Sözler

The Thirty-Second Word

Source: risaleinur multilingual dataset, risale.site source · Risale-Nur multilingual research corpus
Risale reading plan
§1

Şu Söz üç mevkıftır. Neno hili ni nyongeza inayofafanua (Neno la ishirini na mbili). Nayo ni tafsiri ya ulimi wa kwanza katika ndimi hamsini na tano katika ndimi ya vilivyomo vyenye kushuhudia juu ya upweke wa Allah (s.w), na ambazo zimeashiriwa katika Risala ya (Tone katika bahari ya Tawhidi) nayo katika wakati huohuo ni hakika katika hakika zilizosheheni aya tukufu: لَوْ كَانَ فِيهِمَا آلِهَةٌ إِلَّا اللَّهُ لَفَسَدَتَا imevaa nguo ya kufananishia.

§2

لَوْ كَانَ فِيهِمَا آلِهَةٌ إِلَّا اللَّهُ لَفَسَدَتَا (Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah peke yake hana mshirika ufalme ni wake na sifa njema ni zake, na ufalme ni wake anahuisha na kufisha naye yu hai hafi mikononi mwake kuna kheri naye juu ya kila kitu ni mweza na marejeo ni kwake). Nilikuwa nimebainisha katika moja ya siku za Ramadhani yenye baraka, hakika katika kila moja katika sentensi kumi na moja katika maneno haya ya kitawahidi kuna bishara ya kufurahisha, na ngazi katika ngazi za Tawhidi. Na hakika nimekunjua maneno ukunjufu unaokaribisha ufahamu wa watu wa kawaida ili kufafanua yaliyomo katika sentensi ya (Hana mshirika) katika maana nzuri, nayo ni katika sura ya mjadala wa kimfano na mahojiano ya kukadiria, na kuchukua ulimi wa hali katika umbo la lugha ya maneno. Na ninauleta hivi sasa mjadala huo kwa kuwasaidia ndugu zangu wapendwa ambao wananisaidia katika mambo yangu, na kukubali matakwa ya marafiki zangu msikitini na kwa kuangalia ombi lao. Nao ni kama ifutavyo: Tukadirie mtu anashika nafasi ya washirika ambao aina zote za watu wa shirki, ukafiri na upotevu mfano wa waabuduo Asili na wanaoitakidi kuathiri kwa sababu. Na tukadirie kwamba mtu huyo aliye kadiriwa anataka kuwa Bwana Mlezi wa kitu katika vilivyomo ulimwenguni, na anadai umiliki wa hakika wa kitu hicho! Na kama hivyo mtu huyo mwenye kudai (Kuwa ni Mungu) kwanza amekutana na kile ambacho ni kitu kidogo kabisa katika vilivyo kuwemo nayo ni atomu, akaiambia kwa ulimi wa asili na kwa lugha ya falsafa ya kimaada kwamba yeye ni bwana wake mlezi na mmiliki wake wa kiuhakika! Ile atomu ikamjibu kwa ulimi wa hakika na kwa lugha ya hekima ya Kiungu iliyowekwa ndani yake: Hakika mimi ninatekeleza majukumu na kazi zisizodhibitiwa na hesabu. Basi ninaingia katika kila kiumbe juu ya tofauti za sampuli zake, basi ukiwa wewe ewe mwenye kudai una elimu pana inazungukia majukumu yote hayo na mwenye uweza wenye kuenea unaoelekeza vyote, na wewe una hukumu yenye kupita na utamalaki kamili juu ya kunitiisha mimi na kunielekeza pamoja na walio kama mimi miongoni mwa atomu zenye kufanya kazi na zenye kutembea katika uwepo. Na vilevile ikiwa una uwezo wa kuwa mmiliki wa kiuhakika wa vilivyomo ambavyo mimi ni sehemu ya hivyo, kama chembe nyekundu (Za damu), na unasarifu ndani yao kwa mpangilio kamili. Basi una haki ya kudai umiliki kwangu, na kuegemeza jambo langu kwa asiye kuwa muumba wangu (s.w), na kama si hivyo basi nyamaza! kwani huwezi kuingilia katika mambo yangu, ukiachilia mbali kuwa wewe huwezi kuwa Bwana Mlezi wangu, kwa kuwa yaliyomo katika majukumu yetu na kazi zetu na michakato yetu katika mpangilio uliowekwa vema ulio kamili kwa kiasi hauwezi ambaye asiyekuwa na hekima ya hali zote na elimu yenye kuzunguka, lau mwingine asiyekuwa yeye ingeharibika. Basi una nini wewe kuweza kunyoosha kidole chako katika mambo yetu na hali ya kuwa wewe ni mwenye kushindwa usiye na uhai kipofu mwenye kutekwa kwa mkono wa asili na sadfa pofu! Mwenye kudai akasema wayasemayo wana maada: (Kwa hiyo kuwa mwenye kumiliki nafsi yako, basi kwa nini unasema kuwa wewe unafanya kwa ajili ya Mwingine?) Atomu ikamjibu: (Ningekuwa na akili jabari kama jua na elimu yenye kuzunguka kama mwanga wake na uweza wenye kuenea kama joto lake na njia za fahamu na utambuzi zenye ukunjufu kama rangi saba katika mwanga wake na uso unaoelekea kila mahali na nazagaa humo na jicho lenye kutazama na maneno yenye kutenda kazi katika kila kilichomo ninachokielekea. Huenda ningekuwa ninajipumbaza kama wewe basi ningedai utawala wa nafsi yangu! nenda mbali nami kwani huna nafasi kwetu). Na mlinganiaji wa shirki alipokata tamaa kutokana na atomu. Alikabiliana na chembe nyekundu ya damu, akitarajia kupata kitu kwake. Akaiambia kwa ulimi wa sababu na lugha ya Asili na mantiki ya falsafa. : (Mimi kwako ni Bwana Mlezi na Mmiliki!). Chembe nyekundu ya damu ikamjibu kwa ulimi wa hakika na kwa lugha ya hekima ya Kiungu: (Hakika mimi sio peke yangu kabisa, kwani mimi na walio kama mimi sote tumo katika jeshi la damu iliyo nyingi, mpangilio wetu ni mmoja na majukumu yetu yameunganishwa pamoja, tunatembea chini ya amri ya mwamuru mmoja. Ikiwa unaweza kumiliki hatamu ya vyote vilivyomo kwenye damu mfano wangu, na una hekima madhubuti na uwezo mkubwa vinavyohukumu utawala wake juu ya atomu zote za mwili ambazo ndani yake tunatembea na tunatumiwa kutekeleza majukumu ndani yake kwa hekima zote na mpangilio, basi zilete. Basi wakati huo huenda madai yako yakawa na maana. Lakini wewe ewe mwenye kudai humiliki isipokuwa nguvu yenye upofu na asili yenye ububu, basi huwezi kuingilia mambo yetu japo kwa kiasi cha atomu, ukiachilia mbali kudai umiliki juu yetu, kwa kuwa nidhamu ambayo inatamalaki juu yetu ni madhubuti na kali kwa kiasi ambacho hawezi kutawala juu yetu isipokuwa anayeona kila kitu na anasikia kila kitu na anajua kila kitu na anafanya anayoyataka. Na kwa ajili hii basi nyamaza. Kwani majukumu yetu matukufu na umadhubuti wake na mapangilio wake hayaachi nafasi kwetu kusikiliza kubwabwaja kwako) na kama hivi chembe nyekundu ya damu inamfukuza. Na huyo mwenye kudai alipokuwa hakupata akitakacho kwake. Akaenda na kukutana na kiini kimoja katika mwili akakiambia kwa mantiki ya falsafa na ulimi wa asili: (Sikuweza kusikilizisha madai yangu kwa atomu, wala kwenye chembe nyekundu ya damu, basi mimi nitapata kutoka kwako sikio lenye kusikiliza, kwa sababu wewe si chochote isipokuwa ni chumba kidogo chenye kubeba vitu mbalimbali! Na kwa ajili hii mimi ni mwenye kuweza kukutengeneza, basi kuwa mtengenezwa na kiumbe wangu kiukweli!) Kiini kikamwambia kwa lugha ya hekima na hakika: (Hakika mimi ni mdogo sana kweli, lakini mimi nina majukumu matukufu na makubwa, nami nina uhusiano na mafungamano madhubuti mno kutokana na viini vyote vya mwili. Basi mimi nina majukumu yaliyowekwa vema kutokana na njia zote za damu ikiwemo mishipa yenye kuendesha na yenye kuhusu hisia pamoja na nguvu zote zinazoratibu mwili kama nguvu yenye kuvuta na yenye kusukuma na yenye kuzalisha na yenye kutia sura na mfanao wa hizo. Basi ewe mwenye kudai ukiwa na elimu pana na uweza wenye kuenea inayounda hiyo mishipa ya aina mbalimbali na nguvu iliyowekwa kwenye mwili na kuziratibu na kuzitumia katika majukumu yake. Na kadhalika ikiwa una hekima yenye kuenea na uweza wenye kutekeleza unaweza kusarifu katika mambo ya ndugu zangu miongoni mwa viini vyote vya mwili, na ambavyo vinarandana katika kuwekwa vema na kupendeza na hali ya kisampuli, basi vidhihirishe. Kisha dai kuwa wewe unaweza kunitengeneza. Na kama sivyo basi usionekane mbele yetu. Hakika chembe nyekundu za damu zinanipatia riziki, na chembe nyeupe zinanikinga kukabiliana na maradhi yenye kushambulia. Basi mimi nina kazi kubwa, usinishughulishe kunako hizo. Hakika mwenye kushindwa mwenye kasoro kipofu mfano wako hana haki ya kuingilia katika kazi zetu madhubuti kamwe; kwa kuwa kwetu kuna mpangilio imara ulio kamili kiasi kama atatutawala asiye mwenye hekima zote na mweza wa hali zote na mjuzi wa hali zote mpangilio wetu ungeharibika na kufunguka fundo letu). Na kama hivi mtoa madai alikata tamaa kutokana na atomu vilevile, lakini aliukabili mwili wa mwanadamu, akamwambia kama wasemavyo wana maada, kwa ulimi wa asili iliyo pofu na falsafa iliyopotoka: (Wewe ni Ufalme wangu. Kwani mimi ndiye ambaye niliye kutengeneza, au kwa uchache mimi nina sehemu kwako!) Ule mwili wa kibinadamu ukamjibu kwa hakika ya mpangilio madhubuti uliyomo kwake: (Ikiwa wewe mtoa madai una ujuzi na uweza wenye kuenea ambao una usarifu wa hali zote katika miili yote ya watu kama mimi, ungeweka alama zenye kupambanua zilizodhihiri kwenye nyuso zetu, na ambayo ndiyo chapa ya uweza na muhuri wa maumbile. Na hivyo hivyo kama ungekuwa na utajiri mkubwa na utawala wenye kutamalaki unaotawalia katika hazina za riziki zangu zenye kuendelea tangu kwenye hewa, maji, mimea na wanyama. Na vilevile ungekuwa una hekima isiyo na mpaka na uweza usio na ukomo kwa hali ambayo unaviwezesha vipole vya kimaanawy vya ngazi ya juu vipana miongoni mwa roho moyo na akili katika chombo kidogo mfano wangu, na kukiendesha kwa hekima iliyopitiliza katika utumishi, basi nioneshe hivyo kisha udai Ubwana Mlezi kwangu, na kama siyo basi nyamaza. Hakika mtengenezaji mtukufu ni mweza juu ya kila kitu, ni mjuzi wa kila kitu, ni mwenye kuona kila kitu, kwa ushahidi wa mpangilio ulio kamilika kikamilifu ambao unaniendesha mimi, na kwa kujulisha kwa chapa ya umoja iliyopo katika uso wangu, basi hawezi Mwenye kushindwa na kupotea mfano wako kunyoosha kidole chake katika kazi yake ya ajabu kamwe wala kuiingilia japo kwa kiasi cha atomu). Akaondoka mlinganiaji wa shiriki ambapo hakukuta mahali pa kuingilia katika mwili, akaikabili sampuli ya mwanadamu, akajadiliana na nafsi yake kwa kusema: (Huenda katika makundi haya yenye kusukana yenye kutawanyika naweza kupata nafasi, nikaingilia katika hali za maumbile yao na uwepo wao kama ambavyo shetani anavyoingilia kwa upotevu wake katika matendo yao ya kihiari na mambo yao ya kijamii. Na hapo nitaweza kupitisha utawala wangu katika mwili wa mwanadamu ambaye amenifukuza yeye na vilivyomo kwake miongoni mwa chembechembe). Na kwa ajili hii aliisemesha sampuli ya mwanadamu kwa ulimi wa asili ziwi na falsafa potofu pia: (Nyinyi enyi watu mnaonekana katika fujo, hata sioni nidhamu inayokupangilieni, basi mimi kwenu ni Mola Mlezi na Mmiliki, au kwa uchache nina hisa kwenu). Aina ya mwanadamu haraka ikamjibu kwa ulimi wa haki na hakika na kwa lugha ya hekima na kupangika: Ukiwa - ewe mwenye kudai - unamiliki uweza uwezo kulivika tufe la Ardhi pambo la kupendeza lenye rangi za kung’ara lilifumwa kwa ukamilifu wa hekima kwa nyuzi za aina za mimea na wanyama ambazo zinavuka sampuli mia moja, zenye kushabihiana na sampuli yetu ya kibinadamu, na ikawa na uwezo wa kufuma busati hilo la ajabu lililotandikwa Ardhini katika matandiko ya mamia ya maelfu miongoni mwa viumbe hai, na ambavyo vimo katika nakshi ya ajabu na iliyo nzuri mno. Na ukiachilia mbali na kuumba busati hili la kupendeza, na kufanyika kwake upya daima na hekima kamili! Ikiwa una uweza wenye kuzunguka na hekima jumuishi kama hii, ambapo unasarifu katika tufe la Ardhi ambalo sisi ni katika matunda yake, na kudabiri mambo ya ulimwengu ambao sisi ni mbegu zake, basi yakatumwa kwa mizani ya hekima mahitaji ya uhai wetu kwetu kutoka katika maeneo ya ulimwengu wote. Na ukiwa – wewe mwenye kudai – unao uwezeshaji unaoumba alama za uweza wa kiungu wenye kupambanuka ulio mmoja kwenye nyuso zetu, na katika walio kama sisi miongoni mwa waliotangulia na wajao, ukiwa mwenye kumiliki tulivyo vitaja basi huenda ukawa na haki ya kudai ulezi (Wa Kiungu) juu yangu. Na kama sivyo basi nyamaza kimya! Na wala usiseme kuwa mimi naweza kuingilia katika mambo ya hawa ambao wanaonekana katika mchanganyiko na kusukana, kwani kwetu mpangilio uko katika ukamilifu wake. Na hali hizo ambazo unazidhania kuwa ni fujo ni kuchukua nakala ya uweza wa kiungu kwa ukamilifu wa kupangika kulingana na Kadari ya kiungu. Basi ikiwa mpangilio ni madhubuti katika daraja ya chini kabisa katika daraja za uhai kama mimea na wanyama na unakataa kuingiliwa kwa namna yeyote iwayo, basi seuze sisi na hali tupo katika kilele cha ngazi za uhai? Je sio ambacho kinaonekana ni mchanganyiko na fujo ni aina katika uandishi wa kiungu wenye hekima? Je inayumkinika kwa ambaye amewezesha nyuzi za nakshi za ajabu za busati hili, kila moja katika mahali pake panapofaa, na katika sehemu yoyote iwayo, kwamba asiwe mtengenezaji wake, siye Muumbaji wake wa kiuhakika, inayumkinika kuwa Muumba wa kokwa siye Muumba wa tunda lake? Na je inayumkinika kuwa Muumba wa tunda kuwa siyo Muumba wa mti wake? Lakini wewe ni kipofu huoni! Je huoni miujiza ya uumbaji usoni mwangu na maajabu ya uumbaji katika umbile langu? Ukiweza kuyaona, basi utatambua kuwa Muumba wangu hakifichiki kwake kitu wala chochote hakiwi kigumu kwake, na chochote hakimshindi. Anaendesha nyota kwa wepesi wa kuendesha Atomu, na anaumba majira ya machipuo makunjufu kwa wepesi wa kuumba ua moja, yeye ndiye aliyeweka faharisi ya Ulimwengu mkubwa katika ainisho langu kwa mpangilio madhubuti, je inayumkinika kwa mwenye kushindwa kipofu mfano wako kujifufua nafsi yake na kuingilia katika ufundi wa huyu Muumba Adhimu na Fundi jalili, na kwa ajili hii basi nyamaza na ondosha sura yako kwangu, basi anakwenda hali ya kuwa ni mwenye kufukuzwa. Kisha anakwenda mwenye kudai huyo katika busati lenye kung’ara lililotandikwa juu ya uso wa Ardhi na pambo la kumeremeta lenye kupambwa lililovikwa, akalisemesha kwa jina la sababu na kwa lugha ya asili na ulimi wa falsafa: (Hakika mimi ninaweza kusarifu mambo yako, basi mimi kwa hiyo ni mmiliki wako na mimi kwako kwa uchache nina hisa). Na hapo lile busati lililorembeshwa na pambo lile lililopendeza likaongea na kumwambia yule mwenye kudai kwa lugha ya hakika na kwa ulimi wa hekima iliyowekwa kwake: (Ikiwa una uweza wenye kutenda na ufundi wa ajabu vinavyo kufanya ufume mabusati yote haya yaliyotandikwa na mapambo yaliyo dhahiri ambayo huondolewa juu ya Ardhi kwa idadi ya karne na miaka kisha unaiondosha kwa mpangilio timamu na kuyakunjua juu ya kamba ya zama zilizopita, na baada ya hapo unashona yanayovuliwa juu yake katika mapambo yenye kung’ara pamoja na nakshi zake na kukata mikato yake katika eneo la Kadari, na kadhalika ukiwa mwenye kumiliki mkono wa kimaanawy wenye uweza na hekima kiasi kwamba unanyooka kukifikia kila kitu kuanzia katika kuumbwa Ardhi hadi kuteketea kwake, bali kutokea azali hadi milele, basi unafanya upya na kubadilisha sehemu za kiungo cha busati hili. Na kadhalika ukiwa unaweza kushika hatamu ya Ardhi ambayo inatuvika na kutusitiri. Naam, ukiwa hivyo basi dai uungu juu yangu. Na kama si hivyo basi toka ukiwa mwenye kutwezwa na kufukuzwa kutoka ardhini. Huna makazi hapa, kwani ndani yetu kuna midhihirisho ya umoja na mihuri ya upweke kwa kiasi kwamba asiyekuwa vitu vyote katika mkono wa usarifu wake na si mwenye kuona vitu vyote na mambo yake yote kwa mkupuo mmoja, asiyeweza kutenda mambo yasiyokuwa na mpaka ndani ya muda mmoja, na asiyekuwa mwenye kuhudhuria na kusimamia kila mahali na mwenye kutakasika na mahali na wakati. Hawezi kuwa mmiliki wetu kamwe, bali hawezi kuwa ni mwenye kuingilia mambo yetu kwa hali zote. Yaani ambaye hakuwa ni mmiliki wa uweza wa hali zote, hekima za hali zote na ujuzi wa hali zote, hawezi kututawalia na kudai umiliki juu yetu). Na kama hivyo mwenye kudai anakwenda na kuisemesha nafsi yake kwa kusema: (Niende katika tufe la Ardhi huenda nikalipata kulighafilisha na nikapata humo nafasi..) akaelekea huko akiliambia kwa jina la sababu na kwa ulimi wa asili kwa mara nyingine: (Hakika ya kuzunguka kwako kama hivi, bila ya kukusudia kunaashiria kwamba wewe upo tu bila ya mmiliki. Na kwa ajili hii inayumkinika kuwa mtiifu wa amri yangu!) Ardhi ikamjibu kwa ukelele kama radi ikikanusha madai yake kwa ulimi wa haki na hakika yenye kudhamiriwa ndani yake: Usilete porojo ewe mpumbavu zuzu! . Vipi niwe mwenye kupuuzwa bila ya Mmiliki wala Mola! Je umeona katika nguo yangu ambayo ninaivaa japo uzi mmoja tu ni wenye kutoka bila ya hekima bila ya kutengenezwa vyema! Hadi unadai kuwa kamba yangu imeachiliwa tu na kwamba mimi nipo bila ya Mola wala Mmiliki? angalia harakati zangu tu, na katika hizo ni mizunguko miwili ya kila mwaka ambayo ninatembea katika mizunguko hiyo masafa ya miaka ishirini na tano elfu ndani ya mwaka mmoja tu, nikitimiza majukumu yangu yaliyokabidhiwa kwangu kwa ukamilifu wa mizani na hekima. Ikiwa una hekima ya hali zote na uweza wa hali zote ukaendesha pamoja nami rafiki zangu sayari kumi katika mfano wangu katika maduara yake makubwa, na kuumba jua lenye kuangaza ambalo ndilo kiongozi na imamu wetu na kinachotufungamanisha nalo ni uvutano wa rehema basi unaliendesha na kutuendesha mimi na sayari zote kuzunguka jua kwa mpangilio timamu na hekima kamili. Naam, ewe mwenye kudai ikiwa una uweza wa hali zote na hekima ya hali zote katika kuendesha mambo haya makubwa na kuyadabiri basi dai madai yako. Na kama si hivyo basi acha hizi porojo zenye kufurutu ada, na usukumwe kuelekea Jahanamu na ubaya ulioje wa mafikio, basi usinishughulishe na majukumu yangu makubwa. Kwani hakika yaliyopo kwetu miongoni mwa mpangilio mzuri na kuratibika kukubwa na utiishaji wenye hekima vinajulisha kwa uwazi kuwa vilivyomo vyote kuanzia Atomu hadi nyota na hadi majua kutii amri ya Mtengenezaji wetu na vyenye kutiishwa kwake, kwani kama anavyopangilia mti kwa wepesi na anapamba matunda yake kwamba kwa wepesi huo analipangilia jua na sayari zake. Yeye ni Mwenye hekima, Mwenye Utukufu, Mtawala wa hali zote na Mwenye ukamilifu. Kisha huyo mwenye kudai analielekea jua baada ya kuwa hakupata nafasi hata ya kuweka unyayo katika ardhi akaisemesha nafsi yake kwa kusema: (Hakika ya jua hili ni kitu kikubwa huenda nitapata humo mwanya wa kupitishia madai yangu na kwa nafasi yangu pia niitiishe Ardhi vilevile). Akaliambia jua kwa ulimi wa ushirikina na kauli potofu za falsafa za kishetani, na kama wanavyolisema hilo Wamajusi: (Wewe ewe jua ni malkia wa ulimwengu, nawe ni lazima kuwa ni mmiliki wa nafsi yako, na unasarifu ulimwenguni jinsi utakavyo). Na papo hapo jua lilimjibu kwa ulimi wa haki na hakika: (Hapana na mara elfu hapana, bali mimi sio isipokuwa ni mwamuriwa mtiifu mwenye kutumika katika jukumu la kunawirisha wageni wa Bwana wangu. Na siyo mmiliki wa nafsi yangu abadani bali siyo mmiliki hata wa ubawa wa nzi umiliki wa kihakika, kwa sababu katika mwili wa nzi kuna baadhi ya johari za thamani za kimaanawy, kama jicho na sikio na katika maajabu ya utengenezaji, katika nisiyolimiliki katu na ambayo yako nje ya uwezo wangu) na kama hivi akimkemea mwenye kudai. Basi anajitokeza mwenye kudai huyo kwa kusema kwa ulimi wa kifalsafa ya ukinzani ya kifirauni: (Maadamu wewe siyo mmiliki wa nafsi yako, bali ni mtumishi, kwa hiyo wewe ni mwenye kumilikiwa na mimi na uko chini ya usarifu wangu kwa jina la sababu). Jua likampa jibu lenye nguvu kwa jina la haki na hakika na kwa ulimi wa utumishi hali ya kusema kuwa: (Hakika si vingine mimi ninakuwa ni mwenye kumilikiwa na yule ambaye ameumba nyota za juu kama mimi, na kuzikalisha katika mbingu zake kwa ukamilifu wa hekima yake, na kuziendesha kwa haiba kamili, na kuzipamba kwa mapambo kamilifu). Kisha yule mwenye kudai akaanza kuzungumza na nafsi yake: Hakika ya nyota zimechanganyika na zimesongamana na zimeparaganyika zimeachana mbali mbali baadhi yake kwa baadhi, basi huenda nikapata humo nafasi kwa jina la mwakilishi wangu nikapata kitu kutokana nazo na anaingia kati ya nyota. Akaiambia kama wasemavyo Masabai waabudu wa nyota kwa jina la sababu na katika njia ya washirika wake na kwa ulimi wa falsafa iliyochupa mipaka: (Nyie nyota hakika ya watawala wengi wanakutawaleni kwa sababu ya kuzidi kutawanyika kwenu). Nyota moja kwa niaba ya nyota zote ikamjibu: Kuzidi kulioje kwa upumbavu wako! Ewe mwenye kudai uliye zuzu. Je huoni alama ya Tawhidi na nembo ya upekee juu ya nyuso zetu, huzifahamu? Je hujui mifumo yetu ya kiwango cha juu na kanuni kali za uja wetu? Je unatudhania bila ya mpangilio? Basi sisi ni mahuluki waja wa Mmoja wa pekee anakamata mkononi mwake mambo yetu na mambo ya mbingu ambazo ni bahari yetu, na viumbe ambavyo ni miti yetu, na anga la ulimwengu mkunjufu ambalo ni njia zetu. Basi sisi ni mashahidi wa kinuru kama taa zinazoangaza katika siku za matamasha tunabainisha ukamilifu wa Rububiyya yake (s.w), na sisi ni hoja za wazi tunatangaza juu ya utawala wa Rububiyya yake, basi kila taifa kati yetu ni watumishi wafanya kazi wenye nuru tunajulisha juu ya utukufu wa mamlaka yake, katika ngazi za juu za chini za kidunia za kibarzakh na kiakhera. Naam, hakika sisi ni muujiza wa dhahiri katika miujiza ya uweza wa Mmoja wa pekee. Na tunda bivu la mti wa umbo, na dalili yenye kuangaza upweke. Basi sisi ni nyumba na ndege na msikiti kwa malaika, na limwengu za juu ni taa na jua. Na ni shahidi juu ya mamlaka ya Kiungu, na katika anga la ulimwengu na kasri lake ni pambo na ua, kana kwamba sisi ni samaki wa kinuru wanaogelea katika bahari ya mbingu, na jicho zuri la uso wa mbingu. Kama kila mmoja wetu ni kama hivi hakika katika jumla yetu kuna kimya katika utulivu. Na mchakato katika hekima, na pambo katika haiba. Na kulingana sawa umbo katika mpangilio. Na kutengeneza vyema kimizania. Na kwa ajili hii tunashuhudia kwa ndimi zisizo na mpaka juu ya umoja wa Mtengenezaji wetu Mtukufu na juu ya upekee wake na samadiya yake (Kutegemewa kwake kwa haja zote) na juu ya sifa za uzuri wake na ukamilifu wake na utukufu wake na tunatangaza ushahidi huu kwa mashahidi wa viumbe wote. Je baada ya hivi unatutuhumu na hali sisi ni waja wataharifu watiifu wenye kutiishwa kuwa tumo kwenye fujo na mchanganyiko na mchezo bali bila ya Mola wala Mmiliki? Basi hakika wewe bila ya shaka unastahiki kuadabishwa kwa tuhuma yako hii, basi nyota moja inamvurumisha yule mwenye kudai na kumtupa huko katika kina cha Jahanamu na ubaya wa mafikio. Pamoja naye inaitupa asili na wadai wake katika bonde la dhana na sadfa inaitupa katika kisima cha kutokuwepo, na washirika kuelekea katika magiza ya kugoma na kuwa muhali. Na falsafa yenye kufanya uadui na dini kwenda chini ya walio chini. Basi nyote ile pamoja na nyota zote inasoma kauli yake Allah (s.w): لَوْ كَانَ فِيهِمَا آلِهَةٌ إِلَّا اللَّهُ لَفَسَدَتَا ikitangaza kuwa katu, hakuna nafasi kwa mshirika yeyote wala hakuna mpaka kwake kuingilia hata katika kitu duni kabisa kwa kuzingatia tangu ubawa wa nzi hadi kandili za mbingu. سُب۟حَانَكَ لَا عِل۟مَ لَنَٓا اِلَّا مَا عَلَّم۟تَنَٓا اِنَّكَ اَن۟تَ ال۟عَلٖيمُ ال۟حَكٖيمُ اَللّٰهُمَّ صَلِّ وَ سَلِّم۟ عَلٰى سَيِّدِنَا مُحَمَّدٍ سِرَاجِ وَح۟دَتِكَ فٖى كَث۟رَةِ مَخ۟لُوقَاتِكَ وَ دَلَّالِ وَح۟دَانِيَّتِكَ فٖى مَش۟هَرِ كَائِنَاتِكَ وَ عَلٰى اٰلِهٖ وَ صَح۟بِهٖ اَج۟مَعٖينَ بِسْمِ اللّٰهِ الرَّحْمٰنِ الرَّحِيمِ فَانظُرْ إِلَى آثَارِ رَحْمَتِ اللَّهِ كَيْفَ يُحْيِي الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا Kifungu hiki cha Kiarabu kinaashiria ua moja katika bustani ya Azali ya aya hii tukufu. حَتّٰى كَاَنَّ الشَّجَرَ ال۟مُزَهَّرَةَ قَصٖيدَةٌ مَن۟ظُومَةٌ مُحَرَّرَةٌ وَ تُن۟شِدُ لِل۟فَاطِرِ ال۟مَدَائِحَ ال۟مُبَهَّرَةَ اَو۟ فَتَحَت۟ بِكَث۟رَةٍ عُيُونُهَا ال۟مُبَصَّرَةَ لِتُن۟ظِرَ للِصَّانِعِ ال۟عَجَائِبَ ال۟مُنَشَّرَةَ اَو۟ زَيَّنَت۟ لِعٖيدِهَا اَع۟ضَائَهَا ال۟مُخَضَّرَةَ لِيَش۟هَدَ سُل۟طَانُهَا اٰثَارَهُ ال۟مُنَوَّرَةَ وَ تُش۟هِرَ فِى ال۟مَح۟ضَرِ مُرَصَّعَاتِ ال۟جَو۟هَرِ وَ تُع۟لِنَ لِل۟بَشَرِ حِك۟مَةَ خَل۟قِ الشَّجَرِ بِكَن۟زِهَا ال۟مُدَخَّرِ مِن۟ جُودِ رَبِّ الثَّمَرِ سُب۟حَانَهُ مَا اَح۟سَنَ اِح۟سَانَهُ مَا اَز۟يَنَ بُر۟هَانَهُ مَا اَب۟يَنَ تِب۟يَانَهُ .خَيَال۟ بٖينَد۟ اَزٖين۟ اَش۟جَار۟ مَلَائِك۟ رَا جَسَد۟ اٰمَد۟ سَمَاوٖى بَا هَزَارَان۟ نَى۟ .اَزٖين۟ نَي۟هَا شُنٖيدَت۟ هُوش۟ سِتَايِش۟هَاىِ ذَاتِ حَى۟ .وَرَق۟هَارَا زَبَان۟ دَارَن۟د۟ هَمَه هُو هُو ذِك۟ر۟ اٰرَن۟د۟ بَدَر۟ مَع۟نَاىِ حَىُّ حَى۟ .چُو لَٓا اِلٰهَ اِلَّا هُو بَرَابَر۟ مٖيزَنَد۟ هَر۟شَى۟ دَمَا دَم۟ جُويَدَن۟د۟ يَا حَق۟ سَرَاسَر۟ گُويَدَن۟د۟ يَا حَى۟ بَرَابَر۟ مٖيزَنَن۟د۟ اَللّٰه۟ وَ نَزَّل۟نَا مِنَ السَّمَٓاءِ مَٓاءً مُبَارَكًا Arabî fıkranın tercümesi: Hata kana kwamba mti uliochanua maua ni kasida iliyotungwa na kuandikwa. Na inaimba kwa ajili ya muumba madihi za dhahiri au imefungua kwa wingi wa macho yake yenye kuona. Ili kuonesha kuwa mtengenezaji ana maajabu yaliyozagaa au imepamba viungo vyake vya kijani kiwiti kwa ajili ya sikukuu yake. Ili Mfalme wake ashuhudie athari zake zenye nuru na kutangaza katika halaiki urembo wa johari. Na kutangaza kwa wanadamu hekima ya kuumbwa mti kwa hazina zake zilizowekezwa kutokana na ukarimu wa mola wa Matunda. Subhana uzuri ulioje wa hisani yake na kupambika kulioje kwa hoja yake na ufasaha ulioje wa ubainisho wake. وَنَزَّلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً مُّبَارَكًا

§3

Basi sikiliza aya tukufu: أَفَلَمْ يَنظُرُوا إِلَى السَّمَاء فَوْقَهُمْ كَيْفَ بَنَيْنَاهَا وَزَيَّنَّاهَا Kisha tazama uso wa mbingu! Jinsi uonavyo ukimya katika utulivu, mchakato katika hekima, mmemetuko katika heshima, tabasamu katika pambo pamoja na kupangika kwa umbo pamoja na kulingamana sawa katika ufundi. Kuzagaza kwa taa yake, kumulika mulika kwa kandili yake, kumemetuka kwa nyota zake, vinatangaza kwa watu wenye akili, ufalme bila ya ukomo. Mafungu haya ya maneno ya (Kiarabu) hakika ni tafsiri ya baadhi ya maana ya aya tukufu iliyotangulia, nayo yanamaanisha kwamba aya tukufu inageuza mtazamo wa mwanadamu katika uso wa mbingu ulio mzuri uliopambwa ili aone kwa angalizo hilo na kutazama kwa makini, ukimya na kunyamaza katika utulivu. Na ili ajue kwamba mbingu imechukua hali hiyo tulivu, kwa amri ya Mweza Mwenye uweza wa hali zote na kwa utiishaji wake. Ambapo bila ya uweza huo wa hali zote, yaani mbingu ingekuwa imeponyoka hatamu, ni huru katika michakato yake na kutulia kwake, maumbo hayo makubwa yangekuwa yenye kuingiliana baadhi yake kwa baadhi, na matufe hayo makubwa, kwa kuzunguka kwake yanatoa sauti ya ngurumo ya kutisha inayosababisha uziwi kwa viumbe wote, na ingezuka na migongano kutokana na ukali wake vingeteketea viumbe vyote. Kwani katika yanayojulikana ni kwamba wangecharuka nyati ishirini kutoka katika shamba mambo yangekuwa shaghala baghala. Na ingesababisha maangamizo fujo na vifo, basi vipi kwa maumbo makubwa ya mbinguni makubwa kuliko ardhi yetu kwa mara elfu, yanakwenda kwa kasi ni ya kasi zaidi kuliko bomu kwa mara sabini, kama ilivyo thibiti katika elimu ya falaki! (Sayansi ya mambo ya anga) basi kutokana na haya fahamu kuwa utulivu unaoenea na sayari kubwa na kutawala mbinguni hakika inabainisha kiasi cha upana wa uweza wa Mwenye uweza Mwenye ukamilifu na kiasi cha kutamalaki kwa utiishaji wa mtengenezaji mtukufu kwa maumbo hayo, na kiasi cha kufuata kwa nyota na kunyenyekea kwake amri zake (s.w). (Mchakato katika hekima): Kisha hakika aya tukufu vilevile inaamrisha kushuhudia yaliyomo katika uso wa mbingu miongoni mwa harakati ndani ya hekima. Kwani hiyo ni michakato mikubwa inakwenda ndani ya hekima madhubuti kunjufu akili zinatahayari na mwanadamu anasimama mbele yake kwa kustaajabu na kutukuza, kama alivyo fundi mahiri anaendesha mashine za kiwanda na meno yake ya mashine kwa mujibu wa hekima maalum, hakika kwa ujuzi wake anabainisha kiwango cha umahiri wake na umakini wa ufundi wake kulingana na ukubwa wa kiwanda na kupangika kwake. Hali kadhalika Mweza Mwenye uwezo wa hali zote aliye Mtukufu. (Na anao mfano wa juu) Ambaye analipa jua na sayari zake hali maalumu inayofanana na hali ya kiwanda kikubwa, Ambaye anaendesha matufe hayo makubwa, kana kwamba ni mawe ya ngumbewe ndogo na masanduku ya kiwanda rahisi, anazizungusha kuzungukia jua, mbele ya macho ili afahamu mwanadamu kwa uwiano huo upeo wa uweza wake na ukunjufu wa hekima yake. (Kumemetuka katika heshima na kutabasamu katika mapambo): Yaani katika uso wa mbingu vilevile kuna mwanga angavu na mmuliko mkubwa, na kutabasamu na bashasha katika mapambo na uzuri, jambo ambalo linabainisha adhama ya mamlaka ya Mtengenezaji Mtukufu, na kiasi cha umakini katika ufundi wake mzuri. Ambapo kama kuwasha taa na nuru na kudhihirisha mionekano ya furaha katika siku ya kusimikwa mfalme kwenye kiti, hakika ni kwa ajili ya kubainisha kiwango cha ukamilifu wake katika muktadha wa maendeleo ya kistaarabu. Vivyo hivyo mbingu kubwa pamoja na nyota zake kubwa zinadhihirishia macho ya mwenye kuchunguza ukamilifu wa mamlaka ya Fundi Mtukufu na uzuri wa ufundi wake wa ajabu. (Pamoja na kupangika kwa umbo pamoja na kulingana sawa kwa vipimo vya ufundi): Ibara inasema: Tazama kupangika kwa viumbe katika uso wa mbingu, na ufahamu uwiano wa vipimo vya vilivyotengenezwa kwa vipimo madhubuti, na utambue kutokana na hili: Ukunjufu ulioje wa uweza wa Mtengenezaji wa viumbe hivi na kuenea kulioje kwa hekima yake! Naam, hakika ya kuendesha maada ndogo au maumbo na wanyama, na kuviendesha na kuvitiisha, na kuvichunga kila kimoja kati ya hivyo katika njia maalum inayobainishwa kwa kipimo mahsusi, inabainisha kiwango cha uweza wa mwenye kuyatenda hayo na kiasi cha hekima yake na kiasi cha utiifu wa maada hizo na wanyama na kufuata kwao amri yake. Na mambo ni hivyo hivyo katika mbingu pana mno. Hakika zinabainisha adhama yake yenye kutahayarisha, na pamoja na nyota zake kubwa bila ya idadi, na kwa nyendo zake za hali ya juu, na pamoja na kutokiuka mipaka iliyokadiriwa japo chanda na kutokuhalifu japo nukta moja, na kutokufanya uzito kwake katika kutekeleza mambo yaliyowakilishwa kwake japo kwa moja ya kumi ya dakika moja, nasema hakika inabainisha kwa watazamao kwamba Mtengenezaji na Muumba wake Mtukufu anadhihirisha Ubwana Mlezi wake kwa kupitisha kwake mambo haya kwa mizani maalum hiyo madhubuti. (Kuzagaza kwa taa yake, kuangaza kwa taa yake na kumetameta kwa nyota zake, kunatangaza kwa watu wenye akili ufalme bila ya ukomo). Yaani hakika kutiisha jua, mwezi na nyota kunakopatikana katika aya nyingi mfano wa aya hii iliyotangulia, na iliyopo katika surat (An-Nabai) na nyinginezo, zote zinabainisha kwamba hakika kaungika kwa taa kama jua katika dari ya mbingu iliyopambwa, nayo ni taa iwakayo ambayo inaangaza mwanga na kueneza joto na kufanya nuru hiyo kana kwamba ni wino wa kuandikia barua za ki samadani (zinazotokana na Allah Mwenye kutagemewa na kila kitu kwa haja zote) juu ya ukurasa wa majira ya joto na baridi kwa hati za usiku na mchana. Na kadhalika kuufanya mwezi kuwa ni mshale wa saa kubwa ya wakati, na zana ya kupimia nyakati na kuiangika juu mfano wa saa zinazowekwa kwenye minara, na hiyo kwa kuifanya kuwa katika vituo mbali mbali vya miezi, hata kana kwamba Allah (s.w) kila usiku mmoja anaweka mwezi mpya usiokuwa ule wa mwanzo juu ya uso wa mbingu, kisha anarejesha na kuikusanya miezi hiyo na kuendesha katika vituo vyake kwa kipimo kamili na hesabu madhubuti. Kisha hakika kupamba uso wa mbingu na kuitia uzuri kwa nyota zenye kumetameta na kutabasamu katika kuba la mbingu, hapana shaka hilo ni katika alama za Rububiyya isiyo na ukomo adhama yake, nazo katika wakati huohuo ni ishara za uungu mtukufu usio na ukomo ukamilifu wake. Yote hayo yanasababisha wenye fikra na akili kuamini na kupwekesha. Tazama ukurasa uliowekwa rangi wenye kuvutia ukurasa wa kitabu cha ulimwengu. Namna kalamu ya kudura ya dhahabu ilivyo usawiri. Haikubaki japo nukta moja yenye giza kwa watu wenye nyoyo. Kana kwamba (s.w) aya zake ameziandika kutokana na nuru. Tazama, ee adhama ya muujiza wa hekima iliyoje, inaongoza katika kukiri! Na mandhari ya ajabu ya hali ya juu yaliyoje katika anga la ulimwengu! Na sikiliza nyota vilevile, utamu wa maneno yake mazuri yenye ladha. Upate kuona yaliyopitishwa na muhuri wa hekima wenye nuru juu ya ulimwengu. Hakika yote hayo yanatoa sauti na kusema kwa pamoja kwa ulimi wa haki: Sisi ni hoja zenye kung’ara juu ya haiba ya Mweza Mwenye utukufu. Sisi ni mashahidi wa kweli juu ya kuwepo kwa mtengenezaji mtukufu juu ya upweke wake na uweza wake. Tunavinjari kama malaika juu ya ile miujiza nyororo ambayo imetia uzuri uso wa Ardhi. Basi sisi ni maelfu ya macho yenye kuona yanayochungulia ardhini kutoka mbinguni na kukaribia peponi. Sisi ni maelfu ya matunda mazuri ya mti wa uumbaji, mkono wa hekima uliyo mzuri wenye utukufu umetuangika hapa katika upande wa mbingu na katika matawi ya njia za sayari. Basi sisi kwa watu wa mbinguni ni misikiti yenye kutembea, na makazi yenye kuzunguka na kambi za hadhi ya juu, na ndege kubwa! Hakika sisi ni miujiza ya uweza ya mweza mwenye ukamilifu na maajabu ya ufundi wa Mwenye hekima zote Mwenye utukufu, na nadira za hekima na vishindo vya umbo na alama za nuru. Kama hivi tunabainisha hoja mia moja elfu na moja, kwa ndimi mia moja elfu na moja, na tunamsikilizisha yule ambaye ni mtu kweli. Limepofuka jicho la mpagani haoni nyuso zetu za nuru, na wala hasikii kauli zetu bayana, hakika sisi ni aya zenye kuzungumza kwa haki. Mhuri wetu ni mmoja, nembo yetu ni moja, wenye kusabihi sisi ni wenye kuabudu Mola wetu, wenye kutiishwa chini ya amri yake. Tunamtaja yeye (s.w) nasi ni majudhubu kwa mahaba yake, tunanasibika na duara la dhikiri la njia ya sayari.

§4

Mwakilishi wa watu wa upotevu na mlinganiaji wake, kama hakupata cha kujengea upotevu wake, na anapokosa ushahidi, na kushindwa hoja, husema: Mimi naona kwamba furaha ya dunia, na kustarehe na utamu wa maisha, na usitawi na ustaarabu, na maendeleo ya kiviwanda, ipo katika kutokukumbuka Akhera, na katika kutokumuamini Allah (s.w), na katika kupenda dunia na katika kujikomboa kutokana na pingu na katika kuijali nafsi na kupendezwa nayo.. Kwa ajili hiyo nimewachunga watu wengi na naendelea kuwachunga - kwa hima ya shetani - kuelekea njia hii. Jawabu: Nasi kwa upande wetu tunasema - kwa jina la Qur’an tukufu - ewe Mwanaadamu mwenye hali mbaya! Rejea kwenye busara yako, usimsikilize mlinganiaji wa watu wa upotevu. Kama utamtegea sikio itakuwa hasara yako, hasara ambayo roho akili na moyo hutetemeka kutokana na kutisha kuifikiria kwake, hivyo mbele yako kuna njia mbili: Ya Kwanza: Ni njia ya mwenye simanzi ambayo anakuonesha mlinganiaji wa upotevu. Ya Pili: Ni njia ya mafanikio ambayo inakubainishia Qur’an tukufu. Na kwa hakika umeona mengi katika ulinganishaji kati ya njia hizo mbili katika sehemu nyingi za kitabu cha “Maneno” na hasa katika maudhui ya “Maneno madogo” na sasa kwenda sawa na mada zingatia katika moja wapo ya maelfu ya milinganisho na vipimo na uyazingatie, nayo: Hakika njia ya shirki, upotevu, ujinga, na uasi humporomosha mwanaadamu katika ukomo wa anguko na katika chini ya walio chini, na kuweka juu ya mgongo wake dhaifu wenye kushindwa katika giza la maumivu yasiyo na mipaka mzigo mzito hauna mwisho wa uzito wake. Na hii ni kwa kuwa Mwanaadamu kama hakumjua Allah (s.w), na kama hakumtegemea, anakuwa kama mnyama mwenye kutoweka anapata maumivu daima na kuhuzunika kwa kuendelea, na kupinduka-pinduka katika kushindwa na udhaifu visivyokuwa na mwisho, na kufululiza katika haja na ufakiri visivyo na kikomo, na kukutana na masaibu yasiyo na mpaka, na kuonja maumivu ya utengano kutoka kwa yule aliyempenda na kufuma kati yake na yeye nyuzi za mahusiano, anaumia – na anaendelea kuumia - mpaka awaache waliyobakia katika wapendwa wake mwisho wa mzunguko na kufarikiana nao akihuzunika mpweke mgeni kuelekea katika aina kwa aina za giza la kaburi. Na ataikuta nafsi yake muda wote wa uhai wake mbele ya maumivu na matumaini yasiyokuwa na mwisho, naye hamiliki kitu isipokuwa sehemu ya utashi tu, uwezo mdogo, uhai mfupi, umri wenye kutoweka na fikira yenye kufifia. Basi juhudi zake katika kuituliza zinapotea bure, na kwenda patupu nyuma ya matakwa yake yasiyokuwa na mipaka. Na namna hii uhai wake unapita pasi na kuvuna matunda. Na unapomuona kuwa ni mwenye kushindwa kubeba mizigo ya nafsi yake, utaona anaubebesha mgongo na hima yake masikini mizigo mikubwa ya dunia, hapo anateseka mateso ya kuunguza na kuumiza kabla ya kufika katika adhabu ya Jahiim. Hakika watu wa upotevu hawahisi maumivu haya machungu na adhabu ya kiroho ya kutisha, kwani nafsi zao wanazitupa vifuani mwa mghafala ili wabatilishe hisia zao na kuzitia ganzi hisi zao kwa muda fulani... Lakini muda mfupi tu mmoja wao anapokaribia ukingoni mwa kaburi tahamaki hisia zake zinashika kasi na huongezwa kwa maumivu haya kwa mkupuo mmoja. Hii ni kwa sababu kama hakuwa mja mwenye ikhlasi kwa Allah (s.w). Atadhani kwamba yeye ni mmiliki wa nafsi yake, pamoja na kuwa yeye ni mwenye kushindwa kwa sehemu ya utashi wake, na uwezo wake mdogo, hata katika kujiendesha yeye mwenyewe peke yake mbele ya hali za dunia hii zenye kupiga dhoruba, kwani anaona ulimwengu wa maadui unamzunguka kuanzia vijidudu vidogo vidogo vya kueneza maradhi na kuishia katika matetemeko yenye kuteketeza wakiwa katika maandalizi timamu ya kumshambulia na kumaliza uhai wake. Hapo viungo vyake vinatetemeka na moyo wake unadundadunda kwa woga na kufazaika kila anapofikiria kaburi na kuliangalia. Na wakati ambapo Mwanaadamu huyu anaumia kutokana na hali yake, wakati huo huo hali mbalimbali za dunia humtopeza daima, na wakati huo hali za wanadamu anaohusiana nao zinamchosha daima, na hii kwa dhana yake kwamba matukio haya yanatokana na mchezo wa asili na upuuzi wa sadfa, na sio kutokana na utendaji wa Mmoja wa Pekee Mwingi wa hekima na Mjuzi, na wala sio kwa makadirio ya Mweza Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu na Mkarimu sana, hivyo huugulia pamoja na maumivu yake maumivu ya watu wengine vilevile. Hivyo matetemeko, tauni, tufani, ukame, ughali, kutoweka, kuondoka na mfano wa hayo huwa ni masaibu yenye kutokea na mabalaa yenye kuhangaisha na kutesa! Basi Mwanaadamu huyu ambaye amejichagulia mwenyewe hali hii ya kutisha, haonewi huruma wala kusikitikiwa... Mfano wake katika hili ni kama mfano uliotajwa katika milinganisho kati ya ndugu wawili katika “Neno la Nane” kwamba mtu ambaye hakukinai na ladha halali na msisimko safi na maliwazo mazuri na matembezi matukufu ya halali, kati ya wapendwa wazuri katika bustani yenye hewa nzuri kati ya ugeni mtukufu, akawa anatumia pombe ya najisi ili apate ladha isiyo ya halali, akalewa mpaka akaanza kuoneshwa katika mawazo yake kwamba yuko mahali pachafu na kati ya wanyama washambuliaji, anapatwa na kutetemeka kama yupo kwenye majira ya baridi kali, akaanza kupiga kelele ya kuomba msaada na hakuna aliyemuhurumia, kwa sababu ameleta taswira ya wale marafiki wema kuwa ni wanyama wakali akawadharau na kuwadhalilisha... Na vyakula vitamu na vyombo visafi ambavyo vipo katika ukumbi wa ugeni akavifikiria kuwa ni mawe yaliyochafuliwa na kuanza kuvivunjavunja... Na vitabu vya thamani na risala adimu zilizopo kwenye baraza alidhani ni nakshi za kawaida na mapambo yasiyo na maana, akaamua kuvichana na kuvitupa chini miguuni... Na namna hii. Basi kama mtu huyu na wengine kama yeye wasivyostahiki kuhurumiwa wala kustahiki kusikitikiwa kwa upole bali anawajibika kutiwa adabu na kukaripiwa. Na ndivyo hali ilivyo kwa mtu anayedhani kwa sababu ya ulevi wa ukafiri na wazimu wa upotevu vinavyotokana na uchaguzi wake mbaya kwamba dunia ambayo ni nyumba ya wageni ya Mtengenezaji Mwingi wa hekima, ameifanya kuwa ni mchezo wa sadfa pofu, na mchezo wa maumbile butu... na anajenga taswira ya kuletwa upya vilivyoundwa kwa udhihirisho wa majina mazuri, na kuvuka kwake kwenda kwenye ulimwengu usioonekana pamoja na mkondo wa muda baada ya kumaliza majukumu yake na kwisha malengo yake, kana kwamba vinamiminwa kwenye bahari ya kutokuwepo, na bonde la kukosekana na kupotea katika fukwe za kutoweka. Na anafikiri sauti za tasbihi na tahmidi zinazojaa ulimwenguni kuwa ni manung’uniko na kelele wanazozitoa wakuondoka na kutoweka katika utengano wao wa milele... Na anadhani kurasa za viumbe vilivyopo ambazo ni barua za kiungu Mkusudiwa kwa kila haja zenye kupendeza, ni mchanganyiko usiokuwa na maana yoyote wala faida... na anafikiri mlango wa kaburi ambao unafungua njia ya kwenda kwenye ulimwengu wa rehema uliyompana kuwa ni handaki linalopelekea kwenye aina ya giza la hali ya kutokuwepo... Na anadhani wakati wa kufa ambao ni wito wa kuungana na kukutana kwa wapenzi wa kweli ni muda wa kutengana kwa wapenzi wote! Naam, hakika mtu anayeishi katika hali hii ya taswira na dhana hizi anajiingiza katika tanuri la mateso ya dunia yaumizayo, ukiachilia mbali kuwa hatostahiki kuhurumiwa na kusikitikiwa, bali anastahiki adhabu kali, kwa kule kudharau kwake viumbe, kwa kuvituhumu kuwa ni upuuzi, na kwa kuyapotosha majina mazuri, kwa kukana kudhihiri kwake, na kukukana barua za kiungu kwa kukataa ushahidi wake juu ya upweke. Basi enyi wapotevu wapumbavu, na enyi wahasirika waovu! Je mnaona kwamba elimu zenu kubwa zinafaa kitu, na majengo makubwa ya ustaarabu wenu, na vyeo vya juu sana vya umahiri wenu na umaridadi wa mipango ya werevu wenu - vinafaa kitu chochote mbele ya kuporomoka huku kunakotisha kwa Mwanaadamu? Na je anaweza kusimama imara mbele ya kukata tamaa huku kunakoteketeza roho ya wanadamu yenye kupenda sana kupata maliwazo? Na je yanaweza mnayoyaita “Maumbile” kwenu, na mnazoziegemezea athari za kiungu katika “Sababu” kwenu, na mnazozinasibishia mema ya kiungu katika “Mshirika” kwenu, na mnayojifaharisha nayo kati ya “Vumbuzi zenu” na mnaojivunia nao miongoni mwa “Watu wenu” na mnavyoviabudu katika “Muabudiwa wenu” batili... Je, wote hao wanaweza kuokoeni kutokana na giza aina kwa aina la kifo ambacho ni kupotezwa kwa milele kwenu? Na je wote hao wanaweza kukupitisheni katika mipaka ya kaburi kwa usalama na katika hadidu za kizuizi cha Barzakh kwa amani? na katika medani ya ufufuo kwa utulivu? Na kuweza kuwasaidieni kuvuka daraja la sirata sawasawa, na kuwafanya wenye kustahiki furaha ya milele na maisha ya milele? Hamna namna mtapita tu katika njia hii, kwani sio uwezo wenu kuufunga mlango wa kaburi kwa mtu yeyote. Hivyo nyinyi ni wasafiri wa njia hii hakuna kimbilio. Na mtu apitaye kwenye njia hii hulazimika ajiegemeze na kufanya tawakkul kwa Mwenye ujuzi wa kuzungukia kila jambo unaenea kwa kila njia zake na matawi yake na mipaka yake mipana. Bali duru zote hizo kubwa zinakuwa chini ya utendaji wake na ndani ya amri yake na hukumu yake. Basi enyi wapotevu wenye kughafilika! Hakika kilichowekwa katika maumbile yenu, katika utayari wa mahaba na ujuzi, na katika sababu za shukurani na njia za ibada ambazo zinabidi zitumiwe kwa ajili ya dhati ya Allah (s.w), na yapasa zielekee kwenye sifa zake tukufu na majina yake mazuri, nyinyi mmezitumia - kwa namna isiyo ya halali - kwa ajili yenu na kwa ajili ya dunia, basi mnapata adhabu yake kwa kustahiki, na hii ni kwa siri ya kanuni: “Hakika matokeo ya mapenzi yasiyo ya halali ni kuumizwa na adhabu pasipo na huruma”. Kwa sababu nyinyi mmezipa nafsi zenu mahaba ambayo yanamhusu Allah (s.w), hivyo mnapata taabu za mabalaa ya mnaowapenda pasipo idadi, pale ambapo hamkuzipa raha zake za kweli... Na hivyo hivyo hamsalimu amari yake kwa kumtegemea mahabubu wa haki naye ni Allah (s.w) Mweza wa kila jambo bila mipaka, hivyo mnapata maumivu daima. Na kama hivyo mmeipa dunia mapenzi ambayo yanarejea kwenye majina ya Allah (s.w), na sifa zake tukufu takatifu. Na mkagawa athari za ufundi wake na kuweka mafungu baina ya sababu za kimaada, basi mnaonja shida ya amali yenu, kwa sababu sehemu ya wapendwa wenu wengi wanakuacheni wakirejea pasipo kuaga, na kati yao ni wale wasiokujueni kamwe, na hata wakikujueni hawakupendeni, na hata wakikupendeni hawakufaeni kitu, basi mnabaki ndani ya adhabu ya kudumu miongoni mwa adhabu za utengano usio na mpaka na katika maumivu ya kutoweka kwa kukata tamaa ya kurejea. Huu ndio ukweli wa wanayodai watu wa upotevu, na kiini cha wanacholingania katika “Furaha ya maisha” na “Ukamilifu wa Mwanaadamu” na “Mazuri ya ustaarabu” na “Utamu wa kujiweka huru”!! Ehe! Uzito ulioje wa pazia la upumbavu na ulevi unaotia ganzi fahamu na hisi! Ehe! Sema: Maangamizi kwa akili ya hao wapotevu! Ama njia iliyonyooka au njia yenye nuru ya Qur’an, inatibu majeraha yote ambayo watu wa upotevu wanateseka nayo na kuyaponya kwa hakika za kiimani, na kuteketeza viza vyote vilivyotangulia kwenye njia hiyo na kufunga njia zote za upotevu, na maangamizi kwa kutumia yafuatayo: Hakika inatibu udhaifu wa Mwanaadamu, kutojiweza kwake, ufakiri wake, na mahitajio yake kwa kumtegemea Mweza wa kila kitu Mwingi wa rehema, hali ya kusalimisha mazito ya maisha na majukumu ya kuwepo kwenye uweza wake (s.w), na kwa rehema zake kunjufu, bila ya kuyabebesha mgongoni mwa Mwanaadamu. Bali anamfanya mwenye kumiliki hatamu ya nafsi yake na uhai wake mwenye kupata kwa hivyo makamo ya kustarehesha na kumtambulisha kuwa yeye sio mnyama mwenye kufikiri, bali yeye ni Mwanaadamu kwa hakika na mgeni mwenye heshima na kutukuzwa mbele ya Mfalme Mwingi wa rehema. Inatibu pia yale majeraha ya kibinaadamu yatokanayo na kutoweka kwa dunia na kuondoka kwa vitu, na kutokana na kupenda vyenye kumalizika inayatibu kwa upole na huruma kwa kumuonesha kuwa dunia ni nyumba ya ugeni ya Mwingi wa rehema na kubainisha kwamba vilivyomo kati ya viumbe ni vioo vya majina mazuri, na hali ya kuweka wazi kwamba vitengenezwa vyake ni barua za kiungu zinazokuwa upya kila zama kwa idhini ya Mola wake, na hivyo kumuokoa Mwanaadamu kutokana na kubanwa na magiza ya dhana. Na inatibu pia yale majeraha ambayo yanaachwa na umauti ambayo watu wa upotevu wanayapata kuwa ni utengano wa milele na wapendwa wote, kwa kubainisha kuwa umauti ni utangulizi wa kuungana na kukutana pamoja na wapenzi ambao walisafiri kwenda kwenye ulimwengu wa Barzakh, na ambao wao hivi sasa wako katika ulimwengu wa kubakia, na inathibitisha kuwa huko kutengana ni hasa kukutana. Na pia inaondosha hofu kubwa ya mwanaadamu kwa kuthibitisha kwamba kaburi ni mlango uliofunguliwa kuelekea katika ulimwengu wa rehema kunjufu, na katika mji wa furaha ya kudumu milele, na katika bustani za pepo na katika miji ya nuru ya Al-Rahamani Al-Rahiim, kwa kubainisha kuwa matembezi ya Barzakh ambayo yana maumivu makali mno na matembezi yenye taabu zaidi kwa watu wa upotevu ni matembezi ya starehe zaidi na yenye kuliwaza na kufurahisha zaidi kwani kaburi sio mdomo wa joka la kutisha bali ni mlango kuelekea katika bustani miongoni mwa bustani za Janna. Na inamwambia muumini: Kama utashi na hiari yako ni ya kisehemu (Juz ‘iyyah) basi salimisha mambo kwa utashi wa mola wako wenye sifa ya kuenea kila kitu... Na kama uweza wako ni dhaifu basi tegemea juu ya uweza wa Mweza bila kikomo... Na ikiwa uhai wako ni wa kutoweka na mfupi basi fikiria uhai wa kubakia wa milele... na ikiwa umri wako ni mfupi basi usihuzunike kwani unao umri mrefu... na kama fikira yako ni fifi basi ingia chini ya nuru ya jua la Qur’an tukufu na tazama kwa kutumia nuru ya imani ili kila aya katika aya za Qur’an tukufu ikupe nuru kama nyota zinazomeremeta, zenye kuangaza badala ya fikira zako zenye kushindwa... Na ukiwa na maumivu na matarajio yasiyokuwa na ukomo hakika thawabu isiyokuwa na ukomo na rehema zisizo na ukomo zinakusubiri... na kama una malengo na makusudio yasiyokuwa na mipaka usitaabike kufikiria kwani hapa duniani hayadhibitiki, bali mahali pake ni katika mji mwingine, na mpaji wake ni Mwema Mkarimu mno, mkunjufu wa kutoa. Inamsemesha Mwanaadamu tena na inasema: Ewe Mwanaadamu! Wewe sio mmiliki wa nafsi yako, bali wewe umemilikiwa na Mweza Mwenye uwezo usiokuwa na ukomo, na Mwingi wa rehema isiyokuwa na ukomo. Usiitaabishe nafsi yako kwa kuibebesha mashaka ya uhai wako, hakika aliyetoa uhai ndiye anayeuendesha. Kisha dunia haikuachwa bila ya Mmiliki, hata uwe na wasiwasi nayo, na kujikalifisha nafsi yako kubeba mizigo yake na kuichosha fikra yako katika hali za hiyo dunia. Hii ni kwa kuwa Mmiliki wake ni Mwingi wa hekima na Mola wake ni Mjuzi wa kila kitu, na wewe ni mgeni wake tu katika hiyo dunia basi usiingilie kwa kuvuka mipaka katika mambo, na wala usiyachanganye bila ya ufahamu. Halafu Mwanaadamu na mnyama sio viumbe waliopuuzwa, bali ni wenye kupewa wadhifa na kuamuriwa chini ya utawala wa Mwingi wa hekima, Mwingi wa rehema, na chini ya uangalizi wake. Roho yako usiitatize kwa maumivu kwa kufikiria katika mashaka ya hao na maumivu yao wala usitangulize huruma yako juu yao mbele ya huruma ya Muumba wao Mwingi wa rehema. Kisha hakika hatamu ya hao ambao wamechukua hatua ya uadui na wewe, kuanzia vijidudu hadi tauni, tufani, na ukame, na matetemeko bali hatamu ya kila kitu iko mkononi mwa huyo Mwingi wa rehema, Mkarimu (s.w). Yeye ni Mwingi wa hekima kwake hakutokei upuuzi, naye ni Mwingi wa rehema mkunjufu wa rehema kila anachokifanya kuna athari ya upole na huruma yake. Na inasema vilevile: Hakika ya huu ulimwengu japokuwa ni wa kutoweka, unaandaa mahitaji ya ulimwengu wa milele... pamoja na kuwa ni wa kutoweka na wa muda mfupi isipokuwa unaleta matunda ya kudumu, na unaonesha madhihirisho mazuri katika madhihirisho ya majina mazuri ya kudumu milele... pamoja na kuwa utamu wake ni mchache na maumivu yake ni mengi, isipokuwa mazuri ya Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu na ukarimu wake na ufadhili wake zenyewe ni tamu za kikweli kweli hazitoweki. Ama maumivu nayo pia huzalisha utamu wa kimaanawi kwa upande wa thawabu za Akhera. Maadamu duara la halali linatosha kuvichukua vyote roho, moyo na nafsi utamu wake na misisimko yake kwa pamoja. Kwa hiyo hapana haja kuingia katika duara la haramu kwa sababu utamu mmoja katika duara hili, inaweza kuwa na maumivu elfu moja na moja, ukiongezea kuwa hiyo ni sababu ya kuzuiliwa kwa ladha ya takrima ya Mwingi wa rehema, Mkarimu ile ladha safi iliyotakata ya kudumu milele na milele. Namna hii, kutokana na yaliyotangulia imebainika: Kwamba njia ya upotevu humtupa mwanaadamu kwenda chini ya walio chini, kwa kiwango ambacho ustaarabu wowote na falsafa yeyote iwayo vinashindwa kuleta ufumbuzi wake, bali maendeleo ya kibinaadamu na kiasi alichofikia cha ngazi za kielimu vinashindwa kumuondoa kutoka katika giza hilo nene katika upotevu. Wakati ambapo Qur’an tukufu inamshika mkono Mwanaadamu, kwa imani na amali njema, na kumnyanyua kutoka chini ya walio chini na kumpandisha juu ya walio juu, na kumbainishia dalili zenye kukata hoja na kukunjua dalili zenye nguvu juu ya hayo mbele yake, na kufukia hayo mahandaki ya kina kwa ngazi za maendeleo ya kimaanawi na kwa vifaa vya muungano wa kiroho... na kwa namna hii inamrahisishia kwa wepesi bila kikomo safari yake ndefu ya kuchosha yenye kupiga dhoruba, inayokwenda kwa kasi kuelekea umilele, na kumrahisishia, na hiyo kwa kudhihirisha nyenzo na vitendea kazi ambavyo anaweza kuvitumia kukata masafa ya miaka elfu, bali miaka hamsini elfu, ndani ya siku moja. Na namna hii humfunika Mwanaadamu joho la utumwa na kumpatia hatua ya mja mwenye kuamuriwa, na mgeni mfanya kazi mbele ya dhati tukufu, na hii kwa kumjulisha kwamba Allah (s.w), ndiye Mmiliki wa tangu na milele, na kumdhaminia raha kamili katika utalii wake duniani katika hali ya ugeni au katika nyumba za kwenye Barzakh na miji ya Akhera... Na kama alivyo mfanya kazi mwaminifu kwa mfalme anatembea kwa wepesi kamili, katika duara la mamlaka ya ufalme na anatembea katika mipaka ya utawala wake kwa vyombo vya usafiri wa haraka kama ndege, meli, na treni, hivyo hivyo Mwanaadamu ambaye anajinasibisha na imani kwa Mmiliki wa tangu anapita na amali njema kutoka katika vituo vya dunia vya ugeni na katika miji ya ulimwengu wa Barzakh na ufufuo na kutoka katika mipaka yake mikunjufu yenye kuenea, kwa wepesi wa umeme na buraki mpaka apate furaha ya milele... Qur’an tukufu inathibitisha hakika hizi kwa uthibitisho wa kukata hoja na kuyaonesha waziwazi kwa wateule na mawalii. Halafu hakika yake inaendelea kwa kusema: Ewe Muumini usipoteze unachomiliki katika ukubalifu usio na mipaka kwa ajili ya kuipenda nafsi yako ambayo ni yenye kuamuru sana maovu, nayo ni mbaya, pungufu yenye shari na yenye kudhuru, wala usiifanye kuwa mpendwa wako wala usiabudu matamanio yake, bali mfanye mpenzi wako yule ambaye anastahiki mapenzi yasiyokuwa na ukomo... huyo ni Mweza wa kukufanyia hisani, hisani isiyokuwa na ukomo, na Mweza wa kukufanya ufurahi furaha ambayo haina kikomo bali atakufurahisha tena kwa hisani zake anazotoa kwa wote ambao unafungamana nao kwa mahusiano, yeye ndiye mwenye ukamilifu usiokuwa na ukomo na uzuri mtakatifu na aliyeepukana na upungufu na kasoro na kuondoka na kumalizika... Uzuri wake hauna mipaka na majina yake yote ni mazuri ya kupendeza. Naam, hakika katika kila jina miongoni mwa majina yake kuna nuru za kupendeza na uzuri zisizokuwa na ukomo; kwa hiyo pepo na mazuri yake yote, urembo wake, na neema zake, hakika hiyo si jambo lingine isipokuwa ni udhihirisho kwa ajili ya kudhihirisha uzuri wa rehema yake na rehema ya uzuri wake, na urembo na uzuri wote, mazuri na makamilifu yenye kupendwa na yenye kupendezesha katika ulimwengu wote, hiyo ni ishara ya uzuri wake na dalili ya ukamilifu wake (s.w). Na inasema tena: Ewe Mwanaadamu! hakika chemchemu za mahaba zenye kupasuka kwenye kina cha ndani yako na zenye kuelekea kwa Allah (s.w), na zenye kuambatana na majina yake mazuri, na zenye kumsifia Mwenyezi Mungu kwa sifa zake tukufu, usizifanye zitumike katika kushikamana na viumbe vyenye kutoweka na wala usizipoteze bure bila ya faida kwa viumbe vyenye kuondoka, hiyo ni kwa sababu athari na viumbe ni vyenye kuondoka, wakati majina mazuri yenye kuonesha udhihirisho wake na uzuri wake kwa athari hizo na hivyo vilivyoundwa, ni yenye kubaki daima. Katika kila jina miongoni mwa majina mazuri ya Allah (s.w), na katika kila sifa miongoni mwa sifa takatifu kuna maelfu ya ngazi za hisani na uzuri na maelfu ya tabaka za ukamilifu. Tazama jina “Ar-Rahman” tu, utaona kwamba pepo ni moja ya madhihirisho yake na furaha ya milele ni moja ya miale yake, na riziki zote na neema zilizotawanywa kote pande za dunia ni moja ya matone yake. Tazama kwa makini sana na uchunguze aya tukufu ambazo zinaashiria ulinganisho huu kati ya hakika ya watu wa upotofu na watu wa Imani kwa upande wa uhai na upande wa jukumu: لَقَد۟ خَلَق۟نَا ال۟اِن۟سَانَ فٖٓى اَح۟سَنِ تَق۟وٖيمٍ ثُمَّ رَدَد۟نَاهُ اَس۟فَلَ سَافِلٖينَ اِلَّا الَّذٖينَ اٰمَنُوا وَ عَمِلُوا الصَّالِحَاتِ na aya nyingine ni: فَمَا بَكَتْ عَلَيْهِمُ السَّمَاء وَالْأَرْضُ وَمَا كَانُوا مُنظَرِينَ Aya hizi zinaashiria mwisho wa kila mmoja kati ya makundi mawili hayo. Zichunguze utaona kiasi cha ukuu wake na miujiza yake katika kubainisha tuliyoyataja katika vipimo na milinganisho. Ama aya za mwanzo tunarejesha kubainisha hakika ya maana yake iliyomo ya miujiza kwa ufupi hadi katika “Neno la Kumi na Moja” ambayo inafafanua kwa uwazi kabisa. Ama aya ya pili tutaashiria - ishara moja tu - kiasi cha kutoa kwake maana ya ukweli mkuu nayo ni kama ifuatavyo. Zinasema kuwa: Hakika mbingu na ardhi havilii kwa kifo cha watu wa upotevu. Na kwa maana ya kinyume chake ni kuwa mbingu na ardhi vinalia kwa kuondoka duniani kwa watu wa imani. Yaani kwa kuwa watu wa upotevu wanakanusha majukumu ya mbingu na ardhi na kuvituhumu kuwa ni upuuzi na hawatambui maana ya majukumu yanayotekelezwa na mbingu na ardhi. Kwa hiyo wanadhulumu haki za mbingu na ardhi. Bali hawamjui Muumba wake wala dalili za Muumba wake (Wa mbingu na ardhi) wanazidharau na wanazishikia msimamo wa uadui kuzidunisha na kubeza, hapana budi kwa mbingu na ardhi kutotosheka na kutokuwalilia tu, bali pia kuwaombea dua mbaya, bali kupumzika kwa kuangamia kwao. Na inasema vilevile kwa maana tofauti: Hakika mbingu na ardhi zinalia kwa ajili ya kufa kwa watu wa Imani, kwa sababu wao wanajua majukumu ya hizo mbingu na ardhi na kuzithamini ukweli wa kuzithamini, na wanakubali kweli zake za hakika na wanafahamu kupitia imani umuhimu na maana yake yanayopatikana, kwani kila wanapozingatia na kuzichunguza husema kwa mshangao: “Uzuri ulioje wa kuumbwa kwake!” Na “Uzuri ulioje wa majukumu yanayotekelezwa na mbingu na ardhi!” Hivyo huzipa thamani na heshima zinazostahiki na kueneza mapenzi kwa hizo mbingu na ardhi kwa kumpenda Mwenyezi Mungu, yaani kwa ajili ya Allah kwa kuzizingatia kuwa ni vioo vya kudhihirishia majina mazuri ya Allah. Kwa ajili hii mbingu hutetemeka na ardhi kuhuzunika, kwa kufa watu wa imani kana kwamba zinalia kwa ajili ya kutoweka kwao. Swali Muhimu Mnasema: Hakika mapenzi si jambo la hiari halipo katika matakwa yetu, basi mimi kwa mujibu wa haja yangu ya kimaumbile ninapenda vyakula vitamu, na matunda mazuri, na ninawapenda wazazi wangu wawili na watoto wangu na mke wangu ambaye ni mwenza wa maisha yangu, na nawapenda manabii watukufu, na mawalii wema, na ninapenda ujana wangu, na uhai wangu, na ninapenda majira ya machipuo na kila kitu kizuri, na kwa maelezo ya ufupi mimi naipenda dunia. Na kwa nini nisipende vitu vyote hivi?... : Lakini vipi nitaweza kuwasilisha aina zote hizi za mapenzi kwa Allah, na kujaalia mapenzi yangu kwa majina yake mazuri na sifa zake tukufu na dhati yake takatifu (s.w)? Hii ina maana gani? Jawabu: Unapaswa kusikiliza nukta nne zifuatazo: Nukta ya Kwanza: Hakika mapenzi hata kama sio ya kihiari, isipokuwa yanaweza kugeuzwa mwelekeo wake kwa matakwa kutoka mpendwa mmoja kwenda mwingine; mathalani kama vile kudhihiri ubaya wa anayependwa na uhakika wake, au kujulikana kwamba ni kizuizi na pazia kwa mpendwa wa hakika anayestahiki mapenzi, au kioo chenye kuakisi uzuri wa huyo mpendwa wa hakika, basi hapo inawezekana kugeuzwa sura ya mapenzi kutoka mpenzi asie wa hakika na kwenda kwa mpenzi wa hakika. Nukta ya Pili: Sisi hatukuambii: Usibebe mapenzi kwa kila ulichotaja hapo nyuma. Lakini tunakwambia yafanye mapenzi yako kwa hivyo ulivyovitaja yawe kwa ajili ya Allah na kwa dhati yake tukufu. Kuburudika na vyakula vitamu na kuonja matunda mazuri pamoja na kukumbuka kuwa hiyo ni hisani kutoka kwa Allah (s.w), na ni neema kutoka kwa Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu, inamaanisha mapenzi kwa jina la “Ar-Rahmaan” na jina la “Al-Mun’imu” katika majina mazuri zaidi, isitoshe hiyo ni shukrani ya kimaanawi, na ambayo inatujulisha kuwa mapenzi haya hayakuwa kwa ajili ya nafsi na matamanio yake bali kwa ajili ya jina la “Ar-Rahman” ni kutafuta riziki ya halali pamoja na kukinai kikamilifu ndani ya duara la halali kisheria na kutumia kwa kutafakari kuwa hiyo ni neema kutoka kwa Allah (s.w), pamoja na kumshukuru. Kisha mapenzi yako kwa wazazi wawili na kuwaheshimu kunarejea katika kumpenda Allah (s.w); kwani yeye ndiye aliyepandikiza kwao upole na huruma mpaka wakakulea kwa huruma na hekima zote. Na alama ya kuwa ni mahaba kwa ajili ya Allah (s.w), ni kuzidisha kuwapenda na kuwaheshimu wanapofikia uzee, na hakubakii tamaa yoyote ndani yako ya kupata chochote kutoka kwao, ukawa unaongeza huruma kwao pamoja na kuwa wanakushughulisha na matatizo na kukuzidishia uzito wa mashaka. Basi aya tukufu: اِمَّا يَب۟لُغَنَّ عِن۟دَكَ ال۟كِبَرَ اَحَدُهُمَٓا اَو۟ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل۟ لَهُمَٓا اُفٍّ Zinawalingania watoto kuchunga haki za wazazi wawili katika ngazi tano, na zinabainisha umuhimu wa kuwafanyia wema na ubaya wa kuwaudhi... Kwani mzazi hakubali kutanguliwa na yoyote isipokuwa mwanawe kwani habebi katika maumbile yake hasadi yoyote dhidi yake jambo ambalo huziba njia kwa mtoto kudai haki yake kutoka kwa mzazi; kwani uhasama ima unatokana na hasadi na kushindana kati ya wawili au hutokana na kudharau haki. Hivyo mzazi yuko salama amenusuriwa na hayo kimaumbile. Kwa hiyo si halali kwa mtoto kuleta madai dhidi ya mzazi wake, bali hata kama ataona kwake uovu hana haki ya kumuasi na kumuudhi. Kwa maana anayewaasi na kuwaudhi wazazi wake wawili huyo hawi ila ni Mwanaadamu aliyegeuzwa umbo na kuwa mnyama mshambuliaji. Ama kuwapenda watoto ni kumpenda Allah (s.w) vilevile na kunarejea kwake. Na hii ni kwa kuwatunza kwa upole na huruma kamili kwa kuwa wao ni hiba kutoka kwa Ar-Rahiim Al-Kariim. Ama alama ya kuwa mapenzi hayo ni kwa ajili ya Allah (s.w) na kwa ajili yake ni kule kusubiri pamoja na kushukuru wakati wa kupatwa na mtihani na hasa wakati wa kifo, na kujiepusha na kukata tamaa na kupuuzia dua, bali inapasa kusalimu amri mbele ya majaaliwa kwa kushukuru. kama kusema: Hakika kiumbe huyu ni mwenye kupendwa mbele ya Mola Muumba Mkarimu na mwenye kumilikiwa naye, na amenikabidhi akiwa ni amana kwa muda fulani, na sasa imeamua hekima yake (s.w), kumchukua kutoka kwangu kumpeleka mahali pa salama na bora zaidi. Ikiwa nina hisa moja tu ya dhahiri, basi yeye (s.w), ana hisa elfu moja za hakika. Hakuna pa kukimbilia kutokana na kujisalimisha na hukumu ya Allah (s.w). Ama kuwapenda maswahiba, wakiwa ni katika watu wa Imani na ucha Mungu basi kuwapenda hao ni katika njia ya Allah (s.w), na kunarejea kwa (s.w) kwa mujibu wa “Kupenda kwa ajili ya Allah (s.w)” Ama kumpenda mke naye ni mwenza wa maisha yako ni juu yako kumpenda akiwa ni zawadi ya maliwazo na nzuri katika zawadi za rehema za kiungu. Na ole wako ufungamanishe na uzuri wa nje ambao huondoka haraka bali ufunge kwa umadhubuti na uzuri usiotoweka wenye kuzidi kung’ara siku baada ya siku nao ni uzuri wa tabia na mwenendo mzuri uliopo kwenye uanauke wake na ulaini wake. Na hakika kilicho kizuri mno kwake katika urembo na kikuu zaidi, ni katika huruma yake ya dhati yenye nuru. Huu uzuri wa huruma na mwenendo mwema hudumu na kuongezeka hadi mwishoni mwa umri, na kwa kuvipenda viwili hivyo ndipo haki za kiumbe huyu mpole mnyonge huweza kulindwa, na kama sivyo, haki zake huzikosa wakati ambapo yeye huzihitajia mno, kwa sababu ya kuondoka uzuri wa nje. Ama kuwapenda Manabii (a.s) na mawalii wema nako pia ni kwa ajili ya Allah (s.w) na katika njia yake kwa kuwa wao ni waja wa Allah (s.w) wateule wenye kukubalika mbele ya Allah (s.w). Hivyo kwa upande huu mapenzi hayo yanakuwa ni kwa ajili ya Allah (s.w). Pia maisha ambayo Allah (s.w) amekutunukia wewe na kwa Mwanaadamu, ni rasilimali adhimu unayoweza kuitumia kuvuna maisha ya akhera ya kubakia milele, nayo ni hazina adhimu yenye kubeba ala na makamilifu ya kudumu... Kwa ajili hii kuyahifadhi na kuyapenda ni kutokana na upande huu, na kuyatumia kwa ajili ya Mola Mlezi (s.w), hurejea kwa Allah (s.w). Kadhalika kuupenda ujana, uzuri, na kupendeza kwake na kuuthamini kwa kuwa ni neema nzuri kutoka kwa Bwana Mlezi, kisha kuutumia vyema, hayo ni mapenzi ya kisheria na bali ni yenye kushukuriwa. Halafu kupenda majira ya machipuo na kuwa na shauku nayo ni kwa ajili ya Allah (s.w), na yenye kuelekea katika majina yake mazuri, kwa kuwa kwake ni ukurasa mzuri wa kuonekana michoro ya majina mazuri yenye nuru na maonesho makuu zaidi kwa ajili ya kuonesha ufundi makini maridadi wa Mola Mlezi. Hivyo kutafakari majira ya machipuo kwa upande huu ni mapenzi yanayoelekea kwenye majina mazuri. Hata kuipenda dunia hugeuka kuwa ni mapenzi kwa ajili ya dhati ya Allah (s.w), pale inapokuwa kuitazama hiyo dunia ni kwa upande wa kuwa ni shamba la Akhera, na kioo cha majina mazuri ya Allah (s.w), na ni barua za Bwana Mlezi katika uwepo na nyumba ya ugeni kwa muda fulani na kwa sharti la kutoingilia nafsi yenye kuamrisha maovu ndani ya mapenzi hayo. Muhtasari: Jaalia kupenda kwako dunia na vilivyomo miongoni mwa viumbe kuwa ni kwa maana “Ya kiherufi” na siyo kwa maana “Ya kijina” yaani kwa maana ya yaliyomo na sio dhati yake yenyewe. Wala usiseme kwa kitu: “Uzuri ulioje wa kitu hiki!” bali sema: “Uzuri ulioje wa umbo la kitu hiki!” au “Umbo lake ni zuri kiasi gani!” Na tahadhari usije ukaacha mwanya wa kumpenda asiyekuwa Allah (s.w) ndani ya moyo wako, kwani ndani yake ni kioo cha AS-Swamad (Mwenye kukusudiwa kwa haja zote), na ni mahsusi na maalum kwa ajili yake Allah (s.w), na useme: Ee Allah! Turuzuku kukupenda na mapenzi yanayotukurubisha kwenye kukupenda Wewe. Kama hivyo, yote tuliyoyataja katika aina za mapenzi endapo yataelekezwa upande sahihi kwa sura iliyotajwa huko nyuma, yaani yanapokuwa kwa ajili ya Allah (s.w), na kwa njia yake, basi yataleta utamu wa ukweli bila ya machungu na yatakuwa ni muungano wa kweli pasi na kutoweka bali yatazidisha mapenzi ya Allah (s.w), ukiachilia mbali kule kuwa hayo ni mapenzi ya kisheria na yanakuwa ni shukurani kwa Allah (s.w) katika ladha hiyo hiyo, na kutafakari juu ya neema zake ndani ya mapenzi yenyewe. Mfano: Ikiwa mfalme mkubwa amekuzawadia tufaha – mathalan- hakika utalipa aina mbili ya mapenzi na utaburudika nalo kwa utamu wa aina mbili: Ya kwanza: Mapenzi ambayo yanarejea kwenye tufaha, kwa kuwa ni tunda zuri lina utamu kiasi cha sifa maalum zilizomo ndani yake, mapenzi haya hayarejei kwa mfalme. Bali anayelila kwa pupa mbele yake huonesha mapenzi yake kwa hilo tunda na sio kwa mfalme, na pengine mfalme asifurahishwe na kitendo hicho, na akachukia mapenzi hayo makubwa kwa nafsi yake. Zaidi ya kuwa utamu wa tufaha ni mdogo nao ni wenye kutoweka kwani mara tu baada ya kumaliza kula tufaha hilo utamu huondoka na kusababisha masikitiko. Ama Mapenzi ya Pili: Ni kwa ajili ya takrima ya kifalme na kuzingatia kwake kwema ambako kumeonekana kwa tufaha... kana kwamba tufaha lile ni kielelezo cha heshima ya kifalme, au ni sifa iliyobeba umbo kutokana na tufaha. Basi anayepokea zawadi ya mfalme kwa mapenzi na takrima, anaonesha mapenzi yake kwa yule mfalme na sio kwa lile tufaha, hali ya kujua kwamba katika tufaha lile ambalo limekuwa ni maonesho ya takrima, lina utamu wa juu mno zaidi ya matufaha elfu moja mengine. Hivyo utamu huu wenyewe ni shukrani, na mapenzi haya ni mapenzi yenye heshima na utukuzo unaoendana na hadhi ya mfalme. Vivyo hivyo Mwanaadamu akielekeza mapenzi yake kwenda kwenye neema na matunda hasa, na akastarehe hali ya kughafilika kwa ladha zake za kimaada tu, hayo ni mapenzi ya kinafsi yanarejea kwenye matamanio ya nafsi, na ladha hizo ni zenye kutoweka na kuumiza. Ama mapenzi yakiwa ni kwa upande wa takrima ya kiungu na upande wa mazuri ya huruma zake (s.w), na matunda ya hisani yake, kwa kuthamini viwango vya hisani na upole hali ya kupata utamu wake kwa hamu kamili, hiyo inakuwa ni shukurani ya kimaanawi, na huo ni utamu usiyosababisha maumivu. Nukta ya Tatu: Hakika mapenzi yanayoelekea kwenye majina mazuri yana tabaka kadhaa: Unaweza kuelekeza mapenzi kwa majina mzuri ya Allah (s.w) kwa kupenda athari za kiungu zilizozagaa ulimwenguni – kama tulivyobainisha huko nyuma - na unaweza kuelekeza mapenzi kwa majina mazuri ya Allah (s.w) kwa kuwa ni anuani ya kamilifu za kiungu zilizo tukufu, na Mwanaadamu anaweza kuwa na shauku ya majina mazuri ya Allah (s.w), kwa haja zake kubwa na hii ni kwa wasifu wake jumuishi na mahitajio yake yasiyo na mipaka, yaani anayapenda majina hayo kwa msukumo wa mahitajio yake kwa majina hayo. Tubainishe hayo kwa mfano: Jenga picha hali ya kuwa unaleta hisia ya udhaifu wako na uhitaji wako mkubwa kwa ambaye atakusaidia kuwaokoa wale unaowahurumia katika hali zao miongoni mwa jamaa wa karibu na mafukara na hata viumbe dhaifu wenye haja, tahamaki mmoja wao anatokeza katika medani, na anafanya wema, ufadhili juu yao na kuwaenezea neema zake kwa namna utakavyo, basi ni kiasi gani nafsi yako huwa vizuri na kustarehe kwa jina lake “Al-Mun’im” na “Al-Kariim” na kiasi gani nafsini mwako hufurahika na kukunjuka kutokana na majina haya mawili. Bali ni kiasi gani mtu huyo atapata pendo na thamani kutoka kwako, na kiasi gani unavyomuelekea kwa mapenzi kwa majina na anuani hizo mbili! Kwa mwanga wa mfano huu zingatia majina mawili tu katika majina mazuri. Nayo: Ni “Ar-Rahman” na “Ar-Rahiim” utaona kuwa waumini wote miongoni mwa kinababa na mababu waliopita na wapenzi wote na marafiki, hawa ambao unawapenda na kuwaweka moyoni sana na kuwahurumia, wananeemeshwa duniani kwa aina za neema zenye utamu, kisha watafurahishwa huko Akhera, kwa kupewa neema zenye ladha na kupendeza, bali Mwenyezi Mungu atawazidishia naye ni Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu kuwapa furaha na neema ya kukutana wao kwa wao na kuona uzuri wa kudumu milele huko Akhera... Basi ni kiasi gani yanakuwa majina mawili ya “Ar-Rahman” na “Ar-Rahiim” yenye kustahiki upendo? Na ni kiasi gani roho ya Mwanaadamu inakuwa na shauku kubwa kwa majina hayo? Pima mwenyewe hayo ili uone kiasi cha usahihi wa kauli yetu: ‘Alhamdulillah kwa sifa yake ya wingi wa rehema na kurehemu.’ Kisha hakika wewe unaambatana na viumbe vilivyotawanywa ardhini, na unapata uchungu kwa taabu zake, mpaka inakuwa kana kwamba ardhi yote ni makazi yako mazuri na nyumba yako uliyoizowea; basi kama utachunguza kwa makini utakuta rohoni mwako kuna shauku kubwa na haja kubwa ya jina la “Al-Hakiim” (Mwingi wa hekima) na anuani ya “Al-Murabbi” (Mlezi) kwa ambaye anapangilia viumbe hivi vyote kwa hekima kamili na nidhamu madhubuti na usimamizi wa hali ya juu na malezi yenye huruma. Kisha kama utatazama kwa makini katika jinsi ya wanaadamu wote utajikuta unaambatana nao na kuumia kwa ajili ya hali zao mbaya na unaumia sana kwa kutoweka kwao na kufariki kwao, tahamaki roho yako inapata shauku ya jina la “Al-Waarithu, Al-Baaithu” (Mrithi wa kila kitu na Mwenye kufufua wafu) na unahitajia anuani ya “Al-Baaqy” (Mwenye kubakia daima) “Al-Kariim” (Mkarimu sana), “Al-Muhyi” (Muhuishaji), “Al-Muhsin” (Mwingi wa hisani) ya Muumba Mkarimu sana ambaye anawaokoa kutoka kwenye giza nene la kutokuwepo na kuwapa makazi mazuri na bora zaidi kuliko dunia. Na kama hivi, na kwa kuwa haiba ya mwanaadamu ni ya juu na umbo lake ni jumuishi, hivyo yeye ni muhitaji wa haja elfu moja na moja majina elfu moja na moja katika majina yake Allah (s.w) yaliyo mazuri na nyingi mno ya ngazi za kila jina. Basi haja yenye kuongezeka ni shauku, na shauku yenye kuongezeka ndiyo mahaba, na mahaba yenye kuongezeka ndiyo ashiki. Hivyo kwa mujibu wa ukamilifu wa roho ya mwanaadamu hufunuka ngazi za mahaba kulingana na ngazi za majina. Na mahaba ya majina yote vilevile hugeuka kuwa mahaba ya dhati yake tukufu (s.w) kwani majina hayo ni anuani na udhihirisho wa dhati yake mtukufu na wa sifa za juu. Na sasa tutabainisha kati ya majina elfu moja na moja kati ya majina mazuri, ngazi moja tu na kwa njia ya mfano kati ya ngazi elfu moja na moja, ya jina la “Al-Adli, Al-Hakamu, Al-Haqq, Ar-Rahiim” kwa mfano ufuatao: Ikiwa unataka kushuhudia yaliyo ndani ya hekima na uadilifu kutokana na jina “Ar-Rahmani rrahiim”, Al-Haqq” jumla ya duara pana kubwa basi zingatia mfano huu: Jeshi linalojumuisha vikosi mia nne tofauti katika askari, kila kimoja ni tofauti na kingine katika mavazi yanayowapendeza na kutofautiana katika vyakula wavipendavyo, na kuwa mbali mbali katika silaha wazitumiazo kwa wepesi, na kuwa aina tofauti katika matibabu wayatumiayo... Basi pamoja na kuwa na tofauti hizo na kuhitilafiana katika kila kitu, hakika vikosi hivyo mia nne havitengani katika matapo na makundi makundi, bali yanashikana pamoja pasi na kubaguka. Kama pakiwepo mfalme mmoja anayelipa kila kundi mavazi yanayowiana nalo, na riziki zinazoendana nalo na matibabu yanayonasibiana nalo, na silaha zinazoafikiana nalo, bila ya kusahau yeyote wala kuchanganya, na bila ya kuwa na msaidizi, bali anazigawa zote kwao yeye mwenyewe, kwa sifa anazosifika nazo ikiwemo rehema, upole, uweza, elimu yenye muujiza na kuyazungukia kikamilifu mambo yote pamoja na uadilifu wa hali ya juu na hekima iliyotimia... Naam, ikiwa atakuwepo mfalme kama huyu asiye na kifani, na ukashuhudia kwa nafsi yako kazi zake muujiza dhahiri, wakati huo utaona kiasi cha uweza wake, upole wake na uadilifu wake. Hiyo ni kwa sababu kuandaa kikosi kimoja chenye watu kumi tofauti kwa zana mbali mbali na mavazi anuwai ni jambo gumu sana mpaka inakimbiliwa katika kuandaa jeshi kwa namna maalumu iliyothibiti katika mavazi na zana vyovyote watakavyotofautiana watu na aina zao. Ukitaka - katika mwanga wa mfano huu - kuona udhihirisho wa jina la Allah “Al-Haqq” na “Ar-Rahmani Ar-Rahiim” ndani ya uadilifu na hekima, basi tembeza mtazamo wako kwenye majira ya machipuo katika mahema yale yaliyosimamishwa juu ya busati la ardhi la mataifa mia nne elfu mbali mbali na makundi tofauti ambayo yanawakilisha jeshi la mimea na wanyama. Tazama kwa makini utakuta kwamba mataifa yote hayo na makundi yote hayo, pamoja na kuwa yameingiliana, na mavazi yao ni tofauti, na riziki zao ni tofauti na silaha zao ni anuwai na njia za maisha yao ni tofauti na mazoezi yao ni tofauti na mafunzo yao ni tofauti. Nao hawamiliki ndimi waweze kutafuta uhakika wa haja zao na kujibu matakwa yao... Pamoja na yote haya kila moja kati yao, huongozwa na kulelewa na kuchungwa kwa jina la “Al-Haqq, Ar-Rahman, Ar-Razzaq, Ar-Rahiim na Al-Kariim” pasi na kuchanganya wala kusahau ndani ya hekima na uadilifu kwa mizani makini na mpangilio wa hali ya juu... Basi shuhudia udhihirisho huu na uzingatie; Je inawezekana kuingilia yeyote asiyekuwa Allah katika kazi hii ambayo inaendeshwa kwa mfano wa mpangilio huu wa ajabu na mizani makini? Na je inawezekana kwa sababu yoyote vyovyote iwavyo kunyoosha mkono wake ili kuingilia katika ufundi huu wa kushangaza na uendeshaji wenye busara na ulezi wenye rehema na uongozi wenye kuenea, ila mmoja wa pekee Mwingi wa hekima “Al-Hakiim”, Mweza “Al-Qadir” juu ya kila kitu?. Nukta ya Nne Unasema mimi ninabeba aina mbalimbali ya mahaba ndani ya nafsi yangu, yenye kuambatana na vyakula vitamu; nafsi yangu, mke wangu watoto wangu, wazazi wangu, wapenzi wangu, marafiki zangu, mawalii wema na manabii watukufu, bali mapenzi yangu yanaambatana na kila kilichokuwa kizuri, na kwa majira ya machipuo yenye kupambika maalumu na dunia kwa ujumla. Aina hizi tofauti za mapenzi ikiwa zitakwenda kulingana na vile ambavyo Qur’an tukufu inaamrisha, matokeo yake yatakuwaje na faida zake ni zipi? Jibu: Kubainisha matokeo hayo na kufafanua faida hizo zote, inahitaji utunzi wa kitabu kikubwa katika jambo hili. Kwa hiyo hapa tutaashiria matokeo mamoja au mawili kati yake kwa ujumla. Na kwanza tutabainisha matokeo ambayo yatadhihiri duniani, kisha baada ya hapo matokeo yatakayodhihiri Akhera. Nayo ni kama yafuatayo: Tumekwishataja huko nyuma: Kwamba aina za mahaba ambayo yapo kwa watu wenye kughafilika na watu wa dunia na ambayo hayatokani na chochote ila kwa ajili ya kushibisha raghba za nafsi, zina matokeo machungu na hatima mbaya katika taabu na mashaka, pamoja na yaliyomo katika msisimko mdogo sana na raha ndogo. Mathalan: Huruma hugeuka kuwa ni balaa lenye kuumiza kwa sababu ya kushindwa, na mahaba hugeuka kuwa ni kuunguza kwa hatari kwa sababu ya utengano, na utamu hugeuka kuwa ni kinywaji cha sumu kwa sababu ya kutoweka... Ama Akhera zitabaki bila ya mafanikio wala manufaa, kwa sababu hazikuwa katika njia ya Allah (s.w) au zitakuwa adhabu iumizayo ikiwa zitapelekea katika haramu. Swali: Vipi yanakuwa mapenzi ya manabii watukufu na mawalii wema, bila ya manufaa au faida yoyote? Jibu: Ni kama Wakristo wenye kuitakidi utatu hawanufaiki na mapenzi yao kwa bwana Issa (a.s), na vilevile Ar-Rawafidh na mapenzi yao kwa Sayyidina Ali (r.a)! Ama ulichokieleza katika aina za mahaba, yakiwa kulingana na maelekezo ya Qur’an tukufu na katika njia ya Allah (s.w) na mahaba ya Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu, hakika matokeo mazuri huzaa matunda duniani, ukiongezea na matokeo mazuri ya kudumu milele Akhera. Ama matokeo yake duniani: Hakika kupenda kwako vyakula vitamu na matunda mazuri, hiyo ni neema ya kiungu haichanganyiki na maumivu, na ladha njema ndani ya shukrani yenyewe. Ama kuipenda nafsi yako, yaani kuionea huruma, na kufanya jitihada ya kuilea na kuitakasa na kuizuia na matamanio mabaya, huifanya kuwa ni yenye kukutii, haikuendeshi wala haikufungi na matamanio yake, bali wewe unaiongoza kuelekea kwenye uongofu na sio matamanio ya nafsi. Ama kumpenda mkeo ambaye ni mwenza katika maisha yako, ni kwa sababu yamejengwa juu ya wema wa mwenendo wake na uzuri wa huruma yake, na kuwa kwake ni hiba kutoka katika rehema ya kiungu. Basi utampa mapenzi ya dhati na huruma ya kweli naye kwa upande wake atabadilishana na wewe mapenzi haya pamoja na heshima na unyenyekevu, na hali hii huongezeka kati yenu kila mnapozeeka kiumri. Mtaishi maisha mema ya raha mustarehe kwa idhini ya Allah (s.w). Lakini kama mapenzi hayo yangekuwa yamejengwa juu ya uzuri wa sura ambao unapendwa na nafsi, kwa hakika, haraka sana hunyauka na kufifia, na kuharibu maisha ya ndoa pia. Ama mapenzi yako kwa baba na mama, hiyo ni ibada ambayo unalipwa thawabu maadamu ni katika njia ya Allah (s.w), na hapana shaka kwamba utazidisha mapenzi na heshima kwao wanapofika uzeeni, na utavuna utamu wa kiroho iliyo safi na raha ya kimoyo timamu katika kuwadumia, kuibusu mikono yao na kuwatukuza kwa dhati. Na hivyo kuelekea kwa Mola Mweza hali ya kuwa unahisi hisia hii ya juu na hima ya kweli, kwamba umri wao urefuke ili upate ziada ya thawabu... Lakini mapenzi hayo na heshima hiyo yakiwa ni kwa ajili ya kuchuma makapi ya dunia, na yanatokana na matamanio ya nafsi, hakika huzaa maumivu ya kiroho totoro yanayotokana na hisia duni iliyoporomoka na hisia ya chini sana, nayo ni kuwakimbia hao watukuzwa wawili ambao walikuwa ni sababu ya uhai wako wewe na kuwaona wazito hali ya kuwa wamefikia uzee na kuwa ni mzigo kwako, kisha la kutisha mno kuliko hilo ni kutamani wafe, na kungojea kutoweka kwao! Ama mapenzi yako kwa watoto wako, yaani kuwapenda kwako wale ambao Allah (s.w) amekupa amana, usimamie malezi yao, na kuwachunga. Basi mapenzi ya hao waliwazaji wapendwa katika viumbe wa Allah (s.w) hakika ni mapenzi yaliyovikwa taji la furaha na sherehe, na ni neema ya kiungu wakati huo huo. Basi ukilihisi hili, isikufunike huzuni juu ya msiba wao wala usipige kelele kwa majonzi juu ya kufa kwao. Kwani - kama tulivyoeleza - hakika Muumba wao ni Mwingi wa rehema kwao, Mwingi wa hekima katika kuendesha mambo yao, na hapo utasema, hakika umauti katika haki ya watu hawa, ni furaha kwao. Kwa jambo hili basi utaokoka kutokana na machungu ya utengano na utatafakari kumiminiwa juu yako rehema zake (s.w) Ama kuwapenda kwako marafiki na ndugu ni kwa ajili ya Allah (s.w), basi kutengana nao wala umauti wao havizuii kudumu kwa undugu wenu, mapenzi yenu, na kuliwazana kwenu; kwa sababu hudumu mafungamano hayo ya kiroho na mapenzi ya kimaanawi ya dhati, kwa duru yake basi hudumu pia ladha ya kukutana na utamu wa kuungana. Lakini mapenzi hayo yasipokuwa kwa ajili yake (s.w) wala katika njia yake, hakika ladha ya kukutana siku moja hurithisha maumivu ya kutengana kwa siku mia moja. Ama kuwapenda kwako Manabii (a.s) na mawalii wema, hakika ulimwengu wa Barzakh ambao ni ulimwengu wa giza unatisha katika mtazamo wa watu wa upotevu na kughafilika, utaona kuwa ni nyumba za nuru zilizonawirishwa na hao wenye nuru, na wakati huo hautaogopa kukutana nao, wala huhofii ulimwengu wa Barzakh, bali utakuwa na shauku nao, na kuupenda bila ya hilo kutibua kustarehe kwako na maisha ya dunia. Lakini mapenzi yao yakiwa yanashabihiana na yale ya watu wa ustaarabu ya kuwapenda watu mashuhuri wa ubinaadamu, basi kule kutafakari tu kuhusu kutoweka kwa mawalii hao wakamilifu, na kuoza mifupa yao katika makaburi ya zamani makubwa, huzidisha maumivu juu ya maumivu ya maisha, na humsukuma mtu kupata picha ya kufa kwake na kutoweka kwake ambapo atasema: Siku moja nitaingia katika makaburi haya ambayo huozesha mifupa ya wakubwa! Atasema hayo kwa machungu yote na majuto yote na hofu... Wakati ambapo katika mtazamo wa awali anawaona wanaishi kwa raha na starehe katika ulimwengu wa Barzakh ambao ni ukumbi wa mustakabali na baraza zake, baada ya kuwa wameacha mavazi yao ya kimwili katika zama zilizopita... Na anatazama makaburi kwa mtazamo wa shauku na maliwazo. Kisha mapenzi yako kwa vitu vizuri na mambo mazuri yakiwa ni mahaba katika njia ya Allah (s.w) na katika njia ya kumjua mtengezaji wake mtukufu, kiasi inakufanya useme: Uzuri ulioje wa uumbaji wake!.. Mapenzi haya yenyewe kwa dhati yake ni tafakuri yenye utamu na burudani, ukiongezea ya kuwa inafungua njia mbele ya vionjo vya kupenda uzuri na shauku ya uzuri ili kuchungulia ngazi za vionjo vya juu zaidi na kuonesha kuwa kuna hazina za thamani basi huisubiria mja kwa msisimko wa hali ya juu; kwa sababu mahaba haya hufungua anga mbele ya moyo ili kugeuza mtazamo wake kutoka athari za fundi mtukufu kuelekea uzuri wa matendo yake ya ajabu, na kutoka uzuri wa matendo kuelekea katika uzuri wa majina yake mazuri, na kutoka katika majina yake mazuri kwenda katika uzuri wa sifa zake tukufu, na kutoka katika uzuri wa sifa zake tukufu kuelekea katika uzuri wa dhati yake takatifu... Basi mahaba haya na kwa njia hii hakika ni ibada tamu na tafakuri ya juu ya kuburudisha wakati huo huo. Ama kupenda kwako ujana, ni kwa sababu ulipenda enzi za ujana wako kwa kuwa kwake ni neema nzuri ya Allah (s.w), bila shaka utautumia katika kumuabudu yeye (s.w) wala hutouua kwa kuzama kwenye upumbavu na kudondokea katika upotevu; kwani ibada ambazo unazivuna wakati wa ujana hakika ni matunda yenye kustawi ya kubaki milele yamezalishwa na enzi hizo zenye kutoweka. Basi kila unapovuka enzi hiyo na kuongezeka katika umri unapata ziada ya matunda yake ya kudumu, na unaokoka kidogo kidogo kutokana na maafa ya nafsi yenye kuamrisha maovu na maovu ya babaiko la ujana. Basi unataraji kutoka kwa Mola Mweza akuwafikishe kuvuna ziada ya ibada uzeeni, ili uwe mwenye kustahiki rehema zake kunjufu. Na kuendeleza nafsi yako na kuepuka kuwa miongoni mwa mfano wa wenye kughafilika ambao wanatumia miaka hamsini katika umri wa uzee wao na ukongwe wao kwa masikitiko na majuto kwa walichokikosa katika starehe za ujana ndani ya miaka mitano au kumi. Hata mmoja wa washairi akaeleza kuhusu majuto na masikitiko hayo kwa kauli yake: لَي۟تَ الشَّبَابَ يَعُودُ يَو۟مًا فَاُخ۟بِرَهُ بِمَا فَعَلَ ال۟مَشٖيبُ Laiti ujana ungerudi siku moja, Nikaueleza kile kilichofanywa na uzee. Ama mapenzi yako kwa mandhari za kupendeza na hasa mandhari za majira ya machipuo, na kwa kuwa ni kushuhudia maajabu ya ufundi wa Allah (s.w) na kuutazama, basi kuondoka kwa majira hayo ya machipuo hakuondoshi utamu wa kushuhudia na starehe ya kutazama, kwani huacha maana yake nzuri nyuma yake, kwa kuwa majira ya machipuo yanafanana sana na ilivyo na risala ya kiungu yenye kupendeza inayofunguliwa kwa ajili ya viumbe. Taswira yako na muda ni vyenye kufanana na mkanda wa sinema vinakudumishia utamu wa kushuhudia huku, na daima vinafanya upya maana zake zinazobeba ujumbe wa majira ya machipuo. Hivyo mapenzi yako kwa hiyo hayawi ya muda mfupi wala kufunikwa na masikitiko na majonzi, bali ni safi, yametakata, matamu na yenye kuleta raha. Ama kupenda kwako dunia, ni kwa kuwa ni mapenzi kwa ajili ya Allah (s.w), hakika vilivyomo ndani yake vyenye kusisimua, kuamsha hofu, na mshangao hugeuka kuwa ni marafiki zako waliwazaji, na kwa kuwa unavielekea kwa mahaba kwa kuwa kwake ni shamba la Akhera, unaweza kuvuna kutokana na kila kitu ndani yake kinachoweza kuwa ni tunda katika matunda ya Akhera, au utavuna kutokana nayo kinachoweza kuwa ni rasilimali ya Akhera. Hivyo misiba yake haikuhofishi na kutoweka kwake na kwisha kwake hakukupi taabu. Na namna hii utatumia muda wa kuishi kwako humo hali ya kuwa wewe ni mgeni mheshimiwa... Lakini kama mapenzi yako kwa dunia ni sawa na yale ya watu wa mghafala, tumekwisha kukuambia mara kwa mara: Utaizamisha nafsi yako na kuiteketeza kwa mapenzi yenye kusaga, kukaba, yenye kutoweka hakuna faida wala manufaa yanayobakia nyuma yake.! Na kwa namna hii, hakika tumejitahidi kuonesha jambo jema moja kati ya mamia ya mema yanayorejea kwa yote uliyoyaeleza. Pale ambapo mapenzi yako kwake ni kwa mujibu wa maelekezo ya Qur’an tukufu, na katika wakati huo huo tumeashiria mojawapo kati ya mamia ya madhara ya mapenzi hayo kama hayakuwa kwa mujibu wa namna Qur’an tukufu inavyoamuru. Ukiwa unataka kudiriki matokeo ya aina hizi tofauti za mahaba katika mji wa kudumu na ulimwengu wa Akhera, kama namna ambavyo aya za waziwazi za Qur’an zimeashiria, tutakubainishia ubainifu wa jumla faida moja ya Akhera katika faida za hizo aina za kihalali miongoni mwa mapenzi, na hii ni katika ishara tisa, baada ya kutanguliza utangulizi kabla yake. Utangulizi Hakika Allah (s.w) - kwa Uungu wake mtukufu, na rehema yake nzuri na ulezi wake mkubwa, na upole wake mwema, na uweza wake mkuu, na hekima yake njema, - amempamba mtu huyu mdogo kwa milango ya fahamu na hisia nyingi sana, na kumfanya kuwa mzuri kwa viungo na mifumo mingi ya viungo mbalimbali; ili amjulishe tabaka za rehema yake yenye kuenea na amuonjeshe aina za neema zake zisizohesabika, na amtambulishe vigawanyo vya hisani zake visivyodhibitika kwa hesabu, na amuoneshe kupitia mifumo na viungo hivyo vingi juu ya aina za madhihirisho yake yasiyo na mpaka ya majina elfu moja na moja katika majina yake mazuri, na kuyapendezesha kwake, na kumfanya ayape hadhi yake vyema vilivyo. Basi kila kiungo miongoni mwa viungo hivyo vingi, na kila mfumo na zana miongoni mwake, kina kazi zake anuwai na ibada zake tofauti kama ilivyo ladha zake mbalimbali na maumivu yake ni tofauti na thawabu zake ni zenye kupambanuka. Basi mathalani: Jicho hushuhudia uzuri katika picha, na linaona miujiza ya kudura ya kiungu iliyo nzuri katika ulimwengu wa kuonekana hivyo hutimiza kazi yake kwa kuleta shukrani kwa Allah (s.w) kupitia mtazamo wake wenye mazingatio. Na haifichikani kwa yeyote kiasi cha yaliyomo katika mtazamo huu katika utamu, na maumivu yapatikanayo kutokana na kutoweka kwake. Kwa hivyo hakuna haja ya utambulisho wa ladha ya kuona na maumivu ya kukosa kuona… Na mathalani: Sikio huhisi uzuri wa rehema ya kiungu inayoenda katika ulimwengu wa vyenye kusikilizwa, kwa kusikia kwake aina za sauti na viimbo vyake vizuri tofauti. Basi lina ibada maalumu kwake, na ladha inayoihusu, na thawabu inayorejea kwake. Mathalani: Hisia ya kunusa ambayo unahisi rehema ya kiungu yenye kunukia vyema kutokana na kunukia kwa aina za uturi na manukato, hakika ina ladha yake maalumu miongoni mwa kutekeleza kwake shukrani yake maalumu na hapana shaka kwamba ina thawabu maalumu kwake... Na mathalani: Hisia ya kuonja ambayo imo kinywani, inatimiza kazi yake na inaleta shukrani yake ya kimaanawi kwa mitindo mbalimbali kupitia utambuzi wake vionjo vya aina za vyakula na ladha zake. Na kama hivi, kila kiungo katika viungo vya mwanaadamu na kila kiungo cha hisia, na kila kilicho laini katika laini zake muhimu - kama moyo, roho, akili n.k. - kina kazi zake mbalimbali, na ladha zake anuwai zilizo mahususi kwake. Basi katika yasiyo na shaka ndani yake kwamba Muumba Mwingi wa hekima ambaye amevifanya viungo hivi vitii kwa kazi hizo atalipa kwa kila mojawapo kwa namna inayoafiki na kustahiki katika malipo. Hakika matokeo ya haraka ya aina nyingi ya mapenzi - yaliyotajwa hapo nyuma - kila mwanaadamu anahisi kwayo hisia ya ndani na kuthibitisha hisia yake hii na kuwa na yakini nayo kwa dhana ya kweli. Ama matokeo yake ya Akhera yamethibitishwa na hakika kumi na mbili katika hakika zenye kung’ara za Neno la Kumi na misingi sita maridhawa ya Neno la Ishirini na Tisa. Ama upambanuzi wake umethibiti kwa hakika kwa Qur’an tukufu ambayo ni maneno ya kweli zaidi na nidhamu fasaha zaidi nayo ni maneno ya Allah Mfalme, Mwenye enzi na Mjuzi wa kila kitu, katika kueleza aya zake za bayana na katika ishara zake na alama zake... Kwa hiyo hatuoni haja ya kuleta hoja ndefu katika jambo hili, kwa kujua kwamba tumehudhurisha hoja nyingi sana katika “Maneno” mengine na katika kituo cha pili cha Kiarabu cha “Neno la Ishirini na Nane” linalohusu pepo na katika “Neno la Ishirini na Tisa”. Ishara ya Kwanza: Hakika matokeo ya Akhera ya mapenzi yaliyo halali yaliyotunukiwa taji la shukrani kwa Allah (s.w), kama vile kwa vyakula vitamu na matunda mazuri duniani, ni vile vyakula na matunda mazuri vinavyoafikiana na pepo ya kudumu... kama inavyoeleza hilo Qur’an tukufu. Mapenzi haya, ni mapenzi yenye shauku na kutamani pepo hiyo na matunda yake. Hadi hakika ya tunda unalokula duniani na kulitamkia "الحَمْدُ للهِ"litafanyika mwili peponi kuwa tunda lake maalumu na wewe utapewa miongoni mwa mazuri ya pepo. Hapa wewe unakula tunda, na huko "الحَمْدُ للهِ" ikiwa imeundika mwili kuwa tunda katika matunda ya peponi... Na kwa kuwa wewe unaleta shukrani ya kimaanawi iliyo tamu kwa kuona kwako neema za kiungu na mgeuko wa kiungu katika vyakula na matunda ambayo unayala hapa, basi huko peponi utapewa zikiwa ni vyakula vitamu na matunda mazuri, kama ilivyothibiti katika hadithi tukufu na kwa ishara za Qur’an tukufu. Na kwa muktadha wa hekima ya kiungu na rehema yake enevu. Ishara ya Pili: Hakika ya matokeo ya mapenzi halali kwa nafsi, yaani mapenzi yake yaliyojengwa duniani kwa kuona mapungufu yake kinyume cha mazuri yake, na kujaribu kuyakamilisha, kuyatakasa, kuyachunga kwa huruma na upole na kuyasukuma katika njia ya kheri, ni kipawa cha Muumba (s.w) kwa wapendwa wenye kulingana nayo na pepo. Basi nafsi iliyoacha duniani matamanio yake na ikaacha raghba zake katika njia ya Allah (s.w), na kutumia yaliyo ndani yake miongoni mwa zana anuwai kwa njia bora zaidi na timamu zaidi, Muumba mtukufu (s.w) ataitunuku malipo kwa ajili ya mapenzi haya ya halali yaliyovikwa taji la uja kwa Allah (s.w), mahurul’aini wenye kujipamba kwa mapambo sabini katika mapambo ya peponi mbalimbali kwa aina ya mazuri yake na mapambo yake, na waliojiremba kwa aina sabini za uzuri na urembo, hadi wanakuwa kana kwamba ni pepo ndogo iliyoundika inayotweta kwa roho na uhai, ili jicho la nafsi ile iliyomtii Allah (s.w) litue na hisia zilizotulia katika amri za Allah (s.w) zipate kutulia... Matokeo hayo hakuna shaka ndani yake kwani aya tukufu zinasema wazi hivyo kwa yakini. Kisha matokeo ya mapenzi yenye kuuelekea ujana duniani yaani kutumia nguvu ya ujana na umaridadi wake katika ibada na ucha Mungu, ni ujana wa kudumu milele katika mji wa kubakia na neema za kudumu. Ishara ya Tatu: Ama matokeo ya Akhera kwa mapenzi ya mke yaliyo asisiwa juu ya uzuri wa mwenendo wake na uzuri wa tabia yake na ulaini wa huruma zake, na ambayo yanamlinda na kuasi na kumuepusha na makosa na madhambi, ni kumfanya mke huyo mwema ni mwenye kupendwa na mpenzi na rafiki mkweli na mwenza mliwazaji peponi. Uzuri wake unang’ara mno kuliko hurul’aini, mapambo yake yanavutia kuliko mapambo yao, uzuri wake unavuka uzuri wao... Anabadilishana mazungumzo na mumewe, wanakumbushana matukio ya siku zilizopita... Na hivi ndivyo ameahidi Mwingi wa rehema Mkarimu sana. Kwa kuwa ameahidi basi kwa hakika atatimiza ahadi yake. Ishara ya Nne: Ama matokeo ya kuwapenda wazazi wawili na watoto ni kuwa Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu (s.w), anatenda wema kwa familia hiyo njema yenye bahati, licha ya kutofautiana ngazi zao huko peponi kwa kukutana wao kwa wao, kuchanganyikana, kukaa pamoja, na kuongea pamoja kati yao kwa hali ambayo inakubaliana na pepo na maisha ya kudumu milele, kama jambo hili lilivyothibiti katika Qur’an tukufu. Na wazazi hao wataneemeshwa kwa kucheza na watoto wao ambao wamefariki duniani kabla ya umri wa kubaleghe, na kuwafanya kwa ajili yao kuwa ni watoto “Wildanun mukhalladina”, katika hali ya upole zaidi na inayopendeza zaidi nafsini mwao, na kwa hivi hutuliza raghba ya kucheza na watoto katika maumbile ya mwanaadamu, na wastarehe kwa starehe ya kudumu na kionjo cha kudumu huko peponi, ambapo wamewekewa wana wao wadogo milele - ambao hawajafikia umri wa kukalifishwa. Na ilikuwa ikidhaniwa kwamba peponi hakuna kucheza na watoto, kwa sababu si mahali pa kuzaana, lakini pepo kwa kuwa inakusanya ladha bora zaidi na uzuri zaidi kuliko za dunia, basi kucheza na watoto hapana budi kuwa hilo lipo huko kwa sura zake zilizo bora na maumbo yake mazuri zaidi. Basi furaha iliyoje ya hao wazazi ambao wamewapoteza watoto wao katika maisha ya duniani! Ishara ya Tano: Hakika ya matokeo ya mapenzi yako kwa ajili ya marafiki na jamaa wa karibu ambayo yanahitajia (mapenzi kwa ajili ya Allah), hakika hiyo ni katika kukaa kwenu kwenye makochi yenye kuelekeana na kuliwazana kwenu kwa kumbukumbu nzuri, kumbukumbu za masiku ya duniani na matukio yake mazuri, na kuishi wakati wa raha na mzuri kwa mazungumzo haya na kukaa pamoja, kama hili lilivyothibiti kwa maelezo ya Qur’an tukufu. Ishara ya Sita: Ama matokeo ya kuwapenda mitume na mawalii wema – amani iwe juu yao - kulingana na Qur’an tukufu ilivyobainisha, ni kuvuna uombezi wa hao manabii wema na mawalii wema katika ulimwengu wa Barzakh, na katika mkusanyiko mkubwa, ukiongezea na kutafuta kumiminiwa – kwa mapenzi hayo –mimiminiko ya makamo yao ya juu, na ngazi zao zilizonyanyuka zinazolingana nao. Naam, hakika ya hadithi tukufu inaeleza kuwa “Mtu yu pamoja na yule ampendaye”. Kwa hiyo mwanaadamu anaweza kupanda makamo ya juu na yaliyonyanyuka zaidi, kwa vile alivyofungamana na sahibu yake katika mapenzi na kwa kunasibiana naye na kumfuata. Ishara ya Saba: Hakika kupenda kwako vitu vizuri, na majira ya machipuo, yaani kuyatazama katika pembe ya kauli yako: “Uzuri uliyoje wa umbo lake!” Na kuelekeza mapenzi yako nyuma ya kitu hicho kizuri katika uzuri wa matendo na mpangilio wake, na yaliyo nyuma ya matendo hayo yaliyoratibika katika uzuri wa madhihirisho ya majina mazuri, na yaliyo nyuma ya majina hayo mazuri katika madhihirisho ya sifa tukufu... Na namna kama hii... Hakika matokeo ya mapenzi haya ya halali ni kushuhudia uzuri mkuu kuliko uzuri huo ambao umeushuhudia katika vilivyotengenezwa kwa maelfu na maelfu ya mara. Yaani kushuhudia madhihirisho ya majina mazuri na uzuri wa sifa tukufu kwa namna inayoendana na pepo na maisha ya kudumu milele. Mpaka Imamu Ar-Rabbani As-Sirhandi (r.a) akasema: “Hakika mazuri ya peponi ni mifano ya majina mazuri” Basi zingatia!. Ishara ya Nane: Ama kuipenda kwako dunia mapenzi ya halali, yaani kuipenda kwako pamoja na kuzingatia na kutafakari katika sura zake mbili nzuri ambazo ni shamba la Akhera, na kioo cha madhihirisho ya majina mazuri ya Allah (s.w), hakika matokeo yake ya Akhera ni kuwa utapewa pepo inayotosha dunia yote, lakini haiondoki kama hiyo dunia bali ni yenye kudumu milele. Na itadhihirishwa kwako katika vioo vya pepo hiyo, madhihirisho ya majina mazuri kwa mng’aro mkubwa mno wa memetuko lake na utukufu wake, ambazo umeona baadhi ya vivuli vyake dhaifu duniani. Kisha kuipenda dunia katika sura yake ambayo ni shamba la Akhera, yaani kuzingatia kuwa dunia ni bustani ndogo sana ya kuotesha mbegu ili ifanye mashuke Akhera na izae matunda huko, hakika matokeo yake ni matunda ya pepo pana inayotosha dunia yote. Hufunuka humo milango yote ya fahamu na hisia za kibinaadamu anazobeba mwanaadamu duniani kama vijimbegu vidogo, kwa mfunuko timilifu na ukuaji kamili na vijimbegu vya maandalizi ya kimaumbile hufanya mashuke ndani yake vikibeba aina zote za ladha na makamilifu... Matokeo haya ni thabiti kwa muktadha wa rehema ya Allah iliyoenea na hekima yake isiyo na ukomo. Na matokeo hayo pia ni thabiti kwa kauli ya hadithi tukufu na ishara za Qur’an tukufu. Na kwa kuwa kuipenda kwako dunia sio kwa sura ile mbaya ambayo ndio kichwa cha kila kosa, bali ni mapenzi yenye kuelekea katika sura zake mbili, yaani katika majina mazuri na Akhera, na umekwishafunga kwa ajili ya mawili hayo mafungamano ya mapenzi pamoja nayo na ukaimarisha sura hizo mbili kwa nia ya ibada, hadi kana kwamba umetekeleza ibada kwa dunia yako yote... Basi hapana budi kwamba thawabu zipatikanazo kutokana na kupenda huku zitakuwa ni thawabu kunjufu mno kuliko dunia yote. Na huu ndio muktadha wa rehema ya kiungu na hekima yake. Kisha kwa kuwa mapenzi hayo yamepatikana kwa kuipenda Akhera na kuwa kwake ni shamba lake, na kwa kumpenda Allah (s.w), na kuwa kwake ni kioo cha kudhihirisha majina yake mazuri... hapana shaka kwamba hukabiliwa na kipendwa chenye upana zaidi kuliko dunia yote nacho sio kingine isipokuwa ni pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi. Swali: Nini faida ya pepo yenye upana sawa na dunia? Jibu: Ingekuwa yawezekana ukatembea kwa kasi ya kufikiria katika pande zote za dunia, na ukazuru nyota karibu zote zilizomo mbinguni, ungesema wakati huo: Hakika ulimwengu wote ni wangu. Uwepo wa malaika, watu wengine na wanyama pamoja nawe hausongamani na hukumu yako hii wala haukanushi katika ulimwengu huu mpana. Na vilevile unaweza kusema: Hakika pepo hiyo ni yangu Na tumebainisha katika risala ya “Pepo” - nayo ni “Neno la Ishirini na Nane” - maana ya hadithi iliyopatikana kuwa watapewa baadhi ya watu wa peponi pepo ambayo upana wake ni miaka mia tano, na tumeshabainisha haya katika risala ya “Ikhlasi”. Ishara ya Tisa Hakika matokeo ya kumuamini Allah (s.w) na kumpenda (s.w) ni kuona uzuri mtakatifu na ukamilifu mtakasifu wa dhati tukufu ya (s.w), kama ilivyothibiti kwa hadithi sahihi na Qur’an tukufu. Kuona huku ambako saa yake moja ni sawa na miaka elfu elfu ya neema za peponi, neema hiyo ambayo saa yake moja inavuka miaka elfu elfu ya maisha mazuri ya duniani, kama ilivyothibiti mbele ya wasomi na wenye kufunuliwa kwa kuafikiana. Na tunaweza kupima kiasi cha shauku na kutamani yanayo kuwamo kwenye maumbile ya mwanaadamu ili kuona uzuri huo mtakatifu na ukamilifu mtakasifu, na kiasi cha yaliyomo katika raghba kali na matamanio makali na kuvutiwa ili kuviona kwa mfano ufuatao: Kila mtu anahisi ndani mwake uhitaji mkubwa wa kumuona Sayyidina Suleiman (a.s) ambaye amepewa ukamilifu, na vilevile anahisi shauku kubwa katika kumuona Sayyidina Yusuf (a.s) ambaye amepewa nusu ya uzuri. Basi ni kiasi gani cha shauku na uhitaji kwa mwanaadamu ili kuona uzuri mtakatifu na ukamilifu uliotakasika kutokana na kasoro zote, ambao katika madhihirisho ya uzuri huo na ukamilifu ni pepo ya kudumu kwa mazuri yake yote na neema na makamilifu yake yote ambayo yanavuka kwa kiasi cha mara kisicho na mpaka mazuri yote ya dunia na makamilifu yake. اَللّٰهُمَّ ار۟زُق۟نَا فِى الدُّن۟يَا حُبَّكَ وَ حُبَّ مَا يُقَرِّبُنَا اِلَي۟كَ وَ ال۟اِس۟تِقَامَةَ كَمَا اَمَر۟تَ وَ فِى ال۟اٰخِرَةِ رَح۟مَتَكَ وَ رُؤ۟يَتَكَ سُب۟حَانَكَ لَا عِل۟مَ لَنَٓا اِلَّا مَا عَلَّم۟تَنَٓا اِنَّكَ اَن۟تَ ال۟عَلٖيمُ ال۟حَكٖيمُ اَللّٰهُمَّ صَلِّ وَ سَلِّم۟ عَلٰى مَن۟ اَر۟سَل۟تَهُ رَح۟مَةً لِل۟عَالَمٖينَ وَ عَلٰى اٰلِهٖ وَ صَح۟بِهٖ اَج۟مَعٖينَ اٰمٖينَ Tenbih Şu sözün âhirinde uzun tafsilatı uzun görme; ehemmiyetine nisbeten kısadır, daha uzun ister. Bütün Sözlerde konuşan ben değilim. Belki işarat-ı Kur’aniye namına hakikattir. Hakikat ise hak söyler, doğru konuşur. Eğer yanlış bir şey gördünüz, muhakkak biliniz ki haberim olmadan fikrim karışmış, karıştırmış, yanlış etmiş.

Private reading note

This note stays on this device and is never uploaded to a server.

Up to 1,200 characters