu dhidi ya khofu au uchache wa subira ambayo ni chachu ya kuongezeka kwa misiba na mitihani ya mwanaadam. Tumbo nalo ni mfano wa kiwanda chenye wafanyakazi, na watumishi wengi, na kwa mwanaadam kuna mafungamano makubwa, na nafsi ikiwa haikusimamisha shughuli zake wakati wa mchana, kwa muda wa mwezi maalum, hivyo utawasahaulisha wafanyakazi na watumishi wake, ibada zao maalum na kuwasababishia kughururika na kuwa chini ya milki yake, na kuwababaisha na kuwafunika ndani ya vishindo vya kiwanda hicho na kuwafunika kwa moshi wake mzito, hivyo wafanyakazi wote na watumishi, watajikuta wameondoshewa mtazamo wao bora na wakasahaulishwa dhidi ya kazi yao tukufu kwa muda, na ndio maana watu wema na mawalii wema, daima hujizoesha kula kidogo na kunywa ili wapande daraja za ukamilifu. Lakini inapoingia mwezi wa Ramadhani, wanadiriki wafanyakazi na watumishi hawa kwamba wao hakika hawakuumbwa kwa ajili ya kiwanda hichi pekee, bali wote kwa pamoja wanataka kupata ladha tamu zaidi ya kiroho na kimalaika ndani ya Ramadhani, na wanazingatia katika kufutari zaidi kuliko, mambo ya laghau yenye kuporomosha amali, hivyo utawakuta waumini ndani ya Ramadhani ni wenye kuchuma faida nyingi za kiroho, kila mmoja kwa mujibu wa daraja yake (ya imani), na kunapatikana kupanda daraja kukubwa kimoyo, kiroho kiakili na mengi ya haya, licha ya tumbo kulia kwa njaa, lakini machumo haya yanaonyesha bashasha na kicheko.
Funga ya Ramadhani ni muhimu katika kuvunja fikira mbovu ya mwanaadam ya kudai ubwana wa nafsi yake, hivyo inaueleza ubwana (rububiya) katika usahihi wake na uwazi kabisa, na hapa tunatoa mfano. Nafsi haitaki wala haipendi kumjua Mola wake, bali ni yenye kutaka kudai ubwana (rububiya), wa kifirauni wa kibabe uliochupa mipaka, hata kama itaadhibishwa, na kuteswa, bado inabakia na mawazo hayo isipokuwa kwa nguvu za njaa. Saumu ya Ramadhani inatoa kichapo kizuri kwa nafsi iliyo na fikra za kifirauni, na kuvunjavunja nguvu zake na kuibainishia udhaifu wake, ufukara wake na kuifahamisha kuwa ni mtumwa wa Mola wake. Imekuja katika baadhi ya mapokezi ya hadithi; kwamba Allah aliiuliza nafsi “Nani mimi na nani wewe?” ikajibu nafsi “Mimi ni mimi na wewe ni wewe”, Allah akaiadhibu na kuitia jahannam, akaiuliza mara nyengine, ikajibu vile vile mimi na wewe ni wewe", Licha ya adhabu zote hizo bado ikawa ni yenye kujifanya ni ngumu, Allah akaitia kwenye adhabu ya njaa, kwa kuiacha bila ya kula, baadae akaiuliza "Ni nani mimi na ni nani wewe?" ikajibu "Wewe ni Mola wangu na mimi ni mja wako nisie na chochote." اَللّٰهُمَّ صَلِّ وَسَلِّم۟ عَلٰى سَيِّدِنَا مُحَمَّدٍ صَلَاةً تَكُونُ لَكَ رِضَاءً وَ لِحَقِّهٖ اَدَاءً بِعَدَدِ ثَوَابِ قِرَائَةِ حُرُوفِ ال۟قُر۟اٰنِ فٖى شَه۟رِ رَمَضَانَ وَ عَلٰى اٰلِهٖ وَ صَح۟بِهٖ وَ سَلِّم۟ سُب۟حَانَ رَبِّكَ رَبِّ ال۟عِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَ وَسَلَامٌ عَلَى ال۟مُر۟سَلٖينَ وَ ال۟حَم۟دُ لِلّٰهِ رَبِّ ال۟عَالَمٖينَ اٰمٖينَ İ’tizar: Şu ikinci kısım, kırk dakikada süratle yazılmasından, ben ve müsvedde yazan kâtip, ikimiz de hasta olduğumuzdan, elbette içinde müşevveşiyet ve kusur bulunacaktır. Nazar-ı müsamaha ile bakmalarını ihvanlarımızdan bekleriz. Münasip gördüklerini tashih edebilirler.
بِسْمِ اللّٰهِ الرَّحْمٰنِ الرَّح۪يمِ شَه۟رُ رَمَضَانَ الَّذٖٓى اُن۟زِلَ فٖيهِ ال۟قُر۟اٰنُ هُدًى لِلنَّاسِ وَ بَيِّنَاتٍ مِنَ ال۟هُدٰى وَ ال۟فُر۟قَانِ

