بِسْمِ اللّٰهِ الرَّحْمٰنِ الرَّح۪يمِ وَيَض۟رِبُ اللّٰهُ ال۟اَم۟ثَالَ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُم۟ يَتَذَكَّرُونَ وَ تِل۟كَ ال۟اَم۟ثَالُ نَض۟رِبُهَا لِلنَّاسِ لَعَلَّهُم۟ يَتَفَكَّرُونَ Watu wawili walioga kwenye hozi kubwa wakafunikwa na hali wasiyo na uwezo nayo wakapoteza fahamu zao. Na punde walipotahamaki kuzinduka wakaona kwamba wameletwa katika ulimwengu wa ajabu usiokuwa ulimwengu wao, na kila kitu humo ni cha ajabu, basi kwa kuzidia kwa mpangilio wake madhubuti kana kwamba ni ufalme ulioratibiwa sehemu zake, na kutokana na kupendeza mno kwa uzuri wake ni sawa na mji wenye kuamirishwa, (Wenye makazi) na kwa kutokana na kuratibika mno kwa nguzo zake, ni sawa na kasri la ajabu. Na wakaanza kuwa wanatazama kwa shauku pembezoni mwao na hali wakiwa wamejawa na kutahayari na kupendezwa kwa waliyoyaona mbele yao katika ulimwengu mkubwa kwa hakika, ambapo ungeangaliwa upande wake ungeshuhudiwa ufalme uliopangika, na ingetazamwa kwa upande mwingine ungeonekana mji uliokamilika pande zake, wakati ambapo ungetazamwa kwa upande mwingine tahamaki ni kasri kubwa linajumuisha ulimwengu mkubwa. Wakaanza kutembea pamoja katika maeneo ya ulimwengu huu wa ajabu, macho yao yakatua kwa viumbe wanaoongea maneno maalum wasiyoyatambua, isipokuwa walielewa kutokana na ishara zao kwamba wanatekeleza kazi kubwa na wanatimiza wajibu muhimu. Mmoja wao alimwambia mwenzake: Hapana shaka kwamba huu ulimwengu wa ajabu kuna mwendeshaji anayeendesha mambo yake, na ufalme huu wa ajabu una mwenyewe anayeutunza, na huu mji wenye kupendeza una Bwana anayetawalia mambo yake, na hili kasri refu lina Mtengenezaji wa ajabu ambaye aliyetengeneza (bila ya ruwaza), basi naona ni jambo la lazima kwetu tujitahidi kumjua, kwani inaonekana kuwa yeye ndiye ambaye ametuleta hapa, na si mwingine yeyote yule. Na kama hatukumjua basi ni nani mwingine atakayetuhudumia na kutusaidia na kukidhi haja zetu hali ya kuwa tupo katika ulimwengu huu mgeni? Na je unaona chembe ya matarajio tunayoyatarajia kutoka kwa hawa wasiojiweza wadhaifu na hali ya kuwa sisi hatutambui lugha yao na wala wao hawasikilizi maneno yetu? Kisha yule ambaye ameujaalia huu ulimwengu mkubwa katika sura ya ufalme ulioratibika na katika umbo la mji wa kupendeza na katika namna ya kasri la ajabu, na kujaalia ni hazina ya mambo yenye kufurutu ada, na akautia uzuri kwa mapambo mazuri mno na uzuri wa kupendeza mno, na akapangilia pande zake zote kwa miujiza yenye kuleta mazingatio yenye hekima, nasema: Hakika Fundi ambaye ana adhama yote hii na haiba na ametuleta hapa – na wanaotuzunguka – hapana shaka kwamba ana jambo katika hili. Basi imepasa kabla ya kila kitu kwanza tumjue ujuzi kamili na tujifunze kutoka kwake anachokitaka kutoka kwetu? Swahiba yake alimwambia: Achana na maneno haya. Kwani mimi si sadiki kwamba mmoja pekee anaendesha ulimwengu huu wa ajabu! Akamjibu kwa kumwomba: Akamwambia ewe swahiba yangu! Je ungeniazima sikio lako! Basi sisi tukipuuzia kumjua yeye katu hatutavuna chochote, na ikiwa katika kupuuzia kwetu kuna madhara basi madhara yake ni ya hakika na makubwa mno. Wakatia ambapo tukijitahidi kumjua basi katika jitihada yetu hii hakuna mashaka na badala yake hatutapata hasara, bali manufaa makubwa. Basi haitufalii sisi kuendelea kubakia hivi tukipuuzia kumjua. Lakini swahiba yake mwenye kughafilika amesema: Mimi siko pamoja nawe katika maneno yako haya. Hakika mimi napata raha yangu na furaha yangu katika kutokutumia fikira katika mambo kama haya, na kutokumjua unayedai kuwa ni mtengenezaji wa ajabu. Sioni haja kutaabisha nafsi yangu katika ambayo akili yangu haiyakubali. Bali ninaona matendo haya yote si lolote isipokuwa ni sadfa na mambo yenye kuingiliana yenye kupishana kwa pamoja yanakwenda na kufanya kazi yenyewe, ninahusika nini mimi na mambo haya? Mwenye akili akamjibu: Nahofia ukaidi wako huu usije ukatutupa sisi na wengine katika masaibu na mabalaa. Je haikuvunjwa miji iliyostawi kutokana na usafihi mwovu na matendo ya muasi? Na kwa mara nyingine yule mwenye kughafilika alifanya kiburi kwa kusema: Na tuyamalize maudhui haya kabisa basi ima unithibitishie kwa dalili ya kukinaisha haikubali shaka kwamba ufalme huu mkubwa una mmiliki Mmoja na Mtengenezaji Mmoja au uniache nilivyo. Rafiki yake akamjibu: Maadamu ewe swahiba yangu unang’ang’ania ukaidi wako kwa kiwango cha wazimu na kuweweseka, mambo ambayo yanatupelekea sisi na ufalme wote kwenda katika kuteketea basi nitaweka mbele yako hoja kumi na mbili kwazo nitathibitisha kwamba ulimwengu huu wenye kupendeza una uzuri wa kasri, na ufalme huu uliopangika kama mji una Mtengenezaji Mmoja wa pekee ndiye ambaye anadabiri mambo yote. Huoni mwanya hata kidogo, wala huoni upungufu katika jambo lolote, basi huyo Mtengenezaji ambaye hatumuoni yeye anatuona na anaona kila kitu, na anasikia maneno ya kila kitu, basi matendo yake yote ni miujiza na ishara na mambo yenye kufurutu ada na mambo ya kupendeza mno. Na viumbe hivi ambavyo hatuzifahamu lugha zao sio lolote isipokuwa ni wenye kuamuriwa na wafanya kazi katika ufalme wake.
Source text is preserved. When a suitable model is available, translation is displayed separately.
Sözler
The Twenty-Second Word
Njoo pamoja nami ewe swahiba yangu tuchunguze vitu na mambo yanayotuzunguka. Je huoni kwamba mkono uliyojificha unatenda nyuma ya mambo yote? Na je huoni kisicho na nguvu asilani wala hakiwezi kujibeba nafsi yake chenyewe kinabeba maelfu ya ratili katika mizigo mizito? Na ushahidi kwamba kisicho na utambuzi na wala hisia kinatenda kazi katika upeo wa hekima? kwa hiyo vitu hivi havitendi kwa kujitegemea vyenyewe, bali hapana budi kwamba vina Bwana Mjuzi, na Mtengenezaji aliye Mweza anaviendesha nyuma ya pazia (Mbali mbali). Kwani ingekuwa ni vyenye kujitegemea vyenyewe na mambo yake yangekuwa mikononi mwake vyenyewe, ingelazimu kila kitu kati ya hivyo hapa ni mmiliki wa muujiza wenye kufurutu ada. Na hii sio isipokuwa ni safsata (mantiki ya upotoshaji) isiyo na maana.
Ewe swahiba yangu njoo pamoja nami, ili tuangalie kwa makini vitu hivi ambavyo vinapamba viwanja mbalimbali, basi katika kila pambo kati ya hayo kuna mambo yanayotupa habari juu ya huyo mmiliki na kutujulisha. Kana kwamba ni muhuri wake. Na vinatujulisha muhuri wake kama nembo ya mfalme na muhuri wake juu ya uwepo wake, na muhuri wake ambao umo kwenye vitu vilivyowekwa muhuri wake unatujulisha kuhusu adhama yake na haiba yake, ukitaka basi tazama huu mwili mdogo mno ambao mwanadamu kamwe hafikii kuutambua kuwa na uzito wowote, na Mola ametengeneza kutokana na marefu kutokana na ufumaji wenye rangi za kuvutia na wenye kurembwa kwa mapambo ya kung’ara na anatoa kutokana nao aina za halawa na mikate yenye kutiwa asali na vyenye ladha mno, basi kama maelfu kati yetu wangevaa kutoka katika hivyo vyenye kufumwa na kula vyakula hivyo visingekwisha. Kisha tazama, kwamba hakika anachukua kwa mkono wake wa kighaibu hiki chuma, mchanga, maji, mkaa, shaba, fedha na dhahabu na kutokana na hivyo vyote anatengeneza kipande cha nyama . Basi ewe mwenye kughafilika, vitu hivi na matendo haya hakika vinamuhusu tu ambaye hatamu ya ufalme huu imo mikononi mwake, na ambaye hakimponyoki chochote na kila kitu ni kitiifu kwa matakwa yake.
Njoo tutazame alivyovitengeneza vya ajabu vyenye kuchakatika . Vyote hivyo vimetengenezwa kana kwamba ni nakala iliyofanywa kuwa ndogo kutokana na hili kasri kubwa, kwani vimo ndani yake vilivyomo ndani ya kasri yote. Je inayumkinika kwa yeyote kuiweka kasri hii ikiwa imefanywa ndogo na kuwekwa katika mashine madhubuti asiyekuwa mtengenezaji wake wa ajabu? Na je inayumkinika kuona mchezo au sadfa katika ulimwengu uliokusanywa ndani ya mashine ndogo? Yaani kila unachokishuhudia miongoni mwa mashine hakika ni sawa na aya inayomjulisha huyo Fundi wa ajabu, bali kila mashine ni dalili juu yake, na ni tangazo linaloweka wazi adhama yake, na inasema kwa ulimi wa hali: Hakika sisi ni katika ubunifu wa aliyebuni ulimwengu huu kwa wepesi wa hali zote na kama alivyotupatisha kwa wepesi wa hali zote.
Ewe ndugu mkaidi! Njoo nikuoneshe kitu chenye kuamsha zaidi mshangao! Tazama, haya hapa mambo katika ufalme huu, yamebadilika na vitu vyote vimegeuka, haya basi ni sisi ambao tunaona kwa macho yetu huku kubadilika, basi hakuna uthabiti kwa kitu katika tunavyoviona bali vyote vinabadilika na kuwa vipya. Basi tazama viwiliwili hivi visivyo na uhai vyenye kushuhudiwa ambavyo hatuoni ndani yake utambuzi, kana kwamba kila kimoja kati ya hivyo kimechukua sura ya mtawala wa hali zote na wengine ni watawaliwa chini ya mamlaka yake, na kana kwamba vyote kati ya hivyo kina tamalaki juu ya vitu vyote, tazama hii mashine ambayo iko karibu nasi kana kwamba inaamrishwa basi inaharakisha kuiendea kutokea mbali na vile ambavyo inavihitaji katika vya lazima kwa mapambo yake na kazi zake, na utazame ule mwili ambao hauna utambuzi kana kwamba unatiishwa kwa ishara iliyojificha kutoka katika mwili mkubwa zaidi katika mambo yake maalum na kuufanya wenye kutii ishara yake, na pima mambo mengine kwa mifano hii miwili. Kama halikuachiliwa jambo la uendeshaji wa ufalme kwa huyo mfalme ambaye hatumwoni, basi juu yako kuelekeza kwa kila chenye kutengenezwa kwa yale yaliyomo kwa Mtengenezaji wa ajabu na makamilifu, hata kama ingekuwa ni jiwe au mchanga au mnyama au mtu au kiumbe katika viumbe. Basi akili yako ikikataa kuwa Mtengenezaji wa ajabu mmoja wa pekee ndiye Mmiliki wa ufalme huu ndiye ambaye anayaendesha, basi sio juu yako isipokuwa kukubali mamilioni ya mamilioni ya watengenezaji, bali kwa idadi ya vilivyomo! Na kila mmoja kati yao ni sawa na mwingine na mfano wake badala yake na mwenye kuingilia katika mambo yake! pamoja na kuwa hakika ya mpangilio uliowekwa vyema wa ajabu unahitajia kutokuingiliwa, ikiwa kuna kuingilia japo ikiwa ni kidogo na kutokana na kitu chochote kiwacho, na katika kila jambo miongoni mwa mambo ya ufalme huu mkubwa, athari yake ingedhihiri wazi wazi, kwani mambo yangechanganyika na kupishana ikiwa kuna mabwana wawili katika kijiji au wakuu wawili katika mji au mfalme katika ufalme. Basi hali ni vipi itakuwa kwa watawala wasio na idadi wala kuhesabika katika ufalme ulioratibika kwa namna ya ajabu?!
Ewe rafiki mwenye shaka, njoo tuchunguze kwa makini nakshi za kasri hili kubwa, na tuangalie vema katika mapambo ya miji huu, na tushuhudie nidhamu ya ajabu ya ufalme huu mpana, na tuchunguze ufundi mzuri wa huu ulimwengu. Basi ni hii tuonavyo kwamba isingekuwa nakshi hizi ni uandishi wa kalamu ya Mmiliki Fundi wa ajabu ambaye hana mpaka kwa miujiza na maajabu yake, na kuegemeza uandishi na nakshi zake kwa sababu ambazo hazina utambuzi, na kwenye sadfa pofu, na kwa Asili ziwi, kwa hiyo ingelazimu iwe katika kila jiwe kati ya mawe ya ufalme huu na nyasi zake mpiga picha wa kimuujiza na mwandishi wa ajabu anaweza kuandika maelfu ya vitabu ndani ya herufi moja, na anaweza kuingiza mamilioni ya kazi zilizofanywa vyema za ajabu katika nakshi moja, hakika unaona kwamba hakika ya nakshi hii ambayo iko mbele yako katika tofali hili inajumuisha nakshi za kasri lote, na inakusanya kanuni zote za mji na mifumo yake, na zinabeba mipango ya kazi zake. Yaani hakika kupatisha nakshi hizi za kupendeza miujiza mikubwa kama kupatisha ufalme wenyewe, basi kila ufundi wa ajabu sio kingine isipokuwa ni ubao wa matangazo unaoweka wazi miongoni mwa sifa za huyo fundi mtengenezaji wa ajabu, na kila nakshi nzuri basi ni muhuri wa wazi katika mihuri yake inayomjulisha yeye. Kama ilivyo kuwa haiyumkiniki kwa herufi isipokuwa inajulisha juu ya mwandishi wake, na haiyumkiniki nakshi yoyote isipokuwa ibainishe mrembeshaji wake, hivyo basi inayumkinika vipi herufi ambayo imeandikwa ndani yake kitabu kikubwa isijulishe juu ya mwandishi wake, na nakshi imenakishiwa maelfu ya nakshi isimjulishe mtia nakshi wake? Kujulisha kwake hakuwi dhahiri na wazi zaidi kuliko kujijulisha mwenyewe?
Rafiki yangu njoo twende kwenye matembezi katika uwanda huu mpana uliotandazwa mbele yetu, na hili hapo jabali gumu, njoo tupande juu yake tupate kushuhudia pande zote kwa urahisi, na tubebe darubini zenye kukuza zinazotukaribishia vilivyo mbali na macho yetu. Basi ufalme huu ndani yake kuna mambo ya ajabu na matukio mageni yasiyopita katika akili ya yeyote. Tazama milima ile na tambarare iliyokunjuka na miji iliyostawi, hakika hilo ni jambo la ajabu kweli hakika yote yanabadilika kwa mkupuo mmoja, bali hakika mamilioni ya mamilioni ya vitendo vyenye kupishana vinabadilika mbadiliko kwa mpangilio na kwa kila uratibu, basi kama vile mamilioni ya urefu katika vilivyofumwa vyenye rangi mbali mbali yenye kupendeza hakika vinafumwa mbele yetu wakati mmoja. Kwa hakika mabadiliko haya ni ya ajabu mno. Basi yako wapi yale maua ambayo yalitabasamu kwa ajili yetu na ambayo tumeliwazika kwayo?. Yamekuwa mbali nasi, na mahala pake zimekaa sampuli tofauti nayo yenye sura yenye kufanana nayo kwa ainisho. Na kana kwamba tambarare hizi zilizokunjuka na milima hii iliyoinuliwa ni kurasa za kitabu katika kila mojawapo kati ya hizo huandikwa vitabu mbali mbali katika upeo wa kutengenezwa vyema bila ya kusahau wala kukosea kisha vitabu hivyo vinafutwa na kuandikwa vingine, Je unaona ewe rafiki yangu kwamba kubadilika kwa hali hizi ambako kunafanyika kwa kila mpangilio na mizania kuwa kunatokea kwa kuzuka wenyewe tu?. Je hilo si muhali katika mihali mikubwa? Haiyumkiniki katu mambo haya ambayo yako mbele yetu nayo yakiwa katika upeo wa kutengenezwa vyema na ufundi kuyahaulisha kwa nafsi yake mwenyewe, basi hilo ni muhali katika muhali. Bali ni dalili za wazi juu ya mtengenezaji wake wa ajabu wazi mno kuliko kujielezea wenyewe, kwani imebainika kwamba mtengenezaji wake wa ajabu hakimshindi kitu, wala hakimuelemei kitu, basi kuandika vitabu elfu moja ni jambo jepesi kwake kama kuandika herufi moja. Kisha zingatia ewe ndugu yangu pande zote utaona hakika mtengenezaji ameweka kwa hekima iliyotimia kila kitu mahali pake panapofaa. Na kila kitu amekikamilishia neema zake na ukarimu wake kwa upole wake na fadhila yake enevu. Na kama anavyofungua milango ya neema zake juu ya viumbe wa ufalme huu wote. Na katika wakati huo huo anatandika meza za kifahari kwa ukarimu na utoaji bali anawaneemesha viumbe wa ufalme huu wote wakiwemo wanyama mimea neema zisizo na mpaka, bali anapeleka kwa kila mmoja kwa jina lake na kuandika kwake na kuhusisha neema zake ambazo zinazomfaa bila ya kosa au kusahau. Je basi kuna muhali mkubwa kuliko wewe kudhania kwamba katika mambo haya kuna kiasi cha sadfa jambo lingekuwa dogo? Au ndani yake kuna kiasi cha mchezo na kutokuwa na faida? Au kwamba mmoja asiyekuwa mtengenezaji wa ajabu ameingilia katika mambo ya ufalme? Au kuweka taswira kutomtii yeye kila kitu katika ufalme wake? Na je unaweza ewe rafiki yangu kupata sababu ya kukataa unayoyaona?..
Na tuachane na vijisehemu ewe swahiba yangu, na tuuchunguze huu ulimwengu wa ajabu, na tushuhudie hali za sehemu zake zenye kukabiliana, basi katika huu ulimwengu wa ajabu katika mpangilio enevu na kupangika kuliko kamilika kana kwamba kila kitu ni chenye kutenda chenye hiari kilicho hai kinasimamia juu ya mfumo wote wa ufalme, na unafanya mchakato kwa kuratibika pamoja na huo mfumo ya jumla. Hata unaona vitu vilivyokuwa mbali kimoja kinakwenda upande wa kingine kwa ajili ya kusaidiana na kutiana nguvu. Tazama! Hakika msafara mkubwa unaotokea katika ghaibu unakuja kwetu. Ni msafara unaobeba sahani za riziki za walio hai, kisha tazama hiyo taa yenye kuangaza iliyoangikwa kwenye kubwa la ufalme inaangazia wote na kuivisha vyakula vilivyoangikwa kwa uzi madhubuti na unahudhurishwa mbele yake kwa mkono usioonekana. Je hugeuki pamoja nami kwa hawa wanyama waliokonda dhaifu wasiojiweza vipi kinatiririka kwenye vinywa vyao chakula murua safi kinabubujika kutoka katika mirija inayoning’inia juu ya vichwa vyao, na inatosha kubandika inatosha vinywa vyao kuviambatanisha na mirija hiyo. Kwa ufupi: Hakika hakuna kitu chochote katika ulimwengu huu isipokuwa ni kana kwamba kinachungulia kitu kingine na kukipa msaada, au inakiona kingine hivyo inakitia nguvu na kukisaidia. Basi kimoja kinakamilisha kazi ya kingine na kinakuwa msaidizi wake na mtegemezi wake, na wote wanaelekea bega kwa bega katika njia ya maisha, na pimia juu ya hivyo basi matukio yote haya yanatujulisha kwa namna ya kukinaisha na kwa yakini ya kukata shauri kabisa hakika hakuna chochote katika kasri hili la ajabu isipokuwa kinatiishwa na Mmiliki wake Mweza wa kila jambo na Mtengenezaji wake wa ajabu na kinatenda kwa jina lake na katika njia yake, bali kila kitu ni sawa na askari mtiifu aliyekuwa tayari kupokea amri. Basi kila kitu kinatekeleza wajibu kilichokalifishwa kuutekeleza kwa nguvu na hila ya Mmiliki wake, basi kinatembea kwa amri yake, na kupangika kwa hekima yake, na kusaidiana kwa fadhila na ukarimu wake, na kwa rehema zake kinawapa wengine msaada. Ukiwa unaweza ewe ndugu yangu kuonesha chochote katika upingaji na shaka mbele ya hoja hii basi kilete.
Ebu ewe swahiba wangu mwenye kujifanya kuwa na akili na ewe mfano wa nafsi yangu yenye kuamrisha maovu ambayo inajihesabu kuwa ni ongofu na kujidhania vyema. Nakuona ewe swahiba wangu unataka kumjua mwenye kasri hili la ajabu, pamoja na kuwa kila kitu kinamjulisha, na kila kitu kinamwashiria, na kila kitu kinashuhudia uwepo wake. Basi vipi unathubutu kukadhibisha shahidi zote hizi?. Hakika ni juu yako kukanusha uwepo wa kasri lenyewe, bali ni juu yako kutangaza kwamba hakuna kasri wala hakuna ufalme na hakuna kitu chochote katika uwepo. Bali na ukanushe nafsi yako na uihesabu kuwa haipo haina uwepo!. Au ni juu yako urudi katika utambuzi wako na unisikilize vyema, haya sasa nakuwekea mbele yako mandhari hii: Zingatia katika chembe hizi na madini ambayo yanaenea ufalme huu na ambazo zipo katika pande zote za kasri hili. Na yajulikana kuwa hakuna kitu chochote kinachozalishwa katika ufalme huu isipokuwa ni kutokana na maada hizo. Basi Mwenye kuwa ni mmiliki wa maada hizo na hizo chembe hivyo basi huyo ndiye Mmiliki wa kila kinachotengenezwa na kuzalishwa humo. Kwani ambaye ni Mmiliki wa shamba, huyo basi ndiye Mmiliki wa mazao, basi na mwenye kuwa ni Mmiliki wa bahari, huyo ndiye Mmiliki wa vilivyomo. Kisha tazama ewe swahiba yangu, hivi vyenye kufumwa na vitambaa vyenye kuwekwa rangi vyenye kupendezeshwa kwa maua. Hakika vinatengenezwa kutokana na maada moja. Basi ambaye ametayarisha maada hizo na kuzifuma hakika huyo ni mmoja, kwa sababu ufundi huo haukubali kushirikiana, basi vilivyofumwa vyema vinamuhusu yeye tu. Kisha geukia hili: Hakika jinsi za hivi vyenye kufumwa zipo katika kila sehemu katika sehemu za huu ulimwengu wa ajabu na vimezagaa kwa maeneo mapana hata ni kuwa vinafumwa kwa pamoja na kuingilia katika wakati mmoja na kwa mtindo mmoja kila mahali. Yaani huo ni utendaji wa mtendaji mmoja, vyote vinashughulika kwa amri moja. Na kama sio hivyo ni muhali kuwepo na uwiano timilifu na kuafikiana kwa wazi katika kutenda kwa wakati mmoja na mtindo mmoja na kwa sampuli moja na umbo moja katika pande zote. Kwa hiyo kila ambacho kimetengenezwa vyema kinajulisha wazi kuwa huyo Mtendaji ambaye hatumwoni, bali kana kwamba kinamtangaza kwa uwazi, bali kana kwamba kila ufumaji uliyotojwa kwa maua, kila mashine ya ajabu, na kila chakula kitamu, hiyo ni alama ya Mtengenezaji Mwenye muujiza na muhuri wake na ishara yake na nembo yake vyote kati ya hivyo vinasema kwa ulimi wa hali: (Ambaye mimi ni mwenye kutengenezwa na yeye, basi mahali ambapo mimi nipo ni ufalme wake). Na kila nakshi inasema: (Hakika aliyetimiza kunifuma na kuniwekea nakshi basi kiasi cha mizunguko ya kitambaa ambayo mimi nimo ndani yake ni ufumaji wake). Na kila tonge lenye ladha linasema: (Hakika anayenitengeneza na kunivisha basi chungu ambacho ninapikiwa ni ufalme wake). Na kila mashine inasema: (Ambaye amenitengeneza basi kila kilichomo ulimwenguni katika mifano yangu ni vilivyotengenezwa na Yeye naye ni Mmiliki wake. Yaani Mwenye kuwa ni Mmiliki wa ufalme na kasri yote basi huyo ndiye ambaye inayumkinika kutumiliki). Na hii ni kwa mfano wa aliyetaka kudai kumiliki vifungo vya sare ya askari na kuweka nembo ya dola juu yake hapana budi kuwa ni Mmiliki wa viwanda vyake vyote hata awe ni Mmiliki wa hakika, na kama si hivyo basi hana isipokuwa kujidai kwa uwongo, bali ataadhibiwa kwa tendo lake na kupatilizwa kwa maneno yake. Muhtasari: Kama chembe za ufalme huu ni maada zilizozagaa katika pande zake basi Mmiliki wake kwa hiyo ni mmoja anamiliki katika ufalme wote, kadhalika vitu mbalimbali vilivyotengenezwa vilivyozagaa katika pande za ufalme kwa kuwa zinashabihiana vinadhihirisha alama moja na kanuni moja, vyote kwa hiyo vinamjulisha huyo Mmoja Mwenye kutamalaki kila kitu. Basi ewe rafiki yangu! Hakika alama ya umoja ni dhahiri katika huu ulimwengu, na ishara ya Tawhidi iko wazi bayana, hiyo kwa sababu sehemu ya vitu licha ya kuwa ni kimoja lakini kipo katika ulimwengu wote, na sehemu nyengine licha ya kuwa na namna nyingi hakika inadhihirisha umoja wa kisampuli pamoja na wenzake kwa kushabihiana kwake na kuzagaa kwake katika pande mbalimbali, ambapo umoja unajulisha juu ya Mmoja kama inavyojulikana, kwa hiyo inalazimu kuwa Mtengenezaji wa vitu hivi na Mmiliki wake ni Mmoja wa pekee. Ongezea juu ya hili hakika unaona inatuletea zawadi za thamani kutoka nyuma ya pazia za ghaibu, basi kuteremsha nyuzi na kamba . zinazobeba vilivyo vya thamani mno kuliko almasi na zamaradi katika neema na hisani. Kwa hiyo basi kadiria mwenyewe ni kiasi gani cha upumbavu wa asiyemjua anayeendesha mambo haya ya ajabu na analeta hizi zawadi za ajabu? Kadiria ubaya wa asiyetimiza shukurani zake juu yake! Kwani kutokumjua kwake kunamlazimisha kutamka ambayo ni sawa na kuweweseka. Kwa – mfano - anasema: Hakika ya hizo lulu zilizopangwa vyema zinajitengeneza zenyewe!. Yaani ujinga wake unamlazimu kuipa maana ya mfalme kila kamba katika kamba hizo! Na hali ya kuwa sisi tunaona kuwa mkono wa ghaibu ndio ambao unanyooka hadi katika kamba hizo na kuzitengeneza na kuzitunuku zawadi. Yaani kila kilichomo katika kasri hii kinajulisha juu ya Mtengenezaji wake wa ajabu kwa namna ya wazi kuliko kinavyojijulisha chenyewe. Basi kama humjui ukweli wa kumjua ewe swahiba wangu kwa hiyo basi utaporomoka katika ngazi ya chini mno kuliko ya wanyama, kwa sababu utalazimika kukanusha vitu vyote hivi.
Ewe rafiki ambaye anatupa maamuzi yake holela, hakika wewe humjui Mmiliki wa kasri hii na wala hutaki kumjua, basi unakana kuwa ina Mmiliki, na unaelekea katika kukanusha hali zake kwa sababu ya kushindwa kwa akili yako kufahamu miujiza hii dhahiri na mazuri ya ajabu, pamoja na kuwa kukanusha kwa hakika, na mishkeli migumu na migumu mno katika mantiki ya akili ni katika kutokumjua Mmiliki na ambayo inakupelekea katika kukanusha maada yaliyotolewa kwako, kwa thamani zake nadira na wingi wake mkubwa. Wakati ambapo tungemjua inakuwa kukubali vilivyomo katika kasri hili, na katika huu ulimwengu ni rahisi na kupokeleka na jambo lenye kuingia akilini sana, kana kwamba ni kitu kimoja, kwani kama tusingemjua na bila ya yeye, wakati huo kila kitu kingekuwa ni kigumu bali hutaona kitu katika ambavyo vipo kwa wingi na kutolewa mbele yako. Ukitaka basi tazama tu katika pakiti za siagi yenye kuning’inia kutokana na nyuzi hizi. Lau isingekuwa ni katika uzalishaji wa jiko hilo la uweza wa muujiza, isingekuwa unaweza kuyapata hayo hata kwa thamani ghali mno. Naam, hakika ya kukanusha na mishkeli na ugumu na kuangamia na muhali hakika hayo ni katika kutokumjua Yeye, kwa sababu kupatisha tunda – kwa mfano - inakuwa ni ngumu na mushkeli kama mti wenyewe ikiwa kila tunda litafungwa katika vituo vingi na kanuni tofauti, wakati ambao jambo linakuwa jepesi na kupokelewa ikiwa kupatisha tunda ni kwa kanuni moja na kutoka katika kituo kimoja basi inakuwa kupatisha maelfu ya matunda kama kupatisha tunda moja. Mfano wake katika hili kama kuandaa jeshi kwa zana, ikiwa kutoka katika chanzo kimoja na kwa kanuni moja na kutoka kwenye kiwanda mahsusi kinacho ihusu, basi jambo ni rahisi na kupokelewa kiakili. Wakati ambapo akiandaliwa kila askari kwa kanuni maalum na akatoka katika chanzo kimoja na kutoka katika kiwanda kinacho ihusu, jambo ni gumu na mushkeli mno, bali huyo askari atahitajia wakati huo viwanda vya zana na vituo vya utayarishaji na kanuni nyingi kwa idadi ya mmoja mmoja ya jeshi kamili. Basi katika mlingano wa mifano hii miwili, hakika kupatisha vitu hivi katika kasri hii kubwa na mji wenye kupendeza, na katika ufalme huu ulioendelea na ulimwengu mkubwa ukiwa umetegemezwa kwa Mmoja wa pekee hakika jambo linakuwa ni jepesi na kupokelewa ambapo inakuwa tunachokiona katika wingi wa vitu ni jambo la wazi, wakati ambao ikiwa haukutegemezwa jambo kwake kupatisha kitu chochote inakuwa ni ngumu mno, bali haiyumkiniki kukipatisha asilani hata kama dunia yote ikitolewa kuwa ni thamani yake.
Ewe rafiki na ewe unajongelea kidogo kidogo katika insafu, basi ni sisi hapa tangu siku kumi na tano , tusingejua mifumo ya nchi hii na kanuni zake tusingemjua Mfalme wake basi adhabu inathibiti juu yetu, kwani hakuna nafasi tena kwetu sisi kutoa udhuru. Hakika wametupa muda masiku yote haya, na hawajatudhuru kwa lolote. Isipokuwa hakika sisi bila ya shaka hatuko huru tusiodhibitiwa, hakika sisi tuko katika ufalme mzuri wa ajabu ndani yake kuna umakini na ulaini na mazingatio katika vyenye kutengenezwa vyema ambao unaashiria adhama ya mfalme wake, hapana budi kuwa sehemu zake zina nguvu pia. Na unaweza kutambua adhama ya mmiliki na uweza wake kutokana na hili: Hakika anapangilia huu ulimwengu mkubwa kwa urahisi upangiliaji sawa na kasri kubwa, na anaendesha mambo ya huu ulimwengu wa ajabu kwa wepesi sawa na kuendesha nyumba ndogo, na anajaza mji huu wenye kustawi kwa mpangilio kamili bila ya kasoro na anauacha mtupu (Kwa kuwaondosha) wakazi wake kwa hekima timilifu kwa mfano wa wepesi wa kujaza sahani na kuipakua. Na anatandika meza za chakula kubwa za aina mbalimbali na anatayarisha vyakula vitamu kwa ukamilifu wa ukarimu wake kwa mkono wa ghaibu na anaitandika kutokea mbali ya ulimwengu hadi mbali yake kisha anaiondosha kirahisi sawa na urahisi wa kuweka meza ya chakula na kuiondosha. Basi ukiwa mwenye busara utafahamu kwamba adhama na haiba hii hapana budi kuwa inabeba ukarimu usio na mpaka na wema usio na mipaka. Kisha tazama kama vilivyo vitu hivi ni shahidi wa ukweli juu ya adhama ya Mmiliki Mweza na juu ya utamalaki wake, na kwamba Yeye ni Mfalme Mmoja wa pekee, kadhalika misafara yenye kubadilishana kwa zamu na mageuzi yenye kufuatana ni dalili juu ya kudumu kwa mfalme huyu na kusalia kwake, Kwa sababu vitu vyenye kutoweka hakika huondoka vilevile sababu zake. Basi vitu na sababu huondoka kwa pamoja, wakati ambapo kinachozifuatia huja kwa upya na kikiwa na athari kama vitangulizi vyake, kwa hiyo hivyo sio kutokana na utendaji wa hizo sababu, bali ni kutoka kwa yule ambaye hazukiwi na kutoweka! Basi kama ilivyo kubakia kwa mng’ao na kumeremeta – baada ya kutoweka kwa mapovu ya mto wenye kutembea – katika linalolifuatia katika mapovu na inatufahamisha kwamba kung’aa huku sio kutokana na mapovu yenye kutoweka bali kutokana na chanzo cha nuru cha kudumu, vilevile kubadilika kwa matendo kwa kasi ya ajabu, na kubeba rangi mbali mbali yale yanayoyafuatia na kuvaa kwake sifa zake kunatujulisha kwamba hakika matendo hayo ni midhihirisho ya Yule ambaye ni wa daima Mwenye kuthibiti hageuki. Na vitu vyote ni nakshi zake na vioo vyake na ufundi wake na si vinginevyo.
Njoo ewe rafiki nikubainishie hoja yenye nguvu ya hoja kumi zilizotangulia. Acha tujiendee na safari ya kibahari, tutapanda jahazi ili twende kwenye kisiwa kilicho mbali na sisi. Je unajua kwa nini tunakwenda huko?. Hakika huko kuna funguo ya mafumbo ya huu ulimwengu na vifungo vya siri na maajabu yake. Je huoni macho ya wote yamekodolea huko, wanangojea tangazo kutoka huko na wanapokea amri kutoka huko. Basi hao sasa tunaanza safari, na hao tumeshafika huko na nyayo zetu zimekanyaga ardhi ya kisiwa. Sisi hivi sasa tupo mbele ya mkusanyiko mkubwa wa watu na watukufu wote wa ufalme wamekusanyika hapa. Rafiki yangu mwangalie kwa makini Raisi wa mkutano wenye haiba. Ebu tuukaribie kidogo ili tuweze kumjua kwa utulivu. Basi huyo hapa ni mwenye kuvaa nishani za hadhi za juu ni zaidi ya elfu moja na anaongea maneno yaliyojaa uturi uaminifu na utulivu. Na ambapo mimi nilikuwa nimejifunza jambo katika anayoyasema ndani ya siku kumi na tano zilizotangulia basi nitakujulisha vitu hivyo. Hakika nazungumzia kuhusu mfalme wa ufalme huu Mwenye miujiza na anasema: Hakika yeye ndiye ambaye amemtuma kwenu. Tazama hakika Yeye anadhihirisha mambo yenye kufurutu ada na miujiza dhahiri kiasi haiachi utata katika kuwa yeye ni mwenye kutumwa ameletwa mahususi kutokea kwa Mfalme Mkuu. Basi sikiliza vyema mazungumzo na maneno yake, basi viumbe vyote ni masikio yenye kumsikiliza yeye, bali ufalme kwa ujumla wake unamsikiliza, ambapo wote wanajitahidi kwenda mbio katika kusikiliza maneno yake mazuri na wanapupia kuona paji lake lenye kung’ara. Na je hivi unadhani kwamba mwanadamu peke yake ndiye anayemsikiliza? Bali wanyama vilevile, bali hata milima na visivyo na roho vinasikiliza amri zake na vinatetemeka kwa kumhofu na kuwa na shauku naye. Itazame miti namna inavyotii amri zake na kuendea katika yale aliyoyaashiria katika maeneo, hakika anabubujiza maji popote atakapo, bali hata kutoka kati ya vidole vyake, wanakunywa watu na kukata kiu kutokana na maji hayo yenye kutiririka. Tazama ile taa inayo ning’inia kutoka katika dari ya ufalme hakika inapasuka vipande viwili kwa kiasi tu cha kuashiria kwake. Basi kana kwamba ufalme huu na vilivyomo vinamjua vyema na vinajua kwa yakini kwamba yeye ni mfanya kazi aliyetumwa kwa jukumu kutoka kwa mfalme, na mfikishaji mwaminifu wa amri zake tukufu. Basi unawaona wanamfuata ufuataji wa askari mtiifu. Basi hapana mtambuzi mwenye akili katika wanaomzunguka isipokuwa anasema kuwa yeye ni Rasuli Mkarimu, na wanamsadiki na kunyenyekea maneno yake, sio hili tu bali wanamsadiki waliomo katika ufalme miongoni mwa milima na taa kubwa . Na wote wanasema kwa ulimi wa hali kwa unyenyekevu: Naam, hakika kila analolitamka ni kweli na uadilifu na lenye kusibu. Basi ewe rafiki mwenye kughafilika! Je unaona kuwa inayumkinika kuwepo kwa uwezekano japo kidogo wa uwongo au hadaa katika maneno ya huyu Mkarimu? Hasha lillah kuwa katika hilo chochote katika maneno yake kamwe. Naye ndiye ambaye mfalme amemkirimu kwa maelfu ya sharafu na nembo za heshima, nazo ni alama za kumsadikisha yeye, na watukufu wote wa ufalme wanamsadiki, na maneno yake yote ni uaminifu na utulivu, basi yeye anajadili katika sifa za Mfalme zenye muujiza na kuhusu amri zake fasaha. Ukiwa unakuta katika nafsi yako chochote katika uwezekano wa uwongo, basi inakulazimu kukadhibisha makundi yote yanayomsadiki yeye, bali ukanushe uwepo wa kasri na taa na ukanushe uwepo wa kila kitu na ukadhibishe hakika yao, na kama si hivyo basi lete uliyonayo ukiwa una chochote, kwani dalili zinatoa changamoto.
Ewe ndugu huenda umeongozeka kwa tuliyoyasema kidogo kidogo. Sasa basi nitakubainishia hoja kubwa zaidi kuliko hoja zote zilizotangulia. Tazama hizi amri za kifalme zinazoshuka kutoka katika anga la juu, wote wanaziheshimu na wanaziangalia kwa utukuzo na kupendezwa, na hakika huyo mtu mkarimu amesimama aliyetukuzwa kwa nishani kando ya hizo amri za nuru na anafasiria makundi yaliyokusanyika maana ya amri hizo. Tazama mtindo wa amri hakika zinaangaza na kumulika hata kuwapeleka wote katika kuvutiwa kwa mshangao mkubwa. Kwani najadili masuala muhimu ni muhimu kwa wote kiasi haachi yeyote ila anamsikiliza. Hakika anapambanua kikamilifu mambo ya Mfalme na matendo yake, amri zake na sifa zake. Kama ilivyo katika hizo amri za kifalme kuna nembo ya Mfalme Mwenyewe basi juu ya kila msitari katika misitari yake vilevile kuna nembo yake, bali ukiangalia kwa makini katika kila sentensi bali kila herufi ndani yake kuna muhuri wake mahususi ukiachilia mbali maana yake na makusudio yake, amri zake na makatazo yake. Muhtasari: Hakika ya hizo amri za kifalme zinajulisha juu ya huyo Mfalme Mtukufu kama kujulisha kwa mwanga juu ya mchana. Basi ewe rafiki: Nakudhania kuwa umerejea katika akili yako na umeamka kutoka katika usingizi wa kughafilika, hakika tuliokueleza na kuyakunjua katika hoja ni zenye kutoshelezea kabisa. Likionekana jambo kwako basi litaje. Haikuwa kwa mkaidi yule ila kuwa amesema: Sisemi hapana: Alhamdulillahi hakika nimeamini na nimesadiki, bali nimeamini imani ya wazi inayoangaza kama jua na kama mchana, na nimeridhia kwamba ufalme huu una Bwana Mlezi Mwenye ukamilifu, na huu ulimwengu una Mola Mwenye utukufu, na kasri hili lina muundaji Mwenye uzuri. Basi akuridhie Allah ewe rafiki yangu wa dhati hakika umeniokoa katika mateka ya inadi na ususuavu mbaya ambao umenifikisha mimi katika hadi ya wazimu na uzuzu, na sikufichi ewe ndugu yangu, hakika hoja ulizozileta, kila moja kati ya hizo ilikuwa ni yenye kujitosheleza kunifikisha mimi katika matokeo haya, isipokuwa mimi nilikuwa nakusikiliza kwa sababu kila hoja kati ya hizo imefungua anga rafiki mno na madirisha angavu zaidi katika kumtambua Allah na kumpenda kwa ikhlasi. Na kama hivi hekaya imekamilika ambayo ilikuwa inaashiria hakika kuu ya Twahidi na kumwamini Allah (s.w). Na katika kituo cha pili tutabainisha kwa fadhili ya Ar-Rahman na kwa mwanga wa Quran tukufu na nuru ya Imani, kwa mkabala na yaliyokuja kutoka katika hoja kumi na mbili katika Hekaya ya kumithilisha ming’ao kumi na mbili katika ming’ao ya jua la Tawhid ya kihakika baada ya kuziandalia Utangulizi. وَ مِنَ اللّٰهِ التَّو۟فٖيقُ وَ ال۟هِدَايَةُ Tunamuomba Allah (s.w) taufiki na mwongozo.

