Tunda kati ya matunda ya gereza la Denizli Risala hii: Ulinzi wa imani unaofanywa na Risale-i Nur ili kuwazuia wazandiki na ukafiri kabisa, hatuna utetezi wa kihakika kuhusu kadhia yetu – katika jela yetu hii - isipokuwa utetezi huu, na sisi hatufanyi jitihada isipokuwa kwa ajili ya imani. Na hili ni wazo la tunda lilizaliwa na jela ya (Denizli) katika siku mbili miongoni mwa siku za Ijumaa Mubarak. Said Nursî
Source text is preserved. When a suitable model is available, translation is displayed separately.
Şualar
The Eleventh Ray
بِس۟مِ اللّٰهِ الرَّح۟مٰنِ الرَّحٖيمِ فَلَبِثَ فِى السِّج۟نِ بِض۟عَ سِنٖينَ Tunafahamu kutokana na siri za aya hii tukufu kwamba Yusuf (a.s) ni kigezo cha wafungwa na kiongozo wao. Kwa hiyo jela inakuwa ni aina katika aina za (Madrasa ya Yusuf). Na kwa kuwa idadi kubwa ya wanafunzi wa nuru wameingia mara mbili katika madrasa hii, kwa hiyo wanapaswa kusoma baina yao na kusomesha sehemu ya katika muhtasari wa masuala ya kiimani ambayo Risale-i Nur imeyathibitisha na yana uhusiano na jela ili kupata mwongozo kwayo, kwa ajili ya kuzinyoosha tabia na maadili mema katika Madrasa hii iliyofunguliwa kwa ajili ya kupokea malezi. Ndiyo hapa sisi tunabainisha sehemu kati ya mihutasari hiyo.
Suala hili linaweza kufupishwa ambalo ufafanuzi wake umefanyika katika (Neno la nne) kama ifuatavyo: Hakika rasilimali za uhai wetu ni hizi saa Ishirini na nne ambazo siku inazileta kwetu zikiwa ni neema safi miongoni mwa neema za Muumba wetu mkarimu (s.w), ili kwa kila saa tupate kuchuma tunachohitajia na kilicho lazima katika uhai wetu wote wa sehemu mbili wa kidunia na kiakhera. Na ikiwa hatujatumia saa moja – nayo inatosha kutekeleza swala zilizofaradhishwa – kwa uhai wetu wa kiakhera wa kudumu milele wakati ambapo tunatumia saa ishirini na tatu kwa ajili ya maisha haya mafupi ya dunia, tunakuwa tumefanya kosa kubwa akili iliyo sawa hailioni sahihi kamwe. Basi hapana shaka kuwa sisi tunasumbuliwa na ugumu wa moyo kutokana na kosa hili baya sana na kufungika na giza la roho kwa ujumla wake hupelekea katika kutibua usafi wa tabia na kuchafua umaridadi wa roho. Na juu ya haya uhai wetu unapita ukiwa ni mpangilio wa kuchosha wenye kukatisha tamaa na usio na maana. Hapo kero hutusibu, hatufaidi kutokana na Madrasa hii ya Yusuf na kutokana na shida ya mtihani na majaribio yanayotulea na kutupandisha, kwa hili tunapata hasara dhahiri. Ama ikiwa tutatumia saa moja katika kutekeleza swala tano, basi kila saa katika saa za balaa na nyakati za mateso inageuka kuwa ni siku kamili ya ibada kana kwamba saa zenye kutoweka zimevuna – kwa baraka ya saa hii – sifa za kuishi milele na kuwa ni katika sifa za saa za kudumu milele, hutanduka moyoni mawingu ya kukata tamaa na kutokomea giza la kukata tamaa katika roho. Saa hii inakuwa katika ibada ambayo ni kafara ya makosa na dhambi zilizofanywa na pengine yalikuwa ndiyo sababu ya kuingia jela. Na kwa hivyo tunagundua hekima ya kupewa kwetu mtihani kwa kufungwa jela na jela inakuwa ni madrasa ambamo tunapokea masomo yenye manufaa na humo pamoja na ndugu zetu kwenye msiba na mateso kitulizo na maliwazo. Imeelezwa katika (Neno la nne) vilevile mfano unaobainisha ukubwa wa hasara ambayo anaipata anayehemea kutafuta fungu lake duniani na kujitenga na Akhera nayo ni: Kuna ambao wanalipa lira tano au kumi kati ya lira ishirini na nne alizonazo katika kununua tikiti ya bahati nasibu – huenda inakuwa uwezekano wa kufanikiwa ni sehemu moja kati ya elfu kwa sababu ya kushiriki pamoja naye watu elfu – wakati ambapo hatumii moja katika saa ishirini na nne aliyonayo katika kununua tikiti inayompa faida ya hazina ya kudumu milele ya kiakhera. Hali ya kujua kwamba uwezekano wa kufanikiwa – kwa waumini ambao amali zao zilihitimishwa kwa wema - yeye ana yakini ya sehemu mia tisa na tisini na tisa katika elfu. Kama walivyo sisitiza hivyo manabii na mitume wote wema (a.s) na kuwasadikisha – kwa kufunuliwa na kwa kuhakikisha – mawalii na wateule ambao hawadhibitiki kwa idadi. Basi darasa hili fasaha kutoka katika Risale-i Nur inapasa wakuu wa jela wasiwe na shaka nalo na kila ambaye yanamhusu mambo ya nchi, kwa kuwa imethibiti kwa uzoefu: Kuongoza watu elfu katika wenye hofu na adhabu ya jela ya jahanamu na wenye kumuomba Allah (s.w) awalinde na adhabu hiyo ni rahisi sana kuliko kuwaongoza watu kumi katika wenye kuacha swala na wenye itikadi na tabia mbovu ambao hawaonyeki ila kwa adhabu na jela ya dunia na wala hawapambanui kati ya halali na haramu.
Kama risala ya (Mwongozo kwa vijana) ilivyofafanua ufafanuzi mzuri kwamba umauti hakuna pa kukimbilia kamwe, na kwamba kuja kwake ni kwa yakini zaidi kuliko yakini ya kuja kwa usiku wa mchana huu, na kufuatia kwa majira ya baridi baada majira haya ya mapukutiko. Na kama jela hii ilivyo ni nyumba ya wageni ya muda mfupi haiwi tupu ila inajazwa tena upya, basi dunia vivyo hivyo ni kama hoteli, na kama nyumba ya mafikio na misafara ambayo imejengwa kwenye njia ya misafara ya haraka. Umauti ambao unaondosha wakazi wa kila mji mara mia moja na kuwasukuma makaburini, hapana budi kuwa unakusudia kitu zaidi kuliko maisha haya ya kutoweka na chenye hadhi ya juu kuliko maisha hayo. Risale-i Nur imefumbua fumbo la hakika hii ya kushangaza na kuweka wazi na muhtasari wake ni: Kwa kuwa umauti hayauliwi, na mlango wa umauti haufungwi, hakika jambo kuu kabisa litakaloshughulisha akili ya mwanadamu na kufanya kuwa ni shida kubwa kwake ni kuokoka kutoka katika mkono wa mnyongaji huyu wa umauti na kukomboka kutokana na jela ya pekee ya kaburi. Risale-i Nur imethibitishwa kwa kukinaisha kabisa – kwa heri itokanayo kwenye nuru ya Qur’an – kwamba shida hii ina tiba na muhtasari wake ni kuwa: Umauti ima ni kunyongwa kwa milele na kutoweka kabisa ambako kunamsibu mtu na wapenzi wake na ndugu zake wa karibu wote, au kuruhusiwa kutokana na kazi kwa ajili ya kwenda kwenye ulimwengu mwingine ulio bora zaidi na hati ya kusafiria ya kuingia katika kasri za furaha kwa shahada na hati ya imani. Ama kaburi ni jela ya pekee yenye giza na lindi lenye kina kirefu au ni mlango kwenda katika mabustani ya kudumu milele na mahali pa wageni penye nuru baada ya kuruhusiwa kutoka katika jela ya dunia. Hakika Risala ya (mwongozo wa vijana) imethibitisha hakika hii kwa mfano nao: Hakika kumewekwa katika uwanja wa jela hii milingoti ya vitanzi ikiegemea kwenye ukuta, nyuma yake kuna afisi kubwa inatunuku zawadi za ukarimu watu wote washiriki. Na sisi wafungwa mia tano tunangojea zamu yetu tuitwe kwenye medani hiyo, tutaitwa huko mmoja mmoja tumependa au tumekataa, hakuna kuokoka! Ima kila mmoja wetu ataambiwa “Njoo upokee amri ya kunyongwa kwako na panda kitanzini” au: “Pokea amri ya jela ya pekee ya milele na uingie kwenye mlango huu ulio wazi” au patasemwa: “Furaha yako! umeshinda tikiti inayokupa faida ya mamilioni ya lira za dhahabu haya chukua”. Basi haya sisi hapa tunashuhudia matangazo ya ulinganio huu umeenea huku na kule na tunaona watu wanapanda kwenye vinyongeo kwa zamu na kati yao wapo wanaoshuka, na miongoni mwao wapo wanaoifanya kuwa ni ngazi ili kufika katika afisi ya zawadi iliyo nyuma yake, na tumeshakuwa katika yakini ya kukinaisha kwa yale yanayoendelea katika afisi ile - kana kwamba tunaiona kwa macho - kwa kuegemea kwenye yale wanayoyasema maafisa wakuu wa afisi hiyo katika simulizi za kweli zisizokubali shaka. Makundi mawili yameingia kwenye jela yetu - wakati huu - mojawapo linabeba zana za muziki na chupa za mvinyo pamoja na halua nje yake ni asali na ndani yake kuna sumu, wameziweka mashetani wa kibinadamu na wanatuletea na kutushawishi kuvitumia. Ama kundi la pili mikononi mwao kuna vitabu vya malezi na vipeperushi vya kitabia pamoja na vyakula vizuri na vinywaji vya baraka, wanatuletea vikiwa zawadi kwetu, na wanatueleza kwa kuafikiana na kwa utulivu kamili na yakini iliyotimia: Hakika ambacho kundi la kwanza inatoa katika vyakula si lolote isipokuwa ni mtihani na majaribio mkivikubali na kuviridhia hatima yenu itakuwa kama inavyodhihiri mbele yenu katika vinyongeo. Ama mkiridhia zawadi zetu – ambazo tunakuleteeni kwa jina la mtawala wa nchi hii na kwa amri yake - na mkasoma maelekezo yaliyomo na dhikiri kwenye vitabu hivyo mtaokoka na kunyongwa na mtapokea tikiti ya zawadi kutoka afisi ile ili mpate kufanikiwa faida kubwa, zawadi kutoka kwa mfalme, ukarimu na fadhila kutoka kwake. Sadikini tunayokwambieni na muitakidi kwa kina kana kwamba mnayaona kwenye mwanga wa mchana. Lakini hadharini na halua hizo zilizotiwa ladha ya asali - za haramu au zenye kutia shaka - ikiwa mtakula katika hizo matumbo yenu yatapata maumivu makali kutokana na athari ya sumu, mtasumbuliwa kutokana nazo maumivu hadi kupanda kwenu kwenye vinyongeo. Na kama hivyo kama ulivyo mfano huu kadari ya kiungu itawatunuku waumini ambao wametumia umri wao kwa utiifu na amali zao kuhitimishwa kwa mema atawatunuku hazina za milele hazikatiki baada ya kukoma kwa uhai wao wa kidunia, ama wale ambao waliopitiliza katika upotevu na ufuska bila ya kurejea kwa mola wao watanyongwa moja kwa moja (kwa wasioamini Akhera) au kuwekwa katika jela ya pekee yenye giza ya milele (kwa mwenye kuendelea katika upotevu wake na usafihi wake pamoja na kuamini kwake kwa kubakia kwa roho) hawa watapokea maamuzi ya mateso yao ya milele kwa yakini inayofikia tisini na tisa kwa mia. Naam, habari hii ya kweli wanaielezea mia moja na ishirini na nne elfu katika manabii (a.s). Na mbele yao kukiwa na miujiza inayowasadikisha na wanaelezea zaidi ya mia moja na ishirini na nne milioni katika mawalii mwenyezi mungu atukuze siri zao wenye kufuata nyayo za manabii (a.s) na wenye kusadikishwa kwa yale waliyoyaeleza kwa kufunuliwa na maonjo, na wanaelezea hilo pia wasiohesabika katika Maulamaa wenye kuhakiki na Mujitahidina na Masidikina ambao wamethibitisha madai yao na kusadikisha kwao kwa akili na fikira kwa dalili zenye nguvu na hoja zenye kukinaisha wakaelezea kwa yakini waliyoyaeleza wapekee hao kutokana na makundi hayo maili. Basi hayo makundi makubwa matatu na mijumuiko mingi katika watu wa kweli na hakika – nao ni viongozi wa utu na majua ya ubinadamu na miezi yake – wote wanaelezea hakika hiyo kwa makubaliano ya pamoja na kwa tawaturi. Hasara iliyoje kwa asiyetilia umuhimu amri zao wala hapiti njia iliyonyooka yenye kupelekea katika furaha ya milele kwa maelekezo yao wala kujali matokeo yake ya kuumiza - nayo kwa yakini inafikia tisini na tisa katika mia - katika wakati ambao hapiti katika njia ambayo ina uwezekano moja wa hatari na kwa kuegemea mwelezaji mmoja, bali atabadilisha njia nyingine japo ikiwa ndefu. Hawa ni mfano wa mlevi mwovu zuzu anayezugika kujali ming’ato ya mbu na kuachana na mashambulizi ya wanyama wakali wenye kumshambulia kwa kuwa amepoteza moyo na akili yake na kuharibu roho yake na kuteketeza utu wake kwa sababu yeye pamoja na taarifa za kweli zinazotokana na hao wapasha habari ambao wasio na idadi, ameacha njia fupi na nyepesi zaidi inayopelekea kwenye kufaulu kwa hakika pepo na furaha ya milele, na kuchagua njia ndefu kuliko hiyo na yenye taabu na dhiki zaidi na ambayo inampelekea katika jela ya jahanamu na mateso ya milele kwa lazima. Wakati ambapo mwanadamu – kama tulivyosema - hapiti njia fupi duniani yenye uwezekano mmoja katika mia wa hatari au yenye jela ya mwezi mmoja na kwa maneno ya mpasha habari mmoja na anaweza akawa ni muongo. Bali anafadhilisha njia nyengine japokuwa ni ndefu au haina manufaa kwa sababu tu ya kutokuwa na madhara. Kwa kuwa ukweli wa mambo ndio huu basi inatakikana kwetu sisi changamano la wenye kupewa mtihani wa jela tukubali kwa ridhaa yote na furaha zawadi za kundi la pili ili tulipe kisasi kwa nafsi zetu kutokana na msiba wa jela kama ilivyokuwa ladha ya dakika moja katika kulipiza kisasi na starehe ya dakika chache au saa katika usafihi zimetusukuma kuingia jela baadhi yetu wanaishi humo miaka kumi na tano au mwaka mmoja au miwili au miaka mitatu kutokea kuhukumiwa. Kwa hiyo basi juu yetu – bila ya hiari ya jela – tubadili kwa kukubali kwetu zawadi za kundi la pili, saa hizi chache kuwa ni siku za ibada kama hizo, na kubadili miaka miwili au mitatu ya kuadhibiwa kwetu kuwa katika miaka ishirini na thelathini ya umri wa milele. Na kubadili kwa miaka ishirini na thelathini ya kukaa kwetu jela kuwa mamilioni ya miaka ya kudumu milele. Hapo basi hukumu zilizotolewa dhidi yetu zitakuwa ni njia ya kuokoka na jela ya jahanamu. Na wakati huo maisha yetu ya Akhera yatatabasamu na furaha baada ya kilio na majonzi ya dunia yetu. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumelipiza kisasi kwa nafsi zetu kutokana na mateso hayo na kwa haki kabisa tutakuwa tumedhihirisha kuwa jela ni madarasa ya kimalezi ya kurekebisha tabia. Basi na washuhudie wakuu na watawala wa jela, hakika wale ambao waliowadhania kuwa ni waovu wauaji na kuwadhania kuwa ni masafihi wenye kukhalifu utaratibu wamekuwa ni wanafunzi wa madrasa ya kimalezi yenye kubarikiwa wanajifunza humo adabu nzuri na tabia iliyonyooka na kuwa raia wema kwa nchi na waja, basi na wamshukuru sana Mola wao.
Nalo ni tukio lenye mazingatio limetangulia kutajwa katika (Mwongozo kwa vijana) kwa upambanuzi, na muhtasari wake ni: Katika moja ya siku za Idi ya jamhuri nikiwa nimekaa mbele ya dirisha la jela ya (Eski şehir) ambayo ni mkabala na shule ya kati ya wasichana, wanafunzi wake chipukizi walikuwa wakicheza katika uwanja wa shule kwa furaha sana, ikaonekana kwangu ghafla katika kioo cha kimaanawy ikajionesha kwangu hali yao itakayokuwa baada ya miaka hamsini. Nikaona: Kwamba kiasi cha mabinti hamsini katika jumla ya wanao karibia wanafunzi sitini wanageuka udongo na kuadhibiwa kaburini na kwamba kumi kati yao wamegeuka kuwa ni vikongwe wabaya waliofikia umri wa miaka sabini na themanini, nimeshuhudia nyuso zao na uzuri wao kuharibika, wanateseka na maumivu kutokana na mitazamo ya kukirihisha kutoka kwa wale ambao walikuwa wanategemea kutoka kwao kuvutiwa na kupendezwa ni kwa kuwa hawakulinda heshima yao siku za ujana wao. Naam, hili nililiona kwa yakini nikalia juu ya hali yao yenye kuumiza kilio kikubwa kilichowazindua baadhi ya wenzangu jela wakanijia haraka wakiniuliza. Nikawaambia: “Niacheni sasa na hali yangu, nendeni niacheni” Ndiyo, nilichokiona ni hakika na sio mawazo ya kufikirika, kama kitakavyo kuja kiangazi hiki na mapukutiko na majira ya baridi hakika kilichopo nyuma ya kiangazi hiki cha ujana na nyuma ya majira ya mapukutiko ya uzee ni majira ya baridi ya kaburi na barazakhi. Lau ingeyumkinika kuonesha matukio fulani ya baada ya miaka hamsini ya mustakabali kama inavyoyumkinika hivyo kwa matukio ya miaka hamsini iliyopita - kwa kifaa kama kifaa cha sinema – na kuhudhurishwa matukio ya watu wa upotevu na hali zao katika mustakabali hivyo wangekirihika na kuumia na kulia kilio kichungu kwa hayo wanayoyafurahia hivi sasa na kuburudika nayo katika mambo yaliyoharamishwa. Na nilipokuwa nimezama katika kutafakari, na kugeukia yanayoonekana katika kioo cha kimaanawy yaliyohudhurishwa mbele yangu katika jela ya (Eskişehir), ikasimama mbele yangu haiba ya kimaanawy kana kwamba inawakilisha shetani wa kibinadamu na kulingania kwenye usafihi na kuchuuza upotevu akiniambia: “Tunataka kustarehe na starehe zote za maisha na kuwastarehesha wengine kwayo tuache na hali yetu na jiepushe nasi”. Nikamjibu kwa kusema: “Maadamu unajitupa katika mikono ya upotevu na usafihi kwa ajili ya starehe ndogo hali ya kusahau umauti na bila kuyajali, kwa hiyo tambua kuwa: Hakika (wakati uliopita) wote – kwa mujibu wa upotevu wako – umekufa umeteketea na kutokomea katika kutokuwepo, ni eneo kubwa la makaburi la kuogofya, mizoga imeoza na athari zimechakaa, kwa hivyo ikwa una gao la akili au ukiwa una moyo wenye kutweta uhai, hakika maumivu yanayotokana - kwa mujibu wa upotevu wako – na umauti wa milele, na kutokana na aina ya utengano usiokuwa na mipaka kwa ndugu na wapenzi wako wasiohesabika yanaondoa starehe hiyo ndogo yenye kulewesha ambayo unaionja katika kipindi kifupi mno. Na kama ilivyo (Muda uliopita) haupo kulingana na wewe, (Mustakabali) pia kwako haupo na hii ni kwa kutokuamini kwako, bali ni uwanda wa kutisha wenye giza mfu. Hakuna yeyote kati ya waliopo masikini atakuja na kudhihiri katika uwepo - kupitia muda uliopo - isipokuwa mnyongaji wa umauti atamkamata na kumtupa kwenye kukosekana. Na wewe kwa kuwa umefungamana na nyakati hizo – kwa kulingana na akili yako – hakika mustakabali unamimina katika kichwa chako chenye kukufuru mvua ya balaa ya machungu yenye kuumiza na shaka kubwa na migongano mikali hadi kufanya starehe zako zote ndogo za kisafihi ni athari baada ya kuwa ni zenye kuonekana. Lakini punde tu utakapo tupilia mbali njia ya upotevu na kuacha mwenendo wa usafihi kwa kuingia katika ngome ya imani ya uhakikisho, kwa hali ya kunyooka juu yake hata uone kwa nuru ya imani kwamba wakati huo uliopita kitambo sana sio kuwa haupo na wala sio mazikoni panapoozesha na kuteketeza kila kitu bali ni ulimwengu wa kinuru hasa ambao unageuka kuwa ni mustakabali, nao ni uwanda wa kungojelea roho zilizobaki zenye kutazamia ufufuo kwa kuingia katika Firdausi ya furaha ya milele iliyoandaliwa kwao; kwa hiyo inakuonjesha na hali ya kuwa ukingali duniani - ladha ya pepo ya kimaanawy kwa kadiri ya kiwango cha imani yako. Kama ulivyo mustakabali sio wenye kuumiza wala kutia dhiki wala sio mahali pa upweke wala sio bonde la giza la kuogofya bali huo kwa nuru ya imani ni mafikio ya furaha za milele za mwingi wa rehema mwenye kurehemu mwenye utukufu na ukarimu, ambaye rehema yake imekienea kila kitu na ukarimu wake umezungukia kila kitu. Kama Allah (s.w) alivyotandika majira ya machipuo na mapukutiko kuwa ni meza mbili zilizojaa aina mbalimbali za neema na vyakula, basi amekunjua (s.w) meza za dhifa zake za fahari katika kasiri hizo ndefu na amefungua maonesho ya hisani yake na neema zake zenye kuenea huko na watu wanatiwa shauku kuzielekea bali wanapelekwa huko. Naam, hivi ndivyo aonavyo muumini katika kioo cha kiimani - kila mmoja kulingana na daraja yake - na anayo nafasi ya kuhisi kitu katika ladha za hizo neema za kudumu. Kwa hivyo, ladha ya hakika safi ambayo haitibuliwi na maumivu hakika iko kwenye imani tu na kwa imani peke yake inayumkinika kuipata. Na kuna maelfu ya matunda matamu ya kiimani katika dunia hii na maelfu ya matokeo na faida isipokuwa sisi tutabainisha moja kati ya hizo kwa mfano: Jenga taswira - kwamba mtoto wako wa pekee unayempenda sana amelala kitandani ana machungu ya kukaribia umauti, na wewe umezama katika fikra ya kukata tamaa yenye uchungu na kuumia maumivu makali sana kutokana na kufariki kwake kwa milele kwenye maumivu. Jenga taswira - ukiwa katika hali hiyo ya kukatisha tamaa - tahamaki daktari bingwa - kama Hidhiri au Luqman - anakuja na kumnywesha mtoto dawa yenye kupambana na sumu ghafla anafungua macho yake kwa furaha kufurahikia maisha na ameokoka kutokana na umauti. Furaha yako unadhani itakuwaje.? Hali ni vivyohivyo kwa wale mamilioni ya waliozikwa katika makaburi ya muda uliopita unaowapenda - kama mtoto huyu – mapenzi makubwa na kufungamana nao kwa mahusiano. Wakati ambo wao wanakaribia kuteketezwa na kutoweka katika uwepo katika makaburi ya muda ulio pita - kwa mtazamo wako - tahamaki hakika ya imani inamulika nuru kupitia dirisha la moyo – kama alivyofanya Luqman Al-hakim kwa yule mtoto - katika eneo lile pana la makaburi ambalo linadhaniwa kuwa ndio kituo cha kunyongea. Na ghafla wafu wako wima wakiwa hai kwa nuru ile - katika ulimwengu wa Barazakhi - wananadi kwa ulimi wa hali: (Sisi sio wafu na hatutakufa kamwe na tutakutana hivi karibuni). Naam, kama uponaji wa mtoto uletavyo furaha na shangwe visivyo na mpaka baada ya kukata tamaa, mambo ni hivyohivyo hapa katika yanayotufanya tuwe na yakini kuwa imani – kwa kuleta kwake furaha hii katika dunia yetu hii - inathibitisha kwamba hakika yake ni mbegu inabeba katika uchangamfu kama ingechukua umbo ingemea juu yake pepo maalum kwa kila muumini na ingekuwa kwake mti wa tuba. Hivi ndivyo nilimwambia yule shetani mkaidi, isipokuwa alinishupalia kwa kusema: (Tuache tuishi japo kama wanyama, tukighafilika na yanayoenda katika mazingira yetu katika mambo haya makini, na tupitishe maisha yetu kwa ladha ya upuuzi na burudani ya mchezo). Nikamjibu: Hakika wewe hulinganishwi na mnyama, na hutokuwa mithili yake, kwa kuwa mnyama hana kinachomfikirisha muda uliopita na mustakabali. Mnyama haoni maumivu na masikitiko kwa yale yaliopita wala haimjii dhiki wala kuhofia mustakabali kwa hiyo anapata ladha yake kamili hivyo anamshukuru Muumba wake mkarimu. Bali hata mnyama aliyeandaliwa kwa ajili ya kuchinjwa hahisi isipokuwa maumivu ya kisu kikipita kwenye koromeo lake, kwa haraka hisia hii huondoka, basi anaokoka na maumivu hayo. Eh! rehema na huruma iliyoje ya Allah (s.w) ukubwa wake uliyoje kwa kudhihiri katika kuficha ghaibu na kusitiri misiba na mabalaa na hasa kwa wanyama. Lakini ewe mwanadamu kimekwishatoka kitu katika muda wako uliopita na mustakabali wako katika ghaibu kwa hukumu ya akili uliyo nayo, wewe umenyimwa kabisa yale wanayoneemeka nayo wanyama katika raha na utulivu kwa kuteremshwa pazia la ghaibu mbele yao, majuto na masikitiko yatokanayo na yaliyopita na aina ya utengano wenye kuumiza na hofu zitokanazo na mustakabali vinaondosha starehe yako ndogo na kutokomeza na kukutosa katika ngazi ya chini mno kuliko mnyama kwa upande wa starehe. Madhali hakika ni hivi, si juu yako kwa hiyo isipokuwa kujiweka mbali na akili yako na kuitupa nje na uihesabu nafsi yako kuwa ni mnyama uokoke, au uinawirishe akili yako kwa nuru ya imani na usikilize sauti tamu ya Qur’an tukufu uwe juu zaidi kuliko mnyama ukivuna ladha safi tohara na hali ukingali katika dunia hii yenye kutoweka. Nikamshinda kwa hoja hii lakini alipinga na kusema: (Kwa uchache tutaishi mfano wa makafiri wa kigeni) Nikamwambia kumjibu: (Hutakuwa hata mfano wa hao makafiri wa kigeni, kwa sababu wao wakimkanusha nabii mmoja wao wanaamini manabii wengine. Na hata kama hawamjui yeyote katika manabii wanaweza wakawa na imani ya Allah (s.w). Na kama hawakuwa na imani hii vilevile huenda wanacho cha kuwafikisha katika ukamilifu katika huluka njema na tabia za kiutu. Ama ikiwa Mwislamu atamkanusha nabii wa mwisho (s.a.w), na kukanusha dini ambayo hakuna dini nyingine isiyo kuwa hiyo ya haki na kujumuisha mambo yote na kuasi kutoka katika duara la uongofu wake na kuweka shingo yake nje yake, hatamridhia nabii mwingine bali hatoikubali imani ya Allah (s.w) kwa sababu hakujua manabii wengine na wala kupata uongofu wa kumwamini Allah (s.w), isipokuwa kwa kupitia kwake (s.a.w) na kwa kufikisha, kuelekeza na mwongozo wake. Kwa hiyo hakibaki chochote kati ya hivyo moyoni mwake isipokuwa kwa kumuamini yeye (s.a.w). Hii ndiyo sababu watu walikuwa tokea zama za kitambo sana katika dini nyingine wanaingia katika Uislamu makundi kwa makundi, wakati ambapo haikutokea kuwa Mwislamu mmoja akawa Yahudi wa kweli au Mmajusi wala Mnasara, na huenda akawa kafiri mharibifu wa imani na mwenendo mwenye kudhuru nchi na waja). Na kwa hivi nilisimamisha hoja juu ya mkaidi yule ya kwamba hawezi kushabihiana hata na makafiri wa kigeni. Na alipokuwa hakupata cha kuegemea alirudi nyuma na kukengeukia kwenye jahanamu na ubaya ulioje wa mafikio. Basi enyi ndugu zangu mliokusanyika katika madrasa hii ya Yusuf! Madhali hakika ndiyo hii, na Risale-i Nur imeeneza nuru yake - na haijaacha kuwa – tungu miaka ishirini ikiwa inavunja ukaidi wa wapingaji na kuwafanya kuwa hawana budi kuamini, basi juu yetu kushikamana na imani na njia iliyonyooka nyepesi yenye manufaa iliyo salama kwetu na mustakabali wetu na Akhera yetu na nchi yetu na uma wetu. Hii ni kwamba tusipoteze wakati wetu katika yasiyo na maana katika mawazo ya kufikirika na matarajio duni, bali tuuhuishe kwa kusoma sura tuzijuazo katika Qur’an tukufu nyakati za usiku na mchana, na kwa kujifundisha maana zake kutokana kwa ndugu zetu wenye kuzitendea kazi, na kulipa swala za faradhi zilizotupita na kwa kuvuna tabia njema kutoka miongoni mwetu, huenda Allah (s.w) akatujaalia kuwa katika wanaopandikiza katika jela hii miche ili itokee kuwa ni miti yenye kunufaisha, na tujibidiishe kwa juhudi ili maafisa wa jela wawe walimu waelekezi wakiwaandaa watu kwenda peponi kutoka katika madrasa hii ya Yusuf, na waangalizi wazuri wakisimamia kuwaelekeza vizuri na siyo maaskari wa mateso dhidi ya wahalifu wauaji.
Ndugu zangu wanaonihudumia siku moja waliniuliza wakisema: Vita vya ulimwengu vimechukua umuhimu kwa watu, na kushughulisha tufe la ardhi na kuliweka katika migongano na shaka na vina uhusiano na majaaliwa ya ulimwengu wa Kiislamu, isipokuwa sisi tunakuona huviulizii pamoja na kuwa zimepita siku hamsini tangu kuanza kwake - bali miaka saba – wakati ambao tunawaona watu wa dini na wanazuoni wanaacha msikiti na jamaa wakiharakisha kwenda kusikiliza redio Je, kuna kadhia kubwa zaidi kuliko hiyo inayoshughulisha akili yako? Au katika kujishughulisha navyo kuna hasara na madhara? Nikawajibu: Kwamba rasilimali ya umri ni chache na msafara wa umri hapa ni mfupi, wakati ambapo wajibu wa dharura na majukumu ambayo tuliyokalifishwa kuyatekeleza ni mengi na mambo hayo ya wajibu ni kama maduara yenye kuingiliana yenye kituo kimoja kwa mwanadamu: Kuanzia kwenye duara la moyo tumbo mwili nyumba mahali mji nchi na tufe la Ardhi na wanadamu, na kukomelea katika duara la walio hai wote na ulimwengu kwa jumla yote, hayo ni maduara yenye kuingiliana baadhi kwa baadhi nyingine. Kila mwanadamu ana aina ya kazi katika kila duara katika maduara hayo lakini wajibu mkubwa na muhimu zaidi bali wa kudumu kwa mujibu wake ni ule uliopo katika duara dogo zaidi na lililo karibu naye zaidi kati ya maduara hayo, wakati ambapo wajibu madogo sana na wenye hadhi chache na kudumu ni katika maduara hayo makubwa zaidi na yaliyo mbali zaidi na yeye. Basi kwa kupimia juu ya hili: Kazi na wajibu yamkini vikanasibiana kwa kinyume pamoja na upana wa duara, yaani kila duara linapokuwa dogo na karibu Jukumu huwa kubwa na kila linapokuwa duara ni kubwa na kuwa mbali umuhimu wa kazi hupungua. Lakini kwa kuwa duara kubwa ni lenye kushawishi na kuvutia linamshughulisha mwanadamu na mambo yasiyo ya lazima kwake na kugeuza fikira yake katika mambo yasiyomhusu chochote hata kumfanya apuuze wajibu wake wa kidharura katika duara dogo lililo karibu na yeye, wakati huo anaharibu rasilimali ya umri wake na kupoteza uhai wake bure bileshi. Ongeza juu ya hapo kuwa moyo wake unaweza kuelemea na kupendelea upande mmoja kati ya pande mbili zenye kuhasimiana kwa kufuatilia kwake kwa hima habari za vita vinavyotimba kati yao. Hapati nafsini mwake kukanusha dhuluma za upande huo, bali anaridhika nazo na anakuwa mshirika katika udhalimu wake. Ama jawabu la nukta ya kwanza ni kwamba mbele ya kila mwanadamu – na hasa Mwislamu – kuna suala muhimu na tukio la hatari ni kuu kuliko ugomvi unaotokea kati ya mataifa makubwa kwa ajili ya kutawala tufe la Ardhi. Suala hilo lina umuhimu na hatari kiasi ambacho laiti mwanadamu mwenye akili angekuwa anamiliki nguvu ya Wajerumani na Waingereza kwa pamoja asingesita kuzitumia zote kwa ajili ya kushinda kadhia hiyo inayotakiwa. Kadhia hiyo ni ile ambayo wameitangaza mia moja elfu kati ya wateule bora na kunyanyua bendera yake kiasi kisicho na mpaka katika nyota wa wanadamu na waelekezi wao wenye kuegemea maelfu ya ahadi za mola mlezi wa walimwengu bali wameshuhudia baadhi yao kwa dhahiri kwamba kadhia hii ni kadhia ya hatima ya mwanadamu nayo: Mwanadamu achume kwa imani au apate hasara kwa kutokuwa na imani, ufalme mkubwa wa kudumu milele na makazi mazuri katika pepo ya kudumu upana wake ni sawa na mbingu na ardhi. Basi asiyefaulu tikiti ya imani na wala hakuichunga haki ya kuichunga ni lazima atapoteza kadhia hiyo na kupata hasara na hiyo ndiyo hasara dhahiri. Na wengi wamepoteza kadhia yao hii katika zama zetu hizi - katika waliotahiniwa kwa tauni ya u-maada – hadi amefunuliwa mmoja wao naye ni katika watu wa elimu na kufunuliwa na ameshuhudia kwamba watu wachache tu katika kila watu arobaini – mahali fulani - ndio ambao waliyo okoka kwa imani katika machungu ya umauti na uhai wao kuhitimishwa kwa wema, ama waliobaki wameangamia! Unaonaje kama mmoja wao angepewa utawala na ufalme wa dunia na mapambo yake badala ya kadhia hiyo kuu, je, badala hii itakuwa ni yenye kufanana na alichokikosa? Au kuchukua nafasi yake kwa hali yoyote? Hapana! Na kwa ajili hii sisi changamani wa wanafunzi wa Nur tunajua kwa yakini kwamba kuacha huduma kubwa ambazo zinatufanya tufaulu kadhia hiyo, na kupuuza majukumu ya wakili wake ambaye anayatunza kwa tisini katika mia na kushughulika na yasiyo na maana miongoni mwa mambo ya nje na kutilia muhimu kusiko na maana kana kwamba dunia ni yenye kudumu milele, sio chochote ila ni uzuzu wa akili na wendawazimu. Hakika sisi tuna yakini na utulivu kamili wa hili kwa hiyo mmoja wetu lau kama angekuwa na akili na utambuzi wa mambo maradufu na maradufu ya aliyonayo hivi sasa angeitoa yote kwa ajili ya kadhia hiyo. Basi enyi ndugu zangu wenye muda wa hivi karibuni katika msiba wa jela! Nyinyi bado hamjafanya mtalaa wa Risale-i Nur bado kama walivyofanya ndugu zangu waliotangulia ambao waliingia jela pamoja nasi, mimi nawasikilizisheni kauli na kukushuhudilieni ndugu hao wote maelfu ya mifano yao na nimesema hilo mara nyingi na nimelithibitisha mara kwa mara: Hakika Risale-i Nur imewapa ushindi wa kadhia hiyo kuu kwa asilimia tisini katika mia kati yao, nayo ndiyo iliyokabidhi hati na tikiti ya kufuzu - nayo ni imani ya hakika – kwa watu ishirini elfu ndani ya miaka ishirini iliyopita. Basi sio ajabu hilo imechimbuka kutoka katika muujiza wa Qur’an tukufu na kuwa mbele ya mawakili wa kadhia kuu na wenye kuitetea katika zama hizi, basi licha ya kumalizika miaka kumi na nane na maadui na wazandiki na wana maada wanasuka aina za njama na hila mbaya na hawajaacha kuwa wanahamasisha baadhi ya maafisa dhidi yetu wakiwatumia kwa lengo la kutuangamiza na hata kutusukumiza kwenye giza la jela mfano wa mara hii. Isipokuwa hawakufanya jambo la kutajika, na - kwa idhini ya Allah (s.w) – hawatofanya, hii ni kwa sababu wao hawakuweza kuidhuru ngome ya chuma cha pua ya Risale-i Nur na wala kugusa zana zake zenye kufikia mia moja na thelathini (Risala) isipokuwa risala mbili au tatu tu kati ya hizo. Basi anayetaka kuweka wakili kutetea kadhia yake yatosha kushikamana na ngome hiyo na kuchota katika nuru yake. Enyi ndugu! Msihofu, Risale-i Nur haitazuiliwa kwenye macho wala haitafunikwa isionekane. Wala haitaondoshwa kati ya watu – kwa idhini ya Allah (s.w) - kwani sehemu zake muhimu zinasomwa - ila risala mbili au tatu – na wawakilishi wa bunge na nguzo za taifa kwa uhuru kamili. Na itafika hiyo siku ambayo maafisa na wakurugenzi wenye hadhi watagawa Risale-i Nur – Inshaallah – kwa wafungwa kama wanavyowagawia mkate na dawa na watayageuza magereza kuwa madrasa za maelekezo, malezi na kutengeneza maadili.
Kama ilivyoelezwa katika Risala ya (Mwongozo kwa vijana): Hakika ya ujana ni wenye kwenda zake na utaondoka hakuna namna, kwani ni kama majira ya joto yanafuatiwa na mapukutiko na majira ya baridi na mchana hufuatiwa na jioni na usiku na ujana pia utageuka kuwa uzee na umauti. Kwa mfano wa hakika hii isiyo na budi. Kijana atakapotumia nguvu aliyonayo ya muda mfupi katika kheri na wema ndani ya duara la usafi, kujizuia na msimamo, kwa hakika amri zote za mbinguni zinambashiria kwamba atavuna kwa ujana huo ujana wenye kubakia usiotoweka, kama ilivyo ghadhabu ya dakika moja inaweza kumsukuma mwanadamu katika kuingia hatia ya kuua akahukumiwa kuteseka mamilioni ya dakika ya mateso na adhabu ya jela, vilevile mihemko ya ujana na usafihi wake na vionjo vyake vya mpito – katika asiyoyahalalisha Allah (s.w) – humsababishia maumivu mengi na yakuendelea ndani ya ladha hiyohiyo, ukiachilia mbali adhabu ya kutisha Akhera na adhabu chungu kaburini, na taabu ya majuto ya kuendelea yatokanayo na kuondoka kwa ladha, na adhabu duniani kutokana na dhambi na maovu. Kila kijana mtambuzi kwa uzoefu alioupata anashuhudia kwa ukweli uwepo wa maumivu haya ndani ya ladha yenyewe. Kwa mfano: Mapenzi yaliyoharamishwa au ashiki kwa namna isiyo ya haki, ina maumivu kiasi cha kuharibu ladha ndogo iliyomo; kati ya hayo ni kuhisi wivu na husuda, na kati ya hayo ni maumivu ya kufarikiana na mpenzi, na kati ya hayo ni kutopata mahaba ya sawa sawa na mengineyo mengi katika yenye kuharibu ambayo hufanya ladha hiyo ndogo kuwa ni sawa na asali iliyowekwa sumu. Ikwa unataka kufahamu kwamba matumizi mabaya ya ujana na israfu yao katika mambo yao huwasababishia magonjwa yanayowapeleka mahospitalini na makaburini. Na ukitaka kufahamu kwamba kudanganyika kwa vijana na kutangatanga kwao huwapeleka magerezani. Na ukiwa unataka kufahamu kuwa yanayowasibu katika maumivu ya kimaanawy na majonzi ya kinafsi – ni kutokana na njaa ya kiroho, njaa ya moyo na kuwa na muda wa bure – vinawapeleka katika milango ya baa na nyumba za starehe. Ndiyo, ukitaka kuhakikisha hili uliza hospitali, magereza, vilabu vya pombe, na makaburi kwa vyovyote utasikia masikitiko na miguno na vilio vikali na malalamiko ya majuto na sauti za kuumia na kujutia huzitoa – aghalabu - vijana waovu ambao wamepata mapigo ya kuumiza kwa kutoka kwao nje ya aliyoyahalalishia Allah (s.w) katika vitu vizuri kwa msukumo wa hisia na israfu zao na uovu wa matendo yao na kutenda kwao mambo yaliyoharamishwa na kufuatilia kwao matamu yenye uovu. Wakati ambao kijana akitumia ujana wake kwa alivyomwamrisha Allah (s.w) na kushika njia ya sawa na akwa na msimamo basi ataifanya kuwa ni neema tamu mno ya kiungu na hiba nzuri mno ya mwingi wa rehema, na kuifanya kuwa ni njia iliyonyooka iliyo nyepesi kuelekea katika matendo mema, na kumpatia ujana wenye kung’ara pia wa kudumu milele huko Akhera badala ya ujana huu unaokwisha na kutoweka. Hilo ndilo ambalo vitabu vya mbinguni na suhufi zilizoteremshwa vyote vinatubashiria vikiongozwa na Qur’an tukufu kwa aya zake tukufu zenye hekima. Maadamu ukweli ndio huu, na maadamu medani ya halali inatosha kwa ajili ya maliwazo, starehe na burudiko, na maadamu ladha moja – ndani ya yaliyo haramishwa – humuonjesha mtendaji maumivu yanayodumu mwaka mmoja ya adhabu ya jela na mara nyingine ni miaka kumi, kwa hiyo ni lazima kutumia kipindi cha ujana kwa kujitunza, usafi na msimamo katika njia ya sawa sawa kwa kutekeleza shukurani ya neema hiyo tamu iliyotunukiwa, bali hili ndio la lazima zaidi.
Suala hili ni ishara kwa muhtasari ya hoja moja tu kati ya maelfu ya hoja za jumla juu ya (Kumwamini Allah (s.w)) na ambayo imeelezwa pamoja na hoja zake za kukinaisha katika sehemu nyingi za Risale-i Nur. Lilinijia kundi katika wanafunzi wa sekondari huko (Kastamonu) wakisema “Tujulishe Muumba wetu kwa sababu walimu wetu hawatuelezi habari za Mungu!”. Nikawaambia: “Kila somo katika masomo mnayosoma daima linaelezea kuhusu Allah (s.w), na kumjulisha Muumba Mkarimu kwa lugha yake maalum. Basi sikilizeni masomo hayo na sio walimu”. Kwa mfano: Lingekuwapo duka la madawa kubwa, katika kila chupa kati ya chupa zake kumewekwa madawa kwa vipimo nyeti na kwa kiasi madhubuti; kama linavyotuonesha kwamba nyuma yake kuna mtaalamu wa madawa mwenye busara, na mkemia mahiri, vivyo hivyo duka la madawa la tufe la ardhi ambalo linajumuisha zaidi ya sampuli mia nne elfu za vilivyo hai ikiwemo mimea na wanyama, na kila moja kati ya hizo kwa hakika ni sawa na chupa ya madawa ya kikemia madhubuti, na chupa ya mchanganyiko ya kiuhai ya ajabu. Basi duka hili kubwa la madawa linamuonesha hata kipofu mfamasia wake mwingi wa hekima mtukufu, na kumtambulisha Muumba wake mkarimu kwa kiwango cha ukamilifu, mpangilio na ukubwa wake, kwa kulinganisha na duka lile la madawa liliopo sokoni, kulingana na vipimo vya (Elimu ya tiba) mnayoisoma. Na kwa mfano: Kama kiwanda cha ajabu kinavyofuma maelfu ya bidhaa anuwai za kufumwa, na vitambaa mbalimbali, kutokana na maada rahisi mno, kinatuonesha pasi na shaka kwamba nyuma yake kuna mhandisi makanika mahiri, na kumtambulisha kwetu; kadhalika mashine hii ya kiungu itembeayo inayoitwa tufe la ardhi, na kiwanda hiki cha kiungu ambacho ndani yake kuna mamia ya maelfu ya viwanda vikuu, na katika kila kimoja kati ya hivyo kuna maelfu ya viwanda bora, kinatujulisha bila ya shaka fundi wake na mmiliki wake kulingana na vipimo vya (Elimu ya makanika) mnayoisoma, kinamtambulisha kwa kiwango cha ukamilifu wa kiwanda hiki cha kiungu, na ukubwa wake kwa kulinganisha na kile kiwanda cha mwanadamu. Na kwa mfano: Kama vile stoo au ghala la vyakula na riziki, na duka kubwa la vyakula lililowekwa kutoka – kila upande - sampuli elfu moja ya bidhaa za vyakula, na kupambanuliwa kila moja dhidi ya nyingine, na kupangwa safu katika mahali pake maalum, linavyotuonesha kwamba lina mmiliki na mwendeshaji; kadhalika ghala hili la Mwingi wa rehema kwa ajili ya vyakula ambavyo vinaenda kila mwaka masafa ya miaka ishirini na nne elfu, katika mpangilio madhubuti maridadi, na ambalo linakusanya ndani yake mamia ya maelfu katika aina za viumbe ambao kila mmoja anahitaji aina maalum ya chakula. Na ambalo linapita katika majira manne linakuja na majira ya machipuo kama lori lililosheheni maelfu ya aina za vyakula tofauti, linavileta kwa viumbe masikini ambao majira ya baridi vyakula vyao vilikwisha. Hilo ndio tufe la Ardhi na jahazi la Subuhana ambalo linajumuisha maelfu ya sampuli za bidhaa na zana na makopo ya vyakula. Ghala na bohari hii ya kiungu – inaonesha – kulingana na vipimo vya (Elimu ya lishe na biashara) mnayoisoma – mwenyewe mmiliki wake na msarifu wake kwa kiwango cha ukubwa wa ghala hili, kwa kulinganisha na ghala lile lililotengenezwa na mwanadamu na inamtambulisha kwetu na kutuelekeza tumpende. Na kwa mfano: Lau ikiwa jeshi kubwa katika kikosi chake kuna aina mia nne elfu za mataifa mbalimbali kila aina ina chakula chake pekee tofauti na aina nyingine, na silaha inayoitumia ni tofauti na silaha ya kundi lingine, na mavazi inayovaa yanatofautiana na mavazi ya kundi lingine, na mtindo wa mazoezi yake na mafunzo yake ni mbali na wa kundi lingine, na muda wa kazi na kipindi cha kupumzika sio muda wa kundi lingine, basi kiongozi wa jeshi hili ambaye peke yake anawapa riziki tofauti, silaha mbali mbali, mavazi tofauti bila ya kumsahau yeyote kati yao wala kuchanganya wala kubabaika ni kiongozi hasa mwenye maajabu bila shaka yoyote; kama kambi hii ya ajabu inavyotuonesha kwa uwazi kiongozi huyo wa kufurutu ada bali inatuelekeza kumpenda kwa heshima zote na kupendezwa; hali kadhalika kambi ya Ardhi katika kila majira ya machipuo inaandikisha upya jeshi kubwa la Subuhana likiundwa na aina mia nne elfu za mataifa ya mimea na wanyama na kuipa kila aina mavazi yake, riziki zake, silaha zake, mazoezi yake na ruhusa zake maalum kutoka kwa kiongozi mkuu mmoja wa pekee mtukufu bila kusahau aina yoyote wala kuchanganya wala kubabaika katika ukomo wa ukamilifu na upeo wa mpangilio. Basi kambi hii kunjufu pana sana ya majira ya machipuo yenye kutandawaa juu ya uso wa Ardhi inaonesha – kwa wenye akili na busara – mtawala wa Ardhi kulingana na (Elimu za kijeshi) mlezi wake na mwendeshaji wake na kiongozi wake mtakatifu sana na mtukufu na kuwajulisha kwa kiwango cha ukamilifu wa kambi hii ya kifahari na kiasi cha ukubwa wake kwa kulinganisha na kambi ile iliyotajwa, bali inaelekeza kumpenda mmiliki wake (s.w) kwa kumsifu, kumtukuza na kumtakasa. Kwa mfano: Fikiria kwamba mamilioni ya taa za umeme zinatembea katika mji wa ajabu bila kuisha mafuta yake wala kuzimika. Je, hazioneshi - kwa mshangao na heshima - kwamba yupo mhandisi bingwa na mtaalamu wa umeme mwerevu mno wa kiwanda cha kufua umeme na wa taa hizo? basi taa za nyota zinazoning’inia katika dari ya kasiri la Ardhi ambazo ni kubwa kuliko tufe la Ardhi yenyewe kwa mara elfu nyingi kulingana na elimu ya falaki na zinakimbia upesi kuliko mfyatuko wa kombora, bila ya kupotosha mpangilio wake au kugongana na wenzake kabisa na bila ya kuzimika, wala kuisha kwa mafuta kulingana na mnayoyasoma katika (Elimu ya falaki). Taa hizi zinaashiria kwa vidole vya nuru katika uwezo wa Muumba wake usio na mpaka. Jua letu kwa mfano ambalo ni kubwa kwa mara milioni kuliko tufe letu la Ardhi na la zamani kuliko ardhi kwa miaka milioni, sio ila ni taa ya daima na jiko lenye kuendelea katika nyumba ya wageni ya mwingi wa rehema. Basi kwa ajili ya kudumisha kuwaka kwake kila siku inalazimu mafuta mithili ya bahari za ardhi, na mkaa kwa kadiri ya milima yake, na kuni kwa kiasi cha maradufu kwa maradufu ya ukubwa wa ardhi, lakini ambaye analiwasha - na kuwasha nyota zote mfano wake bila mafuta wala mkaa wala zeti na bila ya kuzimika na kulikimbiza kwa kasi kubwa kwa pamoja bila kugongana, hakika ni uwezo usio na ukomo na ufalme mkubwa usio na mipaka. Basi ulimwengu huu mkubwa na taa zilizomo zenye kuangaza, na kandili zenye kuning’inia unabainisha kwa uwazi – kwa mujibu wa vipimo vya elimu ya umeme - mfalme wa maonesho haya na tamasha kubwa, na unamtambulisha mnawirishaji wake na mwendeshaji wake wa ajabu na mtengenezaji wake mtukufu, kwa ushahidi wa hizi nyota zenye kumemetuka, na kuelekeza kumpenda kwa wote kwa kumsifu, kumtakasa na kumtukuza, bali inawapeleka kwenda kumwabudu (s.w). Na kwa mfano: Lau kingekuwapo kitabu katika kila mstari wa kitabu hicho kimeandikwa kitabu kwa hati makini na kuandikwa katika kila neno miongoni mwa maneno yake sura ya Qur’an, na masuala yake yote yakawa na maana ya kina, na yote yanaungana mkono, basi kitabu hiki cha ajabu bila shaka kinabainisha umahiri wa mwandishi wake wa hali ya juu, na uwezo wa mwandishi wake uliokamilika. Yaani mfano wa kitabu hiki kinamtambulisha mwandishi na msanifu wake utambulisho ulio wazi kama ulivyo mchana, na unabainisha ukamilifu wake na uweza wake na unachochea kupendezwa na kuheshimu mbele ya wenye kukitazama kiasi hawana la kusema mbele yake ila kukariri: (Tabarakallah, Subhanallah, Mashaallah!) katika maneno ya kusifia uzuri na kupendezwa; vivyo hivyo kitabu hiki kikubwa cha ulimwengu katika ukurasa mmoja wa kitabu hicho ambao ni uso wa ardhi na jozi moja ya sahifa yake nayo ni majira ya machipuo huandikwa aina za vitabu tofauti mia tatu elfu ambazo ni makundi ya wanyama na mimea kila moja ni sawa na kitabu, vyote hivyo vinaandikwa kwa pamoja na vikiwa vimeingiliana pasi na kuchanganyika, kukosea au kusahau, na katika ukomo wa mpangilio na ukamilifu, bali huandikwa kasida kamili ya kupendeza katika neno moja kama mti, na katika kila nukta kama mbegu huandikwa faharisi ya kitabu kamili. Kama linavyo shuhudiwa hili na lilivyo kiuhalisia mbele yetu linatuonesha kwa misisitizo kwamba nyuma yake kuna kalamu inayotiririka inayoandika, ni wajibu wenu sasa kukadiria kiasi cha kujulisha kwa kitabu cha ulimwengu kikubwa ambacho katika kila neno lake kuna maana lundo na hekima tofauti, na kiasi cha kujulisha kwa Qur’an hii kubwa mno iliyopata umbo ambayo ni ulimwengu, Muumba wake (s.w) na mwandishi wake (s.w) kwa kulinganisha na kile kitabu kilichotajwa katika mfano. Na hii kwa muktadha wa mnachosoma katika (Elimu ya hekima ya vitu) au (Sanaa ya usomaji na uandishi) na muichukue kwa kipimo kikubwa zaidi, na kwa mtazamo mpana katika ulimwengu huu mkubwa. Na kwa hivyo mtafahamu ni vipi kinamtambulisha Muumba mtukufu kwa (Allah akbar), na vipi kinafundisha kutakasa kwa (Subhanallah) na vipi humpendezesha Allah (s.w) kwetu kwa kusifu (Alhamdulillah). Na kama hivi hakika kila elimu miongoni mwa elimu nyingi mno inajulisha juu ya Muumba wa ulimwengu (s.w) - kwa kulinganisha na yaliyotangulia – na inamtambulisha kwetu (s.w) kwa majina yake yaliyo mazuri na kutuelimisha kwa sifa zake tukufu na makamilifu yake. Na hii ni kwa yale iliyonayo miongoni mwa vipimo vikunjufu na vioo maalum na macho makali yenye kuona na mitazamo yenye mazingatio. Nikawaambia wanafunzi wale vijana: Hekima ya kukariri kwa Qur’an tukufu. ﴾خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ﴿ na ﴾رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ﴿ Hakika ni kwa ajili ya kuelekeza katika hakika hii iliyotajwa, na kufundisha hoja hii ya wazi ya Tawhid, na kwa ajili ya kututambulisha Muumba wetu mtukufu (s.w). Wakasema: Shukurani kwa mola wetu Muumba bila mpaka, juu ya somo hili ambalo lenyewe ni hakika ya hali ya juu. Allah akulipe malipo yaliyo bora na akuridhie. Hakika mwanadamu ni mashine yenye uhai, huumia kwa maelfu ya aina ya maumivu na kupata ladha kwa maelfu ya aina za ladha, pamoja na kuwa yuko katika ukomo wa kutojiweza, ana maadui wasio na mpaka sawa ni wa kimaada au wa kimaanawy, na pamoja na kuwa yupo katika ufukara, ana matakwa ya ndani na ya nje yasiyohesabika; ni kiumbe masikini anayepata maumivu ya mapigo ya kutoweka na utengano kwa kuendelea. Na pamoja na yote haya anapata kwa kujinasibisha na mfalme mtukufu kwa imani na uja maegemeo yenye nguvu, na ngome kubwa anayojihami nayo katika kuwazuia maadui wake wote, na humo pia anapata pa kuomba msaada anaomba kwa ajili ya kukidhi mahitaji yake na kujibu matakwa yake na matarajio yake yote. Kama kila mmoja anavyojinasibu kwa bwana wake na kujifaharisha kwa utukufu wa kujinasibisha naye na anajienzi kwa nafasi ya cheo chake kwake, vivyo hivyo kujinasibu kwa binadamu - kwa imani - kwa mweza ambaye uweza wake hauna ukomo, na kwa mfalme mwingi wa rehema mwenye rehema kunjufu, na kuingia katika uja wake utiifu na shukurani, hubadili muda wa umri na umauti kutokana na kunyongwa kwa milele kuwa tikiti ya kupita na ruhusa ya kwenda kwenye ulimwengu wa kudumu! Ni juu yenu kukadiria ni kiasi gani mwanadamu anakuwa mwenye kupata ladha ya uja mbele ya Bwana wake, na kuneemeka na imani ambayo anaiona moyoni mwake, na mwenye kufurahi kwa nuru za Uislamu, na mwenye kujifaharisha kwa Bwana wake Mweza Mwingi wa rehema akiwa mwenye kumshukuru kwa neema ya imani na Uislamu. Kama nilivyowaambia hayo ndugu zangu wanafunzi ndivyo ninavyo waambi vilevile wafungwa: Hakika aliyemtambua Allah na kumtii ni mwenye furaha japo akiwa katika giza la jela. Na mwenye kughafilika naye na kumsahau ni mwenye mateso japo akiwa kwenye kasri kubwa. Mdhulumiwa siko moja alipiga kelele na kusema mbele ya madhalimu hali akipanda kizimba cha kunyongwa akiwa mwenye furaha akasema: “Hakika mimi siishii katika kutoweka wala sinyongwi, bali ninaachiliwa huru kutoka katika jela ya dunia kwenda katika furaha ya milele, lakini ninakuoneni kuwa nyinyi ndio mmehukumiwa kifo cha milele kwa vile mnavyoona kuwa umauti ni kutoweka na kukosekana. Kwa hiyo nafsi yangu imeshalipa kisasi kwenu” akasalimisha roho yake akiwa ameridhia akikariri: (لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ). سُب۟حَانَكَ لَا عِل۟مَ لَنَٓا اِلَّا مَا عَلَّم۟تَنَٓا اِنَّكَ اَن۟تَ ال۟عَلٖيمُ ال۟حَكٖيمُ
Tunda lililoiva siku ya Ijumaa katika siku za jela ya Denizli وَمَٓا اَم۟رُ السَّاعَةِ اِلَّا كَلَم۟حِ ال۟بَصَرِ اَو۟ هُوَ اَق۟رَبُ مَا خَل۟قُكُم۟ وَلَا بَع۟ثُكُم۟ اِلَّا كَنَف۟سٍ وَاحِدَةٍ فَان۟ظُر۟ اِلٰٓى اٰثَارِ رَح۟مَتِ اللّٰهِ كَي۟فَ يُح۟يِى ال۟اَر۟ضَ بَع۟دَ مَو۟تِهَا اِنَّ ذٰلِكَ لَمُح۟يِى ال۟مَو۟تٰى وَهُوَ عَلٰى كُلِّ شَى۟ءٍ قَدٖيرٌ Siku moja nilikuwa nimetoa somo (Kastamonu) kwa lugha ya elimu za shule kwa baadhi ya wanafunzi wa sekondari ambao walikuja kuniuliza: “Tutambulishe Muumba wetu” kama ilivyokuja katika suala la sita lililoelezwa huko nyuma, walilipata baadhi ya walioweza kuwasiliana nami katika wafungwa huko (Denizli), wakapata utulivu wa imani na ukinaifu kamili uliowafanya wapate shauku kubwa kuhusiana na Akhera, wakaharakisha kusema: “Tujulishe Akhera yetu vilevile kwa ukamilifu, kiasi baada ya hapo tusipotezwe na nafsi zetu na mashetani wa enzi hizi vikatutupia kwenye jela kama hizi”. Na kuitikia ombi lao na kusaidia haja ya wanafunzi wa Risale-i Nur katika jela ya (Denizli) na kwa matakwa makubwa kutoka kwa wale waliopitia (Suala la sita) nikaona ni jambo la lazima juu yangu nibainishe muhtasari mdogo kuhusu nguzo ya imani muhimu: (Akhera). Basi ninasema kwa muhtasari kutoka kwenye Risale-i Nur: Kama tulivyouliza katika (Suala la sita) ardhi na mbingu kuhusu Muumba wetu (s.w), zikatujibu kwa ulimi wa elimu za sasa na kutujulisha kuhusu Muumba wetu ujuzi wa wazi uwazi sawa na jua, kadhalika tutamuuliza kwanza Mola wetu mlezi tuliyemjua kwa yakini kuhusu Akhera yetu kisha tutamuuliza mtume wetu mtukufu (s.a.w), kisha Qur’an yetu tukufu, kisha baki ya manabii (a.s) na vitabu vitakatifu, kisha malaika kisha viumbe. Haya sasa ndio tupo katika ngazi ya mwanzo tunamuuliza Allah (s.w) kuhusu (Akhera) anatueleza (s.w) kwa amri zake zote na kwa mitume yake yote na kwa majina yake mazuri yote na sifa zake tukufu zote kwa kusema: Akhera haina shaka na mtapelekwa huko. Na kwa kuwa (Neno la kumi) limethibitisha Akhera kwa hakika kumi na mbili za kukinaisha safi kwa dalili za sehemu za majina mazuri; kwa hiyo tunaashiria hapa - ishara fupi - kwenye dalili hizo kwa kutosheka na ufafanuzi huo. Naam, ni kwamba hakuna mfalme mkuu bila ya kuwa na zawadi kwa watiifu na adhabu kwa waasi. Hivyo hapana budi kwamba mfalme wa milele - naye yuko juu katika hali ya juu ya Rububiyya ya moja kwa moja - ana zawadi kwa wenye kujinasibisha kwake kwa imani na wenye kusalimu amri zake kwa utiifu. Na ana adhabu kwa wale waliokanusha ukuu wake na enzi yake kwa ukafiri na uasi. Hapana budi kwamba zawadi hiyo itakuwa yenye kulingana na rehema yake na uzuri wake, na hiyo adhabu itakuwa inawiana na enzi yake na utukufu wake. Na kwa hivi linatujibu jina la (As-Sultan Ad-dayyan) na (Rabbul alamiin) swali letu kuhusu Akhera. Kisha tunaona kwa macho yetu – kwa uwazi sawa na jua - kwamba rehema enevu na huruma yenye kuzunguka na ukarimu wenye kuenea kwenye uso wote wa ardhi; majira ya machipuo yenye kupambika hayaingii hadi unaona rehema inapamba miti, mimea na matunda na kuivika mavazi ya kijani kana kwamba hao ni mahuri wa peponi, na kusalimisha mikononi mwake aina mbalimbali za matunda tofauti, na kutuletea kwa kusema: (Hivyo hapo kuleni na stareheni...) na unaiona ikitulisha asali safi yenye kuponya yenye ladha kupitia mdudu mwenye sumu! na kutuvika hariri laini inayofumwa na mdudu asiye na mkono! na kuhifadhi katika gao la mbegu ndogondogo na punje, maelfu ya tani za chakula na kuzibadili kuwa ni hazina ya akiba kwetu. Basi ambaye ana rehema hii kunjufu na huruma hii enevu na ukarimu wenye kuenea hapana shaka kwamba yeye hata wafanya waja wake waumini wapendwa kwake kutoweka na kutokuwepo kabisa, wale ambao amewalea na kuwaneemesha na kuwakirimu kwa kiwango hiki cha upole ulaini na uangalizi. Bali ataweka ukomo wa jukumu lao katika uhai wa dunia ili kuwaandaa kwa rehema kunjufu na kubwa zaidi. Na kwa hivi jina la Allah (Ar-Rahaman) na (Al-Kariim) katika majina mazuri yanajibu swali letu kuhusu Akhera yakitwambia: (Pepo ni haki). Kisha tunaona majukumu ya viumbe yakifumwa kwa mtindo wa hekima na kupimwa kwa mizani ya uadilifu. Navyo ni katika umakini na unyeti kiasi mwanadamu hajengi taswira bora kuliko viwili hivyo. Basi tunaona hekima ya kiazali imemtunuku mwanadamu uwezo wa kuhifadhi – kama punje ya haridali kwa ukubwa – na imeandika humo maelezo ya uhai wake na matukio yanayomhusu yasiyohesabika, kana kwamba hiyo ni maktaba ndogo sana yenye hati za kumbukumbu, na imeyaweka kwenye pembe moja ya ubongo wake, ili daima imkumbushe siku ya hesabu, siku yatakapo kunjuliwa yaliyomo katika nyaraka za amali. Na tunaona uadilifu wa moja kwa moja unaweka kila kiungo katika kiumbe hai mahali pake panapofaa kwake, na kuratibu kwa mizani madhubuti nyeti – kuanzia kijidudu kidogo hadi mnyama mkubwa kabisa, na kutoka katika nyuki dhaifu hadi kipanga wa kutisha, na kutokana na ua maridadi hadi majira ya machipuo yenye kupambika kwa mamilioni ya maua, na tunaona unakipa kila kiungo mpangilio usiokuwa na mchezo ndani yake, na mizani sawa isiyo na upungufu, na mpangilio huoni ndani yake isipokuwa ufundi wa ajabu, yote hayo ndani ya uzuri wenye kurembeka na urembo wenye kudhihirika hata viumbe vinakua ni vielelezo vilivyochukua umbo kwa ajili ya ufundi utengenezaji vema na uzuri, ukiachilia mbali kuwa unatunuku kila mwenye uhai haki ya kuishi; humrahisishia njia za maisha, na kumwekea vipimo vya uadilifu vya hali ya juu; basi malipo ya wema ni wema mfano wake na malipo ya ovu ni ovu mfano wake, na wakati huohuo unafahamisha nguvu na umilele wake, kwa unayoyateremsha katika adhabu yenye kudamirisha juu ya wachupao mipaka na madhalimu tangu enzi za Adamu (a.s). Kama isivyokuwepo jua bila mchana, basi hekima hiyo ya kiazali na uadilifu huo wa milele haviwezi kuthibiti kuwepo kwake kikamilifu isipokuwa kwa maisha ya Akhera ya kudumu milele, na kwa hiyo haviridhii wala kusamehe kwa hali yoyote juu ya mwisho usio na uadilifu wala hekima wala kuhakikisha haki, huo ndio umauti ambao hauna ufufuo baada yake, na ambapo huwa sawa madhalimu wakaidi pamoja na wenye kudhulumiwa na kudhuriwa! kwa hiyo hapana budi nyuma yake kuwepo uhai mwingine wa kudumu milele ili hekima na uadilifu vikamilishe uhakika wake. Na kwa hivi linatujibu – jibu la kukinaisha – jina la Allah (s.w) (Al-Hakiim) na (Al-Hakamu) na (Al-Adlu) (Al-Adilu) katika majina mazuri kuhusu swali letu juu ya Akhera. Kisha tunamwona kila kiumbe hai hupewa mahitaji yake ambayo hayako katika uwezo wake kuyapata, na yanajibiwa maombi yake yote anayoyaomba – kwa aina ya dua – sawa kwa ulimi wa haja zake za kidharura, au kwa lugha ya maandalizi yake ya kimaumbile, na hukabidhiwa katika wakati munasibu sana na ulio bora kutokea kwenye mkono mrehemevu mkunjufu wa rehema, msikivu wa kila hali na mpole ambaye upole wake ni wenye kuenea, na pia aghalabu ya dua za mwanadamu za kihiari zinajibiwa na hasa dua za wateule kati ya watu, na hasa zaidi dua za manabii (a.s), - ambazo aghalabu yake hujibiwa kwa namna ya kufurutu ada - kujibiwa huko kunatufahamisha kwa yakini kwamba nyuma ya pazia kuna mwenye kusikia kila kitu mwenye kujibu anasikia miguno ya kila mwenye msiba na kuugua kwa kila mwenye ugonjwa na anasikiliza dua ya kila muhitaji na anaona haja duni kabisa ya kiumbe mdogo kabisa na anasikia kuugua kulikojificha sana kwa kiumbe mnyonge sana anamjumuisha kwa upole wake na kumpa msaada hasa na kumridhisha. Maadamu mambo yako hivi dua ya furaha ya kiakhera, kubakia, na kukaa milele – ambayo ni dua bora na enevu zaidi na inagusa viumbe vyote na inafungamana na majina yote mazuri na majina yote matukufu - dua hii anaiomba kiumbe bora zaidi - ambaye ni mwanadamu – na mja mtukufu mno na kipenzi mno mbele ya Allah (s.w) anaijumuisha katika dua zake, huyo ni mtume mtukufu (s.a.w), naye ni imamu wa manabii (a.s) ambao ni majua ya wanadamu na viongozi wao na kila muumini katika uma wake anaitikia amina kwa dua yake hii, bali kila muumini husema amin kwa kumsalia kila siku mara kadhaa kwa uchache, bali wanashirikiana viumbe wote katika dua yake kwa kusema: (Jibu ewe mola wetu mlezi jibu dua yake hakika sisi tunaomba na kunyenyekea kwako kama yeye). Basi dua kama hili lenye kujumuisha kudumu na furaha ya milele kutoka kwa mtume kama huyu kipenzi (s.a.w) na ndani ya masharti haya ambayo hayakataliwi, hapana shaka hilo peke yake ni lenye hoja na sababu tosha ya kupatisha kwa pepo ya kudumu milele na kuzusha Akhera kati ya sababu zisizohesabika wala kudhibitika za kuipatisha. Ukiachilia mbali kwamba kuipatisha ni jambo jepesi kwa uweza wake (s.w) na rahisi kwake kama kuumba majira ya machipuo. Na kama hivi jina la Allah (s.w) (Al-Mujiib), (As-Samii) na (Al-Rahiim) katika majina mazuri yanatujibu juu ya swali letu kuhusu Akhera. Kisha yaliyo katika kubadilika kwa majira mbalimbali miongoni mwa matukio ya umauti na ufufuo juu ya Ardhi yote yanajulisha kwa uwazi – kama kujulisha kwa mchana juu ya jua – kwamba nyuma ya pazia kuna Bwana mlezi anayeendesha Ardhi kubwa kwa upeo wa mpangilio na ukomo wa wepesi – sawa na kuendesha bustani ndogo bali kama kuendesha mti mmoja kwa mpangilio – na anaendesha majira ya machipuo makubwa sawa na wepesi wa kuendesha ua moja na kwa mapambo yake yaliyokuwa kwenye vipimo, na anaandikia kwenye ukurasa wa ardhi aina mia tatu elfu za makundi ya mimea na wanyama ambayo ni mfano wa aina mia tatu elfu za vitabu vinavyoonesha vielelezo na mifano ya ufufuo. Basi mola huyu mweza ambaye anaandika vielelezo hivi vyenye kuingiliana bila ya kubabaika wala kuchanganya na bila ya kusahau wala kukosea na kwa namna nzuri, mpangilio na maana fasaha pamoja na kuwa kwake kama nyavu na kushabihiana, inadhihirisha ndani ya utukufu mkubwa uweza wenye nguvu wenye kurehemu wenye wingi wa hekima, basi yeye (s.w) anaeneza uwepo wote kwa rehema yake na hekima yake hii anampa mwanadamu makamo ya juu na kumdhalilishia ulimwengu mkubwa na anamfanyia kuwa ni makazi na matulio kwake, kisha anamtawaza kuwa khalifa kwenye ardhi na anambebesha amana kubwa ambayo mbingu na ardhi na milima imeikataa kuibeba na anamfadhilisha kuliko viumbe wote, Na kumtukuza kwa maneno yake ya kiungu – mazungumzo yake ya ki Subuhana na kuwa msaidizi wake, ukiachilia mbali kuwa amekata ahadi juu ya nafsi yake na kumwahidi mwanadamu huyu ahadi fulani - katika vitabu vyake vyote vilivyoteremshwa - kwamba atamweka milele kwa furaha ya kudumu na kubakia kiakhera. Hapana shaka kwamba yeye atamfungulia milango ya furaha ya kudumu, na kuleta ufufuo na kiama kwa lazima na hilo ni jepesi kwake kuliko majira yenyewe ya machipuo. Na kwa hivi majina ya Allah (s.w) (Al-Muhyi), (Al-Mumiit), (Al-Hayyu), (Al-Qayyum), (Al-Qadiir) na (Al-Aliim) yanatujibu swali letu kuhusu Akhera. Kwa kweli hakika uweza wa kiungu ambao unahuisha mashina ya miti na majani kwa ujumla katika kila majira ya machipuo na kupatisha vielelezo vya aina mia tatu elfu ya ufufuo katika wanyama na mimea yote, bali unadhihirisha mifano elfu moja ya ufufuo na dalili elfu moja katika majira elfu mbili ya machipuo inapotazamwa kimawazo miaka elfu moja kati ya miaka ambayo waliyoishi watu wote kati ya nabii Muhammad na Musa (a.s) na kulinganishwa pamoja! basi vipi ikanushwe kukufuliwa viwiliwili kwa uweza huu wa hali zote? Kukanusha hilo haiwi upofu usiozidiwa na upofu wowote? Kisha mia moja na ishirini na nne elfu katika binadamu bora nao ni manabii (a.s), wametangaza furaha ya milele na kudumu milele Akhera hali wakiwa wameafikiana na wenye kuegemea katika maelfu ya makamio na ahadi ambazo amezikata Allah (s.w) juu ya nafsi yake. Na wakathibitisha ukweli wao kwa miujiza iliyo kuwa wazi. Na kwamba idadi kubwa mno ya mawalii na waja wema wanathibitisha hakika hiyohiyo kwa ufunuo na maonjo. Hapana budi kuwa hakika hiyo ni dhahiri udhahiri sawa na wa jua katikati ya mchana mwenye kutilia shaka hilo amenyimwa akili: Kwa sababu maamuzi ya bingwa mmoja au wawili katika elimu au kazi kwenye suala lililomo ndani ya ujuzi wake, yanaangusha kuzingatiwa kwa uzito wa maoni na fikira ya wapingaji elfu moja wasiobobea katika elimu au kazi hiyo hata kama ni wabobezi katika elimu nyingine. Na kwamba hukumu ya mashahidi wawili wa kuthibitisha katika suala fulani hupewa uzito dhidi ya maelfu ya wakanushaji au wanaokataa suala hilo. Kama ilivyo katika kuonekana kwa mwezi mwandamo wa Ramadhani katika Yawmu ash-Shakk au kudai kuwepo kwa mashamba ya minazi yanayofanana na makopo ya maziwa ardhini; hii ni kwa sababu mwenye kuthibitisha anashinda kadhia kwa kiasi tu cha kuiashiria au kudhihirisha nazi au kubainisha ilipo. Ama mkanushaji anayekataa uwepo wake hawezi kuthibitisha madai yake isipokuwa atakapo tafuta na kutembea katika pande zote za ulimwengu na kuthibitisha madai yake kwa umakini katika mahali pote. Na kama hivi ambaye anaelezea kuhusu pepo na nyumba ya furaha na kuishi milele hakika anathibitisha hilo na kushinda kadhia kwa kiasi tu cha kudhihirisha kwake athari mojawapo katika athari za pepo, au alama moja katika alama zake, au kivuli katika vivuli vyake kwa kufunua; wakati ambapo anayekanusha uwepo wake hawezi kupata uwanja wa kukanusha kwake – vyovyote atakavyojitahidi - isipokuwa atakaposhuhudia na kuwashuhudisha wengine limwengu zote na zama zote kuanzia azali hadi milele, na akadhihirisha kutokuwepo kwake na akathibitisha hilo!! Basi kwa ajili ya hekima hii wanazuoni wahakiki wameridhia kanuni ya msingi ambayo ni: (Haiwezekani kuthibitisha ukanusho usio ainishwa mahala pake maalum - kama hakika za kiimani za jumla kwa ulimwengu wote - kama jambo lenyewe sio muhali). Kwa msingi wa hakika hii ya kukinaisha kukanusha kwa maelfu ya wanafalsafa na kupinga kwao hakuwezi kuleta utata wowote wala wasiwasi mbele ya mpasha habari wa kweli katika maswala kama haya ya kiimani. Uzuzu uliyoje kwa ambaye anajichafua kwa utata – vyovyote iwavyo - katika nguzo za imani kwa kiasi tu cha kukanusha wachache kati ya wanafalsafa wa kiyakinifu ambao akili zao zimeteremka katika macho yao hawaoni isipokuwa maada bali nyoyo zao zimekufa hawahisi vitu vya kimaanawy, wakati ambapo wameafikiana juu ya nguzo hizo mia moja na ishirini elfu katika wenye kuthibitisha wenye ubobezi miongoni mwa manabii wa kweli (a.s), na katika wasiohesabika katika wenye kuthibitisha na wenye kubobea katika watu wa hakika mawalii na wanazuoni watu wa tahakiki. Na kadhalika sisi tunashuhudia, sawa sawa katika nafsi zetu au katika vinavyotuzunguka rehema enevu na hekima jumuishi na uangalizi wa kudumu wenye kutawanya nuru yake kama mchana, na tunaona vilevile athari kubwa za kiungu na nuru za uadilifu zenye busara, na midhihirisho ya taratibu tukufu azizi, bali tunaona (Hekima) inaupa mti hekima kwa idadi ya maua yake na matunda yake, na tunaona (Rehema) inasimamisha kwa kila mwanadamu hisani na vipawa kwa idadi ya milango yake ya fahamu na nguvu zake na viungo vyake. Na tunauona (Uadilifu) wenye enzi kwa adhabu yake kali unaangamiza waasi mithili ya kaumu za Musa, Nuhu, Hud, Saleh na kaumu ya Adi, Thamudi na Firauni, nao ni wenye uangalizi vilevile unahifadhi haki za kiumbe mdogo na dhaifu mno. Aya tukufu ifuatayo inabainisha kwa ufupi wa kimuujiza ukuu wa ulezi huo wa kiungu mtukufu na haiba yake ya hali zote: وَمِنْ آيَاتِهِ أَن تَقُومَ السَّمَاء وَالْأَرْضُ بِأَمْرِهِ ثُمَّ إِذَا دَعَاكُمْ دَعْوَةً مِّنَ الْأَرْضِ إِذَا أَنتُمْ تَخْرُجُونَ Ambapo inabainisha kwamba mbingu na Ardhi vinatekeleza amri za kiungu kama wanajeshi waliopiga kambi na waliolala katika kambi mbili. Kama wanavyoharakisha katika kuchukua nafasi zao na kuchukua silaha zao kwa wito kutoka kwa kiongozi na kwa mpulizo wa tarumbeta, kadhalika mbingu na Ardhi ni kama kambi mbili kwa vile maiti huitwa katika kambi mbili hizo kwa baragumu la Israfil (a.s), tahamaki wanatoka makaburini kwa haraka wakiwa wamevaa mavazi ya mwili. Bali tunaona taadhima hii na utiifu katika kila majira ya machipuo, ambapo wanakusanywa askari waliopo katika kambi ya Ardhi na kutawanywa kwa mpulizo wa tarumbeta la malaika wa radi. Kwa msingi wa hakika zilizopita, hapana budi kuwa hizo rehema, hekima, uangalizi, uadilifu na ufalme wa milele malengo na shabaha zake zitathibiti katika maisha ya Akhera, Yaani yahitajia ufufuo kwa dharura, kama (Neno la kumi) lilivyothibitisha hilo; kwani hapana shaka katika ujio wa Akhera, bali kutokuja kwake ni muhali kwani kukosekana kwake kuna maana ya kuwa: Kubadilika kwa (Rehema) ambayo imo katika ukomo wa uzuri kuwa ni ukatili katika ukomo wa ubaya na ina maana akuwa: Kugeuka kwa ukamilifu wa (Hekima) kuwa ni kasoro ya mchezo wenye hali ya upungufu na upeo wa israfu, na ina maana ya mapinduzi ya (Uangalizi) ambao uko katika ukomo wa uzuri na upole kuwa dharau katika ukomo wa ubaya na uchungu na ina maana: Kughairisha (Uadilifu) ambao uko katika ukomo wa insafu na haki kwenda katika giza katika ukatili mkubwa na ubatili, ongezea kwamba kutokuja kwa Akhera kuna maana vilevile ya kuanguka kwa haiba ya ufalme wa milele wenye enzi na kubomoka utukufu na nguvu yake, na ina maana ya kutuhumu ukamilifu wa ulezi wa kiungu kwa kushindwa na upungufu. Na vyote hivi ni batili na muhali akili ya mwanadamu hailikubali hili vyovyote iwavyo, nalo ni jambo lisilokuwa na liko nje ya eneo la uwezekano; kwa kuwa kila mwenye utambuzi anafahamu kwamba Allah (s.w) amemuumba mwanadamu huyu katika umbo bora kabisa na kumlea malezi mazuri sana na kampatia zana na viungo – kama akili na moyo - hali anayotazamia kwayo furaha ya milele na kumpeleka upande huo, na inatambulika pia kiasi cha udhalimu na ukatili ikiwa hatima ya mwanadamu huyu aliyetukuzwa kuwa katika kukosekana kwa milele! Na inafahamika pia kiasi cha kukosekana hekima katika kutofufuliwa ambako kunafanya zana na nguvu zote za kimaumbile - ambazo zina maelfu ya masilahi na faida – bila mafanikio na bila ya thamani - wakati ambapo Allah (s.w) ameweka mamia ya hekima na faida katika ubongo wake tu! Na inafahamika vilevile kiasi cha kushindwa kwa dhahiri na ujinga timamu wenye kukinzana kwa jumla na adhama ya ufalme huo na ukamilifu wa malezi ya kiungu katika kutotimiza maelfu ya makamio na ahadi? Ametakasika Allah (s.w) na hayo kutakasika kukubwa. Pima kwa hili vyote (Uangalizi) na (Uadilifu). Na kama hivi yanatujibu majina: ya (Ar-Rahman) (Al-Hakim) (Al-Adlu) (Al-Kariim) na (Al-Hakim) katika majina mazuri kwa hakika hiyo iliyoelezwa kuhusu swali letu tulilouliza juu ya Akhera na yanatuthibitishia uthibitisho usio na utata bali ni wazi bayana kama uwazi wa jua. Kisha tunaona (uhifadhi) mkubwa wenye kuzunguka dhahiri wenye kuonekana unahukumu juu ya kila kitu kilichokuwa hai, na kutawalia kila kitu, unahifadhi sura zake nyingi, unasajili kazi za majukumu yake ya kimaumbile, unasajili tasbihati zake – kwa ulimi wa hali – mbele ya majina mazuri, unazisajili katika mbao za kimfano, katika mbegu zake na kokwa zake ndogo, na katika nguvu yake ya kuhifadhi nazo ni vielelezo vilivyopewa maumbo madogo ya Lauhul Mahfudh - na hasa katika kumbukumbu ya mwanadamu ambayo ni maktaba kubwa iliyopewa umbo dogo mno iliyowekwa kwenye ubongo wake, unavisajili kwenye vioo vingine na viakisi vya kimaada na kimaanawy. Na hayaji majira ya machipuo - ua hilo lililopewa umbo la kudura ya kiungu – hadi uhifadhi unatudhihirishia maandishi hayo ya kimaanawy yakiwa dhihiri yenye kushuhudiwa yakiwa yamechukua umbo. Na unahudhurisha katika ua hilo kubwa hakika ya ufufuo ambayo iliyomo ndani ya aya tukufu: (وَإِذَا الصُّحُفُ نُشِرَتْ) na kuitangaza kwa ndimi za mamilioni ya mamilioni ya mifano na dalili, na kutusisitizia kwa yakini kwamba vitu vyote - na hasa walio hai – havikuumbwa ili viishie katika kutoweka, wala kuporomoka katika kutokuwepo, wala kufutwa kuwa sio chochote - na hasa mwanadamu - bali vimeumbwa ili kuendelea kupanda kwao katika kubakia – na ili kuingia kwa kutakasa nafsi zao katika ulimwengu wa uhai wa kudumu milele, na kwa ajili ya kuingia kwa maandalizi ya kimaumbile katika jukumu la milele linalowangojea katika makazi ya milele. Naam, hakika kila mti na shina na kila punje na kokwa katika mimea isiyo na mipaka ambayo ilikufa katika kiama cha mapukutiko, haingii ufufuo wa machipuo ila inasoma aya tukufu: وَإِذَا الصُّحُفُ نُشِرَتْ kwa ulimi wake mahususi na kutafsiri maana katika maana zake, na hii kwa kutenda kila sehemu kati ya sehemu zake mfano wa nyadhifa za kimaumbile ambazo imezitenda katika miaka iliyopita na kubainisha wakati huohuo – adhama ya uhifadhi katika umbali wake mkunjufu zaidi kama ilivyo katika aya tukufu: هُوَ الْأَوَّلُ وَالْآخِرُ وَالظَّاهِرُ وَالْبَاطِنُ na inatuelekeza katika hakika nne za wazi katika kila kitu na kusimamisha hoja yenye nguvu juu ya ulazima wa ufufuo kama ulazima wa kuja kwa majira ya machipuo na wepesi wake. Naam, hakika nuru za majina haya mazuri manne inaelekea na kufanya kazi kuanzia sehemu ndogo zaidi hadi kwenye sehemu kubwa zaidi hebu tufafanue hili kwa mifano: Mbegu ambayo ndio asili ya mti inabainisha adhama ya uhifadhi kwa kupokea kwake nuru ya jina la Allah (Al-Awwal) na hiyo ni kwa ajili ya mpango madhubuti ulio kamilika wa mti uliomo ndani ya hiyo mbegu Na zana za kiufundi inazozikusanya za kuufanaye uwepo na kukuwa kwake ukiwa kamili bila upungufu na yaliyomo katika masharti ya kuundika kwa mti pamoja na kuwa hiyo mbegu ni pakiti ndogo sana. Na tunda vilevile linashuhudia ushahidi wa kweli juu ya uhifadhi huokwa kupokea kwake nuru za jina la (Al-Akhir) na hiyo ni kwa yale inayobeba katika faharisi za kazi zote za kimaumbile za mti huo na n nyaraka za matendo yake inazozikusanya na kanuni zilizomo za maisha yake ya pili hali ya kujua kwamba hilo ni sanduku dogo sana. Ama dhahiri ya mti iliyopewa umbo inadhihirisha adhama ya uweza na ukamilifu wa hekima na uzuri wa rehema ndani ya uhifadhi wa hali zote na unaidhihirisha kwa ajili ya kuonekana waziwazi ikishuhudiwa kwa kupokea kwake nuru za jina la Allah (Adh-dhahir) na hii kwa mapambo yake yenye kujitokeza yakirembeshwa kwa nakshi za kupendeza aina kwa aina na nishani zilizopangika kana kwamba ni nguo za Mahuri al-aini zenye kutiwa rangi namna sabini. Ama zana za ndani za mti huo ambao umekuwa kama kioo chenye kuakisi nuru zaa jina la Allah (s.w) (Al-Batin) nazo pia zinathibitisha – uthibitisho wenye kung’ara kama jua – ukamilifu wa uweza na uadilifu na uzuri wa Rehema na Hekima kwa kuwa huo mti ni kiwanda kamili chenye mpangilio wenye kufurutu ada bali ni maabara kubwa ya kikemia bali ni ghala la chakula na riziki haliachi tawi wala tunda wala jani isipokua huipa chakula inachokihitajia kama vyote mbegu na tunda na nje ya mti na ndani yake vinavyodhihirisha midhihirisho ya majina ya Allah (s.w) yaliyo mazuri (Al-Awwal, Al-Akhir, Adh-Dhaahir na Al-Baatin) basi tufe la Ardhi pia linayadhihirisha na kuyabainisha wazi kwamba Al-Hafiidh (Mwenye kuhifadhi vyema kila kitu) mwenye utukufu na ukarimu hakika anafanya kwa uweza na uadilifu na hekima na rehema kwa hali zote kwani hilo tufe la Ardhi kama mti kwa upande wa kubadilika kwa majira ya mwaka basi kokwa zote na punje ambazo zimehifadhiwa kwenye majira ya mapukutiko – kwa kudhihiri kwa jina lake Allah (s.w) (Al-Awwal) hali ya kuwa ni amana kwa Uhifadhi inatuma kiasi kisichohesabika katika mashina na miundi ya miti na matawi na kuipeleka kaika pande mbali mbali na inafungua kiasi kisichohesabika cha maua yenye kupendeza na matunda mazuri, huivisha ardhi mtandio wa kufurahisha wa majira machipuo. Kwa sababu kila moja kati yake ina madaftari madogo ambayo ndani yake kumeandikwa amri za kiungu mola mlezi Na inasitiri kurasa ndogo ndogo yameandikwa humo matendo yaliyotendwa katika mwaka uliopita bali mbegu na kokwa hizo mambo yote yanayorejea katika muundo wa mti mkubwa wa Ardhi. Ama mwisho wa kila mwaka wa mti wa Ardhi ni yale yanayo yaweka katika pakiti ndogondogo mno katika kazi zote ambazo mti umezitenda ndani majira ya mapukutiko na tasbihati zote na Dhikiri zote za kimaumbile ambazo imezitimiza kwa upande wa majina mazuri na yote yanayoyumkinika kuyaeneza katika ufufuo wa majira ya machipuo yajayo miongoni mwa kurasa za matendo na zote hizi hukabidhiwa katika mkono wa Hekima wa muhifadhi wa kila kitu vema mtukufu kwa hivi ikiwa inasoma jina la Allah (s.w) (Al-Akhir) kwa ndimi zisizo na ukomo juu ya masikio ya viumbe na mifano yake. Ama nje ya mti huu ni: Maua hayo ya jumla aina mbali mbali ambayo yanabainisha juu ya aina mia tatu elfu ya mifano ya ufufuo na lama zake nazo ni ni meza zile zilizotandikwa za mwingi wa Rehema Mwenye kurehemu na Mtoa riziki aliye Karimu nayo nizile dhifa zilizofunuliwa kwa ajili ya wote wenye uhai basi kila kilichomo nje ya nti huo kinataja na kusoma jina la Allah (s.w) (Al-Dhaahir) kwa ndimi za matunda yake na maua yake na ladha zake zikidhihirisha hakika ya وَإِذَا الصُّحُفُ نُشِرَتْ iking’ra kama jua katikati ya mchana. Ama ndani ya mti huu ni maabara na kiwanda kinachakata kiasi kisichohesabika wala kudhibitika katika mashine yaliyopangika na maabara madhubuti hata kwamba inaandaa tani moja ya vyakula na kuivisha kutoka na dirhamu moja ya maada na kuwafikishia wenye njaa. Na inatekeleza kazi katika ukomo wa umakini kiasi kisichotoa nafasi ya sadfa kucheza katika hilo basi uso wandani wa Ardhi unataja jina la Allah (s.w) (Al-Matin) bali inalithibitisha na ulitangaza kwa aina mia moja elfu ya mitindo na picha kama sehemu ya malaika ambao wanafanya tasbihati kwa ndimi mia moja elfu wanavyolitangaza jina hilo. Kama ilivyo Ardhi kwa upande wa uhai wake wa kila mwaka kama mti imebainisha (Uhifadhi) uliopo katika majina hayo mazuri manne kwa ufasaha na kuyafanya kuwa ni ufunguo wa mlango wa ufufuo hiyo nayo kama mti uliopangika sana kwa upande wa maisha ya enzi na dahari kwani hutuma matunda yake – kwa kitambo cha enzi na dahari – kwenda kwenye soko la Akhera. Kama hivyo Ardhi yote inakuwa ni kioo kipana sana kwa ajili ya midhihirisho ya majina hayo manne na inafungua njia apana sana kwenda Akhera kiasi akili zetu zitabaki na lugha zetu ni pungufu na zenye kushindwa kuzungukia hilo kwa kulifahamu kwa hiyo tunatosheka na yafuatayo wala hatuzidishi: Kurabu za saa ambazo zinahesabu sekunde na dakika na saa na siku zinashabihiana baina yake moja inajulisha nyingine na kuikumbusha basi anayefuatilia mwendo wa kurabu ya sekunde analazimika kusadiki mwendo wa meno mengine. Hali kadhalika dunia ni kama saa kubwa ya Muumba mbingu na Ardhi ambapo siku zinahesabu sekunde za saa hii kubwa zinafanana na miaka ambayo inahesabu dakika zake na enzi ambazo zinadhihirisha saa zake na karne nyingi ambazo zinajulisha masiku yake basi pamoja nakufanana kwake nyakati hizi kila mmoja inajulisha juu ya mwingine na kuuthibitisha Na kwa pembe hii Ardhi tunaiona inaelezea kwa lama zisizo na mpaka juu ya ujio wa majira ya machipuo ya kudumu milele na asubuhi ya milele baada ya majira ya baridi ya dunia yenye kutoweka yenye giza. Inaelezea hilo kwa ulazima wa kuja kwa asubuhi kwa usiku huu na kwa kukata shauri la ujio wa majira ya machipuo kwa majira haya ya baridi. Na kwa hakika hii jina (Al-Hafiidh) linatujibu pamoja na majina manne mazuri (Al-Awwal, Al-Akhir, Adh-Dhaahir na Al-Baatin) juu ya swali letu ambalo tumeuliza kuhusu ufufuo midhali tunaona kwa macho yetu na kufahamu kwa akili zetu kwamba mwanadamu: Ni hitimisho la matunda ya mti wa ulimwengu na ndiye jumuisho la kila kitu katika sifa zote zilizomo katika ulimwengu. Na yeye ndiye mbegu yake ya asili kwa upande wa hakika ya Muhammad (s.a.w). Na yeye ni aya kubwa ya ulimwengu ya Qur’an ya ulimwengu. Bali ni aya yenye kubeba madhihirisho ya jina Kuu katika hilo Qur’an ya kiulimwengu kama Ayat Al-kursy ndani ya Qur’an tukufu. Na yeye ni mgeni mtukufu mno katika kasiri ya ulimwengu. Naye ni mfanya kazi hodari zaidi aliyepewa idhini kusarifu katika wakazi wa kasiri hiyo. Na yeye ndiye aliyepewa mari aliye kalifishwa kulima shamba la Ardhi na mwangalizi masuuli juu ya bidhaa zake na matumizi yake kwa vipawa alivyotunukiwa katika mamia ya elimu na maelfu ya sifa. Na yeye ni khalifa wa Ardhi na mkaguzi mtafiti katika Milki ya Ardhi na aliyetumwa kutoka kwa Mfalme wa azali na milele na mtendaji chini ya uangalizi wake. Naye ndiye mwenye kusarifu katika mambo ya Ardhi pamoja na kusajiliwa kikamilifu kazi zake madogo na makubwa yake. Naye ni mja mjumuishi mwenye kukalifishwa kwa ibada pana yenye kukusanya na mchukuzi wa amana kubwa ambayo mbingu na Ardhi na milima vilikataa kuibeba mbele yake zikapachana njia mbili: Mojawapo ni ya wabaya na nyingine ni ya wema. Na yeye ndiye ambaye anakisi kama kioo midhihirisho yote ya majina mazuri na kwake linadhihiri jina Kuu la Allah (s.w). Na yeye ndiye msemeshwa aliyekusudiwa kwa mazungumzo ya kisubuhana na mwenye kufahamu sana maneno ya mola mlezi. Naye ndiye mhitaji na mshindwe zaidi fakiri bila mipaka pamoja na kuwa ana maadui na vya kumpa udhia bila idadi na makusudio na maumivu bila mpaka naye ni tajiri mno wa kuandaliwa kati ya wenye uhai. Naye ni mwenye utambuzi mkubwa na hisia kali ya maumivu – ndani ya ladha ya uhai – ambapo ladha zake zinachanganyika na maumivu yenye kutibua. Na yeye ndiye mwenye shauku kubwa ya kubakia na mwenye haja sana ya kuishi milele bali ndiye mwenye kustahiki zaidi kwa hilo. Na yeye ndiye anayeomba kwa unyenyekevu ili abakie milele kwa dua zisizo na mipaka angepewa starehe zote zilizomo duniani zisingekonga kiu chake cha kudumu milele. Na huyu ndiye ambaye anampenda aliyemneemesha kwa kiwango cha kumwabudu na kumpendezesha kwa wengine naye ni mwenye kupendwa vilevile. Na yeye ni muujiza mkuu katika miujiza yauweza wa Allah (s.w) mwenye kutegemewa kwa haja zote bali yeye ni ajabu ya uumbaji kwa vile ulimwengu mkubwa ulivyoingia ndani yake na kwa kuwa viungo vyake vyote vinashuhudia kwamba yeye ni kiumbe aliyeimbwa ili kuendelea mbele katika kudumu milele. Mwanadamu huyu ambaye anafungamana na mfano wa hakika hizi ishirini za kiujumla kwa jina la Allah (s.w), (Allah) mwenye mafungamano madhubuti na jina la Allah (s.w) (Al-Hafiidh) ambaye hakimpiti kitu mbinguni na Ardhini anaona haja duni kabisa ya mdogo sana aliye hai na anasikia mnada wa haja yake anamsaidia waandishi wake watukufu wanasajili matendo yote ya huyu mwanadamu yenye kuambatana na viumbe Mwanadamu huyu – kwa hukumu za hakika hizi ishirini – hapana budi kuwepo kwa kukusanywa na kutawanywa - na hapana budi kwamba atalipwa – kwa jina la (Al-Haqq) – kwa huduma na matendo aliyotanguliza na atapata jaza ya kasoro aliyofanya hakuna utata kwamba atapelekwa katika mahesabu na kuulizwa kuhusu matendo aliyosajili - kwa jina la (Al-Hafiidh) madogo na makubwa na hakuna shaka kwamba utafunguliwa mbele yake mlango wa furaha ya milele na dhifa ya kudumu milele au milango ya magereza ya kutisha na mateso ya kudumu na kwamba haiyumkiniki kwamba asihesabiwe na kujificha asionekane na mdhibiti amewaongoza wengi wa viumbe wa ulimwengu huu na kuingilia katika mambo yao na haiyumkiniki kuwa asizindushwe kutoka katika usingizi wake! Kwa sababu haingii akilini katu kusikilizwa dua hafifu kuliko king’ong’o cha mbu na kukusaidiwa kiuhakika kwa kupewa mahitaji ya muhimu katika maisha kisha zisisikike dua zenye nguvu ya kutetemesha Arshi na tandiko na ambazo zinatamka kutoka katika hakika zile ishirini na kuomba kubakia na kudumu milele. Wala haingii akilini katu - bali ni nje ya yamkini – kwa haki hizo nyingi kupotezwa kabisa bali haiyumkiniki kwa hekima isiyo na mchezo katu japo kwa kiasi cha ubawa wa nzi kwa ushahidi wa kupangiliwa kwake na kuwekwa vema – kufanya mchezo kabisa na maandalizi ya mwanadamu yenye kufungamana na hakika hizo na kuchezea matarajio yake yote na matakwa yake yenye kuendelea hadi katika kudumu milele na kuchezea mafungamano yote hayo na hakika za viumbe mbalimbali ambao wanakuza maandalizi na matakwa hayo kwa sababu dhana hii ni dhuluma mbaya sana viumbe wote waliopo wanaikataa kwa kusema: Hakika hilo ni muhali ndani ya muhali kwa pande mia moja na ni jambo lisilowezekana kabisa kwa namna elfu nyingi. Bali vitu vyote vilivyopo vyenye kushuhudia majina mazuri: Al-Haqq, Al-Hafiidh, Al-Hakiim, Al-Jamiil na Ar-Rahiim vinaikataa. Namna hii majina ya mazuri yanatujibu: Al-Haqq, Al-Hafiidh, Al-Jamiil na Ar-Rahiim” swali letu kuhusu Akhera majina hayo yazungumza na sisi kwa kusema: Hakika ya ufufuo ni haki hauna shaka nayo ni hakika yenye nguvu haina mabishano mithili ya kuwa sisi ni haki na mithili itushuhudiavyo hakika ya kuthibiti kwa vilivyopo. Suala hili lau lisingekuwa wazi kuliko jua ningeongeza kubainisha lakini nimefupisha kwa kutosheka na mifano iliyotajwa na kwa kupimia yaliyomo kwenye vifungu vilivyotangulia hakika kila jina katika majina mazuri mia moja bali elfu yenye kuelekea katika ulimwengu yanathibitisha linathibitisha mwenye majina hayo (s.w) kwa dhahiri kwa midhihirisho yake na kwa vioo vyake ambavyo ni viumbe vilivyomo kama yanavyodhihirisha ufufuo na maisha ya Akhera na kuithibitisha kwa namna ya kukinaisha. Kama anavyotujibu mola wetu (s.w) jibu takatifu na kukinaisha kwa amri zake zote katika vitabu vyake vyote alivyoviteremsha na kwa majina yake yote aliyoiita nafsi yake swali letu ambalo tumemuuliza kuhusu Akhera, kadhalika Allah (s.w) anatujibu kwa ndimi za malaika wake na kutujulisha Akhera kwa mtindo mwingine ambapo malaika wanasema: Kuna alama na dalili zisizo na mpaka juu ya kuwepo kwetu na ulimwengu wa kiruhani na imepita mijadala na mazungumzo na kutambuana baina yenu na sisi na baina ya maruhani tangu zama za Adam (a.s) nayo ni matukio ya yakini yenye kupokelewa kwa tawaturi hayakubali shaka na hakika tulieleza na daima tunaeleza tunayoyaona wakati wa matembezi yetu katika nyumba za Akhera na kumbi zake kwenda kwa manabii wenu nyakati za kukutana na kwetu pamoja nao: Hakika tunakubashirieni bishara isiyo na shaka kwamba hizi kumbi za kudumu nyuma yake kuna kasri za kudumu milele na nyumba zenye kuandaliwa kwa yakini zimeandaliwa kwa ajili ya mapokezi ya wageni watukufu wenye kutukuzwa na kutayarishwa kwa ujio wao. Kwa hivi malaika wanajibu swali letu kuhusu Akhera Kisha hakika Muumba wetu mkarimu ametuteulia mwalimu mkuu na Ustadhi mkamilifu mno ruwaza ya kweli sana na kiongozi mnyofu sana. Naye ni Mwarabu wa tumbo la Bani Hashim (a.s) na hakika amemtuma kuwa Mwisho wa mitume watukufu (a.s) – kwa hiyo basi ni juu yetu – na kabla ya kila kitu - tumuulize ustadhi wetu yale tuliyomuuliza Muumba wetu Mwenye ushindi na utukufu kuhusu Akhera huenda tukakamilika katika maarifa yetu na kupanda kutoka katika ngazi ya Elimu ya yakini hadi Dhati ya yakini na haki ya yakini kwa sababu Nabii huyu kipenzi Mkweli mwenye kusadikishwa kutoka kwa Muumba mjuzi wa kila kitu kwa maelfu ya miujiza kama ambavyo ni muujiza wa Qur’an tukufu akathibitisha kwa ulimwengu wote kwamba hicho ni kitabu cha walimwengu batili haikifikii kutoke mbele yake wala nyuma yake Qur’an tukufu pia imekuwa ni muujiza katika miujiza yake (s.a.w) na dalili juu yakuwa yeye ni mkweli mwenye kusadikishwa na kwamba yeye ni mjumbe wa Mlezi wa walimwengu. Basi miujiza yote hiyo miwili - mmojawapo ni ulimi wa ulimwengu wa kushuhudia pamoja nao sadikisho la Manabii wote (a.s) na mawalii na mwingine ni ulimi wa ulimwengu wa ghaibu wenye kujumuisha vitabu vyote vya mbinguni na hakika zote za ulimwengu - imesimamisha hoja juu ya kukusanywa na kutawanywa (ufufuo) ikiwa na nguvu wazi kama jua na mchana. Kwa uhai wote wa muujiza wa kwanza na maelfu ya aya za muujiza wa pili. Kweli (Suala la ufufuo na Akhera) ni katika maswala ambayo ni juu ya uwezo na mipaka ya akili ya mwanadamu wala hayafahamiki ila kwa mafunzo ya hawa Maustadhi wawili wenye muujiza (Qur’an karimu na mtume mahabubu (s.a.w)) na miongozo yao. Ama kwa nini manabii waliotangulia hawakuweka wazi kwa nyumati zao suala la ufufuo kama ilivyo wazi katika Qur’an karimu? Ni kwa kuwa enzi zao zilikuwa enzi za uchanga wa kibinadamu na ujima wa utu na ufafanuzi unakuwa mfupi katika masomo ya msingi kama ijulikanavyo. Na teuzi ya kauli: Maadamu mengi ya majina mazuri yanahitajia na yanajulisha juu ya hilo, basi hapana budi kuwa hoja na dalili zenye kujulisha majina mazuri kwa nafasi yake yenyewe ni dalili za kuthibitisha Akhera na kusimama kwake. Na madhali malaika wanapasha habari yale wanayoyashuhudia katika nyumba za Akhera na ulimwengu wa kudumu milele, hapana budi kuwa dalili zenye kushuhudia juu ya kuwepo kwa malaika na ulimwengu wa kiruhani na ibada zao ni dalili za kuthibitisha juu ya Ulimwengu mwingine. Maadamu muhimu zaidi aliyotangaza Muhammad (s.a.w) wakati wa uhai wake twahara wenye baraka na msingi wa aliyolingania - baada ya Tawhiid – nayo ni Akhera, basi hapana budi kwamba hoja na miujiza yote inayojulisha juu ya utume wake na ukweli wake (s.a.w) zenyewe kwa nafasi zao ni shahidi juu ya hakika ya ujio wa Akhera. Na maadamu robo ya Qur’an inachambua juu ya Ufufuo na Akhera na kusimamisha dalili juu yake kwa maelfu ya aya zake na inapasha habari kuhusu hilo, hapana budi kwamba shahidi, hoja, dalili na vithibitisho vyenye kujulisha vyote juu ya kuwa Qur’an ni , kwa nafasi zake ni shahidi juu ya kuthibiti kwa Akhera. Na kama hivi zingatieni katika nguzo hii kuu ya imani ili mutathmini kiasi cha kukinaisha (Kuamini Akhera) na kiasi cha uthabiti na uimara wake.
Tulitaka katika (Suala la saba) kuulizia ufafanuzi wa suala la ufufuo katika ngazi nyingi, isipokuwa jibu la Muumba wetu kwa majina yake mazuri lilikuwa lenye kukidhi na kutosheleza sana limeleta yakini kabisa na kukinaisha kikamilifu likatutosheleza kiasi cha kutohitajia maelezo mengine yoyote. Huko tulichukua uthibitisho huo tu. Ama katika Suala hili tutafupisha moja kati ya mamia ya matunda faida na tija zinazopatikana kwa (Kuamini Akhera). Kati yake ni ile inayohusu furaha ya mwanadamu Akhera na nyingine inahusu furaha yake duniani. Ama ambayo furaha yake inahusu Akhera hakuna ufafanuzi mwingine baada ya ufafanuzi wa Qur’an, na ikarejewe hiyo Qur’an, ama inayohusu (Furaha ya dunia), Risale-i Nur inaifafanua, na hapa tutabainisha - kwa ufupi – baadhi ya natija tu baina ya mamia kati ya natija inayopatikana kwa (Kuamini Akhera) ili kumpa furaha mwanadamu katika maisha yake ya kibinafsi na kijamii. Tunda la kwanza Kama alivyo mwanadamu - tofauti na mnyama – ni mwenye mahusiano na nyumba yake, kadhalika ana mafungamano madhubuti na dunia. Na kama alivyo mwenye mafungamano na jamaa zake kwa mafungamano mbalimbali vilevile anayo nasaba ya kimaumbile na wanadamu wote. Na kama alivyo kwamba anapenda kubakia katika dunia ya kutoweka hakika anapenda sana kubakia katika nyumba yenye kubaki milele. Na kama anavyojitahidi daima kwa ajili ya usalama wa tumbo lake katika chakula analazimika kwa maumbile yake – bali anajitahidi – kwa ajili ya usalama wa vyakula vya akili yake, moyo, roho yake na utu wake na kuvila katika meza pana upana wa dunia, bali yenye kuendelea hadi milele, kwa vile alivyo navyo miongoni mwa matarajio na mahitaji ambayo hayashibishwi ila na furaha ya milele. Niliyaambia mawazo yangu ya kufikirika enzi za utoto wangu: Unafadhilisha lipi kati ya mambo mawili? Kuishi umri wa furaha utakaodumu miaka elfu pamoja na ufalme wa dunia na utukufu wake kwa sharti kwamba mwisho wake uwe kutoweka kabisa, au kuishi katika uwepo wenye kubaki milele pamoja na maisha ya kawaida yenye taabu? Nikayaona yanataka (Maisha) ya pili na kukereka na ya kwanza kwa kusema: Hakika sipendi kutoweka bali kubakia japokuwa katika jahanamu!. Maadam ladha zote za duniani hazishibishi mawazo ya kitaswira ambayo ni moja ya watumishi wa ainisho la mwanadamu, hapana budi kwamba hakika ya ainisho la mwanadamu lenye kujumuisha sana limefungamana kimaumbile na kubakia milele. Kwa hiyo ni kiasi gani inakuwa (Kuamini na Akhera) ni hazina kubwa yenye kutosheleza na kukidhi kwa mwanadamu huyu ambaye ana mafungamano madhubuti na matakwa na matarajio haya yasiyoisha, naye hamiliki chochote isipokuwa sehemu ndogo ya Ikhtiyari al-Juz’iy (Sehemu ndogo sana ya hiari), na anagaagaa katika ufukara wa hali zote! na kiasi gani imani hii inakuwa ni mhimili wa furaha inayotafutwa na ladha inayotakiwa? na kiasi gani inakuwa ya kurejewa, mahali pa kupata msaada na maliwazo kwake mbele ya majonzi ya kidunia yasiyodhibitika? lau mtu huyu angejitolea uhai wake wote ili apate kufanikiwa matunda na faida hizi ingekuwa bado ni kitu kidogo sana! Tunda la pili Linaekea katika maisha binafsi ya mwanadamu Hakika kinachomtia wasiwasi mwanadamu daima na kutibua maisha yake ni kufikiria kwake daima juu ya hatima yake, na namna atakavyoingia kaburini, kama ilivyomalizikia hatima ya wapendwa wake na jamaa zake. Basi dhana ya huyu mwanadamu masikini –ambaye anajitolea mhanga maisha yake kwa ajili ya rafiki mpenzi – na kujenga kwake picha kwamba maelfu bali mamilioni kwa mamilioni katika ndugu zake wanadamu wanaishia katika kutoweka nako ni umauti - huo utengano wa milele ambao hakuna kukutana baada yake - picha ya mawazoni ya namna hii itamuonjesha maumivu makali yenye kutabiri maumivu ya jahanamu. Wakati mwanadamu huyu akisumbuka na adhabu yenye kuumiza itokanayo na mawazo hayo, (Kuamini Akhera) kunakuja kufungua busara yake na kuondoa kifuniko kwenye macho yake kwa kumwambia: (Tazama) basi anaangalia kwa nuru ya imani, tahamaki anavuna ladha ya kina inayotabiri ladha ya pepo, kwa anayoshuhudia katika kuokoka kwa wapenzi wake na wote kukomboka na kifo cha moja kwa moja na kutoweka na kuoza na kupotea na kutokana na kubakia kwao milele katika ulimwengu wa nuru ya milele wakingojea ujio wake kwao. Tunafupisha kwa haya ambapo Risale-i Nur imeelezea natija hii pamoja na hoja zake. Tunda la tatu Lenye kuelekea katika mahusiano ya mwanadamu Hakika makamo ya juu ya mwanadamu na kuwazidi kwake viumbe hai wengine na kupambanuka nao hakika ni kwa sababu ya sifa zake na maandalizi yake ya kimaumbile yenye kujumuisha, uja wake wa jumla, na kwa sababu ya upana wa maduara ya uwepo wake, kwa hiyo mwanadamu ambaye amejihusisha na muda wa sasa tu na kujivua na muda uliopita, wenye kukatwa mawasiliano na mustakabali - na hali ya kuwa zama hizo hazipo ni mfu na zenye giza kwa mujibu wa matazamo wake - mwanadamu huyu anachuma tabia za murua, mapenzi na udugu wa kibinadamu kwa msingi wa muda wake wa sasa ulio finyu, na zinakuwa maalumu kwake kwa mujibu wa vipimo vyake vidogo, huelekeza mapenzi kwa baba yake, ndugu yake, mke wake au mama yake na huwahudumia kwa mujibu wa vipimo hivyo finyu kana kwamba yeye hawajui tangu hapo kabla na hatowaona huko mustakabali, hatapanda abadani katika ngazi ya ukweli katika utambuzi wa fadhila, wala nafasi ya ikhlasi katika urafiki, wala katika ngazi ya mapenzi yaliyotakasika na vyenye kutibua mapenzi, wala heshima iliyoepukana na lengo (binafsi); kwa sababu upana wa tabia hizo na makamilifu yake umepungua na kuwa mdogo kwa kiwango hicho hicho, na wakati huo mwanadamu anaporomoka katika ngazi ya chini ya mnyama duni kabisa kiakili. Lakini (Kuamini Akhera) hakuji kwa mwanadamu huyu kwa ajili ya kumuokoa na kumpa msaada hadi inabadilisha muda huo finyu – ambao ni kama kaburi – kuwa muda mpana mkunjufu sana kiasi inajumuisha muda uliopita na mustakabali kwa pamoja na kumuonesha uwepo mpana kwa upana wa dunia, bali kwa wasaa unaotandawaa kutoka azali hadi milele. Na hapo mwanadamu huyu atafanya heshima kwa mazazi wake na kumtukuza kwa ukomo wa ubaba unaoendelea hadi katika nyumba ya furaha na ulimwengu wa roho – na atamsaidia ndugu yake – kwa tafakuri hiyo - kwa udugu unaoendelea hadi milele na atampenda mkewe na kusuhubiana naye na kumsaidia kwa sababu kwake yeye ni sahiba mzuri sana wa maisha hadi peponi, hafanyi duara hili pana la uhai – na huduma muhimu zilizomo – kuwa ni njia ya kuendea mambo duni ya kidunia wala malengo yake madogo madogo na manufaa yake duni. Hivyo hupata urafiki uliotimia, utambuzi safi wa fadhila na ikhlasi iliyotimia, katika mahusiano yake na huduma zake, na makamilifu na tabia zake njema zinaanza kupanda na kuwa juu kwa kiwango hicho hicho na utu wake unakuwa juu na kila mmoja kwa mujibu wa daraja yake. Mwanadamu huyo ambaye hakuwa mwenye kupanda katika ngazi ya kinega katika kuonja kwake maisha - sasa amekuwa – kwa fadhila ya kuamini Akhera – ni mgeni mheshimiwa duniani, kiumbe mwenye furaha, na kiumbe wa kipekee humo duniani anashika nafasi ya juu kuliko wanyama wote, bali anakuwa kiumbe mpendwa zaidi na mja aliyetukuzwa sana mbele ya mlezi na mfalme wa ulimwengu. Tumetosheka na kiasi hiki katika kubainisha natija hii kwani Risale-i Nur imezibainisha kwa hoja na dalili mbali mbali. Faida ya nne ambayo inaangalia katika maisha ya kijamii Ni ile ambayo (Mwale wa tisa) umeibainisha na muhtasari wake ni: Kwamba (Watoto) ambao wanawakilisha robo ya wanadamu hawawezi kuishi maisha ya mwanadamu mnyoofu mwenye silka za kiutu ila kwa kuamini Akhera. Kwani bila ya imani hii wangelazimika kuishi maisha yaliyojaa ubaya, migongano na majonzi ya kuumiza. Hawapati raha wala maliwazo na michezo yao, kwa sababu umauti ambao unawasibu watoto wenzao wanao wazunguka unaathiri mno katika nafsi ya kila mtoto, na katika hisia zake ndogo laini, na katika moyo wake ambao kwenye mustakabali utakuwa na matarajio na matakwa yake mengi, na katika roho yake ambayo haiwezi kuhimili hivyo itasibiwa na wasiwasi na kutahayari, hata maisha yake na akili yake kuwa ni nyenzo za mateso kwake, michezo anayojisitiri ndani yake haimpi manufaa yoyote wala kuyapatia majibu maswali yake na tahayari yake, isipokuwa mwongozo wa imani ya (Kuamini Akhera) unamfanya kuisemesha nafsi yake kwa kusema: “Hakika rafiki yangu – au ndugu yangu ambaye amefariki, hivi sasa amekuwa ndege katika ndege wa peponi, yeye ana maliwazo zaidi kuliko sisi na kufurahia matembezi huko peponi. Na hakika mama yangu – japo amefariki – ila yeye amekwenda katika rehema pana ya mwingi wa rehema na atanikumbatia tena katika kifua chake cha upendo mwingi huko peponi, basi namwona mzazi huyo mwenye huruma”. Na kwa hivi anaweza kuishi kwa utulivu maisha ambayo yanamstahiki mwanadamu. Vilevile (Wazee) ambao wanawakilisha robo ya wanadamu, hakika wao hawapati maliwazo kwa kuzimika kwa maisha yao hivi karibuni, na kuingia kwao chini ya udongo, hali ya kuwa dunia nzuri tamu imeshafunga milango yake mbele yao isipokuwa kwa (Kuamini Akhera). Kwani bila ya imani hii wazazi hao wenye kuheshimiwa wenye huruma, na kina mama hao wenye kujitolea muhanga, wenye huruma nyingi wangeteseka na balaa baada ya balaa, na wangekuwa katika hali ya kinafsi dhalili mno na katika wasiwasi mzito wa moyo, na dunia ingekuwa finyu kwao kama jela, na maisha yenyewe yangekuwa ni adhabu ya kudumu isiyowezekana. Wakati ambapo imani ya Akhera inawanong’oneza kwa kusema: “Wazee msihuzunike na wala msijali sana, kwani mnao ujana wa kudumu milele na hapana budi ujana huo utakuja na kwamba maisha angavu ya furaha na umri mrefu wenye kuendelea milele unakungojeeni, na mtakutana na watoto zenu na ndugu zenu ambao mmewakosa, na mema yenu yote yamehifadhiwa na mtachukua thawabu zake.” na kama hivi (Imani ya Akhera) inatoa maliwazo na furaha kwao, kwa namna ambayo kama mmoja wao atabebeshwa mizigo ya uzee mara mia moja angeubeba kwa kustahamili na kwa kusubiri akingojea yatakayofuatia katika maisha ya kiakhera yenye furaha. Na kadhalika (Vijana) ambao wanawakilisha theluthi ya wanadamu, huenda wasisikilize sauti ya akili zao za uthubutu. Matakwa yao na matamanio yao yanachemka, nao ni wenye kuzidiwa na hisia na mihemko yao, vijana hawa wakiikosa (Imani ya Akhera) na kama hawakukumbuka adhabu ya jahanamu, hakika mali, heshima za watu na raha za wanyonge, na heshima ya wazee vinakuwa kwenye hatari, kwani huenda mmoja wao anaweza kuharibu furaha ya nyumba yenye amani na starehe kwa ajili ya ladha wa kupita, na kwa hivyo akaonja matokeo ya ubaya wa jambo lake – adhabu ya miaka mingi katika jela kama hizi na kuporomoka na kuwa kama mnyama wa mwitu. Lakini ikiwa (Imani ya Akhera) itampa msaada basi ni haraka sana anarejesha akili yake na kuiambia nafsi yake kwa kusema: “Licha ya polisi wa serikali na wapelelezi wake hawawezi kuniona kwa kuwa niko kwenye kificho hakika malaika wa mfalme mkuu mwenye utukufu ambaye anamiliki jela ya jahanamu ni ile jela kuu ya kudumu wananisajilia maovu yangu, kwa hiyo mimi siko huru mwenye kuachiliwa kamba, bali mimi ni mgeni anayepita mwenye jukumu, na nitakuwa – hakuna namna – katika siku fulani dhaifu na mzee kama wao”. Yatajitokeza matone ya rehema, upole na huruma – wakati huo – kutoka katika kina cha moyo wake na atahisi kuwaheshimu wale ambao aliotaka kukiuka haki zao kwa udhalimu. Na kwa kuwa Risale-i Nur imefafanua maana hii tunafupisha kwa kiasi hiki. Na kadhalika (Wagonjwa na wenye kudhulumiwa na wenye misiba mithili yetu na mafukara na wafungwa) ambao wamehukumiwa adhabu kali, wote hao wanawakilisha sehemu muhimu sana ya wanadamu, kama (Kuamini Akhera) hakukuwasaidia na kama hawakuliwazika nayo basi kifo wanachokiona mbele yao daima kutokana na maradhi waliyonayo, na hakika udhalilishaji ambao wanauona kutoka kwa madhalimu - bila ya kuweza kuwalipizia kisasi wala kuokoa heshima yao kutoka katika makucha yao – hakika kukata tamaa kuchungu kunakotokana na upotevu na majanga yaliyosibu mali na watoto wao, na hakika dhiki kali inayotokana na maumivu na mateso ya jela kwa miaka mingi matokeo ya ladha fupi kabisa haimalizi dakika au saa kadhaa, yote hayo yaifanya dunia - bila shaka – kuwa ni jela kubwa kwa hawa waliofikwa na majanga na kufanya maisha yenyewe ni adhabu iumizayo kwao! Lakini imani ya Akhera haiwapi msaada wa pole na maliwazo ila haraka wanakunjuka nyoyo zao na wanavuta pumzi wakiwa na faraja kutokana na dhiki, kukata tamaa, wasiwasi, babaiko na usongo wa kisasi inayowaondolea kwa ujumla au kiasi kidogo kila mmoja kulingana na ngazi za imani yake. Hata inayumkinika kwangu kusema: Kwamba isingekuwa imani ya Akhera ambayo imenipa mimi na ndugu zangu katika msiba wetu wakutisha na huku kuingia kwetu jela – pasipo na dhambi yoyote tuliyoitenda – ingekuwa kuhimili uchungu wa siku moja katika siku za mateso ni kama umauti wenyewe, na msiba huu ungetusukuma katika kuacha maisha na kuyasusa. Lakini shukrani kwa Allah (s.w) - bila idadi wala mpaka – kwa kunifanya kustahamili maumivu mengi kutokana na ndugu zangu ambao ni wapenzi zaidi kwangu kuliko nafsi yangu na kustahamili upotevu wa maelfu ya Risale-i Nur ambayo ni tukufu zaidi kuliko macho yangu, na ninastahamili kukosa vingi katika vitabu vikubwa vya kupendeza vyenye thamani na ninastahamili huzuni na majonzi yote haya kwa imani hiyo ya Akhera, licha ya kuwa nisingeweza kustahamili idhilali yoyote na kushinikizwa na yeyote vyovyote awavyo, basi mimi nina kuapieni – mpate kutulia – hakika nuru ya imani ya Akhera na nguvu yake vimenipa subira, ushupavu kupozwa, liwazo, ugumu na shauku ya kufuzu thawabu ya jihadi kubwa katika mtihani huu kwa kiasi kwamba nina hesabu nafsi yangu kuwa katika madarasa yote ni kheri tupu na uzuri. Ni haki kuitwa (Madrasa ya Yusuf) kama nilivyolieleza hilo mwanzoni mwa risala hii na lau isingekuwa maradhi ambayo yalikuwa yakinisumbua wakati mwingine na kama si shida za ukongwe ningefanya jitihada zaidi ili nipate masomo yangu kwenye madrasa hii pamoja na utulivu wa moyo nilio nao. Kwa hali zote tumetoka kwenye maudhui nataraji masamaha kwa nyongeza hii. Kadhalika hakika (Nyumba ya kila mwanadamu) ni dunia yake ndogo bali ni pepo yake ndogo, kama haikuwa (Imani ya Akhera) mwamuzi na mtawala wa furaha ya nyumba hii, kila mmoja katika watu wa nyumba hiyo mgogoro wenye kuumiza, na mateso makali katika mahusiano ya wao kwa wao kwa kiwango cha ngazi za upole wake na mapenzi yake kwao, basi itageuka pepo hiyo na kuwa ni jahimu isiyowezekana, na anaweza kuilewesha akili yake kwa pumbao na usafihi wa muda mfupi, katika hili anakuwa mithili yake ni mithili ya mbuni anapomwona mwindaji huficha kichwa chake mchangani ili yule mwindaji asimuone na hali ya kuwa anashindwa kukimbia na kuruka, naye vilevile anazamisha kichwa chake katika ghafla ili umauti kutoweka na utengano visimwone, akipuuza utambuzi wake kwa muda kwa upumbavu na kana kwamba amepata tiba ya kinachomsumbua! Kwa mfano mama – ambaye anajitolea mhanga kwa ajili ya mwanawe - kila anapoona mwanawe anaingia katika hatari hutetemeka kwa kumhuzunikia na kumhofia mwanawe. Na watoto kadhalika pale wanaposhindwa kuwaokoa wazazi wao na ndugu zao kutoka katika misiba isiyokatika, huwa kwenye wasiwasi ya kudumu na wanahisi hofu ya kuendelea. Kwa kupimia hili basi maisha ya familia ambayo yanadhaniwa kuwa ni maisha ya furaha, hukosa furaha yake katika dunia hii yenye migogoro yenye kutoweka ambapo haitoi mafungamano kati ya watu, wala uhusiano wa undugu kati yao – ndani ya maisha mafupi sana – urafiki wa hakika, utambuzi wa fadhila wa dhati na ikhlasi kamili, na huduma na mapenzi yalio safi, bali tabia zina kuwa ndogo na kusinyaa kwa kulingana na ufupi wa uhai wenyewe na pengine hudondoka na kukosekana jumla. Lakini Imani ya (Kuamini Akhera) haiingii katika nyumba hiyo hata inanawirisha maeneo yake moja kwa moja na kuangaza, kwa sababu uhusiano wa undugu, upole na mapenzi ambayo yanawafunganisha wakati huo hayapimwi ndani ya muda mfupi sana, bali hupimwa kulingana na mahusiano yanayoendelea hadi katika kubaki na kudumu kwao mlele huko Akhera na furaha ya milele - wakati huo - kila mmoja atafanya heshima ya dhati kwa wengine na kuwaelekezea mahaba safi na kudhihirisha upole wa kweli na kuonesha urafiki mwema, bila ya kuangalia mapungufu. Hapo tabia hupanda na kuwa juu na furaha ya kibinadamu ya kweli inaanza kustawi katika nyumba hiyo. Madhumuni haya yamebainishwa katika Risale-i Nur hapa tumetosheka kwa yaliyotangulia. Na kadhalika kila (Mji) kwa dhati yake ni nyumba pana kwa wakazi wake. (Imani ya Akhera) isipokuwa ni yenye kutawalia watu wa familia hii kubwa, itawatawalia chuki, manufaa binafsi, hila, ubinafsi, kujikalifu, ria, rushwa na hadaa badala ya misingi ya tabia njema ambazo ni ikhlasi, murua, fadhila, mahaba, kujitolea muhanga na radhi ya Allah (s.w) na thawabu Akhera. Na maana za ugaidi na fujo na ushenzi ni vyenye kutawala na kuendesha chini ya jina la mfumo, usalama, na ubinadamu ambayo wanayadhihirisha, na wakati huo maisha ya mji huo yanashika alama na watoto wanasifika kwa ubaya na uzembe na vijana wanasifika kwa ulevi na uhuni na wenye nguvu watasifika na dhuluma na ukiukaji na wazee watasifika kwa kilio na manung’uniko. Na kwa kulinganishia hili (Miji) kwa ukamilifu wake si kingine bali ni nyumba pana sana. Na taifa ni nyumba ya familia ya umma. Kama (Imani ya Akhera) ikitawalia katika nyumba hizi, fadhila hufunuka na kuwa wazi, na heshima ya kubadilishana itadhihiri na huruma ya kweli, na mahaba ya dhati bila badala, na kusaidiana pamoja na huduma ya kweli bila hila, na kutangamana na hisani bila ya ria, na fadhila na heshima bila ya kiburi, na fadhila nyengine zitaenea ambapo Imani ya Akhera itanong’ona kwa watoto kwa kuwaambia: “Acheni ubaya na uzembe kwa sababu mbele yenu kuna pepo yenye neema basi msijishughulishe nafsi zenu mbali na hiyo kwa michezo”. Inamakinisha tabia kwao kwa mwongozo wa Qur’an tukufu. Na inawasemesha vijana kwamba: “Mbele yenu kuna moto wa jahanamu komeni ulevi na uhuni”. Na kuwafanya wazinduke na kumsemesha dhalimu: “Tahadhari hakika adhabu kali itakuthibitikia” hapo humkomesha na udhalimu na kumfanya kutosheka na uadilifu, na kuwasemesha wazee: “Furahini kwani mbele yenu kuna ujana wa kudumu wenye mng’ao, na furaha ya akhera ya daima yenye kubaki inawangojeeni ni ya thamani zaidi kuliko mlizozikosa katika aina za furaha na ni ya juu zaidi kuliko hizo basi njooni mjitahidi kupata mafanikio hayo”. Hapo hugeuza kilio chao kuwa ni sherehe na furaha. Kulinganishia hili (Imani ya Akhera) inabainisha taathira yake nzuri na kutuma mionzi ya nuru yake katika kila kundi, sehemu yake na jumla yake, enevu yake na mahsusi yake, chache yake na nyingi yake. Na wasikilize kwa makini Wataalamu wa elimu jamii na wa tabia miongoni mwa wadau wa mambo ya mwanadamu! Yakilinganishwa tuliyoyataja huko nyuma katika faida za kuamini Akhera itafahamika wazi na kwa namna ya kukinaisha kwamba mhimili wa furaha katika makazi mawili na katika maisha yote hayo mawili si vyovyote isipokuwa ni Imani peke yake. Hakika yamekuja katika (Neno la ishirini na nane) na katika Risale-i Nur nyingine majibu yenye nguvu mno kujibu utata wa kipuuzi kuhusu: (Ufufuo wa kimwili), (Kufufuliwa mwili) tunatosheka nayo ila hapa tutaashiria kwa ufupi sana: Hivyo tunasema: Mengi ya majina mzuri ya kiungu yanadhihirika katika hali ya kimwili ni kioo chake jumuishi zaidi, na kwamba makusudio ya mbali ya kiungu katika kuumba viumbe yanadhihirika katika hali ya kimwili, ni kituo tajiri mno cha makusudio na yenye kutenda kazi zaidi, na kwamba nyingi ya aina mbali mbali za hisani za Mola mlezi na neema zake enevu hubainika katika hali ya kimwili, na kwamba aghalabu ya mbegu za dua anazoziomba mwanadamu kwa ulimi wa haja zake, na misingi mingi ya shukurani na himidi zinazopelekwa kutoka kwake na kwenda kwa Muumba wake Mwenye kurehemu zinatokana na hali ya kimwili, na kokwa zenye kuzidia zaidi kuwa katika aina mbalimbali katika ulimwengu wa kimaanawy na kiroho pia zimo katika hali ya kimwili. Basi kwa kupimia hili: Hakika hali ya kimwili ina misingi inajikita ndani yake mamia ya hakika za jumla, kwa hiyo Muumba Mkarimu hukithirisha na kuongezea hali ya kimwili katika uso wa dunia ili hakika hizo zilizoelezwa zipate kudhihiri, hutunuku viumbe uwepo kwa kasi mno na kwa nguvu ya ajabu, msafara baada ya msafara ikivituma katika huu ulimwengu wa maonesho, kisha hukomesha huduma zake na baada yake hutuma viumbe wengine kwa mfululizo. Na kama hivi anajaalia mashine ya viumbe katika kazi na shughuli ya kudumu, ikifuma mazao ya kimwili juu ya ardhi ikijaalia ardhi kuwa ni shamba la Akhera na kitalu cha pepo hata Allah (s.w) ili kulituliza tumbo la mwanadamu la (kimwili) na kulifanya kuwa katika shukurani na kuridhia husikia dua lake inaloliomba kwa ulimi wa hali kwa ajili ya kubaki kwake na anaijibu kwa hakika, kwa vyakula anavyoumba visivyojulikana idadi, vitamu na vimetengenezwa vyema, na kwa kufanya neema za thamani sana ziwepo kwa mamia ya maelfu ya sampuli, jambo ambalo lina dhihirisha kwa uwazi na bila shaka kwamba aghalabu ya aina za ladha za kimaada zenye kuhisiwa peponi hakika ni za kimwili. Na kwamba neema kuu ya furaha ya milele wanayoitafuta viumbe wote na kuliwazika nazo ni za kimwili pia. Je, inayumkinika na kuingia akilini na je, upo uwezekano katu Mweza wa kila kitu Mwenye kurehemu mjuzi wa kila kitu mkarimu kukubali daima dua ya ulimi wa hali wa tumbo rahisi kwa ajili ya kubakia kwake, na kuliitikia kwa kusudio na kimatendo hasa - bila ya kuingia kwa sadifu - kwa vyakula vya kimaada vyenye kuhisika anavyoliumbia katika ukomo wa ufundi na muujiza kwa kufanya hivyo huliridhisha tumbo, kisha Allah (s.w) asikubali dua za jumla na dua zisizo kuwa na ukomo ambazo huombwa na tumbo kubwa la wanadamu na maumbile yake ya asili, na asiwape ladha tele za kimwili huko Akhera zile ambazo kimaumbile wanaliwazika nayo bali wanaitarajia katika maisha ya umilele? na je inayumkinika asijibu maombi hayo kimatendo na asitekeleze ufufuo wa kimwili?! na asimridhishe mwanadamu huyu - ambaye ni natija ya viumbe na khalifa wa Ardhi na mja aliyetukuzwa na kupewa heshima sana – kuridhika kwa milele? Kamwe kisha kamwe! Hili ni muhali katika muhali mia moja bali ni batili kijumla kwani ni vipi asikie king’ong’o cha nzi wala asisikie radi za mbingu na vipi atachunga maandalizi ya askari wa kawaida wala asijali jeshi kubwa! basi ametakasika Allah (s.w) na hayo kutakasika kukubwa. Naam, hakika uwazi unaokinaisha wa aya tukufu: وَفِيهَا مَا تَشْتَهِيهِ الْأَنفُسُ وَتَلَذُّ الْأَعْيُنُ unabainisha kwamba zaidi ya anacholiwazika nacho mwanadamu katika tamu za kimaada zenye kuhisika – na ambazo huonjwa mifano yake duniani – ataviona na kuvionja kwa sura yake inayolingana na hali ya peponi. Na kwamba thawabu ya yanayofanywa na ulimi, jicho, sikio, na viungo vingine katika shukurani ya dhati na ibada za dhati zitatunukiwa ladha hizo za kimwili zinazohusiana nazo. Basi ufafanuzi wa Qur’an tukufu kwa ladha za kimwili ni wazi upeo wa uwazi kiasi haiwezi kuchukua taawili (Tafsiri ya undani) yoyote inayogeuza kutoka katika maana ya dhahiri, bali inakataa kutokukubali maana ya kiudhahiri. Na kama hivi matunda ya imani ya Akhera na natija zake yanadhihirisha kwamba mfano wa namna inavyojulisha hakika ya tumbo la mwanadamu na mahitaji yake ujulisho wa kukinaisha juu ya kuwepo kwa vyakula, basi hakika ya mwanadamu na makamilifu yake na haja zake za kimaumbile na matarajio yake ya milele na hakika zake na maandalizi yake vinahitajia natija na faida zilizotajwa za kuamini Akhera, na vinajulisha kwa kukinaisha juu ya Akhera, pepo na ladha zake za kimaada na kuhisiwa na kubakia milele, na vinashuhudia kuthibiti kwake. Na kwamba hakika ya makamilifu ya huu ulimwengu na aya zake za kimaumbile zenye hekima na hakika zake zote zilizofungamana na hakika za kiutu zinajulisha kwa kukinaisha pia juu ya kuwepo kwa Akhera na juu ya kuthibiti kwake na kushuhudia ushahidi wa ukweli juu ya ujio wa ufufuo na kufunguka kwa milango ya pepo na moto. Na kwa kuwa Risale-i Nur imelithibitisha suala hili kwa namna ya kupendeza na kwa hoja zenye nguvu mno bila ya kubakisha vumbi la utata na hasa (Neno la kumi) na la (Ishirini na nane) - pamoja na vituo vyake viwili – na la (Ishirini na tisa) na (Mwale wa tisa) na (Risalat al-Munajaat) kwa hiyo tutatosheka nayo. Hakika ya ufafanuzi wa Qur’an tukufu katika yahusuyo jahanamu uko wazi mno haukuacha nafasi ya ufafanuzi mwingine wowote, ila tutabainisha kwa muhtasari sana yanayotoa baadhi ya utata duni katika nukta mbili, tukielekeza maelezo yake katika Risale-i Nur: Nukta ya kwanza Hakika kufikiria na kuhofia jahanamu hakuondoshi ladha ya matunda ya imani yaliyotajwa, kwa kuwa rehema ya Mola mlezi iliyo kunjufu humnong’oneza huyo mwenye kuhofia: “Njoo kwangu chini yako kuna mlango wa toba ingia kupitia mlango huo”. Hakika kuwepo kwa jahanamu sio kwa ajili ya kutisha bali ni kwa ajili ya kukujulisha ladha za pepo kwa maarifa kamili na ili kukuonjesha hiyo pepo kikamilifu na kukulipizia kisasi wewe na kwa viumbe wasio na mpaka katika waliovunja haki za wote na kuzikiuka, na ili kuwafurahisha hao wote kwa hili na kuingiza furaha kwao. Basi ewe mwenye kuzama katika upotevu - na asiyeweza kutoka humo – kuwepo kwa jahanamu ni bora zaidi kwako kuliko kutokuwepo milele kwani katika kuwepo kwake kuna aina ya rehema hata kwa makafiri wenyewe, kwa sababu mwanadamu – na wanyama wenye kuzaliwa – hustarehe kwa kustarehe kwa ndugu zake na wanawe na wapenzi wake na kufurahika - kwa upande fulani – kwa furaha yao. Basi ewe kafiri! Ima wewe utaanguka kwenye shimo la kutokuwepo – kwa kuzingatia upotevu wako - au utauingia moto wa jahanamu. Na ilivyo kuwa kutokuwepo ni shari tupu kwa hivyo kunyongwa moja kwa moja kwa wapendwa wako wote na wale unaofurahi kwa kufurahi kwao katika ndugu, wazazi na kizazi chako, kutaunguza roho yako na kuuadhibu moyo wako na kuiumiza hakika yako ya utu zaidi kuliko adhabu ya jahanamu kwa mara elfu, kwa sababu kama kusinge kuwapo jahanamu, basi na hata pepo isingekuwapo vilevile, kila kitu kwa hiyo kinadondoka kwa ukafiri wako kwenda katika kutokuwepo. Lakini ukiingia jahanamu na ukabaki ndani ya uwepo hakika wapenzi wako na ndugu zako ima watapata raha peponi au watakuwa ndani ya duara za uwepo chini ya rehema za Allah (s.w). Basi huna pa kukimbilia ila ukubali uwepo wa jahanamu kwani uadui dhidi ya uwepo wake - na kuikataa – yaani ni kujitenga katika kukosekana kutupu, ambako ni kuteketeza furaha ya wapenzi wote na marafiki na kuwafanya watoweke! Naam, hakika jahanamu ni makazi ya uwepo inatekeleza jukumu la mahakama ya Mwingi wa Hekima Mtukufu na uadilifu wake, na ni mahali pa kutisha mno ndani ya duara la uwepo ambao ni kheri tupu, zidisha juu ya hilo, ina majukumu mengine na huduma tukufu na hekima tofauti zinazohusu ulimwengu wa kubakia. Hayo ni makazi yenye utukufu na haiba kwa wengi ya wenye uhai mfano wa malaika wa adhabu. Nukta ya pili Hakika ya kuwepo kwa jahanamu na adhabu yake kali hakupingani – kabisa – na rehema isiyokuwa na mpaka wala uadilifu wa hakika, wala hekima yenye kipimo ambayo haina israfu ndani yake, bali hakika ya rehema, uadilifu na hekima vinataka uwepo wa jahanamu na vinauhitajia, kwa sababu kumuua mnyama aliyeshambulia wanyama mia moja au kuteremsha adhabu kwa dhalimu ambaye amevunja heshima za elfu moja ya watu wasio na hatia, ni huruma kwa mara elfu maradufu kwa waliodhulumiwa kupitia uadilifu. Na hakika ya kumsamehe dhalimu huyo kutokana na adhabu au kumuachia na kumwacha yule mnyama mwitu akiwa huru kuna dhuluma mbaya na kutokuwa na huruma kwa mamia ya masikini kwa mamia ya maradufu, mkabala na huruma isiyokuwa mahali pake. Na mfano wa hili pia kafiri kabisa – ambaye anaingia jela ya jahanamu – kwani yeye kwa ukafiri wake anakanusha haki za majina ya kiungu yaliyo mazuri, yaani anazikiuka haki hizo na kwa kukadhibisha kwake ushahidi wa vilivyomo - vyenye kushuhudia majina hayo – anakiuka haki zao pia, na kwa kukanusha kwake majukumu matukufu ya viumbe – nazo ni tasbihi zake kwa majina – na anakiuka haki zake na kwa kupinga kwake aina za ibada ambazo wanazitekeleza waja kukabiliana na kudhihiri kwa ulezi na uungu wa Allah (s.w) - nalo ndio lengo la kuumbwa kwake na sababu katika sababu za kuwepo na kubakia kwake – anakiuka vibaya sana haki za viumbe wote, kwa hiyo ukafiri ni jinai kubwa na dhuluma mbaya ubaya wake unavuka mipaka yote ya msamaha kwa hiyo inathibiti kwake hofisho la aya tukufu: إِنَّ اللّهَ لاَ يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ Bali kutomtupa mtu kama huyu katika jahanamu kwa kumuhurumia ni jambo linalopingana na huruma yenyewe moja kwa moja katika haki za hizi idadi kubwa za halaiki na viumbe ambavyo haki zao zimevunjwa. Na kama hivyo kama wanavyotaka wenye madai kuwepo kwa jahanamu, hakika enzi ya utukufu wa Allah (s.w) na adhama ya ukamilifu wake (s.w) vinaitaka kwa yakini. Naam, mpumbavu au mwovu, asi akimwambia mtawala mtukufu wa nchi: “Wewe huwezi kunitupa jela na hutaweza hilo kamwe” kwa kukiuka mpaka wake na utukufu wa mtawala huyo na adhama yake, hapana budi kuwa mtawala huyo ataanzisha jela kwa ajili ya huyo safihi mkiukaji hata kama kusingekuwa katika nchi hiyo kuna jela. Vivyo hivyo mambo kwa kafiri halisi basi yeye kwa ukafiri wake anakiuka vikali enzi ya utukufu wake (s.w), na kwa kukanusha kwake anapinga adhama ya uweza wake na kwa kukiuka kwake anagusa ukamilifu wa ulezi wake wa kiungu, kusingekuwepo hata hizo sababu zenye kupasisha na hizo nyudhuru nyingi na hekima nyingi na majukumu mengi kwa jahanamu na kwa kuwepo kwake, hakika kuumba jahanamu kwa ajili ya mfano wa hawa makafiri na kuwatupia humo ni katika hali ya enzi na utukufu huo. Kisha hali ya ukafiri yenyewe inafahamisha jahanamu kwa sababu kama ilivyo hali ya imani ikiundika mwili inaweza kujenga kwa ladha zake na neema za uzuri wake pepo maalum kwenye dhamira ya mwanadamu na moyo wake, ni pepo ndogo inaashiria na kupasha habari kuhusu pepo ya kudumu milele wanayoingojea huko Akhera, vivyo hivyo ukafiri - na hasa hasa ukafiri halisi – unafiki na kuritadi yapo maumivu na mateso ya kutisha kwa namna ambayo kama yangefanyika mwili na kujikita katika nafsi ya mwenye nayo ingemtengenezea jahanamu yake maalum ambayo inaashiria yale atakayo yafikia huko Akhera katika jahanamu ambayo ni kali zaidi kitisho na kwa mateso. Tumethibitisha hili kwa dalili za kukinaisha kwenye Risale-i Nur na imeashiriwa pia mwanzoni mwa suala hili. Na kwa kuwa hii dunia ni shamba la Akhera, hakika ndogo ambazo huzaa matunda na kuweka mashuke Akhera, basi mbegu hii yenye sumu (Ukafiri) inaashiria kwenye pembe hii kwenye ule mti wa Zaqqum na kusema: “Mimi ni shina la mti ule na johari yake, basi atakayenibeba moyoni mwake katika wenye kusibiwa na majanga nitamzalia matunda ya kielelezo maalum kutoka katika mti ule uliolaaniwa”. Na kwa kuwa ukafiri ni kukiuka haki zisizokuwa na mpaka, na ukiukaji wenye kufedhehesha, kwa hiyo ukafiri ni jinai isiyokuwa na mpaka, kwa hiyo unamfanya mwenye nao kuwa anastahiki adhabu isiyokuwa na mpaka. Ikiwa kuua ambako hutokea katika dakika moja tu humfanya muuaji aonje adhabu ya miaka kumi na tano (Muda unao karibia dakika milioni nane) na huo unazingatiwa kuwa unaafikiana na uadilifu wa kibinadamu, hesabu yake ni yenye kufaa masilahi ya umma na haki zake, hakuna makosa kwamba dakika moja ya ukafiri halisi – kwa kuuzingatia ukafiri ni mauaji elfu – kwa hiyo ikikabiliwa kwa adhabu inayokaribia mamilioni ya dakika kulingana na uadilifu huo wa kibinadamu basi anayemaliza mwaka mmoja kamili katika umri wake katika ukafiri kwa hiyo anastahiki adhabu ya dakika trilioni mbili na themanini na nane bilioni yaani anakuwa ni mstahiki wa: خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا Hivyo, hakika mtindo wa kimuujiza wa Qur’an tukufu katika kubainisha kwake pepo na moto na yaliyomo katika (Risale-i Nur) – ambayo ni neema kutokana nayo na tafsiri yake – katika hoja kuhusu kuwepo kwake hazikuacha nafasi ya ufafanuzi mwingine wowote basi aya nyingi mno mfano: وَيَتَفَكَّرُونَ فٖى خَل۟قِ السَّمٰوَاتِ وَال۟اَر۟ضِ رَبَّنَا مَا خَلَق۟تَ هٰذَا بَاطِلًا سُب۟حَانَكَ فَقِنَا عَذَابَ النَّارِ رَبَّنَا اص۟رِف۟ عَنَّا عَذَابَ جَهَنَّمَ اِنَّ عَذَابَهَا كَانَ غَرَامًا اِنَّهَا سَٓاءَت۟ مُس۟تَقَرًّا Na aghalabu wa alilokuwa mtume (s.a.w) akilirudia rudia katika dua zake kila wakati, na Manabii (a.s) na watu wa hakika kama: “Tuepushe na moto”.. “Tuokoe na moto”.. “Tukomboe na moto” ambalo kwao imepata ukinaifu kamili kwa msingi wa wahy ulioshuhudiwa, yote hayo yametubainishia kuwa kadhia kubwa sana ya mwanadamu juu ya Ardhi hakika sio nyingine isipokuwa ni kuokoka kutokana na moto, na kwamba hakika kuu zaidi na ya kushangaza mno katika hakika za viumbe, bali muhimu zaidi sio nyingine bali ni (Jahanamu) ambayo wanaishuhudia baadhi ya hao wenye kuhakiki na watu wa ushahidi na ufunuo, na wengine wanaona ndimi zenye kuwaka na giza jeusi na baadhi yao wanasikia mrindimo wa kuwaka kwake na kufoka kwake basi wanapiga kelele kutokana na kishindo chake: “Tuepushe na adhabu ya moto”. Naam, hakika ya kukabiliana kwa kheri na shari katika ulimwengu huu, ladha na maumivu, nuru na giza, joto na baridi, uzuri na ubaya, uongofu na upotevu, na kuingiliana kati yao hakika hilo ni kwa hekima kubwa kwani kama kusingekuwapo shari isingefahamika kheri, na kusingewapo maumivu ladha isingefahamika, na mwanga bila giza sambamba nao haidhihiri uzuri wake, na viwango vya joto huthibiti kwa kuwepo kwa baridi, na inakuwa hakika moja ya uzuri elfu moja katika hakika kwa kuwepo kwa ubaya, bali huvuna maelfu ya aina za uzuri na ngazi za uzuri. Na nyingi ya ladha za peponi hujificha kwa kutokuwepo kwa jahanamu. Basi kwa kupimia hili inayumkinika kujulikana kila kitu kwa upande wa dhidi yake, na kwa kuwepo kwa dhidi inayumkinika hakika moja kutoa matunda ya hakika nyingi. Kwa kuwa vilivyomo hivi vyenye kuchanganyika vinamiminika kumiminika kutoka makazi ya kutoweka kwenda katimka makazi ya kubakia, hapana budi kwamba kheri, ladha, nuru, uzuri, imani na mifano ya hayo kumiminika kuelekea peponi na inadondoka shari, maumivu, giza, ubaya, ukafiri na mifano ya hayo katika mambo ya kudhuru kwa jahanamu. Humimina mifereji ya viumbe hivi vyenye kugongana daima kuelekea katika birika hizo mbili na kutulia tuli kwenye viwili hivyo mwishoni mwa safari. Kwa kadiri hii tunatosheka na tunaelekeza katika yaliyokuja katika (Neno la ishirini na tisa) katika nukta za mfano. Enyi wenzangu katika masomo katika madarasa hii ya Yusuf! Hakika njia nyepesi ya kuokoka na jela ya milele ya kutisha (Jahanamu) hakika ipo katika kutumia kwetu fursa ya kubakia kwetu kwenye jela ya kidunia, hii ambayo imefupisha mikono yetu kutenda madhambi mengi ikatuokoa nayo. Kwa hiyo basi sio juu yetu ila kufanya istighfari (kuomba msamaha) na kutubia dhambi tulizozifanya katika siku zilizotangulia pamoja nakutekeleza faradhi, ili tugeuze kila saa moja katika saa za jela hii kwa hukumu ya siku moja ya ibada, hivyo hii kwetu ni fursa bora kwetu ili kuokoka kutokana na jela ya milele na kwa ajili ya kuingia kwetu pepo yenye nuru. Na kama tukiikosa fursa hii Akhera yetu itazama katika mikasa kama ilivyo hali ya dunia yetu na itathibiti kwetu kauli yake Allah (s.w): خَسِرَ الدُّنْيَا وَالْآخِرَةَ Sauti za takbira ya Idi al-Adh’ha mubarak zilikuwa zikipaa juu wakati mada hii ikiandikwa, mawazo yakanipeleka ya kwamba moja ya tano ya wanadamu wanakariri:(Allah Akbar), na kwamba zaidi ya Waislamu mia tatu milioni wanakariri kwa pamoja, kana kwamba sauti ya (Allah Akbar) inakuwa juu kwa ukubwa wa tufe la Ardhi na kwa upana wake kwa hiyo ardhi inazisikilizisha ndugu zake sayari nyingine neno hili takatifu katika pande za mbingu. Na kuna zaidi ya mahujaji ishirini elfu katika Arafa na Idd kwa pamoja wanakariri mwangwi wa aliyoyasema mtume mtukufu (s.a.w) na kuyaamrisha kabla ya miaka elfu moja na mia tatu pamoja na jamaa na swahaba wema. Nikahisi hisia kamili bali nimekinai kikamilifu kwamba miangwi hiyo, sauti na kukariri hakika ni uja mpana wa kijumla unakabiliana na kudhihiri kwa ulezi wa kiungu wa jumla kwa utukufu wa (Mola Mlezi wa Ardhi) na (Mola Mlezi wa walimwengu). Kisha nikaiuliza nafsi yangu: Je, ukoje uhusiano baina ya Akhera na neno hili takatifu (Allah Akbar)? Nikakumbuka haraka kwamba neno hili pamoja na maneno mazuri yenye kubakia yalio mema: (subahanallah, walhamadulillah, walaailaha illa Allah) na mfano wa hayo katika maneno ya alama za Kiislamu hukumbusha – bila shaka – Akhera sawa kwa sura ya kisehemu au kiujumla na yanaashiria kuthibiti kwake. Hakika upande mmojawapo wa maana ya (Allah Akbar) ni: Hakika ya uweza wa Allah na ujuzi wake ni juu ya kila kitu na ni kubwa na tukufu kuliko kila kitu, basi hakitatoka kitu chochote kiwacho katika duara la ujuzi wake na hakitakimbia usarifu na uweza wake, na hakitamponyoka kamwe, basi yeye (s.w) ni mkuu kuliko kila mkubwa tunayemuhofia na kumtukuza. Yaani ni mkuu kuliko kuleta ufufuo katika uwepo ambao tunauona kuwa ni mkubwa – na mkuu kuliko kutuokoa kwetu kutoka katika kutokuwepo na mkuu kuliko kutupa kwetu furaha ya milele. Yeye ni mkuu kuliko kila kitu ambacho tunakistaajabia na kuliko kitu chochote kilicho nje ya akili yetu ambapo Allah (s.w) anasema: مَّا خَلْقُكُمْ وَلَا بَعْثُكُمْ إِلَّا كَنَفْسٍ وَاحِدَةٍ Basi uwazi wa aya hii tukufu unabainisha kwamba kukusanya na kutawanya (ufufuo) kwa wanadamu wote ni rahisi kwa uweza wa kiungu kama kufanya nafsi moja iwepo, basi hakuna ajabu kupita katika maneno ya mithali kauli ya mwanadamu: (Allah Akbar, Allah Akbar) kila aonapo kitu kikubwa au msiba mkubwa au lengo kubwa, akiiliwaza nafsi yake kwa kauli hiyo na akifanya nguvu kubwa anayoegemea kutokana na neno hili kubwa. Naam, hakika neno hili pamoja na wenzake: (Subhanallah, walhamdulillah) ni faharisi za ibada zote na mbegu na muhtasari wake (kama ilivyokuja katika (Neno la kumi na tisa)). Hivyo kukariri kwa maneno haya – na hizo ni hakika kuu tatu katika swala na katika dhikiri zake - hakika ni kwa ajili ya kutia nguvu maana ya swala, kuipa kina na kuiimarisha. Nayo ni jawabu la kukinaisha la maswali yanayotokana na kustaajabia, ladha na haiba ambayo yanayokuwa nafsini mwa mwanadamu wakati akishuhudia ulimwengu na kuona yanayomwamsha hisia na kumfanya atahayari na yanayompeleka katika kushukuru na ambayo ni uwanja wa adhama na kiburi katika mambo ya ajabu, mazuri, makuu, mengi na yale ambayo ni juu ya aliyoyazoea. Naam, hakika askari anaingia katika hadhara ya mfalme na diwani yake (Makazi ya mfalme) siku ya Iddi kwa mfano wa kuingia kwake kiongozi mkuu, wakati ambao nyakati nyengine mfalme wake anamtambua kwa cheo cha kamanda na katika makamo yake - kama ilivyokuja mwishoni mwa (Neno la ishirini na sita) – basi kila mtu pia katika haji anaanza kumtambua mola wake wa haki (s.w) kwa jina la (Rabbil Ardhi wa Rabbil Alamiin) ujuzi unaofanana sana na inavyokuwa utambuzi wa mawalii wema. Na kila ngazi ya ukuu inapofunguka na adhama ya kiungu ndani ya roho yake hujibu kwa (Allah Akbar), kwa sababu ya maswali yanayomtawala yanayojirudia yenye msisitizo na kuleta tahayuri, basi (Allah Akbar) ni jawabu la kukinaisha kwa vitimbi vya hila za Shetani kama ilivyokuja katika (Mng’ao wa kumi na tatu). Naam, basi kama lilivyo neno hili (Allah Akbar) linajibu swali letu kuhusu Akhera majibu mafupi na yenye nguvu katika wakati huohuo, basi hakika fungu la maneno (Alhamdulillah) nalo pia linakumbusha ufufuo na kuuhitajia. Ambapo linatwambia: (Maana yangu haitimii bila ya Akhera) kwa sababu maana yangu yanafidisha kuwa: (Kila himidi au shukurani inayotoka kwa yeyote Mwenye kuhimidi na kutuka juu ya yeyote Mwenye kuhimidiwa awaye, kuanzia tangu azali hadi milele, ni mahususi kwake yeye (s.w)), na kwa kuwa furaha ya milele ndio asili ya neema zote na kilele chake, na ndio inayogeuza neema kuwa neema za hakika hazigeuki wala kuondoka, nayo ndio ambayo inayookoa wenye utambuzi kutokana na masaibu ya kutokuwepo na kuwakomboa nayo, kwa hiyo hayo peke yake yanaweza kukabili maana yangu ya kiujumla. Naam, hakika ya kurudia kila muumini kila siku baada ya swala kwa vile inavyoamuru sharia zaidi ya mara mia moja na hamsini (Alhamdulillah) kwa uchache, na ambalo linafidisha hamdi na thanai na shukurani kunjufu inaendelea kutokea azali hadi milele hakika hiyo ni thamani anailipa kwa kutanguliza kwa ajili ya kupata furaha ya milele peponi, kwani haiyumkiniki kuyafunga maana ya hamdi katika neema za dunia fupi za kutoweka zenye kutibuliwa kwa machungu wala haiyumkiniki kuwa yenye kuishia juu yake. Bali hata lau ungezingatia katika hizo neema zenyewe utaziona kuwa sio isipokuwa ni nyenzo za neema za milele za kudumu zinazostahiki shukurani juu yake. Ama neno (Subhanallah) hakika linamaanisha: Kumtakasa Allah (s.w) na kumtukuza kutokana na kila mshirika na kutenda upungufu na kasoro na dhuluma na kushindwa na ukatili na uhitaji na hila, na kila kinachohalifu ukamilifu wake na uzuri wake na utukufu wake. Na maana hii inakumbusha furaha ya milele na kujulisha juu ya Akhera ambayo ni mhimili wa adhama yake (s.w), utukufu wake na ukamilifu wake. Na pia inaashiria yale yaliyomo katika makazi hayo miongoni mwa pepo ya neema na kuijulisha. Na kama sio hivyo isingekuwa huko kuna furaha ya milele hakika vidole vya tuhuma vingeelekea kwenye adhama yake (s.w), ukamilifu wake, utukufu wake, uzuri wake na rehema zake, basi hapo vingepatwa na upungufu na kasoro, ametukuka Allah (s.w) na hayo kutukuka kukubwa. Yaani hakika ya Akhera haina shaka, kwani hiyo Akhera ni mahitajio ya ufalme wa Allah, ukamilifu wake, utukufu wake, uzuri wake na rehema yake (s.w). Na kama hivi hakika ya maneno haya matakatifu matatu pamoja na (Bismillah) na (لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ) na baki ya maneno yenye kubarikiwa, kila moja kati yao ni mbegu katika mbegu za nguzo za kiimani na kila moja kati ya hizo ni muhutasari wa hakika za nguzo za kiimani na hakika za Qur’an. Na kama yalivyo haya maneno matatu ni kokwa za swala na mbegu zake hizo basi ni kokwa za Qur’an pia. Kama unavyoshuhudia mwanzoni mwa baadhi ya sura za dhahiri ambapo zinafungua zikiwa kana kwamba ni johari yenye kung’aa mwanzoni mwake. Nazo ni hazina za hakika na misingi madhubuti za juzuu za Risale-i Nur ambazo zinaanza kwa vipawa vya Tasbihati, nazo pia ni nyiradi za Twarika ya Muhammad hutajwa mwishoni mwa swala ndani ya duara pana mno la uwalii wa Muhammad na uja wa Muhammad, kwa kiasi kwamba katika kila swala kuna zaidi ya mia moja milioni waumini katika mzingo huo mkubwa wa dhikiri wanarudia rudia kwa pamoja mara thelathini na tatu (Subahanallah) na mara thelathini na tatu (Alhamdulillah) na mara thelathini na tatu (Allah Akbar). Basi hapana budi kwamba unatambua kiasi cha umuhimu wa kusoma maneno hayo matatu yenye baraka. Ambayo ni mbegu za Qur’an na Imani na swala na ni muhutasari wake. Na kiasi cha thawabu za kuyarudiarudia kwa mara thelathini na tatu baada ya swala ndani ya huo mzingo mpana. Na kama hivi kama kwamba (Suala la kwanza) katika Risala hii lilikuwa somo muhimu sana katika swala, hakika mwisho huu wa Risala – bila hiari yangu – ni somo muhimu kuhusu Adhkari za swala! اَل۟حَم۟دُ لِلّٰهِ عَلٰى اِن۟عَامِهٖ na Alhamdulillah kwa neema zake. سُب۟حَانَكَ لَا عِل۟مَ لَنَٓا اِلَّا مَا عَلَّم۟تَنَٓا اِنَّكَ اَن۟تَ ال۟عَلٖيمُ ال۟حَكٖيمُ
بِس۟مِ اللّٰهِ الرَّح۟مٰنِ الرَّحٖيمِ اٰمَنَ الرَّسُولُ بِمَٓا اُن۟زِلَ اِلَي۟هِ مِن۟ رَبِّهٖ وَال۟مُؤ۟مِنُونَ كُلٌّ اٰمَنَ بِاللّٰهِ وَمَلٰٓئِكَتِهٖ وَكُتُبِهٖ وَرُسُلِهٖ لَا نُفَرِّقُ بَي۟نَ اَحَدٍ مِن۟ رُسُلِهٖ ... اِلٰى اٰخِرِ ال۟اٰيَة Hakika sababu ambayo imepelekea kufafanua aya hii yenye kujumuisha ya hadhi ya juu tukufu na kuhitajia kuibainisha, ni hali mahususi maalum iliyotokana na suala la kimaanawy lenye kuchokoza, na kufunuka kwa neema ya kiungu kubwa, kama ifuatavyo: Limepita katika roho swali hili: Kwa nini anazingatiwa kuwa ni kafiri yule anayekanusha sehemu ya hakika ya kiimani, na wala hahesabiwi kuwa ni Mwislamu asiyeikubali pamoja na kuwa nuru ya Imani ya kumwamini Allah na siku ya mwisho ni kama jua inatokomeza kila giza? Kisha kwa nini anakuwa mwenye kuritadi anayekanusha hakika moja au nguzo moja ya Imani na kumtupa katika ukafiri halisi, na asiyeikubali anatoka katika duara la Uislamu. Wakati ambapo inatakikana imani yake ya nguzo nyingine imwokoe – ikiwa imepatikana – kutoka katika ukafiri huo halisi? Jibu: Imani ni hakika moja inayotokana na nguzo sita zilizoungana na kuwa kitu kimoja hazikubali kutenganishwa, nayo ni kitu kizima hakikubali kugawanyika katika sehemu, nayo ni yote nguzo zake hazikubali kugawanyika, na hiyo ni kwa sababu kila nguzo katika nguzo hizo za imani – pamoja na hoja zake ambazo zinaithibitisha – inathibitisha nguzo nyingine zilizobaki. Hapo inakuwa kila nguzo basi ni hoja ya kukinaisha kubwa ya kila nguzo katika nguzo nyingine. Kwa hiyo basi ambaye hawezi kujeruhi nguzo zote pamoja na dalili zake zote anashindwa jumla – kwa upande wa hakika – kukanusha nguzo moja katika hizo, na kuivunja hakika moja katika hakika zake, isipokuwa mkanushaji afumbe macho yake na ang’ang’anie kutokukubali au kukataa, wakati huo basi atauingia ukafiri wa kupinga, na kwa kupita kwa muda hilo litampeleka katika ukafiri halisi, basi ubinadamu wake unakosekana na kuelekea katika moto wa kimaada, achilia mbali ambao yeye yumo ndani yake miongoni mwa moto wa kimaanawy. Kama tulivyobainisha kwa ufupi katika masuala ya (Tunda), kujulisha kwa nguzo za imani juu ya ufufuo vivyohivyo hapa tutabainisha kwa ishara za muhtasari mno na majumuisho wa maana ya kina kubwa ya aya hii tukitegemea uangalizi wake (s.w). Na hiyo ni katika nukta sita: Nukta ya kwanza Hakika imani ya (Kumwamini Allah) kwa hoja zake za kukinaisha inathibitisha imani ya Akhera pamoja na kuthibitisha kwake baki ya nguzo nyingine za imani. Kama ilivyowekwa wazi katika (Suala la saba). Naam, hakika ufalme wa kiungu na uweza wake wa azali na nguvu yake yenye kubaki na utajiri wake wa hali zote na utawala wa kiungu wa milele wa kudumu ambao unaendesha ulimwengu huu usio na mpaka - pamoja na mahitaji yake yote ya lazima na yaliyo muhimu - kama kuendesha kasri au mji. Na ambayo inasarifu mambo yake yote ndani ya mpangilio na mizani na kuigeuza kulingana na hekima nyingi. Na ambayo inaendesha atomu na sayari na kumwandaa nzi na nyota kwa pamoja kama askari watiifu wa jeshi lililonadhimiwa, na ambayo inaendesha vyote - ndani ya matakwa yake na amri yake - katika maonesho makubwa ya jumla ya uja ulio takata, kupitia mazoezi matukufu, majaribio na mazoezi ya majukumu na kuyafundisha, kwa utendaji na uchangamfu wa kudumu na kutembea na kuzunguka kwa kuendelea. Je, inayumkinika, au je inaingia akilini, hapana bali je, kuna uwezekano wowote katu ya kuwa kusiwepo makao ya kubakia, na mamlaka ya kudumu, na kudhihiri kwa kudumu milele na udhihirisho wa milele katika makazi ya milele kwa mfano wa ufalme huu wa milele na kwa mfano wa utawala huu wa kubakia daima? Hasha na sivyo hivyo! Na mara elfu sivyo hivyo. Basi ufalme wa Uungu wa Allah (s.w) na adhama yake kwa hiyo, na aghalabu ya majina ya Allah Mazuri – kama ilivyokuja katika (Suala la saba) - na dalili zote na hoja za kupasa kuwepo kwake (s.w), zote zinashuhudia juu ya Akhera na kuihitajia. Basi ni ngome kuu ilioje nguzo hii adhimu ya imani na ni nukta madhubuti ilioje kuiegemea! ehe basi tambua hilo na ulisadiki kana kwamba unaliona. Kisha hakika imani ya (Kuamini Allah (s.w)) kama isivyowezekana kuwa bila ya (Imani ya Akhera), vivyo hivyo haiyumkiniki wala haingii akilini kuwepo (Imani ya Allah (s.w)) bila ya (Imani ya mitume) - kama ilivyoelezwa kwa ufupi katika (Risala ya ufufuo) -. Na hiyo: Hakika Allah (s.w) ambaye ameumba ulimwengu huu kwa kudhihirisha kuwa yeye ni Mungu na Mwabudiwa kwa namna ya kitabu cha Mtegemewa na waja chenye kupewa mwili kiasi kila ukurasa katika kurasa zake unaelezea maana ya kitabu, na kila mstari katika mistari yake unadhihirisha maana ya ukurasa, na ameiumba kwa umbo la Qur’an ya subuhana yenye kupewa mwili kwa kiasi kwamba kila aya katika aya zake za kimaumbile, na kila neno katika maneno yake, bali hata herufi kati yake na kila nukta ni katika nafasi ya muujiza inamtukuza na kumtakasa, na ameiumba katika sura ya msikiti wa Mwingi wa rehema mkubwa na ameupamba kwa kiasi kisichokuwa na mpaka katika aya na nakshi zenye hekima, kiasi kwamba kila pembe katika pembe zake kuna kundi lililozama katika aina ya ibada ya kimaumbile kwa Muumba wao Mwingi wa rehema. Je, inayumkinika kwamba huyu Muumbaji Mwaabudiwa wa haki asitume Maustadhi ili wasomeshe maana ya yaliyomo kwenye kitabu kikubwa na kuelimisha yaliyomo ndani yake? Au Je, inayumkinika asitume wafasiri ili wafasiri aya za Qur’an hiyo iliyopewa mwili ya Mtegemewa na kila mja?. Na je, inayumkinika kwamba asiteue maimamu wa msikiti huo mkuu ili kuwaongoza wale wanaoabudu kwa mitindo na namna mbali mbali za ibada?. Au je, inayumkinika Maustadhi wafasiri na maimamu hao asiwape amri za kifalme? Hasha na hapana na mara elfu hapana! Kisha hakika Muumba Mwenye kurehemu Mwenye ukarimu ambaye ameumba ulimwengu huu ili kudhihirisha uzuri wa rehema yake kwa wenye utambuzi na wema wa upole wake kwao na ukamilifu wa ulezi wake kwao, na ili awahimize kushukuru na kuhimidi ameuumba kwa namna ya nyumba kubwa ya ugeni na maonesho ya kupendeza mapana na mahali pa matembezi pazuri pa kupendeza. Na ameandaa ndani yake kiasi kisicho na mpaka katika neema zenye ladha anuai na amepangilia humo kiasi kisichokuwa na mpaka katika maajabu ya ufundi yenye kupendeza. Je, inayumkinika kwamba huyu Muumba Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu asizungumze kupitia Wajumbe wake na wenye utambuzi katika viumbe vyake katika nyumba ya ugeni yake hii ya kifahari. Au je, inaingia akilini kwamba asiwajulishe majukumu ya shukurani yao na namna ya kukiri kwao mkabala na neema hizo kubwa, na majukumu ya uja wao upande wa rehema zake enevu na upendo wake wa dhahiri?! Hapana, kisha mara elfu elfu hapana! Kisha hakika Muumba ambaye anapenda uumbaji na ufundi wake na anataka kuleta kumstaajabia na kumthamini bali anataka watu watambue uzuri wake na kumtukuza kwa dalili ya kuweka kwake hisia kwa maelfu ya aina za vionjo kwenye vinywa basi Allah (s.w) hujitambulisha kwa kila kiumbe katika viumbe vyake na kwa hiyo anadhihirisha aina fulani katika uzuri wake na kuufanya mahali pa upendo wa viumbe wake, akaupamba ulimwengu huu kwa uzuri wa ufundi wake na viumbe wake. Basi je, inaingia akilini kwamba huyu Muumba Fundi wa ajabu asizungumze na mwanadamu ambaye ni Bwana wa viumbe?. Na je inayumkinika kwamba asitume Wajumbe kutokana na watukufu hawa, ziwe hizo kazi nzuri bila kuthaminiwa na uzuri wa majina hayo mazuri yenye kufurutu ada bila kutambuliwa uzuri wake wala kustaajabiwa, na utambulisho wake na kupendezesha kwake kusiwe na mkabala wowote?! hasha na hapana kisha mara elfu hapana! Kisha hakika mzungumzaji mjuzi ambaye anaitikia – katika wakati munasibu - maombi ya wenye uhai wote, akiitikia mahitaji yao ya kimaumbile na kutoa msaada kwa unyenyekevu wao na matakwa yao yanayoelekezwa kwake kwa ulimi wa hali, basi anaongea kwa uwazi na kimatendo na kwa hali kwa hisani zake kwao zisizokuwa na ukomo na neema zake kwao zisizokuwa na mpaka hali akiwa anadhihirisha makusudi, hiari na matakwa. Basi je, inayumkinika na je, inaingia akilini mzungumzaji huyu mjuzi azungumze na kiumbe mdogo mno aliye hai kwa kimatendo na kwa hali na kusaidia ugonjwa wake na kumsaidia kwa hisani yake na kukidhi haja zake, kisha asiweke wakuu wa kimaanawy kwa mwanadamu ambaye ni bwana wa viumbe wengi wa ardhini, na yeye ni khalifa wa Allah (s.w) katika ardhi yake, na yeye ni natija iliyoteuliwa kutoka katika viumbe?. Na je inaingia akilini asiseme nao kwa kauli na maneno kama anavyoongea na kila mwenye uhai kimatendo na kwa hali?. Na je, inawezekana asitume pamoja naye amri zake, nyaraka na vitabu vyake vitakatifu? Hashalillah, kisha mara elfu hapana! Na kama hivi (Imani ya kuamini Akhera) pamoja na hoja zake thabiti za kukinaisha inathibitisha (Kuamini vitabu vyake) vitakatifu (Mitume wake) watukufu (a.s). Kisha ambaye ameufanya ulimwengu ungurume kwa hakika ya Qur’an na kuremba sauti kwa hakika hiyo, na ambaye amemjua na kumjulisha Muumba wa ajabu kwa namna kamili zaidi akampenda na kuwafanya wengine wampende, na akatimiza shukurani yake kwake na kuwajulisha wengine kumshukuru, bali ameifanya ardhi inakariri (Subuhanallah, Alhamdulillah na Allahu Akbar) hata ikazisikilizisha mbingu za juu, ambaye amekutanisha ulezi wa kiungu uliyo dhahiri wa Muumba kwa uja mkunjufu wa jumla, akaongoza robo ya wanadamu kwa idadi na nusu yao kwa aina ndani ya miaka elfu moja na mia tatu uongozi ambao kutumia uongozi huo ameamsha hisia za bara na bahari na kuzijaza shauku na mapenzi, na ambaye ameinong’oneza Qur’an katika sikio la ulimwengu na kwa kitambo cha zama zote kuhusu makusudio ya kiungu, akatoa somo kubwa na akalingania malinganio matukufu, akidhihirisha majukumu ya mwanadamu na thamani yake, na kwa kubainisha cheo chake, huyo ni Muhammad (s.a.w) mwaminifu mkweli mwenye kusadikishwa kwa miujiza elfu moja na mmoja. Je, inayumkinika mja huyu mtukufu mteule asiwe mtume mtukufu zaidi wa mwaabudiwa wa haki?. Na je, inayumkinika asiwe mtume wake mtukufu?. Hasha na hapana, mara elfu elfu hapana. Basi hakika ya (أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا الله) pamoja na hoja zake kwa hiyo inathibitisha hakika ya (أَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا رَسُوْلُ الله) Kisha hakika Muumba ambaye amejaalia viumbe wake wanabadilishana maneno kwa maelfu ya lugha na yeye ndiye ambaye anasikia maneno ya wote na kuyaelewa, je, inayumkinika kwamba yeye asiongee? Hapana kisha hapana! Na je, inaingia akilini kwamba asijulishe makusudio yake ya kiungu kwa kitabu kikubwa kama Qur’an tukufu ambayo inajibu maswali matatu ambayo akili zina tahayari mbele yake: Wapi vinatokea viumbe hivi? Na hatima ni wapi? Na kwa nini vinakuja baada ya vingine kisha havikai bila kupotea? Hapana. Qur’an tukufu ambayo imetia nuru karne kumi na tatu na kuzipa mwanga, na ambayo wanapokezana kila saa ndimi mia moja milioni kwa heshima na utukuzo wote, na iliyoandikwa vifuani mwa mamilioni ya mahafidhi kwa kila heshima na utukufu, na ambayo imeongoza kwa kanuni zake sehemu kubwa ya wanaadamu, na imelea nafsi zao na kutakasa roho zao na kusafisha nyoyo zao na kuziongoza akili zao, na ambayo ni muujiza wa milele kama tulivyobainisha muujiza wake kwa namna arobaini katika Risale-i Nur, ikabainisha kwamba ina muujiza kwa watu kila tabaka miongoni mwa tabaka arobaini (kama ilivyokuja katika (Andiko la kumi na tisa) lenye karama ya ajabu). Qur’an hii tukufu kwa haki kabisa imestahiki kuitwa: (Maneno ya Allah (s.w)) Muhammad (s.a.w) akawa pamoja na maelfu ya miujiza yake ni muujiza wake wa dhahiri. Je, inayumkinika Qur’an hii tukufu isiwe maneno ya yule mzungumzaji wa azali (s.w)? Na je, inayumkinika zisiwe amri za Muumba huyo wa milele (s.w)? Hashalillah na hapana na hapana mara elfu elfu hapana! Basi (Imani ya Allah) pamoja na hoja zake kwa hiyo inathibitisha kuwa Qur’an ni maneno ya Allah (s.w). Kisha hakika Mfalme mtukufu ambaye anajaza uso wa dunia kwa wenye uhai kisha anaupakua, hali ya kuimarisha dunia yetu kwa wenye utambuzi ili wamtambue (s.w), kumwabudu na kumsabihi. Je, inayumkinika kwa mfalme huyu mwenye utukufu aziache mbingu na nyota zikiwa tupu, wala asiziimarishe kasri hizo za mbinguni kwa wenyeji na wakazi wanaolingana nazo? Je inayumkinika kuacha (Mfalme huyu mtukufu) ufalme wa ulezi wake wa kiungu katika mamlaka zake kunjufu zaidi bila ya haiba na utukufu na bila wafanya kazi wenye kuamriwa na bila ya mabalozi Mitume na bila ya watazamaji waangalizi na bila watazamaji wenye kupendezwa, na bila waja wakirimiwa na bila ya raia watiifu? Hashalillah (s.w) na hapana kwa idadi ya malaika. Hakika Mtawala Mwingi wa hekima Mjuzi wa kila kitu Mwenye kurehemu ambaye ameandika huu ulimwengu kwa muundo wa kitabu, hata amesajili historia ya maisha ya kila mti katika kila mbegu miongoni mwa mbegu zake, na kusajili majukumu ya maisha ya kila jani na majukumu ya kila ua katika kokwa zake zote. Na akaandika matukio yote ya uhai ya kila mwenye utambuzi katika nguvu zake za kuhifadhi ndogo kama punje ya haridali. Na kuhifadhi kila amali katika ufalme wake wote na kwa kila tukio katika ofisi za ufalme wake kwa kuchukua picha zake mbali mbali, na ambaye ameumba pepo, moto Sirata na mizani kubwa kwa ajili ya midhihirisho na kuthibiti kwa uadilifu, hekima, na rehema ambayo ni msingi muhimu kabisa wa ulezi wa kiungu. Je inayumkinika kwa mtawala huyu Mwingi wa hekima na huyu Mjuzi Mwenye kurehemu asisajili matendo ya mwanadamu ambayo yanaambatana na viumbe?. Na je inayumkinika kwamba asiandike matendo yake kwa ajili ya thawabu na adhabu na asiandike maovu yake na mema yake katika mbao za Kadari?! Hashalillah na hapana kwa idadi ya herufi za yaliyoandikwa katika Lauhul Mahafudhi kwa ajili ya Kadari. Yaani hakika ya (Kumwamini Allah) pamoja na hoja zake inathibitisha hakika ya Imani ya (Kuamini malaika) kama inavyothibitisha pia hakika ya (Kuamini Kadari) uthibitisho wa kukinaisha kama jua ambalo linadhihirisha mchana na mchana ambao unajulisha jua. Na kama hivi nguzo za kiimani zinathibitishana. Nukta ya pili Hakika yote ambayo vitabu na nyaraka za mbinguni zimelingania na mbele yake ni Qur’an tukufu na Daawah zote ambazo wamezitekeleza manabii (a.s) na mbele yao ni Muhammad (s.a.w), zinazunguka katika misingi thabiti na nguzo maalum. Na wote wamejitahidi kuthibitisha misingi na kuifundisha kwa wengine. Kwa hiyo hoja zote na dalili zote zinazoshuhudia unabii wao na ukweli wao zote kwa pamoja zinaelekea katika misingi hiyo na nguzo hizo jambo ambalo linaongeza nguvu na ustahiki. Na misingi hiyo si mingine isipokuwa ni kuamini Allah (s.w), siku ya mwisho, malaika wake, vitabu vyake, mitume wake na kadari kheri yake na shari yake ni kutoka kwa Allah (s.w). Kwa hiyo haiyumkiniki kutenganisha kati ya nguzo sita za imani kabisa, kwani kila nguzo katika nguzo zinathibitisha nguzo zote kwa ujumla, bali inahitajia na kuilazimisha, kwa hiyo nguzo sita zote hazikubali kugawika kamwe, na jumla isiyokubali kugawanyika abadani. Kama ilivyo kila tawi miongoni mwa matawi ya mti uliobarikiwa (Mti wa Tuba) ambao shina lake linaloendelea mbinguni, na kila tunda katika matunda yake na kila jani katika majani yake linaegemea juu ya uhai wa milele wa mti huo, haiyumkiniki kwa yeyote kukanusha uhai wa jani moja linaloungana na mti huo maadamu hawezi kukanusha uhai wa mti huo uliyo dhahiri udhahiri wa wazi kama jua. Na ikiwa ataukanusha mti huo utamkadhibisha kwa idadi ya matawi yake, matunda yake, na majani yake na kumnyamazisha, kadhalika imani na nguzo zake sita ipo katika sura hiyo hiyo. Nia ilikuwa imefungwa juu ya kubainisha nguzo sita za imani katika nukta sita na katika kila nukta moja kuna nukta tano zenye maana. Na makusudio yalikuwa kujibu swali lenye kuamsha mawazo lililopatikana kwenye utangulizi kwa ufafanuzi zaidi na ulio wazi, isipokuwa vizuizi na vipingamizi vimezuia hilo. Licha ya kuwa ninafikiri kwamba (Nukta ya kwanza) haikuacha njia yoyote ya kufafanua zaidi kwa wenye ufahamu kwa sababu hiyo ni kipimo tosha cha maudhui. Na kama hivi imefafanuliwa kikamilifu kwamba, ikiwa Mwislamu atakanusha hakika yoyote ya imani, hakika ataporomoka katika ukafiri halisi, kwani nguzo za imani ni mnyororo iliyoungana pamoja, Uislamu umepambanua na kubainisha yale yaliyofupishwa katika dini nyingine. Basi Mwislamu ambaye hamtambui Muhammad (s.a.w) na hamsadiki hatomjua Allah (s.w) (kwa sifa zake) na hataitambua Akhera vilevile. Imani ya Mwislamu ni yenye nguvu na imara kwa kiwango ambacho haitetereki kamwe na wala haiachi nafasi ya kukanusha kamwe, kwa sababu ya kuegemea kwake hoja nyingi sana hata kana kwamba akili inalazimika kukubali imani hii. Nukta ya tatu: Mara moja nilisema: “Alhamdulillah” kisha nikatafuta neema kubwa sana iliyo sawa na maana yake kunjufu mno ikapita kwenye moyo fungu la maneno lifuatalo: اَل۟حَم۟دُ لِلّٰهِ عَلَى ال۟اٖيمَانِ بِاللّٰهِ وَعَلٰى وَح۟دَانِيَّتِهٖ وَعَلٰى وُجُوبِ وُجُودِهٖ وَعَلٰى صِفَاتِهٖ وَاَس۟مَائِهٖ حَم۟دًا بِعَدَدِ تَجَلِّيَاتِ اَس۟مَائِهٖ مِنَ ال۟اَزَلِ اِلَى ال۟اَبَدِ [Alhamdulillah kwa kumwamini Allah, na juu ya upekee wake, na juu ya kupasa kuwepo kwake na sifa zake, na majina yake, shukurani kwa idadi ya midhihirisho ya majina yake kutokea azali hadi milele]. Nikaichunguza na kuiona inaendana kabisa na maana, nayo ni kama ifuatavyo:
[Jibu la kutosheleza na kukinaisha juu ya upingaji kuhusu kukariri ndani ya Qur’an] Ndugu zangu wapendwa wa dhati! Nilikuwa ninasumbuliwa na hali mbaya ya mgongano wakati nikiandika maudhui hii, kwa hiyo imechukuliwa na kiasi fulani cha kufumbika maana kwa sababu ya kubaki kwake kama ilivyo kuja kwa msukumo wa mawazo. Lakini nimetambua kwamba hizo ibara zenye kuchanganya zinabeba muujiza wa kuvutia. Basi ee majuto yangu mimi! Kwa kushindwa kwangu kutimiza haki ya muujiza huu katika ufundi wa kuelezea vema. Basi ibara za risala vyovyote zitakavyo kuwa zenye nuru fifi isipokuwa zinahesabika - kwa upande wa kuambatana kwake na Qur’an tukufu - ni (ibada ya kifikira) na (chombo) lenye kukusanya lulu za nafsi za juu, basi matarajio ni kuwa msiangalie gamba lake mtazame kwa makini lulu zake zenye kung’ara zilizomo ndani yake. Mkiziona zenye kufaa hasa basi zifanyeni (Suala la kumi) la Risala ya matunda, na kama si hivyo basi ifanyeni kuwa ni barua tu ya majibu kuhusu pongezi zenu. Ilikuwa dharura kwangu kuiandika kwa ufupi sana kutokana na hali niliyokuwa ninasumbuka nayo ya mlo mbaya na maumivu ya maradhi, hadi kwamba nimeingiza katika kifungu kimoja cha maneno ya Risala hiyo hakika na hoja nyingi, na niliikamilisha – kwa fadhila ya Allah (s.w) - katika siku mbili za masiku ya mwezi wa Ramadhani yenye baraka basi nataraji msamaha ikiwa kuna kasoro zitakazojitokeza kwangu. Ndugu zangu wa dhati wa kweli Nilipokuwa ninasoma Qur’an – yenye ufasaha wa muujiza – katika mwezi wenye baraka (Ramadhani), nilizingatia maana ya aya thelathini na tatu – ambayo ishara yake ipo katika Risale-i Nur katika (Mwale wa kwanza) - nikaona kwamba kila aya kati yake – bali aya katika ukurasa huo kwenye msahafu na maudhui yake – kana kwamba zinachungulia kwenye Risale-i Nur na wanafunzi wake kwa upande wa kupata sehemu ya mwanga wake na kiasi cha maana yake na hasa aya ya nuru katika Surat An-Nur inaashiria Risale-i Nur kwa vidole kumi, kama vilevile aya ambazo zinazoifuatia – nayo ni aya ya giza - inaangalia wapingaji wa Risale-i Nur na maadui wake bali inawapa fungu kubwa, kwani haifichiki kwamba makamo ya aya hizo na malengo na shabaha zake haziishii katika wakati na mahali maalum, bali inajumuisha zama na mahali pote, yaani inatoka katika hali ya sehemu ya mahali na zama kwenda katika hali ya ujumla, kwa hiyo nimehisi kwamba Risale-i Nur na wanafunzi wake katika zama zetu hizi wanawakilisha – haki ya kuwakilisha – mtu mmoja katika watu wa jumla hiyo yenye kuenea. Hakika ya kauli ya Qur’an tukufu imevuna sifa ya ujumla, ukunjufu kabisa, hali ya juu na kuzungukia kwa ujumla, kwa sababu ya kuwa inatoka moja kwa moja kutoka katika makamo makunjufu kabisa ya ulezi wa kiungu wa jumla wa Mzungumzaji wa azali (s.w), na inaivuna kutoka katika makamo makunjufu makubwa kwa yule ambaye kitabu hiki kimeteremshwa juu yake, ni huyo mtume mtukufu (s.a.w) mwakilishi wa sampuli ya wanadamu na msemeshwa kwa jina la wanadamu wote, bali kwa viumbe wote, na inaipata pia kutokana na waliosemeshwa katika makamo kunjufu pana kabisa la tabaka la wanadamu wote na kwa zama zote, inapata pia kutoka katika makamo makubwa yenye kuzunguka yenye kuchimbuka kutoka kwenye ufasaha wenye kutosheleza wa kanuni za Allah (s.w) zinazoambatana na dunia na Akhera, kwa Ardhi na Mbingu, kwa azali na Milele, kanuni ambazo zinahusu ulezi wake wa kiungu na unajumuisha mambo ya viumbe wote. Basi kauli hii tukufu ambayo imevuna ukunjufu, kuinuka kuzunguka, kuenea kiasi cha kuvuna, inadhihirisha muujiza wa kuvutia na kuzunguka kwenye kuenea kwa kiasi kwamba: Ngazi zake za nje na za kimaumbile ambazo zinapendeza fahamu za watu wa kawaida - nao ndio walio wengi wa wanaosemeshwa - wakati huo huo inatunuku sehemu kubwa kwa ngazi za juu sana za kifikra na tabaka za juu za kiakili, haiwapi wasemeshwa wake kitu kutoka katika maelekezo yake tu, wala haiwatengi wao peke yao kwa mazingatio kutoka katika masimulizi ya kihistoria tu, bali pamoja na hivyo inasemesha kila tabaka kila zama - kwa kuwa kwake ni mmoja katika watu wa kanuni ya jumla - maelezo ya ulingano maridadi mapya kana kwamba ni hivi sasa yanashuka. Na hasa hasa wingi wa ukariri wake: (الْظَّالِمِينَ) …(الْظَّالِمِينَ) na makemeo yake makali kwao na maonyo yake ya kutisha kutokana na kuteremka masaibu ya mbinguni na Ardhini kwa sababu ya dhambi zao na dhulma zao, huzindua macho – kwa kukariri huku – katika kutazama dhuluma zisizokuwa na kifani katika zama hizi, kwa kuonesha aina ya adhabu na masaibu yaliyoshuka kwa kaumu ya Adi, Thamuda na Firauni. Na wakati huo huo inapeleka maliwazo na utulivu katika nyoyo za waumini wenye kudhulumiwa, kwa kueleza kwake kuokoka kwa Mitume watukufu mfano wa Ibrahimu na Musa (a.s). Hakika hii Qur’an tukufu inaongoza kila tabaka la kila zama maongozi ya wazi kwa muujiza wa kupendeza ikibainisha kuwa: (Zama zilizopita) na enzi zilizoondoka ambazo katika mtazamo wa wenye kughafilika wapotevu ni bonde la kukosekana la kitambo sana lenye kutisha na makaburi yaliyoteketea yenye uchungu na huzuni, inayaonesha hali ya kuwa ni ukurasa ulio hai hutoa mazingatio na masomo, na ulimwengu wa ajabu unatweta uhai na kububujika uhai kutoka mawanda ya mbali hadi mbali yake zaidi, na ufalme wa kiungu inafungamana nasi kwa mahusiano inaibainisha kwa – muujiza wake wa kuvutia – ukiwa wazi kana kwamba inashuhudiwa imehudhurishwa mbele yetu kwenye kioo cha sinema, basi wakati mwingine huja na enzi hizo zikiwa hadhiri mbele yetu na wakati mwingine inatuchukua katika zama hizo. Na kwa muujiza wenyewe huo huo inabainisha (Ulimwengu) ambao wenye kughafilika wanauona kuwa ni anga lenye kuogofya bila ya ukomo, na vitu visivyo na uhai vyenye kugongana bila roho yoyote vinabimbirika katika balaa la utengano na maumivu, inaainisha Qur’an ukiwa ni kitabu fasaha, amekiandika Mpweke Mtegemewa kwa haja zote, na mji ulioratibika ameuimarisha Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu, na maonesho mazuri ameyaweka Bwana mlezi Mkarimu ili kutangaza kazi zake. Kwa ufafanuzi huu anatia uhai katika vitu hivyo visivyo na uhai na kujaalia baadhi yake hujitahidi kuvipa msaada vingine, na kila sehemu inaisaidia nyingine kana kwamba inafanya mazungumzo nayo kwa mapenzi ya dhati kabisa, kila kitu kimetiishwa na kila kitu kimekabidhiwa jukumu na wajibu, na kama hivi Qur’an inatoa masomo ya hekima ya hakika na elimu yenye kunawirisha kwa wanadamu, majini na malaika wote. Basi hapana shaka kwamba Qur’an hii tukufu - ambayo ina muujiza huu katika kubainisha – ni yenye kustahiki kuwa na sifa maalum za hali ya juu na sifa pambanuzi takatifu za kuheshimika sana mfano: Katika kila herufi yake moja kuna mema kumi bali wakati mwingine mema elfu moja, bali maelfu ya mema katika nyakati nyingine, na majini na watu wameshindwa kuleta mfano wake japo wangali kusanyika kwa hilo, na kuzungumza kwake na wanadamu wote bali viumbe wote mazungumzo ya ufasaha na yenye hekima. Na pupa ya mamilioni ya watu katika kila zama katika kukihifadhi kwa moyo kwa shauku na kufurahia, na kutochoka kutokana na kukisoma mara nyingi licha ya kukariri kwake, na kutulia kwake tuli kwenye fahamu za watoto wadogo nyororo nyepesi pamoja na kuwemo na vifungu na maeneo yenye kuwachanganya, na kupata ladha wagonjwa na wenye kukata roho kwa kuisikiliza - ambao husumbuka kusikiliza japo maneno madogo sana – na kupita kwa hiyo Qur’an kwenye masikio yao ikiwa tamu nzuri. Na nyingi nyinginezo katika sifa tukufu ilizonazo Qur’an tukufu, hivyo inawapa wasomaji na wanafunzi wake aina kwa aina za furaha za makazi mawili. Na inadhihirisha muujiza wake mzuri pia katika (Mtindo wa maelekezo yake ya fasaha) ambapo imechunga vema hali ya mfikishaji wake ya kuwa ni Ummiyyu (Sio msomaji wa maandishi) kwa kuhifadhi kikamilifu urari wake wa kimaumbile, ni tukufu zaidi kukaribiwa na taklifa, kujifanyisha au ria - vyovyote iwavyo aina yake – basi mtindo wake ni wenye kuchukulika kwa watu wa kawaida ambao wao ndio wenye kusemeshwa walio wengi ikielekeza upole kwenye wepesi wa fahamu zao kwa kushuka kwa maneno yalio karibu na fahamu zao, hali ya kukunjua mbele yao kurasa zilizo wazi kabisa kama kudhihiri kwa mbingu na ardhi, Ikielekeza macho kwenye miujiza ya kiuweza wa kiungu na mistari ya hekima yake ya upeo, vyenye kudhamiriwa chini ya vitu na mambo ya kawaida. Kisha Qur’an tukufu inadhihirisha aina moja wapo katika aina za muujiza wake wa ajabu pia katika (Kukariri kwake kwa ajabu) kwa fungu moja la maneno, au kisa kimoja, na hii wakati wa kuashiria tabaka mbali mbali za wenye kusemeshwa katika maana chungu nzima na mazingatio mengi kwenye aya au kisa hicho, ikahitajika kukariri kwa kuwa hicho ni kitabu cha dua, daawah kama kilivyo pia ni kitabu cha dhikiri na tawhiid, na kila moja kati ya haya yanahitajia kukariri, kila kilichokaririwa katika Qur’an tukufu kwa hiyo katika aya au kisa hakika kinabeba maana mpya na mazingatio mapya. Na inadhihirisha muujiza wake pia wakati wa kuongelea (Matukio ya kisehemu) yaliyotokea wakati wa masahaba wema wakati wa kuteremka kwake na kusimika jengo la Uislamu na misingi ya sharia, hivyo basi unaiona inayachukulia matukio hayo kwa mtazamo wa kutilia muhimu sana, kwa kubainisha kupitia matukio hayo kwamba mambo nyeti zaidi ya matukio madogo mno ya kisehemu, hakika hayo katika mtazamo wa rehema yake (s.w), na yapo ndani ya duara la uendeshaji wake na utashi wake, ukiachilia mbali ya kwamba kwa matukio hayo inadhihirisha sunna za kiungu zinazopita kwenye ulimwengu na kanuni za jumla zenye kuenea. Ongezea juu ya hayo kwamba matukio hayo - ambayo ni sawa na mbegu wakati wa kuasisi Uislamu na sharia – zitatoa matunda katika nyakati zijazo matunda manono ya hukumu na faida mbali mbali. Hakika kukariri kwa uhitaji kunalazimu kukariri, hii ni kanuni iliyothibiti, kwa hiyo Qur’an tukufu imejibu maswali mengi yaliojirudia rudia ndani ya miaka ishirini, ikaelekeza tabaka tofauti za wanaosemeshwa kwa kujibu kwake kwa namna ya kurudiarudia, inakariri mafungu ya maneno ambayo yenye maelfu ya natija, na inakariri maelekezo ambayo ni matokeo ya dalili zisizo na mpaka. na hii wakati wa kutilia mkazo katika fahamu na kuthibitisha kwenye nyoyo juu ya mapinduzi makubwa na mabadiliko ya kutisha kwenye ulimwengu yatakayotokea na kudamirika kutakaousibu ulimwengu na kuvunjika vunjika sehemu, (Zinazounda vitu mbali mbali) na hali itakayofuatia ya ujenzi wa Akhera ya kudumu milele ya kupendeza badala ya ulimwengu huu wenye kutoweka. Kisha inakariri mafungu hayo ya maneno na aya vilevile wakati wa kuthibitisha kwamba sehemu zote (zinazo unda vitu vizima) na jumla (Vitu vizima) kuanzia atomu hadi nyota hakika vipo katika shiko la mmoja wa pekee (s.w) na ndani ya usarifu wake (s.w). Na inakariri pia katika ufafanuzi wake ghadhabu ya kiungu na kuchukia kwa Mola mlezi dhidi ya mwanadamu mwenye kutenda dhuluma nyingi wakati wa kukiuika kwake lengo la kuumbwa, dhuluma ambazo zinachokoza hisia za viumbe na Ardhi na mbingu na chembe za vitu na kukoleza ghadhabu yake dhidi ya watendaji wa dhuluma hizo. Kwa hiyo kukariri kwa sentensi hizo na aya katika kubainisha mambo kama haya makubwa ya kutisha sio tu haihesabiwi kuwa ni upungufu katika ufasaha bali ni katika muujiza katika ubora na ufundi mkubwa na ufasaha wa hali ya juu sana na uwazi – bali ufasaha – wenye kuendana na muktadha wa hali kikamilifu. Kwa mfano: Hakika fungu la maneno (بِسْمِ اللهِ الرَّحْمنِ الرَّحِيمِ) ni aya moja imekariri mara mia moja na kumi nne ndani ya Qur’an Tukufu ni kwa sababu aya hiyo ni hakika kubwa inajaza ulimwengu nuru na mwanga, na kushikamanisha tandiko na arshi kwa fungamano madhubuti - kama tulivyobainisha katika mng’ao wa kumi na nne - hakuna yeyote ila anayo haja kubwa ya hakika hii katika kila wakati - ikiwa hakika hii kuu itakariri mamilioni ya mara uhitaji bado upo unaendelea kuwepo haitazima kiu, kwani sio haja ya kila siku kama mkate bali pia kama hewa na mwanga ambavyo huhitajika sana na kufanyiwa shauku kila dakika. Na hakika ya aya tukufu: (وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ) inakariri mara nane katika Surat Al- Shuaraa, kukariri kwa aya hii tukufu ambayo inabeba maelfu ya hakika katika sura inayoelezea kuokoka kwa manabii (a.s) na adhabu ya kaumu zao, hakika sio kwa sababu yoyote ila ni kwa ajili ya kubainisha: Kwamba dhuluma ya kaumu zao zinagusa lengo la kuumbwa, na kuingilia katika adhama ya ulezi usiyo na mpaka, enzi ya kiungu inahitajia kuwaadhibu kaumu hizo dhalimu kama rehema ya kiungu inavyohitajia kuokoka kwa manabii (a.s). Ikiwa aya hii itakariri maelfu ya mara bado haja na shauku isingemalizika, kukariri hapa ni ufasaha wa hali ya juu wenye muujiza na muhtasari. Vilevile aya tukufu: (فَبِأَيِّ آلَاء رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ) iliyokariri katika Surat (Al- Rahman) na aya tukufu (وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ) iliyokariri katika Surat (Al-Mursalat) zote hizo zinapiga kelele usoni mwa zama zote na kutangaza wazi wazi katika maeneo ya mbingu na Ardhi kwamba ukafiri wa majini na watu na kukanusha kwao neema, na dhuluma zao mbaya kunaamsha ghadhabu za viumbe na kujaalia mbingu na ardhi katika kero na hasira juu yao. Na kuhalifu hekima na makusudio ya kuumbwa kwa ulimwengu. Na kukiuka haki za viumbe wote na kudharau adhama ya kiungu na kuikanusha pia, kwa hiyo aya hizi mbili zinafungamana na maelfu ya mfano wa hakika hizi, na zina umuhimu na nguvu ya maelfu ya masuala, ikiwa zitakariri maelfu ya mara katika kauli ya jumla iliyoelekezwa kwa majini na watu bado dharura ingeendelea kuwepo na haja ingebakia kuwepo. Kwa hiyo kukariri hapa ni balagha ya muhtasari tukufu na muujiza mzuri. Na tunaelezea mfano mwingine kuhusu hekima ya ukariri katika hadithi ya Nabii (s.a.w), Munaajaat wa mtume unaoitwa (Al-Jaushan al-kabiir) ni Munaajaat mzuri wenye kuendana na hakika ya Qur’an tukufu na ni kielelezo kilichopatikana kutokea huko. Tunaona ndani yake fungu la maneno: (سُبْحَانَكَ يَا لاَإِلَهَ إِلَّا أَنْتَ الأَمَانُ الأَمَانُ خَلِّصْنَا مِنَ النَّارِ.. أَجِرْنَا مِنَ النَّارِ.. نَجِّنَا مِنَ النَّارِ) vifungu hivi vinajirudia mara mia moja, vingejirudia maelfu ya mara visingeleta uchovu kwa sababu vinabeba hakika tukufu katika ulimwengu, nayo ni Tawhid na jukumu tukufu sana la viumbe kumwelekea Mola wao mlezi mtukufu nayo ni Tasbihi, Tahamiid na Takdisi na kadhia kuu kabisa ya kihatima ya wanadamu nayo ni kuokoka kutokana na moto na kukomboka kutokana na mateso ya milele, na lengo la lazima sana la uja na la kushindwa kwa mwanadamu nayo ni dua. Na kama hivi tunaona mifano ya misingi hii katika yaliyomo katika aina za ukariri ndani ya Qur’an tukufu. Hata tunaona kwamba inaelezea zaidi ya mara ishirini kuhusu hakika ya tawhiid – kwa uwazi au kwa madhumuni – ndani ya ukurasa mmoja wa Msahafu na hiyo ni kulingana na muktadha na haja ya lazima katika kufahamisha, na balagha ya ufasaha, huamsha shauku kwa kukariri kisomo na kwa hivyo kuipa nguvu balagha na heshima bila ya kusababisha uchovu au unyong’onyo. Sehemu za Risale-i Nur zimefafanua hekima ya kukariri katika Qur’an tukufu na kubainisha hoja zake na kuthibitisha kiasi cha uwiano wa kukariri na kuchukuana kwake na balagha na kiasi cha uzuri wake na kupendeza kwake mno. Ama tofauti ya hekima za sura za Makka na za Madina kwa upande wa balagha na kwa upande wa muujiza na katika upambanuzi na kujumuisha ni kama ifuatavyo: Hakika ya safu ya kwanza ya watu waliosemeshwa na wapingaji huko ndani ya Makka walikuwa Washirikina wa kikuraishi na ni wajinga hawakuwa na kitabu, balagha ikahitajia mtindo wa hali ya juu wenye nguvu na ujumuishi wa kimuujiza wenye kukinaisha, na ukariri unaolazimu kuthibitisha maana katika fahamu, na kwa hiyo aghalabu ya sura za Makka zimeelezea nguzo za imani na ngazi za Tawhiid kwa mtindo uliyo katika upeo wa nguvu na kiwango cha juu, na kwa muhtasari wa kimuujiza mno na kukariri sana imani ya kuamini Allah (s.w) na mwanzo na Akhera, bali imeeleza nguzo hizo za kiimani katika kila ukurasa au aya au katika fungu moja la maneno au katika neno moja, pengine huelezea katika herufi moja, katika kutanguliza na kuchelewesha, au katika maana mahususi au maana ya jumla, katika kuacha kutaja au kutaja. Ikathibitisha nguzo za imani katika mifano ya hali hizo na miundo ya kibalagha kuthibitisha kulikowafanya wanazuoni wa balagha na viongozi wao wasimame kwa kutahayari wakishangazwa mbele ya mtindo huu wa kimuujiza. Risale-i Nur imefafanua na hasa (Neno la ishirini na tano (Miujiza ya Qur’an)) – na nyongeza zake – muujiza wa Qur’an kwa namna arobaini katika namna zake, na kadhalika tafsiri ya (Ishaarat al-I’jazi fy madhan al-Ijaz) kwa lugha ya Kiarabu ambayo inabainisha vizuri muujiza wa Qur’an kwa upande wa namna ya utungo baina ya aya za Qur’an. Risala zote mbili zimethibitisha hasa kuwa juu kwa mtindo wa kibalagha wa kipekee na kuwa juu kwa muhtasari wa kimuujiza. Ama aya za Madina na sura zake katika safu ya kwanza ya wasemeshwa wake na wapingaji wake walikuwa katika Mayahudi na Manasara nao ni watu wa kitabu wenye kumuamini Allah (s.w), kanuni za balagha na mitindo ya kuelekeza na misingi ya tablighi ilihitajia maelezo yenye kuelekezwa kwa watu wa kitabu yawe yanaambatana na hali yao halisi, ikaja na mtindo mwepesi wa wazi laini pamoja na ubainifu na ufafanuzi katika sehemu ndogo ndogo – bila ya mashina na nguzo za imani – kwa sababu sehemu hizo ndogo ndio chimbuko la hukumu za kimatawi na kanuni za kijumla, na eneo la hitilafu katika sharia na hukumu. Kwa ajili hiyo aghalabu tunaziona aya za Madina zikiwa wazi nyepesi kwa mtindo wa ubainifu wa kimuujiza maalum kwa Qur’an tukufu. Lakini kutaja kwa Qur’an mjengo wa nguvu au natija iliyofupishwa au hitimisho lililopangika au hoja yenye nguvu baada ya tukio la sehemu ndogo la kitawi, hufanya tukio hilo la sehemu ndogo kuwa ni kanuni ya jumla enevu, na baada ya hapo hudhamini utekelezaji wake kwa kuimarisha imani ya kuamini Allah (s.w) ambayo huhakikishwa na kutaja vipambanuzi hivyo vya mwisho vilivyofupishwa vya tawhidi, imani na Akhera. Utaona kwamba makamo hayo ya wazi, mepesi yanapata nuru na kuinuka juu kwa vipambanuzi hivyo vya mwisho. - Hakika Risale-i Nur imebainisha na kuthibitisha hata kwa wakaidi kiasi cha balagha ya hali ya juu na sifa pambanuzi za juu na aina za usheheni wa thamani madhubuti za hali ya juu katika mijengo hiyo na vipambanuzi nayo katika sifa kumi na nukta kumi katika nuru ya pili katika mwako wa pili katika neno la ishirini tano linalohusu muujiza wa Qur’an – ukitaka tazama: (إنَّ اللّهَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ) (وَهُوَ الْعَزِيزُ الْرَّحِيمُ) (وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ) (أنَّ اللَّهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ) na mifano yake katika aya ambazo zinafidisha tawhidi na kukumbusha Akhera, na ambazo huishia aghalabu ya aya tukufu, utaona kwamba Qur’an tukufu katika kubainisha hukumu za kisharia za kimatawi na kanuni za kijamii huinua mtazamo wa msemeshwa katika mawanda ya juu ya jumla matukufu, na kubadilisha - kwa vipambanuzi hivi vya kuhitimishia - Mtindo huo mwepesi ulio wazi, mtindo wa ngazi ya juu, Kana kwamba inamhamisha msomaji kutoka katika darsa la kisheria na kwenda katika darsa la tawhiid. Hivyo basi kuthibitisha kuwa Qur’an ni kitabu cha shari, hukumu na hekima, kama kilivyo ni kitabu cha itikadi na imani, nacho pia ni kitabu cha dhikiri na tafakuri, kama pia ni kitabu cha dua na daawah. Na kama hivyo utaona kuwa kuna namna wa ufupisho wa muujiza wenye kung’ara katika aya za Madina ambao sio ile balagha ya aya za Makka kulingana na tofauti ya muktadha na aina za makusudio ya uongozi na ufikishaji. Unaweza kuona namna hii katika maneno mawili tu: ( رَبُّكَ) na (رَبِّ الْعَالَمِينَ) kwani inajulisha upweke kwa ibara ya (رَبُّكَ) na inaelewesha umoja kwa (رَبِّ الْعَالَمِينَ), kwa kujua kwamba umoja unajumuisha pia upekee. Bali unaweza kuona mtindo huo wa balagha ndani ya fungu moja la maneno unakuonesha kwa mfano katika aya moja utendaji wa ujuzi wake mahali pa atomu katika kipenyo cha jicho na mahali lilipo jua katikati ya anga, na kuzunguka kwa uweza wake ambao kwa zana moja unaweka kila kimoja katika mahali pake, ukijaalia jua kana kwamba ni jicho la mbingu unafuatilishia: (وَهُوَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُور) baada ya aya ﴾يُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَيُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ﴿ yaani unafuatilishia utendaji wa ujuzi wake (s.w) katika vilivyojificha vifuani baada ya kutaja kwake adhama ya mbingu na ardhi na kuikunjua mbele ya macho, unafanya ithibiti katika fahamu kwamba yeye anajua yanayopita kwenye nyoyo na mambo yake yaliyojificha ndani ya utukufu wa uumbaji wake wa Mbingu na Ardhi na uendeshaji wa mambo yake. Kimalizio hiki: (وَهُوَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُور) ni aina ya ufasaha unabadilisha mtindo huo mwepesi ulio wazi wa kimaumbile – ulio karibu katika fahamu za watu wa kawaida - unaugeuza kuwa ni mwongozo wa ngazi ya juu na tablighi enevu ya kuvutia. Swali: Hakika mtazamo wa juu juu wa mpito hauwezi kuona yanayoletwa na Qur’an tukufu miongoni mwa hakika zenye umuhimu wala haujui aina ya munasaba na uhusiano kati ya vipande vinavyoelezea Tawhiid ya ngazi ya juu au kufidisha kanuni ya kiujumla, na kati ya tukio la sehemu ndogo lenye kuzoeleka kwa ajili hii baadhi wanadhani kuwa kuna chochote cha kasoro kwenye balagha, kwa mfano haudhihiri munasaba wa kibalagha katika kutaja kanuni kuu: (وَفَوْقَ كُلِّ ذِي عِلْمٍ عَلِيمٌ) kufuatia tukio la sehemu ndogo nalo ni Yusuf (a.s) kumpa makao ndugu yake kwa mpango wa busara. Inaombwa kubainisha siri katika hilo na kufunua pazia la hekima yake? Jibu: Kwamba aghalabu ya sura ndefu na za kati kati - ambazo kila moja kati ya hizo ni kana kwamba ni Qur’an pekee - haitosheki na makusudi mawili au matatu katika makusudio ya Qur’an tukufu manne (Nayo ni: Tawiid, Unabii, Ufufuo, Uadilifu pamoja na Uja) bali kila moja kati ya hizo inabeba kiini cha Qur’an yote na makusudio manne kwa pamoja, yaani kila moja ni kitabu cha dhikri, imani na fikira, kama kitabu cha sharia, hekima na mwongozo. Kila sura katika sura hizo inakusanya vitabu vingi, na inaelekeza masomo mbali mbali, Utaona kwamba kila kituo - bali hata ukurasa mmoja – unafungua milango ya imani mbele ya mwanadamu inahakikishia kuthibiti makusudio mengine, ambapo Qur’an inaeleza yaliyoandikwa kwenye kitabu kikubwa cha ulimwengu na kukibainisha kwa ufasaha, inatia nguvu fahamu za kina za muumini kuzungukia ulezi wake wa kiungu (s.w) kwa kila kitu, na kumwonesha midhihirisho yake ya kutisha katika anga na katika nafsi. Hakika kinachoonekana kuwa uwiano dhaifu, hujengewa makusudio ya jumla, hapo hukutana uwiano madhubuti na mahusiano ya nguvu kwa uwiano huo dhaifu kwa nje, kwa hiyo mtindo unawiana kabisa na muktadha huo, kwa hiyo ngazi yake ya kibalagha inapanda na kuwa ya juu. Swali lingine: Ni nini hekima ya Qur’an kuelezea maelfu ya dalili kwa ajili ya kuthibitisha mambo ya Akhera na kufundisha Tawhiid na kuwapa thawabu wanadamu? Na kuna siri gani katika kuzindua watu watazame mambo hayo kwa uwazi na kwa madhumuni na kwa ishara katuika kila sura bali katika kila ukurasa kwenye Msahafu na katika kila kituo? Jibu: Kwa kuwa Qur’an tukufu inamtanabahisha mwanadamu kuhusu mapinduzi makubwa mno yatakayotokea ndani ya viumbe na katika eneo la yamkini katika historia ya Ulimwengu, nayo ni Akhera. Na inamwongoza kwenye suala kubwa linalomhusu naye akiwa ndiye mbebaji wa amana kubwa na Ukhalifa wa ardhi, hilo ni suala la Tawhiid ambalo furaha na mateso yake ya milele yanazunguka katika eneo hilo. Na wakati huo huo Qur’an inaondoa mfereji wa utata mwingi uliopo bila kukatika, na kuvunja aina ngumu zaidi ya upingaji na ukanushaji wenye chuki. Kwa ajili hiyo lau kama Qur’an itaelekeza mitazamo kwenye kuamini hayo mageuzi ya ajabu na kuwafanya wengine kusadikisha suala hilo kuu kidharura kwa Wanadamu, Naam, ingefanya hivyo maelfu ya mara na kukariri masuala hayo mamilioni ya mara, kwake haihesabiwi kuwa ni Israfu katika Balagha katu, kama kufanya hivyo kusivyoleta uchovu wala unyong’onyo kabisa, bali haja ya kukariri usomaji wa Qur’an haikatiki kwani hakuna suala muhimu wala kubwa zaidi katika uwepo kuliko tawhiid na Akhera. Mathalani: Hakika ya aya tukufu: إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ذَلِكَ الْفَوْزُ الْكَبِيرُ ni bishara ya furaha ya kudumu milele inaieleza aya hii tukufu kwa mwanadamu masikini ambaye anakutana na hakika ya umauti kila wakati, bishara hii kwa hiyo inamwokoa kutokana na kuleta taswira ya umauti kuwa ni kunyongwa kwa milele na kumwokoa – na ulimwengu wake na wapendwa wake wote – kutokana na shiko la kutoweka bali inamtunuku ufalme wa milele na kumpa mavuno ya furaha ya kudumu. Ikiwa aya hii tukufu itakariri mabilioni ya mara katu kukariri kwake hakuhesabiwi kuwa ni Israfu katu wala hakigusi kitu chochote balagha yake. Na kama hivi unaona Qur’an tukufu ambayo inashughulikia mifano ya masuala haya muhimu na kujitahidi kuwakinaisha walengwa wa masuala hayo kwa kusimika hoja zenye nguvu, inayaweka kwa kina kwenye akili na nyoyo mageuzi hayo makubwa na mabadiliko makubwa kwenye ulimwengu, na kufanya kuwa mepesi na wazi mbele yao kama kubadilika nyumba na kugeuka kwa umbo lake. Hapana budi kwamba kuzindua mitazamo kuelekea masuala kama haya – kwa uwazi na kwa madhumuni na kwa ishara - kwa maelfu ya mara ni jambo la kidharura sana bali hilo ni kama dharura ya mwanadamu kuhitajia mkate, hewa na mwanga ambavyo uhitaji wa mwanadamu kwa vitu hivyo hukariri daima. Na mathalani: Hekima ya kukariri kwa Qur’an tukufu وَالَّذِينَ كَفَرُوا لَهُمْ نَارُ جَهَنَّمَ إِنَّ الظَّالِمِينَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ na mfano wa hizo katika aya za kuonya na vitisho. Na kuelezea kwake kwa miundo iliyo katika upeo wa ukali - ni kama vile tulivyothibitisha katika Risale-i Nur kwa namna ya kukinaisha – hakika ukafiri wa mwanadamu hakika ni kukiuka – kukiuka kwa hali ya juu – haki za viumbe na mno ya viumbe, jambo ambalo linaamsha ghadhabu ya mbingu na Ardhi na kujaza kero na chuki katika nyoyo za aina mbali mbali juu ya makafiri, hadi aina hizo zinapiga kofi makafiri hao kwa tufani na mengineyo. Bali hata moto wa jahimu unawaghadhibikia ghadhabu ambayo inakaribia kulipuka kutokana na ukali wake kama ilivyo wazi katika aya: إِذَا أُلْقُوا فِيهَا سَمِعُوا لَهَا شَهِيقًا وَهِيَ تَفُور۞ تَكَادُ تَمَيَّزُ مِنَ الْغَيْظ Lau kama angekariri mfalme wa ulimwengu katika amri zake jinai hilo kubwa (kufuru) na adhabu yake kwa mtindo wa upeo wa kukemea na ukali maelfu ya mara, bali mamilioni ya mara, bali mabilioni ya mara isingehesabiwa hiyo ni israfu kabisa wala upungufu katika balagha, kwa kuangalia ukubwa wa jina hiyo ya jumla na kukiuka haki zisizokuwa na mpaka, na kwa msingi wa kudhihirisha hekima ya haki za raia wake (s.w) na kudhihirisha ubaya usiokoma katika ukafiri wa wakanushaji na udhalimu wao mbaya. Kwani hakariri hilo kwa sababu ya udogo wa mwanadamu na uduni wake bali kwa ukubwa wa ukiukaji wa kafiri na ukubwa wa dhuluma yake. Kisha hakika tunaona kwamba mamia ya mamilioni katika watu tangu elfu na mamia ya miaka wanaisoma Qur’an kwa pupa na shauku na kwa kuihitajia sana bila unyong’nyo wala uchovu. Naam, hakika kila wakati na kila siku hakika ni ulimwengu unaopita na ni mlango unaofungulia ulimwengu mwingine, na kwa hiyo kukariri kwa: (لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ) kwa shauku ya kuihitajia maelfu ya mara kwa ajili ya kuangazia limwengu hizo zenye kutembea zote na kuzinawirisha kwa nuru ya Imani, inafanya fungu hilo la kitawhiid kana kwamba ni taa yenye nuru katika mbingu za limwengu hizo na masiku. Basi kama jambo hili lilivyo hivi katika: (لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ) kadhalika kusoma Qur’an tukufu hutokomeza giza lililogubika juu ya uwingi huo chungu tele katika shahidi zenye kutembea, na kwa limwengu hizo zenye kutembea zenye kurudia upya, na kuondosha kuharibu sura zake zenye kuakisi katika kioo cha uhai, na kufanya hali hizo zinazokuja kuwa ni mashahidi wake siku ya kiama na sio mashahidi dhidi yake. Na kupanda katika ngazi ya maarifa ya ukubwa wa malipo ya jinai, na kumfanya atambue thamani ya maonyo yaliojificha ya mfalme wa azali na milele ambazo zinatawanya ukaidi wa madhalimu matwaghuti, na kumpa shauku akomboke na uchupaji wa nafsi yenye kuamrisha maovu, basi kwa ajili ya hekima hizi zote Qur’an tukufu inakariri inayokariri katika upeo wa hekima kwa kudhihirisha kwamba maonyo mengi ya Qur’an tukufu ni kwa kiasi hiki, na kwa nguvu na ukali na ukariri huu ni hakika kubwa, Shetani anashindwa kwa kuidhania kuwa ni batili na anakimbia kuifikiria kuwa ni mchezo. Naam hakika adhabu ya jahanamu ndio uadilifu wenyewe kwa ajili ya hao makafiri ambao hawasikilizi kabisa maonyo. Na katika vinavyokaririwa vya Qur’an (Visa vya manabii (a.s)), basi hekima katika kukariri kwa kisa cha Musa (a.s) – mathalani - ambacho kina hekima na faida ambayo imo katika fimbo ya Musa (a.s), na kadhalika hekima katika ukariri wa visa vya manabii hakika ni kwa ajili ya kuthibitisha utume wa Muhammad (s.a.w), na hii ni kwa kudhihirisha unabii wa manabii wote ni hoja ya u-haki wa utume wa nabii Muhammad (s.a.w) na ukweli wake, kiasi kwamba hawezi kukanusha isipokuwa anayekanusha unabii wao wote, basi kuutaja basi ni dalili ya utume. Kisha hakika wengi wa watu hawawezi kila wakati na wala hawawafikishwi katika kusoma Qur’an tukufu yote, bali wanatosheka na kilichokuwa chepesi kwao katika Qur’an. Na kutokea hapa hekima inaonekana kuwa wazi katika kufanya kila sura ndefu na ya kati na kati kwa mfano wa Qur’an ndogo, na hivyo kukariri kwa visa ndani ya sura hizo ni kwa mfano wa kukariri kwa nguzo za Imani za lazima. Yaani kwamba kukariri kwa visa ni hitajio la kibalagha na katika kufanya hivyo katu hakuna israfu. Ongezea juu ya hilo ndani yake kuna ujulisho kwamba tukio la kudhihiri kwa Muhammad (s.a.w) ni tukio kubwa sana kwa Wanadamu na suala muhimu mno katika masuala ya ulimwengu. Naam, hakika kuipa dhati ya mtume (s.a.w) makamo makuu na ya juu zaidi katika Qur’an tukufu, na kujaalia (Muhammad Rasulullah) - ambayo inajumuisha nguzo nne katika nguzo za imani - ikiunganishwa na (لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ) ni dalili – na dalili iliyoje – kwamba utume wa Muhammad (s.a.w) ni hakika kubwa ulimwenguni na kwamba Muhammad (s.a.w) ni mbora mno wa viumbe wote na kwamba hakika ya Muhammad (s.a.w) ambayo inawakilisha al -Shakhsiyyat al maanawiyyat (Haiba ya pamoja) ya ujumla ya Muhammad (s.a.w) ni taa yenye kuangaza kwa limwengu zote mbili, na kwamba (s.a.w) ni mwenye stahiki ya makamo haya yenye kufurutu ada kama ilivyo thibitishwa hivyo katika sehemu za Risale-i Nur kwa hoja na dalili nyingi kwa namna ya kukinaisha. Hapa tunaileta mojawapo kati ya elfu moja kama ifutavyo: Hakika yote waliyofanya umati Muhammad wote (s.a.w) katika mema katika zama zote huandikwa mfano wake katika daftari la mema yake mtume (s.a.w), na hii kulingana na kanuni: (Sababu kama mfanyaji) na hakika kutia kwake nuru kwa hakika zote za viumbe kwa nuru aliyokuja nayo haifanyi majini, wanadamu na malaika na wenye uhai katika kushukuru na kuridhia wao peke yao, bali inajaalia ulimwengu wote na mbingu na ardhi vyote kuwa vyenye kumridhia na kuzungumza fadhila zake, na hakika mamilioni ya dua ambazo wema wa umma huu wanazozielekeza kila siku na pamoja na wema katika mabilioni ya dua za kimaumbile zenye kujibiwa ambazo hazirejeshwi - kwa dalili za kukubaliwa kimatendo kunakoshuhudiwa kwa dua za mimea kwa ulimi wa kimaandalizi, na dua za wanyama kwa ulimi wa haja ya kimaumbile - na kutokana na dua za rehema kwa kumswalia na kumsalimu yeye na wanayoyatuma katika waliyoyavuna miongoni mwa mavuno ya kimaanawy na mema kama zawadi, hakika hupelekwa kwake kwanza. Ukiachilia mbali yale yanayoingia katika daftari la mema yake (s.a.w) miongoni mwa nuru zisizo na mipaka kwa wanachosoma umma wake – kwa kusoma tu – Qur’an tukufu ambayo kwa kila herufi miongoni mwa herufi zake – ambazo zinazidi mia tatu elfu – mema kumi na matunda kumi ya kiakhera bali mia bali elfu ya mema. Naam, hakika ya mjuzi wa mambo ya ghaibu (s.w) imetangulia elimu yake na kushuhudia kwamba hakika ya Muhammad ambayo ni haiba ya kimaanawy ya pamoja ya dhati hiyo yenye baraka, itakuwa kama mfano wa mti wa Tuba huko peponi, kwa hiyo akaipa umuhimu mkubwa katika Qur’an yake umuhimu huo mkubwa ambapo yeye ndiye mwenye kustahiki makamo hayo ya juu. Na akabainisha katika amri zake kwamba kupata shufaa yake hakika huwa tu kwa kumfuata yeye na kufuata sunna yake tukufu nalo ni suala kubwa mno katika masuala ya mwanadamu. Bali amechukua kwa jicho la mazingatio – mara kwa mara – hali zake za kibinadamu ambazo ni sawa na mbegu ya mti wa Tuba katika pepo. Na kama hivi hakika za Qur’an zilizokariri zina thamani hii ya juu na ndani yake kuna hekima kiasi kilichomo ndani yake katika hekima, maumbile salama yanaona kwamba katika kukariri kwake kuna muujiza wa kimaanawy wenye nguvu na mpana, isipokuwa ambaye moyo wake na hisia zake za ndani zimeugua kwa tauni ya mrengo wa kimaada, basi anaingia katika kanuni mashuhuri: قَد۟ يُن۟كِرُ ال۟مَر۟ءُ ضَو۟ءَ الشَّم۟سِ مِن۟ رَمَدٍ وَ يُن۟كِرُ ال۟فَمُ طَع۟مَ ال۟مَاءِ مِن۟ سَقَمٍ Huenda mtu akakanusha Mwanga wa jua kwa sababu ya maradhi ya macho Na kinywa hukanusha ladha ya chakula kutokana na ugonjwa
Sehemu ya kwanza: Masikio yangu yaligongwa na habari kabla ya miaka kumi na mbili kwamba mzandiki mkaidi nia yake mbaya imefedheheka na uhabithi wa makusudio yake kwa kutaka kuitafsiri Qur’an, akasuka mpango wa kutisha ili kuidhalilisha heshima yake kwa kujaribu kuitafsiri. Na akasema wazi: Ifasiriwe Qur’an ili idhihiri thamani yake? Yaani ili watu wapate kuona kukariri kwake kusiko kwa lazima! Na tafsiri yake isomwe badala yake! Hadi mwisho wake katika fikira zenye sumu. Isipokuwa Risale-i Nur - kwa fadhili ya Allah (s.w) - imevunja fikira hiyo na kuporomosha mpango huo kabla haujazaliwa kwa hoja zake zenye nguvu na kwa kuenea kwake kupana kila mahali, Ikathibitisha kwa uthibitisho wa kukinaisha kwamba haiwezekani kamwe kuitafsiri Qur’an tafsiri ya hakika na kwamba lugha yoyote isiyokuwa lugha ya Kiarabu fasaha haina uwezo wa kuhifadhi sifa bainifu za Qur’an tukufu na nukta zake nyororo za kibalagha, na kwamba tafsiri za kawaida za kibaadhi ambazo wanadamu wanazifanya hazikai - kwa hali yoyote ile – mahali pa maelezo yenye kujumuisha yaliyo muujiza ya maneno ya Qur’an ambayo katika kila herufi moja miongoni mwa herufi zake kuna mema yanayopanda kutokea kumi hadi elfu, na kwa hiyo haiwezekani kamwe kusoma tafsiri ikiwa badala yake. Licha ya kwamba wanafiki ambao waliojifunza kwa yule mzandiki wamejitahidi kwa majaribio ya hasira katika njia ya shetani ili kuzima nuru ya Qur’an tukufu kwa vinywa vyao. Lakini nilivyokuwa sikutani na yeyote sina ninalojua kuhusu hakika ya hali zinayoendelea, lakini dhana yangu mno niliyoyaeleza huko nyuma ndiyo sababu iliyopelekea kuandika (Suala hili la kumi) juu yangu licha ya dhiki inayonizingira. Sehemu ya pili ya maelezo: Siku moja nilikuwa nimekaa katika ghorofa ya juu ya Hoteli ya (Şehir) baada ya kuruhusiwa kwetu kutoka jela ya (Denizle), nikichunguza miti iliyonizunguka ya (matete) iliyo mingi katika viunga venye sauti za kupendeza na bustani nzuri, niliiona ikiwa na furaha na kwa harakati zake ya kucheza na kuvutia, ikiyumbayumba kwa mashina na matawi yake, na majani yake kutetemeka kwa mguso mdogo sana wa upepo mbele yangu ikadhihiri kwa sura ya wazi na ya kupendeza mno kana kwamba inamsabihi Allah katika duara za dhikiri a tahalili. Mchakatiko huu nyororo umegusa mishipa ya moyo wangu wenye huzuni kutokana na kutengana na ndugu zangu, nami nikiwa na majonzi kutokana na kubakia kwangu peke yangu, ikapita akilini – ghafla – majira mawili ya mapukutiko na ya baridi, mghafala ukanichukua wakati majani yatakapopukutika maji yakaondoka na uzuri pia. Nikawa ninayasikitikia yale mabua mazuri na kuwasikitikia wengine walio hai ambao hudhihiri kwao furaha hiyo ya hali ya juu masikitiko makubwa mpaka macho yangu yalilengalenga machozi na huzuni zikajikusanya juu ya kichwa changu zilizofoka kwa kasi kutokana na kutoweka na utengano unaojaza hii pazia iliyopambwa yenye kufurahisha kwa viumbe! Wakati ambapo nikiwa katika hali hii ya kuhuzunisha tahamaki nuru ambayo hakika ya Muhammad imeileta ikanipa msaada – kama inavyompa msaada kila muumini – ikabadilisha huzuni hizo na majonzi makubwa na kuwa furaha isiyo na mipaka. Nikawa katika neema ya milele na kuridhika kwa daima kutokana na hakika ya Muhammad ambayo imeniokoa neema moja katika neema za nuru zake zisizokuwa na mpaka neema hiyo ikaeneza maliwazo katika pande za nafsi zangu na katika kina cha moyo wangu na hiyo ilikuwa kama ifuatavyo: Mtazamo huo wenye kughafilika umeonesha majani hayo laini na miti yenye matawi yenye kubaki bure bila jukumu lolote na bila manufaa yoyote na kwamba hayatikisiki mtikisiko mpole kutokana na ukali wa shauku na furaha bali yanatetemeka kutokana na kishindo cha kukosekana na pia kutengana. Ole wake kwa mtazamo wa mghafala umesibu nukta ya maumbile yaliyowekwa kwangu – na kama kwa mwenzangu – ya kutamani kubakia na kupenda kuishi na kufitinika na mazuri na huruma kwa wana wa kundi moja – ikabadili dunia kuwa ni jahanamu ya kimaanawy na akili kuwa ni kiungo cha mateso na adhabu. Nilipokuwa nina machungu ya hali hii ya kuumiza, tahamaki kwa nuru ambayo Muhammadi ameitumia kunawirisha wanadamu wote inaondosha funiko na kuondosha kizuizi na inaonesha hekima na maana na kazi na majukumu mengi mno yanayofikia idadi ya majani ya miwilo. Risale-i Nur imethibitisha kwamba nyadhifa na hekima hizo zinagawika katika sehemu tatu: Sehemu ya kwanza: Nayo inayaelekea majina mazuri ya Fundi mtukufu. Kama ilivyo fundi mahiri anapotengeneza mashine ya ajabu, wote humsifia na kuipa thamani kazi yake na kubariki ufundi wake, hakika ya mashine hiyo nayo kwa nafasi yake vilevile inambariki fundi wake na kumsifia kwa ulimi wa hali yake, hufanya hivyo kwa kumwonesha kikamilifu natija zilizokusudiwa kwake. Sehemu ya pili: Ni yenye kuangalia katika mitazamo ya wenye uhai na utambuzi katika viumbe yaani inakuwa ni mahali pa mtalaa na mazingatio matamu, hivyo kinakuwa kila kitu kana kwamba ni kitabu cha maarifa na elimu, na hauachi ulimwengu huu - ulimwengu wa kushuhudiwa - ila baada ya kuweka maana yake katika fahamu za wenye utambuzi na kuchapa picha zake katika kumbukumbu zao, na kuingia chapa ya picha yake katika mbao za mifano ya mafaili ya elimu ya Ghaibu yaani haiondoki kutoka katika ulimwengu wa kushuhudiwa kwenda katika ulimwengu wa ghaibu ila baada ya kuingia kwake katika jumla ya maduara ya uwepo mengi na kuchuma aina za uwepo wa kimaanawy, kighaibu na wa kielimu. Naam, madhali Allah yupo, na ujuzi wake unazungukia kila kitu, hapana budi kusiwepo katika ulimwengu wa muumini kukosekana, kutoweshwa, kutokuwepo, mchezo, kufutwa na kutoweka katika pembe ya hakika, wakati ambapo dunia ya makafiri imejaa kukosekana kutengana na kutokuwepo na imejaa mchezo na kutoweka. Na katika yanayofafanua hakika hii yale yanayozunguka katika ndimi ya kauli mashuhuri ambayo: (Mwenye kuwa na Allah (s.w) anacho kila kitu na asiyekuwa na Allah hana chochote). Muhtasari: Hakika imani kama inavyomwokoa mwanadamu kutoka katika kunyongwa kwa milele wakati wa umauti, unaokoa dunia ya kila mtu vilevile kutoka katika giza la kutokuwepo. kukosekana na mchezo. Wakati ambapo ukafiri - na hasa ukafiri halisi - hakika kwa umauti unamfanya huyo mwanadamu asiwepo na kuifanya dunia yake inayomhusu isiwepo na kumtupa katika magiza ya jahanamu ya kimaanawy hali ya kugeuza tamu za maisha yake kuwa ni machungu na maumivu. Na yasikie masikio ya wale ambao wanapendelea zaidi maisha ya dunia kuliko Akhera, na waje na ufumbuzi wa jambo hili ikiwa wao ni wa kweli au waingie ngome ya Imani na wazikomboe nafsi zao kutokana na hasara hii kubwa. سُب۟حَانَكَ لَا عِل۟مَ لَنَٓا اِلَّا مَا عَلَّم۟تَنَٓا اِنَّكَ اَن۟تَ ال۟عَلٖيمُ ال۟حَكٖيمُ Ndugu yenu anayetarajia dua zenu na mwenye shauku nanyi Said Nursî Onuncu Mesele Münasebetiyle Hüsrev’in Üstadına Yazdığı Mektup Çok sevgili üstadım efendim! Cenab-ı Hakk’a hadsiz şükürler olsun, iki aylık iftirak üzüntülerini ve muhaberesizlik ızdıraplarını hafifleştiren ve kalplerimize taze hayat bahşeden ve ruhlarımıza yeni, safi bir nesîm ihda eden Kur’an’ın celalli ve izzetli, rahmetli ve şefkatli âyetlerindeki tekraratın mehasinini ta’dad eden, hikmet-i tekrarının lüzum ve ehemmiyetini izah eden ve Risale-i Nur’un bir hârika müdafaası olan Denizli Meyvesinin Onuncu Meselesi namını alan “Emirdağı Çiçeği”ni aldık. Elhak, takdir ve tahsine çok lâyık olan bu çiçeği kokladıkça ruhumuzdaki iştiyak yükseldi. Dokuz aylık hapis sıkıntısına mukabil, Meyve’nin Dokuz Meselesi nasıl beraetimize büyük bir vesile olmakla güzelliğini göstermiş ise Onuncu Meselesi olan çiçeği de Kur’an’ın îcazlı i’cazındaki hârikaları göstermekle o nisbette güzelliğini göstermektedir. Evet, sevgili üstadım, gülün çiçeğindeki fevkalâde letafet ve güzellik, ağacındaki dikenleri nazara hiç göstermediği gibi; bu nurani çiçek de bize dokuz aylık hapis sıkıntısını unutturacak bir şekilde o sıkıntılarımızı da hiçe indirmiştir. Mütalaasına doyulmayacak şekilde kaleme alınan ve akılları hayrete sevk eden bu nurani çiçek, muhtevi olduğu çok güzelliklerinden bilhassa Kur’an’ın tercümesi suretiyle nazar-ı beşerde âdileştirilmek ihanetine mukabil; o tekraratın kıymetini tam göstermekle, Kur’an’ın cihan-değer ulviyetini meydana koymuştur. Sâliklerinin her asırda fevkalâde bir metanetle sarılmaları ile ve emir ve nehyine tamamen inkıyad etmeleriyle, güya yeni nâzil olmuş gibi tazeliği ispat edilmiş olan Kur’an-ı Mu’cizü’l-Beyan’ın, bütün asırlarda, zalimlerine karşı şiddetli ve dehşetli ve tekrarlı tehditleri ve mazlumlarına karşı şefkatli ve rahmetli mükerrer taltifleri, hususuyla bu asrımıza bakan tehdidatı içinde zalimlerine misli görülmemiş bir halette, sanki feze’-i ekberden bir numuneyi andıran semavî bir cehennemle altı yedi seneden beri mütemadiyen feryad u figan ettirmesi ve keza mazlumlarının bu asırdaki küllî fertleri başında Risale-i Nur talebelerinin bulunması ve hakikaten bu talebeleri de ümem-i sâlifenin enbiyalarına verilen necatlar gibi pek büyük umumî ve hususi necatlara mazhar etmesi ve muarızları olan dinsizlerin cehennemî azapla tokatlanmalarını göstermesi hem iki güzel ve latîf hâşiyelerle hâtime verilmek suretiyle çiçeğin tamam edilmesi, bu fakir talebeniz Hüsrev’i o kadar büyük bir sürurla sonsuz bir şükre sevk etti ki bu güzel çiçeğin verdiği sevinç ve süruru, müddet-i ömrümde hissetmediğimi sevgili üstadıma arz ettiğim gibi kardeşlerime de kerratla söylemişim. Cenab-ı Hak, zayıf ve tahammülsüz omuzlarına pek azametli bâr-ı sakîl tahmil edilen siz sevgili üstadımızdan ebediyen razı olsun. Ve yüklerinizi tahfif etmekle yüzlerinizi ebede kadar güldürsün, âmin! Evet, sevgili üstadım, biz; Allah’tan, Kur’an’dan, Habib-i Zîşan’dan ve Risale-i Nur’dan ve Kur’an dellâlı siz sevgili üstadımızdan ebediyen razıyız. Ve intisabımızdan hiçbir cihetle pişmanlığımız yok. Hem kalbimizde zerre kadar kötülük etmek için niyet yok. Biz ancak Allah’ı ve rızasını istiyoruz. Gün geçtikçe, rızası içinde, Cenab-ı Hakk’a vuslat iştiyaklarını kalbimizde teksif ediyoruz. Bilâ-istisna bize fenalık edenleri Cenab-ı Hakk’a terk etmekle affetmek ve bilakis bize zulmeden o zalimler de dâhil olduğu halde, herkese iyilik etmek, Risale-i Nur talebelerinin kalplerine yerleşen bir şiar-ı İslâm olduğunu, biz istemeyerek ilan eden Hazret-i Allah’a hadsiz hudutsuz şükürler ediyoruz. Çok kusurlu talebeniz Hüsrev
Hakika ya mti mtakatifu wa nguzo za imani za kijumla una matunda manono mojawapo ni pepo, na lingine ni furaha ya milele, na la tatu ni kumwona Allah (s.w). Na kwa kuwa Risale-i Nur imeweka wazi mamia ya matunda hayo - ya jumla yake na baadhi yake – pamoja na hoja zake zenye nguvu katika (Siraji an-Nur) tunaelekeza huko na hapa tunaashiria vielelezo vichache tu vya matunda ya kisehemu bali sehemu ya sehemu na iliyo mahususi katika matunda hayo mazuri. Mojawapo: Siku moja nilikuwa ninaomba dua lenye ujumbe huu: “Ewe mola nakuomba kwa kutawasali kwako kwa utukufu wa Jibril, Mikail, Israfil na izrail na kwa shufaa yao unihifadhi kutokana na shari za majini na watu” na mara nilipolitaja jina la Izrail – ambao utajo wake unawajaza watu hofu na kutetemeka - nilihisi hali yenye ladha katika upeo wa utamu na maliwazo, nikamshukuru Allah (s.w) kwa kusema: (Alhamdulillah), na nikaanza kumpenda Izrail mapenzi ya dhati kwa kuwa yeye ni mmoja kati ya malaika ambao inazingatiwa kuamini uwepo wao nguzo katika nguzo za imani. Tutaashiria kwa muhtasari sana tunda dogo kutoka katika matunda mengi ya kumwamini malaika huyu. Katika hizo: Hakika ya thamani ya aliyokuwa nayo mwanadamu na kikubwa sana anachokipupia na kukitetea na anajitahidi kukihifadhi, bila shaka ni roho yake. Hakika nilihisi kwa yakini furaha ya kina kwa mwanadamu kusalimisha kitu kitukufu mno alichonacho – nacho ni roho yake – mkononi mwa (Mwenye nguvu mwaminifu) ili aihifadhi isichezewe, isipotee na kutoweka. Kisha nikakumbuka malaika waliowakilishwa kusajili amali za mwanadamu nikakuta kuwa wana matunda matamu mno kama haya: Kati ya hayo: Kila mwanadamu ili amali zake nzuri zipate kukaa milele na maneno yake mazuri yabakie hujitahidi kuyahifadhi na kuyalinda yasipotee sawa iwe kwa njia ya kuandika au ushairi au hata kwa mkanda wa sinema, na hasa ikiwa amali hizo zina matunda yake ya kubaki peponi, hupata shauku sana kuyahifadhi. Na waandishi watukufu wamesimama karibu ya mabega ya mwanadamu ili wamdhihirishe katika shuhuda za milele, na ili wapige picha amali zake katika mandhari ya kudumu milele, ili wenye amali hizo walipwe na wapate zawadi za kudumu na za thamani. Nimepata ladha ya matunda haya kwa utamu nisioweza kuuelezea. Na waliponiepusha watu wa upotevu na sababu za maisha ya kijamii na kuniweka mbali na vitabu vyangu, wapendwa wangu na wahudumu wangu na kila kilichokuwa kikinipa maliwazo, na wakanitupa katika makazi ya ugeni na upweke, na nilikuwa katika dhiki na kukereka kutokana na hali yangu kwa kiwango cha kuwa nikihisi kuwa dunia iliyo tupu itavunjikia kichwani kwangu. Wakati nikiwa katika hali hiyo tahamaki tunda moja katika matunda ya kuamini malaika ikaja kunipa msaada na ikaangazia pande za dunia yangu yote na kunawirisha ulimwengu unaonizunguka na kuuimarisha na malaika na kujaza wakazi wa roho nzuri hadi ikaingia furaha kila mahali. Na pia ikanionesha vipi dunia ya watu wa upotevu ilivyojaa kelele za upweke na majuto ya mchezo na giza. Wakati mawazo yangu yakiwa yanafurahia kupata ladha ya tunda hili tahamaki inapokea tunda katika matunda mengi – yalio mfano wa haya – ya kuamini mitume (a.s), ikaonja hasa na moja kwa moja nikahisi kuwa Imani yangu imepanuka na kukunjuka hadi ikawa kitu kizima jumuishi, ambapo zama hizo zilizopita zote ziliangaza kwangu na kuangaza kwa nuru ya kusadiki na kuwaamini, hata nikahisi kana kwamba ninaishi pamoja nao, akawa kila nabii katika manabii anasadikisha kwa maelfu ya usadikishaji juu ya nguzo za imani ambazo amekuja nazo na kuzilingania nabii wa mwisho Muhammad (s.a.w), jambo ambalo lilimnyamazisha Shetani. Kisha swali lenye jibu la kutosheleza lililopo katika mng’ao (Hekima ya kujikinga) likaja haraka moyoni nalo ni: Kwamba watu wa imani ambao wana mfano wa matunda haya ya imani na mfano wa faida hizi na natija tamu bila ukomo na wana natija nzuri za mema na manufaa yake mengi, na wana uangalizi wa kudumu kutoka kwa (Arhamu Ar-Rahimina) na tawfiki yake na rehema yake, vyote hivyo vinawapa nguvu na egemeo, basi ni kwa nini watu wa upotevu aghalabu wanawashinda, bali ishirini katika watu wa upotevu wanaweza kuwashinda mia moja kati yao na kuwateketeza?! na katikati ya tafakuri hii ilipita moyoni mwangu: Ni kwa nini Qur’an tukufu inakusanya mkusanyo huu mkubwa kwa watu wa Imani kwa kutaja msaada wa Allah (s.w) kwao kwa kuwaleta malaika na hali ya kuwa wanakabiliana na madhila duni dhaifu ya kishetani? Kwa kuwa Risale-i Nur imefafanua hekima ya hilo kwa hoja zenye kukinaisha hapa tutaashiria jibu la swali hilo kwa ufupi mno: Naam, wakati mwingine watu mia moja wanalinda kasri, wakati mmoja wa watu wa shari au mtu yeyote mharibifu anapojaribu kurusha moto katika kasri hiyo kwa siri ili kuliteketeza, au huenda akaombwa mfalme au taifa kuhifadhi kasri hiyo, hii ni kwa kuwa kubakia jengo la kasri kunahitajia masharti yote na nguzo na sababu zenye kupelekea kuhitajia kubaki. Ama kuliharibu na kulivunja huwa kwa kukosekana sharti moja tu. Na katika mfano kama huu tunafahamu namna mashetani wa majini na watu wanavyofanya uharibifu wa ajabu na uchomaji moto mkubwa kwa matendo machache mno, kama ambavyo mshari anavyoteketeza jengo kubwa kwa kutupia kijiti cha kibiriti. Naam, msingi na hamira ya shari na maovu na makosa yote ni kukosekana na kuvunja, na kinachoonekana katika uwepo wake wa dhahiri kinaficha chini yake ufisadi, kuharibu na kukosekana. Na kwa kuegemea nukta hii, hakika mashetani wa majini na watu na wenye shari wanaweza kwa nguvu ndogo dhaifu mno kuzuia nguvu isiyo na mpaka ya watu wa haki na hakika na kuwafikisha mlangoni kwa Allah (s.w) na kujitahidi kumwendea daima. Na kwa sababu hii Qur’an tukufu inaweka maandalizi hayo makubwa ili kuwalinda, na kukabidhi mikononi mwao majina mazuri tisini na tisa, na kutoa amri kali wapate uthabiti mbele ya maadui hao. Na kutokana na jawabu hili ghafla umedhihiri msingi wa suala la kushangaza na mwanzo wa hakika kuu nayo: Kama ilivyo pepo inahazini mavuno ya limwengu zote za uwepo na matokeo yake, na kuizalisha kokwa iliyopandwa ardhini duniani na kuifanya inatoa chakula chake kila wakati. Hakika jahanamu inakusanya mavuno ya kutokuwepo kwa ajili ya kudhihirisha matokeo yenye kuumiza sana ya limwengu za kukosekana na kutoweka kusiko na mipaka, basi kiwanda cha jahanamu ya kutisha - licha ya majukumu yake mengi – kinatakasa yaliyopo katika ulimwengu wa uwepo kutokana na takataka za ulimwengu wa kukosekana. Tutafafanua baadaye Inshallah suala hili kuu kwa sababu hatutaki kufungua mlango wake hapa. Vivyo hivyo, sehemu ya matunda ya imani ya malaika ni ile inayorejea kwa Munkar na Nakir, nayo ni kama ifuatavyo: Siku moja nilisema: (Hakika mimi sina budi – kama mtu yeyote awaye – ni mwenye kuingia kaburini hapana namna). Nikaingia humo kimawazo na nilipokuwa ninahisi upweke hali ya kukata tamaa na jela ya pekee ya kaburi na kuachana na kila kitu kabisa, bila ya msaidizi mahali hapo pembamba penye giza na baridi, ghafla wanatokea marafiki wawili wema katika kundi la (Munkar na Nakiir) na kuja kwangu na kuanza mjadala na mimi, walikunjua vyote moyo wangu na kaburi langu, wakaleta mwanga na joto na kufunguliwa madirisha yanayokabiliana na ulimwengu wa roho. Nilifurahishwa kutokea kina cha roho yangu na nikamshukuru sana Allah (s.w) kutokana na hali nilizoziona ambazo lazima zitatimia katika mustakabali japokuwa kwa sasa naziona kimawazo. Kama ilivyokuwa wakati alipofishwa mwanafunzi wakati wa kujifunza Sarufi na Nahau, Munkar na Nakiir walimuuliza kaburini: “man Rabbuka” (Mola wako ni nani?) akajibu: (man ni kiima na Rabbuka ni kielezi cha kiima. Niulizeni swali lingine gumu hili ni rahisi!!) - anadhani kuwa bado yuko madrasa akipokea somo - kama pia jibu hili lilivyo wachekesha malaika na roho zilizokuwepo na yule walii mwema ambaye kaburi lilimfunukia akashuhudia tukio hili, bali limefanya rehema ya Allah (s.w) itabasamu ikamuokoa kutokana na adhabu. Vivyo hivyo, shahidi hodari katika wanafunzi wa Risale-i Nur naye ni (Al-hafiz Ally) alifishwa jela hali akiwa anaendelea kusoma na kuandika (Risala ya Matunda) kwa ukamilifu wa shauku, alijibu maswali ya malaika wawili wa kaburini – kama alivyojibu mahakamani – kwa kutumia hakika za (Risala ya Matunda). Nami vilevile na wanafunzi wengine wa Risale-i Nur tutajibu inshallah maswali hayo ambayo ni hakika huko mustakabali, na ni majazi katika wakati uliopo. Tutayajibu kwa hoja za Risale-i Nur zenye kumulika na dalili zake zenye nguvu na kuwaelekeza kwa hoja hizo katika kusadikisha kusifu, uzuri na kuthamini. Na vivyo hivyo hakika kielelezo cha sehemu ya kuamini malaika ikiwa ni mhimili wa furaha ya dunia ni kuwa: Wakati ambapo mtoto asiye na hatia akipokea masomo yake katika misingi ya fiqhi, ghafla mtoto mwingine anamjia akiwa analia akihuzunika kwa kifo cha ndugu yake asiye na hatia basi anamtuliza na kumliwaza kwa kusema: (Usilie ewe ndugu yangu, bali mshukuru Allah (s.w) kwa sababu ndugu yako amekwenda pamoja na malaika na kwenda peponi atazunguka na kutembea huko kwa uhuru kamili kama malaika na atapata furaha na starehe bora kabisa na ataruka kama malaika na kushuhudia kila mahali). Akabadilisha kilio, kelele na masikitiko yake kuwa ni tabasamu na furaha. Na mimi vilevile kama mtoto huyu mwenye kulia katika hali ya machungu, pamoja na hali niliyokuwamo na katika majira haya ya baridi ya kuhuzunisha nilipokea habari ya vifo vya wawili na kuwahuzunikia kwa masikitiko na machungu makubwa mno. Moja wapo: Ni mtoto wa ndugu yangu marehemu (Fuad) ambaye alifanikiwa kupata daraja ya kwanza katika shule ya juu naye ndiye mwenezi wa hakika za Risale-i Nur. Pili: Ni yule aliye hiji na kutufu nyumba ya Allah na akiwa katika machungu ya kukata roho na alisalimisha roho yake akiwa kwenye tawafu, naye ni marehemu dada yangu mwanazuoni: (Khanim). Wakati vifo viliponiliza vya hawa ndugu wawili kama kumlilia kwangu (Abdul Rahmani) - iliyotajwa katika (Risala ya wazee) - niliona kwa nuru ya Imani – kwa moyo na maana - urafiki wa malaika na usuhuba na mahuru al-aini kwa kijana yule mzuri: (Fuad) na kwa yule bibi mwema, badala ya urafiki wa watu, na nimeona kuokoka kwao kutokana na maangamizo ya dunia na kukombolewa kutokana na makosa yake. Nikaanza kumshukuru Allah (s.w) - na yeye ni Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu – shukurani elfu moja na moja, jambo ambalo limegeuza huzuni hiyo kali kuwa hisia ya furaha, na nikaanza kuwapongeza na kumpongeza ndugu (Abdul Majid) (Baba Fuad) na ninaipongeza nafsi yangu vilevile. Hili limeandikwa na kusajiliwa hapa ili marehemu hawa wawili wapate baraka ya dua. Hakika yote yaliyomo kwenye Risale-i Nur katika vipimo na milinganisho hakika ni kwa ajili ya kubainisha matunda ya furaha ya imani na matokeo yake yanayorejea katika maisha ya dunia na Akhera, hayo matunda ya jumla makubwa huonyesha furaha ya maisha duniani na kuonjesha ladha zake ndani ya umri, kama inavyoelezea kwamba imani ya kila muumini itampa furaha ya milele huko Akhera, bali itazaa matunda na kufunuka na kukunjuka kwa sura hiyo hiyo huko Akhera. Basi katika mifano ya matunda hayo mengi ya jumla nimeandika matunda matano kati ya hayo kwamba hayo ni ya (Miiraji) mwishoni mwa (Neno la thelathini na moja) na matunda matano katika (Tawi la tano katika neno la ishirini na nne). Kama tulivyotaja karibuni kwamba kila nguzo miongoni mwa nguzo za imani ina matunda mengi sana bila mipaka, basi jumla ya nguzo za imani kwa pamoja zina matunda yasiyo na mpaka pia: Moja wapo: Pepo kuu. Nyengine: Furaha ya milele. Ya Tatu: Ni yenye ladha zaidi ambayo ni kumwona Allah (s.w) huko. Imefafanuliwa kwa uwazi katika mlinganisho uliyofanywa mwishoni mwa (Neno la thelathini na mbili) baadhi ya matunda ya imani ambayo ni muhimili wa makazi mawili. Hivyo, na dalili kwamba (Kuamini Kadari) ina matunda yake ya thamani pia hapa duniani ni jambo linalozunguka katika ndimi za wote, hadi imekuwa ni ya kupigiwa mithali: (Mwenye kuamini kadari amesalimika na huzuni), na mwishoni mwa (Risala ya Kadari), nimebainisha moja ya matunda yake ya jumla kwa mfano nao: Kuingia kwa watu wawili katika kasri ya kifalme. Hata nimeshuhudia katika uhai wangu kwa maelfu ya uzoefu wangu na nikatambua kuwa hakuna furaha katika maisha ya dunia bila ya kuamini Kadari, bila ya imani hii basi furaha hiyo ingefutwa na kutoweka. Bali nilikuwa kila nilipotazama masaibu ya kuumiza katika pembe ya kuamini Kadari, masaibu hayo yalikuwa na tahafifu na shida yake inapungua kwangu, Nikawa ninauliza kwa tahayuri: Vipi mtu asiyeamini Kadari anaweza kuishi? Imeashiriwa katika moja ya matunda ya kiujumla ya nguzo ya imani: (Kuamini malaika) (Katika Kituo cha pili cha neno la ishirini na mbili) kama ifuatavyo: Hakika Izrail (a.s) alisema akiongea na mola wake: Hakika waja wako watanilalamikia na kunichukia wakati wa kutekeleza kwangu jukumu la kutoa roho. Akajibiwa: Nitajaalia maradhi na masaibu kuwa ni pazia za jukumu lako ili malalamiko yao yapate kuelekea huko na sio kwako. Na jukumu la Izrail lenyewe vilevile ni pazia katika pazia hizo ili malalamiko batili yasielekee kwa Mola wa haki (s.w), kwa sababu hekima, rehema, uzuri na masilahi yaliopo katika umauti huenda asiyaone kila mmoja, kwani anaangalia nje ya mambo na anaanza kupinga na kulalamika. Kwa ajili ya hekima hii - yaani malalamiko ya batili yasielekee kwa Mwingi wa rehema wa hali zote – Izrail (a.s) amekuwa ni pazia. Na mfano wa hili kabisa wanayotenda malaika na sababu zote za dhahiri katika majukumu, hakika hizo ni pazia za Izza ya Ulezi wa kiungu, ili Izza ya uweza wa kiungu na utakatifu wake na rehema ya Allah (s.w) yenye kuzungukia kila kitu na enevu zibakie zimehifadhika katika mambo na vitu ambavyo pande za uzuri uliomo hauonekani, na wala haijulikani hakika za hekima ndani yake, pasipo kuwa ni shabaha ya upingaji batili. Wakati huo basi haionekani kwa mtazamo wa dhahiri utendaji wa mkono wa kudura katika mambo ya kibaadhi na yenye kupingana na rehema na vitu duni. Hivyo, na hakika Risale-i Nur imethibitisha kwa dalili zake nyingi, kwamba sababu yoyote ile katika sababu mbalimbali haina taathira ya hakika na wala haina nguvu ya kupatisha kitu asilani. Hakika mihuri ya Tawhiid isiyo na mpaka imeweka katika kila kitu na kwamba uumbaji na upatishaji unamhusu yeye (s.w), sababu sio chochote isipokuwa ni pazia, na malaika – nao ni wenye utambuzi – hawana isipokuwa ni sehemu katika hiari ya kisehemu (Eneo dogo analo miliki hiari) ambayo yeye ana nafasi ya kuchuma na sio kupatisha, nayo ni aina ya huduma ya kimaumbile na aina ya uja wa kimatendo na sio vinginevyo. Naam, hakika ya enzi na adhama vinahitajia kuweka sababu za dhahiri ni pazia mbele ya macho ya akili, isipokuwa Tawhidi na utukufu hunyanyua mikono ya sababu na kuizuia kuhusu taathira ya kihakika. Na kama hivi kama malaika na sababu za dhahiri zinazotumika katika mambo ya kheri na uwepo, ni nyenzo za utukuzo wa kiungu na utakaso katika yasiyoonekana wala kujulikana uzuri wake katika vitu, na hiyo ni kwa kuutakasa uweza wa kiungu na kuuhifadhi dhidi ya kasoro na dhuluma, vilevile kuwatumia mashetani wa kijini na wanadamu na vitu vyenye kudhuru katika mambo ya shari na kukosekana nayo ni aina nyingine ya kuhudumia tasbihi za kiungu na ni nyenzo ya kutukuza, kutakasa na kuweka mbali na kila kinachodhaniwa kuwa ni upungufu na kasoro katika viumbe na hiyo ni kwa sababu ya kulinda uweza wa kiungu, isije kuwa ni shabaha inayohusishwa na dhulma na kuelekezwa upinzani wa batli kwake, kwa sababu kasoro zote hutokea kwenye kukosekana, kushindwa, uvunjaji na kuzembea wajibu – ambayo yote ni kukosekana – na kutoka katika visivyokuwa na uwepo katika matendo ya kutokuwepo. Basi pazia hizi za kishetani zenye shari zimekuwa ni nyenzo za kumtakasa Mola wa haki (s.w) kwa yale mambo zilizoyabeba – kwa kustahiki – upingaji huo na malalamiko hayo kwa kuwa ndio marejeo na chanzo cha kasoro hizo. Wakati amali za shari na za kukosekana na kiharibifu hazihitajii – asilani – nguvu na uweza, basi matendo machache au nguvu ya kisehemu bali kuzembea wajibu fulani wakati mwingine, hupelekea katika aina za kukosekana na ufisadi. Kwa hiyo inadhaniwa mwenye kutenda matendo hayo ya shari kuwa mwenye uweza, wakati ambapo mambo yalivyo kwa hakika ni kwamba hana taathira isipokuwa kutokuwepo na hana nguvu isipokuwa kuchuma kwa kisehemu (Sehemu ndogo ya hiari). Na ilipokuwa shari hizo zinatokana na kutokuwepo basi watu hao wa shari wanahesabiwa kuwa ndio watendaji wa hakika wa mambo hayo, ikiwa ni katika wenye utambuzi wanastahiki kuonja matokeo mabaya ya jambo lao. Na hii inamaanisha kuwa hao wa shari mafisadi ni watendaji wa maovu. Ama katika mema na kheri na matendo mema kwa kuwa ni vya hali ya uwepo, walio wema sio watendaji wa hakika wa matendo hayo, bali wao wanastahiki ili matendo mazuri kupita kwenye mikono yao na basi wanapokea ukarimu wa kungu. Na kuwalipa hao kwa amali zao sio lolote isipokuwa ni ukarimu na neema tupu ya kiungu. Na Qur’an tukufu inafafanua hili kwa amri yake: مَّا أَصَابَكَ مِنْ حَسَنَةٍ فَمِنَ اللّهِ وَمَا أَصَابَكَ مِن سَيِّئَةٍ فَمِن نَّفْسِكَ Muhtasari: Hakika limwengu za uwepo na limwengu za kukosekana kusiko na mpaka zinapogongana kwa pamoja na zinapozaa matunda ya pepo na moto, na wakati limwengu zote za uwepo zinaposema: (Alhamdulillah, Alhamdulillah) na limwengu zote za kukosekana zinarudia kusema: (Subhanallah, Subhanallah) na hata malaika na mashetani wanapopambana, na kheri na shari, bali hata unapotokea mjadala katika moyo kati ya ilhamu na wasiwasi, wakati yanatokea yote haya kwa kanuni ya mkabala yenye kuzunguka hudhihiri tunda katika matunda ya (Kuamini malaika), kadhia inamalizwa na kutatuliwa tatizo ikinawirisha viumbe vyenye giza ikitudhihirishia nuru katika nuru nyingi za: اللَّهُ نُورُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ Hivyo inatuonjesha utamu wake utamu uliyoje wa nuru hiyo!! Na ladha yake iliyoje!! Hivyo, hakika vyote katika neno la (Ishirini na nne) na (Neno la ishirini na tisa) yameashiria katika tunda la jumla lingine na yamethibitisha uthibitisho wa uwazi uwepo wa malaika na kazi zao. Naam, hakika ulezi wa kiungu wenye rehema mkunjufu ambao umejitambulisha na kupendezesha katika uliyoyaeneza katika pande za ulimwengu sawa yawe ya kiujumla au kisehemu, utukufu huo na rehema hiyo utambulisho huo na kupendezesha huko kunapasa kukabiliwe na uja mkunjufu wenye kuzungukia kila hali enevu wenye shukurani ndani ya utukuzo, shukurani na kusifu. Hakika ya visivyo na uhai na nguzo kuu za ulimwengu ambazo hazina utambuzi huwezi kutimiza uja (utumishi) huu mkubwa, hivyo hawatimizi kwa niaba yao isipokuwa kiasi kisichohesabika cha malaika, hawa ndio wanaoweza kuwakilisha - kwa hekima zote na utukufu – shughuli za ufalme wa ulezi wa kiungu katika kila nguzo katika nguzo za ulimwengu, na katika kila sehemu miongoni mwa sehemu zake kutokea kwenye mchanga hadi kwenye Thurea (aina ya nyota) kutokea katika vina vya ardhi hadi kwenye anga. Kwa mfano: Hakika taswira inayowekwa na kanuni mfu za falsafa za kuumbwa kwa ardhi na kazi yake ya kimaumbile kwa namna ya kutisha yenye giza, tunda hili la imani inaigeuza taswira hiyo na kuwa ni taswira yenye kuliwaza yenye kuangaza ambapo malaika wawili wanaoitwa Ng’ombe na Samaki, wanabeba juu ya mabega yao – yaani chini ya uangalizi wao – dunia, ambapo mada hiyo ya kiakhera imeletwa kutoka peponi, na hakika hiyo ya kiakhera inayoitwa (Jiwe) lipate kuwa jiwe la msingi lenye kubakia la hili tufe la Ardhi lenye kutoweka, ikiashiria kwamba sehemu fulani ya ardhi itapakuliwa na kugeuzwa kuelekea kwenye pepo ya kubaki, Jiwe limekuwa ni nukta ya kuegemea malaika wawili: (Ng’ombe na Samaki), kama hivi riwaya hii imesimuliwa kutoka baadhi ya manabii Waizraili wa mwanzo nayo imesimuliwa pia kutoka kwa Ibn Abbas (r.a) lakini cha kusikitisha mno tashibiha hii ya upole na maana hii ya juu kugeuka kwa kupita kwa muda kuwa ni hakika ya kimaada yenye kupewa mwili kwa watu wa kawaida, kiasi imekuwa nje ya eneo la akili, kwa kuwa malaika wanaweza kupita na kuzunguka katika udongo na katika mawe na katikati ya ardhi kama kutembea kwao hewani, kwa hiyo hawana haja kabisa – wala tufe la ardhi halina haja – ya jiwe la kimaada katika hali ya kimwili wala ng’ombe na samaki wa kimaada katika hali ya kimwili! Kwa maana riwaya hiyo sio vingine isipokuwa ni kwa Tashbiha. Mathalani: Kwa kuwa tufe la ardhi linamsabihi Allah kwa idadi ya vichwa vya aina zilizopo ndani yake, ikiwemo wanyama, mimea na visivyo na uhai na kwa idadi ya ndimi za kila moja ya aina hizo, na kwa kiasi cha viungo vya kila moja, na kwa idadi ya majani yake na matunda yake, hakika kutanguliza uja huu wa kimaumbile usio wa kiutambuzi mkubwa sana, na kuwepo kwake na kuonesha kwa ujuzi na utambuzi mbele ya hadhara ya kiungu tukufu, Inahitajia kwa lazima malaika mwenye kuwakilishwa ambaye ana vichwa arobaini elfu, na katika kila kichwa kuna ndimi arobaini elfu, kwa kila ulimi anasabihi kwa tasbihi arobaini elfu, kama mpashaji habari wa kweli alivyoelezea hakika hii hii. Naam, ni katika yanayolazimu utukufu wa ulezi wa kiungu, adhama na ufalme wake kwamba Jibril awe katika haiba ya ajabu na yeye ndiye mwenye sifa ya kufikisha mahusiano ya kiungu kwa mwanadamu ambaye ndiye matokeo muhimu ya kuumbwa kwa ulimwengu, na wawe Izrail na Israfil (a.s) katika haiba ya ajabu vilevile, nao wanawakilisha – ni kuwakilisha tu – shughuli maalum za kiungu za Muumba (s.w) na kusimamia kwa uja (Utumishi) wa dhati juu ya kitu adhimu sana katika ulimwengu wa wenye uhai, nacho ni ufufuo na umauti. Na Mikail (a.s) awe katika haiba ya ajabu, ambapo anawakilisha kwa utambuzi kamili aina za shukurani zisizo za kiutambuzi juu ya hisani za mwingi wa rehema katika riziki ambayo ni duara jumuishi zaidi katika duara za maisha na kunjufu zaidi na lenye hali nyingi za kuonja, licha ya uangalizi wake juu ya jambo hili. Naam, ni mambo ya lazima ya utukufu wa ulezi wa kiungu na heshima yake kubakia kwa roho na kuwepo kwa mifano ya malaika kama hawa kwa haiba ya ajabu mno, kwa kuwa uwepo wa hawa na kuwepo kwa kila kundi maalum kati yao ni wenye kuthibiti kimkataa na hakuna shaka katika hilo kwa hali zote, nalo ni lenye kuthibiti kwa kiwango kinacholingana na uthabiti wa kuwepo kwa utukufu na ufalme wa dhahiri katika ulimwengu kama jua. Na mada nyengine zinazohusu malaika zipimiwe hili. Naam, hakika ambaye anaumba katika tufe la ardhi mia nne elfu aina za walio hai, bali anaumba wenye roho kwa wingi mkubwa kutokana na maada rahisi mno na kutokana na uozo, na anaimarisha pande za ardhi kwa kuwaweka wao na kuwajaalia kuwa wanatamka kwa ulimi wao kwa kupendezwa: (Mashaallah, Baarakallah, Subhanallah), mbele ya miujiza ya ufundi wake (s.w), na ambaye amefanya hata wanyama wadogo mno wanatamka: (Alhamdulillah wa Ash-shukru lillah wallahu akbar) mbele ya hisani za rehema kunjufu na neema zake. Hakika ya huyu Mweza mwenye utukufu na uzuri, hakika ameumba bila shaka wala utata wakazi wa kiruhani wenye kuwiana na mbingu zenye mawanda makubwa sana katika ambao hawaasi amri yake na wanamwabudu yeye daima, kwa kuwatumia wao anaimarisha mbingu bila ya kuiacha tupu kame. Akapatisha aina nyingi mno katika malaika ambao ni wengi mno kuliko aina za walio hai na makundi yao, sehemu kati yao ni ndogo sana wanapanda matone ya mvua na chenga za barafu na wanabariki ufundi wa kiungu wakifanya tahalili kwa rehema zake kunjufu kwa ulimi wao maalum, na sehemu kati yao wanapanda migongo ya sayari zenye kutembea hivyo huelea katika anga la ulimwengu hali ya kuwa wanatangazia ulimwengu wote uja wao kwa takbira na tahalili mbele ya adhama ya ulezi wa kungu na enzi yake na utukufu wake. Naam, hakika kuafikiana vitabu vyote vya mbinguni na dini zote tangu zama za Bwana wetu Adam (a.s), juu ya kuwepo kwa malaika na uja wao, na yaliyopokewa katika riwaya zenye tawaturi ya kuongea na malaika ndani ya zama zote, imethibitisha kwa kukinaisha kuwepo kwa malaika na uhusiano wao na sisi kwa kiwango cha kuthibiti kwa kuwepo kwa watu marekani ambao hatujawaona. Na sasa tazama kwa nuru ya imani katika tunda hili la jumla la pili na ulionje uone vipi kwamba limetia furaha viumbe mwanzoni mpaka mwishoni mwao na kuwaimarisha na kuwapamba na kuwafanya kuwa ni msikiti mkubwa na mahali pakubwa pa kufanyia Ibada. Basi ulimwengu wenye giza baridi ambao hauna uhai ndani yake – kama mrengo wa kimaada wa kisayansi na falsafa unavyoleta taswira – kwa imani unakuwa ni ulimwengu wenye uhai na utambuzi na wenye nuru na maliwazo na wenye ladha, tunda hili basi linawaonjesha wenye imani mwale katika ladha ya maisha ya kubakia milele na hali ya kuwa bado wakiwa wangali kwenye dunia kila mmoja kulingana na daraja yake. Ukamilisho: Kama ilivyo kwamba kwa siri ya umoja na upekee hupatikana uwezo uleule na jina lilelile na hekima ileile na ufundi uleule, katika kila upande kwenye pande miongoni mwa pande za ulimwengu, kila kilichotengenezwa kinatangaza – kiujumla au kisehemu – kwa ulimi wake wa hali: Umoja wa Muumba (s.w), usarifu wake, upatishaji wake, ulezi wake wa kiungu, hali ya uumbaji wake na hali ya utakatifu wake, kadhalika yeye (s.w) anaumba malaika katika pande zote za ulimwengu ili watimize – kwa ndimi zao zenye kudhukuru zenye kuhimidi – kwa tasbihi kila kiumbe anazitimiza kwa ulimi wa hali yake bila hisia. Malaika hawamwasi Allah kwa anayowaamrisha, na hawana isipokuwa ni uja wa dhati na hawana upatishaji wowote uwao, na hawana kuingilia bila idhini, na haiwi kwao shufaa bila idhini kutoka kwake (s.w), na kwa ajili hii wamepata utukufu wa: بَلْ عِبَادٌ مُّكْرَمُونَ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ

