Ujumbe huu ulikuwa ni kumbukumbu ya kumi na sita kutoka katika (mwale wa kumi na saba), ila kwamba umuhimu wake wa hali ya juu, umeufanya kuwa ni (mwale wa ishirini na tatu) kwani unateketeza mikondo ya ukafiri inayotokana na mtazamo wa Asili, kuteketeza kabisa na kulisaga jiwe la msingi la ukafiri na kuvunja ngome yake ya msingi. Tanbihi: Kumbukumbu hii imebainisha kiini cha mrengo ambao wanaopita wapingaji miongoni mwa wana Asili, na imefafanua kiasi gani mrengo wao huo ni mbali na vipimo vya akili, na kiasi cha udhaifu wake na uzushi wake, na hii ni kupitia muhali tisa ambazo zimefupishwa kutoka katika muhali tisini kwa uchache. Na ilipokuwa sehemu ya muhali hizo imeshafafanuliwa katika risala nyingine, hapa imekuja ikiratibiwa sehemu ya muhali nyingine, au imekuja kwa muhtasari kidogo. Na swali ambalo linapita moyoni ni: Vipi wanafalsafa mashuhuri na wanazuoni maarufu wameridhia uzushi huu wenye kufedhehesha na kuzisalimisha hatamu za akili zao? Jibu: Hakika ya hao wanafalsafa hawakubaini ukweli wa maslaki yao, (mrengo), wala undani wa madhehebu yao, na hawakutambua maslaki yao yanavyolazimu kufahamika katika muhali, na yanavyolazimu mambo kadhaa yasiyofaa na kushindikana kwa akili, na ambayo yametajwa mwanzoni mwa kila muhali uliyokuja kwenye risala hii. Na mimi niko katika utayari kamili kusimamisha hoja zenye kuvunja batili na za wazi, ili kuweza kuthibitisha hayo kwa kila ambaye inamnyemelea shaka na nitawabainishia kwa ukunjufu na upambanuzi. بِسْمِ اللّٰهِ الرَّحْمٰنِ الرَّح۪يمِ قَالَت۟ رُسُلُهُم۟ اَفِى اللّٰهِ شَكٌّ فَاطِرِ السَّمٰوَاتِ وَال۟اَر۟ضِ Aya hii tukufu na yaliyomo yote miongoni mwa maulizo ya namna ya hali ya ukanushi, yanajulisha kwa namna ya kukata shauri kabisa juu ya kuwepo kwa Allah (sw), na upekee wake kwa uwazi mno. Na kabla ya kuweka wazi siri hii, tunapenda kutanabahisha yafuatayo: Nilialikwa kuzuru Ankara mwaka 1338 (1922 AD) na nikashuhudia furaha, na sherehe za waumini kwa kushindwa kwa Wagiriki mbele ya jeshi la kiislamu, isipokuwa niliona katikati ya wimbi la furaha hii ukafiri wa kutisha unaonyemelea kwa uovu na hila, na kujipenyeza kwa mitazamo yake mibaya kuelekea kwenye itikadi thabiti za watu wa imani kwa kutafuta kuziharibu na kuzitia sumu. Nikasikitika kutokea kina cha roho yangu na nikapiga kelele kwa kuomba msaada kwa Allah Mtukufu Mwenye uweza, na kushikamana na ngome ya aya hii tukufu kutokana na zimwi hili la kutisha ambalo linataka kuingilia nguzo za imani, nikaandika ushahidi wa nguvu mkali unaokata kichwa cha ukafiri huo, katika risala kwa lugha ya kiarabu na nikachota maana yake na fikira zake kutoka katika nuru ya aya hii tukufu, ili kuthibitisha udhahiri wa kuwepo kwa Allah (sw), na upweke wake. Nimeichapisha kwenye kiwanda cha kuchapa cha Yeni kon huko Ankara. Isipokuwa sikuona athari madhubuti katika kupambana na makafiri na kusimamisha kutambaa kwake kuelekea katika fikira za watu. Na sababu yake ni kuwa muhtasari wa jumla sana, ukiachilia mbali uchache wa wanaojua vema lugha ya kiarabu nchini Uturuki, na kuwa nadra kwa wenye kutilia umuhimu lugha hiyo wakati ule, na kwa ajili hiyo mawazo potofu ya kufuru yakaenea na kuanza kuharibu katika safu za watu kwa masikitiko makubwa, jambo ambalo limenilazimisha kuandika tena risala ile pamoja na hoja zake kwa lugha ya Kituruki pamoja na kiasi kidogo cha ufafanuzi, hivyo ikawa risala hii. Kwa kuwa baadhi ya sehemu ya hoja hizo zimefafanuliwa vya kutosha katika baadhi ya Risale-i Nur, hapa tutazitaja kwa muhtasari, kama zilivyo baadhi ya hoja nyingine zilizotawanywa ndani ya risala nyingine zinaonekana kuingia katika risala hii, kana kwamba kila hoja kati yake ni sehemu ya risala hii.
Source text is preserved. When a suitable model is available, translation is displayed separately.
Tabiat Risalesi
The Twenty-Third Gleam
Ewe mwanadamu! Tambua kwamba kuna maneno ya kutisha ambayo kutokana na maneno hayo harufu mbaya ya ukafiri inanuka. Maneno yatokayo kwenye vinywa vya watu, na watu wa imani wanayarudiarudia maneno hayo pasi na kujua hatari ya maana ya hayo wanayoyasema. Tutabainisha matatu kati ya maneno hayo ambayo ni katika upeo wa hatari: Kwanza: Kusema kwao kuwa (kitu kimepewa uwepo na sababu), yaani sababu ndizo zilizofanya uwepo wa kitu maalumu. Pili: Kusema kwao kuhusu kitu kuwa (kimejiunda chenyewe), yaani kitu kinajiunda chenyewe kujifanya kiwepo chenyewe na kuishia katika sura yake ambayo iliyokuwa kama ilivyo. Tatu yake: Kusema kwao kuwa kitu (Asili imekilazimisha na kukifanya kiwepo), yaani kwamba kitu ni cha kiasili na kwamba Asili ndiyo iliyokijaalia kiwepo na kukilazimisha. Ndio, kwa kuwa viumbe vipo na vyenye kusimama mbele yetu kwa namna ambayo haiwezekani kukanusha hilo kabisa, na kwamba kila kiumbe huja katika uwepo katika upeo wa uzuri na hekima, naye sio wa tangu azali, bali ni mwenye kuzushwa mpya. Ewe mwenye kukana Mungu! Ima wewe unasema kuwa hiki kiumbe kwa mfano iwe mnyama huyu sababu za ulimwengu hufanya apatikane, huvuna uwepo ikiwa ni matokeo ya kukusanyika sababu za kimaada au amejitengeneza mwenyewe au hupatikana katika uwepo kwa kulazimishwa na Asili na hujitokeza kwa kuathiri kwake! Au ni juu yako kusema: Kwamba uweza wa Muumba Muweza Mwenye utukufu ndio ambao unamfanya awepo. Kwani hakuna njia ya kuzuka kwake isipokuwa njia hizi nne, kulingana na vipimo vya akili. Itakapothibitishwa uthibitisho wa kukata shauri kwamba njia tatu za mwanzo ni muhali, batili, zenye kushindikana, haziyumkiniki basi kwa dharura na udhahiri inathibiti njia ya nne, nayo ni njia ya upweke wa Muumba; kwa yakini ya kuamua kabisa hapana shaka ndani yake.
Ambayo ni kusema kuwa: (Kukusanyika sababu za ulimwengu huumba viumbe na kuvifanya viwepo na kupelekea kuunda vitu) katika hilo tutataja muhali tatu tu, kati ya muhali nyingi sana. MUHALI WA KWANZA: Acha tuufafanue kwa mfano huu: Duka la dawa lina mamia ya gudulia na chupa ndogo ndogo zilizojaa maada za kikemia anuwai tukahitajia maajuni kwa sababu maalumu (mchanganyiko wa dawa za unga na maji) ya kiuhai kutokana na maada na dawa hizo; ili kutengeneza maada ya ajabu yenye kupambana na sumu. Tulipoingia kwenye duka la dawa tukakuta humo idadi kubwa mno katika aina za maajuni ile ya kiuhai na katika maada ile ya kiuhai yenye kukinzana na sumu, na tulipoanza kupembua kila maajuni tulikuta kuwa imetengenezwa hali ya kuandaliwa kwa umakini ikitofautiana kutokana na maada mbalimbali kulingana na vipimo vilivyohesabiwa. Kutokana na gudulia hizo imechukuliwa kiasi cha gramu moja kutokea hapa, na tatu kutoka pale, na gramu kumi kutoka katika chupa nyingine, hivyo hivyo imechukuliwa kutokana na zote hizo viwango tofauti, kwa namna ambayo kama ingekuwa kilicho chukuliwa humo ni kichache kuliko gramu moja, au kuzidishwa, basi maajuni ile ingekosa sifa zake maalumu za uhai. Na sasa tumekuja katika (maada ya uhai yenye kupambana na sumu) na tukaitazama kwa makini kikemia, tukaiona kuwa imetengenezwa kwa vipimo maalumu vimechukuliwa kutoka katika magudulia yale kwa mujibu wa vipimo nyeti kwa kiasi ambacho hupoteza uwezo wake wa kufanya kazi kama tungekosea katika mahesabu, maada zilizotengenezewa zikazidi au kupungua kwa kiasi cha Atom (chembe ndogo kabisa kuliko vumbi isiyoweza kugawika zaidi kwa udogo). Tunafupisha: Kwamba, maada tofauti zimeandaliwa kwa viwango tofauti kulingana na vipimo madhubuti. Je, inawezekana au inaingia akilini kuwa maajuni hiyo iliyohesabiwa kila sehemu miongoni mwa sehemu zake mahesabu madhubuti eti yatokane na usadifu wa ajabu, au kutokana na matokeo ya kugongana kwa magudulia, kwa kutokea kwa tetemeko la ardhi lililolikumba duka la dawa imepelekea kutiririka viwango hivyo kwa vipimo vyake maalumu, na kuungana pamoja sehemu yake na nyingine, na kutengeneza maajuni ya kiuhai? Je, kuna muhali wowote wa ajabu kuliko huu? Na wa mbali zaidi na akili na mantiki? Je, kuna uzushi wa kioja zaidi kuliko huu? Je, kuna batili ya wazi zaidi kuliko hii? Hata punda mwenyewe, laiti upumbavu wake ungeongezeka na akaweza kutamka angesema: Ee, upumbavu ulioje wa anayesema kauli hii! Katika mwanga wa mfano huu tunasema: Kwamba kila kiumbe hai ni kitu kilichoundwa na sehemu mbalimbali hai, maajuni yenye uhai, na kwamba kila mmea ni mfano wa dawa ya uhai dhidi ya sumu; kwani imeundwa kutokana na sehemu tofauti na kulingana na vipimo madhubuti katika ukomo wa unyeti. Hapana shaka kuegemeza uumbaji wa kiumbe huyu wa ajabu kwa sababu za kimaada na chembe, na kusema kuwa: Sababu zimefanya kiwepo ni batili na muhali mbali na vipimo vya akili, kama mfano wa ubatili wa kuwa muhali kwa kufanyika maajuni ya uhai yenyewe kutokana na kutiririka kwa maada hizo kutoka katika gudulia. Kwa ufupi: Kwamba maada za uhai zilizoandaliwa, kwa mizani ya hukumu na Qadar ya Mwingi wa hekima, Mjuzi wa kila kitu katika ulimwengu huu mkubwa, ambao ni duka kubwa la dawa la kushangaza na kupendeza haliwezi kupatikana isipokuwa kwa hekima zisizo na mpaka, elimu isiyo na ukomo, na utashi unaokienea kila kitu na kukizungukia kila kitu, na kama siyo hivyo, shida ilioje kwa anayedhania kuwa viumbe hivi ni matokeo ya vijisehemu vya ulimwengu mzima, nazo ni pofu kiziwi katika kutembea kwake na kufoka kwake au, ni katika mambo ya Asili ya maada au kutokana na kazi ya sababu za kimaada! Hapana shaka mwenye dhana hii ni muovu mno kuliko wote ulimwenguni, mpumbavu zaidi, na mwenye kuweweseka kuliko mlevi aliyepoteza fahamu anapofikiria akilini mwake kuwa dawa ile ya ajabu imejitengeneza yenyewe kupitia mgongano wa chupa na kutiririka vilivyomo! Naam, ukafiri huo ni kuweweseka kwa bahau na wazimu wa mlevi. MUHALI WA PILI: Ni kwamba, kama uumbaji wa kila kitu haukuegemezwa kwa Mmoja wa pekee, Muweza Mtukufu, na kuegemezwa kwa sababu za kimaada, hapo italazimu aghalabu ya chembe za ulimwengu na sababu zake ziwe zenye kuingilia na kuathiri katika uwepo wa kila chenye ya uhai, na hali ya kuwa kukusanyika sababu zinazokinzana na kutofautiana kati yake, kwa mpangilio kamili, na kwa kipimo madhubuti kwa kuafikiana kikamilifu ndani ya mwili wa kiumbe mdogo kama nzi kwa mfano, hilo ni muhali dhahiri kwa kiasi ambacho mwenye akili japo kidogo kiasi cha ubawa wa nzi atalikataa, na kupinga kwa kusema: Hili ni muhali, batili, haliyumkiniki! Na hiyo ni kwa sababu mwili mdogo wa nzi una uhusiano na ghalibu ya chembe za viumbe, pamoja na mionekano yake na sababu zake kimaada, bali huo ni muhtasari uliofupishwa kutokana na viumbe hivyo. Kama uumbaji wake haukuegemezwa kwa uweza wa kiungu usio na kikomo, italazimu hizo sababu za kimaada ziwepo na zikusanyike kando ya mwili huo sawia wakati wa uumbaji wake, bali italazimu kuingia ndani ya mwili wake mdogo, bali inapasa ziingie katika kijichumba cha jicho ambalo linashika nafasi kama kielelezo cha mwili; kwa sababu kama zitakuwa ni za kimaada inalazimu ziwe karibu na ndani ya msababishwa, na hapo itapasa kuingia chembe zote katika pembe zote za ulimwengu, pamoja na Asili zake tofauti ndani ya msababishwa huyo kuingia kimaada, na kufanya kazi katika hicho chumba kidogo kupita kiasi kwa umahiri na ustadi. Hivi haogopi na kuona haya kutokana na kauli hii, hata mpumbavu mkubwa kuliko wanafalsafa wapotevu (safsatiyyin). MUHALI WA TATU: Kwamba kiumbe kikiwa na sehemu za namna moja, hapana budi ziwe zinatokana na kiathiri kimoja, mkono mmoja, kulingana na kanuni dhahiri isemayo (kimoja hakitokani ila kwa mmoja). Ikiwa hicho kiumbe kiko katika upeo wa mpangilio na ukomo wa umakini na ufundi, na kuwa na uhai wa jumla, iliyo dhahiri ni kuwa kiumbe hicho katu hakikutokea kutoka kwa mikono mingi ambayo inapelekea hitilafu na kugombana, bali hapana budi kuwa hicho kimetokana na mkono mmoja wa mmoja pekee, Muweza wa kila kitu, Mwingi wa hekima, kwa ajili hiyo, kuegemeza kiumbe kilichopangiliwa, kuratibiwa, kuwa katika vipimo, kimoja, kwenda katika mikono ya sababu za kiasili pofu, kiziwi, mfu, zisizodhibitika, hazina hisia wala akili, nazo zikiwa katika mchanganyiko sana unazidi kuliko upofu wake na uziwi wake, kisha kudai kuwa sababu hizo ndizo zenye kuumba kiumbe huyo wa ajabu, na kumchagua kati ya yamkini na makisio yasiyo na mpaka. Nasema kuwa kukubali kutegemeza huku na madai haya, kwa hakika ni kukubali muhali mia moja na moja, kwani ni mbali mno na vipimo vya akili. Ebu tuache muhali huu na tuuvuke kwa muda, tutazame taathira ya sababu za kimaada, ambayo hutimia kwa kuungana na kugusana. Wakati ambapo tunaona kugusana kwa sababu hizo za kiasili ni kugusana na kiumbe hai kwa nje tu, na tunaona ndani ya kiumbe hicho ambako mikono ya hizo sababu za kimaada hazifikii na haziwezi kugusa kwa chochote, ndiko kwenye mpangilio madhubuti mno, na kwenye kusukwa vyema zaidi kuliko nje, bali ni laini mno kwa umbo na kumetengenezwa kwa ustadi uliokamilika mno. Bali viumbe hai vidogo vidogo na ambavyo sababu hizo za kimaada haziwezi kuvienea kabisa na wala mikono yake haifikii wala nyenzo zake, viumbe hivyo ni vya ajabu zaidi kuliko viumbe vikubwa na vina maumbo ya kushangaza zaidi. Hivyo, kurejesha uumbaji wake kwa hizo sababu za kimaada pofu, ziwi, mfu, ngumu, zilizo mbalimbali, na kinzani, haiwi ila ni upofu ambao hakuna upofu mwengine baada ya huo na uziwi hakuna zaidi yake uziwi mwingine.
Kusema kwao kuhusu kitu: (Kimejiunda chenyewe), hii inabeba muhali nyingi, na ubatili wake na kuwa kwake muhali kunabainika kwa pande nyingi sana, isipokuwa hapa tutaelezea muhali tatu tu kati ya hizo kama mifano na si vinginevyo: MUHALI WA KWANZA: Ewe mpingaji mkaidi! Kuchupa mipaka kwa ghururi yako, kumekufanya udondoke katika uzuzu mkubwa na kuendea kukubali muhali mia moja na moja! Ewe mpingaji mkaidi! Upo bila shaka, nawe hutokani na maada ndogo kabisa na mfu ambayo inakataa kubadilika, bali wewe ni maabara kubwa iliyotengenezwa kwa ufundi, zana zake zinakuja upya daima, nawe ni kama kasri nzuri, pande zake ni zenye kudumu kubadilika, basi chembe za uwepo wako wewe zinafanya kazi daima na bila ya kusimama zinafungamana na mafungamano na mahusiano pamoja na ulimwengu unaokuzunguka, zimo katika kuchukua na kutoa pamoja na viumbe, na hasa upande wa riziki na upande wa kubaki kwa sampuli (yaani aina ya kila kiumbe). Hakika ya chembe ndogo kabisa zinazofanya kazi mwilini mwako zinafanya jitihada ili mafungamano hayo yasiharibike, na kuepuka kukatika uhusiano huo. Kwa hiyo, kufanya kwake hivyo huchukua tahadhari na kushika msimamo ufaao kwake kulingana na mahusiano hayo, kana kwamba inatazama viumbe vyote, na kisha kuangalia hali yako wewe, na kwa zamu yako pia unafaidika kwa mujibu wa hali hiyo ya ajabu ya hivyo vichembe vidogo vidogo kabisa na unanufaika na kustarehe kwa hisia zako na milango yako ya fahamu ya ndani na nje. Kama huitakidi kuwa hizo chembe ni wafanyakazi wadogo wa Muweza wa kila kitu wa azali, viamuriwa, vitiishwa, na vyenye kufuata kanuni zake (sw), au ni askari waliowekwa katika jeshi lake lililoundwa katika nidhamu, au ni mahitimisho ya kalamu ya qadar ya kiungu, au ni nukta zinazoandikwa na kalamu ya kudura ya kiungu, itakulazimu kusema kuwa: Kwa kila chembe moja ina mfanyakazi katika jicho lako kwa mfano kuna jicho pana lionalo linaona sehemu zote za mwili wako na zinashuhudia viumbe vyote vinavyofungamana nalo, linajua muda wako wote uliopita, na muda wako wa baadaye, na linajua Asili yako, na baba zako, na babu zako pamoja na kizazi chako, na wajukuu wako, na linajua vyanzo vya chembe zako, na hazina za riziki zako, kwa hiyo jicho hilo lina akili sana! Ewe usiyeifanyisha kazi akili yako katika masuala kama haya! Je, haiwi kutegemeza ujuzi huu na hisia hizi na akili ambayo inatosheleza watu elfu moja kama mfano wa (Plato) kwa chembe, katika akili ya asiyeimiliki kama wewe, ni uzushi mbovu na uzuzu uliopitiliza? MUHALI WA PILI: Mwili wako ewe mwanadamu unafanana na kasri kubwa linalokaliwa, lina makuba elfu moja na moja, na katika kila kuba moja kati ya hayo kumetundikwa mawe, na yamepangwa kwa kushikana yenyewe kwa yenyewe katika jengo lililojengwa vema pasina nguzo, bali uwepo wako ungefikiri ni wa ajabu mno kuliko kasri hii mara elfu nyingi, kwa sababu kasri la mwili wako linarudia upya bila kukoma hufikia ukamilifu katika mpangilio na kupendeza mno. Tungaligeuza kuangalia kwetu katika yale uyabebayo ikiwemo roho, moyo na hali nyororo za kimaanawi, nayo yenyewe ni muujiza, na tukaangalia kwa jicho la mazingatio na kutafakari kiungo kimoja chochote kati ya viungo vya mwili wako tungeuona kuwa kinafanana na nyumba yenye makuba (Matungi). Basi chembe za Atom ambazo zilizomo zimesaidiana na kukumbatiana baadhi kwa baadhi nyingine kwa mpangilio timamu, na uwiano wa vipimo uliokamilika kama mawe katika makuba yale, na kuunda jengo la ajabu na ufundi wa kupendeza mno, zikadhihirisha kwa watazamaji muujiza wa ajabu katika miujiza ya uweza wa kiungu (kama jicho na ulimi) kwa mfano. Kama Atom hizo zisingekuwa zinaamrishwa, zenye kufuata amri ya mtengenezaji, muweza, basi kila Atom moja kati ya hizo, haina budi kuwa mtawala bila mpaka kwa Atom nyingine za mwili na yenye kutawaliwa na Atom nyingine vilevile, na kuwa mfano wa kila moja wapo kati ya hizo, na dhidi ya kila moja kati ya hizo, kwa upande wa kiutawala, wakati huohuo, na iwe marejeo ya ghalibu ya sifa tukufu ambazo hasifikani nazo ila Allah (sw) na ziwe zimefungika kiujumla na huru wakati huohuo. Basi kilichotengenezwa kimoja ambacho kimepangika vema, ambacho haiwezekani kuwa kwa siri ya upekee, isipokuwa athari katika athari za mmoja pekee, ni muhali kuegemeza katika Atom zisizokuwa na mipaka bali ni muhali kati ya muhali mia moja! Hilo analitambua kila aliyekuwa na chembe ya akili. MUHALI WA TATU: Ikiwa uwepo wako huu haukuandikwa na kalamu ya mmoja wa pekee, muweza, wa azali, na ikawa umechapwa kwa viwanda vya Asili na sababu mbalimbali, italazimu wakati huo kupatikana vyombo vya kiasili kwa idadi ya elfu ya maelfu katika vyombo vilivyojumuishwa, vilivyopangika vizuri vyenye kufanya kazi katika mwili wako, na ambavyo havidhibitiki kwa idadi, kuanzia chembe ndogo kabisa za mwili wako zenye kufanya kazi kwa umadhubuti wa hali ya juu hadi kuishia vyombo vikubwa zaidi, vyenye kufanya kazi mwilini mwako. Na kufahamu muhali huu tunakichukua kitabu tulichonacho mbele yetu kuwa ni mfano: Kama utaitakidi kuwa kitabu hiki kimeandikwa kwa mkono, basi inatosha kalamu moja tu kukiandika, elimu ya mwandishi wake inaitikisa kalamu hiyo ili iandike anachotaka, lakini kama haikuitakidiwa kuwa kimeandikwa kwa mkono wala kuegemezwa kwa kalamu ya mwandishi, na ikadhaniwa kuwa kimejiunda chenyewe au uandishi wake ukaegemezwa kwenda kwa Asili, wakati huo italazimu kuwa kila herufi moja katika herufi zake iwe na kalamu maalumu ya madini, na ziwe idadi ya kalamu sawa na idadi ya herufi, kwa mfano wa uwepo wa herufi za madini katika mashine ya chapa, na ambazo kwa idadi ya herufi na aina zake, yaani inalazimu kuwepo kwa kalamu kwa idadi ya herufi badala ya kalamu moja kwa ajili ya kuandika, na huenda ikawa katika herufi hizo, herufi nyingine kubwa zilizoandikwa ndani yake kwa mwandiko mwembamba yaliyomo katika ukurasa wote kamili, kwa hiyo italazimu kuandika mfano wa herufi hizi kubwa maelfu ya kalamu nyembamba. Sasa unasemaje kama ingekuwa hizo herufi zimeingiliana baadhi kwenye baadhi ya herufi nyengine kwa mpangilio kamili, na kuchukua umbo la mwili wako? Wakati huo italazimu kuwa kila sehemu miongoni mwa sehemu za kila duara miongoni mwa maduara yaliyotajwa iwe na vyombo vingine kwa idadi ya mjumuisho huo ambao haudhibitiwi na hesabu! Pengine unasema katika hali hii ambayo yenye muhali mia moja, kwamba hali hiyo inawezekana kutokea! Basi hata katika hali hii, tuseme kuwa inawezekana, je, haitalazimu kutengeneza kalamu hizo na kufanya vyombo hivyo na herufi za madini kuwepo kwa kalamu, na vyombo, na herufi kwa idadi yake, ili zimwage na kumimina ndani yake ikiwa ufundi wake haukurejeshwa wote kuelekea kalamu moja? Hiyo ni kwa sababu vyote hivyo vimetengenezwa na kuzushwa katika hali ya kupangiliwa, na vinahitajia fundi wa kuvitengeneza, na mzushaji wa kuvizusha, na hivi hivi jambo hili linafanya mnyororo unaoungana kila unavyoendelea ndani zaidi. Basi fahamu kutokana na hili kiasi gani cha ubatili wa fikra hii ambayo ndani yake kuna muhali na uzushi kwa idadi ya chembe chembe za mwili wako! Basi ewe mpingaji! Rudi kwenye akili yako na utupe upotevu huu mbaya!
Nalo ni kauli yao kuhusu kitu: “Asili imekilazi- misha” hukumu hii ina muhali nyingi sana tunataja muhali tatu miongoni mwa hizo kwa mfano: MUHALI WA KWANZA: Ni ufundi na uumbaji mambo mawili yenye kusifika kwa busara na hekima katika viumbe kwa dhahiri mno, hususani katika vilivyo hai, kama hayakurejeshwa mawili hayo kwa kuelekea kalamu ya “Qadar ya kiungu” na kuelekea uweza wake usio na mipaka, na ikarejeshwa kwa “Asili” pofu, kiziwi, jinga, na kuelekea kwenye (nguvu), Asili italazimu iumbe kwa ajili ya kuumba viwanda na mashine za kimaanawi zisizo na mpaka katika kila kitu, au iingize katika kila kitu uwezo uwezao kuumba ulimwengu wote, na hekima inayoendesha ili kutawala mambo yake yote. Mfano wa hilo: Hakika ya madhihirisho ya jua na akisi za mwanga na umeta wa miale inayoonekana juu ya matone ya maji mepesi yenye kumetameta, au juu ya vipande vya vioo vilivyotawanyika hapa na kule juu ya sura au uso wa ardhi, ambayo mtazamaji wa mtazamo wa juu juu humfanya adhanie kuwa hizo ni picha za majua mengi ya mfano. Kama akisi hizi na miale hii haikunasibishwa kwa jua la kweli ambalo linatuonesha mionzi yake yenye kumulika, italazimu kuitakidi jua la kiasili la kimaumbile dogo la nje kuwa lina sifa za jua lenyewe, na kusifikana kwa sifa zake zote maalumu zikiwemo kikweli kweli ndani ya hicho kipande cha chupa kidogo ambacho hakitoshelezi kwa kitu kidogo zaidi, yaani inalazimu kuitakidi kuwepo kwa majua mengi kwa idadi ya punje za vipande vya chupa. Katika mwanga wa mfano huu tunasema: Kama uumbaji wa viumbe na walio hai haukurejeshwa moja kwa moja kwenda kwenye madhihirisho ya majina ya Allah (sw) mazuri, ambayo ni nuru ya mbingu na ardhi, hapo itabidi kuitakidi kuwepo kwa Asili, na nguvu zinazomiliki uweza usiyo na mipaka, na ujuzi wa kila kitu, na utashi usio na mipaka, na hekima kuu isio na mipaka katika kila chenye uwepo katika vilivyo kuwepo, na hasa hasa vilivyo na uhai, yaani italazimu kukubali uungu na utawala katika kila kilicho na uwepo. Mtindo huu wa kufikiri uliokwenda upogo ni batili mno kuliko muhali mwingine wowote, na ni uzushi zaidi kuliko wowote, ambaye anarejesha alichobuni vema Muumbaji Mtukufu katika ufundi wa kustaajabisha kwa uzuri wake madhubuti, ni tukio la wazi hata katika kiumbe mdogo zaidi kwenda katika mkono wa Asili inayodhaniwa, ambayo ni duni haimiliki hisia, hapana shaka huyo anaporomoka na fikra yake hadi katika ngazi ya chini ya upotevu zaidi kuliko ya mnyama. MUHALI WA PILI: Kwamba viumbe hivi ambavyo viko katika upeo wa mpangilio, na ukomo wa kupendeza, na vipimo sawasawa, na ustadi timamu kabisa, na ukamilifu wa hekima na kulingana sawa, kama haukurejeshwa (uumbaji) kwa yule ambaye ni Muweza kwa uweza usio na mipaka, na Mwingi wa hekima ambayo haina mipaka, na kurejeshwa kwenda kwenye Asili, hapo Asili italazimu ilete katika kila gao la mchanga, maabara na mashine za kuchapa kwa idadi ya maabara za Ulaya na mashine zake za kuchapa, ili hilo gao kuweza kuwa ni mahali pa kuanzishia maua matunda mazuri nyororo, kwa sababu gao hilo la mchanga ambalo linatimiza jukumu la jumla dogo la maua linaonesha ukubalifu wa hakika wa kuotesha na kusawiri yanayoingizwa kwa zamu kutokana na mbegu za kila aina ya maua ya ulimwengu na matunda yake, na kwa aina zake zote, maumbo yake, na rangi zake. Kama ukubalifu huu haukurejeshwa kwenda kwa uweza wa Muumba Mtukufu awezaye kila jambo, kwa hiyo hapana budi kuwepo katika gao lile la mchanga mashine ya kimaanawi ya kiasili maalumu kwa kila ua miongoni mwa maua ya ulimwengu, na kama siyo hivyo haiwezekani kutokea tunachokiona katika sampuli za maua na matunda katika uwepo! Kwani mbegu kama manii na mayai pia, maada zake zinafanana zimechanganyika na kusongwa pamoja pasi na umbo maalumu, na ndio mahali pa kuzaliwa maji, asidi na maada ya Ukaa na Azwet. Hali ya kujulikana kuwa vyote ikiwemo hewa maji, joto, na mwanga, ni vitu rahisi havimiliki akili wala hisia, navyo vinabubujika kama mfereji katika kila kitu pasina kidhibiti chochote, kuunda maua hayo yasiyo na mipaka kutoka katika gao hilo la mchanga kwa sura zake mbalimbali za ajabu, na maumbo yake tofauti ya kupendeza mno hali yakiwa katika ukomo wa mpangilio, na ustadi kwa dhahiri inalazimu na kwa dharura kuwepo ndani ya gao lile la mchanga viwanda na mashine za kimaanawi kwa vipimo vidogo sana zaidi kuliko vilivyomo Ulaya, ili viweze kufumwa hivyo vifumwa hai ambavyo havihesabiki na kudarizi nakshi hizo zenye kung’ara anuwai zisizohesabika. Ee umbali ulioje wa fikra ya wana Asili ya kipingaji na kuacha njia ya akili salama! Elewa hili, na upime kiasi cha umbali wa wale ambao wanadai kuwa wao ni wenye akili na wanasayansi, kuwa mbali na vipimo vya akili na elimu kwa kudhania kwao kuwa Asili ni yenye kuvileta vitu katika uwepo, wale ambao wamejifanyia uzushi ukataao na usiowezekana kabisa kuwa ndio njia yao ikawadhalilisha na kuwadunisha. Mtu anaweza kuuliza: Sahihi kuwa muhali ni mwingi na ugumu mkubwa hutokea pale uumbaji wa viumbe utakapo egemezwa kwa Asili, lakini matatizo haya yataondoka vipi na ugumu huo utatatuka vipi, kama tutaegemeza kazi ya kuumba yote kwa aliye mmoja pekee mwenye kutegemewa kwa haja zote? kushindikana huko kugumu kunageukaje kuwa kupasa kwepesi? Jawabu: Udhihirisho wa jua na akisi zake kama ilivyotajwa katika muhali wa awali imejionesha nafsi yake kwa wepesi wote, na bila takilifu, au ugumu katika maada zote kuanzia visivyohisi vidogo vilivyo pindukia kwa udogo kama vipande vya chupa hadi kwenye sura pana zaidi za bahari, ikadhihirisha kwa wote umwagaji wake na athari yake katika upeo wa wepesi, kana kwamba vyote hivyo ni majua ya kimfano, kama litakatwa egemeo la uakisi huo kwenda kwa jua la hakika, hapana budi kuitakidi kuwepo kwa jua la Asili katika kila chembe ndogo uwepo wa kidhati yake wa nje, na hili ni jambo ambalo akili hailikubali bali hilo ni jambo linaloshindikana na ni muhali. Kama ilivyo jambo katika mfano huu ulivyo hivi, kadhalika kuegemeza kila kilichopo uegemezaji wa moja kwa moja kwa mmoja, mpweke wa pekee, mtegemewa kwa haja zote kuna wepesi wa upeo wa mwisho kwa kiwango cha kuwa wajibu, kwani yawezekana kuunga kinacholazimu kila chenye uwepo kwake, kwa wepesi wote, na hii ni kwa kunasibika na kudhihirisha. Wakati ambapo kunasibishwa huko kukikatwa, na kugeuka kutumika na kupewa jukumu na utiifu na kuwa kuponyoka katika amri na uasi na kukiacha kila kilichopo huru kinaenda namna kitakavyo, au jambo likaegemezwa kwa Asili, itatokeza mamia ya maelfu ya matatizo na ugumu kwa kiwango cha kushindikana, hadi tunaona kwamba kuumba nzi mdogo inahitaji kuwepo kwa Asili pofu iliyopo ndani yake yenye kumiliki uweza bila kikomo ambayo kwayo itaweza kuumba ulimwengu wote, na iwe pamoja na hayo, na hekima ya upeo itawezekana kwayo kuitawala, kiasi kwamba nzi pamoja na udogo wake ameundwa kwa ajabu, anabeba ghalibu ya maumbo ya viumbe kana kwamba ni faharisi ya muhtasari wake. Na hili sio muhali mmoja tu bali ni muhali elfu moja na mmoja. Kwa ufupi: Kama ilivyo muhali na lenye kushindikana kuwepo mwenza au mshirika wa Allah (sw) katika uungu wake, kadhalika ni jambo linaloshindikana, na muhali mfano wake kuwepo na uingiliaji kutoka kwa mwengine asiye kuwa yeye katika rububiyya yake, au kushirikiana kutokana na yeyote katika kuvileta vitu kwenye uwepo au kuviumba. Ama matatizo ambayo yamo katika (muhali wa pili) ambayo tuliyoyathibitisha katika risala nyingi nayo ni: Kama uumbaji wa vitu vyote utaegemezwa kwa mmoja wa pekee, uumbaji huo unakuwa mwepesi kama unavyokuwa mwepesi uumbaji wa kitu kimoja. Wakati ambapo kama uumbaji utaegemezwa kwenda kwenye sababu, na Asili ya uumbaji wa kitu kimoja unakuwa ni tatizo gumu, kama kuumba vitu vyote. Na kwa kuwa tumekwisha tangulia kuthibitisha jambo hili kwa hoja zenye nguvu, hapa tutaleta muhtasari wa hoja moja tu: Mmoja kama atajinasibisha kwa mfalme kwa kazi ya kiaskari au kiserikali, huweza kutekeleza mambo maradufu ya maradufu ya yale awezayo kuyatimiza kwa uwezo wake binafsi, na hii kwa sababu ya nguvu ya kule kujinasibisha kwa ufalme. Kwa mfano anaweza kumteka kiongozi mkubwa kwa jina la mfalme wake, pamoja na kuwa yeye ni askari. Kwa kuwa hazina za mfalme na idara za jeshi hubeba zana azitumiazo kutekeleza matendo mbalimbali, wala habebi peke yake, kama ilivyo kuwa yeye halazimiki kuzibeba. Yote hayo ni kwa fadhila ya kule kujinasibisha kwake kwa mfalme, kwa ajili hii hujitokeza kwake kazi zinazofurutu ada kana kwamba ni kazi za mfalme mkuu, na hudhihiri kwake athari juu ya yanayodhihiri kwake kwa kawaida kana kwamba ni kazi za jeshi kubwa, pamoja na kuwa yeye ni mtu mmoja. Mdudu chungu kwa upande wa jukumu hilo anaweza kuteketeza Kasri la Firauni muovu, na mbu anaweza kumuangamiza Namrudh jeuri kwa nguvu ya huko kujinasibisha na mbegu ndogo ya msonobari zinazofanana na punje ya ngano kwa kujinasibisha huko huanzisha zana zote za mti wa msonobari mkubwa. Kama kujinasibisha huko kutakatika, na kusamehewa kilichopo katika jukumu hilo, basi juu yake kubeba begani pake nguvu ambayo hutimiza kazi na kumtopea mzigo wake kwa zana na vifaa vyake. Na kwa hiyo hawezi kutimiza kazi isipokuwa zile zinazowiana na nguvu hiyo ndogo sana zilizomo kwenye mkono wake, kwa namna inayoendana na vifaa na zana kidogo anazozibeba mgongoni mwake, kama atatakiwa kutenda matendo aliyokuwa akiyatenda kwa wepesi katika hali ya mwanzo ataonesha kushindwa kwake, isipokuwa kama ataweza kubebesha mkono wake nguvu ya jeshi kamili, na kuweka mgongoni kwake mashine za zana za kivita za dola. Mwenye mawazo haya yanayoogelea kwenye anga la dhana na uzushi hurudi nyuma kwa kuhofia ayasemayo. Muhtasari wa yote yaliyotangulia: Kusalimisha jambo la kila kilichopo na kukinasibisha kwa aliyewajibu kuwepo (sw), ndani yake upo urahisi kamili kwa kiwango cha kuwa wajibu. Ama kuegemeza uumbaji wake kwa Asili ni jambo gumu kwa kiwango cha kushindikana na ni nje ya duara la akili. MUHALI WA TATU: Muhali huu tunaufafanua kwa mifano miwili am-bayo tumeibainisha katika risala nyingine nayo: Mfano wa kwanza: Bedui mwenye fikra ya kawaida anaingia, hakuwa ana taswira yoyote ya kimji hapo kabla, mtu huyu anaingia kwenye kasri kubwa zuri la ajabu linalovutia kwa mapambo yake na kushangaza kwa namna ya juu iliyokwisha kufikiwa na ustaarabu katika njia za kifahari na starehe, na kumeremeta kwa mwangaza wake katika giza la uwanda mtupu wa kuogofya, anatembea polepole kuelekea na kuzunguka pande zake, unamshangaza ufundi wa ujenzi wake, na nakshi za kuta zake, na ustadi wake mzuri sana, na kwa taswira yake, na ubahau wake huipa kasri hilo uhai, na kuipa uwezo wa kujijenga lenyewe pamoja na vyumba vyake vyote, na uzuri wake na sura na nakshi zake zinazovutia mno, hakuna lolote isipokuwa ni kwa sababu ya kuwa yeye ni mwenye kushindwa kufikiria kuwepo kwa yoyote nje ya kasri hili, na katika uwanda huu awezaye kumnasibishia ujenzi wa kasri hili, kwa hiyo akaanza kutafuta mjenzi ndani ya kasri huenda atamkuta kati ya vitu vya kasri, hakuna kitu kilichotua jicho lake juu yake ila huenda humo na kutilia shaka kuwa kwake ni muweza kufanya kasri kama hii iwepo, ambayo inajaza nafsi na akili kwa kupendeza kwa uzuri wake, miguu yake inamuongoza katika pembe ya kasri humo ghafla anakuta daftari la kumbukumbu lilikuwa limeandikwa ndani yake ramani iliyopambanuliwa ya kazi ya ujenzi wa kasri, na ndani yake kumeandikwa vilevile faharisi ya vilivyomo vyote na kanuni za kuendesha mali zake, pamoja na kuwa daftari hilo ni kama vilivyomo, halihusiki na kujenga kasri na kulipamba, kwani halimiliki mkono wa kufanyia kazi, wala uoni wa kuonea, isipokuwa ameambatana nayo alipokuta kuwa kimeendana kwa vilivyomo pamoja na jumla ya vitu vya kasri, na kuendana sawa na mwenendo wa kazi ndani yake kwa kuwa hiyo ni anuani ya kanuni za Allah (sw) za kiutendaji, kwa hiyo akasema hali ya kuwa amelazimika: (Hakika daftari hili ndilo lililojenga kasri hili na kuliweka katika mpangilio na kulipamba, na ndilo lililofanya vitu hivi viwepo na kuviratibu kwa utaratibu huu na kuweka sawa namna hii). Kwa maneno haya amefichua kiasi gani kina cha ujinga wake na uzuzu wake. Na kwa mfano kama huu kabisa, anatembea katika kasri la ulimwengu mkubwa ambao una mpangilio makini zaidi na ustadi kamilifu zaidi, muundo mzuri mno, na urembo wa kuvutia zaidi, kuliko kasri lile finyu lililotajwa hapo nyuma katika mfano, kwa namna ambayo haikubali kupishia nao, kila upande katika pande zake hung’ara miujiza ya ajabu, na hekima ya hali ya juu anatembea mmoja katika wafuasi wa fikra za Asili, na wanaokanusha ukuu wa uungu katika kasri hili, akiweka mawazoni mwake, tangu kabla kupinga yaliyotawanywa mbele yake katika athari za ufundi wa Allah (sw) aliyetakasika na viumbe, aliye juu ya vyenye kuyumkinika, na anaanza kutafuta na kupekua kuhusu sababu iliyofanya vitu viwepo ndani ya vyenye yamkini, na viumbe! Akaona kanuni za kawaida za kimungu na fahari za ufundi wa Bwana Mola Mlezi, na ambazo anazipa kimakosa, na kosa kubwa jina la Asili ambayo yaweza kuwa inafanana na ukurasa katika daftari la kugeuza na kubadilisha kwa kanuni za mwenendo wa uweza wa kimungu, na kama mfano wa ubao wa kufuta na kuthibitisha Qadar ya kimungu, lakini anajitokeza na kusema: Muda wa kuwa vitu hivi vinahitajia kuwepo kwa sababu yenye kupatisha kufanya viwepo, na hakuna kitu chenye mafungamano makubwa navyo kuliko daftari hili, hivyo ninahitimisha kutokana na hivyo kuwa daftari hili, na vyote vilivyomo katika kanuni za kufuta, na kuthibitisha ndizo zilizopatisha vitu zilizoleta vitu katika uwepo; kwa kuwa haiwi vema kwangu kuitakidi na kuamini Fundi Mtukufu (sw). Pamoja na kuwa akili iliyotakasika na utashi mbaya wa nafsi inakataa moja kwa moja ndani ya mantiki yake kunasibisha mambo ya kiungu yasiyo na mipaka, na ambayo yanahitajia nguvu isiyo na mipaka kwa daftari hili pofu kiziwi dhaifu. Nasi tunasema: Ewe mpumbavu kuliko habannaqah, chomoza kwa kichwa chako kutoka chini ya dimbwi la Asili, upate kuona kazi za kifundi za mtukufu ambaye vilivyomo vyote vinamshuhudia, kuanzia chembe ndogo kama mdudu chungu hadi sayari, kwa ndimi anuwai, na kuashiriwa na ishara mbalimbali, shuhudia madhihirisho ya mtia sura huyo mtukufu ambaye amesimamisha kasri la ulimwengu la kifahari, na akaandika ramani yake mpango wake, na kanuni zake katika daftari hilo, na uiokoe nafsi yako kutokana na weweseko hilo la dhambi rahisi. Mfano wa pili: Mtu aliye mbali na ulimwengu wa kimji na ustaarabu, anaingia katikati ya kambi ya kutisha, yanamshangaza anayoyashuhudia, ikiwemo mazoezi mbalimbali yanayofanywa kwa nidhamu ya hali ya juu, uhodari, utiifu na ufuasi, na wanajeshi wa kambi hii, anatazama harakati zao zilizopangiliwa kana kwamba ni mchakato mmoja unaofanywa na wote, kundi, kikosi, na kombania kwa mchakato wa mmoja kati yao, na wanatulia wote kwa kutulia kwake, na wote wanafyatua risasi mfyatuo mmoja baada ya amri anayoamrisha mtu huyo, akashangaa katika jambo lake, na akili yake duni haikuwa yenye kutambua kuwa uongozi wa kiongozi mkuu ndiye ambaye amri zake zinatekelezwa kwa mifumo ya dola na amri ya sultani, akadhani kuwa kamba hufungwa askari wale wao kwa wao kisha akaanza kufikiri kwa kimawazo tu, ni ajabu kiasi gani ya kamba hii ya kufikirika mshangao wake ukaongezeka, na kubabaika kwake kukazidi kiwango kisha akaendelea na hali yake. Na anaingia msikiti mkubwa wa (Aya sofia) siku ya Ijumaa, na kushuhudia mikusanyiko ya wenye kuswali nyuma ya mtu mmoja wanatekeleza kwa wito wake katika kusimama kwao, na kukaa kwao kusujudu, na kurukuu kwao, na kwa kuwa hakuwa anajua kitu kuhusu sharia ya kimungu, na kanuni za kimaanawi za amri za mwenye sharia, hivyo anapata taswira, kwamba kundi hili limefungamana kwa pamoja sehemu zake kwa kamba za kimaada halisi na kwamba kamba hizi zimefunga mitikisiko ya kundi na kuwashikilia, na ndizo zinazowatikisa na kuwasimamisha wasitikisike. Na kama hivyo anaendelea na nyendo yake hali ya kuwa akili yake imejawa na makosa ya taswira zake, ambayo inakaribia kucheza shere na dharau hata mbele za watu wasio na ustaarabu kabisa. Na katika mwanga wa mfano huo, mpingaji anakuja katika ulimwengu huu ambao ni kambi ya kutisha ya kupendeza kwa askari wa mfalme mtukufu, nao ni msikiti mkuu humo anaadhimishwa yule Muabudiwa wa azali na kutukuzwa, anaujia na hali akibeba fikra ya Asili yenye ukinzani, huo ujinga uliopandana. Basi anajenga taswira ya kanuni za kimaanawi ambazo zinashuhudiwa athari zake katika kufungamanisha mifumo ya ulimwengu wa kupendeza ajabu, na zinazotokana na hekima ya hali ya juu ya Muumba mtia sura (sw), anazipa picha kana kwamba ni kanuni za kimaada, hivyo anazichukulia katika tafiti zake kama anavyofanya na maada, na vitu visivyo na uhai. Na anadhani mawazoni mwake kuwa hukumu za kanuni za rububiyya ambazo ni kanuni za kimazingatio, na taratibu za sharia za kimaumbile za kiulimwengu za Muabudiwa wa azali, na ambazo kwa ujumla wake ni za kimaanawi kabisa, hazina uwepo ila ni uwepo wa kiujuzi, anazidhania kana kwamba ni vilivyomo halisi na ni vitu vya kimaada. Na kuziweka kanuni hizo zinazotokana na elimu ya kiungu na maneno ya kiungu ambayo yana uwepo wa kielimu tu, pahala pa uweza wa kiungu, kuzimilikisha uumbaji na kuleta vitu katika uwepo, na kuzipa jina la (Asili) hali ya kuijengea taswira nguvu ambayo ni udhihirisho miongoni mwa dhihirisho za uweza wa kiungu kwamba zenyewe ndio mmiliki wa uweza wa kutenda na Muweza Mwenye kujitegemea kwa uweza wenyewe: Je, baada ya huu, kuna ujinga na Ujuha mwingine tena! Je, kuna ujinga baada ya huu maradufu na maradufu ya uliomo katika mfano huu: Ufupisho: Hakika Asili ambayo wanaambatana nayo wana Asili, jambo hilo la kufikirika ambalo halina hakika yoyote, likiwa na hapana budi kuwa lina uwepo halisi, basi (uwepo) huo kwa hakika sio vinginevyo bali ni ufundi uliofanywa na fundi na hauwezi kuwa ndio fundi mwenyewe, nao ni nakshi na hauwi mchora nakshi, na mkusanyiko wa hukumu na hauwi muweka hukumu, na sharia ya kimaumbile, na hauwi ndiye muweka sharia, na pazia ya kiumbe wa mwenye ushindi asiyeshindwa Allah (sw), na siyo muumba, maumbile yenye kuathiriwa na utendaji na hauwi muumba mtendaji, na mkusanyiko wa kanuni na haziwi muweza na msitari na hauwi chanzo. Hitimisho: Muda wa kuwa vitu vipo kwa hakika na akili inashindwa kupata taswira zaidi ya njia nne ili kufikia kutokea kilichopo (kiumbe), kama tulivyoeleza hilo katika utangulizi na imethibiti kwa kukata shauri ubatili wa tatu kati ya njia hizo nne, na hiyo kwa kubainisha muhali tatu dhahiri waziwazi katika kila mmoja, hapana budi na kwa dharura kuthibiti kwa yakini hakuna njia kabisa ya kushuku njia ya nne, nayo ni njia ya upweke njia ambayo Aya tukufu inaiangazia: اَفِى اللّٰهِ شَكٌّ فَاطِرِ السَّمٰوَاتِ وَال۟اَر۟ضِ Na ambayo inajulisha wazi na kwa yakini juu ya kuwepo kwa mwenye wajibu wa kuwepo, na uungu wake unaotawala kila kitu na kutokea kila kitu kutokana na mkono wa uweza wake, na kwamba hatamu za mbingu na ardhi ziko mkononi mwake (sw), basi ewe muabudia sababu! Ewe maskini uliyefitinishwa na Asili! Muda wa kuwa Asili ya kila kitu ni kiumbe kama kitu chenyewe, kwa sababu kufanyika kwake ni jambo lililozuka sio la tangu, na juu yake kuna alama ya kutengenezwa na ustadi, na kwamba sababu ya kuwepo kwa hicho kitu cha dhahiri nayo pia ni yenye kutengenezwa yenye kuzuka. Na kwa kuwa uwepo wa kitu chochote unahitajia nyenzo na zana na vifaa vingi sana, kwa hiyo, hapana budi kuwepo kwa muweza asiye na mipaka ili aumbe hiyo Asili ndani ya kitu, na kupatishia hiyo sababu na hapana budi huyo muweza mwenye uweza usio na mipaka awe mwenye kujitosheleza kabisa, hashirikishi wakaa kati wasioweza katika kukifanya kitu kiwepo na katika kutawalisha kwake uungu wake juu yake. Basi Allah (sw) aepushe mbali, kuwa mwengine ndiye muweza anayejitosheleza mwenye sifa za juu, bali yeye (sw), huumba chenye kusababishwa pamoja na sababu, uumbaji wa moja kwa moja na hufanya kupatikane kati yake usababu wa nje na kisura, na kukutanisha kati ya viwili hivyo kupitia uratibu na mpangilio, hali ya kujaalia kutokana na sababu na Asili, pazia ya mkono wa uweza wake mtukufu, na kizuizi cha kuonekana ukuu wake, na kibriyai chake, na ili ubaki ushindi wake usiyoshindwa ukiwa takatifu katika cheo chake cha juu, na kujaalia hizo sababu ni mahali pa kulalamikiwa kwa yanayoonekana kwa nje katika upungufu, na kwa picha ya dhulma inayopatikana kwa nje ya vitu. Kipi kati ya viwili ni chepesi kukifahamu, na karibu mno kiakili katika ubongo kufikiria uwepo wa fundi saa, anatengeneza meno ya saa, na zana zake kisha anapanga kulingana na mpangilio wa meno yake, na kupima kati ya mitikisiko ya akrabu (mishale) zake kwa umakini wa ukomo (hali ya juu) wa juu, au kufikiria kuwa fundi saa anatengeneza katika meno ya saa na akrabu zake na zana zake makini, mashine ya matendo ya ajabu inasalimisha ufundi wa saa kwa ufu wa mikono yake? Sema pamoja nami: Je, haya si maneno matupu yasiyokuwa na maana, muhali na nje ya mipaka ya uwezekano? Basi haya ongea na akili yako iliyovuliwa maana, na uwe ni hakimu na mwamuzi. Na lipi kati ya mawili linapendeza na kukubalika katika mantiki ya akili? Fikiria kuwa kuna mwandishi anaandika kitabu mwenyewe baada ya kuandaa zana za kuandikia, ikiwemo wino, kalamu na karatasi, au fikiria mwandishi kufanya kiwanda maalumu cha kuchapa kinakuwepo na kupatikana kwa ajili ya kitabu hicho, nacho ni changamani zaidi, na nyeti zaidi kuliko kitabu chenyewe anaiachia jambo la uandishi wa kitabu hiki na kuongea nayo kwa kusema: Haya anza kuandika kitabu bila ya yeye kuingilia kwa namna yoyote? Je, mfano kama huu wa mawazo yenye ugonjwa si tatizo kwa akili? Na ni mushkeli kwa maradufu ya kuandika kwenyewe? Ukisema: Hakika kufanya uwepo wa kiwanda cha kuchapa kitabu ni changamani zaidi na ngumu mno kuliko kitabu chenyewe, isipokuwa mashine ya kuchapa ina uwezo wa kutoa maelfu ya nakala katika muda mfupi na hii ni njia ya kurahisisha. Jibu: Hakika Muumba mtia sura (sw), ameumba kwa uweza wake usiyo na mipaka, kwa kufanya upya dhihirisho za majina yake mazuri, na kuyaonesha kwa maumbo tofauti, miundo ya vitu na sura zake maalumu kwake kwa namna ambayo kiumbe mmoja hashabihiani na kiumbe mwingine kwa kushabihiana kikamilifu na kuambatana kamwe, na hicho ni kitabu cha mkusudiwa kwa haja zote, na andiko la kiungu. Naam, kwa ajili ya kila kiumbe atimize maana ya uwepo wake, hapana budi kuwa na alama atakazotambulika nazo na kuhitilafiana na wengine kwa alama hizo, na sura za kutofautiana na zile za wengine, basi tazama na tazama kwa makini katika uso wa mwanadamu, utaona kuwa alama zenye kutenganisha zimejikusanya katika uso huu mdogo, kwa namna ambayo alama hizi zinapambanua mwenye nazo na kumtofautisha na nyuso zote nyingine zenye kufuatana tangu zama za Adamu (as) hadi leo, na mpaka milele, licha ya kushabihiana na kuafikiana katika uhalisia wa ubinadamu na hali ya kuwa ya kibinadamu na jambo liko wazi mno na thabiti kabisa. Alama za kila uso ni kitabu maalumu cha uso wenyewe, nacho ni kitabu chenye kujitegemea hakitegemei kitabu kingine, kwa ajili ya kutoa kitabu hiki maalumu, na kutengenezwa vema na kupangiliwa vema, jambo hili linalazimu kuwepo kwa kundi la herufi za abjadia (abatathi) kamili, na zenye kuwiana nacho kwa ukubwa, na itahitajia kuratibu herufi hizi mahali pake katika ubao wa kuratibia ili ipatikane utunzi maalumu wa sura hii tofauti na utunzi wa wengine. Na jambo hili litalazimu kuleta maada za kutengenezea maalumu kwake, kisha kuziweka katika mahali pake maalumu kwa ajili yake, kisha kuingiza kila kinacholazimu uwepo wa uso huu ndani ya uso wenyewe katika nyenzo za ujenzi. Na haya yote hapana shaka yanahitaji kiwanda kinachojitegemea maalumu kwa ajili hiyo, yaani kiwanda maalumu kwa ajili ya vitu vyake vyote kwa kila uso kati ya nyuso. kisha je, mashine hii maalumu haihitaji tuseme kwa mfano upo mpangilio maalumu na uratibu mahsusi, hilo jambo la kuchapa lenyewe achilia mbali upangaji wa herufi na kuziratibu, na lenyewe pia linahitaji mpangilio? Maada zilizokuwepo katika kila mwili wa kiumbe hai ni changamani sana na nyeti mno kwa mpangilio kuliko maada za mashine ya kuchapa kwa mamia ya maradufu yake, kuleta maada hizo kutoka pande za ulimwengu kulingana na hesabu maalumu na vipimo madhubuti, kisha kuyapanga kulingana na mahitajio yalivyo, mwishowe kuyaweka chini ya mkono wa mashine hiyo ya kuchapa mlolongo huu mrefu wa taratibu za kupitia unahitajia kwanza na kabla ya kila kitu, mpatishaji wa kufanya mashine hiyo inayokadiriwa ipatikane (iwepo), nayo si nyingine ila uweza unaoumba wa Muumba Mwenye wingi wa Qudura na irada (kutaka) yake inayotimiza mambo bila kushindwa. Kwa hiyo kwa kuchukulia kuwa Asili kana kwamba ni mashine ya kuchapa, ni uzushi wa kufedhehesha hauna maana yoyote kabisa! Na kama hivi kwa mfano wa haya tuliyoshuhudia katika mfano wa (saa na kitabu): Hakika Fundi Mwenye utukufu na Yeye ni Muweza juu ya kila kitu, Yeye Mwenyewe ndiye Muumba wa sababu na Muumba wa vyenye kusababishwa, na ndiye ambaye anafungamanisha visababishwa, na sababu kwa hekima (sw). Hakika amepambanua kwa irada yake hali ya vitu, na amevifanya kuwa kioo chenye kuakisi dhihirisho za sharia kuu ya kimaumbile ambazo zimeumbiwa ulimwengu, na ambazo ni kanuni za Allah (sw), na kawaida zake zinazokwenda ambazo zinahusu upangiliaji wa mambo ya ulimwengu, hakika kwa uweza wake amepatisha (amefanya vipatikane katika uwepo wa ulimwengu) sura ya Asili ambayo ulimwengu wa kushuhudiwa wa uwepo halisi unasimamia kanuni hizo, kisha akaumba vitu na kuvianzisha katika hali ya Asili hiyo, na kuchanganya kati yake kwa hekima timamu kabisa. Na sasa tunalipeleka jambo hili katika insafu ya akili yako iliyoondoshwa sitara yake ipate kuona, ni kipi kati ya mawili hayo kinachopendeza akili yako na kuitakidi hilo inakuwa rahisi? Je, ukweli huu unaoingia akilini unaofuatia hoja zenye nguvu zisizo na mipaka ni wenye kulazimisha kwa kiwango cha kuwajibika, au kutoa yanayolazimu katika vitu ikiwemo vifaa na viungo visivyo na mpaka, na kuegemeza matendo yenye kusifika na hekima na busara kwa kitu chenyewe? Au kuinasibisha kwa kile mnachokiita kuwa ni (Asili), na sababu ambazo ni maada zisizo na uhai zisizo na hisia nazo ni zenye kuumbwa na kutengenezwa? Je, huu sio uzushi usiowezekana na uko nje ya eneo la kuwezekana? Mwabudu wa Asili anamjibu yule mpingaji kwa kusema: Maadamu unaniita katika kufanya insafu basi ninakiri: Kwamba njia tuliyoipita ya kupoteza hadi sasa kama ilivyo kuwa ni muhali kwa muhali mia moja basi ni yenye kudhuru madhara makubwa sana, na iko katika ukomo wa ubaya na ufisadi (kutofaa). Hakika mwenye kuwa na gao la akili kiasi kidogo atatambua kutokana na maamuzi yenu ya kiakili, na uhakiki wenu wa kielimu unaoegemea hoja, na uliotajwa hapo nyuma, kwamba kuegemeza uletaji wa vitu katika uwepo na uumbaji kwa sababu, na kwa Asili ni jambo lisilowezekana kiakili, na ni muhali kabisa, bali la wajibu na la lazima lenye kulazimisha akili ikubali, ni kuegemeza kila kitu moja kwa moja kwa aliye wajibu kuwepo (sw). Namshukuru Allah (sw) ambaye ameniongoza katika imani hii. Lakini imebakia kwangu jambo moja tu lenye kunichanganya nalo: Mimi nina muamini Allah (sw), ni Bwana Mola Mlezi, na kwamba yeye ni Muumba wa kila kitu, lakini ninajiuliza: Kinadhuru nini utukufu wake (sw) na ufalme wake (sw) tukielekeza baadhi ya sifa kwa baadhi ya sababu ndogo ndogo katika kufanya viwepo vitu vidogo duni, je, hilo linapunguza chochote katika ufalme wake (sw)? Jibu: Kama tulivyothibitisha katika baadhi ya risala zetu uthibitisho wa kukata shauri: Kwamba jambo la utawala (kukataa kuingilia) kwa hali zote, bali mtawala wa chini kabisa, au mwenye wadhifa yoyote wa kawaida hakubali kuingiliwa hata kutoka kwa mwanawe ndani ya mipaka ya utawala wake, bali kudhania kuingiliwa katika utawala kumewasukuma baadhi ya wafalme kuwauwa watoto wao wasiyokuwa na hatia, licha ya kuwa na kiasi fulani cha uchaji mungu na wema, katika mambo yanayoonesha kiasi gani cha kina cha msingi wa kanuni hii, kanuni ya kukataa kuingiliwa katika utawala, hii inafanya kazi katika kila kitu kuanzia kwa wahasimu wawili katika kuongoza utawala wa upande mmoja mdogo, hadi kufikia Wafalme wawili wanaogombana kwa ajili ya mamlaka ya pekee katika nchi, na kama hivyo imeshaonesha kwa hali isiyokubali shaka yanayolazimu kujitegemea kwa utawala kutokana na kanuni ya kuzuia kushirikiana, na imeweka wazi nguvu yake ndani ya historia ndefu ya mwanadamu, na yaliyopelekea katika misukosuko, mauaji, kufukuzana, na mito ya damu zilizomwagwa. Mchunguze mwanadamu ambaye anashindwa kuiendesha nafsi yake na anahitajia kusaidiana na wengine, na hamiliki kitu katika utawala na uwezo wa kuamuru isipokuwa kivuli fifi, naye anakataa kuingiliwa katika utawala kwa kiwango hiki, na anakataza kuingilia kwa wengine kwa kiasi hiki, na anakataa kushirikiana na wengine katika utawala wake, na kujitahidi kwa kutumia nguvu aliyonayo kushikilia upekee wa cheo chake, zingatia hili, kisha muangalie mtawala asiyekuwa na mipaka hali yakuwa ametawala katika kiti cha enzi cha ubwana mlezi, na amri isiyokuwa na mipaka na yeye ni mtawala mwendeshaji kwa hali ya kiungu, na mwenye kujitegemea bila mipaka kwa umoja na upekee, na yeye ni mkwasi bila mipaka kwa uweza usiyo na mipaka, huyo hasa ndiye Allah (sw) Bwana Mlezi wetu Mwenye utukufu. Je, ni kiasi gani inakuwa lazima na jambo la dharura kukataa kuingiliwa, huku kulingana na yeye na kuzuia kushirikiana, na kumfukuza mshirika katika utawala wake usio na mipaka, na kiasi gani ilivyo katika mambo ya lazima ya utawala huu na wajibu wake mkubwa sana? Sasa linganisha na upime kati ya utawala wa mwanadamu ulio finyu, wenye kuhitajia wengine, na utawala wa Allah (sw) usiyo na mipaka unaoenea kila kitu. Ama upande wa pili katika utata wako nao ni kwamba: Kama zitakusudiwa baadhi ya sababu kwa baadhi ya ibada, katika baadhi ya mambo madogo, je, hilo linapunguza jambo katika ibada za viumbe ambazo zinaelekea zote kwa Allah (sw) Muweza kuanzia katika chembe vumbi ndogo sana na kuishia katika sayari na nyota kubwa kubwa? Jibu: Hakika Muumba Mwingi wa hekima Mjuzi wa kila kitu (sw), ameumba ulimwengu huu kwa mfano wa mti, na akafanya wenye hisia ndio matunda yake kamili, na kumkirimu mwanadamu kwa kumzingatia kuwa ni tunda lenye wasifu wa jumla zaidi kwa wenye hisia, na kufanya shukrani na ibada ndio bora zaidi kinachozaliwa na uhai wamwanadamu, bali shukrani na ibada ni matokeo na upeo wa kuumbwa kwake, na tunda la uhai wake. Kisha je, inawezekana kwa akili kwa mtawala huyu asiye na mipaka na muamrishaji wa pekee na yeye ni mmoja wa pekee, asalimishe jambo la mwanadamu ambaye ndiye tunda la ulimwengu wote kwa asiye kuwa yeye miongoni mwa (sababu), na kusalimisha tunda la uhai wake, nalo ni shukrani na ibada kwa wengine, baada ya kuwa ameumba ulimwengu wote kwa kujulikana kwa uungu wake, na kwa mahaba ya ubwana mlezi wake, na je, inawezekana afanye matokeo ya uumbaji, na matunda ya ulimwengu yadondoke kinywani mwa uozo wa mchezo? Hasha! Kwa Allah (sw) apishe mbali na sivyo hivyo, ametakasika Allah (sw) na hayo wanayomshirikisha nayo. Kisha je, inayumkinika kwamba Allah (sw) ataridhia yale yanayohalifu hekima yake na uungu wake kwa kufanya baadhi ya sababu ziwe zenye kukusudiwa kwa ibada za viumbe? Hali ya kujua kwamba Yeye (sw) ameitangaza dhati yake, kuitambulisha na kuipendezesha kwa matendo yake, na huruma zake katika ulimwengu huu? Basi vipi ataridhia (sw) baada ya yote haya aache kujipendekeza kwa mbora wa viumbe wake, na mkamilifu zaidi kwa uja na shukrani kwa viumbe wengine? Na vipi ataruhusu viumbe wake wamsahau baada ya kuwa ameonesha kwa matendo yake makusudio yake makuu ulimwenguni? Nayo ni kumtambua, kisha kumwabudu? Hasha! Na si hivyo, basi ametakasika Allah (sw) na hayo wanayoyasema kwa utukufu mkubwa kabisa. Unasema nini ewe rafiki kwa haya uliyokwisha yasikia? Tahamaki anajibu na kusema: Alhamdulillah! Namshukuru Allah (sw), ambaye amenirahisishia kufumbua utata wa mambo haya mawili, hakika umenidhihirishia upekee wa Allah (sw), Muabudiwa wa haki anayestahiki kuabudiwa peke yake, dalili mbili zenye nguvu zilizo wazi ambazo haiwezekani kuzikana, na je, kuna mtu atakayekanusha mwanga wa jua isipokuwa mwenye kiburi na ukaidi?
Mtu wa Asili anasema na ameshaacha nyuma yake fikira zake na mawazo yake, na ameingia katika ngome ya imani kwa fikira mpya ya kiimani: Alhamdulillah! Nakiri kuwa utata wangu wote umekwishaondoka, lakini bado kwenye nafsi yangu kuna jambo linalonipa wasiwasi na kusababisha shaka zangu nyingi, kutokana na maswali yapitayo nafsini mwangu ambayo sijui majibu yake. Swali la kwanza: Tunasikia kwa wengi miongoni mwa wavivu, na wenye kujibweteka na kuacha kufanya ibada, na hasa wenye kuacha swala, kwamba wanasema: Mola mlezi (sw), mkwasi aliyesimama kwa dhati yake ana haja gani na ibada zetu hata anatukemea katika kitabu chake kitukufu, na kutukamia kwa adhabu kali katika moto wa jahannam, mtindo huu wa kivitisho mkali utaendana vipi na kosa hili dogo duni mathalan, na mtindo wa kimiujiza laini tulivu na laini uliomo katika sehemu nyingine? Jibu: Ni kweli hakika Allah (sw) aliye mkwasi kwa dhati yake, katu hana haja na ibada yako wewe ewe mwanadamu, bali yeye (sw), hana haja na kitu chochote katu, lakini wewe ndiye mhitaji wa ibada, kwani wewe kimaanawi ni mgonjwa, na ibada ndiyo ponyo lenye kutibu majeraha ya roho yako, na maumivu ya nafsi yako, na maneno haya tumeyathibitisha katika risala kadhaa. Kwa mfano ikiwa mgonjwa atamwambia daktari mwenye huruma anayemuhurumia na kumkazania atumiae dawa inayoponesha inayohusu ugonjwa wake, kama atamwambia kulingana na kumkazania kwake kwa kusema: Una haja gani na dawa hii hata unaniwekea mkazo namna hii kutumia dawa? Je, kutokana na maneno yake haya haifahamiki kiasi cha uduni, udhaifu na upumbavu wa akili yake? Ama onyo la Qur’an tukufu, katika yanayohusu kuacha ibada na matisho yake yakuogofya kwa adhabu kali, basi hii hapa tafsiri yake: Kama vile mfalme anavyo muadhibu mtu duni anayetenda kosa linalogusa haki za wengine kwa adhabu kali kwa ajili ya kuhifadhi haki za raia wake, kadhalika mfalme wa azali na milele anamuadhibu mwenye kuacha ibada na swala kwa adhabu kali, kwani anakiuka ukiukwaji unaovunja haki za vilivyomo na kuvidhulumu kimaanawi, dhuluma mbaya kabisa na kuziharibu haki zao kwa namna mbaya sana, hivyo viumbe ambavyo ndivyo raia zake na viumbe vyake, hiyo ni kwa sababu ukamilifu wake huonekana katika sura ya tasbihi na ibada katika uso wake, unaoelekea kwa Muumba Mwingi wa hekima (sw). Mwenye kuacha ibada haoni ibada za vilivyomo na hatoiona, bali anaikana, na katika hili kuna mapunjo makubwa ya thamani ya vilivyomo, ambavyo vyote kati ya hivyo ni andiko tukufu ya inayomhusu Mola mkusudiwa wa kila kitu, limeandikwa kwa aya za ibada na tasbihi ikiwa limeelekea kwa aya zake na tasbihi zake upande wa mwenye kufanya vitu viwepo Muumba Mtukufu aliyetukuka, na kila mojawapo kati ya hizo, vilevile ni kioo cha kuoneshea majina ya kiungu inayotoa mionzi ya nuru, anavishusha vitu hivi vilivyomo katika uwepo kwa kanus- ho hili kutoka katika hadhi yake ya juu, na haoni katika uwepo wake isipokuwa mchezo mtupu usio na maana yoyote, na kuiondoshea jukumu lake la kuumbwa kwake, na kuvidhania ni kitu kilichoanguka kilichopotea kisicho na umuhimu wowote, kwa hali hii anakuwa amedhalilisha vilivyokuwemo na kuvidharau, na kudhalilisha heshima yake, na kukanusha sifa zake kamilifu, na kudhuru ukweli wa uwepo wake. Naam, hakika kila mwanadamu huangalia ulimwengu kwa mtazamo wake maalumu, na kwa namna kioo chake kinavyompa taswira, amemuumba Muumba Mwenye kutia sura (sw), kwa sura ambayo anaweza kuupima ulimwengu kwayo, na kuupima kwa kipimo chake, amempa ulimwengu maalumu kwake kutokana na ulimwengu huu mkuu anaupamba ulimwengu wake maalumu kwa namna anavyoitakidi katika itikadi moyoni mwake. Mwanadamu mwenye huzuni, mkata tamaa, mlizi, ataona vitu vyote kuwa vinalia na hali mbaya, wakati ambapo mwenye furaha ataviona kuwa vyenye kutabasamu, kucheka, na kufurahi. Kadhalika ambaye anatimiza ibada na dhikiri kwa namna ya bidii na kwa hisia timamu na kwa kutafakari na kuzingatia, atagundua kitu katika ibada ya vilivyomo katika uwepo, na tasbihi zake, bali anaweza kuziona hali ya kuwa ni hakika iliyopo iliyothibiti, ama ambaye anaacha ibada kwa kughafilika au kwa kukanusha, hudhani vilivyomo kwenye uwepo, dhana ya makosa sana na yenye kupingana kabisa na hakika ya sifa zake kamilifu, na hapo anakuwa amedhuru haki zake kimaana. Zaidi ya hayo, mwenye kuacha swala pia huidhulumu nafsi yake kwa kuacha swala, kwani yeye hamiliki nafsi mwenyewe, hiyo nafsi ni mja mwenye kumilikiwa na mmiliki wake, Mola wake, Muumba wake, kwa ajili hii mola wake wa haki anamuonya maonyo makali, na kumhofisha kwa nguvu apate kuchukua haki ya mja wake huyo, kutoka katika nafsi yake yenye kuamrisha uovu, ukiachilia mbali kwamba alipoacha ibada ambayo ndiyo tija ya kuumbwa kwake, na lengo la kuumbwa kwake, anakuwa amekiuka mpaka wake upande wa hekima ya kiungu, na matakwa ya kiubwana mlezi, kwa sababu hiyo anaadhibiwa adhabu kali kwa jambo hilo. Hitimisho: Kwamba mwenye kuacha ibada kama ilivyokuwa anaidhulumu nafsi yake, na nafsi ni mali ya Al-Haq (sw) na mja wake, hivyo anachupa haki za makamilifu ya viumbe na pia kuzidhulumu, naam, kama ukafiri ulivyo ni udhalilishaji na dharau kwa viumbe, kuacha ibada ni kukanusha ukamilifu wa viumbe na kukiuka hekima ya kiungu, kwa hiyo anayeiacha anastahiki matisho na adhabu kali. Kwa sababu hii Qur’an tukufu inachagua mtindo wa kuogofya na kuonya ili kuelezea kustahiki huku, na kuhusu ukweli huu uliotajwa hapo nyuma, kwa hiyo mtindo huu unakuwa ni wa haki na unaambatana kikamilifu, na kwa mujibu wa hali ilivyo ambayo hasa ndiyo balagha (ufasaha). Swali la pili: Rafiki yetu ambaye ameiacha fikra ya Asili, na kujitenga nayo na kukaribia kumuamini Allah (sw). Hakika kufuata kwa kila kilichopo, katika kila jambo lake, na katika kila sehemu kati ya sehemu zake ndogo ndogo, na katika kila alitendalo na kulitimiza, ufuataji wa jumla kwa matakwa ya kiungu, na uweza wa kiungu, huu ni ukweli mkuu mtukufu kabisa, kwa utukufu wake na upana wake akili zetu zenye uchofu zenye upungufu haziwezi kuufahamu, hali ikijulikana kuwa tunaona waziwazi wingi wa viumbe teletele, na wepesi usio na mipaka katika uumbaji wa vitu, na imethibiti kuwa wepesi wa kuvifanya viwepo, ambao ni katika mambo ya lazima ya upweke kwa hoja madhubuti mlizozitoa, zaidi ya kuwa kwamba Qur’an tukufu imeelezea wepesi wa bila mipaka kwa uwazi katika aya tukufu nyingi tu mfano: مَا خَل۟قُكُم۟ وَلَا بَع۟ثُكُم۟ اِلَّا كَنَف۟سٍ وَاحِدَةٍ وَمَٓا اَم۟رُ السَّاعَةِ اِلَّا كَلَم۟حِ ال۟بَصَرِ اَو۟ هُوَ اَق۟رَبُ Zote hizi zinafanya ukweli huu mkuu wepesi wa kufanya vitu viwepo ni suala linalokubalika sana na kupokelewa kwa akili, wapi siri ya wepesi huu ilipo, na kuna hekima ipi nyuma yake? Jibu: Siri hiyo imekwisha fafanuliwa waziwazi katika andiko la ishirini, katika kufafanua kwake aya tukufu: وَهُوَ عَلٰى كُلِّ شَى۟ءٍ قَدٖيرٌ Kwa namna inayotosha kuonesha tu, na hasa katika nyongeza yake, ambapo ufafanuzi umekuja wa kutosheleza na kukidhi haja sana, na kukinaisha kwa dalili, hoja na uthibitisho wa kukata maamuzi, na muhtasari wake ni: Kwamba inapoegemezwa kufanya uwepo wa vilivyomo vyote kwa mtengenezaji mmoja huwa wepesi jambo hilo kama wepesi wa kufanya uwepo wa kiumbe mmoja, wakati ambapo kama itaegemezwa kwa wengi hua vigumu kwa wingi huu kufanya uwepo wa kiumbe mmoja kwa kadiri ya ugumu wa kufanya uwepo wa viumbe vyote, hapo inakuwa kuumba mbegu moja ni ngumu na tatizo kama kuumba mti, lakini kama kufanya vitu viwepo kutaegemezwa kwa mtengenezaji wake wa kweli (sw), jambo hili linakuwa lepesi, hadi inakuwa kufanya vitu vyote viwepo ni kama kuleta katika uwepo mti mmoja, na mti kama mbegu, na pepo kama majira ya machipuo, na majira ya machipuo ni kama ua, jambo linakuwa rahisi jepesi. Hapa tutaonesha kwa ufupi dalili moja au mbili kati ya mamia ya dalili ambazo tumezifafanua kwa upambanuzi katika risala nyingine, dalili hizo ambazo zinabainisha yanayozunguka miongoni mwa siri, na hekima zilizofichana katika tuyashuhudiayo ikiwemo wingi wa viumbe visivyojulikana idadi na urahisi wake, na wingi wa wahusika wa kila sampuli kati yao, na kupatikana katika uwepo kwa mpangilio, ufundi, na kwa wepesi wote. Mfano wa hili: Kuongoza askari mia moja chini ya uongozi wa kamanda mmoja, ni wepesi maradufu kwa mara mia moja, kuliko kuongoza askari mmoja chini ya uongozi wa makamanda mia moja. Na pale ambapo linawekwa jukumu la kuandaa jeshi kamili kwa mahitaji ya kiaskari, kutoka kituo kimoja, na kwa kanuni moja na kutoka kiwanda kimoja kwa amri anayoitoa kiongozi mmoja, hilo linakuwa jepesi kwa upande wa kiasi na wingi, sawa na wepesi wa kumuandaa askari mmoja. Wakati ambapo kuweka jukumu la kuandaa askari mmoja kwa mahitaji ya kiaskari yaliyokamili kutokea vituo vingi na viwanda vingi, kwa viongozi wengi ni tatizo na gumu kwa upande wa kiasi, na wingi vilevile kwa ugumu sawa na wa kuandaa jeshi kamili, kwani inatakiwa ikiwa hivyo kuwepo kwa viwanda vingi vya maandalizi ya mahitaji kwa idadi inayolazimu jeshi kamili kwa ajili ya kumuandaa askari mmoja. Na inashuhudiwa vilevile kwamba mti mmoja ambao hupata maada za lazima kwake kutokea kwenye shina moja, kutokea kwenye kituo kimoja, na kwa mujibu wa kanuni moja huzaa matunda mengi, na hilo hutendeka kwa urahisi kana kwamba mti huo una tunda moja. Wakati ambapo kama umoja utabadilishwa kwa wingi na kupitwa njia ya wingi badala ya njia ya umoja, na kupewa kila tunda maada za lazima kwa ajili ya uhai kutoka kwenye vituo tofauti tofauti na mashina mbalimbali, kufanya tunda moja liwepo inakuwa ni tatizo, na ni jambo gumu kama kuufanya mti wenyewe uwepo, bali yawezekana kufanya uwepo wa mbegu ambayo ni mfano mdogo wa mti na faharisi yake ni jambo gumu, na mgogoro kama kufanya uwepo wa mti wenyewe, kwa sababu yale yanayolazimu uhai wa mti katika maada za dharura yanalazimu pia mbegu hiyo. Kuna mamia ya mifano kama hii, na yote inabainisha kwamba kupatikana kwa maelfu ya viumbe kwa wepesi kabisa kwenye uwepo katika umoja ni rahisi zaidi kuliko kupatikana kwa kiumbe mmoja kwenye uwepo kwa wingi. Tulipokuwa tumethibitisha hakika hii katika risala nyingine kwa yakini ya kukata shauri kabisa tunaelekeza huko, lakini hapa tutabainisha siri kuu tu ambayo inahusiana na wepesi huu kwa upande wa mtazamo wa kiungu, Qadar ya kiungu na uweza wa kiungu Bwana Mola Mlezi, na siri hii ni: Wewe upo miongoni mwa vilivyo kuwapo, kama utasalimisha nafsi yako kwa mkono wa Muweza wa kila jambo asiye na mipaka katika uweza wake, hakika atakuumba kwa amri moja na kwa uweza wake wa kila kitu usio na kikomo kwa mpepeso wa jicho kutoka katika hali ya kutokuwepo, bila kuwa kitu, lakini kama hutasalimisha nafsi yako kwake, bali ukaiegemeza kwa Asili na kuisalimisha kwa sababu za kimaada, hapo italazimu kukufanya wewe uwepo, kazi ya utafiti makini sana ili kukusanya maada yote yaliyo katika uwepo wako katika maeneo ya ulimwengu mzima, na kuyasaka katika pembe za ulimwengu wote, na kuyapitisha katika visafishio na majaribio mengi madhubuti sana, na kuyapima kwa vipimo nyeti. Hii ni kwa sababu wewe ni muhtasari uliopangika vema wa ulimwengu, na tunda lake nono, na faharisi yake ndogo na mkoba wake uliokusanya maada za ulimwengu wote. Kwa kuwa sababu za kimaada hazina chochote isipokuwa kuunganisha na kukusanya, kwani ni jambo lililothibiti kwa watu wenye akili, kwamba haiwezekani kwa sababu za kimaada kufanya viwepo vitu visivyokuwepo humo, kutoka katika hali ya kukosekana na kutokana na hakuna, kwa ajili hii zinalazimika kukusanya maada za lazima za mwili wa kiumbe hai mdogo kutoka katika pande za ulimwengu wote. Kwa kuwa sababu za kimaada hazina lolote isipokuwa kuunganisha na kujumuisha, kwani ni thabiti kwa watu wenye akili kwamba haiyumkiniki kwa sababu za kimaada kupatisha kisichokuwamo ndani yake kutoka katika hali ya kutokuwepo na kutokana na hali ya kutokuwepo kitu chochote; kwa hiyo inalazimika kukusanya maada za muhimu kwa ajili ya mwili wa kiumbe hai mdogo kutoka katika sehemu zote za ulimwengu Basi kutokana na hili fahamu kiasi gani cha urahisi wa moja kwa moja katika umoja na upekee, na kiasi cha ugumu na matatizo katika shirki na upotevu. Pili: Kuna wepesi wa moja kwa moja katika ku-umba na kufanya uwepo wa vitu unaotokana na pembe ya kutazama (ujuzi wa kiungu) na upambanuzi wake kama ifuatavyo: Hakika Qadar ya kiungu ni aina katika ujuzi wa kiungu, huainisha kiwango cha kila kitu kana kwamba ni kitu cha kimaanawi chake, na kinaihusu kiasi hicho cha kiqadar, kinakuwa ni sawa na mpango wa kitu hicho, na kwa hukumu ya mtindo mfano mdogo wake, wakati inapoileta katika uwepo (uweza wa kiungu), hufanya kiwepo kwa kiasi hicho cha kiqadar kwa wepesi wote. Kama haukunasibishwa upatishaji wa kitu hicho kwa ambaye ana ujuzi wenye kuzungukia kila kitu bila mipaka ujuzi wa azali, naye ni Allah (sw) Muweza wa kila jambo Mwenye utukufu hakutokei maelfu ya matatizo tu, bali kutatokea mamia ya muhali vilevile, kama ilivyoelezwa huko awali kwa sababu kisipo kuwepo kiasi hicho cha kiqadar na kiasi cha kielimu, italazimu kutumia maelfu ya vitu vya kimaada na vya nje ya mwili kwa ajili ya mwili mdogo wa mnyama! Basi fahamu kutokana na hili siri katika siri za wepesi wa moja kwa moja, bila mipaka katika umoja na upekee, na wingi wa matatizo yasiokoma katika wingi na shirki. Na ujue kiasi cha ukweli mtukufu wenye kusibu, ambao aya tukufu ifuatayo inauelezea: وَمَٓا اَم۟رُ السَّاعَةِ اِلَّا كَلَم۟حِ ال۟بَصَرِ اَو۟ هُوَ اَق۟رَبُ Swali la tatu: Aliyekuwa anashambulia mwanzo na sasa amewafikishwa katika imani na kuongoka anasema: Baadhi ya wanafalsafa wana jambo gani wanachupa mipaka katika enzi zetu hizi, wanaelezea maneno ya: “Hakizushwi kitu kutokana na kutokuwepo, na wala hakitoweki kitu kutoka katika uwepo”, na kwamba kinachouendesha ulimwengu huu, si kingine bali ni muundo wa maada na uchangukaji wake na sio vinginevyo! Elcevap: Nur-u Kur’an ile mevcudata bakmayan feylesofların en ileri gidenleri bakmışlar ki tabiat ve esbab vasıtasıyla bu mevcudatın teşekkülat ve vücudlarını –sâbıkan ispat ettiğimiz tarzda– imtina derecesinde müşkülatlı gördüklerinden, iki kısma ayrıldılar. Kundi moja wamekuwa Wanasafsata na kuichukia akili ambayo ndiyo sifa maalumu ya mwanadamu, na kuangukia katika ngazi ya chini kabisa ya wanyama, kiasi cha kuwafikisha mawazo yao katika kukanusha uwepo kwa jumla, bali hata kukanusha uwepo wao wenyewe, na hii ni pale ambapo walipoona kukanusha huku kunafaa sana kwa akili, na kwepesi zaidi kwake na salama zaidi kuliko kufikiria Asili na sababu kuwa ndiye mwenye kumiliki hatamu ya kufanya vitu vyote viwepo, wakakanusha uwepo wao na uwepo wa vilivyomo vyote, wakaanguka katika lindi la ujinga mkubwa. Ama kundi la pili: Wameangalia vilivyomo kwamba kama kuvifanya viwepo kutasalimishwa kwa sababu, na Asili kama ilivyo hali ya watu wa upotevu, kufanya kiwepo kitu kidogo sana kama mbu na mbegu kuna matatizo yasiokuwa na mpaka, na kunahitajia uweza mkubwa sana ambao akili haifikii kiasi chake, wakajikuta wanalazimika kukanusha hata upatishaji, kuvifanya vitu viwepo, wenyewe wakasema: “Hakizushwi kitu kutoka katika hakuna”, na wameona kuwa kuondoa kitu katika uwepo ni muhali pia, wakatamka kuwa hakitoweki kilichopo. Wakajenga picha za mawazoni kutokana na hali za kufikiria kuwa zinakwenda kati ya kuchanguka, na kuundika, na kutawanya, na kukusanya, kunakotokana na michakatiko ya Atom na mfereji wa sadifu! Zingatia hawa ambao wanajidhani kuwa katika kilele cha akili wameanguka katika dimbwi la upumbavu na ujinga, elewa kutokana na hili, namna upotevu unavyomshusha mwanadamu huyu aliyetukuzwa, wakati anapopuuza imani yake, na kuwekwa mahali pa kudharauliwa na kukebehiwa na kila mmoja. Na sisi tunauliza: Je, ni vipi itawezekana kukanusha kupatishwa kitu fulani (kufanywa kiwepo) kutokana na uweza usio na mipaka, ambao unafanya kuwepo juu ya uso wa ardhi kila mwaka sampuli mia nne elfu za vilivyo hai? Na ambao umeumba mbingu na ardhi ndani ya siku sita? Na ambayo huanzisha katika kila majira ya machipuo chini ya uoni wa mwanadamu na usikivu wake, katika uso wa ardhi, kiumbe hai miongoni mwa mimea na wanyama ambao ni ustadi ulio wazi zaidi, na hekima iliyo bayana zaidi kuliko ulimwengu wote, katika wiki sita? Vipi ikanushwe kuweza kuumba viumbe kielimu ambavyo vimeainishwa mipango yake, na viwango vyake ndani ya duara la elimu ya kiungu ya azali unaviumba kwa wepesi kabisa, sawa na wepesi wa kuonesha maandishi yasiyoonekana kwa kupitisha maada ya kikemikali juu yake. Basi kukanusha kuweka uwepo wa nje katika vilivyo kuwepo kielimu, na ambavyo kwa nje havipo kutokana na Qudura hiyo ya kiungu ya azali, kisha kukanusha kupatisha (kufanya vitu viwepo), kwenyewe ni upumbavu na ujinga zaidi kuliko ujinga wa Wanasafsata wanaojulikana na ujinga wao. Na kwa kuwa nafsi za watu hawa walioharibikiwa, wenye kushika njia ya ufirauni dhaifu, udhaifu mkubwa kabisa, na ambao hawamiliki isipokuwa sehemu ndogo tu ya kufanya hiyari wasioweza kuondoa chochote katika uwepo, na kukifanya kisiwepo, na kufanya iwepo Atom yoyote, au maada kutokana na hali ya kutokuwepo, na ilivyokuwa Asili na sababu ambazo wanajifaharisha kwa kuziabudia, ni dhaifu nazo pia, na sio katika uwezo wake jambo la kupatisha (kufanya kitu kiwepo), pasipo na kutokana na kitu chochote, tunawaona wanatoa hukumu ya jumla: Kwamba maada haitoweshwi wala haizushwi, na wanajaribu kujumuisha hukumu ya msingi huu ya batili ya makosa hata juu ya uweza wa Muweza wa kila kitu, asiye na mipaka ya uweza (sw). Naam, hakika Muweza wa kila kitu ambaye hana mipaka ya uweza wake, Mwenye utukufu na ukarimu, ana aina mbili za kupatisha (kufanya uwepo wa kitu): Kwanza: Kwa kubuni na kufanya bidaa (yaani kuanzisha kitu pasipo na mfano wa kabla yake), yaani Allah (sw) anaanzisha uwepo kutoka katika hakuna kwa kuanzisha pasipo na chochote, na kupatisha kila kinacholazimu uwepo huu miongoni mwa vitu kadhaa kutokana na hakuna, na kuvipa hicho kilichoanzishwa. Nyengine: Kwa kuanzisha na kutengeneza na kufanya vizuri, yaani anaanzisha sehemu katika vilivyomo kutokana na nyenzo za ulimwengu wenyewe, ili kudhihirisha ukamilifu wa hikima yake, na kubainisha madhihirisho ya majina yake mazuri, na mifano yake katika hekima madhubuti, hutuma kwa vitu hivyo vilivyomo Atom, na maada zenye kutii amri zake kwa mujibu wa kawaida za Al-Razzaaqiyya (sifa ya utoaji riziki) za kiulimwengu, na kuvidhalilisha kwa ajili yake ili akamilishe uundaji wa uwepo huu, na kama hivi Muweza huyu asiye na mipaka ya uweza ana mitindo miwili ya kupatisha (kufanya uwepo wa vitu) na sura zake: Kufanya bidaa na kuunda. Kutowesha vilivyokuwepo, na kupatisha visivyokuwepo, ni jambo jepesi sana kwake na rahisi mno, bali hiyo ni kanuni yake ya jumla ya kudumu. Basi aonaye kuwa ni jambo lisilowezekana kutokana na uweza wenye kuumba, ambao unaumba kutokana na kutokuwepo mia tatu elfu sampuli mia tatu elfu ya viumbe na vilivyo hai, na kuvipa maumbo yake, na jinsi zake na hali zake kutokana na zisizokuwa Atom zake, na kusema: “Kwamba haiwezi kuleta kisichokuwepo, lazima apondokee katika giza la kukosekana”. Anasema ambaye ameitupa Asili na kuingia katika njia ya hakika: Alhamdu lillah, himidi zenye kukithiri kwa idadi ya Atom, ambaye ameniwafikisha mimi kufuzu ukamilifu wa imani, na kuniokoa kutokana na dhana na mawazo ya upotevu, zikaondoka kwa fadhila zake utata na shaka zote nilizokuwa nazo. اَل۟حَم۟دُ لِلّٰهِ عَلٰى دٖينِ ال۟اِس۟لَامِ وَ كَمَالِ ال۟اٖيمَانِ Alhamdulillah juu ya dini ya kiislamu, na ukamilifu wa imani. سُب۟حَانَكَ لَا عِل۟مَ لَنَٓا اِلَّا مَا عَلَّم۟تَنَٓا اِنَّكَ اَن۟تَ ال۟عَلٖيمُ ال۟حَكٖيمُ

