Linahusu Kubakia kwa Roho, Malaika na Ufufuo اَعُوذُ بِاللّٰهِ مِنَ الشَّي۟طَانِ الرَّجٖيمِ بِسْمِ اللّٰهِ الرَّحْمٰنِ الرَّحِيمِ تَنَزَّلُ ال۟مَلٰٓئِكَةُ وَالرُّوحُ فٖيهَا بِاِذ۟نِ رَبِّهِم۟ قُلِ الرُّوحُ مِن۟ اَم۟رِ رَبّٖى (Kituo hiki kina Makusudio Mawili ya Msingi pamoja na Utangulizi)
Source text is preserved. When a suitable model is available, translation is displayed separately.
Sözler
The Twenty-Ninth Word
Ni sahihi kusema kuwa uwepo wa Malaika na ulimwengu wa kiroho vimethibiti kama kuthibiti kwa uwepo wa mwanadamu na mnyama. Kama tulivyobainisha katika ngazi ya kwanza ya “Neno la Kumi na Tano”: Kuwa ukweli unalazimu bila ya shaka yoyote, na hekima inahitajia kwa yakini, mbinguni - kama ilivyo ardhini kuwepo na wakazi. Na lazima wawe ni wenye hisia, na ni wenye kuendana nayo kikamilifu. Na katika istilahi ya kidini, hao wakazi ambao wanatokana na jinsi tofauti wanaitwa “Malaika” na “viumbe vya kiroho”. Naam, hakika ukweli unalazimu hivi… Pamoja na udogo wa tufe la ardhi yetu ukilinganisha na mbingu, hakika kujaa kwake viumbe vyenye hisia, baina ya wakati na mwengine, na kutoweka kwao na kuipamba kwa wengine wapya, inaashiria bali inatangaza bayana: Kuwa mbingu zenye buruji madhubuti kana kwamba ni makasri yaliyopambwa, lazima zitakuwa zimejaa pia, viumbe wenye uhai na wenye utambuzi, ambao ni nuru ya uwepo, na wenye hisia ambao ni mwanga wa vyenye uhai. Na kuwa viumbe hivyo - kama wanadamu na majini - wao pia ni wenye kushuhudia kasri la ulimwengu huu mkubwa… Na wenye kusoma kitabu cha ulimwengu huu… Na walinganiaji waelekezi kwa ufalme wa kiungu wa Bwana Mlezi… Na wanaleta kwa ibada yao ya jumla na yenye kuenea tasbihi za viumbe na nyiradi za vilivyopo vikubwavikubwa. Naam, hakika uwepo wa aina tofauti za viumbe hivi unajuulisha uwepo wa Malaika. Kwa sababu kuwapamba viumbe visivyohesabika kwa ufundi wa kina na ulio mzuri, na mazuri yenye maana na nakshi zenye hekima, kunahitajia kiakili mitazamo ya wenye kufikiri na wenye kupendezwa na wenye kuthamini… yaani inalazimu uwepo wao. Naam, kama ambavyo uzuri unahitaji mwenye kuupenda… na chakula hupewa mwenye njaa… basi lazima chakula cha roho na cha nyoyo katika ufundi huu wa kiungu ulio mzuri na wa kupendeza kijulishe juu ya uwepo wa Malaika na ulimwengu wa kiroho na kuwaelekea. Na ilivyokuwa mapambo haya hayana mwisho katika ulimwengu yanahitaji mazingatio na ibada visivyokuwa na mpaka. Na kuwa wanadamu na majini hawawezi kuufanya wadhifa huu usiokuwa na mwisho isipokuwa kiasi kidogo sana - moja katika milioni. Kutokana na mtazamo huu wa hekima, na kutokana na uja huu mpana… ni lazima nyadhifa hizi zisizokuwa na mwisho na ibada anuai ziwe za aina zisizokuwa na mwisho pia za Malaika na aina za “viumbe” vya kiroho zisizokuwa na mpaka, ili wauimarishe kwa safu zao zilizoshikana na kuujaza msikiti huu mkubwa… ulimwengu huu. Naam, katika kila upande wa ulimwengu huu, na katika kila kitengo kuna “watumishi” katika tabaka la “Malaika na viumbe vya kiroho” wamepewa jukumu la kufanya ibada maalumu... Kwa kuegemea ishara za baadhi ya Hadithi tukufu za Mtume (s.a.w) kwa upande mmoja na kupata ilhamu ya hekima ya kupangika kwa ulimweng huu kwa upande mwengine, inafaa kusema: Hakika ya baadhi ya maumbo ya kimaada yenye kutembea kuanzia nyota na kuishia kwenye matone ya mvua, hayo ni majahazi na vipando vya baadhi ya Malaika. Wanayapanda kwa idhini ya kiungu, na wanashuhudia ulimwengu wa kushuhudia wakiogelea humo… Na wanaleta “tasbihi” za vipando hivyo... Na kwa kuwa mashahidi “roho zao zimo ndani ya tumbo la ndege wa kijani zikitembetembea Peponi”, kama ilivyokuja katika Hadithi tukufu ya Mtume (s.a.w.). Hivyo inafaa kusema: Kuanzia kilichoashiriwa na Hadithi tukufu kuanzia “ndege wa kijani” hadi nyuki miongoni mwa viwiliwili hai, ni ndege wa aina za roho. Vinaingia kwenye miili ya viumbe hai hivyo kwa amri ya Allah Al-Haqq na kushuhudia ulimwengu wa kimaada kwa viungo vyake vya hisia kama macho na masikio, na kutazama miujiza ya ajabu ya kimaumbile humo. Na kwa hivyo wanatekeleza tasbihati zake maalumo… Na namna hii, kama ukweli ulivyolazimu uwepo wa Malaika na viumbe vya kiroho, vile vile hekima inalazimu: Kwa sababu Muumba Mwenye hekima ambaye anaumba kwa kuendelea na kwa ufanisi mkubwa maisha mazuri yenye utambuzi wenye nuru, kutokana na udongo huu mwingi juu ya udogo wa uhusiano wake na roho, na kutokana na maji machafu katika sehemu ya kuhusiana kwake na nuru ya maisha. Lazima awe pia na viumbe wengi sana wenye hisia, walioumbwa kutokana na bahari ya nuru, na hata kutokana na bahari ya giza, na kutokana na hewa na umeme, na baki ya maada nyepesi ambazo ni zenye kufaa zaidi kwa roho na zenye kuendana na maisha na zenye kuvikaribia.
“Kuamini Malaika ni Nguzo Miongoni mwa Nguzo za Imani” Katika kusudio hili kuna nukta nne za msingi
Hakika ukamilifu wa uwepo upo pamoja na uhai, bali hakika ya uwepo wa kweli wa uwepo upo katika uhai. Hivyo uhai ni nuru ya uwepo, na hisia ni mwanga wa uhai… Na uhai ni kichwa cha kila kitu na msingi wake… Nao ndio unaofanya kila kitu kiwe ni miliki ya kila kiumbe hai. Unakifanya kitu kimoja hai kiwe sawa na mmiliki wa vitu vyote. Kwa sababu ya uhai, kitu chenye uhai kinaweza kusema: “Vitu hivi ni vya kwangu, dunia ni makazi yangu, na viumbe vyote ni ufalme aliyonipa Mmiliki wangu”… Kama ambavyo mwanga ni sababu ya kuona vitu na ni sababu ya kudhihiri kwa rangi - kwa kauli – vilevile uhai ni wenye kudhihirisha vilivyopo na ni sababu ya hivyo vilivyopo kuonekana, na ni sababu ya kupatikana aina tofauti tofauti… Nao ndio unaofanya sehemu moja kati ya mbili kuwa sawa na kitu kamili na cha jumla, na ni sababu ya kuviweka vitu vya kiujumla katika sehemu, na ni sababu ya makamilifu yote ya uwepo; kama kushirikisha na kuunganisha vitu vingi na kuvifanya ni kitu kimoja na udhihirisho wa roho moja… Hadi kwamba uhai ni aina ya udhihirisho wa umoja katika matabaka ya wingi wa viumbe. Basi uhai ni kioo cha umoja wa pekee katika wingi… Na sasa tuweke wazi: Tazama kiwiliwili cha kimaada hata ukiwa ni mlima mrefu basi ni wa ajabu… ni yatima… ni mpweke… kwani uhusiano wake unafungika na mahali ulioko tu, na vitu vinavyoungana nao tu. Na yaliyopo kwa viumbe wengine hayapo kwake, na hiyo ni kwa sababu hauna “uhai” mpaka uungane navyo, wala “hisia” mpaka ufungamane navyo. Kisha tazama kwenye kiwiliwili kidogo cha kiumbe hai kama nyuki kwa mfano, katika wakati ambao anaingiwa na “uhai” basi huwa anatengeneza mkataba wa kibiashara na mafungamano na viumbe na vilivyopo vyote, na hasa pamoja na mimea ya ardhini na maua yake ambapo inawezekana kusema: “Hakika ardhi yote ni bustani na sehemu yangu ya biashara”… Ukiachana na hisia maarufu za dhahiri na za ndani kwa vyenye uhai, kuna misukumo ya kimaumbile mengine isiyokuwa maarufu kama hisia zenye kusukuma zenye kutia shauku zinazompa nyuki fursa ya kutenda na uwezekano wa kuhisi kuwa pamoja na kujumuika na kubadilishana na aina nyingi zaidi za vilivyopo katika dunia. Na ikiwa uhai unaonesha taathira yake namna hii kwa kiumbe hai mdogo, basi lazima kila unapopanda ngazi ya juu na kutukuka ambayo ni ngazi ya uwanadamu, hakika taathira yake inaenea na kuwa kubwa na kupata nuru, ambapo mwanadamu huyu anatembea kwa akili yake na hisia yake – ambayo ni mwanga wa uhai – katika limwengu za juu na za kiroho na za kimaada kama anavyozunguka katika vyumba vya nyumba yake. Na hii ina maana kuwa kama anavyosafiri kiumbe hai huyo mwenye hisia kwenye limwengu hizo za kimaanawy, basi limwengu hizo zinakuja na kuwa ni wageni wa kioo cha roho yake kwa kujitengeneza sura na kujimithilisha humo. Na uhai wenyewe ni dalili ya wazi mno ya upweke wa Allah (s.w.) na mawanda mapana sana ya neema yake kubwa, na udhihirisho laini zaidi kati ya madhihirisho ya rehema yake, na ni nakshi ya kina zaidi kati ya nakshi za ufundi wake safi uliojificha. Naam, hakika umejificha na wa kina sana; kwani kuzinduka kwa “fundo la uhai” yaani kufunguka kwake na kukua kwake katika mbegu – ambako ni ngazi ya kwanza ya uhai katika mimea ambako kunawakilisha aina ya chini zaidi ya uhai – umebaki umesitiriwa kutokana na mtazamo wa wanaadamu tokea zama za Adamu (a.s.) pamoja na kudhihiri kwake sana, wingi wake na kuuzoea. Na hakika yake haijadhihiri kwa uwazi kwenye akili ya mwanadamu hadi sasa. Na uhai ni msafi ambapo sura zake mbili – mulku na malakuti – ni safi na angavu; kwani mkono wa uweza unasimamia kazi zake humo bila ya kuweka pazia la sababu, katika wakati ambapo umezifanya sababu za dhahiri kuwa ni pazia la utendaji wake katika baki ya mambo mingine. Ili iwe ni chanzo cha mambo duni na namna zisizo safi ambazo zinaenda kinyume na utukufu wa uweza kwa dhahiri. Muhtasari: Inafaa kusema: Kama hakuna uhai basi uwepo si uwepo, na hautofautiani na kutokuwepo. Hivyo uhai ni mwanga wa roho, na hisia ni nuru ya uhai. Na ilivyokuwa uhai na hisia vina umuhimu huu, na madamu tunashuhudia mpangilio huu uliofanywa vyema katika ulimwengu huu, na tunaona umakini huu na kutenda vyema kulikotimia, na kuendana kuliko kamilika ulimwenguni, na maadamu tufe la dunia yetu - ambayo ni kama atomu ukilinganisha na ulimwengu – imejaa wasiyohesabika miongoni mwa waliyo na roho, hisia na utambuzi, basi lazima iamuliwe kwa welevu wa kweli na ithibitishwe kwa yakini ya hakika kuwa pande za makasri haya ya mbinguni na buruji ndefu wanatembea humo wakazi miongoni mwa viumbe hai na wenye hisia kwa namna inayoendana nao. Kwani kama ambavyo samaki huishi katika maji, vilevile inawezekana kupatikana wakazi wa kinuru katika mwako wa jua ambao wanaoendana nalo. Kwa sababu moto hauiunguzi nuru bali inaikoka na kuidumisha. Na maadamu uweza wa kiungu unaumba viumbe hai na wenye roho wasio na idadi kutokana na maada za kawaida sana, bali kutokana na elementi nyingi, na maada nyingi nzito hubadilishwa kwa uhai kuwa ni maada laini kwa uangalizi mkubwa na ufundi. Na husambaza nuru ya uhai katika kila kitu kwa wingi. Na kuvipamba aghlabu ya vitu kwa mwanga wa hisia, basi hapana budi kuwa mweza huyo mwenye hekima hatopuuzia kwa uweza wake kamili na hekima yake iliyotimia, nuru na maada ya etha na mfano wa hivyo katika vimiminika laini na vilivyo karibu, bali zinazoendana na roho, na sio uhai. Melâikelerin ve ruhanîlerin kesretle vücudlarını kabul etmek ne derece hakikat ve bedihî ve makul olduğunu ve Kur’an’ın beyan ettiği gibi onları kabul etmeyen, ne derece hilaf-ı hakikat ve hilaf-ı hikmet bir hurafe, bir dalalet, bir hezeyan, bir divanelik olduğunu şu temsile bak, gör: İki adam; biri bedevî, vahşi; biri medeni, aklı başında olarak arkadaş olup İstanbul gibi haşmetli bir şehre gidiyorlar. O medeni muhteşem şehrin uzak bir köşesinde pis, perişan, küçük bir haneye, bir fabrikaya rast geliyorlar. Görüyorlar ki o hane; amele, sefil, miskin adamlarla doludur. Acib bir fabrika içinde çalışıyorlar. O hanenin etrafı da zîruh ve zîhayatlarla doludur. Fakat onların medar-ı taayyüşü ve hususi şerait-i hayatiyeleri vardır ki onların bir kısmı âkilü’n-nebattır, yalnız nebatat ile yaşıyorlar. Diğer bir kısmı âkilü’s-semektir, balıktan başka bir şey yemiyorlar. O iki adam, bu hali görüyorlar. Sonra bakıyorlar ki uzakta binler müzeyyen saraylar, âlî kasırlar görünüyor. O sarayların ortalarında geniş tezgâhlar ve vüs’atli meydanlar vardır. O iki adam, uzaklık sebebiyle veyahut göz zayıflığıyla veya o sarayın sekenelerinin gizlenmesi sebebiyle; o sarayın sekeneleri, o iki adama görünmüyorlar. Hem şu perişan hanedeki şerait-i hayatiye, o saraylarda bulunmuyor. O vahşi bedevî, hiç şehir görmemiş adam, bu esbaba binaen görünmediklerinden ve buradaki şerait-i hayat orada bulunmadığından der: “O saraylar sekenelerden hâlîdir, boştur, zîruh içinde yoktur.” der, vahşetin en ahmakça bir hezeyanını yapar. İkinci adam der ki: “Ey bedbaht! Şu hakir, küçük haneyi görüyorsun ki zîruh ile amelelerle doldurulmuş ve biri var ki bunları her vakit tazelendiriyor, istihdam ediyor. Bak, bu hane etrafında boş bir yer yoktur. Zîhayat ve zîruh ile doldurulmuştur. Acaba hiç mümkün müdür ki şu uzakta bize görünen şu muntazam şehrin, şu hikmetli tezyinatın, şu sanatlı sarayların onlara münasip âlî sekeneleri bulunmasın? Elbette o saraylar, umumen doludur ve onlarda yaşayanlara göre başka şerait-i hayatiyeleri var. Evet, ot yerine belki börek yerler; balık yerine baklava yiyebilirler. Uzaklık sebebiyle veyahut gözünün kabiliyetsizliği veya onların gizlenmekliği ile sana görünmemeleri, onların olmamalarına hiçbir vakit delil olamaz. Adem-i rü’yet, adem-i vücuda delâlet etmez. Görünmemek, olmamaya hüccet olamaz. İşte şu temsil gibi ecram-ı ulviye ve ecsam-ı seyyare içinde küre-i arzın hakaret ve kesafeti ile beraber bu kadar hadsiz zîruhların, zîşuurların vatanı olması ve en hasis ve en müteaffin cüzleri dahi birer menba-ı hayat kesilmesi, birer mahşer-i huveynat olması, bizzarure ve bilbedahe ve bi’t-tarîkı’l-evlâ ve bi’l-hadsi’s-sadık ve bi’l-yakîni’l-kat’î delâlet eder, şehadet eyler, ilan eder ki: Şu nihayetsiz feza-yı âlem ve şu muhteşem semavat, burçlarıyla, yıldızlarıyla zîşuur, zîhayat, zîruhlarla doludur. Nârdan, nurdan, ateşten, ışıktan, zulmetten, havadan, savttan, rayihadan, kelimattan, esîrden ve hattâ elektrikten ve sair seyyalat-ı latîfeden halk olunan o zîhayat ve o zîruhlara ve o zîşuurlara, şeriat-ı garra-yı Muhammediye aleyhissalâtü vesselâm, Kur’an-ı Mu’cizü’l-Beyan “Melâike ve cânn ve ruhaniyattır.” der, tesmiye eder. Melâikenin ise ecsamın muhtelif cinsleri gibi cinsleri muhteliftir. Evet, elbette bir katre yağmura müekkel olan melek, şemse müekkel meleğin cinsinden değildir. Cin ve ruhaniyat dahi onların da pek çok ecnas-ı muhtelifeleri vardır. Mwisho wa Nukta Hii ya Msingi Hakika imethibiti kwa majaribio kuwa maada sio msingi na asili ili uwepo ubaki ukitumikishwa kwa ajili ya maada hiyo na kuwa ni mfuasi wake, bali ni yenye kusimama kwa “maana”. Na maana hii ndio uhai… Ndio roho… Na kuona na kuzingatia pia vinatuonesha kuwa maada si yenye kutiiwa kiasi cha kila kitu kurejeshwa kwake, bali ni njia yenye kutii yenye kutumikia ili kukamilisha ukweli maalumu… Ukweli huu ndio uhai… Na msingi wake… ndio roho. Na ni wazi kuwa maada si yenye kuhukumu hata iombwe mlangoni pake, na kutakiwa au kusubiriwa kutoka kwake makamilifu na mifano bora, bali ni yenye kuhukumiwa inayotembea kwa mujibu wa msingi maalumu na kutenda kwa ishara ya msingi huo… Msingi huu ni uhai… Ni roho, ni hisia. Na dharura inahitajia pia, matendo na mifano kutofungamana na maada wala kujengwa kwa mujibu wake. Kwani hiyo sio kiini, wala asili, wala msingi, wala uthabiti uliyojikita. Bali ni ganda, ni jalada, ni kitu povu, ni picha iliyoandaliwa kupasuka, ni kuyayuka, na ni kuchanika. Hivi haishuhudiwi vipi kuwa wanyama wadogo ambao haiwezekani kuwaona kwa jicho pekee wanamiliki hisia kali na zenye nguvu hadi kwamba wanasikia minong’ono ya wanyama wenzao na kuona maada za riziki zao!! Hakika hili linatubainishia kwa uwazi kuwa maada kila inapokuwa ndogo basi huongezeka kuendana na alama za uhai na athari zake kwake, na nuru ya roho hushitadi ndani yake. Yaani maada kila inapokuwa ndogo na kuwa mbali na umaada wake ni kana kwamba inakaribia zaidi kwenye ulimwengu wa roho, na ulimwengu wa uhai, na ulimwengu wa hisia, basi nuru ya uhai na joto la roho vinadhihiri kwa nguvu zaidi… Je ni katika yumkini kudondoka tunachokiona katika matone ya uhai, hisia na roho na kuchuruzika hali ya kung’aa kutoka katika vifuniko vya maada, wala ulimwengu wa ndani uliyo chini ya stara ya maada hauwi wenye kujawa na wenye hisia na wenye roho? Na je ni katika yumkini kurejea kwenye maada na kuegemezwa kwake na kwenye harakati zake kila kilichomo kwenye ulimwengu wa kushuhudiwa miongoni mwa matone yasiyo na mpaka ya maana, roho na ukweli na chimbuko la ming’ao yake na matunda yake, na kuwa wazi kwa hayo pekee!? Sivyo hivyo tena sivyo… Bali mandhari hizi zisizo na mpaka zenye kutona, na kung’aa kwake kunatuonesha kuwa ulimwengu huu wa kushuhudiwa wa kimaada si chengine ila ni stara iliyonakishiwa iliyopambwa ikawekwa kwenye ulimwengu wa malakuti na roho.
Inasihi kusema kuwa kuna maafikiano yasiyowekwa wazi - pamoja na kutofautiana kwa maelezo - juu ya kuwepo ukweli wa malaika na kuthibiti kwa ulimwengu wa kiroho, baina ya watu wote wa akili na mapokeo, iwe wamejua au hawakujua… Hawakupinga “maana” ya malaika hata wafuasi wa Aristoteli miongoni mwa wanafalsafa Waishiraki ambao wamezama katika maada; kwani walieleza kuhusu “maana” ya malaika kwa kusema: “Kuna utambulisho uliyojitenga wa kiroho wa kila aina”. Na wengine katika Waishiraki walipolazimika kukubali maana ya malaika waliwaita kwa makosa: “Akili kumi na mabwana wa aina za viumbe”. Na katika yanayojulikana ni kuwa watu wa dini zote wanaamini kuwa kila aina miongoni mwa aina za vilivyopo ina malaika aliyewakilishwa kwao, anapata ilhamu kutoka katika wahyi wa kiungu na mwongozo wake. Basi wanawaita kwa majina: Malaika wa milima, Malaika wa bahari, Malaika wa mvua… Na hata wanamaada na wana Asili, ambao akili zao zimeporomokea machoni mwao, na waliojivua utu kimaanawy, waliyodondoka kwenye ngazi ya vitu, hawakuweza kukanusha “maana” ya malaika na ukweli wa roho. Wakaiita ile nguvu iliyopo katika sharia za maumbile jina la “nguvu yenye kutembea”. Huu ukawa ni usadikisho wa lazima kutoka kwao – japo kwa sura iliyopotoshwa – ya maana ya malaika. Basi ewe mwanadamu masikini mwenye kusitasita katika kukubali uwepo wa malaika na ulimwengu wa kiroho! Juu ya kitu gani unaegemea? Na kwa ukweli gani unajifaharisha? Hata ukabiliane na yale waliyoafikiana wote wenye akili, iwe wamejua au hawakujua, miongoni mwa kuthibiti maana na hakika ya uwepo wa malaika na kuthibiti ulimwengu wa kiroho? Maadamu uhai - kama tulivyothibitisha katika msingi wa kwanza – ni wenye kuonesha vilivyopo bali ni matokeo yake na muhtasari wake… Na hakika wenye akili wote wameafikiana bila ya kutoa ufafanuzi, ingawa wametofautiana katika maelezo, juu ya maana ya malaika… Na kuwa ardhi yetu hii ni imeamirishwa kwa hawa wenye uhai na wenye roho wote. Basi inawezekana vipi anga hii pana isiwe na wakaazi wake, na mbingu hizo za ajabu nzuri zisiwe na wakaazi wake?! Na wala isipite akilini mwako kuwa sheria na kanuni zilizo katika ulimwengu ni zenye kutosha kuwafanya viumbe viwe ni vyenye uhai… Kwa sababu sheria hizo na kanuni zenye kutawala ni amri za kimazingatio, na ni katiba za kufikirika, hazizingatiwi wala kuhesabika kuwa ni kitu asilani. Kama hakuna waja wa Allah wanaoitwa “malaika” wanaochukua kanuni hizi na kuzidhihirisha na kuzitekeleza, basi kanuni na sheria hizo hazilazimu uwepo wowote ule, wala hautajulikana utambulisho wake. Hivyo hizo sio ukweli wa nje katu, na hali ni kuwa uhai ni ukweli wa nje. Na jambo la kudhaniwa haliwezi kubebeshewa ukweli wa nje. Tunafanya muhtasari wa hili: Maadamu watu wa hekima, watu wa dini, watu wa hoja za kiakili na za mapokezi ni wenye kukubaliana bila ya kuweka wazi kuwa vilivyopo havipo tu katika ulimwengu huu wa kushuhudiwa pekee, na kuwa ulimwengu wa kushuhudiwa wa dhahiri na wa kushikika ambao haukaribii kuafikiana na kuishi kwa roho na kuundika kwake kuwa umepambika kwa idadi hii kubwa ya vyenye roho na viumbe. Hivyo uwepo hauwezi kuwa kwake pekee. Bali kuna tabaka nyingine nyingi za uwepo, ambapo ulimwengu wa kushuhudiwa kwa viumbe hivyo unakuwa ni pazia lililodariziwa. Na maadamu ulimwengu wa ghaibu na ulimwengu wa maana ni zenye kuendana na roho – kama kuendana kwa bahari na samaki – hapana budi kuwa zimejaa roho zenye kuendana nazo. Na ilivyokuwa mambo yote yameshuhudia juu ya uwepo wa maana ya malaika, hivyo hapana shaka kuwa sura nzuri zaidi ya uwepo wa malaika na hakika za kiroho, na hali bora na namna yake, kiasi kwamba akili salama zinazikubali na zinapendezwa nazo, basi bila ya shaka ni kile kilichochambuliwa na kubainishwa kwa uwazi na Qur’an tukufu. Basi Qur’an tukufu inawataja malaika kuwa ni: عِبَادٌ مُّكْرَمُونَ لَا يَعْصُونَ اللَّهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ Wao ni viwiliwili vya kinuru vilivyo vyepesi vinavyogawika katika aina tofauti. Naam, kama ilivyokuwa wanadamu ni umma wanaobeba na wanaotekeleza sharia ya kiungu inayokuja kutokana na sifa ya maneno, vilevile malaika ni umma mkubwa sana kiasi kwamba sehemu ya watendao kati yao wanabeba na kutekeleza sharia ya kimaumbile inayokuja kutokana na sifa ya “utashi”. Nao ni aina katika waja wa Allah wenye kutii amri za Mwenye kuathiri wa kweli ambaye ndiye uweza wenye kuumba na utashi wa kiungu kwa utii kamili. Mpaka wamejaalia kila nyota katika nyota za mbinguni zilizo juu kuwa kama vile msikiti na sehemu yao ya ibada.
Hakika suala la kuthibiti malaika na ulimwengu wa kiroho ni katika masuala yanayoendana na kanuni ya kimantiki: “Kwa kuthibiti kwa sehemu moja hufahamika kuthibiti kwa kitu chote. Yaani kwa mtu mmoja kumuona malaika, hujulikana uwepo wa aina yote; kwa sababu anayekanusha mmoja anawakanusha wote. Pindi mtu mmoja akiikubali aina hiyo, basi ni juu yake kuikubali aina yote. Hivyo zingatia: Hivi huoni na kusikia kuwa watu wa dini zote, katika zama zote, tokea zama za Bwana wetu Adam (a.s.) hadi leo hii, wameafikiana juu ya uwepo wa malaika na kuthibiti ulimwengu wa kiroho, na kwamba makundi ya wanadamu wamekubaliana juu ya uwezekano wa kuongea na malaika na kuwaona na kupokea kutoka kwao kama vile wanavyozungumza, kuonana na kusimuliana mapokezi baina yao. Basi je, inawezekana kutokea kwa maafikiano ya pamoja kama haya, na kudumu kwa itifaki hii, kwa namna hii ya mutawatir yenye kuendelea katika jambo la kiuwepo, chanya, ikiegemea kwa mashahidi, kama mmoja wa malaika hakushuhudiwa bayana na kwa dhahiri? Au haikujulikana kuwepo mtu au watu kati yao kwa sura ya kuona kiuhakika? Je haikuhisiwa kuwepo kwao kwa dhahiri na kwa kuona? Na je ni katika yumkini chanzo cha itikadi hii kuu kisiwe ni misingi ya lazima na mambo ya waziwazi? Na je ni katika yumkini kuendelea na kubaki kuwa ni dhana isiyo na ukweli katika imani zote za binaadamu na katikati ya mlundikano wa mageuzi ya kibinaadamu? Na je ni katika yumkini kuwa maafikiano haya makubwa ya watu wa dini, hayaegemei welevu wa kukinaisha na juu ya yakini ya kushuhudia? Na je ni katika yumkini kuwa welevu huu wa kukinaisha na yakini ya kushuhudia haviegemei kwenye kisichohesabika wala kudhibitika katika dalili na alama? Na kwamba dalili hizi haziegemei katika maono halisi? Na kuwa maono haya halisi hayaegemei katika misingi ya lazima isiyo na shaka wala utata? Na ilivyokuwa jambo liko hivyo, hakika misingi na nyaraka za imani ya watu wa kawaida katika watu wa dini ni misingi ya lazima, iliyotokana na tawatur ya kimaanawy inayotokana na kuona mambo ya kiroho na kuwaona malaika mara kwa mara. Basi hiyo ni misingi iliyothibiti kwa hakika. Na je ni katika yumkini au lenye kuingia akilini kuingia utata katika uwepo wa malaika na ulimwengu wa kiroho na kuwashuhudia ambako kumeelezwa na kushuhudiwa na manabii na mawalii wema kwa ushuhuda mutawatir na kwa nguvu ya maafikiano ya pamoja yasiyowekwa wazi. Nao ni majua ya uhai wa kijamii wa wanaadamu na nyota zake na miezi yake, na hasa kwamba wao ni “watu waliyobobea” katika saula hili; kwani ni katika yanayojulikana kuwa wawili katika watu waliyobobea wanakuwa na uzito zaidi kuliko maelfu ya wengineo. Nao pia ni “watu wa kuthibitisha” katika suala hili. Na ni katika yanayojulikana kuwa watu wawili wanaothibitisha pia wana uzito zaidi ya maelfu ya “watu wanaokanusha”. Na je ni katika yumkini kuingia utata wowote na hasa katika yale yaliyotajwa na Qur’an yenye hekima na ya muujiza ambayo inang’aa katika mbingu ya viumbe daima bila ya kupotea, hiyo ni jua la majua ya ulimwengu wa ukweli, na kwa alichokishuhudia na kukiona Nabii mtukufu (s.a.w.) na yeye ni jua la utume? Na ilivyokuwa kuthibiti uwepo wa kiumbe wa kiroho mmoja - katika wakati fulani – kunadhihirisha ukweli wa uwepo wa aina yake yote, na hili kwa hakika limetimia. Hapana budi kuwa sura bora yenye kuingia akilini na yenye kukubalika ya ukweli wa uwepo wao ni kama vile sharia tukufu ilivyochambua, na kuelezwa na Qur’an tukufu, na kushuhudiwa na mhusika wa miiraji (s.a.w.).
Tukitazama kwa makini katika vilivyopo ulimwenguni tutaona kuwa: “Mikusanyiko, kama vilivyo vipande vya sehemu, ina haiba ya kimaanawy, ambapo inazidhihirishia wadhifa wa jumla”. Kama lilivyo ua - mathalani – kwa kudhihirisha kwake ufundi wa kina ndani yake linafanya tasbihi kwa ulimi wa hali yake kwa majina ya muumba wake. Basi bustani ya ardhini yote pia ni sawa na ua hilo, ina wadhifa wa kitasbihi wa jumla katika upeo mkubwa wa mpangilio. Na kama ambavyo tunda linaeleza na kutangaza kwa mpangilio wake wa ajabu wenye kuratibika vyema kutokana na tasbihi zake, basi vile vile mti mrefu kwa ujumla wake, una ibada na wadhifa wa kimaumbile katika mpangilio timamu zaidi. Na kama ambavyo mti mrefu una tasbihi kwa kumhimidi Mola wake Mlezi kwa maneno ya majani yake, maua yake na matunda yake; hakika pande za mbingu pana zina tasbihi zake kwa muumba Mwenye hekima kwa maneno ya majua yake, nyota zake, na miezi yake; nazo zinamhimidi na kumtukuza Muumba wake Jalla Jalaluhu. Na namna hii kwa viumbe vya nje vyote – ingawa havina uhai wala hisia ya dhahiri – bali vina wajibu na tasbihi kwa kumhimidi Mola wake Mlezi katika ukomo wa kusisimua na uchangamfu. Malaika kwa vile wanawakilisha viumbe na kueleza tasbihi zao katika ulimwengu wa malakuti, basi viumbe hao kwa upande wao ni sawa na makazi na misikiti kwa malaika katika ulimwengu wa ufalme wa ardhini na kushuhudiwa. Na kwa hakika tumebainisha katika “Neno la Ishirini na Nne” katika tawi lake la nne kuwa Mmiliki wa kasri la ulimwengu huu mkubwa na Mtengenezaji wake Jalla Jalaaluh anatumia katika kujenga ufalme wake aina nne za wafanyakazi, wakitanguliwa na Malaika na viumbe vya kiroho. “Mimea na visivyo na uhai” vinafanya kazi zake bila ya kujua kusudio la Mtengenezaji Mwenye hekima, na bila ya kuchukua ujira kwa utumishi wake mkubwa. Lakini vinafanya hivyo kwa utawala wa anayejua kusudio la Mmiliki. Na “wanyama” wanafanya utumishi mkubwa wa jumla bila ya kujua pia, lakini kwa sehemu ya ujira. Na “mwanadamu” anatumiwa katika kazi zinazoafikiana na kile anachojua katika makusudio ya Mtengenezaji Mwenye utukufu kwa ujira wa aina mbili: Wa baadaye na wa sasa, pamoja na kuchukua sehemu ya nafsi yake pia katika kila kitu, na kuwachunga wafanyakazi wengine: Mimea na wanyama… Naam, maadamu kutumia aina hizi ni jambo lenye kushuhudiwa kwa macho, basi hapana budi kuwepo aina ya nne. Bali wao ni wa mbele katika safu za watumishi na wafanyakazi. Wao wanafanana na mwanadamu kwa upande mmoja, ambapo wanajua makusudio ya jumla ya Mtengenezaji Mwenye utukufu, basi wanamuabudu kwa harakati zao zenye kuafikiana na amri zake, lakini wanatofatiana na mwanadamu kwa upande mwingine. Nao ni kuwa wao wamekosa mahitaji ya nafsi na kuchukua ujira wa sehemu fulani, kwani wanatosheka na wanachokipata katika ladha, kionjo, ukamilifu na furaha kwa kutazamwa tu na (s.w.), na kwa kutokana na amri zake kwao, na kuwaelekea, na ukaribu wao kwake, na kujinasibisha kwao kwake. Basi wanafanya juhudi kwa ajili yake, na kwa jina lake, kwa yale matendo yanayowahusu kwa ikhlasi yote... Na hao ndiyo malaika. Basi nyadhifa za uja wao zinakuwa za aina nyingi kwa mujibu wa maumbile yao, na kwa mujibu wa aina za vilivyopo ulimwenguni; kwani ni kama ilivyo serikali ina maafisa tofauti kwa mujibu wa idara zake tofauti na anuai, vilevile hutofautiana tasbihati na nyadhifa za uja kwa kutofautiana kwa idara katika ufalme wa rububiyya. Mathalan: Sayyidina Mikail (a.s.) kwa amri ya Allah na kwa ajili yake, na kwa uweza wake na nguvu yake, ni kama msimamaizi mkuu – kama itafaa kueleza hivyo – kwa viumbe wote wa kiungu waliyowekwa katika shamba la ardhi. Yaani yeye ni raisi wa wote ambao ni sawa na mkulima katika malaika. Na Muumba Mwenye hekima Jalla Jalaaluh vilevile ana malaika mkuu aliyewakilishwa kusimamia kwa idhini yake, amri yake, nguvu yake na hekima yake uongozi wa wachungaji wote wa kimaanawy wa wanyama wote. Maadamu kila aliyekuwepo katika vilivyopo vya dhahiri ana malaika aliyewakilishwa, anayetekeleza kinachodhihirishwa na vilivyopo hivyo miongoni mwa nyadhifa za uja na tasbihi kwenye ulimwengu wa malakuti na kuviwasilisha kwa kujua kwenye hadhara takatifu ya kiungu. Hivyo hapana budi tufahamu kuwa kilichosimuliwa kutoka kwa mwenye kutoa habari na mkweli (s.a.w.) kuhusu malaika miongoni mwa sura ambazo ni taswira nzuri zaidi na karibu zaidi na akili na kwa namna sahihi yenye kunasibikiana na kuendana. Mathalan: Imepokelewa kuwa Mtume (s.a.w.) amesema: “Hakika Allah ana malaika wana vichwa arobaini – au arobaini elfu. Katika kila kichwa kuna midomo arobaini elfu, na katika kila mdomo kuna ndimi arobaini elfu zinafanya tasbihi arobaini elfu” au kama alivyosema... Basi ukweli wa Hadithi hii una maana, na una sura. Ama maana yake ni: Ibada ya malaika ipo katika upeo mkubwa wa mpangilio na ukamilifu. Nayo ipo katika ukomo wa upana na ujumla pia. Ama sura yake ni: Kuwa kuna baadhi ya vilivyopo vya viwiliwili vikubwa vinatekeleza nyadhifa za uja wao kwa vichwa arobaini elfu na kwa aina na mitindo arobaini elfu. Mbingu matahalan inafanya tasbihi kwa majua na nyota, na ardhi pia ingawa ni moja ya viumbe, kwani inatekeleza nyadhifa za uja wake na tasbihi zake kwa Mola wake Mlezi kwa vichwa laki moja, na katika kila kichwa kuna mamia ya maelfu ya midomo, na katika kila mdomo kuna mamia ya maelfu ya ndimi. Basi ili malaika aliyewakilishwa kusimamia tufe la ardhi adhihirishe maana hii kwenye ulimwengu wa malakuti, lazima huyo mwengine adhihiri kwa namna na sura hiyo. Hadi nimeona matawi yanayokaribia arobaini – yanayofanana na kichwa – kwa mti wa wastani katika miti ya mlozi, na kwa hiyo nikatazama moja ya matawi yake likawa lina matawi madogo mfano wa ndimi yanayokaribia arobaini. Na nikaona huko maua arobaini yamechanua kutoka moja ya ndimi hizo. Nikayatazama kwa makini na kwa hekima maua hayo, tahamaki katika kila ua kuna nyuzinyuzi zipatazo arobaini za kina zilizopangiliwa vyema na zenye rangi za ajabu na umakini wa kupendeza, ambapo kila uzi kati ya nyuzinyuzi hizo unadhihirisha dhihirisho katika madhihirisho ya majina ya Mtengenezaji mwenye utukufu na kutamkisha jina katika majina yake mazuri. Je ni katika yumkini kuwa mtengenezaji wa mlozi Mwenye utukufu, naye ni Mwenye hekima na Mwenye uzuri, ambaye ameubebesha mti huo usiyo na hisia nyadhifa zote hizo kisha asiuwekee malaika msimamizi, anayenasibiana nao, na kuwa sawa na roho kwake, na akafahamu maana ya uwepo wake, na akaieleza maana hiyo na kuitangaza kwa viumbe na kuinyanyua kwenye hadhara takatifu?. Ewe rafiki! Hakika tulichokibainisha mpaka sasa, kilikuwa ni utangulizi ili kiuhudhurishe moyo kukubali, na kuilazimu nafsi kujisalimisha, na kuiandaa akili kutii. Ikiwa umefahamu, na unataka kukutana kikweli na malaika, basi jiandae na jitakase kutokana na dhana potovu na duni. Mbele yako kuna ulimwengu wa Qur’an tukufu milango yake ipo wazi. Hakika ya Pepo ya Qur’an milango yake ipo wazi daima... Basi ingia... Na tazama sura nzuri zaidi ya malaika katika Firdausi ya Qur’an... Basi kila aya miongoni mwa aya za Tanzili ni roshani… Na katika roshani hizo… Simama... Tazama... Na ufurahie: وَال۟مُر۟سَلَاتِ عُر۟فًا فَال۟عَاصِفَاتِ عَص۟فًا وَالنَّاشِرَاتِ نَش۟رًا فَال۟فَارِقَاتِ فَر۟قًا فَال۟مُل۟قِيَاتِ ذِك۟رًا وَالنَّازِعَاتِ غَر۟قًا وَالنَّاشِطَاتِ نَش۟طًا وَالسَّابِحَاتِ سَب۟حًا فَالسَّابِقَاتِ سَب۟قًا فَال۟مُدَبِّرَاتِ اَم۟رًا تَنَزَّلُ ال۟مَلٰٓئِكَةُ وَالرُّوحُ فٖيهَا بِاِذ۟نِ رَبِّهِم۟ عَلَي۟هَا مَلٰٓئِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَا يَع۟صُونَ اللّٰهَ مَٓا اَمَرَهُم۟ وَ يَف۟عَلُونَ مَا يُؤ۟مَرُونَ Kisha sikiliza sifa zao: ﴿بَلْ عِبَادٌ مُّكْرَمُونَ۞ لَا يَسْبِقُونَهُ بِالْقَوْلِ وَهُم بِأَمْرِهِ يَعْمَلُونَ﴾ Na kama unataka kukutana na jinni, basi ingia katika ngome ya sura: قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ الْجِنِّ فَقَالُوا.. Kisha wasikilize nini wanasema… Na uzingatie... Hakika wanasema: اِنَّا سَمِع۟نَا قُر۟اٰنًا عَجَبًا يَه۟دٖٓى اِلَى الرُّش۟دِ فَاٰمَنَّا بِهٖ وَلَن۟ نُش۟رِكَ بِرَبِّنَٓا اَحَدًا
Kiama, Kubomoka kwa Dunia na Maisha ya Akhera Kuna misingi mine pamoja na utangulizi
Mtu yeyote akidai kuwa mji huu au kasri hili litabomolewa, na kujengwa upya ujenzi madhubuti na thabiti, basi hapana shaka kuwa madai yake haya yatapelekea katika maswali sita: Swali la Kwanza: Kwa nini linabomolewa? Na je, kuna sababu? Akithibitisha kuwa ndio, hapo sasa atajibiwa: Swali la Pili: Je, huyo anayebomoa na kujenga upya ana uwezo wa kufanya hivyo? Akithibitisha hili pia, litafuatia: Swali la Tatu ni hivi: Je, inawezekana kulibomoa? Na swali lingine: Na je, litabomolewa kweli? Inapothibiti kuwa inawezekana kulibomoa na kuwa atalibomoa kweli basi maswali mawili yatakuja. Je, inawezekana kujenga upya mji huu mzuri au kasri hili? Jawabu likiwa: Ndio inawezekana. Swali litakuja: Je, atalijenga kweli? Jibu likiwa: Ndio na akathibitisha yote hayo, hapo hakutabakia mwanya wowote wa kuingia utata wowote au shaka au dhana potovu katika pande zote za suala hili. Na hivihivi kwa mfano huu, kuna sababu cha kulibomoa na kuliteketeza kasri la dunia na mji wa viumbe hivi, na kisha kuliimarisha na kulijenga. Na kuwa kuna Mweza na Mdhibiti wa hilo, na hivyo anaweza kulibomoa, na atalibomoa kweli. Na kisha anaweza kulijenga na atalijenga tena upya kweli. Na yatathibiti kwetu masuala haya baada ya Msingi wa Kwanza.
Hakika ya roho ni yenye kubakia bila ya shaka. Kwani dalili zilizojulisha juu ya uwepo wa malaika na viumbe vya kiroho katika “Kusudio la Kwanza” hizohizo ni dalili za suala letu hili la “Kubakia kwa Roho”. Na kwangu suala hili ni thabiti kwa kiasi kwamba inakuwa ni upuuzi kuliingia kuliweka wazi. Naam, masafa ni mafupi na madogo kati yetu na misafara isiyohesabika ya roho zenye kubakia katika ulimwengu wa Barzakh na ulimwengu wa roho na zenye kungojea kuelekea Akhera, ambapo hatuhitaji dalili ili kuliweka wazi; mikutano kati yake na wasiyohesabika katika watu wa ufunuo na kushuhudia na kuonwa na watu wa ufunuo wa makaburi, na mahusiano ya jumla ya watu na mafungamano yao pamoja nao katika ndoto za kweli, na mazungumzo ya sehemu ya watu wa kawaida pamoja nao… Yote hayo yameifanya roho na kubakia kwake – kwa wingi wa tawatur – kuwa katika uelewa wenye kujulikana na watu. Ingawa fikra ya kimaada katika zama zetu hizi imewalevya wengi katika watu ikaingiza dhana potovu na utata katika mambo mepesi ya kiakili. Basi ili kuondosha dhana hizi potovu na wasiwasi, tutaashiria “vyanzo vine” tu, kati ya vyanzo vingi vilivyosheheni vya welevu wa kimoyo na utii wa kiakili tukianzia na “utangulizi”. Utangulizi Kama ilivyothibitishwa katika hakika ya nne kutoka “Neno la Kumi” kuwa uzuri wa ajabu wa kudumu milele ambao hauna mfano unahitaji kudumu kwa wenye kupendezwa nao na kubakia kwao, na wao ni kama kioo chenye kuakisi uzuri huo. Na kuwa ufundi kamili wa milele usio na upungufu unahitaji kudumu kwa wenye kuuhitaji wenye kutafakari. Na kuwa rehema na ihsani visivyo na mwisho, vinahitaji kudumu kuneemeka kwa wenye kuvishukuru viwili hivyo wenye kuvihitaji… Basi huyo mwenye kupendezwa ambaye ni kama kioo kilichosafishwa… Na huyo mwenye kuita mwenye kutafakari… Na huyo mwenye kushukuru-mwenye kuhitajia, si vinginevyo ila ni roho ya mwanadamu kwanza; Hivyo roho ni yenye kubakia ikiambatana na uzuri huo, ukamilifu huo na rehema hio... kwenye njia ya kudumu na ya milele. Na tumethibitisha vilevile katika hakika ya sita kutoka “Neno la Kumi” kuwa sio roho ya kibinaadamu pekee haikuumbwa kwa ajili ya kutoweka, bali hata viumbe wadogo kabisa pia hawakuumbwa kwa ajili ya kutoweka, bali wana aina ya kubakia. Basi ua dogo – mathalani – ambalo halina roho kama sisi, hilo pia linapoondoka kidhahiri kutoka kwenye uwepo, sura yake inabaki imehifadhiwa katika kumbukumbu nyingi, kama inavyodumu kanuni ya miundo yake katika mamia ya mbegu zilizo katika upeo wa udogo, na kwa hivyo huwakilisha kielelezo cha aina ya kubakia kwa maelfu ya njia. Na madamu kielelezo cha sura ya ua na kanuni ya muundo wake, inayofanana na roho kwa sehemu fulani, ni chenye kubakia na kuhifadhiwa na Al-Hafidh Mwenye hekima katika mbegu zake ndogo kwa mpangilio kamili katikati ya mlundikano wa mabadiliko mengi. Basi hapana shaka kuwa roho ya mwanadamu – ambayo ni kanuni ya amri ya kinuru inayomiliki ainisho tukufu, nayo ni yenye uhai na hisia, na sifa pekee zenye kukusanya na kujumuisha na za juu sana, na imevishwa uwepo wa nje – hapana shaka kuwa ni yenye kubakia milele na yenye kufungashwa na umilele na yenye mafungamano na umilele bila ya shaka yoyote. Na vipi unadai kama hujafahamu hili: Kuwa mimi ni mwanadamu mwenye utambuzi..? Na je, inawezekana kuulizwa Mwenye hekima na Mwenye utukufu na Al-Hafidh Mwenye kubaki ambaye ametengeneza mti mrefu na kuhifadhi kanuni za muundo wake inayofanana na roho katika mbegu ndogo mno: Vipi anahifadhi roho za wanadamu baada ya kufa kwao? Chanzo cha Kwanza: Cha Kinafsi Yaani kila anayetazama maisha yake kwa umakini na kutafakari ndani ya nafsi yake atafahamu kuwa kuna roho yenye kubakia. Naam, ni jambo la wazi kiakili kuwa kila roho pamoja na mabadiliko yanayotokea mwilini kupitia miaka ya umri inabaki vivyohivyo baila ya kuathirika. Hivyo maadamu mwili unaondoka na kufanyika upya, pamoja na kuthibiti kwa roho, basi hapana budi kuwa roho hata wakati wa kutoka kwake kikamilifu kwa sababu ya kufa, na kuuacha mwili wote, kubakia kwake hakuathiriki wala ainisho lake halibadiliki... Yaani ni yenye kubaki thabiti pamoja na mabadiliko yote haya ya kimwili. Na kilichopo ni kuwa mwili unabadili nguo zake hatua kwa hatua muda wote wa maisha yake pamoja na kubakia kwa roho. Ama wakati wa mauti huondolewa moja kwa moja na kuthibiti roho. Hivyo kwa welevu wa uhakika bali kwa kushuhudia tunaona kuwa mwili unaitegemea roho, yaani sio roho inayoutegemea mwili, bali roho ni yenye kujitegemea na kujitawala wenyewe. Na kwa hivyo, hutengana na mwili kwa namna yoyote ile, na kuwa pamoja nao hakudhuru wala kuharibu kujitegemea kwa roho. Mwili ni kiota cha roho na ni nyumba yake na sio vazi lake. Bali vazi la roho ni gamba laini na umbo la mfano-thabiti kwa kiasi fulani na ni yenye kunasibiana nayo kutokana na ulaini wake. Hivyo roho haiwi tupu kikamilifu hata wakati wa mauti, bali hutoka kwenye kiota chake ikiwa imevaa umbo lake la kupigiwa mfano na vazi lake maalum. Chanzo cha Pili: Cha Kiulimwengu Nayo ni hukumu inayotokana na maono yanayojikariri na matukio mengi na uzoefu mwingi. Naam, ikifahamika kubakia kwa roho moja baada ya mauti, hilo linalazimisha kubakia kwa “aina” ya roho hiyo kwa ujumla. Kwani inafahamika kwenye elimu ya Mantiki kuwa inapodhihiri “sifa ya kidhati” kwa mtu mmoja, basi inahukumiwa kuwepo kwa sifa hiyo kwa watu wote; kwa sababu ni sifa ya kidhati, hivyo ni lazima iwepo kwa kila mtu. Na ilivyo ni kuwa kubaki kwa roho hakujadhihiri kwa mtu mmoja pekee, bali athari zenye kuegemea katika yaliyoshuhudiwa ambayo hayahesabiki na dalili zinazojulisha juu ya kubakia kwake ni thabiti kwa sura ya kukinaisha kwa kiasi kuwa kama ilivyokwa hatuna shaka kabisa juu ya uwepo wa Bara la Amerika lililogunduliwa hivi karibuni na kuwekwa wakaazi, vilevile haiwezekani kuwa na shaka kwamba kwenye ulimwengu wa malakuti na wa roho sasa hivi kuna roho nyingi za wafu, zina uhusiano na sisi, kwani hakika zawadi zetu za kimaanawy zinaenda kwenye roho hizo, na kutujia kutoka kwao neema za kinuru. Na pia inawezekana kuhisi – kimoyo kwa welevu wa uhakika – kwamba nguzo ya msingi katika umbile la mwanadamu inabakia baada ya kufa kwake. Na nguzo hiyo ya msingi ni roho. Kwa sababu roho haipo katika hatari ya kupotea na kuharibika; kwa sababu ni ndogo na ina sifa ya upweke. Kwani kutoweka na kuharibika ni sifa mbili za wingi na vitu vilivyoundwa. Na kama tulivyobainisha hapo kabla kwamba hakika maisha yanalinda aina ya umoja ndani ya wingi, na kuwa ni sababu ya aina fulani ya kubaki. Yaani umoja na kubakia ni mambo ya msingi ya roho ambapo inapita kutoka hapo kwenda katika wingi. Hivyo kutoweka kwa roho ima iwe kwa kubomoka na kupotea au kwa kuifanya isiwepo; ama kubomoka, umoja na upweke hauviruhusu kuingia viwili hivyo, wala udogo hauviachi vikaharibika. Ama kutoweka, rehema kunjufu ya Mkarimu wa hali zote na ukarimu wake usio na mpaka unakataa kutaka kurudi kile alichokitoa katika neema ya uwepo ya roho ya mwanadamu yenye kufaa na yenye kupenda uwepo huo. Chanzo cha Tatu Roho ni kanuni ya kiamri, hai, yenye hisia, ya kinuru, na yenye hakika jumuishi, iliyoandaliwa kuvuna ujumla na ainisho jumuishi. Na imevishwa uwepo wa nje; kwani ni katika yanayojulikana kuwa amri dhaifu zaidi za kikanuni, uthabiti na kubakia vinadhihiri juu yake. Kwa sababu tukitazama kwa makini tunaona kuwa kuna “ukweli thabiti” katika aina zote zilizohatarini kubadilika, ambapo zinaviringika katika mabadiliko na hatua za maisha zikibadilisha sura na namna tofauti, lakini zinabakia hai na hazifi milele. Basi kanuni inayotenda kwa “aina” ya viumbe hai vingine inatenda pia kwa mtu “mmoja” kwa wanadamu; kwani mwanadamu “mmoja” kwa mujibu wa ujumuishi wa ainisho lake na ujumla wa hisia zake na taswira zake, amekuwa ni sawa na “aina” ingawa bado atakuwa ni mtu mmoja; kwa sababu Muumba mtukufu amemuumba mwanadamu huyu kuwa ni kioo jumuishi, pamoja na utumishi timamu, na ainisho la hadhi ya juu. Basi uhakika wake wa kiroho ndani ya kila mmoja haufi kamwe – kwa idhini ya Allah – hata ukibadilisha mamia ya maelfu ya sura, roho yake inaendelea kuwa hai kama ilivyoanza kuwa hai. Hivyo roho ambayo ni ukweli wa hisia za mtu huyo na kipengele cha maisha yake yenye kubakia ya kudumu milele kwa kubakishwa na Allah na kwa amri yake na idhini yake (s.w). Chanzo cha Nne Hakika kanuni zinazotawala na kutenda katika aina nyingi zinafanan na roho kwa kiasi fulani. Kwa sababau zote zinakuja kutoka katika ulimwengu wa “amri na utashi”. Hivyo huwa zinawafikiana na roho kwa kiasi cha sehemu fulani maalumu kutokana na kupatikana kutoka kwenye chanzo hicho hicho. Lau kama tutatazama kwa makini katika sheria na kanuni zenye kutenda katika aina ambazo hazina hisia ya dhahiri, itatudhihirikia kuwa kama zitavishwa kanuni hizo za kiamri uwepo wa nje zingalikuwa ni sawa na roho kwa aina hizi, kwani kanuni hizi ni thabiti, zenye kuendelea na zenye kubaki daima. Basi mabadiliko hayaathiri katika umoja wake wala mageuzi hayauharibu. Mathalan: Mtini unapokufa na kutawanyika basi kanuni ya muundo wake na ukuaji wake ambayo ni sawa na roho yake inabaki hai katika mbegu yake ndogo mno. Yaani upekee wa kanuni hizo hauharibiki wala kuathirika na mabadiliko na migeuko yote. Na kwa kuwa kanuni ndogo zaidi na dhaifu zaidi za kiamri zimefungamana na udaima na kubakia, basi inalazimu kuwa roho ya mwanadamu haifungamani na kubakia tu bali pamoja na udaima wa milele. Kwa sababu roho kwa maandiko ya Qur’an tukufu: مِنْ أَمرربِّي inakuja kutoka ulimwengu wa amri. Basi hiyo ni kanuni yenye hisia na sheria yenye uhai, uweza wa kiungu umeivisha uwepowa nje. Hivyo kama ambavyo kanuni zilivyokuwa si zenye hisia zinazokuja kutoka ulimwengu wa “amri” na sifa ya “utashi” inabakia daima au mara nyingi, basi vivyohivyo roho ambayo ni mfano wake inakuja kutoka ulimwengu wa “amri”. Nayo ni dhihirisho la sifa ya “utashi”. Hiyo ni yenye kustahiki zaidi kubakia na yenye kufaa kwa hilo. Yaani kubakia kwake ni bora kwa kuthibiti na uhakika; kwa kuwa ina uwepo na umiliki wa uhakika wa nje, nayo ina nguvu na ipo juu kuliko kanuni zote. Hiyo ni kwa kuwa ina hisia, na ni yenye kudumu zaidi na ni yenye thamani zaidi kwa sababu inamiliki uhai.
Hakika kuna ulazima na muktadha wa furaha ya milele.. Na Yule ambaye anatunuku maisha hayo na furaha ya kudumu ni Mweza... Na hakika kubomoka kwa ulimwengu na kufa kwa dunia ni jambo linalowezekana… Na hilo litatokea kweli… Na hakika ufufuo na kufufuliwa upya ulimwengu linawezekana pia… Na tukio hilo litatokea kweli. Haya ni masuala sita, tutayabainisha kwa kufuatana na kwa muhtasari wenye kukinaisha akili, bila ya kusahau kuwa tumetaja katika “Neno la Kumi” hoja zilizozifanya nyoyo kupanda katika ngazi ya imani kamilifu. Lakini hapa tutazileta tu kwa namna itakayokinaisha akili na kuinyamazisha, kama alivyofanya “Said wa zamani” kwenye Risala “Nukta katika nuru ya kumjua Allah (s.w)”. Naam, hakika kuna kinacholazimisha uwepo wa maisha mingine, na kuna sababu ya furaha ya kudumu, na hakika hoja ya uhakika inayojulisha ulazima huu ni welevu unaotona kutoka katika vyanzo na mihimili kumi: Mhimili wa Kwanza: Kama tutatazama kwa makini pande za ulimwengu tutaona kuwa kuna nidhamu iliyokamilika, na uratibu wa kupendeza uliokusudiwa katika sehemu zake zote. Basi tunashuhudia matone ya utashi na hiari, na min’gao ya makusudio katika kila upande… Hadi tunaona nuru ya “makusudio” katika kila kitu, na mwanga wa “utashi” katika kila jambo, na kung’aa kwa “hiari” katika kila harakati, na mwako wa “hekima” katika kila muundo. Basi kushuhudia matunda ya yote yaliyotangulia kunaleta mazingatio. Na namna hii kama kutakuwa hakuna maisha mingine na furaha ya milele, basi nidhamu hii imara inamaanisha nini? Itabaki sura dhaifu tu na itakuwa ni nidhamu ya uongo bila ya msingi wowote; na maana, mafungamano na nasabu - ambayo ndio roho ya nidhamu hiyo na kuendana vyema – vitakuwa ni vumbi lililotawanywa... Yaani maisha mingine na furaha ya milele, ndivyo vilivyoifanya nidhamu hii kuwa ni nidhamu haswa na kuipa maana. Hivyo nidhamu ya ulimwengu huu inaashiria katika furaha hiyo ya kudumu na maisha ya milele. Mhimili wa Pili: Hakika katika uumbaji wa viumbe hudhihiri hekima ya wazi. Naam, hakika hekima ya kiungu ambayo inaashiria uangalizi wake wa kiazali wa wazi kikamilifu; hivyo kuchunga maslahi ya kila kiumbe, na kushikamana na faida na hekima ndani yake ni jambo la wazi kote, na kunatangaza kwa ulimi wa hali yake kwamba furaha ya kudumu ipo; hiyo ni kuwa kama hakuna maisha mingine ya kudumu inatulazimu tukanushe – kwa ukaidi na inda – hekima zote zilizopo katika viumbe hawa na faida thabiti za wazi. Tunafupisha namna hii tukitosheka na ukweli wa kumi wa “Neno la Kumi” umedhihirisha ukweli huu kama jua. Mhimili wa Tatu: Imethibiti kiakili, kihekima, kitafiti na kimajaribio: Kuwa hakuna upuuzi wala israfu katika uumbaji wa viumbe, na kuwa kukosekana kwa viwili hivyo kunaashiria furaha ya kudumu na makaazi ya Akhera. Na dalili ya kuwa hakuna israfu katika maumbile wala upuuzi katika uumbaji, ni kuwa Muumba (s.w.) amechagua njia ya karibu ya kuumba kila kitu, upande wa karibu, na namna nyepesi na nzuri. Kwani anaweza kukipa kitu kimoja nyadhifa mia moja, na kufungamanisha na kitu kimoja kidogo malengo na matokeo elfu moja. Kwa kuwa hakuna israfu, wala haiwezekani kuwepo upuuzi, basi hapana budi kutimia kwa maisha hayo mingine ya kudumu. Na hiyo ni kuwa kama hakutakuwa na kurejea upya katika maisha, basi hakika ya kutokuwepo kunageuza kila kitu kuwa upuuzi. Kwa maana ya kwamba kila kitu kilikuwa israfu na kupoteza. Isipokuwa kutokuwepo israfu iliyo thabiti kwa mujibu wa elimu ya nyadhifa za viungo katika maumbile yote, akiwemo mwanadamu, inatubainishia kuwa haiwezekani kupotea bure. Basi maandalizi yote ya kimaanawy, matumaini yasioyokuwa na kikomo na fikra na mitazamo yakawa ni israfu… Ambapo kuelemea kiasili kwenye ukamilifu kulikowekwa ndani ya kina cha mwanadamu kunaeleza kuhusu uwepo wa ukamilifu maalumu, na kuwa kumili kwake na kutazamia furaha kunatangaza wazi kuhusu uwepo wa furaha ya kudumu na kuwa yeye ni mteuliwa wa furaha hiyo. Jambo likiwa sio hivyo, maana thabiti na matumaini ya hadhi ya juu ambavyo vinaasisi ainisho la kweli la mwanadamu, yote hayo yanakuwa – Allah ametakasika na hayo – israfu na upuuzi na kuenda patupu, kinyume na hekima iliyopo kwenye viumbe wote. Tunatosheka na kiasi hiki kwa kuwa tumeshathibitisha hapo kabla katika ukweli wa kumi na moja kutoka “Neno la Kumi”. Mhimili wa Nne: Hakika mabadiliko na mageuzi yanayotokea katika aina nyingi, hata katika usiku na mchana, na katika majira ya baridi na machipuo, na hewani, na hata katika mwili wa mwanadamu kipindi cha uhai wake, na usingizi ambao ni ndugu yake kifo… Yanafanana na ufufuo. Nayo ni aina ya Kiama kwa kila mojawapo. Na inajulisha na kueleza kwa alama kutokea kwa Kiama kikuu. Kama vile saa yetu inavyohesabu siku, saa, dakika na sekunde kwa mwendo wa gia zake, basi mishale yake inaeleza kwa miendo yake kuhusu kila mmoja kati yake, na kile kinachofuatia – yaani kila kimoja kinakitangulia kile kinachofuata. Vilevile dunia hii ni kama saa kubwa ya kiungu, inafanyakazi kwa mzunguko wake na kufuatana kwake ikihesabu siku na miaka, kila mshale unaeleza kuhusu ule unaofuata, nao unakuwa utangulizi wake. Basi kama saa hiyo inavyoleta asubuhi baada ya usiku na majira ya machipuo baada ya majira ya baridi, vilevile inatueleza kwa ishara kuhusu kutokea kwa asubuhi ya Kiama baada ya mauti na kutokea kwake kutoka katika saa hiyo kubwa. Na kuna aina nyingi tofauti katika aina za Kiama ambazo mwanadamu anazipitia katika kipindi cha uhai wake. Katika kila usiku kuna aina ya mauti na asubuhi anaona aina ya ufufuo. Yaani anaona kile kinachofanana na dalili za ufufuo, bali anaona namna zinavyobadilika atomu zote za mwili wake katika miaka kadhaa, hata anaona kielelezo cha Kiama na ufufuo hatua kwa hatua mara mbili kwa mwaka mmoja katika mabadiliko hayo ambayo yanatokea katika pande za mwili wake wote. Na anashuhudia pia ufufuo na Kiama cha aina fulani katika kila majira ya machipuo katika zaidi ya aina laki tatu katika aina za mimea na wanyama… Mkusanyiko huu wa dalili na ishara zisizo na mpaka juu ya ufufuo, na kiasi hiki cha alama zisizohesabika juu ya kufufuliwa… si vinginevyo ila nisawa na matone kwa Kiama kikuu yanayoashiria juu ya ufufuo mkuu. Basi kutokea kwa mfano wa Kiama hiki cha aina yake na kinachofanana na kukusanywa na kufufuliwa na Muumba Mwenye hekima katika aina nyingi, kwa kuyahuisha mashina yote na sehemu ya wanyama haohao, na (s.w.) kuvirejesha vitu vyote, majani, maua, matunda kwa mfano wake; yaweza kuwa ni dalili juu ya Kiama binafsi kwa kila mwanadamu ndani ya Kiama cha jumla. Ambapo “mwanadamu” anatofautiana na “aina” katika viumbe vingine; kwa sababu nuru ya fikra imetoa wasaa mkubwa kwa matumaini yake na fikra zake kiasi kwamba anaweza kujua muda uliopita na ujao, bali akiimeza dunia hatashiba... Ama katika aina nyingine ainisho la mtu ni la sehemu ndogo, thamani yake ni ya kibinafsi, mtazamo wake ni finyu, akili yake imefungwa, maumivu yake ni ya muda, na ladha yake ni ya mpito; wakati ambapo mwanadamu ainisho lake ni tukufu, sifa zake ni za juu, na thamani yake ni ghali, mtazamo wake ni jumuishi, na ukamilifu wake hauzuiwi na kitu, na sehemu ya maumivu yake na ladha zake za kimaanawy ni za kudumu. Hivyo yanayoshuhudiwa katika kukariri kwa mitindo ya Kiama na ufufuo katika baki ya aina yanaeleza na kuashiria kuwa kila mwanadamu atarejeshwa yeye huyohuyo na kufufuliwa katika Kiama kikuu cha jumla. Na kwa vile tumeshathibitisha katika ukweli wa tisa wa “Neno la Kumi” kwa namna ya uhakika kama anavyothibitisha matokeo ya anayezidisha mbili mara mbili ni sawa na nne, basi hapa tumeshafupisha. Mhimili wa Tano: Wanazuoni wahakiki wanona kuwa fikra za wanadamu na tasawuri zake za kibinaadamu zisizo na mwisho zinazotokana na matumaini yake yasiyo na mpaka, yanayotokana na mambo ayapendayo yasiyo na mpaka, yanayotokana na ukubalifu wake usiyodhibitika, uliyoambatana na maandalizi yake ya kimaumbile yasiyo na mpaka, yaliyo katika kiini cha roho yake, yote hayo yananyoosha vidole vyake yanaashiria na kutazamia kwa uoni wake kuelekea katika ulimwengu wa furaha ya milele nyuma ya ulimwengu huu wa kushuhudiwa. Basi maumbile ambayo kamwe hayadanganyi na ambayo ndani yake kuna kuegemea sana na kwa uhakika kusikotetereka kuelekea furaha ya Akhera ya milele, yanaupa moyo welevu wa uhakika juu ya kutokea kwa uhai wa Akhera na furaha ya milele. Tunatosheka na hapa na kwa kiasi hiki kwa kuwa ukweli wa kumi na moja wa “Neno la Kumi” umedhihirisha ukweli huu waziwazi kama mchana. Mhimili wa Sita: Hakika rehema ya Muumba wa ulimwengu ambaye ni Ar-Rahman Ar-Rahim inajulisha juu ya furaha ya milele. Naam, hakika kilichoifanya neema kuwa ni neema hasa na kuiokoa kutokana na adhabu, na kuviokoa vilivyopo kutokana na kilio cha utengano wa milele… ni furaha ya milele na makaazi ya milele. Na ni tabia ya rehema hiyo ambayo haiwanyimi wanadamu kutokana na hayo. Kwani kama hawatapewa furaha hiyo na makaazi ya milele ambavyo ndiyo kichwa cha kila neema na lengo lake na matokeo yake ya msingi, yaani dunia isipofufuliwa baada ya mauti yake kwa sura ya “Akhera”... neema zote zitabadilika na kuwa adhabu... Na hili linalazimu kukana reheme ya kiungu inayoshuhudiwa na ya dhahiri kiakili na ya lazima ulimwenguni, na thabiti kwa ushuhuda wa viumbe vyote na ambayo ni hakika thabiti ya wazi kuliko jua. Ukijaalia kuwa mwisho wa maisha ya mwanadamu unaelekea katika utengano wa milele na kutokuwepo, kisha ukatazama kwa umakini kwenye baadhi ya athari nzuri za “rehema” hiyo na nuru zake katika neema za upendo, wema na akili… kwa hakika utaona kuwa upendo huo unakuwa ni msiba mkubwa… Na wema huo mtamu unakuwa ni maradhi mabaya... Na akili hiyo ya kinuru inakuwa ni balaa kubwa… Kwa hiyo, rehema – kwa kuwa ni rehema – haiwezi kulinganishwa kati ya upendo wa kweli na utengano huo wa milele na kutoweka. Yaani hapana budi kuwepo maisha mingine… Tumefupisha ukweli huu hapa ambapo ukweli wa pili kutoka katika “Neno la Kumi” limeweka wazi vizuri. Mhimili wa Saba: Hakika mema na makamilifu yote, shauku na mazuri, na mivuto na huruma zote tunazozijua na kuziona katika viumbe hivi si vingine ila ni maana, na madhumuni, na maneno ya kimaanawy, yanayoubainishia moyo kwa uwazi wote na kuidhihirishia akili kwa uwazi wote, kuwa hayo ni madhihirisho ya ukarimu wa Muumba mtukufu na hisani yake, na kuwa hayo ni madhihirisho ya rehema yake ya milele na upole wake wa kudumu (s.w.). Na kwa kuwa kuna “ukweli” thabiti katika ulimwengu wetu, na rehema ya kweli na ya wazi, basi hapana budi kuwepo kwa furaha ya milele. Ukweli wa nne pamoja na wa pili kutoka katika “Neno la Kumi” umebainisha ukweli huu kama jua. Mhimili wa Nane: Hakika moyo wenye hisia wa mwanadamu ambao ni maumbile yake, unajulisha juu ya maisha mingine na kuashiria furaha ya milele. Naama, hakika anayesikiliza moyo wake uliyo macho basi bila ya shaka anasikia “milele… milele” hata moyo huo ukipewa kila kilicho katika viumbe, basi hakitoshelezi haja yake ya kuelekea umilele. Kwa maana kwamba moyo huo umeumbwa kwa ajili ya umilele huo, na kuwa mvuto huu na mvutiko wa kimoyo hakuwi ila kwa mvuto kutoka katika lengo la kweli na chenye kuvutia kikweli. Na hitimisho la ukweli wa kumi na moja kutoka katika “Neno la Kumi” umedhihirisha ukweli huu. Mhimili wa Tisa: Hakika maneno ya Nabii mkweli mwenye kusadikishwa na kusadikiwa Muhammad Mwarabu Al-Hashimy (s.a.w.) amefungua milango ya furaha ya milele, na hakika hadithi zake tukufu ni madirisha yaliyofunguliwa kwa furaha hiyo ya milele kupita. Naye kwa kumiliki nguvu ya maafikiano ya manabii wote (a.s.) na tawatur za mawalii wakweli wote, amethibitisha kwa yakini thabiti madai yake yote kwa nguvu yake yote, baada ya kumpwekesha Allah (s.w.) juu ya nukta hii ya msingi, ambayo ni ufufuo na maisha ya Akhera. Je, kuna kitu kinachoweza kuitikisa nguvu hii imara? Ukweli wa kumi na mbili kutoka katika “Neno la Kumi” umeweka wazi ukweli huu kikamilifu. Mhimili wa Kumi: Ni ufukishaji wa wazi wa Qur’an tukufu ambayo imetunza muujiza wake – kwa namna saba – kipindi chote cha karne kumi na tatu na bado inaendelea kufanya hivyo, kama tulivyothibitisha aina arobaini za muujiza wake katika “Neno la Ishirini na Tano”. Naam, hakika kueleza kwa Qur’an yenyewe kuhusu ufufuo wa kimwili ni mwanga unaotosheleza na wenye kuubainisha. Ni ufunguo wa hekima iliyowekwa kwa viumbe na wa siri iliyofungwa ya ulimwengu. Na Qur’an hii tukufu imelingania mara kwa mara kutafakari na kutazama maelfu ya dalili za kiakili-za-uhakika. Aya tukufu mfano:- وَقَدْ خَلَقَكُمْ أَطْوَارًا قُلْ يُحْيِيهَا الَّذِي أَنشَأَهَا أَوَّلَ مَرَّةٍ… Kwa hakika ni vielelezo vya kipimo cha mifano ya aina yake. Na kuwa: وَمَا رَبُّكَ بِظَلَّامٍ لِّلْعَبِيدِ ni kielelezo kingine kinachoashiria dalili ya uadilifu ulimwenguni. Na aya nyingine nyingi ambapo miwani “vifaa chunguzi” zenye lenzi nyingi za kukuza ili kupitia hizo uangalie kwa umakini furaha ya milele katika ufufuo wa kimwili. Na tumeweka bayana katika risala ya “Nukta” kipimo cha mfano kilichopo katika aya mbili za mwanzo pamoja na aya nyinginezo. Na muhtasari wake ni kuwa: Mwandamu kila anapohama kutoka hatua moja kwenda nyingine anapita katika mageuzi ya ajabu yaliyoratibika vyema. Basi kuanzia katika tone (la manii) kuwa pande la damu, na kutoka pande la damu kuwa pande la nyama, na kutoka pande la nyama kuwa mfupa, kisha nyama. Na baada ya hivyo, kuwa ni kiumbe kipya. Yaani kugeuka kwake kuwa sura ya mwanadamu kunafuata kanuni makini. Kila hatua ina kanuni maalumu na nidhamu maalumu na harakati zilizopangika, kiasi kwamba inaonesha kilicho ndani yake katika nuru za kusudio, utashi, hiari na hekima. Na kwa njia hiyohiyo hakika Muumba Mwenye hekima anaubadilisha mwili huu kila mwaka kama kubadilisha nguo. Basi mwili huo kuwa na haja ya muundo mpya ili ubadilike na kuwa hai, na una haja ya kuweka atomu imara mpya mahali ambapo za mwanzo zimetoweka katika viungo vyake. Hivyo kama ambavyo mwili unabomoka vijivyumba vyake kwa kanuni ya kiungu iliyoratibika, pia unahitaji maada nyepesi kwa jina la “riziki” ili ujengeke upya kwa kanuni ya kiungu wa Mola Mlezi iliyo makini… Basi Mruzuku wa kweli anagawa kwa kanuni maalumu kwa kila kiungo miongoni mwa viungo vya mwili tofauti, na kwa kiasi maalumu, kianachohitaji katika maada tofauti. Na sasa tazama hatua za maada hiyo nyepesi iliyotumwa kutoka kwa Mwenye kuruzuku na Mwenye hekima, utaona kuwa atomu za maada hiyo ni kama msafara uliotawanywa hewani… ardhini… katika maji… Wakati ikiwa imetawanya huku na kule, tahamaki huwekwa tayari na kukusanyika kwa namna maalumu, kana kwamba kila atomu ina jukumu la wadhifa imetumwa pahala maalumu kwa wajibu rasmi. Na hivyo hukusanyika wenyewe kwa mpangilio mkubwa, jambo linaloonesha kuwa ni harakati iliyokusudiwa. Basi mwenendo wake huu unabainisha kuwa: Mtendaji Mwenye utashi anazipeleka atomu hizo kwa kanuni yake maalumu kutoka ulimwengu wa vitu kuelekea ulimwengu wa viumbe hai. Na hapa baada ya kuingia katika mwili maalumu, kuwa ndio riziki yake, zinapita kwa mujibu wa nidhamu maalumu na harakati zilizoratibika na kwa mujibu wa kanuni maalumu. Kwani baada ya kuiva katika majiko manne na kupitia mageuzi manne ya ajabu na kuchujwa kwa machujio manne, huandaliwa kwa ajili ya kusambazwa katika sehemu za mwili na viungo vyake tofauti kwa mujibu wa mahitaji tofauti ya kila kiungo, na chini ya uangalizi wa Mwenye kuruzuku wa kweli na matunzo yake na kanuni zake zilizoratibika. Kama utaitazama kwa jicho la hekima atomu yoyote katika atomu hizo basi utaona kuwa anayeiendesha atomu hiyo anaiendesha kwa uoni mkubwa, kwa nidhamu, na kwa ujazo wa usikivu na elimu yenye kuzungukia kila kitu... Haiwezekani kwa namna yoyote ile kuingia humo “maafikiano ya upofu”, “bahati isiyo na mpangilio”, “Asili ziwi” na “sababu zisizo na utambuzi”; kwa sababu kila atomu katika atomu hizo ilipoingia kwenye hatua yoyote katika hatua hizo, kuanzia ilivyokuwa elementi kwenye upande wa nje na kuishia ndani ya seli ndogo ya mwili, kana kwamba inatenda kwa utashi na hiari kwa mujibu wa kanuni maalumu katika kila hatua kati ya hizo. Kwani inapoingia huingia kwa nidhamu, na inapoelekea katika ngazi moja kati ya hizo huelekea kwa hatua zilizopangika kwa kiasi inadhihiri wazi kuwa kana kwamba amri ya Mwendeshaji Mwenye hekima anaiendesha. Na kwa namna hii na kwa nidhamu kamili, kila atomu inavyopita kutoka hatua kwenda nyingine na kutoka daraja kwenda jingine haiendi upogo na lengo lililokusudiwa, hadi inapofika katika ngazi maalumu iliyoandaliwa kwa ajili yake kwa amri ya kiungu Mola Mlezi katika mboni ya jicho la “Tawfiq” mathalani… Na huko inasimama ili kufanikisha nyadhifa zake maalumu na kutekeleza kazi zake. Na namna hii, hakika kudhihiri kwa rububiyya katika riziki kunabainisha kuwa atomu hizo, tokea hapo mwanzo, zilikuwa maalumu na zenye kuamuriwa, na zilikuwa na jukumu la wadhifa fulani, na zilikuwa zimeandaliwa kufika katika ngazi hizo zilizoandaliwa kwa ajili yake. Kana kwamba kila atomu imeandikwa katika paji lake la uso kile itakachoishia. Yaani itakuwa ni riziki ya seli fulani. Jambo ambalo nidhamu hii nzuri linatuashiria kuwa jina la kila mwanadamu limeandikwa juu ya riziki yake, kama ambavyo riziki yake imeandikwa katika paji lake la uso kwa kalamu ya kadari. Je, yawezekana kuwa Mola Mlezi Mwenye rehema Mwenye uweza wa hali zote na hekima yenye kuzungukia kila kitu asianzishe “maumbile mengine” au ashindwe kufanya hivyo? Naye ana ufalme wa mbingu na ardhi nazo zimekunjwa mkononi mwake kutoka atomu hadi vyenye kuelea na kuvisimamia vyote kwa nidhamu iliyopangika vyema na kipimo makini… Basi ametakasika Allah kwa yale wanayomsifu. Hivyo, aya nyingi za Qur’an tukufu zinaelekeza mtazamo wa mwanadamu kwenye “maumbile ya mwanzo” ya hekima kama mfano wa kipimo wa “maumbile mengine” katika ufufuo na kiama, na hiyo ili ziweke mbali kukanusha kwenye akili ya mwanadamu na kusema: قُلْ يُحْيِيهَا الَّذِي أَنشَأَهَا أَوَّلَ مَرَّةٍ... Yaani yule aliyewaumbeni - na hali ya kuwa hamkuwa kitu chenye kutajwa – kwa sura hii ya hekima ndiye ambaye atakupeni uhai huko Akhera. Na unasema: وَهُوَ الَّذِي يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ وَهُوَ أَهْوَنُ عَلَيْهِ… Yaani kukurejesheni na kukuhuisheini huko Akhera ni jambo jepesi zaidi kuliko kukuumbeni duniani. Kwani kama vile askari wanapotawanyika kwa ajili ya mapumziko, yawezekana kuwarejesha kwenye maeneo yao chini ya bendera ya kikosi kwa mpulizo tu wa firimbi ya kiaskari. Basi kuwakusanya namna hii kutoka mapumzikoni katika sehemu maalumu ni jambo jepesi sana kuliko kuanzisha kikosi kipya cha askari. Pia atomu za msingi ambazo zimezoeana na kufungamana kwa kuchanganyika kwake katika mwili maalumu pale malaika Israfil (a.s.) anapopuliza parapanda lake kwa mpulizo mmoja litavuma likisema: Tumeitika amri ya Muumba mtukufu, na kukusanyika. Basi kukusanyika kwake pamoja na nyingine kwa mara nyingine hapana shaka kuwa ni jambo jepesi kiakili, kuliko kuzileta atomu hizo kwa mara ya kwanza. Yawezakuwa isiwe lazima kukusanyika kwa atomu zote, bali zinatosha atomu za msingi ambazo nisawa na mbegu kwa miili. Kama Hadithi tukufu ilivyoeleza “maajabu ya dhambi” ambazo ni sehemu ya msingi, na atomu asilia inayotosha peke yake kuwa ndio msingi wa kuanzisha maumbile mengine juu yake. Basi Muumba Mwenye hekima anaujenga upya mwili wa mwanadamu kwa msingi huo. Ama kipimo cha kiuadilifu ambacho aya tukufu inakiashiria: وَمَا رَبُّكَ بِظَلَّامٍ لِّلْعَبِيدِ Muhtasari wake: Sisi tunaona sana katika ulimwengu wetu, kuwa madhalimu na waovu wanaishi maisha yao kwenye starehe na raha kamilifu. Ama waliodhulumiwa na wenye kushikamana na dini wanaishi maisha magumu na yenye kuchosha... Na hivyo, mauti yanapokuja yanawachukua wote wawili kwa pamoja bila ya kubagua. Basi lau kusingalikuwa na mwisho uliokusudiwa na maalumu, basi dhulma ingedhihiri katika jambo hilo. Hivyo hapana budi kuwepo mkutano wa Akhera baina yao ili wa mwanzo apate adhabu yake na wa pili apate thawabu zake; kwani aliyetakasika na dhulma ni (s.w.) ambaye ni Mwadilifu Mwenye hekima kwa ushuhuda wa viumbe vyote, haiwezekani kwa namna yoyote ile uadilifu wake na hekima yake kukubali dhulma hii na haiwezekani kuiridhia. Basi, mwisho uliyokusudiwa ni thabiti; kwa sababu kuona kwa mwanadamu huyu mwenye kujituma na kutaabika malipo yake na thawabu zake – kwa mujibu wa maandalizi yake – yanamfanya kuwa ni alama ya uadilifu safi na mhimili wake na dhihirisho la hekima ya kiungu Mola Mlezi, mwenye kuendana na vilivyopo vyenye hekima ulimwenguni na kaka yao mkuu. Naam, hakika makazi ya dunia hii fupi hayatoshi – kama ambavyo sio kasha – kudhihirisha maandalizi yasiyo na ukomo yaliyo ndani ya roho ya mwanadamu na kufanya yatoe matunda. Basi hapana budi mwnadamu huyu kupelekwa katika ulimwengu mwingine… Naam, hakika kiini cha mwanadamu ni kitukufu, hivyo yeye ni alama ya umilele na mteule wa hilo. Na ainisho lake ni la hadhi ya juu; hivyo kosa lake limekuwa ni kubwa; hafanani na viumbe wengine, na nidhamu yake ni nzuri na ya kina, basi mwisho wake hauwezi kuwa bila ya nidhamu, na hatapuuzwa na kwenda patupu, na hatahukumiwa kutoweka kabisa-kabisa na kukimbia kuelekea katika kutokuwepo. Na hakika Jahanamu itafungua kinywa chake wazi… ikimsubiri… Na Pepo inamnyooshea mikono ili imkumbatie… Tumefupisha hapa kwa vile ukweli wa tatu kutoka katika “Neno la Kumi” umebainisha ukweli huu kwa uwazi. Na namna hii tumezileta aya hizi mbili zikiwa ni mifano, ni juu yako kupima na kufuatilia mfano wake katika aya nyingine tukufu ambazo ndani yake kuna hoja za kiakili nzuri na nyingi. Basi hivyo ni vyanzo na mihimili kumi ambayo inatoa welevu wa kweli na hoja ya uhakika juu ya ufufuo. Kama ambavyo welevu huu thabiti na hoja yenye nguvu ni dalili ya uhakika ya kutokea kwa Kiama na ufufuo wa kimwili na unahitajia hivyo. Pia majina mazuri ya kiungu: Mwenye hekima, Mwenye rehema, Al-Hafidh, Mwadilifu, na majina mazuri mengi yanahitajia siku ya Kiama na furaha ya milele, na yanajulisha juu ya kutokea kwake kwa uhakika, kama tulivyothibitisha katika “Neno la Kumi”. Hivyo, yanayopelekea ufufuo na Kiama yamekuwa kwetu ni yenye nguvu na imara kwa kiasi ambacho haiwezekani humo kuingia utata wala shaka kabisa.
Naam, kama ilivyokuwa hapana shaka kabisa kwenye mahitaji ya ufufuo, pia hapana shaka kabisa kwenye uweza usio na mpaka wa Yule anayeleta ufufuo. Hapana upungufu katika uweza wake, kwani kubwa na dogo kwake ni sawa, na ni sawa kwake pia kuumba majira kamili ya machipuo na kuumba ua moja. Naam, hakika Mwenye uweza ambaye ulimwengu huu unashuhudia utukufu na uweza wake kwa ndimi za majua yake, nyota zake, na limwengu zake hata kwa ndimi za atomu zake na yaliyo ndani yake, je, ni haki kwa dhana potovu au wasiwasi wowote kuutupilia mbali uweza huo wa hali zote wa kufufua kimwili? Hakika Mwenye uweza Mwenye utukufu anaumba limwengu mpya zilizoratibika katika kila zama ndani ya ulimwengu huu mkubwa, bali anaumba katika kila mwaka dunia nyingi zitembeazo, mpya na zilizoratibika; bali huumba kila siku limwengu mpya zilizoratibika. Basi huumba mfululizo limwengu na dunia nyingi na limwengu zenye kutoweka na zenye kufuatana, na huzibadilisha kwa hekima yote juu ya uso wa dunia na mbingu, akisambaza na kuangika kwenye mapito ya zama limwengu zilizoratibika kwa idadi ya zama na miaka, bali kwa idadi ya siku. Na anaonesha kwa mambo hayo ukubwa wa uweza wake (s.w.). Naye ndiye aliyepamba bustani kubwa na pana ya majira ya machipuo kwa mamia ya maelfu ya nakshi za ufufuo, anaipa taji dunia kwa mapambo hayo kana kwamba ni ua moja. Na hivyo kutudhihirishia uzuri wa ufundi wake na ukamilifu wa hekima yake. Je, yawezekana kuna mtu anayethubutu kumwambia huyu Mwenye uweza na utukufu: Vipi analeta Kiama? Au vipi ataibadilisha dunia hii kwa Akhera? Basi aya tukufu: مَا خَل۟قُكُم۟ وَلَا بَع۟ثُكُم۟ اِلَّا كَنَف۟سٍ وَاحِدَةٍ Inatangaza kuwa huyu Mwenye uweza (s.w) hakimshindi kitu, kila kitu kikubwa na kidogo ni chepesi kwake. Na kubdi kubwa kwa idadi yake isiyo na mpaka ni kama mtu mmoja kwake… Na tumebainisha ukweli wa aya hii mwishoni mwa “Neno la Kumi” kwa ujumla, na katika Risala ya “Nukta ya Nuru ya Kumjua Allah (s.w.)” na “Andiko la Ishirini”. Ama hapa tutabainisha kwa ufupi katika masuala matatu: Hakika uweza wa kiungu ni wa kidhati; hauwezi kuingiwa na kushindwa… Nao unafungamana na umalakuti wa vitu, basi vizuizi haviingii humo kamwe… Na uwiano wake ni wa kikanuni; kwani sehemu inafanana na kitu kizima, na wa sehemu ndogo unakuwa sawa na wa kijumla… Tutathibitisha na kubainisha masuala haya matatu: Suala la Kwanza: Hakika uweza wa kiungu wa azali ni wa lazima kwa dhati tukufu iliyotakasika. Yaani kwa hakika ni lazima kwa adhati tukufu, kwani haiwezekani kwa uweza uachane na dhati hiyo kabisa. Hivyo ni wazi kuwa kutokuweza ambako ni kinyume na kuweza hakuwezi kutokea kwa dhati tukufu ambayo imelazimu uwepo uweza, kwa sababu hapo vitakusanyika viwili ambavyo ni kinzani, na hilo ni muhali. Maadamu kushindwa hakuwezi kutokea kwenye dhati, ni wazi kuwa hakuwezi kuingilia uweza wa lazima kwa dhati hiyo pia. Na maadamu kushindwa hakuwezi kamwe kuingia katika uweza huo, ni wazi kuwa uweza huo wa kidhati hauna daraja, kwa sababu uwepo wa daraja katika kila kitu unakuwa kwa kuingia vinyume vyake pamoja nacho, kama ilivyo katika daraja za joto ambazo zinakuwa kwa kuingiza baridi, na daraja za uzuri ambazo zinakuwa kutokana na kuingia ubaya… na pima namna hii. Ama katika vinavyowezekana ni kwa kuwa hapana ulazima wa kidhati wa uhakika au wa kufuatia; vinyume vimekuwa vinaingiliana wenyewe kwa wenyewe, daraja zikapatikana na kuzaa khitilafu, kutokana na hayo, yakapatikana mabadiliko ya ulimwengu. Na kwa kuwa hakuna daraja kamwe katika uweza wa kiungu wa kiazali, hivyo vyenye kukadiriwa hapana shaka ni vimoja kwa mujibu wa uweza huo. Basi kilicho kikubwa sana kinakuwa sawa na kidogo sana, na nyota huwa ni sawa na atomu, na kufufua watu wote kunakuwa sawa na kufufua nafsi moja... Na pia kuumba majira ya machipuo ni kama kuumba ua moja, ni jambo jepesi mbele ya uweza huo... Na lau uumbaji ungeegemezwa kwenye sababu za kimaada pasi na kuegemezwa kwenye uweza usio na mpaka, hapo kuhuisha ua moja kunakuwa ni vigumu kama kuhuisha majira ya machipuo. Na kwa hakika tumethibitisha kwa hoja za wazi katika tanbihi ya kifungu cha mwisho cha ngazi ya nne katika ngazi za “Allahu Akbar” kutoka katika kituo cha pili cha neno hili, na katika “Neno la Ishirini na Mbili” na “Andiko la Ishirini na Nyongeza yake” kwamba katika kuegemeza uumbaji wa vitu kwa mmoja wa pekee huwa ni rahisi kuumba vyote kama kuumba kitu kimoja, na unapoegemezwa uumbaji wa kitu kimoja kwenye sababu za kimada huwa ni vigumu sana na ni tatizo kama kuumba vyote. Suala la Pili: Hakika uweza wa kiungu unafungamana na umalakuti wa vitu… Naam, hakika kila kitu ulimwenguni kina pande mbili kama kioo: Moja wapo: Ni upande wa “Umulku” nao ni kama upande wenye rangi wa kioo. Na mwingine: Ni upande wa Malakuti nao ni kama upande unaong’aa wa kioo. Upande wa umulku, ni uwanja wa kutembea kwa vinyume na mahali pa kutokea kwa mambo ya uzuri na ubaya, kheri na shari, udogo na ukubwa, ugumu na wepesi na mfano wa hayo.. Hivyo, Muumba Mwenye hekima ameweka sababu za dhahiri kuwa ni pazia la matendo ya uweza wake, ili mkono wa uweza wenye hekima usidhihiri wenyewe moja kwa moja kwa mambo ya sehemu fulani ambayo yanadhihiri kwenye akili pungufu zinazoyaona juu-juu kana kwamba ni duni na yasiyofaa, kwani utukufu unahitajia hivi… Isipokuwa Yeye (s.w) hakuzipa sababu na njia hizo taathira ya kweli; kwa kuwa upekee wa umoja wake unalazimisha hivi pia. Ama upande wa malakuti, ni wenye kuonesha, msafi, umetakasika katika kila kitu, rangi na mapambo ya tashihisi hayachanganyiki pamoja nao… Upande huu unaelekea kwa Muumba wake bila ya kiunganishi chochote. Ndani yake hakuna kupangika wala kufuatana kwa sababu na visababishwa, wala usababu na usababishwa, hauingii humo, wala vizuizi haiviingiliani. Basi atomu humo huwa ni ndugu wa jua. Tunafupisha kutokana na yaliyotangulia: Kuwa uweza huo upo pekee, yaani haukuundwa kutokana na vitu, nao upo huru hauna npaka, na ni wa dhati yake pia. Ama mahali pa kufungamana kwake na vitu ni kuwa hauna kiunganishi, ni safi usio na taka, na ni bila ya pazia, na bila ya kuchelewa. Hivyo kubwa kwake haliwi kubwa mbele ya dogo, wala kundi halifanywi bora kuliko mtu mmoja, wala jumla haijifaharishi mbele ya sehemu katika uweza huo. Suala la Tatu: Kiwango cha uweza kisheria Ni kuwa unatazama kichache na kingi, kidogo na kikubwa mtazamo mmoja uliyo sawa. Suala hili tata tutalisogeza akilini kwa baadhi ya mifano. Uangavu, kukabiliana, kulingana, kupangika, kujitenga na utiifu… Kila moja kati ya hayo katika ulimwengu huu ni jambo linalofanya kingi kuwa sawa na kichache, na kikubwa kuwa sawa na kidogo. Mfano wa Kwanza: Uangavu Kwamba dhihirisho la mwanga wa jua linaonesha utambulisho wenyewe juu ya mgongo wa bahari au juu ya kila tone la bahari. Basi lau dunia ingelikuwa imeundwa kutokana na vipande vya vigae vidogo, vyenye kuonesha na tofauti vinalikabili jua bila ya kizuizi kunachozuia, basi mwanga wa jua wenye kudhihiri juu ya kila kipande juu ya mgongo wa ardhi na juu ya mgongo wa ardhi wote hufanana na kuwa sawa bila ya mchanganyiko na bila ya kugawanyika wala kupungua… Kama tutajaalia kuwa jua ndilo tendaji lenye utashi na likatoa nuru yake na miale ya sura yake kwa utashi wake juu ya ardhi, hapo haiwi kusambaza nuru yake nyingi juu ya ardhi yote ni jambo gumu zaidi kuliko kuipa atomu moja nuru hiyo. Mfano wa Pili: Kukabiliana Jaalia kuwa kulikuwa na duara pana la watu kila mmoja kati yao amebeba kioo mkononi mwake, na katikati ya duara kuna mtu aliyebeba mshumaa unaowaka, hakika ya mwanga unaosambazwa kutoka katikati kuelekea kwenye vioo vilivyozunguka ni mmoja, na unakuwa kwa kiasi kimoja, bila ya upungufu, bila ya mchanganyiko, wala kuachana. Mfano wa Tatu: Kulingana Ikiwa tuna mizani ya uhakika, kubwa na makini sana na katika vitanga vyake viwili kuna majua mawili au nyota mbili au milima miwili au mayai mawili au atomu mbili… Nguvu inayotumika ni ileile ambayo inaweza kuinua moja ya vitanga vyake viwili juu na kukiteremsha kingine chini. Mfano wa Nne: Kupangika Inawezekana kuiongoza meli kubwa mno kwa sababu imepangika sana kama mfano wa mdoli mdogo mno wa watoto. Mfano wa Tano: Kujitenga Kirusi ni kama faru, kinabeba utambulisho wa mnyama na sifa zake za pekee, na samaki mdogo sana anamiliki sifa hiyo ya kipekee na utambulisho huo wa kipekee kama nyangumi mkubwa, kwa sababu utambulisho wa kipekee kama vile umbo na kufanyika mwili vinaingia katika sehemu zote za mwili kuanzia mdogo kuliko wote hadi mkubwa kuliko wote, na kuelekea huko bila ya upungufu na bila ya kugawanyika. Basi umahususi wa aina na sifa za dhahiri za mwili havishawishiwi wala kuingiliana pamoja na utambulisho na umahususi wa kipekee na wala haubadilishi muonekano wa umahususi huo wa kipekee. Mfano wa Sita: Utii Kiongozi wa jeshi kwa kuamrisha kwake “nenda mbele” kama anavyomfanya mwanajeshi mmoja kusogea basi pia analisogeza jeshi lote kwa amri hiyohiyo. Basi ukweli wa siri ya utii ni kuwa kila kitu ulimwenguni – kama inavyoshuhudiwa kwa uzoefu – kina nukta ya ukamilifu, na kinaegemea kwenye nukta hiyo. Basi umaradufu wa kuegemea unazalisha uhitaji, na umaradufu wa uhitaji unageuka kuwa ni shauku, na umaradufu wa shauku unatengeneza mvuto. Mvuto, shauku, uhitaji, na kuegemea... vyote hivyo ni mbegu za kutekeleza amri za kimaumbile za Mola Mlezi kwa upande wa utambulisho wa vitu. Ukamilifu wa hali zote wa utambulisho wa vyenye kuwezekana ni uwepo wa hali zote, lakini ukamilifu wake maalumu ni uwepo wake maalumu, unatoa maandalizi yake ya kimaumbile yaliyojificha kutoka katika sura ya nguvu kwenda sura ya matendo. Hivyo, kutiisha viumbe kwa amri ya “kuwa” ni kama kutiisha atomu moja ambayo ni sawa na mwanajeshi mtiifu. Na viumbe katika kutekeleza na kutii amri ya azali ya “kuwa” inayotokana na utashi wa kiungu, maegemeo, shauku na uhitaji; vyote vinaambatana kwa pamoja, na kila moja kati ya hivyo ni udhihirisho katika madhihirisho ya utashi huo pia. Hata kwamba maji yenye kutiririka yanapochukua – kwa kuegemea kidogo – amri ya kuganda, yanadhihirisha siri ya nguvu ya utii kwa kukibomoa chuma. Ikiwa mifano hii sita inatubainishia katika nguvu ya vinavyowezekana na viumbe na katika kutenda kwake, nayo ni pungufu na yenye ukomo na dhaifu na haina taathira ya kweli, hivyo inapasa kuwa sawa vitu vyote mbele ya uweza wa kiungu unaodhihirika kwa athari ya ukubwa wake... Nao hauna ukomo na ni wa azali nao ndio ulioleta viumbe vyote kutokana na kutokuwepo kabisa na kuzifanya akili zote zitahayari. Hivyo hakuna kitu kigumu kwake. Na tusisahau kuwa uweza mkuu wa kiungu haupimwi kwa vipimo vyetu hivi dhaifu, wala havinasibiani nao, lakini hutajwa kuuweka karibu kwenye akili na kuondosha kutowezekana si vinginevyo. Matokeo ya Msingi wa Tatu na Muhtasari Wake: Maadamu uweza wa kiungu hauna ukomo, na ni wa lazima kwa dhati tukufu iliyotakasika, na kuwa upande wa “malakuti” wa kila kitu unakabiliana nao na kuuelekea bila ya pazia na bila ya dosari, na kuwa huo ni wenye kulingana kwa kuzingatia uwezekano ambao ni kulingana kwa pande mbili, na kwamba mpangilio wa kimaumbile ambao ni sharia kuu ya kimaumbile ni wenye kutii maumbile na kanuni za Allah, na kwamba upande wa “malakuti” ni wa pekee na usio na vizuizi na umahususi tofauti. Hivyo kitu kikubwa zaidi ni kama kidogo zaidi mbele ya uweza huo. Basi haiwezekani kitu kuwa kikubwa kwake vyovyote kiwavyo au kuasi. Hivyo, kuhuisha viumbe hai vyote siku ya ufufuo ni jambo jepesi kwake kama kuhuisha nzi majira ya machipuo. Na hivyo aya tukufu: مَّا خَلْقُكُمْ وَلَا بَعْثُكُمْ إِلَّا كَنَفْسٍ وَاحِدَةٍ Ni jambo la haki na la kweli lililo wazi hapana uongezaji chumvi ndani yake abadan. Na kwa namna hii inathibitika kwetu kuwa mtendaji tunayemzungumzia ni Mweza na hakimzuii kitu.
Kama ambavyo kuna muktadha na sababu ya uwepo wa Kiama na Ufufuo, na kuwa Mtendaji ambaye ataleta ufufuo ni Mweza, vilevile hii dunia ina utayari wa Kiama na ufufuo pia. Basi madai yetu haya ya “utayari wa dunia” yana masuala manne: Kwanza: Kufa kwa ulimwengu huu ni jambo linalowezekana na si muhali. Pili: Kutokea kiuhakika kwa mauti hayo. Tatu: Ni jambo linalowezekana kufufua dunia iliyoboboka na kuijenga kwa sura ya “Akhera”. Nne: Kutokea kiuhakika kwa ufufuo huu na kujenga huku. Suala la Kwanza: Ni jambo linalowezekana kufa kwa ulimwengu huu na kutoweka kwa viumbe hivi. Hiyo ni kuwa ikiwa kitu kipo ndani ya sheria ya ukamilifu, basi katika kila hali kuna kukua na kuongezeka. Na kwamba kukua huku na kuongezeka kunamaanisha kuwa kuna umri wa kimaumbile katika kila hali, na kuwa umri wa kimaumbile unamaanisha kuwa kwa hali yoyote una mwisho wa kimaumbile. Na hii ina maana kuwa vitu vyote haviwezi kuokoka na mauti. Na hili limethibiti kwa utafiti wa jumla na kufuatilia kupana. Naam, kama ambavyo mwanadamu ni ulimwengu mdogo hana budi kuangamia, pia ulimwengu ni mwanadamu mkubwa hawezi kujinasua na shiko la mauti, hana budi kufa, kisha kufufuliwa, au kulala na kufumbua macho yake alfajiri ya siku ya ufufuo. Na kama ambavyo mti ambao ni nakala ndogo ya viumbe hauwezi kuokoka kutokana na kutoweka na kubomoka, vilevile mnyororo wa viumbe vilivyotokana na mti wa viumbe hauwezi kuokoka kutokana na kuchanika na kutoweka kwa ajili ya kujengwa na kufanywa upya. Na lau kama haikotokea kwa dunia kabla ya mwisho wake wa kimaumbile, na kwa idhini ya Allah, tukio lenye kuangamiza au maradhi ya nje, au Muumba wake Mwenye hekima hakuharibu mpangilio wake, basi hapana shaka – kwa hesabu ya kisayansi – kuwa itakuja siku ambayo mwangwi utakariri humo: إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ وَإِذَا النُّجُومُ انكَدَرَتْ وَإِذَا الْجِبَالُ سُيِّرَتْ ﴿إِذَا السَّمَاء انفَطَرَتْ (١) وَإِذَا الْكَوَاكِبُ انتَثَرَتْ (٢) وَإِذَا الْبِحَارُ فُجِّرَتْ (٣)﴾ Wakati huo maana za aya hizo na siri zake vitadhihiri kwa idhini ya Mweza wa azali. Na kwamba hii dunia ambayo ni kama mwanadamu mkubwa itaanza kulewa, kugeukageuka na kukoroma kwa sauti ya ajabu kisha itapiga kelele kwa sauti ya juu na kubwa itakayojaa angani... Kisha itakufa na kufufuliwa kwa idhini ya Allah… Suala la Ishara la Kina Kama ilivyokuwa lafudhi nzito inaleta madhara kwenye maana, na kiini kinakuwa na nguvu kuliko ganda, na roho inadhoofika kwa ajili ya mwili, na mwili unadhoofika kwa ajili ya nguvu ya roho... Vilevile ulimwengu wetu huu uliyojaa, kila masanduku ya uhai yanapotenda yanakuwa mepesi na kulainika katika njia ya ulimwengu mzuri... ambao ni Akhera… Uweza wenye kuumba kwa harakati zake za ajabu unazambaza nuru ya uhai katika sehemu zilizokufa, ngumu na nyingi zilizozimika na hivyo kuziyeyesha na kuzilainisha na kuziangaza sehemu hizo kwa nuru ya uhai huo ili ukweli wake upate nguvu na uwe tayari kwa ulimwengu mzuri... Namaanisha Akhera. Naam, ukweli vyovyote uwavyo dhaifu haufi abadani na wala haiwezekani kufutwa kama picha, bali unatembea na kuzunguka kwenye picha, utambulisho na miundo tofauti, kwani unakua na kudhihiri kila unavyoendelea, kinyume na ganda na picha, kwani vinadhoofika na kuchanika na kuwa upya ili vidhihiri katika pambo zuri na jipya linaloendana na nguzo za ukweli zilizo thabiti zenye kukua na kubwa. Basi ukweli na picha vinanasibiana kinyume katika kuzidi na kupungua. Yaani kila picha inavyokuwa ngumu ukweli unakuwa mlaini, na kila picha inavyodhoofika ukweli unapata nguvu kwa kiasi hich hicho. Na hii ni kanuni enevu kwa vitu vyote viingiavyo kwenye kanuni ya kukamilika. Itakuja ile zama ambayo kwa idhini ya Muumba Mtukufu – ulimwengu wa kushuhudiwa ambao ni picha ya ukweli mkuu wa viumbe na ganda lake utachanika, na kwa hiyo utafanyika upya kwa sura nzuri zaidi, na hapo itathibiti hekima ya aya tukufu: يَوْمَ تُبَدَّلُ الأَرْضُ غَيْرَ الأَرْضِ... Tunafupicha kutokana na yaliyotangulia: Kwamba mauti ya dunia na kubomoka kwake ni jambo linalowezekana, hapana shaka kabisa katika hilo. Suala la Pili: Kutokea mauti ya dunia kwa uhakika. Na ushahidi wa suala hili ni: Kuafikiana kwa dini zote za mbinguni, na ushuhuda wa kila maumbile salama, na kinachoashiriwa na mabadiliko ya viumbe hivi, na kufa kwa limwengu zenye uhai na zenye kutembea, nayo ni kwa idadi ya zama na miaka, katika nyumba ya ugeni wa dunia hii... Yote hayo ni ishara na dalili za kufa kwa dunia yetu yenyewe. Na ukitaka kujenga picha ya sakarati ya dunia kama aya tukufu zinavyoashiria, basi zingatia katika sehemu za ulimwengu huu ambazo ni zenye kufungamana baadhi yake kwa nyingine kwa mpangilio wa kina na wa juu, na kushikamana kwa mfungamano mzuri wa kina na mwepesi, ni zenye mpangilio madhubuti kiasi kwamba sayari moja ikipokea amri ya “kuwa” au “toka katika njia yako”, basi ulimwengu wote unasumbuka na kulewa. Basi nyota na sayari zainagongana na kutikisika kwa sauti ya mamilioni ya mizinga, na kurusha cheche ya moto mfano wa ardhi yetu hii, bali kubwa zaidi ya ardhi katika anga pana na milima kupeperuka na bahari kuunguzwa... Hivyo ardhi huwa tambarare. Na namna hii Mweza wa azali anautikisa ulimwengu kwa kifo hichi, na kuuchanganya na kulewa huku na maumbile yote kutikisika na viumbe kupambanuka baadhi yake kutokana na vingine... Basi Jahanamu huboreka na kupata thamani kwa watu wake na mada yake. Na Pepo hudhihiri na kuwekwa karibu ikikusanya mazuri yake ikiyapata kutokana na vipengele vyake vinavyoendana nayo... Na kutokea kwa ulimwengu wa Akhera kwa ajili ya uwepo wa milele. Suala la Tatu: Uwezekano wa kuufufua ulimwengu ambao utakufa. Kama tulivyothibitisha huko nyuma katika msingi wa pili kuwa hakuna upungufu kabisa katika uweza wa kiungu, na kwamba sababu ni yenye nguvu sana ya uwepo wa Akhera, na kuwa suala hili lenyewe ni katika yanayowezekana. Ikiwa kuna sababu ya nguvu kwa suala linalowezekana, na kuwa mtendaji ni Mweza wa uweza usio na kikomo, basi halitazamwi kuwa ni katika yanayowezekana, bali ni jambo lenye kutokea kikweli. Nukta ya Ishara Tukiutazama ulimwengu huu kwa kina na mazingatio, tutagundua kuwa ndani yake kuna vipengele viwili vinavyokunjuka katika pande zote, kwa mizizi yenye kutofautiana; kama kheri na shari, uzuri na ubaya, manufaa na madhara, ukamilifu na upungufu, mwanga na kiza, uongofu na upotevu, nuru na moto, imani na ukafiri, utii na uasi, hofu na upendo... Vinyume hivi vinagongana vyenyewe kwa vyenyewe kwa matokeo yake na athari zake vikionesha mabadiliko bila ya kukoma kana kwamba vinajiandaa na ulimwengu mwingine. Hapana budi kuwa matokeo na mwisho wa vipengele hivi viwili vyenye kukinzana vitafika milele na kupambanuka na kutofautiana vyenyewe kwa vyenyewe huko. Na hapo vitadhihiri katika muundo wa Pepo na Moto... Na ilivyokuwa ulimwengu wa kubaki utajengwa kutokana na ulimwengu huu huu wa kutoweka, basi vipengele vya msingi vya ulimwengu wetu bila ya shaka vitapelekwa na kutumwa kwenye kubakia na umilele. Naam, Moto na Pepo ni matunda ya tawi lenye kuning’inia kuelekea katika umilele la mti wa uumbaji. Viwili hivyo ni matokeo ya mnyororo huu wa viumbe. Navyo ni hazina ya mtiririko wa mambo ya kiungu. Navyo ni madimbwi ya mawimbi ya vilivyopo vyenye kuelekea katika umilele. Navyo ni madhihirisho mawili katika madhihirisho ya upole na kuteza nguvu. Mkono wa uweza unapoutikisa kwa nguvu ulimwengu huu, madimbwi mawili hujaa kwa maada na vipengele vinavyonasibiana na kila moja ya madimbwi hayo. Kuiweka Wazi Nukta Hii ya Ishara: Kwamba Mwenye hekima wa azali kwa muktadha wa hekima yake ya azali na uangalizi wake wa milele, ameuumba ulimwengu huu ili uwe ni mahali pa majaribio na uwanja wa mtihani, na kioo cha majina yake mazuri na ukurasa wa kalamu ya uweza wake na kadari yake. Basi majaribio na mtihani ni sababu ya kukua na kuongezeka. Navyo ni sababu ya kudhihiri kwa maandalizi ya kimaumbile, na kudhihiri kwa maandalizi ni sababu ya kudhihiri kwa utayari. Na kudhihiri kwa utayari ni sababu ya kudhihiri kwa ukweli wenye uwiano. Na kweli hizi zenye uwiano ni sababu ya kudhihiri kwa madhihirisho ya nakshi za majina mazuri ya Muumba mtukufu na kuwageuza viumbe kuwa katika sura ya maandishi ya Mkusudiwa wa haja Mola Mlezi. Na namna hii, hakika siri hii ya taklifu na hekima ya mtihani inapelekea katika kuchuja viini vya roho za juu ambazo ni kama almasi, kutokana na mada za roho duni ambazo ni kama mkaa, na kuzipambanua baadhi yake kutokana na nyingine. Kwa mfano wa siri hizi zilizotangulia, na tusizozijua katika hekima za kina na nzuri, Mwenye hekima na Mweza ameuleta ulimwengu kwa sura yake hii, na akataka kubadilika kwake ni kwa ajili ya hekima na sababu hizo. Na kwa ajili ya mabadiliko na mageuzi amechanganya vinyume baadhi yake pamoja na vingine kwa hekima, na akavifanya vikabiliane wenyewe kwa wenyewe. Hivyo, vyenye madhara vimechanganywa na vyenye manufaa, na shari zimeingiliana na kheri, na mabaya yamekusanyika na mazuri... Na namna hii mkono wa uweza umechanganya vinyume na kuvifanya viumbe viwe ni vyenye kufuata kanuni ya mabadiliko na sheria ya mageuzi na ukamilifu. Kisha baraza la mtihani lilipoisha na wakati wa majaribio kuisha, na majina mazuri kudhihirisha hukumu yake, na kalamu ya kadari kutimiza maandishi yake, na uweza kukamilisha nakshi za kuumba kwake vizuri, na viumbe kutimiza nyadhifa zake, na viumbe kumaliza kazi zake, na kila kitu kueleza maana na makusudio yake, na dunia kuotesha mavuno ya Akhera, na ardhi kuonesha miujiza yote ya uweza na maajabu ya ufundi wa Muumba na Mweza, na ulimwengu huu wenye kutoweka kuthibitisha mabango ya mandhari za kudumu juu ya mkanda wa zama... Hapo hekima ya milele na uangalizi wa azali wa Mwenye utukufu na ukarimu unalazimu kudhihiri kwa hakika za matokeo ya mtihani na majaribio hayo, na hakika za madhihirisho ya majina hayo mazuri, na hakika za maandishi ya kalamu hiyo ya kadari, na misingi ya vielelezo hivyo vya uzuri wa ufundi wake (s.w.) na faida na makusudio ya nyadhifa hizo za vilivyopo, na malipo ya huduma na kazi hizo kwa viumbe, na hakika za maana ya maneno hayo ambayo kitabu cha ulimwengu kimejuulisha, na kudhihiri kwa mashuke ya mbegu za maandalizi ya kimaumbile, na kufunguliwa milango ya mahakama kuu, na kudhihirisha mandhari za kupigiwa mfano zilizochukuliwa duniani, na kuyachanachana mapazia ya sababu za dhahiri, na kila kitu kujisalimisha moja kwa moja kwa amri ya Muumba wake Mwenye utukufu… Na siku utashi wake utakapoelekea kudhihirisha hakika zilizotajwa ili uokoe viumbe kutokana na mageuzi ya mabadiliko na kutoweka na kuwatunuku umilele, na ili upambanue baina ya vinyume hivyo, na kutofautisha baina ya sababu za mabadiliko na maada za kutofautiana, Allah (s.w.) atasimamisha Kiama bila ya shaka, na atachekecha mambo ili kudhihirisha matokeo hayo. Na Jahanamu mwisho wake itachukua sura ya milele, mbaya na ya kutisha, na itawatisha viongozi wake kwa kusema: وَامْتَازُوا الْيَوْمَ أَيُّهَا الْمُجْرِمُونَ Na Pepo itadhihiri kwa uzuri wake na shamrashamra zake za milele na walinzi wake watasema kuwaambia watu wake: سَلَامٌ عَلَيْكُمْ طِبْتُمْ فَادْخُلُوهَا خَالِدِينَ Na Mwenye uweza na Mwenye hekima kwa uweza wake uliyo kamili atawapa watu wa nyumba hizi mbili za milele uwepo thabiti wa kudumu na wa milele hautapatwa na mabadiliko, uharibifu, uchakavu wala kutoweka. Hakuna sababu za mabadiliko yenye kupelekea kutoweka, kama ilivyotolewa hoja katika “Neno la Ishirini na Nane, Ngazi ya Kwanza, Swali la Pili”. Suala la Nne: Ni kwamba kufufuliwa kutatokea bila ya shaka. Naam, hakika dunia baada ya kuteketea na kufa kwake itafufuliwa kuwa ni “Akhera”. Na kwamba Muumba Mweza ambaye ameiumba kwa mara ya kwanza ataijenga vizuri zaidi ya hapo mwanzo baada ya kubomoka kwake, na ataifanya kuwa ni nyumba katika nyumba za Akhera. Na dalili kubwa juu ya hili ni Qur’an tukufu kwanza, kwa aya zake zote ambazo zinakusanya maelfu ya hoja za kiakili, na vitabu vyote vya mbinguni vinavyoafikiana na Qur’an tukufu kwenye suala hili, na pia sifa za utukufu na uzuri wa kiungu na majina yote mazuri ya dhati tukufu, vyote hivyo vinajulisha kwa dalili ya hakika juu ya kutokea kwa Ufufuo huu. Na pia amri zake zote (s.w.) zilizofunuliwa kwa Manabii na Mitume wote (a.s.) na ambazo ameahidi kwa amri hizo kutokea kwa Ufufuo na Kiama. Na kwa kuwa ameahidi, basi atatimiza ahadi yake bila ya shaka. (Rejea hakika ya Nane ya Neno la Kumi), na pia yote aliyoyaeleza Nabii Ummiy Muhammad (s.a.w.) na ana maelfu ya miujiza, kuhusu kutokea kwa ufufuo na wanaafikiana nae Manabii, Mitume, wateule, mawalii, na wakweli wote katika kutokea kwa huu ufufuo. Hii ni pamoja na tunayoelezwa na aya zote za uumbaji kwenye ulimwengu huu mkubwa juu ya kutokea kwa ufufuo huu. Muhtasari: Kwamba hakika zote za “Neno la Kumi”, na hoja zote “hasa” katika “Ngazi ya Pili ya Neno la Ishirini na Nane” ambayo imeandikwa kwa lugha ya Kiarabu katika “Al-Mathnawy Al-Araby An-Nuury”; vimedhihirisha kwa uhakika kamili, kama kuchomoza kwa jua baada ya kuzama kwake, kwamba jua la ukweli litachomoza kwa sura ya uhai wa Akhera baada ya kuzama kwa uhai wa kidunia. Na namna hii, yote tuliyoyaeleza tokea mwanzoni katika misingi minne, ilikuwa ni kutokana na jina la “Al-Hakim” na kupata faida kutokana na baraka ya Qur’an tukufu ili kuuandaa moyo kukubali na kuiweka tayari nafsi kusalimu amri na kuhudhurishwa moyo kutii. Na sisi ni kina nani hata tuzungumizie jambo kama hili. Kauli ya mwisho ni ile ambayo Mmiliki wa dunia hii anaisema, na Muumba wa huu ulimwengu, na Mola Mlezi wa ulimwengu huu!? Ama sisi hatuna nafasi yoyote isipokuwa kunyenyekea, kunyamaza na kutii... Anapozungumza Mola wa mbingu na ardhi, basi ni nani anastahiki zaidi kuzungumza kuliko Yeye (s.w.)?! Muumba huyu Mkarimu anaelekeza mazungumzo ya azali kwa safu zote za makundi ya viumbe katika eneo la msikiti wa dunia na madrasa ya ardhi vilivyojificha nyuma ya zama, na ambaye anautikisa ulimwengu wote: إِذَا زُلْزِلَتِ الْأَرْضُ زِلْزَالَهَا وَأَخْرَجَتِ الْأَرْضُ أَثْقَالَهَا ۞وَقَالَ الْإِنسَانُ مَا لَهَا ۞يَوْمَئِذٍ تُحَدِّثُ أَخْبَارَهَا ۞بِأَنَّ رَبَّكَ أَوْحَى لَهَا ۞يَوْمَئِذٍ يَصْدُرُ النَّاسُ أَشْتَاتًا لِّيُرَوْا أَعْمَالَهُمْ ۞فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُ ۞وَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُ Na mazungumzo ambayo yamewafurahisha viumbe wote na kuchochea shauku ndani mwao ni: وَبَشِّرِ الَّذِين آمَنُواْ وَعَمِلُواْ الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الأَنْهَارُ كُلَّمَا رُزِقُواْ مِنْهَا مِن ثَمَرَةٍ رِّزْقاً قَالُواْ هَذَا الَّذِي رُزِقْنَا مِن قَبْلُ وَأُتُواْ بِهِ مُتَشَابِهاً وَلَهُمْ فِيهَا أَزْوَاجٌ مُّطَهَّرَةٌ وَهُمْ فِيهَا خَالِدُونَ Basi ni juu yetu kusikiliza na kunyamaza mbele ya mazungumzo hayo yanayotoka kwa Mfalme wa wafalme na Mola Mlezi wa Dunia na Akhera na tuseme: Tumeamini na kusadiki. سُب۟حَانَكَ لَا عِل۟مَ لَنَٓا اِلَّا مَا عَلَّم۟تَنَٓا اِنَّكَ اَن۟تَ ال۟عَلٖيمُ ال۟حَكٖيمُ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذ۟نَٓا اِن۟ نَسٖينَٓا اَو۟ اَخ۟طَا۟نَا اَللّٰهُمَّ صَلِّ عَلٰى سَيِّدِنَا مُحَمَّدٍ وَ عَلٰى اٰلِ سَيِّدِنَا مُحَمَّدٍ كَمَا صَلَّي۟تَ عَلٰى سَيِّدِنَا اِب۟رَاهٖيمَ وَ عَلٰى اٰلِ سَيِّدِنَا اِب۟رَاهٖيمَ اِنَّكَ حَمٖيدٌ مَجٖيدٌ

