Hakika hoja hii ya nane ya kiimani; ambapo inashuhudia juu ya wajibu wa kupasa kuwepo kwake (s.w) na juu ya upweke wake, basi inashuhudia juu ya kuzunguka kwa ulezi wake, na adhama ya uwezo wake kwa dalili zenye kukinaisha, na pia inathibitisha kuzunguka kwa utawala wake, na inajulisha juu ya kuenea kwa Rehema yake, kama inavyoithibitisha kuzunguka kwa Hekima yake, na kuenea kwa ujuzi wake sehemu zote za ulimwengu. Ufupi: Hakika kwa kila utangulizi katika hoja hii ya nane ya kiimani ina matokeo manane, nayo yanathibitisha katika kila utangulizi katika tangulizi nane, matokeo manane pamoja na dalili zake; kwa hiyo imekuwa hoja hii ya kiimani ya nane sifa pambanuzi za juu na sifa mahususi za hadhi ya juu. (Hakika ya Risala ya Munajat) inathibitisha kupasa kwa kuwepo, umoja, upweke, utukufu wa ulezi wa kiungu, adhama ya uwezo, ukunjufu wa Rehema, ujumla na ueneaji wa utawala, kuzunguka kwa ujuzi, kuenea kwa hekima na kama hiyo katika misingi ya kiimani, inaithibitisha kwa njia nyepesi fupi ya ajabu na kwa kukinaisha zaidi ya haja na kwa hali ya ikhlasi na yakini. Na kwamba kuashiria kwake ufufuo kuna nguvu mno na hasa iliyomo katika hitimisho lake. Said Nursî
Source text is preserved. When a suitable model is available, translation is displayed separately.
Şualar
The Third Ray
بِسْمِ اللّٰهِ الرَّحْمٰنِ الرَّحِيمِ اِنَّ فٖى خَل۟قِ السَّمٰوَاتِ وَال۟اَر۟ضِ وَاخ۟تِلَافِ الَّي۟لِ وَالنَّهَارِ وَال۟فُل۟كِ الَّتٖى تَج۟رٖى فِى ال۟بَح۟رِ بِمَا يَن۟فَعُ النَّاسَ وَمَٓا اَن۟زَلَ اللّٰهُ مِنَ السَّمَٓاءِ مِن۟ مَٓاءٍ فَاَح۟يَا بِهِ ال۟اَر۟ضَ بَع۟دَ مَو۟تِهَا وَبَثَّ فٖيهَا مِن۟ كُلِّ دَٓابَّةٍ وَتَص۟رٖيفِ الرِّيَاحِ وَالسَّحَابِ ال۟مُسَخَّرِ بَي۟نَ السَّمَٓاءِ وَال۟اَر۟ضِ لَاٰيَاتٍ لِقَو۟مٍ يَع۟قِلُونَ Risala hii ya (Munajat) ambayo ni (Mwale wa tatu) ni aina ya tafsiri ya aya tukufu iliyotajwa juu yake. Ewe Mola wangu na Ewe Bwana wangu Mlezi! Hakika mimi ninaona kwa uoni wa imani na kwa mafunzo ya Qur’an na nuru yake na kwa darasa la Mtume Mtukufu (s.a.w) na kile ambacho jina La Allah (Al-Hakim) inakionesha kuwa: Mbinguni hakuna mzunguko wala mchakato isipokuwa unaashiria kuwepo kwako na kujulisha juu yako; kwa mpangilio wake huu wa ajabu. Na hakuna umbo katika maumbo ya mbinguni isipokuwa linashuhudia juu ya Ubwana ulezi wako na kuashiria ishara katika upweke wako; kwa utulivu wake katika kutekeleza kazi yake bila zogo, na kwa kubakia kwake bila nguzo. Na hakuna nyota isipokuwa inashuhudia juu ya adhama ya Upweke wako; kwa umbo lake lililopimwa na kwa hali yake iliyopangika na kwa tabasamu lake la kinuru na kwa kufanana kwake na kushabihiana kwake na nyota zote. Na hakuna sayari katika sayari kumi na mbili isipokuwa inashuhudia kupasa kuwepo kwako na kuashiria katika ufalme wa Uungu wako; kwa mchakato wake wa Hekima na kujidhalilisha kwake kwa utiifu na kazi yake iliyopangika na vifuasi vyake muhimu. Naam, mfano ambavyo mbingu zinashuhudia pamoja na wakazi wake, na kila mbingu kwa dhati yake hasa, hakika zote pamoja na inayo yashuhudia kwa uwazi ushahidi dhahiri juu ya kupasa kuwepo kwako ewe Muumba wa mbingu na ardhi, na zinashuhudia ushahidi wenye nguvu wa kweli juu ya upekee wako, ewe ambaye unaendesha Atomu pamoja na vinavyoiunda vilivyopangika na unaviendesha na ewe unayeendesha sayari pamoja na vifuasi vyake vilivyopangika na unavidhalilisha kwa kukutii, ushahidi wa dhahiri wenye nguvu hoja za nuru unausadikisha, na dalili za wazi, idadi ya nyota ambazo zipo katika uso wa mbingu. Basi mbingu hizi safi tohara nzuri zinajulisha kujulisha dhahiri juu ya haiba ya ulezi wako na adhama ya uweza wako wa kutenda wa ajabu. Na zinaashiria ishara yenye nguvu juu ya wasaa wa utawala wako wenye kuzunguka mbingu pana, na katika rehema zako kunjufu zenye kukukusanya kila chenye uhai, na kushuhudia bila shaka juu ya uenevu wa hekima yako kwa kila tendo na kuzunguka ujuzi wako kwa kila kitu, vyenye kupanga katika kabidhi yake mambo yote ya viumbe wote wa mbinguni na namna zake; kwa maumbo yake ambayo yako katika upeo wa ukubwa na katika upeo wa kasi, na kwa kudhihirisha kwake hali za jeshi lililopangiliwa na tamasha la kutisha lenye kupambwa kwa taa zenye kutoa mwanga. Basi huo ushahidi na dalili ni matukio mawili yaliyo wazi kana kwamba nyota ni maneno ya ushahidi kwa mbingu yenye kushuhudia na dalili zake za kinuru zilizo katika umbo, ama nyota zenye kuogelea katika bahari ya mbingu na anga lake, hakika zinadhihirisha kumetameta kwa ufalme wa Uungu wako; kwa hali zake zinazo mithiliana na wanajeshi wenye kujipanga na majahazi yaliyonadhimika na ndege zenye kufurutu ada na taa za ajabu. Na marafiki wa jua letu ambalo ni nyota katika jeshi hilo wanaangalia katika limwengu za Akhera na sio kwamba hazina kazi, kwa dalili za majukumu ya jua katika sayari zake na katika Ardhi yetu, na huenda ni majua ya limwengu zenye kubakia. Ewe uliye wajibu kuwepo, ewe Mmoja, ewe wa pekee! Hakika ya hizi nyota zenye kufurutu ada na majua haya makubwa na miezi ya ajabu imetiishwa na kunadhimiwa na kupewa majukumu katika ufalme wako Wewe, na katika mbingu zako Wewe, kwa amri yako Wewe, na kwa nguvu na uwezo wako Wewe, na kwa uongozi na kupangilia kwako Wewe. Basi hayo maumbo yote makubwa ya juu yanafanya tasbihi na yanaleta takbira kwa Muumba mmoja ambaye ameyaumba na kuyaendesha, na yanasema kwa ulimi wa hali: سبحان الله، الله أكبر Nami niko pamoja nayo ninakutakasa kwa tasbihi zake zote. Ewe uliyejificha kwa kuzidi kudhihiri! Na ewe uliyejificha kwa adhama ya ukubwa! ewe Mweza Mwenye utukufu! Ewe Mweza wa uweza wa hali zote! Hakika nimetambua kwa kusoma Qur'an yako yenye hekima na kwa mafunzo ya Mtume Mtukufu (s.a.w) kwamba: Kama zinavyoshuhudia mbingu na nyota juu ya kuwepo kwako na juu ya upweke wako, anga la mbingu linashuhudia vilevile juu ya kupasa kuwepo kwako na upweke wako kwa mawingu yake, umeme wake, radi zake, pepo zake na mvua zake. Naam, hakika kutuma kwa mawingu yasiyokuwa hai yasiyo na utambuzi mvua iletayo uhai, kuwasaidia wenye kudhikika katika walio hai, si vinginevyo isipokuwa kwa Rehema yako na Hekima yako Wewe, hakuna mwingiliano humo wa sadfa ya kiholela katu. Na vivyo hivyo umeta ambao ni nguvu kubwa ya umeme, unatia shauku kwa miale yake kwa faida za kinuru, na unatia nuru uweza wako utendao angani kwa sura iliyo bora zaidi. Na vivyo hivyo radi ambayo ni mbashiri wa kuja kwa mvua, na ambayo inalitamkisha anga pana kwa tasbihi zake, basi kutoa kishindo katika pande za mbingu, inakusabihi na kukutakasa inashuhudia kwa ulimi wa maneno juu ya Rububiyya yako. Na kadhalika pepo zenye kutiishwa kwa majukumu mbalimbali - kama kubeba riziki zinazo lazimu kwa maisha ya walio hai na iliyo nyepesi kwa kutumia na kwa faida, na kutunuku pumzi na kupumzisha nafsi na mengine mengi - yanaonesha utendaji wa uweza wako Wewe, na yanashuhudia ushahidi wa kuwepo kwako, kwa kubadilisha kwake anga - kwa hekima - Kana kwamba ni (Ubao wa kufuta na kuthibitisha) basi unaandika yanayoleta faida na unafuta yaliyoleta faida. Kama ilivyo (Rehema) inayonyonya kwa Rehema yako kutoka kwenye mawingu yaliyotumwa kwa walio hai, hiyo vilevile inashuhudia juu ya ukunjufu wa Rehema yako na Upole wake; kwa maneno ambayo matone yake matamu mapole yaliyopimwa na kunadhimika. Ewe Msarifu ewe Mtendaji! Ewe uliyejaa ewe Mwenye sifa za juu! Mfano wa mawingu yalivyoshuhudia, umeme, radi, upepo na mvua - kila moja kwa peke yake - juu ya kupasa kuwepo kwako, hakika vyote hivyo vinaashiria juu ya umoja wako na upekee wako, kwa sifa ya kuafikiana, upamoja na kuingiliana, na vyote baadhi kutia nguvu baadhi nyingine, licha ya kuwa mbali katika sampuli na kutofautiana katika ainisho. Na kama chembe hizo za anga zinavyoshuhudia juu ya utukufu wa Rububiyya yako inayofanya anga pana ni mahali pa kukusanyika maajabu kwa kujaza kwake na kuacha kwake tupu mara nyingi na pengine katika siku moja, hakika hiyo inashuhudia adhama ya uweza wako wenye kusarifu na kuenea kwake kila kitu, na ambao unaandika anga hilo kunjufu na kulibadili kana kwamba ni (Ubao wa kunadikia) na unakamua mawingu ili kunyeshea bustani ya Ardhi maji mengi. Licha ya kujulisha kwake upana wa hali zote kwa rehema zako na utawala wako na kutekelezeka katika kila kitu, na kuzungusha kwao tufe la Ardhi lote na viumbe wote chini ya funiko la anga. Na kadhalika hewa yenye kuenea angani inatumika katika majukumu chungu nzima utumiaji wa kihekima, na mawingu na mvua hutumika katika faida nyingi utumizi wa kiujuzi, kwa namna ambayo isingekuwa elimu yenye kuzunguka kila kitu na hekima yenye kuenea kila kitu, isinge wezekana kutumia huko. Ewe Mwenye kufanya alitakalo! Hakika kudhihirisha kielelezo cha ufufuo na kiama kila wakati kwa utendaji wako katika hewa ya anga, na kubadili majira ya joto kuwa majira ya baridi na majira ya baridi kuwa ya joto ndani ya saa moja, na kuleta ulimwengu na mwingine kuutuma katika ghaibu na mifano ya hayo katika uweza wako wenye kudhihiri. Unaashiria katika kubadilisha kwake dunia kwenda akhera, na utadhihirisha mambo ya kimilele huko akhera. Ewe Mweza Mwenye Utukufu! Hakika hewa, pepo, mawingu, mvua, umeme na radi katika anga la mbingu vyote hakika ni vyenye kutiiwa na kupewa majukumu katika ufalme wako wewe, na kwa nguvu na uweza wako wewe, basi viumbe wa anga hili licha ya umbali katika maainisho yake vinasabihi kwa kumhimidi mwamrishaji wake na kumsifu mtawala wake ambaye anavinyenyekesha katika amri za punde katika ukomo wa kasi, na kwa waamrishaji wenye kasi haraka. Ewe Muumba wa Ardhi na Mbingu! Ewe Mwenye Utukufu! Na hakika nimeamini na kujua kwa mafunzo ya Qur’an yako yenye hekima na kwa darasa la Mtume Mtukufu (s.a.w) kwamba: Mfano wa ambavyo mbingu pamoja na nyota zake, na hewa ya anga na vilivyomo ndani yake, vinashuhudia juu ya kupasa kuwepo kwako na upekee wako, vivyo hivyo ardhi na viumbe wake wote na hali zake, vinashuhudia shahidi na kuashiria ishara, kwa idadi ya vitu vyake vilivyomo juu ya kuwepo kwako na upweke wako. Naam hakuna kugeuka katika ardhi wala badiliko humo – kama miti na wanyama kubadili mavazi yao kila mwaka - ujumla au iwe kwa sehemu, isipokuwa pia huashiria kwa mpangilio wake na kuratibika kwake uwepo wako na umoja wako. Na hakuna mnyama isipokuwa anashuhudia juu ya kuwepo kwako na upweke wako, kwa riziki ambayo inapelekwa kwake kwa rehema, na kwa zana zake za kidharura kwa uhai wake zilizowekwa kwake kwa hekima, kila mmoja kulingana na uhitaji wake na udhaifu wake. Na hakuna mmea na mnyama inatimia kupatishwa kwake mbele ya watazamaji wetu kila majira ya machipuo isipokuwa inakujulisha kwamba, kwa ufundi wake wa ajabu na kwa mapambo yake maridadi na kupambanuka kwake timilifu na kwa kupangika kwake na kupimika kwake. Basi kuumba vinavyojaza Ardhi ni katika miujiza ya uweza wake inayoitwa kuwa ni mimea na wanyama, kutokana na mayai na viyai na matone na vitone vya manii na punje na vipunje. Licha ya kuwa maada yake ni ndogo mno na ni moja yenye kurandana, umbo kamili la sawa na lenye kupambwa kwa pambo, na kupambanuka kwa alama zenye kutenganisha. Ni ushahidi wenye nguvu kuliko ushahidi wa mwanga juu ya jua na mwangavu kuliko hilo juu ya kuwepo kwa mtengenezaji wake Mwingi wa hekima, na juu ya upweke wake na hekima yake na uweza wake wa hali zote. Na hakuna chembe kama hewa, maji, nuru, moto na mchanga isipokuwa inamiliki ushahidi juu ya upweke wako na juu ya kuwepo kwako; kwa kutekeleza kwake kwa nyadhifa zenye kukamilisha kwa hisia za upeo, licha ya kukosa kwake utambuzi, na kuleta kwake matunda na mavuno anuwai katika upeo wa mpangilio kutoka katika hazina ya ghaibu, licha ya urahisi wake na kuvuka baadhi kwa baadhi nyingine na kutopangika kwake na kurandana kwake kila mahali. Ewe Muumba ewe Mweza ewe Mfunguzi ewe Mjuzi wa kila kitu ewe Mtendaji ewe Muumba! Kama ilivyo Ardhi kwa wakazi wake wote juu ya kuwa Muumba wake ni wajibu kuwepo, inashuhudia vilevile juu ya umoja wako na upweke wako – ewe mmoja na ewe mpweke na ewe Mwenye upole ewe mneemeshaji, ewe mtoaji hiba ewe mwenye kuruzuku - kwa muhuri wake ambao uko juu ya uso wake, na kwa mihuri ambayo imo kwenye nyuso za wakazi wake, na kwa upande wa umoja na kuafikiana na kuingiliana na kusaidiana baina yao, na umoja ya majina ya Rububiyya na matendo yake yenye kutazama huko yote. Basi yanashuhudia shahidi – kwa daraja ya uwazi bali kwa idadi ya vilivyomo - juu ya umoja wako na juu ya upweke wako. Na kama hivyo kama inavyojulisha Ardhi, kwa hali yake yenye kurandana na kambi, maonesho na medani ya mazoezi, na kwa kutunuku zana mbali mbali kwa mpangilio hadi mia nne elfu katika jamii mbali mbali ambalo linakusanya kundi la mimea na wanyama, juu ya utukufu wa Rububiyya yako, na kwa kufanya kazi kwa uweza wako katika kila kitu, na vivyo hivyo riziki anuwai za walio hai wasio na mpaka na yenye kutokea kutokana na mchanga mkavu rahisi, na kuzituma kwa kila ukarimu na rehema kwa kila aliye hai mmoja mmoja katika nyakati zake na kufuata kwa hao mmoja mmoja wasio na mpaka na kutii kwao utiifu kamili kwa amri za kiungu na kujitiisha kwake kikamilifu kwazo, inadhihirisha uenevu wa rehema yako kwa kila kitu na kuzunguka utawala wako kila kitu. Na kama hivyo kuendesha misafara ya viumbe yenye kuwekwa daima kwenye kubadilika katika Ardhi, na kupelekwa kwake na kupokezana kwake kwa umauti na uhai, na kuongoza na kuendesha wanyama na mimea ambayo haiyumkiniki kutimia isipokuwa kwa ujuzi unaoambatana na kila kitu, na kwa hekima isiyokoma inayodhibiti kila kitu, inaonesha juu ya kuzunguka kwa ujuzi wako na hekima yako. Na vilevile hakika umuhimu huu mkubwa, na huku kutoa na kugawa kusiko na mpaka, na hii midhihirisho ya kiungu ya hali zote, na haya masemesho ya kisubhana yasiyo na mipaka, na hizi hisani za kiungu zisizo na ukomo kwa mwanadamu huyu ambaye anatenda katika vilivyomo Ardhini naye ndiye aliye kalifishwa kwa majukumu yasiyo na mpaka ndani ya kitambo kifupi na mwenye kupewa maandalizi na zana za kimaanawy yanamtayarisha kwa maisha marefu katika wakati usio na mpaka, hakuna namna kwamba hayajifungi katika madrasa ya hii dunia tu, na katika kambi hii ya Ardhi ya muda, na katika maonesho haya ya ulimwengu ya muda, wala hajifungi katika umri huu mfupi wenye huzuni wenye kutibuliwa, wala katika uhai huu uliochafuka na usio na raha, wala si katika ulimwengu huu wenye kutoweka uliojaa mabalaa na majanga. Kwa yote haya inaashiria bila shaka umri mwingine wa milele na furaha ya kubakia milele na inaashiria hisani ya kiakhera katika ulimwengu wa kubakia, bali inaishuhudia. Basi ewe Muumba wa kila kitu! Hakika viumbe wote wa Ardhi wanaendeshwa wakitiishwa katika ufalme wako wewe, kwa hila yako na nguvu yako wewe, kwa uweza wako na utashi wako wewe na kwa ujuzi wako na hekima yako wewe. Na hakika ya Rububiyya (Ulezi wa kiungu) unaoshuhudiwa utendaji wake juu ya uso wa Ardhi unadhihirisha kuzunguka na kuenea, kwa sababu kuendesha kwake na kuongoza kwake na malezi yake ni katika unyeti wa upeo wa ukamilifu. Na hakika taratibu zake zenye kuenea katika kila upande ni katika umoja na upamoja na wenye kurandana. Kwa kiasi inajulikana hakika hiyo ni Rububiyya ya jumla na usarifu wa jumla haukubali kutenganishwa mafungu katu. Nayo ni katika hukumu ya ujumla haikubali kugawanyika katu. Basi Ardhi na wakazi wake wote inamsabihi na kumtakasa Muumba wake kwa ndimi zisizo na mpaka fasaha na bayana zaidi kuliko ulimi wa maneno, Vinamhimidi Mruzuku wake Mtukufu na kumsifia kwa ndimi za hali kwa idadi ya neema zake ambazo zisizo hesabika na kudhibitika. سبحانك يامن اختفى بشدة الظهور، سبحانك يامن احتجب بعظمة الكبرياء. Mimi ninakutakasa na kukusabihi kwa tukuzo zote za Ardhi na tasbihi zake kutokana na kasoro na kushindwa na mshirika, nami ninakuhimidi na kukusifu kwa himidi zote za Ardhi na nimekusifia. Ewe Bwana Mlezi wa bara na bahari! Hakika nimejifunza kwa darasa ya Qur'an na kwa mafunzo ya mtume mtukufu (s.a.w) kwamba: Mfano ambao mbingu, anga na Ardhi vinashuhudia umoja wako na juu ya kuwepo kwako, basi bahari na mito na madimbwi na chemchem vilevile vinashuhudia ushahidi – kwa daraja ya uwazi – juu ya kupasa kuwepo kwako na juu ya umoja wako. Naam, hakuna kilichopo bali hakuna tone la maji katika bahari za Dunia hii nayo ni chimbuko la maajabu – kama ni vyungu vya mvuke – isipokuwa inajulisha muumba wake; kwa kuwepo kwake, kwa kupangilika kwake, kwa manufaa yake na kwa hali yake. Na hakuna kiumbe yeyote katika viumbe vigeni ambavyo vinatumiwa riziki zake utumwaji kamili na katika mchanga rahisi na maji rahisi, wala mnyama katika wanyama wa bahari ambao wako katika upeo wa ukamilifu wa umbo na hasa samaki ambao wanaziweka vizuri bahari kwa mmoja wapo anayetoa mamilioni ya mayai, isipokuwa inaashiria kwa Muumba wake na kumshuhudia mruzuku wake kwa majukumu yake, kwa uendeshaji wake, kutoa kwake maisha, kwa kuongoza mambo yake na kwa ulezi wake. Na kadhalika hakuna katika bahari johari yoyote miongoni mwa johari hizo za thamani na lulu zilizopambwa za thamani zenye sifa mahsusi za tunu ambazo hazikujui wala kukujulisha; kwa umbo lake zuri na kwa maumbile yake ya kuvutia na kwa sifa zake mahususi zenye kunufaisha. Naam, basi kama inavyoshuhudia kila johari moja, basi hakika johari hizo kwa ujumla wake pamoja zinashuhudia umoja wako pia, na yaliyomo miongoni mwa kuafikiana, kuingiliana, kuchanganyika, umoja wa muhuri wa umoja, upeo wa wepesi katika kupatisha na upeo wa wingi katika mmoja mmoja. Na hakika kujaalia bahari zinazozungukia Ardhi ikiwa imeangikwa mbinguni pamoja na nchi kavu yake pana, na hali ikiwa inaogelea kuzunguka jua bila ya kumwagika kabisa, na bila ya kuparaganyika kwa kufurika, na bila ya kutawalia uyabisi, na kuumbwa wanyama wake anuwai na johari zake zilizonadhimika kutokana na mchanga wake rahisi na maji yake rahisi, na kuendesha riziki za viumbe hivyo na mambo yake mengine uendeshaji wa kiujumla, na kusimamia uendeshaji wake na kutoharisha uso wake kutokana na majeneza yasiyokuwa na ukomo, inashuhudia kwa idadi ya vilivyomo vyake, ya kwamba wewe upo na ni wajibu kuwepo. Na kama hiyo inajulisha ujulisho wa dhahiri waziwazi juu ya utukufu wa ufalme wako wa ulezi wako wa kiungu, na juu ya Adhama ya uweza wako wenye kuzunguka kila kitu, basi hiyo inajulisha vilevile juu ya ukunjufu wa hali zote wa rehema yako na utawala wako ambavyo vinatamalaki juu ya kila kitu, na kuipa msaada kila kitu, kuanzia kwenye nyota kubwa na zenye kupangika katika maeneo ya juu ya mbingu hadi samaki wadogo wenye kupangika kuwapa maisha katika vina vya bahari, na inaashiria ujuzi wako unaozunguka kila kitu na hekima yako yenye kuenea kwa kila kitu; na kwa kupangika kwake na faida zake na hekima zake na mizani yake na kwa vipimwa vyake. Na hakika ya kupatisha birika za Rehema kama hizi kwa mwanadamu anayekuja akiwa ni mgeni katika nyumba hii ya wageni duniani, na kuidhalilisha kwake kwa kwenda kwake, kutalii kwake, kwa jahazi lake na kwa manufaa yake, inaashiria kwamba hakika ya ambaye anawakirimu wageni wake ndani ya usiku mmoja, katika makazi ya mapumziko aliyo wajengea katika njia ya safari yao, kwa ukarimu huu mkubwa kutokana na zawadi za bahari na vipawa, hapana budi kuwa amehudhurisha katika makao ya ufalme wake wa milele bahari yake ya milele kunjufu kwa namna kwamba sehemu inayoshuhudiwa katika rehema hiyo si chochote isipokuwa ni vielelezo tu vya kutoweka na ndogo mbele ya hiyo ya milele. Na kama hivi hakika ya kupatikana kwa bahari kwa mtindo huu wenye kufurutu ada na kwa hali yake ya ajabu katika pande za Ardhi na kuendesha viumbe wake na kusimamia malezi yake katika upeo wa mpangilio - kwa uwazi – vyote vimetiishwa katika ufalme wako wewe, na kwa amri yako na kwa nguvu yako na uweza wako na kwa uendeshaji wako na uongozi wako peke yako, basi hivyo vinamtukuza Muumba wake kwa ndimi za hali zao zikitoa sauti Allah Akbar! Ewe Mweza ewe Mwenye Utukufu! Ewe uliyejaalia milima ni vigingi vyenye hazina kwa safina la Ardhi. Hakika nimejua kwa mafunzo ya mtume (s.a.w) na kwa kusoma Qur'an yako yenye hekima kwamba: Mithili ya bahari zinavyo kutambua na kukutambulisha kwa maajabu yake na mageni, na vivyo hivyo milima inakutambua na kukutambulisha, kwa huduma zake na kwa hekima zake, kwa kuaminisha utulivu wa Ardhi kutokana na taathira na matetemeko na kudamirika, na kwa kuituliza Ardhi kutokana na vitisho vyake vinavyoendelea ndani yake, na kuiokoa Ardhi kutokana na mafuriko ya bahari na kuchupa kwa dhoruba zake, na kuisafisha hewa kutokana na gesi zenye kudhuru, na kwa kuhifadhi kwake maji na kudhamini akiba yake, na kuhazini kwake madini ya lazima kwa mahitaji ya walio hai. Naam, basi hakuna aina yoyote katika aina za mawe yaliyo kwenye milima, wala sehemu katika aina ya maada ambayo ni matibabu ya maradhi mbalimbali na ndwele, na hakuna jinsi katika jinsi za madini anuai mno na ambazo zinawalazimu walio hai na hasa mwanadamu, wala sampuli katika sampuli za mimea iliyopambwa kwa maua yake milima na kwa matunda yake Ardhi kame. Isipokuwa inashuhudia – kwa uwazi – juu ya kupasa kuwepo mtengenezaji mwenye uweza usiyo na ukomo, hekima isiyo na ukomo, rehema isiyo na ukomo na ukarimu usiyo na ukomo, na yaliyomo ndani yake miongoni mwa hekima na mpangilio na uzuri wa uumbaji na faida, hali ambayo haiyumkini kuinasibisha na sadifu. Kwa yaliyomo ndani yake katika tofauti kubwa ya maonjo, pamoja na kurandana kwa nje – na hasa katika makundi ya madini kama chumvi, chumvi ya tindi kali, safa na shabu – na hasa mimea, kwa aina zake mbalimbali nyingi zinazotokana na mchanga rahisi, na kwa maua yake na matunda yake. Ukiachilia mbali kuwa hiyo inashuhudia juu ya umoja wa mtengenezaji na juu ya upekee wake; katika hali yake ya jumla ya umoja wa uendeshaji na uongozi, chimbuko, makazi na uumbaji, na usawa katika ufundi, pamoja na urahisi, wepesi, wingi na kasi katika uumbaji. Na vivyo hivyo hakika ya kuumba kila aina katika aina ya vitengenezwa vilivyokuwepo katika vilele vya milima na ndani yake, yenye kuenea kila upande katika pande za Ardhi, na kuvipatisha katika kipindi kimoja na kwa mtindo mmoja bila ya kosa wala kuchanganya, licha ya kuwa kuingiliana ndani ya aina nyingine, katika upeo wa ukamilifu na kasi na bila ya kukushughulisha kitendo na kitendo chochote. Inajulisha juu ya haiba ya Rububiyya yako na Adhama ya Uweza wako ambao haukishindi kitu. Na vivyo hivyo hakika kujaza vilele vya milima kwa miti na mimea, na matumbo yake kwa madini yenye kupangika na kuitiisha kwa kuitikia mahitaji ya walio hai wote utiishaji unaodhamini hata maradhi yao anuwai bali maonjo yake mbali mbali, na kushibisha hamu zake mbali mbali, unajulisha juu ya ukunjufu wa hali zote wa rehema yako na juu ya ukunjufu usiyo na ukomo wa utawala wako. Na vivyo hivyo kuhudhurisha kila chenye kujificha na kuchanganyika, na katika giza la matabaka ya udongo, mahudhurisho yaliyopangika kwa ujuzi na busara na bila ya mkanganyiko na kulingana na uhitaji. Inajulisha juu ya kuzunguka ujuzi wako wenye kuambatana na kila kitu, na juu ya hekima yako iliyopangika kwa kila kitu, na kuvienea vitu vyote. Na vivyo hivyo kuhudhurisha madawa na kulimbikiza maada ya kimadini inaashiria kwa uwazi na kujulisha dhahiri juu ya mazuri ya uongozi wako wa Rububiyya yako yenye wingi wa rehema na ukarimu na juu ya sifa nyororo za malimbikizo ya uangalizi wako. Na vivyo hivyo kufanya milima mirefu ni hazina za akiba zilizopangika na ghala zenye kukamilisha hazina za kidharura kwa maisha ya wageni wanaokuja katika nyumba ya wageni ya Ardhi na kukidhi haja zao katika mustakabali. Inaashiria na kujulisha bali na inashuhudia kwamba fundi wake ana ukarimu huu mkunjufu na mkarimu mwingi wa hekima mwenye upole na Mweza Mlezi. Hapana budi kuwa ana hazina za milele za neema zake za milele katika ulimwengu wa milele wa hao wasafiri na wageni wenye kupendwa kwake. Basi huko nyota zinatimiza jukumu ambalo milima hapa inalitimiza. Ewe Mweza juu ya kila kitu! Hakika milima na vilivyomo ndani yake miongoni mwa viumbe ni vyenye kutiishwa na vimewekwa akiba katika ufalme wako wewe, na kwa uweza wako wewe na kwa ujuzi wako na hekima yako wewe. Hakika inasabihi na kumtukuza Muumba wake ambaye amevipa majukumu na kuvitiisha kwa sura hii. Ewe Muumba Ewe Rahman! Ewe Rabi na ewe Rahiim! Hakika nimejua kwa mafunzo ya Mtume Mtukufu (s.a.w) na kwa darasa la Qur'an yenye hekima kwamba: Mithili ya mbingu, anga, ardhi, bahari na mlima inakutambua na kukutambulisha kwa yaliyomo na viumbe vyake, vilevile miti yote na mimea Ardhini inakutambua na kukutambulisha - kwa daraja la uwazi – kwa majani yake na maua yake na matunda yake, basi kila jani katika majani ya miti na mimea yenye kutetemeka kwa mawimbi ya dhikiri na shauku yake, na kila ua katika maua yenye kusifia na kutambulisha majina ya mtengenezaji wake kwa mapambo yake na kila tunda katika matendo yake yenye kutabasamu katika vipole vyake kwa kudhihiri rehema ndani yake. Vyote vinashuhudia, kwa nidhamu ambayo katika ufundi wake wa kufurutu ada, kwa kipimo ambacho kimo kwenye mpangilio, kwa pambo ambalo liko kwenye kipimo, kwa nakshi ambazo zimo katika mapambo na kwa ladha mbali mbali katika harufu nzuri za matunda, ni ushahidi wa kiwango cha uwazi haiyumkini kuinasibisha na sadifu juu ya kupasa kuwepo kwa mtengenezaji asiye na kikomo na rehema yake na wala hakuna ukomo wa ukarimu wake. Kama lilivyo jambo kama hivi kwa kila mmoja, basi miti yote na mimea kwa pamoja vivyo hivyo inashuhudia kwa uwazi juu ya umoja wa huyu Mtengenezaji ambaye ni wajibu kuwepo kwake na juu ya upekee wake; kwa umoja wake, kuafikiana kwake na upamoja wake juu ya uso wa Ardhi yote na kwa kurandana kwake na muhuri wa uumbaji na kwa kufungamana kwake katika kuendesha na kuongoza na kuafikiana kwake katika yanayo ambatana nayo katika matendo ya kupatisha na majina ya kiungu na kwa kuendesha vitu visivyokuwa na idadi vya sampuli mia moja elfu pamoja na kuingiliana kwake moja kwa pamoja bila ya mkanganyiko wala makosa. Na kadhalika kama ambavyo hao wanavyo shuhudia juu ya kupasa kuwepo kwako na juu ya umoja wako, hakika kutoa, kusimamia maisha na kuendesha vitu visivyo na mpaka ya kundi kubwa la walio hai katika jeshi kubwa lililoundwa kutokana na laki nne ya mataifa juu ya uso wa Ardhi uendeshaji kwa ufundi kamili na kwa mamia ya maelfu ya mitindo ya kulisha na kuendesha ambayo inatimia kwa ukamilifu wa mpangilio bila ya kusahau au kuchanganya. Yanajulisha juu ya utukufu wa Rububiyya yako (Ulezi wako wa kiungu) na haiba yake katika upekee wako, na juu ya Adhama ya uweza wako ambao unaumba majira ya machipuo kwa wepesi kupatisha ua na kuambatana kwake na kila kitu, na inajulisha kwa kukinaisha juu ya upana wa rehema yako ya hali zote ambayo inatayarisha mafungu ya vyakula anuwai mbalimbali na visivyokuwa na mpaka na kuvihudhurisha kwa wanyama wasio na mpaka na kwa binadamu katika kila upande miongoni mwa pande za Ardhi hii kubwa. Na hakika kwenda kwa mambo hayo, maneemesho, miundo ya uendeshaji na aina za kutunuku maisha na taratibu zisizo na mpaka, kwa ukamilifu wa mpangilio, na kufuata kila kitu na kunyenyekea kwake hata Atomu kwa amri na taratibu hizo, kunajulisha kwa kukinaisha kabisa juu ya ukunjufu wa hali zote wa utawala wako. Hakika kufanya kila kitu kwa kila jani, ua na tunda, na kwa kila shina na tawi, katika miti hiyo na mimea, kutenda kwa ujuzi na busara kulingana na zinavyohitajia faida na masilahi na hekima, inajulisha juu ya kuzunguka kwa ujuzi wako kila kitu na kuenea hekima yako kwa kila kitu ujulisho wa dhahiri shahiri, na inaashiria katika hayo kwa vidole vyake visivyo na mpaka. Na hakika hayo yanahimidi na kusifu kwa ndimi zake zisizo na mpaka juu ya uzuri wa ufundi wako na hali ukiwa katika ukomo wa ukamilifu, na juu ya ukamilifu wa neema yako nayo ipo katika ukomo wa uzuri. Na vivyo hivyo hakika ya hisani hizi za thamani na neema za thamani zenye kuenea, na matumizi haya na takirima hizi ambazo zinavuka juu ya mpaka,zinatufikia kwa mikono ya miti na mimea katika makazi haya ya muda na makao ya kutoweka ya wageni, na katika muda mfupi na umri mchache, zinaashiria bali zinashuhudia kuwa Mwingi wa rehema Mwenye uweza na ukarimu ambaye amezileta hapa kwa ajili ya wageni wake rehema zote hizi, hapana budi kuwa ameandaa miti yenye kuzaa matunda na mimea yenye kuchanua maua yenye kudumu milele kwa inavyowiana na Pepo ya kudumu milele katika ulimwengu wa milele katika ufalme wa milele kwa ajili ya waja wake ambao atawaweka milele na milele, ili azuilie mageuzi ya matokeo ya matumizi yake na neema zake ambazo amezigawa kwa ajili ya kutaka kupendwa kuwa dhidi ya hivyo - yaani wasiseme viumbe wote: Hakika ametuonjesha neema ile na katunyonga kabla hatujazitumia - na ili azuilie dhidi ya kuangusha haiba ya Uungu wake, na dhidi ya kukanusha ukunjufu wa rehema yake, na dhidi ya kugeuka wapendwa wake wote wenye kuwa na shauku naye kuwa ni maadui kwa kuwanyima. Ndiyo, hakika amezileta kutoka katika hazina za rehema za kudumu na katika pepo zake za kudumu. Na ambazo zilizopo hapa sio lolote isipokuwa ni kielelezo cha maonesho kwa wateja tu. Na kama ilivyo miti na mimea yote inakutukuza na kukusabihi na kukuhimidi kwa maneno ya majani yake na maua yake na matunda yake, kadhalika kila neno katika maneno hayo yenyewe yanakutukuza vilevile, na hasa kuumba matunda uumbaji wa ajabu na viini vyake anuwai, na ufundi wake wa ajabu na mbegu zake zenye kufurutu ada, na kuweka sahani za chakula hizo katika mikono ya miti na kuziweka juu ya vichwa vya mimea na kuzituma kama hivi kwa wageni wake hai kama anavyojaalia tasbihi za ndimi za hali yake kuwa ni dhahiri na wazi kabisa inafikia daraja ya ulimi wa maneno. Basi vyote hivyo ni vyenye kutiishwa katika ufalme wako wewe, na kwa nguvu yako na uweza wako wewe, na kwa kutaka kwako na hisani zako wewe na kwa rehema yako na hekima yako wewe, hakika ni yenye kufuata yenye kutii kwa kila amri itokayo kwako. Basi ewe aliyejificha kwa kuzidi kudhihiri! Na ewe aliyejifunika kwa adhama ya ukubwa! Ewe Mtengenezaji! Ewe Hakiim! Ewe Muumba ewe Mwenye Kurehemu! hakika mimi ninakuhimidi na kukusifu nikikutukuza wewe tu kuepukana na kasoro, kushindwa na kuwa mshirika, kwa ndimi za miti yote, mimea na majani yote na maua yote na matunda na kwa idadi yao. Ewe Muumba ewe Mweza! Ewe Mwenye kufanya tadbiri ewe Mwenye Hekima zote! ewe Mlezi ewe Mwenye kurehemu! Hakika nimejua kwa mafunzo ya Mtume Mtukufu (s.a.w) na kwa somo la Qur'an iliyojaa hekima na nimeamini kuwa: Kama ilivyo mimea na miti inakutambulisha na kukujulisha sifa zako takatifu na majina yako mazuri, basi hakuna katika walio hai wenye roho kama mwanadamu na wanyama hata mmoja asiyeshuhudia juu ya kupasa kuwepo kwako, na juu ya kuthibiti kwa sifa zako, kwa viungo vya mwili wake vya ndani katika hivyo na vya nje, vyenye kufanya kazi na vinavyopelekwa katika kufanya kazi – kama saa zilizopangika - na kwa ala zake na milango yake ya fahamu iliyowekwa mwilini mwake kwa nidhamu katika ukomo wa umakini na kwa mizani katika ukomo wa hisia kali na faida zenye umuhimu, na kwa vifaa vyake vya mwili vilivyoumbwa katika upeo wa ufundi, na kutandikwa katika ukomo wa hekima na vilivyowekwa katika upeo wa mizani. Kwa sababu ufundi huu makini kwa busara, na kwa hekima nyororo kwa utambuzi, na kulingamana mizani kutimilifu kwa tadbiri haiwezekani kuingilia ndani yake nguvu pofu wala asili bubu wala sadifu ya kiholela, wala haiyumkini kuwa mambo haya ni katika kazi zake. Ama kuundika kwake kwa nafsi yake mwenyewe hilo ni muhali katika mihali mia moja; kwa sababu yatakikana kila atomu katika atomu zake itambue na iyone na ifanye kila kinachohusu uundaji wa mwili wake, bali kila kitu kinachoambatana nayo duniani, basi imiliki elimu na uweza sifa mbili zenye kuzunguka kana kwamba hiyo atomu ni Mungu, kisha iyumkinike kuelekezwa uundaji mwili kwake na isemwe: Hakika hiyo imejiunda kwa nafsi yake yenyewe! Na kadhalika hakuna namna ya walio hai kwa ujumla; katika umoja wa uendeshaji na umoja wa uongozi na umoja wa sampuli na umoja wa jinsi na umoja wa muhuri wa umbile – vinavyo shuhudiwa kuafikiana kwake katika sura zake kwa jumla ikiwemo jicho, sikio na kinywa na kadhalika – na katika umoja wa muhuri wa hekima - wenye kudhihiri katika alama ya kila mmoja katika moja ya sampuli moja – na kutokana na upamoja katika kupewa maisha na kupatisha pamoja na kuingiliana baadhi yake katika baadhi. Isipokuwa inajumuisha ushahidi wa kukinaisha juu ya umoja wako na kuashiria upekee wako katika sifa ya umoja kwa kile ambacho anamiliki kila mmoja kati yao katika kudhihirisha majina yote yenye kuangalia kwenye ulimwengu. Na vivyo hivyo kama ilivyo kutiisha mamia ya maelfu miongoni mwa sampuli za wanyama zilizoenea pamoja na mwanadamu juu ya uso wa tandiko lote na uandaaji wake na mafunzo yake na kuzifanya kuwa ni tiifu kana kwamba ni jeshi lililopangika, na kupita amri za Rububiyya ndani yake kwa nidhamu ya hali ya juu inajulisha juu ya kiasi cha utukufu wa Rububiyya yako hiyo, hakika thamani ghali ya viumbe hivyo pamoja na kuwa viko katika upeo wa wingi, na kuvipatisha katika ukomo wa kasi pamoja na kuwa vimo katika upeo wa ukamilifu, na kuviumba katika ukomo wa wepesi pamoja na kuwa vimo katika ukomo wa ufundi, inajulisha kwa kukinaisha juu ya Adhama ya uweza wako. Na kadhalika kufikisha kwa riziki zako kwa viumbe hivyo vilivyoenea katika maeneo ya mbali ya mashariki na magharibi na kaskazini na kusini kuanzia kwenye kimelea kidogo na kukomea kwa mnyama mkubwa zaidi, na kutokea kwa mdudu mdogo zaidi na kwenda kwa ndege mkubwa, yanajulisha juu ya ukunjufu wa rehema zako za hali zote. Na vivyo hivyo kubadilika kwa uso wa Ardhi kila majira ya machipuo kuwa ni kambi kwa viumbe hivyo badala ya vile ambavyo huduma zake zimemalizwa katika majira ya mapukutiko na kutekeleza kila moja kati yake jukumu lake la kimaumbile kana kwamba ni askari mtiifu anakimbia upya, kunajulisha kwa namna ya kukinaisha juu ya ukunjufu wa utawala wako wa hali zote. Na vilevile kama ilivyo mnyama anavyoashiria ishara kwa idadi ya wanyama katika kuzunguka kuwa ujuzi wako unakizunguka kila kitu, na kuenea kwa hekima yako kwa kila kitu, kwa kuumba kwake kama nakala ndogo ya viumbe, kwa ujuzi katika upeo wa kina, na hekima katika upeo wa umakini, bila ya kuchanganya kati ya sehemu zenye kuchanganyika, bila kukanganyika kati ya sura zenye kutengana za wanyama wote, bila kosa, bila kusahau na bila kupunguza katika ufundi mwema na uzuri, katika yanayoifanya kuwa ni muujiza katika ufundi na kifurutu ada katika hekima. Inaashiria ukamilifu wa uzuri wa ufundi wako wa kiungu, na upeo wa uzuri wake, ufundi huo ambao unaupenda na unataka kuuonesha na kuusambaza. Na vilevile malezi ya kila mmoja kati yao na hasa wadogo malezi yaliyo katika upeo wa ulaini na upole, na kuitikia matakwa yao yote na matarajio yao, inaashiria ishara zisizo na mpaka uzuri wa kupendeza wa uangalizi wako. Ewe Rahman ewe Rahiim! Ewe Mkweli wa ahadi Mwaminifu! Ewe Mwenye kumiliki siku ya malipo! Hakika nimejua kwa mafunzo ya Mjumbe wako Mtukufu (s.a.w) na kwa maelekezo ya Qur'an yako yenye hekima tele kuwa: Maadamu uhai ni matokeo makuu zaidi yaliyochaguliwa kutoka katika ulimwengu, na roho ni muhtasari uliochaguliwa kutoka katika uhai, na wenye hisia ni matokeo safi kati ya vigawanyo vya wenye roho, na mwanadamu ni mwenye kukusanya sifa zote za wenye hisia, na viumbe wote kwa duru yao ni vyenye kutiishwa na vinajitahidi kutenda kwa ajili ya uhai, na wenye uhai ni wenye kutiishwa kwa wenye roho na wameletwa duniani kwa ajili yao, na wenye roho ni wenye kutiishwa kwa ajili ya mwanadamu na wapo katika kumsaidia yeye daima, na watu wanampenda Muumba wao mahaba safi kwa umbile lao, na Muumba wao anawapenda anapendezesha dhati yake kwao kwa kila njia, na maandalizi na utayari wa mwanadamu na zana zake za kimaanawy vinaangalia ulimwengu wa kubakia na uhai mwingine wa milele, na kwamba moyo wake na hisia zake vinataka kubakia, na kwamba ulimi wake unaomba kwa Muumba wake kwa dua zisizo na mpaka ukiomba kubakia, basi haiyumkini kwa hali zote kuwaghadhibisha watu wapenzi na wapendwa na kuwakasirisha kwa uadui wa milele kwa kutowafufua baada ya kuwafisha, nao asili wameumbwa kwa ajili ya mahaba ya milele na wameletwa katika dunia hii kwa hekima kwa ajili ya kupata maisha ya furaha katika ulimwengu mwingine wa milele. Kisha hakika majina mazuri yenye kudhihiri katika mwanadamu yanaashiria kwamba ambaye ni kioo chenye kuakisi midhihirisho ya majina hayo katika uhai huu mfupi wa kutoweka atapata midhihirisho ya milele katika ulimwengu wa kubakia. Naam, hakika mwandani wa kweli wa mwenye kubaki milele atakuwa wa milele, na kwamba kioo chenye kutambua cha mwenye kubakia kinalazimu kubakia, na kama inavyofahamika kutoka katika riwaya sahihi: Hakika roho za wanyama zitabaki daima, na kwamba roho za baadhi ya vitu maalum miongoni mwa wanyama zitapita kuelekea katika ulimwengu wa kubakia pamoja na viwiliwili vyake; kama hudihudi na mdudu chungu wa Suleiman (a.s), ngamia wa Salehe (a.s), na mbwa wa As’habul Kahfi, na kwamba kila sampuli kati ya hao itachukua mwili ili kuutumia wakati mwingine, basi hekima na hakika na vivyo hivyo rehema na Rububiyya (Ulezi wa kiungu) vyote vinahitajia hilo. Ewe Mweza Msimamizi! Hakika wote wenye uhai na roho na wenye utambuzi wamepewa majukumu ya kimaumbile katika ufalme wako wewe, na wametiishwa kwa amri za Rububiyya yako wewe, na kwa nguvu zako wewe na uweza wako peke yako, na utashi wako na uongozi wako na rehema yako na hekima yako. Na hakika ya fungu kati yao limetiishwa na kudhalilishiwa kwa ajili ya mwanadamu kutoka katika rehema yako, sio kwa nguvu yake na kushinda kwake bali kwa udhaifu wake na kushindwa kwake kimaumbile. Basi kila mnyama anatekeleza ibada yake mahsusi kwake, kwa ulimi wa hali na kauli kwa kumsabihi Muumba wake, Mtengenezaji na Mwabudiwa wake hali ya kumtakasa yeye kutokana na kasoro na shirki hali ya kuhimidi na kushukuru kwa neema zake. Subhanaka Ewe uliyejificha kwa kudhihiri mno! Subhanaka ewe uliyejifunika kwa Adhama ya ukubwa! Hakika mimi nakutakasa kwa tasbihi za wenye roho wote hali nikinadi: Subhanaka, ewe uliyejaalia kutokana na maji kila kitu hai. Ewe Mlezi wa Walimwengu! Ewe Mola wa Awali na wa Mwisho! Ewe Mlezi wa Mbingu na Ardhi! Hakika nimejua kwa mafunzo ya Mjumbe wako mtukufu (s.a.w) na kwa darasa la Qur'an yenye hekima tele na nimeamini kwamba: Kama zilivyo Mbingu, anga, Ardhi, bara, bahari, miti, mimea na wanyama, vinakutambua kwa mmoja mmoja wake na sehemu zake na Atomu zake, na vinashuhudia juu ya kuwepo kwako na juu ya umoja wako, na vinajulisha hayo na kuashiria, basi hakika ya Manabii, Mawalii na Wateule ambao wao ni muhtasari wa sampuli ya mwanadamu ambaye ni muhtasari wa wenye uhai ambao ni muhtasari wa ulimwengu, wanashuhudia na kuhabarisha wajibu wa kuwepo kwako, umoja wako na upekee wako, kuhabarisha kwenye kukinaisha kwa nguvu ya mamia ya ijmai na mamia ya Tawatur yenye kuegeme shahidi za nyoyo zao na akili zao na funuo zake na matoleo yao na ukinaifu wao, na wa nathibitisha maelezo yao kwa miujiza yao na karama zao na hoja zao za yakini. Naam, hakuna wazo la ghaibu nyoyoni linaloashiria dhati yenye kuelezea hilo kwenye sitara ya ghaibu, na humo hakuna ilhamu ya kweli inawajibisha kuona dhati yenye kuleta ilhamu humo, na hakuna humo itikadi ya yakini inafunua sifa zako za utakatifu na majina yako mazuri kufunua kwa haki ya yakini, na hakuna katika Mitume na Mawalii moyo wa kinuru unaoshuhudia nuru za ambaye ni wajibu kuwepo kwa dhati ya yakini, na hakuna katika wateule na masidikina akili yenye nuru inayosadikisha aya za kupasa kuwepo kwa Muumba wa kila kitu na anayethibitisha hoja za umoja wake kwa elimu ya yakini, isipokuwa na inashuhudia kwa ushahidi na inamiliki kujulisha na inaonesha ishara juu ya kupasa kuwepo kwako na juu ya sifa zako tukufu na juu ya umoja wako na juu ya Upekee wako na juu ya majina yako mazuri. Na hakuna muujiza katika miujiza ya dhahiri yenye kusadikisha habari za Bwana wa Manabii wote, Mawalii, Wateule, Masidikina na Raisi wao, mchujo wao ni huyo Mtume Mtukufu (s.a.w), na hakuna hakika katika hakika zake za hadhi ya juu yenye kudhihirisha uhakika wake, na hakuna aya katika aya za Tawhidi zenye kukinaisha ya Qur'an yenye ubainifu wa kimiujiza ambayo inaweka muhtasari wa vitabu vyote vitakatifu vya haki, wala Suala la kiimani katika masuala yake matakatifu, isipokuwa yanashuhudia ushahidi na yanamiliki ujulisho na kuonesha ishara juu ya wajibu wa kuwepo kwako katika sifa zako takatifu na juu ya umoja wako na juu ya upekee wako na juu ya majina yako mazuri na juu ya sifa zako za dhahiri. Na kama wanavyoshuhudia wote hao waelezaji wa kweli ambao wanahesabiwa kwa mamia ya maelfu - hali ya kuegemea katika miujiza yao na karama yao na hoja zao – juu ya kuwepo kwako na juu ya umoja wako, hakika wao wanaelezea – na wanathibitisha kwa ijmai na kwa kuwafikiana – juu ya kiasi cha ukubwa wa utukufu wa Rububiyya tukufu inayokwenda kuanzia katika kuendesha mambo ya jumla ya Arshi tukufu yenye kuzunguka kila kitu, hadi katika kutambua michakato iliyojificha zaidi na mawazo ya kisehemu ya nyoyo, siri zake na matumaini yake na dua zake na kuzisikiza na kuziendesha. Na wanatangaza kiasi cha utukufu wake na uweza wake ambao unapatisha vitu mbali mbali visivyo na mpaka - mbele ya macho yetu – mkupuo mmoja, na unaumba kitu kikubwa mno kwa wepesi wa kuumba mdudu mdogo mno, bila ya tendo kuzuia tendo lolote. Na kama ambavyo wanavyoelezea – na wanathibitisha hilo kwa miujiza yao na hoja zao – juu ya ukunjufu wa Rehema yako ya hali zote ambayo imeufanya ulimwengu katika hali ya Kasri kubwa la wenye roho na hasa kwa mwanadamu, na ambayo imeandaa pepo na furaha ya milele kwa majini na watu, na ambayo katika hali zote haisahau kiumbe mdogo zaidi aliye hai na inafanya hima kuutuliza moyo wenye kushindwa zaidi na kuufanyia upole. Na juu ya ukunjufu wa utawala wako wa hali zote ambao unatiisha, kupanga majukumu na kunyenyekesha kwa amri zake sampuli zote za viumbe kutokea kwenye Atomu hadi kwenye sayari. Hakika wanashuhudia na kujulisha na kadhalika wanaashiria – kwa ijmai na kuafikiana – katika kuzunguka ujuzi wako wenye kuzunguka kila kitu ambao umeijaalia Ardhi kuwa hali ya kitabu kikubwa kinajumuisha barua kwa idadi ya sehemu zake, na ambayo imesajili matukio yote ya viumbe katika (إمَام مُبِيْن) na katika (كِتَاب مُبِيْن) nazo ni daftari mbili za (اللَّوْحٍ المَحْفُوْظ), na ambaye amezipa mbegu mihtasari ya miti na mifumo yake yote, na ambaye ameelekeza katika nguvu zote za kuhifadhi (Utunzaji wa kumbukumbu) katika vichwa vya wenye utambuzi historia za maisha yao kwa mpangilio na bila ya kukosea. Na wanashuhudia vilevile juu ya kuenea kwa hekima yako takatifu kila kitu, ambayo imevika kila kilichopo hekima nyingi mno, hata kwamba imeupa kila mti matokeo kwa idadi ya matunda yake kwa vile inavyosaidia, na kwa maslahi iliyoyaweka kwa kila chenye uhai kwa idadi ya viunge vyake, bali kwa idadi ya sehemu zake na seli zake, hata kwamba pamoja na kukabidhi kwake majukumu kwa ulimi wa mwanadamu majukumu mengi basi amemuandaa vilevile na vipimo vya kivionjo kwa idadi ya maonjo ya vyakula. Nao wanashuhudia vilevile juu ya kuendelea midhihirisho ya majina ya utukufu na uzuri – iliyo dhahiri athari zake kwenye hii dunia - na kudumu kwake kwa sura angavu mno na wazi mno katika milele na milele, na kuendelea neema zako zenye kushuhudia mifano yake katika dunia hii yenye kutoweka na kubakia kwake kwa udhahiri mno na mng’aro mno katika makazi ya furaha, na juu ya kuafikiana kwake na wenye shauku ambao wameipata katika hii dunia na kusuhubiana nao katika kudumu milele. Basi Mtume Mtukufu (s.a.w) – katika utangulizi – akiwa ameegemea katika mamia ya miujiza ya dhahiri, na Qur'an tukufu kwa kuegemea aya zake zenye kuamua, kisha manabii wote (a.s) nao ni wenye roho zenye nuru, na mawalii wote nao ni mihimili ya wenye nyoyo za kinuru, wanawabashiria watu na majini furaha ya milele na wanawaonya wapotevu na Jahanamu - nao wanaamini hili na wanashuhudia juu yake - kwa kuegemea niliyoyataja mara kwa mara na kwa kukariri katika ahadi na makemeo katika vitabu vyote vya mbinguni na sahifa takatifu, na kwa kutegemea sifa zako na mambo yako matakatifu kama uweza na rehema na uangalizi na hekima na Jalali na uzuri, na kwa kuaminika kwa enzi ya Jalali yako na ufalme wa Rububiyya yako, na wanabashiria kwa funuo zao na shuhuda zao na kwa itikadi yao iliyojikita kwa elimu ya yakini. Ewe Mweza Ewe Mwenye hekima zote, Ewe Rahman Ewe Rahiim, Ewe Mkweli wa ahadi, Mkarimu, Ewe Mteza nguvu, Mwenye Jalali na Ewe Mwenye Ushindi na Utukufu na Adhama na Jalali! Hakika wewe ni Mtukuzwa wa hali zote, nawe ni mwenye sifa za juu mtakaswa wa hali zote za kusifiwa na uongo idadi yote hii ya mawalii wako wa kweli, ahadi zako nyingi, sifa zako tukufu na mambo yako matakatifu, unasitiri yanayohitajia kwa hali inayolazimu ufalme wa Ulezi wako wa kiungu na unajibu kiasi kisichohesabika cha dua zinazotoka kwa wasio hesabika katika waja wako wenye kukubaliwa ambao umewapenda nao wakakupenda na wakazipendezesha nafsi zao kwako kwa imani na kusadikisha na utiifu. Basi hakika yako wewe umetakasika na hakika yako wewe una sifa za juu wa hali zote ni mkwasi wa kusadiki kwa watu wa upotevu na ukafiri ambao wanapinga Adhama ya Ukubwa wako katika kukanusha kwao ufufuo, na wanasababisha kukiuka enzi ya utukufu wako, na wanagusa haiba ya Uungu wako na upole wa Rububiyya yako kwa ukafiri wao na uasi wao na kukukanusha kwao wewe katika ahadi yako. Basi mimi ninatukuza uadilifu wako na uzuri wako na Rehema yako isiyokoma - bila mpaka wala ukomo – na ninautakasa na dhulma hii na ubaya visivyokoma na ninapenda nisome kwa idadi ya Atomu uwepo wangu aya tukufu: سُبْحَانَهُ وَتَعَالَى عَمَّا يَقُولُونَ عُلُوًّا كَبِيرًا bali hakika ya Mitume yako ya kweli - hao ambao wao ndio walinganiaji wa hakika wa ufalme wako - wanashuhudia na wanabashiri na wanaashiria kwa haki ya yakini na kwa dhati ya yakini na ujuzi wa yakini katika hazina za rehema yako za kiakhera na hifadhi ya neema zako katika ulimwengu wa kubakia, na katika kufunuka kwa midhihirisho ya majina yako mazuri midhihirisho timamu yenye kufurutu ada katika nyumba ya furaha, na wanawaelekeza waja wako waumini kwamba mwonzi mkubwa wa jina la ( الحقّ ) ambalo ni rejea ya hakika zote na jua lake na mlinzi wake ni hakika ya ufufuo mkubwa. Ewe Bwana Mlezi wa Manabii na Masidikina! Hakika ya hao wote ni wenye kutiishwa na kupewa majukumu katika ufalme wako wewe, kwa amri yako, uweza wako Wewe, kwa kutaka na kuendesha kwako Wewe, kwa elimu yako na hekima yako Wewe, na wamekwisha dhihirisha tufe la Ardhi kwa kutukuza, tasbihi, takbira, tahmidi na tahalili katika hali ya mahali pakubwa mno kwa dhikiri na kuudhihirisha ulimwengu kuwa katika hali ya msikiti mkubwa mno. Ewe Bwana mlezi wangu, na ewe Bwana Mlezi wa Mbingu na Ardhi! Ewe Muumba wangu, na ewe Muumba wa Kila Kitu! Kwa haki ya uweza wako na utashi wako na hekima zako na utawala wako na rehema yako ambayo umezitiisha mbingu kwazo kwa nyota zake, Ardhi na vilivyomo, na viumbe vyote kwa hali zake zote na sampuli zake: Nitiishie nafsi yangu, nitiishie matulubu yangu na zitiishe nyoyo za watu kwa Risale-i Nur ili waitumikie Qur'an na Imani. Na nitunuku mimi na ndugu zangu Imani kamili na mwisho mwema. Na kama ulivyoitiisha bahari kwa Musa (a.s), na umeutiisha moto kwa Ibrahim (a.s), na umeutiisha mlima na chuma kwa Daudi (a.s), na umetiisha watu na majini kwa Suleiman (a.s), na umetiisha Jua na Mwezi kwa Muhammad (a.s), tiisha nyoyo na akili kwa Risale-i Nur. Na unihifadhi na uwahifadhi wanafunzi wa Risale-i Nur kutokana na shari ya nafsi na Shetani na kutokana na adhabu ya kaburi na kutokana na Moto wa Jahanamu, na utupe furaha katika Firdausi ya Peponi. Amin, Amin, Amin. سُب۟حَانَكَ لَا عِل۟مَ لَنَٓا اِلَّا مَا عَلَّم۟تَنَٓا اِنَّكَ اَن۟تَ ال۟عَلٖيمُ ال۟حَكٖيمُ وَ اٰخِرُ دَع۟وٰيهُم۟ اَنِ ال۟حَم۟دُ لِلّٰهِ رَبِّ ال۟عَالَمٖينَ Hakika ya somo hili ambalo nimelichota kutoka katika Qur'an tukufu na kutoka katika Al–Jawshan Al-Kabiir - ambao ni Munajat wa Mtume (s.a.w) - ninauonesha katika mlango wa Bwana wangu Mlezi Mwingi wa rehema ikiwa ni ibada ya kifikra. Ikiwa umepatikana kutoka kwangu upungufu basi mimi nakimbilia hifadhi kwa rehema yake kwa kutaka shufaa ya Qur'an tukufu na Al-Jawshan al-Kabiir hali ya kutarajia msamaha kunako upungufu wangu. Said Nursî

