Sözler

The Twenty-Seventh Word

Source: risaleinur multilingual dataset, risale.site source · Risale-Nur multilingual research corpus
Risale reading plan
§1

Kabla ya miaka mitano hivi au zaidi niliandika somo kuhusu Ijtihad katika Risala kwa Kiarabu kuitikia matakwa ya ndugu wawili wapendwa nimeandika neno hili ili kumwongoza asiyejua mpaka wake katika suala hili ili atambue yanayopasa asimame mbele yake. بِسْمِ اللّٰهِ الرَّحْمٰنِ الرَّحِيمِ وَلَو۟ رَدُّوهُ اِلَى الرَّسُولِ وَ اِلٰٓى اُولِى ال۟اَم۟رِ مِن۟هُم۟ لَعَلِمَهُ الَّذٖينَ يَس۟تَن۟بِطُونَهُ مِن۟هُم۟ Hakika mlango wa Ijtihad uko wazi, isipokuwa kuna vizuizi sita katika zama hizi vinavyozuilia kuingia humo.

§2

Kama yanavyozibwa matundu japo madogo zama za kuzidi kwa pepo wakati wa majira ya baridi, na wala haiwi haki kufungua milango mipya, na kama isivyofunguliwa mianya kwa ajili ya kuziba kuta na kuimarisha maboma zuizi wakati wa mkumbo wa mifereji, kwa sababu hilo hupelekea katika kuzama na kuangamia. Na kadhalika ni katika jinai kwa Uislamu kufungua milango mipya katika kasri lake kubwa, na kupasua nyufa katika kuta zake katika yanayoandaa njia kwa waviziaji na waharibifu kwa jina la Ijtihad, na hasa katika zama za maovu, na wakati wa hujuma ya desturi za kigeni na kutawala kwake, na wakati wa kukithiri kwa bidaa na kusongamana kwa upotevu na kuteketeza kwake.

§3

Hakika ya mambo ya kidharura ya kidini ambayo hayana uwanja wa Ijtihad katika mambo hayo kwa ukinaifu wake na kuthibiti kwake, na ambayo ni katika hukumu ya chakula na lishe, yamepuuzwa wakati wa sasa na yameanza kuweka nyufa, basi wajibu unalazimisha kutumia juhudi na kutoa hima wote kwa ajili ya kuhuisha mambo haya ya dharura na kuyasimamisha, ambapo hakika pande za kinadharia za Kiislamu zimefadhilisha fikira za salafu wema na zimekunjuka kwa jitihada zao za ikhlasi hata zimekuwa haziwi finyu kwa zama zote, kwa hiyo kuziacha Ijtihad hizo safi na kuzigeuka na kuelekea katika Ijtihad mpya kufuatia matamanio ya nafsi hakika hilo ni hiana iliyozushwa.

§4

Kama bidhaa inavyotangazwa sokoni kulingana na misimu na kuraghibishwa katika bidhaa hizo, kadhalika masoko ya maisha ya kijamii na maonesho ya ustaarabu wa wanadamu ulimwenguni, basi unaona bidhaa inaraghibishwa katika zama fulani, basi inakuwa na tija, basi macho huelekezwa katika bidhaa hiyo, na mawazo huvutwa upandwe wake, basi shauku huogelea juu yake. Basi mathalani: Hakika bidhaa ambayo macho yanaigeukia katika enzi zetu za sasa na kuraghibishwa ni kujishughulisha na mambo ya kisiasa na matukio yake, na kuaminisha starehe katika maisha ya Dunia na kutoa hima yote katika hilo, na kueneza fikira za kimaada na kuzieneza. Wakati ambapo tunaona hakika ya bidhaa ghali ya thamani, na bidhaa inayoenea na kukubaliwa katika enzi za salafu wema na wingi wa kinachoraghibishwa katika enzi hizo katika soko la zama zao ni kumridhisha Bwana Mlezi wa mbingu na Ardhi na kusimama mbele ya mipaka yake, na kuchukua amri zake na makatazo yake kutoka katika maneno yake matukufu, na kujitahidi ili kupata njia za kufikia katika furaha ya milele ambayo Qur’an tukufu imefungua milango yake hadi milele na Nuru ya Unabii iangazayo. Basi zikawa akili na nyoyo zote zimeelekea – katika enzi hiyo – na kwa nguvu zake zote katika kutambua radhi za Allah (s.w) na kutambua makusudio ya maneno yake, hata ikawa uelekea wa maisha yao na hali zao tofauti na mafungamano yao kati yao na matukio yao na mazungumzo yao vyote vinaelekea katika kumridhisha Bwana Mlezi wa Mbingu na Ardhi, kwa ajili hiyo basi katika mfano wa uhai huu ambao yanapita kwa pande zake mbali mbali kulingana na radhi za Bwana wa walimwengu wote (s.w) matukio yanakuwa kulingana na mwenye maandalizi na ukubalifu wa kimaumbile ni masomo na mazingatio kwa namna asiyohisi, na kana kwamba moyo wake na umbo lake yanapokea masomo na maelekezo kutokana na kila kinachozunguka pembezoni mwake, na vinapata faida viwili hivyo kutokana na kila tukio, mazingira na hatua. Na kana kwamba kila kitu kinatimiza duru ya mwalimu mwelekezi anafundisha umbile lake na kulifunza na kulielekeza na kuliandaa kwa ajili ya Ijtihad, hata mafuta ya busara yake yanakaribia kuangaza japo moto wa kuchuma haujayagusa. Basi mfano wa mtu huyu mwenye kujiandaa katika mfano wa jamii hii, katika Ijtihad katika zama zake, hakika maandalizi yake yanapata siri katika siri za (نُوْرٌ عَلَي نُوْرٍ) na anakua katika wakati wa karibu mno na wa haraka kuwa ni Mujitahid. Wakati ambapo katika enzi za sasa: Hakika ya kutawala kwa ustaarabu wa kiulaya, na kushika mamlaka kwa falsafa ya kimaada na fikra zake, na kuchangamana kwa mahitaji ya maisha ya kila siku. Vyote hivyo vinapelekea kuparaganyika kwa fikra na kutahayari kwa nyoyo na kutapanyika kwa hima na kudhoofu kwa utiliaji mkazo, mpaka mambo ya kimaanawy yamekuwa ni mageni katika akili. Kwa ajili hiyo, angepatikana hivi sasa ambaye ana busara za (Sufyan bin Uyayna) ambaye amehifadhi Qur’an tukufu na amekaa na wanazuoni na hali ya kuwa yuko katika mwaka wanne katika umri wake, angehitaji mifano kumi ya aliyohitajia Ibn Uyayna ili afikie daraja ya Ijtihad, yaani kwamba ingekuwa ni wepesi kwa Sufyan Ibn Uyayna kufanya Ijtihad katika miaka kumi basi yule ambaye yumo katika zama zetu hizi angeipata katika miaka mia moja, na hii ni kwa sababu msingi wa kujifunza kwa (Sufyan) wa kimaumbile wa Ijtihad unaanza kutokea katika mwaka wa upambanuzi na kuandaa utayari wake kidogo kidogo kama utayari wa kibiriti kwa moto, ama mweza wake katika wakati wa sasa fikra yake imezama katika dimbwi la falsafa ya kimaada na akili yake kutembea katika matukio ya kisiasa, na moyo wake umetahayari mbele ya mahitajio ya kimaisha, na utayari wake umekuwa mbali na ukubalifu wake na Ijtihad, basi hapana shaka utayari wake kuwa umekuwa mbali na uwezo wa Ijtihad za kisharia kwa kiwango cha kuwa na fani mbali mbali katika elimu za sasa za kidunia, na kupungukiwa na kuipata daraja ya ijtihad kwa kiwango cha kutabahari kwake katika elimu za kidunia, kwa ahiyo haiyumkiniki kusema kwa nini siwezi kufikia daraja ya Sufyan bin Uyayna nami ni kama yeye kaika akili ? naam, hana haki yeye kusema hivyo kama ambavyo hatalingana naye na wala hatafikia upeo wale kamwe.

§5

Hakika mwili kupenda kujipanua kwa ajili ya kukua ikiwa ni kwa ndani ni dalili ya kujikamilisha, wakati ambapo ikiwa ni kutokea nje inakuwa ni sababu ya kupasuka kwa mfuniko na ngozi, yaani ni sababu ya kuvunjika na uharibifu na sio kukuana kupanuka. Na namna hii, hakika kuwepo kwa ijtihad na kupenda kujipanua katika dini kwa wale ambao wanazunguka katika duara la Uislamu na wanaujia kupitia mlango wa Ucha Mungu na hofu kamili na kwa njia ya kutekeleza mambo ya dharura ya Kiislamu, ni dalili ya ukamilifu na kujikamilisha, na shahidi mwema kwa hilo ni salafu wema. Ama kutazamia ijtihad na kupenda kujipanua katika dini ikiwa kunatokana na wale mabao wameacha mambo ya dini ya kidharura na kupendelea maisha ya dunia na kuchafuka na falsafa ya kimaada, ni nyenzo ya kuharibu uwepo wa Kiislamu na kufungua hima ya Uislamu kutoka shingoni.

§6

Kuna nukta tatu zinahitajia taamuli na kutazama,, zinazipa jitihada za zama hizi sifa ya kiardhi, na kuzipora roho yake ya kimbinguni, wakati ambapo sharia ni ya mbinguni na jitihada kwa nafasi yake ni za mbinguni, kwa kudhihirisha kwake hukumu zake zilizojificha, na nukta ni hizi zifutazo: Kwanza: sababu ya kila mhukumu hutofautiana na “ hekima yake” hekima na masilahi na ni sababu ya kutia uzito na sio chanzo cha kuwepo wala sio chanzo cha kuwepo kwa hukumu hiyo wakati ambapo “ sababu” ni chanzo cha kuwepo kwa hukumu. Basi na tufafanue hili kwa mfano: swala hupunguzwa safarini, na kuswaliwa rakaa mbili. kitendo cha ruhusa hii ya kisharia. hekima yake ni mashaka. ikipatikana safari na hakukua na mashaka basi swala hupunguzwa. kwa sababu sababu ipo nayo ni safari wakati ambapo hakukuwa na safari na kukawa na maradufu ya mardufu ya mashaka, mashaka hayo hayatakuwa ni sababu ya swala kupunguzwa. Na tofauti na hakika hii mtazamo wa jitihada katika zama hizi katika kusimamisha masilahi na hekima badala ya sababu, na hutolewa hukumu yake kwa mwanga wa hiyo hekima, hapana shaka kwamba jitihada kama hizi ni ya kiardhi na siyo ya kimbinguni. Pili: Hakika mtazamo wa zama hizi unaelekea kwanza na hasa kuhakikisha usalama wa furaha ya dunia, na hukumu zinaelekezwa upande huo, na hali kuwa kusudio la Sharia kwanza kabisa linaelekea na hasa katika furaha ya Akhera, na kutazama furaha ya dunia kwa daraja ya pili. Na kuifanya kuwa ni nyenzo kwa maisha ya Akhera. yaani mwelekeo wa zama hizi ni mbali kabisa na roho ya sharia na makusudio yake, haziwezi kujitahidi kwa jina la sharia.. Tatu: Hakika ya kanuni ya kisharia (Dharura zinahalalisha yaliyozuiliwa) sio ya jumla, kwa sababu dharura ikiwa inatokana na njia ya haramu haiwi sababu ya kuhalalisha haramu. Na kama si hivyo basi dharura ambayo imetokana na ubaya wa uchaguzi wa mtu, kwa njia zisizo za kisharia haiwi hoja wala sababu ya kuhalalisha wala eneo la hukumu za ruhusa. Basi mathalani: Ikiwa mmoja amejilewesha - kwa uchaguzi wake mbaya - basi matendo yake mbele ya wanazuoni wa Sheria ni hoja dhidi yake, yaani hasameheki, na ikiwa atamwacha mkewe basi talaka yake imetuka, na ikiwa atatenda kosa ataadhibiwa kwa kosa hilo, lakini ikiwa pasi na hiari yake, basi haituki talaka yake, wala haadhibiwi kwa jinai aliyoifanya basi bozi wa pombe - mathalani - hapaswi kusema kwamba ni dharura kwangu, kwa hiyo pombe kwangu ni halali, hata angekuwa ni mwenye kujaribiwa kwa hiyo pombe kwa kiwango cha dharura kulingana na yeye. Basi kutokana na mtazamo huu hakika kuna mengi ya mambo katika wakati wa sasa watu wamejaribiwa nayo na yamekuwa ni dharura kwa kulingana na wao, hata yamechukua namna ya (Mabalaa yenye kuenea) basi hii ambayo inaitwa ni dharura, haitakuwa hoja ya hukumu ya ruhusa, wala kwa ajili yake havihalalishwi vilivyozuiliwa, kwa sababu hayo yametokana na ubaya wa kuchagua kwa mtu na kutokana na matakwa yasiyokuwa ya kisharia na kutokana na miamala iliyoharamishwa. Na kwa kuwa watu wa Ijtihad wa zama hizi wamejaalia dharura hizo ni mzunguko wa hukumu za kisharia, kwa hiyo Ijtihad zao ni za kiardhi na zenye kufuata matamanio na zenye kuchanganyika na falsafa ya kimaada, kwa hiyo Ijtihad hizo sio za kimbinguni, na haisihi kuziita kuwa ni Ijtihad za kisharia kabisa, hii kwa sababu kila kitendo katika hukumu za Muumba wa mbingu na Ardhi na kuingilia kokote katika ibada ya waja wake bila ya ruhusa au idhini ya kimaanawy hilo ni lenye kurudishwa. Na tutoe mfano wa hilo: Wanaona vizuri baadhi ya wenye kughafilika kutoa hotuba ya Ijumaa na mifano yake katika alama za Kiislamu kwa lugha ya kienyeji ya kila watu isiyokuwa Kiarabu na wanatoa hoja ya huku kuona kwa vizuri kwa sababu mbili: Kwanza: (Ili waweze watu wa kawaida Waislamu kufahamu matukio ya kisiasa)! Pamoja na kuwa yameingiwa na uongo, fitina na hadaa mambo ambayo yameyafanya kuwa katika hukumu ya wasiwasi wa mashetani! wakati ambapo mimbari ni mahali pa kufikisha wahyi wa Kiungu, nao ni wa juu na mtukufu mno kuliko kupanda wasiwasi wa kishetani juu yake. Pili: (Hotuba ni kwa ajili ya kufahamu nasaha zinazoelekezwa na baadhi ya sura za Qur’an). Naam, wangekuwa wengi wa Waislamu wanafahamu mambo ya kukukubalika kisharia na hukumu zinazojulikana katika Dini kwa dharura, na kuyatekeleza, basi huenda ingekuwa inakuwa vizuri wakati huo kuleta hotuba kwa lugha inayojulikana kwao, na ingekuwa kutafsiri sura katika Qur’an ina hoja – ikiwa kutafsiri kunawezekana - na hii ili wafahamu nadharia za kisharia na masuala nyeti na nasaha zilizojificha. Ama ikiwa zimepuuzwa katika zama zetu hizi hukumu za wazi zenye kujulikana; kama wajibu wa swala, zaka, saumu, uharamu wa kuua, zinaa na pombe, na kwamba watu wa kawaida hawana haja ya masomo katika kujua wajibu huu na uharamu ule kwa kiasi walivyo na haja ya kutekeleza hukumu hizo na kuzifuata katika maisha yao. Na hilo halitimii isipokuwa kwa kuwakumbusha na kuwahimiza kufanya amali na kuamsha hima na kuchokoza ghera ya Uislamu katika mishipa yao, na kuharikisha hisia za kiimani kwao ili waamke katika kutekeleza na kufuata hukumu hizo takasifu. Basi Mwislamu wa kawaida - vyovyote utakavyo fika ujinga wake - anatambua maana hii ya jumla kutoka katika Qur’an tukufu, na kutoka katika hotuba ya Kiarabu. Na anajua katika tulio la moyo wake kwamba mtoa hotuba na msomaji wa Qur’an anamkumbusha – na anawakumbusha wengine pamoja naye - nguzo za Imani na misingi ya Uislamu ambayo inajulikana katika Dini kwa dharura. Na hapo moyo wake hujawa na shauku za kutekeleza hukumu hizo. Laiti ningetambua ni maelezo gani ulimwenguni kote yanaweza kusimama juu ya miguu yake mbele ya muujiza wa kupendeza katika Qur’an tukufu inayoungana na Arshi tukufu. Na uraghibishaji upi na mahofisho yapi na bayana ipi na ukumbusho yamkini kuwa bora kuliko hiyo Qur’an!?

§7

Hakika ukaribu wa Mujitahidina wakuu katika salafu wema na enzi za sahaba wema ambayo ni enzi ya hakika na enzi ya nuru umewarahisishia kuchukua nuru safi kutoka katika vyanzo vyake vya karibu mno, wakaweza kufanya Ijtihad zao za ikhlasi, wakati ambapo Mujitahidina wa enzi za sasa wanatazama kitabu cha hakika kutokea masafa ya mbali mno na nyuma ya sitara na vizuizi vingi mno hata inakuwa ni ngumu kwao kuona herufi ya wazi sana katika hiyo Qur’an. Ukisema: Hakika eneo la kuzunguka Ijtihad na chanzo cha hukumu za kisharia ni uadilifu wa sahaba na ukweli wao, hata umma umeafikiana kwamba wao ni waadilifu wa kweli, hali ya kujua kwamba wao ni wanadamu mithili yetu, hawaepukani na kosa! Jibu: Hakika sahaba (r.a) ni viongozi wa haki na waashiki wake, nao ndio wenye shauku ya ukweli na uadilifu. Na hakika imebainika katika enzi zao ubaya wa uongo na maovu yake, na uzuri wa ukweli na mema yake kwa uwazi kamili, ambapo imekuwa mtengano ni mpana kati ya ukweli na uongo kama umbali wa Thurea na mchanga na baina ya Arshi na tandiko!! Ambapo tofauti hiyo kubwa inafafanua baina ya Mtume Mtukufu (s.a.w) aliyesimama juu ya kilele cha daraja za ukweli na katika juu ya walio juu na kati ya Musailama Al-Kadhaab ambaye alikuwa chini ya waliokuwa chini na katika chini ya ngazi za uongo. Basi kilichomuangusha Musailama hadi katika ngazi hizo za chini duni ni uongo na kilichompandisha (Muhammad Mwaminifu) (s.a.w) hadi katika ngazi hizo za juu ni ukweli na unyofu. Kwa hiyo sahaba wema (r.a) ambao walikuwa wanamiliki hima za juu na tabia zilizonyanyuka na kupata nuru kwa nuru ya usuhuba wa jua la Unabii, hapana shaka kwamba wao walijiinua juu mbali na uongo unaochukiwa mbaya uliopo katika bidhaa ya Musailama Al-Kadhaab na najisi zake zenye kupasisha udhalili na kutwezwa – kama ilivyo thabiti – na walijiepusha na uongo kama kujiepusha kwao ukafiri ambao ni mwenza wake, na walikwenda mbio kwa pupa katika kutafuta ukweli, unyofu na haki, na wakautafuta kwa makini kwa kila walichopewa katika nguvu na azma. Wakavutiwa nayo na hasa katika mapokezi ya hukumu za kisharia na kuzifikisha, hizo hukumu zenye alama ya uzuri na urembo wenye kubebwa na haiba na fahari, ambayo ni njia ya kukwea kwa kupanda juu katika hadhi ya juu na ukamilifu, na yenye kuunganishwa sababu yake na utukufu wa Mtume (s.a.w) ambaye maisha ya wanadamu yamechukua nuru ya mwale wake. Ama sasa, masafa yamekuwa finyu kati ya ukweli na uongo, na yamepungua hata yamekuwa karibu bali vimeshikamana bega kwa bega, na imekuwa kugura kutoka kwenye ukweli kwenda kwenye uongo ni rahisi na kwepesi mno bali uongo umekuwa unafadhilishwa kuliko uongo katika propaganda za kisiasa. Basi ikiwa kitu kizuri mno kinauzwa pamoja na kibaya mno katika duka moja ubavu kwa ubavu na kwa thamani hiyohiyo, basi yatakikana kwa mnunuzi wa lulu ya ukweli ulio ghali asitegemee maneno ya mwenye duka na maarifa yake bila ya kuchunguza na kupembua.

§8

Na sheria hubadilika kwa kubadilika kwa enzi, na zinaweza kuja Sharia tofauti, na hutumwa mitume watukufu katika enzi moja, kulingana na kaumu. Na hili limetokea kimatendo. Ama baada ya kuhitimu kwa Unabii, na kutumwa Mwisho wa manabii na mursali (a.s) hakuja baki haja ya sharia nyingine. Kwa sababu Sharia yake kuu inatosha kwa kila kaumu na kila enzi. Ama sehemu ndogo ndogo za hukumu zisizoelezwa na ambazo zinahitajia kubadilika kwa kufuatia mazingira, basi ijtihad za wanazuoni wa madhehebu zinabeba ushughulikaji wa kubadilisha. Basi kama nguo zinavyo badilishwa kwa kubadilika kwa misimu, na kubadilishwa dawa kulingana na haja ya wagonjwa, kadhalika sharia hubadilishwa kwa kubadilika kwa enzi, na hukumu zinazunguka kulingana na utayari wa nyumati kimaumbile, kwa sababu hukumu za kisharia za kimatawi hufuata hali za wanadamu, na zinakuja zikiafikiana nao na kuwa ni dawa ya ugonjwa wao. Basi katika zama za manabii waliotangulia (a.s) tabaka za wanadamu zilikuwa mbalimbali, pamoja na yaliyo kuwamo kwao katika utengano na ukali wa tabia, basi walikuwa karibu zaidi wanavyo kuwa katika ubedui katika fikira, kwa ajili hiyo sharia zimekuja katika zama hizo zikiwa mbalimbali na zimetofautiana, pamoja na kuafikiana na hali zao na kuwiana na mazingira yao, hata wamekuja manabii wengi na sharia tofauti katika eneo moja na katika enzi moja. Lakini kwa ujio wa mwisho wa mitume naye ni nabii wa zama za mwisho (s.a.w), wanadamu wamekamilika na kana kwamba wamepanda kutoka katika ngazi ya masomo ya msingi na sekondari kwenda katika ngazi ya masomo ya juu na wamekuwa ni wenye kustahiki kupokea somo moja, na kumsikiliza mwalimu mmoja, na kufanyia kazi Sharia moja. Basi pamoja na kukithiri kwa hitilafu hakuja bakia haja tena ya Sharia nyingi wala dharura ya walimu wengi. Lakini kwa kushindwa kwa wanadamu kufika wote katika ngazi moja, na kutokuweza kwao kuenda katika mtindo mmoja katika maisha yao ya kijamii basi Madhehebu ya kifiqhi yamekuwa mengi katika matawi. Lau wanadamu wangeweza – kwa wingi wao wa hali zote – kuishi maisha ya kijamii mamoja, na kuwa katika ngazi moja, basi wakati huo itayumkinika kuunganisha madhehebu. Lakini kama ilivyo hali za ulimwengu na tabia za watu haziruhusu, kufikia hali hiyo, basi hakika madhehebu ni kadhalika hayawi mamoja. Ukisema: Hakika haki ni moja, basi vipi itayumkinika kuwa hukumu tofauti za madhehebu manne na kumi na mbili kuwa ni haki? Jibu: Maji huchukua vionjo vitano tofauti kulingana na maonjo ya wagonjwa mbalimbali na hali zao: Ni dawa ya mgonjwa kulingana na uelekea wake, yaani kuitumia ni wajibu juu yake kitiba. Na huenda ikasababisha madhara kwa mgonjwa mwingine hiyo ni kama sumu kwake, yaani ni haramu juu yake kitiba, na inaweza kuzalisha madhara machache kwa mgonjwa mwingine kwa hiyo basi hiyo ni makuruhu kwake kitiba, na inaweza kuwa yenye manufaa kwa mwingine bila ya kumdhuru, basi ni sunna kwake kitiba, na inaweza isimdhuru mwingine wala kumnufaisha, basi hiyo kwake ni Mubaha kitiba basi na afurahie kuinywa. Basi tunaona kutokana na mifano iliyotangulia: Hakika haki imekuwa nyingi hapa, basi mafungu matano yote ni haki, je una nafasi ya kusema: Hakika maji ni tiba na si vinginevyo, au wajibu tu, au haina hukumu nyingine? Na kama hivi – kwa mfano wa yaliyotangulia – hukumu za kiungu hugeka kwa mwendo wa hekima ya kiungu na kulingana na wafuasi wake. Basi inabadilika haki, na kubakia haki na inakuwa kila hukumu kati yake ni haki na inakuwa ni masilahi. Basi mathalani: Tunaona walio wengi ambao wanamfuata Imamu Shafi (r.a) ni wa karibu zaidi kuliko Wa Ah’Nafi na ubedui na maisha ya kijijini, maisha ambayo yenye kupungua kunako maisha ya kijamii yanayounganisha kundi. Kila mtu anataka kuchanua anachokipata nafsini mwake kwa mwenye kukidhi haja kwa utulivu wote na uhadhiri wa moyo, na anatafuta haja yake mahususi kwa nafsi yake na kutaka hifadhi kwake, anasoma sura Al-Fatihat yeye mwenyewe licha ya kuwa ni mwenye kumfuata Imamu. Na hii ni dhati ya haki, na hekima tupu katika wakati huo huo. Ama ambao wanamfuata Al-Imam Al-A’dham (Abu Hanifa An-Nuuman) (r.a), wao kwa wingi wao wa hali zote wako karibu zaidi katika ustaarabu na maisha ya miji iliyopata sifa ya maisha ya kijamii, na hii ni kwa hukumu ya kushikamana kwa aghalabu ya serikali za Kiislamu na madhehebu hayo. Ikawa jamaa moja katika swala kana kwamba ni mtu mmoja, na amekuwa mtu mmoja kama anazungumza kwa jina la wote, na ambapo wote wanamsadiki na wanafungamana naye kwa moyo, hakika kauli yake inakuwa katika hukumu ya kauli ya wote, basi mtu kutosoma (Sura al Fatiha) nyuma ya Imamu ni haki yenyewe na dhati ya hekima. Na mathalani: Ilipokuwa Sharia inaweka vizuizi ili kuzuia watu wasivuke mipaka yao, iwanyoshe na kuwaadibisha nayo, iilee nafsi yenye kuamrisha uovu, basi hapana budi udhu utenguke kwa kumgusa mwanamke na uchache wa najisi unadhuru, kwa mujibu wa madhehebu ya Shafi ambayo wengi wa wafuasi wake ni katika watu wa vijijini na nusu ya mabedui na wenye kuzama katika kazi. Ama kwa mujibu wa madhehebu ya Hanafi ambao wao kwa wingi wao wa hali zote wameingia maisha ya kijamii, na wamechukua hatua ya nusu wastaarabu udhu hautenguki kwa kumgusa mwanamke, na yanaruhusu kiasi cha Dirhamu ya najisi. Na sasa na tumtazame mfanya kazi na Afisa, basi mfanya kazi kwa hukumu ya kuishi kwake kijijini hua katika nafasi ya kuchanganyika na kugusana na wanawake wa kando na kukaa pamoja chini ya jiko moja, na kuingia katika maeneo yaliyochafuliwa basi yeye anajaribiwa na yote haya kwa hukumu ya kazi yake na maisha yake, nafsi yake yenye kuamrisha uovu huweza kukuta uwanja mbele yake wa kuvuka mipaka yake, kwa hiyo sharia inaweka katika moyo wa huyu mwangwi wa mbinguni basi inazuia uvukaji huo kwa kumwamrisha (mfanya kazi). Usiguse kinachotengua udhu, swala yako isibatilike. Ama yule afisa, basi yeye kwa mujibu wa mazowea yake ya kijamii hawi na nafasi ya kuchanganyika na wanawake wa kando – kwa sharti awe mwenye kujiheshimu – wala hajichafui sana na najisi, hali ya kuwa mwenye kuchukua sababu za usafi wa kistaarabu. Kwa hiyo sharia haikumkazania, bali imemdhihirishia upande wa ruhusa – kinyume cha azma – kwa jina la madhehebu ya Hanafi na kumfanyia tahafifu kwa kusema: Mkono wako ukimgusa mwanamke wa kando udhu wako hautenguki, na hakuna madhara juu yako ikiwa hukustanji kwa maji kwa sababu ya kuwaonea haya waliokuwapo, basi kuna msamaha kwa kiasi cha dirhamu ya najisi kwa jambo hili humkomboa na wasiwasi, na kumuokoa na kusitasita. Basi matone haya mawili kutoka baharini ya bahari tunayaeleza kwa mfano, yatumie kuwa ni kipimo na ikiwa utaweza kupima Sharia kwa vipimo vya Al-Shaarany kwa uelekea huu basi fanya. سُب۟حَانَكَ لَا عِل۟مَ لَنَٓا اِلَّا مَا عَلَّم۟تَنَٓا اِنَّكَ اَن۟تَ ال۟عَلٖيمُ ال۟حَكٖيمُ اَللّٰهُمَّ صَلِّ وَ سَلِّم۟ عَلٰى مَن۟ تَمَثَّلَ فٖيهِ اَن۟وَارُ مَحَبَّتِكَ لِجَمَالِ صِفَاتِكَ وَ اَس۟مَائِكَ بِكَو۟نِهٖ مِر۟اٰةً جَامِعَةً لِتَجَلِّيَاتِ اَس۟مَائِكَ ال۟حُس۟نٰى وَ مَن۟ تَمَر۟كَزَ فٖيهِ شُعَاعَاتُ مَحَبَّتِكَ لِصَن۟عَتِكَ فٖى مَص۟نُوعَاتِكَ بِكَو۟نِهٖ اَك۟مَلَ وَ اَب۟دَعَ مَص۟نُوعَاتِكَ وَ صَي۟رُورَتِهٖ اَن۟مُوذَجَ كَمَالَاتِ صَن۟عَتِكَ وَ فِه۟رِس۟تَةَ مَحَاسِنِ نُقُوشِكَ وَ مَن۟ تَظَاهَرَ فٖيهِ لَطَائِفُ مَحَبَّتِكَ وَ رَغ۟بَتِكَ لِاِس۟تِح۟سَانِ صَن۟عَتِكَ بِكَو۟نِهٖ اَع۟لٰى دَلَّالٖى مَحَاسِنِ صَن۟عَتِكَ وَ اَر۟فَعَ ال۟مُس۟تَح۟سِنٖينَ صَو۟تًا فٖى اِع۟لَانِ حُس۟نِ نُقُوشِكَ وَ اَب۟دَعِهِم۟ نَع۟تًا لِكَمَالَاتِ صَن۟عَتِكَ وَ مَن۟ تَجَمَّعَ فٖيهِ اَق۟سَامُ مَحَبَّتِكَ وَ اِس۟تِح۟سَانِكَ لِمَحَاسِنِ اَخ۟لَاقِ مَخ۟لُوقَاتِكَ وَ لَطَائِفِ اَو۟صَافِ مَص۟نُوعَاتِكَ بِكَو۟نِهٖ جَامِعًا لِمَحَاسِنِ ال۟اَخ۟لَاقِ كَافَّةً بِاِح۟سَانِكَ وَ لِلَطَائِفِ ال۟اَو۟صَافِ قَاطِبَةً بِفَض۟لِكَ وَ مَن۟ صَارَ مِص۟دَاقًا صَادِقًا وَ مِق۟يَاسًا فَائِقًا لِجَمٖيعِ مَن۟ ذَكَر۟تَ فٖى فُر۟قَانِكَ اِنَّكَ تُحِبُّهُم۟ مِنَ ال۟مُح۟سِنٖينَ وَ الصَّابِرٖينَ وَ ال۟مُؤ۟مِنٖينَ وَ ال۟مُتَّقٖينَ وَ التَّوَّابٖينَ وَ ال۟اَوَّابٖينَ وَ جَمٖيعِ ال۟اَص۟نَافِ الَّذٖينَ اَح۟بَب۟تَهُم۟ وَ شَرَف۟تَهُم۟ لِمَحَبَّتِكَ فٖى فُر۟قَانِكَ حَتّٰى صَارَ اِمَامَ ال۟حَبٖيبٖينَ لَكَ وَ سَيِّدَ ال۟مَح۟بُوبٖينَ لَكَ وَ رَئٖيسَ اَوِدَّائِكَ وَ عَلٰى اٰلِهٖ وَ اَص۟حَابِهٖ وَ اِخ۟وَانِهٖ اَج۟مَعٖينَ اٰمٖينَ بِرَح۟مَتِكَ يَا اَر۟حَمَ الرَّاحِمٖينَ

§9

Inahusu Sahaba Wema (r.a) Nasema kama alivyosema maulana Jame: Ewe mjumbe wa Allah haidhuru Ningeingia peponi pamoja na wenye kuingia Kama mbwa wa As’habul Kahf Katika kundi la sahaba wako wa Awali Ni yupi afaaye zaidi kuingia peponi mimi au aliyelinda pango miaka Yeye ni mbwa wa As’habul Raqiimi Na mimi ni mbwa wa As’habil Amini. بِاس۟مِهٖ سُب۟حَانَهُ وَ اِن۟ مِن۟ شَى۟ءٍ اِلَّا يُسَبِّحُ بِحَم۟دِهٖ بِسْمِ اللّٰهِ الرَّحْمٰنِ الرَّحِيمِ مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّهِ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاء عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ تَرَاهُمْ رُكَّعًا سُجَّدًا يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّهِ وَرِضْوَانًا سِيمَاهُمْ فِي وُجُوهِهِم مِّنْ أَثَرِ السُّجُودِ ذَلِكَ مَثَلُهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَمَثَلُهُمْ فِي الْإِنجِيلِ كَزَرْعٍ أَخْرَجَ شَطْأَهُ فَآزَرَهُ فَاسْتَغْلَظَ فَاسْتَوَى عَلَى سُوقِهِ يُعْجِبُ الزُّرَّاعَ لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِنْهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا Ewe ndugu yangu unauliza: Hakika kuna mapokezi yanafidisha kuwa wakati wa kuenea kwa bidaa yamkini wakafika waumini wa kweli daraja ya sahaba watukufu (r.a) na huenda wakawashinda, je mapokezi haya ni sahihi? Na ikiwa hivyo nini hakika yake? Jibu: Hakika ya ijmai ya Ahlu Sunna Wal Jamaa ni hoja yenye kukata kwamba sahaba wema ni watu bora zaidi baada ya manabii (a.s), basi kilicho sahihi kutokana na mapokezi hayo inahusu fadhila za kibaadhi na sio fadhila za kiujumla, kwani aweza kuzidi uzito mwenye kuzidiwa katika fadhila za kibaadhi na katika ukamilifu mahususi maalum, na kama si hivyo hafikii yeyote kwa upande wa fadhila za kiujumla cheo cha sahaba wema ambao Allah (s.w) amewasifu katika Qur’an yake iliyo bayana na amewasifu katika Taurati na Injili kama ilivyo mwishoni mwa Sura Al-Fat’h. Basi tutabainisha tatu katika hekima zilizo na sababu tatu kati ya nyingi miongoni mwa sababu na hekima.

§10

Hakika tumethibitisha katika yote maneno ya (Kumi na mbili na ishirini na nne na ishirini na tano): Hakika ya uwiano wa unabii kwenda kulinganisha na Uwalii ni kama uwiano wa jua lenye kushuhudiwa kwa dhati yake kwa kulinganisha na sura yake ya kimfano inayoonekana katika kioo, kwa hiyo hakika hadhi ya juu ya cheo cha wenye kutenda katika eneo la unabii nao ni sahaba wema ambao walikuwa ni nyota za karibu kuelekea lile jua lenye kung’ara, na kunyanyuka kwa cheo chao juu ya mawalii wema ni kwa uwiano wa hadhi ya juu ya eneo la Unabii na kunyanyuka kwake juu ya eneo la uwalii, bali hata angechuma mmoja wa mawalii cheo cha uwalii mkuu, nacho ni cheo cha warithi wa Manabii na masidikina na uwalii wa sahaba, hakika hafikii makamo ya wale wateule waliotangulia katika safu ya awali (r.a). Tutabainisha pande tatu kati ya pande nyingi za hii sababu ya tatu: Upande wa Kwanza Haiwezekani kuwafikia sahaba wema katika Ijtihad, yaani katika kuzitoa hukumu, yaani kutambua yanayomridhisha Allah (s.w) kupitia maneno yake; kwa sababu mhimili wa mapinduzi hayo makubwa ya kiungu yaliyotokea wakati huo yalikuwa yanazunguka katika kumridhisha Allah (s.w) kupitia kuzifahamu hukumu za kiungu. Basi akili zote zilikuwa zimefunguliwa kuelekea katika kutoa hukumu, na nyoyo zote zilikuwa na shauku ya kujua: Nini Mola wetu anataka kutoka kwetu? Basi mazungumzo na majadiliano yalikuwa yamejumuisha maana haya, na mazingira na matukio yanapita katika mwanga wake. Na kwa kuwa kila kitu katika wakati huo na kila hali na kila mjadala na baraza za pamoja na mazungumzo na masimulizi huenda kwa vile ambavyo maana hayo yanaelekeza na kujulisha, kwa hiyo - ilikuwa mazingira hayo - yanakamilisha kukubalika kwa hali za sahaba wema na kunawirisha fikira zao na kuandaa utayari wao wa kuchukua harubu zake kwa ajili ya Ijtihad na kutoa hukumu, ambapo walikuwa wanavuna kutokana na uwezo wa Ijtihad na kutoa hukumu katika siku moja au katika mwezi mmoja kiasi kisichoyumkinika kukipata katika wakati huu mtu ambaye ni katika kiwango cha busara zao na utayari wao katika miaka kumi, bali katika miaka mia moja, kwa sababu macho katika wakati uliopo yameelekea katika kupata maisha ya dunia ya starehe sio furaha ya Akhera ya milele na maisha ya neema za kudumu humo, basi macho yameondoshwa na hilo. Basi huzuni za maisha ambazo zinaongezeka kwa kutokumtegemea Allah (s.a.w) zinaweka uzito wake juu ya roho ya mwanadamu na kumfanya kuwa katika kubabaika na wasiwasi, na falsafa ya kimaada na kiasili inaichosha akili na kupofua uoni. Basi inaona mazingira ya kijamii yaliyopo kama ambavyo hayasaidii akili ya mtu huyo (mwenye busara) wala haimarishi utayari wake wa kimaumbile kuelekea kwenye Ijtihad ukiachilia mbali kwamba yanamparaganyisha na kumchosha zaidi. Hakika tumefungamanisha mlinganisho katika Risala ya (Ijtihad) kati ya Sufyan Bin Uyayna na ambaye yupo katika kiwango cha busara yake katika enzi hizi, na kuhitimisha katika mlinganisho kwamba alichokipata Sufyan katika enzi zake kutokana na uwezo wa kutoa hukumu ndani ya miaka kumi haiyumkiniki kupata ambaye yuko katika kiwango cha busara yake katika enzi hizi ndani ya miaka mia moja. Upande wa Pili Haiyumkiniki kuwafikia sahaba wema katika ukaribu wao kwa Allah kwa hatua za Uwalii, hiyo ni kwa sababu Allah (s.w) yeye yu karibu nasi kuliko mshipa wa shingo, ama sisi tuko mbali naye umbali wa hali zote, na mwanadamu yamkinika yeye akapata ukaribu naye kwa sura mbili zifuatazo: Sura ya kwanza: Kwa upande wa kufunuka kwa ukaribu wake (s.w) kwa mja. Basi ukaribu wa Unabii kwake (s.w) ni kutokana na kufunuka huku. Na sahaba wema kwa kuwa wao ni warithi wa unabii na usuhuba wa kinabii wanapata kufunuka huku. Sura ya pili: Kwa upande wa kuwa mbali kwetu na Allah (s.w), basi kutafuta utukufu kwa kitu katika ukaribu wake (s.w) inakuwa kwa kukata ngazi kumwelekea. Na mno ya njia za uwalii, na yaliyomo miongoni mwa mwenendo na maadili yanakwenda katika sura hii sawa katika hizo mwendo wa kinafsi au wa kianga. Basi sura ya kwanza ambayo ni kufunuka ukaribu wake (s.w) - yaani kuwa kwake (s.w) karibu na mja - ni hiba tupu kutoka kwake (s.w) na sio kuvuna katu, yaani ni kuvutika kwa kiungu na kuvuta kwa urehemevu, na upendo wa ikhlasi. Basi njia ni fupi, isipokuwa ni thabiti imara, nayo ni ya juu iliyonyanyuka ya hadhi iliyoinuka mno, na safi tohara hakuna kivuli wala kutibuka ndani yake. Ama sura nyingine ya kukaribia kwa Allah, ni kwa kuchuma kurefu, kuna vitibuzi na vivuli ndani yake, pamoja na kuwa mambo yake yenye kufurutu ada ni mengi hakika sura hiyo haifikii sura ya kwanza kwa upande wa umuhimu na ukaribu kwake (s.w). Na tufafanue hilo kwa mfano: Ili kuipata jana kutokana na siku hii kuna njia mbili: Kwanza: Kujivua kutokana na matukio ya zama na kwenda kwake kwa nguvu ya kiutakatifu, na kupaa kwenda juu ya zama, na kuiona jana ipo hadhiri kama leo. Pili: Ni kukata masafa ya mwaka mmoja kamili ili kukutana na jana upya, na pamoja na hivyo haiyumkiniki kuishika, kwa sababu inakuacha na kuondoka. Na kama hivi jambo katika kufanyika kutoka katika dhahiri kwenda katika hakika, ni kwamba liko katika sura mbili: Kwanza: Kuvutika katika hakika moja kwa moja na kuipata hakika katika dhati ya dhahiri yenye kushuhudiwa, bila ya kuingia katika kizuizi cha njia. Pili: Kukata ngazi nyingi kwa kwenda na kupitia maadili. Basi watu wa uwalii licha ya kuwa wanaafikishwa kumalizika kwa nafsi yenye kuamrisha maovu na wanaiua, hakika wao hawafikii ngazi za sahaba wema, kwa kuwa nafsi za sahaba zilikuwa zimetakaswa, wakapata mengi katika aina za ibada na mitindo mbalimbali katika aina za shukurani kwa zana nyingi za nafsi, wakati ambapo ibada za mawalii – baada ya kumalizika kwa nafsi – inakuwa nyepesi na rahisi. Upande wa Tatu: Haiyumkiniki kuwakuta sahaba wema katika fadhila za amali na thawabu ya matendo na malipo ya Akhera, kwa kuwa askari mwenye kufungamana na mapambano katika saa moja ya muda katika mazingira magumu yanayo mzunguka, na katika mahali muhimu pa kutisha, anavuna fadhila na thawabu inalingana na mwaka mmoja wa ibada, na akisibiwa na pigo moja ndani ya dakika moja, hakika huyo anapanda hadhi katika ngazi ambayo haiyumkiniki kuifikia katika ngazi za Uwalii isipokuwa ndani ya siku arobaini kwa uchache wa makadirio. Kadhalika jambo lilivyo katika jihadi ya sahaba wema katika kusimika nguzo za Kiislamu, na kueneza hukumu za Qur’an, na kutangaza kwao vita kwa ulimwengu mzima kwa jina la Uislamu, hiyo ni ngazi kubwa na huduma tukufu, mwaka kamili wa amali kwa wengine haufikii dakika moja ya amali yao, bali inasihi kusemwa: Hakika dakika za umri wa sahaba wema zote - katika huduma hiyo takatifu - hakika ni kwa mfano wa dakika ambayo amekufa shahidi ndani yake askari, na hakika saa za umri wao zote ni kwa mfano wa saa ya huyo askari wa kujitolea mwenye kufungamana na mapambano katika mahali pa hatari pa kutisha. Basi amali ni chache, isipokuwa malipo ni makubwa, thawabu ni nyingi, umuhimu ni mtukufu. Naam! Hakika sahaba wema hakika wanawakilisha tofali la awali katika kuasisi jengo la Uislamu, nao ni safu ya awali katika kueneza nuru za Qur’an, basi wao wana fungu kubwa kutokana na mema yote ya umma, kwa mujibu wa kanuni (Sababu kama mtendaji). Basi umma wa Kiislamu wakati wa kukariri kwao: ( اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى سَيِّدِنَا مُحَمَّد وَعَلَى آلِهِ وَأَصْحَابِهِ وَسَلَّم ) hakika unabainisha fungu kubwa walilo nalo Ali na sahaba wema katika mema yote ya umma. Na ili tufafanue yanayofuatia katika matokeo makubwa juu ya athari ndogo tu mwanzoni tunaeleza mifano ifuatayo: Sifa mahususi ndogo muhimu katika shina la mmea linachukua sura kubwa katika matawi yake, basi sifa hiyo maalum katika shina ni kubwa kuliko tawi kubwa, na mwinuko mdogo mwanzoni hua kidogo kidogo ni mkubwa huko mwishoni, na kwamba ziada ndogo katika nukta ya katikati – japo kwa kadri ya chanda – wakati mwingine hua kwa kadri ya mita kamili katika duara linalozunguka. Na kama hivi hakika sahaba wema wao ni waasisi wa Uislamu, na mashina ya mti wa Uislamu yenye kung’aa, na kuanza misitari ya msingi wa jengo la Uislamu, na nguzo ya jamii ya Kiislamu na viongozi wake, na watu wa karibu zaidi na jua la Unabii lenye kunawiri na taa ya hakika, basi amali chache kutoka kwao ni kubwa na tukufu, na huduma ndogo wanayoitoa ni kubwa na nyingi, basi haiwezekani kuwafikia na kuwapata isipokuwa mtu awe ni sahaba mfano wao. اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى سَيِّدِنَا محَمَّد ambaye amesema: (Sahaba wangu ni kama nyota yeyote mtakayemfuata mmeongoka) na (Ubora wa karne ni karne yangu) سُب۟حَانَكَ لَا عِل۟مَ لَنَٓا اِلَّا مَا عَلَّم۟تَنَٓا اِنَّكَ اَن۟تَ ال۟عَلٖيمُ ال۟حَكٖيمُ Swali: Inasemwa hakika sahaba wema wamemwona mtume bayana kisha wakamwamini na kumsadiki, ama sisi tumemwamini bila ya kumwona, kwa hiyo imani yetu ni yenye nguvu zaidi kuliko imani yao, ukiachilia mbali kuwa kuna mapokezi yanayotilia nguvu rai tunayoishika!! Jibu: Hakika sahaba wema - (r.a) - wamesimama mbele ya mirengo yote ya kifikira ulimwengu mzima na ambayo ilikuwa inashambulia hakika za Uislamu na kuzizuia. Wakaamini imani iliyojikita ya kweli ya ikhlasi pamoja na kuwa wao hawakuona kutoka kwa Mtume (s.a.w) bado isipokuwa dhahiri ya sura yake ya kibinadamu, bali walimwamini - mara nyingine - bila ya kuona muujiza kutoka kwake, na ikawa imani yao katika kujikita na umadhubuti ni ambayo haitetereshwi na fikira zote hizo zinazofanya kazi zenye kupingana na Uislamu, bali hazikuathiri kwa utata au wasiwasi japo kidogo. Ama nyinyi hamkuiona sura yake ya dhahiri na haiba yake ya kibinadamu ambayo ni sawa na kokwa ya mti wa Tuba wa Unabii, hakika fikira za ulimwengu wa Kiislamu zinakaza imani yenu na kuisaidia na kuitia nguvu, ukiachilia mbali kwamba nyinyi mnaona – kwa jicho la akili – haiba ya mtume mtukufu ya kimaanawy (s.a.w) yenye kunawirishwa kwa nuru ya Uislamu na hakika za Qur’an tukufu, haiba hiyo yenye heshima kwa maelfu ya miujiza yake iliyo thabiti. Italinganishwa imani yenu hii na imani yao kubwa?. Basi iko wapi imani yenu ambayo inaporomoka katika nyavu ya utata kwa maneno tu anayatoa mwanafalsafa wa kimaada wa Ulaya, na imani yao ambayo ilikuwa kama jabali imara halitetereki mbele ya vimbunga ambavyo vinavyochokozwa na watu wote wa ukafiri na kukana Mungu, Wayahudi na Wanasara na wenye hekima? Basi ewe mwenye kudai! Iko wapi imani yako iliyoshuka ambayo yaweza isiwe na nguvu kutekeleza faradhi kwa namna yake na umadhubuti na nguvu ya imani yao na ukubwa wa uchaji wao na wema wao ambao umefika katika ngazi ya Ihsani? Ama yaliyo kuja katika hadithi tukufu ambayo maana yake ni hakika ambao hawakuniona mimi na wameniamini wao ni bora kuliko nyinyi. Basi hiyo inahusu fadhila mahususi, na hii ni kuwahusu baadhi ya watu. Wakati ambapo somo letu hili ni katika fadhila za jumla na yanayorudi katika wingi wa hali zote. Swali la Pili: Wanasema Hakika mawalii wema na wenye ukamilifu wameiacha dunia na kujitenga na vilivyomo, kwa makusudio ya yaliyokuja katika hadithi tukufu: (Kupenda dunia ni kichwa cha kila kosa), wakati ambapo sahaba wema wamechukua mambo ya dunia na kuyaelekea na hawakuyaacha, bali baadhi yao waliwatangulia watu wa Ustaarabu katika kuchukua kwao mahitaji ya kidunia. Basi unasemaje: Hakika sahaba mdogo kabisa katika mifano ya hawa ni kama walii mkubwa katika mawalii wa Allah walio wema ? Jibu: Hakika tumethibitisha uthibitisho wa kukinaisha katika kituo cha pili na cha tatu kutoka katika neno la thelathini na mbili: Hakika dunia ina pande tatu: Basi kudhihirisha mahaba katika sura za dunia zenye kuangalia majina mazuri na Akhera sio upungufu katika utumishi, bali hilo ni sifa ya ukamilifu wa mwanadamu na hadhi ya imani yake, kwani kila mwanadamu anapojitahidi katika mahaba yake kwa sura hizo mbili huvuna salafu mengi katika ibada na zaidi katika kumtambua Allah (s.w). Na kutoka hapa dunia ya sahaba wema ilikuwa imeelekea katika sura hizo mbili, wakaihesabu ni shamba la Akhera na wakalima mema na wakavuna matunda yaliyonona ya thawabu nyingi na ujira mkubwa, na wakazingatia dunia na vilivyomo kana kwamba ni vioo vinaakisi nuru za udhihirisho wa majina mazuri, wakazingatia katika hayo na wakafikiri katika pande zake kwa pupa na shauku, wakajikurubisha zaidi kwa Allah (s.w), na katika wakati huohuo waliacha sura ya tatu ya dunia nayo ni sura yake inayotoweka inayoangalia matamanio ya mwanadamu na matashi ya nafsi yake. Swali la Tatu: Hakika ya njia ya za kisufi ni njia za kufika katika hakika, na mashuhuri na ya hadhi ya juu zaidi ni twarika ya Nakshabandi ambayo inahesabiwa kuwa ni barabara kubwa, baadhi ya Makutubu wake wamefupisha kanuni zake kama hivi: دَر۟ طَرٖيقِ نَق۟شِبَن۟دٖى لَازِم۟ اٰمَد۟ چَار۟ تَر۟ك۟ : تَر۟كِ دُن۟يَا تَر۟كِ عُق۟بٰى تَر۟كِ هَس۟تٖى تَر۟كِ تَر۟ك۟ yaani: Inalazimu katika njia ya Nakshabandi kuacha mambo manne: Kuacha dunia kwa kutoifanya ndio mlengwa kwa dhati yake, kuacha Akhera kwa hesabu ya nafsi, kuacha nafsi yaani kuisahau na kuacha kuacha. Yaani: Usifikirie kuacha huku, ili usije kuangukia katika ujubu (Kuistaajabikia nafsi yako) na fahari. Kwa maana kwamba kumtambua Allah na makamilifu ya kibinadamu ya hakika yanapatikana katika kuacha kisichokuwa yeye (s.w). Jibu: Mwanadamu angekuwa ni moyo tu? basi ingekuwa juu yake aache kisichokuwa yeye (s.w), bali aache hata majina na sifa, na moyo wake ufungamane na dhati yake (s.w). Lakini mwanadamu ana vipole vingi kama moyo, miongoni mwa hivyo ni akili, roho na siri, kila kipole katika hivyo kimekalifishwa jukumu na kimeamrishwa kutekeleza kazi maalum kwake. Basi mkamilifu ni – kama sahaba wema – anapeleka vyote hivyo katika makusudio yake ya msingi nayo ni kumwabudu Allah (s.w). Basi moyo kama kiongozi unapeleka kila kipole na kukielekeza upande wa hakika kwa njia ya utumishi wake mahususi. Kwa hapo wingi sana unakwenda katika vipole vikiwa ni majeshi katika misafara mikubwa na katika medani pana kunjufu, kama ilivyo kwa sahaba wema (r.a). Na kama si hivyo moyo kuacha askari wake na kwenda peke yake kujiokoa nafsi yake, si katika fahari na kuwa na enzi, bali ni matokeo ya kudharurika na si vingine. Swali la Nne: Kudai ubora mbele ya sahaba wema kunatokea wapi? Na ni nani hawa wanaoibua madai haya? Na kwa nini yanaibuliwa maswala haya wakati huu ? na kunatokea wapi kudai kufikia Mujitahidina wakubwa? Jibu: Ambao wanasema masuala haya ni sehemu mbili: Sehemu Kati Yao: Wameziona baadhi ya Hadithi tukufu na walizieneza ili kuchochea shauku kwa wacha Mungu na watu wema katika wakati huu na kuwapendezesha katika dini. Basi hawa ni watu wa dini na elimu, na ni wenye ikhlasi. Na hatuna cha kueleza juu yao, nao ni wachache na wanazinduka kwa haraka. Ama Sehemu Nyingine: Wao ni watu wamepata ghururi sana, na wenye kustaajabia nafsi zao ajabu iliyoje, wanataka kueneza kujivua kwao kutoka katika madhehebu ya kifiqhi chini ya kujidai kuwa wao wako katika ngazi ya Mujitahidina wakubwa, bali wanajaribu kupitisha kukana kwao na kujivua kwao kutoka kwenye dini kwa kudai kwamba wao wapo katika ngazi ya sahaba wema, basi wapotevu hawa wameanguka: Kwanza: Katika shimo la usafihi hata wamekuwa wenye kuzoea hilo, na hawawezi kuacha walichokizoea, na kutimiza lazima za sharia ambazo zinawazuia na usafihi. Basi utamwona mmoja wao huipa sababu nafsi yake kwa kusema: (Hakika ya masuala haya hakika ni maswala ya kijitihada, na madhehebu ya kifiqhi ni yenye kutofautiana katika masuala kama haya, nao ni marijali wamejitahidi na sisi vilevile ni marijali mfano wao, tunaweza kujitahidi mithili yao, na huenda wanakosea mithili yetu, na kwa hiyo tunatekeleza ibada kwa namna ambayo inatupendeza sisi, yaani si wenye kulazimika kuwafuata!!). Basi hawa walioharibikiwa wanafungua kifungo cha kufuata madhehebu mbali na nafsi zao kwa ushawishi huu wa kishetani. Basi ushawishi wa chini ulioje huo na sababu rahisi iliyoje hiyo! Na tumethibitisha hilo katika Risala ya (Ijtihad). Pili: Walipoona kuwa ushawishi wao haukamilishi vikuku vyake katika mpaka wa kuwakabili Mujitahidina walianza kuwakabili masahaba wema (r.a) ambapo hakika Mujitahidina wanabeba nadharia za kidini pekee, na hawa wapotevu wanakusudia kuvunja mambo ya dharura za kidini na kuyageuza, basi lau wangesema: Sisi ni bora kuliko Mujitahidina kadhia yao isingekwisha, ambapo medani ya Mujitahidina ni kutazama katika masuala ya kimatawi, na sio nassi za kisharia, kwa hiyo unawaona na hali ya kuwa wamejivua kutokana na madhehebu wanaanza kuwagusa sahaba wema ambao wao ni wachukuzi wa mambo ya dharura ya kidini. Lakini wapi na wapi! basi sio mfano wa hawa wanyama ambao wamo katika sura ya mwanadamu, bali hata mwanadamu wa hakika, bali walio kamili miongoni mwao nao ni wakubwa wa mawalii wema, hawawezi kuvuna madai ya kufaana pamoja na sahaba mdogo sana mtukufu. Kama tulivyo thibitisha hilo katika Risala ya Ijtihad. اَللّٰهُمَّ صَلِّ وَ سَلِّم۟ عَلٰى رَسُولِكَ الَّذٖى قَالَ : لَاتَسُبُّوا اَص۟حَابٖى لَو۟ اَن۟فَقَ اَحَدُكُم۟ مِث۟لَ اُحُدٍ ذَهَبًا مَا بَلَغَ نِص۟فَ مُدٍّ مِن۟ اَص۟حَابٖى Ambaye amesema: (Msiwatukane sahaba wangu msiwatukane sahaba wangu, lau mmoja wenu angetoa dhahabu mfano wa Uhud asingefikia kibaba cha mmoja wao wala nusu yake) صَدَقَ رَسُولُ اللّٰهِ سُب۟حَانَكَ لَا عِل۟مَ لَنَٓا اِلَّا مَا عَلَّم۟تَنَٓا اِنَّكَ اَن۟تَ ال۟عَلٖيمُ ال۟حَكٖيمُ

§11

Hakika ya usuhuba wa Unabii ni dawa kubwa, ina taathira ya kufurutu ada. Katika mambo yanayowafanya ambao wanajitukuza kwa usuhuba huo wa dakika moja, wanapata kutokana na nuru za hakika kiasi asichokipata ambaye anatumia miaka katika umri wake katika mwenendo na maadili, na hii ni kuwa katika Usuhuba wa kinabii kuna kupokea rangi ya uhakika , na kuakisi kwa nuru zake, ambapo mtu anaweza kwa kuakisi hiyo nuru tukufu akapanda katika ngazi za juu na daraja zilizoinuka, na kufaulu ufuasi na kujinasibisha kwa makamo ya juu mno. Mfano wake katika hili ni mfano wa mtumishi wa mfalme, ambaye anaweza kufika katika maeneo ya juu wasioweza kuyafikia viongozi wa mfalme na maamiri wake. Na kutokana na hili tunaona kwamba walii mkubwa kabisa katika mawalii wema wa Allah hawezi kupanda hadi ngazi ya sahaba mwema wa mtume mtukufu (s.a.w), bali hata wakijitukuza mawalii wema mara nyingi kwa usuhuba wa mtume (s.a.w), katika hali ya kuwa macho, kama Jalalu Ad-diin As-Suyuty – mathalani - na waliokirimiwa kukutana naye katika ulimwengu huu, hawafiki vilevile daraja ya sahaba kwa sababu usuhuba wa sahaba wema wa mtume (s.a.w), ulikuwa kwa nuru ya unabii, ambapo walikuwa wakisuhubiana naye hali akiwa ni nabii rasuli. Ama mawalii wema hakika kumwona kwao yeye, ni baada ya kufariki kwake, yaani baada ya kukatika kwa wahyi, huo ni usuhuba kwa nuru ya uwalii, yaani kutokea na kudhihiri kwa mtume (s.a.w) kwa mtazamo wao hakika ni kwa upande wa uwalii wa Muhammad, na sio kwa mazingatio ya unabii. Basi maadam jambo liko hivi, basi hapana budi suhuba hizi mbili zitofautiane kwa kiasi cha hadhi ya juu ya daraja ya unabii na kunyanyuka kwake juu ya cheo cha uwalii. Na ili iwe wazi taathira ya kufurutu ada na nuru kubwa, iliyopo katika usuhuba wa kinabii. inatosha kuzingatia yafuatayo: Wakati ambapo Bedui mwenye moyo mgumu anamzika binti wake kwa mkono wake, tahamaki anavuna kwa kuhudhuria kwake baraza ya Mtume (s.a.w), na kutokana na kusuhubiana naye saa katika wakati, anavuna upole wa moyo na ukunjufu wa kifua na uangavu wa roho kiasi kinacho mfanya anajiepusha kumuua sisimizi mdogo. Na mwingine hajui Sharia za ustaarabu na Elimu zake, anahudhuria baraza ya mtume mtukufu (s.a.w), anageuka kuwa mwalimu wa mataifa yaliyoendelea zaidi yaliyostaarabika kama India na china - na anatawala kati yao kwa uadilifu dhahiri, na anakuwa kwao ni mfano wa juu na ruwaza njema.

§12

Hakika tumethibitisha katika risala ya Ijtihad, kuwa sahaba wema wapo katika kilele cha ukamilifu wa kibinadamu, ambapo mageuzi makubwa ambayo yameletwa na Uislamu katika mapito ya maisha wakati huo, sawa katika jamii au kwa mtu binafsi, yamedhihirisha uzuri wa heri na haki na kuonesha umaridadi wake ulio wazi, na umefichua uovu wa shari na batili na umebainisha kuchukiza na ubaya wake, hata vikawa wazi vyote haki na batili na ukweli na uongo kwa uwazi timamu, mtu anakaribia kuugusa ugusaji wa mkono, na yakatanuka masafa kati ya heri na shari na baina ya ukweli na uongo, kiasi cha baina ya imani na ukafiri bali kiasi cha baina ya pepo na moto. Kwa hiyo sahaba wema (r.a) ambao wamepewa umbo salama na hisia za hali ya juu, nao ni wenye shauku kubwa na mambo ya juu na tabia njema walimwangalia kwa makini yule ambaye amekwea kilele cha juu ya juu ya kamilifu na mlinganiaji wa heri na ukweli na haki, bali yeye ni mfano ulio kamili zaidi na kielelezo kilichotimia zaidi, huyo ni bwana Mtume mtukufu (s.a.w) kipenzi cha Bwana Mlezi wa Ulimwengu Muhammad, wakatoa kila ambacho Allah (s.a.w) amewatunuku katika nguvu kujikusanya chini ya bendera yake (s.a.w), kwa muktadha wa tabia yao takasifu na umbo lao safi, na hakukuonekana kwao kuyumba kokote kwa maelezo ya batili ya Musailamatul Kaddhabu ambaye ni mfano wa uongo na shari na batili na uzushi. Na ili kuweka wazi jambo hili tunaleta mfano huu: Mara nyingine huoneshwa katika soko la ustaarabu wa wanadamu na maonesho ya maisha ya kijamii, vitu ambavyo vina baadhi ya athari mbaya za kutisha na matokeo ya shari mabaya kiasi kilichomo katika sumu kali kwa jamii. Basi kwa kila ambaye ana maumbile salama anavikimbia vikali na anaviepuka wala havikaribii. Na kadhalika huoneshwa vitu vingine na bidhaa za kimaanawy kwenye soko hilohilo, vina matokeo mazuri na athari njema ambayo hukusanya macho kuvitazama, kana kwamba ni dawa yenye kuponya maradhi ya kijamii, kwa ajili hiyo huziendea wenye maumbile ya heri na wema. Na kama hivi, basi katika zama za mafanikio za Mtume (s.a.w) na bora ya karne kwa hali zote, yalioneshwa katika soko la maisha ya kijamii mambo. Basi ni dhahiri kabisa sahaba wema kuendea ukweli, heri na haki kutokana na umbo safi wanalo miliki na tabia za hadhi ya juu, na ni dhahiri kabisa vilevile kukimbia na kujiepusha na kila ambalo lina matokeo mabaya na uovu wa dunia na Akhera kama uongo, shari na ukafiri, wakaizunguka bendera ya mtume (s.a.w) na wakajiepusha na maneno ya kipuuzi ya Musailamat al Kaddhaab ambaye anawakilisha uongo, shari na batili. Pamoja na kuwa mambo yamegeuka kidogo kidogo na kwa kupita kwa muda hayakubaki katika hali yake kama yalivyokuwa katika karne za heri, yakafinyika masafa baina ya uongo na ukweli kidogo kidogo kila tunapokaribia katika enzi zetu za sasa hadi vimekuwa viwili hivyo vyenye kufuatana vyenye kushikamana katika enzi za sasa, umekuwa ukweli na uongo vinaoneshwa kwa pamoja katika maonesho mamoja, na vinatolewa pamoja kutoka katika chanzo kimoja, basi tabia za kijamii zimeharibika na kuvurugika vipimo vyake. Na propaganda za kisiasa zimezidisha kuficha ubaya wa uongo wenye kutisha na kufunika uzuri wa ukweli ulio dhahiri. Je kuna yeyote mwenye nguvu ya ujasiri katika enzi kama hizi na kudai: Naweza kukaribia ngazi za hao watukufu wakubwa ambao wamefikia katika yakini na Ucha Mungu na uadilifu na ukweli na kujitolea nafsi na kilicho ghali katika njia ya haki kiasi asichofikia yeyote, seuze kuwashinda? Nitaeleza hali imenipitia inafafanua sehemu ya suala hili: Limepita swali moyoni mwangu siku moja nalo: Kwa nini watu mfano kama Muhyi Ad-diin ibn Araby hawafikii ngazi ya sahaba wema? Kisha nikaona wakati wa kusema kwangu katika sijida ndani ya swala: ( سبحان ربي الأعلى ) hakika kitu katika hakika za wazi ya maana ya neno hili zuri imefunuka kwangu, si semi yote, bali yamefunuka kiasi katika maana hayo. Nikasema moyoni mwangu: Laiti ningepata swala kamili yanafunguka kwangu katika maana yake kile kilichofunuka katika maana ya neno hili kwani ni bora kuliko ibada ya mwaka mmoja kamili katika Sunna Kisha nikatambua mwishoni mwa swala kwamba wazo hilo na hali ile ilikuwa ni jibu kwa swali langu, na maelekezo ya kuwa ni muhali mmojawapo katika watu kuifikia daraja ya sahaba wema katika ibada, hii ni kwa kuwa mabadiliko ya kijamii makubwa ambayo Qur’an imeyaleta kwa nuru zake zenye kuangaza yamepambanua dhidi baadhi yake kuwa mbali na baadhi nyingine, basi shari na viambata vyake vyote na giza lake vimekuwa katika kukabiliana na heri na makamilifu pamoja na nuru zake zote na matokeo yake. Basi katika hali hii inayochochea kufunguka kwa hisia za heri na shari kutoka katika vidhibiti vyake, zimezinduka kwa watu wa heri hisia zake, ikawa kila dhikiri na tasbihi na tahmidi inafidisha kwao maana yake kamili na kuyaelezea kwa maelezo maridadi mazuri. Hisia zao zenye shauku na vipawa vipole vyao vitakatifu bali hata mawazo yao na siri yao zikachukua kinywaji cha maana ya hadhi ya juu mengi ya hizo dhikiri uchukuaji safi ulio macho kulingana na vionjo vyao laini. Na kwa msingi wa hekima hii, hakika sahaba wema ambao walikuwa wanamiliki hisia kali mno yenye shauku na milango ya fahamu yenye kuzinduka na vipole vilivyo macho, wanapotaja hayo maneno yenye baraka yenye kukusanya nuru za imani, tasbihi na tahmidi wanahisi kwa maana yake yote na wanachukua fungu lao humo kwa vipole vyao yote vitakasifu. Licha ya kuwa mambo hayajabaki katika hali hiyo maridadi na nzuri na umakini, yamebadilika kidogo kidogo kwa kupita kwa wakati hadi vipole vikafunikwa katika usingizi mzito, na hisia zimeghafilika na milango ya fahamu na zimeachana na hakika, vizazi vijavyo vikakosa kidogo kidogo uwezo wao katika kuonja uzuri wa maneno yale mazuri na kupata ladha na utamu wake na uzuri wake. Ikawa kwao kama matunda yaliyokosa uzuri wake na kupendeza kwake, hata kama vile yamekauka na kuwa hayawabebei tena isipokuwa ni kiasi kidogo tu cha uzuri, haupatikani isipokuwa baada ya kufanya kazi kwa akili na kutafakari kwa kina, na kutoa juhudi na kutumia nguvu. Kwa hiyo basi sahaba mtukufu ambaye anapata makamo na fadhila katika dakika arobaini mwingine hayapati isipokuwa ndani ya siku arobaini, bali katika miaka arobaini na hii ni kwa fadhila ya usuhuba wa unabii Mtukufu.

Private reading note

This note stays on this device and is never uploaded to a server.

Up to 1,200 characters