Sözler

The Thirty-Third Word

Source: risaleinur multilingual dataset, risale.site source · Risale-Nur multilingual research corpus
Risale reading plan
§1

Nalo ni madirisha thelathini na tatu Neno hili ni la (Thelathini na tatu) kwa upande mmoja na ni (Andiko la thelathini na tatu) kwa upande mwingine. بِسْمِ اللّٰهِ الرَّحْمٰنِ الرَّح۪يمِ سَنُرٖيهِم۟ اٰيَاتِنَا فِى ال۟اٰفَاقِ وَفٖٓى اَن۟فُسِهِم۟ حَتّٰى يَتَبَيَّنَ لَهُم۟ اَنَّهُ ال۟حَقُّ اَوَلَم۟ يَك۟فِ بِرَبِّكَ اَنَّهُ عَلٰى كُلِّ شَى۟ءٍ شَهٖيدٌ Swali: Tunataraji utufafanulie ufafanuzi wa jumla na muhtasari, yaliyomo katika aya hizi mbili zenye kukusanya dalili juu ya kupasa kwa uwepo wa Allah (s.w), na juu ya umoja wake na sifa zake tukufu na mambo yake ya kiungu, sawa ikiwa upande wa dalili katika ulimwengu mdogo au ulimwengu mkubwa, yaani katika mwanadamu au ulimwengu. Hakika wamefurutu wakanaji na kupitiliza katika upotevu wao hata wameanza kudhihirisha kauli yao: Hadi lini tuna nyanyua mikono yetu na kuomba: (Naye juu ya kila jambo ni mweza)? Jibu: Hakika kilichoandikwa katika kitabu cha (Maneno) katika (Maneno thelathini na tatu), sio isipokuwa matone thelathini na tatu yametona kutoka katika neema ya aya hii tukufu. Mnaweza kukuta kinacho wakinaisheni kwa kuzirejea. Ama hapa tutaashiria kwa kiasi cha kuashiria tu katika vitone vya tone kutoka katika bahari hiyo kubwa. Tunatangulizia mfano: Hakika ambaye anamiliki uweza wa muujiza na umahiri wa hali ya juu ikiwa anataka kujenga kasri kubwa hapana shaka kwamba kabla ya kila kitu anasimika kwa mpangilio mzuri, na kuweka misingi yake kwa hekima kamili, na kuiratibu kwa utaratibu unaowiana na malengo yaliyojengwa kwa ajili yake na matokeo yanayotegemewa. Kisha anaanza kuigawa na kuigawa kwa umahiri na ufundi katika sehemu na duru na vyumba, kisha tunamwona anatazama vyumba hivyo na kuvipamba kwa maajabu ya nakshi nzuri, kisha anainawirisha kila nguzo katika nguzo kwa taa kubwa za umeme, kisha kwa ajili ya kufanya upya hisani zake na kudhihirisha umahiri wake katika vitu na kuzibadili na kuzigeuza. Kisha katika kila chumba kati ya hivyo akafunga simu maalum inayowasiliana na makamo yake, na anafungua dirisha katika kila chumba chake kupitia hiyo huonekana makamo yake ya juu. Na kwa mfano huu - na Allah ana Mfano wa juu - basi fundi mtukufu, ambaye ana majina elfu moja na jina moja katika majina mazuri, mifano: Mtawala mwenye hekima zote, Mwadilifu mwenye kuhukumu na Muumba mtukufu ambaye hakuna mithili yake kitu chochote. Ametaka, na kutaka kwake kunatimia, kuumba mti mkubwa wa viumbe, na kupatisha kasri ya ulimwengu ya ajabu. Huu ulimwengu mkubwa, akaweka misingi ya kasri hiyo na mashina ya mti huo ndani ya siku sita kwa taratibu za hekima yake yenye kuzungukia kila kitu na kanuni za elimu yake ya kiazali. Kisha akaisawiri kwa uzuri wa sura kwa taratibu za Qadhaa na Kadari na kuipambanua upambanuzi madhubuti katika matabaka na matawi ya juu na chini. Kisha alitazama katika kila kundi katika viumbe na kila tabaka zake kwa taratibu za uangalizi na hisani. Kisha akapamba kila kitu na kila ulimwengu kwa uzuri unao wiana nao – mathalani amepamba mbingu kwa nyota na akapendezesha ardhi kwa maua – kisha akanawirisha medani za kanuni hizo za kiujumla na anga za taratibu hizo enevu kwa midhihirisho ya majina ya Allah (s.w), kisha akawapa msaada ambao wanamwomba msaada kutokana na dhiki za kanuni hizo za jumla, akawakabili kwa jina ﴾ الرحمن الرحيم ﴿, yaani ameweka ndani ya kanuni zake za jumla na taratibu zake za jumla katika hisani maalum na misaada maalum na midhihirisho maalum ambayo inawezesha kila kitu kumwelekea (s.w) kila wakati na kumwomba kila kinachokihitaji. Na kufungua kila nyumba, na kila tabaka, na kila ulimwengu, na kila kundi, na kila mtu, na kila kitu madirisha inakiangalia na kukidhihirisha, yaani inabainisha uwepo wake wa haki na Upekee wake, akaweka simu katika kila moyo inawasiliana naye. Na baada ya hayo, hatutaingiza nafsi yetu katika jambo tusilokuwa na uwezo nalo katika kutafiti madirisha haya ambayo hayahesabiki wala hayadhibitiki kwa idadi, bali tunaiacha katika elimu ya Allah (s.w) yenye kuzungukia kila kitu, isipokuwa ishara tunayoashiria za muhtasari tu katika madirisha thelathini na tatu, iliyong’ara katika ming’ao ya aya za Qur’an tukufu likawa neno la (Thelathini na tatu) au (Andiko la thelathini na tatu) na tumeyafupisha ndani ya madirisha thelathini na tatu kwa kutabaruku na dhikiri ambazo zinakuja baada ya swala tano. Na fafanuzi zake tunaziacha katika Risala nyingine.

§2

Tunashuhudia katika vilivyomo na hasa vilivyo hai kati yao kuhitajia mahitaji mbalimbali na matakwa anuwai yasiyohesabika. Hakika ya mahitaji hayo hupelekwa huko kwa namna isiyotarajiwa, na matakwa huiendea kila wakati wake muwafaka. Hali ya kujua kwamba mikono ya haja inashindwa kufikia mahitaji yake ya chini ukiachilia mbali malengo yake mapana sana na makusudio yake. Ukitaka chunguza nafsi yako utaikuta imefungwa mikono miwili upande wa mengi ya lazima kwa milango yako ya fahamu, au kushibisha matakwa yako ya ndani. Basi pimia kwa nafsi yako nafasi za wenye uhai wote, na uvichunguze utakuta kila kiumbe kati yao kinashuhudia ufakiri wake na mahitaji yake yenye kukidhiwa pasina hila wala nguvu kutoka kwake kwa aliye wajibu kuwepo, na vinaashiria kwavyo katika upekee wake (s.w), kama inavyoijulisha kama kukujulisha kwa mwanga wa jua kwa jua lenyewe na inabainisha kwenye akili yenye kufanya insafu kwamba (s.w) yuko katika ukomo wa ukarimu na rehema na ulezi na uendeshaji. Ujinga wako mbaya kiasi gani, na kughafilika kwako kwa laana, ewe mjinga mwenye kughafilika na mwenye kiburi, vipi utafasiri utendaji kazi huu wenye hekima na busara na hali ya rehema?! Je kwa Asili kiziwi? Au kwa nguvu pofu? Au kwa sadfa ya holela? Au kwa sababu zisizo na uhai zisizo na uwezo?

§3

Wakati ambapo vitu vinasita kati ya uwepo na kushika umbo na kutahayari kati ya njia za yamkini na uwezekano zisizokoma, tahamaki zinatunukiwa sura yenye kuvipambanua, upeo wa mpangilio na hekima. Chunguza alama zenye kutenganisha zilizopo katika uso wa kila mwanadamu, zile alama ambazo zinapambanua kila mmoja katika wana wa jinsi yake, na itazame kwa makini milango ya fahamu iliyo dhahiri aliyoiweka humo kwa hekima ya ajabu na hisia za ndani, je hilo halithibitishi kuwa uso huu mdogo ni ishara yenye kuangaza ya upweke? Kama ulivyo kila uso unajulisha - kwa mamia ya dalili - juu ya kuwepo kwa mtengenezaji mwenye hekima, na unashuhudia upekee wake, basi vilevile jumla ya sura, na katika vilivyo hai vyote vinabainisha kwa uoni mkali kuwa hivyo ni ishara kuu ya dhahiri ya muumba mmoja wa pekee. Basi ewe mwenye kukanusha, je unaweza kuzuia alama hizi na mihuri hii ambayo haiigwi, au kuegemezwa Ishara kuu kwa wa pekee mwenye kutegemewa kwa kila haja ishara angavu katika mkusanyiko wake kwa asiye kuwa muumba wake mwenye kutia sura?

§4

Hakika ya aina za mimea, na makundi ya wanyama, yenye kuenea juu ya Ardhi ni zaidi ya mia nne elfu , na kama kwamba ni jeshi kubwa, basi tunaona hakika kila aina katika jeshi hili lina riziki yake tofauti na ya lingine na sura yake tofauti, na silaha zake anuwai na mavazi yao yenye kupambanuka na mazoezi yake mahususi, na ruhusa zao tofauti kuachana na huduma, na yote haya yanapita katika mpangilio uliowekwa vema, na kulingana na makadirio madhubuti. Basi kuongoza jeshi hili kubwa, na kulea watu wake, bila ya kumsahau hata mmoja na bila ya kuchanganya, hakika ni ishara yenye kuangaza kama jua ya mmoja wa pekee. Basi ni nani huyu awezaye kunyosha mkono wa kuingilia katika uendeshaji huu wa muujiza minghairi ya mmiliki wake muweza ambaye uweza wake hauna mpaka, na hakuna mipaka ya ujuzi wake, wala hakuna ukomo wa hekima yake! Hii ni kwa sababu ambaye anashindwa kuendesha na kulea aina hizi zenye kuingiliana na nyumati zilizobebana baadhi ndani ya baadhi mkupuo mmoja na katika muda mmoja, anashindwa kiujumla kukutana katika kufanya kiumbe mmoja kati yao, kwani ungepatikana mwingiliano katika yeyote kati yao athari yake ingedhihiri, na upungufu na kasoro vingebainika فَارْجِعِ الْبَصَرَ هَلْ تَرَى مِن فُطُورٍ Hakuna dosari wala upungufu, kwa hiyo hapana mshirika.

§5

Ni kule kuitika kwa Muumba dua zote zinazotokana na ulimi wa utayari wa mbegu, na kwa ulimi wa mahitaji ya wanyama, na kwa ulimi kwa wenye kuhemewa kati ya wanadamu. Naam, hakika kujibu maombi yote haya yasiyo na mpaka kujibu kimatendo, kupo wazi mbele yetu, tunakushuhudia kwa kuona kwa macho. Basi kama yote haya yanavyoashiria kwa (Aliye wajibu kuwepo) na katika upekee, hakika jumla ya miitikio hiyo kwa uwazi inajulisha na kwa kipimo kipana zaidi na kikubwa zaidi juu ya Muumba Mwingi wa Rehema Mkarimu sana mwenye kuitikia, kuyaelekeza macho kwake (s.w).

§6

Tukiangalia vitu kwa makini, na hasa vilivyo hai, tunavishuhudia kana kwamba vikiwa vimetoka punde tu kutoka katika mkono wa Muumba wake, Na vimedhihiri katika uwepo kudhihiri kwa ghafla. Wakati ambapo vitu vilivyochangamanishwa vinatakikana kuwa kwa wakati na kwa haraka vyenye muundo mwepesi na yenye umbo lililovurugwa, na bila ya kuwekwa vema, tunaviona vinaumbwa katika umbo lililo bora sana na la kupendeza zaidi, kuweka vema huku na kupendezesha ambako kunahitajia umahiri wa hali ya juu. Na tunaviona katika nakshi ya kuvutia kabisa na sura madhubuti, kuvutia huku na umadhubuti ambako kunahitajia subira kubwa na muda mrefu. Tunaviona katika mapambo ya kifahari na uzuri wenye kushika nyoyo, mapambo haya na uzuri ambavyo vinahitajia zana za urembo anuwai, na nyenzo nyingi za mapambo. Basi uwekaji vema huu wa kimuujiza, na sura ya ajabu, na umbo lililopangika, na upendezeshaji wa haraka, vyote hivyo vinashuhudia juu ya uwepo wa Mtengenezaji Mwenye Hekima zote, na unaashiria juu ya upekee wake na Ulezi wake. Kama ilivyo jumla yake kwa uwazi inabainisha (Aliye wajibu kuwepo) mweza wa kila kitu Mwingi wa Hekima, na inabainisha upekee wake (s.w). Basi ewe mwenye kughafilika na mola wako, mwenye kutahayari katika jambo la vyenye kuwepo. Haya, utafafanua na kulifasiri vipi jambo hili? Je utalifasiri kwa asili yenye kushindwa zuzu jinga? Au kwa ujinga wako unataka kutenda kosa lisilo na mipaka, uivike asili sifa za Uungu, na uinasibishie kwa hoja hii miujiza ya uweza wa yule Mtengenezaji Mtukufu aliyetakasika na kila upungufu na aibu, utende muhali elfu moja na mmoja.

§7

اِنَّ فٖى خَل۟قِ السَّمٰوَاتِ وَال۟اَر۟ضِ وَاخ۟تِلَافِ الَّي۟لِ وَالنَّهَارِ وَال۟فُل۟كِ الَّتٖى تَج۟رٖى فِى ال۟بَح۟رِ بِمَا يَن۟فَعُ النَّاسَ وَمَٓا اَن۟زَلَ اللّٰهُ مِنَ السَّمَٓاءِ مِن۟ مَٓاءٍ فَاَح۟يَا بِهِ ال۟اَر۟ضَ بَع۟دَ مَو۟تِهَا وَبَثَّ فٖيهَا مِن۟ كُلِّ دَٓابَّةٍ وَتَص۟رٖيفِ الرِّيَاحِ وَالسَّحَابِ ال۟مُسَخَّرِ بَي۟نَ السَّمَٓاءِ وَال۟اَر۟ضِ لَاٰيَاتٍ لِقَو۟مٍ يَع۟قِلُونَ Aya hii tukufu kama inavyobainisha kuwepo kwa Allah (s.w) na kujulisha upekee wake, aya hiyo kwa hakika ni dirisha kubwa sana linaangalia jina tukufu katika majina mazuri. Na ubora wa muhtasari wake: Hakika limwengu zote za uwepo za juu na za chini, kati yake zinajulisha kwa ndimi tofauti juu ya matokeo mamoja, yaani juu ya Ubwana Mlezi wa Mtengenezaji mwingi wa hekima Mmoja, na kama ifutavyo: Hakika kutembea kwa maumbo makubwa (Mbinguni) kwa ukomo wa mpangilio kwa kufikia shabaha tukufu, na matokeo ya hali ya juu - kwa taarifa ya elimu ya falaki - hakika si vingine bali kunajulisha juu ya kuwepo kwa Mungu Mweza mwenye Utukufu na kunashuhudia juu ya upekee wake na Ubwana Ulezi wake kamili. Kama kwamba mabadiliko yenye kupangika katika (Ardhi) na yenye kushuhudiwa katika majira ili kupata manufaa makubwa na masilahi mbali mbali - kwa taarifa ya jiografia - hakika si jambo lingine bali inajulisha ujulisho wa wazi juu ya huyo mweza mwenye utukufu, na inashuhudia juu ya upekee wake na ubwana ulezi wake mkamilifu. Kisha (Wanyama) wote ambao wanajaza bara na bahari na ambao riziki ya kila mmoja kati yao inatumwa kwa Rehema kunjufu, na kuvikwa kwa nguo anuwai, kwa hekima iliyotimia, na kuandaliwa kwa milango ya fahamu mbalimbali, kwa Ubwana Ulezi mkamilifu, kila moja kati ya hayo inaashiria kwa huyo Mweza mwenye utukufu, na inashuhudia upekee wake, kama ilivyo jumla yake kama yote kwa pamoja inajulisha na kwa kipimo kipana sana adhama ya Uungu mwabudiwa wa haki na ukamilifu wa ubwana ulezi. Na hali vivyo hivyo katika (Mimea) iliyowekwa kwenye mizani na mpangilio ambayo inatandika Ardhi, mabustani na mimea, na kila moja kati ya hayo inajulisha juu ya yule mtengenezaji mwenye hekima zote, na inaashiria upekee wake kwa maua mazuri inayobeba, na matokeo yanayoletwa na maua haya miongoni mwa matunda yenye kuwekwa kwenye mizani, na yaliyomo katika matunda haya miongoni mwa nakshi za kupendeza, kama kila moja kati ya hayo peke yake inajulisha juu ya mtengenezaji hakika jumla yake inadhihirisha uzuri wa rehema yake, na ukamilifu wa ubwana ulezi wake. Kisha hakika matone yenye kutiishwa kwa hekima za kimaumbile, na kwa ajili ya shabaha za hali ya juu na manufaa matukufu, na faida kemkem, na ambayo yanatumwa kutoka kwenye mawingu mazito yaliyoangikwa kati ya mbingu na ardhi, yanajulisha kwa idadi ya matone juu ya huyo mtengenezaji mwenye hekima zote, na kushuhudia juu ya upweke wake na ukamilifu wa ubwana ulezi wake. Kama ilivyo kwamba (Milima) mikubwa, na yaliyomo ndani yake miongoni mwa madini, na sifa mahususi za kila moja kati yao, na yaliyowekwa humo katika shabaha mbali mbali, na yaliyoandaliwa kwa ajili ya maslahi mbali mbali, kila moja kati yao kwa upekee na kwa ujumla wake kwa pamoja, yanajulisha ujulisho wenye nguvu kuliko majabali marefu juu ya yule mtengenezaji mwenye hekima zote na juu ya upekee na ukamilifu wa ubwana ulezi wake. Kisha hakika ya aina za (Maua) mazuri na maridadi yaliyotawanywa kwenye vilima na vizio vya milima na majangwa, na hali zimeongezewa mvuto na uzuri, kila moja kati ya hivyo inajulisha juu ya upekee wake, mfano wa kwamba majumuisho yake ya jumla inajulisha utukufu wa ufalme wake na ukamilifu wa ubwana ulezi wake. Kisha aina za (Majani) na maumbo yake yaliyoratibiwa, na mitetemeko yake ya upole ya kuvutia katika mimea na miti na majani kwa ujumla inashuhudia kwa idadi ya majani juu ya huyo mtengenezaji mwingi wa hekima, na juu ya upekee wake na ukamilifu wa ubwana ulezi wake. Kisha hakika (Kukua kwa miili) kwa hatua zenye kulenga na kuongozwa, na kutayarishwa kila moja kwa aina ya mifumo inayoelekea kwa pamoja katika kuunda matunda, na kana kwamba ni mwelekeo wa kihisia, unafanya kila mwili wenye kukua kwa sehemu zake na ujumla wake, unamshuhudia huyo fundi Mwingi wa hekima na kuashiria juu ya upekee wake, na inajulisha ujulisho mkubwa juu ya uweza wake unaozungukia kila kitu, na hekima yake yenye kuenea, na ufundi wake mzuri, na ubwana ulezi wake uliokamilika. Kisha kuiweka (Nafsi) kwenye mwili, na kuituliza roho kwa kila kiumbe cha kiunyama kwa hekima timilifu, na kumpa silaha anuwai, na kumpa zana mbali mbali kwa mpangilio kamili, na kumwelekeza katika majukumu matukufu, na kumtumikisha katika nyadhifa anuwai kwa hekima timilifu, inaashiria kwa ishara kwa idadi ya wanyama bali kwa idadi ya mifumo yake na viungo vyake katika uwepo wa mtengenezaji mwingi wa hekima, na inashuhudia juu ya upekee wake, mfano ilivyo jumla yake ya jumla, inajulisha ujulisho angavu juu ya uzuri wa rehema yake na ukamilifu wa ubwana ulezi. Kisha (ilhamu) zote za kighaibu ambazo zinaelekeza nyoyo za watu na kuzifahamisha kielimu na hakika, na zinamfundisha mnyama kuongoza katika kupata mahitaji yake mbali mbali anayoyahitaji. Ilhamu hizi za kighaibu kwa aina zake mbalimbali zinamtambulisha kila mwenye busara kuwepo kwa bwana mlezi mwingi wa rehema na inaashiria juu ya ubwana ulezi wake. Kisha (Hisia) na milango yote ya fahamu mbali mbali - iliyo dhahiri na ya ndani - inavuna maua ya kimaanawy kutoka katika bustani za ulimwengu, na kila mlango wa fahamu katika milango hiyo kuwa ni ufunguo wa ulimwengu katika limwengu katika ulimwengu mkunjufu, zinajulisha kama jua juu ya kuwepo kwa mtengenezaji mwenye hekima zote Mjuzi wa kila kitu, Muumba mwingi wa rehema na Mruzuku Mkarimu sana, na zinashuhudia juu ya umoja na upekee wake na ukamilifu wa ubwana ulezi wake. Basi haya madirisha kumi na mbili, kila moja kati ya hayo yanawakilisha upande mmoja wa dirisha kunjufu, basi yanajulisha kwa namna kumi na mbili katika aina za hakika juu ya upekee wa Allah (s.w), na upekee wa ukamilifu wa ubwana ulezi wake. Basi ewe mwongo mwovu!. Vipi utaweza kuzuia dirisha hili kunjufu sawa na ukunjufu wa ardhi, bali ni kunjufu ukunjufu wa mzunguko wake wa mwaka?!. Na kwa kitu gani utaweza kuzima chanzo cha nuru hii yenye kuangaza kama jua?. na kwa pazia gani katika pazia za kughafilika unaweza kulificha nalo?!.

§8

Hakika kinachodhihiri bayana katika vyote vilivyotengenezwa vyote vilivyotawanywa juu ya kurasa za ulimwengu katika mionekano ya mpangilio na kulingamana kuliko timia, na sura za mapambo na uzuri zinazoumbika, na kinachoshuhudiwa katika wepesi wa ukomo katika kuja kwake katika uwepo na kutamalaki kwake katika uhai, na kushabihiana kuliko nako baadhi kwa baadhi nyingine katika mionekano na ainisho licha ya miitikio yake ya kimaumbile moja kwa matukio ya kiulimwengu, kila moja katika mionekano hii na sifa mahususi ni dalili za wasaa kwa wasaa wa ulimwengu juu ya Muumba mweza, na ushahidi wa kweli juu ya umoja wake (s.w) na uweza wake wa hali zote. Na vivyo hivyo (Kupatisha vyenye kuchangamanishwa) vilivyopangika visivyohesabika wala kudhibitika idadi katika sehemu zisizo hai zenye miundo rahisi, kunashuhudia ushahidi wa kukinaisha kwa idadi ya vyenye kuchangamanishwa juu ya huyo Muumba Mweza aliye wajibu kuwepo (s.w), na inaashiria ishara ya wazi juu ya umoja wake, licha ya kuwa mjumuisho wake wa jumla unabainisha kwa uwazi ukamilifu wa uweza wake na umoja wake. Na vivyo hivyo hakika ya yanayo shuhudiwa katika (Kupambanuka) kuliko wazi na (Kutofautiana) kabisa wakati wa kuja upya kwa viumbe – kwa uchambuzi na uunganishi – licha ya kuwa kwake katika ukomo wa kuchanganyika inajulisha kwa uwazi juu ya yule Mwenye Hekima zote Hekima za hali zote, na Mjuzi wa elimu ya hali zote na mweza uweza wa hali zote, na inaashiria katika kupasa kuwepo kwake (s.w) na ukamilifu wa uweza wake. Basi chukua kwa mfano: Kutoa mashuke kwa punje zilizozikwa katika tumbo la Ardhi, na kukua kwa mashina ya miti katika mimea tofauti na miti yenye kutofautiana, licha ya kuchanganyika na kupishana, na vilevile kupambanuka kwa maada mbalimbali zinazoingia katika mimea na miti anuwai katika majani yenye kushamiri na rangi nzuri, na matunda maridadi licha ya kuchanganyika mno. Bali hata kupambanuka na kugawika visehemu maada za lishe madhubuti zenye kuingia kwenye vyumba vidogo vya mwili kwa hekima kamili uzani madhubuti pamoja na kuchanganyika. Na vilevile kutiishwa kwa (Atomu) zisizo na uhai zisizo jiweza zisizo na ujuzi kwa kutimiza majukumu katika upeo wa mpangilio, utambuzi, uwezo na hekima, na kujaalia ulimwengu wa atomu hali inayoshabihiana na shamba kubwa kila wakati hulimwa humo limwengu, na nyingine huvunwa kwa hekima timamu. Zote hizo ni dalili za wazi juu ya huyo Mweza mwenye utukufu. Na huyo ni Muumba mwenye ukamilifu, na inashuhudia ushahidi wa nguvu juu ya ukamilifu wa uweza wake, na Ubwana Ulezi wake mkuu, na juu ya umoja wake na ukamilifu wa Ubwana Ulezi wake. Na kama hivi njia hizi nne kunjufu zinatupelekea katika dirisha kubwa mno linafunguka katika maarifa ya Kiungu, ambapo kutokana na dirisha hilo linatazama mtazamo wa akili kali juu ya kuwepo kwa Muumba mwingi wa hekima. Basi ewe mwenye kughafilika mwovu kwa kughafilika kwake! Baada ya haya yote ikiwa hukutaka kumwona na maarifa yako jihesabu nafsi yako katika wanyama!

§9

Hakika manabii wote (a.s) ambao ni wenye roho zenye nuru katika sampuli ya mwanadamu wakiegemea miujiza yao ya dhahiri na wazi, na mawalii wote ambao wanawakilisha mihimili ya nyoyo zenye nuru wakitegemea kufunuliwa kwao na karama zao, na wateule wote ambao wanawakilisha wenye akili za kinuru wakiegemea tahakiki zao za kielimu. Wote wanashuhudia juu ya kupasa kuwepo kwa mmoja wa pekee Muumba wa kila kitu, na wanajulisha juu ya ukamilifu wa Ubwana Ulezi wake na umoja wake. Dirisha hili ni kunjufu mno na lenye nuru lenye kuangaza, nalo liko wazi milele ili kudhihirisha makamo hayo ya hali ya juu ya Ubwana Mlezi. Basi ewe Mwenye kukanusha mwenye kutahayari! Unajihesabu kwa kitu gani na kujifaharisha, hata usitegee sikio hakika hizi?! Huenda unadhani kwa kufumba kope zako unaweza kuufanya mchana wa dunia kuwa ni usiku. Eeh, mbali gani!.

§10

Hakika (Ibada) ambazo viumbe wanazitekeleza kwa jumla yake kwa uwazi zinajulisha juu ya Mwaabudiwa wa haki kwa hali zote. Naam, hakika ya utumishi uliotakata ambao malaika wanautekeleza na maruhani kwa jumla, uliothibiti kwa ushahidi ya wale waliovuka katika ulimwengu wa roho miongoni mwa wanadamu, na kuingia ndani kwenye sehemu za ndani za uwepo. Na huko wakakutana na malaika na viumbe wa kiroho, na wamewashuhudia katika ibada zao na tasbihi zao. Na wote wenye uhai kutimiza - vyovyote walivyo - kwa majukumu yao ambayo wameumbiwa kwa ajili yake kwa mpangilio ulio timamu kabisa, na kutekeleza kwao amri za kiungu utekelezaji wa mja mwenye kuamuriwa, na vyote visivyo na roho kutekeleza huduma zake zenye kushika alama ya uja uliokamilika bali utiifu timamu kabisa, hakika ya ibada zote hizi zenye kushuhudiwa zinaashiria kwa Mwaabudiwa wa haki ambaye ni wajibu kuwepo na katika umoja wake. Na kwamba (Maarifa) yote ambayo wajuzi wote wanayabeba yakiwa ni matokeo ya utumishi wao kwa Allah. Na shukurani yenye kuzaa matunda inayotoka ndani ya nyoyo za wenye kushukuru, na dhikiri zenye nuru ambazo zinarutubisha ndimi za wenye kudhikiri, na shukurani ya ziada kwa neema ambayo wanaitamka wenye kuhimidi, na Tawhidi ya hakika yenye kusadikishwa kwa ishara za vyote vilivyomo ambayo wanaitoa wenye kupwekesha, na mapenzi ya kiungu na ashiki yake ya kweli ambayo wanaizagaza wenye kupenda na wenye mahaba ya ndani ya moyo, na matakwa ya muridi wenye ikhlasi kwa ajili ya Allah (s.w), na kushika matakwa yao katika kuyaendea, na kurejea kwa kweli, na tawasali yenye huzuni mbele ya wenye kurejea kwa unyenyekevu. Mionekano yote hii itokanayo kwa wote hawa ambao kila mmoja kati yao anabeba nguvu ya Tawatur na ijmai, inajulisha ujulisho wenye nguvu juu ya kupasa kuwepo huyo mwaabudiwa wa azali, mwenye kujulikana, mwenye kutajwa, mwenye kushukuriwa, mwenye kuhimidiwa, mmoja mwenye kupendwa, mwenye kuraghibiwa na mwenye kukusudiwa, na inajulisha juu ya ukamilifu wa Ubwana Ulezi wake na umoja wake. Kisha hakika ya ibada zote zenye kukubaliwa ambazo wanaabudu kwazo watu wenye kukamilika, na yanayotokana na ibada hizo zenye kuridhiwa miongoni mwa miminiko za kheri na munajat, mambo ya kushuhudiwa na kufunuliwa, yote yanajulisha ujulisho wenye nguvu mno juu ya huyo mwenye kuwepo wa kubakia, na huyo Mwaabudiwa wa milele na juu ya upekee wake na ukamilifu wa Ubwana Ulezi wake. Basi dirisha hili lenye kuangaza na kunjufu mno, linafunguka kutokea pande tatu kufungukia umoja wake.

§11

وَاَن۟زَلَ مِنَ السَّمَٓاءِ مَٓاءً فَاَخ۟رَجَ بِهٖ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِز۟قًا لَكُم۟ وَسَخَّرَ لَكُمُ ال۟فُل۟كَ لِتَج۟رِىَ فِى ال۟بَح۟رِ بِاَم۟رِهٖ وَسَخَّرَ لَكُمُ ال۟اَن۟هَارَ وَسَخَّرَ لَكُمُ الشَّم۟سَ وَال۟قَمَرَ دَٓائِبَي۟نِ وَسَخَّرَ لَكُمُ الَّي۟لَ وَالنَّهَارَ وَاٰتٰيكُم۟ مِن۟ كُلِّ مَا سَاَل۟تُمُوهُ وَاِن۟ تَعُدُّوا نِع۟مَتَ اللّٰهِ لَا تُح۟صُوهَا Hakika kusaidiana kwa vilivyomo baadhi kwa baadhi nyingine na kuitikiana kwao kati yao, na kuegemeana katika majukumu na wajibu, kunajulisha kwamba viumbe vyote viko chini ya malezi na uchungaji wa Mlezi mmoja Pekee. Na kwamba wote wako chini ya mwendeshaji mmoja wa pekee. Na kwamba wote wako chini ya usarifu wa mmoja pekee. Hii ni kwa sababu (Utaratibu wa kusaidiana) kati ya vilivyomo unapita kuanzia kwenye jua, ambalo kwa amri ya Allah linatayarisha mambo ya kilazima ya uhai kwa ajili ya walio hai, na kutoka katika mwezi ambao unatujulisha nyakati, na kuishia katika kutoa mwanga, hewa na maji na chakula kwa wenye uhai, na kutoa mimea kwa ajili ya wanyama, na kutoa wanyama kwa ajili ya mwanadamu, bali hata kutoa kila kiungo msaada kwa kiungo kingine cha mwili, na kutoa atomu za chakula kwa ajili ya vyumba vidogo vya mwili, basi kutii kwa hivi vilivyomo visivyo na roho visivyo na utambuzi na kufuata utaratibu wa kusaidiana na kufungamana pamoja kwa mafungamano ya kufahamiana na kuitikiana katika ukomo wa hekima, na katika ukomo wa kumpendelea kheri mwingine na ukarimu, na kujaalia kila mmoja kati ya hivyo kinajitahidi kukipa msaada kingine na kukisaidia mahitaji ya lazima ya uhai, na kuharakisha kukidhi mahitaji yake na kukiauni, chini ya kivuli cha kanuni ya ukarimu na sharia ya upole na utaratibu wa huruma, yote hayo yanajulisha wazi kwamba vyote hivyo ni viumbwa vyenye kuamuriwa na vyenye kutiishwa na kumtumikia mmoja wa pekee, mmoja mwenye kutegemewa na kila kitu, mweza uweza wa hali zote, mjuzi ujuzi wa hali zote na mkarimu ukarimu wa hali zote. Basi ewe mwenye kuleta falsafa muflisi! Unasema nini katika dirisha hili kubwa? Je inayumkinika kwa sadfa unayoitakidi kuingilia katika mambo haya?

§12

اَلَا بِذِك۟رِ اللّٰهِ تَط۟مَئِنُّ ال۟قُلُوبُ Hakika hakuna ukombozi wa moyo na roho katika kushikwa na wasiwasi wa kutisha, na katika majanga ya babaiko na khofu, na kutokana na kiu cha upotevu na kuunguza kwa moto wa kuwa mbali na Allah (s.w) ila kwa kumtambua Muumba mmoja wa pekee. Kwani mambo ya nyoyo na roho, na mambo ya vilivyomo vyote havisalimishwi kwa Muumba mmoja wa pekee hadi zinapata raha yake, na kufanikiwa ukombozi wake kutakana na taabu ya matetemeko ya kinafsi yenye kudamirisha na kutulia kutokana na wasiwasi huo na kutuama. Kwa sababu ikiwa halikuegemezwa jambo la vilivyomo vyote kwa mmoja wa pekee, basi kwa hiyo utapelekwa uumbaji wa kila kitu kwa idadi isiyo na mpaka ya sababu, na hapo itakuwa kupatisha kitu kimoja ni mushkeli na jambo gumu kama kuumba vilivyomo vyote, na hakika tumethibitisha katika neno la ishirini na tatu kwamba ikiwa imeegemezwa jambo la uumbaji kwa Allah (s.w), kwa hiyo itakuwa imeegemezwa idadi isiyo na mpaka ya vitu kwa mmoja wa pekee, na kama si hivyo litakuwa jambo la kila kitu mkononi mwa idadi isiyo na mpaka ya sababu, na katika hali hii inakuwa kuumba tunda moja mathalani ndani yake kuna mishkeli na magumu kwa kiasi cha ulimwengu wote, bali zaidi. Ebu tufafanue hilo kwa mfano: Kama ilivyo kuegemeza uongozi wa askari mmoja kwa maamiri wengi kuna mishkeli mingi mno, wakati ambapo kuegemeza uongozi wa askari mia moja kwa kamanda mmoja kuna wepesi mkubwa kama kuongoza askari mmoja, vivyo hivyo kuafikiana kiasi kisicho na mpaka cha sababu katika kupatisha kitu kimoja kuna mamia maradufu ya mishkeli, wakati ambapo katika kupatisha kwa mmoja wa pekee kwa vitu vingi, kuna mamia maradufu ya wepesi. Na kama hivyo basi anachohisi mwanadamu miongoni mwa shauku ya hakika, inamfanya kuwa mwenye kudumu na wasiwasi na babaiko ikiwa hataifikia, hatapata utulivu isipokuwa kwa kumpwekesha muumba na kumtambua Allah (s.w) kwa sababu kupita njia ya ukafiri ambayo ndani yake kuna kiasi kisicho na mpaka cha misukosuko na mishkeli ni muhali, na haina hakika asilani. Wakati ambapo katika Tawhidi kuna wepesi wa hali zote katika kuumba vilivyomo kwa wingi huu na kupendezesha kwa kiasi haimwachii mwanadamu uwanja wowote isipokuwa mwenendo wake, na hakuna shaka kwa sababu ni jambo la asili na hakika. Ewe unayefuata upotevu, na ewe mwovu masikini! Chunguza njia ya upotevu giza lilioeje la njia hiyo na maovu makubwa kiasi gani ya njia hiyo kwa moyo wa mwanadamu, usijaribu kuikata kamwe, kisha chunguza njia ya Tawhidi, usafi wake ulioje na ucheshi wake ulioje basi ipite njia hiyo uiokoe nafsi yako!

§13

سَبِّحِ اس۟مَ رَبِّكَ ال۟اَع۟لٰى اَلَّذٖى خَلَقَ فَسَوّٰى وَالَّذٖى قَدَّرَ فَهَدٰى Aya hizi tukufu zinatuelekeza kuwa hakika ya vitu vyote na hasa vilivyo hai hudhihiri katika uwepo kana kwamba vimetoka kwenye mwili ulioundwa vyema kwa hekima unatunuku kila kitu kiasi kilichopangika na sura ya ajabu inayobainisha hekima ya wazi. Na katika mwili tunaona misitari iliyopandana, na miinamo na mikunjo ambayo faida mbali mbali zinatokana nayo kwa mwili, na manufaa kemkem ambayo yanarahisisha jambo la kutekeleza jukumu lake ambalo imeumbwa kwa ajili yake kwa namna ya utimilifu mno. Kilichokuwepo ni chenye sura ya kimaanawy katika elimu ya Allah inayowakilisha makadirio yake ya kiuhai, nayo inaambatana na sura ya kimaada na kuhama nayo katika ngazi za makuzi yake, kisha sura hiyo inabadilika na viwango katika mwendo wa uhai wake mabadiliko yanayolingana na hekima katika uumbaji wake na kuchukuana kiujumla pamoja na maslahi yanayoundwa juu yake, katika yanayojulisha kwa uwazi kwamba sura ya miili hiyo na viwango vyake zinapambanuliwa na kukadiriwa makadirio maalum katika duara la qadar ya Kiungu, Mtukufu mwingi wa hekima mwenye ukamilifu, na sura hizo zinapangiliwa na kuratibiwa kwa mkono wa uweza wa Kiungu na kuzitunuku uwepo maalum wenye kukadiriwa. Basi hivyo vilivyopo visivyo na mpaka vinajulisha juu ya aliyewajibu kuwepo, na vinashuhudia kwa ndimi zisizo na mpaka juu ya umoja wake na ukamilifu wa uweza wake. Zingatia yaliyomo katika mwili wako na viungo vyako ewe mwanadamu miongoni mwa mipaka yenye kupanda na mikato madhubuti, na zingatia faida zake na matokeo ya huduma zake na shuhudia ukamilifu wa uweza wa Kiungu katika ukamilifu wa hekima.

§14

وَ اِن۟ مِن۟ شَى۟ءٍ اِلَّا يُسَبِّحُ بِحَم۟دِهٖ Hakika kila kitu kinamtaja muumba wake na kumtakasa kwa ulimi maalum, kama inavyofahamika kutokana na aya hii tukufu. Naam, hakika ya tasbihi zinazoinuliwa kutokea upande wa vilivyopo sawa kwa ulimi wa hali au wa kauli, zinajulisha ujulisho wa wazi juu ya kuwepo kwa dhati yenye kutukuzwa ya mmoja wa pekee. Naam, hakika ujulisho wa maumbile ni wa kweli, na ushahidi wake haurudishwi, na hasa ikiwa ushahidi unatokana na ujulisho wa hali, na hasa ikiwa yanapopatikana majulisho kutokana na pande mbali mbali, basi huo ni ushahidi wa kweli haukubali shaka kabisa. Chunguza sasa sura zilizoratibika za vilivyomo, utaona zimeafikiana kama yanavyoafikiana maduara yenye kuingiliana katika kuelekea kwake upande wa nukta ya katikati, kwa hiyo zinabeba majulisho kwa ulimi wa hali na kwa mitindo isiyo na mipaka na kwa shahidi za maumbile kwa namna zisizo na mpaka, kwani kila sura kati yake ni ulimi wenye kushuhudia wenyewe kwa dhati yake. Na umbo lake lenye kuratibika lenyewe ni ulimi wa kweli wenye kushuhudia kweli, bali wa uhai wote wa kilichopo ni ulimi wenye kutaja kwa tasbihi. Hakika tumethibitisha katika (Neno la ishirini na nne), kwamba tasbihi zote hizi zenye kudhihiri kwa ajili ya mazingatio, na zinazotokana kwa ndimi za hali au kauli kutoka katika vyote vilivyomo na maamkizi yake na shahidi zake zenye kujulisha juu ya dhati takatifu tofauti, zinadhihirisha kwa uwazi yule Mmoja wa pekee ambaye ni wajibu kuwepo, na kujulisha juu ya ukamilifu wa Uungu wake (s.w).

§15

قُلْ مَن بِيَدِهِ مَلَكُوتُ كُلِّ شَيْءٍ وَإِن مِّن شَيْءٍ إِلاَّ عِندَنَا خَزَائِنُهُ مَّا مِنْ دَآبَّةٍ إلَّا هُوَ ءَاخِذٌ بِنَا صِيَتِهَآ إِنَّ رَبِي عَلَى كُلِّ شَئٍ حَفِيْظٌ Inafahamika kutokana na aya hizi tukufu kwamba kila kitu, katika kila hali miongoni mwa hali zake, kinamhitajia Muumba mmoja wa pekee mwenye utukufu. Basi kwa kutupia jicho lenye kuchunguza katika ambayo yamekunjuka mbele yetu katika vilivyomo ulimwenguni, tunashuhudia mandhari ya nguvu ya hali zote yanachuja kupitia udhaifu wa hali zote wenye kushuhudiwa, na tunashuhudia athari ya uwezo wa hali zote zinabainishwa kati kati ya kushindwa kwa hali zote kunako fahamika wazi. Kama hali za kufurutu ada ambazo zinadhihirishwa na mbegu za mimea na mashina yake katika kukua kwake na kuzinduka kwa mafundo ya kiuhai ndani yake. Na vilevile tunaona mandhari za utajiri wa hali zote yanaonekana ndani ya ufakiri wa hali zote na ukame kamili. Kama katika utajiri kemkem, na mazingira ya rutuba yenye kuenea ardhi na mimea kwenye majira ya machipuo baada ya kuwa katika uyabisi na ukame kwenye majira ya baridi. Na tunaona kutona kwa uhai wa hali zote ndani ya ukame wa ufu wa hali zote, na kuzima kabisa, kama katika kugeuka kwa chembe zisizo hai - kama mchanga na maji - katika maada yenye kutweta uhai kwenye viumbe hai. Na tunaona mandhari za utambuzi kamili ndani ya ujahili wenye tabaka, kama ilivyo katika michakato na kutembea kwa kila kitu - kuanzia kwenye atomu hadi kwenye sayari - michakato hiyo yenye kusifika kwa utambuzi kamili na kuratibika kikamilifu pamoja na mpangilio wa ulimwengu wote, na wenye kuwiana uwiano timilifu pamoja na mahitajio ya maisha na matakwa ya hekima iliyokusudiwa kwenye uwepo. Basi uweza uliopo kwenye unyonge na kushindwa, na nguvu ambayo inaonekana ndani ya madini ya udhaifu, na utajiri na ukwasi vinavyoonekana kwenye nafsi ya ufakiri wenyewe, na nuru za uhai na utambuzi wenye kuzunguka wenye kung’aa kupitia ufu na ujinga. Basi kila mandhari katika mandhari hizi kwa upande wake yanafungua kwa uwazi madirisha yanadhihirisha wazi na kwa dharura kupasa kwa kuwepo na upekee wa dhati takatifu ya muweza mwenye uweza wa hali zote na mkwasi mwenye ukwasi wa hali zote, na mwenye nguvu za hali zote na mjuzi ujuzi wa hali zote, na aliye hai mwenye kusimamia kila kitu. Ukiachilia mbali kuwa jumla yake yanashuhudia juu ya upekee wake, na kubainisha njia ya sawa ubainifu wa wazi na kwa kipimo kikubwa zaidi. Basi ewe mwenye kughafilika uliyedondoka katika dimbwi la asili! Ukiwa hujui adhama ya uweza wa kiungu, na kama hujatupilia mbali dhana ya uumbaji wa asili, basi sio juu yako isipokuwa kuegemeza kila kitu katika uwepo, bali hata katika atomu, nguvu kubwa isiyo na mipaka, uwezo mkubwa usio na ukomo, hekima fasaha isiyo na mpaka wa mipaka yake na umahiri wa hali ya juu bila ukomo. Bali ni juu yako kuegemeza kwa kila kitu jicho linaloona vema katika kila kitu, na uongozi madhubuti unaozungukia kila kitu!!.

§16

الَّذِي أَحْسَنَ كُلَّ شَيْءٍ خَلَقَهُ Kila kitu kimewekwa vema kwa urefu wa kimo chake, kuwekwa vyema, kupimwa kwa mizani madhubuti iliyokamilika uzito wake, kupangiliwa mpangilio timamu, kuratibiwa kwa umaridadi sana, kutengenezwa kwa umahiri, kuvikwa sura nzuri mno, nguo nzuri mno, na aina ya kuvutia mno kutokana na njia ya karibu zaidi kwake, umbo jepesi mno linalolisaidia kutekeleza jukumu lake na kutunukiwa uwepo unaonesha hekima hakuna mchezo ndani yake wala israfu. Basi kwa mfano chukua, ndege, vazi lake ni hariri nyororo maridadi. Je inayumkinika kuvikwa nguo inayowiana naye na kwa hekima ya muumba wake kuliko vazi hili nyororo. Upole ulioje na uzuri wakati wanalisafisha! Na wepesi ulioje na urahisi wakati wanaitikisa na kuitumia katika mambo yake mbali mbali ya kimaisha! Na kama hivi, kila kilichomo katika uwepo ni shahidi mwenye kutamka, kama mfano huu, juu ya Muumba mwingi wa hekima. Na kila moja kati yake ni ishara ya wazi kwa Mweza Mjuzi Mwenye uweza usio na mpaka na ujuzi wa hali zote.

§17

Hakika yanayoshuhudiwa juu ya uso wa Ardhi katika mpangilio na mfuatano katika kuumba viumbe, na kuongozwa kwa mambo yake, na kuyafanya upya kwa mfululizo katika kila msimu, kwa uwazi inaonesha juu ya hekima ya jumla inayoenea vilivyokuwepo. Hekima hii ya jumla kwa dharura inajulisha juu ya Mwingi wa hekima wa hekima za hali zote, kwani hakuna sifa bila Mwenye kusifiwa. Kisha aina za mapambo yenye kupendeza ambayo yanafunua pazia ya hekima ya jumla ambayo uwepo hujifunika nayo, kwa uwazi inajulisha juu ya uangalizi wa hali ya juu wa jumla, na uangalizi huu unajulisha kwa vyovyote juu ya Muumba Mkarimu, na hakika aina za upole na ukarimu, na aina za upole na hisani vilivyochorwa juu ya pazia la uangalizi ambao unafunika uwepo wote, kwa uwazi inajulisha juu ya rehema ya wasaa, na rehema hii yenyewe wasaa kwa dharura inajulisha juu ya (Mwingi wa rehema mwenye kurehemu), kisha hakika sampuli za riziki, na mitindo ya kufanya maisha, yenye kustawi maua juu ya matawi ya rehema ambayo hutia kivuli kila kitu kwa matawi yake, na yenye kuandaliwa kwa ajili ya walio hai wenye kuhitajia riziki, na kuvipa maisha yanayowiana kikamilifu, kwa uwazi inajulisha juu ya uruzuku wenye malezi na uchungaji, ulezi wenye upole na huruma na malezi haya na uendeshaji, kwa dharura vinajulisha juu ya Mtoa riziki Mkarimu. Naam, vilivyomo juu ya Ardhi miongoni mwa viumbe vinavyolelewa kwa hekima kamili, na kupambwa kwa uangalizi kamili, na kuenezewa neema kwa rehema kamili, na kupewa nyenzo za maisha yake kwa huruma kamili, basi kila moja kati ya hayo ni ulimi unaotamka na kuashiria kwa Allah Mwingi wa hekima, Mkarimu, Mwingi wa rehema na Mwenye kuruzuku. Na kila moja kati ya hizo vilevile inaashiria katika umoja wake. Kama ilivyo kwamba vilivyomo juu ya Ardhi miongoni mwa hekima za dhahiri huangaliwa ndani yake kusudio na utashi, , na uangalizi wa jumla uliyomo ambao unabeba hekima hiyo, na huruma iliyomo juu yake inayoenea uwepo na ambayo inabeba uangalizi na hekima, na riziki enevu yenye kuenea walio hai na utunuku wa maisha ulio mwema na mpole, ambao unabeba rehema na uangalizi na hekima, basi kila moja katika mandhari haya na kwa ujumla wake inajulisha ujulisho mkubwa sana juu ya Mwingi wa hekima, Mkarimu, Mwenye hekima na Mtoa riziki, na inajulisha juu ya wajibu wa kuwepo kwake (s.w) na juu ya umoja wake na ukamilifu wa uungu wake. Kwani hakika ya uangalizi uliyomo kwenye hekima, na rehema iliyomo kwenye uangalizi, na utoaji maisha uliyomo kwenye rehema, na utoaji maisha na riziki uliyomo kwenye rehema ni dalili za kukinaisha na kwa kipimo kipana mno juu ya aliye wajibu kuwepo, kwa mfano wa kujulisha kwa rangi saba juu ya mwanga wa jua ambao unajaza mwanga mchana. Basi ewe mwenye kughafilika mwenye kutahayari mkanaji! Vipi utafasiri malezi haya yaliyovikwa taji kwa hekima ya hali ya juu, ukarimu enevu, rehema kunjufu, riziki tele na mandhari haya utayafafanua kwa jambo gani? Je inayumkinika kuyafasiri kwa sadifu ya kiholela? Au inayumkinika kuifafanua kwa nguvu mfu ufu sawa na wa moyo wako? Au inayumkinika hilo kwa asili kiziwi uziwi sawa na wa akili yako? Au kwa sababu zenye kushindwa zisizo hai zisizo na ujuzi mfano wako? Au unataka kutenda kosa kubwa - hakuna kosa baada yake - nalo ni kutoa kwako sifa za Muumba Mtukufu aliyeepukana na upungufu Mwenye sifa za juu na Mweza mjuzi wa kila kitu mwenye kusikia kila kitu na mwenye kuona kila kitu, kwa (Asili) yenye kushindwa isiyo na ujuzi kiziwi pofu? Basi kwa nguvu gani unaweza kuzima taa ya hakika hii yenye kung’ara mng’aro wa jua? Na chini ya pazia gani miongoni mwa pazia za kughafilika unaweza kuifunika?

§18

اِنَّ فِى السَّمٰوَاتِ وَال۟اَر۟ضِ لَاٰيَاتٍ لِل۟مُؤ۟مِنٖينَ Tukichunguza uso wa Ardhi iliyokunjuliwa mbele yetu tunaona kwamba ukarimu wa hali zote unadhihiri katika kupatisha vitu. Wakati ambapo ukarimu unahitajia vitu kuwa katika ghasia na kutokuwa na mpangilio, tahamaki tunashuhudia vikiwa katika upeo wa kuratibika na ukomo wa kupangika. Shuhudia mimea yote ambayo inapamba uso wa Ardhi utaona hakika hii. Vilevile tunaona kasi ya hali zote inabainika katika kupatisha kwa vitu. Wakati ambapo kasi inahitajia vitu kuwa na sura zilizoharibika, kuwa na maada yenye dosari, kugongana kwa kipimo, na kupungukiwa na ufundi, tahamaki tunaishuhudia ikiwa katika upeo wa makadirio, udhibiti na ubora, ukomo wa umadhubuti na kuwiana kwa vipimo. Chunguza matunda yote ambayo yanaremba uso wa ardhi ambapo hakika hii inadhihiri humo kwa namna nzuri zaidi. Na vilevile tunaona hali ya wingi mno wa hali zote katika kupatisha vitu. Wakati ambapo wingi unahitajia vitu viwe duni na rahisi na pengine vibaya, tahamaki tunashuhudia vikiwa vimetengenezwa vyema sana, ufundi wa ajabu na uzuri wa kuvutia mno. Zingatia na chunguza katika maua yote ambayo yanapamba uso wa ardhi kwa mpangilio mzuri. Je haidhihiri humo kikamilifu!. Na vilevile tunaona urahisi wa hali zote unadhihiri katika kupatisha vitu. Wakati ambapo urahisi unahitajia vitu kuwa rahisi na vyenye kukosa ufundi na umahiri. Tahamaki tunashuhudia vikiwa katika ukamilifu wa ufundi na umahiri wa kupendeza mno. Shuhudia mbegu na chunguza kwa makini kokwa, hizo pakiti madhubuti katika maada ya muundo wake imebeba faharisi za zana za miti na ramani za miili ya mimea. Na vilevile tunaona umbali wa hali zote unapambanuliwa kati ya nyakati na mahali pa kupatisha kwa vitu, wakati ambapo masafa haya ya mbali ya kutisha yanahitajia kwamba vitu vije vikiwa vimetofautiana mno, tahamaki tunashuhudia vikiwa katika kuafikiana kikamilifu katika sifa zake na hali zake mahususi. Shuhudia sampuli za nafaka zenye kulimwa katika maeneo yote ya ardhi licha ya umbali wake wa wakati na mahali ambao unatenganisha kati yao. Na tunaona vilevile kuchanganyika kwa hali zote, na kuingiliana kwa umadhubuti katika kupatisha kwa vitu. Wakati ambapo kuchanganyika huku kunahitajia kuingiliana kwa maada baadhi yake ndani ya baadhi nyingine na kutandiana, tahamaki tunavishuhudia vikiwa katika kupambanuka kikamilifu, na umahususi uliopangika. Shuhudia mbegu zilizotawanywa zilizozikwa chini ya mchanga, na tazama kwa makini katika kutengana kwake wakati wa kukua kwake na kubeba kwake mashuke, licha ya kushabihiana kwa maumbo yake. Na chunguza maada mbali mbali zinazoingia katika mjengo wa miti, na kugeuka kwake katika maumbo mbalimbali katika majani mepesi, na maua ya kupendeza, na matunda nyororo. Na chunguza katika sampuli za chakula na milo mbalimbali inayoingia tumboni, na kutengana kwake, na kila aina ya chakula huingia katika kiungo kinachowiana nacho bali katika chumba kidogo ambacho kinalingana nacho kwa mtengano wa wazi, shuhudia athari za uweza wa moja kwa moja, kupitia hekima ya moja kwa moja. Na tunaona vilevile wingi usio na ukomo katika vitu, na wingi uliokithiri katika sampuli zake na maumbo yake. Wakati ambapo wingi huu unahitajia vitu kuwa rahisi, tahamaki tunashuhudia vikiwa katika ukomo wa thamani na ukomo wa ubora. Shuhudia athari za kupendeza zilizoandaliwa kwa ajili ya meza ya chakula ya Ardhi, na tazama kwa makini katika tunda moja, na liwe kwa mfano tunda la tut. Je tunda hili haliwakilishi kielelezo cha kupendeza cha halua iliyotengenezwa kwa mkono wa uweza wa Allah (s.w)? Shuhudia ukamilifu wa rehema, katikati ya ukamilifu wa kiufundi. Na ni kama hivi tunashuhudia juu ya uso wa Ardhi yote, ubora na thamani katika vilivyotengenezwa licha ya wingi wake usio na ukomo. Na tunaona ndani ya wingi huu kupambanuka kwa vilivyomo licha ya kuchanganyika kwake na kuingiliana kwake. Na tunakuta katika huku kuchanganyika na kuingiliana kuafikiana na kushabihiana katika vilivyomo licha ya umbali kati yake. Na tunaona kati kati ya kuafikiana huku uzuri wa kupendeza katika vilivyomo na uchungaji mkubwa licha ya urahisi wa ukomo katika kuvipatisha. Na tunaona ndani ya uchungaji huu uliotimia makadirio makini bila israfu na uwiano wa vipimo nyeti licha ya kasi katika kuvipatisha. Na tunaona ndani ya makadirio haya na uwiano wa mizani na kutokuwepo kwa israfu maajabu katika ufundi na kupendeza katika hilo licha ya wingi wake wa ukomo. Na tunashuhudia ndani ya kupendeza huku katika ufundi mpangilio wa ajabu licha ya ukarimu wa hali zote katika kuvipatisha. Tukichunguza mambo yote haya, tunayaona yanajulisha ujulisho wa wazi wazi zaidi kuliko kujulisha kwa mchana kwa mwanga, na angavu zaidi kuliko kujulisha kwa mwanga juu ya jua, juu ya kupasa kwa uwepo wa Mweza mwenye utukufu, mwenye hekima zote mwenye ukamilifu na mwenye kurehemu mwenye uzuri, na yanashuhudia juu ya umoja wake na upekee wake, na ukamilifu wa uweza wake na uzuri wa ulezi wake, na yanabainisha kwa dhahiri siri katika siri za aya tukufu لَهُ الأَ سْمَآءُ الْحُسْنَى Na baada ya hayo, basi ewe mwenye kughafilika mkaidi, na ewe usiye fahamu masikini! Utafasiri vipi hakika hii kubwa ambayo unaiona kwa macho yako dhahiri? Na utafafanuaje hali hizi zenye kufurutu ada zilizohudhurishwa mbele yako? Na utaegemeza kwa nani hivi vilivyotengenezwa vya kupendeza vya ajabu? Na kwa pazia gani katika pazia za kughafilika utaweza kulifunika dirisha hili pana upana wa Ardhi yenyewe? Iko wapi sadfa unayoiitakidi na asili unayoitegemea nayo haina utambuzi? Bali ziko wapi dhana za upotevu ambazo unazoegemea, na kuwa nazo na kusuhubiana nazo kwa urafiki?! Viko wapi vyote mbele za hakika hizi zenye kutia tahayari na hali za kupendeza mno za kushangaza? Je sio muhali katika muhali mia moja kuingia kwa sadfa katika mambo kama haya? Au sio muhali katika muhali elfu moja kuegemezwa moja katika mambo haya kwa asili achilia mbali kuegemezwa kwa mambo hayo yote?! Au kwamba wewe unaitakidi asili isiyo na uhai yenye kushindwa, uwezekano wa kumiliki kwake mashine za kimaanawy katika kila kitu? na kwa idadi ya vitu vyote? Basi ee upotevu ulioje!

§19

اَوَلَم۟ يَن۟ظُرُوا فٖى مَلَكُوتِ السَّمٰوَاتِ وَ ال۟اَر۟ضِ Zingatia katika mfano huu ambao hapo kabla tumeutaja katika (Neno la ishirini na mbili): Hakika athari ya kupendeza kama kasri kubwa, iliyokamilika sehemu zake, imepangika nguzo zake na imejengwa vema, kwa uwazi inajulisha juu ya Mtengenezaji vema. Yaani hakika ya jengo linajulisha juu ya ufundi wa mjenzi na utendaji wake. Na kitendo kamili kilichofanywa vema kwa vyovyote kinajulisha juu ya mtendaji hodari, na mtaalamu mahiri wa ujenzi. Na anuani hizi, Mtendaji hodari Mtaalamu wa ujenzi mahiri Mjenzi mwema, kwa uwazi zinajulisha juu ya sifa kamili hakuna upungufu ndani yake anasifika nazo Mtendaji huyo, yaani zinajulisha juu ya uwezo wa kutengeneza vema kwake. Na kwamba sifa kamili na uwezo wa kutenda vema kwenye kukamilika, kwa uwazi kunajulisha juu ya kuwepo utayari kamili na ukubalifu uliotimia. Na maandalizi kamili hii inajulisha juu ya dhati ya juu na roho ya juu. Na kama hivi - na Allah (s.w) ana mfano wa juu - basi athari hizi zenye kufanyika upya zilizo wazi kuonekana dhahiri na ambazo zinajaza ardhi bali ulimwengu, kwa uwazi zinajulisha juu ya matendo yapo kwenye ukomo wa ukamilifu. Na kwamba anuani za matendo haya yanayodhihiri kupitia ukomo wa kufanywa vema na upeo wa hekima kwa uwazi yanajulisha juu ya Mtendaji kamili mwenye kutakasika na upungufu katika anuani zake na majina yake. Kwa sababu matendo yaliyowekwa vema na ya hekima yanajulikana kwa uwazi kabisa kwamba hayapatikani pasipo na Mtendaji. Na kwamba anuani ambazo zimo katika ukomo wa ukamilifu zinajulisha sifa ambazo zimo katika ukomo wa ukamilifu kwa sababu kama linavyopasuliwa jina la mtendaji kutoka katika mzizi kwa mujibu wa elimu ya Sarufi, hakika chanzo cha anuani na mizizi ya majina ni sifa. Na sifa ambazo zimo katika ukomo wa ukamilifu, na ukubalifu wa kidhati au mambo yale ya kidhati ambayo tunashindwa kuyaelezea, yanajulisha kwa haki ya yakini juu ya dhati yenye kutakasika katika ukamilifu wa hali zote. Na kwa kuwa kila athari katika athari za ajabu zilizopo mbele yetu katika ulimwengu na katika viumbe wote ni kamili yenye kupendeza kwa dhati yake. Na kwamba athari hii yenye kupendeza inashuhudia kitendo, na kitendo kinashuhudia juu ya jina. Na jina linashuhudia juu ya sifa, na sifa inashuhudia shani (Ya Allah), na shani inashuhudia juu ya dhati. Kwa hiyo kila moja kati yake kama inavyoshuhudia ushahidi wa kweli juu ya Fundi Mtukufu Mmoja wa pekee wajibu kuwepo, na inaashiria katika upekee wake. Yaani kama ilivyo kuwa kuna shahidi na ishara kwa idadi ya viumbe kwelekea kwenye Tawhidi, hakika kila moja vilevile pamoja na jumla ya athari na viumbe kwenye ulimwengu hakika ni Miiraji kubwa kwa ajili ya kumjua Allah (s.w), inayo kiasi cha nguvu ya viumbe wote, ukiachilia mbali kuwa ni hoja yenye nguvu ya ukweli, haiwezekani kukaribia utata wowote vyovyote iwavyo. Na sasa ewe Mwenye kughafilika Mkanaji! Kwa jambo gani utaweza kuishinda hoja hii yenye nguvu sawa na nguvu ya ulimwengu? Na kwa jambo gani utafunika dirisha hilo pana ambalo linabainisha miale ya hakika kutokana na madirisha elfu moja na moja, bali kutokana na madirisha kwa idadi ya viumbe, na kwa kifuniko gani cha kughafilika unaweza kuzificha?!

§20

فَسُبْحَانَ الَّذِي بِيَدِهِ مَلَكُوتُ كُلِّ شَيْءٍ وَإِن مِّن شَيْءٍ إِلاَّ عِندَنَا خَزَائِنُهُ وَمَا نُنَزِّلُهُ إِلاَّ بِقَدَرٍ مَّعْلُومٍ * وَأَرْسَلْنَا الرِّيَاحَ لَوَاقِحَ فَأَنزَلْنَا مِنَ السَّمَاء مَاء فَأَسْقَيْنَاكُمُوهُ وَمَا أَنتُمْ لَهُ بِخَازِنِينَ Kama inavyoshuhudiwa ukamilifu wa hekima, na uzuri wa kutengeneza vema katika sehemu ndogo na matawi madogo madogo, na katika matokeo na faida, hakika chembe na jumla, na viumbe vikubwa ambavyo vinadhihiri na kuwa vimechanganyika na kupishana na kutandawaana, na kuleta dhana kuwa huo ni mchezo wa kusadifiana, vilevile hujifanyia hali zake na kusifika kwa hekima na kuwa vema, licha ya kuchanganyika kunakoonekana juu yake. Mathalani: Nuru au mwanga, kwa kujulisha kwa kazi zake za hekima nyingine hakika ni kwa ajili ya kutangaza kuhusu vitengenezwa vya Allah (s.w), na kuvionesha kwa idhini yake mbele ya macho. Yaani mwanga ni wenye kutiishwa kutoka kwa Muumba mwenye hekima zote, ili kwa mwanga huo Allah (s.w) apate kudhihirisha maajabu ya viumbe wake, na kuonesha chini ya mwale wake maajabu ya alivyovitengeneza, katika maonesho ya soko la ulimwengu. Sasa tazama pepo, tunaona kwamba zinatembea ili kutimiza kazi na majukumu na huduma tukufu, hili linashuhudiwa na manufaa mema yanayobebeshwa katika kazi zake zenye hekima. Kwa hiyo mawimbi ya vimbunga, ni usarifu na utiishaji kutoka kwa Muumba Mwenye hekima zote. Na yanayoshuhudiwa katika kuvuma kwake na kupepea kwake kwa nguvu, ni kwa ajili ya kuharakisha kwake kwenda kutekeleza amri za kiungu Bwana mlezi na kutekeleza hukumu zake. Basi sasa tazama kwenye mifereji, madimbwi na mito, na zingatia katika kububujika kwake kutoka katika Ardhi na milima, utakuta kwamba hakuna kusadifiana humo na wala hakuna mchezo tu. Kwani hufuatia hali hizo faida na masilahi ambayo ni athari za Rehema za kiungu zikiwa wazi, ama matokeo yaliyopatikana katika mambo hayo ni yenye kupimwa na kuhesabiwa. Na vilevile kulimbikiza kwake na kuhazini kwake milimani hakika kuna kwenda ndani ya hesabu makini, na kuafikiana na haja za walio hai, na baada ya hapo kuibubujiza na kuituma kwa mizani ambayo ni upeo wa hekima. Yote hayo ni dalili na shahidi zenye kutamka kwamba utiishaji huo na ulimbikizaji huo hakika unatimia tu kutokana na Mlezi Mwenye hekima zote. Na tunachokiona katika ukali wa kufoka kwake na kububujika kwake kutokea kwenye Ardhi hakika ni kupenda kwake kukubwa katika kutekeleza amri za Kiungu Bwana Mlezi wakati zinapotoka tu. Na sasa tazama mawe na maumbo ya mawe, na johari madhubuti, na sifa za madini, na tazama katika kutiwa kwake mapambo na sifa zake bainifu zinazofuatana na manufaa mbalimbali, utakuta yanayoambatana nayo katika faida zenye hekima, na katika kuratibika kikamilifu baina ya matokeo yake yanaishia, na mahitajio ya kimaisha, na kwa hiyo kuwiana kwake na mambo yanayotakikana kwa mwanadamu, na kukidhi kwake haja zake na haja nyingine za viumbe. Yote hayo ni dalili za kwamba kupamba huko, kunadhimu na kupangilia na kusawiri, hakika ni kutoka kwa Bwana mlezi Mwingi wa hekima. Na sasa tazama maua na matunda, utaona kuwa furaha ya nyuso zake, utamu wa vyakula vyake, uzuri wake wenye kuvutia sana, nakshi zake za kiajabu, na manukato ya uturi wake mzuri, vyote hivyo ni sawa na walinganiaji na madalali katika makaribisho ya wageni ya Bwana Mlezi mkarimu, na Mneemeshaji Mwenye kurehemu. Nazo ni barua za utambulisho mbele ya meza zilizowekwa kwenye Ardhi yote. Kila rangi miongoni mwa rangi mbalimbali, na kila harufu katika harufu anuwai. Na kila ladha katika ladha mbalimbali, inajulisha juu ya muumba karimu, na inamtambulisha Mneemeshaji mwenye kurehemu kwa ulimi wake maalum. Na sasa tazama ndege, utakuta sauti zake na miruzi yake na kuimba kwake, sio isipokuwa ni katika utamkishaji wa muumba mwenye hekima zote. Basi mazungumzo yao ya wao kwa wao, na wanayoleta katika sauti zao miongoni mwa nyimbo ni katika yanayokamata akili. Na tazama sasa mawingu mazito, utakuta kwamba sauti za kunyesha kwa mvua zinazotokana nazo, na mingurumo ya radi za mbingu sio mchezo katu. Kwani kutoa sauti hizo za ajabu katika anga pana, na kuteremsha matone yenye kuleta uhai, na kukamua kwake kutokana na mawingu mazito, na kuwanyonyeshea walio hai, na kuwapa msaada wenye kuyahitajia, kwa uwazi kabisa kunabainisha hakika ya sauti hizo za mvua na mingurumo ya radi zinabeba baadhi ya hekima fasaha na maana ya kina, hata kana kwamba matone hayo yananong’ona amri ya bwana Mlezi karimu kwa hao wenye kiu wenye kuomba msaada kwa kusema: Furaha yenu, ni sisi tunakuja kwenu kutoka kwa Bwana Mlezi mwingi wa rehema. Na sasa tazama mbinguni, angalia kwa makini mwezi peke yake, kati ya sayari za mbingu ambazo hazina idadi, na kwamba harakati zake zote kati yake ni mwezi ni zenye kuratibika utaratibu mzima na mwema zaidi, na zenye kukadiriwa kwa makadirio kwa mkono wa Mweza Mwenye hekima zote, ambapo zinaambatana na hekima nyingi, zina mahusiano makubwa na Ardhi. Na kwa kuwa tumefafanua hili mahali pengine, hapa tunatosheka na kiasi hiki. Na kama hivi yote tuliyoyaeleza katika chembe za jumla, kuanzia kwenye mwanga na kumalizia kwenye mwezi, ni dirisha pana sana linabainisha kuwepo kwa Allah (s.w) na kudhihirisha upekee wake, na linatangaza ukamilifu wa uweza wake na ukubwa wa ufalme wake, kwa kipimo kitukufu na kikubwa na kwa rangi mbalimbali na aina mbalimbali. Basi ewe mwenye kughafilika! ukiwa unaweza kuzinyamazisha sauti hizi zinazonguruma kama radi za mbingu, na ukiwa unaweza kuizima mianga hii yenye kuangaza, hapo utaweza kumsahau muumba mkarimu. Na kama sio hivyo basi rudi katika akili yako, na uelekee katika nusu ya akili yako na useme: Ametakasika ambaye: تُسَبِّحُ لَهُ السَّمَاوَاتُ السَّبْعُ وَالأَرْضُ وَمَن فِيهِنَّ

§21

وَالشَّمْسُ تَجْرِي لِمُسْتَقَرٍّ لَّهَا ذَلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ Hakika jua ambalo ni taa ya viumbe hivi, hakika hilo ni dirisha lenye kuangaza kama nuru yake, viumbe kupitia dirisha hilo wanachungulia kuwepo kwa muumba wa ulimwengu na upekee wake. Basi sayari kumi na mbili - pamoja na tufe letu la Ardhi - na ambalo linapewa jina la (Mfumo wa jua) zinatembea kwa mpangilio mzuri mno, kulingana na hekima timamu, na kulingana na mizani madhubuti, licha ya kuhitilafiana kukubwa kati yake, kwa upande wa ukubwa wake na maumbo yake na kwa upande wa udogo wake na ukubwa wake, na licha ya kutofautiana kupana kati yake kwa upande wa ukaribu wake na umbali wake kutoka kwenye jua, na licha ya kuwa na aina nyingi katika nyendo zake na kasi zake. Naam, licha ya haya yote, sayari zinatembea katika njia zake zikiwa zinaogelea zikifungwa madhubuti na jua, vikifungamana nalo kwa kanuni ya kiungu, kanuni hii ni ile ambayo wanazuoni wa falaki wanaliita jina la (Nguvu za uvutano). Hizo zinaenda kwa kanuni makini bila ya kosa, japo kwa kiasi cha sekunde, na kufuata ufuataji timamu, na kwa utiifu wa hali zote kwa kanuni hii, kama kufuata kwa maamuma kwa Imamu wao, na hii ni dalili na dalili iliyoje, kwa kipimo kipana na adhimu sana kwa adhama ya uweza wa kiungu na umoja wa kiungu, ukiweza kukadiria ukubwa wa jambo hili kwa nafsi yako basi fanya, ili uone kiasi cha utukufu na hekima katika kufanya sayari zisizokuwa na uhai, na maumbo hayo makubwa yasiyo na utambuzi yanakwenda katika ukomo wa mpangilio na ukamilifu wa mizani, na katika upeo wa hekima, Na katika sura zinazotofautiana na ndani ya masafa mbalimbali, na kwa miendo anuwai, na baada ya hapo kuvitiisha vyote kulingana na mpangilio wa ajabu na wa kuvutia! Ingekuwa kuna kuingia kwa namna yoyote kwa kusadifiana, kwa vyovyote itakavyokuwa kidogo katika mfano wa mambo haya makubwa na kutegemea kwetu kutokea kwa makosa ambayo kutokana nayo hutokea kuponyoka kukubwa kwa ulimwengu, na migongano mikubwa, inayoharibu ukweli na kuufanya kuwa ni wenye kupeperuka kama vumbi. Na lau ingeruhusiwa kusadifu kucheza mchezo wake, huenda mojawapo ya sayari hizi kubwa ikazisimamisha – bila ya sababu – na kuitoa katika muhimili wake, na kwa ajili hiyo huandaa njia ya migongano isiyo na mpaka kati ya sayari zisizo na udhibiti wa idadi. Kwa hiyo kadiria kwa hiyo kwa kiasi gani cha ukubwa wa kutisha unaotokana na kugongana kwa sayari kubwa kuliko tufe letu la Ardhi kwa maelfu ya maradufu. Tunayaacha maajabu ya mambo ya mfumo wa jua na mageni yake kwa ujuzi wa kiungu, unaozunguka kila kitu, na kuifungia akili yetu katika kuchunguza tufe letu la Ardhi, ambayo ni kiamuriwa kimoja katika sayari kumi na mbili na tunda katika matunda yaliyopevuka ya mti wa mfumo wa jua, basi tunaona: Hakika ya sayari yetu hii inatiishwa kwa amri ya kiungu, kama tulivyobainisha katika (Andiko la Tatu), ili kutimiza huduma tukufu na majukumu makubwa, ndani ya mwendo na kuzunguka kurefu, inazunguka nyuma pembezoni mwa jua kwa kutembea kwake idhihirishe na kuzunguka kwake huku adhama ya Uungu na ukubwa wa kiungu, na ukamilifu wa rehema na hekima. Kana kwamba ardhi ni jahazi kubwa la Bwana Mlezi wa walimwengu imeshehenishwa maajabu ya viumbe wake (s.w), au kama makazi yenye kutembea ya wenye uhai na utambuzi katika waja wake, amewapa makazi humo na anawaendesha nayo kwa ajili ya matembezi na kuvinjari katika maeneo ya anga hili. Na mwezi vilevile kana kwamba ni kurabu za saa, zimefungwa na radhi zinatujulisha muda na nyakati, na zimepewa majukumu mengine - yasiyokuwa ni saa ya Ardhi - katika vituo vingine vya anga hili. Na kama hivi inabainika kwamba sayari yetu hii iliyobarikiwa, imepewa katika hekima madhubuti na majukumu matukufu katika kutembea kwake huku, katika yanayothibitisha na kujulisha hali zake, na kushuhudia ushahidi wenye nguvu, kama nguvu ya Ardhi na ukubwa wake juu ya mweza mwenye uweza wa hali zote na juu ya umoja wake. Na pimia yaliyobakia katika Ardhi yetu. Kisha hakika ya kujaalia Ardhi inazunguka mzunguko wa hekima pambizoni mwa mhimili wa jua na kuzifunga kwa kamba za kimaanawy - inayoitwa jina la uvutano – na jua na baada ya hapo kupangilia uendeshaji wake na kuratibu mambo yake yote, hakutimilii isipokuwa kwa kukadiria Mweza Mwenye hekima zote, ukiachilia mbali kwamba kulipeleka jua lipate kutembea kwa kasi ya kushangaza linakata masafa ya masaa matano ndani ya sekunde moja katika sayari (Hiraklet) au aina ya (Jua la majua), kulingana na makadirio ya wanazuoni, sio isipokuwa kwa amri ya mfalme wa azali na milele na kwa uweza wake wa hali zote na kana kwamba (s.w) anaonesha kwa jeshi la mfumo wa jua na askari wake wenye kufuata amri yake anabainisha mazoezi ya kijeshi ili kudhihirisha Ubwana mlezi wake kwa vimbe wote. Basi ewe anayeiona nafsi yake kuwa amejifunza kitu katika elimu ya falaki! Niambie kwa haki ya mola wako je, inayumkinika kwa kusadifiana kuwa na jambo katika mambo makubwa kama haya? Au inayumkinika kwa sababu miongoni mwa sababu ambazo unaziona kuwa zenye taathira katika matukio ya limwengu kufika mkono wake huko? Au kwa nguvu yoyote iwayo kuikaribia? Je, unaitakidi kwamba mfalme mwenye enzi na utukufu anaruhusu mshirika yeyote awaye aingilie katika jambo la ufalme wake mkubwa, kwa kufanya hivi akiwa anadhihirisha kushindwa kwake na upungufu wake?! Hashalillah na sivyo hivyo. Au je inayumkinika kuyasalimisha (s.w) mambo ya wenye uhai ambao wao ndio matunda ya ulimwengu na matokeo yake na shabaha yake na muhtasari wake kuwaachia wengine?! Au aruhusu japo kwa kiasi kidogo mno kwa kuingilia kwa hawa wengine katika mambo yake yenye hekima? na je, akili inaridhia kuachwa bure bure muhtasari wa matunda hayo na matokeo yake kamili mno na khalifa wa Ardhi na mgeni mkirimiwa kwa Mfalme kuachiliwa mambo yake kwa asili na sadfa, kwa kufanya hivyo utukufu wa ufalme uporomoke na ukamilifu wa hekima?! Hashalillah na sivyo hivyo. Na ametukuka Allah na hayo kutukuka kukubwa!

§22

أَلَمْ نَجْعَلِ الْأَرْضَ مِهَادًا * وَالْجِبَالَ أَوْتَادًا * وَخَلَقْنَاكُمْ أَزْوَاجًا فَانظُرْ إِلَى آثَارِ رَحْمَتِ اللَّهِ كَيْفَ يُحْيِي الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا إِنَّ ذَلِكَ لَمُحْيِي الْمَوْتَى وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ Lau tungeleta picha kwamba tufe la Ardhi ni kichwa cha kiumbe mkubwa, hakika sisi tunakuta katika kichwa hiki kikubwa katika ukubwa vinywa mia moja elfu na kila kinywa kina ndimi mia moja elfu na kila ulimi unabainisha kwa hoja mia moja elfu aliye wajibu kuwepo, mmoja wa pekee, mweza juu ya kila kitu, na mjuzi wa kila kitu. Na kila ulimi unazungumza kwa shahidi mia moja elfu za kweli juu ya umoja wake (s.w), sifa zake takatifu na majina yake mazuri. Basi haya tuangalie Ardhi mwanzoni mwa kuumbwa kwake, ipo katika hali ya kumiminika na unyevunyevu, basi yameumbwa katika hali hiyo mawe magumu na umeumbwa mchanga kutokana na hali hiyo, lau Ardhi ingekuwa ni yenye kubakia katika hali yake ya mwanzo ya unyevunyevu maisha yangeshindikana humo na ingeshindikana kuifanya kuwa ni makao yenye kufaa ya aina yote katika aina za ukaaji. Lau hilo jiwe kubwa gumu - lililogeuka kutoka katika hali ya unyevunyevu - ni lenye kubakia katika ugumu wake ingekuwa ugumu kufaidika nalo. Kwa hiyo yule ambaye ameitunuku Ardhi hali inayowiana na maisha hapana budi kuwa ni yule muumba mwenye hekima zote ambaye anaona kwa hekima yake ya hali zote waliomo kwenye Ardhi wote na kuwaandalia haja zao wote. Kisha tuchunguze milima mirefu ambayo inaegemeza Ardhi na kuishika na kukaza umbo lake wakati wa kuzunguka kwake. Basi tunaona kwamba mageuzi mengi yanatokea ndani ya Ardhi, mageuzi haya yanazalisha gesi na mivuke mingi huitema na kuipumua kupitia kwenye milima kwa sura ya matetemeko na volkeno. Ili isiiondoshe kunako kutimiza mwendo wake uliopangika na kutimiza majukumu yake ya kimsingi yale matukio yanayotokea ndani yake. Kama vilevile hiyo Ardhi miinuko yake inatengeneza kinga mbele ya mafuriko ya bahari na michanga yake na ili ziwe ni hazina za maji ya akiba kwa ajili ya mahitaji ya walio hai na kuchanua hewa na kusafisha kutokana na gesi zenye kudhuru ili iwe ni yenye kufaa kuipumua na ili kukusanya mitawanyiko ya maji kutoka kila mahali na kuiwekeza kwa ajili ya walio hai na ili ziwe ni hazina za madini anuwai yanayosimamia udumishaji wa maisha ya viumbe. Basi hali hizi na nyingi nyinginezo, zinashuhudia ushahidi wenye kutamka juu ya mweza wa hali zote mwenye hekima zote na mwenye kurehemu. Na juu ya umoja wake (s.w). Basi ewe mwenye kujifaharisha kwa elimu ya jiografia! Niambie vipi unafasiri mambo haya? Ni sadfa gani inayoweza kushika hatamu ya Ardhi iliyoshehenishwa vilivyotengenezwa vya ajabu na kuifanya inaogelea katika anga ndani yake kuna masafa ya miaka ishirini na nne. Ndani ya mwaka mmoja, bila kutapanyika vilivyomo juu yake miongoni mwa maonesho ya maajabu?! Kisha tazama vilivyomo juu ya Ardhi katika maajabu ya ufundi na vipi kwamba chembe zote zimetiishwa kwa majukumu yenye hekima, hata unaziona kana kwamba zinatazama mtazamo wa kutukuza na kuheshimu kwa wageni wa mweza mwenye hekima, wenye kukaa pambizoni mwa meza ya Ardhi, kwa hiyo inaharakisha kwenda kuwahudumia wote. Kisha chunguza kwa makini katika mandhari za Ardhi na alama zake, katika mitindo ya mapindo yake, nakshi za miinamo ya uso wake na matengenezo ya mwili wake na chunguza umbo lake na rangi zake za kuvutia aina kwa aina kwa kuwa udongo wake ni wa aina kwa aina na ambao unasifika kwa hekima, kupendeza, kuamsha tahayuri na kustaajabu. Basi hiyo mbele yake mito, vimwagiliaji, bahari, marambo na vilele vya milima, hakika vyote hivyo vimeandaliwa na kutayarishwa ili viwe ni makazi ya viumbe na njia ya kuwasafirisha kutoka mahali na kwenda mahali pengine. Kisha je, huoni kwamba kujaa kwake – yaani ardhi – ni kwa hekima kamili na nidhamu ya kupendeza kwa mamia ya maelfu ya jinsi za mimea na sampuli za wanyama na kutia maisha ya furaha katika viumbe hivyo, na kisha kuvipa msamaha kwa umauti kutokana na majukumu yake waliyokuwa wanayatekeleza, tukio hili linafululiza na kufuatana kwa mpangilio madhubuti. Hata Ardhi ikiachwa tupu kutokana na vitu hivyo huanzwa upya kwa kuijaza. Je, hili halimaanishi kwamba (Ufufuo baada ya kifo) ni haki hakuna shaka ndani yake. Na je matukio yote haya sio shahidi za kweli zenye kutamka kwa mamia ya maelfu ya ndimi juu ya Mweza mwenye utukufu, mwenye hekima zote mwenye ukamilifu na juu ya upekee wake?! Hitimisho: Hakika Ardhi ambayo ni sawa na moyo wa ulimwengu, umekuwa mahali pa matangazo ya maajabu ya vilivyotengenezwa na Allah vyenye kupendeza, mkusanyiko wa mageni ya viumbe vyake vizuri, na mapito ya msafara wa vyake vilivyomo vingi, msikiti wa waja wake wenye kujipanga safu juu yake, na kituo cha kutekeleza ibada zao. Hii Ardhi inadhihirisha kutokana na mionzi ya Tawhidi kiasi cha kujaza Ardhi nuru na mwanga. Basi ee mwenye kuihesabia elimu ya jiografia! Ikiwa kichwa cha hii Ardhi kinamtambulisha Bwana Mlezi wa walimwengu kwa vinywa mia moja elfu, na katika kinywa kuna ndimi mia moja elfu, nawe unapuuza utambulisho huu, na unazamisha kichwa chako kwenye dimbwi la Asili, kwa hiyo basi fikiri hatima ya hatia yako. Kupuuza huku na kukanusha kunakupeleka katika adhabu gani?. Tahadhari na uzinduke na nyanyua kichwa chako kunako dimbwi lililovunda na sema: Nimemwamini Allah ambaye mkononi mwake kuna ufalme wa kila kitu.

§23

اَلَّذٖى خَلَقَ ال۟مَو۟تَ وَال۟حَيٰوةَ Hakika uhai ni muujiza angavu na mzuri mno katika miujiza ya kiungu, ni hoja yenye nguvu zaidi na yenye kuwa wazi mno katika hoja za umoja na kioo chenye kukusanya zaidi na chenye kung’aa zaidi. Naam, hakika uhai peke yake unabainisha aliye hai mwenye kusimamia kila kitu kwa majina yake mazuri, sifa zake tukufu na mambo yake yenye hekima. Basi uhai ni kama nuru, basi kama ilivyo nuru ya jua hupatikana kutokana na kuchanganyika kwa rangi saba ya umbo la jua, vilevile (Maisha) hupatikana kutokana na kuchanganyika kwa sifa nyingi kuchanganyika kwa umadhubuti. Na huo uhai ni kama dawa itokanayo na kuchanganyika kwa maada nyingi anuwai mchanganyiko uliokadiriwa makadirio ya kiufundi sana. Kwa hiyo basi uhai ni hakika changamani kutokana na sifa nyingi mno. Basi sehemu ya sifa za hakika hiyo hukunjuka na kufunuka na hudhihiri kutengana kwake na kuhitilafiana kwake baadhi kwa baadhi nyingine, kupitia mmiminiko wake katika mikondo ya milango ya fahamu ambayo inachukua kila mlango mmoja kati yake rangi moja katika rangi ya sifa hizi na majina. Ama sehemu yake kubwa hakika inajitangaza yenyewe kupitia hisia zilizowekewa (Uhai). Kisha hakika (Uhai) unajumuisha riziki, rehema, uangalizi na hekima, ambazo kila moja kati yake inakwenda katika viumbe na kutawalia jambo lake na kulipangilia, kana kwamba uhai unaongoza vyote hivyo pamoja nao popote unapokuwapo. Kwani mara tu (Uhai) unapokuwa kwenye mwili, tahamaki jina la (Al-Hakim) linadhihiri ndani yake vilevile. Ambapo linaanza kujenga kiota chake mjengo wa kuwekwa vema na kuupangilia mpangilio wenye hekima. Na katika wakati huo huo linadhihiri jina (Al-Karim) vilevile ambapo linaratibu masikani yake na kuyapangilia na kuyapamba kulingana na haja zake, na wakati huo linadhihiri jina la (Ar-Rahiim) vilevile likidhihirisha likieneza fadhila zake na uneemeshaji wake kwa ajili ya kudumisha uhai na kufikia ukamilifu wake, na katika wakati huo huo linadhihiri jina la (Ar-Razzaaq) likawa waziwazi kuonekana ambapo linaandaa mahitajio muhimu ya kilishe - ya kimaada na kimaanawy - ili kubakia huo uhai na kukunjuka kwake, bali sehemu yake huiweka akiba mwilini. Yaani Uhai ni kama mboni ambayo hukusanyika hapo mionzi ya mwanga mbalimbali, basi sifa anuwai zinaingilia katika maisha baadhi yake ndani ya baadhi uingiliaji ambao unafanya kila sifa kati ya hizo ni sawa na nyingine, kana kwamba uhai kwa ukamilifu wake ni (Elimu) kama ambavyo huo uhai ni (Uweza) wakati huo huo, nao ni (Hekima) na (Rehema) sawa kwa sawa. Na kama hivi (Uhai) umekuwa kwa msingi wa ainisho lake hili lenye kujumuisha ni kioo kinachoakisi (Hali ya mkusudiwa kwa haja zote) ambayo ndani yake kunapatikana mambo ya dhati ya kiungu. Na kutokana na siri hii vilevile tunakuta kwamba (Aliye hai Msimamizi wa kila kitu (s.w)), ameumba uhai kwa wingi mno na wingi wa kuenea na ameutawanya katika maeneo yote ya uwepo, akijaalia kila kitu kuwa kinaogelea kuzunguka uhai na kinatiishwa kwa ajili yake, basi hapana shaka kwamba jukumu la uhai ni tukufu. Naam, hakika kutekeleza jukumu la (Kioo chenye kuakisi) kwa ajili ya midhihirisho ya kiungu (Mwenye kukusudiwa kwa kila haja) sio jambo jepesi wala jukumu rahisi, ambapo tunaona mbele yetu likiwa dhahiri kwa kuonekana aina zisizohesabika wala kudhibitika za (Uhai) zinaumbwa kila wakati, na kwamba roho zake ambazo ndio mashina yake na dhati zake, zinaumbwa mkupuo mmoja kutoka katika kutokuwepo na kutumwa aina kwa aina nyingi za walio hai katika medani ya uhai moja kwa moja. Je, hayajulishi yote haya juu ya kupasa kuwepo kwa dhati tukufu takatifu sana na (Al-Hayyu Al-Qayyum) ambayo ina sifa takatifu na majina mazuri wazi mno kuliko kujulisha kwa mng’ao wa vitu vya ardhi juu ya jua? Basi kama ambavyo ambaye haitakidi kuwepo kwa jua, na kujifanya hajui sifa zake zenye kushuhudiwa kwenye vitu, hapana shaka kwamba mtu huyo analazimika kuukana mchana uliojaa nuru ya jua, hali kadhalika yule ambaye haitakidi kwa uwepo wa huyo (Al-Hayyu, Al-Qayyuum, Mwenye kuhuisha na Mwenye kufisha) ambaye nuru yake inadhihiri kwa jua la upekee juu ya uwepo wote, basi mtu huyo analazimika vilevile kukanusha uwepo wa walio hai ambao wanajaza Ardhi, bali wanajaza wakati uliopita na wakati ujao kwa pamoja. Na wakati huo hataona mahali kwa ajili ya nafsi yake isipokuwa baina ya wanyama au wapotevu zaidi kuliko hao wanyama na hapo atakuwa katika ngazi ya visivyo na roho.

§24

لَٓا اِلٰهَ اِلَّا هُوَ كُلُّ شَى۟ءٍ هَالِكٌ اِلَّا وَج۟هَهُ لَهُ ال۟حُك۟مُ وَ اِلَي۟هِ تُر۟جَعُونَ Hakika umauti kama uhai ni hoja angavu ya kiungu ya Bwana Mlezi, nayo ni hoja katika upeo wa nguvu juu ya umoja, mfano wa uhai, kwani kwa kujulisha kwa aya ﴾ الَّذِي خَلَقَ الْمَوْتَ وَالْحَيَاةَ ﴿. Hakika umauti sio kutokuwepo, wala kutoweshwa au kumalizika, wala mchezo wa puo, na wala kumalizika kwa dhati pasi na mtendaji, bali ni kuruhusiwa kutoka katika majukumu, kutoka kwa Mtendaji Mwingi wa hekima, nako ni kubadilisha kwa mahali kwenda mahali pengine, kubadilisha mwili kwa mwili mwingine, kukoma kwa majukumu, na kuwa huru kutoka kwenye jela ya kiwiliwili, na umbo lililopangika jipya kulingana na hekima ya kiungu. Kama tulivyobainisha katika (Andiko la kwanza). Naam, kama ilivyo kwamba vilivyomo vilivyo hai vilivyosambazwa Ardhini kote, uhai wake unaashiria kwa Muumba mwenye hekima zote na katika umoja wake. Basi hivyo vilivyo hai kwa kufa kwake vinashuhudia vilevile juu ya umilele wa huyo aliye hai Mwenye kubakia, na kuashiria katika umoja wake (s.w). Na kwa kuwa sisi tumejadili katika (Neno la ishirini la na mbili) hakika hoja ya kukinaisha juu ya umoja na hoja yenye nguvu juu ya umilele, kwa hiyo tunaelekeza huko. Isipokuwa sisi hapa tutabainisha nukta muhimu tu nayo ni: Hakika walio hai uwepo wake kama unavyojulisha juu ya Muumba Aliye hai hakika vinashuhudia kwa kufa kwake juu ya umilele wa Aliye hai Mwenye kubakia na juu ya umoja wake. Na tuchukue uso wa Ardhi kuwa ni shahidi wa hilo, hakika ya mpangilio mzuri uliokunjua umiliki wake juu ya Ardhi yote na ambao unadhihiri kwetu kupitia mandhari yake wazi wazi unashuhudia ushahidi wa kweli juu ya fundi Mweza. Wakati majira ya baridi yanapofunika sanda yake ya barafu nyeupe juu ya uso wa Ardhi ya majira ya machipuo, na walio hai waliokuwa wakipamba kwa uhai juu yake wanakufa, hakika ya mwonekano wa umauti huu huhamisha mtazamo wa mwanadamu kwenda mbali ya wakati uliopo, basi anapanda ndani ya chombo cha mawazo ya kufikirika kuelekea wakati uliopita ambao yamepitia juu yake majeneza ya kila majira ya machipuo yaliyoondoka, wakati huo hufunguka mbele ya macho mandhari ya umauti na uhai kunjufu zaidi kuliko uhai huu uliofungika kwenye muda uliopo sasa. Kwa sababu kila majira ya machipuo katika kiasi kisichodhibitika katika majira manne, yalikuwa yameshehenishwa ujazo wa Ardhi kwa miujiza ya uweza wa kiungu, na yanamtambulisha mwanaadamu kwa ujio wa vilivyomo vyenye kutoa kwa machipuo uhai na kujaza Ardhi yote katika majira ya machipuo yafuatayo. Kwa hivi tunakuta kwamba majira ya machipuo yanashuhudia ushahidi kwa kipimo kikubwa sana na kwa sura ya kupendeza sana na kwa daraja ya nguvu zaidi, juu ya Muumba Mwenye Utukufu, Mweza mwenye Ukamilifu, Hai Mwenye kusimamia kila kitu na nuru ya milele, yanaashiria juu ya Umoja wake, na umilele wake (s.w). Basi umauti huu unabainisha dalili za wazi kufikia hadi inakulazimisha pamoja nayo kusema kwa dhahiri: (Nimemwamini Allah Mmoja wa pekee). آمَنتُ بِالله الوَاحِدِ الأَحَد Hitimisho: Ni kwamba kwa mujibu wa hekima iliyomo ndani ya aya: وَيُحْيِي الْأَرْضَ بعْدَ مَوْتِهَا hakika ya Ardhi hii hai kama inavyomshuhudia Muumba Mwingi wa Hekima (s.w) kwa uhai wake, hakika kwa umauti wake huugeuza uoni katika kuchunguza miujiza ya uweza wa Kiungu ambao unazifuma mbawa mbili za wakati, uliopita na mustakabali, Allah huonesha kwa umauti huu mbele ya macho ya mwanadamu maelfu ya majira ya machipuo badala ya majira moja ya machipuo, basi badala ya kushuhudia muujiza mmoja tu juu ya uweza wake (s.w) nao hapa ni (Majira yaliyopo ya machipuo) kwa umauti huu ulioingia kwenye majira ya machipuo unashuhudia maelfu ya miujiza. Basi kila majira moja ya machipuo kati hayo maelfu ya majira ya machipuo, yanashuhudia ushahidi wenye nguvu mno juu ya umoja kuliko majira ya machipuo yaliyopo, kwa sababu yaliyoondoka kuelekea upande uliopita yameondoka kuelekea huko kwa sababu za dhahiri za kuja kwake ambazo hazina sifa ya kubakia, basi sababu ambazo huondoka na kuja hazina taathira katu katika kuleta majira mapya ya machipuo baada ya majira ya machipuo yaliyoondoka, bali Mweza Mwenye utukufu ambaye hageuki wala hatoweki ndiye ambaye ameyaumba upya na kayafungamanisha kwa hekima zake na sababu zenye kuonekana na kuyatuma katika sura ya kupendeza kuelekea medani ya kushuhudia. Ama sura za ardhi ambazo zitakazokuja kwenye muda wa baadaye, na yenye kupambika maua kwa majira ya machipuo yenye kutweta kwa uhai, yanashuhudia ushahidi wenye nguvu zaidi kuliko kushuhudia kwake juu ya majira ya machipuo ya sasa, kwa sababu kila majira ya machipuo yanayokuja mustakabali kwa hakika huja huko kutoka katika hali ya kutokuwepo, na kutokana na kisicho kitu, na kuletwa kutoka mahali maalum, na kwa ajili hiyo hubebeshwa jukumu maalum. Basi ewe mwenye kughafilika uliyefutwa katika tope la asili, na mwenye kuzama humo! hakika ambaye mkono wa uweza wake haudhihiri katika Mustakabali ijayo yote, na asiyeacha alama za mkono huu juu ya muda uliopita wote, vipi ataweza – na umbali ulioje kwake jambo hilo – kuingilia katika uhai wa Ardhi? Na je inayumkinika kwa sadifa na Asili ambazo hazitokani na kitu viingilie katika jambo la uhai juu ya Ardhi? Ukiwa ni mkweli na unataka kuiokoa nafsi yako kutokana na dhiki hii, basi karibiana na hakika na useme: Hakika Asili ikiwa ni kitu kilichopo basi ni daftari la uweza wa kiungu na si vingine. Ama kusadifiana sio isipokuwa ni pazia ya hekima ya kiungu iliyojificha ambayo inafunika ujinga wetu.

§25

Hakika chenye kupigwa kwa vyovyote kinajulisha juu ya mtendaji, naye ni mpigaji, na kilichotengenezwa vema kinapasisha fundi mtengenezaji vema, na kuwepo kwa mtoto kunahitajia ulazima wa kuwepo mzazi, na chini kunalazimu juu, na kama hivyo. Na wanazuoni wameyapa jina mfano wa mambo haya kwa istilahi ya (Mambo ya nyongeza) yaani ya uwiano, yaani halipatikani moja bila ya mwingine. Basi yote katika mambo haya kutokana na (Yamkini) sawa katika mambo madogo ya sehemu za ulimwengu au ya jumla yake, yanajulisha kupasa. Na yanayoshuhudiwa katika yote katika marejesho ya vitendo yanajulisha juu ya kitendo cha mmoja, na yanayoshuhudiwa katika yote kutokana na hali ya uumbaji yanajulisha juu ya hali ya Muumba, na yanayoshuhudiwa humo kutokana na wingi na uchangamani yanalazimisha umoja, basi kupasa, kitendo, hali ya uumbaji na umoja, kwa uwazi vinalazimu na kwa vyovyote ambaye mwenye kusifika na (Aliye wajibu, Mtendaji, Muumbaji na Mmoja) ambaye sio wa yamkini, wala mwenye kutendeka, wala mwenye kuumbwa, wala sio Mwingi na wala sio changamani. Na kwa msingi huu hakika ya vilivyomo ulimwenguni katika yamkini, yaliyomo katika kutendeka, yaliyomo katika hali ya kuumbwa, yaliyomo katika wingi na yaliyomo katika uchangamani, yanashuhudia ushahidi wa wazi juu ya dhati iliyo wajibu kuwepo, moja ya pekee, Muumba wa kila kitu na Mwenye kutenda tu anayoyataka. Hitimisho: Kama inavyoshuhudiwa (Kupasa) kupitia hali ya (Yamkini) na inashuhudiwa (Tendo) kupitia (Matendo) na inashuhudiwa (Umoja) kupitia (Wingi), kama inavyojulisha kuwepo kwa kila moja kati ya hivyo juu ya kuwepo kwa kingine ujulisho wa kukinaisha, vivyo hivyo sifa zenye kushuhudiwa juu ya vilivyomo kama hali ya (Kuumbwa na kuruzukiwa) (Yaani kiumbe kuwa kimeumbwa na chenye kupewa riziki) kunajulisha mambo (Uumbaji na utoaji riziki) ujulisho wa kukinaisha, basi kuwepo kwa sifa hizi vilevile kwa vyovyote kunajulisha na kwa uwazi juu ya (Muumba wa kila kitu Mtoa Riziki na Fundi Mwenye kurehemu). Yaani hakika kila kilichopo kinashuhudia juu ya (Dhati takatifu mno ya aliye wajibu kuwepo) na juu ya mamia ya majina yake mazuri katika yanayobeba miongoni mwa mamia ya mifano ya sifa hizo. Ikiwa hujakubali ewe mwanadamu shahidi zote hizi kwa hiyo inatakikana kwako kukanusha sifa hizo zote.

§26

Hakika aina za uzuri unaong’aa, na maumbo ya uzuri wenye kuvutia, ambao unameremeta juu ya sura za viumbe vinavyotoweka haraka, kisha kufuatana kwa uzuri huu na kufanyika kwake upya kwa kufanyika upya kwa viumbe hivi, na kuendelea kwake kwa kuendelea kufuatana kwake. Hakika si vingine bali inadhihirisha kwamba ni kivuli katika vivuli vya midhihirisho ya uzuri wa kudumu haugeuki wala hautoweki. Timamu kama ilivyo kumeremeta kwa mapovu katika uso wa maji laini, na kufuatana kwa mng’ao huu katika kufuatana kwa mapovu inajulisha hakika ya mapovu na mawimbi yanayoelea kwenye utandaaji wa maji hakika vinashika nafasi ya vioo vyenye kuakisi mionzi ya jua lenye kubakia. Inang’aa aina za uzuri vilevile katika vilivyomo vyenye kumiminika katika mto wa wakati unaotembea unaashiria uzuri wa milele, na inajulisha kwamba hivyo vilivyomo hakika vinashika nafasi ya alama katika uzuri huo. Kisha kinachotetemesha moyo wa ulimwengu kutokana na mapenzi ya dhati na ashiki ya kweli inajulisha mwashikiwa wa kudumu na kubakia, ambapo kama hakidhihiri jambo katika tunda la mti wa ulimwengu maadamu halipo kwenye mti wenyewe, na hivyo hivyo ashiki ya kiungu tamu ambayo inatawalia moyo wa mwanadamu, naye ni tunda la mti wa ulimwengu, inabainisha ashiki safi na mahaba ya kweli kwa maumbo mbalimbali, imewekwa katika hakika ya ulimwengu wote na kudhihiri dhihiri kwa maumbo mbalimbali. Mapenzi haya yenye kumiliki moyo wa ulimwengu hubainisha mpendwa wa kudumu milele. Kisha yanayoendeshwa na nyoyo za walio macho waongofu katika wateule wa watu, na kuvutika wanakohisi, na mapenzi yanayowazidia, na jaziba wanazohisi, na kutamani na mapenzi yanayotoka kwa kasi kutoka vifuani mwao, hakika yanaonesha mapindo ya mbavu za ulimwengu yanasumbuliwa na yanayomsumbua mwanadamu, na inakaribia kuchanika chanika kutokana na ukali wa kuvutika kwake na ukubwa wa mivuto yake, ambayo inadhihiri kwa sura mbalimbali. Na kuvutika huku hakutokani isipokuwa kwa kivutio cha hakika, na uvutano wakubaki wa milele. Kisha laini mno wa watu kwa tabia na wapole zaidi kwa hisia, na wenye kunawiri zaidi kimoyo, nao ni mawalii wema katika watu wa kufunuliwa na kushuhudia wametangaza kwa kuafikiana kwamba giza la nafsi zao limetokomea kwa kung’ara kwa nuru ya midhihirisho ya mwenye utukufu, na wakaonja utamu wa utambulisho wa Mzuri Mwenye utukufu, na kujipendezesha kwao. Basi tangazo lao hili ni ushahidi unaotamka juu ya aliye (Wajibu kuwepo) na anajitambulisha kwa mwanadamu kupitia wao. Kisha kalamu ya kuweka uzuri na kupendezesha ambayo inaweka vizuri nakshi zake katika uso wa viumbe, inajulisha kwa uwazi juu ya uzuri wa majina ya mmiliki wa kalamu ya mpendezeshaji. Na kama hivyo uzuri ambao unang’aa kutoka kwenye uso wa Ardhi, na ashiki ambayo kwayo moyo wake unaopiga. Na kuvutika ambako kunakojaa moyo wake, na kufunuliwa na kushuhudia kunakoonwa na jicho lake. Na mvuto na kupendezesha katika mkusanyiko wa ulimwengu wote, inafungua dirisha maridadi mno na la kinuru lenye kuangaza mbele ya akili na nyoyo zilizo macho, anadhihiri kutokana nayo yule Mzuri mwenye utukufu, ambaye ana majina mazuri, na huyo mpenda mwenye kubaki na mwaabudiwa wa azali. Basi ewe mwenye kughurika mpotevu katika giza la kimaada! Na ewe mwenye kughafilika mwenye kupinduka katika giza la dhana na mwenye kusakamwa na kamba za mambo yenye kuchanganya! rejea katika fahamu yako, na upande hadhi inayolingana na mwanadamu, tazama kupitia madirisha haya manne, na ushuhudie uzuri wa umoja, na upate ukamilifu wa Imani, na uwe mwanadamu wa kweli.

§27

اَللّٰهُ خَالِقُ كُلِّ شَى۟ءٍ وَهُوَ عَلٰى كُلِّ شَى۟ءٍ وَكٖيلٌ Kutokea kwenye dirisha hili tutatazama katika yaliyomo kwenye ulimwengu (Miongoni mwa sababu na vyenye kusababishwa), basi tunaona kwamba hakika sababu za hadhi ya juu na tukufu mikono yake ni mifupi kufikia vyenye kusababishwa duni na ni zenye kushindwa kutambua yanayotokana nazo. Kwa hiyo sababu si chochote isipokuwa ni pazia na vizuizi, basi anapatisha (Vyenye kusababishwa) sio sababu zenyewe. Na tufafanue maneno haya kwa mfano: Uwezo wa kutunza kumbukumbu katika ubongo wa mwanadamu, nao una ukubwa wa punje ya haridali iliyowekwa kwenye pembe katika pemba za ubongo, tunauona kana kwamba ni kitabu chenye kukusanya, bali ni maktaba ya taarifa muhimu ya maisha ya mwanadamu, ambapo inakusanya nyaraka za kumbukumbu za matukio yote ya maisha yake bila ya kuchanganya wala kusahau. Je ni sababu ipi miongoni mwa sababu yawezekana kudhihiri kwa ajili ya kufafanua na kutafsiri muujiza huu wa dhahiri wa uweza wa kiungu? Je ni hiyo mizingo ya ubongo? Au hakika ya atomu za vyumba vya vidogo vidogo vya ubongo navyo vikiwa bila ya utambuzi vinaweza kuhifadhi na kusajili? Au pepo za sadfa za holela? Wala haiyumkiniki muujiza huu wa wazi isipokuwa kutokana na utengenezaji wa (Fundi Mwenye hekima) amejaalia (Nguvu hiyo ya kutunza kumbukumbu) kuwa ni maktaba au mahali au daftari linalokusanya nyaraka za amali za mwanadamu, ili kumkumbusha kwamba Mola wake Mlezi haachi dogo wala kubwa isipokuwa amelidhibiti, na ili kulionesha mbele ya mahala pa maonesho makubwa siku ya hisabu. Chukua (Nguvu yenye kutunza kumbukumbu) kwenye akili ya mwanadamu, na uipimishe na vitu vingine vyenye kusababishwa miongoni mwa mayai, kokwa, mbegu na mfano wake katika miujiza ya ajabu iliyodogeshwa, utaona popote utakapoelekeza jicho lako na katika chenye kutengenezwa chochote kiwacho, hakika upo mbele ya maajabu ya utengenezaji vema sababu yoyote katika sababu haiwi na nguvu kwa jambo hilo, bali hata zikikusanyika sababu zote ili kupatisha ufundi huo wenye kufurutu ada ungedhihirisha kushindwa kwake kushindwa kabisa japo wao kwao watakuwa ni wenye kusaidiana. Tulichukue jua kwa mfano, ambalo linadhaniwa kuwa ni sababu kubwa, kama lingeambiwa hilo jua kwa kukadiria kuwa lina utambuzi na hiari: (Ewe jua kubwa! Je unaweza kupatisha mwili wa nzi mmoja?) basi bila shaka hakika jua hilo litajibu likisema: (Hakika alichonipa Bwana wangu Mlezi miongoni mwa mwanga na kunijazia joto na rangi, hakunipi sifa ya uumbaji, wala hainipi yanayohitajika kupatisha nzi ikiwemo macho na usikivu na uhai, mimi si mmiliki wa chochote kati ya hivyo katu, basi jambo hili ni juu ya uwezo wangu kabisa). Naam, kama ufundi wa ajabu unaodhihiri kwenye (Vyenye kusababishwa) na kuvutia kwa uzuri wake umeziondosha sababu na kuzinyang’anya uweza wa kuumba, na vimetujulisha kwa ulimi wa hali zake juu ya mwenye kusababisha sababu, na kusalimisha mambo yote mkononi mwa Allah (s.w) kama ilivyokuja kwenye aya tukufu. وَإِلَيْهِ يُرْجَعُ الأَمْرُ كُلُّهُ kadhalika matokeo ambayo yamekabidhiwa kwa vyenye kusababisha na shabaha zinazotokea na faida zinazopatikana kutokana nazo, vyote vinadhihirisha wazi kwamba nyuma ya pazia ya sababu kuna Bwana Mlezi Mkarimu, Mwingi wa hekima, na mwenye kurehemu, na hakika tunachokiona katika vitu sio kingine isipokuwa ni katika utengenezaji wake na ufundi wake (s.w). Hii ni kwa kuwa (Sababu) ambazo zenyewe zipo bila ya utambuzi ni zenye kushindwa kwa ujumla kutazama, japo kutazama, shabaha ya kitu kilichosababishwa, wakati ambapo kiumbe yeyote anapita kwenye uwepo hakusudiwi hekima moja tu bali hekima nyingi sana na faida tele na shabaha mbalimbali. Yaani hakika Bwana Mlezi Mwingi wa Hekima Mkarimu ndiye ambaye hupatisha vitu kisha kuvituma kwenda katika ulimwengu huu na kujaalia faida hizo ni malengo ya kuwepo kwake. Basi Mathalani: Hakika sababu zenye kudhihiri za kuwepo kwa mvua ni zenye kushindwa kwa hali zote, na ziko mbali umbali wote na kuwahurumia wanyama, au kutazama mambo yao na kuwahurumia na iteremke kwa ajili yao. Kwa hiyo basi ambaye amedhamini kuwaruzuku ni Muumba Mtukufu ambaye anatuma mvua na kuwasaidia akiwa anawahurumia, na kana kwamba hiyo mvua ni rehema iliyofanyika mwili kwa wingi wa yaliyomo katika athari za rehema na faida tele. Na kwa sababu hii mvua imepewa jina kuwa ni (Rehema). Kisha hakika mapambo ya ajabu na uzuri wenye kutabasamu kwa mimea na wanyama ambayo inajaza uso wa viumbe kwa ujumla, na mandhari zote za kiurembo juu yake, yanajulisha kwamba nyuma ya pazia la ghaibu kuna mwendeshaji anataka kuitambulisha nafsi yake na kuipendezesha kwa viumbe hivi vizuri vya ajabu na yanajulisha juu ya kupasa kuwepo kwake na umoja wake. Kwa hiyo upambaji wenye kupendeza katika vitu na yaliyomo katika mandhari yake miongoni mwa uzuri wa ajabu na namna yale yenye alama ya hekima, yote yanajulisha kwa kukinaisha juu ya sifa mbili za kutambulisha na kupendezesha. na hizi sifa mbili (Kujitambulisha na kupendezesha) zinashuhudia kwa uwazi juu ya Fundi Mweza Mwenye kutambuliwa mwenye kupendwa, ukiachilia mbali kushuhudia kwake juu ya umoja wake (s.w). Hitimisho: Hakika ya sababu ambayo tunaiona ni kitu cha kawaida kabisa, na yenye kushindwa ushindwaji kabisa, imeegemea kwake chenye kusababishwa katika ukomo wa ufundi na thamani. Basi (Chenye kusababishwa) hiki kilichotengenezwa vema bila shaka kinaiondoa hiyo sababu yenye kushindwa kutekeleza upatishaji wake, kisha hakika ya shabaha ya (Chenye kusababishwa) na faida zake inaziondosha sababu ambazo hazina ujuzi na hazina uhai kati yake na kuzisalimisha kwenye mkono wa Mtengenezaji Mwenye hekima zote, kisha hakika ya mapambo yenye kuwekwa nakshi katika mionekano ya chenye (Kusababishwa) na maajabu ya rehema yanayodhihiri juu yake yanaashiria kuwa Mtengenezaji mwingi wa hekima anataka kutambulisha uweza wake kwa mwenye utambuzi katika viumbe wake, na kukijipendezesha kwao. Basi ewe mwenye kuabudu sababu ewe masikini!. Nini tafsiri ya hakika hizi tatu muhimu ambazo tumeziweka mbele yako? Na vipi utaweza kuikinaisha nafsi yako kwa dhana zako? Ukiwa mwenye akili basi chana pazia za sababu na useme: (Ni yeye mwenyezi mungu peke yake hana mshirika) na ukomboke kutokana na dhana zenye kupoteza.

§28

وَمِن۟ اٰيَاتِهٖ خَل۟قُ السَّمٰوَاتِ وَال۟اَر۟ضِ وَاخ۟تِلَافُ اَل۟سِنَتِكُم۟ وَ اَل۟وَانِكُم۟ اِنَّ فٖى ذٰلِكَ لَاٰيَاتٍ لِل۟عَالِمٖينَ Ukichunguza viumbe hivi tutashuhudia kwamba katika kila kitu kuanzia kwenye vyumba vidogo vya mwili na kuishia katika jumla ya ulimwengu wote, ni hekima enevu na mpangilio uliowekwa vema. Basi katika kupekua kwetu vyumba vidogo vya mwili tunakuta kwamba udabiri wa ukomo wa umuhimu ukipangilia mambo ya vyumba hivyo vidogo mno, unavipanga kulingana na amri ya anayeona masilahi ya mwili wote, na kuendesha mambo yake. Kama ilivyo kwamba sehemu ya vyakula huwekwa akiba mwilini kwa sura ya shahamu ya ndani hutumika wakati wa haja, hivyo hivyo tunakuta katika kila kimoja kati ya hivyo vyumba vidogo ukubalifu madhubuti wa kuhifadhi. Kisha tunatazama mimea tunaikuta hakika inaishi katika starehe ya ukarimu wenye kuenea. Na tunatazama katika nguzo kuu za ulimwengu tunakuta kwamba kutawala na kunawirisha katika upeo wa utukufu unauhifadhi kutoka pande zake zote na kuitimizia shabaha kubwa tukufu. Na tunatazama jumla ya ulimwengu wote, tahamaki unadhihiri mbele yetu kana kwamba ufalme ulioratibika sehemu zake, au mji wenye kupendeza sana kwa uzuri, au kasri refu la kifahari, tahamaki tuko mbele ya mifumo madhubuti inapandisha kasri hiyo kufikia hekima za juu na shabaha za thamani. Kama tulivyothibitisha katika (Kituo cha kwanza) katika (Neno la thelathini na mbili): Hakika ya vilivyomo vimefungamana baadhi yake kwa kufungamana kimaanawy madhubuti hadi kwamba hakuachi nafasi katu ya kuingilia kwa mshirika yeyote, hata kwa kiasi cha atomu ya kuingilia, kuanzia kwenye atomu na kukomea kwenye mfumo mkubwa wa sayari nyota na sayari. Basi asiyekuwa Mtiishaji wa hukumu yake mifumo yote ya anga, nyota na sayari na anamiliki hatamu ya mambo yake na kusarifu katika funguo za mambo yake, haiwezekani kuangusha hukumu yake, na kupitisha amri yake kwenye atomu moja. Yaani kwa ibara nyingine, mwenye kuwa Bwana Mlezi wa hakika juu ya atomu moja yatakikana pia kuwa Mmiliki wa funguo za ulimwengu wote. Na katika mwanga wa tuliyofafanua na kuthibitisha katika (Kituo cha pili) cha (Neno la thelathini na mbili): Kwamba anayeshindwa kutamalaki mbingu zote atashindwa kuchora misitari ya alama za mwanadamu, yaani asipokuwa Bwana Mlezi wa vilivyomo vya mbingu na Ardhi, hawezi kuchora mionekano ya uso wa mwanadamu na kuweka juu yake alama zake zenye kumpambanua. Na kama hivyo unakuta mbele yako dirisha pana upana wa ulimwengu wote ukiangalia kupitia dirisha hilo utakuta – hata kwa jicho la akili – hakika aya tukufu ijayo, imeandikwa kwa herufi kubwa za wazi juu ya kurasa za ulimwengu wote. اللَّهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ ۞ لَهُ مَقَالِيدُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ kwa hiyo basi asiyeweza kuona herufi dhahiri kubwa zilizoandikwa juu ya ukurasa wa viumbe, sio isipokuwa ni mmoja katika aina tatu: Ima ni asiyekuwa na akili, asiye kuwa na moyo au ni mwanadamu kwa sura ya mnyama wa matazamio.

§29

وَ اِن۟ مِن۟ شَى۟ءٍ اِلَّا يُسَبِّحُ بِحَم۟دِهٖ Nilikuwa nikitembea katika usuhuba wa ugeni wangu, natembea na fikira, na nazunguka pamoja na mawazo na mazingatio, miguu yangu ikaniongoza kwenye uso wa konde lililoshehenishwa kijani kiwiti, likanipigia sauti – kwa kustahi – kutokea kati kati ya busati hili la kijani kiwiti, ua la njano lenye kung’ara umanjano likaelekeza shingo yake kwangu likiongea nami kwa mapenzi na mahaba, likaamsha hisia zangu na shauku zangu kuelekea maua mfano wa hilo nilikuwa nikiyakuta katika maeneo ya mji wangu (Van) na katika baki ya miji mengine ambayo ilikuwa inakaribisha ugeni wangu mara baada ya nyingine, maana hii ikaingia ghafla moyoni mwangu, na sasa hapa ndio mimi ninaelezea kama ilivyokuja: Ua hili la hadhi ya juu sio chochote isipokuwa ni mwandiko wa aina moja katika ukurasa wa uzuri, na muhuri anapiga chapa kwa muhuri huo Muumba wa uzuri barua yake ya kijani kiwiti kwenda kwa ulimwengu. Basi mwenye kuwa ua hili ni uandishi wake na nakshi yake juu ya busati la kijani kiwiti hakika sampuli zote za ua hili kwa hiyo maua hayo ni mihuri yake katika busati la Ardhi yote, na alama ya umoja wa ufundi wake. Na mwisho wa sura hii yenye kufikirika imepatikana moyoni taswira hii, hakika ya muhuri ulioigiwa barua yoyote iwayo, hakika si jambo lingine bali inajulisha juu ya mwenye barua hiyo. Basi ua hili hakika ni muhuri wa ki Rahmani juu ya barua ya Ar-Rahamani. Na barua hii ni kilele cha kilima kidogo kilichoandikwa ndani yake maneno ya fasaha ya mimea na majani, na kilichochimbwa juu yake aina za mapambo yenye kutengenezwa kwa hekima. Kwa hiyo barua hiyo inarudi kwa mwenye muhuri huu. Kisha nikazama kwenye kuchunguza zaidi na zaidi, tahamaki kilele hiki kizuri kinageuka katika kuangalia kwangu na kinachukua sura ya muhuri mkubwa na wa wazi juu ya barua ya uwanda huu ulioendelea mbali. Na tambarare iliyokunjuka ikanyooka mbele ya mawazo yangu barua ya ki Rahmani yenye kupendeza, muhuri wake ni hiki kilele kizuri, hakika taswira hii imenipelekea katika hakika hii: Kama ilivyo kila muhuri juu ya barua yoyote unaashiria kwa mwenyewe, basi kila kitu ni kama muhuri kinaegemeza vitu vyote inavyovizunguka kwa muumba wake Mrehemevu. Na kama hivyo, hakuna kitu isipokuwa kinakuwa ni dirisha kubwa la Tawhidi kwa kiwango kwamba linasalimisha vitu vyote kwa Mmoja wa pekee. Kila kitu hasa vilivyo hai kinamiliki katika nakshi na hekima na ufundi wa ajabu kwa namna ambayo hakika ya ambaye amekiumba kwa sura hii ya ajabu ni mweza wa kuumba vitu vyote, yaani ambaye hawezi kuumba vitu vyote haiyumkiniki kuumba kitu kimoja. Ewe mwenye kughafilika! Zingatia katika uso wa viumbe hivyo si kingine isipokuwa ni sawa na barua zenye kuingiliana baadhi yake ndani ya baadhi nyengine, imetumwa kutoka kwa yule wa pekee Mwenye kutegemewa katika haja zote. Na kwamba kila barua kati ya hizo imepigwa muhuri kwa kiasi kisichohesabika katika mihuri ya Tawhidi. Je, ni nani anayethubutu kukadhibisha shahidi za mihuri hii isiyokuwa na ukomo? Ni nguvu ipi inayumkinika nguvu hiyo kuficha sauti za shahidi hizi za kweli? Nawe ukisikiliza kwa sikio la moyo kwa yoyote kati ya hizo unaisikia inarudia rudia: أَشْهَدُ أنْ لاَ إلهَ إِلاَّ الله

§30

لَوْ كَانَ فِيهِمَا آلِهَةٌ إِلَّا اللَّهُ لَفَسَدَتَا كُلُّ شَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ لَهُ الْحُكْمُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ Hili ni dirisha ambalo wanachungulia kutokea humo watu wa elimu ya Al-Kalam ambao wamepita katika kuthibitisha kuwepo kwa Allah (s.w) njia iliyoimarishwa kwa dalili za (Yamkini) na (Kuzuka). Nasi tunapoelekeza maelezo ya ufafanuzi wa dalili hizo katika dhana zake katika vitabu vikubwa vya wanazuoni wakubwa kama (Sharhul Mawaqifi) na (Sharhula maqasid) tunataja hapa katika mionzi ya mimuliko ya nuru ya Qur’an iliyofunika moyo, na kupenya kwake kupitia dirisha hili. Hakika sifa za Kuamrisha na Kutawala zinahitajia kukataa mashindano, na kukataa ushirikiano, na kukinga kuingiliana kwa namna yoyote iwayo. Na kutokana na hapa tunaona kwamba wakipatikana wachaguliwa wawili katika kijiji, mfumo wa kijiji utaharibika na kutetereka kwa amani ya watu na raha yao, iwapo kuna wakurugenzi wawili upande mmoja, au wakuu wawili katika jimbo moja, hapo mambo yatavurugika na kuchanganyika, na watakapo kuwapo wafalme wawili katika nchi hakika fujo litapiga vitambo vyake katika vituo vyote vya nchi, na kusababisha wasiwasi na migongano ambayo mwisho wake sio mzuri. Basi ikiwa mwanadamu ambaye ni mshindwa na muhitaji wa msaada wa wengine, na ambaye anabeba kivuli cha kisehemu dhaifu katika sifa ya kuamrisha na kutawala, hakubali kuingilia kwa yeyote miongoni mwa mfano wake katika mambo yake, na anakataa vikali kushindana. Naam, ikiwa mwanadamu mshindwa hii ndio hali yake basi vipi kwa sifa ya kuamrisha ya Mweza wa hali zote na utawala wa Mfalme Mkuu Mlezi wa walimwengu? Pima wewe mwenyewe vipi itatawala kanuni ya kukataa kuingiliana na kutamalaki katika ulimwengu wote. Yaani hakika ya umoja au upweke ni katika mambo ya lazima ya Uungu, na mahitajio ya Ubwana, ambayo hayaachani nayo. Ukitaka hoja ya kukinaisha juu ya hili, na ushahidi wa kweli juu yake, basi mbele yako mfumo uliokamilika, na mpangilio mzuri mno vyenye kushuhudiwa ulimwenguni. Unakuta mpangilio wa ajabu umeenea katika kila kitu kuanzia kwenye ubawa wa nzi na kuishia kwenye kandili za mbingu, hata mpangilio huu uliowekwa vema unaifanya akili kuwa yenye kushangazwa mbele yake na inakariri kutokana na kuajabia kwake: (Subhanallah, Mashaallaah kaana, Tabaarakallah) na kuporomoka hali ya kusujudu kwa utukufu wa mtengenezaji wake wa ajabu. Kungekuwapo mahali japo kwa kiasi cha atomu pa mshirika vyovyote awavyo, au kuingiliana katika mambo ya ulimwengu vyovyote vile, nidhamu ya mbingu na Ardhi ingeharibika na athari za uharibifu zingedhihiri wazi wazi, na isingekuwa sura hii ya ajabu ambayo ipo mbele yetu. Na amesema kweli Allah Mtukufu ambaye anasema: لَوْ كَانَ فِيهِمَا آلِهَةٌ إِلَّا اللَّهُ لَفَسَدَتَا kwa kujua kwamba aya tukufu ifuatayo: فَارْجِعِ الْبَصَرَ هَلْ تَرَى مِن فُطُورٍ * ثُمَّ ارْجِعِ الْبَصَرَ كَرَّتَيْنِ يَنقَلِبْ إِلَيْكَ الْبَصَرُ خَاسِأً وَهُوَ حَسِيرٌ Hakika vyovyote awavyo mwanadamu kuwa mwenye bidii katika kupekua kwake kasoro, atarudi patupu, jambo ambalo linatujulisha kuwa nidhamu na mpangilio vimo katika upeo wa ukamilifu. Yaani kupangika kwa viumbe ni ushahidi wa kukinaisha juu ya umoja. Ama kwa mnasaba wa (Kuzuka) wamesema wanazuoni wa Al-Kalam: Hakika ulimwengu ni wenye kubadilika, kila chenye kubadilika ni chenye kuzuka, na kila chenye kuzushwa hapana budi kuwa na Mzushaji, yaani Mpatishaji, kwa ajili hiyo ulimwengu hauna budi kuwa na (Mpatishaji wa Tangu). Nasi tunasema: Naam, hakika ya ulimwengu ni wenye kuzuka, ambapo tunashuhudia katika kila zama na katika kila mwaka bali katika kila msimu ulimwengu unasafiri na kukaa mahali pake mwingine, viumbe vinapita, na vinakuja vingine. Basi mweza mwenye utukufu ndiye ambaye anapatisha ulimwengu huu kutoka kwenye kutokuwapo kila mwaka, bali katika kila msimu, bali katika kila siku, na kuyahudhurisha mbele ya wenye utambuzi kisha anayachukua kuelekea kwenye ghaibu, na mahali pake analeta kingine, na kama hivi hufufuliwa mmoja kufuatia mwingine katika mfuatano wenye kuendelea, hali ya kuambatanisha limwengu hizo kwa namna ya kufuatana kwenye mkanda wa zama. Basi unaona majira ya machipuo ni muujiza wazi katika miujiza ya mweza Mtukufu, ndani yake anapatisha vitu kutoka katika hali ya (Kutokuwepo) na anazileta upya limwengu hizo pana pasina kitu chenye kutajwa. Basi ambaye anabadilisha limwengu hizo na kuzileta upya ndani ya ulimwengu mkubwa, sio mwingine isipokuwa Bwana Mlezi wa walimwengu ambaye amekunjua utandao wa ardhi kuwa ni meza ya vyakula iliyojaa wageni wake watukufu, Ama maudhui ya (Yamkini) wana elimu ya Al-Kalaam wamesema: Hakika (Yamkini) ni yenye kulingana sawa ncha mbili, yaani ikiwa iko sawa kutokuwepo na kuwepo kulingana na kitu fulani, hapana budi kuwepo kihusishi na kitilia uzito na kipatishaji. Kwa sababu kilicho yamkini kwa uwazi hakiyumkiniki kupatisha yamkini nyingine mfano wake, yaani haiyumkiniki kupatisha yamkini nyingine, kwa sababu kuwepo kwake kutakuwa ni mfuatano wa duara lililofungwa la (Yaliyo yamkini). Kwa hiyo hapana budi kuwepo (Aliye wajibu kuwepo) anayepatisha vitu vyote. Wanazuoni wa elimu ya Al-Kalaam wameivunja fikira ya (Mzunguko na kufuatana mnyororo) na wakathibitisha ubatili wake kwa hoja kumi na mbili zimeitwa kuwa ni hoja za (Kiarshi na kingazi) na wamekata mfuatano wa sababu na vyenye kusababishwa na kwa hivyo wamethibitisha (Aliye wajibu ku wepo). Nasi tunasema: Hakika kudhihirisha muhuri mahususi wa Muumba Mtukufu juu ya kila kitu kilichopigwa muhuri kila kitu ni hoja nyepesi na yenye nguvu na iliyo wazi mno kuliko hoja ya (Kukatika kwa mfuatano wa mnyororo wa sababu) kisha kufikia kumthibitisha Muumba (s.w). Hakika yamepita kwa neema ya Qur’an (Maneno) yote na (Madirisha) katika mapito haya mepesi ya kukinaisha, na pamoja na hayo hakika mjadala wa (Yamkini) ni mpana mno, ambapo unambainisha muumba kwa pande mbali mbali zisizo na idadi, na zisizofungika na mule walimo pita wanazuoni wa Al-Kalaam katika njia ya kuthibitisha Mtengenezaji kwa uthibitisho wa kukatika mfuatano wa mnyororo, basi njia ni pana mno bila mipaka, ambapo inapelekea katika maarifa yasiyo na mipaka ya kujua aliyewajibu kuwepo. Na ufafanuzi wa hilo kama ifuatavyo: Wakati ambapo tunaona kila kitu, katika kuwepo kwake na katika sifa zake na katika muda wa kubaki kwake na uhai wake, kinarudiarudia ndani ya njia za yamkini na ya uwezekano zisizo na mpaka, tahamaki tunashuhudia kati ya pande hizo ambazo hazina mpaka imepita njia iliyopangika mahususi kwake, na kupewa kila sifa katika sifa zake vile vile kwa mtindo huu uliowekwa mahususi, bali hutunukiwa kwa uhusishaji maalum wa sifa na hali anazozibadilisha kwa mfululizo ndani ya uhai wake na kubakia kwake. Kwa hiyo kupeleka kila kitu katika njia maalum, na kuchagua njia inayopelekea katika hekima maalum, kati ya njia zisizo na ukomo, hakika ni kwa kutaka kwa mwenye kuhusisha, na kwa kuchagua kwa mchaguaji, na kwa kupatisha mpatishaji Mwenye hekima zote. Ambapo utaona kitu kinavikwa vazi la sifa zilizopangika, na hali zilizoratibika maalum mahsusi kwake, kisha unakiona kinapelekwa – yaani kitu hiki – ili kiwe ni sehemu ya mwili changamani, kwa hili hutoka katika kuwa pekee, na wakati huo huongezeka zaidi njia za yamkini, kwa sababu sehemu hii inaweza kuchukua maelfu ya maumbo na mitindo katika huo mwili changamani, na hali ya kuwa sisi tunaona kwamba linatunukiwa hali maalum yenye faida na masilahi, na inachaguliwa hali hii kati ya hali zisizokuwa na mpaka ambayo haina manufaa kati hizo. Yaani zinapelekwa katika kutimiza majukumu muhimu na kufikia manufaa mengi ya mwili huo changamani. Kisha tunakiona hakika kimefanywa kuwa ni sehemu ya mwili changamani mwingine, hapo zinaongezeka zaidi njia za yamkini, kwa sababu mwili huu vilevile huenda ukachukua maumbo kwa maelfu ya namna, wakati ambapo tunaona umechaguliwa hali maalum jumla ya maelfu kwa maelfu katika mitindo na aina mbalimbali, basi unapelekwa katika kutekeleza majukumu mengine. Na kama hivi ulipozama katika yamkini imebainika kwako kwa dhahiri kwamba njia zote hizi zinakufikisha kwa Mwendeshaji mwenye hekima, inakufanya ukinaike ukinaifu uliotimia kwamba kila kitu kinapelekwa katika jukumu kwa amri ya mwamrishaji Mjuzi wa kila kitu. Ambapo vilivyo changamani vyote ni vyenye kuunganishwa kutokana na sehemu, na hii imeunganishwa kutokana na sehemu nyingine. Na kama hivi basi kila sehemu imewekwa katika mahali maalum katika changamani, na ina majukumu yake mahususi katika mahali hapo. Hiyo inashabihiana na uhusiano wa askari pamoja na kikundi chake, kikosi chake askari palatuni yake, trupu, brigedi yake, divisheni yake na jeshi lote. Ana mahusiano maalumu yenye hekima pamoja na miundo yote hiyo ya kiaskari yenye kuingiliana, na ana majukumu yenye kuratibika maalumu pamoja na kila moja kati yake. Na kwa mfano wa seli ambayo kwenye mboni ya jicho lako ina uhusiano wa jukumu na jicho lako, na ina jukumu lenye hekima na masilahi na kichwa chote, hata ikiwa kimechanganyika na kitu cha kisehemu na seli hiyo ungevurugika uongozi wa mwili na afya yake, na ina mahusiano maalum pamoja na mishipa ya shingo na misuli, bali mahusiano na majukumu pamoja na mwili wote, katika mambo yanayotuthibitishia kwamba hiyo seli imepewa mahali hapo maalum katika mboni ya jicho na imechaguliwa mahali hapo kati ya maelfu ya mahali, ili kutimiza majukumu hayo. Na hiyo si kwa vyovyote isipokuwa kwa hekima ya Fundi Mwenye hekima zote. Vyote vilivyopo vya ulimwengu viko katika namna hii, kila moja kati yake kinatangaza kwa dhati yake na sifa zake, kuhusu mtengenezaji wake kwa ulimi wake mahususi, na kinashuhudia juu ya hekima yake kwa kupita kwake katika njia maalum ndani ya njia za yamkini zisizokuwa na mpaka. Na kila ilipoingia katika mwili changamani hutangaza kwa ulimi mwingine kuhusu Mtengenezaji wake ndani ya hizo njia ambazo hazina mpaka katika yamkini. Na kama hivi kila kitu kinashuhudia juu ya Mtengenezaji wake Mwenye Hekima zote na utashi wake na hiari yake, ushahidi kwa idadi ya hizo njia katika njia za yamkini zisizo na mpaka, na kwa idadi ya vilivyounganishwa na yamkini zake na uhusiano wake uliopo, hadi unafika kwenye changamani kubwa. Kwa sababu ambaye anatengeneza kitu fulani kwa hekima kamili katika vyote changamani, na anachunga mahusiano hayo kati yake hawezi kuwa isipokuwa muumba wa vitu vyote changamani. Yaani kitu kimoja ni sawa na shahidi kwa maelfu ya ndimi juu ya Allah (s.w). Bali hakuna maelfu ya shahidi juu ya kuwepo kwake (s.w) na hekima yake na hiari yake peke yake, bali shahidi zipo vilevile kwa idadi ya viumbe, bali kwa idadi ya sifa za kila kilichomo na kwa idadi ya changamani zake. Na kama hivi inapita katika upande wa (Yamkini) shahidi zisizo na mpaka juu ya (Aliye wajibu kuwepo). Basi ewe mwenye kughafilika! Niambie kwa haki ya mola wako, je sio uziwi wa masikio kunako shahidi zote hizi ambazo mwangwi wake unajaa ulimwengu wote huo hakika ni uziwi hakuna baada yake uziwi, na ujinga hakuna baada yake ujinga?

§31

لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ فِي أَحْسَنِ تَقْوِيمٍ وَفِي الْأَرْضِ آيَاتٌ لِّلْمُوقِنِينَ *وَفِي أَنفُسِكُمْ أَفَلَا تُبْصِرُونَ Hapa sisi tupo mbele ya dirisha la mwanadamu, tunachungulia kupitia nafsi ya mwanadamu katika nuru ya Tawhidi, nasi wakati tunaelekeza maelezo ya hilo katika vitabu vidogo na vikubwa vilivyoandikwa kutokana na maelfu ya mawalii na wema ambao wametafiti kwa kina nafsi ya mwanadamu, tunapenda kuashiria ishara chache ambayo ni ilhamu iliyopatikana kutoka katika mwanga wa nuru ya Qur’an tukufu, kama ifuatavyo: Hakika ya mwanadamu ni nakala jumuishi ya sifa mahususi zilizomo kwenye uwepo, ambapo Allah wa haki (s.w) anamtambulisha majina yake yote mazuri yenye kudhihiri kwa sifa pambanuzi zenye kukusanya ambazo ameziweka katika nafsi ya mwanadamu. Tutosheke katika kubainisha hili kwa yale tuliyoyataja katika (Neno la Kumi na moja) na katika Risala nyingine, isipokuwa sisi tutabainisha hapa nukta tatu tu: Nukta ya kwanza: Hakika ya (Mwanadamu) ni kioo chenye kuakisi cha midhihirisho ya majina mazuri ya kiungu, naye ni kioo chenye pande tatu: Upande wa kwanza: Kama ilivyo kuwa giza ni sababu ya kuona nuru, hakika ya giza la usiku na ukali wake hubainisha mwanga na kuudhihirisha kwa namna ya uwazi zaidi. Basi mwanadamu vilevile anatambulisha kwa udhaifu wake na ufakiri wake na kushindwa kwake na ufakiri wake na haja zake, upungufu wake na kasoro zake, anatambulisha uweza wa mweza mwenye utukufu, nguvu yake kuu, utajiri wake wa hali zote na rehema zake kunjufu. Hivyo mwanadamu anakuwa kwa hili kana kwamba ni kioo chenye kuakisi kwa midhihirisho mingi ya sifa za kiungu tukufu. Bali hata udhaifu mkubwa, anaoubeba na maadui alionao wasio na mipaka, vinamfanya anatafuta daima nguzo ya kuishikilia, na maegemeo ya kuegemea. Moyo wake wenye shida haukuti ila Allah (s.w). Naye ni mwenye kulazimika vilevile kutafuta nukta ya kutaka msaada anapata msaada wa haja zake zisizo na ukomo kutoka katika nukta hiyo, na kuziba ufakiri wake usiokoma, na kushibisha matumaini yake yasiyo na ukomo, wala hakuti katika kina cha kutafuta kwake isipokuwa kuegemea, kutokea upande huu, kwenda kwenye mlango wa Mkwasi Mwenye kurehemu, basi ananyenyekea kwake kwa dua na tawasali. Yaani katika kila moyo kuna madirisha mawili madogo kwa upande wa nukta ya kuegemea na kuomba msaada, mwanadamu anatazamia kutokana na pande mbili hizo daima katika uwanja wa rehema ya aliye wa tangu Mwenye kurehemu. Ama upande wa pili: Ni kwamba binadamu ni kioo cha midhihirisho ya majina mazuri, kwani alivyopewa katika vielelezo vya kisehemu katika (Elimu, uwezo, kuona, kusikia, kumiliki na utawala) na mifano yake katika sifa za kisehemu, hufanya kioo chenye kuakisi hujulikana kutakana nacho sifa za hali zote za Allah (s.w), na kudiriki elimu yake na uweza wake na kuona kwake na kusikia kwake na utawala wake na Ubwana wake, basi hufahamika sifa hizo za hali zote za kiungu kwa mnasaba wa hali ya mipaka yake kwake. Na hapana shaka kwamba baada ya hapo atasema na nafsi yake na kusema kwa mfano: Kama mimi nilivyojenga hii nyumba, na ninajua pambanuzi zake, na ninashuhudia pande zake zote na sehemu zake, na ninaiendesha mwenyewe, basi mimi ni mmiliki wake, vilevile hapana budi kwa ulimwengu huu mkubwa kuwepo mtengenezaji wa ajabu na mmiliki anayetambua sehemu zake utambuzi kamili, anaona kila dogo na kubwa ndani yake na anaiendesha. Upande wa tatu: Kwa kuwa mwanadamu ni kioo chenye kuakisi majina mazuri, basi yeye vilevile ni kioo cheye kuakisi hayo kwa upande wa nakshi zake zilizo dhahiri juu yake. Hili limekwisha kufafanuliwa kwa kiasi cha upambanuzi mwanzoni mwa (Kituo cha tatu) kutoka katika (Neno la thelathini na mbili) kwamba ainisho lenye kujumuisha la mwanadamu, ndani yake kuna zaidi ya nakshi sabini zenye kudhihiri katika nakshi za majina ya kiungu yalio mazuri. Basi kwa mfano: Mwanadamu anabainisha kwa kuwa kwake ni mwenye kuumbwa, jina la mtengenezaji (Muumba), na anadhihirisha kutokana na kuumbwa kwake vema jina la (Mwingi wa Rehema Mwenye kurehemu), na anajulisha kutokana na namna ya malezi yake na uchungaji wake jina la (Al-Kariim) na jina la (Mpole). Na kama hivi mwanadamu anaweka wazi nakshi aina mbali mbali na tofauti za majina mazuri aina mbali mbali kwa viungo vyake vyote na zana zake, na viungo vyake vya harakati na kwa vipole vyake vyote na hali zake za kimaanawy, na milango yake yote ya fahamu na hisia zake. Yaani kama ilivyo katika majina mazuri kuna jina kuu la Allah (s.w), basi kuna nakshi kuu katika nakshi za majina hayo na hiyo ni mwanadamu. Basi ewe anayeihesabu nafsi yake kuwa ni mwanadamu kweli, soma nafsi yako kwa nafsi yako, na kama hukufanya basi huenda ukaanguka kutoka ngazi ya ubinadamu kwenda katika ngazi ya wanyama. Nukta ya pili: Nukta hii inaashiria kwenye siri muhimu katika siri za upekee, na kuifafanua kama ifuatavyo: Kama ilivyo roho ya mwanadamu, inafungamana na mahusiano na mafungamano pamoja na sehemu zote za mwili wa mwanadamu, mpaka inafanya viungo vyake vyote na sehemu zake zote, katika kusaidiana kikamilifu kati yao. Yaani hakika roho, ambayo ni pole ya kiungu na kanuni ya kiamri imevika uwepo wa nje kwa amri za kimaumbile ambazo ni udhihirisho wa utashi wa kiungu, hakiizuilii kitu kunako kuendesha mambo ya kila sehemu miongoni mwa sehemu za kiwiliwili, wala hakiishughulishi kitu katika kukagua kwake na kutimiza haja za mwili kwa kila sehemu katika sehemu zake, basi kilicho mbali na karibu kwake ni sawa, wala kitu hakizuii katu, ambapo inaweza kukipa kiungo kimoja misaada kutoka viungo vingine, na vinaweza kupelekea katika kuhudumia viungo vingine. Bali inaweza kujua haja zote za kila sehemu katika sehemu za mwili, na kuhisi kupitia sehemu hii kwa hisia zote, na kuendesha mwili mzima kutokea kwenye sehemu hii moja, bali roho inaweza kuona na kusikia kwa kila sehemu katika sehemu za mwili ikiwa kimevuna hali ya kinuru zaidi. Basi maadamu roho ambayo ni kanuni ya kiamri katika kanuni za Allah (s.w), ina uwezo huu kudhihirisha mfano wa hatua hizi katika ulimwengu mdogo nao ni mwanadamu, basi vipi itakuwa ugumu kwa utashi wa hali zote – Allah ana mfano wa juu –, na kwa uweza wake wa hali zote kutekeleza matendo yasiyo na ukomo katika ulimwengu mkubwa, nao ni ulimwengu, na kusikia sauti zisizo na ukomo humo, na kujibu maombi yasiyo na ukomo yanayotokana kwa vilivyomo vyake? Basi yeye (s.w) anafanya atakalo ndani ya muda mmoja, hakimtopei kitu wala hakizuiliki kwake kitu, wala kitu hakimzuilii kitu, wala hakimshughulishi kitu akawa mbali na kitu. Vyote anaviona katika muda mmoja, wa karibu na wa mbali kwake ni sawa, akitaka kitu hukielekea kila kitu. Anaona kila kitu kutoka kitu chochote kiwacho, anasikia sauti za kila kitu na anajua kila kitu kwa kila kitu, kwani yeye ni Bwana mlezi wa kila kitu. Nukta ya tatu: Hakika maisha yana ainisho kubwa muhimu, na jukumu lenye umuhimu mkubwa, kwa kuwa somo hili limefafanuliwa katika (Dirisha la maisha) kutoka (Dirisha la ishirini na tatu) na katika andiko la Ishirini, neno la nane katika hilo, tunaelekeza mjadala huko, na hapa tunatanabahisha yafuatayo: Hakika ya nakshi zilizochanganywa kwenye uhai ambazo zinadhihiri kwa sura ya hisia, nakshi hizi zinaashiria majina mengi mazuri ya kiungu, na kwenye mambo ya kidhati ya Allah (s.w). Basi uhai unakua kwa upande huu ni kioo chenye kuakisi chenye kuangaza kwa midhihirisho ya mambo ya kidhati ya aliye hai Msimamizi wa kila kitu. Na kwa kuwa wakati wetu hautoshi kwa kufafanua siri hii kwa wale ambao hawajaridhia Allah kuwa Bwana Mola wao, na ambao hawajafika bado ngazi ya imani ya yakini, kwa ajili hii tutaufunga mlango huu.

§32

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَكَفَى بِاللَّهِ شَهِيدًا ۞ مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّهِ قُلْ يَا أَيهَا النَّاسُ إِنِّي رَسُولُ اللّهِ إِلَيْكُمْ جَمِيعًا الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ لا إِلَهَ إِلاَّ هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ Dirisha hili ni dirisha linalohusu jua la mbingu ya utume, bali jua la majua ya unabii, kipenzi cha Bwana wa walimwengu, Muhammad (s.a.w). Hakika durisha hili ni lenye kuangaza sawa na kuangaza kwa jua, na pana upana wa ulimwengu, na lenye kunawirisha sawa na kunawirisha kwa mchana. Na kwa kuwa tumethibitisha (Utume) Uthibitishaji wa kukinaisha katika (Neno la thelathini na moja), risala ya (Miiraji) na katika neno la kumi na tisa, (Dalili za Unabii) na katika (Andiko la kumi na tisa), risala ya (Al-Muujizat Al-Ahmadiyya) kwa hiyo tunarejesha hapa kumbukumbu yetu baadhi ya yaliyotajwa katika risala hizo, na tunaelekeza huko, isipokuwa tunasema: Hakika Mtume Mkarimu (s.a.w), ambaye yeye ni hoja ya Tawhidi yenye kutamka, ametangaza na kudhihirisha Tawhidi kwa uwazi, na kuibainisha kwa wanadamu ubainishaji fasaha, katika sira yake yote ya uturi, na kwa nguvu zote alizompa Allah (s.w), yeye ndiye ambaye anamiliki kwa mbawa mbili za Utume na Uwalii nguvu ya Ijmai na tawatur za Manabii wote ambao wamekuja kabla yake, na nguvu ya tawatur na Ijmai ya mawalii na wateule ambao wamekuja baada yake. Na kwa nguvu hii kubwa akafungua dirisha pana kubwa upana wa ulimwengu wa Kiislamu upande wa kumtambua Allah (s.w), wameanza kuangalia kupitia dirisha hili mamilioni ya wanazuoni wahakiki na wateule na masidikina mfano: Imamu Al-Ghazali, Imamu Ar-Rabbany, Muhyi Ad-Din Bin Al-Araby na Sheikh Al-Kaylany, basi hawa na wengine wanachungulia kupitia dirisha hili lililo wazi, na wanayabainisha kwa wengine. Je kuna pazia yoyote - kwa maoni - inayumkinika kuifunika juu ya dirisha hili kubwa! Na je ambaye hatazami kupitia dirisha hili ana akili japo kidogo, basi hukumu wewe!

§33

الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي أَنزَلَ عَلَى عَبْدِهِ الْكِتَابَ وَلَمْ يَجْعَل لَّهُ عِوَجَا الَر كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ لِتُخْرِجَ النَّاسَ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ Zingatia na jua kwamba hakika yaliyoelezwa katika (Madirisha) yote yaliyotangulia hiyo sio ila ni matone machache kutoka katika bahari ya (Qur’an tukufu). Ikiwa jambo ni kama hivi hakika yako unaweza sasa kupimia mwendelezo mkubwa wa nuru za Tawhidi ambazo zinamimina kutoka katika bahari ya uhai ya Qur’an tukufu, lau tungetazama – kiasi cha kutazama kidogo tu – kutoka katika chanzo cha madirisha yote hayo, na hazina na asili yake, nayo ni Qur’an Tukufu, tungeliona ni dirisha lenye kukusanya angavu linamulika nuru yenye kuangazia isiyo na mpaka, na kwa kuwa (Neno la ishirini na tano) (Risalat iijaz Al-Qur’an) na Ishara ya kumi na nane kutoka katika (Andiko la kumi na tisa), yameangalia upana wa dirisha hili na uangavu wake, kwa kiasi ambacho kinatosha, kwa hiyo tunaelekeza mjadala huko. Na hitimisho tunanyanyua viganja vyetu tukinyenyekea mbele ya Arshi ya Mwingi wa Rehema (s.w) ambaye ametuteremshia hii Qur’an tukufu ikiwa ni rehema na nuru na mwongozo na ponya na tunasema: رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذ۟نَٓا اِن۟ نَسٖينَٓا اَو۟ اَخ۟طَا۟نَا رَبَّنَا لَا تُزِغ۟ قُلُوبَنَا بَع۟دَ اِذ۟ هَدَي۟تَنَا رَبَّنَا تَقَبَّل۟ مِنَّا اِنَّكَ اَن۟تَ السَّمٖيعُ ال۟عَلٖيمُ وَ تُب۟ عَلَي۟نَا اِنَّكَ اَن۟تَ التَّوَّابُ الرَّحٖيمُ

§34

Andiko hili la (Thelathini na tatu) ambalo linajumuisha madirisha thelathini na tatu, tunamwomba Allah mtukufu iwe ni zawadi kwa asiye na Imani, imwite katika ngome ya Imani na kuikaza imani ya ambaye anakuta katika Imani yake kuna udhaifu hivyo kuitia nguvu. Na ajaalie imani yenye nguvu ya kuiga kuwa ni imani ya kuhakikisha yenye kujikita. Na kumpa ambaye imani yake ni kunjufu ngazi za kupanda katika kumtambua Allah ambao ndio msingi katika ukamilifu wa hakika, na kufungua mbele yake ya kushuhudiwa yenye nuru zaidi na kuangaza zaidi. Kwa ajili hii, hauna haki kusema: Natosheka na dirisha moja na sio lingine, hiyo ni kwa sababu moyo hutafuta fungu lake japo kuwa akili imenufaika, na roho nayo pia ni nyengine inatafuta fungu lake, bali hata mawazo ya kufikirika yanatafuta cha kuchota kutoka katika nuru hiyo. Yaani hakika kila dirisha katika madirisha yana faida aina kwa aina, na manufaa mbali mbali. Hakika alikuwa anayesemeshwa wa msingi katika Risala ya (Al-Miiraji) iliyopita, ni Muumini, kafiri alikuwa katika nafasi ya kusikiliza, ama Risala hii msemeshwa wa msingi humo ni mkanushaji mpingaji, na muumini yupo katika nafasi ya kusikiliza. Na nilivyokuwa nimeandika andiko hili katika upeo wa haraka kwa msingi wa sababu muhimu - kwa hiyo imebaki katika hali yake, sikuurejea mswada wake, na sikuingiza humo marekebisho yoyote, hakuna ajabu kuwa kitakuwa humo kitu katika upungufu na kubabaisha katika baadhi ya ibara, na katika njia ya kuelezea. Basi nataraji kutoka kwa ndugu zangu walitazame kwa njia ya kuachilia na msamaha, na wasahihishe – ikiwa wataweza – yaliyojitokeza kwangu katika makosa, na waniombee maghufira. وَالسَّلَامُ عَلٰى مَنِ اتَّبَعَ ال۟هُدٰى وَال۟مَلَامُ عَلٰى مَنِ اتَّبَعَ ال۟هَوٰى سُب۟حَانَكَ لَا عِل۟مَ لَنَٓا اِلَّا مَا عَلَّم۟تَنَٓا اِنَّكَ اَن۟تَ ال۟عَلٖيمُ ال۟حَكٖيمُ اَللّٰهُمَّ صَلِّ وَ سَلِّم۟ عَلٰى مَن۟ اَر۟سَل۟تَهُ رَح۟مَةً لِل۟عَالَمٖينَ وَ عَلٰى اٰلِهٖ وَ صَح۟بِهٖ وَ سَلِّم۟ اٰمٖينَ

Private reading note

This note stays on this device and is never uploaded to a server.

Up to 1,200 characters