Sözler

The Eleventh Word

Source: risaleinur multilingual dataset, risale.site source · Risale-Nur multilingual research corpus
Risale reading plan
§1

بِسْمِ اللّٰهِ الرَّحْمٰنِ الرَّحِيمِ وَالشَّمْسِ وَضُحٰيهَا ❀ وَالْقَمَرِ اِذَا تَلٰيهَا ❀ وَالنَّهَارِ اِذَا جَلّٰيهَا ❀ وَالَّيْلِ اِذَا يَغْشٰيهَا ❀ وَالسَّمَٓاءِ وَمَا بَنٰيهَا ❀ وَالْاَرْضِ وَمَا طَحٰيهَا ❀ وَنَفْسٍ وَمَا سَوّٰيهَا ❀ اِلخ Ewe ndugu! Ukiwa unataka kufahamu kitu katika siri za hekima ya ulimwengu na talasimu lake, na fumbo la kuumbwa kwa ulimwengu, na alama za hakika ya swala, basi zingatia pamoja nami hekaya hii fupi ya kupigiwa mfano: Hapo zamani za kale, kulikuwepo na mfalme mwenye mali nyingi na hazina kubwa yenye aina zote za johari, almasi na zumaradi, pamoja na hazina nyingine za siri za ajabu mno! Na alikuwa ni mwenye elimu pana mno na maarifa mengi kamilifu, na mwamko wenye kukusanya sayansi za kuzungumza zisizo na mpaka, pamoja na stadi za juu na maarifa ya ufundi. Kwa kuwa kila mwenye uzuri na ukamilifu huwa anapenda kuushuhudia na kushuhudiwa uzuri wake na ukamilifu wake, kadhalika kwa mfalme huyu mtukufu. Alitaka kufungua maonesho makubwa ili aoneshe kazi za ufundi wake makini ili ayavute macho ya raia wake juu ya fahari ya ufalme wake na adhama ya utajiri wake. Na awadhihirishie katika yenye kufuru ada ya ufundi wake makini na maarifa yake ya ajabu na mageni yake. Ili ashuhudiwe uzuri wake na ukamilifu wake wa kimaanawi kwa namna mbili: kwanza: aone kwa dhati maonesho ya kazi zake kwa jicho lake linaloona vizuri na makini. Na pili: azione kwa jicho la mwingine. Na kwa ajili ya hekima hii, mfalme huyu alianza kujenga kasri kubwa na refu mno, na akaligawanya kwa namna ya kiufundi kuwa nyumba na vitengo kadhaa huku akiipamba kila sehemu kwa mapambo ya hazina zake anwai, na kulipendezesha kwa yaliyofanywa na mikono yake katika athari nyororo za utengenezaji wake na zilizo nzuri zaidi. Akalipangilia vyema na kuliratibu kwa fani za kina mno za ujuzi wake na hekima yake. Basi akaliandaa na kulipendezesha kwa athari za ajabu za mambo yenye kufurutu ada ya ujuzi wake. Baada ya kulitimiza na kulikamilisha, aliweka kwenye kasri hiyo meza za vyakula za kifahari na zenye kuleta furaha zinazojumuisha vyakula vyake vyote vitamu, na neema zake bora na za thamani, akihusisha kwa kila kundi kile kinachostahikia na kuafikiana nacho katika meza za vyakula. Kwa hivyo, akaandaa dhiifa ya fahari ya jumla, akibainisha wema, ufundi na ukarimu ambao haujawahi kushuhudiwa mfano wake. Hadi kana kwamba kila meza ya vyakula imejaa mamia ya kazi nzuri za ufundi makini na athari zake kwa neema alizoweka juu yake miongoni mwa neema ghali zisizodhibitika. Kisha, akawaita watu wa miji ya ufalme wake na raia wake ili washuhudie, watembee na waburudike. Akamfundisha mkuu wa wajumbe wakirimiwa wa kasri hilo yale yaliyomo katika kasri hilo kubwa miongoni mwa hekima za kuvutia, na yaliyomo pembezoni mwake na yanayojumuisha katika maana za kina. Akimhusisha yeye kuwa ndio mwalimu kiongozi na ustadhi mbobezi juu ya raia wake ili awafundishe watu adhama ya mjenzi wa kasri hilo na fundi wa vilivyomo miongoni mwa nakshi zenye kupendeza zilizowekwa kwenye vipimo. Na awe ndiye mtambulishaji wa alama zake na yanayohusu mapambo haya yaliyopangiliwa kwa kila waingiao, na ishara za kina zilizomo ndani yake, na upeo wa hoja yake juu ya adhama ya mwenye kasri na ukamilifu wake wa hali ya juu na uamhiri wake makini. Kwa kuwabainishia pia maelekezo ya sherehe za heshima, yakiwemo katika hayo adabu za kuingia na kutembea-tembea, na misingi ya kutembea kulingana na yanayomridhisha mfalme ambaye haonekani isipokuwa kwa nyuma ya pazia. Mwalimu huyu mzoefu anakaa katikati ya wanafunzi wake katika eneo pana mno miongoni mwa maeneo ya kasri kubwa. Wasaidizi wake walikuwa wametawanyika katika kila moja kati ya vitengo vyengine vya kasri. Mwalimu huyu alianza kutoa maelekezo yake kwa watazamaji wote kwa kusema: “Enyi watu hakika Bwana wetu mfalme wa kasri hili pana na la kuvutia, kwa kuijenga hivi na kwa kudhihirisha mnayoyaona mbele ya macho yenu katika mandhari, anataka ajitambulishe kwenu. Basi mjueni na mjitahidi kumjua vizuri. Na kwamba yeye kwa mapambo haya ya uzuri, anataka aipendezeshe nafsi yake kwenu. Basi jipendezesheni kwake. Kwa kutambua kwenu uzuri wa kazi zake na kuthamini kwenu ufundi wake. Na kwamba yeye anajipendeza kwenu na kukuonesheni mahaba yake kwa yale anayokupeni kwa wingi katika mema yake, neema zake na fadhila zake. Basi mpendeni kwa kuzisikiliza vyema amri zake na kwa nyinyi kumtii yeye. Kwa hakika anakudhihirishieni upole wake na huruma yake kwa takrima hii na kumimina neema. Basi nyinyi muadhimisheni kwa kushukuru. Kwa hakika anataka kukudhihirishieni uzuri wake wa kimaanawi kwa athari za ukamilifu wake katika vitu hivi vizuri na kamili vilivyotengenezwa. Basi na nyinyi dhihirisheni shauku yenu na pupa yenu kwa kukutana naye na kumwona na kupata radhi zake. Na kwamba yeye anakutakeni mumjue kwamba yeye ndio mfalme wa pekee katika utawala na uhuru kwa mnayoyaona katika alama zake maalumu, na muhuri wake mahususi, na nembo yake ambayo haiigiki juu ya vyote vilivyotengenezwa... Basi kila kitu ni chake na ni mahususi kwake. Kimetoka katika mkono wa uweza wake. Basi ni juu yenu mtambue vyema kuwa hakuna mfalme wala mtawala isipokuwa yeye. Basi yeye ni mfalme mmoja wa pekee ambaye hana mwenza wake wala mithili...” Mwalimu huyu mkubwa alikuwa anaongea na wenye kuingia katika kasri na watazamaji, mfano wa maneno haya ambayo yananasibiana na makamo ya mfalme na adhama yake na hisani yake. Kisha waingiaji wakagawika katika makundi mawili: Kundi la Kwanza: Ni wale wenye akili zenye nuru, na nyoyo safi zilizotulia na wenye kujitambua kadiri yao. Basi popote wanapotembea katika maeneo ya kasri hili kubwa na kutawanyika kwa wao kuyatazama maajabu yake wakisema: Hapana budi katika hili kuna jambo kubwa!! Na hapana budi kwamba nyuma yake kuna shabaha ya hadhi ya juu!.. Wakajua kwamba hakuna upuuzi, wala huo si mchezo wala si puo la kitoto... Na kutokana na tahayuri yao wameanza kusema: Unaona wapi upo ufumbuzi wa fumbo la kasri hili, na nini hekima ya tuliyoyashuhudia na tunayoyashuhudia?! Wakiwa wanatafakari na wanajadiliana katika jambo hili, tahamaki wanasikia sauti ya hotuba ya ustadhi mjuzi na taarifa yake ya kuvutia. Wakatambua kwamba yeye ana funguo za siri zote na fumbuzi za mafumbo yote. Wakamwendea kwa haraka: Assalamu alaykum ewe ustadh! Hakika kasri kama hili la fahari linapasa liwe na mtambulishaji, mkweli, makini na mwaminifu kama wewe. Basi tunakuomba utufundishe yale aliyokufundisha Bwana wetu Mtukufu. Ustadhi akawakumbusha hotuba yake iliyotajwa muda mfupi uliopita. Wakamsikiliza kwa khushui, na wakayakubali maneno yake kwa ridhaa yote na utulivu. Basi wakavuna kiasi kilioje cha ngawira. Kwani walitenda yale yanayomridhisha mfalme wao. Basi mfalme akawaridhia kwa yale waliyoyaonesha katika kuridhia na kufurahia amri zake. Akawaita katika kasri kubwa zaidi na la juu zaidi lisilokaribia kusifika. Akawakirimu kwa furaha ya kudumu kwa yale yanayostahiki kwa Mfalme Aljawad Alakariim (Mwema na Mkarimu), na kwa yale yanayowiana na wageni hawa wakarimu wenye adabu. Ni jambo linalofaa kwa watiifu hawa wenye kufuata amri. Ama Kundi Lingine: Hawa ni wale ambao akili zao zimeharibika, na mwamga wa nyoyo zao umezimika. Basi haikupita punde, wao kuingia tu katika kasri hilo, matamanio yao yakawaghilibu. Basi hawakuwa wakigeuka-geuka isipokuwa kwa yale ambayo nafsi zao zinayatamani miongoni mwa vyakula vitamu. Wakigeuza macho yao kuepuka mazuri yote hayo. Wakiziba masikio yao dhidi ya maelekezo yote yatokayo kwa huyo mwalimu mkuu na maelekezo ya wanafunzi wake... Wakaelekea kwenye vyakula kwa pupa na kufakamia, kama wanyama. Wakafunikwa na mghafala na usingizi. Wakafunikwa na ulevi mpaka wakazipoteza nafsi zao kwa wingi wa walivyopitiliza katika kunywa kwa namna wasivyoidhinishwa. Wakawasumbua wageni wengine kwa wazimu wao na fujo zao. Wakazikosea adabu kanuni za mfalme mwadhama na mifumo yake. Kwa ajili hii, askari wake waliwachukua na kuwapeleka jela la kutisha ili wapate adhabu yao ya haki, kuwa ndio malipo mwafaka kwa waliyoyafanya kutokana na tabia mbaya. Basi ewe unaye sikiliza pamoja nami hikaya hii, hapana budi kwamba wewe umefahamu kuwa mfalme yule amejenga kasri hili kubwa kwa ajili ya makusudio hayo yaliyotajwa. Basi ili kuyafikia makusudio hayo, kunasimamia juu ya mambo mawili. Moja Wapo: Awepo mwalimu huyo ambaye ni ustadhi tuliyemshuhudia na kusikia hotuba yake. Ambapo bila ya huyo (mwalimu), yangeondoka makusudio hayo kwa kupeperuka kama vumbi. Kama kitabu chenye fumbo ambacho maana yake haifahamiki, wala haibainishwi na ustadhi yoyote. Basi yanabaki kuwa ni makaratasi tu yasiyokuwa na maana! Ya Pili: Watu kusikiliza kwa makini maneno ya mwalimu huyo, na kuyakubali. Kwa maana kwamba kuwepo kwa ustadhi ni kielelezo cha kuwepo kwa kasri. Na watu kumsikiliza ni sababu ya kubakia kwa kasri hilo. Kwa hiyo, inafaa kusema: Mfalme mkuu hakuwa ni mwenye kulijenga kasri hili bila ya ustadhi huyu. Na vilevile inafaa kusema: Wakati ambapo watu wanakuwa hawamsikilizi wala hawazingatii maneno yake, basi mfalme ataligeuza kasri hili na kulibadilisha. Mpaka hapa kisa kimeisha ewe rafiki yangu. Ikiwa umefahamu siri ya hekaya hii, basi tazama ndani yake kwenye sura ya uhakika: Kwa hakika kasri hilo ni huu ulimwengu, uliowekewa dari kwa mbingu hii yenye kumemetuka kwa nyota hizi zenye kutabasamu, na uliotandikwa kwa Ardhi hii iliyopambwa kutoka mashariki hadi magharibi kwa maua yenye kuja upya kila siku. Na huyo mfalme mtukufu ni Allah (s.w.), mfalme wa azali na milele, Al-Maalikul Qudduus Dhul-Jalaali wal-Ikram تُسَبِّحُ لَهُ السَّمَاوَاتُ السَّبْعُ وَالأَرْضُ وَمَن فِيهِنَّ ambapo كُلٌّ قَدْ عَلِمَ صَلَاتَهُ وَتَسْبِيحَهُ Na Yeye ni Mweza الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَى عَلَى الْعَرْشِ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ يَطْلُبُهُ حَثِيثًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ وَالنُّجُومَ مُسَخَّرَاتٍ بِأَمْرِهِ. Ama vituo vya kasri hilo ni limwengu elfu kumi na nane, ambazo kila mmoja kati ya limwengu hizo umepambwa na kupangika kwa yanayowiana na viumbe... Ama matendo ufundi wa ajabu katika kasri hilo ni miujiza ya uweza wa kiungu yenye kudhihiri katika ulimwengu wetu kwa kila mwenye macho na busara... Na unavyoviona katika vyakula vyenye ladha vilivyomo ndani yake ni alama za rehema za kiungu katika matunda mazuri ambayo yanashuhudiwa kwa uwazi kabisa katika misimu yote ya mwaka na hasa wakati wa majira ya joto, na hasa zaidi katika bustani za “Barla”. Jiko la kasri hili ni mgongo wa Ardhi na ndio moyo wake unaowaka moto. Ulichokiona ndani ya hekaya miongoni mwa johari za hazina hizo za siri, kiuhalisia, ni mifano ya kudhihiri kwa majina mazuri matakatifu. Na tulichokiona katika nakshi na alama zake ni hivi viumbe vyenye kuupamba ulimwengu. Navyo ni nakshi zenye kuwekwa kwa vipimo kwa kalamu ya uweza wa kiungu, zenye kujulisha majina ya Mwenye uweza na Mwenye utukufu. Ama huyo mwalimu ustadhi, basi huyo ni Bwana wetu na Bwana wa limwengu mbili, Muhammad (s.a.w.). Wasaidizi wake ni hao manabii watukufu (a.s.). Wanafunzi wake ni mawalii wema na wanazuoni waaminifu. Ama wahudumu wa mfalme mkuu, hao ni ishara ya malaika (a.s.) katika ulimwengu huu. Ama wale wote walioitwa katika makazi ya ugeni Duniani, basi hao ni ishara ya wanadamu na majini na wanaowatumikia wanadamu katika wanyama na wanyama hoa. Ama makundi mawili: La Kwanza: Hao ni watu wa imani ambao wanajifunza katika meza ya Qur’an tukufu yale ambayo yanazifasiri aya za kitabu cha ulimwengu. Na Lingine: Ni watu wa ukafiri na dhulma; viziwi, mabubu na wapotevu ambao wamefuata matamanio yao na shetani. Hawakuutambua uhai isipokuwa kijuu-juu. Basi hao ni kama wanyama. Bali wao ni wenye kupotea njia zaidi. Ama kundi la kwanza ambao ni wema wenye furaha; kwa hakika wamemsikiliza mwalimu mtukufu na ustadhi mtukufu mwenye hakika mbili; kwani yeye ni mja na yeye ni mjumbe. Kwa upande wa uja, anamtambulisha Mola wake na kumsifia kwa sifa zinazomstahikia katika sifa za utukufu. Yeye ni sawa na mwakilishi wa umma wake mbele ya hadhara ya kiungu... Na kwa upande wa ujumbe, anafikisha hukumu za Mola wake Mlezi kwa majini na watu wote kwa Qur’an tukufu. Basi kundi hili lenye furaha, baada ya kumsikiliza huyo Mjumbe mkarimu (s.a.w.) na kizitii amri za Qur’an Al-Hakim, tahamaki wanaona nafsi zao wamekabidhiwa majukumu mazuri yanayotukuka ndani ya makamo mengi ya hadhi ya juu. Hiyo ni swala, faharisi ya aina za ibada. Naam, hakika wameshuhudia kwa uwazi maelezo ya faradhi ya swala na kupanda hadhi katika makamo yake ya juu ambayo dhikiri zake na harakati zake mbalimbali zinayaashiria kwa namna ifuatayo: Kwanza: Kwa wao kushuhudia athari za kiungu zilizoenezwa kwenye ulimwengu, wamejikuta wamo katika makamo ya wenye kuyashuhudia mazuri ya adhama ya kiungu kwa muamala wa kighaibu. Wakatimiza jukumu la takbira na tasbihi kwa kusema; Allah Akbar. Pili: Kwa wao kudhihiri katika makamo ya walinganiaji na waelekezaji katika maajabu ya ufundi wake (s.w.) na athari zake zenye kuangaza ambazo ni ming’ao ya majina yake mazuri, wametekeleza jukumu la kutakasa na kuhimidi kwa kauli yao subhanallah walhamdulillah. Tatu: Katika makamo ya kutambua neema zilizowekezwa katika hazina za rehema ya kiungu na kuzionja kwa milango ya fahamu ya dhahiri na ya ndani, wameanza (kutenda) jukumu la shukurani na himidi. Nne: Katika makamo ya kutambua johari za hazina za majina mazuri na kuyaheshimu kwa haki ya kuyaheshimu kwa vipimo vya zana za kimaanawi zilizowekwa ndani yao, wameanza jukumu la kutakasa na kusifia. Tano: Katika makamo ya kutalii risala za kiungu zilizoandikwa kwa kalamu ya uweza wake (s.w.) kwenye ukurasa wa kudura, wameliingia jukumu la kutafakari na kustaajabu na kuhisi wema. Sita: Katika makamo ya kutakasa kwa kuburudisha jicho katika upole makini katika kuumba vitu, na ulaini wa uzuri katika kutengenezwa vizuri, wameuingia wadhifa wa mahaba na shauku kwenye uzuri wa Muumba mtukufu na Fundi mzuri. Na namna kama hii... Baada ya kutekeleza majukumu haya katika makamo yaliyotangulia na kutenda ibada iliyolazimu kwa utendaji wa kigahibu, mbele ya kushuhudia kwa viumbe, wamepanda hadhi hadi daraja la kutazama muamala wa Mtengenezaji Mwenye hekima zote na wao kushuhudia, na muamala wa matendo yake kwa muamala wa kihadhira. Hayo ni kwamba wao: Wameupokea kwanza utambulisho wa Muumba mtukufu yeye mwenyewe kwa wenye utambuzi kwa miujiza ya ufundi wake... Wamempokea kwa maarifa yaliyojaa kustaajabu na kutahayari wakisema: subhaanak (umetakasika) hatukukutambua haki ya kukutambua ewe maarufu kwa miujiza ya viumbe wako wote. Kisha wakaitikia kwa kujipendezesha kwa Huyo Ar-Rahman kwa matunda ya rehema zake (s.w.) kwa mahaba na shauku kubwa huku wakikariri: اِيَّاكَ نَعْبُدُ وَ اِيَّاكَ نَسْتَع۪ينُ Kisha wakauitikia urehemevu wa huyo mneemeshaji wa uhakika kwa neema zake nzuri na kudhihirisha upole wake kwao kwa shukurani na himidi na kwa wao kusema: Subhaanaka hatukukushukuru haki ya kukushukuru ewe Mwenye kushukuriwa kwa ndimi za hali fasaha zinazozitamka hisani zako zote zilizotawanywa kwenye ulimwengu. Na zinatangaza himidi na sifa njema kwa kutangaza neema zako zilizoandaliwa katika soko la ulimwengu na zenye kutawanywa juu ya Ardhi yote. Basi matunda yote yaliyowekwa juu ya meza ya chakula ya rehema zako kunjufu, na vyakula vyote vilivyopimwa, na neema zako enevu, vinatimiza shukurani zake kwa kuushuhudia wema wako na ukarimu wako mbele ya macho ya viumbe. Kisha kule kudhihirisha kiburi cha uzuri wake, utukufu wake na ukamilifu wake (s.w.) katika vioo vya vilivyopo vyenye kubadilika juu ya uso wa ulimwengu, wakakukabili kwa wao kusema: Allahu Akbar na wakarukuu kwa sababu ya kutojiweza kulikovikwa taji la taadhima na wakaporomoka kusujudu katika mahaba yaliyojazwa udhalili na kutoweka kwa ajili ya Allah na katika kuzama kwa kustaajabu na kuadhimisha na kutukuza. Kisha wakajibu kumdhihirisha huyo mkwasi wa hali zote (s.w.) kwa utajiri wake ambao haumaliziki, na rehema zake ambazo zimekienea kila kitu, kwa dua yenye kusisitiza na kuomba kwa bidii, kwa kudhihirsha ufukara wao na uhitajia wao wakisema: إِيَّاكَ نَسْتَعِينُ Kisha wakalikabili onesho la Muumba huyo mtukufu kwa ufundi wake maridadi na maajabu yake ya kuvutia na kuyaeneza katika maonesho mbele ya macho ya viumbe, kwa kushangaa na kuthamini kulikokuwa ni kwa lazima, wakisema: Maa shaa Allah, tabaaraka Allah uzuri ulioje wa umbo la hiki... Hali ya kuwa ni wenye kushuhudia na wenye kuukubali uzuri wa (umbo) hilo, wakisema kwa mayowe: Njooni mushuhudie maajabu haya, njooni kwenye kufaulu... Yashuhudieni na kuweni mashahidi juu yake. Kisha wakajibu ilani ya mfalme huyu mtukufu - mfalme wa azali na milele – kwa uungu wa ufalme wake katika ulimwengu wote na kuudhihirisha umoja wake wa pekee kwa uwepo wote kwa wao kusema: Tumesikia na tumetii... Wakasikia, wakafuata na kutiii. Kisha wakaitikia kwa ajili ya kuudhihirisha uungu mtukufu wa Bwana Mlezi wa walimwengu, kwa kuufanyia ikhlasi uja unaotokana na udhaifu wao uliofichikana ndani ya ajizi yao na ufukara wao ulio ndani ya mahitaji yao... Hiyo ni swala. Na namna hii kwa mfano wa nyadhifa hizi anwai za uja, wametekeleza faradhi ya umri wao na jukumu la uhai wao katika msikiti huu mkubwa unaoitwa makazi ya Dunia. Mpaka wakajifanyia sura ya umbo bora kabisa, na wakapanda cheo cha juu kuliko viumbe wote kwa ujumla. Ambapo wamekuwa ni makhalifa waaminifu katika Ardhi, kwa imani na uaminifu alioweka kwao... Baada ya kuisha muda wa mthani na kutoka katika mshike-mshike wa jaribio, Mola wao Mlezi Mkarimu anawaita kwenye furaha ya milele na neema za kudumu kuwa ni tahawabu za imani yao. Anawaruzuku kuingia katika makazi ya amani (Peponi) kuwa ni malipo ya Uislamu wao. Anawakirimu - na kwa hakika amekwishawakirimu – kwa neema ambazo hakuna jicho limeziona, wala sikio kuzisikia na wala kupitikia katika moyo wa mtu. Kwani mwenye kushuhudia na mwenye shauku ya uzuri wa milele na mwenye shauku kubwa (mwenye kupenda mno) ambaye anaakisi kama kioo, hapana budi awe ni mwenye kubaki na kupita hadi milele. Haya ndio matokeo ya wanafunzi wa Qur’an... Ewe Mola tujaalie tuwe miongoni mwao! Ama kundi lingine ni la wale waovu na washari. Mara tu wanapoliingia kasri la ulimwengu huu kwa umri wa kubaleghe, walilikabili kwa kuzikufuru dalili za umoja-pekee zote, na kwa kuzikufuru neema zinazoneemeshwa juu yao. Wakavituhumu vilivyopo vyote kuwa ni ovyo (kuwa havina maana). Wakavidharau kuwa ni upuuzi. Wakakataa midhihiriko ya majina ya kiungu juu ya vilivyopo vyote. Wakatenda kosa kubwa katika muda mfupi. Jambo ambalo limepelekea wastahiki adhabu ya milele. Naam, hakika mwanadamu hakutunukiwa rasilimali ya umri, na havikuwekwa kwake nyenzo za kibinadamu za hadhi ya juu isipokuwa vimpe sifa ya kutekeleza majukumu matukufu yaliyotajwa. Basi ewe nafsi yangu yenye kutahayari, na ewe rafiki yangu uliyepumbazwa na matamanio ya nafsi! Hivi mnadhani kwamba “Jukumu la uhai wenu” limefungika tu (linaishia) katika kuitikia matakwa ya nafsi yenye kuamrisha uovu na kuichunga kwa nyenzo za kiustaarabu ili kuyashibisha matamanio ya tumbo na utupu? Au mnadhani kwamba shabaha ya kuingiza alivyoweka kwenu katika vipawa vya kimaanawi ni nyepesi, na zana na viungo vyenye kuhisi, na viungo na zana za kupendeza, na hisia na milango ya fahamu yenye kufanya uchunguzi; kwamba hivyo ni kwa ajili ya kuvitumia tu kwa lengo la kuyashibisha mahitaji duni ya raghba za nafsi duni katika uhai huu wenye kutoweka? Hasha wakalla!! Bali kwa hakika kuumbwa kwa vipawa hivyo na milango ya fahamu na hisia katika uwepo wenu na kuviingiza katika umbile lenu, kwa hakika kunaegemea katika misingi miwili: Kwanza: Kukujaalieni mpate hisia ya kushukuru kwa kila aina miongoni mwa aina za neema ambazo amekupeni Mneemeshaji (s.w.). Yaani ni juu yenu kuzihisi na kumshukuru (s.w.) na kumwabudu. Pili: Kukujaalieni nyinyi mtambue vigawanyo vya midhihiriko ya majina mazuri ambayo yanauenea uwepo wote kwa kuvitambua na kuhisi maonjo yake kimojakimoja. Yaani, ni juu yenu kuyaamini majina hayo na kuyatambua kwa utambuzi safi wa kimaonjo. Kwa misingi hii miwili, makamilifu ya kibinadamu hupevuka, na kwa misingi miwili hiyo mwanadamu anakuwa mwanadamu kweli. Basi sasa tazama kupitia mfano huu ili ujue kwamba mwanadamu, kinyume na mnyama, hakupewa zana (viungo) ili kuvuna maisha haya ya Dunia tu: Bwana alimpa mtumishi wake Lira ishirini ili ajinunulie koti kutokana na kitambaa maalumu. Mtumishi alikwenda na kulinunua kutokana na vitambaa bora zaidi na akalivaa. Kisha Bwana yule akampa mtumishi mwingini Lira elfu moja lakini akaweka mfukoni mwake karatasi ya maelekezo na kumtuma kwa ajili ya biashara. Basi kila mwenye gao la akili anatambua kwa yakini kwamba kiasi hiki sio kwa ajili ya kununua koti. Kwani mtumishi wa kwanza alishalinunua kwa Lira ishirini! Lau kama huyu wa pili asingesoma alichoandikiwa kwenye karatasi ile, na akatoa kila alichonacho kumpa mwenye duka na kununua suti - kwa kumuiga yule rafiki yake mwingine – na katika makoti mabaya zaidi, je hatakuwa ametenda wazimu wa mwisho, inapasa kumuadabisha kwa nguvu na kumwadhibu adhabu kali? Basi ewe rafiki yangu kipenzi, na ewe nafsi yangu yenye kuamrisha uovu! Kusanyeni akili zenu wala msiiangushe rasilimali ya umri wenu. Wala msiteketeze nguvu za uhai wenu na matayarisho yake kwa ajili ya Dunia hii yenye kutoweka na yenye kuondoka, na katika njia ya ladha ya kimaada na burudani ya kinyama... Basi mwisho ni mbaya, kwani mtarejeshwa katika daraja la chini kuliko mnyama dhalili zaidi. Kwa kujua kwamba rasilimali yenu ni ya thamani zaidi kuliko mnyama wa hadhi ya juu kabisa! Basi ewe nafsi yangu iliyoghafilika! Ikiwa unataka kufahamu kitu katika: Shabaha ya uhai wako, uhalisia wa uhai wako, sura ya uhai wako, siri ya uhakika wa uhai wako, ukamilifu wa furaha ya uhai wako... Basi tazama jumla ya “shabaha za uhai wako”. Kwani, kwa hakika ni mambo tisa: La Kwanza: Kutekeleza shukurani jumla na kuzipima neema zenye kulimbikizwa katika hazina za rehema ya kiungu kwa vipimo vya milango ya fahamu iliyowekwa kwenye mwili wako. La pili: Kufungua hazina zilizofichikana za majina mazuri ya kiungu, kwa funguo za zana zilizowekwa katika umbile lako, na kumtambua Allah (s.w.) kwa hayo majina mazuri. La Tatu: Kutangaza vilivyopandikizwa kwako na majina mazuri katika vipawa vya midhihiriko na maajbu ya kutengenezwa kwake, na kudhihirisha hivyo vipawa vya kupendeza mbele ya macho ya viumbe kwa ujuzi na hisia, na kwa pande zote za uhai wako katika maonesho ya Dunia hii. La Nne: Kudhihirisha uja wako mbele ya adhama ya uungu wa Muumba wako, kwa ulimi wa hali na maneno. La Tano: Kujipamba kwa sifa pambanuzi za vipawa vya kiubinadamu ambavyo umetunukiwa na midhihiriko ya majina hayo, na kuidhihirisha mbele ya mtazamo wa Shuhuda wa azali (s.w.)... Mfano wako wewe katika hili ni kama mfano wa askari ambaye anavaa beji mbalimbali ambazo mfalme amezitunuku katika minasaba rasmi, na anazionesha mbele ya macho yake ili adhihirishe athari za takrima yake kwake na matunzo yake kwake. La Sita: Kushuhudia mandhari ya uhai kwa wenye uhai; kushuhudia kwa kujua na kuona. Kwani hayo ni maamkizi yake na dalili zake kwa uhai wake kwa Muumba wake (s.w.)... Na kuona kwa tasbihi zake kwa Muumba wake; kuona kwa kutafakari na mazingatio. Kwani hizo ni alama za uhai wake... na kuonesha ibada zake kwa mwenye kutunuku uhai (s.w.) na kuushuhudia. Kwani hilo ndio shabaha ya uhai wake na matokeo yake. La Saba: Kutambua sifa za hali zote za Muumba mtukufu, na mambo yake yenye hekima, na kuzipima kwa alivyovitunuku kwenye uhai wako vikiwemo kiasi kidogo cha elimu, kiasi kidogo cha uwezo na utashi wa kiasi kidogo. Yaani kwa kuvijaalia kuwa ni vielelezo vilivyodogeshwa na kifaa cha kupimia ili kutambua sifa hizo za hali zote zilizo tukufu. Basi Mathalani: Kama wewe ulivyojenga nyumba hii kwa nidhamu kamili, kwa uwezo wako wa sehemu ndogo na utashi wako wa sehemu ndogo na ujuzi wako wa sehemu ndogo, basi kadhalika ni juu yako kufahamu – kwa mnasaba wa ukubwa wa kujenga kasri la ulimwengu na mpangilio wake uliofanywa vyema – kwamba mjenzi wake ni mweza, mjuzi, mwenye hekima zote, na mwenye kupangilia kwa makini. La Nane Yake: Kufahamu kauli zenye kutokana na kila kilichokuwepo katika ulimwengu na kutambua maneno yake ya kimaanawi – kila moja kulingana na lugha yake mahsusi – katika yale yanayohusu umoja-pekee wa muumba wake na uungu wa mwanzilishi wake. La Tisa: Kudiriki daraja za uweza wa kiungu na utajiri wa kiungu wa Bwana Mlezi katika hali zote, kwa vipimo vya ajizi, udhaifu na ufukara na haja iliyomo ndani ya nafsi yako. Kwani ni kama unavyodiriki aina za vyakula, daraja zake na utamu wake; kwa daraja za njaa na kiasi unachokihitajia. Vivyohivyo ni juu yako kufahamu daraja za uweza wa kiungu na utajiri wake wa hali zote kwa ajizi yako na ufukara wako visivyokuwa na ukomo. Basi mambo haya tisa na mfano wake ni jumla ya “shabaha za uhai wako”. Ama “uhalisia wa uhai wako wa dhati” basi jumla yake ni: Faharisi ya mageni ambayo yanahusu majina mazuri ya kiungu... na kipimo kilichodogeshwa ili kujua mambo ya kiungu na sifa zake tukufu... Na vipimo vya limwengu ambazo zimo kwenye ulimwengu... Na orodha ya hukumu za ulimwengu huu mkubwa... Na ramani ya ulimwengu huu mpana... Na muhtasari wa kitabu kikubwa cha ulimwengu... Na mkusanyiko wa funguo zinazofungua hazina zilizojificha za uweza wa kiungu... Na umbo bora kabisa la makamilifu yaliyotawanywa katika vilivyopo na kuenezwa katika nyakati na zama... Basi haya na mifano ya haya ni “uhalisia wa uhai wako”. Na sasa ikufikie “Sura ya Uhai Wako” na mtindo wa jukumu lake. Nayo ni kwamba: Uhai wako ni neno lenye hekima lililoandikwa kwa kalamu ya uweza wa kiungu... Nao ni makala fasaha yenye kujulisha majina mazuri yenye kushuhudiwa na yenye kusikiwa... Basi haya na mifano ya haya ndiyo sura ya uhai wako. Ama “Hakika ya Uhai Wako”, na siri yake ni kwamba: Ni kioo cha kudhihiri kwa upekee, na mwanga wa Swamadiya (mwenye kukusudiwa kwa kila haja). Yaani uhai wako ni kama kioo kinachoakisi juu yake udhihiri wa dhati ya Mmoja-Pekee Alswamad (Mwenye kukusudiwa kwa kila haja) kwa udhihiri wa ujumla. Kana kwamba uhai wako ni nukta kuu ya kukusanya aina za midhihiriko ya majina ya kiungu yenye kudhihiri juu ya ulimwengu wote. Ama “Ukamilifu wa Furaha ya Uhai Wako” ni: Kuyahisi yanayodhihiri miongoni mwa nuru za ming’ao ya kiungu katika kioo cha uhai wako na kuipenda. Kuonesha shauku kwake, na wewe ukiwa ni mwenye kumiliki utambuzi huo. Kisha kutoweka katika mahaba yake, na kuzikita nuru hizo zenye kuakisi na kuziweka katika mboni ya jicho la moyo wako. Kwa ajili hii, imesemwa kwa Kiajemi maana hii ya Hadithi Qudsy ya Mtume ambaye amekutukuza juu ya walio juu: مَنْ نَه گُنْجَمْ دَرْ سَمٰوَاتُ وزَمِينْ ❀ اَزْ عَجَبْ گُنْجَمْ بَقَلْبِ مُوٴْمِنِينْ Basi ewe nafsi yangu! Hakika uhai wako ambao unaelekea kwenye mfano wa shabaha hizi za kupigiwa mfano, ambazo zinakusanya mfano wa hazina hizi za thamani... Je, inafaa kiakili na kwa insafu kutumika katika majaaliwa ya ovyo, kwa ajili ya kuitikia raghba za nafsi yenye kuamrisha, na kwa ajili ya kustarehe kwa ladha tamutamu za Dunia yenye kumalizika, yaporomoke na kupotezwa baada ya hayo?! Basi ikiwa unataka yasipotee burebure, basi fikiria na uzingatie kiapo na jibu la kiapo hicho katika Surat “As-Shams”. Kisha tenda amali ukikumbuka hekaya iliyotolewa mfano iliyotajwa katika utangulizi, ambayo inaweka alama kwenye Sura hiyo. وَالشَّمْسِ وَضُحٰيهَا ❀ وَالْقَمَرِ اِذَا تَلٰيهَا ❀ وَالنَّهَارِ اِذَا جَلّٰيهَا ❀ وَالَّيْلِ اِذَا يَغْشٰيهَا ❀ وَالسَّمَٓاءِ وَمَا بَنٰيهَا ❀ وَالْاَرْضِ وَمَا طَحٰيهَا ❀ وَنَفْسٍ وَمَا سَوّٰيهَا ❀ فَاَلْهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقْوٰيهَا ❀ قَدْ اَفْلَحَ مَنْ زَكّٰيهَا ❀ وَقَدْخَابَ مَنْ دَسّٰيهَا اَللّٰهُمَّ صَلِّ وَسَلِّمْ عَلٰى شَمْسِ سَمَاءِ الرِّسَالَةِ وَقَمَرِ بُرْجِ النُّبُوَّةِ وَعَلٰى آلِهِ وَاَصْحَابِهِ نُجُومِ الْهِدَايَةِ وَارْحَمْنَا وَارْحَمِ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ آمِينْ آمِينْ آمِينْ

Private reading note

This note stays on this device and is never uploaded to a server.

Up to 1,200 characters