Sözler

The Ninth Word

Source: risaleinur multilingual dataset, risale.site source · Risale-Nur multilingual research corpus
Risale reading plan
§1

بِسْمِ اللّٰهِ الرَّحْمٰنِ الرَّحِيمِ فَسُبْحَانَ اللّٰهِ ح۪ينَ تُمْسُونَ وَح۪ينَ تُصْبِحُونَ ❀ وَلَهُ الْحَمْدُ فِي السَّمٰوَاتِ وَالْاَرْضِ وَعَشِيًّا وَح۪ينَ تُظْهِرُونَ Ndugu yangu! Unauliza kuhusiana na hekima iliyomo ndani ya nyakati za swala tano tunazosali kila siku. Nitaonesha hekima yake moja tu kati ya nyingi. Ndio, kama ilivyo kila wakati wa swala unaashiria mwanzo wa mageuzi muhimu, basi pia kila wakati ni mfano wa kioo kinacho akisi matumizi ya Kiungu pamoja na neema zake zilizoenea kila sehemu kwa kule kutumika kwake. Kwa hivyo, katika nyakati hizo, kumeamrishwa kumtukuza na kumsifu zaidi Mwenye uwezo wote, na kumsifu na kumshukuru zaidi kwa neema zote zisizohesabika zilizolimbikizana baina ya kila moja ya nyakati hizo, na hii ndio maana ya swala za faradhi. Ili kupata ufahamu wa maana ya ndani zaidi, sikiliza nukta tano zifuatazo pamoja na nafsi yangu.

§2

Maana ya swala ni kufanya utukuzaji, kusifu na kumshukuru Allah (s.w), yaani kusema “Ametakasika Allah” kwa maneno na vitendo mbele ya utukufu na fahari ya Allah, ni kumtukuza, kumuabudu na kutangaza “Allah ni Mkubwa Zaidi” kwa njia ya maneno na vitendo mbele ya ukamilifu Wake, ni kumtukuza na kumuadhimisha Yeye. Na kusema “Kila sifa njema anastahiki Allah” kwa moyo, ulimi na mwili, ni kumpa shukurani mbele ya uzuri wake mkamilifu. Maana yake, jambo la kumpa fahari, utukuzaji na kumsifu ni mbegu za swala, ndio maana zipo katika kila kipengele cha swala, katika matendo na maneno yote. Ndio pia sababu ya mafungu hayo ya maneno yaliyobarikiwa kurudiwa mara thelathini na tatu kila moja baada ya swala, ili kuimarisha na kurudiarudia maana zake. Maana ya swala inathibitishwa katika makala hizi fupi.

§3

Maana ya ibada ni hii, kuwa mja anaona makosa yake, udhaifu, umaskini, na anamsujudia Allah kwa mapenzi na kustaajabia ukamilifu wa mmiliki, rehema za Allah, na uwezo wa Mwenye Kuombwa Milele. Inamaanisha, kama mamlaka yanavyotaka ibada na utii, ndivyo pia utukufu wa kimamlaka unavyotaka kuwa mja akiri makosa yake kwa kuomba msamaha na kwa kutukuza na kutamka “Utukufu ni wa Allah” kutangaza kuwa Mola wake ni msafi na ametakasika dhidi ya upungufu wowote, na ameepukana mbali na dhana potovu za wapotovu na ameepukana na makosa yote ulimwenguni. Pia, uwezo kamili wa mamlaka unahitaji kwamba kwa kuufahamu udhaifu wake na wa viumbe wengine, mja anatangaza “Allah ni Mkubwa Zaidi” katika kustaajabia na kupendezwa na ukubwa wa kazi za Mwenye Kuombwa Milele, na huku akisujudu kwa unyenyekevu mkubwa, anaomba hifadhi kwake na kumtumaini Yeye. Pia hazina ya milele ya rehema Yake inahitaji kuwa mja ajulishe haja yake na haja za viumbe wote kwa ulimi wa kuomba na kufanya dua, na atangaze neema na zawadi za Mola wake Mlezi kwa kutamka shukrani na sifa na kusema “Kila sifa njema ni za Allah”. Maana yake, maneno na vitendo vya swala vinajumuisha maana hizi na zimewekwa kwa upande wa Uungu.

§4

Kama ilivyo kwamba mwanaadamu ni mfano katika mfano mdogo wa ulimwengu mkubwa na Sura al-Fatiha sampuli inayong’aa ya Qur’an ya Mungu Mweza, basi ndivyo swala za faradhi zilivyo kielelezo cha ufahamu na chenye kutoa nuru katika namna zote za ibada na ramani tukufu inayoashiria vivuli vyote vya ibada za matabaka yote ya viumbe.

§5

Mshale wa sekunde, mshale wa dakika, mshale wa saa na mshale wa siku wa saa inayohesabu wiki inaangaliana, ni mfano wa mtu kwa mwingine, na kufuatana mmoja na mwingine. Halikadhalika, kubadilika usiku na mchana, ambayo ni kama sekunde za dunia hii – saa kubwa ya Allah (s.w) – na miaka inayohesabu dakika zake, na hatua za maisha ya mwanadamu inazohesabu saa, na vipindi vya muda wa kuishi duniani vinavyohesabu siku hutazamana, ni mifano ya kila kimoja kuhusika na kingine, kufanana na kukumbukana. Kwa mfano: Wakati wa Fajr, asubuhi ya mapema: Saa hii mpaka mawio inafanana na kuleta akilini majira ya mapema ya kuchipua, kitambo cha utungaji mimba katika tumbo la uzazi la mwanamke, na siku ya kwanza kati ya sita za kuumbwa kwa mbegu na ardhi, inakumbusha matendo ya kiungu yaliyomo humo. Wakati wa Dhuhr, baada tu ya jua la utosi: Hii inashabihiana na kuashiria katikati ya majira ya joto, na katikati ya ujana, na kipindi cha kuumbwa mwanadamu katika kipindi cha uhai wa dunia, na inaleta akilini madhihirisho ya rehema na neema nyingi zilizomo humo. Wakati wa ‘Asr, alasiri: Huu ni kama majira ya kuchipua, na uzee, na wakati wa Nabii wa mwisho (s.a.w) kinachojulikana kama zama za upeo wa furaha na kukumbuka matendo ya kiungu na fadhila za Mwingi wa Rehema zilizomo humo. Wakati wa Maghrib, kuchwa kwa jua: Kwa kukumbuka kuondoka kwa viumbe wengi mwishoni mwa majira ya kupukutika majani, na mauti ya mwanadamu, na kuangamia dunia wakati wa mwanzo wa ufufuo, kwa wakati huu inatia akilini madhihirisho ya utukufu wa kiungu na unyenyekevu, na kumuamsha mwanadamu kutoka katika usingizi wake wa kughafilika. Wakati wa ‘Isha, giza la usiku. Kuhusu wakati huu, kwa kutia akilini dunia yenye giza, kufunika vitu vya dunia ya mchana kwa kifuniko cheusi, na majira ya baridi kwa kuficha uso wa dunia iliyokufa kwa utando wake mweupe, hata kazi zinazosalia za watu wanaokufa na kuondoka chini ya kizuizi cha kusahaulika, na dunia uwanja wa mtihani kufungwa milele, inatangaza upangaji wenye heshima na mkubwa wa Mwenye Utukufu wote na Mwenye Kutiisha Mwenye Nguvu. Ama kuhusu usiku, kwa kutia akilini majira ya baridi na Ulimwengu wa Kati na Kati, unamkumbusha mwanaadamu jinsi roho ya mwanadamu inavyohitaji sana rehema za Mwingi wa Rehema, na tahajjud inamjulisha jinsi nuru ilivyo muhimu sana kwa ajili ya usiku wa kaburi na giza la Ulimwengu wa Katikati, inamuonya juu ya hili, na inakumbushia neema zisizohesabika za Mpaji wa Kweli, inatangaza namna anavyostahiki kusifiwa na kupewa shukrani. Na asubuhi ya pili inakumbusha asubuhi ya ufufuo. Kwa hakika, vyovyote ilivyo na mantiki, muhimu na uhakika, asubuhi ya usiku huu, basi asubuhi ya ufufuo na majira ya kuchipua yanayofuatia Ulimwengu wa Kati na Kati ni hakika kwa kiwango hicho hicho. Yaani, kama ilivyo kila wakati katika nyakati hizi tano unaashiria kuanza kwa mzunguko muhimu na kukumbushia mizunguko mingine mikubwa, basi kwa upaji mkubwa wa kila siku wa uwezo wa Mwenye Kuombwa Milele, kila mmoja unaita akilini miujiza ya uwezo wa kiungu na zawadi za rehema ya kiungu kwa kila mwaka, kila umri na kila kipindi. Maana yake, swala za faradhi, ambazo ni wajibu wa kwanza na msingi wa ibada na deni lisilopingika, hufaa na kuendana vyema na nyakati hizo.

§6

Kwa kawaida, mwanaadamu ni dhaifu sana, na bado kila kitu kinamgusa na kumhuzunisha. Pia ni mwenye kukosa sana uwezo, na bado majanga na maadui wanaomkumba ni wengi sana. Pia ni mwenye haja sana, na bado haja zake ni nyingi kwa hakika. Pia ni mvivu na asiyejiweza, na bado majukumu ya kimaisha ni mzigo mzito. Utu wake umemuunganisha na ulimwengu mzima, lakini kuangamia na kupotea kwa vitu alivyovizoea kunaendelea kumuumiza. Mantiki yake pia yanamwonesha malengo matukufu, na matunda ya kudumu, na bado mkono wake ni mfupi, uhai mfupi, uwezo finyu, na subira yake ni ndogo. Inaweza kufahamika vyema kutokana na hayo jinsi ilivyo muhimu kwa roho iliyo katika hali hii katika wakati wa Fajr mapema alfajiri kuwa na njia na kupeleka ombi mbele ya Utukufu wa Ambaye ni Mwenye Uwezo Wote, Mwingi wa Rehema kupitia katika swala na dua, kutafuta mafanikio na msaada kutoka kwake, na hiyo ni nukta muhimu sana ya msaada ili aweze kukabiliana na mambo yatakayomkuta katika siku inayofuata na kukabili majukumu yatakayomkabili. Wakati wa Adhuhuri baada tu ya jua la utosi ni saa ya anga la mchana na mwanzo wa kupinduka kwake, ni wakati ambapo kazi za kila siku zinapokaribia kuleta matunda, wakati wa mapumziko mafupi kutokana na shinikizo la kazi, wakati roho inataka pumziko kutokana na kughafilika na ugumu unaoletwa na bidii, na neema za kiungu juu ya wakati zinadhihirika. Basi mtu yeyote anaweza kufahamu namna zilivyo njema na zenye kukubalika, namna ilivyo muhimu na inavyofaa kwa roho ya mwanaadamu kuswali swala ya adhuhuri, inayomaanisha kuachiliwa huru kutokana na shinikizo, kutingishwa na ughafilikaji na kuyaacha mambo ya kipuuzi na ya mpito na kushika kwa nguvu katika hadhara ya Mpaji wa Riziki wa kweli, Mwenye Kujitosha milele, kumshukuru na kumsifu kutokana na zawadi Zake zote, na kumwomba msaada, na kwa mtu kuinama ili kudhihirisha udhaifu wake mbele ya utukufu na ukubwa Wake na kusujudu na kutangaza kustaajabu kwake, mapenzi na unyenyekevu. Mtu asiyefahamu haya si mwanaadamu wa kweli. Ama kuhusu wakati wa Alasiri, unaingiza akilini msimu wa majira ya kupukutika majani na hali ya kimajonzi ya uzee na kipindi cha majonzi mwishoni mwa wakati. Pia ni wakati ambapo mambo yote ya siku yanafikia tamati yao, na wakati ambapo neema za kiungu kama vile afya, siha, na shughuli zenye manufaa zilizopatikana katika siku hiyo hufanya jumla kuu na muda unaota kwa jua lenye nguvu lenye kudokezea kwa kuanza kumzamisha mtu huyo ni mgeni mheshimiwa na kuwa kila kitu ni cha mpito na si chenye kuendelea. Sasa roho ya kibinadamu inataka uhai wa umilele na iliumbwa kwa ajili hiyo, inaabudu ukarimu na inaumizwa na utengano. Hivyo, yeyote aliye mwanadamu kikweli ataweza kufahamu ni lipi jukumu tukufu, huduma gani inayofaa, njia gani inayostahili ya kulipa deni la asili ya kibinadamu, kwa hakika, furaha kubwa iliyoje kwa kuswali swala ya alasiri. Kwa kuomba dua katika mahakama ya milele ya aliye wa tangu, Mwenye kujitosha milele, ina maana ya kujihifadhi katika madaha ya rehema zisizo na ukomo, na kwa kutoa shukurani na sifa mbele ya neema zisizohesabika, na unyenyekevu mkubwa mbele ya uwezo wa Mmiliki, na kwa kupenya kwa unyenyekevu wote kwenye udaima wa uungu wake, kwa kutafuta faraja ya kweli ya moyo na wepesi wa roho, na kwa kujitayarisha kufanya ibada mbele ya utukufu Wake. Wakati wa Maghrib wakati wa machweo unakumbusha kupotea katikati ya kuagana kunakohuzunisha kwa viumbe laini wenye kupendwa wa dunia ya majira ya joto na ya kupukutisha majani mwanzoni mwa majira ya baridi. Unaingiza akilini muda ambapo kwa mauti yake, mwanadamu atawaacha wote anaowapenda katika hali ya majonzi na kuingia kaburini. Unaleta akilini ambapo wakati wa mauti ya dunia hii katikati ya msukosuko wa maumivu makubwa ya mauti, wakazi wake watahamia katika dunia nyingine na taa ya mahali hapa pa mtihani itazimwa. Ni wakati unaotoa onyo kali kwa wenye kuabudu wapendwa wa mpito na wa muda mfupi tu. Hivyo, katika muda wa swala ya Maghrib, roho ya mwanadamu ambayo kwa hali yake ya kawaida ni kioo chenye kutaka uzuri wa Milele, inageuzia uso wake upande wa kiti cha enzi cha uweza mkubwa wa Aliye hai daima, Mstahamilivu bila kikomo, anayefanya kazi hizi kubwa sana na kugeuza na kubadili dunia hizi kubwa sana, na kutamka “Allah ni Mkubwa Zaidi” juu ya viumbe hivi vya mpito, akijitoa kutoka kwao. Mwanadamu anashikilia kwa nguvu kumtumikia Mola wake na anapanda katika uwepo wa Mstahamilivu daima, na kusema: Alhamdulillah anatukuza ukamilifu Wake usio na dosari, uzuri Wake usio na kifani, rehema Yake isiyo na mipaka. Kwa kutamka, اِيَّاكَ نَعْبُدُ وَ اِيَّاكَ نَسْتَعِينُ anatangaza ibada yake na kutaka msaada kutoka katika miliki Yake isiyosaidiwa, Uungu wake usio na mshirika. Kisha anarukuu, na kutamka pamoja na ulimwengu wote, udhaifu wake na kushindwa kwake, umaskini wake na kutegemea utukufu usio na mpaka, uwezo usio na ukomo, na nguvu kubwa sana za Mwenye Kustahamili Milele, anasema: سُبْحَانَ رَبِّىَ الْعَظِيم na anamtukuza Mola wake Mlezi. Na kusujudu mbele ya uzuri usiokufa wa dhati Yake, sifa Zake tukufu zisizobadilika. Ukamilifu wake unaoendelea daima, mwanadamu anaviacha vitu vyote isipokuwa Yeye na anatangaza mapenzi na ibada yake kwa kustaajabu na kujidhalilisha. Na kusema: سُبْحَانَ رَبِّىَ اْلاَعْلَى anamtangaza Mola Wake Mlezi Aliye wa Juu zaidi kuwa hana upungufu na ameepukana na dosari yoyote. Kisha anashuhudia tawhid ya Allah na utume wa Muhammad (s.a.w). Anakaa kitako na kwa ajili yake anampa zawadi Yule Mwenye Utukufu Wake, maamkizi bora kabisa na dua. Na kumpa salamu Mjumbe Mtukufu Zaidi wa Allah (s.a.w), anafanya upya ahadi yake ya kumtii na kutangaza utii wake kwa amri zake. Ili afanye upya na kuitia nuru imani yake, anachunga amri yenye hekima katika kasri hili la ulimwengu na kushuhudia Umoja wa (s.w). Na anashuhudia ujumbe wa Muhammad Mwarabu (s.a.w), ambaye ni mpiga mbiu wa mamlaka ya Allah, mwenye kutangaza mambo yenye kumpendeza, mfasiri wa alama na aya za kitabu cha ulimwengu. Kuswali swala ya Magharibi ndivyo hivyo. Basi, mtu atakuwaje mwanadamu asiyefahamu jinsi swala ilivyo nzuri na safi wakati wa machweo, ukubwa ulioje wa utukufu na kitendo cha furaha, kuafikiwa kulioje na kitendo cha kufurahisha cha ibada, jambo hilo ni la umakini sana, na namna gani mazungumzo yasiyokwisha na furaha ya milele ilivyo katika nyumba hii ya wageni ya mpito? Katika wakati wa ‘Isha usiku, alama za mwisho za mchana zilizobakia angani zinapotea na dunia ya giza inakumbatia ulimwengu. Wakati Mwenye nguvu zote (s.w), Mwenye kubadili usiku na mchana, anabadili ukurasa mweupe wa mchana na kuwa ukurasa mweusi wa usiku, kwa kupanga nguvu za mamlaka yake, inakumbushia shughuli za kiungu za ukamilifu wa Mwingi wa hekima, Mwenye Kutiisha jua na mwezi, na kubadili ukurasa uliopambwa chanikiwiti wa kiangazi na kuwa ukurasa mweupe wa majira ya baridi. Na kwa kazi zilizosalia za kiumbe aliyeondoka aliyefutwa duniani kwa kupita kwa wakati, inakumbushia matendo ya kiungu ya Muumbaji na uhai na mauti katika kuelekea kwao dunia nyingine tofauti kabisa. Ni wakati ambapo huingiza akilini utaratibu wa Muumba Mbingu na Ardhi na udhihirisho wa uzuri Wake katika kuhiliki kabisa kwa dunia hii finyu, ya mpito na dhalili, maumivu ya kifo cha kutisha cha maradhi yake, na katika kukunjuka kwa dunia pana, ya milele na tukufu ya akhera. Na mmiliki wa ulimwengu, Mpangaji Wake wa Kweli, Mpendwa wa kweli na Mwenye kukusudiwa kwa ibada anaweza tu Yule Mwenye kubadili kwa urahisi usiku kuwa mchana, majira ya baridi kuwa ya kuchipua, na dunia kuwa akhera kama kurasa za kitabu; anayeziandika na kuzifuta na kuzigeuza. Hivyo, wakati wa utusitusi wa usiku, roho ya mwanadamu ambayo haijiwezi kabisa, dhaifu, na masikini kabisa na yenye haja sana, na imetumbukia katika giza nene la wakati ujao, na kuzama katikati ya mambo yasiyohesabika, inaswali swala ya ‘Isha, yenye maana kama vile Ibrahim anavyosema: لاَ اُحِبُّ اْلآفِلِينَ na anaomba hifadhi kwa dua kwa Mwaabudiwa Asiyefikwa na Mauti, Mwenye Kupendwa Milele, na katia dunia hii ya mpito na maisha ya muda mfupi na dunia ya giza na wakati mweusi ujao, anamuomba Mwenye Kustahamili na Wa Milele, na kwa kitambo cha mazungumzo yasiyofikia mwisho, sekunde chache za maisha yasiyo na mauti, anaomba kupata fadhila za rehema za Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu na nuru ya uongofu Wake, zitakazozagaza nuru katika dunia yake na kutia nuru wakati wake ujao na kuponyesha majeraha yanayotokana na kuondoka na kuangamia kwa viumbe wote na marafiki. Katika muda mfupi, mtu anasahau dunia iliyojificha, ambayo imemsahau, na anamwaga majuto mbele ya Rehema kwa kilio chake, na kwa vyovyote, kabla ya kulala – kunakofanana na mauti – anatekeleza wajibu wake wa mwisho wa ibada. Na ili kufunga vyema kumbukumbu za kila siku za matendo yake, anainuka kwa ajili ya swala; yaani, anainuka ili kwenda mbele ya Mwenye kupendwa Milele na Mwabudiwa badala ya vyote avipendavyo vyenye mauti, mbele ya Mwenye Nguvu Kabisa na Mwingi wa Ukarimu badala ya viumbe wote wasiojiweza anaowaomba, mbele ya Mhifadhi Mwingi wa Rehema ili kuweza kunusurika dhidi ya viumbe waovu anaowatetemekea. Anaanzia Sura al-Fatiha, yaani, badala ya kusifu na kuwajibika kwa viumbe wenye ulemavu na masikini ambao hapo si stahiki yao, anamtukuza na kumsifu Mola Mlezi wa Ulimwengu, Ambaye ni Mkamilifu kabisa na mwenye kujitosha kabisa, na Mwingi wa Rehema na Mkarimu Sana. Halafu anaendelea katika tamko: اِيَّاكَ نَعْبُدُ Yaani, licha ya udogo wake, dhalili na mpweke, kupitia katika kuunganika kwa mwanadamu na Mwenye Kumiliki Siku ya Malipo. Ambaye ni mtawala wa milele na milele, anapata daraja ambapo yeye ni mgeni mwenye kuendekezwa ulimwenguni na afisa muhimu anayetamka اِيَّاكَ نَعْبُدُ وَ اِيَّاكَ نَسْتَعِينُ anamletea Yeye kwa ajili ya viumbe wote ibada na anaomba msaada wa hadhara yenye nguvu kubwa na jamii kubwa ya ulimwengu. Halafu kwa kusema; “Tuongoe Njia iliyo nyooka,” anaongoza njia iliyonyooka inayoelekea kwenye furaha ya milele na hiyo ni njia yenye nuru. Na sasa anafikiri kuhusu nguvu za Mwingi wa Rahma, Ambaye kama mimea iliyolala usingizi na wanyama, majua yaliyofichikana na nyota tulivu, vyote hivyo na wanajeshi wenye kutii amri Yake, na taa na watumishi katika nyumba hii ya wageni ya dunia, na kutamka: “Allah ni Mkubwa Zaidi,” anarukuu. Kisha anatafakari kusujudu kukubwa kwa viumbe wote. Yaani, katika amri ya كُنْ فَيَكُونُ namna zote za viumbe kwa kila mwaka na kila karne – hata dunia na ulimwengu – kila kimoja kama jeshi lenye nidhamu nzuri kabisa, au mwanajeshi mtiifu, ameachiliwa kutoka katika wajibu wake, yaani kila kimoja kinapotumwa kwenye Dunia ya Ghaibu, kwa njia ya kusujudu mauti na kifo katika mpangilio wake kamili, kinatamka “Allah ni Mkubwa Zaidi,” na kinainama kwenda kusujudu. Kama viumbe walivyohuishwa, baadhi yao kwa sehemu na wengine kikamilifu, katika wakati wa majira ya kuchipua kwa kichocheo cha mlio wa baragumu la kuhuisha kutoka katika amri ya كُنْ فَيَكُونُ na wao wanafufuka na wamevalishwa tayari ili kumuabudu Mola wao, na mwanadamu dhalili kadhalika, atawafuata na kutamka “Allah ni Mkubwa Zaidi,” mbele ya Mwingi wa rehema za ukamilifu, mwenye kurehemu katika mapenzi yaliyojaa hali ya kustaajabu na unyenyekevu mkubwa na kujionea haya, na kwenda chini kusujudu, yaani, anafanya namna ya kupaa. Hakika, sasa utakuwa umefahamu jinsi unavyokubalika, mzuri na wa kufurahisha na ulivyo juu, ulivyo mtukufu na wenye kuleta furaha, na ulivyo na mantiki na kufaa, wajibu, kuabudu na kitendo cha ibada, na jinsi kulivyo muhimu kuswali swala ya ‘Isha. Hivyo, kwa kuwa kila mojawapo katika nyakati hizi tano inaashiria katika mzunguko wenye nguvu kubwa, ni alama inayoonesha shughuli kubwa ya kimamlaka na ishara ya neema za ujumla za Allah, ni hekima kamili kuwa jambo la swala za faradhi kuwa deni na wajibu liwekwe katika nyakati hizo. سُبْحَانَكَ لَا عِلْمَ لَنَٓا اِلَّا مَا عَلَّمْتَنَا اِنَّكَ اَنْتَ الْعَل۪يمُ الْحَك۪يمُ اَللّٰهُمَّ صَلِّ وَسَلِّمْ عَلٰى مَنْ اَرْسَلْتَهُ مُعَلِّمًا لِعِبَادِكَ لِيُعَلِّمَهُمْ كَيْفِيَّةَ مَعْرِفَتِكَ وَالْعُبُودِيَّةِ لَكَ وَمُعَرِّفًا لِكُنُوزِ اَسْمَائِكَ وَتَرْجُمَانًا لِآيَاتِ كِتَابِ كَائِنَاتِكَ وَمِرْآةً بِعُبُودِيَّتِهِ لِجَمَالِ رُبُوبِيَّتِكَ وَعَلٰى آلِهِ وَصَحْبِهِ اَجْمَعِينَ وَارْحَمْنَا وَارْحَمِ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ آمِينَ بِرَحْمَتِكَ يَا اَرْحَمَ الرَّاحِمِينَ

Private reading note

This note stays on this device and is never uploaded to a server.

Up to 1,200 characters