Miiraji Ya Mtume (s.a.w) Tanbihi Hakika masuala ya Miiraji ni matokeo yanayokuja juu ya misingi ya imani na nguzo zake. Ni nuru inayochukua mwanga wake kutoka katika nuru za nguzo za kiimani. Hazisimamishwi hoja juu ya kuthibitisha Miiraji yenyewe hasa kwa makafiri wapingaji wa nguzo za Imani, bali haitajwi asilani kwa asiye amini Allah (s.w), wala hamsadiki mtume (s.a.w) au anakanusha malaika na mbingu, ila baada ya kutangulia kuwathibitishia nguzo hizo. Kwa hivyo muumini ambaye zinamtembelea shaka na dhana na kuiweka mbali Miiraji (kuona haiwezekani), tutamfanya kuwa shabaha ya mazungumzo yetu, tutambainishia yanayomfidisha na kumtosheleza Biidhinillah. Lakini tunamuona nyakati nyingine huyo kafiri ambaye anavizia katika nafasi ya usikilizaji hivyo tutamwelezea pia maneno yanayomfaidisha. Hakika imetajwa ming’ao ya hakika ya Miiraji katika risala nyingine, tukaomba msaada kutoka kwa Allah (s.w) – pamoja na kushikilia kwa ndugu zangu wapendwa – kukusanya ming’ao hiyo iliyotawanyika, na kuifungamanisha na asili ya hakika yenyewe ili kuifanya ni kioo kinachoakisi mkupuo mmoja makamilifu ya uzuri wa mtume (s.a.w). بِسْمِ اللّٰهِ الرَّحْمٰنِ الرَّحِيمِ سُب۟حَانَ الَّذٖٓى اَس۟رٰى بِعَب۟دِهٖ لَي۟لًا مِنَ ال۟مَس۟جِدِ ال۟حَرَامِ اِلَى ال۟مَس۟جِدِ ال۟اَق۟صَى الَّذٖى بَارَك۟نَا حَو۟لَهُ لِنُرِيَهُ مِن۟ اٰيَاتِنَا اِنَّهُ هُوَ السَّمٖيعُ ال۟بَصٖيرُ اِن۟ هُوَ اِلَّا وَح۟ىٌ يُوحٰى عَلَّمَهُ شَدٖيدُ ال۟قُوٰى ذُو مِرَّةٍ فَاس۟تَوٰى وَ هُوَ بِال۟اُفُقِ ال۟اَع۟لٰى ثُمَّ دَنَا فَتَدَلّٰى فَكَانَ قَابَ قَو۟سَي۟نِ اَو۟ اَد۟نٰى فَاَو۟حٰٓى اِلٰى عَب۟دِهٖ مَٓا اَو۟حٰى مَا كَذَبَ ال۟فُؤَادُ مَا رَاٰى اَفَتُمَارُونَهُ عَلٰى مَا يَرٰى وَلَقَد۟ رَاٰهُ نَز۟لَةً اُخ۟رٰى عِن۟دَ سِد۟رَةِ ال۟مُن۟تَهٰى عِن۟دَهَا جَنَّةُ ال۟مَا۟وٰى اِذ۟ يَغ۟شَى السِّد۟رَةَ مَا يَغ۟شٰى مَا زَاغَ ال۟بَصَرُ وَمَا طَغٰى لَقَد۟ رَاٰى مِن۟ اٰيَاتِ رَبِّهِ ال۟كُب۟رٰى Tunataja alama mbili tu, kutoka katika hazina kubwa kutoka katika aya tukufu iliyotangulia, nazo ni alama mbili zinazoegemea katika kanuni ya kibalagha kwenye dhamiri (Hakika yeye) na hii ni kwa uhusiano wake na suala letu hili, kama tulivyobainisha katika Risala ya (Al-Muujizat al-Qur’aniyyah). Hakika Qur’an tukufu inahitimisha aya iliyotajwa hapo juu kwa: إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ البَصِيرُ hiyo ni baada ya kutaja kwa Israa ya Mtume Mpendwa (s.a.w), kutokea mwanzo wa Miiraji, yaani kutoka msikiti Mtukufu wa Makka hadi msikiti wa Aqsaa, na ukomo wake ambao surat An-Najm inauashiria. Basi dhamiri katika (Hakika yeye) ima irejee kwa Allah (s.w), au kwa Mtume mtukufu (s.a.w). Ikiwa inarejea kwa Mtume (s.a.w), hakika kanuni za balagha na uwiano wa urari wa maneno vinafaidisha kuwa hakika ya matembezi haya ya kisehemu (kiasi kidogo) ndani yake kuna mwendo wa kiujumla na kupanda kiujumla kwa namna ambayo mtume (s.a.w) amesikia na kushuhudia kila alichokutana nacho kwa macho yake na masikio yake katika Ishara za kiungu, na maajabu ya ufundi wa kiungu wakati wa kupanda kwake katika ngazi za kiujumla za majina ya kiungu yaliyo mazuri zifikazo hadi kwenye Mkunazi wa ukomo. Hadi alikuwa ukaribu wa pinde mbili au karibu zaidi, katika yanayojulisha kwamba matembezi haya ya kisehemu yamo katika hukumu ya Ufunguo wa matembezi ya kiujumla yenye kukusanya maajabu ya ufundi wa kiungu. Na ikiwa dhamiri inarejea kwa Allah (s.w), wakati huo maana inakuwa: Hakika yeye (s.w), alimwita mja wake kuhudhuria na kuwepo mbele zake ili amkabidhi jukumu na kumkalifisha kazi, kwa hivyo akampeleka kutoka msikiti mtukufu wa Makka hadi msikiti wa Aqsaa, ambao ni makutano ya manabii. Na baada ya kukutana nao na kumdhihirisha kwamba yeye ndiye mrithi kwa hali zote wa misingi ya Dini za manabii wote. Alimpeleka katika matembezi ndani ya ufalme wake na utalii ndani ya maeneo mengi ya ufalme wake, hadi kumfikisha katika Mkunazi wa ukomo akawa ukaribu wa pinde mbili au karibu zaidi. Na kama hivyo, utalii au mwendo huo, ingawa ni Miiraji ya kisehemu, na kwamba aliyepelekwa Miiraji ni mja, isipokuwa mja huyu anabeba amana kubwa inayoambatana na viumbe wote, na ana nuru pamoja ya dhahiri inaangaza viumbe, na anabadilisha maana ya mandhari yake na kupamba kwa pambo lake, ukiachilia mbali kwamba anao ufunguo anaweza kufungulia mlango wa furaha ya milele na neema za kudumu. Kwa ajili ya yote haya, Allah (s.w) anasifu nafsi yake: إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ البَصِير ili aonyeshe kwamba katika amana hiyo na katika nuru hiyo na katika ufunguo huo, kuna hekima tukufu zinazojumuisha viumbe wote na kuzunguka ulimwengu wote. Na siri hii ina misingi minne: Kwanza: Nini siri ya ulazima wa Miiraji? Pili: Nini hakika ya Miiraji? Tatu: Nini hekima ya Miiraji? Nne: Nini matunda na faida za Miiraji?
Source text is preserved. When a suitable model is available, translation is displayed separately.
Sözler
The Thirty-First Word
Siri na hekima ya ulazima wa Miiraji Kwa mfano husemwa: Hakika ya Allah (s.w) naye ametakasika na mwili mahali na yuko karibu zaidi ya kila kitu kuliko kila kitu kama aya tukufu inavyoeleza: وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْ حَبْلِ الْوَرِيدِ Hata kila walii katika mawalii wema wa Allah anaweza kukutana na mola wake mlezi na kuongea naye moyoni mwake. Kwa nini kila walii anawafikishwa kuongea na Allah (s.w) ndani ya moyo wake, wakati ambapo uwalii wa Muhammad unawafikishwa kuongea naye baada ya mwendo mrefu na matembezi marefu kwa Miiraji?. Jibu: Tunaisogeza siri hii iliyojifumba katika ufahamu kwa kutaja mifano miwili, isikilize, na mifano hiyo imetajwa katika (Neno la kumi na mbili) katika kutaja siri ya muujiza wa Qur’an na hekima ya Miiraji. Mfano wa kwanza: Hakika ya mfalme ana aina mbili za mazungumzo na kukutana, na sampuli mbili za kuongea, takrima na kuonesha umuhimu. Kwanza: Mazungumzo maalum kupitia simu maalum, na mmoja wa raia wake katika watu wa kawaida, katika jambo dogo linalohusu haja mahususi kwake. Na nyingine: Mazungumzo kwa niaba ya ufalme mkuu na kwa anuani ya Ukhalifa mkuu, na kwa sifa ya utawala ya jumla, kwa jambo la hadhi ya juu tukufu anadhihirisha adhama yake na kubainisha heshima yake, inakusudiwa kwa mazungumzo hayo kueneza amri zake za kifalme katika pande mbali mbali. Ni mazungumzo yanapita pamoja na mmoja wa wajumbe wake katika ambao amri hizo zinawahusu, au pamoja na mmoja wa wakubwa wa maafisa wake katika ambao amri hizo zinawahusu. Na kama hivi, kwa mfano kama huu - na Mwenyezi Mungu ana mfano wa juu - hakika Muumba wa ulimwengu wote na mmiliki wa ufalme na falme zote, na mtawala wa kiazali kwa hali zote, ana sampuli mbili za mazungumzo na kuonesha umuhimu na takirima: Ya kwanza: Ni ya sehemu ndogo na mahususi: Na nyingine: Ni ya sehemu nzima na ya jumla. Basi Miiraji ya mtume (s.a.w), ni mwonekano wa heshima wa hali ya juu ya uwalii wa Muhammad uliodhihiri kwa hali ya ukamilifu wote unaopita uwalii wote na kwa cheo na kuwa juu ya uwalii wote, kwani yeye (s.a.w) amepata heshima ya kuongea na Allah (s.w), na kuzungumza naye kwa karibu kwa jina la mola wa walimwengu na kwa anuani ya muumba wa vilivyomo. Mfano wa pili Mtu anashika kioo kuelekea jua, kwa hiyo kioo kinachota kulingana na uwezo wake, mwanga unaobeba rangi saba kutoka kwenye jua. Hapo mtu anakuwa na uhusiano na jua kulingana na kile kioo, na anaweza kufaidika kutokana nalo ikiwa atakielekeza kwenye chumba chake chenye giza au katika bustani yake maalum ndogo iliyowekewa paa, licha ya kuwa kufaidika kwake na mwanga kunaishia tu kwa kadiri ya upokeaji wa kioo kwa mwanga unaoakisi kutoka kwenye jua na sio kwa kadiri ya ukubwa wa jua. Wakati ambapo mtu mwingine anaacha kioo, na kulielekea jua moja kwa moja, na anashuhudia haiba yake na kutambua adhama yake, kisha anapanda juu ya mlima mrefu sana na anaangalia katika mmuliko wa utukufu wake mkubwa sana, na kulielekea kwa dhati bila ya pazia, kisha anarejea na kufungua madirisha mapana upande wa jua hali ya kuwa liko juu sana mbinguni kutoka katika nyumba yake ndogo au katika bustani yake yenye paa, na kufanya mazungumzo na mwanga wa kudumu wa jua la kihakika. Na kama hivi mtu huyu anaweza kufanya mkabala huu na mazungumzo haya yenye kuliwaza yaliyovikwa taji la shukurani na kukiri neema, na kuzungumza na jua kwa kusema: “Ewe jua! Ewe uliyetandawaa katika kiti cha enzi cha uzuri wa ulimwengu! Ewe kipole cha mbingu na mwanga wake! Ewe uliyeweka juu ya Ardhi furaha na nuru na kutunuku tabasamu na furaha kwa maua! hakika umeipa nyumba yangu na bustani yangu ndogo joto na mwanga kwa pamoja, kama ulivyoipa dunia nuru na Ardhi joto. Wakati ambao mwenye kioo wa awali hawezi kuzungumza na jua kwa mfano wa mazungumzo haya, kwa sababu athari za mwanga wa jua zina ukomo wa mipaka ya kioo na masharti yake. Na unaishia tu kulingana na uwezo wa kioo kupokea mwanga. Na kama hivi inaonekana kudhihiri kwa dhati ya Allah wa pekee mwenye kukusudiwa kwa haja zote (s.w). Na yeye ni nuru ya Mbingu na Ardhi na Mfalme wa azali na milele juu ya hakika ya kibinadamu kwa sura mbili, ambazo zinabeba viwango visivyo na mpaka. Sura ya kwanza: Kudhihiri katika kioo cha moyo kwa mafungamano ya kiungu mola mlezi na kunasibika kwake, kiasi kwamba hakika kila mwanadamu ana fungu na nuru hiyo ya kiazali, na ana mazungumzo nayo ni sawa tu iwe katika hali ya sehemu, au hali ya kiujumla, kulingana na u- tayari wake na kulingana na kudhihiri kwa majina na sifa, na hiyo ni katika mwendo wake ndani ya ngazi hizo. Basi ngazi za walio wengi katika uwalii unaoenda chini ya vivuli vya majina mazuri na sifa tukufu na ngazi zake zinatokana na sehemu hii. Sura ya pili: Kudhihiri kwa Allah (s.w) kwa mtu mtukufu mno katika sampuli ya wanadamu na mbora wao wote kwa jumla, kudhihiri kwa dhati yake (s.w), na kwa ngazi kuu kabisa katika ngazi za majina yake mazuri, kwa kuwa mwanadamu ni mwenye kuweza kudhihirisha midhihirisho ya majina ya Allah (s.w) mazuri yenye kudhihiri katika Uwepo wote kwa mkupuo mmoja katika kioo cha roho yake, kwa kuwa yeye ndiye tunda lenye nuru zaidi la mti wa viumbe na mwenye kujumuisha zaidi kwa upande wa sifa na maandalizi. Hakika kudhihiri huku ndio siri ya Miiraji ya Mtume (s.a.w), kiasi kwamba uwalii wake ni mwanzo wa ujumbe wake. Uwalii ambao unatembea ndani ya kivuli, kama mtu wa kwanza katika mfano wa pili, wakati ambapo hakuna kivuli katika utume, bali unaelekea kwenye dhati tukufu moja kwa moja, kama mtu wa pili katika mfano wa pili. Ama Miiraji kwa kuwa ni karama kubwa ya uwalii wa Muhammad na ngazi zake za juu, imepanda na kugeuka katika ngazi ya utume. Basi ndani ya Miiraji kuna uwalii, kwani amepandishwa kutoka kwa viumbe kwenda kwa Mola wa haki (s.w), na dhahiri ya Miiraji ni ujumbe; kwa vile unatoka kwa Mola wa haki (s.w), kwenda kwa viumbe wote, basi uwalii ni kupita katika ngazi za ukaribu kuelekea kwa Allah (s.w), nao unahitaji muda na kupita ngazi nyingi. Ama utume ambao ni nuru kuu kabisa, unaelekea katika kufunuka siri ya kuwa karibu zaidi kwa kiungu; ambayo inatosha punde kidogo sana na muda unaokwenda haraka. Na kwa sababu hii ndio maana imepokewa katika hadithi tukufu kinachofidisha kwamba yeye alirejea haraka papo hapo. Na sasa tunaelekeza maneno yetu kwa yule kafiri ambaye amekaa mkao wa kusikiliza, basi tunasema: Kwa kuwa ulimwengu huu unafanana na nchi ya kifalme iliyo katika mpangilio mkubwa, na mji ambao uko katika upeo wa kuratibiwa, na kasri yenye upeo wa mapambo na uzuri, hapana budi kuwa una mtawala, mmiliki, na mtengenezaji. Na kwa kuwa mmiliki huyo mtukufu na Mtawala mkamilifu na fundi mzuri yupo, na kuna mtu mwenye mtazamo wa kiujumla na mwenye mahusiano enevu kwa milango yake ya fahamu na hisia zake pamoja na ulimwengu huo, na nchi hiyo ya kifalme na kasri hiyo, hapana budi kwamba fundi huyo mtukufu atakuwa na uhusiano mtukufu wenye nguvu, pamoja na mwanadamu huyu mwenye kumiliki mtazamo wa kiujumla na hisia enevu, na hapana shaka atakuwa na mazungumzo matakatifu na mwelekeo wa hadhi ya juu. Na kwa kuwa Muhammad (s.a.w), Nabii asiyejua kusoma (maandishi) amedhihirisha uhusiano huo wa hadhi ya juu kati ya wale ambao waliopata heshima hiyo tangu zama za Bwana wetu Adamu (a.s), kwa sura kuu na tukufu zaidi, kwa ushahidi wa athari zake, yaani kwa utawala wake kwa nusu ya Ardhi na sehemu ya tano ya wanadamu, na kubadilisha mwonekano wa kimaanawy wa viumbe na kuviangazia nuru, kwa hiyo yeye ni mwenye kustahiki zaidi kupata utukufu wa Miiraji ambayo ni ngazi kuu kabisa katika ngazi za uhusiano huo.
Ni nini hakika ya Miiraji? Jibu: Miiraji ni kwenda kwa dhati ya Muhammad na kupita kwake katika ngazi za ukamilifu. Na hii ina maana kwamba ishara za kiungu na athari zake ambazo amezidhihirisha (s.w) katika kupangilia viumbe, kwa majina na anuani tofauti, na amedhihirisha adhama ya Uungu wake kwa kupatisha na kuendesha katika mbingu ya kila duru katika duru alizozitengeneza vyema, kila mbingu kuna eneo kubwa la arshi ya ulezi wa kiungu na kituo kitukufu katika kusarifu kwa uungu. Ishara hizi kuu na athari tukufu, Allah (s.w) alizionesha moja moja kumwonesha mja huyo aliyefanywa kuwa mahususi mteule, buraq alikwenda naye juu na kukata ngazi kama umeme kutoka duru moja kwenda duru nyingine na kutoka kituo hadi kituo, kama vituo vya mwezi, ili amwoneshe Rububiyya ya Uluhiyya yake mbinguni, na kumkutanisha na ndugu zake mitume mmoja mmoja, kila mmoja katika makamo yake katika mbingu hizo, hadi akampandisha katika makamo ya (Ukaribu wa pinde mbili) akamtukuza kwa upweke, kuongea naye na kwa kumuona, ili kumjaalia mja huyo kuwa ni mja mwenye hali jumuishi za makamilifu yote ya kibinaadamu, akiwa mwenye kupata midhihirisho yote ya kiungu, akiwa ni mwenye kushuhudia juu ya matabaka yote ya viumbe, mlinganiaji katika mamlaka ya kiungu, mfikishaji wa vyenye kuridhiwa na Allah (s.w), mwenye kufumbua talasimu (fumbo) la viumbe. Inawezekana kuiona hakika hii ya thamani kupitia mifano miwili: Mfano wa kwanza Tumeufafanua katika (Neno la ishirini na nne), kwamba mfalme ana anuani tofauti katika ofisi za Serikali yake, na sifa mbalimbali kulingana na matabaka ya raia wake, na majina na alama mbali mbali katika ngazi za ufalme wake, kwa mfano: Ana jina la mtawala mwadilifu katika ofisi za haki na anuani ya mfalme katika ofisi za kiraia, wakati ambao ana jina la kamanda mkuu katika ofisi za kiaskari na anuani ya khalifa katika ofisi za kisharia, na kama hivi ana majina mengine na anuani, ana katika kila ofisi miongoni mwa ofisi za dola yake makamo na kiti kwa hali iliyo kama kiti cha enzi chake cha kimaanawy, na kwa hivi inayumkinika kwa mfalme huyu mmoja kuwa ni mmiliki wa majina elfu moja na moja katika ofisi za ufalme huo na katika ngazi za tabaka za serikali, yaani anaweza kuwa na viti vya enzi elfu moja na kimoja vyenye kuingiliana, na hata kana kwamba mtawala huyu yupo katika kila ofisi miongoni mwa ofisi za dola yake, na anajua yanayotokea humo kwa haiba yake ya kimaanawy, (mfumo unaotenda kama mtu mmoja) na ujumbe wake maalum. Na anashuhudiwa na kushuhudia katika kila tabaka, kwa kanuni yake na mfumo wake na wawakilishi wake, na anaangalia na kuongoza kutokea nyuma ya pazia kila ngazi kati ya ngazi hizo kwa hekima yake, ujuzi wake na kwa nguvu yake, na kila ofisi ina kituo kinachoihusu na mahali maalum, hukumu zake ni tofauti, tabaka zake ni tofauti. Mfano wa mfalme huyu humwendesha amtakaye na amteuaye katika msafara mpana kwenye msafara huo anatembelea ofisi zote za ufalme huo, hali ya kumwonesha haiba ya dola yake na adhama ya ufalme wake, akimwonesha amri zake zenye hekima ambazo zinahusu kila ofisi, akimtembeza kutoka ofisi kwenda ofisi kutoka tabaka moja kwenda tabaka lingine, mpaka anamfikisha kwenye makamo ya kuhudhuria kwake, na baada ya hapo anamtuma kuwa ni mjumbe kwa watu, akimkabidhi baadhi ya amri zake za jumla enevu zenye kuhusiana na ofisi zote hizo. Na kama hivi tunatazama kwa darubini ya mfano huu na tunasema: Hakika Bwana mlezi wa walimwengu na yeye ni mfalme wa azali na milele, ndani ya ngazi za ulezi wake wa kiungu ana mambo na anuani mbali mbali. Lakini yanarandana baadhi yake na baadhi nyingine, na ndani ya ofisi zake za kiungu (Mola Muabudiwa) kuna alama na majina tofauti, lakini baadhi yake hushuhudiwa ndani ya nyingine, na katika shughuli zake kuu ana midhihirisho na maonesho yenye kutofautiana, lakini yanarandana, na ndani ya usarifu wa Uweza wake kuna anuani tofauti, lakini hutambuana baadhi yake na baadhi nyingine, na ndani ya midhihirisho ya sifa zake kuna mandhari takatifu mbalimbali, lakini baadhi yake huyadhihirisha baadhi nyingine. Na ndani ya midhihirisho ya vitendo vyake kuna usarifu tofauti, lakini mmoja huukamilisha mwingine. Na ana ulezi mkubwa wenye kubadilika ndani ya ufundi wake na alivyovitengeneza, lakini kimoja wapo kinakiona kingine. Kwa msingi wa siri hii kuu, Allah (s.w) ameufuma ulimwengu kulingana na mpangilio wa ajabu unaoamsha tahayuri na kustaajabia, kwani kutokea kwenye atomu ambazo zinahesabiwa ni viumbe vidogo kabisa hadi kwenye mbingu, na kutokea kwenye tabaka lake la kwanza na hadi kwenye kiti kikuu cha enzi, mbingu zilizojengwa baadhi ya nyingine, kila mbingu ni kwa mazingatio ya dari ya ulimwengu mwingine, na kwa nafasi ya arshi ya Uungu wake (hali ya Ubwana mlezi wa kila kitu) na kituo cha Usarifu wa mambo ya kiungu (Mola Muabudiwa wa haki). Na pamoja na kuwa yawezekana kudhihiri kwa majina yote kwa anuani zote katika ofisi hizo na katika tabaka kwa kuzingatia upekee, isipokuwa kama inavyokuwa anuani ya Mtawala mwadilifu ni mwenye kutawalia na ni shina katika ofisi ya mambo ya uadilifu, na anuani nyingine zenye kumhusu zenye kungojea amri yake, vilevile - na Allah (s.w), ana mfano wa juu – kuna jina la kiungu na anuani ya kiungu yenye kutawala na kutamalaki katika kila tabaka katika tabaka za viumbe na katika kila mbingu, na baki ya anuani zimo ndani yake. Kwa mfano: Katika mbingu ambayo Bwana wetu Issa (a.s), aliyepata utukufu kwa jina la (Al-Qadiir), amekutana na Bwana wetu Mtume (s.a.w), basi Allah (s.w) ni mwenye kujidhihirisha katika duru ya mbingu hiyo kwa dhati kwa anuani ya (Al-Qadiir). Kwa mfano: Hakika ya anuani ya Mwongeaji ambayo Bwana wetu Musa (a.s) amepata utukufu wake ni yenye kutawalia katika duru ya Mbingu ambayo ni kituo cha Bwana wetu Musa (a.s). Na kama hivi, Mtume mtukufu (s.a.w), kwa kuwa amebahatika jina kuu, na kwa kuwa unabii wake ni enevu wenye kukusanya, na amepata midhihirisho yote ya majina mazuri, kwa hiyo ana uhusiano na duru zote za kiungu, hapana budi kwamba hakika ya Miiraji yake inahitajia yeye kukutana na manabii na wao ni wenye makamo katika duru hizo, na kupita katika tabaka zote. Mfano wa pili Hakika ya anuani ya (Amiri jeshi mkuu) ambayo ni katika anuani za mfalme, ina udhihiriko katika kila cheo katika vyeo vya kiaskari kuanzia kwenye cheo cha (Kamanda mkuu) na mkuu wa vikosi – cheo kikunjufu cha kiujumla – hadi kwenye cheo cha koplo nacho ni cheo cha kisehemu maalumu. Kwa mfano: Hakika mwanajeshi mmoja anaona kielelezo cha uongozi mkuu na mfano wake katika haiba ya Koplo, anamwelekea na kupokea amri kutoka kwake. Na hali ambapo Koplo anakuta anuani ya uongozi huo katika cheo cha mkuu wake, mkuu wa makoplo na kumwelekea. Na anapokuwa mkuu wa makoplo anaona kielelezo cha jumla na udhihiri wake katika cheo cha Luteni. Na ana kiti maalum katika kituo hicho. Na kama hivi inaonekana anuani ya uongozi huo mkuu katika kila cheo katika vyeo vya Kapteni Meja Jenerali na Fidmashali kulingana na upana wa cheo au ufinyu wake. Na sasa huyo kiongozi mkuu akitaka kukabidhi jukumu linalohusu vyeo vyote vya kiaskari kwa mwanajeshi mmoja, na akataka kumpandisha cheo cha juu, kinachoshuhudiwa upande wa vyeo hivyo na wote wanakishuhudia, kana kwamba ni mwangalizi wake, hakika yeye (Kamanda mkuu) bila shaka atampitisha mwanajeshi huyo mmoja katika vyeo hivyo kuanzia cheo cha koplo na kuishia katika duru yake kuu, duru hadi katika cheo chake kikuu, ili apate kushuhudia na kushuhudiwa kutokea hapo, kisha anamkubali katika makamo ya hadhara yake na kumpa utukufu kwa kuongea naye na kumkirimu kwa amri zake na nishani zake, kisha anamtuma kule alikotoka wakati mmoja na katika punde hiyo hiyo. Inapasa tugeuze mtazamo katika nukta moja kwenye mfano huu nayo: Ikiwa mfalme sio mwenye kushindwa, ana uwezo wa kiroho wa kimaanawy na kama alivyo na nguvu dhahiri, hakika hatawawakilisha watu mfano wa generali na fidmashali na Luteni, bali atahudhuria mwenyewe kila mahali, na kutoa amri yeye mwenyewe moja kwa moja akiwa amejificha kwa baadhi ya pazia, na nyuma ya watu wenye hadhi, kama inavyosimuliwa kwamba wafalme walikuwa mawalii wakamilifu walitekeleza amri zao katika duru nyingi katika sura ya baadhi ya watu. Ama hakika ambayo tunaitazama kwa miwani ya mfano huu, nayo ni kuwa amri na utawala inakuja moja kwa moja kutoka kwa kiongozi mkuu kwenda kila duru katika duru, na kutekelezwa huko kwa amri yake na matakwa yake na nguvu yake kwa hali ambayo hakuna kushindwa ndani yake. Vivyo hivyo kwa mfano sawa na huu: Katika kila tabaka miongoni mwa tabaka za viumbe na makundi yaliyokuwepo, kutoka katika atomu hadi kwenye sayari na kutoka kwenye vidudu hadi mbinguni, vinavyopita humo na kutekelezwa kwa utiifu kamili, na kutekeleza amri ya mfalme wa azali na wa milele na mambo ya mtawala wa Ardhi na mbingu, Mwamrishaji wa hali yote Mmiliki wa amri: كُنْ فَيَكُوْنُ hushuhudiwa, katika kila moja miongoni mwao, duru ya Uungu Bwana mlezi uliyo mtukufu na tabaka la kiutawala lenye kutamalaki, kwa matabaka ya aina tofauti tofauti na makundi mbalimbali, madogo na makubwa, ya kisehemu au kiujumla, kila moja ikiielekea nyingine. Kwa ajili ya kufahamu makusudio yote ya kiungu (Mola Muabudiwa wa haki) ya juu na matokeo makuu yaliopo kwenye ulimwengu, kupitia kushuhudia majukumu ya kiuja ya aina mbali mbali kwa tabaka zote, na ili kutambua yanayomridhisha Allah Mwenye utukufu na ukubwa, kwa uoni wa ufalme wake wa kiungu mtukufu na haiba ya utawala wake wenye ushindi usioshindwa, na ili awe Mlinganiaji kwa Allah (s.w), hapana budi kuwepo na matembezi katika tabaka hizo na kupita katika duru hizo hadi aingie katika arshi tukufu ambayo ni anuani ya duru yake kubwa na kuingia katika (قَابَ قَوْسَيْنِ) yaani aingie katika makamo kati ya (imkani na wajibu) kulikoashiriwa kwa (قَابَ قَوْسَيْنِ) na kukutana na dhati tukufu iliyo nzuri. Mwendo huu na kupita huku na kukutana ndio hakika ya Miiraji. Na kama inavyopatikana kwa kila mwanadamu mwendo kwa akili yake kwa kasi ya kufikirika, na kila walii ana matembezi kwa moyo wake kwa kasi ya umeme, na kila malaika ana mzunguko kwa mwili wake wa kinuru kwa kasi ya roho, kutoka kwenye kiti cha enzi hadi kwenye tandiko na kutoka kwenye tandiko hadi kwenye kiti cha enzi, na watu wa peponi wana kupanda Miiraji kwa kasi ya Buraki, kutoka katika medani ya ufufuo hadi peponi na katika umbali unaozidi miaka mia tano elfu, hakika mwili wa Muhammad (s.a.w), ambao ni ghala la viungo vyake vitukufu na eneo la majukumu yasiyo kuwa na mpaka ya roho yake ya hadhi ya juu, itafuatana na roho hiyo ya Muhammad ambayo ni nuru, na katika upokeaji wa nuru, na mpole kuliko nyoyo za mawalii, na laini kuliko roho za maiti, na angavu kuliko viwiliwili vya malaika, na vyenye kupendeza zaidi kuliko kiwiliwili cha nyota na mwili wa kimfano, atafuatana nayo kwa vyovyote na kupanda nayo hadi kwenye kiti cha enzi tukufu. Na sasa tumtazame kafiri ambaye yuko katika nafasi ya kusikiliza: Inapita mawazoni kwamba huyu kafiri anasema moyoni mwake: Mimi siamini Allah (s.w), na wala simjui mtume (s.a.w), basi vipi nitasadiki Miiraji? Na sisi tunamwambia: Kwa kuwa viumbe hivi vipo kwa hakika, na kunashuhudiwa ndani yake matendo na upatishaji, na kwamba tendo lililopangika haliwi bila ya mtendaji, na kitabu chenye fasaha hakiwi bila ya Mwandishi, nakshi ya kupendeza haiwi bila mtia nakshi. Hakuna budi kuwepo kwa mtendaji wa matendo haya yenye hekima yaliyojaa kwenye viumbe, na hapana budi kuwepo mtia nakshi na mwandishi kwa nakshi hizi za kupendeza na barua za fasaha ambazo zinajaa uso wa Ardhi na kuja upya kila majira na majira, na kwa kuwa kuwepo kwa watawala wawili katika jambo fulani kunaharibu nidhamu ya kitu hicho, na kwamba kuna mpangilio kamili na uratibu uliotimia, kuanzia kwenye ubawa wa mbu hadi kwenye kandili za mbinguni, kwa hiyo basi Mtawala huyo ni Mmoja wa pekee, kwa kuwa utengenezaji na hekima katika kila kitu ni katika ufundi wa ajabu na kufanya vizuri kiasi kwamba inalazimu kuwa mtengenezaji wa kitu hicho ni Mweza wa hali zote, mweza juu ya kila kitu na mjuzi wa kila kitu, kwani kama asingekuwa mmoja ingelazimu kuwepo miungu kwa idadi ya vilivyopo, na kila Mungu angekuwa dhidi ya mwingine na mfano wake! Na wakati huo inakuwa kubakia kwa nidhamu hii bila ya kuharibika ni muhali katika Muhali elfu moja! Kisha hakika ya tabaka za vilivyomo visingekuwa vyenye mpangilio sana, na vyenye kutii sana amri kwa mara elfu kuliko jeshi liliopangiliwa, kama inavyoshuhudiwa kwa dhahiri, kwani kila mpangilio katika mipangilio ya harakati za nyota, jua na mwezi hadi mpangilio wa maua ya lozi unadhihirisha mpangilio wa ajabu na kamili katika aliyotunuku Mweza wa azali katika nishani na kuvivika mavazi yenye kupambika, na kuyatengea harakati na matendo, yanazidi yale yanayooneshwa na jeshi, katika nidhamu na utiifu mara elfu, kwa hiyo viumbe hivi vina Mwenye hekima wa hali zote amefichikana nyuma ya ghaibu, vilivyopo vinangojea amri yake ili kuzitekeleza. Na kwa kuwa huyo mwenye hekima kwa hali zote ni mfalme mwenye utukufu, kwa ushahidi wa kazi zake zenye hekima, na kwa athari tukufu zinazoonekana dhahiri, na mola Mwingi wa rehema Mkunjufu wa Rehema, kwa neema anazozidhihirisha, na fundi wa ajabu anayependa sana ufundi wake, kwa kazi zake za ufundi wa ajabu alizozionesha, na Muumbaji, Mwingi wa hekima, anataka kuamsha kupendezwa na wenye utambuzi na kuleta usifiaji wao mzuri, kwa mapambo mazuri na kazi za kupendeza alizozieneza, na inafahamika katika uzuri wa aliyotengeneza, unaochukua akili katika kuumba ulimwengu, ya kwamba yeye anataka kuwajulisha wenye utambuzi kutokana na viumbe wake: Nini makusudio ya upambaji huu? Na wapi viumbe vinatokea? Na hatima yake ni wapi? Hapana shaka hakika Mtawala huyu Mwingi wa hekima na fundi Mjuzi wa kila kitu atadhihirisha Uungu wake (Bwana Mlezi wa kila kitu) Mtukufu. Na kwa kuwa yeye anataka kuitambulisha nafsi yake na kuipendezesha kwa wenye utambuzi, kwa athari za upole na huruma alizozidhihirisha, na kwa maajabu ya ufundi aliyoyaeneza, hapana shaka kwamba atapasha habari kwa kupitia mfikishaji mwaminifu, anayoyataka kutoka kwa wenye utambuzi, na kwa kile atakachowaridhia nacho? na kwa hiyo kwa vyovyote atatangaza Uungu wake (wa hali ya kuwa Bwana Mlezi) kwa kupitia kwa mwenye kumteua mahususi katika wenye utambuzi na kumpa utukufu mlinganiaji miongoni mwa wenye utambuzi kwa ukaribu wa kuhudhuria kwake, akimjaalia kuwa ni wasita (mkaa kati) wa kutangaza kuhusu kazi za ufundi wake zenye kupendwa kwake, na atamteua mwalimu anayedhihirisha makamilifu yake kwa kufundisha makusudio yake ya juu kwa wengine wenye utambuzi, na atamteua kiongozi anayejulisha maana ya vilivyokuwepo ili katika vilivyoingizwa katika ulimwengu huu isibaki talasimu yoyote (Fumbo) bila ufumbuzi na yaliyofichwa katika hivi vilivyokuwepo katika mambo ya kiungu (Hali ya kuwa Bwana Mlezi) bila maana yoyote, na atamteua kiongozi anayefundisha makusudio yake ili yasibaki kuwa ni mchezo bila ya manufaa yale aliyo yadhihirisha katika mazuri ya utengenezaji (wake) au kuyaeneza mbele ya macho, na atamnyanyua mmoja wao na kumpandisha katika makamo ya juu katika wenye utambuzi wote na amfundishe yanayomridhisha na kumtuma kwao. Na kwa kuwa hakika na hekima vinahitajia hili, mwenye kustahiki zaidi wa kutimiza haki ya majukumu hayo ni Muhammad (s.a.w), ametekeleza majukumu hayo hasa kwa sura yake kamilifu zaidi, na shahidi Mwadilifu Mkweli juu ya hilo ni alichoasisi katika ulimwengu wa Kiislamu na aliyoyadhihirisha katika nuru ya Uislamu iliyo dhahiri. Kwa hiyo kwa ajili ya yaliyotangulia inalazimu kumpandisha na kumuinua nabii huyu mtukufu uinuaji wa moja kwa moja kuelekea katika makamo ya juu yaliyo juu ya viumbe wote na kuvuka vyote vilivyokuwepo, ili abahatike kutokea mbele ya Bwana Mlezi wa walimwengu. Miiraji ina maanisha hakika hii. Muhtasari Hakika ya mwingi wa hekima wa hali zote amevipamba viumbe hivi vikuu na kuvipangilia kwa kudhihirisha mifano ya makusudio haya makuu na shabaha tukufu, na kwamba katika hivi vilivyomo imo sampuli ya mwanadamu ambaye anaweza kushuhudia Uungu huu (Hali ya Bwana mola Mlezi) ya ujumla na sehemu zake zote ndogo mno, na Uungu huu mtukufu (hali ya kuwa Mola Muabudiwa wa haki) kwa hakika zake zote, hapana shaka kwamba huyo Mwingi wa hekima wa hali zote ataongea na mwanadamu na kumjulisha makusudio yake. Na kwa kuwa kila Mwanadamu hawezi kupanda katika makamo ya juu sana ya kiujumla akiwa mwenye kuepukana na hali ya kisehemu na kihali ya chini, hakuna shaka kwamba baadhi ya watu mahususi kati ya hao watu atakalifishwa jukumu hilo, ili awe na uhusiano pamoja na pande mbili kwa pamoja, yaani awe mwanadamu anayewafundisha watu, na katika wakati huo huo awe mwenye roho iliyo katika upeo wa hadhi ya juu ili apate utukufu wa maongezi ya kiungu moja kwa moja. Na baada ya hayo, kwa kuwa aliyefikisha makusudio ya Bwana Mlezi wa walimwengu kati ya wanadamu, na kufumbua talasimu (fumbo) lake na kutatua kitandawili cha kuumbwa na mkamilifu zaidi aliyelingania adhama ya mazuri ya Uungu (Bwana mlezi) ni Muhammad (s.a.w), hapana shaka kuwa atakuwa na mwenendo wa kimaanawy wa hadhi ya juu baina ya wanadamu, kiasi atakuwa na Miiraji kwa sura ya mwendo na utalii katika ulimwengu wa kimwili, na atakata ngazi hadi zilizokuwa nyuma ya tabaka za vilivyokuwepo na kizuizi cha majina na kudhihiri kwa sifa na matendo yanayoyaelezea kwa pazia sabini elfu. Basi hii ndio Miiraji. Na inapita mawazoni vilevile, hakika wewe msikilizaji unasema katika vina vya moyo wako: Hakika Bwana mlezi yuko karibu mno na sisi kuliko kila kitu, nini inamaanisha kuwepo mbele yake baada ya kukata masafa ya maelfu ya miaka na kupita katika pazia sabini elfu? Vipi nitaitakidi hili? Na sisi tunasema: Hakika Allah (s.w) yuko karibu na kila kitu kuliko kila kitu, isipokuwa kila kitu kiko mbali na yeye umbali wa hali zote, tukikadiria kwamba jua lina utambuzi kamili, linaweza kuongea na wewe kwa kioo ambacho kiko mkononi mwako, na linasarifu kwako namna lipendavyo, wakati ambapo liko karibu kwako kuliko mboni ya jicho lako lenye kufanana na kioo, wewe uko mbali nalo takriban kwa miaka elfu nne. Na haiyumkiniki kwako kulikaribia kwa hali yoyote iwayo, hata kama ungepanda hadi katika makamo ya mwezi, na kuinuka juu hadi katika nukta ya kukabiliana nalo moja kwa moja, hautakuwa isipokuwa ila kama kioo chenye kuliakisi jua. Na kama hivyo (s.w), naye ni jua la azali na milele - na Allah ana mfano wa juu - yuko karibu na kila kitu kuliko kila kitu, pamoja na kuwa kila kitu kiko mbali naye kwa hali zote, isipokuwa yule anaye kata vyote vilivyopo, na kukomboka na hali ya u-sehemu na kupanda katika ngazi za ujumla akipenda kutoka ngazi hadi ngazi na anapita kupitia maelfu ya pazia na analikaribia jina lenye kuzungukia vilivyokuwepo vyote, na kukata ngazi nyingi mbele yake, kisha baada ya hapo anapata utukufu wa aina fulani ya ukaribu. Na mfano mwingine: Hakika mwanajeshi mmoja yuko mbali kabisa na haiba ya kimaanawy ya kiongozi mkuu, yeye anamtizama kiongozi wake kutoka masafa ya upeo wa umbali na kupitia pazia nyingi za kimaanawy, anamwona katika kielelezo kidogo katika cheo cha Koplo. Ama kutaka ukaribu wa hakika wa haiba ya kimaanawy ya kiongozi mkuu, hiyo inamlazimu kupita katika ngazi nyingi za kiujumla kama ngazi ya Luteni na kapteni na Meja na kadhalika. Wakati ambao kiongozi mkuu yupo kwake na anamuona kwa amri yake na kanuni yake, na uangalizi wake, hekima yake na ujuzi wake, naye akiwa yupo kwa dhati yake mkabala wake ikiwa ni kiongozi katika maana – na roho – kama ilivyo katika sura na dhahiri. Na ilivyokuwa hakika hii imethibitishwa kwa ithibati ya kukinaisha katika (Neno la kumi na sita) hapa tunatosheka kwa kiasi hiki cha muhutasari. Na inapita kwenye mawazo vilevile, kwamba wewe unasema kwa moyo wako wote: Mimi ninakana kuwepo kwa mbingu na wala siamini malaika, vipi basi nitasadiki kwenda kwa mwanadamu na kutembea kwake mbinguni na kukutana kwake na malaika? Naam, hapana shaka kwamba kuonesha kitu na kufahamisha jambo kwa mtu kama wewe, na kifuniko kimefunikwa kwenye uoni wake na akili yake imeshuka hadi kwenye jicho lake haoni tena isipokuwa maada, ni jambo gumu mno, lakini kwa sababu ya haki kuwa wazi sana, hata vipofu wanaiona. Kwa hiyo tunasema: Ni kwamba watu wanaafikiana kwamba, anga la juu limejaa (Ether). Mwanga, umeme na joto na mfano wa hayo ni katika vyenye kumiminika vipole, ni dalili ya kuwepo kwa maada yenye kujaa mbinguni. Kwa kuwa ulimwengu wa juu umejengwa kwa namna mbali mbali, kila moja kati yake inabainisha hukumu tofauti katika mazingira mbali mbali, chanzo cha maamuzi hayo, yaani mbingu, zinazotofautiana pia, kama ilivyo kwa mwanadamu kuna aina za uwepo wa kimaanawy, isipokuwa mwili wa kimaada, kama akili, moyo na roho, na mawazo ya kufikirika na kumbukumbu na kadhalika, na katika ulimwengu vilevile ambao ni katika sura ya mwanadamu mkubwa, na katika viumbe ambavyo ni mti wa tunda la mwanadamu, limwengu nyingine zisizokuwa ulimwengu wa kimwili, ukiachilia mbali kwamba kila ulimwengu katika limwengu mbali mbali una mbingu yake kuanzia kutoka katika ulimwengu wa Ardhi hadi ulimwengu wa pepo. Kwa mnasaba na Malaika tunasema: Ardhi nayo ni katika sayari za ukubwa wa kati na kati na ndogo na nyingi kulingana na nyota, ikiwa ni zenye kujaa kwa kiasi kisichohesabika katika mitindo ya maisha na utambuzi, na hivyo ni kitu cha thamani zaidi katika vilivyopo na vyenye nuru zaidi. Basi vipi mbingu ambazo ni bahari pana nyota huogelea humo kana kwamba ni majengo makubwa yenye kuratibika na kasri ndefu kulingana na Ardhi ambayo ni nyumba ndogo yenye giza? Kwa hiyo mbingu basi ni makazi ya wenye utambuzi na uhai, na jinsi anuai na kwa idadi isiyohesabika wala kudhibitika, nao ni Malaika na Maruhani, na kwa kuwa tumeshathibitisha kwa namna ya kukinaisha, kuwepo kwa mbingu na wingi wake katika tafsiri yetu iitwayo: (Ishaaratul iijaz fy madhannil iyjaz) nayo ni tafsiri ya kauli yake: ثُمَّ اسْتَوَى إِلَى السَّمَاء فَسَوَّاهُنَّ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ na kadhalika tumethibitisha kuwepo kwa malaika uthibitisho ambao shaka haiukaribii katika (Neno la ishirini na tisa), hapa tunafupisha mada hii na tunaielekeza katika risala hizo mbili. Muhtasari: Hakika kuwepo kwa mbingu ambazo zimesawazishwa kutokana na Ether na kuwa mwendo wa mwanga na joto na nguvu ya uvutano na mifano ya hivyo katika vimiminiko nyororo, na kuwa ni vyenye kuwiana na harakati za nyota na sayari kama hadithi tukufu ilivyoashiria (Mbingu ni wimbi lililozuiliwa) imechukua hali tofauti na maumbo mbalimbali, kutoka katika njia kuu ya sayari, (Inayoitwa njia za mbingu) hadi sayari ya karibu mno na sisi, katika tabaka saba, kila moja inachukuliwa kuwa ni dari ya ulimwengu mwingine, kutoka katika ulimwengu wa Ardhi hadi ulimwengu wa kizuizi hadi katika ulimwengu wa mfano, hadi katika ulimwengu wa Akhera, kama hivi hekima na mantiki ya akili vinahitajia hayo. Na inapita mawazoni vilevile: Ewe kafiri! Wewe unasema: Sisi hatupandi kwa ndege kwenda maeneo ya juu ila kwa mashaka ya nafsi na tunafika kwa ugumu mno hadi masafa ya kilo mita chache, basi vipi inayumkinika kwa mwanadamu kukata kwa mwili wake masafa ya maelfu ya miaka kisha arudi alipotoka ndani ya dakika chache?! Nasi tunasema: Mwili mzito kama ardhi hukata kwenye dakika moja masafa ya takriban saa mia moja na themanini na nane kwa mwendo wake wa mwaka, kulingana na mliyoyafikia katika elimu. Yaani Ardhi inakata masafa ya miaka ishirini na tano elfu ndani ya mwaka mmoja! Je, hawezi huyo Mweza wa kila kitu mwenye utukufu ambaye anaye endesha Ardhi hii kwa nyendo hizi zilizopangika madhubuti, kumleta mwanadamu kwenye kiti cha enzi? na kwamba isiweze hekima hiyo ambayo inaendesha ardhi nzito – kama Muriid mevlevi - kwa kanuni ya kiungu (Bwana mlezi) inayoitwa nguvu ya uvutano wa jua, kupandisha mwili wa mwanadamu kwenda kwenye kiti cha enzi cha Mwingi wa Rehema kama umeme, kwa nguvu ya mvuto wa rehema ya Mwingi wa Rehema Mwenye kurehemu, na kwa kuvutika kwa mahaba ya nuru ya mbingu na Ardhi? Na inapita kwenye akili kwamba wewe unasema: Na iwe kwamba anaweza kupanda na kwenda Miiraji mbinguni lakini kwa nini alipandishwa? na kuna dharura ipi ya kwenda Miiraji? Je, haikuwa inamtosha kupanda Miiraji kwa moyo wake na roho yake kama wanavyofanya hivyo Mawalii wema? Na sisi tunasema: Madhali fundi mtukufu ametaka kudhihirisha ishara zake kubwa kwake (s.a.w) katika ufalme wake na falme zake, na kataka kumwonesha katika vyanzo na viwanda vya huu ulimwengu, na kataka kumwonesha matokeo ya kiakhera ya amali za wanadamu, basi hapana shaka kwenda pamoja naye hadi kwenye kiti cha enzi, macho yake ambayo yanazingatiwa kuwa ni ufunguo wa ulimwengu wa vyenye kuonekana kwa macho, na sikio lake ambalo anasikilizia ishara za ulimwengu wa vyenye kusikilizwa. Kama katika yanayolazimu akili na hekima kwenda pamoja naye kwenye kiti cha enzi, mwili wake wenye kubarikiwa vilevile ambao unazingatiwa kuwa ni mashine za zana na vifaa ambavyo hutendeka juu yake majukumu ya roho yake yasiyo na mpaka. Kama hekima ya kiungu inavyojaalia mwili ni rafiki wa roho peponi, kwa sababu mwili ni mahali pa majukumu mengi ya kiuja na kisicho na mpaka cha ladha na machungu, hapana budi kwamba huo mwili wenye kubarikiwa utakuwa pamoja na roho. Na kwa kuwa mwili utaingia peponi na roho, ni katika hekima tupu pia kuufanya mwili wake wenye kubarikiwa mshirika wa dhati ya Muhammad (s.a.w), ambao alipandishwa nao hadi Mkunazi wa Ukomo ambao ni mwili wa pepo ya Maawa. Na inapita kwenye akili kwamba wewe unasema: Ya kwamba ni muhali kiakili kukata masafa ya maelfu ya miaka, ndani ya dakika chache? Na sisi tunasema: Hakika ya michakato katika alivyovitengeneza mtengenezaji Mtukufu vinatofautiana sana, basi kwa mfano: Hakika kiasi cha kutofautiana kwa kasi ya sauti, mwanga, umeme, roho na mawazo kinajulikana kwetu. Basi vilevile kasi ya sayari – kama inavyojulikana kisayansi – kuna tofauti za kuzifanya akili zitahayari. Basi vipi uonekane mwendo wa mwili wake nyororo (s.a.w), ambao umepata kasi kwa kupanda Miiraji, na ikafuata roho yake ya hadhi ya juu, kasi hiyo ya haraka sana kasi ya roho ni kinyume na akili? Wewe kwa nafsi yako ukilala dakika kumi, unapitia hali ambazo huzipitii katika hali ya kuwa macho kwa mwaka. Hata anachokiona mtu kwenye ndoto kwenye dakika moja na maneno anayosikia humo na maneno anayotamka humo kama yatajumuishwa na kukusanywa pamoja, inalazimu muda wa siku moja au zaidi katika ulimwengu wa kuwa macho. Basi wakati mmoja kwa hiyo kulingana na watu wawili inaweza kuwa sawa na siku moja kwa mmoja wao na mwaka mmoja kwa mwingine. Basi angalia maana hii kwa mtazamo wa mfano huu: Tukadirie kuwepo kwa saa ya kupima kasi ya nyendo ya mwanadamu na risasi, sauti, mwanga, umeme, roho na mawazo. Na katika saa hii kuna kurabu, kurabu moja inahesabu saa, na nyingine inahesabu dakika, katika mzunguko mpana zaidi kuliko wa awali mara sitini, na kurabu nyingine inahesabu sekunde, katika duara pana zaidi kuliko hili kwa mara sitini, hivyo hivyo kurabu za robo, humusi, sudusi na sehemu ya saba na sehemu ya tisa na sehemu ya kumi. Yaani saa inakuwa na kurabu za ajabu kila moja inazunguka katika duara pana zaidi kuliko la kabla yake kwa mara sitini mara dufu. Ikiwa kurabu inayohesabu saa kwa kiwango cha saa zetu ndogo za mkononi, italazimu duara la kurabu linalohesabu sehemu ya kumi kwa kiwango cha mzunguko wa mwaka wa Ardhi au mkubwa zaidi kuliko huo. Na sasa hebu tukadirie kwamba kuna watu wawili: Mmoja wao: Kana kwamba amepanda kurabu ya saa anatazama na kuangalia yanayomzunguka, na mwingine amepanda kurabu ya sehemu ya kumi na kushuhudia yanayomzunguka. Tofauti kati ya vitu wanavyoshuhudia hawa watu wawili katika wakati mmoja, ni uwiano wa tofauti kulingana na saa zetu za mkono na mzunguko wa ardhi wa mwaka, yaani tofauti ni kubwa mno. Na vivyo hivyo, kwa kuwa muda ni aina katika aina za mwendo na pambo lake au mkanda wake, basi uamuzi unaopita katika nyendo huamuliwa pia katika wakati, wakati tunashuhudia katika saa moja kiasi cha anachoshuhudia mpandaji mwenye utambuzi juu ya kurabu ya saa, na hakika ya umri wake ni kwa kiasi hicho hicho, hakika Mtume mtukufu (s.a.w), katika wakati huo huo – kama aliyepanda juu ya kurabu ya sehemu ya kumi – katika hiyo saa maalum anapanda buraq wa taufiki ya kiungu na anakata duru zote za yamkini kama umeme na anaona ishara za ufalme na falme na anapanda katika duru ya wajibu, na kupata utukufu kwa kukutana na kuongea, na anafaulu kupata kuona uzuri wa kiungu na kutekeleza ahadi na amri ya kiungu ili kutekeleza jukumu kisha anarudi. Na amerudi hasa. Naye ni kama hivyo. Na inapita kwenye akili vilevile: Kwamba nyinyi mnasema: Naam, inajuzu, na pengine inayumkinika kutokea! lakini sio kila kinachotazamiwa na yamkini kutokea hutokea kweli, je, vipi itasihi kuhukumiwa juu ya kitu kisicho na mfano, kwa sababu tu ya kuwepo uwezekano wa kutokea kwake? Nasi tunasema: Hakika mifano ya Miiraji ni mingi kupita kiasi, basi kila mwenye uoni kwa mfano anapanda na uoni wake kutoka ardhini hadi katika sayari ya (Neptune), ndani ya dakika moja, na kila mwenye ujuzi anakwenda kwa akili yake akiwa amepanda kanuni za falaki hadi maeneo ya nyuma ya nyota na sayari ndani ya dakika moja, na kila mwenye imani hupandishwa fikira yake kwenye matendo ya swala na nguzo zake hali akiviaga viumbe nyuma ya mgongo wake anakwenda kwenye hadhira ya kiungu kwa hali inayoshabihiana na Miiraji, na kila mwenye moyo na walii mkamilifu anaweza kwenda kwa mwendo na kupita kutokea katika kiti cha enzi na kutoka katika duru ya majina na sifa ndani ya siku arobaini, hata kwamba Sheikh al-Kailany na Imamu al-Rabbany na wengine katika watu wa kipekee imepatikana kwao kupanda Miiraji ya kiroho kwenda kwenye Arshi ndani ya dakika moja, kama wanavyoelezea kwa masimulizi ya kweli. Na kwamba malaika ambao ni viwiliwili vya kinuru inapatikana kwao kwenda na kurudi kutoka katika kiti cha enzi hadi kwenye tandiko na kutoka kwenye tandiko hadi kwenye kiti cha enzi, katika muda mfupi mno. Na watu wa peponi watapanda kutoka katika mahali pa kukusanywa (Siku ya kiama) hadi katika bustani za pepo katika muda mfupi. Kiasi hiki cha mifano mingi kinabainisha kwa kukinaisha kwamba mfalme wa mawalii na mitume na kiongozi wa waumini wote na bwana wa watu wote wa peponi na mpokewa na malaika wote, ambaye ni mtume mtukufu, bila shaka itapatikana kwake Miiraji iwe ni eneo la mwendo na kupita kwake kuelekea kwa Allah (s.w), kwa namna inayowiana na makamo yake ya hadhi ya juu. Hii ndiyo hekima yenyewe hasa, na inakubalika vilivyo kiakili. Na imetokea kiuhalisia pasi na shaka japo kidogo.
Nini hekima ya Miiraji? Jibu: Hekima ya Miiraji ina hadhi ya juu sana kiasi kwamba fikira ya kibinadamu inashindwa kuitambua, na ina kina kirefu sana kiasi inashindikana kuifikia, nayo ni nyeti na nyororo sana kwa kiasi ni vigumu kwa akili pekee kuiona. Lakini licha ya kutokuwa na uwezo wa kutambua hakika za hekima hii na kuzifahamu, inawezekana kutambua kuwepo kwake kwa ishara kama ifuatavyo: Kwa ajili ya kudhihirisha nuru ya umoja wake Allah (s.w), na kudhihirika kwa upekee wake katika tabaka za viumbe, muumba wa viumbe na mola mlezi wa ulimwengu amemteua mtu mwenye sifa za kipekee kwenda Miiraji, ambaye ni kama uzi wa mawasiliano ya kinuru kati ya ukomo wa tabaka za wingi wa vilivyopo hadi katika chanzo cha umoja, akimfanya kuwa ni mlengwa wa mazungumzo yake, kwa niaba ya viumbe vyote, akimfundisha yeye na kwa kumtumia yeye, makusudio yake ya kiungu kwa niaba ya wenye utambuzi. Ili ashuhudie kwa macho yake uzuri wa ufundi wake na ukamilifu wa Uungu wake (Hali ya kuwa Bwana mlezi wa walimwengu) katika kioo cha viumbe vyake, na kuwashuhudisha wengine athari za uzuri na ukamilifu. Kwa hiyo, madhali Bwana mola mlezi wa ulimwengu ana uzuri wa hali zote na ukamilifu wa hali zote - kwa ushahidi wa athari zake na alivyovitengeneza - na uzuri na ukamilifu ni vyenye kupendwa kwa dhati ya viwili hivyo, basi mmiliki wa uzuri huo na ukamilifu ana mahaba yasiyo na ukomo ya uzuri wake na ukamilifu wake, na mahaba hayo yanadhihiri kwa sura tofauti na mitindo mingi katika vilivyotengenezwa, Allah (s.w) huelekeza mahaba yake kwa vitengenezwa vyake, kwa ayaonayo kwenye vitu hivyo katika athari ya uzuri wake na ukamilifu wake. Na ilipokuwa kipenzi zaidi katika alivyovitengeneza na chenye hadhi ya juu mno kuliko vyote ni wenye uhai, na vipenzi zaidi kati ya wenye uhai ni wenye utambuzi – kwa kuzingatia mkusanyiko wa maandalizi – ni ndani ya mwanadamu – na mwanadamu kipenzi zaidi kwa hiyo ni yule mtu mmoja ambaye maandalizi yake yamekuwa wazi kikamilifu akadhihirisha kikamilifu vielelezo vya makamilifu yake (s.w), ambavyo vimeenea katika alivyovitengeneza na kudhihiri humo. Na kama hivi, basi fundi wa vilivyopo kwa ajili ya kushuhudia aina zote za kudhihiri kwa mahaba yaliyotawanywa katika vilivyomo vyote, katika nukta moja, ndani ya kioo. Na kwa ajili ya kudhihirisha aina zote za uzuri wake – kwa siri ya upekee – amemteua ambaye ni tunda lenye nuru katika mti wa uumbaji na ambaye moyo wake unazingatiwa kuwa ni kokwa yenye uwezo wa kuhifadhi hakika za mti huo za kimsingi, akamteua kwa Miiraji, yeye ni kama kamba ya mawasiliano ya kinuru baina ya mbegu na tunda, yaani kutokea chanzo cha awali hadi kwenye ukomo, akionesha hali ya kupendwa kwa mtu huyo wa kipekee mbele ya viumbe, akampandisha katika hadhira yake, na akampa utukufu kwa kuona uzuri wake, na kumkirimu kwa kumwamrisha, na akamkabidhi jukumu la kufanya hekima takatifu aliyo nayo ienee kwa wengine. Tutaitazama hekima hii ya kiungu kupitia mifano miwili: Mfano wa Kwanza: Nao ni yale tuliyoyabainisha kwa upambanuzi katika (Neno la kumi na moja) kama ifuatavyo: Ikiwa itakuwepo hazina nyingi mno za mfalme zenye ujazo wa aina zisizo na hesabu za johari za thamani na almasi za kipekee, na zikawa na ufundi wa hali ya juu katika maajabu ya kiufundi, naye ana maarifa mapana kwa sanaa mbali mbali za ajabu zisizohesabika, na ujuzi kamili kuzungukia vyote hivyo, na uoni wenye kuenea juu ya elimu za ajabu zisizo na mpaka, na elimu kamili juu ya vitu hivyo. Hapana shaka kwamba mfalme huyo mwenye maajabu na fani pana atataka kufungua maonesho ya jumla, ataonesha humo bidhaa zake za thamani – kwa kuwa kila mwenye uzuri na ukamilifu anataka kushuhudia na kuonesha uzuri wake na ukamilifu wake – na hii ili aelekeze macho ya wakazi katika kuona adhama ya ufalme wake na awashuhudishe mmemetuko wa utajiri na yaliyofurutu ada ya ufundi wake na maajabu ya maarifa yake, hiyo ili ashuhudie uzuri wake na ukamilifu wake wa kimaanawy kwa pande mbili: Upande: Kwa uoni wake mkali madhubuti, na Mwingine: Kwa uoni wa wengine. Kwa Msingi wa hekima hii, mfalme huyu kwa vyovyote ataanza kusimamisha kasri kubwa pana ya haiba, na kuigawanya kwa ustadi katika duru na tabaka na vigawanyo vikubwa, hali ya kupamba kila sehemu kwa johari na mapambo ya hazina zake mbali mbali na kuiweka uzuri wa kiwango cha juu kinachofanywa na mkono wa ufundi wake na maridadi zaidi, akipangilia kwa mipangilio madhubuti zaidi ya sanaa yake na hekima yake. Na baada ya hapo atatandika meza pana zilizoamirishwa, kwa kinachowiana na kila kundi, akiandaa kwa meza hizo karamu ya wageni ya jumla ya ukarimu yenye kusheheni sampuli za neema zake na aina za vyakula vyake vitamu. Kisha anawaita raia wake katika karamu hii ya ukarimu, na kushuhudia makamilifu yake ya ajabu, na mmoja wao anamjaalia kuwa ni mtume kati yake na wao, na anamwita kwake, hali akipita kutoka kwenye tabaka za chini mno hadi za juu yake, na kumwendesha duru hadi duru, na tabaka juu ya tabaka, akimshuhudisha vituo vya kazi ya ufundi huo wa ajabu na ghala za kuhifadhia mavuno yanayopatikana duniani, hadi anamfikisha katika duru yake maalum, na anampa utukufu wa kumkubalia katika hadhara yake, akimdhihirishia dhati yake yenye kheri nyingi, ambayo ndio asili ya makamilifu yake yote. Na kumjulisha makamilifu yake ya kidhati na kumwongoza katika hakika za kasri. Na kumtunuku jukumu la Mwelekezi kiongozi wa watazamaji na kumtuma kwao ili awajulishe wakazi, mtengenezaji wa kasri, kwa yaliomo katika kasri ikiwemo nguzo za nakshi na maajabu ya ufundi wake. Na kumjulisha alama zilizomo kwenye nakshi na ishara zilizomo kwenye kazi za ufundi, na kuwatambulisha wenye kuingia kwenye kasri, ni nini haya marembo yaliyopangiliwa na nakshi zilizowekwa kwa vipimo? na vipi kwamba hizo zinajulisha makamilifu ya mmiliki wa kasri na ufundi wake? na awaongoze katika adabu za kutembea na kutazama na kuwafundisha taratibu rasmi za kuhudhuria mbele ya mfalme mkuu ambaye haonekani. Yote hayo kulingana na yanayomridhisha na anayoyataka. Na kama hivi - na Allah (s.w) ana mfano wa juu – hakika fundi mtukufu, Mfalme wa azali na milele, ametaka kuona na kuonesha uzuri wake wa hali zote, na makamilifu yake ya hali zote, akajenga kasri hili la ulimwengu kwa namna ya uzuri mno uwavyo, kiasi kwamba kila kilichomo ndani yake kinataja makamilifu yake, kwa ndimi nyingi, na kujulisha uzuri wake kwa ishara nyingi, hata kwamba viumbe vinadhihirisha kwa kila kilichomo ndani yake, na ngapi katika hazina za kimaanawy zimefichwa ndani ya kila jina miongoni mwa majina ya Allah mazuri, na ngapi katika yenye upole yenye kujificha ndani ya kila anuani takatifu!. Bali huku kujulisha kwake kuna uwazi uliofanya sanaa zote na elimu pamoja na kanuni zake zote, zinashindwa kufikia yaliyomo kwenye kitabu cha ulimwengu, katika dalili za ajabu tangu zama za Adamu (a.s), hali ya kujua kwamba kitabu hicho hakijaweka wazi bado moja ya kumi ya maana ya majina na makamilifu ya kiungu. Kama hivi basi fundi mwenye utukufu, uzuri na ukamilifu ambaye amesimamisha kasri hii ya ajabu ikiwa ni maonesho ya kuona uzuri na ukamilifu wake wa kimaanawy na kuonesha, hekima yake inahitajia kumjulisha mmoja wa wenye utambuzi katika Ardhi maana ya aya za kasri hilo, ili maana yake yasibakie kuwa ni mchezo yasiyo na manufaa kwao. Na ampandishe katika ulimwengu wa juu ambao ni vyanzo vya maajabu yaliyomo kwenye kasri hilo, na hazina za mavuno yaliyomo. Na kumnyanyua hadi daraja ya juu iliyo juu ya viumbe wake wote na kumpa utukufu wa kukaribia hadhara yake na kumtembeza katika limwengu za akhera akimkalifisha majukumu ili awe mwalimu kwa waja wake wote. Hali ya kuwalingania kwenye ufalme wa Uungu wake. Akiwafikishia kazi za mambo ya kuridhiwa na Uungu wake. Akiwafasiria aya zake za kimaumbile kwenye kasri. Na mifano kama hiyo ya majukumu mengine ambayo Allah (s.w) hubainisha kwayo kwa walimwengu wote, fadhila za mteule na ukubwa wa cheo chake kwa nishani alizomvika za miujiza, na awafundishe kwa Qur’an tukufu kwamba yeye ni mfikishaji mkweli na mkalimani mwaminifu. Na kama hivi, tumebainisha hekima chache za Miiraji kati ya hekima zake nyingi, na hiyo kwa mwanga wa mfano huu, na ni juu yako kupimia hekima zilizobaki kwa mfano wake. Mfano wa pili: Mtu mjuzi akitunga kitabu cha muujiza ambapo kila ukurasa wa kitabu hicho umesheheni hakika za yaliyomo kwenye vitabu mia moja, kila mstari wa kitabu hicho unabeba maana nyororo ya yaliomo kwenye kurasa mia moja, na kila neno lake linabeba hakika zilizomo kwenye mistari mia moja, na kila herufi yake inaelezea maana ya yaliomo kwenye maneno mia moja. Maana yote ya kitabu hicho na hakika zake zote vimekuwa, vinaashiria katika makamilifu ya kimaanawy ya mwandishi huyo wa ajabu wa muujiza na vinaelekea upande wa makamilifu hayo. Jambo likiwa hivi, hapana shaka basi kwamba huyo mwandishi wa muujiza hakiwachi kitabu chake hiki cha muujiza bila faida na wala hafungi milango ya hazina hii isiyomalizika, bali ni muhali kuiacha bure bila lengo nyuma yake. Kwa hiyo atawaelimisha watu maalum maana ya kitabu hicho, ili kisibakie kitabu hicho cha thamani chenye kupuuzwa bila maana, na ili yadhihiri makamilifu yake yaliyojificha, na kupata njia yake kuelekea kwenye ukamilifu, na kushuhudisha uzuri wake wa kimaanawy ushuhudiwe ili apendwe na kupendezeshwa mwenyewe, yaani atamjulisha mmoja misamiati ya kitabu hicho, kwa maana yake yote na hakika zake akimsomesha somo kwa somo kutokea ukurasa wa mwanzo humo hadi ukurasa wa mwisho. Hadi amtunuku shahada juu ya hilo. Na kama hivi, mtia sura mzuri (s.w), ambaye ameandika viumbe hivi kudhihirisha makamilifu yake, na kuweka wazi uzuri wake na hakika za majina yake matakatifu, ameviandika kwa uandishi wa ajabu, hakuna ajabu zaidi ya hiyo, kwani vyote vilivyomo bila ya mpaka katika pande zilizopo, vinajulisha juu ya majina yake mazuri na sifa zake tukufu na makamilifu yake ya hali zote na kuyaelezea. Na katika yanayojulikana, kwamba kitabu, vyovyote kitakavyokuwa, kama hakijulikani maana yake, kitapeperuka kama vumbi lenye kutawanywa, na thamani yake itaporomoka hadi kwenye kutokuwepo. Basi vipi kitabu kama hiki ambacho kila herufi ndani yake inabeba maelfu ya maana? Katu thamani yake haiwezi kuporomoka na haiwezi kupeperuka kama vumbi katu! Mwandishi wa kitabu hicho cha muujiza kwa vyovyote atakifundisha na kujulisha sehemu yake, kulingana na utayari wa kila kundi, ambaye mwenye uoni enevu zaidi na utambuzi jumuishi zaidi na utayari mkamilifu zaidi. Na kwa ajili ya kudurusisha mfano wa kitabu hiki na kukielimisha kiujumla na yenye kukusanya hakika zake zote, hekima inahitajia mwendo na kupita katika upeo wa hadhi ya juu, yaani inalazimu kushuhudia na mwendo kuanzia tangu mwisho wa tabaka za vilivyomo vingi, ambao ndio mwanzo wa kurasa za kitabu hiki, na kukomea katika duru ya upekee ambao ndio ukomo wa kurasa zake. Na kama hivi, unaweza kushuhudia kitu katika hekima za hadhi ya juu ya Miiraji katika mwanga wa mfano huu. Na sasa tunamgeukia kafiri ambaye yupo katika nafasi ya kusikiliza, na tusikilize yanayotembea moyoni mwake ili tushuhudie ni hatua gani ambayo amechanganyikiwa nayo. Yanayopita kwenye mawazo ni kuwa moyo wake unasema: Nimeanza kupiga hatua katika njia ya imani, lakini kuna mishkeli mitatu na magumu matatu siwezi kuitatua na kuifahamu! Kwanza: Kwa nini hii Miiraji tukufu imefanywa mahususi kwa Muhammad (s.a.w). Pili: Vipi awe nabii huyu mtukufu (s.a.w) kuwa ni mbegu ya hivi viumbe? Mnaposema: Hakika ya viumbe vimeumbwa kutokana na nuru yake na wakati huo huo yeye ndiye tunda la mwisho kabisa katika matunda ya viumbe na mwenye nuru zaidi! Maneno haya yanafidisha nini?. Tatu: Mnasema katika mliyotangulia kuyabainisha: Hakika kupanda Miiraji katika ulimwengu wa juu, hakika ilikuwa ni kwa ajili ya kushuhudia maeneo ya kazi na viwanda msingi kwa athari zilizomo ulimwenguni, na kwa ajili ya kuona hazina na ghala ya matokeo ya matendo, maneno haya yana maana gani? Mushkeli wa kwanza Jibu: Hakika mushkeli wenu huu wa kwanza, umetatuliwa kwa upambanuzi katika maneno ya thelathini na tatu ndani ya kitabu (Maneno), isipokuwa sisi hapa tutaashiria kwa ufupi tu kwa sura ya faharisi ya muhtasari ya makamilifu ya Mtume (s.a.w), na dalili za unabii wake, na kwamba yeye ndiye Mstahiki wa Miiraji hii tukufu. Kwanza: Hakika vitabu vitakatifu, Taurati, Injili na Zaburi vina bishara za unabii wa Mtume Mtukufu (s.a.w), na ishara kwa hilo, pamoja na kukutana na upotoshaji katika zama zote, na katika zama zetu hizi Mwanazuoni mhakiki Husein Al-Jisri ametoa bishara mia moja na kumi na kuzithibitisha katika kitabu chake kinachoitwa (Al-Risalat al-Hamiidiyya). Pili: Imethibiti kihistoria na kupokewa kwa masimulizi sahihi, bishara nyingi walizobashiri makuhani mfano wa makuhani wawili mashuhuri: Shikki na Sateeh. Muda mfupi kabla ya kupewa utume mtume (s.a.w) na wamepasha habari kuwa yeye ni nabii wa zama za mwisho. Tatu: Kilichotokea usiku wa kuzaliwa kwake (s.a.w) kama kuanguka masanamu ndani ya Al-Kaaba na kupasuka vibaraza vya kisra na mfano wa hayo katika mamia ya Irhaasati na ya kufurutu ada mashuhuri katika vitabu vya historia. Nne: Kutoka maji kati ya vidole vyake vitukufu na kulinywesha jeshi kwa maji hayo, na kunung’unika kwa shina kavu lililokuwa katika msikiti wa Mtume (s.a.w) kwa ajili ya kutengana nalo na kutoa sauti ya kilio mbele ya kundi kubwa la masahaba watukufu, na kupasuka kwa mwezi kama ilivyoeleza aya tukufu: وَانشَقَّ الْقَمَرُ Na mfano wa hiyo katika miujiza yenye kuthibiti mbele ya wanazuoni wenye kuhakiki na ambayo inafikia elfu imethibitishwa na vitabu vya Sira na historia. Tano: Wameafikiana maadui na wapenzi kwa lisilo na shaka ndani yake kwamba tabia njema anazojipamba nazo nabii Muhammad (s.a.w) ni katika daraja za juu sana, na mambo mazuri aliyosifika nayo katika da’wa yake ni katika ngazi za juu sana, hayo yanashuhudiwa na kuishi kwake na watu na mwenendo wake, na kwamba sharia yake maridadi inajumuisha mambo mazuri yaliyo kamilika mno, hayo yanashuhudiwa na tabia njema katika dini yake nyoofu. Sita: Tumeashiria katika ishara ya pili ya (Neno la kumi) kwamba Mtume mtukufu (s.a.w) ndiye ambaye aliyeonesha kiwango cha juu sana cha uja na chenye hadhi ya juu kabisa katika utumishi mtukufu katika dini yake kwa kuitikia utashi wa Allah (s.w) katika kudhihiri kwa Uungu wake kwa muktadha wa hekima. Ni kama hivyo, iko wazi – yeye ni mjulishaji mtukufu zaidi juu ya uzuri katika ukamilifu wa hali zote wa Muumba wa ulimwengu na mtambulishaji bora zaidi aliyeitikia utashi wa Allah (s.w) katika kudhihirisha uzuri huo kupitia mjumbe kama hekima na hakika vinavyohitajia hilo. Na kwamba yeye yuko hivyo – kama inavyoshuhudiwa – mjulishaji mtukufu zaidi juu ya ukamilifu wa ufundi wake katika uzuri wa hali zote wa Mtengenezaji wa Ulimwengu, na kwa ulingano mtukufu zaidi na sauti yenye mvuto zaidi, akaitikia utashi wa Allah (s.w) katika kuleta macho kuangalia ukamilifu wa ufundi wake na kuutangaza. Na kwamba vivyo hivyo – kwa dharura – yeye ni mkamilifu zaidi aliyetangaza kuliko wote ngazi zote za Tawhiid, akaitikia utashi wa Bwana mlezi wa walimwengu katika kutangaza upekee katika tabaka za wingi wa viumbe. Na yeye yuko hivyo – kwa ulazima – ni kioo chenye kuonesha zaidi na kisafi mno kwa kuakisi mazuri ya uzuri wa Mmiliki wa ulimwengu na yaliyo laini ya uzuri wake uliotakasika na upungufu – kama zinavyoashiria hilo athari zake za kupendeza – na yeye ndiye mbora aliye mpenda na kumpendezesha, akitikia utashi wake (s.w) katika kuona uzuri huo mtakatifu na kumwonesha kwa kulingana na hakika na hekima. Na kwamba yeye yuko hivyo – kwa uwazi – ni mkuu zaidi ambaye ametambulisha yaliyoko kwenye hazina za ghaibu ya fundi wa ulimwengu huu, hazina hizo zilizojaa maajabu mno ya miujiza na johari za thamani mno, na yeye ni mbora aliyetangaza hayo na kuyasifia, akaitikia utashi wake, katika kudhihirisha hazina hizo zenye kufichwa. Na kwamba yeye yuko hivyo – kwa uwazi – ni mwelekezi mkuu wa Qur’an tukufu kwa majini na wanadamu bali kwa wenye roho na malaika, na mtukufu aliyebainisha maana za athari za mtengenezaji wa viumbe hivi ambavyo amevipamba kwa mapambo mazuri sana na kuwaweka humo wenye Utambuzi katika viumbe vyake ili watazame vema na kutafakari na kuzingatia, akaitikia utashi wake (s.w) katika kubainisha maana ya athari hizo na makadirio ya thamani yake kwa watu wa fikra na kushuhudia. Na kwamba yuko hivyo – kwa uwazi – ni mbora zaidi aliyefunua hakika za Qur’an kuhusu maana ya makusudio katika mageuzo ya viumbe na shabaha yake, na mkamilifu zaidi aliyefumbua fumbo la vilivyokuwepo. Nayo ni maswali magumu matatu: Nani wewe? Unatoka wapi? Na unakwenda wapi? akaitikia utashi wake (s.w) katika kufumbua talasimu (fumbo) hilo lililofumbwa kwa wenye utambuzi kupitia mjumbe. Na kwamba yeye yuko hivyo – kwa uwazi – ni mkamilifu aliyebainisha makusudio ya kiungu kwa Qur’an tukufu na mbora aliyeweka wazi njia katika anayoyaridhia mola mlezi wa walimwengu, akaitikia Utashi wake (s.w) katika kutambulisha analolitaka kutoka kwa wenye utambuzi na anayoyaridhia kwao kwa kupitia mjumbe, baada ya kuwa amejitambulisha kwao kwa kazi zake zote alizotengeneza za ajabu na kuzipendesha kwao kwa neema ghali alizowaenezea. Na yeye yuko hivyo – kwa uwazi – ni mtukufu zaidi aliyetimiza jukumu la utume kwa Qur’an tukufu, na kuitekeleza kikamilifu, katika ngazi ya hadhi ya juu na sura fasaha zaidi na mtindo mzuri zaidi, akaitikia Utashi wa Bwana Mlezi wa walimwengu, katika kugeuza uso wa mwanadamu huyu kutoka kwenye wingi na kwenda kwenye umoja na kutoka katika chenye kutoweka na kwenda kwenye cha kubaki, ni mwanadamu huyo ambaye Allah (s.w) amemuumba kuwa ni tunda la ulimwengu wote na kumpa matayarisho yenye kuenea ulimwenguni kote na akamuandaa kwa ajili ya uja wa kiujumla na akampa mtihani na hisia zenye kuelekea kwenye wingi na dunia. Na kwa kuwa kwamba watukufu zaidi kati ya vilivyomo ni wenye uhai, na wabora zaidi kati ya walio hai ni wenye utambuzi, na watukufu zaidi kati ya wenye utambuzi ni binadamu wa kweli wakamilifu, kwa hiyo yule ambaye ametekeleza katika wanadamu wenye kutukuzwa majukumu yale yaliyotajwa huko nyuma na kuyapa haki yake, hapana shaka kwamba huyo atapandishwa – Miiraji tukufu – atakuwa mkabala wa pinde mbili – au karibu zaidi, na atagonga mlango wa furaha ya milele na atafungua hazina za rehema kunjufu, na ataona hakika za imani ya ghaibu kuona kwa kushuhudia, na nani atakuwa huyo kama si huyo Nabii mkarimu (s.a.w)?. Saba: Mwenye kuzingatia ataona katika hivi vilivyotengenezwa vilivyotawanywa katika ulimwengu kwamba ndani yake kuna utendaji wa uzuri katika ukomo wa uzuri, na tendo la upambaji katika ukomo wa kupendeza, basi ni jambo la dhahiri kwamba mfano wa upendezeshaji huu na upambaji huu vinajulisha kuwepo utashi wa kupendezesha na kukusudia kupamba kwa fundi wa hivyo vilivyotengenezwa. utashi huo mkali unajulisha kwa vyovyote kuwepo kwa utashi wenye nguvu wa hadhi ya juu, na mahaba matakatifu kwa fundi huyo kwa ufundi wake. Kwa hiyo ni katika yaliyo wazi kuwa kiumbe mpendwa kabisa mbele ya muumba mkarimu ambaye anapenda vitu vyake alivyovitengeneza ni yule anayesifika kwa jumla ya sifa hizo, na anayedhihirisha katika dhati yake sifa laini za ufundi kikamilifu, na anayezitambua na kuzitambulisha, na anayependezesha nafsi yake na kutambulisha – kwa mshangao na kuthamini – uzuri wa vilivyotengenezwa vinginevyo. Basi nani ambaye amejaalia mbingu na Ardhi inagonga sauti ya mwangwi (Subhanallah, Maashaallah, Allahu Akbar) katika dhikiri za kushangaa kwa kupendezwa na tasbihi na takbira kwa yule anayepangilia vilivyotengenezwa kutokana na sifa za pekee zinazovipamba na mazuri ya kuvipendezesha na yalio nyororo na makamilifu yanayovinawirisha? Na ni nani ambaye ametetemesha kwa naghama za Qur’an tukufu ikavutika bara na bahari kuielekea katika shauku kubwa kutokana na kuhisi uzuri na kuthamini katika kutafakari na kuitangaza, katika dhikiri na tahalili? Ni ipi itakayo kuwa hiyo dhati yenye kubarikiwa kama siyo Muhammad mwaminifu (s.a.w)?. Na basi mfano wa nabii huyu mtukufu (s.a.w) ambaye katika kitanga cha mema yake huongezwa mfano wa waliofanya umma wake katika mambo mema kwa siri ya: (Sababu ni kama mtendaji). Na ambaye inaongezwa katika makamilifu yake ya kimaanawy swala ambazo umma wote unazitekeleza. Na ambaye humiminwa kwake rehema ya kiungu na mahaba yake ambayo hayapingwi na mpaka wowote, ukiachilia mbali anayoyapata katika matunda ya majukumu ya utume wake aliyoyatekeleza katika thawabu kubwa ya kimaanawy. Naam, Mfano wa nabii huyu mtukufu (s.a.w) hapana shaka kwamba kwenda kwake peponi, na kwenye Sidrat al-Muntaha, na katika kiti cha enzi kitukufu, basi na kuwa ukaribu wa upinde na mshale au karibu zaidi, hakika ni ndio ukweli wenyewe, na hakika yenyewe halisi, na hekima tupu. Mushkeli wa pili Ewe uliyekaa katika nafasi ya kusikiliza! hakika hii uliyoifanya kuwa ni mushkeli yenyewe ina kina kirefu, nayo ni ya juu yenye hadhi kiasi akili haiifikii, bali haiikaribii, na pamoja na hivyo huonekana kwa nuru ya imani. Na sisi hapa tutajaribu kukaribisha kitu kwenye fahamu katika hakika hiyo ya juu kwa baadhi ya mifano, ambayo inasaidia hilo, nayo ni kama ifuatavyo: Vikiangaliwa hivi viumbe kwa mtazamo wa hekima, vinadhihiri kana kwamba ni mti mkubwa na katika maana yake, kama ulivyo mti una matawi, majani, maua na matunda, basi katika ulimwengu wa chini, ambao ni upande wa mti wa uumbaji, inashuhudiwa vilevile kwamba chembe chembe ni sawa na matawi yake, na mimea na miti ni sawa na majani yake, na wanyama kana kwamba ni maua yake, na watu kana kwamba ni matunda yake. Basi kanuni ya kiungu inayopita kwa miti inalazimu kupita vilevile katika mti huu mkubwa, na hii kwa muktadha wa jina la Allah (s.w), (Al-Hakiim). Kwa hiyo kulingana na hekima ni kuwa mti huu wa uumbaji unatokana vile vile na mbegu, na iwe hiyo mbegu ni yenye kukusanya vielelezo na misingi ya limwengu nyinginezo ukiachilia mbali kubeba kwake ulimwengu wa kimwili; kwa sababu mbegu ya kiasili ya viumbe inayokusanya maelfu ya limwengu na chanzo chake haiyumkiniki kuwa ni maada isiyo na uhai katu. Na kwa kuwa hakuna mti usio kuwa na mti wa aina za viumbe ulioutangulia, basi hakika maana na nuru ambayo ni sawa na chanzo na mbegu yake imekuwa mwili kwa tunda katika mti wa viumbe na kuvikwa mavazi ya tunda, na hii ni kwa sababu mbegu haiwi tupu bila nguo daima, kwa hiyo madhali haikuvaa vazi la tunda mwanzoni mwa uumbaji, italivaa mwishoni. Na madhali mwanadamu ni hilo tunda, na kwamba bora ya matunda ya sampuli ya wanadamu na mwenye nuru zaidi na mzuri zaidi mkuu na mtukufu zaidi na mpole zaidi na mwenye manufaa zaidi ni Muhammad (s.a.w), kama ilivyotangulia kuthibitishwa, ambaye ameleta mtazamo wa jumla ya viumbe kwa fadhila zake, na ambaye amedhibiti nusu ya mtazamo wa nusu ya Ardhi na moja ya tano ya wanadamu katika dhati yake iliyobarikiwa na kukusanya mitazamo ya walimwengu katika mazuri yake ya kimaanawy kwa mahaba, kutukuzana na kupendezwa, hapana budi kwamba nuru ambayo ni mbegu ya kuundika kwa viumbe itakuwa mwili katika dhati yake (s.a.w) na itadhihiri kwa sura ya tunda la hitimisho. Ewe msikilizaji! usiweke mbali uumbaji wa viumbe hivi vya ajabu vikubwa kutokana na kiini cha kisehemu cha mwanadamu. Hakika Mweza mwenye utukufu ambaye anaumba mti mkubwa wa msonobari, kana kwamba ni ulimwengu kwa dhati yake, kutokana na kokwa yake ndogo, vipi asiumbe, au ashindwe kuumba viumbe kutokana na nuru ya Muhammad (s.a.w)?. Naam, hakika mti wa viumbe unashabihiana na mti wa Tuba wa peponi, shina lake na mizizi yake imekwenda mbali kwenye ulimwengu wa juu, na matawi yake na matunda yake yako chini chini kuelekea ulimwengu wa chini, kwa hiyo kuna uzi wenye uhusiano wa kinuru kuanzia katika kituo cha tunda chini hadi katika kituo cha kokwa ya asili. Kwa hiyo Miiraji ya Mtume ni sura na mfuniko wa uzi wa uhusiano huo wa kinuru, ambapo mtume mtukufu (s.a.w) amefungua njia hiyo na kupanda humo kwa uwalii wake, na amerejea kwa utume wake, na kuacha mlango ukiwa wazi, ili waupite mawalii wa umati wake ambao wanamfuata kwa kupita kwa roho na moyo, hivyo kupanda katika njia hiyo ya kinuru chini ya vivuli vya Miiraji ya kiutume, na kupanda humo hadi katika makamo ya juu kila mmoja kulingana na utayari wake na upokeaji wake. Na tumetangulia kuthibitisha kwamba fundi mtukufu ameanzisha viumbe hivi na kuvipamba kana kwamba ni kasri la ajabu kwa ajili ya makusudio na shabaha tukufu, basi Mtume Mtukufu (s.a.w) ambaye yeye ndiye Mhimili wa makusudio hayo, na ndio uwanja wake, hapana budi kuwa ndio mahali pa uangalizi wake (s.w) kabla ya kuumba viumbe, na awe ni wa kwanza aliyepata udhihirisho wake (s.w), kwa hiyo yeye ni wa kwanza kimaana na wa mwisho kwa uwepo. Na kwa kuwa Mtume Mtukufu (s.a.w) ni mkamilifu zaidi wa matunda ya uumbaji na uwanja wa thamani ya matunda yote, na mhimili wa kudhihiri kwa makusudio yote, inalazimu iwe nuru yake ndio ya kwanza iliyopata udhihirisho wa uumbaji. Mushkeli wa tatu Hakika hii ina wasaa kiasi cha kutoweza akili zetu za kibinadamu zilizo finyu kuweza kuifahamu, lakini tunaweza kuitazama kutokea mbali. Naam, hakika mashine za kimaanawy za ulimwengu wa chini, na kanuni zake za kiujumla, hakika ziko katika ulimwengu wa juu. Na kwamba matokeo ya matendo yasiyokuwa na mpaka katika viumbe ambavyo vinaishi ardhini, na hivyo vyenyewe kwa dhati yake ni mkusanyiko wa kazi zilizotengenezwa, na vivyo hivyo matunda ya matendo ambayo wanayatenda majini na watu, vyote hivyo hupatikana katika limwengu za juu vilevile. Hata ishara za Qur’an tukufu na muktadha wa jina la Allah “Al-Hakiim" na hekima inayoingia katika viumbe, pamoja na shahidi za mapokezi mengi na alama zisizo na mipaka, zinajulisha kwamba matendo mema huchukua sura ya matunda ya peponi na matendo maovu huchukua umbo kwa sura ya zaqqumi ya jahanamu. Naam, hakika vilivyomo vingi vimeenea juu ya uso wa Ardhi ueneaji mkubwa, na mitindo ya uumbaji imetanzuka kwa kiasi kikubwa, kwa kiasi kwamba makundi ya viumbe na sampuli za vilivyotengenezwa ambavyo hubadilika na kwa vitu hivyo ardhi hujazwa na kuachwa tupu yanapita sana vilivyotengenezwa vilivyoenea katika ulimwengu wote. Na kama hivi, vyanzo vya wingi huu na vijisehemu na madini yake ya msingi, hapana budi kuwa ni kanuni za kiujumla, na midhihirisho ya kiujumla ya majina mazuri, kwa kiasi kwamba mandhari ya kanuni hizo za kiujumla na midhihirisho hiyo ya kiujumla na majina hayo yenye kuzungukia kila kitu, ni mbingu, ambazo ni rahisi (sio changamani) na ni safi kwa kiasi fulani na ambayo kila moja kati ya hizo ni katika nafasi sawa na Arshi ya ulimwengu, na dari yake, na kituo cha usarifu. Hata moja ya limwengu hizo ni pepo ya Maawa ambayo ipo mbele ya Sidrat al-Muntaha. Mpashaji wa kweli amepasha habari (s.a.w) ambayo maana yake: Hakika tasbihati na tahmidati ambazo zinatajwa ardhini hufanyika mwili kwa sura ya matunda ya peponi. Basi nukta hizi tatu zinatubainishia kwamba hazina za yaliomo ardhini katika matokeo na matunda yapatikanayo kwa hakika yapo huko, na kwamba mavuno yake yanaelekea na kupelekwa huko. Usiseme – ewe msikilizaji – vipi inakuwa “Alhamdulillah“ ambayo ninaitamka hewani iwe ni tunda peponi? Kwa sababu wewe unapotamka neno zuri na hali ya kuwa uko macho mchana inaweza kuonekana kwako katika njozi kwa sura ya tufaha tamu na unalila. Na vilevile maneno yako mabaya mchana unaweza kuyameza ndotoni kikiwa ni kitu kichungu cha kumezwa kwa taabu. Ukimsengenya mtu yeyote unatahamaki kuwa unalazimishwa kumla maiti!. Kwa hiyo maneno yako mazuri au mabaya ambayo unayatamka katika ulimwengu wa dunia ambao ni ulimwengu wa kulala, utayala katika ulimwengu wa Akhera ambao ni ulimwengu wa kuwa macho, na kama hivi haitakiwi kukanusha kula kwako huku.
Nini matunda ya Miiraji na faida zake? Jibu: Miiraji hii kuu ambayo ni mti wa Tuba wa kimaanawy ina faida kubwa nyingi, na matunda manono yapo hadi chini kiasi zaidi ya matunda na faida mia tano. Isipokuwa tutataja hapa matano tu kati ya hayo kwa njia ya mfano: Tunda la kwanza Ni kuona hakika za nguzo za Imani, kuona kwa jicho hasa, yaani kuona malaika, pepo na Akhera, bali hata kuiona dhati tukufu, kuona huku na kushuhudia kwa hakika kumeipa viumbe wote na wanadamu kwa sifa maalum hazina kubwa isiyokwisha, na nuru ya kiazali haififii, na zawadi ya milele ya thamani, kwani nuru hiyo imevitoa viumbe vyote katika inayodhaniwa kwamba vinaporomoka katika hali za kutoweka, kuondoka vya migongano na ya machungu, na kuvidhihirisha katika hakika yake kwamba ni maandishi ya kiungu Mtegemewa na kila kitu, na barua za kiungu Mola mlezi zilizo takatifu, na vioo vizuri vinaakisi uzuri wa upekee, jambo lililoingiza furaha katika nyoyo za wenye utambuzi wote bali limewafurahisha viumbe wote. Na kama hiyo nuru ilivyowatoa viumbe kutoka kwenye hali za maumivu za kudhaniwa, imemtoa mwanadamu asiyejiweza mbele ya maadui wasio na mpaka, fukara wa mahitajio mengi kutokana na hali za kutoweka za kupotea anababaika nazo. Ikaweka wazi sura yake ya hakika kwamba ni muujiza katika miujiza ya uweza wa Allah (s.w), na kiumbe wake ambaye yuko katika umbo bora kabisa, na nakala jumuishi ya barua zake za kiungu, na msemeshwa mtambuzi wa Mfalme wa azali na milele na mja wake mahususi, na mwenye kuhisi makamilifu yake na mwandani wake mpendwa, na mwenye kupendezwa kwa uzuri wake mtakatifu na mpendwa, na mgeni mwenye kukirimiwa mbele yake na mwenye kupitishwa kuingia pepo yake ya kubaki milele. Ee, furaha kubwa iliyoje isiyo na ukomo! Na shauku kubwa isiyo na mwisho nuru hii humpa kila mwenye kujizingatia kuwa yeye ni mtu. Tunda la pili Nalo ni kwamba ameleta misingi ya Kiislamu ikitanguliwa na (Swala). Misingi ambayo inawakilisha mambo yanayomridhisha mola mlezi wa walimwengu, Mtawala wa azali na milele. Hakika amezileta zikiwa ni zawadi na tunu nzuri kwa majini na watu wote. Hakika kuyajua hayo yanayomridhisha Mola Mlezi peke yake huamsha kwa mwanadamu mapenzi na shauku na kutazamia kutaka kuyajua kwa kiasi kisicho yumkinika kukielezea, ukiachilia mbali furaha na ukunjufu inayoleta, kwani hakuna shaka kwamba kila mwanadamu anataka kwa bidii kujua, japo kutokea mbali, yale ambayo Mfalme wake anayataka ambaye amemneemesha, na ana shauku kwa pupa ajue nini anataka kwake ambaye amempa neema zake na kumtendea wema? Na hata anapojua yanayomridhia humjaa furaha kubwa na kumuenea ridhaa na utulivu, bali hata anatamani kutoka moyoni mwake wote kwa kusema: “Ee laiti kungekuwapo na mkaa kati baina yangu na mola wangu ili nijue anachokitaka kutoka kwangu, na nini anataka niwe kwake”?. Naam, hakika mwanadamu ambaye ni muhitaji sana kwa mola wake (s.w) kila wakati, na katika kila hali zake na mambo yake, na amepata fadhila zake tukufu, na neema zake enevu kiasi kisichohesabika, na yeye ana yakini kwamba vilivyopo vyote vipo katika mkono wa usarifu wake (s.w), na yanayoshamiri katika nuru ya uzuri na ukamilifu juu vilivyokuwepo, si kingine isipokuwa ni kivuli dhaifu ukilinganisha na uzuri wake na ukamilifu wake (s.w), nasema: Je, ni kiasi gani mwanadamu huyu anakuwa na shauku na pupa ya kutambua yanayomridhisha bwana Mlezi, na kutambua anachotaka kutoka kwake! huenda unathamini hili!. Basi huyo hapo Mtume Mtukufu (s.a.w) amekuja na mambo yanayomridhisha Mola Mlezi wa walimwengu na hakika ameyasikia kwa moja kwa moja kwa haki ya yakini nyuma ya pazia sabini elfu, ameyaleta hayo ikiwa ni tunda katika matunda ya Miiraji na kuyaleta yakiwa ni zawadi nzuri kwa watu wote . Naam, Hakika ya mwanadamu ambaye anataka kujua nini kinatokea mwezini? Na akienda mmoja wao huko na kurudi na kueleza yalioko huko pengine atajitolea kwa wingi kwa ajili ya habari hiyo, itamchukua tahayuri na kupendezwa kila anapotambua habari za yaliyo huko!!. Ninasema ikiwa hali ya mwanadamu ni kama hivi na habari za aliyekwenda mwezini, basi vipi itakuwa pupa yake na shauku yake kupokea habari za anaye kuja kutoka kwa Mmiliki wa ufalme mwenye utukufu ambaye mwezi katika ufalme wake sio chochote isipokuwa kama nzi anaye ruka kuzunguka kipepeo, huyo kipepeo anaruka kuzunguka taa miongoni mwa maelfu ya mataa ambazo zinaangazia mahali pake pa wageni. Naam, hakika Mtume (s.a.w) aliona mambo ya huyu mfalme mtukufu (s.w) na kashuhudia maajabu ya utengenezaji wake na hazina za rehema zake katika ulimwengu wa kubakia. Na amerejea baada ya kuona hayo na kuwasimulia watu aliyoyaona na kuyashuhudia. Kama watu hawakumsikiliza Mtume huyu mtukufu (s.a.w) kusikiliza kwa shauku na utashi na kwa utukuzo wote na kupendezwa, basi fahamu kiasi cha kujitenga kwao na akili na kuepuka kwao hekima. Tunda la tatu Hakika ameshuhudia kanzi za furaha ya milele na neema madhubuti za kudumu, na kupokea ufunguo wake, na kuuleta ikiwa ni zawadi kwa wanadamu na majini. Naam, ameshuhudia kwa jicho lake kwa Miiraji pepo ya kudumu milele, na ameona midhihirisho ya milele ya rehema ya mwingi wa rehema Mwenye kurehemu (s.w), na ametambua utambuzi kwa haki ya yakini furaha ya milele, akaleta habari njema ya kuwepo kwa furaha ya milele kwa majini na wanadamu, habari hiyo kubwa ambayo wanaadamu wanashindwa kuielezea. Wakati ambapo hali ya kudhania inamzunguka jini na mwanadamu, ambapo vyote vilivyomo vinapigwa kofi kwa makofi ya kutoweka na utengano katika dunia isiyo na utulivu, na kutiririka kwa muda na harakati za Atomu huzoazoa kwenda kwenye bahari ya kukosekana na utengano wa milele, naam, katika hali hizi za kuumiza ambazo zinatoa roho za majini na wanadamu zinawazunguka kwa kila upande, tahamaki habari hiyo ya kufurahisha inawajia, pima katika mwanga wa hili, ni kiasi gani kinacholetwa na habari hizo njema cha furaha kwa majini na wanadamu ambao wanadhani kwamba wamehukumiwa dhidi yao kunyongwa kwa milele, na kwamba hao wawili ni wenye kutoweka kabisa! kisha fahamu baada ya hapo thamani ya habari hiyo njema! Mwenye kuhukumiwa kunyongwa angeambiwa wakati akipiga hatua zake kuelekea kwenye kitanzi: (Hakika Mfalme amefanya ukarimu kwa kukusamehe, isitoshe amekupa nyumba kwake). Una nafasi ya kupata picha ya kiasi maneno haya yanavyofungua mawanda ya furaha kwa huyo aliyehukumiwa kunyongwa. Na ili uweze kupata picha ya thamani ya tunda hili na habari hii njema sana, kusanya furaha zote hizo kwa idadi ya majini na watu ili ukadirie umuhimu wa habari hiyo njema!. Tunda la nne Ni kuona uzuri wa Allah (s.w), kama alivyotunukiwa hilo mtume (s.a.w) imekuja (habari) kwamba inayumkinika kwa kila muumini kupata hilo tunda lililobaki vilevile. Kwa hili ametoa zawadi kubwa kwa majini na watu. Na huenda unaweza kukadiria kiasi cha ladha iliyomo katika tunda hilo lililotolewa zawadi na kiasi cha utamu wake na uzuri wake na ughali wake kupitia mfano huu: Hakika kila anayebeba moyo ulio hai, bila shaka anampenda mwenye kuwa na uzuri na ukamilifu na hisani, na mapenzi haya yanazidi kulingana na daraja za huo uzuri ukamilifu na hisani, hata inafikia daraja ya ashiki na kuabudu, basi mwenye nayo hayo anajitolea anachomiliki kwa ajili ya kuona uzuri huo, bali anaweza kujitolea dunia yake yote kwa ajili ya kuuona mara moja. Na tukijua kwamba uwiano wa katika vilivyokuwepo katika uzuri ukamilifu na hisani, kuwianisha na uzuri ukamilifu na hisani yake (s.w) haufikii kuwa ving’ao hafifu kuwiana na jua lenye kuangaza. Kwa hiyo unaweza kutambua – ukiwa kweli ni Mtu – kiasi kinacholeta katika furaha ya kudumu na kiasi kinacholeta katika furaha, ladha na neema, kuwafikishwa kumuona ambaye mwenye kustahiki mapenzi bila ukomo na kumuona bila ukomo katika furaha bila ukomo. Tunda la tano Nalo ni kwamba mwanadamu – kama ilivyofahamika kutoka kwenye Miiraji – ni tunda la thamani katika matunda ya viumbe, mwenye cheo kitukufu, na kiumbe aliyekirimiwa mpendwa mbele ya Mtengenezaji Mtukufu. Tunda hili zuri mtume (s.a.w) amekuja nalo kwa Miiraji, ikiwa ni zawadi kwa majini na watu, Tunda hilo likamnyanyua mwanadamu kutoka katika kuwa kwake ni kiumbe mdogo na mnyama dhaifu na mwenye utambuzi asiyejiweza hadi makamo ya juu na ngazi ya juu, bali kwenda katika makamo ya juu mno yenye utukufu na kukirimiwa kuliko viumbe wote. Tunda hili hivyo basi limempa mwanadamu furaha ya dhati kiasi cha kushindwa kuielezea. Kwa sababu mwanajeshi mmoja akiambiwa: Umekuwa afisa wa cheo cha juu katika jeshi, kiasi gani atahisi kuwa amefanyiwa wema na shukurani yake na furaha yake na ridhaa yake itakuwaje? Haikadiriwi kwa vyovyote, wakati ambapo kiumbe dhaifu na mnyama mwenye kufikiri, na asiyejiweza mwenye kutoweka, aliye dhalili mbele ya dhoruba za kuondoka na kutengana, angeambiwa: Hakika wewe utaingia pepo ya milele na kupata neema za Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu kunjufu ya kubaki, utembee katika ufalme na falme zake ambao una upana wa Mbingu na Ardhi, na ustarehe nao kwa mapendeleo yote ya moyo katika kasi ya kufikirika na kwa upana wa roho na kutembea kwa akili, na juu ya yote haya utapata kuuona uzuri wake katika furaha ya milele. Kila mwanadamu, ambaye utu wake haujaporomoka anaweza kutambua kiasi cha furaha zinazomjaa yule ambaye anayeambiwa mfano wa maneno haya. Na sasa tunaelekea kwa yule aliyekaa katika nafasi ya usikilizaji, tunamwambia: Chana kanzu ya ukafiri, na uitupe mbali, na usikilizie kwa sikio la muumini, na uweke macho ya Mwislamu, nitakubainishia thamani ya matunda machache kupitia mifano midogo miwili: Mfano wa kwanza: Kwa mfano tuko pamoja nawe katika ufalme mpana. Kila unapoelekeza macho yako kuangalia huoni isipokuwa uadui, kila kitu ni adui yetu, na kila kitu kinadhamiria uadui kwetu, kila kilichomo humo ni kigeni kwetu hatukitambui, Na kila pembe yake imejaa majeneza yanayoamsha woga na mshangao. Na zinapaa sauti huku na huko ni sauti za maombolezo na kuomba msaada kwa mayatima na wadhulumiwa. wakati tukiwa katika majonzi na maumivu haya, ghafla mmoja anakwenda kwa mfalme wa ufalme na anakuja kutoke huko na habari njema ya kufurahisha kwa wote. Basi hapo ikiwa habari hiyo ya furaha itabadilisha vilivyokuwa vigeni kwetu na kuwa wapenzi, ikibadilisha umbo la tuliyekuwa tunamwona ni adui na kuwa katika sura ya ndugu mpenzi. Na ikidhihirisha kwetu majeneza mfu yenye kuhofisha katika sura ya waja wenye kumdhukuru Allah (s.w) wenye kumsabihi kwa kumsifu, na ikageuza kelele hizo na maombolezo hayo kuwa katika mfano wa himidi, kusifia na kushukuru. ikiwa itabadili wale maiti na upokonyaji kuwa ni ruhusa na kusamehewa kutokana na mizigo ya majukumu. Na tukiwa tunashirikiana na wengine katika furaha yao ukiachilia mbali furaha yetu. Hapo utaweza kukadiria kiasi gani cha furaha ambayo inatuenea kwa sababu ya habari hiyo njema. Na kama hivi, moja ya matunda ya Miiraji ni nuru ya Imani, dunia isingekuwa na tunda hili, yaani ikiwa viumbe vitaangaliwa kwa mtazamo wa upotevu, vilivyokuwepo hutuviona isipokuwa vigeni vya kuogofya, vyenye kukera, na vyenye kudhuru, na miili mikubwa – kama milima – kuwa ni majeneza yanayoamsha mshangao na hofu. Na muda uliopangwa ni mnyongaji anakata shingo za vilivyokuwapo na kuvitupa katika kisima cha kutokuwepo. Na sauti zote na miangwi yote si chochote isipokuwa ni kelele na maombolezo hutokana na kutengana na kutoweka. Wakati ambapo upotevu unakupa sura kama hivi ya vilivyokuwepo, tahamaki tunda la Miiraji ambalo ni hakika za Imani linanawiri vilivyokuwepo vyote na linabainisha kwamba hivyo ni wapenzi wenye kuishi kidugu, katika tasbihi na kumdhukuru Mola wao Mlezi, na umauti na kuondoka ni ruhusa kuachiliwa huru kutokana na majukumu na kupumzishwa nayo. Na hizo sauti ni tasbihati na tahmidati, na kama hivi, ukitaka kuona hakika hii kwa sura yake iliyokuwa wazi zaidi rejea (Neno la pili) kutoka katika (Maneno mafupi). Mfano wa pili: Kwa mfano kwamba tupo na wewe katika jangwa kubwa. Pepo za michanga kutoka kila upande zinatuzunguka, na giza la usiku linatuzuia kona kila kitu hata tunakaribia kutoona mikono yetu. Na njaa inatushambulia na kiu kina unguza nyoyo zetu, na hatuna msaidizi wala hatuna makimbilio. Chukua picha ya hali hii ambayo tunasukwasukwa ndani yake, tahamaki mtu mkarimu ana chana pazia ya giza kisha anakuja kwetu, akiwa na kipando cha kifahari akituletea zawadi kwetu, na kutuchukua hadi kwenye mahali panapofanana sana na ilivyo pepo. Kila kitu ndani yake kiko katika hali nzuri, na kila kitu kimetayarishwa na kukusudiwa sisi, anatutawalia yule ambaye yupo katika ukomo wa rehema, huruma na upole, na hakika ametuandalia sisi kila tunachohitaji miongoni mwa nyenzo za kula na kunywa na ninakudhania sasa unathamini kiasi gani tuwe ni wenye kushukuru fadhila ya huyo mtu mwema, ambaye ametuchukua kutoka mahali pa kukata tamaa na kuvunjika moyo kwenda mahali ambapo pote ni matumaini na furaha. Basi jangwa hilo kubwa ni hii dunia, na hivyo vimbunga vya mchanga ni harakati za Atomu na mitiririko ya wakati ambazo husukwasukwa vilivyokuwamo kwa vimbunga hivyo na huyu mwanadamu masikini. Kila mwanadamu ana hofu mwenye kuhofia yale yanayofichwa na siku zake za usoni zenye giza zenye kutisha, kama hivi upotevu unamwonesha na wala hajui atake msaada kwa nani? Na hali ya kuwa anapata picha ya njaa na kiu. Na kama hivi, kujua mambo yanayomridhisha Allah (s.w), nalo ni tunda katika matunda ya Miiraji, kunafanya hii dunia kuwa ni mahali pa wageni pa mwenyeji mwema mkarimu, na kufanya watu kuwa ni wageni waliokirimiwa, na wenye kuamrishwa na yeye katika wakati huo huo, na amewadhaminia mustakabali wenye kung’ara kama pepo ya starehe na yenye ladha kama rehema, na yenye kung’ara kama furaha ya milele. Ukiwa na picha hii na ile, wakati huo unaweza kupimia kiasi cha ladha ya tunda hilo, uzuri wake na utamu wake!. Hakika aliyekuwa katika nafasi ya usikilizaji anasema: Himidi kwa Allah (s.w) na shukurani kwa Allah shukurani elfu kwa fadhila zake nimeokoka na ukafiri, nikapita njia ya imani na tawhiidi. Na nimevuna imani Alhamdulillah. Na sisi tunamwambia: Ewe ndugu! Tunakupongeza kwa imani, na tunamwomba Allah (s.w) atujaalie tuwe katika watakaopata shufaa ya Mtume (s.a.w). اَللّٰهُمَّ صَلِّ عَلٰى مَنِ ان۟شَقَّ بِاِشَارَتِهِ ال۟قَمَرُ وَ نَبَعَ مِن۟ اَصَابِعِهِ ال۟مَاءُ كَال۟كَو۟ثَرِ صَاحِبُ ال۟مِع۟رَاجِ وَ مَا زَاغَ ال۟بَصَرُ سَيِّدِنَا مُحَمَّدٍ وَ عَلٰى اٰلِهٖ وَ اَص۟حَابِهٖ اَج۟مَعٖينَ مِن۟ اَوَّلِ الدُّن۟يَا اِلٰى اٰخِرِ ال۟مَح۟شَرِ سُب۟حَانَكَ لَا عِل۟مَ لَنَٓا اِلَّا مَا عَلَّم۟تَنَٓا اِنَّكَ اَن۟تَ ال۟عَلٖيمُ ال۟حَكٖيمُ رَبَّنَا تَقَبَّل۟ مِنَّا اِنَّكَ اَن۟تَ السَّمٖيعُ ال۟عَلٖيمُ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذ۟نَٓا اِن۟ نَسٖينَٓا اَو۟ اَخ۟طَا۟نَا رَبَّنَا لَا تُزِغ۟ قُلُوبَنَا بَع۟دَ اِذ۟ هَدَي۟تَنَا رَبَّنَٓا اَت۟مِم۟ لَنَا نُورَنَا وَاغ۟فِر۟لَنَا اِنَّكَ عَلٰى كُلِّ شَى۟ءٍ قَدٖيرٌ وَ اٰخِرُ دَع۟وٰيهُم۟ اَنِ ال۟حَم۟دُ لِلّٰهِ رَبِّ ال۟عَالَمٖينَ Nyongeza Ya
Muujiza Wa Kupasuka Kwa Mwezi بِسْمِ اللّٰهِ الرَّحْمٰنِ الرَّحِيمِ اِق۟تَرَبَتِ السَّاعَةُ وَ ان۟شَقَّ ال۟قَمَرُ وَاِن۟ يَرَو۟ا اٰيَةً يُع۟رِضُوا وَ يَقُولُوا سِح۟رٌ مُس۟تَمِرٌّ Hakika ya wanafalsafa wa kimaada, na wanaowaiga kiupofu, wanataka kufuta na kufunika muujiza wa kupasuka kwa mwezi wenye kung’ara kama mwezi wa badri, wanaamsha dhana potofu kuhusu jambo hilo, kwa kuwa wanasema: (Ingekuwa kupasuka kwa Mwezi kumetokea kweli ulimwengu ungejua hilo, na vitabu vyote vya historia vingelitaja jambo hilo!). Jibu: Hakika kupasuka kwa mwezi ni muujiza wa kuthibitisha kwa utume, umetokea mbele ya wale ambao walisikia da’wah na kuikanusha, na ilitokea usiku, katika wakati ambapo umeenea mghafala, na limedhihirishwa kwa muda mfupi, ukiachilia mbali kutofautiana Matlai na kuwepo kwa mawingu na mfano wa hivyo katika vizuizi mbali mbali vinavyozuilia mwezi kuonekana. Hali ya kujua kwamba kazi za kufuatilia anga na nyenzo za ustaarabu wakati huo havikuwa vimeenea, kwa hiyo hailazimu kuona watu wote kupasuka kwa mwezi, kila mahali, na hailazimu vilevile kuingia katika vitabu vya historia. Sasa sikiliza nukta tano tu kati ya nyingi kati ya hizo, zitatokomeza kwa idhini ya Allah (s.w) mawingu ya dhana ambazo zimegubika uso wa muujiza huu wa dhahiri: Nukta ya kwanza: Hakika ukaidi wa makafiri katika zama hizo ni wenye kujulikana na ni mashuhuri kwa historia, wakati Qur'an ilivyotangaza: وَانشَقَّ الْقَمَرُ Na Mwangwi wake kufika angani, hakuthubutu yeyote katika makafiri, na hali ya kuwa wao wanapinga Qur’an, kuikadhibisha aya hii tukufu. Yaani kukanusha kutokea kwa tukio hilo. Kwa sababu isingekuwa tukio limetokea kiuhalisia wakati huo, na halikuwa limethibiti kwa hao makafiri, wangejitokeza kwa nguvu ili kubatilisha madai ya utume, na kumkadhibisha Mtume (s.a.w). Wakati ambapo vitabu vya historia na sira havikunakili chochote katika kauli za makafiri kuhusu kukanusha kwao kutokea kwa kupasuka mwezi, isipokuwa yale yaliyobainishwa na aya: وَيَقُولُوا سِحْرٌمُّسْتَمِرٌّ Nayo kwamba wale walioshuhudia muujiza katika makafiri walisema: Huu ni uchawi tumeni watu waende kwa watu wa mbali mkatazame je, waliona hilo au hapana?. Na asubuhi ilipofika misafara kutoka Yemen iliwasili na mingineyo wakawauliza, wakawaeleza: Kwamba wao wameona mithili ya hivyo. Wakasema: “Hakika Uchawi wa yatima wa Abu Talib umefika mbinguni!” . Nukta ya pili: Wamesema wengi wa wakubwa wa Elimu ya Al-Kalam, mfano wa Saad Attaftazaany kuwa: Kupasuka kwa mwezi ni Mutawatir, mfano wa kumiminika maji kati ya vidole vyake vitukufu (s.a.w) na kunywa jeshi maji hayo, na mfano wa kulia kwa shina kutokana na kutengana kwake na Mtume (s.a.w) ambalo alikuwa akiegemea wakati wa hutuba, na kusikia kilio chake kundi la masahaba, yaani tukio wamelinakili kundi kubwa kutoka kwa kundi kubwa ni muhali kulingana kwao juu ya uongo. Tukio ni la mutawatir kwa namna ya kukinaisha kama kudhihiri kwa nyota kabla ya miaka elfu na kama kuwepo kwa kisiwa cha Serandib ambacho hatujakiona. Na kama hivi unaona kwamba kuamsha shaka kuhusu suala hili la kukinaisha na mfano wake katika masuala yaliyoshuhudiwa kwa macho dhahiri hakika ni upumbavu na uzuzu, kwani inatosha katika matukio hayo kwamba hayo ni katika yamkini na wala sio muhali. Kwa kujua kwamba kupasuka kwa mwezi ni yamkini kama kupasuka kwa Mlima kwa volkeno. Nukta ya tatu: Hakika muujiza huja kwa ajili ya kuthibitisha madai ya utume, na sio kuwalazimisha kuamini kwa njia ya kuwakinaisha wakanushaji. Kwa hiyo inalazimu kuudhihirisha kwa wale waliosikia madai ya utume, kinachowafikisha katika kukinai na kutulia juu ya ukweli wa utume. Ama kuudhihirisha mahali pote, au kuudhihirisha kwa namna ya waziwazi kiasi watu watalazimika kukubali na kutii, hilo linakinzana na hekima ya Mwingi wa hekima mwenye utukufu, na ni tofauti vilevile na siri ya kulazimisha kwa kiungu. Kwa sababu siri ya kulazimisha kwa kiungu kunahitajia kufungua uwanja mbele ya akili bila kuinyang’anya hiari. Angekuwa muumba mkarimu ameacha muujiza wa kupasuka kwa mwezi umebaki kwa muda wa saa mbili, na kuudhihirisha kwa ulimwengu wote na kuingia ndani ya historia kama wanavyoutaka wanafalsafa, makafiri wangekuwa wanasema hakika hilo ni tukio la kifalaki la kawaida, na isingekuwa hoja ya ukweli wa Mtume (s.a.w), wala muujiza unao muhusu mtume mtukufu (s.a.w). Au ungekuwa ni muujiza wa wazi unaolazimisha akili kuamini na kuinyang’nya hiari, na wakati huo zitakuwa sawa roho za chini kama mkaa duni mfano wa Abu Jahli, na roho za juu safi kama Almasi mfano wa Abu bakr Al-Siddiq (r.a), yaani ingekuwa inapotea siri ya kulazimishwa ya kiungu. Na kwa ajili ya hili muujiza ulitokea kipindi kifupi sana, na usiku, na wakati mghafala unaenea, na ikawa tofauti za matalai na mawingu na mfano wa hayo ni vizuizi vya watu kuuona. Na haukuingia ndani ya vitabu vya historia. Nukta ya nne: Hakika ya muujiza huu uliotokea wakati wa usiku, na kipindi kifupi tu, na katika wakati wa mghafala, hawauoni watu wote bila shaka kila mahali. Bali hata ungedhihiri kwa baadhi yao, wasinge sadiki macho yao, na kama angesadiki, hakika ya tukio kama hili limepokewa kutoka kwa mtu mmoja lisingekuwa na thamani katika historia. Wanazuoni wahakiki wamejibu yaliyozidishwa katika mapokezi ya muujiza kwamba mwezi baada ya kupasuka kwake uliteremka Ardhini! Wamesema: Pengine baadhi ya wanafiki wameiingiza ziada hii ili waangushe thamani ya mapokeo na kudhalilisha hadhi yake. Kisha katika wakati huo mawingu ya ujinga yalikuwa yanagubika katika mbingu ya Uingereza, na wakati unakaribia magharibi huko Hispania, na Marekani ikiwa katika hali ya mchana kweupe, na asubuhi imeingia huko China na Japani. Na kwengineko kulikuwa na vizuizi vya kuoneka muujiza huu mkubwa, hauonekani huko. Ukijua hili basi zingatia maneno ya anayesema: “Historia ya Uingereza, China, Japani Marekani na mfano wa nchi hizo haitaji tukio hili, kwa hiyo halikutokea!”. Mzaha gani huu. Ehe, kuangamia kuwe kwa wale wanaokula makombo ya Ulaya. Nukta ya tano: Kupasuka kwa mwezi sio tukio lililotokea lenyewe, kwa misingi ya sababu za kiasili na kwa njia ya sadfa! Bali amelifanya litokee Muumba Mwingi wa hekima, Bwana Mlezi wa jua na mwezi, ni tukio lililofurutu ada ya kanuni za kimaumbile, ili kusadikisha utume wa mtume wake mpendwa (s.a.w), na kutangaza ukweli wa madai ya da’wa yake, akalidhihirisha (s.w) kulingana na hekima yake na kwa hitajio la siri ya kuongoza na kulazimisha na hekima ya kufikisha ujumbe, na ili asimamishe hoja kwa amtakaye katika wenye kulishuhudia hilo, wakati ambapo amelificha, kwa hitajio la hekima yake (s.w) na utashi wake, kwa wale ambao haikuwafikia da’wa ya nabii wake (s.a.w) katika wakazi wa maeneo mbali mbali ya ulimwengu, na akawazuia kuliona kwa mawingu na kwa tofauti za Matlai na kutokuchomoza kwa mwezi, au kuchomoza kwa jua katika baadhi ya nchi na kuangaza kwa mchana katika nchi nyingine, na kuzama kwa jua katika nyinginezo, na sababu nyingine mfano wa hizo ambazo zinapelekea kuzuilika kuonekana kwa kupasuka kwa mwezi. Muujiza huu ungedhihirishwa kwa watu wote ulimwenguni, ima kwamba ungekuwa unadhihiri kwao ikiwa ni matokeo ya ishara ya mtume mtukufu (s.a.w) na kudhihirisha kwa muujiza wa unabii wake, na wakati huo utafika katika udhahiri mno, yaani watu wote watalazimika kusadiki, yaani itanyang’anywa kwao hiari, na hapo siri ya taklifa itapotea. Wakati ambapo Imani inahifadhi uhuru wa akili katika hiari wala haiipokonyi, au litadhihiri kwao kama tukio la mbingu tu, na wakati huo uhusiano wake na utume wa Muhammad utakatika na hautabakia na upekee mahususi. Muhtasari: Hakika kupasuka kwa mwezi hakuna shaka ndani yake. Hakika kumethibitishwa kwa namna ya kukinaisha. Hapa tutaashiria kutokea kwake kwa hoja sita za kukinaisha kati ya nyingi miongoni mwake, Nazo: kukubaliana kwa masahaba watukufu kwa pamoja (r.a) nao ni waadilifu na kuwafikiana kwa wanazuoni wahakiki miongoni mwa wafasiri katika kufasiri kwao: وَانشَقَّ الْقَمَرُ Na kunakili wanazuoni wote wa hadithi walio wa kweli katika mapokezi yao kutokea kwake kwa isinadi nyingi na kwa njia lukuki . Na kushuhudia watu wa Kashf na Ilhamu katika mawalii wa kweli wema. Na kusadiki viongozi wa elimu ya Al-Kalamu wabobezi pamoja na kutofautiana kwa maslaki zao na masharibu (vyanzo) zao. na kukubali kwa umma ambao haukubaliani kwa pamoja juu ya upotevu kama hadithi tukufu ilivyoeleza juu ya hilo . Yote hayo yanabainisha kupasuka kwa mwezi na kuuthibitisha kwa namna ya kukinaisha mfano wa jua katika ufasaha wake. Kwa ufupi Somo lilikuwa hadi hapa kwa jina la uhakiki wa kisayansi, ili kumlazimisha adui. Ama baada ya hili maneno yatakuwa kwa jina la hakika na kwa ajili ya imani. Uchambuzi wa kisayansi umetamka hivi. Ama hakika tunasema: Hakika mwisho wa diwani ya utume (s.a.w) na yeye ni mwezi wenye kuangaza wa mbingu ya utume, uwalii wa utumishi wake ni wa hadhi ya juu hadi katika daraja kuwa mpendwa, ukadhihirisha karama kubwa na muujiza mkuu kwa Miiraji. Yaani kwa kutembea kwa mwili wa kiardhi katika anga za mbingu za juu, na kumtambulisha kwa wakazi wa Mbingu, kwa muujiza huo ulithibitisha uwalii wake mkubwa kwa Allah (s.w) na kupendwa kwake kwa dhati na hadhi yake ya juu kwa wakazi wa mbingu na hadhara ya juu. Hali kadhalika Allah (s.w) alipasua mwezi uliotundikwa Mbinguni na wenye kufungamana na Ardhi kwa ishara kutoka kwa mja wake akiwa Ardhini, akadhihirisha Muujiza wake huu, kuthibitisha utume wa huyo Mja mpendwa, Mpaka akawa (s.a.w) kama vipande viwili vyenye kutoa nuru kwa mwezi, alipaishwa hadi katika anga za makamilifu kwa mbawa mbili za uwalii na utume za nuru, hata akafika ukaribu wa pinde mbili au karibu zaidi na akawa ni fahari ya wakazi wa Mbingu kama alivyo kuwa ni fahari kwa wakazi wa Ardhi. عَلَيْهِ وَعَلٰى آلِهِ الصَّلَاةُ وَالتَّسْلِيمَاتُ مِلْاَ الْاَرْضِ وَالسَّمٰوَاتِ سُبْحَانَكَ لَاعِلْمَ لَنَٓا اِلَّا مَاعَلَّمْتَنَا اِنَّكَ اَنْتَ الْعَل۪يمُ الْحَك۪يمُ اَللّٰهُمَّ بِحَقِّ مَنِ انْشَقَّ الْقَمَرُ بِاِشَارَتِهِ اجْعَلْ قَلْبِي وَقُلُوبَ طَلَبَةِ رَسَائِلِ النُّورِ الصَّادِقِينَ كَالْقَمَرِ فِي مُقَابَلَةِ شَمْسِ الْقُرْآنِ آمِينَ آمِينَ Inahusu Miiraji ya Mtume Dirisha la Thelathini na Moja

