Ni Vituo Viwili Somo hili linaonekana kwa dhahiri ni risala ndogo, isipokuwa kwa hakika ni risala kubwa yenye nguvu na pana sana. Nalo ni tunda la imani la Qur’an la kifirdausi limepevuka kutokana na maisha yangu ya kifikra na kutokana na kuungana kwa ulimwengu wa elimu ya yakini na kuona kwa yakini katika uhai wa nuru wa kimaanawy wa kuthibitisha. Said Nursî
Source text is preserved. When a suitable model is available, translation is displayed separately.
Şualar
The Fifteenth Ray
Kina Sehemu Tatu
Kutoka katika somo ambalo limetolewa katika shule ya Yusuf ya tatu.
بِسْمِ اللّٰهِ الرَّحْمٰنِ الرَّحِيمِ وَ بِهٖ نَس۟تَعٖينُ Ambaye ametumia miaka thelathini na tano hali ya kujitenga na watu, na ameiaga dunia na kuisahau, na hasa katika nyakati za usiku, hata akawa mbali na watu, kwa wingi wa taabu alizopata kutokana na uangalizi wa kudumu na kulindwa daima kwa kazi zake ulinzi wenye chuki na tabia mbaya, muda wa miaka ishirini na tatu, hata akawa anaona dhiki kupitisha saa ya wakati wake pamoja na mtu na sehemu moja, isipokuwa mwenye shauku na Risale-i Nur na anayeisaidia. Nasema: Wamemuhamisha mnyonge huyu - mimi mnyonge - kwenda kwenye chumba cha tano cha gereza kwa lazima, ambapo kuna msongamano kwa kiasi kikubwa. Na wakawazuia ndugu zangu kunitembelea, kwa hoja ya kupeleka kwangu madai mahakama ya rufaa kuhusu hali yangu kwenye gereza la peke yangu miezi kumi na moja. Nilipokuwa katika hali mbaya na hofu juu ya kutohimili maisha katika msongamano mkubwa, tahamaki hali ya hewa inakuwa baridi kali – kuwa ni alama ya hasira – kwa hali ambayo ningekuwa mahali pangu pa zamani nisingeihimili kamwe. Ugumu ukageuka kwangu kuwa wepesi, na shida ile ikashuka kwangu ikiwa ni rehema kutoka kwa Allah (s.w). Yakapita mawazo moyoni: Pamoja na wanafunzi wa Risale-i Nur kutimiza majukumu yao – na kwa niaba yako – katika kufikisha hakika za Risale-i Nur kwa bidii na Ikhlasi, katika kila rad’ha katika rad’ha za gereza, hakika rad’ha hii ya tano yenye kufanana na mahali pa kujitenga kwa wenye kuipa nyongo dunia inakuwa mpya daima na kubadilika, kwa hiyo basi inahitaji mno masomo ya nuru. Na vilevile vijana na wazee hapana shaka wana haja mno na masomo ya kiyakini ya kina katika kuthibitisha uwepo wake (s.w) na upweke wake. Ambapo wanasoma yanayoandikwa na magazeti katika hujuma ya Urusi kwa imani hujuma za ukafiri za kutisha, na kumkana Muumba mtukufu. Yaliyopita katika moyo nyakati za dhikiri baada ya swala ni haya. Na kwa upande wangu nikataja tahalili ambayo ninaitaja tangu zamani mara kumi baada ya swala ya alfajiri, nayo ni: (Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah (s.w) hana mshirika na kila sifa njema zinamstahiki yeye anahuisha na kufisha naye ni hai hafi mikononi mwake mna kheri zote naye ni mweza kwa kila jambo na kwake tu ndio marejeo). Tahalili hii tukufu na Tawhid tukufu ambayo inabeba jina kuu - kulingana na riwaya moja - imebainishwa na (Andiko la Ishirini) tukufu kwa namna ya uwazi wenye kuangaza kama jua, na hii ni katika maneno kumi na moja katika maneno yake katika hoja kumi na moja miongoni mwa hoja za wajibu wa uwepo wake (s.w) na upweke wa uungu wake, na limeleta bishara kumi na moja katika bishara za kufurahisha. Naam, nilikuwa ninakariri sentensi hii takatifu kwa mazingatio ya kina pamoja na kutafakari katika muhtasari wa andiko la ishirini, ikapita moyoni ghafla: Toa muhtasari huu ukiwa ni somo kwa mwanazuoni mtukufu (Nadir) na wanao kaa hapa katika vijana. Nami kwa upande wangu nikasema: Bismillahi, nikaanza kutoa somo: Hakika katika maneno haya ya kitawhidi kuna bishara kumi na moja, na hoja kumi na moja za kiimani, nitaashiria hoja peke yake kwa ishara fupi sana kwa kuhaulisha fafanuzi zake na bishara zake kwenda katika (Andiko la ishirini) na katika sehemu za Risale-i Nur. Na nilipoandika somo hili, nimeona inafaa sana kuingiza maneno na nukta ambazo sikuzieleza kwa wafungwa. Na kama hivi, maneno kumi na moja ya maneno hayo ya kitawhidi ni haya yafuatayo: Neno la kwanza (لاَ إِلهَ إِلاَّ الله) Hakika hoja ya kiimani katika neno hili ni risala ya (Al-Ayatul kubra), ni risala ya ajabu ambayo haina kifani. Risala hiyo imepelekea wanafunzi wa Risale-i Nur wapate kuachiliwa huru mahakamani, na kudhihiri kwao katika Gereza la (Denizli) na kushinda katika mahakama zote za (Denizli na Ankara) na kuenea kwake kwa kificho kwa namna ya kuathiri. Kama ilivyokuwa kuchapwa kwake kwa siri sababu ya kuwekwa kizuizini wanafunzi wake kwa muda wa miezi tisa. Naam, hakika Mwale wa (Al-Ayatul kubra) umedhihirisha ijmai thelathini na tatu kubwa na hoja za kijumla katika ulimwengu wote, pamoja na kuashiria kwake katika kila hoja ya kijumla hoja zisizo na mpaka zinathibitisha wajibu wa uwepo wa ambaye ni wajibu kuwepo, na upweke wake kwa uthibitisho angavu uliokuwa wazi kama mchana. Unatamkisha mbingu kwa maneno ya nyota katika utangulizi kisha ardhi kwa sentensi za wanyama na mimea na kama hivyo hadi anautamkisha ulimwengu wote kwa maneno ya hakika za kuzuka, yamkini na mabadiliko. Basi ni juu ya wale wanaotafuta imani madhubuti isiyotetereka na wanaotafuta upanga mkali usiodugika mbele ya fujo la ukafiri kuipitia risala ya (Al-Ayatul kubraa). Neno la pili: (وَحْدَه) Na ishara fupi katika hoja iliyomo humo ni: Hakika katika kila upande wa huu ulimwengu na kila sehemu ina shuhudia umoja ulio wazi: Kwa mfano: Ulimwengu wote ulivyo ni wenye kufanana sana na mji uliostawi, na kasri kubwa na kitabu fasaha chenye kuonekana, kwa kiasi kwamba kila aya ndani yake, bali kila herufi miongoni mwa herufi zake, bali kila nukta katika nukta zake ni katika hukumu ya muujiza na Qur’an iliyo kimwili. Naam, kama ambavyo hili linabainisha umoja ulio kuwa wazi katika ulimwengu, basi taa ya kasri hii ni taa moja na kandili yake inayobainisha nyakati pia ni moja, na mpishi wake mmiliki wa moto ni mmoja, na mnyweshaji maji wake ni mmoja na kama hivyo mmoja, mmoja, mmoja, hadi inafikia elfu moja na moja katika moja na umoja. Na kwa ulimwengu kudhihirisha umoja huu katika kila kitu, inathibitisha kwamba mwenye kasri hiyo na mji huo na kitabu hicho, hiyo Qur’an kubwa iliyo katika mwili, na mwandishi wake na msanifu wake yupo na mmoja wa pekee. Neno la tatu: (لاَ شَرِيْكَ لَهُ) Na ishara ya muhtasari sana kwa hoja iliyomo nayo ni: aya tukufu قُل لَّوْ كَانَ مَعَهُ آلِهَةٌ كَمَا يَقُولُونَ إِذًا لاَّبْتَغَوْاْ إِلَى ذِي الْعَرْشِ سَبِيلاً ambayo ndio chimbuko la mwale wa (Al-Ayatul kubraa) na Ustadhi wake na msingi wake. Naam, ingekuwa pamoja naye kuna miungu na wanaingilia katika uumbaji, kupatisha na uungu mpangilio wa ulimwengu wote ungeharibika. Wakati ambapo unashuhudiwa mpangilio mkubwa na madhubuti katika kila kitu kuanzia katika ubawa wa nzi mdogo, na kutokea katika kiini cha jicho lake na kutoka katika chumba chake kidogo na kukomelea katika ndege wa angani, ndege hao wasiohesabika na kumalizwa, hadi kwa mfumo wa jua. Basi katika kila kitu kwenye uwepo unaonekana mpangilio mkamilifu mno sawa iwe ni sehemu au yote, ndogo au kubwa. Jambo lenye kuthibitisha mpangilio huu mkamilifu mno uthibitisho usiokubali shaka kwamba ushirikina ni muhali kuwepo, na kwamba haupo kabisa. Na linathibitisha pia kuwepo kwa wajibu wa kuwepo na upweke wake. Neno la nne: (لَهُ المُلْكُ) Na ishara fupi sana kwa yaliyomo kutokana na hoja ndefu nayo: Hakika tunashuhudia kwa macho yetu kwamba nyuma ya pazia la ghaibu yupo ambaye anasarifu mambo mmiliki wa uweza huria hapingwi na mpaka wowote, na mmiliki wa elimu isiyopingwa na mipaka kwani amejaalia uso wa ardhi kuwa ni shamba kunjufu sawa na ukunjufu wa ardhi yote, kila majira ya machipuo anatawanya humo mbegu zaidi ya aina mia moja elfu za mimea, anazitawanya zote kwa pamoja na kwa hali ya kuwa zimechanganyika, kisha kuvuna mazao yake mavuno yenye kupambanuka bila kuchanganyika au kuvurugika pamoja na mpangilio kamili, na anagawa kwa mkono wa rehema na hekima kwa aina mia mbili elfu za wanyama kile kinachowiana nao katika riziki maalum kulingana na mahitajio yao. Kwa namna hii anasarifu mambo kwa ukunjufu wa ufalme wake mkunjufu na wenye nafasi, mkwasi mtoaji sana, na hasa shamba la ardhi. Basi asiyemuamini msarifu huyu Mwingi wa hekima na Mfalme mwingi wa rehema analazimika kukanusha ardhi hii pamoja na mazao yake na anakuwa kama Wanasafsata wapumbavu. Neno la tano nalo ni: (وَلَهُ الحَمْدُ) Hakika ishara ya muhtasari sana katika hoja kunjufu sana iliyomo ndani yake ni: Hakika sisi tunashuhudia kwa macho yetu na kutambua kwa akili zetu utambuzi kwa kiwango cha uwazi kabisa: Kwamba Mruzuku Mkarimu na Mhisani Mkarimu anasarifu na kuendesha mambo ya mji wa ulimwengu na anachunga mambo ya mtaa wa ardhi, na analea kambi ya mwanadamu na mnyama, hata kwamba yeye amegeuza Ardhi kuwa ni jahazi la kibiashara, na kuwa gari moshi la kuleta riziki, ili apate kushukuriwa na kuhimidiwa kwa neema tele anazomimina ambazo hazihesabiki akiwa amejaalia kutokana na majira ya machipuo yaliyokunjuliwa juu ya uso wa ardhi ambayo ni mfano wa gari moshi, lililoshehenezwa kwa aina mia moja elfu za vyakula, na kujaza chuchu ambazo ni shabihi ya mikebe ya maziwa mazuri kwa ajili ya kuwapa msaada wenye uhai wenye uhitaji ambao chakula chao kimekwisha mwishoni mwa majira ya baridi. Basi mwenye kuwa na chembe ya akili bila shaka ataamini kwamba jambo hili si vingine ila ni kutokana na matendo ya Mruzuku Mwingi wa rehema. Na asiyeamini haya na kupotea upotovu wa wazi kabisa analazimika kukana neema zote zilizotengwa na riziki maalum zenye kupelekea kushukuru, naye si mwingine isipokuwa ni mnyama mpumbavu mno mwenye kudhuru. Neno la sita nalo ni: (يُحْيي) Hakika ishara ya muhtasari sana kwa hoja iliyomo ndani yake nayo ni: Iliyothibitishwa katika (Neno la kumi) na katika sehemu za Risale-i Nur kwa hoja zenye nguvu kwamba: Huletwa katika uso wa ardhi kila majira ya machipuo jeshi kubwa la kiungu limeundwa kutokana na aina mia tatu elfu za wenye uhai na kiasi kisichokuwa na mpaka katika vitu kwenye maumbo mbalimbali. Basi hupewa uhai, na kuandaliwa kila kinacholazimu uhai kwa mpangilio kamili, jambo linalotubainishia vielelezo mia moja elfu katika vielelezo vya Ufufuo mkuu, bali katika alama zake. Basi ambaye anahuisha viumbe hao anuwai bila mpaka kwa pamoja, na hali ya kuwa vimechanganyika na kuchukuana na kusukana baadhi yake kwa baadhi nyingine, bila ya kusahau wala kukosea wala kupungua, na bila ya kutahayari, na kuvipambanua pamoja na kuchanganyika kwake, na bila ya kusahau, na kuvipa uhai kwa ukamilifu wa mizani na mpangilio na kuvipa kutokana na manii zake ambazo ni matone ya maji yenye kufanana, na kutokana na kokwa zake zinazofanana, na kutokana na punje zake ndogo ndogo zisizotofautiana isipokuwa kidogo, na kutokana na vijiyai vya wadudu ambavyo ni sawa na vingine na kutokana na manii ya ndege, na kutokana na vijiyai vyake ambavyo ni sawa na vingine au kwa tofauti ndogo sana. Basi ambaye anahuisha mamia hayo katika maelfu katika wenye uhai ambao hujumuisha idadi isiyohesabika, yenye kutofautiana kwa sura, muundo na maisha, na kufufua mamia hayo katika maelfu miongoni na vilivyo hai, na kuandika vitabu mia moja elfu tofauti juu ya ukurasa wa ardhi na majira ya machipuo, anaiandika pamoja na hali ya kuwa imeingiliana na bila ya kukosea maandishi yalio katika hali nzuri kabisa, na anasarifu katika maandishi hayo kwa uangalizi usio na mpaka na kutenda kwa hekima isiyo na ukomo ndani yake. Naam, hakika ambaye anatenda haya ndiye muumbaji mjuzi wa kila kitu naye ndiye mhuishaji na aliye hai msimamizi wa kila kitu. Na asiyeitakidi hili hapana shaka analazimika kukanusha nafsi yake na kukanusha walio hai wote waliosambaa katika ardhi yote na waliotundikwa katika mkanda wa zama katika misimu yote ya machipuo iliyopita na waliopo juu ya ardhi hai na anga hai, na huyo si yeyote isipokuwa ni mpumbavu wa walio hai na mwovu wao wote. Neno la saba: nalo ni (وَيُمِيْتُ) Hakika ishara iliyo katika ukomo wa muhtasari katika hoja zake nayo ni: Hakika tunashuhudia wakati sampuli mia tatu elfu za walio hai zinaachiliwa huru kutokana na majukumu yao kwa jina la umauti wakati wa mapukutiko, hakika kila sampuli na kila mmoja huweka mbegu zake katika mkono wa hekima kwa mhifadhi mtukufu, zile mbegu ambazo ni mikebe ya kurasa za matendo yake na faharisi za matendo yake, na orodha ya atakayoyafanya katika majira ya machipuo yajayo, nayo inafanana na roho yake yenye kubaki kwa upande mmoja – kama mbegu za tini ndogo ndogo mno ambazo zinabeba kanuni zote za uhai za mti wake, hiyo ni sawa na roho yake yenye kubakia - muumbaji mwingi wa hekima anaandika humo, aliye hai ambaye hafi, kwa kalamu ya kadari – kama kuandika katika nguvu yenye kuhifadhi - historia ya maisha ya mti kana kwamba ni kitabu kikubwa. Basi asiyemwamini muumba huyu mwingi wa hekima aliye hai ambaye hafi sio tu ni mtu mpumbavu na mnyama asiye na hisia, bali vilevile mtu huyo ni mbaya zaidi kuliko Shetani unawashwa kwake moto wa Jahannam na amehukumiwa umauti wa milele. Naam, hakika matendo haya yaliyotajwa na ambayo yanaashiria hoja za maneno haya, nayo ni matendo yenye hekima ya jumla na kufunika na katika ukomo wa muujiza na yanajumuisha miujiza na mambo chungu nzima yenye kufurutu ada. Matendo haya haiyumkiniki kuwa bila ya mtendaji kabisa, bali hilo ni muhali kwa muhali mia moja, na ni batili kabisa, kuyaegemeza kwa sababu pofu kiziwi zenye kushindwa zisizokuwa na utambuzi, mfu zenye kuchanganyika na zisizo tawalia zisizo pangika, ni jambo lisilowezekana kwa mara elfu na moja na halina msingi kabisa. Kama yatakabidhiwa matendo hayo yenye hekima kwa asiye mtendaji mwingi wa hekima ingelazimu kuwepo kwa uweza huria na hekima huria na ufundi mzuri wa jumla unahusu kuundika mimea yote na maua katika kila atomu moja katika atomu za udongo, na inapasa kuwepo kwa ukubalifu wa kufahamu na kufahamisha kauli na mazungumzo na maneno ya sauti zote na redio katika kila atomu miongoni mwa atomu za hewa kama ilivyoelezwa katika nukta ya kitawhidi katika neno (Huwa) katika (Mwongozo kwa vijana). Na mtazamo huu wa ajabu haumfalii Shetani yeyote yule awaye kumkinaisha yeyote katu, ukafiri na kukanusha ambako kuko nje ya eneo la akili kwa kiwango hiki, nao uko mbali sana na uhakika na ni udhalilishaji kwa viumbe wote na kudhuru haki zao, hauna malipo isipokuwa moto, na huo ndio uadilifu hasa. Basi yatakikana kusema kuwa: (Na iishi jahannam kwa ajili ya watu mfano wa hawa wakanushao). Neno la nane: (وَهُوَ حَيٌّ لاَ يَمُوْتُ) Hakika ishara ya muhtasari mno katika hoja iliyomo nayo: Hakika ya majua madogo yenye kushuhudiwa kwa mfano nyakati za mchana juu ya mapovu ya uso wa bahari na juu ya uso wa mto unaotembea, hufichikana kwa kuondoka kwa mapovu hayo, hapo hudhihiri majua madogo ambayo huyafuatia kama yale yaliyotangulia, hili linaashiria jua ambalo lipo mbinguni na kulishuhudia. Na kwa kutoweka na kufa kwake yanajulisha uwepo wa jua la kudumu na la kubakia. Vivyo hivyo, viumbe katika uso wa bahari ya ulimwengu wenye kubadilika daima na katika anga lake lenye kufanyika upya lisilo na mpaka, na katika shamba la atomu zake, viumbe hivi huchuruzika haraka na kwa mwendelezo katika mto wa zama ambao hupiga mawimbi kwa kukumbatia matukio yote ya vilivyomo vyenye kutoweka, na kufa pamoja na sababu zake za kiudhahiri. Ulimwengu fulani huonja umauti kila mwaka, na kila siku, na kushika nafasi yake ulimwengu mwingine mpya, na hufa dunia zenye kutembea kwa mfululizo na limwengu zenye kumiminika katika shamba la atomu baada ya kuchukua mavuno katika mashamba hayo. Kama mapovu na majua madogo kwa kutoweka kwake hubainisha jua la kudumu, basi kifo cha viumbe hao wasio kuwa na mpaka na kuondoka kwa mavuno hayo, na kuviachia pamoja na sababu zake za kidhahiri kuachilia huru kwa mpangilio kamili, hujulisha kabisa kama mchana angavu na jua katika mwanga wa mchana juu ya kupasa kuwepo kwa aliye hai asiye kufa, juu ya jua la milele, juu ya muumbaji mwenye kubakia, juu ya mwamrishaji mtakatifu, na juu ya upweke wake (s.w), na juu ya uwepo wake, kujulisha kuliko dhahiri mno kuliko uwepo wa viumbe vyenyewe kwa mara elfu, na chenye kushuhudia hili ni kila kilichopo kwa dhati yake na vilivyopo vyote kwa pamoja. Hapana shaka kuwa mmetambua kiwango cha upumbavu, uziwi na jinai ya yule asiyesikia sauti hizi za juu ambazo zinajaza anga lote la ulimwengu na shahidi hizi zenye nguvu na za kweli. Neno la tisa: ni (بِيَدِهِ الخَيْرُ) Ishara katika ukomo wa muhtasari katika hoja iliyomo humo ni: Hakika tunashuhudia katika kila duara katika maduara ya ulimwengu huu na katika kila aina miongoni mwa aina zake na katika kila tabaka katika tabaka zake hata katika kila mmoja mmoja miongoni mwa vilivyomo ndani yake, bali katika kila kiungo miongoni mwa viungo vyake, bali katika kila kijichumba miongoni mwa vyumba vya mwili wake, kuna hazina ya akiba na ghala la kuhifadhi riziki, na shamba na hazina inayotayarisha mahitaji yake na kinga yake, na mkono wa ghaibu hukabidhi kwa mkono wa kiumbe huyo - vilivyomo humo - katika wakati mnasibu sana na kwa namna asiyotarajia, bali kwa namna ilio nje ya uwezo wake na utashi wake, ndani ya mpangilio timamu kulingana na kipimo madhubuti, na yote hayo hufanyika katika ukomo wa hekima na upeo wa uangalizi. bali katika kila mwanadamu na katika kila kiungo miongoni mwa viungo vyake kuna hazina na ghala la kuhifadhia akiba, bali hata katika kila kijichumba miongoni mwa vyumba vya mwili vilevile ni hazina ndogo inayowiana nao kwa ajili ya kuhifadhi chakula cha akiba, na vivyo hivyo katika kila kilichomo kuna hazina, hata kwamba hazina ya akhera ni makazi ya dunia, na shamba la pepo na ghala lake ni ulimwengu wa Uislamu na ulimwengu wa utu wa kweli, ambao huchimbuka humo mazuri, uzuri na nuru. Na hazina katika hazina za jahannam ni maada mbovu na makundi yenye kuchafuka ambayo hutoa mimea ya shari, ubaya na ukafiri, shari hizo zinazotokana na kutokuwepo na zenye kuchafua limwengu za uwepo ambazo ni kheri. Na hazina ya joto la nyota na mapito yake ni jahannam, na hazina ya nuru zake na chanzo chake ni pepo. Kama hivi hakika neno (Biyadihil khairu) kwa kuashiria kwake hazina zote hizo zisizo na mpaka linabainisha hoja ya wazi sana. Naam, hakika neno hilo na pia ibara ya (Biyadihi makaaliidu kulli shayin) ni hoja mbili za uungu na upweke zisizo na ukomo wa ukunjufu wake, nazo ni zenye maajabu na miujiza bila mipaka, zinabainishwa na sentensi hizi mbili kwa asiyepofuliwa macho yake. Tazama kwa mfano katika hazina hizo funguo hizo tele bila ukomo katika haya tu basi: Hakika Mwendeshaji Mwingi wa hekima mmiliki wa funguo za mbegu na kokwa, hizo hazina ndogo ambazo kila moja kati ya hizo inajumuisha zana za njia ya vikadiriwa vya mti mkuu au ua lenye harufu nzuri, kama anavyoamsha mlango wa mbegu kwa amri yake (Amka) kwa ufunguo wa utashi, na kwa mizani ya mpangilio kamili, vivyo hivyo anafungua hazina ya ardhi kubwa kwa ufunguo wa mvua, basi anafungua hazina zote ndogo yaani punje ndogo ambazo ni mbegu za uhai za mimea na vyanzo vya wanyama, na matone ambayo ni mbegu za uhai za ndege na vijidudu vyenye kuundika kutokana na hewa na maji, anazifungua zote na kwa pamoja na bila kosa kwa kupokea kwake amri ya kufunguka na kufunukana. Na Allah (s.w) anafungua katika muda huohuo hazina zote za ulimwengu za jumla na za sehemu, za kimaada na kimaana, kwa ufunguo maalum kwa kila moja kati ya hizo kwa mkono wa hekima, utashi, rehema na kutaka. Ikiwa unataka kujua hili na kuliona basi tazama katika hazina zako ndogo ambazo ni moyo wako ubongo wako mwili wako na tumbo lako (mfuko wa chakula). Na tazama bustani yako majira yako ya machipuo ambayo ni pambo la ardhi na maua yake na matunda yake, hakika yake (s.w) anazifungua kwa funguo zake kwa mikono ya mkono wa ghaibu kwa funguo mbalimbali anuwai zinazotokana na kiwanda cha كُنْ فَيَكُوْن. Anazifungua kwa ukamilifu wa mpangilio, vipimo, rehema na hekima, basi hutoa ratili moja au mia moja ratili za vyakula wakati mwingine kutokana na aunsi moja kutokana na mikebe midogo, anazitoa kwa mpangilio kamili na vipimo kwa kutumia vyakula hivyo hali ya kuweka karamu ya fahari kwa wenye uhai. Je, ni katika yumkini kwa nguvu pofu na asili kiziwi na sadifu ya kiholela na sababu zisizo na hisia jinga zenye kushindwa kuingilia katika kutenda yasiyo na ukomo yenye kupelekea katika daraja hii ya mpangilio, elimu na busara, na katika ufundi makini wenye hekima timamu sadifu haiikaribii kabisa, na katika usarifu wenye kupimwa hakuna kosa ndani yake kabisa, na katika ulezi mtukufu wa kiungu adilifu uadilifu uliotimia hakuna dhuluma ndani yake asilani? Na je, inayumkinika kwa asiyeona vitu vyote katika wakati mmoja na hawezi kuviendesha vyote kwa mkupuo mmoja, na wala hajaalii atomu na nyota za angani kuwa chini ya amri yake kwa pamoja, kuingilia katika uendeshaji huu na kusarifu mambo ambayo pande zake zote ni zenye hekima, muujiza na mizani? Na kama hivi basi asiyemwamini mfano wa huyu Msarifu wa mambo, Mwendeshaji mwingi wa rehema, na Bwana Mlezi Mwingi wa hekima, na ambaye mikononi mwake kuna kheri zote, naye ana funguo za kila kitu, na anapotea upotevu wa mbali, hana isipokuwa moto ambao unawaka na kughadhibika hata تَكَادُ تَمَيَّزُ مِنَ الْغَيْظِ kama alivyosema Allah (s.w). Jahanamu inasema kwa ulimi wa hali yake: Hakika anastahiki adhabu yangu ya kudumu, yeye si mwenye kustahiki rehema. Neno la kumi: nalo (وَهُوَ عَلَي كُلِّ شَيْئٍ قَدِيْرُ) Hakika ishara ya muhtasari sana katika hoja iliyomo ni: Hakika kila chenye utambuzi huja katika dunia hii ya ugeni, na kufungua jicho lake na kuona: Uweza unaoshika ulimwengu wote katika fumbato lake, na kukusanya elimu ya kiazali kabisa hapotei wala kusahau na hekima ya milele haina mchezo ndani yake kabisa na inajumuisha uangalizi wa hali ya juu, kiasi hufanya kila moja kati ya walio katika jeshi la atomu yenye kuvutika kwa mvuto wa kimawlawy, hivyo kuvitumia katika majukumu mbalimbali, na kuendesha tufe la ardhi katika punde hiyohiyo katika duara pana masafa yake yanafika miaka ishirini na nne elfu ndani ya mwaka mmoja na kuizungusha kama Muashiki wa kimawlawy kwa kanuni hiyohiyo. Wakati inaleta mavuno ya misimu kwa wanyama na mwanadamu, wakati huohuo kwa kanuni hiyohiyo inafanya jua ni chombo cha anga na kukiendesha katika mhimili wake mzunguko wa kuvutika kwa Mwashiki vilevile hali ya kuzitiisha nyota za angani ambazo ni sehemu ya jeshi za mfumo wa jua katika huduma na majukumu matukufu kwa ukamilifu wa mizani na mpangilio. Na hakika ya uweza huohuo huandika kwa kanuni ya hekima ileile, katika wakati huohuo mamia ya maelfu ya sampuli juu ya ukurasa wa ardhi yote, na ambazo kila moja kati ya hizo ni katika nafasi ya mamia ya maelfu ya vitabu, inaziandika kwa pamoja na hali ya kuingiliana, bila kuchanganya wala kusahau, huku ikidhihirisha kwayo vielelezo vya Ufufuo mtukufu. Na kwamba uweza huohuo, katika wakati huohuo hugeuza ukurasa wa hewa kuwa ni ubao wa kufuta na kuthibitisha, ukiwa unajaalia kutokana na atomu zake zote kana kwamba ni ncha za kalamu za kitabu hicho na nukta zake, ukizitumia katika nyadhifa nyingi katika yanayohusishwa na mambo, amri na utashi wa kiungu. Hata hakika yake imetoa ukubalifu kwa kila moja miongoni mwa hizo atomu ili zipokee maneno na mazungumzo yote kana kwamba zinajua kwa maneno hayo na kuyaeneza bila ya kosa wala kubabaika kana kwamba hizo atomu ni vijisikio vidogo na vilimi vidogodogo sana. Katika ambayo yanathibitisha kwamba chembe ya hewa ni kiti cha enzi cha amri na utashi wa kiungu. Na kama hivi basi kwa kulinganishia ishara hii ya muhtasari: Basi yule ambaye ameujaalia huu ulimwengu katika hukumu ya mji uliopangika na kasri yenye kuimarika, karamu ya fahari, kitabu cha muujiza, na Qur’an yenye fasaha, na kushika katika fumbato la uweza wake kwa mizani ya elimu na mpangilio wa hekima tabaka zote za viumbe na duru zake na mataifa yake kwa kuanzia katika atomu moja kati ya atomu zake na kumalizia katika mkusanyiko wa ulimwengu wote, na kuendesha mambo yake na kuyasarifu, na kudhihirisha hekima yake ya hali ya juu jumla ya uweza wake mtukufu na rehema zake kunjufu, na hujulisha kupitia uungu wake mkunjufu, na kutambulisha uwepo wake na upweke wake, utambulisho wa dhahiri kama jua katikati ya mchana. Kupitia kujitambulisha kwake anataka atambulike kwa imani, na kupitia kujipendekeza kwake anataka apendwe kwa ibada, na kupitia neema zake anataka ashukuriwe na kuhimidiwa. Basi wale ambao hawamjui huyu Mwingi wa Rehema Mwenye kurehemu wala hawajibidiishi kwa uja kwa ajili ya kumpenda, bali wanapotelea katika kukanusha na kudhamiria aina fulani ya uadui upande wake. Hawa sio ila ni mashetani katika sura za watu na katika hukumu ya kina Namrudi wadogo na kina Firauni wadogo. Na hapana shaka kwamba wao wanastahiki adhabu ya kudumu isiyo na ukomo. Neno la kumi na moja nalo: (وَإِلَيْهِ المَصِيْرُ) Yaani mafikio ni katika eneo la hadhara yake, na katika ulimwengu wake wa kubaki, na katika maisha ya akhera yake, na katika nyumba ya furaha yake ya kudumu, kama alivyo kuwa yeye ni marejeo ya viumbe vyote vya ulimwengu vinaegemea kwake na kurejea katika uweza wake nyororo zote za sababu, ikijulikana kwamba sababu ni pazia zimewekwa mbele ya utendaji wa hiyo kudura, kwa ajili ya kuhifadhi haiba yake na utukufu wake mtakatifu. Basi sababu zote za kiudhahiri ni pazia hazina taathira kabisa katika upatishaji. Na kama sio amri yake (s.w) na utashi wake kisingeweza chochote – hata atomu – kutikisika. Tunaashiria kwa muhtasari hoja iliyomo katika neno hili kwa hiyo tunasema: Kwanza: Hakika ya ufufuo na akhera na uhai wa kubaki ambao neno hili takatifu linauelezea tunahaulisha uthibitisho wake katika (Neno la kumi) na nyongeza zake na katika (Neno la ishirini na tisa) ambalo linathibitisha kutokea kwake kwa hakika ya moja kwa moja kama kutokea kwa majira ya machipuo, na katika (Suala la saba katika Risala ya matunda), na katika Mwale wa (Al-Munajat), na katika juzu za kiimani za Risale-i Nur. Ni kweli kwamba Risala hizo zimethibitisha nguzo hii ya kiimani kwa hoja zisizo na ukomo, kwamba kutokea kwa akhera ni thabiti kwa daraja ya kutokea uwepo wa dunia ambayo wanasadiki hata wakanushaji wakaidi mno. Pili: Hakika theluthi ya Qur’an inajadili akhera na ufufuo, na kujengea madai yote katika hakika hiyo, kwa ajili hii kama ilivyo miujiza yote ya Qur’an na hoja zake, ambazo zinathibitisha haki yake zinajulisha juu ya uwepo wa akhera, hali kadhalika miujiza yote ya Mtume (s.a.w) yenye kushuhudia juu ya ukweli wa utume wake na hoja zote za ukweli wake zinashuhudia juu ya akhera na ufufuo, kwa sababu kitu kikubwa alicholingania Mtume huyu mtukufu (s.a.w) muda wote wa uhai wake ni akhera, kama walivyo mitume watukufu laki moja na ishirini na nne elfu wote walilingania juu ya uhai wa kubakia na furaha ya milele na wamewabashiria hilo wanadamu na wamethibitisha ukweli wa madai yao hayo kwa chungu tele ya miujiza na dalili zenye nguvu. Hapana shaka miujiza yao yote na hoja zao zenye kujulisha juu ya utume wao na juu ya ukweli wao katika madai yao inashuhudia pia juu ya akhera na uhai wenye kubakia ambayo ndio malinganio yao makubwa na ya kudumu zaidi. Kwa kulinganisha juu ya hili kwamba dalili zote ambazo zinathibitisha nguzo nyingine za imani zinashuhudia kwa nafasi yake juu ya kutokea kwa akhera na juu ya kufunguka kwa milango ya furaha ya kudumu. Tatu: Hakika ya muumba wa ulimwengu huu ambaye ameuumba kwa atomu zake zote na sayari zake na sehemu zake na tabaka zake hali ya kuweka katika kila kimoja jukumu bali majukumu mengi kwa ukamilifu wa hekima na huku akitiishia kwa mfululizo kwa kudhihirisha ukamilifu wake uweza wake na uungu wake, na ambaye anatuma makundi ya viumbe msafara baada ya msafara bali anatuma dunia zinazofuatana kufanyika upya zikimiminika katika mahali hapa pa karamu ya wageni pa ulimwengu huu na katika medani ya mtihani ya maisha haya ya kidunia, ili kuonesha midhihirisho isiyo na kikomo ya majina yake mazuri ya milele na ili kuchukua picha za viumbe hao na amali zao na sifa zao kwa kamera za kibarzakh na sinema za kiakhera zimewekwa katika ulimwengu wa kimithali. Na baada ya kuwaruhusu hutuma makundi mengine msafara baada ya msafara, bali anatuma aina katika dunia zenye kwenda na kumiminika katika medani hiyo, ili kuweza kushika nafasi ya kilele ya nyadhifa tukufu na kuwa ni vioo vya midhihirisho ya majina yake mazuri. Je ni katika yanayo yumkinika kwa huyu muumba mzuri, fundi mtukufu, Allah (s.w) mwenye ukamilifu, asifanye makao ya thawabu na malipo? Na kwamba asisimamishe ufufuo kwa sampuli ya mwanadamu ambaye anayekabiliana kwa utambuzi na akili katika dunia hii ya kwisha na makusudio yote ya muumba huyu mtukufu, na ambaye anampenda huyo muumba na anampendezesha kwa maandalizi yake yote, na ambaye anamjua na kumjulisha, na kuomba kwa unyenyekevu kwake kwa dua zisizo na mpaka ili kufikia mafanikio ya milele na kubaki kiakhera, na ambaye anaomba maisha ya kudumu ambayo yenyewe ni ladha kabisa, anayaomba kwa maumbile yake yote na roho yake na maandalizi yake kwa maumivu yasiyo na mpaka anayoumia kwa akili aliyonayo. Basi je inayumkinika mwanadamu huyu asiwe na thawabu wala adhabu? hasha kwa Allah na hapana mara elfu. Hakika maelezo na ufafanuzi wa ishara hii fupi yapo kwa sura zake angavu na hoja zake zenye nguvu sana katika Risale-i Nur, kwa hiyo tunaelekeza huko na suala hili refu sana tunalifupisha. سُب۟حَانَكَ لَا عِل۟مَ لَنَٓا اِلَّا مَا عَلَّم۟تَنَٓا اِنَّكَ اَن۟تَ ال۟عَلٖيمُ ال۟حَكٖيمُ
Muhtasari wa Surat (Al-Fatiha) Kutoka katika somo moja tu lililotolewa katika shule ya Yusuf ya tatu katika kipindi kifupi sana wakati wa kuhamishwa kwangu katika kutengwa na jela ya pekee kwenda katika mahali pa jumla na kuchanganyika na wengine. Kielelezo cha somo fupi sana lililotolewa kwa wanafunzi wa nuru jela (Al-Fatiha) ambayo imo katika swala, imeamrisha moyo kubainisha tone katika bahari yake na mng`aro katika miminiko za rangi saba za jua lake. Na tumeandika nukta maridadi katika upeo wa uzuri wa hazina hii kuu ya Qur’an katika maandiko ya ishirini na tisa - sehemu yake - na hasa katika matembezi ya kufikirika katika (Nuun) ya neno (Naabud) na katika Risala ya (Al-Rumuuz al-Thamaniya), na katika tafsiri ya (Isharat al-I’jaz) na katika sehemu nyingine za Risale-i Nur. Isipokuwa nimelazimika - kwa upande mmoja - kuandika tafakuri yangu katika swala ya ishara ya muhtasari huo wa Qur’an mzuri katika nguzo za imani na hoja zake tu na muhtasari wake ambao ni mfupi mno kama sehemu ya kwanza. Naanza kwa بِس۟مِ اللّٰهِ الرَّح۟مٰنِ الرَّحٖيمِ بِسْمِ اللّٰهِ الرَّحْمٰنِ الرَّحِيمِ اَل۟حَم۟دُ لِلّٰهِ رَبِّ ال۟عَالَمٖينَ ... الخ Neno la kwanza: nalo ni (الْحَمْدُ للّهِ) Hakika ishara kwa muhtasari mno katika hoja yake ya kiimani ni: Kwamba kichocheo cha himidi na shukurani ulimwenguni, ni neema ambazo zinaletwa kwa wingi kwa makusudi na hasa kuleta maziwa safi mazuri kwa wanywaji katikati ya kinyesi na damu kwa vichanga na watoto wasio weza lolote, na hisani na zawadi za hiari, na takrima na dhifa za rehema ambazo zimefunika uso wa ardhi yote, bali zimeenea ulimwengu wote, na kwamba thamani na kima kinachotolewa kwa ajili yake ni: (Bismillah) mwanzo kisha (Alhamdulillah) mwisho, na kati ya mawili hayo ni kuhisi kuneemeshwa ndani ya neema yenyewe, kisha kutokea hapo kufikia hadi katika kumtambua mola mlezi mtukufu. Basi jitazame nafsi yako hasa na tumbo lako na milango yako ya fahamu! Ni kiasi gani inahitajia mambo mengi na neema nyingi! na kiasi gani inahitaji riziki ladha na maonjo kwa thamani ya himidi na shukurani! Tazama hili na kipime kila chenye uhai kwa nafsi yako. Na kama hivi hakika himidi isiyo na kikomo itokanayo katika ndimi za hali na kauli, kupitia neema hizi zenye kuenea, inabainisha kama jua liangazalo hali ya ulezi wa kiungu wa jumla na uwepo wa mwaabudiwa mhimidiwa na mneemeshaji mwingi wa rehema. Neno la pili: nalo (رَبِّ الْعَالَمِينَ) Hakika ishara fupi katika hoja iliyomo ni: Hakika tunashuhudia kwa macho yetu kwamba katika ulimwengu huu kuna maelfu ya ulimwengu na limwengu ndogondogo, bali mamilioni, na ghalibu yake zimeingiliana, pamoja na kuwa uendeshaji wa kila moja kati ya hizo na masharti ya kutawalia mambo yake ni tofauti, inaongozwa kwa ulezi uendeshaji utawala mkubwa mno. Ulimwengu wote ni ukurasa uliokunjuliwa mbele ya uoni wake (s.w) nyakati zote, na limwengu zote zinaandikwa kama msitari kwa kalamu ya uweza wake na kadari yake, na kufanywa upya na kugeuzwa. Basi shahidi za jumla na sehemu hujitokeza na kwa idadi ya atomu na vilivyomo vyenye kupatikana kutokana na muundo wake, kila punde kidogo na kila wakati, juu ya kupasa kwa uwepo wa mlezi wa walimwengu na upweke wake, ambaye anaendesha mamilioni haya ya limwengu na viumbe vyenye kumiminika kwa ulezi huria wenye elimu na hekima zisizo na mwisho na zenye uangalizi na rehema zenye upana kukifikia kila kitu. Hakika asiyesadiki ulezi mtukufu unaolea na kuendesha mambo, kuanzia katika shamba la chembe ndogo mno hadi katika mfumo wa jua na katika duara la njia kubwa za sayari, na kutoka katika kijichumba katika mwili hadi katika bohari ya ardhi na katika ulimwengu wote, unalea na kuendesha mambo yake kwa kanuni hiyohiyo na kwa ulezi huohuo na kwa hekima hiyohiyo, wala hahisi wala hayatambui wala hayaoni, hakika anajaalia nafsi yake kuwa ni mstahiki wa adhabu ya kudumu na anainyang’anya kuhurumiwa. Neno la tatu nalo ni: (الرَّحْمنِ الرَّحِيمِ) Ishara fupi mno katika hoja iliyomo nayo: Ni kwamba inashuhudiwa kwa uwazi sawa na mwanga wa jua uwepo wa rehema isiyokoma ulimwenguni na hakika yake. Basi rehema hii pana inashuhudia ushahidi wa kukata shauri kabisa – kama ushahidi wa mwanga juu ya jua – juu ya mwingi wa rehema mwenye kurehemu aliyejificha kwa sitara ya ghaibu. Naam, sehemu muhimu ya rehema ni riziki, ambapo jina la Allah (s.w) (Ar-Rahman) hupewa maana ya Ar-Razzaq. Na riziki yenyewe inajulisha juu ya Al-Razzaq Ar-Rahiim kwa uwazi kwa kiasi kwamba humfanya mwenye utambuzi alazimike kusadiki na kuamini. Kwa mfano: Hakika (s.w) anatayarisha riziki za wenye uhai wote, na hasa wasiojiweza na hususan watoto, nao wameenea katika ardhi yote na katika anga lote, na anawaandalia kwa namna ya ajabu nayo ikiwa nje ya eneo la hiari yao na uwezo wao, kutokana na pasipo na chochote, kutokana na mbegu yenye kufanana, kutokana na matone ya maji, na kutokana na punje za mchanga. Hata kwamba anawadhalilishia vifaranga dhaifu visivyoweza kuruka na vilivyokaa kwenye viota vyake vileleni mwa miti, mama zao kama wanajeshi wenye kungojea amri, huzunguka kwenye mimea na kutafuta maji ili kuviletea riziki. Bali anamdhalilisha simba mwenye njaa kwa ajili ya mtoto wake, anamlisha nyama anayoipata bila ya kuila. Na anapeleka maziwa safi mazuri kwa wanywaji, kati ya kinyesi kichafu na damu nyekundu, kwenda kwa watoto wa wanyama na mwanadamu, na anapeleka kutokea kwenye chemchem za chuchu, pasipo kuchanganyika wala kuchafuka, akijaalia huruma za mama zao ni zenye kuwasaidia. Na kama anavyotoa riziki munasibu kwa miti yote yenye kuhitajia kwa aina ya riziki kwa namna ya ajabu, ananeemesha hisia za mwanadamu ambazo zinahitajia aina fulani ya riziki za kimaada na kimaanawy, na kufanya vizuri kwa ajili ya akili yake moyo na roho yake hali ya kuwa ni meza ya chakula pana mno ya riziki mbalimbali. Hata kana kwamba viumbe ni mamia ya maelfu ya meza za vyakula za neema zenye kuingiliana na mamia ya maelfu ya vyungu vya vyakula tofauti, vikihifadhiana kama majani ya ua na kama vifuniko vya vikonyo, kifuniko ndani ya kifuniko. Inajulisha kwa asiyepofuka macho yake, juu ya mwingi wa rehema mtoa riziki na mwenye kurehemu mkarimu kwa ndimi kwa idadi ya vyungu hivyo vilivyotandazwa na kwa kiasi cha vyakula vilivyomo, ndimi mbalimbali kiujumla na kwa sehemu. Na ikisemwa: Kwamba yaliyo hapa duniani miongoni mwa misiba na mabaya na shari ni mambo ambayo yanapingana na rehema hiyo pana ambayo imekienea kila kitu, na kutibua usafi wake! Jibu: Sehemu za Risale-i Nur zimetosheleza jibu hili, na hasa Risala ya (Kadari). Tunaelekeza huko na huku tukiashiria ishara fupi: Hakika kila kijisehemu na kila aina na kila kilichopo, kina kazi mbalimbali za jumla na za sehemu, na kila moja katika majukumu hayo kuna matokeo tele na matunda mengi. Na wingi kabisa kati yake ni matokeo mazuri na masilahi yenye manufaa, kheri na rehema nyingi. Na sehemu ndogo kati ya hizo huwa ni shari, ubaya kwa sehemu na kwa nje na dhuluma kwa yule ambaye amekosa hali ya ukubalifu, na wenye kukabiliana nayo kimakosa, au wenye kustahiki malipo na kutiwa adabu, au kwa yale yanayokuwa ni nyenzo ya uzalishaji mkubwa. Kama rehema ingezuilia kijisehemu hicho na hicho kilicho kwa ujumla kutimiza jukumu hilo ili kuzuia isije shari hiyo ndogo, hivyo basi yasingepatikana matokeo yake yote mengine mazuri yenye kheri. Na hapo zitatokea shari na mabaya kwa idadi ya matokeo hayo, kwani kukosekana kwa kheri ni shari, na kuharibu uzuri ni ubaya. Kwa maana kwamba mamia ya shari na dhuluma hutendwa kwa kuzuia isije kutokea shari moja, na jambo hili linapingana kabisa na hekima na masilahi na rehema ambayo ulezi wa kiungu unasifikana nayo. Mfano wa hilo: Hakika barafu na baridi na moto na mvua na aina mbalimbali mfano wa hayo hubeba kila moja kati yake mamia ya hekima na masilahi, kama mmoja kati ya wazembe akitenda shari kwa uchaguzi wake mbaya katika haki ya nafsi yake kama kuwa ameingiza mkono wake kwenye moto kisha akasema: Katika kuumbwa kwa moto hakuna rehema, hakika faida za moto wenye kheri na huruma – wenye manufaa nazo hazihesabiki – zinakadhibisha kauli yake na kumpiga kofi katika kinywa chake. Kisha matashi ya mwanadamu na hisia zake duni ambazo hazioni mwisho, haziwi – moja kwa moja – kuwa ni kipimo na mizani sahihi kwa kanuni za wingi wa rehema na wingi wa hekima na ulezi wa kiungu unaopita katika ulimwengu, kwani anaona uwepo kupitia hisia hizo kulingana na rangi za kioo chake. Basi moyo wenye giza usiokuwa na rehema huona viumbe vinalia vibaya vinachanika kati ya kucha za dhuluma na kugeuka katika msongo wa giza. Wakati ambapo akivitazama kwa jicho la imani angeviona katika sura ya mwanadamu mkubwa mwenye kuvaa mpambao sabini elfu yenye kupendeza mno yenye kushonwa kwa rehema, kheri na hekima, zikipandiana hizi juu ya hizi kana kwamba ni huri kutoka peponi amevaa mapambo yake sabini elfu, na kumwona daima mwenye kutabasamu kucheka na mwenye furaha. Na kuona sampuli ya mwanadamu ambaye ndani yake ni ulimwengu uliofanywa mdogo, na kila mwanadamu ni ulimwengu mdogo, basi atasema kutokea katika kina cha moyo na roho yake. الْحَمْدُ للّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ۞ الرَّحْمنِ الرَّحِيمِ ۞ مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ Neno la nne: nalo ni (مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ) Ishara kwa muhtasari sana katika hoja iliyomo ndani yake ni: Kwanza: Hakika dalili zote zenye kuashiria ufufuo na akhera na zenye kushuhudia hoja ya (Wailayhil Al-Maswiir) mwishoni mwa sehemu ya kwanza ya somo hili, zinashuhudia vilevile juu ya hakika ya kiimani pana ambayo inaziashiria. مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ Pili: kama ilivyo ulezi wa kiungu wa mtengenezaji wa ulimwengu huu na rehema yake pana na hekima yake ya milele, na kadhalika uzuri wake, utukufu wake na ukamilifu wake wa Azali na milele, na vilevile sifa zake tukufu zisizo na mipaka na mamia ya majina yake mazuri, yote yanahitajia kabisa Akhera –kama ilivyosemwa mwishoni mwa neno la kumi – basi kadhalika Qur’an tukufu kwa maelfu ya aya zake na hoja zake. Na vivyo hivyo mjumbe mtukufu Muhammad (s.a.w) kwa mamia ya miujiza na hoja zake. Pia na mitume wote Anbiyaa na Mursalina (a.s). Na vilevile vitabu vya mbinguni na sahifa takatifu kwa dalili zake zisizo na mipaka, zote zinashuhudia akhera. Na baada ya hayo, ambaye haamini maisha ya kudumu katika makao ya akhera hakika anaitupa nafsi yake kwenye Jahannam ya kimaanawy inayoletwa na ukafiri, hivyo atateseka na adhabu daima, na hali ya kuwa bado yungali duniani, ambapo nyakati zote zilizopita na zijazo na viumbe na vilivyomo kwa kutoweka kwake na utengano wao vitanyesha mvua mbaya juu ya roho yake na moyo wake na kumuonjesha machungu yasiyo kuwa na ukomo na dhambi kama adhabu za Jahannam kabla hajaingia huko akhera kama hilo lilivyowekwa wazi katika risala ya Mwongozo kwa vijana. Tatu: Tunaashiria kwa alama مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ katika hoja tukufu na yenye nguvu ya ufufuo. Lakini hali maalum iliyotokea kwa ghafla imesababisha kuahirisha hoja hiyo hadi muda mwingine. Na pengine hoja hiyo haihitajiki tena, kwa kuwa Risale-i Nur imethibitisha kwa mamia ya hoja zenye nguvu za kukata shauri kwamba kuchomoza kwa Asubuhi ya Ufufuo na kuingia majira ya machipuo ya kiama ni yakini kama ujio wa mchana baada ya usiku na ujio wa machipuo kufuatia majira ya baridi. Neno la tano nalo ni: إِيَّاكَ نَعْبُدُ وإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ Kabla ya kuashiria hoja iliyomo umepita kwenye moyo ufafanuzi wa matembezi ya kifikira yenye hakika, ufafanuzi mfupi kwa msingi wa kuweka wazi (Andiko la ishirini na tisa) nayo ni kama ifuatavyo: Nilipokuwa ninatafuta miujiza ya Qur’an, kama ilivyobainishwa katika Risale-i nur, katika tafsiri ya (Isharaat al-I’jaz) na katika Risala ya (Ar-Rumuuz al-Thamaniya). Na nilipoona miujiza kadhaa kuhusu maelezo ya ghaibu katika aya ya mwisho kwenye sura Al-Fathi, na muujiza wa kihistoria katika: فَالْيَوْمَ نُنَجِّيكَ بِبَدَنِكَ bali nimeona ming’aro ya miujiza mbalimbali sehemu nyingi katika maneno ya Qur’an na nukta za kimiujiza makini katika baadhi ya herufi zake. Na wakati huu nikiwa ninasoma surat Al-Fatiha ndani ya swala limejitokeza swali moyoni mwangu, ili linifundishe muujiza kati ya miujiza ya (Nun) ambayo imo katika (Na’budu wanastaiin). Na swali ni kwamba: Kwa nini amesema (Na’budu..nastaiin) kwa nuun ya mzungumzaji na mwingine na hakusema (A’bud ... astaiin)? Na ghafla ilifunguliwa mbele ya mawazo yangu uwanja mpana wa matembezi kutokana na mlango wa (Nun) hiyo. Nikajua kwa kiwango cha kushuhudia siri kubwa iliyomo kwenye sala ya jamaa, na nikashuhudia manufaa yake matukufu na nikajua kwa yakini kwamba herufi hii moja yenyewe kwa dhati yake ni muujiza, nao ni: Nilipokuwa nikiswali wakati huo katika msikiti wa (Bayazid) na wakati wa kusema kwangu: إِيَّاكَ نَعْبُدُ وإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ nikaona kwamba jamaa ya msikiti huo wanaunga mkono madai yangu haya kwa kusema kwao kama nisemavyo mimi, na wanashirikiana nami ushirikiano kamili katika madai yangu haya na katika dua langu ambalo limo katika إِهْدِنَا wakinisadikisha mimi. Katika wakati huu hasa ilifunuliwa pazia mbele ya mawazo yangu nikaona kana kwamba misikiti ya Istanbul yote imegeuka kuwa ni (Msikiti wa Bayazid) mkubwa na wenye kuswali humo wote wanasema kama mimi: إِيَّاكَ نَعْبُدُ وإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ wakisadikisha na kuitikia amina katika dua yangu. Na katika kuchukua kwao sura ya waombezi wangu, ikafunguliwa pazia nyengine mbele ya mawazo yangu, nikaona kwamba ulimwengu wa Kiislamu umechukua sura ya msikiti mkubwa sana na kuchukua Makka tukufu na Al-Ka’ba ni mihirabu ya msikiti huo mkuu na wenye kuswali wote waliojipanga safu wameelekeza nyuso zao kwa mzunguko kuelekea mihirabu hiyo takatifu nao wakisema mfano wangu: إِيَّاكَ نَعْبُدُ وإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ ۞ اهدِنَا.. na kila mmoja anasadikisha wote na kuomba kwa jina lao, na kuwafanya wanaosali wote ni waombezi wake. Na nilipokuwa nikifikiria kwamba njia wanayopita jamaa kubwa kwa kiasi hiki haiwi njia ya upogo hata kidogo na maombi yake hayawi isipokuwa ni yenye kusibu, na wala maombi yao hayarudishwi bali hufukuzwa shubuhati za shetani, wakati nikisadikisha manufaa makubwa ya swala katika jamaa usadikishaji wa kiushuhuda, ikaondoshwa pazia nyingine, nikaona: Kana kwamba ulimwengu ni msikiti mkubwa na mataifa yote ya viumbe wamezama katika swala kubwa ya jamaa, كُلٌّ قَدْ عَلِمَ صَلَاتَهُ وَتَسْبِيحَهُ wanatekeleza aina ya swala yao maalum kwa ulimi wa hali, kwa kutimiza utumishi mpana mkubwa sana mbele ya ulezi wenye kuzunguka kila kitu wa mwaabudiwa mtukufu, wote kati yao wanasadikisha ushaihidi wa wote juu ya tawhidi kwa kiasi kila mmoja kati yao hupata ithibati ya matokeo hayohayo, nilipokuwa nikishuhudia mambo haya, pazia nyingine ilinyanyuliwa, na nikaona: Kama ulivyo ulimwengu ambao ni mwanadamu mkubwa unasema kwa ulimi wa hali na ulimi wa maandalizi na haja ya kimaumbile ya sehemu zake nyingi, na kwa ulimi wa kauli kwa wenye utambuzi kati ya vilivyomo: إِيَّاكَ نَعْبُدُ وإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ wakidhihirisha utumishi wao kwa muumba wao mbele ya ulezi wake wa kiungu wenye rehema, vivyo hivyo mwili wangu, huu ulimwengu mdogo, kama mwili wa kila mwenye kuswali na mimi katika jamaa ile kubwa unasema kwa Atomu zake na nguvu zake na hisia zake pia: إِيَّاكَ نَعْبُدُ وإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ kwa ulimi wa utii na uhitaji mbele ya ulezi wa muumba wake, akifuata amri ya mola wake hali ya kusalimu amri kwa utashi wake (s.w), na nikaona kwamba jamaa ile miongoni mwa chembe vumbi na nguvu na hisia kila wakati inaonesha uhitaji wake kwa uangalizi wa muumba wake mtukufu na kukunjua mbele ya rehema zake na msaada wake. Na nikashuhudia kwa kuvutiwa kwa siri ya hali ya juu ya jamaa katika swala, na nimeona muujiza mzuri wa (Nuun) ya naabudu. Na nikaaga matembezi hayo ya kimawazo mbele ya mlango wa (Nun) nilioingia kupitia hapo. Na nikamhimidi Allah (s.w) kwa kusema: Alhamdulillah na nikatembea niseme: إِيَّاكَ نَعْبُدُ وإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ kwa ulimi wa jamaa zile tatu, wale marafiki wakubwa na wadogo. Na sasa utangulizi umekwisha, na turudi katika mazungumzo yetu. Nayo ni ishara fupi katika hoja ambayo inaashiria إِيَّاكَ نَعْبُدُ وإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ Kwanza: Hakika tunashuhudia kwa macho yetu utendaji na uumbaji mkubwa wenye kudumu katika mpangilio na uwiano unaotokea ulimwengu mzima na hasa katika uso wa ardhi. Na tunashuhudia ulezi bila mpaka wenye rehema wenye kuendesha ndani ya huu utendaji na uumbaji unaitikia maombi ya msaada yanayotokea kwa wenye uhai wasio na ukomo na dua zao za kimatendo na kihali na kikauli mwitikio wenye sifa ya ukamilifu wa hekima na ukomo wa uangalizi. Na tunaona midhihirisho ya uungu usio na mipaka na sifa ya kuabudiwa ya jumla ndani ya ulezi huu na ndani ya matukio ya kumwitikia kila kiumbe mmojammoja uitikiaji wa kimatendo kukabiliana na maelfu ya aina ya ibada za kimaumbile na kihiari ambazo viumbe wote wanazitekeleza na hasa wenye uhai na hasa mataifa ya mwanadamu, akili iliyosalimika inaona na imani pia inaona hilo. Kama vitabu vyote vya mbinguni vinavyoelezea hilo na manabii watukufu (a.s). Pili: Hakika kujishughulisha kwa kila jamaa katika jamaa hizo tatu zilizotajwa hapo mwanzo, na ishara inayo ashiriwa na (Nuun) ya Na’budu, kujishughulisha wote kwa pamoja na ibada za kimaumbile na za hiari na kwa namna mbalimbali kunajulisha waziwazi kwamba ni mkabala wa shukurani mbele ya uungu wenye kuabudiwa na ni ushahidi wenye nguvu kabisa juu ya uwepo wa mwaabudiwa mtakatifu. Na kwamba kila jamaa kati ya jamaa tatu zilizotajwa na katika kila kundi kati ya makundi yake, na kila mmoja kati yao kuanzia katika mkusanyiko wa ulimwengu wote hadi katika jamaa ya atomu za kiwiliwili kimoja, ina msaada wa kimatendo na kihali, na kila moja kati yao kuwa na dua maalum kwake kama inavyo ashiria hilo (Nuun) ya Nastaiin. Utendaji wa kusaidia kila mmoja kati ya hao, kuwaokoa na kujibu dua zao, ni ushahidi wa kweli haukubali shaka kabisa juu ya mwendeshaji Mpole Mwingi wa rehema. Mathalani: Kama (Neno la ishirini na tatu) lilivyotaja: Hakika kuitikia maombi ya aina tatu yanayoombwa na viumbe wote ardhini kote, mwitikio wa ajabu mno na kwa namna isiyodhaniwa, kunashuhudia bila shaka yoyote kuwepo kwa Mola mlezi Rahimu Mujibu. Naam, kama tunavyoshuhudia kwa macho yetu, kuitikiwa kwa dua ya kila kokwa na kila mbegu inayomuomba muumba wake kwa maandalizi ili iwe mti na shuke. Vivyo hivyo tunashuhudia kupelekwa kwa riziki kwa wanyama wote ambao mikono yao ni mifupi kuweza kuzifikia, na kuwapa yanayolazimu katika maisha yao, na kuitikia maombi yao ambayo yapo nje ya uwezo wao, na ambayo wanayaomba kutoka kwa mmoja wa pekee kwa ulimi wa uhitaji wa kimaumbile. Basi uitikiaji huu na misaada inashuhudia ushahidi wa kweli juu ya muumba mkarimu ambaye anaitikia maombi yote hayo yatokanayo na ulimi wa uhitaji wa kimaumbile, kama tunavyoshuhudia kwa macho yetu wazi kabisa, na kulazimisha viumbe wa ajabu wasio na hisia kuwasaidia wanyama hao katika wakati munasibu na katika hekima timamu kabisa. Na kama hivi basi kwa kupimia sehemu hizi mbili, hakika kuitikiwa kwa aina zote za dua ambazo zinaombwa kwa ulimi wa kauli, na hasa dua za Manabii (a.s) na viumbe mahususi, kuitikiwa kwa ajabu, kunashuhudia juu ya hoja ya upekee ambao umo katika وإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ. Neno la sita اهدِنَا الصِّرَاطَ المُستَقِيمَ: Hakika ishara fupi mno katika hoja yake ni: Kama ilivyo njia fupi kabisa kati ya njia zinazoelekea kutoka mahali hadi mahali pengine ni njia iliyonyooka sawasawa, na kwamba misitari mifupi kabisa iliyonyooka kati ya nukta moja na nyingine iliyo mbali nayo ni msitari ulionyooka, kadhalika hakika njia yenye kusibu zaidi katika mambo ya kimaanawy na katika njia za kimaanawy na katika masilaki (Mwelekeo wa kisufi) ya kimoyo na yenye kunyooka zaidi ni ile fupi na nyepesi. Mathalani: Hakika vipimo vyote katika Risale-i Nur kati ya njia ya imani na ukafiri vinabainisha kwa kukata shauri kwamba njia ya imani na tawhidi ni fupi yenye kusibu, nyepesi na yenye msimamo zaidi. Ama njia za ukafiri na kukanusha ni ndefu mno na zenye matatizo na hatari. Hapana shaka ulimwengu huu ambao unaendeshwa katika njia yenye kunyooka na hekima – nayo ni njia fupi na nyepesi zaidi katika kila kitu – haiwezekani ndani yake kuwemo hakika ya ushirikina na ukafiri. Wakati hakika za imani na tawhidi ni wajibu na lazima katika ulimwengu huu kama ulazima wa kuwemo jua. Vilevile hakika njia nyepesi mno katika tabia za kibinadamu, zenye kufaa, fupi, na salama zaidi ni katika njia iliyo nyooka na katika msimamo. Mathalani: Kama nguvu ya akili ikikosa mpaka wa katikati, nayo ni hekima na msimamo, ambayo ni mwepesi na wenye manufaa, huanguka katika mapungufu na kupitiliza viwango katika mvurugiko wenye kudhuru na upumbavu wenye balaa, na kuteseka na maangamivu katika njia zake ndefu. Kama nguvu ya ghadhabu haikupita katika njia ya ushujaa ambayo ndio mpaka wa msimamo ulio nyooka, huporomoka katika kupitiliza viwango katika jeuri yenye madhara makubwa na dhulma mbaya mno, na katika kupunguza viwango kuangukia katika kiasi kingi cha kujiweka kwenye hofu yenye kudhalilisha na kuumiza, basi kupata mateso ya kimoyo daima hayo yakiwa ni malipo kutokana na makosa waliyoyafanya yaliyowakosesha mpaka wa msimamo ulio nyooka. Na nguvu ya matamanio aliyonayo mwanadamu, ikipoteza njia ya unyofu salama na kujihifadhi, itadondokea kwa kuvuka kiwango katika maovu ambayo yana misiba, na katika kupunguza kiwango hupelekea katika kuzimika, yaani kuzuilika na maonjo na ladha za neema, na hapo kuteseka na machungu ya maradhi hayo ya kimaanawy. Na kama hivi kwa kupimia yaliyoelezwa, unyofu ndio njia yenye kufaa zaidi nyepesi na fupi zaidi kati ya njia zote zenye kupitwa katika maisha ya mwanadamu ya kibinafsi na kijamii. Mwanadamu anapokosa njia iliyo nyooka basi njia hizo huwa ndefu sana na zenye mabalaa na misiba na madhara mengi. Kwa maana kwamba إِيَّاكَ نَعْبُدُ وإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ ni dua yenye kujumuisha na uja mpana, na pia hiyo ni ishara katika hoja ya tawhidi na somo katika hekima na kufundisha tabia. Neno la saba: nalo ni صِرَاطَ الَّذِينَ أَنعَمتَ عَلَيهِمْ: Ishara fupi ya hoja iliyomo ni: Kwanza: Nani mkusudiwa katika عَلَيْهِمْ? Aya tukufu inaifasiri: وَمَن يُطِعِ اللّهَ وَالرَّسُولَ فَأُوْلَئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللّهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاء وَالصَّالِحِينَ kwani inabainisha makundi manne katika sampuli ya mwanadamu waliopata neema ya kupita njia ya unyofu, kwa kuashiria (An-Nabiyyiin) kwa Bwana wao Muhammad (a.s), na kwa (As-Swiddiqin) kwa Abu bakar As-Swiddiq (r.a), na (As-Shuhdaa) kwa Omar, Othman na Ali. Aya tukufu inaelezea ghaibu na kubainisha mng’aro wa kimuujiza kwamba wanaokuja baada ya mtume (s.a.w), ni As-Swiddiq kisha Omar kisha Othmani kisha Ali. Mungu awaridhie wote, watakuwa makhalifa na kufa mashahidi. Pili: Makundi haya manne ambayo wao ni wa kweli kuwazidi wote katika sampuli ya wanadamu na wenye tabia iliyo nyooka zaidi na wenye hadhi ya juu zaidi, wamelingania kwa nguvu zote walizopewa na kwa kiasi kisichohesabika katika hoja, miujiza, karama, dalili na mafunuo; wamelingania hakika ya tawhidi, na habari zao wamezisadikisha aghalabu ya wanadamu tangu Bwana wetu Adamu (a.s). Hapana shaka kwamba hakika hiyo ni hakika ya kukata shauri kama kuthibiti kwa jua, kwa hiyo kuafikiana kwa kundi hili kubwa katika wabora wa wanadamu wote katika waliodhihirisha ukweli wao na uadilifu wao kwa mamia ya maelfu ya miujiza na hoja ambazo zisizo na mipaka, na kukubaliana kwao wote katika maswala ya kiwajibu kama tawhidi na kupasa kwa uwepo wa muumba, ni hoja ya nguvu inaondosha kila shaka. Naam, hakika tukufu ambayo yameamini makundi hayo manne yaliyoelezwa ambayo yanawakilisha sampuli ya watu wanyoofu zaidi ya mwanadamu ambaye ndiye matokeo muhimu ya kuumbwa kwa ulimwengu na khalifa wa ardhi, na ndiye mwenye sifa jumuishi zaidi ya viumbe hai kwa maandalizi na mwenye hadhi ya juu zaidi, bali ni viongozi wao wa kweli zaidi wenye kusadikisha, na viongozi wao katika makamilifu. Hawa wameeleza kwa pamoja na kuafikiana kuhusu hakika hiyo ambayo wameiamini na kuitakidi itikadi ya kuamua kwa haki ya yakini na kwa elimu ya yakini na kwa dhati ya yakini, na wametulia nayo utulivu usiotetereka wakiudhihirishia ulimwengu na vilivyomo vyote kwa dalili. Je hawi yule anayekanusha na wala hatambui hakika hii tukufu kuwa anatenda jinai, na kustahiki adhabu ya kudumu.?! Neno la nane: Nalo ni غَيرِ المَغضُوبِ عَلَيهِمْ وَلاَ الضَّالِّينَ: Hii ni ishara fupi ya hoja iliyomo humo: Hakika historia ya mwanadamu na vitabu vitakatifu, vinaeleza kwa kuafikiana maelezo ya kukata shauri na kwa uwazi kamili, kwa kuegemea katika tawaturi na matukio ya jumla yaliyothibiti na maarifa ya mwanadamu na mambo yenye kushuhudiwa na mwanadamu, kwamba kujibiwa maombi ya Manabii (a.s) nao ni watu wa njia iliyo nyooka kwa maombi ya ghaibu zaidi ya kawaida katika maelfu ya matukio, na kutimizwa maombi yao hasa, na kuteremka ghadhabu na misiba ya mbinguni kwa maadui wao makafiri katika mamia ya matukio, inajulisha bila shaka yoyote kwamba ulimwengu huu na kwa sampuli ya mwanadamu ambaye yumo ndani yake, vina mola mwenye kuhukumu mwadilifu mwema mkarimu mshindi asiyeshindwa mwendeshaji wa mambo mtiishaji, amewapa ushindi wenye kuungwa mkono na uokovu wa ajabu manabii wema wengi mfano wa Nuhu, Ibrahim, Musa, Hud na Swaleh (a.s) katika matukio mapana ya kihistoria, na wakati huohuo akateremsha duniani misiba ya mbinguni yenye kutisha juu ya watu madhalimu makafiri mfano wa Thamud, Ad, na Firauni mkabala na kuasi kwao mitume. Naam, hakika mirengo miwili mikubwa imepita kwa mwanadamu ikipingana tangu zama za Adamu (a.s). Kwanza: Ni watu wa utume na wema na imani ambao wamepata neema na furaha ya makao mawili kwa kupita kwao njia iliyonyooka, kwa mwenendo wao mwema matendo yao na shughuli zao vikawiana pamoja na uzuri wa hakika wa ulimwengu nidhamu yake kupangika kwake na ukamilifu wake, kwa ajili hiyo wakapata huruma za bwana mlezi wa walimwengu, na furaha za makao mawili, na wakawa ni sababu ya kumwinua mwanadamu kwenda katika ngazi za malaika bali hata za juu kuliko hizo, wakavuna na kuwavunisha wengine pepo ya kimaanawy hata katika dunia, pamoja na furaha ya kudumu huko akhera, yote hayo kwa siri ya hakika za imani. Mrengo wa pili: Ni wale ambao wamepotea njia ya sawa kwa kupitiliza na kupunguza, wameifanya akilia ni nyenzo ya adhabu na zana ya kukusanyia maumivu, hivyo wakauporomosha ubinadamu katika ngazi za chini za upotevu zaidi kuliko wanyama, wakastahiki ghadhabu za kiungu yakawashukia mapigo ya masaibu ikiwa ni malipo ya dhulma yao waliyoitenda duniani. Zaidi ya hayo, kwa upotevu waliokuwa nao na kwa akili inayofungamana na vilivyomo, wamejaalia ulimwengu kuwa ni mahali pa huzuni, machungu na matanga ya jumla, na machinjio ya wenye uhai, wanageuka geuka katika shida za kutoweka na utengano, na machuno machafu na fujo zimekwenda mbali katika anga. Kwa hiyo, roho ya mpotevu imejifunga na moyo wake kwa jahannam ya kimaanawy duniani, na kuwa mwenye kustahiki adhabu iumizayo huko akhera. Vilevile hakika aya tukufu ambayo imo mwishoni mwa sura Al-Fatiha: الَّذِينَ أَنعَمتَ عَلَيهِمْ غَيرِ المَغضُوبِ عَلَيهِمْ وَلاَ الضَّالِّينَ inabainisha mirengo hii mikubwa miwili. Chimbuko la vipimo vyote vilivyoelezwa katika Risale-i Nur na msingi wake na mwongozo wake ni aya hii tukufu. Na kwa kuwa Risale-i Nur imeifasiri aya hii tukufu kwa mamia ya vipimo vyake. Hivyo basi tunaelekeza katika hizo Risala hali ya kuwa tunatosheka na ishara hii. Neno latisa : nalo ni آمين Ishara fupi sana ni: Kwa kuwa (Nuun) ambayo imo katika نَعْبُدُ na نَسْتَعِينُ inatubainishia makundi makubwa matatu, na hasa kundi lenye kupwekesha katika msikiti wa ulimwengu wa Kiislamu na hasa mamilioni ya wenye kuswali ambao wakati huo wanatekeleza swala, na kutufanya tuwe sehemu ya safu zao, ikitufungulia njia iliyonyooka mbele yetu ili tuvune sehemu ya maombi yao, na ili tupate kusadikisha kwao kwetu kwa kutamka kwao mithili ya tunavyotamka sisi, na ili tupate aina katika shufaa yao, basi nasi vilevile kwa kusema kwetu: (Amin) tunatia nguvu maombi ya hao wapwekeshaji wenye kuswali, na tunasadikisha dua zao, na tunataraji kwa Neno (Amin) Allah (s.w) aitikie maombi yao, hali ya kugeuza uja wetu mdogo na maombi yetu madogo kwenda katika uja wa jumla, dua ya jumla na madai ya jumla mbele ya Rububiyya ya jumla yenye kuenea. Kwa maana kwamba neno (Amin) hufanya kuvuna ujumla mpana bali yaweza kuwa sawa na mamilioni ya (Amin) kwa siri ya udugu wa kiimani na umoja wa Kiislamu na kwa kupitia kwenye Radio za kimaanawy na muungano wa umoja wa kundi linalovuka mamilioni ya wenye kuswali, waliojipanga katika swala katika msikiti wa ulimwengu wa Kiislamu. Na kama hivi mtu wa kawaida anapochukua kitu kwa kiasi cha kokwa. basi mtu kamili ambaye kiroho amepanda juu anachukua fungu kama Mtende. Kila mmoja kulingana na ngazi yake. Lini ambaye bado hajapanda. Haitakikani kwake kukumbuka maana haya kwa makusudi wakati wa kusoma kwake Surat Al-Fatiha ili asipoteze utulivu wake na umakini wake, pindi anapopanda katika makamo hayo hakika maana hayo yatadhihiri yenyewe. (Mtunzi) Hakika tumemuuliza Ustadhi wetu ufafanuzi wa neno (kwa makusudi) lililopo katika maelezo haya ya pembeni na tumeandika chini yake aliyoyaeleza kama alivyosema: Kwa jina la wanafunzi wa Nur Katika shule ya Yusuf ya Tatu Jaylan Naona ni kuwa inayumkinika kutafakari kwa maana mapana ya juu ya tashahudi na Surat Al-Fatiha, lakini hayakusudiwi maana hayo kwa kukusudiwa, bali ni kwa sura ya kufuatia, kwani yanayosababisha uhadhiri wa moyo kupata kughafilika ni yale maelezo yake. Wakati ambapo maana yake ya ujumla hutokomeza mghafala na kunawirisha ibada na Munajati na kuung’arisha. Basi hudhihirisha kikamilifu thamani za hali ya juu za swala Al-Fatiha na Tashahhudi. Ama lenye kutakiwa kutokana na (kutokushughulika kwa makusudi) kulikopatikana katika sehemu ya pili ni kuwa kushughulika na maelezo ya maana hayo hasa wakati mwingine huweza kusahaulisha swala na wakati mwingine huharibu umakini wa moyo na kuwa hadhiri. Na kama si hivyo hakika mimi ninahisi faida zake kubwa ikiwa kutafakari ni kwa hali ya kufuatia na kwa namna ya ufupi. (Mtunzi) اَل۟حَم۟دُ لِلّٰهِ رَبِّ ال۟عَالَمٖينَ سُب۟حَانَكَ لَا عِل۟مَ لَنَٓا اِلَّا مَا عَلَّم۟تَنَٓا اِنَّكَ اَن۟تَ ال۟عَلٖيمُ ال۟حَكٖيمُ بِسْمِ اللّٰهِ الرَّحْمٰنِ الرَّحِيمِ وَ بِهٖ نَس۟تَعٖينُ
Somo hili lilitolewa katika shule ya tatu ya Yusuf Utangulizi Sehemu ya pili imeandikwa kwa amri ya kimaanawy iliyotoka katika sura (Al-Fatiha) ambayo imo katika swala na kwa miminiko la nuru ya neno la shahada: Ash hadu an la ilaha illa Allah. Na kadhalika sehemu hii nimelazimika kuiandika kwa msukumo – unaotokana na sababu tatu sina idhini ya kuzibainisha kwa sasa – kwa tanbihi ya kimaanawy yenye kupatikana katika sentensi: Ash hadu anna Muhammada Rasulullah, na kwa kheri ya nuru ya aya tukufu ambayo imo mwishoni mwa surat Al-Fat’hi na ambayo imedhihirisha miujiza mitano ya ghaibu, nayo ni kauli yake Allah (s.w): ﴿هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَكَفَى بِاللَّهِ شَهِيدًا ۞ مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّهِ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاء عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاء بَيْنَهُمْ….﴾ Mpaka mwisho wa aya… Ama maelezo ya sehemu hii na ufafanuzi wake na hoja zake zenye kuegemezwa na dalili, basi nazielekeza katika Risala za (Al-Mu’jizaat Al-Ah’madiyyah) iliyochapishwa ikiwa katika jumla ya (Dhu al-Fiqar) na katika Al-Hizbul An-Nury ambayo imeandikwa kwa lugha ya Kiarabu. Itaashiriwa kwa ishara tatu fupi sana. Katika ishara ya pili na ya tatu itaandikwa mfano wa tafsiri ya fungu la kwanza linalo husu shahada (Muhammad Rasulu Allah) katika Risala ndogo iliyoandikwa hapa, na iliyochotwa kutokana na ufupi wa ufupi wa Al-Hizbul An-Nury Al-Araby, na ambayo ni uradi wangu wa kudumu na kutafakari kwa Kiarabu pamoja na kalimatul tawhidi ambalo ninalikariri katika dhikiri. Ishara ya kwanza Muhammad (s.a.w) ambaye amepokea mionekano ya Rububiyya ya Bwana mlezi wa walimwengu wote, na umilele wa uungu wake, na neema zake zenye kuenea na ambazo hazihesabiki, amezipokea kwa uja wa jumla na kumtambulisha mola wake mlezi mtukufu. Nabii huyu mtukufu ni jambo la dharura kama dharura ya jua kwa ulimwengu huu, kwani yeye ni ustadhi mkuu wa wanadamu, na ni Nabii wao mkuu (s.a.w), na fahari ya ulimwengu, aliyekusudiwa kwa kuambiwa: “لَوْلَاكَ لَوْلَاكَ لَمَا خَلَقْتُ الأَفْلَاكَ”. Kama ilivyo hakika yake (Yaani hakika ya Muhammad (s.a.w)) ndiyo sababu ya kuumbwa kwa ulimwengu, matokeo yake na tunda lake lililo kamili zaidi, na vilevile hukamilika kwa hakika hiyo na kwa ujumbe wa Muhammad makamilifu ya kihakika ya viumbe wote, kwa kuwa huwa ni vioo vyenye kudumu kwa mzuri mtukufu wa milele zikiakisi midhihirisho ya sifa zake tukufu, na athari zake za thamani zenye kupewa majukumu mbele ya vitendo vyake vyenye hekima (s.w), na barua zake za fasaha zenye kutumwa kutoka hadhara tukufu kabisa na kuwa yenye kubeba ulimwengu wenye kubaki, wenye kuzalisha makao ya furaha ya milele na makazi ya akhera ya kudumu ambayo wenye utambuzi wote wanashauku nayo, na mfano wa hayo katika mifano ambayo inatimia kwa hakika ya Muhammad (s.w) na ujumbe wake. Kwa ajili hiyo kama unavyo shuhudia huu ulimwengu kwa ushahidi wa kukata shauri, na kwa nguvu na uthabiti mno juu ya utume wake (s.w), na kadhalika wanadamu wote bali wote wenye utambuzi na mbele yao ni ulimwengu wa Kiislamu, wote wanashuhudia juu ya ambayo ujumbe wa Muhammad umeyabashiria na hakika ya Muhammad ubashiri wenye nguvu wenye kukata shauri, hayo ndiyo maisha ya kudumu ambayo wanadamu wanayaomba kwa ashiki ya kudumu na shauku yenye kuambatana kila wakati, wanayaomba kwa nguvu zote za hakika yao jumuishi na kwa ndimi za maandalizi yao yote, na kwa ndimi za ibada zote, unyenyekevu na tawassuli zenye kupelekwa kwa mola mweza, huomba uhai wa kubakia milele, kuokoka na kukosekana, mchezo na kunyongwa kwa milele na kutoweka kabisa ambako ni kwenye kutisha zaidi na kuumiza zaidi kuliko Jahannam. Kama wanadamu wanavyo shuhudia hili kwamba yeye Muhammad (s.a.w) ndiye fahari ya wanadamu na bora wa viumbe wote, vivyo hivyo mfano wa mema yote na kheri zote ambazo wanavuna kila siku waumini mia tatu na hamsini milioni kila zama, kuingia katika daftari la mema yake (s.a.w) kwa mujibu wa kanuni ya (Sababu kama mtendaji), na haiba hiyo ya Muhammad ya kipekee kupata makamo ya juu yenye kupata uja wa jumla na kheri za kiungu kwa kiasi cha ibada ya mamia ya mamilioni bali mabilioni miongoni mwa wenye kuabudu wema, ni ushahidi wenye nguvu sana juu ya utume wake (s.a.w). Ishara ya pili Kifungu kifuatacho ambacho ninakizingatia sana ni katika nyiradi zangu, ni kinaashiria zaidi ya shahidi ishirini juu ya utume wa Muhammad (s.a.w), tunafupisha yaliomo kwa muhtasari. Nacho ni: (Muhammad mtume wa Allah mkweli wa ahadi mwaminifu kwa ushahidi wa kudhihiri kwake kwa mkupuo mmoja pamoja na kutokujua kwake kusoma, amekuja na dini kamilifu mno ya Kiislamu na sharia, na imani yenye nguvu mno, itikadi na ibada, na ulinganio wa juu mno na munaajati na maombi, na ufikishaji muhimu mno na umadhubuti timamu mno wa ajabu wenye kuleta matunda yasiyo na mfano). Moja ya shahidi hizo ni: Hoja ya utume unaochimbuka kutokana na hali kumi na moja katika hali zake (s.a.w). Naam, yeye pamoja na kuwa hajui kusoma hakujifunza kusoma na kuandika, amekuja na dini iliyowaingiza wenye akili wa karne kumi na nne na wanafalsafa wake katika tahayari, kupendezwa na mshangao, na amezivuka dini za mbinguni na amedhihirisha kwa mkupuo mmoja bila ya kuwa na majaribio yaliyotangulia, na hii ni hali isiyo na mfano wake. Na vilevile Uislamu uliochimbuka kutokana na kauli zake, matendo yake na hali zake, na kuongoza kwake wanadamu mia tatu na hamsini milioni wakati wote, hali ya kulea roho zao, kutakasa nafsi zao, kunawirisha akili zao na kuwapeleka katika kupanda kimaanawy, na hii ni hali haina mfano wake. Na vilevile ameleta sheria angavu kubwa kiasi ambacho ametawala kwa kanuni zake za uadilifu humsi ya wanadamu kipindi chote cha karne kumi na nne utawala ambao umeuhakikishia kunyanyuka kimaada na kimaanawy na hii ni hali isiyokua na mfano wake. Na vilevile kudhihiri kwake kwa imani yenye kujikita madhubuti na itikadi isiyotetereka kwa kiasi kwamba watu wa hakika wanapata ilhamu kutoka kwake kila wakati na kusadikisha kwa maafikiano kwamba yeye yupo katika daraja ya juu mno na ngazi tukufu zaidi, ukiachia mbali kutoleta walio dhidi yake na maadui wake na wapinzani wake wakati huo - utata wowote - wala wasiwasi wala shaka katu, jambo lenye kubanisha kwa uwazi kwamba hana mfano wake katika nguvu ya imani pia hakuna mwenza wa imani yake ya juu ya kiujumla. Na vivyo hivyo amedhihirisha uja na ibada kubwa kiasi ameunganisha pamoja msingi na ukomo, bila ya kumwiga yeyote hali ya kuzingatia siri madhubuti za ibada, na kuzichunga hata katika nyakati za misukosuko mikubwa na amezitekeleza katika sura kamilifu mno na nzuri zaidi. Na hii ni hali isiyo na mfano wake. Na vivyo hivyo amenyenyekea kwa mola wake mkarimu na kuomba maombi ya upole laini kiasi hakufikia yeyote ngazi ya maombi hayo na munajaati hadi zama hizi pamoja na kukutana kwa fikira mbali mbali. Kwa mfano: Amejaalia majina elfu na moja katika majina ya mwenyezi mungu kuwa yenye kuombea dua yake katika munajaati ya (Al-Jawashan al-Kabiir) akamsifu muumba wake mtukufu wasifu wa kupendeza unaofaa kwa makamo yake, na akamtambulisha utambulisho usiokuwa na mfano kabisa. Na kama hivi kutofikia yeyote alipofikia katika kumjua Allah (s.w), ni hali isiyo na mfano wake katu. Na vilevile yeye amewalingania watu katika dini ulinganifu ulio jaa uaminifu na amefikisha ujumbe wake kwa ushujaa na uthubutu kwa namna ambayo upinzani wa watu wake na ami yake na madola makubwa ulimwenguni na wafuasi wa dini zilizotangulia na uadui wao, haikumpa hofu wala kurudi nyuma kabisa, bali aliwapa changamoto walimwengu na kuwashinda wote, na hii ni hali isiyo na mithili yake. Na kama hivi hakika jumla ya hali hizi nane za ajabu ambazo hazina mfano wake ni ushahidi katika ukomo wa nguvu juu ya ukweli wake mtume (s.a.w) na kuthibiti kwa malinganio yake. Na hizo ni hali ambazo zinadhihirisha kiasi cha kutulia kwake na ukomo wa bidii yake, kisi kikubwa cha uhakika wake, ukamilifu wa ukweli wake na uadilifu wake. Kwa hiyo ulimwengu wa Kiislamu unampongeza na kumbariki Nabii huyu mtukufu s.a.w kwa kusema katika kila kikao cha tashahudi katika swala kila siku na kwa mamilioni ya ndimi: “As-Salaamu alayka ayyuha An-Nabiyyu warahmatullahi wabarakatuhu” kwa kuwasilisha utii wake kwa jukumu la unabii, na kumsadikisha katika ubashiri wake wa furaha ya milele aliyokuja nao, unampokea kwa utambuzi wa wema mkubwa na shukurani yenye kuenea mkabala na kufungua njia iliyonyooka kuelekea katika maisha ya kudumu ambayo wanadamu wanaitafuta kwa ashiki iliyojificha, yenye kina, na shauku ya kimaumbile kubwa na kwa maandalizi yenye nguvu mno, kwa kusema: “As-Salaamu alayka ay-Yuuha An-Nabiyyu” ukielezea kwa tamko hilo juu ya ziara ya kimaanawy kwake (s.a.w) na kukutana naye, na kumkaribisha na kumpongeza yeye kwa jina la mia tatu na hamsini milioni bali mabilioni ya waumini. Ushahidi wa pili katika shahidi ishirini za jumla na ambazo zinakusanya shahidi nyingi zaidi nao ni: [Na kwa ushahidi wa hakika za imani zote katika kumsadikisha] Yaani hakika za nguzo sita za imani na kuthibiti kwake na ukweli wake na kusibu kwake vinashuhudia ushahidi wa kukata shauri juu ya utume wa Muhammad (s.a.w) na juu ya ukweli wake na kusibu kwake, kwa sababu haiba ya kimaanawy ya maisha ya utume wake, na msingi wa malinganio yake yote, na hakika ya unabii wake, hakika ni hizo nguzo sita, na kwa hiyo dalili zote zenye kujulisha juu ya kuthibiti kwa nguzo hizo zinajulisha kwamba utume wa Muhammad (s.a.w) ni kweli na yeye ni mkweli mwenye kusadikishwa, kama risala ya matunda ilivyobainisha (Matunda ya imani) na nyongeza za (Neno la kumi) nguzo nyingine za imani kujulisha juu ya kuthibiti kwa Akhera, hali kadhalika kila nguzo kati ya hizo pamoja na hoja zake zote zinathibitisha Utume wake (s.a.w). Ushahidi wa jumla wa tatu ambao unakusanya maelfu ya shahidi (Na kwa kushuhudia kwa dhati yake (a.s) kwa maelfu ya miujiza yake na makamilifu yake na tabia zake njema) Yaani yeye ni kama jua ni dalili kwa nafsi yake. Kama risala ya ajabu ilivyo thibitisha, risala ya (Miujiza ya Muhammad) rehema na amani zimwendee mwenye miujiza hiyo, katika zaidi ya miujiza mia tatu kwa mapokezi sahihi, vilevile kupasuka kwa mwezi pande mbili kwa kidole katika kiganja chake chenye baraka (s.a.w) kama aya inavyoweka wazi: وَانشَقَّ الْقَمَرُ. Vilevile kutiririka maji kutoka katika vidole vyake vyenye baraka na kufoka kama yanavyofoka kutoka katika chemchemu tano, na kunywa jeshi kamili na kushuhudia kwao hilo, kulikonakiliwa kwetu kwa mapokezi sahihi ya tawatur, ukiachilia mbali kukariri kwa tukio hili la ajabu mara mbili katika maeneo mengine. Na vilevile kurusha kwake gao la mchanga kwa kiganja hichohicho kwa jeshi la adui linaloshambulia na kuingia kwa mchanga kwenye jicho la kila mmoja wao na kushindwa kwao wakati wa kushambulia kama uwazi wa aya tukufu: وَمَا رَمَيْتَ إِذْ رَمَيْتَ vilevile jiwe kusoma tasbihi kwenye kiganja hichohicho, tasbihi wazi ya bayana ambayo imepokelewa kwa mapokezi sahihi, na mfano wa hiyo miongoni mwa miujiza ambayo imedhihiri kutoka katika mkono wake uliobarikiwa na sehemu yake imesimuliwa katika vitabu vya sira na historia kwa mapokeo yaliyokuja kwa tawatur ya kukata shauri na ambayo inazidi mamia bali inafika elfu kwa wanazuoni wahakiki. Vilevile maafikiano ya mawalii na maadui kuwa yeye yuko katika kilele cha tabia njema na kuafikiana watu wote wa tahakiki wenye kupita njia yake kwa kufuatilia nyayo zake wenye kufikia makamilifu na wenye kutambua hakika kwa dhati ya yakini, na kusadikisha kwao wote kwa haki ya yakini, kwamba makamilifu ya Muhammad ni katika kilele cha daraja, kama zinavyojulisha hilo kheri za ulimwengu wa Kiislamu, zenye kutokana na dini yake (s.a.w), na hakika za dini tukufu ya uislamu. Hapana shaka kwamba mtume huyo mtukufu anashuhudia ushahidi mpana wa jumla wenye kuangazia juu ya utume wake yeye mwenyewe. Ushahidi wa nne ambao unabeba shahidi nyingi zenye nguvu: [Na kwa ushahidi wa Qur’an kwa hakika na hoja zisizo na mpaka] Yaani Qur’an yenye muujiza wa bayana inashuhudia kwa hakika zake na hoja zake, ambazo hazihesabiki juu ya Utume na ukweli wake (s.a.w). Naam, Qur’an ambayo ni muujiza mkubwa kwa pande arubaini (Kama ilivyothibitisha Risala ya Muujiza wa Qur’an iliyochapishwa katika jumla ya machapisho ya Dhu al-Fiqar), na ambayo imetia nuru karne kumi na nne, na ambayo imeongoza nusu ya kanuni zake zilizonyooka ambazo hazibadiliki, na ambayo imetoa changamoto na bado inaendelea kutoa changamoto kwa wapinzani wote hata hakuthubutu kuipinga yeyote hadi sasa japo kwa sura moja. Bali pande zake sita ni za nuru haziingii shaka kabisa, na makamo sita makubwa yanasadikisha juu ya ukweli na uadilifu wake, na inaegemea hakika sita zisizotetereka, kama ilivyothibitishwa katika risala ya (Al-Ayatu al-Kubra), na ambacho kinasomwa wakati wote kwa ndimi za mamia ya mamilioni na kwa kila shauku na heshima, na ambayo inaandikwa katika nyoyo za mamilioni ya mahafidhi kila dakika uandishi mtukufu, na ambacho kinatona kutokana na shahidi zake shahidi zote na imani ya ulimwengu wa Kiislamu, na inanasibiana kutoka katika chimbuko lake elimu zote za kimani na Kiislamu. Kama inavyosadikisha vitabu vya mbinguni vilivyotangulia, inapata usadikishaji wa kimaanawy vilevile kutoka katika vitabu vyote na suhuf za mbinguni. Basi Qur’an hii tukufu pamoja na hakika zake zote, na hoja zake zinazothibitisha ukweli wake na uadilifu wake, inashuhudia juu ya ukweli wake na utume wake. Ushahidi wa jumla wa tano, sita, saba na nane: [Na kwa kushuhudia Al-Jawshanu kwa utakatifu wa ishara yake, na Risale-i Nur kwa nguvu ya dalili zake, na zenye kupita kwa tawatur ya Irhasat (miujiza yake kabla ya utume), na kupokelewa kwa kusadikishwa na maelfu ya matukio yake]. Yaani kama ilivyo (Al-Jawshan al-Kabiir) ambayo inajumuisha majina elfu moja na moja katika majina ya kiungu kwa uwazi na kwa kuashiria, na inatokana - upande mmoja – kutoka katika Qur’an tukufu, huu munajati wa mtume wa ajabu ambao unapita munaajati wa wajuzi wote wa Allah ambao wamepanda katika ngazi za kumjua Allah (s.w), na kushika nafasi za juu, ameileta Jibril (a.s) ikiwa ni wahay katika vita akisema: (Vua nguo ya vita (Al-Jawshan) na soma Jawshan hii). Hakika ambazo zimebebwa katika munajati huu na sifa zenye kuelekezwa ndani yake kwa mola wake mtukufu kwa dhati yake inashuhudia ushahidi wa kweli juu ya ukweli wa Muhammad (s.a.w) na juu ya Utume wake. Vilevile Risale-i Nur inayotona kutoka katika Qur’an tukufu na yenye kuchotwa - kwa upande mwingine - kutokana na (Al-Jawashan al-Kabiir) ni hoja moja juu ya utume wa Muhammad kwa sehemu zake zenye kufikia risala mia moja na thelathini na hii kwa uthibitisho wake wa kiakili na kimantiki hakika zote za utume wake (s.a.w), bali kuzifundisha na kuzifahamisha kwa wepesi jambo ambalo falsafa inashindwa na kuyaelezea mambo ambayo yapo mbali sana na akili na kuyaonesha kuwa ni maswala yenye kukubalika na kuingia akilini kana kwamba yanaonekana. Risala hizi zinazofikia mia moja na thelathini zinashuhudia ushahidi wa ujumla juu ya ukweli wa Muhammad (s.a.w) na juu ya utume wake. Halikadhalika muda uliopita ni ushahidi wa kiujumla juu ya utume wake, kwani Irhasat ambazo ni mambo yaliyo furutu ada yametangulia kipindi cha utume na zinahesabiwa ni katika miujiza ya mtume (s.a.w) ambaye atakuja, matukio mengi yameelezwa katika vitabu vya sira na historia maelezo ya tawatur kabisa. Basi irhasat hizi zinashuhudia ushahidi wa kweli juu ya utume wake. Na hizi irhasat ni aina nyingi sehemu yake itabainishwa katika ushahidi ujao, sehemu yake nyingine imeelezwa katika mkusanyiko wa (Dhu al-Fiqar) na vitabu vya historia vimenakili kwa usahihi. Kwa mfano: Kutuma ndege ili kulirushia vijiwe jeshi la Abraha ambalo limekuja kwa ajili ya kuvunja Al-Kaaba vijiwe vya moto kabla ya kuzaliwa kwake (s.a.w), na kudondoka masanamu kwenye Al-Kaaba usiku wa mazazi yenye baraka, na kuvunjika vibaraza vya kisra, na kuzimika kwa moto wa majusi ambao ulikuwa unawaka tangu miaka elfu, na mtume (s.a.w) kufunikwa na kiwingu kama alivyosimulia Bahira padri na Halima As-Saadiyya. Na mfano wa hayo katika matukio mengi ambayo yameelezea utume wake (s.a.w) kabla ya kupewa kwake utume. Na vivyo hivyo mustakabali, yaani matukio ambayo yametokea baada ya kutawafu kwake (s.a.w), aliyoyaelezea nayo ni mengi sana na aina nyingi mno, kati ya hayo: Kuelezea kwake kwa ghaibu kunakohusu jamaa na masahaba wema, na ushindi wa Kiislamu, na imeshathibitishwa katika Risala ya Al-Muujizaat Al-Ahmadiyya (Iliyochapishwa ikiwa ni sehemu ya mkusanyiko wa Dhu al-Fiqar) kwa mapokezi sahihi matukio manane yametokea kama alivyoelezea. Mfano: Kufa shahidi Sayyidina Uthumani (r.a) wakati akisoma msahafu mtukufu, na kufa shahidi Sayyidina Husein ra. huko karbala, na kufungua nchi za Shamu, Uajemi na Istanbul, na kusimama kwa dola la Al-abbasiyya na kuanguka kwake na kuteketea kwake kwa mkono wa Jenkiz Khan na Holako, na mfano wa hayo katika miujiza yake katika kuelezea kwake ghaibu ambako kumedhihiri katika matukio manane, katika yaliyo nakiliwa kwetu kwa usahihi kwa kuegemea vitabu vya sira na historia ambavyo nimevieleza kwa ufafanuzi. Basi maelezo haya ya ghaibu na baki ya aina yake ambayo yanajulisha ukweli wake (s.a.w) na matukio ya mustakabali mengi sana yanajulisha ukweli wake (s.a.w), yaani mustakabali unashuhudia ushahidi wenye nguvu wa kijumla juu ya Utume wa Muhammad (s.a.w). Ushahidi wa tisa, kumi, kumi na moja, na kumi na mbili ambao unaashiria: [Na kwa ushahidi wa ali zake kwa nguvu ya yakini yao, katika kumsadikisha kwa daraja ya haki ya yakini, na masahaba kwa ukamilifu wa imani yao katika kumsadikisha kwa daraja ya dhati ya yakini, na wateule kwa nguvu ya uhakiki wao katika kusadikisha kwao kwa daraja ya elimu ya yakini, na maqutubu kwa kulingana sawa kwao juu ya Utume wake kwa kufunuliwa na maono kwa yakini] Basi kutokea katika ushahidi ya kiujumla ambao unashuhudia kwa ukweli juu ya ukweli wa Muhammad (s.a.w) na uadilifu wake: Ushahidi wa tisa: Nao ni ushahidi wa jamaa zake Muhammad (s.a.w) ambao wamepata ngazi ya (wanazuoni wa Umma wangu ni kama manabii wa wana wa Izraili) na mabao wanalingana na jamaa wa Ibrahimu a.s, katika swala za tashahudi, nao ni mawalii wakubwa na maimamu kumi na mbili (r.a), na anawatangulia wote hao imamu Ali, Hasan na Husein Mungu awaridhie, na sheikh Al-Kaylany, Ahmad Al-Rifaiy, Ahmad Al-Badawy, Ibrahim Ad-Dusuqy, Abu Al-Hasan Al-Shadhily (Q.S) na mfano wa hao katika maaqtabu na maimamu, wote wanashuhudia na kwa kuafikiana kwa itikadi yao ya yakini na kwa kufunuliwa, maono, karama na mwongozo waliyoidhihirisha katika umma, hivyo wanasadikisha kwa imani yao madhubuti Utume wa Muhammad (s.a.w) na ukweli wa mtume mtukufu. Ushahidi wa kumi: Ni ushahidi wa maswahaba watukufu ambao ni bora wa watu wenye daraja ya juu zaidi baada ya manabii (a.s), na ambao wameuongoza ulimwengu kutokea mashariki hadi magharibi kwa uadilifu na usawa baada ya kunawirika na nuru ya Muhammad (s.a.w) katika kipindi kifupi licha ya kuwa kwao ni mabedui wasiojua kusoma na kuandika. Na kushinda madola makubwa na kuwa ni maustadhi wa mataifa yalioendelea yenye ustaarabu na elimu na siasa, na walimu wao na wanasiasa wenye kuhukumu kwa uadilifu, wakaigeuza karne hiyo kuwa karne bora kabisa na enzi za furaha. Masahaba hawa wema baada ya kuchunguza sana kila hali katika hali za Muhammad (s.a.w) na kushuhudia kwao kwa macho yao nguvu ya miujiza yake mingi, waliacha uadui wao uliotangulia, na wakaikataa njia ya mababu zao wakajitolea kwa nafsi na kilicho ghali kujitolea kwa heshima na hadhi na kujiunga chini ya bendera ya Uislamu, kama Khalid bin Waliid, Ikrima bin Abi Jahali na mfano wa hao katika walioacha wazazi wao na kabila lao. Hakika imani ya masahaba hawa watukufu inayofikia daraja ya dhati ya yakini, ni ushahidi wa kweli wa jumla juu ya ukweli wa Muhammad (s.a.w) na kuwa utume wake ni wa haki. Ushahidi wa kumi na moja: Nao ni ushahidi wa maelfu wa watu wa uhakiki, yaani ushahidi wa mujtahidina na maimamu wanazuoni wakubwa na wanazuoni wahakiki ambao wote hao wanaitwa: Wateule na masiddikina, na wanafalsafa hodari mfano wa Ibn sina na Ibn Rushd ambao wameamini imani ya kimantiki na kiakili, pamoja na kutofautiana maslaki ya kila mmoja na mwingine kati yao, wakiegemea maelfu ya hoja zenye nguvu na dalili madhubuti, mpaka walifika daraja ya elimu ya yakini, hakika imani ya watu wote hawa kumwamini Muhammad (s.a.w) na utume wake na ukweli wake na kusibu kwake ni ushahidi wa jumla kwa kiasi ambacho haiwezekani kuupinga ila mtu ambaye mwenye busara inayolingana sawa na busara zao. Na Risale-i Nur ni mojawapo kati ya mashahidi hao wa kweli katika zama hizi, ambao hawahesabiki, lakini hoja ilipoanguka katika mikono ya wakanushaji na hawakuwa na pakugeukia, walijaribu kuituliza kwa mahakama kwa kuwadanganya watu wa usalama na vyombo vya sheria. Ushahidi wa kumi na mbili: Ni ushahidi wa al-Aqtabu ambao kila mmoja kati yao anajumuisha sehemu muhimu katika umma wa Kiislamu ndani ya duara la somo lake na maelekezo yake, na kwa maelekezo ya ajabu na mwongozo wenye kusibu na karama za wazi wamewapeleka katika kupanda kimaanawy wakiegemea katika maeneo ya hoja mambo waliyoshuhudia na kufunuliwa. Hawa ni watu wa kipekee wa uhakiki na hakika, kwa kufunuliwa kwenye kupanda kwao kiruhani wameshuhudia ukweli wa Muhammad (s.a.w) na ukweli wa utume wake na kwamba yuko kwenye kilele cha ngazi za ukweli, uadilifu na haki. Basi ushahidi wa watu hawa kwa kuafikiana na kuchukuana sawa, juu ya utume wake (s.a.w) ni uthibitisho wenye nguvu kwa kiasi ambacho haiwezekani kuukosoa ila kutoka kwa aliyepata ukamilifu na fadhila sawa na waliyopata watu hawa. Ushahidi wa kumi na tatu: Ni hoja nne zenye nguvu pana za kiujumla: [Na kwa ushahidi wa zama zilizopita kwa tawatur ya bishara za makuhani na sauti na watambuzi katika duru za waliopita na kwa kushuhudia kwa bishara za mitume mursalina na Anbiya na kwa ushahidi wao na bishara zao (a.s) kwa utume wa Muhammad (s.a.w) ndani ya vitabu vitakatifu]. Yaliyomo katika fungu hilo kwa ufupi yatafafanuliwa hapa, ama ufafanuzi wake kamili na hoja zake umo mwishoni mwa Risala ya (Al-Muujizat Al-Ahmadiyya) sehemu ya mkusanyo ya Dhu Al-Fiqar Na fungu hili lina maana kuwa watu mashuhuri katika zama zilizopita, wakitanguliwa na manabii watukufu (a.s) na watambuzi na makuhani na sauti, wameeleza kwa kuafikiana kuja kwa Muhammad (s.a.w), na kuhusu utume wake, habari ambazo zinaitwa (Irhasat) maelezo hayo yako wazi na yamekaririwa na kutajwa katika vitabu vya historia na sira na hadithi tukufu, kwa mapokeo sahihi na sehemu kati yake ni mutawatir. Risala ya (Al-Muujizatul Al-Ahmadiyyah) imeelezea na kubainisha Irhasat ambazo zina nguvu na zilizothibiti zaidi kati ya maelfu ya hizo, basi tunaelekeza huko kwa ishara ya muhtasari mno. Ama kuelezea kwa manabii kumetajwa katika (Andiko la kumi na tisa) ishara ishirini zinazohusu utume wa Muhammad (s.a.w) kwa kiasi kinachokaribia kwa uwazi na mamia ya aya zilizomo katika vitabu vya mbinguni kama Taurati, Injili na Zaburi, Husein Al-Jisr kwenye kitabu chake amekusanya ishara mia moja kati hizo zinazobashiri utume wa Muhammad (s.a.w) pamoja na upotoshaji mwingi uliotokea kwenye vitabu hivyo kwa upande wa Wakristo na Mayahudi. Ama makuhani mbele yao kuna makuhani wawili mashuhuri (Shaq na Satiih) wanaelezea ghaibu kupitia maruhani na majini. Wakaelezea Riwaya sahihi zilizopokelewa kwa tawatur na za wazi hakuna shaka yoyote katika habari hizo kuhusu ujio wa mtume (s.a.w) na kuondosha kwake Dola la Uajemi. Na kudhihiri kwa nabii karibuni huko Hijazi. Na Kaab bin Luayy ameeleza – ni katika mababu wa Mtume (s.a.w) - na Seif bin dhi Yazin miongoni mwa wafalme wa Yemen na Tubbai miongoni mwa wafalme wa Uhabeshi na mfano wao kati ya watambuzi, mawalii wa zama hizo, wameeleza waziwazi kuhusu utume wa Muhammad (s.a.w) na kuutangaza kwa mashairi. Hata mmoja wa wafalme hao alisema: “Mimi nachagua kumhudumia Muhammad kuliko huu ufalme”. Na mwingine alisema: “Ningemkuta ningekuwa ni bin ami yake” yaani ningekuwa kama Ali (r.a) mwenye kujitole na waziri wake. Imetajwa katika (Andiko la kumi na tisa) habari muhimu na thabiti katika habari hizi. Kwa hali yoyote hawa watambuzi wanashuhudia ushahidi wa kweli wa kiujumla wenye nguvu juu ya utume wa Muhammad (s.a.w) na juu ya ukweli wake, kama vitabu vya historia na sira vilivyoeleza habari hizi kwa ukunjufu kamili. Vilevile maruhani, hawaonekani lakini husikika kauli zao na wanaitwa: Hawatifu na wanashuhudia ushahidi wa kweli kama watambuzi na makuhani, juu ya utume wa Muhammad (s.a.w) kwa uwazi sana. Na vilevile wengi kati ya waelezaji, bali hata wanyama dhabihu zinazo chinjwa kwenye madhabahu yao kwa ajili a masanamu, na masanamu yenyewe na ushahidi wa makaburi wote hao wameelezea kuhusu unabii wake (s.a.w). Wanashuhudia ushahidi wa kweli juu ya utume wake na haki yake kwa ulimi wa historia. Ushahidi wa kumi na nne: ushahidi wenye nguvu wa ulimwengu unaashiriwa na kifungu hiki cha Kiarabu: [Na kwa ushahidi wa viumbe kwa malengo yake na makusudio ya kiungu kwao juu ya utume wa Muhammad (s.a.w) ambao ni jumuishi, kwa sababu ya uhitaji wa kupatikana kwa malengo ya viumbe na makusudio ya kiungu kutegemea hilo na kuthibiti thamani yake na majukumu yake na kudhihiri kwa uzuri wake na ukamilifu wake na kutimia kwa hukumu ya hakika zake juu ya utume wa Ubinadamu hasa kwa utume wa Muhammad (s.a.w), kwani ndiyo wenye kudhihirisha na uwanja ulio kamili, bila utume huo, viumbe hivi vyenye kukamilisha na kitabu kikubwa chenye maana ya milele ingekuwa ni vumbi lenye kupeperushwa, maana yale yenye kuruka mbali na ukamilifu wake ungedondoka na jambo hilo ni muhali kwa namna mbalimbali] Risala ya (Ishara kuu) imeeleza yanayohusu fungu hili la Kiarabu yafuatayo: Ulimwengu huu kama unavyojulisha juu ya fundi wake na mwandishi wake na mtia sura wake ambaye ameupatisha na anayeuendesha na kupangilia na anausarifu kwa kuupa sura kukadiria na kuendesha kana kwamba ni kasri kubwa na kana kwamba ni kitabu kikubwa au kama ni maonesho ya ajabu au kama ni makusanyo makubwa, basi vilevile hakuna namna unahitajia kuwepo kwa atakayeelezea yaliyomo katika kitabu hiki kikubwa maana yake mbalimbali, na anayejua na kujulisha makusudio ya kiungu nyuma ya uumbaji wa ulimwengu, na kubainisha hekima za kiungu, katika mabadiliko yake, na kusomesha matokeo ya michakato yake ya kimajukumu, na kutangaza thamani ya hakika yake na ukamilifu wa viumbe vilivyomo, kufafanua na kujibu maswali ya kutisha na yanayosababisha kutahayari, vilivyomo vinatokea wapi hivi, na hatima ni wapi, na kwa nini havikai hapa bali vinapita na kuondoka haraka? Na kufafanua maana ya kitabu hicho kikubwa na kufasiri hekima za aya zake za kimaumbile. Yaani unahitajia mlinganiaji mkubwa, mwitaji wa kweli, ustadhi wa hakika na mwalimu hodari. Ulimwengu kwa muktadha huu unajulisha na kushuhudia ushahidi wenye nguvu na wa kiujumla juu ya ukweli wa nabii mtukufu (s.a.w), na kusibu kwake, ambaye ndiye mtu bora zaidi aliyetimiza majukumu haya. Na kwa kuwa yeye ni mtume bora na mkweli zaidi aliyetumwa na Bwana mlezi. Basi ulimwengu unashuhudia kwa kusema: Ash hadu ann Muhammadan Rasuulu Al-Lah. Naam, hakika ya ulimwengu, thamani yake na sifa zake pambanuzi hutimia kwa nuru ambayo amekuja nayo Muhammad (s.a.w) na kwa nuru hiyo hujulikana kazi za vilivyomo na matokeo yake na majukumu yake na thamani yake, na kwa nuru hiyo ulimwengu unazingatiwa kuwa ni maandishi fasaha ya kiungu na Qur’an ya kiungu yenye umbo na maonesho ya athari za kiungu za kutisha. Kwani bila ya nuru yake (s.a.w) ulimwengu ungekuwa ni matanga wenye kutisha na uharibifu wa kuogofya wenye michanganyiko yenye kushabihiana na misukosuko yenye kufuatana unaoangukia kwenye giza la kukosekana, mchezo, na kutoweka. Kwa msingi wa hakika hii hakika sifa za ulimwengu na makamilifu yake na mabadiliko yake yenye hekima na maana yake ya kudumu milele yanasema kwa nguvu: Nash hadu anna Muhammdan Rasulu Allah. Ushahidi wa kumi na tano ambao unakusanya ushahidi mwingi: Nayo ni: Hakika mabadiliko yote, michakato, utulivu, uhai, umauti, na mfano wa hayo miongoni mwa matendo yanayoendelea ulimwenguni hutimia kwa amri itokanayo na nguvu ya dhati takatifu ambayo ni wajibu kuwepo ambayo inasarifu katika ulimwengu huu kuanzia atomu (chembe vumbi ndogo kabisa) hadi katika sayari, basi vinashuhudia matendo ya Rububiyya yake na matendo ya rehema zake juu ya utume wa Muhammad (s.a.w). Fungu lijalo la Kiarabu linaelezea ushahidi huu mtukufu wa hali ya juu: [Na kwa kushuhudia mwenye viumbe na muumba wake na msarifu wake juu ya utume wa Muhammad (s.a.w), kwa matendo ya rehema zake na matendo ya Rububiyya yake, kama utendaji wa hali ya rehema kwa kumteremsha Qur’an ya muujiza ya ubainifu, na kwa kudhihirisha aina ya miujiza kupitia yeye, na kumwafikisha na kumhami katika hali zake zote, na kwa kudumisha dini yake kwa hakika zake zote, na kuinua makamo ya utukufu wake juu ya viumbe wote kwa kuonekana waziwazi, na kama utendaji wa Rububiyya yake kwa kufanya ujumbe wake ni jua la kimaanawy kwa viumbe, na kwa kufanya dini yake ni faharisi ya makamilifu ya ibada zake, na kwa kufanya hakika yake ni kioo chenye kukusanya midhihirisho ya Uungu wake, na kwa kumpa nyadhifa za dharura za lazima kwa uwepo wa viumbe katika viumbe hivi kama ulazima wa rehema, hekima, na uadilifu na kama dharura ya ulazima wa chakula, maji, hewa na mwanga.] Maelezo ya ushahidi huu mkubwa wenye kukata shauri ambayo ni mapana sana tunaelekeza kwenye Risale-i Nur, na tunatazama maana yake ya jumla kwa ishara fupi mno: Hakika tunashuhudia kwenye ulimwengu kwa macho yetu kwamba katika ada ya Rububiyya inayoendelea kila wakati kwa uadilifu, hekima na uangalizi, kuwahami wema na kuwatia adabu waongo na waharibifu, tunashuhudia hayo ndani ya matendo yake (s.w) yaliyopangika. Kwa mujibu wa matendo yake ya rehema kuteremsha Qur’an ambayo ni muujiza wa bayana juu ya Muhammad (s.a.w), na kudhihirisha aina ya miujiza mingi yenye kufikia kiasi cha miujiza elfu moja mikononi mwake, na kumhami chini ya ubawa wa upole wake wenye huruma katika hali zake zote bali katika mazingira yake magumu hatari mno, hata kumlinda kwake kwa njiwa na buibui! Na kumwafikisha kwa taufiki yenye kutia nguvu katika majukumu yake, na kuidumisha dini yake na hakika zake zote, na kuvika taji ardhi na wanadamu kwa Uislamu wake. Na kunyanyua makamo na utukufu wake kwenda katika makamo matukufu zaidi, na kumfanya kuwa bora juu ya viumbe wote kwa kumtunuku makamo ya kuridhiwa na kukubaliwa na daima yanayovuka bora wa wanadamu, na kumpa haiba inayobeba tabia nzuri mno kwa maafikiano ya wanaompenda na maadui hata ikafanywa humsi (moja ya tano) ya watu ni katika umma wake, yote hayo yanashuhudia kwa ukweli bila shaka yoyote juu ya ukweli wake (s.a.w) na utume wake. Na kadhalika tunashuhudia kwa upande wa matendo ya Rububiyya yake (s.w): Kwamba msarifu wa ulimwengu huu na mwendeshaji wa mambo yake amejaalia utume wa Muhammad (s.a.w) ni jua la kimaanawy la ulimwengu. Hakika imethibitishwa katika Risale-i Nur: kwamba ametokomeza giza lote kwa utume huo, hali ya kudhihirishia hakika za kinuru za kiulimwengu, na amefurahisha wote wenye utambuzi bali ulimwengu wote, kwa bishara ya maisha ya kudumu. Na kufanya dini yake vilevile ni faharisi ya makamilifu ya waja wake wote wenye kukubaliwa, na mwongozo ulionyooka wa matendo ya uja. Na kufanya hakika ya Muhammad (s.a.w) nayo ni haiba yake ya kimaanawy ni kioo chenye kujumuisha midhihirisho ya uungu wake, kwa dalili ya Qur’an tukufu na Al-Jawshan al-Kabir, bali amemjaalia kuwa anapata - zaidi ya hakika tulizoashiria - mfano wa mema ya uma wake wote kwa kila siku kwa muda wa karne kumi na nne, na kumleta kwa wanadamu wote na kumkabidhi majukumu matukufu, na kumfanya kigezo chema na kiongozi bora na Bwana mtukufu zaidi kwa wanadamu wote, kwa dalili ya athari zake katika maisha ya kijamii, ya kimaanawy na kiutu, na kufanya wanadamu wote wanahitajia dini yake na sharia yake na hakika zake ambazo amezileta katika Uislamu , haja yake ya rehema, hekima, uadilifu, chakula, hewa, maji na mwanga, hoja zote hizi za kiujumla zenye kukata shauri zinazofikia hoja kumi na mbili, ni ushahidi wenye nguvu wa hali ya juu wa utume wa Muhammad (s.a.w). Je inayumkinika kwamba utume wa Muhammad usiwe jua la kimaanawy la ulimwengu hai ya kuwa umepata idadi hii ya ushahidi wa kiujumla mpana kutoka kwa bwana mlezi wa walimwengu wote ambaye hapuuzii kuchunga na kupangilia chochote vyovyote kiwavyo hata ubawa wa nzi na ua dogo sana. Kila ushahidi katika shahidi hizi kumi na tano zinajumuisha shahidi nyingi mno, hata ushahidi wa tatu umethibitisha madai: Ash hadu anna Muhammadan Rasuulullah kwa kukata shauri kabisa na nguvu iliyojikita kwa kuingia chini yake shahidi elfu moja kwa ulimi wa miujiza, na zimetangaza kutimia kwake na thamani yake na umuhimu wake mkuu kiasi mamia ya mamilioni ya ndimi urefu wa ulimwengu wa Kiislamu na upana wake zinatangaza madai hayo kwa ulimwengu kila siku mara tano. Kama ilivyo mabilioni ya watu wa imani wameridhia na kusadikisha bila shaka kwamba msingi wa madai hayo - nayo ni hakika ya Muhammad (s.a.w) - ni mbegu ya asili ya ulimwengu na sababu ya kuumbwa kwake na ukamilifu wa tunda lake, na kwamba Bwana mlezi wa walimwengu wote (s.w) amejaalia hiyo haiba ya Muhammad (s.a.w) ni mlinganiaji wa hali ya juu kwa ufalme wa Rububiyya yake, ufumbuzi wa kweli wa fumbo la viumbe na funiko la viumbe, na ni mfano wenye kuangaza wa upole wa rehema zake, na ulimi wenye ufasaha wa huruma yake na mapenzi yake, na mbashiri mkuu wa furaha ya kudumu katika ulimwengu wa milele, na aliyeletwa mwisho na mkuu kati ya mitume wake (s.a.w). Basi hasara iliyoje kwa mtu ambaye haamini ukweli wenye hakika hii, au hauthamini! Ubaya uliyoje na ukubwa wa kutenda kwake upumbavu na jinai kubwa. Kama ilivyo sura (Al-Fatiha) ambayo imo kwenye swala kwa ishara zake kwenye sehemu ya pili inabainisha hoja za kukata shauri juu ya madai ya hakika ya Tawhidi katika (Ash hadu an laa ilaha illa Llah) na kuweka kiasi kisicho na mipaka cha alama ya kusadikisha, vivyo hivyo inaleta katika sehemu hii ya tatu vilevile mashahidi wenye nguvu wanasadikisha yaliyomo katika Tashahudi (Ashahadu anna Muhammadan Rasuulullah) na wanaweka alama nyingi za kusadikisha zisizo na hesabu. فيا ارحم الراحمين بحرمة هذا الرسول الأكرم ﷺ، وفِّقنا لنيل شفاعته واتباع سنته السنية، واجعلنا بجوار آله وأصحا به الكرام في دار السعادة الأبدية. آمين آمين آمين. اَللّٰهُمَّ صَلِّ وَ سَلِّم۟ عَلَي۟هِ وَ عَلٰى اٰلِهٖ وَ صَح۟بِهٖ بِعَدَدِ حُرُوفِ ال۟قُر۟اٰنِ ال۟مَق۟رُوئَةِ وَ ال۟مَك۟تُوبَةِ اٰمٖينَ سُب۟حَانَكَ لَا عِل۟مَ لَنَٓا اِلَّا مَا عَلَّم۟تَنَٓا اِنَّكَ اَن۟تَ ال۟عَلٖيمُ ال۟حَكٖيمُ
[Na nyakati zilizopangwa maalum na riziki zilizowekewa kanuni] Hakika ya nyakati maalum na riziki ambazo kwa nje zinaonekana kana kwamba zisizojulikana na zisizokuwa maalum, isipokuwa katika uhalisia ni kuwa hayo ni mambo yaliyokadiriwa chini ya pazia la kutojulikana katika daftari la Qadhaa na Kadari la azali, na katika ukurasa wa makadirio ya kiuhai. Muda wa umri uliyopangwa lazima kutimia kwa kila mwenye uhai umekadiriwa na kuwekwa maalum hautangulii saa wala kuchelewa, na riziki ya kila chenye roho imeainishwa na kuhusishwa, na vyote hivyo vimeandikwa katika ubao wa Qadhaa na Kadari, Zipo kiasi kisichokua na mpaka cha dalili juu ya hukumu hii, miongoni mwa hizo: Hakika kufa kwa mti mkubwa na kurithisha mbegu zake ambazo ni sawa na aina ya roho yake, ili zitimize majukumu iliyokuwa unayatekeleza, hakutimii isipokuwa kwa kanuni ya mwenye hekima ya mjuzi wa kila kitu Mwenye kuhifadhi kila kitu. Hakika yanayobubujika kutoka katika chuchu ambayo ni maziwa safi na riziki kwa mtoto, na kutoka kwake kati ya kinyesi na damu bila kuchanganyika, yakiwa safi twahara, na kutiririka kwake kwenda kwenye kinywa chake, inajibu jibu lenye nguvu dhidi ya uwezekano wa kutokea hayo kwa kusadifiana, na inabainisha kutokea kwake wazi kabisa kuwa ni kupitia katika kanuni yenye huruma iliyowekwa kutoka kwa Mtoaji riziki mjuzi wa kila kitu mwenye kurehemu. Na pimia baki ya wenye uhai na roho kwa vielezo hivi viwili ambavyo ni sehemu ndogo. Hakika ya mambo ni kuwa umri ni maalum na umekadiriwa, na riziki hivyohivyo, vimewekwa katika daftari la vikadiriwa na kila moja kati yao imejaaliwa kuwa ni maalum. Lakini viwili hivyo vinaonekana - katika hali ya nje - vimeambatana katika nyuzi za kutojulikana, visivyoonekana kudhihiri kana kwamba sio maalum hasa, na kana kwamba zimefungwa kwenye kusadifiana, yote hayo ni kwa ajili ya hekima makini na upeo wa umuhimu! Ingekuwa muda wa kifo ni maalum kama kuzama kwa jua mwanadamu angekuwa anatumia nusu aya umri wake katika tabaka la ghafla na kuupoteza, hali ya kuwa mbali na jitihada ya akhera kisha anaingia katika nusu nyingine ndani ya hofu za kutisha, atakuwa kama mtu ambaye kila siku anapiga hatua moja kuelekea katika milingoti ya mahali pa kunyongea, na msiba ambao ungekuwa umeingia katika siku ya kifo unaongezeka kwa mamia! Na kwa ajili ya siri hii makini - misiba ambayo humrejea mwanadamu kwa kawaida - imebakishwa chini ya pazia la ghaibu. Bali hata siku ya mwisho wa dunia yenyewe ambayo ni kiama ameificha (s.w) - kwa rehema na huruma zake – chini ya pazia la ghaibu kwa sababu hiyohiyo. Ama riziki, kwa sababu ni hazina kubwa inaleta neema baada ya neema ya uhai, na chimbuko tajiri mno huelekewa kwa shukrani na sifa njema, na hazina jumuishi mno ya uja na dua na mahali na njia za matarajio, imeoneshwa katika sura yake ya dhahiri kana kwamba haijulikani na imefungwa na kusadifiana, na hii ni kwa sababu mlango wa kutafuta riziki usifungwe kwa dua kutoka kwa mwenye kuruzuku Mkarimu kila wakati, na ili mlango wa kukimbilia na maombi yenye kutumiwa shufaa kwa sifa njema na shukurani kwa Allah (s.w) usifungwe, kwani kama riziki ingekuwa ni maalum (inajulikana) kama kuchomoza kwa jua na kuzama kwake, hakika yake ingekuwa imegeuka kabisa, na ingekuwa milango ya matarajio na madirisha ya unyenyekevu na ngazi za dua ambazo zote zimejazwa shukurani nzuri na ridhaa njema ingefungwa hadi mwisho wake, bali ingekuwa milango ya uja wenye khushui, nyenyekevu imefungwa moja kwa moja. Dalili ya tisa na kumi: Nazo ni: [Ufundi fani kwa fani na umuhimu uliowekewa mapambo] Yaani kila kilichotengenezwa katika viumbe vyote vizuri vilivyotawanywa ardhini kote, na hasa katika majira ya machipuo kinabainisha midhihirisho ya uzuri wa kudumu milele. Kwa mfano chukua: Maua na matunda na ndege wadogo na vijidudu na hasa wenye rangi ya dhahabu ya kung’ara, katika kuumbwa kwao na katika sura zao na katika zana zao kuna umahiri na muujiza na ufundi makini wa ajabu na ukamilifu wenye muujiza wa fundi wake mtukufu, katika maumbo anuwai na namna tofauti na mashine makini kuna kinachojulisha waziwazi juu ya ujuzi wenye kuzungukia kila kitu na uwezo wa kielimu wenye stadi na fani mbalimbali - ikifaa maelezo hayo –, na kinashuhudia kwa ukweli kwamba kuingilia sadifu na sababu zenye kusongana zisizokuwa na utambuzi, ni muhali katika muhali. Na kwamba maelezo: (Na umuhimu uliwekewa mapambo) yanamaanisha: Kwamba katika hivyo vilivyotengenezwa vizuri kuna upambaji maridadi mtamu na mapambo ya fahari yenye kupendeza sana na urembo wa ufundi unaovutia anafanya uyafanyayo kwa ujuzi usio na ukomo, na anajua hali nzuri zaidi na hali maridadi zaidi ya kila kitu, na anataka kuonesha uzuri wa ukamilifu wa upendezeshaji na ukamilifu wa uzuri wake kwa wenye utambuzi kwa kiasi anaumba ua dogo sana la kisehemu na mdudu mdogo sana na kumtia sura kwa kumtilia umuhimu wa kiwango kikubwa na kwa umahiri wa hali ya juu na kwa ufundi wa ajabu. Huku kupamba na kurembesha ambako kuna sifa ya kutilia umuhimu na utunzaji, kunajulisha wazi juu ya ujuzi wenye kuzungukia kila kitu na kunashuhudia juu ya kupasa uwepo wa fundi mjuzi mwenye uzuri kwa idadi ya viumbe wazuri. Dalili ya kumi na moja yenye kukusanya dalili tano na hoja tano: [Na upeo wa ukamilifu wa mpangilio, kulingana vipimo, kupambanuka, bila mipaka na kwa wepesi usio na mipaka. Na uumbaji vitu kwa wingi usio na mipaka pamoja na uzuri usio na mipaka. Na katika kasi isio na mipaka pamoja na kulingana vipimo bila mipaka. Na katika upana usio na mipaka pamoja na ukamilifu wa ufundi mzuri. Na katika umbali usio na mipaka pamoja na kuafikiana kusiko na mipaka. Na katika mchanganyiko usio na mipaka pamoja na kupambanuka kusiko na mipaka] Dalili hii ni tamko lingine la dalili iliyoelezwa mwishoni mwa kifungu cha Kiarabu kilichopita na ni kizuri zaidi kuliko hicho, nao ni ufafanuzi wa dalili tano na sita ambazo ni pana, tunaiashiria kwa upeo wa kufupisha kwa sababu ya maradhi makali. Kwanza: Tunashuhudia ardhini kote kwamba ufundi wa mashine za ajabu, kwa wepesi wote na urahisi kwa mkupuo, kunatokana na ujuzi kamili na umahiri uliotimia, bali baadhi yake kutengenezwa kwenye dakika moja, kwa namna iliyopangika yenye kupimwa, pamoja na tofauti na viumbe wengine mfano wake, kunajulisha kikamilifu juu ya ujuzi usio na kikomo, na juu ya ukamilifu wa ujuzi huo, kwa kiwango cha wepesi na urahisi unaotokana na umahiri wa kiujuzi katika utengenezaji. Pili: Hakika kuumba viumbe katika wingi wa kupindukia usio na ukomo na idadi kubwa isiyokuwa na mipaka kwa ufundi na bila kukosea wala kubabaika kunajulisha juu ya ujuzi usio na mipaka ndani ya uweza usio na ukomo, na unashuhudia shahidi zisizo na mpaka juu ya mjuzi asiye na mipaka na mweza asiye na mipaka. Tatu: Hakika kuumba viumbe ambavyo viko katika upeo wa mizani na kipimo katika ukomo wa kasi, kunajulisha juu ya ujuzi usio na mipaka, kunashuhudia kwa idadi ya viumbe hivyo juu ya mjuzi wa kila kitu bila mipaka na mweza wa kila kitu bila mipaka. Nne: Hakika kuumba vyenye uhai visivyodhibitika na hesabu katika ukunjufu usio na mipaka unaotosha ardhi yote, katika ufundi ulio timamu mno katika kutengeneza na katika kupamba, na ukamilifu wa uzuri wa kutengeneza, kunajulisha juu ya ujuzi wenye kuzungukia kila kitu, usio potea wala kusahau na unaona vitu vyote mkupuo mmoja wala hakimzuii kitu chochote na chochote, kila kilichopo kinashuhudia na vyote kwa pamoja ya kwamba ni kazi iliyotengenezwa na mjuzi wa kila kitu na mweza juu ya kila kitu. Tano: Hakika kuumba kila kimoja ya aina ambazo zinatenganishwa kati yake na masafa makubwa, mojawapo iko mashariki na nyingine iko magharibi na nyingine iko kaskazini na nyingine iko kusini, katika wakati mmoja, na kwa namna moja ikiwa inashabihiana na kufanana pamoja na kupambanuka kila moja kati yao na nyingine katika mwonekano, haiwezekani kuwa isipokuwa kwa uweza wa mweza wa kila kitu mwenye uweza usio na mipaka anatawalia ulimwengu wote kwa uweza wake na ujuzi wake anavizungukia vilivyomo pamoja na hali zake. Kwa hiyo viumbe hivi vinashuhudia ushahidi usio na mipaka juu ya ujuzi yenye kuzungukia kila kitu na juu ya mjuzi wa mambo yote ya ghaibu. Sita: Hakika kuumba mashine mengi yenye uhai katika mpambanuko maalum timamu na alama zenye kutenganisha na nyingine kama hizo, pamoja na kuwa katika msongamano mkali na katika mahali mwa giza – kama kokwa ambayo ipo chini ya udongo – na bila kuchanganyika wala kukosea wala kubabaika pamoja na kuwa imo katika mchanganyiko usio na mipaka, na kuumba zana za kila moja kati yao bila kasoro uumbaji wa muujiza, unajulisha kwa uwazi kama jua juu ya ujuzi wa azali na unashuhudia kwa bayana kama mchana juu ya Rububiyya na uumbaji wa mweza asiye na mipaka na mjuzi wa kila kitu asiye na mipaka. Tunalifupisha somo hili refu sana tukielekeza maelezo yake kwenye Risale-i Nur. Na sasa tunaanza suala la (Utashi) ambalo limo katika muhtasari wa muhtasari. [Allah ni mkubwa kuliko kila kitu kwa uweza na ujuzi, kwani yeye ni mwenye utashi wa kila kitu, anachotaka Allah huwa na asichokitaka hakiwi, kwa sababu mpangilio wa kupatisha vilivyotengenezwa kwa dhati, sifa, haiba na wasifu ni kati ya yamkini zisizo kuwa na mipaka na njia zisizo na tija na uwezekano wenye kubabaisha na mifano yenye kushabihiana, na ni katikati ya mifereji ya vipengele vyenye kusongana, kwa mpangilio huu makini nyororo, na kupimwa kwake kwa mizani hii nyeti sana, na kuipambanua kwa mifano hii yenye kushabihiana na ainisho zilizopambwa na kupangika, na kuumbwa viumbe vyenye kunadhimika hai kutoka katika rahisi na uhai mfu, kama mwanadamu na zana zake zote kuanzia kwenye manii na ndege na viungo vyake vyote kutokana na yai na mti na viungo vyake kutokana na kokwa na punje inajulisha kuwa kila kitu ni kwa utashi wake (s.w), uchaguzi wake, makusudio yake na majaaliwa yake, kama ilivyo kuafikiana kwa vitu katika misingi ya viungo ya kiaina na jinsia inajulisha kuwa mtengenezaji wa vitu hivyo ni mmoja wa pekee, vilevile kupambanuka kwake kwa aina zilizopambika na maumbo yenye kupambanuka inajulisha kuwa fundi huyo mmoja wa pekee ni mtendaji mwenye hiari anafanya anachokitaka na anahukumu anachokitaka]. Kifungu hiki ni dalili moja ndefu na ya jumla katika dalili za (Utashi wa kiungu) inajumuisha hoja za jumla nyingi sana, tunabainisha pamoja na kutafsiri yaliomo kwa muhtasari, dalili inayothibitisha utashi wa kiungu, hiari na kutaka kwake kwa namna ya kukinaisha, ukiachilia mbali kwamba dalili zote za (Ujuzi wa kiungu) zilizotajwa hapo kabla ni dalili za Utashi wa kiungu vilevile, kwa kuwa midhihirisho ya (Ujuzi na utashi wa kiungu) na athari zake zinashuhudia kwa pamoja katika kila kilichotengenezwa. Muhtasari wa yaliyomo katika kifungu hiki cha Kiarabu ni: Kwamba kila kitu hupatikana kwa Utashi wake (s.w), basi akitakacho hua na asichokitaka hakiwi, hufanya atakacho, na hakiwi chochote asichokitaka. Na hoja moja katika hoja zake ni: Hakika tunashuhudia kila kilichotengenezwa kati ya hivi vilivyotengenezwa kimepambanuka kwa dhati maalum na sifa mahsusi na haiba yake maalum, na sura yenye alama zenye kutenganisha na kupambanua. Na wakati ambapo inayumkinika hali zote hizi ndani ya yamkini na ya yawezekanayo yenye kubabaisha bila mipaka, na kupita katika njia nyingi zisizo na tija wakati wa maingiliano ya mifereji ya vipengele na ndani ya mifano yenye kushabihiana yenye kusababisha kusahau na kuchanganya, kwani kuumba kwake – sambamba na hali hizi zenye kugongana na kuchanganyika – ndani ya mpangilio makini uliopimwa na kuratibiwa, na kila moja kati ya viungo vyake na zana zake kuchukua mizani nyeti yenye hisia sana, na kila moja kati yake kuituliza mahali pake panapofaa, kuikabidhi nyadhifa, na kutunuku uso wake alama za haiba maalum nzuri zenye kupambwa, na kuumba viungo vyake vyenye kuhitilafiana kuwa mbalimbali kutokana na maada rahisi mfu, ikiwa na uhai imewekwa vizuri kiufundi, kama kumuumba mwanadamu ambaye anabeba mamia ya zana anuwai katika sura ya muujiza kutokana na tone la maji. Na kumuumba ndege kwa zana na viungo tofauti anuwai kutokana na yai jepesi, na kuanzisha mti pamoja na matawi yake yenye kusongana na kupachana na sehemu tofauti, kutokana na mbegu ndogo sana yenye kuundwa kutokana na vitu rahisi mfu ambazo ni kaboni na azuweti na kizalishi cha tindi kali na kizalishi cha maji (Oksijeni na Haidrojeni), na kuwekea umbo lililopangika na lenye tija, inathibitisha bila shaka na uwazi na ukinaishi usio na shaka bali kwa kiwango cha wajibu na dharura na ulazima kwamba kila kilichotengenezwa kati ya hivi vilivyotengenezwa hupewa hali hiyo maalum kamili kwa atomu zake zote na zana zake na sura yake na haiba yake, kwa utashi wa mweza mwenye uwezo usio na mipaka, kwa kutaka kwake, hiari yake na makusudio yake (s.w). Na kwamba hicho kilichotengenezwa kinatii maamuzi na utashi wenye kuenea kila kitu. Ni hivi hakika ya kujulisha kwa hiki kilichotengenezwa kimoja kwa hali isiyo na shaka ndani yake juu ya (Utashi wa kiungu) kunabainisha kwamba vyote vilivyotengenezwa vinashuhudia ushahidi wa ukweli fasaha usio na ukomo na kwa idadi ya kila kimoja kwa ukinaishi dhahiri kama jua na mchana juu ya (Utashi wa kiungu) wenye kuenea katika kila kitu. Na kwamba hizo ni hoja za kukinaisha hazina mpaka juu ya kupasa kuwepo mweza mwenye utashi. Kisha dalili zote za (Ujuzi) zilizoelezwa huko nyuma ndiyo dalili za (Utashi wa kungu) vilevile, kwani zote hizo mbili zinafanya pamoja na (Uweza wa kungu) haiachani moja wapo na nyingine. Kama ilivyo kwamba kuafikiana kwa viungo vya kiaina na kijinsia kwa watu wa kila jinsia na kila aina kunajulisha kwamba mtengenezaji wake ni mmoja pekee, vilevile tofauti katika alama za nyuso zao tofauti yenye hekima, kunajulisha kwa kukinaisha kabisa kwamba huyo fundi mmoja wa pekee, ni mtendaji mwenye uchaguzi, anaumba kila kitu kwa kutaka, kuchagua, kupenda na makusudio. Na kama hivi ufafanuzi wa tafsiri ya muhtasari imekwisha ya kifungu cha Kiarabu kilichoelezwa, kinachojulisha kwa ujumla wa kipekee juu ya (Utashi wa kiungu). Nilikuwa nimeazimia kuandika nukta muhimu sana zinazohusu (Utashi wa kiungu) kama ilivyo kwenye suala la (Ujuzi wa kungu), isipokuwa maradhi yanayotokana na kutiliwa sumu yametia uchovu katika ubongo wangu, hivyo ninayaahirisha hadi wakati mwingine kwa kupenda kwake Allah (s.w). Ama fungu ambalo linahusu Uweza wa kiungu ni: [Hakika Allah (s.w) ni mkubwa kuliko kila kitu kwa uweza na ujuzi kwani yeye ni mweza juu ya kila kitu kwa uweza usio na mipaka wenye kuzungukia kila kitu wa dharura wenye kuanzisha wenye kulazimu wa kidhati takatifu, basi ni muhali kuingilia dhidi yake, na hakuna ngazi katika huo, kwa mnasaba wake vinakuwa sawa atomu, nyota, sehemu, kitu kizima, cha sehemu, cha kitu kizima, kokwa, mti, ulimwengu na mwanadamu, kwa siri ya kushuhudia upeo wa ukamilifu wa mpangilio, kulingana vipimo, kupambanuka na kutengeneza uzuri kusiko na mipaka. Pamoja na wepesi katika wingi, kasi na mchanganyiko usio na mpaka. Na kwa siri ya hali ya nuru, uangavu, kukabiliana, kuendana vipimo, kupangika na utekelezaji. Na kwa siri ya msaada wa Umoja, wepesi wa Umoja na kudhihiri kwa upekee. Na kwa siri ya kupasa, kutakasa na kutofautiana kwa hakika. Na kwa siri ya kutofungika, kutokushika upande maalum na kutokugawanyika katika sehemu mbalimbali. Na kwa siri ya kupinduka kwa vikwazo na vizuizi kwenda katika nafasi ya nyenzo na virahisishi. Na kwa siri ya kuwa atomu, kijisehemu, kokwa na mwanadamu sio kitu kichache kwa kutengenezwa na wepesi kuliko nyota, kitu kizima, cha jumla, mti na ulimwengu, basi muumba wake ndiyo muumba wa hii kwa mawazo ya kiushahidi. Na kwa siri kwamba kilichozungukwa na vijisehemu ni kama mifano iliyoandikwa iliyowekwa katika umbo dogo au kama nukta zilizokamuliwa sana. Basi hapana budi mzunguko na vitu vizima kuwa katika udhibiti wa muumba wa vyenye kuzungukwa na vijisehemu ili kuingiza mifano yake humo kwa vipimo vya ujuzi wake au kuvikamua kutokea humo kwa kanuni za hekima yake. Na kwa siri ya kama ilivyo Qur’an ya utukufu iliyoandikwa kwenye atomu inayoitwa kwa jina la johari pekee kwa atomu za Athiir sio yenye ujazo wa uchache na ajabu wa ufundi kuliko Qur’an ya U-adhama iliyoandikwa kwenye ukurasa wa mbingu kwa wino wa nyota na majua, vilevile ua sio la uchache kwa ujazo na ufundi kuliko nyota ya zuhura yenye kumetameta wala mdudu chungu kuliko tembo, wala kimelea kulinganisha na genosera, wala nyuki kuliko mtende, kwa mnasaba wa uweza wa muumba wa viumbe. Kama ilivyo kwamba upeo wa ukamilifu wa wepesi na urahisi katika kupatisha vitu kumewaingiza watu wa upotevu katika mgogoro unaolazimiana wa muhali zisizokuwa na mpaka zinazomiminwa na dhana, vivyo hivyo imewathibitishia watu wa hidaya kusawazika kwa nyota pamoja na atomu mbele ya uweza wa muumba wa viumbe (s.w) lailaha illa Huwa Allahu Akbar]. Kabla ya kuingia katika kubainisha yaliyomo katika kifungu hiki kitukufu ambacho kinahusu (Uweza wa kiungu) na ambayo ni sawa na tafsiri na madhumuni yake, tunabainisha hakika iliyopitishwa moyoni nayo: Hakika kuwepo kwa uweza wa kiungu ni kwenye kukinaisha zaidi kuliko kuwepo kwa ulimwengu, bali viumbe wote na kila kiumbe kwa dhati yake, ni maneno yalio kwenye mwili ya uweza huo, yanaibainisha na kuidhihirisha kwa dhati ya yakini, nazo ni shahidi kwa idadi yake juu ya mwenye kusifika wake mweza asiye na mipaka, kwa hiyo hapana haja ya kuthibitisha uweza huo kwa hoja na dalili. Bali inalazimu kuthibitisha hakika tukufu inahusu uweza na mbayo ni msingi muhimu katika imani na jiwe la msingi madhubuti la ufufuo na kukusanywa na eneo la lazima la masuala mengi ya kiimani na hakika tukufu za Qur’an na madai yanayotolewa na Aya tukufu: مَّا خَلْقُكُمْ وَلَا بَعْثُكُمْ إِلَّا كَنَفْسٍ وَاحِدَةٍ na ambayo yamefanya akili kuhemewa kuhusiana nayo na kubakia katika tahayuri na kutojiweza, bali baadhi yake zimepotea. Basi msingi huo na hilo jiwe la nguzo ya pembeni na nyanja hiyo na madai hayo na hakika hiyo ndiyo maana ya aya tukufu iliyotajwa. Yaani enyi majini na wanadamu hakika kuwaumbeni na kuwafufua siku ya kiama ni jambo jepesi kwa uweza wangu sawa na wepesi wa kupatisha nafsi moja, yeye ndiye ambaye anaumba majira ya machipuo mfano wa kuumba kwake ua moja kwa wepesi na urahisi, hakuna tofauti kulingana na uweza huo kati ya sehemu, kitu kizima, kidogo, kikubwa, kichache na kingi, uweza huo unaendesha sayari kwa wepesi ule wa kuendesha atomu. Basi kifungu hicho cha Kiarabu kilichoelezwa kinabainisha suala hili tukufu kwa hoja yenye nguvu ya kukinaisha katika ngazi tisa. Hakika ya kifungu kifuatacho kinaashiria katika msingi wa ngazi na kufupisha kifungu cha Kiarabu kwa muhtasari sana: [Kwa kuwa yeye ni Mweza juu ya kila kitu kwa uweza usio na mipaka wenye kuzungukia kila kitu wa dharura wenye kuanzisha wenye kulazimu kidhati, kwa dhati takatifu. Basi ni muhali kuingilia dhidi yake, hakuna ngazi katika uweza huo, hivyo vinakuwa sawa kwa mujibu wake atomu, nyota, sehemu, kitu kizima, cha sehemu, cha kitu kizima, kokwa, mti, ulimwengu na mwanadamu]. Yaani ni mweza juu ya kila kitu kwa uweza wenye kuzungukia kila kitu, na wenye kulazimu kwa ulazima wa kidhati na ni wa wajibu wa kidharura wenye kuanzisha - kama katika elimu ya mantiki - kwa ambaye ni wajibu kuwepo, ni muhali kuachana kwake na haiyumkiniki hivyo kabisa. Kwa kuwa mfano wa uweza huu ni wenye kuambatana kama hivi na dhati takatifu, hapana shaka kutojiweza ambako ni dhidi ya uweza hakuingii kwa upande wowote uwao, hakiwi kipingamizi cha dhati tukufu. Kwani kuwepo kwa ngazi katika kitu, ni kwa kuingilia dhidi yake ndani yake - kwa mfano: Ngazi za joto na viwango vyake ni kwa kuingia ubaridi, na viwango vya urembo ni kwa kuingilia ubaya – basi ni muhali kukaribia kwa kutojiweza ambako ni dhidi ya uweza, katika uweza huu usio na mipaka, na kwa kuwa hakuna ngazi ndani yake, nyota na atomu mbele yake huwa sawasawa, na hakuna tofauti kati ya sehemu moja na sampuli yake yote na mwanadamu na ulimwengu kwa mnasaba na uweza huo. Na kuhuisha kokwa moja na mti uliostawi na nafsi moja na wote wenye roho katika ufufuo ni sawa kwa upande wa uweza huo na ni rahisi kwake. Basi kwake hakuna tofauti kati ya mkubwa na mdogo na chache na nyingi. Chenye kushuhudia kwa ukweli wa kukinaisha juu ya hakika hii ni kile tunachokishuhudia katika uumbaji wa vitu kutokana na ukamilifu wa ufundi mpangilio na vipimo na kupambanuka na wingi katika kasi kubwa bila ukomo pamoja na wepesi usio na ukomo na urahisi uliotimia. Hakika hii iliyoelezwa ni madhumuni ya ngazi ya kwanza ambayo: [Na kwa siri ya kushuhudia upeo wa ukamilifu wa mpangilio, kulingamana vipimo, kupambanuka na kutengenezwa vema kusiko na mipaka, pamoja na wepesi usio na mipaka katika wingi na kasi na mchanganyiko]. Ngazi ya pili: Nayo ni: [Na kwa siri ya Nuru, uangavu, kukabiliana, kuendana vipimo, kupangika na utekelezaji]. Ufafanuzi wa ngazi hii na maelezo yake tunaelekeza mwishoni mwa (Neno la kumi) na katika (Neno la ishirini na tisa) na kwenye (Andiko la Ishirini) na hapa tunaashiria kwa ufupi: Naam, kama kuingia kwa mwanga wa jua na sura yake – kwa upande wa kinuru – kwa uweza wa kiungu katika uso wa bahari na vipovu vyake vyote ni jambo jepesi, kama kuingia kwake vyote sawasawa katika kipande cha chupa. Na vivyo hivyo uweza wa kinuru wa ambaye yeye ni nuru ya nuru, kuumba kwake mbingu na nyota na kuviendesha ni rahisi juu yake kama kuumba nzi na atomu na kuviendesha, hakuna kigumu kwake. Na kama inavyopatikana – kwa sifa ya uangavu – sura ya jua ya kimfano katika kioo kidogo na katika kiini cha jicho kwa uweza wa kiungu, basi kwa wepesi huohuo hutoa mwanga huo na sura hiyo kwa amri ya kiungu kwenda kwenye vitu vyote vyenye kung’ara na kwenye matone yote na atomu zote angavu na katika uso wa bahari. Vivyo hivyo hakika ya kudhihiri kwa uweza wa kiungu kusiko na mipaka na kuathiri kwake katika kupatisha nafsi moja nayo ni kwa wepesi huohuo katika kuwaumba wanyama wote kwa kuwa upande wa Kiufalme na hakika ya vyenye kutengenezwa na angavu na ng’avu. Hakuna tofauti kwa mnasaba wa uweza huo kati ya kichache na kingi kidogo na kikubwa. Kama ikiwa zitawekwa jauzi (punje kama karanga) mbili katika vitanga viwili vya mizani nyeti iliyotengenezwa vizuri sana inayopima milima, kisha ikawekwa kokwa ndogo kumojawapo kati ya vitanga viwili mizani hiyo itainyanyua kwa wepesi hadi kilele cha mlima na kushusha kingine hadi chini ya bonde, na ikiwa itawekwa milima miwili iliyo sawasawa badala ya jauzi mbili, hakika moja ya milima miwili utanyanyuka hadi mbinguni na mwingine utashuka hadi kwenye vina vya mabonde kwa urahisi uleule kama ingewekwa kokwa ndogo katika kitanga kimojawapo, vilevile (uwezekano ni wa sawasawa pande mbili) kwa mujibu wa maelezo ya elimu ya al-Kalaam, yaani uwepo wa vitu vya yamkini - yaani visivyokuwa vya lazima wala kuzuilika – na kukosekana kwake ni sawasawa, hakuna tofauti kati ya kuwepo kwake na kukosekana kwake kama haikuwepo sababu. Katika yamkini hii na kuwa sawasawa kati ya uwepo na kukosekana, huwa sawa chache na nyingi, ndogo na kubwa, na kama hivyo viumbe ni yamkini, na kwa kuwa uwepo wake na kukosekana kwake ni sawasawa ndani ya duara la kuyumkinika. Hakika uweza wa aliye wajibu kuwepo wa azali bila mipaka kama unavyotunuka uwepo kwa yamkini moja kwa wepesi sana, hukivika kila kitu uwepo unaoafikiana nao ukinyongesha mizania kati ya uwepo na kukosekana. Na kuiondoshea vazi la uwepo wa nje ikiwa jukumu lake limekwisha, na kuipeleka katika kukosekana kwa sura na dhahiri, bali katika uwepo wa kimaanawy kwenye uwanja wa ujuzi. Kwa maana ikiwa vitategemezwa vitu kwa mweza wa kila kitu na kukabidhi mambo yake kwake (s.w) hakika kuhuisha majira ya machipuo inakuwa rahisi kama kuhuisha ua moja, na kuhuisha watu wote kwenye ufufuo kunakuwa rahisi kama kuhuisha nafsi moja. Wakati ambao ikiwa itategemezwa uumbaji wa vitu kwenye sababu inakuwa kuumba ua moja ni ngumu kama ugumu wa kuumba majira kamili ya machipuo, na kuumba nzi mmoja kama kuumba walio hai wote. Na vivyo hivyo hakika ya jahazi moja kubwa na ndege kubwa hutembea kwa kiasi tu cha kugusisha ufunguo kwenye vyombo hivyo, kwa siri ya mpangilio, kwa wepesi wa kufungua saa na kufanyisha kazi. Vivyo hivyo hakika kukipa kila kitu kiwe kizima au sehemu, kidogo au kikubwa, kichache au kingi, wasifu wa kimaanawy, na kiwango maalum na mipaka maalum, kwa taratibu za ujuzi wa kiazali, na kwa kanuni za hekima ya milele, na kwa misingi maalum, na midhihirisho ya kiujumla ya utashi wa kiungu, hufanya vitu vyote kuwa ndani ya mipangilio ya kielimu kamili na kanuni ya Utashi. Hapana shaka kuendesha mfumo wa jua kwa uweza wa Mweza wa hali zote na kuendesha jahazi la ardhi katika mzunguko wake wa kila mwaka ni kwa wepesi sawa na uendeshaji wa damu na vilivyomo miongoni mwa chembe nyekundu na nyeupe na kuendesha atomu zake, mwendo na mzunguko ndani ya mpangilio na hekima hadi kwamba unaumba mwanadamu pamoja na zana zake za ajabu kutokana na tone la maji ndani ya mpangilio wa ulimwengu bila taabu wala uchovu. Kwa maana ikiwa kupatisha ulimwengu kutaegemezwa kwa uwezo huo wa azali wa hali zote mambo yanakuwa mepesi kama kupatisha mwanadamu mmoja, na kama hakukuegemezwa kwake basi kumuumba mwanadamu mmoja pamoja na zana zake za ajabu na hisia zake nyeti, itakuwa ni tatizo na jambo gumu kama kuumba ulimwengu wote. Na vivyo hivyo kama ilivyo kiongozi mmoja kwa kumwamrisha askari mmoja kushambulia itampelekea katika kushambulia, kwa siri ya utiifu na kutekeleza na kupokea amri, mtu huyo kwa amri hiyohiyo na kwa wepesi huohuo, vilevile atalipeleka jeshi kubwa tiifu kwenda kushambulia. Halikadhalika vilivyotengenezwa vipo katika ukamilifu wa utiifu wa kanuni za utashi wa kiungu kupokea ishara za amri za bwana mlezi za kimaumbile, nazo ni kama askari aliyekuwa tayari na kama mtumishi mwenye kuamuriwa katika mwelekeo wa kimaumbile na shauku ya kimaumbile ndani ya duara la taratibu za mstari wa kupita ambao ujuzi wa azali na hekima ya azali zimeuainisha, nao ni wenye utiifu zaidi na kufuata amri kwa mara elfu kuliko utiifu wa askari jeshi, hivi vilivyotengenezwa na hasa vilivyo na uhai kati yao kila mmoja anapopokea amri ya kungu Bwana mlezi: (Toka kwenye kutokuwepo nenda kwenye uwepo na shika jukumu) huivika uweza wa kiungu kwa wepesi wa hali zote uwepo maalum kwa namna ambayo ujuzi umeiainisha na kwa sura ambayo utashi umeihusisha na kuishika mkono wake hadi kwenye medani ya uwepo. Na kama hivyo, kwa wepesi huohuo na kwa nguvu na uweza huohuo Allah (s.w) huumba jeshi la walio hai katika majira ya machipuo na hulikabidhi majukumu. Kwa maana kwamba kila kitu kikiegemezwa kwenye uweza huo, hakika kupatisha majeshi ya atomu zote na makundi ya nyota zote ni rahisi kama urahisi wa kupatisha atomu moja na nyota moja, wakati ambapo ikiwa itaegemezwa kwenye sababu kuumba atomu katika kiini cha jicho la kiumbe hai na katika ubongo wake – hali ya ukubalifu ili iweze kutekeleza majukumu ya ajabu – inakuwa ni jambo lenye mishkeli na ugumu kama kuumba wanyama wote. Ngazi ya tatu: [Na kwa siri ya msaada wa Umoja na wepesi wa umoja na kudhihiri upekee] Tutaangalia madhumuni yake kwa ishara fupi sana: Kama kiongozi mkuu na mfalme mwenye haiba kwake huwa rahisi kuendesha mambo ya nchi pana na taifa kubwa kama wepesi wa kuendesha wakazi wa kijiji kimoja, na hiyo ni kwa umoja wa utawala wake na raia wake kufanya kulingana na amri zake peke yake. Kwa sababu kwa upande wa umoja katika utawala wake watu wa taifa hilo wanakuwa kama askari mmoja mmoja katika jeshi ni nyenzo za kurahisisha, hivyo amri na kanuni hutekelezwa kwa wepesi. Wakati ambapo mambo yakikabidhiwa kwa watawala tofauti, licha ya kuanguka katika lindi la mivutano na migongano kwa hakika kuendesha kijiji kimoja bali nyumba moja inakuwa na mishkeli kama kuendesha nchi pana. Kisha kila mtu katika watu wa taifa hilo tiifu lenye kufungamana na kiongozi mmoja tu, kama askari anaegemea kwenye nguvu ya kiongozi huyo na anategemea ghala la zana zake katika jeshi lake kubwa, na kwa ajili hiyo anaweza kumteka mfalme katika wafalme, na kutimiza kazi ambazo zaidi ya anazozifanya katika kazi zake binafsi. Kunasibiana na huyo mfalme kunakuwa ni nguvu kuu isiyo na ukomo na uwezo usio na mipaka kwa hiyo hutekelezea matendo makubwa matukufu, wakati ambapo kujinasibu huko kukikatika, hiyo nguvu kuu inaondoka na kupeperushwa na upepo, hawezi kutimiza kazi isipokuwa kiasi kilichomo kwenye mkono wake cha nguvu ya sehemu ndogo, na zana chache anazozibeba mgongoni mwake na mirusho michache. Kama askari huyu atatakiwa kutekeleza kazi anazotekeleza yule askari aliyeelezwa ingelazimu kuwepo nguvu ya jeshi kamili mkononi mwake na hazina za zana za mfalme ziwe mgongoni mwake! Jambo liko vivyo hivyo, hakika mfalme wa azali na milele, fundi mweza, kutokana na umoja wa ufalme wake na umoja wa utawala wake wa hali zote huendesha ulimwengu kwa wepesi sawa na kuendesha mji mmoja, na anaumba majira ya machipuo kwa wepesi wa kuumba bustani moja, na kuhuisha wafu wote katika ufufuo kwa wepesi wa kuumba majani ya miti ya bustani hiyo na maua yake na matunda yake kwenye majira ya machipuo yajayo, na anaumba nzi kwa mfumo wa kipanga mkubwa kwa wepesi na urahisi, na anajaalia mtu kuwa katika hali ya ulimwengu mkuu kwa wepesi na urahisi pia. Wakati ambapo jambo likiegemezwa kwenye sababu hakika kuumba kidudu kimoja inakuwa ni ngumu ugumu wa kuumba kifaru mkubwa, na kuumba tunda katika matunda ni kwa ugumu wa kuumba mti kamili wenye mishkeli. Bali inapasa kila Atomu katika Atomu zenye kufanya kazi ilizopewa katika majukumu ya ajabu katika vyumba vidogo vya mwili wa kiumbe hai kuwa na macho ya kuonea kila kitu na elimu ya kutambua kila kitu, ili iweze kutekeleza majukumu hayo ya kiuhai yaliyo madhubuti yaliyowekwa vyema. Kisha wepesi na urahisi yanafikia katika umoja kwa kiwango, kiasi inakuwa rahisi kupatikana maandalizi ya jeshi kamili kutoka katika mkono mmoja kutoka kiwanda kimoja, kama wepesi wa kuandaa askari mmoja kwa zana za kiaskari, na pindi itakapoingilia mikono mbalimbali mingine na kuchukuliwa kila kifaa katika vifaa hivyo anuwai kutoka katika viwanda mbalimbali, hakika kumwandaa askari mmoja – kwa upande wa kiasi - haiwezekani isipokuwa kwa mishkeli elfu moja na mmoja, kwani mambo huwa ni magumu ugumu ule wa kuandaa askari elfu ambapo wakuu wengi wanaingilia na makamanda wengi. Hakika kuongoza askari elfu moja na kuwa mkuu juu yao kukiegemezwa kwa kamanda mmoja, inakuwa rahisi urahisi wa kumwongoza askari mmoja, kwa upande mmoja, wakati ambapo uongozi ukiachwa kwa makamanda kumi au kwa askari wenyewe. Hapo kutatokea mchanganyiko mwingi na fujo na mishkeli. Na mambo yanakuwa hivyo hivyo kila kitu kinapoegemezwa kwa mmoja wa pekee hakika kinakuwa rahisi kama wepesi wa kitu kimoja. Wakati ambapo yakiegemezwa kwa sababu, hakika jambo la kiumbe hai mmoja linakuwa gumu na zito kama ardhi yote, bali linakuwa haliyumkiniki kabisa. Kwa maana katika Umoja kuna urahisi kwa kiwango cha kuwa wajibu na ulazima na katika wingi na mwingiliano wa mikono hufikia ugumu kwa kiwango cha kutoyumkinika. Basi kama ilivyoelezwa katika (Al-Maktubati) kutoka katika mkusanyiko wa Risale-i Nur ikiwa kuhitilafiana kwa usiku na mchana, harakati za nyota na kugeuka majira ya mwaka kama mapukutiko, baridi, machipuo na majira ya joto ikiwa yatakabidhiwa kwa mwendeshaji mmoja na mtoa amri mmoja, hakika mwamrishaji huyo mkuu anaiamrisha ardhi ambayo ni askari katika askari wake kuwa: simama, zunguka, tembea, nayo kwa nafasi yake inasimama ikiwa imevutika kwa uchangamfu wa amri na inachakatika kama Ashiki wa kimaulawy michakato miwili ya siku na mwaka, na kuwa ni nyenzo rahisi mno ya mabadiliko ya majira na michakato ya nyota ya dhahiri na kufikirika, ikidhihirisha urahisi kamili na wepesi wa ukomo katika umoja. Lakini kama jambo litaachwa – sio kwa yule mwamrishaji mmoja - bali kwa sababu na katika matashi ya nyota na matakwa yake, na ikaambiwa ardhi: Simama usitembee. Huenda katika hali ya ardhi ikatokea katika kupata majira na usiku na mchana kwa kukata maelfu ya nyota na majua ambayo ni makubwa kuliko ardhi kwa mara elfu nyingi ya masafa yanayofikia mamilioni ya miaka bali mabilioni ya miaka katika kila usiku na katika kila mwaka! Yaani jambo linakuwa gumu na ni mushkeli kwa kiwango cha muhali na lisiloyumkinika. Kilichomo kwenye ngazi ya tatu: Katika neno la (kudhihiri kwa upekee). Linaashiria hakika yenye ukomo wa upana, kina, umadhubuti na adhama. Tunaelekeza ufafanuzi wake na uthibitishaji wake kwa Risale-i Nur tukibainisha nukta moja katika nukta zake kwa kutoa mfano mfupi mno. Naam, kama lilivyo jua linatia nuru ardhi yote kwa mwanga wake. Na linakuwa ni Mfano wa umoja, kwa kuwepo kwa sura yake na mfano wake kwa rangi zake saba na sura yake ya dhati katika kila kinachokabiliana nalo katika vitu angavu kama kioo ndani yake linakuwa ni mfano wa upekee. Ingekuwa jua lina ujuzi, uweza na hiari na vikawa vipande vya kioo, matone ya maji na mapovu ambavyo majua madogo yanaakisi humo upokeaji. Lingekuwa linapatikana jua kamili kwa kanuni ya utashi wa kiungu katika kila mojawapo na pembeni mwa kila moja kati yake, vinapatikana kwa sifa yake na sura yake, bila ya kuzuia au kupunguza uwepo wake katika maeneo mengine katika utendaji wake hata kidogo. Inakuwa sababu ya mionekano mingi mno, kwa amri ya uweza wa kiungu na kuathiri kwake na hukumu yake. Basi inabainisha yaliyomo katika upekee miongoni mwa urahisi juu ya kawaida. Kadhalika mtengenezaji mtukufu hakika kwa kuzingatia umoja anaona vitu vyote naye ni mwangalizi wake kwa ujuzi wake, utashi wake na kwa uweza wake wenye kuzungukia kila kitu, kama kwamba yeye kwa upande wa upekee na kwa udhihiri wake yupo kando ya kila kitu na hasa vyenye uhai, kwa majina yake na sifa zake tukufu, kwa kiasi anaumba kwa urahisi uliotimia katika muda mmoja anaumba nzi katika mpangilio wa kipanga, na mwanadamu katika nidhamu ya ulimwengu mkubwa. Anaumba wenye uhai kwa miujiza mingi mingi kwa kiasi kwamba lau zingekusanyika sababu zote ili kumuumba kasuku mmoja au nzi mmoja zingeshindwa. Basi anayeumba kasuku ni muumba wa ndege na sio mwingine na ambaye anaumba mwanadamu ndiye muumba wa ulimwengu na sio mwingine. Ngazi ya Nne na tano: Nazo [Na kwa siri ya kupasa, kutakasika na kutofautiana kwa ainisho, na kwa siri ya kutokufungika, kutokuchukua mahali na kutogawika katika sehemu]. Hakika kunakili faida inayotokana na ngazi hizi mbili katika fahamu za watu wa kawaida ni kugumu sana. Kwa hiyo tunabainisha yaliyomo katika ngazi hizo kwa muhtasari pamoja na kutaja nukta chache fupi kutoka katika ngazi hizo. Yaani hakika Mweza wa hali zote anamiliki uwepo ambao ni wa nguvu na madhubuti mno wa ngazi za uwepo nayo ni ngazi ya kupasa ambao ni wa azali na wa milele na mwenye kutakasika na hali za kimaada na mwenye kuepukana nazo, na anabeba ainisho takatifu lenye kuwa mbali na ainisho zote, huyu mweza wa hali zote ni rahisi kwa uweza wake uendeshaji wa nyota kama kuendesha Atomu, na ufufuo mkuu ni rahisi kwake kama Majira ya machipuo, na kuhuisha watu wote katika ufufuo ni kwepesi kwake kama kuhuisha nafsi moja. Kwa sababu kiasi cha chanda katika aina ya nguvu katika tabaka za uwepo hushika mlima mkubwa kwa tabaka hafifu za tabaka za uwepo na kuuendesha. Basi mathalani kioo, na utunzaji kumbukumbu, na hivyo ni uwepo wa nje - nao ni uwepo wenye nguvu – yamkini viwili hivyo kuunganisha na kuendesha milima mia moja na vitabu elfu moja kutoka katika uwepo wa kimfano na wa kimaanawy ambao ni dhaifu na hafifu, na kama hivyo, ni kiasi duni kiasi gani kwa upande wa nguvu uwepo wa kimfano kulinganisha uwepo wa nje. Hakika aina za uwepo wenye kuzuka na kupita wa vya yamkini, vilevile ni duni mno kwa maelfu ya ngazi na hafifu mno kuliko uwepo wa wajibu wa milele wa azali, kwa kiasi kwamba hakika ya udhihirisho katika uwepo huo mtakatifu kwa kadiri ya Atomu unaendesha Ulimwengu wa vya yamkini. Nasikitika hakika sababu tatu zinafanana na maradhi yatokanayo na kupata sumu wakati huu. Haziruhusu kubainisha hakika hii kuu kwa nukta zake. Hivyo ninazielekeza kwenye Risale-i Nur na kwa wakati mwingine kwa kutaka kwa Allah (s.w). Ngazi ya sita: Nayo ni [Na kwa siri ya kupinduka kwa vikwazo na vizuizi kuwa sawa na nyenzo zenye kurahisisha]. Yaani kama ilivyo kwa kanuni katika midhihirisho ya utashi wa kiungu na amri ya kiuumbaji – ambayo elimu za kisasa wanizingatia kuwa ni fundo la kimaisha – inapeleka maada za lazima na riziki kwa kuelekea kwa utashi huo na amri kutoka katika hilo fundo la kimaisha ambalo ni kama msukumaji na mapigo yake kuelekea katika matunda ya mti mkubwa usio na utambuzi na kwenye majani yake na matunda yake. Na hayawi matawi yake yenye kutanzuka wala mashina yake yenye nguvu makakamavu hayawi vikwazo na vizuizi dhidi yake, bali yanakuwa ni nyenzo za kurahisisha na vikaao kati vya kurahisisha. Vivyo hivyo katika kuumba ulimwengu na kupatisha viumbe vyote vinaacha vikwazo vyote na vizuizi vigome na kujizuia mbele ya udhihirisho wa utashi wa kiungu na kwa kuelekea kwa amri ya kungu na kuwa ni nyenzo ya kurahisisha. Basi uweza wa milele unaumba ulimwengu na viumbe vya ulimwengu vyote kwa wepesi wa kuumba huo mti, haiwi ugumu kwake kitu chochote. Viumbe visingeegemezwa kwenye uweza huo hakika kuanzisha mti huo mmoja na kuuendesha inakuwa ni ngumu sawa na ugumu wa kuendesha miti yote, bali litakuwa ugumu sawa na kuumba ardhi na kuiendesha. Kwa sababu kila kitu wakati huo, kinakuwa ni kizuizi na kipingamizi. Na lau zingekusanyika sababu zote katika hali hii haziwezi kutuma riziki za lazima kutoka katika tumbo la fundo lake la kiuhai na mienendo yake ya amri na utashi, na kuifikisha kwa mpangilio hadi katika matunda yake, majani yake na matawi yake. Isipokuwa ikiegemezwa katika sehemu katika sehemu za mti bali hata katika kila Atomu katika Atomu zake jicho linaloona mti wote na kila sehemu yake na kila Atomu katika Atomu zake, na ujuzi wenye kuzungukia kila kitu na uweza uwezao kila kitu. Na kama hivyo panda ngazi hizi tano na uangalie ni kiasi gani katika ushirikina na ukafiri kuna mishkeli na muhali. Na ujue kiasi cha kuzuilika kwake na umbali wake na vipimo vya akili na mantiki, na kiasi cha urahisi katika njia ya Imani na Qur’an bali kiasi cha haki na hakika zilizomo zenye kukubalika kwa kiwango cha kupasa. Na kiasi cha kuingia kwake akilini na ukinaifu wake na urahisi wake kwa kiwango cha ulazima. Shuhudia hakika hii na useme: Alhamdulillah juu ya neema ya Imani. (Mikandamizo na kero zimesababisha kuahirisha sehemu iliyobakia katika ngazi hii kuu katika wakati mwingine apendapo Allah). Ngazi ya saba: [Na kwa siri ya kwamba Atomu, sehemu, kipande cha sehemu, kokwa na Mwanadamu sio ya uchache kwa ufundi na ukuu kuliko nyota, jumla, sehemu ya jumla, mti na ulimwengu]. Tanbihi: Hakika misingi ya hakika ya ngazi hizi tisa na hazina zake na jua lake ni katika Aya mbili za Surat Al-Ikhlasi: قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ ۞ اللَّهُ الصَّمَدُ Hiyo ni Ishara fupi ya ming’ao ya midhihirisho ya siri ya upekee na kutegemewa kwa haja zote. Tutatupa jicho katika yaliyomo kwenye ngazi hii ya saba kwa nukta moja au mbili tukielekeza maelezo yake kwenye Risale-i Nur. Na hiyo inamaanisha hakika ya Atomu ambayo inatekeleza majukumu ya ajabu kwenye jicho na ubongo sio ya uchache wa kiufundi na kupendezesha kuliko nyota, na sehemu sio ya uchache kwa ukuu kuliko jumla yake yote. Basi mathalani: Ubongo na jicho sio ya uchache kutengenezwa vema na kupendezeshwa kuliko mwanadamu. Wala kiungo cha sehemu ni cha uchache wa kupendezeshwa kuliko sampuli ya jumla, kwa upande wa uzuri wa kutengenezwa vema na ajabu katika kuumba. Wala mwanadamu sio wa uchache kiufundi kuliko jinsi ya wanyama kwa ujumla, kwa upande wa viungo vyake vya ajabu. Wala mbegu ambayo ni sawa na faharisi na programu na kumbukumbu sio ya uchache wa kutengenezwa vyema kuliko mti wake ulio stawi, kwa upande wa ukamilifu wa ufundi na kuhazini. Wala mwanadamu ambaye ni ulimwengu mdogo sio mchache kwa kutengenezwa kwa kupendeza kuliko ulimwengu mkubwa, kwa kiasi kwamba yupo katika umbo lililo bora kabisa na anamiliki viungo vyenye kufurutu ada vyenye kujumuisha vimeandaliwa kutimiza maelfu ya majukumu ya ajabu. Basi ambaye anaumba Atomu kwa hiyo hashindwi kuumba nyota, na ambaye anaumba Ulimi – nacho ni kiungo katika Mwanadamu – anaumba mwanadamu kwa urahisi na wepesi bila shaka. Na ambaye anamuumba mwanadamu katika umbo bora mno hapana shaka kwamba yeye ni mweza kuumba wanyama wote kwa wepesi kamili, mfano wa anavyowaumba mbele ya macho yetu. Na ambaye anaumba kokwa kwa ainisho la Faharisi na orodha ya misamiati, na daftari la kanuni za amri, na fundo la kiuhai, hapana shaka ndiye ambaye atakuwa Muumba wa miti yote. Na ambaye amemjaalia mwanadamu kuwa anafanana sana na mbegu ya kimaanawy ya ulimwengu na tunda lake lenye kukusanya na mahali pa kuonekana kwa majina yake yote ya kiungu na kioo chake na mwenye kufungamana na viumbe vyote na khalifa wa Ardhi, hapana shaka kwamba anamiliki uweza wenye kuweza kuumba ulimwengu wote na kuuratibu kwa urahisi wa kumuumba mwanadamu. Na kwa ajili hii basi mwenye kuwa ni muumba, mtengenezaji na Bwana Mlezi wa Atomu, sehemu, kinachohusiana na sehemu, kokwa na mwanadamu, basi kwa uwazi na hapana shaka kuwa yeye ndiye muumba wa nyota, sampuli, vyote, mikusanyiko ya jumla, miti, viumbe vyote na mtengenezaji wake, na mola wake mlezi hasa, basi ni muhali kuwa mwingine na ni jambo lisilowezekana kabisa. Ngazi ya Nane: [Kwa siri ya kwamba kilichozungukwa na vijisehemu ni kama mifano iliyoandikwa midogo au kama matone yaliyokamuliwa, basi hapana budi kuwa mzungukaji na mikusanyiko ya jumla katika mshiko wa muumba wa chenye kuzungukwa na vinavyohusiana na sehemu ndogo ili aingize mfano wake ndani yake kwa mizani ya ujuzi wake au kukamua kutokea humo kwa taratibu za hekima yake]. Yaani, hakika ya uwiano wa vijisehemu vyenye kuzungukwa, kila moja, kokwa, na mbegu ambazo zinabebwa na vyote, mjumuiko wa hadi kwenye mikusanyiko mikubwa na yenye kuzunguka, ni vyenye kurandana na vielelezo vilivyowekwa katika umbo dogo na mifano iliyoandikwa ndani yake kama yaliyoandikwa timamu katika yote na mikusanyiko uandishi madhubuti unaowiana na vipande hivyo vidogo. Na kwa ajili hii basi mikusanyiko ya jumla yenye kuzunguka iko katika mshiko wa Muumba wa hivyo visehemu na bila shaka chini ya usarifu wake na hiyo ili aingize kitabu cha mzunguko huo mkubwa kwa vipimo vya ujuzi wake na kwa kalamu zake madhubuti katika mamia ya vipande na madaftari madogo. Kisha uwiano wa sehemu na vijisehemu vilivyozungukwa kwa majumuisho yenye kuzunguka na mifano yake, vinashabihiana na matone yanayokamuliwa au kutoka kwenye mijumuiko yenye kuzunguka. Basi kwa mfano kokwa ya tikiti ni kama tone lililokamuliwa kutoka pande zote za aina ya tikiti au ni nukta iliyoandikwa ndani yake kitabu kamili cha tikiti hata kwamba hiyo kokwa inabeba faharisi yake, orodha yake ya yaliyomo na programu yake. Basi kwa kuwa jambo liko hivi, hivyo vijisehemu na matone na nukta na kila moja vinalazimu kuwa kwa mkono wa Mtengenezaji wa jumla hiyo yenye kuzunguka na mikusanyiko hiyo yenye kuzunguka, ili akamue kila moja, matone, na nukta kutokana nazo kwa taratibu za hekima yake nyeti. Kwa maana kwamba Muumba wa kokwa moja na kitu kimoja ndiye muumba wa jumla hiyo kubwa na mikusanyiko, na muumba wa mikusanyiko na jinsi ambazo zinazizidi ukubwa na kuzizungukia vilevile na sio mwingine. Na kwa ajili hii basi muumba wa nafsi moja anaumba watu wote, na ambaye anafufua maiti mmoja anafufua majini na wanadamu na wafu wote siku ya ufufuo, na atawafufua. Na kama hivi shuhudia kiasi cha ukweli wa madai مَّا خَلْقُكُمْ وَلَا بَعْثُكُمْ إِلَّا كَنَفْسٍ وَاحِدَةٍ na kiasi cha kuthibiti kwake na ukinaishi wake, shuhudia kwa sura yake angavu na dhahiri mno. 'Ngazi ya Tisa: [Na kwa siri kama ilivyo Qur’an ya utukufu iliyoandikwa kwenye Atomu inayoitwa kuwa ni Johari ya pekee kwa Atomu za Ether (Athiir) sio ya uchache kiukuu na ufurutu wa kiufundi kuliko Qur’an ya Adhama iliyoandikwa juu ya ukurasa wa Mbingu kwa wino wa nyota na majua, vivyo hivyo hakika ua la mti wa maua sio la uchache wa ukuu na ufundi kuliko nyota ya aina ya zuhura, wala nyenyere kuliko tembo, wala kirusi kuliko kiboko, wala nyuki kuliko mtende, kwa mujibu wa uweza wa muumba wa viumbe. Na kama ilivyo upeo wa ukamilifu wa kasi na urahisi katika kupatisha vitu kumewaingiza watu wa upotevu katika kuchanganya kuunda na kuundika kunakolazimu mihali isiyo na mipaka inayotolewa na dhana, vilevile imethibitisha kwa watu wa uongofu kuwa sawa kwa nyota pamoja na Atomu kwa mujibu wa uweza wa Muumba wa viumbe (s.w) na lailaha illa huwa Allah Akbar]. Nilikuwa nataka kubainisha maana ya ngazi hii ya mwisho kwa urefu lakini kwa masikitiko taabu na dhiki itokanayo na udhibiti wa kiusumbufu vimezuilia jambo hili. Na udhaifu ambao uliokuwa mwilini mwangu kutokana na kuingiwa na sumu ukiachilia mbali maradhi yenye kuumiza. Kwa hivyo nimelazimika kutosheka na ishara fupi kwenye maana yake. Nayo ina maana: Kama ingeandikwa Qur’an kubwa kwenye Atomu – ambayo inayoitwa katika Elimu ya Al-Kalaam na Falsafa kuwa ni Johari ya pekee ambayo haikubali kugawanyika - kwa Atomu za Ether ambazo ni ndogo kuliko hizo, na vilevile ingeandikwa Qur’an kubwa nyingine kwenye kurasa za mbingu kwa nyota na majua, kisha zikalinganishwa baina yake, hapana shaka kwamba Qur’an iliyoandikwa kwa johari ya pekee sio ya uchache kwa ukuu, muujiza na kupendezeshwa kuliko Qur’an adhimu kubwa ambayo imetia uzuri uso wa mbingu, na huenda hiyo ni yenye ukuu zaidi kuliko hiyo kwa upande mmoja. Vivyo hivyo ua sio la uchache wa ukuu na ufundi kuliko nyota ya aina ya Zuhura wala nyenyere sio duni mno kuliko tembo bali kidudu kidogo ni cha ajabu zaidi kuliko kifaru kwa umbo na nyuki kwa maumbile yake ya ajabu ni ajabu zaidi kuliko mtende kwa kulingana na uweza wa muumba wa viumbe. Kwa maana kwamba muumba wa nyuki anaumba wanyama wote, na ambaye anaifufua nafsi moja anawakusanya watu kwenye eneo la ufufuo na kuwafufua wote, na kuwakusanya kwa vyovyote. Hakiwi kigumu kwa uweza huo kitu chochote. Kama mamia ya vielelezo vya ufufuo vinavyoshuhudiwa mbele ya macho yetu kila majira ya machipuo. Maana ya kifungu cha Kiarabu cha mwisho na yaliyomo kwa muhtasari ni: Hakika watu wa upotevu kwa ujinga wao wa hakika zilizothibiti na imara za ngazi zilizotangulia, na kwa kudhihiri kwa vilivyomo kwenye uwepo katika ukomo wa wepesi na urahisi, imechanganyika kwao kuundwa kwake na kupatishwa kwake kwa uweza wa mtengenezaji mweza uweza wa hali zote, pamoja na kuundika kwake na kupatikana kwake kwa nafsi yake, wakijifungulia wenyewe milango ya upotofu na mihali isiyo na mipaka inayokataliwa na dhana na akili. Kwani katika hali hiyo – mathalan – inalazimu kuipa kila Atomu miongoni mwa Atomu za kiumbe hai uweza uwezao kutengeneza kila kitu na ujuzi na macho yanayoona kila kitu. Yaani kwa kutokubali kwao Mungu mmoja wa pekee wamelazimika kukubali Miungu mingi kwa idadi ya Atomu kwa mujibu wa mrengo wao wa kifikra. Wakistahiki kuingia chini ya chini ya jahanamu. Ama watu wa uongofu hakika zenye nguvu kwa ngazi zilizopita na hoja zilizopangika imara zimetunuku katika nyoyo zao salama na akili zao zenye kusibu ukinaifu wa kukata shauri na imani yenye nguvu na kusadiki kwa dhati ya yakini, hata wakaitakidi pasipo na shaka wala utata na kwa kila utulivu wa moyo kwamba hakuna tofauti kati ya nyota na Atomu na kitu kidogo mno na kikubwa zaidi mbele ya uweza wa kiungu, ambapo tunashuhudia mbele yetu viumbe hivi vya ajabu. Kila ufundi wa ajabu kati yake unasadiki madai ya aya tukufu مَّا خَلْقُكُمْ وَلَا بَعْثُكُمْ إِلَّا كَنَفْسٍ وَاحِدَةٍ na kushuhudia kwamba hukumu yake ndio dhati ya haki na hakika tupu. Na unasema kwa ulimi wa hali Allah Akbar. Nasi kwa nafasi yetu tunasema Allah akbar kwa idadi ya viumbe tukisadiki hukumu ya Aya hii tukufu kwa nguvu yetu yote na kukinai kwetu na tunashuhudia kwamba hukumu yake kuwa ndiyo haki na hakika yenyewe kwa hoja zisizo na ukomo. سُب۟حَانَكَ لَا عِل۟مَ لَنَٓا اِلَّا مَا عَلَّم۟تَنَٓا اِنَّكَ اَن۟تَ ال۟عَلٖيمُ ال۟حَكٖيمُ اَللّٰهُمَّ صَلِّ وَسَلِّم۟ عَلٰى مَن۟ اَر۟سَل۟تَهُ رَح۟مَةً لِل۟عَالَمٖينَ وَ ال۟حَم۟دُ لِلّٰهِ رَبِّ ال۟عَالَمٖينَ
Watumishi wa juu wa dini wanaoelezewa katika hadithi ya kuja mwanzoni mwa kila karne si wenye kuleta upya, wao ni wafuasi. Hiyo ni kusema, wao hawabuni chochote kipya wao wenyewe hawaleti sheria zozote mpya; wao wanaweka sawa na kuimarisha dini kwa njia ya kufuata kikamilifu maandiko, misingi na sheria ya dini na sunna za Nabii Muhammad (s.a.w); wanatangaza ukweli na maana asilia ya dini; Wanaondoa na kuzingatia kuwa ni batili mambo yasiyo ya msingi ambayo yamechanganywa nayo; wanakataa na kuteketeza mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya dini; wanaweka amri, wanatangaza na kutambulisha utukufu na adhama ya sheria tukufu. Ila tu bila ya kuvuruga hali ya msingi au kuharibu roho asilia, wanatekeleza majukumu yao kupitia njia mpya ya ushawishi unaoliangana na ufahamu wa wakati uliopo na kwa mtindo na maelezo mapya. Maafisa hao wa kiutawala wanathibitisha nafasi zao kutokana na matendo na kazi zao. Wanatimiza jukumu lao la kuakisi uimara wa Imani yao na ikhlasi yao. Wanadhihirisha katika matendo yao kiwango chao cha imani. Wanaonesha kwamba wanafuata kama yalivyoandikwa matendo ya Muhammad (s.a.w) na kwamba ni kweli wamevikwa taji la utume. Kwa ufupi: Kwa jamii ya Muhammad (s.a.w) wanaunda ruwaza kamilifu katika kuheshimu matendo na maadili na kufuata na kuendana na sunna ya mtume (s.a.w); wao ni mifano inayofaa kufuatwa. Kazi wanazoandika zinafafanua kitabu cha Allah na kuweka wazi maelekezo ya dini, wanawasilisha haya kwa mujibu wa ufahamu wa sasa na kiwango chake cha kujifunza, sio matunda ya akili yao ya juu yenye rutuba; wao si matokeo ya werevu na ujuzi wao. Ni moja kwa moja hayo ni wahyi na maelekezo ya msingi safi wa utume, ambaye ni chanzo cha wahyi. Jaljalutiyya, Mathnawi-i Sharif, na futuh al-Ghayb na kazi kama hizo zote ni za aina hii. Watu hao watukufu wana sehemu katika kupangilia zile kazi za hiari, na katika namna ya kuwa wazi; hiyo ni kuwa; wao ni mahali ambapo maana yake yanadhihirishwa na kuakisiwa. Kuja katika Risale-i Nur na mfasiri wake: Kwa kuwa katika kazi hii ya fahari iko katika mwangaza wa hali ya juu na ukamili usiyo na mwisho haijapata kuonekana kabla katika kazi yoyote kama hiyo; na kwa kuwa inashuhudiwa kwamba ni urithi wa mwangaza wa Qur’an ambayo ni taa takatifu na jua la mwongozo na mwezi wa furaha; ni hakika iliyo wazi kama jua inabeba mwangaza wa nuru ya Muhammad (s.a.w) kwa kiasi kikubwa kuliko kuwa ni kazi ya mawalii, kwamba kushiriki ndani yake, na kuhusika nayo, na katika idhini takatifu ya msingi safi wa utume (s.a.w) ni kubwa zaidi kuliko katika mawalii, na ufikiaji na ukamilifu wa ambaye ni mfasiri na mahali pa udhihirisho ni wa hali ya juu na isiyo na kifani kwa kiwango hichohicho. Ndiyo wakati akiwa bado ni mdogo na bado kamwe hajawa amesoma katika kitambo cha miezi mitatu ili kuweza kuokoka na wageni, mfasiri wa Risale-i Nur alifanywa kuwa mrithi wa elimu za zamani na sasa, elimu ya kiimani, hakika za mambo, siri za ulimwengu na hekima ya kiungu ambayo hakuna yeyote aliyetunukiwa kabla. Mafunzo na maadili yake ikiwemo na kuwa amepewa wasifu wa mbele na ujasiri usio wa kawaida na kujitegemea kikamilifu, alikuwa ni muujiza wa maumbile ni kuundika kwa fadhila za kiungu, uwezo wake ulikuwa ni tunuku za kiungu. Akiwa ni mwanazuoni asiyelinganishwa na yeyote, mjuzi wa ajabu akiwapa changamoto ulimwengu wote wa kujifunza kabla ya kufikia umri wa kubaleghe, aliwanyamazisha wanazuoni wote aliofanya nao mdahalo, alijibu kwa usahihi hasa na pasi na kubabaika karibu maswali yote aliyoulizwa, alibeba nafasi ya muhimili ya Ukuu kuanzia umri wa miaka kumi na nne, na kwa mfululizo aliangaza nuru ya elimu na mwanga wa hekima. Kwa umakini kwa kina cha ufafanuzi, ufahamu na ufasaha wa maelezo yake na uoni wake wa werevu na mwanga wa hekima, aliwashangaza wanazuoni na wasomi kwa ustahiki kabisa alipata cheo cha utambulisho kuwa (Bediuzzaman) (maajabu ya zama). Kama mtu ambaye kwa wasifu wake wa juu na thamani za kiusomi aliitangaza na kuithibitisha kikamilifu sana Dini ya Muhammad (s.a.w), alipata kwa hakika fadhila kubwa za mola wa mitume na alikuwa katika ulinzi wake imara na himaya yake. Bila ya shaka yeye alikuwa mmoja wa thamani tukufu ambaye alipanda hadi katika daraja la utume mtukufu, na alitenda chini ya amri yake na alikuwa ni mrithi wa kweli zake na kuakisi nuru yake. Kama ilivyoashiriwa katika kufanya kwake nuru na elimu ya Muhammad (s.a.w) na mwangaza wa mshumaa wa kiungu (Qur’an) kung’ara kwa uwazi mno, na umuhimu wa kimahesabu wa Qur’an na hadithi kukamilishwa kwake na udhihirisho wa kimahesabu wa aya zinazoelezea matamshi ya mtume (s.a.w) zinazopatikana kwake mwenyewe, hakuna shaka kwamba alikuwa ni kioo kilichoangazwa cha utume mtukufu katika kuhudumia maudhui ya imani na tunda la mwisho lenye kung’ara la mti wa utume, na kinywa cha mwisho cha hakika kuhusiana na ulimi wa haiba ya utume, na mbeba furaha wa mwisho wa mshumaa mtukufu kuhusiana na kuhudumia imani. Kwa niaba ya wanafunzi wa Risale-i Nur ambao wamehudhuria somo moja la madrasa ya tatu ya Yusuf, ikiwa imejumuisha ushahidi angavu na Zuhreti’n-nur, Ahmed feyzi, Ahmed Nazif, Salahaddin, Zubeyir, Ceylan, Sungur, Tabancali, wamenipa fungu kubwa kuliko ninavyostahiki. Lakini kukosa ujasiri wa kuwaudhi watia saini hawa nimebaki kimya na nimekubali wasifu wao kwa niaba ya haiba ya pamoja ya wanafunzi wa Risale-i Nur. Said Nursî Kwa jina lake mtukufu! Na hakuna chochote isipokuwa kinamtakasa kwa kumsifu. Assalam alaykum wa Rahamatullah wabarakatuh daima abadan! Bwana wetu mpendwa sana, mheshimiwa mwema! Mheshimiwa bwana wetu, ambaye ameachana na matakwa yake na kuacha mambo yote kwa matakwa ya utawala wa Allah, ambaye anaona huruma na hekima ya Kadari katika kila janga la dhahiri na shida na kwa kutegemea kikamilifu na kusalimu amri akingojea kwa subira matokeo ya dhihirisho ya kiutawala wa kiungu! Katika karne hii yenye balaa wakati katika mahali pengine katika mambo ambayo wanayoyategemea waumini yameanza kuporomoka, na bayana wakipinga nguzo za imani wakanushaji wa Allah wanajitanua wazi na kwa kiburi na kutenda kwa kupinga amri za Qur’an na kutoamini nguvu za kiroho, na kunasibisha haki ya kuumba kwa Asili isiyokuwa na utambuzi, pofu na bubu, vinazingatiwa kuwa alama za ustaarabu na kuwa na mila adhimu na kuwa na busara, katika wakati ambao mkuu wetu ameandika Risale-i Nur muujiza wa Qur’an ikitoa ponya yake kwa nyoyo zilizoharibikiwa zenye haja ya maji ya Uhai wa imani, amewapa habari njema ya furaha ya milele. Katika barabara yake kuu ya uhakika ambayo inathibitisha mafundisho yake kwa dalili na hoja za kukinaisha na zilizopangika, kupitia siri ya kiongozi wetu wa wazi (s.a.w), kwake inarejewa (sababu ni sawa na mfanyaji) sawasawa ya matendo yote yaliyotekelezwa na mamia ya maelfu ya wanafunzi wa Risale-i Nur ambao wameokoa imani yao kupitia Risale-i Nur imepita kwenye daftari la matendo yake! Kama ilivyokuwa katika jela ya Denizli Allah (s.w) amefadhili matunda ya imani, ambayo ponya zake zilikuwa zinatosha kwa hakika kabisa kumaliza kabisa majonzi ya kuzuiliwa, na manukato mazuri ya waridi yaliyo ondosha maumivu yote ya miba na kutokomeza maumivu yetu yote ya muda mfupi; kwa hiyo vilevile hapa katika jela ya Afyuni hali ya kudhikika kimwili kwa siku moja ambako ni sawa na dhiki ya mwezi mzima katika jela ya Denizli, mwingi wa Rehema mwenye ukarimu wa uzuri ametunuku kupitia mikono ya mkuu wenu hoja zenye nguvu zinathibitisha umoja wa kiungu na utume wa Muhammad (s.a.w), ambazo ni tiba na ponya. Sisi wanafunzi wako wakosaji mno, ambao kupitia mwanga wa Risale-i Nur tumejifunza kusoma na kuandika, tunazingatia risala zote hizi tatu kuwa ni shahidi za kukinaisha za ukweli wa Risale-i Nur, na ni namna ya muhtasari wake, katika hali hiyohiyo kwamba programu na faharisi ya mti maridadi wa msonobari umejumuishwa katika mbegu zake. Hatuna uwezo wa kuelezea thamani ya maandiko haya matatu lakini katika kuyasoma roho zetu zinahisi faraja kubwa, maumivu yetu ya kimwili yamegeuzwa kuwa ni furaha na yanatuletea matunda yasiyohesabika kutoka katika bustani ya imani. Na dalili zake kumi na moja za umoja wa kiungu, ya kwanza kati ya hizo inatokomeza giza la ukafiri, upotevu na hali ya sasa. Ya pili inachambua kwa dalili tukufu za imani surat Al-fatiha, chanzo, misingi na mfano mkuu kuliko yote katika Risale-i Nur. Na ya tatu inafafanua kwa ufasaha katika namna kwamba inayohakikisha uhakika kamili wa sehemu ya pili ya utume wa Muhammad (s.a.w) iliyoletwa kwako bwana wetu, hapa katika jela ya Afyuni. Japo kwa vyovyote hatuna ubora wa chochote, tutajitahidi kwa nguvu zetu zote kutangaza kazi hizi tulizozipokea. Tukitoa shukurani zetu zisizokuwa na mwisho kwa mola wetu mtukufu, Tunamwomba kwa kusema: “Mwingi wa rehema wa warehemevu! Tunakuomba umridhie mkuu wetu daima milele na milele!” Mwenye kubaki, ndiye mwenye kubaki! Kwa jina la wanafunzi wa Risale-i nur, Zubeyir, Ceylan, Sungur, Ibrahim
Kwa jina lake mtukufu! Hakuna chochote isipokuwa kinamtakasa kwa kumtukuza yeye Assalaam alaykum warahamatullah wabarakatuhu milele na milele! Ndugu zangu wapendwa wa dhati! [Kwa hadhiri ya mustakabali, Saidi wa zamani amefahamu kweli zilizoandikwa katika hotuba hii ya Kiarabu, ambayo, kwa msisitizo wa mamlaka za kidini za Damascus, aliitoa miaka Arobaini iliyopita katika msikiti wa Umayya kwenye mkusanyiko wa takriban watu elfu kumi, uliojumuisha mamia ya wanazuoni wa kidini; alitoa habari za kweli hizo kwa uhakika kabisa kana kwamba zitatokea punde tu. Hata hivyo, vita vikuu viwili vya dunia na miaka ishirini na tano ya kuondoshwa kwenye nafasi kabisa ilichelewesha kutokea kwake; ni wakati huu ambapo ishara zilizobashiriwa wakati huo, zinaanza kuonekana katika ulimwengu wa Uislamu. Kwa hiyo kama unazingatia kuwa inafaa, mnaweza kuchapisha tafsiri ya sehemu hii yenye maelekezo muhimu na yenye kuelimisha mno, sio kama hotuba ya zamani iliyopitwa na wakati, lakini kama mpya maelekezo muwafaka kwa masuala ya kijamii na Kiislamu yakiyaelekea moja kwa moja katika mwaka 1371 badala ya 1327, mkusanyiko wa watu mia tatu na sabini (sasa ni zaidi ya milioni) katika msikiti wa ulimwengu wa Kiislamu ukiachilia msikiti wa Umayya.] Inafaa kuandika hapa jibu muhimu kabisa kwa swali muhimu kabisa. Kwa Saidi wa zamani aliandika kwa kutabiria katika somo hilo miaka arobaini iliyopita kana kwamba anayaona mafundisho ya kushangaza ya Risale-i Nur na athari zake. Ni kwa sababu hii ninaandika swali hilo na jibu hapa. Ni kama hivi: Wengi wameniuliza mimi na wanafunzi wa Risale-i nur: “Ni kwa nini kwamba iko hivi Risale-i Nur haishindwi mbele ya upinzani mkubwa na wanafalsafa wakaidi na makafiri? Kwa kuzuia kuendelea kubomoka kwa mambo mengi ya thamani, vitabu sahihi kuhusu imani na Uislamu kwa kupitia matashi yao mbalimbali ya kidunia na dhambi zao, wamewazuia vijana wengi na wengine katika hakika za imani. Lakini mashambulizi yao makali zaidi, miamala mibaya, uongo na propaganda vimeelekezwa katika Risale-i Nur, kuiharibu na kuwaogofya watu wajiweke mbali nayo na kuwafanya watu kuachana nayo kabisa. Licha ya hivi, Risale-i Nur imeenea haijapatapo kuonekana katika kazi nyengine yeyote, nakala mia sita elfu za risala zake zimeandikwa kwa mkono kwa juhudi kubwa na kuchapishwa kwa siri. Ni vipi kwamba inasababisha kusomwa kwa hamasa kiasi hiki, kote ndani na nje ya nchi? Nini sababu ya hili? Kujibu maswali mengi sana ya aina hii, tunasema: Kuwa mfasiri wa kweli wa Qur’an tukufu kupitia siri ya muujiza wake Risale-i Nur inaashiria kwamba katika upotevu kuna aina ya jahanamu hapa duniani wakati katika imani kuna aina ya pepo. Inaashiria maumivu makali yaliopo katika dhambi, matendo mabaya na starehe zilizokatazwa na kuthibitisha kwamba katika matendo mazuri na maadili na ukweli wa sharia kuna furaha kama furaha ya pepo. Kwa namna hii inawaokoa wenye akili katika wale ambao wamedondokea katika maasi na upotevu. Kwa sasa kuna hali mbili za kutisha: Ya kwanza: Kwa kuwa mihemko ya mwanadamu, ambayo haioni matokeo ya vitu na kufadhilisha aunsi ya furaha ya sasa kuliko tani za furaha ya mustakabali, imekuja kutawalia akili na hoja, njia pekee ya kuwaokoa waliopotoka kutoka katika maasi yao ni kuwaonyesha maumivu ya sasa katika furaha zao na kuishinda mihemko yao. Japo kuwa wanajua mavuno ya mithili ya almasi na furaha za kama aya isemavyo: الَّذِينَ يَسْتَحِبُّونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا inaashiria, wakati wa kuwa waumini, watu wa upotevu wanachagua starehe za dunia ambazo ni kama vipande vya chupa punde vitavunjika. Njia pekee ya kuwaokoa kutoka katika mapenzi haya ya ulimwengu na kutokana na hatari ya kuangukia humo ni kwa kuwaonesha mateso ya kijahanamu na maumivu wanayoteseka nayo japo katika ulimwengu huu. Hii ndiyo njia ambayo Risale-i Nur inaichukua kwa kuwa wakati huu kutokana na uharibifu unaotokana na ukafiri wa kupindukia na ulevi unaofanywa na maasi na upotevu unaotokana na sayansi, huenda ni mmoja tu kati ya kumi anaweza kushawishiwa kuachana na tabia zake mbaya kwa kuthibitisha uwepo wa jahanamu na mateso yake baada ya kumwambia kuhusu Allah mtukufu. Kwa kusikia hili watu kama hao wanaweza kusema: “Allah (s.w) ni mwingi wa kusamehe na kurehemu na jahanamu ni safari ndefu hadi kuifikia” na kuendelea na makosa yao. Nyoyo na roho zao zimeelemewa na mihemko yao. Na kama hivi, kwa kuonesha kupitia mingi katika mifano yake matokeo mabaya na ya kutisha katika ulimwengu huu wa ukafiri na upotevu, Risale-i Nur huwafanya hata wale watu jeuri na wenye kiburi kuchukia starehe hizo za haramu, huwapelekea kutubu. Mifano mifupi katika neno la sita, saba na nane na ndefu katika kituo cha tatu katika neno la thelathini na mbili inamfanya mwanadamu kuhisi kujuta juu ya uovu juu ya upotevu wa njia aliyoichukua na kumsababishia kukubali mafunzo yanayotolewa nayo. Kwa mfano nitaeleza kwa ufupi hali niliyokuwa katika safari ya kimawazo ambayo kwa hakika ilikuwa ni kweli. Kwa wale wanaohitaji maelezo zaidi wanaweza kutazama mwishoni mwa (Muhuri wa kusadikisha ghaibu). Nikiwa katika safari hiyo ya kimawazo nilitazama sampuli ya wanyama kupitia macho ya falsafa ya Wanamaada na watu wa upotevu na mghafala, mahitaji yasiyo na idadi ya wanyama na njaa yao kali pamoja na udhaifu wao na kutojiweza kwao, ilidhihiri kwangu kama ni jambo la kuhurumiwa na kusikitikiwa sana. Nililia kisha nikaangalia kupitia kikuza umbo cha busara ya Qur’an na imani kwamba jina tukufu la mwingi wa rehema limeinuka katika ishara ya mtoaji kama jua lenye kung’ara: likimulika kwa huruma zake ule ulimwengu wa wanyama wenye njaa ulioteketea. Halafu nikaona ndani ya ulimwengu wa wanyama ulimwengu mwingine wa kuhuzunisha ambao ulikuwa umemezwa kwenye giza na kumfanya kila mtu kuwa na majonzi ambamo wadogo walikuwa wakihangaika katika mahitaji yao na kukosa nguvu kwao. Nilihuzunika niliangalia kupitia macho ya watu wenye upotevu. Tahamaki imani ikanipa miwani nyingine na nikaliona jina la mwenye kurehemu likiinuka katika ishara ya mneemeshaji; iligeuza na kuangazia ule ulimwengu wenye kusikitikiwa na kuwa katika hali ya furaha na uzuri; ikibadili machozi yangu ya malalamiko na huzuni kuwa machozi ya furaha na shukurani. Kisha ulimwengu wa wanadamu ukaonekana kwangu kana kwamba katika kioo cha sinema niliangalia kupitia darubini ya watu wa upotevu na kuuona ulimwengu huo kuwa wenye giza sana na kutisha hadi nikalia kutokea kwenye kina cha moyo wangu “Eeh!” nikalia kwa sababu wao wana matamanio na matumaini ambayo yanakunjuka hadi milele, fikira na mawazo yanayouenea ulimwengu, matamanio ya kumiliki furaha ya milele na pepo, na uwezo wa kimaumbile na nguvu ambazo hazikuwekewa kikomo na ambazo zilikuwa ni huru, bado licha ya mahitaji yao yasiyo na idadi na udhaifu wao na kutojiweza kwao wana hatari ya kushambuliwa na maadui wasio na idadi na dhoruba za majanga yasiyo na idadi. Chini ya kitisho cha kudumu cha umauti wameishi katika maisha yao mafupi na yenye dhiki katika mazingira ya kuharibika. Wakiangalia kwenye kaburi ambalo kwa wapotevu ni mlango wa kuelekea kwenye giza la milele, waliteseka na mapigo ya mfululizo ya kifo na utengano, hali ya kuumiza kabisa kwa moyo na ufahamu. Niliona hivyo kwa mmoja-mmoja na kwa makundi yakiwa yanatupiwa kwenye kisima hicho cheusi. Katika kuangalia ulimwengu wa mwanadamu katika giza hili nilikaribia kulia kwa moyo, roho na akili, na vipawa vyote nyororo vya ndani, kwa kweli sehemu zote za uwepo wangu, ilipotangulia nuru na nguvu kutoka katika Qur’an na kuvunja miwani hizo za upotevu na kunipa maono. Nikaliona jina tukufu la mwadilifu likichomoza kama jua katika ishara ya mwingi wa hekima, jina la mwingi wa rehema likichomoza katika ishara ya mwenye kurehemu, jina la mkarimu lilichomoza katika ishara, ni kusema, kwa maana ya mwingi wa msamaha, jina la mwenye kufufua limechomoza katika ishara ya mrithi wa kila kitu, jina la Al-Muhyi (Mtia uhai) likichomoza kwa ishara ya mneemeshaji, na jina la Ar-Razzaq (Mtoa riziki) likichomoza katika ishara ya mmiliki. Yameangaza ulimwengu mzima wa binadamu na ulimwengu wote ndani yake. Yametokomeza hali zote za jahanamu, yamefungua limwengu zenye kung’ara za akhera, na kutawanya nuru kwenye ulimwengu wa binadamu. Nikasema: “Alhamdulillah kwa namba za chembe zote katika uwepo!” Nilifahamu kwa uhakika kamili kuwa katika imani kuna aina ya pepo katika ulimwengu huu, pia katika upotevu kuna aina ya jahanamu. Kisha ulimwengu wa ardhi ulidhihiri, katika safari hiyo ya kimawazo kanuni za kinadharia zenye giza za falsafa zisizotii dini zimeonesha ulimwengu wa kutisha. Anga lenye kusafiri katika jahazi la ardhi yenye miaka mingi - ambayo inasafiri mara sabini zaidi kuliko risasi ya bomu masafa miaka ishirini na tano ndani ya mwaka mmoja, muda wote ikiwa katika hatari ya kuvunjika, ndani yake kuna hali ya vurugiko - hali ya mwanadamu mwenye hali mbaya ilidhihiri kwangu katika giza lenye kutenganisha. Macho yangu yaliingia giza. Nilitupa chini miwani ya falsafa nikizivunja. Na halafu nikaangalia kwa matazamo ulionawirishwa kwa hekima ya Qur’an na imani na nimeona majina ya Muumba wa mbingu na Ardhi, Mweza, Mjuzu wa kila kitu, Mtoa riziki, Allah Mruzuku wa mbingu na Ardhi, Mteza nguvu wa jua na mwezi, yamechomoza kama majua katika ishara ya rehema, mpaji na utawala. Vimeangaza giza lile la ulimwengu wa kutengwa na kutisha na kwa hiyo tufe la ulimwengu lilidhihiri katika macho yangu ya imani likiwa ni jahazi lililopangika vema, kutezwa nguvu, lenye kupendeza, na salama, au ndege au gari moshi. Ilikusanya riziki ya kila mmoja, na imerembeshwa kwa ajili ya biashara na furaha na kuchukua viumbe wenye roho ndani ya ulimwengu wa kiutawala kuzunguka jua. Niliguta: “Alhamdulillah kwa idadi ya chembe za neema ya imani.” Hili limethibitishwa kwa mifano mingi katika Risale-i Nur kwamba wale ambao wanafuata uasi na upotovu wanateseka na maumivu ya kijahanamu katika ulimwengu huu pia, wakati kupitia midhihirisho ya kiimani, waumini na watu wema wanaweza kuonja raha za peponi kupitia matumbo ya imani na ubinadamu. Wanaweza kunufaika kulingana na kiwango cha imani yao. Lakini katika nyakati hizi za dhoruba, mawimbi yanayotia ganzi hisia na kutawanya mkazo wa binadamu katika masuala ya ziada, yakimtosa humo, yameua fahamu zake na kumchanganya. Kama matokeo ya hili watu wa upotevu kwa muda mfupi wanashindwa kuhisi mateso yake, wakati watu wa uongofu wamekumbwa na kughafilika hawawezi kiukweli kufaidi furaha zake. Hali ya pili ya kutisha ya enzi hizi: Katika nyakati zilizopita kulinganisha na sasa kulikuwa na kiasi kidogo sana cha kutoamini kabisa, au upotevu unaotokana na sayansi, au kutoamini kunakotokana na kiburi cha kupindukia. Mafunzo ya wanazuoni wa Kiislamu wa nyakati hizo na hoja zao kwa hiyo zilikuwa zinatosha kwa haraka kutokomeza ukafiri wowote unaotokana na shaka. Kuamini Allah kulikuwa kwa jumla na waliweza kuwashawishi watu zaidi kuachana na upotevu wao na matendo mabaya kupitia kuwafundisha kuhusu Allah (s.w) na kuwakumbusha na moto wa jahanamu. Lakini kwa sasa kuna makafiri mia moja katika mji mdogo mmoja badala ya pengine mmoja katika nchi nzima. Wale ambao wanapotea njia yao kwa sababu ya sayansi na elimu na kwa ukaidi wanapinga kweli za imani wameongezeka mara kumi zaidi kulinganisha na zamani. Kwa majigambo kama yale ya firauni na upotevu wao mbaya kabisa hawa Wazandiki wanapinga kweli za imani. Ukweli mtakatifu kwa hiyo unahitajika sana ambao utaharibu kabisa misingi yao ya ukafiri katika dunia hii kama bomu la atomu, na kukomesha mashambulizi yao na baadhi yao kuwaleta katika imani. Alhamdulillah kwa kuwa kwa mifano yake mingi kama tiba kamili ya majeraha ya wakati huu, Risale-i Nur muujiza wa Qur’an yenye ufasaha wa kimuujiza ikiendelea katika Mwanga wake imeng’oa hadi wazandiki wakaidi kabisa kwa upanga wa almasi wa Qur’an. Dalili na hoja zake kwa idadi ya atomu za ulimwengu zikiashiria umoja wa kiungu na kweli za imani zinaonyesha kwamba katika miaka ishirini na tano haikushindwa usoni mwa mashambulizi makali bali imeweza kuenea na yenyewe na kuibuka mshindi. Naam, kwa mifano yake ya imani na ukafiri na uongofu na upotevu, Risale-i Nur imethibitisha hoja hizo kwa kujieleza wenyewe. Mazingatio yakichukuliwa kwa mfano wa hoja na ming’ao ya kituo cha pili cha neno la ishirini na mbili, makamo ya awali ya kisimamo cha kwanza cha neno la thelathini na mbili, ‘Madirisha’ ya andiko la thelathini na tatu, na dalili kumi na moja za (Fimbo ya Musa), itaeleweka kwamba ni kweli za Qur’an zilizodhihirishwa kwenye Risale-i Nur ambazo zitavunja na kuharibu ukafiri na kukabiliana na upotevu wakati huu. Kwa namna hiyohiyo kwamba sehemu za Risale-i Nur ambazo zinafumbua siri kubwa ya dini na fumbo la kuumbwa kwa ulimwengu zimekusanywa pamoja katika mkusanyiko wa ‘Mafumbo’ (Tılsımlar Mecmuası), sehemu zinazoelezea jahanamu katika ulimwengu huu wa watu wa upotevu na furaha za mfano wa pepo kwa watu wa uongofu na kuonesha kwamba imani ni kama mbegu ya pepo wakati ukafiri ni mbegu ya mti wa zakkum wa jahanamu, zitawekwa pamoja katika mkusanyiko mdogo inshaAllah na kuchapishwa. Said Nursî بِاس۟مِهٖ سُب۟حَانَهُ وَ اِن۟ مِن۟ شَى۟ءٍ اِلَّا يُسَبِّحُ بِحَم۟دِهٖ Aziz, sıddık, sarsılmaz, sebatkâr, fedakâr, vefadar kardeşlerim! Bilirsiniz ki Ankara ehl-i vukufu Risale-i Nur’a ait kerametleri ve işaret-i gaybiyeleri inkâr edememişler. Yalnız yanlış olarak o kerametlerde beni hissedar zannedip, itiraz ederek “Böyle şeyler kitapta yazılmamalı idi, keramet izhar edilmez.” diye hafif bir tenkide mukabil müdafaatımda onlara cevaben demiştim ki: Onlar bana ait değil ve o kerametlere sahip olmak benim haddim değil. Belki Kur’an’ın mu’cize-i maneviyesinin tereşşuhatı ve lem’alarıdır ki hakiki bir tefsiri olan Risale-i Nur’da kerametler şeklini alarak, şakirdlerinin kuvve-i maneviyelerini takviye etmek için ikramat-ı İlahiye nevindendir. İkram ise izharı bir şükürdür, caizdir hem makbuldür. Şimdi ehemmiyetli bir sebebe binaen cevabı bir parça izah edeceğim. Ve ne için izhar ediyorum ve ne için bu noktada bu kadar tahşidat yapıyorum ve ne için birkaç aydır bu mevzuda çok ileri gidiyorum, ekser mektuplar o keramete bakıyor, diye sual edildi. Elcevap: Risale-i Nur’un hizmet-i imaniyesinde bu zamanda binler tahribatçılara mukabil yüz binler tamiratçı lâzım gelirken hem benimle lâekall yüzer kâtip ve yardımcı bulunmak ihtiyaç varken değil çekinmek ve temas etmemek, belki millet ve ehl-i idare takdir ile ve teşvik ile yardım ve temas etmek zarurî iken ve o hizmet-i imaniye hayat-ı bâkiyeye baktığı için hayat-ı fâniyenin meşgalelerine ve faydalarına tercih etmek ehl-i imana vâcib iken, kendimi misal alarak derim ki: Beni her şeyden ve temastan ve yardımcılardan men’etmek ile beraber aleyhimizde olanlar bütün kuvvetleriyle arkadaşlarımın kuvve-i maneviyelerini kırmak ve benden ve Risale-i Nur’dan soğutmak ve benim gibi ihtiyar, hasta, zayıf, garib, kimsesiz bîçareye binler adamın göreceği vazifeyi başına yüklemek ve bu tecrit ve tazyiklerde maddî bir hastalık nevinde insanlar ile temas ve ihtilattan çekilmeye mecbur olmak hem o derece tesirli bir tarzda halkları ürküttürmek ile kuvve-i maneviyeyi kırmak cihetleriyle ve sebepleriyle, ihtiyarım haricinde bütün o manilere karşı Risale-i Nur şakirdlerinin kuvve-i maneviyelerinin takviyesine medar ikramat-ı İlahiyeyi beyan ederek Risale-i Nur etrafında manevî bir tahşidat yaptırmak ve Risale-i Nur kendi kendine, tek başıyla –başkalarına muhtaç olmayarak– bir ordu kadar kuvvetli olduğunu göstermek hikmetiyle bu çeşit şeyler bana yazdırılmış. Yoksa hâşâ kendimizi satmak ve beğendirmek ve temeddüh etmek ve hodfüruşluk etmek ise Risale-i Nur’un ehemmiyetli bir esası olan ihlas sırrını bozmaktır. İnşâallah Risale-i Nur kendi kendine hem kendini müdafaa ettiği hem kıymetini tam gösterdiği gibi bizi de manen müdafaa edip kusurlarımızı affettirmeye vesile olacaktır. Umum kardeşlerimin ve hemşirelerimin, hâssaten duaları makbul ve mübarek masumlar taifesi ve muhterem ihtiyarlar cemaatinden her birerlerine binler selâm ve dua ederek ramazan-ı şeriflerini tebrik ederiz, dualarını rica ederiz. Hasta kardeşiniz Said Nursî بِاس۟مِهٖ سُب۟حَانَهُ Bu âciz kardeşiniz hem itiraz eden o eski dost zata hem ehl-i dikkate ve sizlere beyan ediyorum ki Kur’an-ı Mu’cizü’l-Beyan’ın feyziyle Yeni Said hakaik-i imaniyeye dair o derece mantıkça ve hakikatçe bürhanlar zikrediyor ki değil Müslüman uleması, belki en muannid Avrupa feylesoflarını da teslime mecbur ediyor ve etmektedir. Amma Risale-i Nur’un kıymet ve ehemmiyetine işarî ve remzî bir tarzda Hazret-i Ali (ra) ve Gavs-ı A’zam’ın (ra) ihbaratı nevinden, Kur’an-ı Mu’cizü’l-Beyan dahi bu zamanda bir mu’cize-i maneviyesi olan Risale-i Nur’a nazar-ı dikkati celbetmesine mana-yı işarî tabakasından rumuz ve îmaları, i’cazının şe’nindendir. Ve o lisan-ı gaybın belâgat-ı mu’cizekâranesinin muktezasıdır. Evet, Eskişehir Hapishanesinde dehşetli bir zamanda ve kudsî bir teselliye çok muhtaç olduğumuz hengâmda, manevî bir ihtarla: “Risale-i Nur’un makbuliyetine eski evliyalardan şahit getiriyorsun. Halbuki وَلَا رَط۟بٍ وَلَا يَابِسٍ اِلَّا فٖى كِتَابٍ مُبٖينٍ sırrıyla en ziyade bu meselede söz sahibi Kur’an’dır. Acaba Risale-i Nur’u Kur’an kabul eder mi? Ona ne nazarla bakıyor?” denildi. O acib sual karşısında bulundum. Ben de Kur’an’dan istimdad eyledim. Birden otuz üç âyetin mana-yı sarîhinin teferruatı nevindeki tabakattan mana-yı işarî tabakasından ve o mana-yı işarî külliyetinde dâhil bir ferdi Risale-i Nur olduğunu ve duhûlüne ve medar-ı imtiyazına birer kuvvetli karine bulunmasını bir saat zarfında hissettim. Ve bir kısmı bir derece izahlı ve bir kısmını mücmelen gördüm. Kanaatime hiçbir şek ve şüphe ve vehim ve vesvese kalmadı. Ve ben de ehl-i imanın imanını Risale-i Nur ile takviye etmek niyetiyle o kat’î kanaatimi yazdım ve has kardeşlerime mahrem tutulmak şartıyla verdim. Ve o risalede biz demiyoruz ki âyâtın mana-yı sarîhi budur. Tâ hocalar فٖيهِ نَظَرٌ desin. Hem dememişiz ki mana-yı işarînin külliyeti budur. Belki diyoruz ki mana-yı sarîhinin tahtında müteaddid tabakalar var. Bir tabakası da mana-yı işarî ve remzîdir. Ve o mana-yı işarî de bir küllîdir, her asırda cüz’iyatları var. Ve Risale-i Nur dahi bu asırda o mana-yı işarî tabakasının külliyetinde bir ferttir ve o ferdin kasden bir medar-ı nazar olduğuna ve ehemmiyetli bir vazife göreceğine, eskiden beri ulema beyninde bir düstur-u cifrî ve riyazî ile karineler, belki hüccetler gösterilmiş iken Kur’an’ın âyetine veya sarahatine değil incitmek, belki i’caz ve belâgatına hizmet ediyor. Bu nevi işarat-ı gaybiyeye itiraz edilmez. Ehl-i hakikatin nihayetsiz işarat-ı Kur’aniyeden hadd ü hesaba gelmeyen istihraçlarını inkâr edemeyen, bunu da inkâr etmemeli ve edemez. Amma benim gibi ehemmiyetsiz bir adamın elinde böyle ehemmiyetli bir eserin zuhur etmesini istiğrab ve istib’ad edip böyle itiraz eden zat, eğer buğday tanesi kadar çam çekirdeğinden dağ gibi çam ağacını halkeylemek azamet ve kudret-i İlahiyeye delil olduğunu düşünse elbette bizim gibi âciz-i mutlak ve fakir-i mutlakta böyle ihtiyac-ı şedit zamanında böyle bir eser zuhuru, vüs’at-i rahmet-i İlahiyeye delildir demeye mecbur olur. Ben sizi ve muterizleri Risale-i Nur’un şeref ve haysiyetiyle temin ediyorum ki: Bu işaretler ve evliyanın îmalı haberleri, remizleri, beni daima şükre ve hamde ve kusurlarımdan istiğfara sevk etmiş. Hiçbir vakitte ve hiçbir dakika nefs-i emmareme medar-ı fahir ve gurur olacak bir enaniyet ve benlik vermediğini, size bu yirmi sene hayatımın gözünüz önünde tereşşuhatıyla ispat ediyorum. Evet, bu hakikatle beraber insan kusurdan, nisyandan hâlî değil. Benim bilmediğim çok kusurlarım var. Belki de fikrim karışmış, risalelerde bazı hatalar olmuş. Fakat Kur’an’ın hurufat-ı kudsiyesinin yerine beşerin tercümesini ikame perdesi altında, noksan huruflarla yeni hat altında tahrifkârane ehl-i dalaletin tevilat-ı fâsideleri âyâtın sarahatini incitmelerine bakmıyor gibi bîçare mazlum bir adamın kardeşlerinin imanını kuvvetlendirmek için bir nükte-i i’caziyeyi beyan ettiği için hizmet-i imaniyesine fütur verecek derecede itiraz, elbette değil ehl-i hakikat zatlar belki zerre miktar insafı bulunan itiraz edemez. Bunu da ilâveten beyan ediyorum. Bu zamanda gayet kuvvetli ve hakikatli milyonlarla fedakârları bulunan meşrepler, meslekler, tarîkatlar, bu dehşetli dalalet hücumuna karşı zâhiren mağlubiyete düştükleri halde benim gibi yarım ümmi ve kimsesiz ve mütemadiyen tarassud altında, karakol karşısında ve müthiş, müteaddid cihetlerle aleyhimde propagandalar ve herkesi benden tenfir etmek vaziyetinde bulunan bir adam, o mesleklerden daha ileri, daha kuvvetli dayanan Risale-i Nur’a sahip değildir ve o eser onun hüneri olamaz, onunla iftihar edemez. Belki doğrudan doğruya Kur’an-ı Hakîm’in bu zamanda bir nevi mu’cize-i maneviyesi olarak rahmet-i İlahiye tarafından ihsan edilmiştir. O adam, binler arkadaşıyla beraber o hediye-i Kur’aniyeye el atmışlar. Her nasılsa birinci tercümanlık vazifesi ona düşmüş. Onun fikri ve ilmi ve zekâsının eseri olmadığına delil, Risale-i Nur’da öyle parçalar var ki bazı altı saatte, bazı iki saatte, bazı bir saatte, bazı on dakikada yazılan risaleler var. Ben yemin ile temin ediyorum ki Eski Said’in (ra) (Hâşiyecik ) kuvve-i hâfızası da beraber olmak şartıyla o on dakika işi on saatte fikrim ile yapamıyorum. O bir saatlik risaleyi, iki gün istidadımla, zihnimle yapamıyorum ve o bir günde altı saatlik risale olan Otuzuncu Söz’ü ne ben ve ne de en müdakkik dindar feylesoflar altı günde o tahkikatı yapamazlar ve hâkeza… Demek biz müflis olduğumuz halde, gayet zengin bir mücevherat dükkânının dellâlı ve bir hizmetçisi olmuşuz. Cenab-ı Hak fazl u keremiyle şu hizmette hâlisane, muhlisane bizi ve umum Risale-i Nur talebelerini daim ve muvaffak eylesin, âmin bihürmeti Seyyidi’l-mürselîn. Said Nursî

