Source text is preserved. When a suitable model is available, translation is displayed separately.
Kurani Tukufu · 91
Ash-Shams Surah
15 Aya
Source: QuranEnc.com
Source · Swahili Translation - Rowad Translation Center
Issued by the Islamic Content Service Association in Languages
Synthetic device voice, not a Quran recitation
- 91:1
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ وَٱلشَّمْسِ وَضُحَىٰهَا
Ninaapa kwa jua na mwangaza wake!
- 91:2
وَٱلْقَمَرِ إِذَا تَلَىٰهَا
Na kwa mwezi unapolifuatia!
- 91:3
وَٱلنَّهَارِ إِذَا جَلَّىٰهَا
Na kwa mchana unapolidhihirisha!
- 91:4
وَٱلَّيْلِ إِذَا يَغْشَىٰهَا
Na kwa usiku unapolifunika!
- 91:5
وَٱلسَّمَآءِ وَمَا بَنَىٰهَا
Na kwa mbingu na kwa aliyeijenga!
- 91:6
وَٱلْأَرْضِ وَمَا طَحَىٰهَا
Na kwa ardhi na kwa aliyeitandaza!
- 91:7
وَنَفْسٍ وَمَا سَوَّىٰهَا
Na kwa nafsi na kwa aliyeitengeneza!
- 91:8
فَأَلْهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقْوَىٰهَا
Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake.
- 91:9
قَدْ أَفْلَحَ مَن زَكَّىٰهَا
Hakika amefanikiwa aliyeitakasa.
- 91:10
وَقَدْ خَابَ مَن دَسَّىٰهَا
Na hakika amehasiri aliyeiviza.
- 91:11
كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِطَغْوَىٰهَآ
Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotovu wao.
- 91:12
إِذِ ٱنۢبَعَثَ أَشْقَىٰهَا
Aliposimama mwovu wao mkubwa.
- 91:13
فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ ٱللَّهِ نَاقَةَ ٱللَّهِ وَسُقْيَـٰهَا
Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipowaambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake.
- 91:14
فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمْدَمَ عَلَيْهِمْ رَبُّهُم بِذَنۢبِهِمْ فَسَوَّىٰهَا
Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa.
- 91:15
وَلَا يَخَافُ عُقْبَـٰهَا
Wala Yeye haogopi matokeo yake.
Source: QuranEnc.com · swahili_rwwad · v1.0.5
Arabic source copyright · Tanzil Project
Tanzil Quran Text (Uthmani, Version 1.1) Copyright (C) 2007-2024 Tanzil Project License: Creative Commons Attribution 3.0 This copy of the Quran text is carefully produced, highly verified and continuously monitored by a group of specialists at Tanzil Project. TERMS OF USE: - Permission is granted to copy and distribute verbatim copies of this text, but CHANGING IT IS NOT ALLOWED. - This Quran text can be used in any website or application, provided that its source (Tanzil Project) is clearly indicated, and a link is made to tanzil.net to enable users to keep track of changes. - This copyright notice shall be included in all verbatim copies of the text, and shall be reproduced appropriately in all files derived from or containing substantial portion of this text. Please check updates at: http://tanzil.net/updates/

