Tanbihi: Sababu ya kuleta mifano kwa namna ya simulizi katika risala hizi ni kusogeza maana karibu ipate kufahamika kwa upande mmoja, na kudhihirisha kiasi gani zilivyo taarifa za Kiislamu katika kukubalika kwake akilini, na upeo wa kuwiana na kupangika kwake kwa upande mwingine, makusudio ya simulizi hizo ni zile natija zinazopatikana mwishoni mwake, na maana inayomaanisha kwa hali ya mafumbo, kwa hivyo basi hizo sio simulizi za kufikirika, bali ni taarifa za kweli. بِسْمِ اللّٰهِ الرَّحْمٰنِ الرَّحِيمِ فَانْظُرْ اِلٰٓى آثَارِ رَحْمَتِ اللّٰهِ كَيْفَ يُحْيِي الْاَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا اِنَّ ذٰلِكَ لَمُحْيِي الْمَوْتٰى وَهُوَ عَلٰى كُلِّ شَىْءٍ قَد۪يرٌ Ewe ndugu yangu! kama unataka ufafanuzi wa jambo la ufufuo na baadhi ya mambo ya akhera kwa sura inayoendana na ufahamu wa watu wa kawaida, basi sikiliza pamoja na mimi hikaya hii fupi. Watu wawili walisafiri pamoja kuelekea kwenye nchi ya kifalme, iliyopambwa kama bustani, - na mfano huu ni kwa dunia - tahamaki wanaona kwamba wakaazi wa nchi ile ya kifalme wameacha milango ya nyumba zao na maduka yao ikiwa wazi wala hawajali kuilinda, kwa maana hiyo mali na fedha zipo katika wasiwasi mkubwa kuchukuliwa pasina kuwepo mtu yeyote anayezilinda, mmoja kati ya wawili wale, kwa kile alichoshawishiwa na nafsi yake, akaanza kuiba na wakati mwingine anapokonya akiwa anatenda kila aina ya dhulma na upuuzi na wala wenyeji wasimjali sana. Rafiki yake akamwambia: “Ole wako, unafanya nini? Hakika utakuja kuadhibiwa, na utanitia mimi katika balaa na masaibu, kwani mali hizi ni mali za dola, na hawa wenyeji kwa familia zao na watoto wao wote wanakuwa kama askari wa dola au maafisa wa dola hii, na wanatumiwa katika nyadhifa hizi wakiwa kama raia wa kawaida, na kwa ajili hiyo ndio maana hawakukutilia maanani sana. Tambua kwamba utawala wa hapa ni mkali sana, maana wapelelezi wa mfalme na wachunguzi wake pamoja na wapeleka habari wake wapo kila mahali, fanya upesi rafiki yangu kuomba msamaha.” Lakini yule rafiki yake mpumbavu alikaidi huku akisema: “Ewe rafiki yangu niache, mali hizi sio za dola, bali ni mali yasiyo na mwenyewe, hayana mmiliki, kila mmoja anaweza kutumia apendavyo, hivyo sioni kinachonizuia kufaidika nayo, au kunufaika na vitu hivi vizuri vilivyo tawanyika mbele yangu, na uelewe kwamba mimi si sadiki jambo lisiloonekana na macho yangu.” Na akaanza kuleta hoja za kifalsafa na kuongea sana maneno ambayo ni sawa na safsatah na hapa ukaanza mjadala mkali baina yao. Maongezi yakazidi pale yule zuzu alipouliza: “Na huyo mfalme ndiye nani? mimi simjui”, rafiki yake akamjibu: “Hakika wewe unajua kuwa hakuna kijiji bila ya kiongozi na hakuna sindano isiyokuwa na mtengenezaji na anaye imiliki, na hakuna herufi bila ya kuwepo mwandishi. Basi vipi uone inafaa kwako kusema: Kuwa hakuna mtawala wa nchi hii ya kifalme yenye kupangika vyema na kupendeza mno? Na vipi yawe mali haya tunu na ya thamani bila ya mmiliki kwa wingi wake? Hadi inakuwa kana kwamba gari moshi lililoshehenezwa aina kwa aina ya riziki za thamani huja kutokea mahali kusiko onekana kila saa na kupakua hapa kisha linaondoka , hivi huoni pande za nchi hii ya kifalme, matangazo na ilani za mfalme, bendera zake zinazopepea kwenye kila mlingoti na muhuri wake maalumu na chapa ya nembo yake juu ya mali zote, basi iweje nchi ya kifalme kama hii bila ya mwenyewe? Inaonekana umejifunza kidogo lugha ya kizungu, lakini huwezi kusoma haya maandiko ya Kiislamu na wala hutaki kumuuliza anaye yasoma na kuyafahamu, kwa hiyo basi njoo nikusomee matangazo hayo, na amri hizo muhimu zaidi kutoka kwa mfalme.” Yule mkaidi akamkatisha kauli yake kwa kusema: “Tukubali kuwa mfalme yupo, lakini kipi kinaweza kumdhuru mfalme na kupunguza katika hazina yake ninachojichukulia kwa mahitaji ya nafsi yangu?. Kisha mimi sioni hapa adhabu yoyote wala jela au chochote kinacho shabihiana na hivyo!” Rafiki yake alimjibu kwamba: Wewe! Kwa hakika, nchi hii ya kifalme tunayoiona si lolote isipokuwa ni uwanja wa mtihani na majaribio tu, na ni eneo la mazoezi na kujiweka tayari, na ni maonesho ya kazi za ufundi za kupendeza za mfalme, na ni mahali pa dhifa ya muda mfupi mno, hivi huoni, kwamba msafara unakuja kila siku na mwengine unaondoka na kutoweka? Basi hii ndiyo hali ya nchi hii ya kifalme iliyostawi makazi yake, inajazwa na kusafishwa kwa mwendelezo, na itakuja kupakuliwa moja kwa moja na kubadilishwa kuwa nchi nyingine ya kifalme ya kusalia na kudumu, na watu wote watahamishiwa huko na kulipwa thawabu au kuadhibiwa kila mmoja kulingana na amali yake. Kwa mara nyingine alikaidi rafiki yake mwenye khiyana huku akisema kwa tahayari: “mimi siamini wala si sadiki! Je, inawezekana kuteketezwa ufalme huu uliostawi makazi yake na watu wake kusafirishwa na kwenda kwenye nchi nyingine ya kifalme?”. Na hapo yule rafiki yake mtoaji nasaha muaminifu akasema: “Rafiki yangu, madhali unashikilia kupinga kama hivi, basi njoo nikubainishie dalili zisizo hesabika wala kudhibitika, zilizojumuishwa katika (Sura kumi na mbili) zinazokuthibitishia kwamba ni kweli kuna mahakama kuu, na upo mji kwa ajili ya thawabu na hisani, na mji mwingine kwa ajili ya adhabu na gereza, na kama unavyopakuliwa ufalme huu na kuondolewa watu wake siku baada ya siku, hivyo hivyo itakuja siku watapakuliwa na kuondoshwa katika nchi hiyo ya kifalme moja kwa moja, na kuangamizwa kabisa kiujumla”.
Source text is preserved. When a suitable model is available, translation is displayed separately.
Haşir Risalesi
The Tenth Word
Hivi inawezekana kwa ufalme, na hasa ufalme kama huu mkubwa kukosa malipo kwa watiifu na kukosa adhabu kwa waasi? Na kwa kuwa adhabu na thawabu vinazingatiwa kuwa havipo ndani ya ulimwengu huu, basi hapana budi kuwepo mahakama kuu katika maisha mengine.
Hebu zingatia mwenendo wa matukio na taratibu za mambo katika nchi hii ya kifalme namna riziki inavyo gawanywa kwa wingi hata kwa kiumbe dhaifu sana na fakiri katika nchi hiyo, na namna uangalizi ulivyo kuwa makini, na jinsi maliwazo yalivyokuwa ya kudumu kwa wagonjwa wote waliokosa muangalizi, na tazama vyakula vya kifahari na vyombo vizuri, na nishani zilizorembwa, na mavazi yaliyopambwa na karamu za vyakula zilizostawi zimetawanywa kila mahali, na hebu tazama! Wote wanatekeleza vyema wajibu wao na majukumu yao isipokuwa wewe na wengine mfano wako miongoni mwa wapumbavu, hata mmoja havuki mpaka wake hata kidogo kiasi cha ukubwa wa ncha ya kidole, mtu mkubwa kabisa anatimiza wajibu aliokabidhiwa kwa unyenyekevu wote, na katika upeo wa utiifu, katika hali ya utukufu wa woga na hofu, hivyo mfalme mwenye utawala wa nchi hii ni mwenye ukarimu mkubwa, mwenye huruma kunjufu, mwenye ushindi mtukufu, mwenye wivu uliyo dhahiri, na mwenye daraja ya hali ya juu, na katika yanayojulikana ni kuwa ukarimu unawajibisha kuwepo kuneemesha, na vilevile huruma haipatikani bila ya kufanya wema, na ushindi unalazimisha uwepo wa wivu, na heshima ya hali ya juu inahitaji kuwatia adabu wale wenye kudharau, wakati katika nchi hii ya kifalme hayatokei hata sehemu moja kati ya elfu ya yanayolingana na huruma hiyo wala heshima hiyo, basi dhalimu ataondoka akiwa na nguvu na ujabari wake na aliyedhulumiwa ataondoka huku akiwa dhalili wa hali na unyonge, hivyo basi kesi kama hizi zimeandaliwa kwenda kuhukumiwa kwenye mahakama kuu.
Tazama, namna kazi zinavyotimizwa hapa kwa hekima ya hali ya juu na kwa mpangilio stadi, na chunguza namna kazi zinavyotazamwa kwa jicho la uadilifu na haki na mizani yenye kusibu. Na katika yanayofahamika ni kuwa hekima na busara ya serikali ni kuwahurumia na kuwakirimu wale wanaotafuta himaya yake na uadilifu wa kweli unataka kuchunga haki za raia ili heshima ya serikali ipate kuhifadhiwa na utukufu wa dola upate kulindwa, isipokuwa hapa haionekani ila sehemu ndogo sana katika kutekeleza yanayoendana na hekima hiyo na uadilifu huo. Basi mfano wako ambao ni katika walioghafilika wataondoka nchi hii ya kifalme bila ya walio wengi kati yao kuiona adhabu yoyote. Hivyo basi kadhia hapa imeahirishwa bila shaka yoyote hadi kwenye mahakama kuu.
Tazama kiwango kisichohesabika wala kudhibitika katika johari adimu zinazooneshwa katika maonesho haya, na vyakula vya pekee vitamu vilivyo pambwa kwenye meza za kulia, mambo yanayotudhihirishia kwamba mfalme wa nchi hii ana ukarimu usio na mipaka, na hazina zilizojaa tele na hazitindiki, lakini ukarimu kama huu wa kudumu, na mfano wa hazina kama hizi zisizokwisha, zinahitajia kwa hakika nyumba ya dhifa ya kudumu milele, humo kuna vile ambavyo nafsi zinatamani, na pia inahitajia kukaa milele kwa wale wenye kuneemeka na kustarehe humo, pasipo kuonja maumivu ya utengano na kutoweka, kwani kama ilivyo kuondoka kwa maumivu ni raha, basi vile vile kuondoka na kutoweka kwa raha ni maumivu, na tazama haya maonesho na angalia kwa makini katika matangazo yale na wasikilize vyema wale wapiga minada waitaji ambao wanasifia maajabu ya kazi za kifundi za mfalme zenye miujiza na wanatangaza kazi hizo, na kudhihirisha ukamili wake na wanaelezea wazi kuhusu uzuri wake wa kimaana ambao hauna kifani, na wanataja sifa za ndani za uzuri wake uliojificha, mfalme huyu kwa hiyo ana ukamilifu uliojitokeza dhahiri, na uzuri wa kimaana wenye kung’ara, vinapelekea kustaajabu. Na bila shaka yoyote, ukamilifu uliojificha ambao hauna upungufu, unahitajia kutangazwa mbele ya macho ya mashahidi miongoni mwa wanaopendezwa na uzuri huo, na unahitajia kutangazwa mbele ya macho ya wenye kuthamini uzuri huo. Ama uzuri uliojificha ambao hauna kifani chake, basi utalazimu kuuona na kuudhihirisha, yaani kuuona uzuri wake kwa sura mbili. Namna ya kwanza: Kuuona wenyewe kwa dhati yake katika kila kitu ambacho uzuri huu unaakisi katika vioo mbali mbali. Namna ya pili: Kuuona kwa mtazamo wa wenye kushuhudia waliokuwa na shauku na kupendezwa na uzuri huo, na hii inamaanisha kwamba uzuri wa milele unahitajia kuonekana na kudhihiri, pamoja na kushuhudia kwa daima, na kuonekana kwa milele, na hii inahitajia kwa lazima kukaa milele kwa wale wanaoshuhudia, na wenye shauku na kuthamini uzuri huo, kwa sababu uzuri wa kudumu hauridhiki na mwenye shauku mwenye kutoweka. Na kwamba mwenye kushuhudia aliyehukumiwa kutoweka, kwa kule kufikiria kutoweka kunabadili mapenzi yake kuwa ni uadui, na kupendezwa kwake kunabadilika kuwa dharau, na kutukuza kwake kunageuka kuwa ni kupuuza, kwani mwanaadamu ni adui kwa kile asichokijua, na asichoweza kukifikia, na kwa kuwa wote wanaondoka na kuacha nyumba hii ya dhifa upesi na kuwa mbali nayo bila ya kukata kiu ya nuru ya uzuri na ukamilifu huo, bali huenda wasione isipokuwa vivuli vyake vyenye kufifia, kupitia mipepeso ya jicho ya haraka haraka, hivyo safari inaelekea katika mahali pa kuonekana daima milele.
Zingatia namna mfalme huyu - asiye na kifani - alivyo na huruma kubwa inayojitokeza katika matukio na mambo haya, anamsaidia muhitaji anayeomba msaada, na kumuitikia muombaji anayetafuta kimbilio, na anapoona haja ndogo kabisa kwa mtu wa kawaida sana miongoni mwa raia wake hakika yeye huitimiza haja hiyo kwa huruma na upole, kiasi ya kwamba anatuma dawa na kumuandaa tabibu wa wanyama kwenda kutibu mguu wa kondoo miongoni mwa kondoo. Rafiki yangu, haya twende katika kisiwa kile kinacho kusanya mjumuiko wa watu wengi mno, kwani watukufu wote wa nchi hii ya kifalme, wamekusanyika huko, tazama huyo mjumbe mtukufu wa kifalme akiwa amevalia nishani mbali mbali tukufu kabisa anatoa hotuba ambamo anawasilisha wito kutoka kwa mfalme wake mpole, na wote walio pamoja naye wanamuafiki na wanamsadikisha na wanaomba anayoyaomba yeye. Sikiliza anachokisema mpenzi wa mfalme mtukufu, hakika anaomba kwa adabu nyingi na unyenyekevu na anasema; “Ewe mfalme uliyeeneza neema zako juu yetu, kwa dhahiri na siri, ewe mfalme wetu, hebu tuoneshe chemchemu na vyanzo vya hivi ulivyotuonesha katika vielelezo na vivuli, tuchukue na utupeleke kwenye makao makuu ya ufalme wako na usituangamize kwa kupotea katika uwanda huu, tupokee na utunyanyue katika viwanja vya ufalme vya hadhara yako. Tuhurumie, tulishe huko ladha za vile ulivyotuonjesha hapa, wala usituadhibu kwa maumivu ya kuwa mbali na kufukuzwa katika hadhara yako, basi hawa hapa raia zako wenye shauku nawe, wenye kukushukuru watiifu kwako, usiwaache wakiwa wanatanga tanga na kupotea, wala usiwaangamize kwa umauti usio na marejeo baada yake. Je, rafiki yangu umesikia anachosema? Kwa kufikiria tu, je, inawezekana kwa mmiliki wa uwezo wote huu wa hali ya juu, na huruma zote hizi zenye kuenea, kwamba asimpe mjumbe wake mtukufu anachokipenda, na wala asiitikie shabaha kuu kabisa na makusudio matukufu kabisa? Na hali ya kuwa yeye anatimiza kwa umuhimu mkubwa na matakwa ya chini kabisa ya mtu mdogo kabisa katika raia wake? Pamoja na kuwa anachokiomba huyu mjumbe mtukufu ni kuhakikisha kupatikana kwa matakwa ya wote na makusudio yao, na hilo ni katika mambo yanayohitajika na uadilifu wake, huruma yake, na radhi zake, kisha jambo hilo ni jepesi na rahisi kwake, hilo sio gumu kuliko alivyodhihirisha, miongoni mwa vielelezo mbali mbali katika pande za nchi hii ya kifalme na maonesho yake, basi midhali ametoa vipawa vingi mno na akaanzisha nchi hii ya kifalme ili kuonesha vielelezo vyake kwa muda mfupi hivyo hapana budi kwamba yeye ataonesha katika makao makuu ya ufalme wake katika hazina zake za hakika na katika kamilifu zake na maajabu yake ambayo yatahemeza akili, kwa hiyo hawa walio katika mji huu wa mtihani hawapo kimchezo wala bure bure tu, bali kasri za mafanikio za kudumu milele kwa milele zinawangoja, au masweko ya magereza ya kuogofya milele.
Njoo, na utazame hizi treni kubwa, na ndege hizi zilizoshehenishwa, na haya maghala makubwa yaliyojaa tele, na haya maonesho yalioratibiwa vyema, na zingatia taratibu na mwenendo wa mambo ulivyo hakika vyote hivyo vinabainisha kwamba uko ufalme mkubwa kweli. unahukumu nyuma ya pazia, mfano wa ufalme huu kwa lazima unahitajia raia wanaoendana nao. Wakati ambapo tunaona kwamba wamekusanyika katika karamu hii ya makaribisho - ya dhifa ya dunia - na nyumba hii ya wageni inawaaga kila siku aina mbali mbali kati yao na kuwapokea aina nyingine. Nao wamehudhuria katika medani hii ya mtihani na majaribio, isipokuwa medani inabadilishwa kila saa moja, nao wanakaa kidogo katika maonesho haya makubwa wanatazama kwa raha sampuli mbali mbali za neema za mfalme zenye thamani kubwa na ufundi wake wa kupendeza, ispokuwa maonesho yenyewe hubadilishwa kila dakika. Aliyesafiri harudi na aliyekuja naye atasafiri vilevile. Mambo haya yanabainisha waziwazi kwa namna ya kukata shauri kwamba nyuma ya nyumba hii ya wageni yenye kutoweka na nyuma ya medani hizi zenye kubadilishwa, nyuma ya maonesho haya yenye kugeuka, kuna kasri za kudumu za makazi mazuri ya daima na mabustani yaliojazwa hakika za sampuli hizi, na hazina zilizosheheneshwa asili zake. Hivyo basi kazi na vitendo kwa hapa sio lolote ila ni kwa ajili ya malipo yaliyo andaliwa huko. Kwani mfalme mwenye uweza anakalifisha hapa na huko anatoa ujira basi kila mtu atapata aina ya maisha ya furaha kulingana na maandalizi yake na ile kheri aliyoiendea.
Njoo tutembee kidogo tuchanganyike na raia ili tutazame hali zao, na mambo yanayoendelea katika mazingira yao, tazama kila pembe kumewekwa vifaa vingi vya kupiga picha vinachukua picha, na kila mahala kuna waandishi wanasajili kila kitu, hata jambo dogo kabisa kuliko yote. Haya, ona mlima ule wenye kimo kirefu sana, kumewekwa kamera kubwa juu yake, inayomhusu mfalme mwenyewe inachukua picha ya yote yanayojiri katika nchi hii ya kifalme. Mfalme ameshatoa amri yake kwamba mambo yote yasajiliwe, au ihifadhiwe miamala yote katika nchi ya ufalme wake, na hii inamaanisha kuwa, mtukufu mfalme, ndiye anayetoa imla ya matukio yote, na anaamrisha kuchukuliwa picha matukio hayo, basi huku kutilia umuhimu kupita kiasi, na huu uhifadhi makini wa mambo yote, nyuma yake kuna kuhesabiwa bila shaka yoyote, kwa sababu itawezekana kweli! Kwa mtawala mwenye kuhifadhi kumbukumbu asiyepuuzia muamala duni kabisa wa raia wake wa kawaida kabisa, halafu eti asihifadhi wala kuweka kumbukumbu matendo makuu ya raia wake wakuu, wala asiwahesabu, wala asiwape malipo yao kutokana na yale waliyoyafanya! Pamoja na kuwa wanayaendea matendo yanayomgusa mfalme ambaye ni Mwenye nguvu na yanaingilia ukuu wake, na hali ya kuwa huruma zake kunjufu zinayakataa matendo hayo? Na kwa kuwa watu hao hawapati adhabu hapa, basi hapana budi kwamba adhabu hiyo imeahirishwa hadi kwenye mahakama kubwa.
Njoo, nikusomee amri hizi zitokazo kwa mfalme, angalia hakika yeye anakariri ahadi na makamio yake kwa kusema: Nitakupelekeni kwenye makao makuu ya ufalme wangu, na nitawafurahisha watiifu miongoni mwenu, na nitawaingiza gerezani waasi miongoni mwenu, na hakika mahali hapo pa muda maalumu nitapateketeza kabisa na nitaanzisha ufalme mwingine ambao ndani yake kutakuwa ni kasri za kudumu na magereza ya kudumu, kwa kujua kwamba ahadi aliyofunga kwa nafsi yake kuwa ni rahisi kwake kuitekeleza na kwamba ni ya umuhimu wa ukomo wa hali ya juu kwa raia wake na ama kukhalifu ahadi yake utukufu wake na uweza wake vinakataa. Basi tazama ewe mwenye kughafilika: Wewe unasadiki uongo na mawazo dhanifu na kuweweseka kwa akili yako na kujihadaa nafsi yako, wala humsadikishi ambaye hahitajii kukukhalifu ahadi kabisa, wala kukhalifu huko hakulingani na ghera na izza (Utukufu) yake asilani, na ambaye mambo yote yanashuhudia ukweli wake, hakika wewe unastahiki adhabu kubwa bila shaka, kwani mfano wako katika hili ni mfano wa msafiri ambaye anafumba macho yake asione mwanga wa jua, na anatafuta maelekezo kupitia maoni yake ya kufikirika, na anataka kuangazia njia yake ya kuogofya kwa kutumia mmemetuko wa akili yake ambao hauangazii isipokua kama mwanga wa kimulimuli (Kipepeo cha usiku). Na kwa kuwa ameahidi, kwa hakika atatimiza ahadi yake tu, kwa sababu kutimiza kwake ni rahisi na kwepesi, na hayo ni katika mahitajio ya ufalme wake, na jambo hilo ni la muhimu sana, kwetu na kwa kila kitu, hivyo kuna mahakama kubwa na furaha kuu.
Njoo tuwatazame maraisi wa duru hizi, sehemu kati yao wanaweza kuwasiliana na mfalme mkuu moja kwa moja kwa simu maalumu, bali sehemu nyengine imepanda hadi katika uwanja wa utakatifu wake, zingatia hawa wanasema nini? Hakika hao wanatuhabarisha sote kwamba mfalme ameandaa mahali pakuu pa kupendeza, kwa ajili ya kuwajazi watenda wema, na mahali pengine pa kutisha, kwa ajili ya waovu, na anaahidi ahadi madhubuti na anakemea makamio makali, na yeye ni mtukufu zaidi na mwenye izza kiasi hawezi kujidhalilisha kwa kwenda kinyume na alivyoahidi na kukemea, hali ya kujua kwamba habari ya wapashaji imefikia katika wingi hadi kiasi cha tawaatur (Upokezi kwa msururu unaoafikiana) na katika nguvu kiwango cha kuafikiana na ijmai hakika wanatueleza wote: Kwamba makao makuu ya ufalme huu mkubwa ambao athari zake na alama zake zinaonekana hapa. Hayo yako katika ufalme mwengine huko mbali, na kwamba majumba katika medani ya mitihani haya ni majengo ya muda mfupi yatabadilishwa yawe kasri za kudumu, na hapo ardhi hii itabadilishwa kwa kuwekwa nyingine. Hakika ufalme huu mkuu ni wa kudumu tena unajulikana kutokana na athari zake, haiwezekani kuishia utawala wake katika mambo kama haya ya kutoweka ambayo hayana kubaki wala ukamilifu wala utulivu wala thamani wala uthabiti, bali unatulia katika hali inayolingana nayo, na ukubwa wake katika mambo yenye wasifu wa udaima, ukamilifu, na ukuu, kwa hiyo kuna maisha mengine, na hapana budi kuwepo safari kuelekea katika makao hayo.
Njoo ewe rafiki yangu, kwani leo ni sikukuu ya kifalme iliyokuwa kubwa kabisa , kutatokea mabadiliko na mageuzi na yatajitokeza mambo makubwa, basi twende pamoja matembezini, katika siku hii ya furaha katika majira ya machipuo kwenda kule uwandani, uliojawa na maua mazuri, tazama watu hawa hapa wanaelekea huko, tazama hapa kuna jambo geni la ajabu, majumba yote yanateketea na yanachukua maumbo mengine, kwa kweli ni jambo la muujiza! Kwani majumba yaliyoteketea yamerejea kujengwa tena haraka, na uwanda huu mtupu umegeuka kuwa mji uliosheheni makazi! Tazama! Inakuonesha kila saa mambo mapya ya kuonekana na kuchukua umbo lingine sio umbo lake lililotangulia – kama kioo cha sinema – chunguza jambo hili kwa makini upate kuona umaridadi wa mpangilio huu mzuri katika kioo hiki cha kuoneshea, ambacho huchanganyika mambo mengi ndani yake ya kuonekana na kugeuka haraka mambo ya hakika yanayoonekana, kila kitu kinachukua mahali pake pa uhakika katika upeo wa umakini na kushikana sawa, hata mambo yaonekanayo ya kufikirika hayafikii kiwango hiki cha kupangilika na kupendeza na kufanywa vizuri. Bali hawawezi mamilioni ya wachawi hodari sana kutenda mfano wa matendo haya ya kupendeza sana. Kwa hiyo mfalme aliyefichwa nasi hatumuoni anayo mengi katika mambo yenye kufurutu ada. Basi ewe uliyeghafilika! Hakika unasema: Vipi inawezekana kubomolewa mamlaka hii tukufu na kujengwa upya sehemu nyengine? Basi hili hapa mbele yako jambo lisilokubalika na akili yako, katika mapinduzi mengi na mabadiliko ya kushangaza, basi upesi huu katika kukutanika na kutengana na huku kugeuka na kubadilika, huku kujenga na kubomoa vyote hivyo vinatoa taarifa ya kuwepo makusudio maalumu, na kubeba lengo maalumu, kwani hutumika kwa ajili ya kukusanyika saa moja kiasi ambacho kinatumika kwa miaka kumi! Hali hizi kwa hiyo hazikusudiwi dhati yake yenyewe, bali ni vielelezo na mifano ya kuonyesha hapa, basi mfalme anamaliza kazi yake kwa namna ya kufanya muujiza, zipate kuchukuliwa sura zake, na kuhifadhiwa matokeo yake, na kuhifadhiwa kila kilichopo katika medani ya mazoezi ya kiaskari. Basi mambo na miamala kwa hiyo yatajiri katika mkutano mkubwa na kuendelea kama ilivyokuwa hapa, na yataoneshwa mambo hayo kwa namna ya kuendelea katika maonesho makuu, yaani hali hizi za kutoweka zinatoa matunda ya kusalia na kuzalisha sura za kudumu milele huko, basi makusudio ya mahafali haya, ni kufikia furaha kuu. Na mahakama kuu na malengo ya upeo wa juu yamefichwa kwetu hatuyaoni.
Njoo ewe rafiki mkaidi, tupande ndege au treni ili twende mashariki na magharibi, yaani kuelekea muda uliopita au muda ujao, ili tupate kushuhudia aliyoyadhihirisha mfalme miongoni mwa miujiza aina mbali mbali katika mahali pengine, basi tulichokiona hapa katika maonesho, au katika medani, au katika kasri, katika mambo ya ajabu yana vielelezo kila mahali, isipokuwa yanatofautiana kwa upande wa umbo na muundo, basi wewe rafiki yangu tazama vyema jambo hili, upate kuona kiasi cha kujitokeza mpangilio wa hekima, na upeo wa uwazi wa ishara za uangalizi, na kiasi cha kudhihiri alama za uadilifu, na kiwango cha kudhihirika kwa matunda ya rehema kunjufu, katika kasri hizo zenye kubadilika, na katika medani zile za kutoweka, na maonesho yanayoondoka, basi ambaye hajapoteza busara yake kwa yakini atafahamu, kwamba haitakuwa bali haiyumkiniki kupata taswira, hekima iliyokamili zaidi kuliko hekima ya mfalme yule, wala uangalizi mzuri zaidi ya uangalizi wake, wala uadilifu mtukufu kuliko uadilifu wake, lakini kwa kuwa nchi hii ya kifalme kama inavyojulikana, yenye kushindwa kudhihirisha hakika za hekima hizi na uangalizi na huruma, na uadilifu, na lau isingekuwepo katika makao ya ufalme wake kama ulivyodhani kasri za kudumu, na mahali pa hali ya juu thabiti, na makazi mazuri ya milele, na wakazi wa kudumu, na raia wenye furaha kutokea kwa hakika ya hekima, rehema na uadilifu, itabidi hivyo kukanusha hekima tunayoiona, tunachokishuhudia katika uangalizi, na kukanusha tukionacho katika huruma, na kukanusha alama hizi, na ishara za uadilifu zilizo dhahiri na bayana. Kukanusha yote hayo kwa upumbavu wenye kufedhehesha kama upumbavu wa mtu aonaye mwanga wa jua na kisha anakanusha kuwepo kwa jua lenyewe, mchana kweupe kabisa! Na inalazimu pia kusema kuwa: Mwenye kufanya haya tuyaonayo katika taratibu za kuendesha mambo yenye kusifika kwa hekima na matendo yenye makusudio mema, na hisani zilizojaa rehema, hakika anafanya pumbao na mchezo na kusaliti, - hasha kisha hasha kwake, - na hili si jambo lingine ila ni kupindua hakika ziende kinyume chake, na hili ni muhali kwa maafikiano ya watu wote wenye akili isipokuwa yule mpumbavu ambaye anakanusha uwepo wa vitu, na hata kuwepo kwa nafsi yake. Hivyo yapo makao yasiyokuwa makao haya, huko kuna mahakama kubwa, na makao ya uadilifu wa juu, na makao makuu ya ukarimu mkubwa ili ipate kudhihiri huko rehema hii na hekima hii na uangalizi huu na uadilifu huu kwa wazi na dhahiri.
Ewe rafiki yangu! Njoo huku na turudi nyuma kidogo tukaonane na makundi haya na viongozi wao tazama zana zao, je, zana hizo wamepewa kwa ajili ya kutumia ndani ya muda mfupi tu? Katika medani hii ya mazoezi, au walipewa zana hizo ili wakaishi maisha ya furaha ya muda mrefu mahali pengine? Na kwa kuwa hatuwezi kukutana na kila mmoja miongoni mwao, na hatuwezi kuchungulia vifaa vyao vyote na maandalizi yao, kwa ajili hiyo tutajaribu kutalii utambulisho na jalada la matendo ya mmoja kati yao kama kielelezo na mfano. Kwani katika utambulisho huo tunapata wadhifa wa cheo cha afisa, mshahara, majukumu, mafao, vitengo vya wadhifa huo na cheo alichonacho, na kila kinachoambatana na hali yake, zingatia, kwamba hakika ya cheo hicho si kwa ajili ya masiku kadhaa, bali ni kwa ajili ya muda mrefu, na katika utambulisho wake kumeandikwa kwamba huyo anapokea mshahara kutoka hazina maalumu, tarehe kadhaa, isipokuwa tarehe hiyo iko mbali sana, na haiji siku hiyo ila baada ya kutimiza majukumu ya mazoezi katika medani hii, na wadhifa huu hauwafikiani na medani hii ya muda mfupi wala haiwiani nao pamoja na cheo chake, bali wadhifa huo ni kwa ajili ya kufuzu maisha ya furaha ya milele kwenye sehemu tukufu mbele ya mfalme Mweza wa yote, ama wajibu nao ni pia hauwezekani uwe kwa ajili ya kukidhi masiku kadhaa ndani ya nyumba hii ya wageni bali ni kwa ajili ya maisha mengine ya furaha na ya milele, inabainika wazi kutokana na utambulisho huo kwamba mwenye utambulisho kama huo ameandaliwa maisha sehemu nyengine, bali pia anakwenda kwa kasi kuelekea ulimwengu mwingine (Akhera). Tazama haya majalada ambayo ndani yake kumeelekezwa namna ya kutumia zana na majukumu yanayofuatana na zana hizo, na kama itakuwa hakuna daraja ya juu ya milele isio medani hii, basi hakuna maana ya kuwepo utambulisho huu uliotengenezwa vyema, na wala hakuna maana ya kuwepo kwa jalada hili lililopangika vyema, na angeporomoka afisa mheshimiwa, kiongozi mwenye kutukuzwa na kuwa katika daraja ya chini na angepata mateso, udhalili, kupuuzwa, maafa na udhaifu, pamoja na ufakiri, pima kwa akili yako kwa kutumia kipimo hiki, basi kila utakapoangusha jicho lako kwa makini na kuchunguza kutazama huko kutakuongoza, na utagundua kuwa kuna kusalia milele baada ya kutoweka huku. Basi ewe rafiki yangu! Hakika nchi hii ya ufalme wa muda mfupi, si lolote isipokuwa ni sawa na mfano wa shamba, au medani ya mafunzo, au soko la biashara hivyo hapana budi baada yake ipatikane mahakama kuu na furaha ya milele. Basi ukikanusha haya utalazimika kukanusha utambulisho wote, na majalada anayomiliki yule afisa, na kila zana na vifaa vyote na maelekezo ya mafunzo, bali utalazimika kukana mifumo yote katika nchi hii ya kifalme, bali kukana kuwepo kwa hata dola yenyewe, na hapo utalazimika kukadhibisha taratibu zote za uendeshaji wa mambo zinazotokea ndani yake, ndipo utakapofikia hatua ya kuwa haiwezekani wewe kufahamika kuwa ni mwanaadamu mwenye hisia na hivyo utakuwa mpumbavu zaidi kuliko wasofisti. Pia tahadhari na tena tahadhari, kudhania kwamba dalili na ishara za kubadilika kwa nchi hii ya kifalme zinaishia katika hizi sura (kumi na mbili) tulizozieleza, kuna kiasi kisichohesabika wala kudhibitika cha alama na dalili kwamba nchi hii yenye kubadilika na kutoweka itageuka kuwa nchi nyengine ya kudumu na yenye kubaki, na kuna ishara chungu nzima zinazojulisha kuwa watu hawa watasafirishwa kutoka nyumba hii ya ugeni wa muda mfupi, na kwenda katika makao makuu ya ufalme wa kudumu na milele. Ewe rafiki yangu! Njoo nikuthibitishie, hoja yenye nguvu zaidi na bayana zaidi kuliko zile hoja kumi na mbili zilizotangulia, njoo umuangalie yule mjumbe mtukufu mwenye nishani za makamo ya juu, ambaye kabla tulishamuona kule kisiwani, hakika anafikisha jambo mbele ya makundi ya watu wengi, ambayo yanaonekana kwetu kwa mbali, basi haya twende tukamsikilize, zinduka! Huyu hapa anafasiri mbele ya mkusanyiko wa watu tangazo la kifalme lenye hadhi ya juu, huku akilibainisha kwa kuwaambia: Jiandaeni! Mtasafiri kuelekea nchi nyingine ya kifalme ya kudumu milele, utukufu ulioje wa nchi hiyo ya kupendeza! Hakika nchi yetu hii ya kifalme inahesabiwa kama gereza kulinganisha na hiyo, kama mtasikiliza jambo hili kwa makini na mkalitekeleza vyema mtakuwa wenye kustahiki kupata huruma za mfalme wetu na hisani zake katika makao yake ambayo mnayaelekea, na kama si hivyo jela za kutisha ni mafikio yenu, ikiwa ni malipo ya kuasi kwenu amri na kutoizingatia. Hakika anawakumbusha hadhira tangazo hili, na unaona juu ya tangazo hilo kuu kuna muhuri wa mfalme ambao hauigwi. Na wote wanatambua kwa yakini, - ila mfano wako katika vipofu, - kwamba mjumbe yule mwenye kuheshimiwa sana, kwa nishani za makamo ya juu ni mfikishaji mwaminifu wa amri za mfalme kwa kuangalia tu zile nishani. Je, unadhani yawezekana kupinga suala la kubadilishwa kwa nchi hii ya kifalme, ambalo analilingania yule mjumbe mtukufu kwa nguvu zote alizopewa, na limo ndani ya tangazo la kifalme la makamo ya juu? Kamwe, hilo haliwezekani kamwe, isipokuwa ukikana vyote uvionavyo katika mambo na matukio mbali mbali. Basi sasa ewe rafiki yangu! Una hiari ya kusema utakacho. Mimi yatarajiwa niseme nini? Je, kumebaki ziada kwa msemaji yeyote baada ya hakika hizi? Na je, inafaa kuuliza jua liko wapi hali ya kuwa liko katikati ya mbingu? Hakika yote niyatakayo kuyasema ni: “الْحَمْدُ لِلَّهِ” na shukrani elfu moja na moja, hakika nimeokoka kutoka katika mshiko wa mawazo ya dhana na matashi, na kukomboka kutoka katika mateka ya nafsi na gereza la milele, hivyo nimeamini kuwa kuna maisha ya furaha mbele ya mfalme muadhimishwa. Nasi tunaandaliwa kwayo, baada ya maisha haya yenye kutoweka na yenye kugongana. Na kwa namna hii hekaya imetimia ambayo ilikuwa ni fumbo la al-hashri na kiama, na sasa tutagura kwa tawfiiq ya aliye juu kuliko chochote, Mweza wa kila jambo katika hakika za juu, tutazibainisha katika (hakika kumi na mbili) na zenyewe zinategemeana na zenye kufungamana, mkabala wa sura kumi na mbili baada ya kuziwekea utangulizi. * * *
Tutaashiria ishara tu, katika masuala ambayo tumeyafafanua mahali pengine, yaani katika maneno ya kumi na tisa, ishirini na tatu, na ishirini na sita.
Zipo hakika tatu kwa yule mpumbavu na rafiki yake mtoa nasaha mwaminifu waliotajwa katika hekaya: Ya kwanza: Nafsi yangu yenye kuamrisha na moyo wangu. Ya pili: Wenye kujifunza falsafa na wanafunzi wa Qur’an tukufu. Ya tatu: Mila ya ukafiri na umma wa kiislamu. Hakika kutokumjua Allah (s.w), ndio jambo lililowaingiza wenye kujifunza falsafa na mila ya ukafiri na nafsi yenye kuamrisha maovu katika upotevu wa kutisha, kama mtoa nasaha muaminifu alivyosema katika hekaya: Kwamba haiyumkiniki kuwepo herufi bila mwandishi, wala kanuni bila hakimu, hali kadhalika tunasema. Ni muhali kuwepo kitabu bila mwandishi na hasa kitabu kama hiki ambacho kinakusanya kila neno katika maneno yake kitabu kilichoandikwa kwa kalamu makini, na ambacho chini ya kila herufi kati ya herufi zake kuna shairi lililofumwa kwa kalamu ya hali ya juu, na vivyo hivyo ni katika muhali wa muhali kwamba ulimwengu huu kuwa pasina mtengenezaji, kwani ulimwengu huu ni mfano wa kitabu kwa namna kubwa kabisa kila ukurasa ndani yake unakusanya vitabu vingi; Hapana, bali kila neno humo ni kitabu, na kila herufi humo ni shairi, basi uso wa ardhi ni ukurasa, na wingi ulioje wa vitabu vilivyomo! Na mti ni neno moja, na wingi ulioje uliomo humo wa kurasa! Na tunda ni herufi, na mbegu ni nukta, na katika nukta hii kuna faharisi ya mti uliostawi kocho kocho na mpango kazi wake, basi kitabu kama hiki hakiwi ila kutokana na ufundi wa kalamu ya mwenye uweza anayesifika kwa uzuri na utukufu, na hekima isiyo na mipaka, yaani kwa kuangalia tu katika ulimwengu na kuushuhudia inalazimu imani hii, isipokuwa yule ambaye upotevu umemlewesha! Na kama isivyoyumkinika kuwepo kwa nyumba bila mjenzi, na hasa nyumba hii ambayo imepambwa kwa mapambo ya kupendeza mno bila kifani, na kuwekwa nakshi kwa nakshi za kuvutia kuliko zote, na kupendeza mno kuliko zote, na imesimamishwa kwa ufundi unavunja kawaida, hadi kila jiwe katika mawe yake inajipanga ndani yake ustadi uliopo katika jengo lote, basi mwenye akili hakubali kuwa nyumba mithili ya nyumba kama hii kuwapo bila ya mjenzi mahiri, na hasa ni kuwa anajenga katika diwani hii kila saa moja, makazi ya kweli yalio na ukomo wa mpangilio na uwiano, na anayabadili kwa mpangilio na wepesi kamili kama wepesi wa kubadili mavazi, bali yeye huanzisha katika kila nguzo vyumba vingi vidogo vidogo, katika hadhara ya kweli. Basi hapana budi kuwa huu ulimwengu mkubwa kuwa una Muumba, mwenye hekima kuliko chochote, mjuzi wa kila kitu, Mweza wa kila kitu bila mipaka, kwani ulimwengu huu mkubwa ni kama kasri ya kupendeza, jua na mwezi ni taa zake, na nyota ni mishumaa na kandili zake, na wakati ni mkanda ambao Muumba anaweka maelezo juu yake, mwenye utukufu mkuu, kila mwaka kuna ulimwengu mwingine anaudhihirisha katika uwepo, akizifanya upya humo picha zilizo pangika ndani ya maumbo na aina mia tatu na sitini, akibadilisha kwa mpangilio timamu, na hekima kamili, hali ya kuwa anajaalia sura ya ardhi ni meza ya chakula ya neema mbali mbali, anapamba katika kila majira ya machipuo, kwa aina mia tatu elfu ya aina za viumbe vyake, na anazijaza kwa kiasi kisicho hesabika wala kudhibitika hesabu yake katika neema zake, pamoja na kuzipambanua kila moja kati ya hizo kikamilifu, pamoja na muingiliano wake na msokotano wake na pimia mambo haya mambo mengine, basi inayumkinika vipi kujisahaulisha kuhusu mtengenezaji wa kasri yenye urefu kama huu? Kisha upumbavu mkubwa kiasi gani kwa yule anayekana uwepo wa jua lililo katikati ya mchana na katika usafi wa mbingu, wakati ambao huonekana mimemetuko ya mionzi yake, na kuakisi mwanga wake, juu ya mapovu ya bahari, na juu ya maada za nchi kavu zenye kung’ara na katika vipande vya barafu nyeupe sana, kwa sababu kukanusha uwepo wa jua moja ni kulikataa, katika hali hii inalazimu kukubali vijua vidogo vya kihakika vyenye uasilia, kwa idadi ya matone ya bahari, na kwa idadi ya mapovu, na kwa idadi ya vipande vya theluji, na kama ilivyo kukubali uwepo wa jua kubwa katika kila kijisehemu, - na hiyo ni sehemu moja ya tisa ya atomu - upumbavu. Basi kutoamini kuwepo Muumba mwenye utukufu mkuu, na kukataa kusadiki sifa za ukamilifu wake Allah (s.w) - pamoja na kuona viumbe hivi vilivyo pangika vinavyobadilika, na kubadilishana zamu kwa hekima, kila wakati na vinavyofanywa upya kwa uwiano na mpangilio katika kila wakati - ni upotevu unaotisha bila shaka yoyote, bali ni kuweweseka na wendawazimu, kwani italazimu wakati huo kukubali uungu wa bila mipaka katika kila kitu hata katika kila atomu! Kwa kuwa kila atomu katika atomu za hewa mathalan inaweza kuingia katika kila ua, tunda au jani, na kuweza kutimiza jukumu lake huko, kama hii atomu haikuamrishwa na kutiishwa ingelazimu iwe na ujuzi wa maumbo ya vile ilivyoweza kuingia ndani yake, na kwa sura yake na muundo wake na namna yake, yaani inapaswa iwe na ujuzi unaozungukia kitu kikiwa katika hali zote, na uwezo wa jumla ili iweze kutenda hilo!! Na kila atomu, katika atomu za udongo mathalan, yaweza kuwa ni sababu ya kutokea kwa mbegu na kukua kwa aina zake zote, kama basi haikuwa yenye kuamrishwa na kutiishwa, ingelazimu iwe imekusanya zana na vyombo vya kimaanawi, kwa idadi ya aina ya mimea na miti, au inabidi kuipa uwezo kiasi kwamba inajua maumbo yote ya miundo yake hivyo itengeneze, na ijue sura zake zote, hivyo iweze kuzifuma, na pimia juu ya kipimo hiki vilivyopo vingine, hadi ufahamu kuwa upekee una dalili za wazi dhahiri katika kila kitu. Naam, hakika kuumbwa kila kitu kutokana na kitu kimoja, na kuumbwa kitu kimoja kutoka kila kitu, hakika hilo si jingine bali ni kazi ya Muumba wa kila kitu, basi chunguza na uzingatie, katika kauli yake Allah (s.w): (وَإِنْ مِنْ شَيْئٍ إِلَّا يُسَبِّحُ بِحَمْدِهِ) Na ujue kuwa kutoitakidi Mungu mmoja wa pekee kunalazimu kuitakidi miungu mingi kwa idadi ya vilivyopo.
Katika hikaya kumekuja kutajwa kwa mjumbe mtukufu na pametajwa kwamba kwa asiyekuwa kipofu atafahamu kutokana na kuona nishani zake: Kwamba hakika yeye ni mtu mkubwa habebi amri isipokuwa ile ya mfalme hivyo yeye ni mfanyakazi wake maalumu. Basi mjumbe huyu hakika si mwingine bali ni mtume wetu mtukufu (s.a.w). Naam, inalazimu mfano wa ulimwengu huu mzuri na mtengenezaji wake mtakatifu kuwa na mjumbe kama huyu mtukufu kama ulazima wa mwanga kuwepo na jua. Kwa sababu kama isivyoyumkinika kwa jua isipokuwa kutoa mwanga, ndio hivyo hivyo isivyoyumkinika kwa uungu ila ujidhihirishe kwa kutuma Mitume watukufu amani iwe juu yao. Je, inawezekana uzuri ulio katika upeo wa ukamilifu usijidhihirishe kwa njia na dalili ya kuujulisha? Na je, yawezekana ukamilifu ambao uko katika upeo wa uzuri usitake kujitangaza kupitia kitu kitakachovutia kwake macho ya watazamaji? Na je, inawezekana ufalme wa jumla wa ubwana na malezi ya jumla wenye kukusanya usitake kutangaza upweke wake na utegemewa wake katika tabaka tofauti kupitia mjumbe mwenye mbawa mbili? Yaani mwenye sifa mbili sifa ya utumwa wa jumla basi yeye ni muakilishi wa tabaka za viumbe mbele ya hadhara ya kiungu na sifa ya utume na ukaribu kwake, basi yeye ni mwenye kutumwa kutoka kwa Allah (s.w) kwa walimwengu wote. Na je, inayumkinika kwa mwenye uzuri usio na mipaka asitamani kushuhudia yeye au kuwashuhudisha viumbe wake mazuri ya uzuri wake, katika vioo vinavyoakisi uzuri huu?, yaani kupitia mjumbe kipenzi, kwani huyo ni kipenzi kwa ajili ya kujipendekeza kwake kwa Allah (s.w) kwa utumishi wake uliotakasika, naye ni mjumbe kipenzi, kwa sababu anampendezesha Allah (s.w) kwa viumbe kwa kudhihirisha uzuri wa majina yake mazuri. Na je, inayumkinika kwa anayemiliki hazina zilizosheheni vitu ghali mno na vya ajabu mno, na vile vinavyoshangaza akili, asitake kudhihirisha ukamilifu wake uliojificha? Na asitake kuuonesha mbele ya macho ya viumbe wote, na kuufunua mahali pa kuonekana nao kupitia mjulishaji hodari na mtangazaji mzuri mwenye kusifia? Na je, inayumkinika, kwa yule aliyepamba ulimwengu huu kwa viumbe vinavyoelezea kuhusu ukamilifu wa majina yake mazuri, na akaufanya kuwa ni kasri la kupendeza na akalitia uzuri ustadi wake usio na kifani wa kushangaza, na kuonesha mbele ya macho kuonekana, kisha asimuakilishe jambo hili la kufafanua hilo kwa muelekezaji mwalimu kiongozi? Na je, inayumkinika kwa mmiliki wa ulimwengu huu asibainishe kupitia mjumbe? Lengo ni nini katika kubadilika badilika kwa huu ulimwengu na makusudio ni nini kwa fumbo hili lililofungwa? Na kwamba asijibu kupitia yeye kuhusu mafumbo ya maswali matatu yanayosumbua, katika vilivyomo nayo ni: Kutoka wapi? Kwenda wapi? Na wewe ni nani? Na je, inayumkinika kwa Muumba mwenye utukufu ambaye amejitambulisha kwa wenye hisia kwa viumbe hivi vizuri, na akavipendezesha kwao kwa neema zake ghali, asiwabainishie kwa kupitia mtume anachokitaka kwao na anachokiridhia kwa neema hizi zilizoenea? Au je, inayumkinika kwa Muumba ambaye aliyeitahini sampuli ya kibinadamu kwa kutofautiana hisia na mielekeo, na akaandaa utayari wake kwa utumishi timamu na kwamba asitake kuelekeza macho ya sampuli hii kutoka katika wingi kwenda katika tauhid kupitia mwelekezi Mtume (s.a.w)? Na kama hivi, hakika zipo dalili nyingine zaidi ya zilizotangulia, zote ni hoja zenye kukata shauri zinazobainisha kazi za mitume na majukumu yao, na kuweka wazi kwamba Uungu hauwi bila utume. Na sasa je, amedhihiri ulimwenguni ambaye ni mwenye wasifu mwingi zaidi, na mwenye kukusanya zaidi sifa hizo, na nyadhifa zilizotajwa kuliko Muhammad wa nasaba ya bani Hashim (s.a.w)? Au yupo ambaye anafaa zaidi kuliko yeye Mtume (s.a.w), kwa cheo cha utume na jukumu la tabligh (ufikishaji)? Na je, zama zimemdhihirishia yeyote mwenye kufaa zaidi kuliko yeye? Hapana, kisha hapana, kwani yeye ni imamu wa Mitume wote, na kitulizo cha jicho la wateule wote, na mfalme wa waelekezi wote, na pambo la wateuliwa wote, na wakurubishwa wote, mwenye maelfu ya miujiza kama kupasuka kwa mwezi, na kutoka maji katika vidole vyake vitukufu, achilia mbali dalili na ishara zake nyengine za utume wake zisizo hesabika, ambazo ni mahali pa ijmai ya watu wenye fadhila na elimu, na ukiacha Qur’an tukufu ambayo ni bahari ya hakika na miujiza tele mikubwa, kwani hiyo Qur’an ni kama jua lenye kuchomoza ni dalili ya kukata ubishi juu ya ukweli wa utume wake (s.a.w). Na hakika tumekwishathibitisha muujiza wa Qur’an kwa namna takriban arubaini katika namna za miujiza kwenye (Risale-i Nur) hasa katika neno la (Ishirini na tano).
Isipite akilini mwa mtu akauliza: Ni upi umuhimu wa huyu mwanaadamu aliyekuwa mdogo kimaumbile na ana thamani gani mpaka imalizike dunia hii na baadaye ifunguliwe dunia nyengine ili ahesabiwe matendo yake na kulipwa! Kwa sababu huyu mwanaadamu, yeye ndiye bwana wa viumbe vyote licha ya udogo wake kimaumbile, kutokana na yale aliyojaaliwa kuwa nayo katika asili ya maumbile yake jumuishi ndio maana amekuwa kiongozi juu ya viumbe wengine, na ni mlinganiaji wa ufalme na uungu wa Allah (s.w), na muwakilishi katika utumishi kiujumla katika kuonesha na kudhihirisha uungu huo, ndio maana amepata umuhimu mkubwa kama huo. Na vile vile isipite akilini kuuliza: Vipi ahukumiwe mwanaadamu huyu adhabu ya milele ilihali umri wake ni mchache mno? Kwa sababu ukafiri ni uhalifu mkubwa, na pia ni jinai isiyo na mipaka, kwani ukafiri unateremsha thamani na daraja ya viumbe, daraja ambayo ni sawa na ile thamani ya barua za Mtegemewa na daraja yake aliyokuwa nayo, hadi katika kina cha mchezo, na kuweka dhana batili kuwa hakuna lengo la kuumbwa kwake, hakika hiyo ni dharau ya wazi kwa viumbe vyote, na kukanusha kinacho shuhudiwa katika nuru ya majina yote ya Allah na kukanusha athari zake katika viumbe hivi, na kwa hiyo ni kukadhibisha kiwango kisichodhibitika cha dalili zinazoonesha juu ya hakika ya kuwepo kwa dhati ya Allah (s.w), na yote haya ni jinai isiyo na mipaka, na jinai isiyo na mipaka inapasisha adhabu isiyowekewa mipaka.
Hakika tumeona katika hekaya kwa sura zake zote kumi na mbili: Kwamba haiwezekani kwa namna yeyote iwavyo kuwa mfalme mkuu awe na nchi ya kifalme ya muda mfupi, kama nyumba ya kukaribisha ya wageni, kisha asiwe na nchi nyingine yenye ufalme wa kudumu wenye utulivu na wenye kuendana na heshima yake na taadhima yake, pamoja na makamo ya ufalme wake uliokuwa wa hali ya juu, na vile vile haiwezekani kwa namna yeyote iwavyo, Muumba wa kudumu asianzishe ulimwengu wa kudumu baada ya kuwepo huu ulimwengu wenye kwisha. Na vile vile wala haiwezekani kwa Muumba mwenye hekima zote na Mweza wa kila jambo kuumba ulimwengu huu wenye nafasi ya maonesho ya jumla na viwanja vya mitihani na shamba la muda maalumu, kisha wala asiumbe nyumba ya akhera ambayo itabainisha malengo yake na makusudio yake! Hakika ya ukweli huu kuingia ndani yake ni kwa kupitia (Milango kumi na miwili) na milango hiyo kumi na miwili hufunguliwa kutokana na Hakika (Ukweli) (Kumi na mbili), tutaanza na hakika fupi na nyepesi zaidi kuliko nyingine.
Mlango wa Rububiyya na Ufalme wa kiungu nao ni kudhihirisha jina la “الرَّبُّ” Je, inawezekana kwa mwenye hadhi ya mola mlezi na ufalme wa kiungu, akauleta ulimwengu unaopendeza kama huu, kwa makusudio ya hali ya juu na malengo yaliyotukuka, na akaudhihirisha ukamilifu wake, kisha asiwe na thawabu kwa waumini ambao wamepokea makusudio hayo kwa moyo wenye imani na kutii amri zake, na asiwaadhibu wapotevu waliokabiliana na makusudio hayo kwa ukanushi na dharau?
Mlango wa ukarimu na rehema nao ni kudhihirisha jina “الْكَرِيْمُ na الرَّحِيْمُ” Je, inawezekana kwa bwana mlezi wa ulimwengu huu na mmiliki wake ambaye ameudhihirisha ukarimu wake bila kikomo kwa athari zake, na rehema zake bila ukomo, na ushindi wake bila kikomo, na ghera yake bila kikomo, asikadirie malipo yanayoendana na ukarimu, rehema zake kwa watendao mema, na wala asiweke kwa waovu uamuzi wa adhabu unaoendana na ushindi wake na ghera yake? Lau mwanaadamu angetazama kwa makini mwenendo wa matukio, kuanzia kwa kiumbe hai dhaifu mno na mwenye kushindwa zaidi na kumalizika kwa kiumbe mwenye nguvu zaidi, angeliona kuwa kila kiumbe inamjia riziki yake kwa ukunjufu kutoka kila mahali, bali Allah (s.w) humtunuku yule dhaifu wao zaidi kwa kumpatia riziki njema na nzuri zaidi, na humuhudumia kila mgonjwa kwa kitu kitakachomtibia, na kwa namna hii kila mwenye haja hutimiziwa haja yake bila ya kutegemea, basi takrima hii ya wageni iliyokuwa njema na ya fahari, na kujazwa neema endelevu, na ukarimu wa hali ya juu, unatujulisha waziwazi kuwa mkono mkarimu wa milele ndio unaofanya kazi na kuendesha mambo. Kwa mfano: Hakika kuivalisha miti yote kwa mapambo ya kijani kiwiti yanayorandana na sundusi kama vile ni mahuri wa peponi, na kuipamba na maua yaliorembeka mazuri na matunda ya kuvutia, na kuitiisha kwa ajili ya kutuhudumia sisi kwa kuzalisha matunda ya kuvutia anuwai na yenye ladha mno mwishoni mwa matawi yake ambayo ndio mikono yake ya kupendeza, na kutuwezesha uvunaji wa asali tamu, ambayo ndani yake kuna ponyo kwa watu, kutokana na kidudu chenye sumu, na kutuvika mavazi mazuri mno na laini mno kutokana na anachokishona mdudu asiyekuwa na mkono, na kutuwekea hazina kubwa ya rehema katika mbegu ndogo sana, yote haya yanatuonesha kwa uwazi kwamba ni ukarimu katika upeo wa uzuri, na huruma katika upeo wa upole. Na kama hivyo, hakika jitihada za viumbe vyote, vidogo na vikubwa, ukimtoa mwanaadamu na wanyama, kwa ajili ya kutimiza nyadhifa zake kwa mpangilio timamu na uangalizi kamili kuanzia kwenye jua, mwezi, na ardhi, hadi kiumbe mdogo kabisa, kwa namna ambayo havuki kiumbe yeyote mpaka wake japo kiasi cha ncha ya kidole, ndani ya utiifu uliotimia na kufuata kuliko kamili vilivyozungukwa na heshima kubwa, ni dhahiri kwetu kwamba viumbe hivi havitikisiki wala havitulii ila kwa amri ya mkuu mwenye nguvu na mtukufu. Na kama hivi, hakika uangalizi wa kina mama kwa watoto wao dhaifu wenye hali ya kushindwa sawa iwe katika mimea, au katika wanyama au wanadamu uangalizi uliojawa na huruma na upole, na kulishwa kwake kwa chakula kizuri chenye kulika kutokana na maziwa, itakuonyesha ukubwa wa madhihirisho, na ukunjufu wa rehema isiyo na ukomo. Basi muda wa kuwa bwana mlezi wa ulimwengu huu, na muendeshaji wake ana ukarimu huu mkunjufu, na rehema hii isiyo na ukomo, na utukufu na izza bila ukomo, na kwamba utukufu na enzi bila ukomo, vinahitajia kuwatia adabu wenye kudharau, na ukarimu mkunjufu usio na ukomo unahitajia kukirimu kusikomalizika, na rehema ambayo imekienea kila kitu, inalazimu hisani inayowiana nayo, wakati ambapo havipatikani vyote hivyo katika dunia hii ya kutoweka, na umri mfupi isipokuwa sehemu ndogo mno, ambayo ni kama tone baharini. Basi hapana budi kwa hiyo kuwepo nyumba ya furaha inayowiana na ukarimu wenye kuenea, na kuenda sawa na rehema ile kunjufu, kama si hivyo italazimu kukanusha rehema hii yenye kushuhudiwa, ambapo pia ni kama kukana kuwepo kwa jua ambalo linajaza mchana mwanga wake, kwa sababu kutoweka ambako hakuna kurejea baada yake kunalazimu kukanushika kwa ukweli wa rehema kuwepo, kwa kule kubadili kwake huruma na kuwa msiba, na mahaba kuwa ni kitu chenye kuunguza, na neema kuwa balaa na ladha kuwa ni maumivu, na akili yenye kusifika kuwa ni kiungo kibaya. Kwa hoja hiyo, hapana budi kuwepo maisha ya malipo yanayonasibiana na utukufu ule na izza ile, na kuwa sawa nayo kwa sababu mara nyingi dhalimu hubaki katika ushindi wake, na mdhulumiwa akiwa katika udhalili wake na unyenyekevu, kisha wanaondoka katika hali zao hizo mbili bila adhabu wala thawabu. Kwa hiyo mambo sio kama yamepuuzwa katu, japo yamepewa muda kwa ajili ya mahakama kubwa, kadhia haijapuuzwa wala haitapuuzwa, bali inaweza kuharakishwa adhabu hapa duniani, kwani kuteremshwa kwa adhabu katika nyumati zilizopita, kwa watu waliyoasi inatubainishia kwamba mwanaadamu hajaachwa huru kama mnyama aende kokote kulingana na yanavyomuagiza matamanio yake, bali huwekwa daima mbele ya vipigo vya Mwenye izza na Al-Jalaal (Mwenye utukufu). Naam, mwanaadamu huyu kwa hakika aliyebebeshwa majukumu makubwa kati ya viumbe, na ametunukiwa utayari wa kimaumbile ulio kamili, kama hatamjua Mola wake kwa imani baada ya kuwa Allah (s.w) amejitambulisha kwa viumbe vyake vizuri vilivyopambika, na kama hakupata mapenzi yake kwa kujikurubisha kwake kwa (ibada) baada ya Allah (s.w) kujipendekeza kwake kwa nafsi yake na kujijulisha kwake kwa vile alivyomuumbia katika matunda ya aina kwa aina yalio mazuri yenye kujulisha juu ya rehema yake pana, na kama hajasimama kwa kumtukuza na kuadhimisha sifa zenye kuendana naye (kwa kuhimidi na kushukuru) baada ya Allah kuonesha mapenzi yake na rehema yake kwake kwa kwa neema zake nyingi, naam, kama mwanaadamu huyu hajamjua Mola wake kwa namna hii, basi vipi ataachwa burebure tu, bila malipo! Na bila Allah (s.w), Mwenye izza na Al-Jalaal kumuandalia nyumba ya adhabu! Na je ni katika yanayoyumkinika kwamba asitunuku huyu Mola mlezi Mwingi wa rehema, makao ya thawabu na furaha ya milele, kwa wale waumini ambao utambulisho wa dhati yake Allah (s.w) walikabiliana nao kwa kumjua kupitia (imani), na mahaba yake kwao kwa mapenzi, na kujipendekeza kwake kwa ibada, na rehema yake kwao wameipokea kwa kutukuza, na kutaka kuheshimiwa kwake kwa kumshukuru?
Mlango wa hekima na uadilifu na kulidhihirisha jina la “الْحَكِيْمُ na الْعَادِلُ. Je, inayumkinika kwa Muumba ambaye mwenye utukufu, aliyedhihirisha ufalme wa uungu wake wa kuwa bwana mlezi kwa kuendesha kanuni ya uwepo kuanzia chembe ya atomu (chembe ndogo kabisa katika vipimo) mpaka kuishia sayari, kwa upeo wa hekima na mpangilio, na kwa ukomo wa uadilifu na mizani, kuwa asiwatendee hisani wale waliojihami kwa hiyo rububiyya yake, na wakafuata hekima hiyo na uadilifu, na asiwalipe wale walioasi kwa ukafiri wao, na kuchupa kwao mipaka juu ya hekima hiyo na uadilifu? Kwa kuwa mwanaadamu hapati anachostahiki katika thawabu na adhabu katika uhai huu wa kutoweka, kwa namna ambayo inayolingana na hekima ile na uadilifu ule isipokuwa kwa nadra sana! Bali inaakhirishwa na waliyo wengi katika wale wapotevu huondoka bila ya kupata adhabu zao, na wengi ya watu wa uongofu wanaondoka bila ya kupata thawabu zao, basi hapana budi kadhia hii ikabidhiwe mahakama adilifu, na makutano yanayokomea katika furaha kuu. Naam, ni jambo lililo wazi kuwa anayetenda katika ulimwengu huu hakika anatenda kwa hekima isiyo na kikomo, je, unataka hoja juu ya hili? Basi tazama uchungaji wake Allah (s.w) masilahi na faida katika kila kitu! Hivi huoni kuwa viungo vyote vya mwanaadamu sawa vikiwa ni mifupa au mishipa na hata chembe ndogo mwilini ya kila sehemu katika viungo hivyo, na kila sehemu imezingatiwa ndani yake faida na hekima mbali mbali, bali katika viungo vya mwili wake kuna baadhi ya faida na siri, kwa kiasi cha vile mfano wa mti mmoja wenye matunda, katika mambo yanayojulisha kwamba mkono mmoja wa hekima unaendesha mambo, ukiachilia mbali mpangilio usio na kifani katika ufundi wa kila kitu, na nidhamu kamili ndani yake, ambao unajulisha kwamba mambo yanatekelezwa kwa hekima isiyo na mipaka. Naam, hakika kuwepo mpango uliokamilika wa waridi zuri ndani ya mbegu ndogo kimaumbile, na kuandikwa kwa ukurasa wa matendo ya mti mkubwa na faharisi ya maisha, pamoja na historia yake, katika mbegu yake kwa kalamu ya Qadar ya kimaana, inatubainishia kwa bayana kabisa kwamba kalamu ya hekima isiyo na mpaka ndio inavyoendesha mambo, na hivyo hivyo, uwepo wa mvuto wa ufundi mzuri na upeo wa uzuri wake, katika uumbwaji wa kila kitu, unadhihirisha kwamba fundi wake ni Mwingi wa hekima bila kikomo, huyo ndiye mwenye utengenezaji huu usio na kifani na mwenye nakshi hizi. Naam, hakika kuorodhesha faharisi ya viumbe vyote, na funguo zote za hazina za rehema na vioo vya majina mazuri yote, katika mwili huu mdogo wa mwanaadamu, hakika ni katika yanayojulisha hekima ya kikomo cha juu, katika utengenezaji usio na kifani, na je, ni katika mambo yanayoyumkinika kwa mfano wa hekima hii inayotawalia juu ya mfano wa taratibu hizi na mambo ya kiungu isiwatendee wema wale ambao waliotafuta kivuli chake na kunyenyekea kwake kwa imani, na asiwalipe thawabu ya kudumu milele kwa milele? Na je, unataka hoja juu ya utekelezaji wa matendo kwa uadilifu na mizani? Hakika kutunuku kila kitu uwepo kwa mizani nyeti, na kwa vipimo maalumu, na kuivika sura maalumu, na kuiweka katika mahali panapofaa, inabainisha kwa uwazi kuwa mambo yanakwenda kulingana na uadilifu, na mizani bila kikomo. Na kama hivyo, kumpa haki yake kila mwenye haki, kulingana na utayari wake na vipawa vyake, yaani kumpa kila kinacholazimu, na kilicho dharura katika kuwepo kwake, na kutoa vyote anavyohitaji kwa kubakia kwake kwa namna iliyo bora sana, inajulisha kwamba mkono wa uadilifu usio na mipaka ndio unaoendesha mambo. Na hivyo hivyo muitikio endelevu na wa kudumu kwa yanayoombwa kwa ulimi wa utayari au haja ya kimaumbile au kwa ulimi wa dharura inadhihirisha kuwa uadilifu usio na kikomo na hekima isiyo na kikomo, ndizo zinazozungusha gurudumu la uwepo. Sasa, je, uadilifu na hekima hii inawezekana kupuuzia haja hiyo kuu? Haja ya kubakia kwa kiumbe mwenye hadhi ya juu kabisa naye ni mwanaadamu? Wakati ambao hujibu haja ya chini mno ya kiumbe dhaifu mno? Na je, inayumkinika kukataa kile muhimu zaidi anachokitarajia mwanaadamu, na kikubwa zaidi anachokitamani, na zisilinde heshima ya rububiyya, na sifa hizo mbili zikengeuke kuitikia haki za waja? Isipokuwa mwanaadamu ambaye anaishi maisha mafupi katika dunia hii, hapati na kwa kweli hatapata uadilifu kama huu. Bali tu unacheleweshwa mpaka ifike kwenye mahakama kuu, mahakama ambayo inalazimu uadilifu wa kweli, mwanaadamu huyu mdogo akutane na thawabu zake na adhabu yake, sio kwa msingi wa udogo wake bali kwa msingi wa ukubwa wa kosa lake, na kwa msingi wa umuhimu wake, na kwa msingi wa ukubwa wa jukumu lake, na kwa kuwa dunia hii ni yenye kupita, iko mbali kwa kila hali ya umbali, kuwa iwe ndio mahali pa uadilifu huu na hekima kwa yanayomhusu mwanaadamu huyu mwanaadamu aliyeumbwa kwa ajili ya uhai wa milele, hapana budi kuwepo kwa pepo ya milele, na Jahannamu ya kudumu ya Mwadilifu الْجَليلُ (Mtukufu) ذُو الْجَمَالِ (Mmiliki wa uzuri wote) na ya الْحَكِيمُ (Mwingi wa hekima) الْجَمِيْلُ (Mzuri kuliko chochote) ذُو الْجَلَالِ (Mwenye utukufu).
Mlango wa ukarimu na mlango huu unadhihirisha jina la “الْجَوَادُ” na “ الجَمِيْلُ” Je, inayumkinika kwa wema na ukarimu bila kikomo, na utajiri na hazina zisizomaliza, na uzuri wa kimilele usio na mithili yake, na ukamilifu wa milele usio na upungufu, visitake nyumba ya furaha na mahali pa dhifa, hapo watakaa milele wahitaji wa ukarimu, wenye kushukuru, na wenye shauku ya uzuri wenye kupendezwa sana na uzuri huo? Kuupamba uso wa ulimwengu kwa hivi vilivyoundwa vizuri maridadi, na kujaalia jua kuwa ni taa na mwezi ni nuru, na utandazo wa ardhi ni karamu ya neema na kuijaza kwa vyakula vyenye ladha zaidi vya kutamanisha aina kwa aina, na miti kuifanya ni vyombo na sahani zinazonawiri upya kila msimu, vyote hivyo vinadhihirisha ukarimu na wema bila kikomo, ni lazima kwa mfano wa ukarimu huu na hazina hizi zisizokwisha, na mfano wa rehema hii ambayo imekienea kila kitu, viwe na nyumba ya dhifa ya kudumu, na mahali pa furaha ya kudumu, inayokusanya yale yanayotamaniwa na nafsi, na kupendezwa na macho na inalazimu moja kwa moja kuwa wanaoburudika kwa raha hizo wakae milele katika nyumba hiyo, na wasalie wakiwa wenye kuambatana na furaha hiyo ili wawe mbali na kutoweka na kutengana, kwani kama ilivyokuwa kutoweka kwa ladha ni maumivu basi kuondoka kwa maumivu ni ladha vile vile, basi ukarimu mithili ya huu, unakataa kabisa kuleta maudhi. Yaani, ni kuwa mambo yanahitajia uwepo kwa pepo ya milele, na kukaa milele humo wale wanaohitaji, kwa sababu wema na ukarimu usio na kikomo vinataka hisani na uneemeshaji bila kikomo, na hisani na uneemeshaji visivyokwisha, vinahitaji kukithirisha uneemeshaji na kukirimu visivyo na mwisho, na hii inalazimu kukaa milele yule anayestahiki kufanyiwa hisani, ili adhihirishe shukrani yake na kuneemeshwa kwake kwa kupokea kwake neema kwa kudumu, mbele ya kuneemeshwa huko kwa kudumu. Na kama si hivyo basi ladha ndogo, ambayo kutoweka na utengano huutibua katika kipindi hiki kifupi mno haviwezi kwenda sawa na wema huu na ukarimu. Kisha tazama maonesho ya pande za ulimwengu, ambayo hali inayoshuhudiwa katika yale yanayoshuhudiwa kwenye uundaji wa kiungu, na zingatia matangazo ya kiungu ambayo yanabebwa na mimea na wanyama juu ya uso wa ardhi. Na wasikilize walinganiaji wanaoelekeza mazuri ya kiungu na rububiyya na hao ni Manabii (as) na mawalii wema, namna ambavyo wanawaongoza watu wote ili kushuhudia ukamilifu wa ufundi wake usiyo na kifani na wanazindua watu waangalie huko. Kwa hiyo, fundi wa ulimwengu huu ana sifa ya ukamilifu wa hali ya juu adhimu sana unaochochea kupendwa, umejificha wa kujisitiri, anataka kuudhihirisha kwa hivi vilivyoundwa visivyo na kifani, kwani ukamilifu uliojificha ambao hauna upungufu ndani yake, unatakikana kuutangaza mbele ya macho ya watu hadharani, kwa mashahidi wenye kuthamini, kuhisi uzuri, na kupendezwa nao, na ukamilifu wa kudumu unahitajia kudhihiri daima, na hii pia kwa upande wake inahitajia kudumu kwa wanaohisi uzuri na wanaopendezwa nao, kwani mpendezwa ambae kusalia kwake hakudumu, hudondoka machoni pake thamani ya ukamilifu Kisha hivi viumbe vya ajabu visivyo kifani madhubuti vya kusisimua vyenye kuenea katika huu ulimwengu, vinajulisha waziwazi - kama ujulishaji wa mwanga wa mchana juu ya uwepo wa jua - kuwepo kwa mazuri ya uzuri wa kimaana usio na mithili, unakuonesha pia mazuri ya uzuri uliyojificha, ambao hauna mwenza, na kwamba kujitokeza kwa uzuri huo wa kushangaza uliotakasika, na huo uzuri wenye kung’ara mtakatifu unaashiria hazina nyingi, zilizojificha zilizopo katika majina mazuri ya Allah (s.w) bali katika kila jina mojawapo kati ya majina hayo. Na kama ambavyo uzuri huu uliojificha wa hali ya juu usio na mithili yake unavyotaka, kuona mazuri yake, katika kioo chenye kuakisi na kushuhudia vipimo vya uzuri wake katika kioo chenye hisia na shauku kwake, Yeye anataka kujitokeza ili aone uzuri wake upendwao pia kwa macho ya wengine, yaani kuutazama uzuri wake kunahitajia kuwe kwa pande mbili. Kwanza: Uzuri wenyewe kujishuhudia katika vioo vya aina tofauti, na upande mwingine kushuhudia uzuri kwa kutazama washuhudiaji wenye shauku wenye kupendezwa na kuhisi uzuri. Yaani kwamba uzuri na kupendeza vinalazimu kushuhudia na kushuhudiwa (kuona na kuonesha) na huku kushuhudia na kushuhudisha kunalazimu kuwepo wenye kushuhudia, wenye shauku wenye kuhisi uzuri wenye kupendezwa. Na ulivyokuwa uzuri na kupendeza ni vya kukaa milele, vinalazimu kukaa milele kwa wenye shauku na kudumu kwao, kwa kuwa uzuri wenye kudumu hauridhii mwenye shauku wa kutoweka anayepotea, kwa hiyo yule mwenye kushuhudia anayehisi kutoweka - na ameihukumia nafsi yake kutorejea katika maisha - yanabadilika mapenzi kwa kule tu kufikiria mawazoni mwake kutoweka kuwa uadui, na kupendezwa kwake kuwa dharau, na heshima yake kuwa kupuuza, kwa sababu mtu mbinafsi kama anavyofanyia uadui asichokijua hukifanyia uadui vile vile ambacho mkono wake haukifikii, basi hudhamiria uadui na chuki na kukanusha uzuri ule ambao unatakikana kupokelewa na yanayostahiki, miongoni mwa mahaba yasiyo na mwisho na shauku isiyo na upeo, na kupendezwa bila mpaka. Na kutokana na hili hufahamika siri ya kuwa kafiri ni adui wa Allah (s.w). Ukarimu huo ulipokuwa katika kutunuku kusikowekewa mipaka, na urembo huo katika uzuri ambao hauna mfanowe, na ukamilifu huo usio na kasoro ndani yake, kunalazimu kuishi milele kwa wenye kushukuru na kusalia hai wenye shauku, wenye kuhisi uzuri, nasi tunashuhudia safari ya kila mtu na kufichikana kwake haraka katika nyumba ya dhifa ya dunia hii, pasina kuburudika na hisani ya ukarimu ule isipokuwa sehemu kidogo ya kiasi cha kufungua hamu yake, na pasina kuona katika nuru ya uzuri ule na ukamilifu ule isipokuwa mpepeso wa mkupuo mmoja, hivyo safari inaelekea katika makazi ya milele na mambo yenye kushuhudiwa ya milele. Kwa ufupi: Kama ulivyo huu ulimwengu unavyojulisha kwa vilivyomo, kwa namna ya moja kwa moja yakini juu ya kuwepo muundaji wake, mkarimu mwenye utukufu, kwani sifa zake takatifu (s.w) na majina yake mazuri, vilevile yanajulisha juu ya maisha ya akhera bila shaka yoyote na kuyaonyesha bali yanalazimisha uwepo wake.
Mlango wa huruma na utumishi wa Muhammad (s.a.w) na hiyo inadhihirisha jina la “الْمُجِيْبُ na “الرَّحِيْمُ” Je, inawezekana kwa bwana mlezi, mwenye rehema kunjufu, na huruma isiyo na kikomo, aione shida yenye kujificha mno ya kiumbe kidogo kabisa, na kumsaidia kutokea upande usiotarajiwa kwa upole usio na kikomo, na rehema ilizoenea, na aisikie sauti ya chini kabisa ya kiumbe aliyefichikana zaidi, na amsaidie, na amuitikie kila muombaji kwa ulimi wa hali na kauli yake, je, inawezekana kwa mola huyu mlezi, asiwatimizie waja wake watukufu na vipenzi vyake katika waja wake, haja yao kuu, na wala asiwasaidie kwa yale wanayotaraji kutoka kwake? Kulea vyema wanyama wadogo na dhaifu, na kuwapa mahitaji ya maisha yao kwa wepesi, na upole dhahiri vinatuonesha kuwa mmiliki wa viumbe hivi anaviendesha kwa malezi yasio na mipaka katika huruma zake, basi haingii akilini kwa haya malezi yenye kusifika kwa ukamilifu wa huruma na upole kwamba yasiitikie dua nzuri kabisa ya mbora zaidi wa viumbe? Na kama nilivyobainisha ukweli huu (katika neno la kumi na tisa) ninarudia kulibainisha hapa. Basi ewe rafiki yangu ambaye anayenisikia pamoja na nafsi yangu! Tumeeleza katika kisa: Kwamba kuna mkutano kisiwani na kwamba mjumbe mtukufu anatoa hotuba huko, basi kilichoashiriwa na kisa hicho ni hiki: Basi njoo na tujikomboe kutokana na pingu za wakati, na twende kwa mawazo yetu hadi enzi za unabii, na maono yetu ya kufikirika hadi katika kisiwa hicho cha kiarabu, tupate bahati ya kumzuru Mtume (s.a.w) akishughulika na jukumu lake kwa ukamilifu wa utumishi wake, tazama! Namna alivyokuwa ni sababu ya furaha kutokana na ujumbe na mwongozo aliokuja nao, kwani yeye Mtume (s.a.w) ndiye anayeomba kuwepo kwa furaha hiyo, na kuumbwa kwa pepo kwa maombi yake na kwa utumishi wake. Mtazame huyu Mtume mkarimu anomba nini! Hakika anaomba furaha ya milele katika swala kuu yenye kukusanya kila kitu, na katika ibada ya hali ya juu inayojumuisha, hata kisiwa cha kiarabu, bali ardhi yote kana kwamba inaswali pamoja na swala yake, na kunyenyekea kwa Allah (s.w) kwa maombi, pamoja na unyenyekeaji wake mzuri. Hiyo ni kwa sababu utumishi wake Mtume (s.a.w) hujumuisha ndani yake utumishi wa umma wake wote, ambao waliomfuata kama inavyojumuisha - siri ya kuafikiana katika misingi - siri ya utumishi wa Manabii wote (as). Basi anaongoza swala kubwa akiwa imamu, uzuri ulioje wa swala hiyo, na anabembeleza kwa dua ya mabembelezo ya upole ulioje! katika tabia njema kabisa kana kwamba wale waliojipamba kwa nuru ya imani, tangu Adam (as) hadi sasa na hadi siku ya kiyama wamemfuata na kuitikia amin juu ya dua yake. Tazama namna anavyomuomba Allah (s.w) mahitaji ya jumla kama mahitaji ya kusalia na kuishi milele! Dua hii ambayo sio tu wakazi wa ardhini peke yao ndio wenye kushiriki dua hiyo, bali pia wakazi wa mbinguni, hapana, bali vyote vilivyomo vinasema kwa ulimi wa hali ya juu: Amin. Kwa dua yake “Ewe mola wetu mlezi, basi sisi tunatawassali kwako na tunanyenyekea kwako mfano wake.” Halafu tazama! Hakika anaomba furaha ile na kuishi milele, kwa upole na huzuni zote, na kwa mapenzi yote na kwa shauku yote na kwa msisitizo na unyenyekevu wote na matarajio, anauhuzunisha ulimwengu wote na kuuliza nao unashirikiana naye katika dua. Kisha tazama na chunguza! Anaomba dua akitaka furaha kwa makusudio makubwa na kwa ajili ya lengo la hadhi ya juu, anayaomba hayo ili amuokoe mwanaadamu na viumbe vyote kutokana na kuporomoka katika shimo chini ya walio chini na huko ndio kutoweka moja kwa moja na kupotea na kufanya mchezo, na kumnyanyua hadi nafasi ya juu ya waliyo juu na huko ni kunyanyuliwa na kusalia, na kubeba wajibu na kupokea majukumu, ili awe mwenye kufaa kwa nafasi hiyo, na kukwea katika ngazi ya maandishi ya kiungu. Tazama namna anavyotafuta msaada akiomba kwa kulia, hali ya kunyenyekea akitarajia kutoka kwenye kina cha moyo wake, akibembeleza kwa msisitizo, hata inakuwa kama vile anasikilizisha viumbe vyote, bali mbingu, bali arshi hivyo anavitetemesha kwa maombi yanayotawala moyo na kwa shauku ya kuomba kwake, na anawafanya warudierudie. Amin. Allahumma Amin. Na tazama, anaomba furaha na kusalia kwa milele, na anayatarajia hayo kutoka kwa Mweza wa kila jambo, Msikivu wa kila kitu, Mwingi wa ukarimu, na kutoka kwa Mjuzi wa kila kitu, anayeona kila kitu, Mwingi wa rehema, anaona na anasikia haja iliyojificha mno kutoka kwa kiumbe dhaifu mno, anaikidhi kwa huruma yake, na anaijibu hata iwe dua kwa ulimi wa hali. Naam, hakika anamuitikia kwa busara na rehema na kumpa msaada kwa hekima, jambo lenye kukanusha utata wowote kwamba uchungaji huo wa hali ya juu hautoki kwingine, ila kwa msikivu wa kila kitu mwenye kuona kila kitu, na kwamba uendeshaji ule madhubuti hautokei ila kwa Mkarimu sana, Mwingi wa rehema. Naam, hakika yule anayeongoza wanadamu wote katika ardhi hii kuelekea katika Arshi tukufu mno, hali akiwa amenyanyua mikono yake, akiomba dua yenye kukusanya ukweli wa utumishi wa (أحْمَدِيَّةٍ), ambao ni ufupisho wa utumishi wa wanadamu wote, yaonekana kuwa anataka nini? Anataka nini huyu ambaye ni utukufu wa ubinadamu wote, fahari ya viumbe wote, wa pekee katika zama zote, na baina viumbe vyote? Tumsikilize, hakika anaomba furaha ya milele kwake, na kwa uma wake, na kwamba anaomba kuishi milele katika nyumba ya kusalia, anaomba pepo na neema zake, naam, anaziomba na kutarajia, pamoja na hayo majina ya kiungu yenye kujidhihirisha kwa uzuri wake katika kioo cha viumbe, hakika anaomba shufaa kwa majina hayo mazuri kama uonavyo. Je, waonaje kama kusingekuwapo chochote katika sababu za kuwajibisha kuwepo kwa akhera, sababu zisizohesabika wala kujulikana jumla yake, na pia kusinge kuwapo chochote katika dalili za kuwepo kwa akhera, hivi si dua moja tu ya Mtume huyu mtukufu (s.a.w) ni sababu tosha ya kupatisha kwa pepo, ambayo ni nyepesi kwa uweza wa Muumba wetu Mwingi wa rehema kama wepesi wa kurejesha uhai katika ardhi ndani ya masiku ya machipuo? Naam, ambaye aliyejaalia utandazo wa ardhi katika majira ya machipuo kuwa ni mfano wa ufufuo, akaweka humo vielelezo mia moja katika vielelezo vyake kwa uweza wake usio na ukomo, vipi itakuwa vigumu juu yake kupatisha pepo? Kwa hiyo kama ulivyokuwa utume wake ni sababu ya kupatikana nyumba hii ya mtihani, na kuwa ni bayana na ufafanuzi wa siri ya (لَوْلَاكَ لَوْلَاكَ لَمَا خَلَقْتُ الْأَفْلَاكَ) basi utumishi wake vile vile umekuwa ni sababu ya kuumbwa nyumba hiyo ya furaha ya milele. Je, ni katika yanayoyumkinika uonavyo, kwa kupangika kwa ulimwengu mkubwa ambako kumetahayarisha akili na ufundi uliofanywa vema, na uzuri wa malezi yake yanayojumuisha katika eneo la rehema yake kunjufu, akubali ubaya mkubwa na dhulma mbaya kabisa, na ghasia yenye kuendelea urefu wake, kwa kutoitikia maombi hayo, yaani bila ya kuchunga na kusikia wala kutimiza matakwa yenye umuhimu mwingi zaidi, na yenye udharura mkubwa zaidi wakati ambapo anachunga kwa kutilia umuhimu wa hali wa juu yale matakwa mepesi na madogo, na anasikiliza sauti za chini mno na kidogo mno, na anamkidhia kila mwenye haja yake! Hapana, kisha hapana mara elfu, mfano wa uzuri huu unakataa kuvurugika, na hautakuwa mbaya. Basi Mtume (s.a.w) anafungua kwa utumishi wake mlango wa akhera kama alivyofungua kwa utume wake mlango wa dunia. عَلَيْهِ صَلَوَاتُ الرَّحْمٰنِ مِلْءَ الدُّنْيَا وَدَارِ الْجِنَانِ اَللّٰهُمَّ صَلِّ وَسَلِّمْ عَلٰى عَبْدِكَ وَرَسُولِكَ ذٰلِكَ الْحَبِيبِ الَّذِي هُوَ سَيِّدُ الْكَوْنَيْنِ وَفَخْرُ الْعَالَمَيْنِ وَحَيَاةُ الدّٰارَيْنِ وَوَسِيلَةُ السَّعَادَتَيْنِ وَذُو الْجَنَاحَيْنِ وَرَسُولُ الثَّقَلَيْنِ وَعَلٰى آلِهِ وَصَحْبِهِ اَجْمَعِينَ وَعَلٰى اِخْوٰانِهِ مِنَ النَّبِيِّينَ وَالْمُرْسَلِينَ آمِينَ
Mlango wa utukufu na umilele unadhihirisha jina la: الْجَلِيلُ na الْبَاقِي. Je, inawezekana kwa Mola mlezi mtukufu anayeendesha viumbe na kuvitiisha kuanzia wingi wa sayari zilizopo hadi miti na hadi dharra (chembe ndogo katika kipimo cha mizani), na vilivyo vidogo kabisa kuliko dharra, kana kwamba askari waliopangwa, ashindwe kueneza ufalme wake kwa masikini wanaotoweka wanapitisha uhai wa muda mfupi katika nyumba ya dhifa ya dunia hii, na asianzishe makao makuu ya kudumu milele na mahali panapozunguka ufalme wake mtukufu wa kubakia kwa ajili yake?! Kwani tunachoshuhudia katika ulimwengu huu miongoni mwa taratibu tukufu kubwa mfano kubadilika kwa majira, na katika matendo makubwa kama mfano wa kuendesha nyota, na katika utiishaji wa kushangaza mfano kuifanya ardhi kuwa ni kama tandiko, na jua kuwa ni taa, na katika migeuko mipana mfano kuhuisha ardhi na kuipamba baada ya ukame na kufa kwake, vinatubainishia kwa uwazi kwamba nyuma ya pazia kuna hali ya ubwana na utawala, mtukufu na mkubwa unaotawala, na kuendesha kwa mamlaka yake matukufu, basi mfano wa mamlaka haya ya kiungu yanalazimu raia wanaowiana nayo, na matukio yanayonasibiana nayo, wakati ambapo unaona ambao wanasifa bora kabisa za kipekee, na zenye kukusanya zaidi katika raia na waja wamekusanyika kwa muda mfupi, wameingia sana katika dhifa ya duniani, na mahali hapo penyewe panajazwa na kupakuliwa kila siku, na raia hawakai humo isipokuwa kwa kiasi cha kutimia jaribio la majukumu yao katika uwanja huu wa majaribio, na medani yenyewe inabadilika badilika kila saa moja, na raia wanasimama dakika chache ili kuona yaliopo katika maonesho ya soko la ulimwengu, katika vielelezo vya neema za thamani za Muumba mwenye utukufu, na wakitazama - kwa ajili ya biashara - ufundi wa pekee wa Allah (s.w), katika maonesho haya makubwa, na kutokea hapo wanapotea, na hayo maonesho yenyewe pia yanabadilika badilika kila dakika, basi anayesafiri harejei, na ajaye atasafiri tu, basi hali hii ni bayana waziwazi, na kwa namna ya moja kwa moja kwamba nyuma ya dhifa hii yenye kutoweka, na nyuma ya medani hii yenye kugeuka, na baada ya maonesho haya yenye kubadilika, kuna kasri za kudumu zinazowiana na ufalme wa kudumu milele, na makazi ya milele, yenye mabustani, na hazina zilizojaa asili halisi za hali ya juu kwa mifano tuionayo hapa duniani, hivyo jitihada ifaayo hapa ni kwa ajili ya kutazamia yale yalioko huko, na kutumia hapa ili kupokea ujira huko, hivyo kila mmoja atapata kulingana na maandalizi yake na jitihada yake atapata furaha tele kama hakuikosa. Naam ni muhali ufalme kama huu kubaki kwa hawa wenye kutoweka, madhalili, tazama ukweli huu kupitia uoni wa mfano huu: Naam, Jaalia unatembea njiani, na unashuhudia kuwa kuna (hoteli kubwa) ameijenga mfalme mkubwa kwa ajili ya wageni wake, na anatumia gharama kubwa kuipamba ili aingize furaha nyoyoni mwa wageni wake, na wazingatie kwa wanayoyaona, japo kuwa wageni hawavinjari isipokuwa kiasi kidogo katika mapambo yale, na hawaonji ila kiasi kidogo katika kidogo kutokana na neema zile, kwa kuwa hawakai ila muda mchache na hapo huiacha hoteli ile kabla hawajazima kiu wala kushiba, ukitoa kiasi wanachochukua miongoni mwa picha za vitu vilivyomo kwenye hoteli kwa zana za kunasa picha wanazomiliki, na kama hivyo ndivyo wafanyavyo wafanyakazi wa hoteli na wahudumu wake, ambapo wanachukua na kusajili michakato ya hawa wageni na kutulia kwao kwa umakini, na uaminifu wote, haya unaona kuwa mfalme kila siku huvunjavunja sehemu kubwa ya mapambo hayo ya thamani, na kuleta mengine mapya kwa ajili ya wageni wapya, hivi baada ya hivi itabakia shaka yoyote kwako kuhusu yule aliyejenga hoteli hii hapo kando mwa njia kuwa anamiliki kasri za kudumu za hali ya juu, na kwamba ana hazina zilizofurika za thamani zisizokwisha, na kwamba yeye ni mwenye ukarimu wa kudumu usiokatika, na kwamba alivyo navyo katika ukarimu kwenye hoteli hii ni kwa ajili ya kuchochea hamu ya wageni wake kwa vitu alivyo navyo, na kwa ajili ya kuamsha raghba zao na kuzishughulisha kwa ajili ya zawadi alizowaandalia? Kama utachunguza kupitia mfano huu wa hali za hoteli hii ya dunia, na kumakinisha kutazama katika hali hizo, kwa ufahamu timamu utafahamu misingi tisa ifuatayo: Msingi wa kwanza: Kwamba utafahamu kuwa hii dunia, inayoshabihiana na hoteli ile, sio kwa ajili yake yenyewe, ni muhali kujifanyia yenyewe sura kama hii na umbo hili, bali hiyo ni nyumba ya dhifa hujazwa na kupakuliwa, na mafikio ya kukaa na kusafirisafiri, imejengwa kwa hekima ya msafara wa viumbe. Msingi wa pili: Utafahamu kwamba wakazi wa hoteli hii ni wageni wasafiri, na kwamba Mola wao mlezi aliye Mkarimu sana anawaita katika nyumba ya salama. Msingi wa tatu: Utafahamu kuwa mapambo katika dunia hii sio kwa ajili ya kupata ladha na kustarehe tu, kwani inakuonjesha ladha kwa saa moja tu, na itakuonjesha maumivu ya kutengana nayo saa nyingi, itakuonjesha na kuichochea hamu yako bila ya kukushibisha, kwa sababu ya ufupi wa umri wake au kwa sababu ya ufupi wa umri wako, kwani hautoshi kushiba, kwa hiyo mapambo yenye thamani ghali, na yenye umri mfupi ni kwa ajili ya mazingatio, shukrani, na kwa ajili ya kuhimiza kufikia matumizi ya mashina yake ya kudumu, na kwa ajili ya makusudio ya juu mengineyo. Msingi wa nne: Utafahamu kuwa mapambo haya hapa duniani . ni mfano wa picha na vielelezo vya neema zilizowekezwa kama akiba mbele ya rehema za kiungu kwa ajili ya waumini huko peponi. Msingi wa tano: Utafahamu kuwa viumbe hivi vyenye kutoweka havipo kwa ajili ya kutoweka, na havikuumbwa ila vionekane kwa muda kisha viondoke vikipeperuka bila faida yoyote, lakini vimekusanyika hapa, na kushika nafasi yake itakiwayo, kwa muda mfupi ili ichukuliwe sura zake, zifahamike maana zake, matokeo yake yasajiliwe, na yasukwe mandhari ya milele ya daima na ziwe ni mahali pa duru ya malengo mengine katika ulimwengu wa kusalia milele. Na inafahamika kutoka katika mfano ufuatao namna vitu hivi kuwa havikuumbwa kwa ajili ya kutoweka bali kwa ajili ya kusalia milele, bali kule kutoweka kwa dhahiri si vingine bali ni kuachwa huru baada ya kwisha kukamilisha majukumu yake, na vipi kitu kinakwisha kwa upande mmoja na kubakia kwa pande nyingi nyingine: Zingatia hili ua, - nalo ni neno katika maneno ya uweza wa kiungu - linatuangalia likitabasamu kwa ajili yetu kwa muda mfupi, kisha linapotea nyuma ya pazia la kutoweka, ni kama neno ambalo tunalitamka ambalo hufikishwa maelfu ya maneno mfano wake kwenye masikio na kubakia maana yake kwa idadi ya akili zenye kuyasikiliza, na kuondoka baada ya kuwa yametekeleza jukumu lake, nalo ni kuleta maana, hivyo ua vile vile husafiri bada ya kuweka picha yake yenye kudhihiri katika kumbukumbu ya kila aliyeliona, na baada ya kuweka kiini chake cha kimaanawi ndani ya mbegu zake ndogo ndogo, kana kwamba kila kumbukumbu na kila mbegu ni sawa na picha za kuhifadhi uzuri wake, mapambo yake na mahali pa kudumisha kusalia kwake, basi ikiwa kilichotengenezwa, hali ya kuwa kiko katika ngazi ya chini kabisa katika ngazi za uhai, zinatendewa kama hivyo kwa ajili ya kubakia daima, basi hali itakuwaje kwa mwanaadamu ambaye yuko katika tabaka la juu zaidi miongoni mwa tabaka za uhai, na ambaye anamiliki roho inayobakia asiwe mwenye kufungamana na kusalia na kukaa milele? Kama ikiwa picha ya mmea uliobeba maua na matunda, na kanuni ya muundo wake inayoshabihiana kidogo na roho, imebakia na kuhifadhiwa kwa mpangilio wote ndani ya mbegu zake ndogo katika kukabiliana na mabadiliko mengi, hivi haifahamiki ni kiasi gani roho ya mwanaadamu inakuwa yenye kubaki na kiasi gani inakuwa imefungwa pamoja na umilele! Kwa kujua kwamba hiyo ni kanuni ya kiamri, na yenye hisia ya kinuru, inamiliki kiini cha daraja ya juu, yenye uhai, yenye sifa maalumu jumuishi na imevikwa uwepo wa nje? Msingi wa sita: Utafahamu kuwa mwanaadamu hakuachwa kamba yake hadi mwisho wake, na hakuachwa huru malisho kokote atakako, bali kazi zake zote zinasajiliwa na kuchukuliwa picha zake, na vitendo vyake vyote vinarekodiwa ili apate kuhesabiwa kwavyo. Msingi wa saba: Utafahamu kuwa umauti na kupukutika kunakotokea wakati wa mapukutiko, kunawasibu viumbe vizuri vya majira ya machipuo na ya joto, sio kutoweka moja kwa moja na kuondoshwa kwa milele, bali ni kusamehewa katika majukumu yake baada ya kuyakamilisha na kuyatekeleza, ni kuachia uwanja na kuacha nafasi kwa ajili ya vinavyokuja majira ya machipuo mapya, miongoni mwa viumbe vipya, ni maandalizi na matayarisho kwa viumbe vijavyo vyenye kuamrishwa na vipya, Nayo ni tanbihi ya kiungu, kwa wenye hisia, ambao mghafala umewasahaulisha majukumu yao na ulevi umewazuia kushukuru. Msingi wa nane: Utajua kuwa mtengenezaji wa milele, wa ulimwengu huu wenye kutoweka ana ulimwengu mwingine usio kuwa huu, nao ni ulimwengu wa kubakia na kudumu milele na anawatia shauku waja wake, Kwake, na kuwachungia kwake. Msingi wa tisa: Utajua kwamba Mwingi wa rehema mwenye kurehemu ambaye ni mtukufu, atawakirimu waja wake waliotakaswa kwa kuwapa vitu ambavyo hakuna jicho lililoona, na wala kusikiwa na sikio lolote, na wala kupita katika moyo wa binadamu, tumeamini.
Mlango wa hifadhi unadhihirisha jina la (الْحَفِيْظُ) na (الرَّقِيبُ). Je, inayumkinika kwa Mwingi wa kuhifadhi na mwangalizi mno wa viumbe ambaye anahifadhi kwa mpangilio na kwa vipimo vilivyomo mbinguni na ardhini, bara na baharini, kati ya vibichi na vikavu wala haachi kidogo wala kikubwa isipokuwa hukidhibiti hesabu yake yote, kwamba mwenye sifa hizo asihifadhi wala asiweke uangalifu katika amali za mwanaadamu ambaye anamiliki umbile la hali ya juu na anashika cheo cha ukhalifa katika ardhi, na anabeba jukumu la maana kuu, je, inawezekana kwamba asihifadhi matendo yake ambayo yanagusa rububiyya yake? Asiyatenge kwa kuyahesabu na kwamba asiyapime kwa uzani wa kuhesabu kwa uadilifu? Wala asimlipe jaza yake mtendaji kwa anayostahiki katika thawabu na adhabu? ametukuka Allah (s.w) utukufu mkubwa kabisa. Naam, hakika yule ambaye anayeendesha mambo ya ulimwengu huu ni yule ambaye anahifadhi kila kitu ndani yake kulingana na nidhamu na mizani, na nidhamu na mizani ni katika mambo mawili yanayoonyesha elimu na hekima pamoja na utashi na uweza, kwani huwa tunashuhudia kwamba kiumbe yeyote yule hakuumbwa wala haumbwi ila kwa upeo wa mpangilio na vipimo, na kwamba sura ambazo huzibadili katika muda wote wa uhai wake, zipo katika mpangilio madhubuti sana kama zilivyo jumla yake ziko katika mpangilio makini madhubuti. Pia tunaona kuwa Mwingi wa kuhifadhi mtukufu anahifadhi picha za kila kitu pale tu kinapomaliza umri wake sambamba na kumaliza jukumu lake na kusafiri kuondoka kutoka ulimwengu wa kushuhudiwa, Allah (s.w) anavihifadhi katika kumbukumbu zinazofanana sana na mbao zilizohifadhiwa, na katika hali inayofanana na vioo vya mfano, huandika kiasi kikubwa cha historia ya maisha yake katika mbegu zake na kuzitia nakshi katika matunda yake, hivyo kudumisha maisha yake na kuyahifadhi katika vioo vya dhahiri na vya siri, basi kumbukumbu za wanadamu, matunda ya mti, mbegu za matunda, mbegu za maua, vyote hivyo vinabainisha ukubwa wa kuzungukia vitu wa uhifadhi. Huoni namna kinavyohifadhiwa kila kitu chenye kubeba maua, na kuzaa matunda, katika majira mapana kunjufu ya machipuo, namna zinavyo hifadhiwa kurasa za amali zake zote zinazomhusu, na kanuni zote za muundo wake, na vielelezo vya picha zake, maandishi yanayowekwa kwenye idadi chache ya mbegu, hadi yanapowadia majira ya machipuo hukunjuliwa kurasa hizo kwa mujibu wa mahesabu madhubuti sana inayowiana nayo, basi huletwa ulimwenguni majira mazuri ya machipuo ya kuvutia katika ukomo wa mpangilio na uwekwaji vyema na sahihi, haya hayajulishi kiasi kwa utendekaji wa uhifadhi na uangalizi na kiasi cha kujumuisha kila kitu? Kama uhifadhi ni kwa ujumuisho wa kiasi hichi na ufundi, katika vitu visivyo na umuhimu na katika vitu vya muda vya kawaida, je, inaingia akilini kwamba amali za wanadamu zenye umuhimu mkubwa zisihifadhiwe ilhali zina matunda mazuri kwenye ulimwengu wa ghaibu na ulimwengu wa akhera na ulimwengu wa roho, na mbele ya mamlaka ya bwana mlezi yasiyo na mipaka? Je, inawezekana kuzipuuza na kutozisajili? Hasha lillah. Naam, inafahamika katika kudhihirika kwa uhifadhi huu, na kwa namna hii, iliyo wazi, kwamba mmiliki wa viumbe hivi ni mwenye kutoa umuhimu mkubwa katika usajili na uhifadhi wa kila kitu, na udhibiti wa kila kinachojiri katika mamlaka yake, anachunga sana utawala wake, na upeo wa kuchunga ufalme na malezi yake, kiasi kwamba anaandika kila tukio japo dogo sana na amali duni sana ya kuweza kupuuzwa kwa kutunza picha za mambo yote yanayotokea kwenye ufalme wake, kwenye kumbukumbu nyingi za kuhifadhia, aina hii ya uhifadhi madhubuti ni dalili kwamba hapana shaka yoyote kwamba litafunguliwa jalada la kuhesabiwa kwa matendo ya waja hasa kwa kiumbe huyu mkarimu aliyepewa heshima na aliyetunukiwa maumbile makuu ya kipekee, naye ni mwanaadamu, amali zake ambazo zina nafasi kubwa, muhimu katika mizani inayohisi kila chembe ya uzito, bila kusaza kitu na hesabu madhubuti, na hapana budi kukunjuliwa kurasa za matendo yake. Hivi unafikiri, kuna akili inayokubali kwamba mwanaadamu huyu ataachwa ambaye amepewa heshima ya khilafa na amana, na ambaye amepanda daraja hadi kufikia cheo cha kiongozi na shahidi juu ya viumbe wengine, kwa sababu ya kuingilia kwake mambo ya ibada ya viumbe walio wengi na tasbihati (nyiradi) zake kwa kutangaza tawhidi (upwekeshaji) katika nyanja za viumbe wengi, na kushuhudia mambo ya jumla yahusuyo bwana mlezi, basi itawezekana vipi mwanaadamu huyu aachwe, aende kaburini akalale kwa utulivu bila ya kuamshwa apate kuulizwa kuhusu kila alilotenda liwe dogo au kubwa, na bila kuchungwa akipelekwa katika uwanja wa mahshari ili ahukumiwe kwenye mahakama kuu? Kamwe hapana, kisha kamwe hapana! Mtu huyu atakwenda vipi katika hali ya kutokuwepo, na namna gani atafichikana kwenye udongo, na kuponyoka kutoka katika mkono wa mwenye uweza wa kila kitu, mwenye utukufu, ambaye matukio yote yanashuhudia kwamba hayo ni miujiza ya uweza wake, katika nyakati zilizopita, juu ya kuwa yeye anaweza mno kufanya yatakayotokea katika nyakati zijazo , uweza ambao unaleta majira ya baridi na majira ya machipuo, ambayo yanashabihiana na kutokea kwa kiama na ufufuo? Na mwanaadamu alipokuwa hahesabiwi katika dunia hii, basi lazima siku moja atakwenda katika mahakama kuiona furaha kuu.
Mlango wa ahadi na makamio unadhihirisha jina la “الْجَمِيلُ” na “الْجَليلُ”. Je, inawezekana kwa muanzilishi wa viumbe hivi na mjuzi asiye na kikomo na Mweza asiye na mpaka, kwamba asitekeleze ambayo Manabii wameyaeleza mara kwa mara, wote kwa tawaatur ikiwemo ahadi njema na makamio ya mabaya, na hayo pia kushuhudiwa na waja wa kweli, mawalii wote kwa ijmaa adhihirishe kwa kufanya hivyo, kushindwa na ujinga? Ameepukana Allah (s.w) na mambo kama hayo kuepukana kukubwa, hali ya kujulikana kwamba mambo aliyoyaahidi na kuyakemea sio mazito katika uweza wake kabisa, bali ni mepesi, kama ilivyokuwa wepesi kurejesha viumbe visivyohesabika vya majira ya machipuo yaliyotangulia, kama vilivyo au mfano wake , katika majira ya machipuo yajayo, ama kutekeleza ahadi kama ilivyo kuwa ni muhimu kwetu na kwa kila kitu, basi ni muhimu vile vile kwa ufalme wa rububiyya yake, kinyume na kuvunja ahadi ambapo ni dhidi ya utukufu na uweza wake usioshindwa na ujuzi wake wa kila kitu unakataa, kwani huku kuhalifu ahadi hakutokei ila kwa sababu ya ujinga au kushindwa. Ewe unayekanusha! je, unajua kiasi gani cha upumbavu wa makosa makubwa unayotenda kwa kufuru na kukanusha kwako! Unasadiki dhana zako za uongo na akili yako inayoweweseka na nafsi yako yenye kudanganya, na unamkadhibisha ambaye halazimiki kuhalifu ahadi yake hata kidogo, bali haiwiani kabisa kuhalifu ahadi na utukufu wake, na kwamba vitu vyote na vinavyoonekana vyote vinashuhudia ukweli wake! Kwa kufanya hivyo basi unatenda kosa kubwa lisilo na ukomo pamoja na kuwa mwili wako ni mdogo kupita kiasi, hakuna shaka kwamba unastahiki adhabu kubwa ya milele, na kupima kiwango cha kosa analotenda kafiri imepokewa hadithi kwamba jino la baadhi ya watu wa motoni ni kama mlima( . mfano wako ni kama msafiri anayetembea hali ya kuwa amefumba macho asione mwanga wa jua na anafuata mawazo yaliyo katika akili yake, halafu anataka aangazie njia yake kwa mwanga uliomo akilini mwake ambao ni mwanga hafifu kama mwanga wa kimulimuli (aina ya vipepeo warukao usiku na kutoa mwanga mwilini mwao). Maadamu Allah (s.w) ameahidi viumbe vyote vilivyopo ni maneno yake yanayosadikisha ukweli wake, na matukio haya ulimwenguni na ishara zake zinazotamka ukweli, kwamba atatekeleza ahadi yake bila kukosa, atafungua mahakama kuu na atatunuku furaha kuu.
Mlango wa kuhuisha na kufisha unadhihirisha jina la: “ الْحَيُّ الْقَيُّومُ na الْمُحْيِي na الْمُمِيْتُ” Je, inawezekana kwa ambaye tayari ameonesha uweza wake kwa kuhuisha ardhi baada ya mauti yake na kukauka, na kufufua zaidi ya viumbe mia tatu elfu, pamoja na kufufuliwa kila aina moja ya viumbe hivyo ni jambo la ajabu kama ajabu ya kufufuliwa kwa wanadamu, na ambaye ameonesha elimu yake iliyotanda juu ya viumbe kwa kumpambanua kila kiumbe kutokana na maingiliano na mchanganyiko mwingi, na ambaye ameelekeza macho ya waja wake wote katika furaha ya milele kwa kuwaahidi ufufuo katika amri zake zote za mbinguni, ambaye ameonesha ukuu wa uungu wake kwa sifa ya bwana mlezi kwa kufanya viumbe vyenye kushikamana na kuhurumiana akaviendesha ndani ya amri na matakwa yake, akiwatiisha na kuwafanya wasaidiane, ambaye amemtwika mwanaadamu umuhimu mkubwa kwa kumfanya ndio tunda linalojumuisha zaidi katika mti wa viumbe na mpole zaidi kuliko wote na wakujibiwa zaidi maombi, akitiishiwa kila kitu, na kumfanya msemeshwa, je, inawezekana kweli kwa mfano wa Mweza kama huyu Mwingi wa rehema, na kwa mjuzi wa kila kitu Mwingi wa hekima aliyempa mwanaadamu umuhimu huu yawezekana kwamba asilete kiama? Asilete ufufuo, au ashindwe kufanya hivyo? Ashindwe kufungua milango ya mahakama kuu, na kuumba pepo na moto? Ametakasika Allah (s.w) na upungufu huo utakatifu mkubwa. Naam, Mola mlezi anayetenda katika ulimwengu huu Jalla jalaaluh anaanzisha kila enzi, mwaka, na siku katika ulimwengu huu wa muda mfupi na finyu, anaanzisha vielelezo na mifano na ishara nyingi za ufufuo mkuu, kwa mfano: Siku chache za majira ya machipuo anafufua na kukusanya pamoja zaidi ya aina ya viumbe laki tatu ikiwemo mimea wanyama wadogo kwa wakubwa, anahuisha mashina ya miti na mimea, anarejesha baadhi ya wanyama na mifano ya baadhi ya wanyama hao pamoja na kuwa tofauti zilizopo katika mbegu ndogo ndogo, ni kidogo sana, lakini hufufuliwa na kurejeshewa uhai kwa utenganisho kamili, na kuunganishwa umbo kwa kasi ya kiwango cha juu, ndani ya siku saba au wiki sita, kwa upeo wa urahisi na wingi, na mpangilio kamili na vipimo madhubuti sana, pamoja na kuchanganyika kwake, je, itakuwa vigumu kwake kitu chochote huyu atendaye mambo haya! au ashindwe kuumba mbingu na ardhi ndani ya siku sita! Au ashindwe kumfufua mwanaadamu kwa ukelele mmoja tu? Ametakasika Allah (s.w) na hayo wamsifiayo. Je, unadhani kama kuna mwandishi mwenye maajabu ambaye anaandika vitabu maelfu kwa maelfu vikafutwa herufi zake kabisa, ndani ya ukurasa mmoja bila kuchanganyika, kusahau, wala upungufu wowote ule na kwa uzuri wa upeo wa juu, na kwamba anaviandika vyote ndani ya saa moja, halafu ukaambiwa kwamba, mwandishi huyu atakuandikia ndani ya dakika moja kutoka katika kumbukumbu yake kitabu chako kilichoingia kwenye maji ambacho kilitungwa na yeye, je, unaweza kumjibu kwa kumwambia kwamba hawezi. Si sadiki?! Au mfalme fulani mwenye kutenda miujiza ananyanyua milima na kuisagasaga na anabadili miji kiujumla, bahari huzigeuza kuwa nchi kavu, ikiwa ishara kutoka kwake kuonesha uwezo wake na kuifanya ni dalili kwa watu, wakati unaona kwake kazi hizi tahamaki jabali kubwa limeviringika katika bonde na kufunga njia kwa wageni wake, na ukaambiwa kwamba: Mfalme huyu ni lazima ataondosha jabali lile kutoka pale njiani, na kuliponda kabisa hata liwe kubwa kiasi gani, kwani hawezi kuwaacha wageni wake njiani, majibu yako yatakuwa ya wehu na kiwendawazimu kiasi gani kama utamjibu kwa kusema: “Hapana! Hawezi kufanya? Au kamanda anaweza kukusanya upya wanajeshi wa jeshi lake, ambalo yeye mwenyewe ndiye aliyeliunda jeshi hilo ndani ya siku moja, na kaambiwa kwamba kamanda huyo atakusanya wanajeshi wa vikosi vya jeshi hilo watajikusanya wote wale waliotawanyika chini ya bendera yake kwa mpulizo wa baragumu, halafu ukamjibu kuwa: Hapana, sisadiki! Hii itamaanisha kuwa ni kitendo cha wazimu, tena wazimu ulioje huo! Ukifahamu mifano hii mitatu basi zingatia huyo Muumba fundi wa kusawiri (s.w) ambaye anaandika mbele ya macho yetu kwa namna nzuri sana na iliyotimia zaidi kwa kutumia kalamu ya uweza, na Kadari zaidi ya sampuli mia tatu elfu juu ya ukurasa wa ardhi, akibadilisha ukurasa wa majira ya baridi yaliyo meupe na kuwa karatasi zilizo wazi kwa ajili ya majira ya machipuo na joto, anayaandika hali ya kuwa yameingiliana bila kuchanganyika, anayaandika bila msongamano wala kuvurugika, pamoja na kutofautiana kwake katika muundo na umbo, kamwe, haandiki kwa makosa, hivi inawezekana kuulizwa Muhifadhi wa kila kitu Mwingi wa hekima ambaye ameweka mpango na mwendo wa mti mkubwa ndani ya mbegu yenye udogo wa kupindukia akiuhifadhi, kuwa atahifadhi vipi roho za wafu? Itawezekana kweli aulizwe Mwenyezi Mweza mwenye utukufu ambaye huiendesha ardhi kwa kasi sana kwenye mzunguko wake, kwamba ataiondoshaje kutoka katika njia ya kuelekea akhera, na ataiangamizaje? Au je, itawezekana kuulizwa Muumba mwenye utukufu na kuneemesha, ambaye amevifanya kuwepo vijisehemu vidogo kutoka katika hali ya kutokuwepo, na ameviratibu vyema kwa amri ya:) (كُن فَيَكُونُ katika miili ya askari waliyo hai, na kutokana na kundi hilo akanzisha majeshi makubwa, vipi atakusanya kwa ukelele mmoja tu vijisehemu vile vya msingi, vilivyojuana na kuungana chini ya kikosi cha mwili na mpangilio wake? Sasa unaona mwenyewe kwa macho yako ni mifano, vielelezo, na ishara ngapi za ufufuo zinazoshabihiana na ufufuo wa majira ya machipuo, ameyatengeneza vema Muumba (s.w) katika kila majira, kila enzi, hata kule kubadilishwa usiku kwa mchana na kuanzishwa kwa mawingu mazito, na kuyamaliza yakatoweka huko angani hiyo ni mifano na alama za kuwepo kwa ufufuo. Na kama utawaza mwenyewe kwa mfano kabla ya miaka elfu moja hivi, na ukakutanisha kati ya pande mbili za wakati uliopita na ujao, utaona mifano ya ufufuo na kiama kwa idadi ya zama na siku, na kama utaona kufufuka kimwili ni jambo lisilowezekana kiakili, baada ya kuwa umeshuhudia kiasi hiki kikubwa cha mifano, basi utajua vile vile kiasi cha upumbavu wa mtu akanushaye ufufuo. Zingatia kanuni kuu inasema nini kuhusu ukweli huu: فَانْظُرْ اِلٰٓى آثَارِ رَحْمَتِ اللّٰهِ كَيْفَ يُحْيِي الْاَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا اِنَّ ذٰلِكَ لَمُحْيِي الْمَوْتٰى وَهُوَ عَلٰى كُلِّ شَىْءٍ قَد۪يرٌ Kwa ufupi: Hakuna chochote cha kuzuia kutokea kwa ufufuo, bali kila kitu kinahitajia na kulazimu kutokea ufufuo. Naam, yule ambaye anahuisha ardhi hii kubwa mno na kuifisha, nayo ni mahali pa maonesho ya maajabu, anaifisha kama mnyama duni kabisa na kujaalia jua kuwa ni taa na mwangaza kwa mahali hapa pa maisha ya wageni, na kufanya sayari na nyota zing’arazo ndio makazi ya ndege na malaika. Sifa ya uungu na malezi ya kudumu milele kwa kiasi hiki, na utawala wa kila kitu kwa mkuu kiasi hiki, havitulii wala kuishia katika mambo ya dunia, yenye sifa ya kutoweka, na dhalili yanayobadilika. Hapana budi kuwa kuna maisha ya kusalia, ya kudumu matukufu makuu ya kutulia, yanayowiana na Allah (s.w). Basi anatuongoza katika kufanya jitihada kubwa kuelekea katika falme hizo na makao hayo, anatuita kwenda huko na anatuhamasisha kwenda huko, wenye roho zenye nuru wanashuhudia haya, mihimili ya nyoyo yenye nuru na wenye akili za kiungu, ambao wamepenya kutoka nje ya mambo hadi kuzama ndani ya ukweli, na ambao wamepata utukufu wa kujikurubisha kwake (s.w), wanatufikishia habari hali ya kuwa wanaafikiana kwamba Allah (s.w) ameandaa thawabu na malipo, na kwamba anaahidi ahadi ya moja kwa moja na kukamia makamio ya moja kwa moja. Kuhalifu ahadi hakuwezi kukaribia utukufu uliotukuka wa Allah (s.w) kwani kufanya hivyo ni udhalili na kujidhalilisha, ama kuhalifu makamio hutokana na kusamehe na kushindwa, hali ya kuwa ukafiri ni kosa kubwa bila mipaka lisilostahiki msamaha, ama Mweza wa kila kitu ametakasika na sifa ya kushindwa, na kwamba wapasha habari na mashahidi ni kwamba wameafikiana kikamilifu juu ya msingi wa suala hili pamoja na kutofautiana masaliki, manhaji na masharibu zao (mapito, mbinu, mifumo na vyanzo vyao) kwa upande wa wingi wamefikia katika tawaatur na kwa upande wa aina wamefikia nguvu ya ijmaa. Na kwa upande wa cheo wao ni nyota wa wanadamu na viongozi wao, na watukufu mno wa watu, na vitulizo vya macho ya makundi ya watu wengi, na kuhusu umuhimu katika suala hili wao (ni watu wa kuhusika zaidi na watu wa ithibati) na inajulikana kuwa maamuzi ya wawili katika watu wa ikhtisas kwenye elimu fulani au tasnia fulani hupewa uzito dhidi ya maelfu ya kauli za wengine wasiokuwa na ubingwa katika nyanja hiyo, na katika kuelezea na kusimulia mapokezi hutiwa nguvu kauli ya wawili katika wanaothibitisha dhidi ya maelfu ya kauli za wenye kukanusha, kama katika kuthibitisha kuonekana kwa mwezi wa Ramadhani, ambapo mashahidi wawili wenye kuthibitisha hutiwa nguvu kauli yao, wakati maelfu ya kauli za wanaokanusha zinatupiliwa mbali. Na kwa ufupi: Hakuna habari ya kweli kuliko hii ulimwenguni, na hakuna kadhia yenye kusibu mno kuliko hii, na hakuna ukweli wa unaodhihiri wa wazi kuliko huu, basi dunia ni shamba bila shaka yoyote, na mahshari (ufufuo) ni mavuno, na pepo na moto ni ghala mbili.
Mlango wa hekima, uangalizi, rehema na uadilifu nao ni udhihirisho wa jina la “ الْحَكِيْمُ” na “الْكَرِيْمُ” na “الْعَادِلُ” na “الرَّحِيْمُ”. Inawezekana vipi kwa mmiliki wa ufalme mwenye utukufu aliyedhihirika wazi ndani ya hii nyumba ya wageni yenye kupita, na katika medani ya kupita hii ya mtihani, na katika ardhi hii ya maonesho yanayobadilika, ameonesha kiasi hiki cha athari za hekima zake kuu na kiasi hiki cha uangalizi wa dhahiri. Kiasi hiki cha uadilifu unaoteza nguvu zote, na kiasi hiki cha rehema kunjufu mno! Halafu asianzishe makazi na wakazi wa kudumu milele katika ufalme na utawala wake, na hadhi za kudumu na viumbe wa kudumu, hakika zote hizi zilizo wazi wazi za hekima na za uangalizi huu, uadilifu na huruma ziende bure bure kama vumbi lenye kupeperushwa na upepo? Je, inaingia akilini kwa Mwingi wa hekima mwenye utukufu aliyemchagua mwanaadamu kati ya viumbe, na kumfanya kuwa msemaji wake wa jumla, na kioo kinachojumuisha majina yake mazuri, na anaheshimu chemchemu za hazina zenye rehema zake, muonjaji na mtambuzi wake? Na ambaye Allah (s.w) ametambulisha dhati yake iliyokuwa tukufu kwake kwa majina yake yote mazuri, akampenda na kumpendezesha kwake. Hivi inaingia akilini baada ya yote hayo, kwamba Allah (s.w) Mwingi wa hekima asimtume mwanaadamu huyu masikini katika ufalme wa kudumu huko? Na asimpe maisha ya furaha katika nyumba hiyo ya furaha baada ya kuwa amemlingania kwenda huko? Au je, inaingia akilini abebeshe kila kilichomo ulimwenguni majukumu mengi, - kiwe kama chembe ndogo ya mbegu - kwa uzito wa mti, halafu kuwekwa juu yake hekima na makusudio kwa idadi ya maua yake, na kuibebesha maslahi kwa idadi ya matunda yake, kisha ajaalie malengo ya kuwepo kwa majukumu hayo, hekima na maslahi vyote ni kiasi hicho tu kidogo kinachoelekea duniani? Yaani ajaalie lengo la kuwepo ni kuishi duniani tu, maisha yasiyokuwa na umuhimu hata uzito wa chembe ya khardali? Na asijaalie majukumu, hekima na maslahi hayo kuwa ni mbegu za ulimwengu wa kimaana, na wala isiwe ni shamba la ulimwengu wa akhera ili malengo yake ya kweli yanayolingana yaweze kuzaa matunda huko. Na je, inaingia akilini matamasha yote haya yaondoke na mahafali makuu ya kupendeza, yakipotea bila lengo maalumu, na bure bila maana yoyote na kwa mchezo pasina hekima yoyote? Au inaingia akilini kweli vyote hivyo visielekezwe katika ulimwengu wa kimaana na ulimwengu wa akhera ili makusudio yake ya asili na matunda yake stahiki yakaonekane huko? Naam, je, inawezekana kweli, aoneshe vyote hivyo kinyume na ukweli ulivyo, kinyume na sifa zake takatifu na majina yake matukufu (Mwingi wa hekima Mkarimu sana Mwadilifu kuliko wote Mwingi wa rehema), hapana, kisha hapana. Je, inawezekana kweli Allah (s.w) akadhibishe ukweli wa viumbe vyote, unaojulisha juu ya sifa zake takatifu, ikiwemo wingi wa hekima, uadilifu na ukarimu na rehema, na kukataa ushahidi wa vyote vilivyomo ulimwenguni? Na abatilishe hoja za vyote vilivyoundwa, ametakasika Allah (s.w) na hayo utakatifu mkubwa kabisa! Je, akili inakubali kwamba ampe mwanaadamu ujira duni wa kidunia, uduni wa unywele mmoja, hali ya kuwa amembebesha dhamana na majukumu mengi, sawa na idadi ya nywele za kichwa chake? Je, inawezekana kutenda kazi kama hii isiyo na maana wala faida yoyote! na kwenda tofauti na uadilifu wake wa kweli, na kusigana na hekima yake ya kweli? Ametakasika Allah (s.w) utakatifu mkubwa na hayo wayasemayo. Inawezekana kwamba Allah (s.w), ambebeshe kila mwenye uhai, bali kila kiungo kilichopo ndani yake, kwa mfano ulimi, bali kila kilichoundwa, baadhi ya hekima na maslahi kwa idadi ya matunda ya kila mti, akionesha hekima yake isiyo na ukomo, halafu asimtunuku mwanaadamu kusalia na kudumu milele, na asimpe furaha ya milele ambayo ndiyo hekima kuu kuliko zote, na maslahi muhimu zaidi na matokeo ya lazima zaidi? Awe ameacha kubakia milele na kukutana na furaha ya milele, ambavyo vimefanya hekima kuwa ni hekima, na neema kuwa ni neema, na rehema kuwa ni rehema ya kweli, bali ndio chimbuko la hekima, maslahi, neema, na rehema na chemchemu yake. Hivi inawezekana aziache na kuzipuuza, na mambo yote hayo yaangukie katika shimo la upuuzi usio na ukomo? Na aiweke nafsi yake – ametakasika Allah (s.w) kutakasika kukubwa kabisa – katika nafasi ya anayejenga kasri kubwa anaweka katika kila jiwe katika kasri hilo maelfu ya nakshi na urembo, na katika kila pembe yake maelfu ya mapambo na kuweka uzuri, na katika kila chumba maelfu ya zana za thamani na mahitaji ya lazima, halafu asiijengee dari ya kuihifadhi?! Na aiache na aache kila kitu kioze na kiharibike! Hasha kwa Allah (s.w). Heri hutokea kutoka kwa heri isiyo na mipaka, na uzuri hutokea kwa mzuri asiye na mipaka, na kutoka kwa mwenye hekima isiyo na kikomo hakutokei upuuzi kabisa. Naam, kwa kila anayefuatilia historia, na kwenda kimawazo huko nyuma katika miaka mingi, ataona kuwa nyumba, maonesho na medani mbali mbali na limwengu zenye kushabihiana na nyumba ya dunia, na medani ya majaribu na maonesho ya vitu katika wakati wetu wa sasa. Pamoja na tofauti ionekanayo kati ya vitu hivyo kwa muonekano na sampuli ni vyenye kufanana katika kupangiliwa vema, kutengenezwa kwa namna ya ajabu na kudhihirisha uweza na hekima ya huyo fundi. Pia ataona vile vile - kama hajapoteza busara - kwamba katika nyumba hizo zenye kubadilika badilika, na katika medani hizo zenye kutoweka, na maonesho hayo ya kuisha, taratibu zilizo wazi za hekima, na ishara zilizo wazi wazi za uangalizi, na alama zenye nguvu na kushinda za uadilifu, na matunda makunjufu ya rehema ambapo atatambua yakini kuwa: Haiwezekani kuwepo hekima kamilifu zaidi kuliko hekima hiyo ionekanayo, na haiwezekani kuwepo uangalizi maridadi zaidi kuliko uangalizi huo unaoonekana athari zake, na haiwezekani kuwepo uadilifu mtukufu zaidi kuliko ambao alama zake zinaonekana, na haiwezekani kuwapo rehema ijumuishayo zaidi kuliko rehema hiyo ambayo matunda yake yanaonekana. Kama itakadiriwa jambo la muhali kutokea, nalo ni kwamba mfalme wa milele ambaye anaendesha mambo haya, na anayewabadili wageni hawa kwa hali ya kuendelea, hana nyumba za kudumu, wala maeneo ya hali ya juu, wala raia wa kudumu milele na makamo thabiti, wala makazi ya kubaki daima wala raia wa kudumu milele, watumishi wenye furaha katika ufalme wake wa kudumu, hapo italazimu kukanusha kweli nne. (Hekima, uadilifu, uangalizi, na rehema) ambazo ni viasili vya jumla vyenye nguvu, kama mwanga, hewa, maji, na udongo, na kukanusha uwepo wake wa wazi kama uwazi wa viasili hivyo, kwa sababu ni katika mambo yanayojulikana kwamba dunia hii na yaliyomo havitoshelezi kudhihiri kwa kweli hizo, kama kusingekuwapo mahali pengine panapostahiki, hapo itapasa kukanusha hekima hii iliyopo katika kila kitu kilichopo mbele yetu, - wazimu wa akanushaye uwepo wa jua ambalo mwanga wake umesheheni mchana wote - kukanusha uangalizi huu, ambao daima tunaushuhudia ndani ya nafsi zetu na katika chungu tele ya vitu, na kukanusha uadilifu huu dhahiri shahiri kwa ishara zake, na kukanusha rehema hii tuionayo kila mahala, kadhalika inalazimu kumzingatia muhusika wa haya tuyaonayo katika taratibu za uendeshaji mambo, zenye kufuata busara na matendo mema, na neema tele, (hasha lillah kisha hasha lillah) kwamba eti awe mwenye kufanya upuuzi, mwenye kucheza, dhalimu mwenye kuhini ahadi, Allah (s.w) ametakasika na hayo sana, haya ni mapinduzi ya hakika za mambo kuwa kinyume chake, na huu ni ukomo wa muhali, hata wafuasi wa (Usofisti) ambao hukanusha uwepo wa nafsi zao wenyewe hawakukaribia kabisa kufikiria muhali kama huu kwa wepesi. Na muhtasari: Hakuna uhusiano au mlingano kati ya haya yanayo shuhudiwa katika mambo ya ulimwenguni, ikiwemo mikusanyiko mikubwa ya maisha, na mitengano ya haraka ya umauti, na mijumuiko mikubwa na miparaganyiko ya haraka, na sherehe kubwa na mionekano ya kupendeza, na yanayojulikana nasi miongoni mwa matokeo madogo na malengo yasiyo na maana ya muda mfupi, na muda mfupi unaorejea katika dunia ya kumalizika, hivyo kufungamanisha kati ya mambo hayo kwa uhusiano wowote au mnasaba wowote, haikubaliani na akili yoyote, na wala haiafikiani na hekima yoyote, hiyo itakuwa kama kufungamanisha hekima kubwa na malengo makubwa kama milima, na changarawe ndogondogo mno, kufungamanisha lengo lisilo na kima chochote la muda mfupi kama ukubwa changarawe, na malengo sawa na mlima mkubwa!! Yaani kukosekana kwa uhusiano huo, kati ya viumbe hivi na mambo yake na kati ya shabaha zake zinazorejea duniani, kunashuhudia kwa ushahidi wenye nguvu na ni dalili ya wazi kuwa viumbe hivi vinaelekea katika ulimwengu wa kimaana, ambako huko vitatoa matunda yake mema yanayo lingana nayo. Na kwamba macho yake yanachungulia katika majina mazuri, na shabaha zake zinaelekea kwenye ulimwengu huo, pamoja na kuwa mbegu zake zinafichikana chini ya udongo wa dunia ila mashuke yake yatachomoza katika ulimwengu wa mfano. Kwa hiyo mwanaadamu, kulingana na utayari wake analima hapa na anavuna huko akhera. Ndiyo, lau ungetazama nyuso za viumbe zinazoelekea kwenye majina mazuri na katika ulimwengu wa akhera, ungeona kwamba kila mbegu moja, na huu ni muujiza wa Qudura ya kiungu, ina malengo makubwa sawa na ukubwa wa mti, na kwamba kila ua moja nalo ni neno la hekima lina maana tele kwa kiasi cha maua ya mti, na kila tunda, na huo ni muujiza wa ufundi na kasida ya rehema, lina kiasi cha hekima zile zilizomo kwenye mti wenyewe, na ama kwa upande wa kuwa hizo ni riziki zetu, hiyo ni hekima moja kati ya maelfu ya hekima, pale ambapo hutimiza majukumu yake hufa na kuzikwa kwenye matumbo yetu. Maadamu vitu hivi vya kutoweka hutoa matunda yake mahali pengine pasipokuwa hapa, na kuacha picha za kudumu kuelezea maana za kudumu, na kuleta dhikri na tasbihi zake za kudumu milele huko, hivyo basi mwanaadamu huwa mwanaadamu wa ukweli muda wa kuwa anatazama, na kuzingatia nyuso hizo zinazoelekea katika maisha ya milele, na hapo anapata njia ya kutokea kwenye kutoweka na kuwa wa kudumu. Hivyo kuna kusudi lingine kati ya viumbe hivi vyenye kukusanyika, na kutawanyika katika kuhudumia uhai na umauti, kwani hali zake hurandana, - na samahani katika kupiga mifano - hali mbali mbali zinazopangiliwa, kwa ajili ya kufanya tamthilia, kwa hiyo hufanywa matumizi makubwa kwa ajili ya kuandaa mikusanyiko na mitawanyiko mifupi, kwa ajili ya kuchukua picha ili kuweza kuzionesha kwenye kioo cha televisheni kwa maonesho ya kudumu. Kama hivyo moja ya malengo ya kumaliza maisha ya binafsi na ya kijamii, ndani ya muda mfupi hapa duniani, ni kuchukua picha na kuziratibu, na kuhifadhi matokeo ya matendo yapate kuhesabiwa katika mkusanyiko mkuu, na ili yaoneshwe mbele ya onesho kuu kabisa, na ili kuweka sawa utayari wake na vipawa vyake kwa ajili ya furaha kuu. Basi hadithi tukufu inasema: (Dunia ni shamba la akhera) inaelezea ukweli huu. Kwa kuwa dunia ni hakika ipo, na humo kuna athari za wazi za hekima, uangalizi, rehema, na uadilifu basi akhera lazima ipo, na ni jambo lililothibiti kwa uthabiti wa kuwepo kwa dunia yenyewe, na ilivyokuwa kila kitu katika dunia hii kinatazamia upande wa ulimwengu huo, kwa hiyo kwenda na safari ni kuelekea huko, kwa hiyo basi kukanusha kuwepo kwa akhera, ni sawa na kukanusha dunia na vilivyomo, kama ilivyokuwa ajali na kaburi vinamsubiri mwanaadamu, basi pepo na moto vivyo hivyo vinamsubiri na kumngojea.
Mlango wa ubinadamu unadhihirisha jina la (الْحَقُّ) Je, inawezekana kwa Allah (s.w) ambaye ni mtenda haki tupu, naye ndiye mwaabudiwa wa kweli Kumuumba mwanaadamu huyu, ili awe mja mtukufu mno kwa rububiyya yake isio na ukomo, na muhimu sana kwa malezi yake ya kiujumla kwa walimwengu wote, na muelewa zaidi kati ya wanaosomeshwa na kufahamu amri zake za utakatifu, aliye katika umbo bora mno hata amekuwa ni kioo kilichokusanya majina yake mazuri, na ili kudhihirisha jina lake kuu na ili kudhihirisha daraja kuu ya jina katika majina haya mazuri, na ili apate kuwa ni muujiza mzuri zaidi kati ya miujiza ya uweza wa kiungu, na tajiri zaidi kwa zana na vipimo, ili kujua na kukadiria vile vilivyomo katika hazina za rehema za kiungu, na ni kiumbe mwenye mahitajio mengi zaidi kuliko wote kwa neema zisizodhibitika jumla yake, na mwenye kuumia zaidi na hali ya kutoweka na mwenye shauku zaidi ya kubakia daima, ni mpole na fakiri zaidi pamoja na kuwa katika upande wa maisha ya dunia, ni mwenye kuangamia zaidi, na kwa upande wa maandalizi ya kimaumbile ni mwenye umbo la hali ya juu zaidi, je, muabudiwa wa haki inawezekana akaumba mwanaadamu kwa wasifu huu kisha asimpeleke katika hali iliyo mnasaba na yeye aliyoandaliwa kwayo na kuwa na shauku nayo katika maisha ya milele?! Na akafuta hakika ya kibinadamu, na afanye jambo linalopingana kabisa na sifa yake Allah (s.w) ya kuwa ni mtenda haki tupu? ametakasika Allah (s.w) na sifa hiyo kabisa! Na je, inakubalika akilini kwa mwenye kuhukumu kwa haki, na mwenye huruma isiyo na kikomo ambaye amemtunuku mwanaadamu huyu maandalizi ya kimaumbile ya hali ya juu, yanayomwezesha kubeba jukumu kuu, ambalo mbingu na radhi na milima vimekataa kulibeba jukumu hilo, yaani alimuumba ili azijue sifa za Muumba wake za jumla, zenye kuzungukia pande zote na mambo yake ya jumla, na madhihirisho yake yasiyo na ukomo, kwa vipimo vyake vidogo, na kwa stadi zake ndogo, na ambaye alimuumba akiwa kiumbe laini zaidi, na mshindwa (dhaifu) mno na mnyonge mno, na viumbe vyote amevitiisha kwa ajili yake, ikiwemo mimea, na wanyama, hata akampa hadhi kuwa mwenye cheo, mpangilio na mwenye kuingilia aina za tasbihi (nyiradi) na ibada zao, na ambaye amemjaalia kuwa kielelezo kwa vipimo vilivyopunguzwa ukubwa wake, kwa ajili ya taratibu za uendeshaji wa mambo ya kiungu ulimwenguni, na mtangazaji wa ilani ya kiungu takatifu, kwa matendo na kauli kwa viumbe, hata akampa cheo kitukufu mno kuliko cheo cha malaika kwa kumnyanyua hadi kufikia ngazi ya ukhalifa, je, Allah (s.w) anaweza kutunuku mwanaadamu nyadhifa zote hizi halafu asimpe malengo yake na matokeo na matunda yake ambayo ni furaha ya milele? Na amtupe katika ngazi ya chini kabisa ya udhalili, msiba, na maradhi, na kumfanya kuwa ni kiumbe wake mteketevu zaidi? Na aifanye hii akili ambayo ni zawadi ya baraka ya nuru kwa hekima yake (s.w), na njia ya kujua furaha iwe ni zana ya kuadhibia na kuharibikiwa, kinyume na hekima yake isiyo na mipaka? Allah (s.w) ametakasika na sifa hiyo utakasifu mkubwa sana! Muhtasari: Kama tulivyoona kwenye kisa katika utambulisho wa afisa askari, na daftari la huduma yake na cheo chake, mshahara wake na matendo yake na zana zake, na ikabainika kwetu kwamba afisa yule hafanyi kwa ajili ya medani hii ya muda mfupi, bali kwa ajili ya medani atakayoisafiria yenye mambo kadhaa ya takrima, na kuneemeshwa kwenye ufalme uliotulia wa kudumu. Kadhalika yaliyomo katika utambulisho wa moyo wa mwanaadamu katika sifa maridadi na milango ya fahamu iliyomo kwenye daftari la kili yake, na zana na silaha zilizomo katika umbile lake, vyote vinaelekea kwa pamoja katika furaha ya milele, bali hakupewa hivyo ila kwa ajili ya furaha hiyo ya milele, na hili ni jambo ambalo wanaliafiki watu wa ujuzi wa hakika na kufunuliwa hali za kweli. Kwa mfano, kama uwezo wa kufikiri mambo ya mbali uliopo ndani ya mwanaadamu ungeambiwa - na huu ni moja ya njia za akili na moja ya vijenzi vya taswira - kuwa: Utapewa ufalme wa dunia na mapambo yake, pamoja na umri ambao unazidi miaka milioni moja, lakini mwisho wako ni kuisha na kutoweka kabisa, tutaiona inanung’unika na kusikitika, kwa kweli ni kwamba kikuu kabisa chenye sifa ya kutoweka - nayo ni dunia na vilivyomo - haiwezi kushibisha zana ndogo sana iliyopo kwa mwanaadamu, nayo ni uwezo wa kuwaza kwa taswira! Inabainika wazi kuwa mwanaadamu huyu mwenye maandalizi haya ya kimaumbile, na ambaye ana matarajio yanayoendelea mpaka milele, (dahari ya zama), na mawazo yanayozunguka ulimwengu, na matashi yanayoenea katikati ya aina mbali mbali za furaha za milele, mwanaadamu huyu alichoumbiwa ni maisha ya kudumu milele, na atasafiri kuelekea katika maisha hayo kwa vyovyote iwavyo, dunia hii si lolote isipokuwa ni makaribisho ya wageni kwa muda mchache na ukumbi wa kungojelea akhera.
Mlango wa Utume na uteremsho nao ni kudhihirika بِسْمِ الله الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ Je, inawezekana kwa mtu ambaye maneno yake yameungwa mkono na mawalii wote, na waja wema wote wenye kutiwa nguvu kwa ufunuo wao na karama zao, na wanazuoni wote wakashuhudia ukweli wake na wateule wanaotegemea umakini wa ujuzi wao, na uhakiki wa taarifa zao, na huyo ni Mtume mtukufu (s.a.w), ambaye kwa nguvu aliyopewa amefungua njia ya akhera na mlango wa pepo, akisadikishwa kwa miujiza yake elfu moja iliyothibiti na kwa maelfu ya aya za Qur’an tukufu, ambayo imethibiti kuwa ni muujiza kwa namna arobaini je, inawezekana kwa dhana zilizo dhaifu kuliko ubawa wa nzi kufunga njia, ambayo Mtume mtukufu (s.a.w) ameifungua kuelekea akhera na mlango wa pepo? * * * Vile vile imefahamika katika kweli zilizotangulia kwamba suala la ufufuo ni hakika iliyothibiti na kujikita kwa nguvu, kiasi hakuna nguvu yoyote iwezayo kuyumbisha ukweli huo vyovyote iwavyo, hata ikiwa na uwezo wa kusogeza mviringo wa ardhi na kuuvunja vunja kabisa, hii ni kwa sababu kwamba Allah (s.w) anakiri ukweli huo kupitia majina yake mazuri yote na sifa zake tukufu zote, na kwamba Mtume wake mtukufu anasadikisha kweli hizo kwa miujiza yake na hoja zake zote, na Qur’an tukufu inathibitisha hilo kwa aya zake zote na maelezo yake. Na ulimwengu unashuhudilia hilo kwa ishara zake zote za kimaumbile, na mambo yake yenye kwenda kwa hekima. Unafikiri inawezekana viumbe vyote viafikiane na Muumba ambaye ni Mwenye sifa ya ulazima wa kuwepo - ukitoa makafiri - juu ya ukweli wa ufufuo. Halafu utata wa kishetani dhaifu uje uyumbishe ukweli huu uliyojikita madhubuti? Hapana, kisha tena hapana. Wala msifikiri kuwa dalili za hashri (ufufuo) zinaishia katika kweli hizo kumi na mbili tulizozijadili, bali kama ilivyo Qur’an tukufu pekee inavyotufundisha kweli hizo, vile vile inaashiria kwa maelfu ya namna na alama zenye nguvu, kwamba Muumba wetu atatuhamisha kutoka ulimwengu wa kuisha na kwenda maisha ya kusalia milele. Wala usifikiri kuwa dalili za ufufuo ni zile tu tulizojadili, katika mahitajio ya lazima ya majina ya Allah (s.w), yaliyo mazuri (Mwingi wa hekima, Mkarimu sana, Mwingi wa rehema, Mwadilifu, Muhifadhi bora kabisa wa kila kitu). Bali majina yote mazuri yenye kudhihiri katika uendeshaji wa ulimwengu, yanahitajia na kulazimu kuwepo kwa akhera. Na usifikiri kwamba dalili za ulimwengu zinazojulisha ufufuo ni zile tulizo zitaja tu. Bali kuna upeo na namna katika viumbe vingi mno vinavyofunguka na kuelekea kulia na kushoto. Kama namna moja inavyoashiria na kutoa ushahidi juu ya fundi muundaji Allah (s.w), namna nyingine inatoa ishara ya kuwepo kwa ufufuo. Kwa mfano: Ufundi mwema uliopo katika kuumbwa kwa mwanaadamu katika umbo lililo bora kabisa, kama ilivyo hii ni ishara ya fundi (s.w). Ndani yake kuna sifa zinazokubali na nguvu za jumla zinazotoweka katika muda mdogo, zinaashiria ufufuo, kiasi kama utaangaliwa upande mmoja tu kwa mara mbili basi unajulisha juu ya fundi na ufufuo kwa pamoja. Kwa mfano: Kama itaangaliwa hali iliyo bayana katika vitu vingi, ikiwemo mpangilio wa hekima, na mapambo ya uangalizi na makadirio ya uadilifu, na upole wa rehema hubainisha kuwa vinatokana na mkono wa Qudura ya fundi bora kabisa, kuliko wote Mwingi wa hekima, mkarimu bila ukomo Mwadilifu kuliko wote, Mwingi wa rehema pia, kama utaangaliwa utukufu wa sifa hizi na nguvu zake na ukunjufu wake, pamoja na ufupi wa uhai wa viumbe hivi hapa duniani, na uduni wake kupitia hivyo hubainika akhera, yaani kila kitu kinatamka kwa ulimi wa hali kwa kusema: آمَنْتُ بِاللهِ وَبِالْيَوْمِ الآخِرَةِ
Kweli kumi na mbili zilizopita zinaungana mkono zenyewe kwa zenyewe na zinakamilishana na kutegemeana na kutiana nguvu, na matokeo yanabainika kwa ujumla wake na kuungana kwake pamoja, ni dhana ya aina gani iwezayo kupenya katika kuta hizi kumi na mbili madhubuti sana za chuma, bali za almasi imara zenye kuzuia, hata iweze kuyumbisha imani ya ufufuo iliyolindwa kwenye ngome madhubuti? Aya inasema: مَا خَلْقُكُمْ وَلَا بَعْثُكُمْ اِلَّا كَنَفْسٍ وَاحِدَةٍ Inamaanisha kuwa kuumba wanadamu na kufufuka kwao ni jambo jepesi juu ya uweza wa kiungu, kama kumuumba mwanaadamu mmoja na kumfufua. Naam, iko hivyo kama ilivyofafanuliwa katika mjadala wa (ufufuo) katika ujumbe wa (Nukta ya nuru ya kumjua Allah Jalla jalaaluh) isipokuwa hapa tutaashiria ufupisho wake, pamoja na kutaja mifano na mwenye kutaka maelezo zaidi na arejee ujumbe huo. Kwa mfano: وَللهِ الْمَثَلُ الأَعْلَى - na hakuna mabishano katika mifano - jua kama linavyopeleka - japo kwa kutaka - mwanga wake kwa wepesi kamili kwenda kwenye chembe moja, ndio kabisa huupeleka mwanga huo kwa wepesi uleule kwenda kwenye maada angavu, kwa idadi isiyo na kikomo, na hii ni kwa siri ya sifa ya hali ya (kinuru). Na kuchukua kwa chembe ndogo angavu ya maji kwa sura ya jua, ni sawa na kuchukua uso mpana wa bahari kwa nuru ya jua hilo, na hii ni kwa siri ya sifa ya (uangavu). Na mtoto, kama awezavyo kutikisa mwana sesele wake shabihi ya jahazi ndivyo awezavyo pia kutikisa jahazi la kweli, na hii ni kwa siri ya (mpangilio) uliopo. Na kwamba kamanda anayeendesha askari mmoja kwa amri ya kusema “tembea” anaendesha jeshi zima kwa amri hiyo hiyo. Na hii ni kwa siri ya (kufuata na utii). Kama tutafikiria kimawazo tu kuwepo kwa mizani nyeti yenye hisia kali huko angani, kiasi cha kuhisi uzito wa jozi ndogo, wakati huo pia yawezekana kuwekwa katika viganja vyake jua moja upande wa kulia, na jua moja upande wa kushoto wa viganja hivyo, na katika viganja hivyo viwili kukawa na jozi mbili na majua mawili, hapo nguvu itakayotumika katika kuinua moja ya viganja hivyo viwili kwenda juu na kingine kuelekea chini ni nguvu ileile, na hii ni kwa siri ya (mizania). Maadamu kitu kikubwa kabisa kinalingana na kidogo kabisa, na vitu visivyo hesabika vinaonekana kama kitu kimoja katika viumbe hivi, na viwezekanavyo vya kikawaida, - hali ya kuwa ni vyenye upungufu sifa ya kutoweka - kwa sifa zilizomo za (kinuru, Uangavu, mpangilio, kufuata na utiifu, na mizania) basi hapana budi vitakuwa sawa mbele ya Mweza wa kila kitu vilivyo vichache na vingi, kidogo na kikubwa, na kumfufua mtu mmoja na watu wote kwa ukelele mmoja tu, na hii ni kwa madhihirisho ya (kinuru) yasiyo na kikomo ya uweza wake wa kidhati usio na kikomo, na yenye upeo wa ukamilifu, na (uangavu), na (hali ya kinuru) katika udhibiti wa kifalme wa vitu vyote na (mpangilio) wa hekima na uweza (na ufuasi na utii) wa viumbe wote kwa amri zake za kimaumbile, kwa namna iliyo kamili kabisa na kwa siri ya (mizania) ya uwezekano wa kuwa, ambao ni kule kuwa sawa kwa viumbe vyote vyenye kuwezekana katika kuwepo na kutokuwepo. Kisha ngazi za nguvu na udhaifu kwa kitu fulani ni kwa kuzingatia muingiliano wa dhidi yake ndani ya kitu hicho, nyuzi joto mathalani hutokana na kuingilia kwa ubaridi, na viwango vya uzuri vinatokana na kuingiliana na ubaya, na matabaka ya mwanga hutokana na kuingia kwa giza, isipokuwa kitu kikiwa ni cha dhati yake na siyo tegemezi, dhidi yake haiwezekani kuingia ndani yake, la sivyo italazimu kukusanyika dhidi mbili pamoja na hilo ni muhali, yaani hakuna viwango katika kitu cha dhati yake na uasilia, na kwa kuwa uweza usio na mipaka wa Mweza wa kila kitu ni wa kidhati, na sio tegemezi kama viumbe vyenye uwepo wa kuwezekana kuwa, ni katika ukamilifu wa kutokuwa na ukomo. Hivyo ni muhali kufikwa na hali ya kushindwa, ambayo ni kinyume cha uweza, yaani kuumba majira ya machipuo kwa Allah (s.w) mwenye utukufu kamili, kwake ni rahisi kama kuumba waridi moja na kufufua watu wote ni rahisi kama kumfufua mtu mmoja kati yao, tofauti na jambo hilo lingetegemezwa kwa sababu za kimaada hapo ingekuwa kuumba waridi moja ni vigumu kama kuumba majira yote ya machipuo. Na mifano yote iliyotangulia na fafanuzi tangu mwanzoni mwa sura za ufufuo, na hakika zake si mengine ila ni kutoka katika bahari ya Qur’an tukufu, na si kwa lengo lolote isipokuwa kuiandaa nafsi na moyo kusalimu amri na kukubali, kwani kauli yenye maamuzi ni Qur’an tukufu na maneno ni maneno yake. Tusikilize na Allah (s.w) ndiye Mwenye hoja yenye nguvu: فَلِلّٰهِ الْحُجَّةُ الْبَالِغَةُ فَانْظُرْ اِلٰٓى آثَارِ رَحْمَتِ اللّٰهِ كَيْفَ يُحْيِي الْاَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا اِنَّ ذٰلِكَ لَمُحْيِي الْمَوْتٰى وَهُوَ عَلٰى كُلِّ شَىْءٍ قَد۪يرٌ قَالَ مَنْ يُحْيِي الْعِظَامَ وَهِىَ رَم۪يمٌ ❀ قُلْ يُحْي۪يهَا الَّذ۪ٓي اَنْشَاَهَٓا اَوَّلَ مَرَّةٍ وَهُوَ بِكُلِّ خَلْقٍ عَل۪يمٌ ❀ يَٓا اَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمْ اِنَّ زَلْزَلَةَ السَّاعَةِ شَىْءٌ عَظ۪يمٌ يَوْمَ تَرَوْنَهَا تَذْهَلُ كُلُّ مُرْضِعَةٍ عَمَّٓا اَرْضَعَتْ وَتَضَعُ كُلُّ ذَاتِ حَمْلٍ حَمْلَهَا وَتَرَى النَّاسَ سُكَارٰى وَمَا هُمْ بِسُكَارٰى وَلٰكِنَّ عَذَابَ اللّٰهِ شَد۪يدٌ اَللّٰهُ لَٓااِلٰهَ اِلَّاهُوَ لَيَجْمَعَنَّكُمْ اِلٰى يَوْمِ الْقِيٰمَةِ لَا رَيْبَ ف۪يهِ وَمَنْ اَصْدَقُ مِنَ اللّٰهِ حَد۪يثًا ❀ اِنَّ الْاَبْرَارَ لَف۪ي نَع۪يمٍ ❀ وَ اِنَّ الْفُجَّارَ لَف۪ي جَح۪يمٍ اِذَا زُلْزِلَتِ الْاَرْضُ زِلْزَالَهَا ❀ وَاَخْرَجَتِ الْاَرْضُ اَثْقَالَهَا ❀ وَقَالَ الْاِنْسَانُ مَالَهَا ❀ يَوْمَئِذٍ تُحَدِّثُ اَخْبَارَهَا ❀ بِاَنَّ رَبَّكَ اَوْحٰى لَهَا ❀ يَوْمَئِذٍ يَصْدُرُ النَّاسُ اَشْتَاتًا لِيُرَوْا اَعْمَالَهُمْ ❀ فَمَنْ يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُ ❀ وَمَنْ يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُ اَلْقَارِعَةُ ❀ مَا الْقَارِعَةُ ❀ وَمَٓا اَدْرٰيكَ مَا الْقَارِعَةُ ❀ يَوْمَ يَكُونُ النَّاسُ كَالْفَرَاشِ الْمَبْثُوثِ ❀ وَتَكُونُ الْجِبَالُ كَالْعِهْنِ الْمَنْفُوشِ ❀ فَاَمَّا مَنْ ثَقُلَتْ مَوَاز۪ينُهُ ❀ فَهُوَ ف۪ي عِيشَةٍ رَاضِيَةٍ ❀ وَاَمَّا مَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ ❀ فَاُمُّهُ هَاوِيَةٌ ❀ وَمَٓا اَدْرٰيكَ مَاهِيَهْ ❀ نَارٌ حَامِيَةٌ ❀ وَ لِلّٰهِ غَيْبُ السَّمٰوَاتِ وَالْاَرْضِ وَمَٓا اَمْرُ السَّاعَةِ اِلَّا كَلَمْحِ الْبَصَرِ اَوْ هُوَ اَقْرَبُ اِنَّ اللّٰهَ عَلٰى كُلِّ شَىْءٍ قَد۪يرٌ Na tusikilize mifano ya aya hizi na tuseme tumeamini na tumesadiki: آمَنْتُ بِاللّٰهِ وَمَلٰئِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَبِالْقَدَرِ خَيْرِهِ وَشَرِّهِ مِنَ اللّٰهِ تَعَالٰى وَالْبَعْثُ بَعْدَ الْمَوْتِ حَقٌّ وَاَنَّ الْجَنَّةَ حَقٌّ وَالنَّارَ حَقٌّ وَاَنَّ الشَّفَاعَةَ حَقٌّ وَاَنَّ مُنْكَرًا وَنَكِيرًا حَقٌّ وَاَنَّ اللّٰهَ يَبْعَثُ مَنْ فِي الْقُبُورِ اَشْهَدُ اَنْ لَااِلٰهَ اِلَّااللّٰهُ وَاَشْهَدُ اَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللّٰهِ اَللّٰهُمَّ صَلِّ عَلٰى اَلْطَفِ وَاَشْرَفِ وَاَكْمَلِ وَاَجْمَلِ ثَمَرَاتِ طُوبَاءِ رَحْمَتِكَ الَّذِي اَرْسَلْتَهُ رَحْمَةً لِلْعَالَمِينَ وَوَسِيلَةً لِوُصُولِنَا اِلٰى اَزْيَنِ وَاَحْسَنِ وَاَجْلٰى وَاَعْلٰى ثَمَرَاتِ تِلْكَ الطُّوبَاءِ الْمُتَدَلِّيَةِ عَلٰى دَارِ الْآخِرَةِ اَىِ الْجَنَّةِ ❀ اَللّٰهُمَّ اَجِرْنَا وَاَجِرْ وَالِدَيْنَا مِنَ النَّارِ وَاَدْخِلْنَا وَاَدْخِلْ وَالِدَيْنَا الْجَنَّةَ مَعَ الْاَبْرَارِ بِجَاهِ نَبِيِّكَ الْمُخْتَارِ آمِينَ Basi ewe ndugu msomaji wa ujumbe huu kwa insafu! Usiseme, kwa nini siwezi kulifahamu neno hili la ‘kumi’ katika ufafanuzi wake wote? usihuzunike wala usione dhiki moyoni mwako, kwa kutoelewa kwani wanafalsafa wakubwa kama; Ibn sina, walisema: “Ufufuo hauko katika vipimo vya kiakili, yaani, tunaamini tu” wala haiwezekani kupita njia yake kwa kutumia akili, na hivyo hivyo wanazuoni wa Uislamu, wameafikiana kwamba kadhia ya ufufuo ni kadhia ya kimapokeo, yaani dalili zake ni za kimapokeo, na haiwezekani kuifikia kwa akili, kwa hiyo njia ngumu na njia ya hali ya juu sana wakati huo huo, haiwezi kuwa ni njia ya watu wote kwa wepesi ambao kila mtu anaweza kupita. Lakini kwa heri za Qur’an tukufu, na kwa rehema za Muumba Mwingi wa rehema, tumeneemeshwa kutembea kwenye njia hii nyembamba, yenye kina kirefu katika enzi hizi ambazo kuiga kumevunjika, ufuasi na utii wa kusalimu amri umeharibika, na hatupaswi isipokuwa kupeleka shukrani kwa Mola Muumba (s.w), kwa hisani yake enevu, na fadhila zake kubwa, kwani kiasi hiki chatosha kuokoa imani yetu na kusalimisha, hatuna budi kusoma kiasi cha ufahamu wetu na tuuongeze kwa kutalii mara kwa mara. Cha kuzingatia ni kwamba mojawapo ya siri za kutoufikia ufahamu wa suala la ufufuo kwa akili, ni kwamba ufufuo mkuu ni katika kudhihirisha jina kuu. Kwa hiyo, kuona na kuonesha matendo makuu yanayotokana na kudhihiri jina kuu, ni katika kudhihirika ngazi kuu ya kila jina mojawapo kati ya majina mazuri, ndiyo yanayofanya wepesi kuthibitisha ufufuo mkuu, na bayana kama kuthibiti na kuthibitisha majira ya machipuo, na ndiyo inayopelekea kukubali kwa moja kwa moja na kuamini kiukweli. Na kwa sura ya namna hii, ndivyo hufafanuliwa ufufuo na umefafanuliwa katika (Neno hili la kumi), kwa kheri za Qur’an tukufu, na kama si hivyo akili ingetegemea vipimo vyake vya jumla, ingebakiwa yenye kushindwa na kulazimika kuiga. * * *
Sehemu ya kwanza Kutoka katika mwendelezo wa neno la kumi na nyongeza yake muhimu. بِسْمِ اللّٰهِ الرَّحْمٰنِ الرَّحِيمِ فَسُبْحَانَ اللّٰهِ ح۪ينَ تُمْسُونَ وَح۪ينَ تُصْبِحُونَ وَلَهُ الْحَمْدُ فِي السَّمٰوَاتِ وَالْاَرْضِ وَعَشِيًّا وَح۪ينَ تُظْهِرُونَ ❀ يُخْرِجُ الْحَىَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَىِّ وَيُحْيِي الْاَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَكَذٰلِكَ تُخْرَجُونَ ❀ وَمِنْ آيَاتِه۪ٓ أَنْ خَلَقَكُمْ مِنْ تُرَابٍ ثُمَّ اِذَٓا أَنْتُمْ بَشَرٌ تَنْتَشِرُونَ ❀ وَمِنْ آيَاتِه۪ٓ أَنْ خَلَقَ لَكُمْ مِنْ أَنْفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِتَسْكُنُٓوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُمْ مَوَدَّةً وَرَحْمَةً إِنَّ ف۪ي ذٰلِكَ لَاٰيَاتٍ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ ❀ وَمِنْ آيَاتِه۪ خَلْقُ السَّمٰوَاتِ وَالْاَرْضِ وَاخْتِلَافُ أَلْسِنَتِكُمْ وَأَلْوَانِكُمْ اِنَّ ف۪ي ذٰلِكَ لَاٰيَاتٍ لِلْعَالِم۪ينَ ❀ وَمِنْ آيَاتِه۪ مَنَامُكُمْ بِالَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَابْتِغَٓاؤُكُمْ مِنْ فَضْلِه۪ اِنَّ ف۪ي ذٰلِكَ لَاٰيَاتٍ لِقَوْمٍ يَسْمَعُونَ ❀ وَمِنْ آيَاتِه۪ يُر۪يكُمُ الْبَرْقَ خَوْفًا وَطَمَعًا وَيُنَزِّلُ مِنَ السَّمَٓاءِ مَٓاءً فَيُحْيِي بِهِ الْاَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا اِنَّ ف۪ي ذٰلِكَ لَاٰيَاتٍ لِقَوْمٍ يَعْقِلُونَ ❀ وَمِنْ آيَاتِه۪ٓ اَنْ تَقُومَ السَّمَٓاءُ وَالْاَرْضُ بِأَمْرِه۪ ثُمَّ اِذَا دَعَاكُمْ دَعْوَةً مِنَ الْاَرْضِ اِذَٓا أَنْتُمْ تَخْرُجُونَ ❀ وَلَهُ مَنْ فِي السَّمٰوَاتِ وَالْاَرْضِ كُلٌّ لَهُ قَانِتُونَ ❀ وَهُوَ الَّذ۪ي يَبْدَؤُا الْخَلْقَ ثُمَّ يُع۪يدُهُ وَهُوَ أَهْوَنُ عَلَيْهِ وَلَهُ الْمَثَلُ الْاَعْلٰى فِي السَّمٰوَاتِ وَالْاَرْضِ وَهُوَ الْعَز۪يزُ الْحَك۪يمُ Katika Mshale huu wa tisa kutaelezwa kinagaubaga nukta tukufu ya aya hizi tukufu, zinazoonesha mojawapo katika ‘nguzo za imani; shuhuda hizi tukufu zenye nguvu za kufufuliwa wafu zitaelezwa. Ni msimamo pambanuzi wa rehema ya kimamlaka kuwa miaka thelathini iliyopita mwishoni mwa kazi yake iliyoitwa Muhâkamat (Utoaji hoja), ambayo iliandikwa ili kuweka kanuni za ufafanuzi wa Qur’an, Said wa zamani ameandika: “Kusudio la Pili: Aya Mbili za Qur’an zenye kudokezea ufufuo wa wafu zitafafanuliwa kinagaubaga. Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.” Akaishia hapo na hakuandika zaidi. Sasa, sifa na shukurani zimwendee Muumbaji Mwingi wa Rehema kwa idadi ya dalili na ishara za ufufuo, kuwa miaka thelathini baadaye Alinipa mafanikio ya kukamilisha hilo. Ndiyo, miaka tisa au kumi iliyopita, Ameneemesha neno la kumi na la Ishirini na Tisa, shuhuda mbili ng’aavu na zenye nguvu zinazodhihirisha hukumu ya Kiungu ya: فَانْظُرْ اِلٰٓى آثَارِ رَحْمَتِ اللّٰهِ كَيْفَ يُحْيِي الْاَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا اِنَّ ذٰلِكَ لَمُحْيِي الْمَوْتٰى وَهُوَ عَلٰى كُلِّ شَىْءٍ قَد۪يرٌ ambayo ilikuwa aya ya kwanza kati ya mbili. Zikawanyamazisha wenye kukanusha ufufuo. Sasa, miaka tisa au kumi baada ya ngome mbili zisizopenyeka za kuamini ufufuo wa wafu, Ameneemesha kwa maandiko ya sasa ya sherehe ya aya mbili hizo tukufu hapo juu. Mshale huu wa Tisa, unajumuisha ‘Vituo’ tisa vya juu vilivyoashiriwa na aya zilizotajwa hapo juu, na Utangulizi muhimu.
[Nukta mbili zenye kujumuisha maelezo ya muhutasari ya moja ya matokeo jumuishi ya manufaa mbali mbali ya kiroho ya kuamini ufufuo na matokeo yake muhimu; kuonesha umuhimu wake katika maisha ya mwanaadamu na hususani kwa uzima wa jamii; muhutasari wa ushahidi mmoja wenye kuenea kutoka miongoni mwa shuhuda nyingi za itikadi ya kuamini ufufuo wa wafu; na kauli ya jinsi isivyo na shaka na yenye kujionesha wazi itikadi hiyo ya imani.]
Tutaonesha, kama kipimo, nne tu kati ya mamia ya shuhuda kuwa kuamini akhera ni msingi kwa maisha ya jamii na ya mtu binafsi, na pia ni msingi wa furaha yake, ustawi, na mafanikio. Mosi: Ni kwa fikra ya Pepo ambapo watoto, wanaounda takribani nusu ya wanaadamu, wangehimili vifo vyote baina yao, vinavyoonekana kwao kuwa huzuni na vyenye kutisha, na kuimarisha nguvu yao dhaifu na nyonge ya kimaumbile. Kwa fikra ya Pepo wanapata matumaini kwenye roho zao zenye kudhurika, zenye kukaribia kulia, na wanaweza kuishi kwa furaha. Mathalani, huku akiitafakari Pepo, mtoto anaweza kusema: “Mdogo au rafiki yangu amefariki na kuwa ndege wa Peponi. Yeye anarukaruka Peponi na kuishi kwa furaha zaidi kuliko sisi.” Vifo vya mara kwa mara mbele ya macho yao yasiyo na furaha vya watoto wenzao au vya wakubwa, vinginevyo vingevunja ukinzani wao wote na hamasa yao yote, na kufanya akili zao pambanuzi, kama vile roho zao, nyoyo, na akili, zilie pamoja na macho yao; ama wataporomoka kihisia kabisa au kuwa wanyama wenye wazimu, na wanyonge. Ushahidi wa pili: Ni kupitia maisha ya akhera tu ambapo wazee, wenye kuunda nusu ya wanaadamu, wanaweza kuhimili ujirani na kaburi, na kufarijika kwa fikra kuwa maisha yao, waliyoshikamana nayo sana, yatazimika hivi karibuni na dunia zao nzuri zitafikia ukomo. Ni kwa kutumainia uzima wa milele tu ndipo wanaweza kukabili ukataji tamaa mkubwa walio nao katika roho zenye hisia kama watoto katika kufikiria mauti. Baba na mama wenye kustahiki na wenye shauku, wenye kustahiki huruma na wana haja ya utulivu na amani ya akili, badala yake watahisi msukosuko wa kiroho na kukata tamaa nyoyoni mwao, na dunia hii itakuwa gereza lenye kiza kwao, na uhai pia, mateso ya kuhuzunisha. Ushahidi wa tatu: Ni fikra ya moto wa jahanamu inayodhibiti hisia zilizovurugika za vijana, kikundi chenye nguvu zaidi katia uzima wa jamii, na kuvuka kwao mpaka katika fujo, kuwazuia dhidi ya ushari, dhuluma, na uharibifu, na kuhakikisha kuwa maisha ya jamii yanaendelea kwa utulivu. Kama si kuhofia Jahanamu, kwa mujibu wa ‘Mwenye nguvu yuko sahihi,’ katika kufukuzia matamanio yao, vijana hao walevi wangezibadili dunia za watu dhaifu wasiojiweza na wasio na nguvu ziwe Jahanamu, na kuufanya utu uwe unyama. Ushahidi wa Nne: Kituo kipana zaidi cha maisha ya kidunia, na kiini chake, na pepo, hifadhi, na ngome ya furaha ya kidunia, ni uzima wa familia. Makazi ya kila mmoja ni dunia yake ndogo. Uzima na furaha ya makazi yake na familia vinawezekana kwa heshima halisi, shauku, na uaminifu na huruma, wepesi, na kujitolea. Heshima hii ya kweli na wema halisi vinaweza kupatikana kutokana na fikra kuwa wanafamilia wanapokuwa na usuhuba wa kudumu na urafiki na upamoja, na mwendelezo wa mahusiano ya kiuzazi, kutoto, kindugu, na kirafiki kwa kudumu katika maisha yasiyo na kikomo, na imani yao katika hili. Mtu anasema, kwa mfano: “Mke wangu atakuwa mwenzangu wa mara zote katika dunia ya milele na uzima wa milele. Haijalishi kama yeye kwa sasa ni mzee na mbaya, kwa kuwa atakuwa na uzuri wa milele.” Atajiambia kuwa atakuwa mwema na kujitolea kadri atakavyoweza kwa ajili ya usuhuba wa milele, na kumfanyia mapenzi na wema mkewe mpendwa na mzee kana kwamba ni hurulaini. Usuhuba uliokuwa uishe katika utengano wa milele baada ya saa moja au mbili ya urafiki mfupi wa juu juu ungekuwa badala yake, wa juu juu tu na wa muda mfupi, wa kubuni, wenye fikra kama za mnyama, na huruma ya uongo na heshima ya kutengeneza. Ama wanyama, kujiona na hisia nyingine zenye kushinda zingeweza kuzidi heshima na huruma, na kuibadili pepo hiyo ya kidunia kuwa Jahanamu. Hivyo, mojawapo kati ya mamia ya matokeo ya kuamini ufufuo yameunganishwa na uzima wa jamii. Kama utafanywa mlinganisho baina ya shuhuda nne za hapo juu kutoka katika mamia ya vipengele na manufaa ya tukio hili moja na mengine, itafahamika kuwa kuutambua ukweli wa ufufuo na kutokea kwake, hizo ni hakika kama ukweli wa juu wa utu na haja yake iliyoenea. Ni dhahiri hata kuliko ushahidi kwa kuwepo chakula kilichotolewa kwa kuwepo wa haja tumboni mwa mwanaadamu, na kueleza kuwepo kwake kwa uwazi zaidi. Pia inathibitisha kuwa kama matokeo ya ukweli wa ufufuo yangelitolewa kutoka katika utu, ambao hali yake halisi ni ya wazi sana, ya juu zaidi, na hai, utu ungeshuka mpaka kuwa mwili ulioharibika na kuliwa na wadudu. Wataalamu wa sayansi ya jamii, wanasiasa, na wahubiri wanaomwongoza mwanaadamu na wanaohusika na masuala yao ya kijamii na kimaadili watambue hili! Wana mapendekezo gani ya kuziba mwanya huu? Majeraha haya makubwa watayatibu kwa dawa ipi?
Hii inaeleza kwa muhutasari ushahidi mmoja - kati ya nyingi – juu ya ukweli kuhusu ufufuo kutokea nguzo nyingine za imani. Ni kama ifuatavyo: Miujiza yote inayoonesha utume wa Muhammad (Rehema na Amani zimwendee) na shuhuda za utume wake, na shuhuda zote juu ukweli wake, pamoja vinashuhudia kuwepo ufufuo na kuukubali. Kwa kuwa baada ya umoja wa kiungu, kila kitu alichosema maishani mwake kote kimefungamana na ufufuo wa wafu. Pia, miujiza yake na shuhuda zenye kuthibitisha, na kuthibitika, mitume wote waliotangulia walithibitisha ukweli huo huo. Pia, ushahidi wa fungu la maneno, “na katika Maandiko Yake,” yanayoshuhudia kikamilifu maneno, “na kwa Mitume wake,” yanathibitisha ukweli huo huo. Kama hivi: Miujiza yote, ukweli, na shuhuda zinazothibitisha kwanza kabisa ukweli wa Qur’an ya Ufafanuzi wa Kimiujiza, vinashuhudia na kuthibitisha ukweli na kutokea ufufuo. Takribani theluthi ya Qur’an ni kuhusu ufufuo, na mwanzoni mwa sura nyingi fupi fupi kuna aya zenye nguvu kuhusu hilo. Inaeleza ukweli huo huo waziwazi na kwa kuashiria kwa maelfu ya aya zake, na kuthibitisha na kuionesha. Kwa mfano: اِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ يَٓا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمْ اِنَّ زَلْزَلَةَ السَّاعَةِ شَىْءٌ عَظ۪يمٌ اِذَا زُلْزِلَتِ الْاَرْضُ زِلْزَالَهَا اِذَا السَّمَٓاءُ انْفَطَرَتْ اِذَا السَّمَٓاءُ انْشَقَّتْ عَمَّ يَتَسَٓاءَلُونَ هَلْ أَتٰيكَ حَد۪يثُ الْغَاشِيَةِ Licha ya kuonesha kwa uhakika kabisa mwanzoni mwa sura thelathini au arubaini kuwa ufufuo ni ukweli muhimu zaidi na wa lazima ulimwenguni, inaleta shuhuda zenye kushawishi kuhusu ukweli huo katika aya zake nyingine. Je, kuna uwezekano wowote kuwa imani ya akhera ni uongo, inayoibuka kama jua kutoka katika maelfu ya matamko na kauli za Kitabu, ishara ya aya mojawapo kati yake imeleta mbele yetu matunda ya ukweli mwingi uliojulikana na wa kiulimwengu mzima katika sayansi ya Kiislamu? Je, kuna uwezekano wowote wa kulikana jua, au kuwepo kwa ulimwengu? Je, hilo halitokuwa muhali na upuuzi? Je, inawezekana kuwa ingawa jeshi linaweza wakati mwingine kuingia vitani ili tu alama ya mfalme isiongope, kuonesha uongo wa maelfu ya maneno, ahadi, na vitisho vya utawala ulio makini zaidi na wa kifahari? Je, inawezekana kuwa hayo yakawa uongo? Ingawa alama moja ya utawala huo mtukufu wa kiroho ambao kwa karne kumi na tatu mfululizo umetawala roho zisizohesabika, akili, nyoyo, na roho ndani ya mipaka ya ukweli na usahihi, na kuwafundisha na kuwaelekeza, ungetosha kuthibitisha ukweli wa ufufuo, umeonesha hilo kwa maelfu ya kauli za dhahiri. Je, adhabu ya moto wa Jahanamu si ya lazima kwa mpumbavu asiyetambua ukweli huu? Je huo si uadilifu halisi? Kwa kuongezea, kuukubali kwao wazi wazi ukweli wa ufufuo, ambao Qur’an - inayotawala mustakabali na nyakati zote, inakariri kuthibitisha kwa upana na kufafanua, maandiko yote na vitabu vitukufu, kila kimoja kilitawala kipindi mahususi, kilithibitisha kwa mujibu wa nyakati na karne zao, lakini bila ya kufafanuliwa, bali imefichwa na kufupishwa, vikithibitisha maelfu ya alama za mafundisho ya Qur’an. Kilichojumuishwa hapa kwa kuwa kinahusiana na mjadala huu ni ushahidi mwishoni mwa Mshale wa Tatu wa nguzo nyingine za imani na hususani “Manabii” na “Maandiko Matakatifu,” mpaka “kuamini Siku ya Mwisho.” Inaunda ushahidi unaokinaisha kuhusu ufufuo, pia ipo katika umbo la dua yenye nguvu ambayo ni yenye maneno mafupi yanayoondoa mashaka yote. Yanasema katika dua: “Ewe Mwenye kuniruzuku Mwenye Huruma!” Nimefahamu kutokana na maelekezo ya Mjumbe Wako Mtukufu (s.a.w) na mafundisho ya Qur’an, kuwa awali ya yote, Qur’an na Mjumbe, na maandiko yote matukufu na manabii, wamethibitisha kwa kauli moja na kuashiria kuwa udhihirisho wa Majina yenye kuhusiana na uzuri na utukufu Wako, mifano yake ni yenye kuonekana duniani, yataendelea kwa nuru zaidi katika muda wote milele, na kuwa neema zako, ambapo sampuli zake ni zenye kuonekana katika dunia hii ya mpito, zitadumu katika makazi ya upeo wa furaha katika hali ya kung’aa zaidi, na kuwa wanaozitaka humu duniani watakuwa pamoja nazo milele. “Pia, kwa kuegemea mamia ya miujiza dhahiri, alama za wazi, na kwanza kabisa Mtume Wako Mtukufu (Rehema na amani zimwendee) na Qur’an yenye Hekima zote, na manabii kwa roho zao zenye nuru, na mawalii, ambao ni nguzo za kiroho kwa nyoyo zao zilizojaa nuru, na wanazuoni waliotwaharika kwa akili zao zenye elimu ya juu, kwa kuegemea vitisho Vyako vyenye kukaririwa na ahadi katika maandiko yote matukufu, na kutumainia sifa Zako tukufu kama vile uwezo, rehema, kufadhili, hekima, utukufu, na uzuri, na juu ya sifa Zako, na heshima ya utukufu Wako, na mamlaka ya utawala Wako, na kwa sababu ya nuru zao na maono na imani kwa kiwango cha ‘elimu ya yakini,’ hutoa bishara kwa watu na majini kuhusu furaha ya milele na kuwajulisha kuhusu Jahanamu kwa waliopotea; wanakuwa na imani yenye nguvu na kukiri.” “Ewe Mweza wa Yote na Mwenye Hekima Zote! Ewe Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu! Ewe Mkarimu Unayetimiza Ahadi! Ewe Jabari Mwenye Utukufu, Mshindi Mtukufu!” “Umetakasika kabisa na umetukuka juu ya kuwaongopea marafiki wengi, na ahadi nyingi, na sifa, na kukanusha amri za hakika za utawala wako na swala na dua za waja wako wa kukubaliwa, Unaowapenda na wanaokupenda kwa kuridhika Nawe na kukutii; na Wewe umetakasika dhidi ya ukanusho wa ufufuo kutoka kwa wapotovu na makafiri, ambao kwa ukafiri, uasi wao na kukana ahadi Zako, wanaukosea ukubwa wa utukufu wako na kukashifu heshima Yako na Uungu wako, na kuondoa huruma ya Mamlaka Yako. Tunatangaza kuwa uadilifu Wako, uzuri, na rehema kutakasika dhidi ya uasi huo usiokoma, ubaya huo. Tunaamini kwa nguvu kuwa ushahidi wa manabii, wanazuoni waliotwaharika, na mawalii, ambao ni wajumbe Wako wa kweli, wapiga mbiu wa mamlaka Yako, katika viwango vya ‘uhakika kabisa,’ ‘elimu ya uhakika,’ na ‘maono ya uhakika,’ katika hazina za rehema Zako huko akhera na maghala ya Neema Zako katika ulimwengu wa milele, na uzuri wa kimiujiza wa udhihirisho wa Majina Yako Mazuri, yatakayodhihirishwa kikamilifu katika makazi ya upeo wa furaha, bila ya shaka ni kweli, na walichoelekeza kinaendana na usahihi bila ya shaka, na kuwa bishara walizotoa ni kweli na zitatokea. Kwa kuamini kuwa mshale mkuu wa Jina la Ukweli, ambalo ni chanzo, jua, na hifadhi ya ukweli wote, ni ukweli huu wa ufufuo na Mkusanyiko Mkubwa, wanaowafundisha waja Wako.” Ewe Allah! Kwa ajili gani wanafundisha na kwa utukufu wa hilo, tupe sisi na wanafunzi wote wa Risale-i Nur imani kamilifu na mauti ya furaha. Utujaalie tupate uombezi wao. Amin! Kwa kuongezea, kama zilivyo shuhuda zote zenye kuonesha utukufu wa maandiko yaliyoteremshwa, na miujiza yote na shuhuda zenye kushuhudia utume wa Kipenzi cha Allah (s.a.w), na wa manabii wote, katika hali isiyo ya moja kwa moja, zinathibitisha ukweli wa akhera, ambacho ndicho wanachofundisha juu ya kila kitu kingine; hivyo ushahidi mwingi wa uwepo na umoja wa Mwenye uwepo wa wajibu unathibitisha kuwepo na kufunguka ulimwengu wa milele wa furaha ya milele, utakaokuwa dalili kuu ya mamlaka na uungu. Kama itakavyoelezwa na kuthibitishwa katika vifungu vifuatavyo, yote mawili, kuwepo kwa mwenye uwepo wa wajibu, na Sifa Zake nyingi, na Majina, kama vile mamlaka, Uungu, rehema, upole, hekima, na uadilifu, hulazimisha uwepo wa akhera kwa uhakika mkubwa sana, na kuhitajia ulimwengu wa milele na ufufuo wa wafu na Hukumu ya Mwisho kwa ajili ya kutoa malipo na adhabu. Kwa kuwa yupo Allah wa tangu na wa Milele, kwa hakika kabisa akhera ipo, uwanja wa milele wa mamlaka ya Uungu Wake. Na kwa kuwa ulimwenguni na hasa kwa viumbe hai kuna utawala kamili wenye rehema na mtukufu mno na wa hekima nyingi, na huo uko dhahiri; kuna uhakika wa kuwepo ulimwengu wa milele wa furaha utakaotukuza utukufu wa utawala huo dhidi ya kuukosea heshima, busara yake kutoka katika kusikokuwa na lengo, na rehema yake dhidi ya ukatili; na ulimwengu huo unapaswa kuwepo. Na kwa kuwa neema zisizokuwa na idadi, fadhila na matukio mengi ya rehema yanayoonekana wazi, yanazionesha akili ambazo hazijazimika na nyoyo ambazo hazijafa kuwa nyuma ya pazia ya Ghaibu kuna Mmoja Mwingi wa Rehema; kwa hakika kuna uhai wa milele utakaohifadhi neema hizo dhidi ya dhihaka, neema dhidi ya ulaghai, upendo dhidi ya uadui, rehema dhidi ya ukatili, huruma na zawadi dhidi ya udanganyifu, na utafanya neema ziwe neema na ukarimu uwe ukarimu. Na kwa kuwa katika majira ya kuchipua katika ukurasa finyu wa ardhi, kalamu ya uwezo huandika maelfu ya malaki ya vitabu bila ya dosari pasi na kuchoka mbele ya macho yetu; na kwa kuwa mwenye kumiliki kalamu ameahidi mara nyingi mno: “Nitaandika kitabu kizuri cha milele katika ulimwengu mpana, kilicho rahisi zaidi ya kitabu hiki cha majira ya kuchipua kilichoandikwa kwenye ulimwengu huu mfinyu, uliovurugika na kuchanganyikana, na nitakuachilia ukisome;” kwa kuwa anataja kitabu kwenye amri zake zote; kwa hakika, sehemu kubwa ya kitabu imeshaandikwa, na kwa ufufuo na Hukumu ya Mwisho kitaongezewa tanbihi chini ya kurasa, na madaftari yote ya amali za watu yataandikwa humo. Na kwa kuwa, kutokana na wingi wa viumbe, ardhi ni makazi, chanzo, kiwanda, udhihirisho, na mahali pa mkusanyiko wa mamia ya maelfu ya viumbe hai vyenye kuendelea kubadilika na viumbe wenye roho, na ni moyo, kituo, muhtasari, na matokeo ya ulimwengu, na sababu ya kuumbwa kwake; umuhimu wake mkubwa, na kuwekwa sawa na mbingu zenye nguvu licha ya udogo wake; katika hukumu za kiungu, mara zote husemwa: رَبُّ السَّمٰوَاتِ وَالْاَرْضِ Na kwa kuwa mwanaadamu, anayetawala ardhi, ambayo kwa hivyo, ana haki ya kuwatumia viumbe wengi, na kuwatiisha viumbe hai kwa kuwakusanya karibu yake; na kwa kuwa anatoa amri, anaonesha, na kukusanya pamoja kila namna nzuri mahali pamoja kama orodha, kwa kuwapamba, kiasi kwamba huvutia, si hisia na mastaajabu ya watu na majini, bali wakazi wa mbingu na ulimwengu, na mtizamo wa kushukuru wa Mwenye kumiliki ulimwengu, hivyo kupata umuhimu mkubwa na kuaminiwa sana; na kwa kuwa anaonesha kwa sayansi na sanaa yake kuwa yeye ni lengo la kuumbwa ulimwengu, na matokeo yake muhimu zaidi, na tunda la thamani zaidi, na khalifa wa Kiungu ardhini; na kwa kuwa kwa sababu kuhusu dunia hii, ameamuru na kuonesha vyema kabisa sanaa ya ajabu ya Muumba dunia, mwanaadamu huachwa duniani licha ya uasi na ukafiri wake, na adhabu imeahirishwa, na kwa sababu ya kazi hii, muda wake umerefushwa ili afanye kazi yake kwa mafanikio. Na kwa kuwa yupo Muumbaji mwenye nguvu, mwenye hekima na mwenye rehema, Anayeumba tufe lenye nguvu na kuwa hazina ya namna zote za metali na madini anayohitaji mwanaadamu kwa namna iliyo nje ya nguvu na utashi wake, ambaye licha ya kuwa dhaifu, mwenye kuhitajia kiasili na kimaumbile, ana haja nyingi na ni pia ni mwenye kupata masumbuko mengi - na kwa kuwa Anaijaalia iwe ghala la kila namna ya chakula, na duka lililosheheni bidhaa za kila namna zenye kumridhisha mwanaadamu, na kumwangalia mtu kwa namna hii, na kumlea, na kumpa anachohitaji. Na kwa kuwa yupo Mwenye kuruzuku Ambaye ni kwa hiyo, Anayempenda mwanaadamu na kumsababisha ampende Yeye, na Ambaye ni mwenye kubaki na ana dunia za milele, na Anayefanya kila jambo kwa haki na hekima; na kwa kuwa fahari ya utawala huo Wenye Enzi wa Tangu na mamlaka Yake ya Milele hauwezi kuwemo tu kwenye maisha haya mafupi ya kidunia, na katika umri wa mpito wa mwanaadamu, na katika ardhi ya muda mfupi na mpito; na kwa kuwa kukithiri kwa uovu na maasi yanayotokea baina ya watu, ambayo yako tofauti na ustawi, haki, urari na uzuri wa ulimwengu, na kukana kwao, udanganyifu, na ukafiri kwa Mpaji wao, Anayewalea kwa wema, kwakuwa hawaadhibiwi humu duniani, na dhalimu katili anaishi kwa raha ilhali wanaodhulumiwa wasio na furaha wanaishi kwa taabu; na kwa kuwa haki kamili ambayo alama zake ni zenye kuonekana ulimwenguni kote ziko tofauti kabisa na mwasi mkatili na wadhulumiwa waliokata tamaa kulingana katika wakati wa mauti, haiwezi kukubali kwa namna yoyote ile. Na kwa kuwa kama ambavyo Mmiliki wa ulimwengu alivyoichagua ardhi kutoka katika ulimwengu, na mwanaadamu kutoka katika ardhi na kumneemesha kwa hadhi ya juu na umuhimu; hivyo kati ya wanaadamu ameteua manabii, mawalii, na watakatifu, wanaadamu wa kweli wenye kuendana na malengo ya mamlaka yake na kupitia imani yao na kujisalimisha kunamfanya Awapende; amewafanya kama marafiki na wasemeshwa wake, na kujaalia miujiza na kufaulu juu yao na kuwaadhibu maadui wao kwa mapigo ya kiungu. Na katika marafiki hawa wapendwa Amemteua kiongozi wao na chanzo cha utukufu, Muhammad (Rehema na amani zimwendee), na kwa karne nyingi ameangazia Nuru yake kwenye nusu ya dunia na sehemu moja kati ya tano za wanaadamu; kana kwamba ulimwengu uliumbwa kwa ajili yake, malengo yake yote yanakuwa dhahiri kupitia kwake, na dini yake na Qur’an. Na ingawa anastahili kuishi wakati mrefu usio na mpaka katika kufidia huduma yake ya thamani kubwa sana, kwa mamilioni ya miaka, aliishi kwa muda mfupi tu wa miaka sitini na mitatu ya taabu kubwa. Basi je, kuna uwezekano wowote kuwa asifufuliwe pamoja na wenzi na marafiki zake? Kwamba kwa sasa asipaswe kuishi kiroho? Kwamba angeangamizwa milele? Allah aepushe hilo! Ndiyo, ulimwengu wote na ukweli wa dunia unahitaji afufuliwe na wanamwomba Mmiliki wa ulimwengu kuwa awe hai. Na kwa kuwa katika Mshale wa Saba, (Ishara kuu), kila moja kwa uimara wa mlima, miafaka thelathini na tatu yenye nguvu imethibitisha kuwa ulimwengu umetoka kwa mmoja na hiyo ni mali ya mmoja; na imedhihirisha Umoja Wake na upweke, ni njia ya makamilifu ya Kiungu; na kupitia umoja na upweke, viumbe wote wanakuwa kama askari chini ya amri na maafisa watiifu; na kwa kuja kwa akhera, makamilifu huokolewa dhidi ya kuporomoka, haki kamili dhidi ya ukatili, hekima yenye kuenea dhidi ya upumbavu, rehema yenye kuenea dhidi ya adhabu, na heshima ya uwezo dhidi ya udhaifu wa kudhalilika, na kuachiliwa huru dhidi ya haya. Kwa hakika na bila ya shaka yoyote, kama ilivyolazimishwa na ukweli katika ‘kwa kuwa’ hizi sita - sita kati ya mamia ya nukta za kumwamini Allah - mwisho wa dunia utafika na ufufuo wa wafu utatokea. Milango ya mlipo na adhabu itafunguliwa ili umuhimu wa ardhi uliotajwa hapo juu, na umuhimu wake, na umuhimu wa mwanaadamu na thamani yake vitambulike, na ili ibaki haki, uadilifu uliotajwa hapo juu, hekima, rehema, na mamlaka ya Mpangaji Mwingi wa Hekima, Ambaye ni Muumbaji wa ardhi na mwanaadamu, na Mwenye kuwaruzuku; na marafiki wa kweli wa Mwenye kuruzuku milele watanusuriwa dhidi ya kuangamia milele; na mkuu zaidi na kustahiki katika marafiki hao atapata malipo ya huduma zake tukufu, zilizofanya viumbe wote wawe radhi na kuwa na deni; na makamilifu ya Enzi ya Milele yatakaswe na kumwepusha mbali na dosari yoyote na upungufu wowote, na uwezo Wake dhidi ya udhaifu, na hekima Yake dhidi ya upumbavu, na haki dhidi ya dhuluma. Kwa kifupi: Kwa kuwa Allah yupo, ndivyo pia akhera, kwa hakika ipo. Kwa kuongezea, kama ambavyo ushahidi wote unathibitisha hayo, nguzo tatu za hapo juu za imani zinathibitisha na zinaashiria ufufuo; ndivyo pia nguzo mbili “na kuamini malaika, na Kudura ya Kiungu, kuwa heri na shari ni kutoka kwa Allah (s.w)” pia inalazimisha ufufuo na kuthibitisha kwa mtindo wenye nguvu kwenye ulimwengu wa milele. Ni kama hivi: Shuhuda zote zinazothibitisha kuwepo kwa malaika na majukumu yao ya ibada, na tafiti zisizohesabika kuwahusu na mazungumzo nao, zinathibitisha moja kwa moja kuwepo kwa Dunia ya Kiroho, na dunia ya ghaibu, na ulimwengu wa milele na dunia ya akhera, na kuwepo kwa makazi ya furaha na Pepo na Jahanamu, ambavyo katika mustakabali vitajaa watu na majini. Kwa idhini ya Kiungu, malaika wanaweza kuziona dunia hizo na kuingia. Na Malaika wengi wa daraja za juu wanaokutana na wanaadamu, kama vile Jibrili, wameeleza kwa kauli moja juu ya kuwepo dunia hizo na wao kusafiri baina ya hizo. Kama tulivyo na uhakika, kutokana na habari ya wanaokuja kutoka Marekani, kuwa bara la Marekani lipo, ingawa hatukupata kuliona, hivyo kutokana na habari kuhusu malaika, ambazo zina miafaka mingi madhubuti, tunapaswa kuamini kwa uhakika huo huo juu ya kuwepo kwa dunia ya milele, ulimwengu wa akhera, na Pepo na Jahanamu. Na hivyo tunaamini. Kwa kuongezea, ushahidi wote unaothibitisha nguzo ya “kuamini Kudura ya Kiungu,” iliyo katika Risala ya Kudura ya Kiungu, (Neno la Ishirini na Sita), unathibitisha moja kwa moja juu ya kufufuliwa wafu, kupimwa amali kwenye mizani kuu, na kusambazwa kurasa za amali. Kuandikwa kwa habari za maisha ya viumbe hai vyote katika kumbukumbu zao, na kuandikwa kwa madaftari ya amali za viumbe wote wenye roho, na hususani wanadamu, katika Ubao Uliohifadhiwa, kudura hiyo pana na utengaji wa hekima na uandishi makini na kuhifadhiwa maandishi kunaweza tu kwa hakika kuwa matokeo ya hukumu kuu katika muundo mtukufu wa kimahakama kushughulikia malipo na adhabu ya milele. Uandishi huo sahihi na hifadhi ungekuwa vinginevyo hauna maana kabisa na hauna lengo, na kinyume na hekima na uhalisia. Pia, kama kusingekuwa na ufufuo, maana zote za hakika za kitabu cha ulimwengu, ikiwa kimeandikwa kwa kalamu ya Kudura ya Kiungu, ingebatilika, jambo ambalo haliwezekani kabisa. Ni kama isivyowezekana kukana kuwepo kwa ulimwengu, kwa hakika, ni kuweweseka. Kwa kifupi: Kwa ushahidi wake wote, nguzo tano za imani zinahitajia kuwepo kwa ufufuo na Hukumu ya Mwisho, na kuwepo kwao, na kuwepo na kufunguka ulimwengu wa akhera, na zinathibitisha hayo na kuyalazimisha. Hivyo, ni kwa sababu kuna hoja na shuhuda kubwa zisizotetereka kuhusu ufufuo, katika kuendana kikamilifu na ukubwa wake, kiasi kuwa takribani theluthi ya Qur’an ya Ufafanuzi wa Kimiujiza imeundwa na ufufuo na akhera, na inaufanya ukweli huo jiwe la msingi la ukweli wake wote, na kukijengea kila kitu juu yake. (Mwisho wa Utangulizi) * * *
Ni makamo ya kwanza katika makamo tisa, katika ngazi za hoja tisa zinazohusu ufufuo, na ambazo kwa namna ya kimiujiza aya tukufu zifuatazo zimeziashiria: ❀ فَسُبْحَانَ اللّٰهِ ح۪ينَ تُمْسُونَ وَح۪ينَ تُصْبِحُونَ ❀ وَلَهُ الْحَمْدُ فِي السَّمٰوَاتِ وَالْاَرْضِ وَعَشِيًّا وَح۪ينَ تُظْهِرُونَ ❀ يُخْرِجُ الْحَىَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَىِّ وَيُحْيِي الْاَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَكَذٰلِكَ تُخْرَجُونَ Insha Allah itabainishwa yale ambayo Aya hizi tukufu zimebainisha miongoni mwa hoja za moja kwa moja juu ya ufufuo , nimeweka wazi katika sifa maalumu ya uhai, sifa ya ishirini na tano, kwamba uhai unathibitisha nguzo sita za imani, na kuelekea na kuashiria juu ya kutokea kwake. Naam, maadamu maisha ndio hekima ya kuumbwa kwa viumbe, na pia ndio matokeo yake muhimu na kiini chake, ukweli huu mtukufu hauishii tu katika maisha haya ya dunia yenye kutoweka yaliyo mafupi, yenye upungufu na kuumiza, bali sifa maalumu ishirini na tisa za maisha na ukubwa wake ulivyo, na kinachofahamika kutokana na upeo wa mti wake na tija yake, na tunda lake stahiki kulingana na ukuu wa mti huo, hayo siyo isipokuwa ni maisha ya milele tu, na maisha ya akhera, na maisha yaliyo na uhai kwa mawe yake, udongo, na miti yake katika mji wa furaha ya kudumu milele, na kama sio hivyo basi italazimu mti wa uhai ulioandaliwa kwa zana hizi nyingi anuwai, kubakia kwa wenye hisia tu na hasa mwanaadamu, pasipo na tija wala faida wala hakika yoyote, na mwanaadamu angebaki kuwa mwenye kuharibikiwa na mwenye mateso dhalili, na wa chini kuliko kinega (ndege mdogo) kwa daraja ishirini, kulingana na furaha ya maisha, pamoja na kuwa yeye ni kiumbe bora sana na mtukufu zaidi kuliko viumbe hai, na wa juu kuliko kinega kwa daraja ishirini, bali akili ambayo ni neema yenye thamani kubwa mno, itageuka kuwa ni msiba na balaa kwa mwanaadamu kwa kutafakari kwake juu ya huzuni za zama zilizopita, na hofu za mustakbali, kwa hiyo anautesa moyo wake daima akitibua kutakata kwa ladha moja kwa maumivu tisa! Hapana shaka kwamba hili ni batili mia kwa mia. Maisha haya ya dunia kwa hiyo yanathibitisha nguzo ya (kuamini akhera), uthibitisho wa kukata shauri kwa yale inayotuonyesha ndani ya kila majira ya machipuo, zaidi ya vielezo laki tatu vya ufufuo. Je, yaweza kufikiriwa kuwa, yawezekana kwa Mola Mweza, anaandaa yanayolazimu katika uhai wako miongoni mwa mahitaji yote yanayolingana na maisha hayo, na kukukamilishia zana zake zote sawa, iwe mwilini mwako au bustanini au nchini mwako, na kuvileta ndani ya wakati wenye mnasaba kabisa kwa hekima, uangalizi na rehema, hata kiasi kwamba anajua matakwa ya tumbo lako katika mahitaji yanayo kuhakikishia kuendelea kuishi, na anasikia unachoomba katika dua maalumu ya sehemu ya kuomba riziki, akionesha kukubali kwake dua hiyo kwa vyakula vitamu visivyo na ukomo alivyovisambaza, ili kutuliza tumbo hilo! Basi je, yawezekana kwa huyu mtawala Mweza kwamba hakujui? Wala hakuoni? Wala haandai sababu za lazima kwa ajili ya lengo kuu la mwanaadamu, nalo ni maisha ya milele? Na wala hatojibu dua kubwa mno muhimu na ya jumla, nayo ni dua ya kudumu milele? Na asiipokee kwa kutotengeneza kwake maisha ya Akhera na kufanya pepo iwepo, na asisikilize dua ya mwanaadamu huyu ambaye ni kiumbe wa hadhi ya juu zaidi ulimwenguni, bali yeye ndiye mfalme wa duniani na matokeo yake, dua hiyo ya jumla yenye nguvu itokayo kwenye kina kirefu cha nyoyo, ambayo inatikisa arshi na matandiko, je, yawezekana asitilie maanani kama anavyotilia umuhimu dua ya tumbo dogo, na asimridhishe mwanaadamu huyu? Na aweke hekima yake kamili na rehema yake isio na mipaka mahali pa kukanushwa? Kamwe kisha kamwe mara elfu elfu kamwe. Je, inakubalika akilini kwamba asikie sauti hafifu mno ya kijisehemu kidogo mno, katika maisha awe anasikia malalamiko yake na kuipa msaada, kuifanyia upole na kuilea kwa uangalizi kamili na kutilia umuhimu kwa kiwango cha juu, na kumtiishia viumbe wake wakubwa sana kwenye ulimwengu wote, kisha asisikie sauti kama mngurumo wa mbingu ya maisha makubwa na ya hadhi ya juu, mazuri na ya kudumu zaidi? Na je, inakubalika akilini, kwamba asisikie maombi yake muhimu, nayo ni dua ya kubaki milele, na asitazame kujinyenyekeza kwake kutarajia kwake, na kujikurubisha kwake kwa kubembeleza? Na awe kama anayeandaa askari mmoja kwa uangalizi kamili na zana za mapigano, na asiwe mwenye kuzingatia jeshi kubwa linalomtii! Na kama anayeona punje ya ufuta na haoni jua! Au kama anayesikia mruzi wa nzi wala asisikie radi za mbingu, hasha! Kwa Allah mara laki moja elfu hasha kwa Allah (s.w). Na je, akili inakubali kwa namna yoyote iwayo, kwamba Mweza Mwingi wa hekima mwenye rehema kunjufu na mwenye mahaba ya juu na mwenye upole wa jumla, na ambaye anapenda sana sanaa yake, na anapendezesha nafsi yake kwayo kwa viumbe wake naye ni Mwingi wa upendo kwa wanaompenda, je, inakubalika akilini kwamba aangamize uhai wa yule ampendaye mno naye ni mpendwa, na mstahiki wa kupendwa, na mwenye kumuabudu Muumba wake kwa kimaumbile? Na kadhalika aangamize kiini na johari ya uhai, nayo ni roho kwa umauti wa milele na kutowesha kwa milele, na kuzalisha pengo kati yake na wanaompenda na kuwaumiza maumivu makubwa mno, na afanye siri ya rehema yake na nuru ya mapenzi yake kuwa ni shabaha ya kukanusha, hasha! Kwa Allah (s.w) mara elfu. Uzuri usio na kikomo ambao kwa kudhihirika kwake umeupamba na kuuremba huu ulimwengu, na huruma isiyo na mipaka iliyowafurahisha viumbe na kuwapamba wote, hapana shaka kwamba hivyo viwili vimeepukana na kutakasika bila ukomo, wala hakuna mpaka wa ukatili huo na ubaya huu usio na mipaka na dhulma isio na kikomo. Matokeo: Maadamu duniani kuna uhai, hapana budi wale wanaojua siri ya maisha katika wanadamu, na hawatumii vibaya uhai wao, watakuwa wanastahiki kwa uhai wa kusalia milele, kwenye mji wa kusalia kwenye pepo ya kukusalia. Tumeamini!. Kisha kumetameta kwa maada zenye kung’ara juu ya sura ya ardhi, na kung’ara kwa mapovu juu ya bahari, kisha kuzimika mng’aro huo na umeme huo kwa kuondoka kwa mapovu na mng’aro unaoufuatia, kana kwamba ni vioo vya majua madogo yakufikirika, inadhihirisha kwetu wazi wazi kwamba ming’aro hiyo si chochote isipokuwa udhihirisho wa kuakisi kwa jua moja la juu, na kutaja kwa lugha mbali mbali kuwepo kwa jua, na inaashiria kwa vidole vya nuru. Na kadhalika kumetameta kwa wenye uhai juu ya sura ya ardhi, na baharini kwa uweza wa kimungu na kwa kudhihiri jina tukufu la المحيِي (Mwenye kuhuisha) jina la mwenye uhai kamili milele, msimamizi wa kila kitu (s.w), na kupotea kwake nyuma ya pazia ya ghaibu ili kuacha nafasi kwa anayefuata baada ya kukariri (Ewe mwenye uhai ulio kamili milele), hizo si vingine isipokuwa ni shahidi na ishara za maisha ya milele na kwa kupasa kuwepo kwa aliye hai, mkamilifu msimamizi wa kila kitu (s.w). Na hivyo hivyo, hakika dalili zote ambazo zinashuhudia elimu ya kiungu, ambazo athari zake zinashuhudiwa kutokana na mpangilio wa viumbe, na dalili zote zinazothibitisha uweza unaofanya kazi ulimwenguni, na hoja zote zinazothibitisha utashi unaotawala katika uendeshaji, na upangiliaji wa ulimwengu, na alama zote na miujiza yote inayothibitisha jumbe, ambazo zimo katika eneo la maneno ya kimungu na wahyi wa kimola, dalili zote hizi zinazoshuhudia na kujulisha juu ya sifa saba tukufu za kiungu, zinajulisha na kushuhudia pia kwa muwafaka wa pamoja juu ya uhai wa (الحيُّ القيوم). Kwani kama kunapatikana uoni katika kitu, basi hapana budi kitu hicho vile vile kiwe na uhai, na kama anasikia basi hiyo ni alama ya uhai, na kama anaongea basi hiyo ni ishara ya kuwepo uhai, na kama kuna hiyari na utashi basi hayo ndio yanayoonesha kuwepo kwa uhai, na vivyo hivyo dalili zote za sifa zilizo wazi, ambazo athari zake zinashuhudiwa na kujulikana uwepo wake wa hakika, mifano ya uweza usio na mpaka, na utashi wa jumla, na ujuzi unaozungukia kila kitu, zinajulisha juu ya kuwepo kwa uhai, wa (الحيُّ القيوم), na wajibu wa kuwepo kwake, na zinashuhudia uhai wake wa milele, ambao umenawiri mwanga kwa muale wake ulimwengu wote, na zikahuisha kwa udhihirisho wake maisha ya akhera yote, kwa punje zake zote kwa pamoja. Na uhai pia unatazama na kujulisha juu ya nguzo ya imani (Kuamini malaika), na inathibitisha kwa alama. Kwa hiyo, maadamu uhai ni matokeo muhimu sana ya ulimwengu, na kwamba wenye uhai kwa thamani yao ndio wengi zaidi kuenea na kuzaana, na ndio ambao wanafuatana, kwenda kwenye nyumba ya ugeni, msafara hadi msafara, basi huimarishwa kwao na kujawa na furaha, na maadamu mviringo wa ardhi ndio mahala pa mfereji huu wa wenye uhai, hujazwa na kupakuliwa kwa hekima ya kuletwa upya, na kuzaliana kwa wingi mfululizo, na kuumbwa kutokana na vitu duni kabisa na uozo vyenye uhai kwa wingi mno, hata mviringo wa ardhi ukawa ni maonesho makuu ya walio hai, na maadamu wanaumbwa kwa wingi wa kutisha juu ya ardhi, muhtasari safi kabisa wa kupata uhai nao ni hisia, akili na roho nyororo yenye johari thabiti, kana kwamba ardhi inahuika na kuwa nzuri kwa uhai, akili, hisia na roho. Basi haiwezekani kuwa maumbo ya mbinguni ambayo ni nyororo zaidi, na yenye nuru nyingi zaidi, na muhimu zaidi kuliko ardhi, ni magumu bila uhai wala hisia, basi hao watakaoishi mbinguni wataishi na kufurahisha ulimwengu wa sayari na nyota, na kuyapa hali ya uhai na wanawakilisha matokeo ya tunda la kuumbwa kwa mbingu, na ambao watatukuka kwa kusemeshwa na masemesho ya kiungu, ni wenye hisia na wenye uhai, miongoni mwa wakazi wa mbinguni na wenyeji wa huko wenye kuwiana kwa kiasi, wapo huko kwa siri ya uhai nao ni malaika. Na hivyo hivyo siri ya uhai na kiini chake kinatazama na kuelekea katika (Kuamini Mitume), na kwa namna ya alama inathibitisha hilo. Naam, maadam ulimwengu umeumbwa kwa ajili ya uhai, na kwamba uhai ndio dhihirisho kubwa zaidi na nakshi kamilifu zaidi na ufundi mzuri zaidi wa الْحَيُّ الْقَيُّوْمُ (s.w), na maadamu uhai wake wa milele unadhihiri na kujifunua wenyewe kwa kutuma Mitume, na kuteremsha vitabu, kwani kama kusingekuwa na Mitume wala vitabu, uhai huo wa milele usingejulikana, kama ilivyo mtu kwa kuongea hubainika hali ya uhai na uhai wake, na vivyo hivyo Mitume (Anbiyaa) na (Rusul) (as), na vitabu vilivyoteremshwa juu yao, wanabainisha na kujulisha juu ya yule mzungumzaji aliye hai, ambaye anaamrisha na kukataza kwa maneno yake na maelekezo yake nyuma ya ghaibu iliyofunikwa nyuma ya pazia ya ulimwengu. Hapana budi kuwa uhai uliopo ulimwenguni, unajulisha kwa dalili ya kukata shauri juu ya (الحَيُّ الأزليُ) (s.w), na juu ya kupasa kuwepo kwake na kama miale ya uhai ya milele pia, na madhihirisho yake yanatazama na kuelekea kwenda kwenye yaliyo na uhusiano, na mafungamano nayo katika nguzo za Imani, mfano (kutuma Mitume) na )kuteremsha vitabu( na inathibitisha hayo kwa namna ya alama, na hasa (Ujumbe wa Muhammad (s.a.w)) na (Wahyi wa Qur’an), kwani inasihi kusema: Viwili hivyo vimethibiti kwa kukata shauri, kama kukata shauri kwa kuthibiti kwa uhai, kwani viwili hivyo ni sawa na roho na akili yake. Naam kama ulivyo uhai ni muhtasari unaofupisha wa huu ulimwengu, hisia ni sehemu ya uhai ni muhtasari wake, na akili ni sehemu ya hisia ni muhtasari wa hisia, na roho ndio johari safi ya uhai ndio dhati yake thabiti iliyo huru, kadhalika uhai wa Muhammad wa kimaada na wa kimaanawi unatokana na uhai na kutokana na roho ya ulimwengu, ni muhtasari wa muhtasari wake, na ujumbe wa Muhammad unatokana na hisia ya ulimwengu na akili yake, ni muhtasari wake safi mno, bali uhai wa Muhammad wa kimaada na kimaanawi kwa ushahidi wa athari zake, ni uhai wa uhai wa ulimwengu, na ujumbe wa Muhammad ni hisia ya hisia ya ulimwengu na ni nuru yake, na wahyi wa Qur’an kwa ushahidi wa hakika za kiuhai, ni roho ya uhai wa ulimwengu, na ni akili ya hisia yake ewala. Ewala Ewala. Nuru ya ujumbe wa Muhammad (s.a.w) ikifarikiana na ulimwengu na kuachana nao, ulimwengu hufa na viumbe pia hufa, na Qur’an ikitoweka na kufarikiana na ulimwengu, hupandwa na wazimu wake na tufe la ardhi hukosa busara zake, akili yake hutetereka, na hubaki bila ya hisia, na hugongana na moja ya sayari za anga na kiama hapo husimama. Na uhai kadhalika, unaangalia nguzo ya imani (الْقَدَر), na unajulisha na kuithibitisha kwa namna ya alama, maadamu uhai ni mwanga wa ulimwengu wa kushuhudiwa, na umeutawalia na kuuzunguka, na ni matokeo ya uwepo, na ndio shabaha yake na kioo kipana zaidi cha udhihirisho wa Muumba wa ulimwengu, na ni faharisi timilifu na kielelezo cha utendaji wa kiungu, hata kama ni mfano wa mpango na njia yake, - kama kufananisha kutafaa - na hapana budi kwamba siri ya uhai inahitajia uwepo pia ulimwengu wa ghaibu, - na hii ni maana ya muda uliopita na ujao, yaani viumbe waliopita na wajao katika nidhamu na mpangilio, na iwe yajulikana na kushuhudiwa, na kupatikana katika hali maalumu, na kuwa katika maandalizi ya kutekeleza amri za hali ya kimaumbile, yaani kana kwamba imo katika uhai wa kimaanawi, mfano wake ni kama ule mfano wa mbegu ya mti wa asili na mashina yake, na kokwa na matunda yaliyomo ndani ya ukomo wake, ambayo yanapambanuka kwa sifa za pekee za aina ya uhai kama mti wenyewe ulivyo, bali huenda mbegu hizo zikabeba kanuni za kiuhai madhubuti zaidi kuliko kanuni za mti wenyewe. Basi kama zilivyo mbegu na mashina ambayo majira ya mapukutiko yaliyopita yaliyaacha nyuma, na kuyaacha majira haya ya machipuo yanachukua nuru ya uhai, na yanakwenda kwa mujibu wa kanuni za kiuhai, kama majira haya ya machipuo yanavyobeba uhai, basi ndivyo hivyo hivyo mti wa viumbe, na kila tawi moja katika mti huo na kila tawi lake lina zamani yake na mustakbali wake, na ina mnyororo uliotungamana ya hatua mbali mbali, zijazo na zilizopita. na kila aina na kila sehemu ina uwepo unaoongezeka mara nyingi, kwa hatua mbali mbali, katika elimu ya kiungu, kwa namna hiyo inaunda mnyororo wa uwepo wa kielimu, na huu uwepo wa kielimu unaofanana na uwepo wa nje, ni muonekano wa kudhihirika kwa kimaanawi wa uhai wa jumla, ambapo makadirio ya kiuhai huchukuliwa kutoka katika mbao hizo za kikadari zenye maana kubwa kabisa. Naam, hakika kujaa kwa ulimwengu wa roho na huo ni aina fulani kati ya ulimwengu wa ghaibu, kwa roho ambazo ni dhati ya uhai, na maada yake na johari yake na nafsi zake, vinalazimu kuwepo kwa muda uliopita na ujao, na hizi ni aina mbili kati ya aina ya ulimwengu wa ghaibu, na sehemu ya pili katika ulimwengu huo uhai unadhihirika ndani yake, na hivyo hivyo utungamano timamu, na mpangilio kamili katika uwepo wa kielimu wa kiungu, kwa mazingira yenye maana nzuri ya kitu fulani na matokeo yake na hatua zake za kiuhai, inabainisha kuwa inastahiki ya aina ya uhai wa kimaanawi. Naam, mfano wa kudhihiri kwa maana hii, kudhihiri kwa uhai ambao ni mwanga wa jua la uhai wa milele, hakutaishia katika ulimwengu wetu huu wa kushuhudiwa tu, wala katika ulimwengu huu wa sasa, wala sio katika ulimwengu huu wa nje, bali hapana budi kila ulimwengu kati ya limwengu kuwa na muonekano, kati ya mionekano ya kudhihiri kwa mwanga huo, kulingana na ukubalifu wake, Ulimwengu kwa hiyo pamoja na vilimwengu vyake vyote, ni hai na mwenge uangazao kwa udhihirisho huo, na kama sio hivyo kila ulimwengu ungekuwa kama unavyoshuhudiwa na jicho la upotevu, ni jeneza la kutisha na kuogofya, chini ya hii dunia ya muda mfupi ionekanayo dhahiri, na ulimwengu mchakavu wa giza. Na kama hivyo, inafahamika sura moja katika sura za imani ya kuamini, kadhaa na Qadar katika siri za uhai na kuuthibitisha, na inabainika wazi kuwa kama inavyodhihiri hali ya uhai wa ulimwengu wa kushuhudiwa, na vilivyopo kwa utungamano wake na matokeo yake, hivyo hivyo viumbe vilivyopita na vijavyo, ambavyo vinahesabiwa katika ulimwengu wa ghaibu, vina uwepo wa kimaanawi, uhai wa kimaanawi, na vina uthibiti wa kielimu, wenye roho kwa namna ambayo unadhihiri kwa jina la makadiriwa athari ya uhai huo wa kimaanawi, kupitia ubao wa kadhaa na qadar.
Swali linakuja Kuhusu Mada Ya Ufufuo Aya zilizokuja ndani ya Qur’an mara kwa mara kama vile: (إِنْ كَانَتْ إِلَّا صَيْحَةً وَاحِدَةً) (وَمَا أَمْرُ السَّاعَةِ إِلَّا كَلَمْحِ الْبَصَرِ). zinatubainishia kwamba ufufuo utadhihiri ghafla katika uwepo, ndani ya punde moja bila ya muda, lakini akili finyu zinatafuta mifano halisi ishuhudiwayo ili zikubali na kukiri kwa tukio hili lenye kufurutu ada sana na suala ambalo halina mithili yake. Jawabu: Katika ufufuo kuna masuala matatu, ambayo ni: Kurejea kwa roho kwenye miili, kuhuishwa kwa miili, na kuundwa kwa miili na kujengwa upya. Suala la kwanza: Kuja kwa roho na kurudi kwake kwenye miili yake na mfano wake ni kuwa: Kukusanyika kwa askari waliotawanyika wakati wa mapumziko na waliosambaa katika pande mbali mbali kwa sauti ya kunguruma ya baragumu la kiaskari. Naam, baragumu ambalo ndio parapanda la Malaika Israfili (as), halipungui kwa baragumu la kiaskari, kama ilivyo utiifu wa roho ambao katika upande wa milele, na ulimwengu wa punje ndogo na ambazo zimejibu kwa قَالُوا بَلَى iliposikia mnada wa (أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ) , unaotoka katika mikondo ya milele, na mpango wake unavuka pasina shaka maradufu na maradufu ule uliopo kwenye jeshi liliopangiliwa (Neno la thelathini), limethibitisha kwa hoja za kushinda kwamba roho sio tu ni jeshi la kisubhana, bali chembe ndogo zote pia ni jeshi lenye kungojea wito wa jumla. Suala la pili: Kuhuisha wafu, na mfano wake ni: Kama inavyowezekana kuwasha mamia ya taa za umeme usiku wa tamasha la mji mkuu, kutoka katika kituo kimoja kwa muda mfupi sana, kana kwamba muda huo hauna kipimo, basi vile vile inawezekana sana kuwasha mamilioni ya taa za viumbe na kuwatoa juu ya mgongo ardhi kutokea kituo kimoja, maadamu umeme ambao ni moja ya viumbe wake Allah (s.w), na mtumishi wa kumulika katika nyumba yake ya wageni, ana sifa na uwezo huu kwa kutekeleza kazi zake kwa mujibu wa ulivyo pokea katika maelekezo na taarifa na mpangilio kutoka kwa Muumba wake, basi hapana budi kwamba ufufuo mkuu utatokea kama kupepesa kwa jicho kwa mujibu wa kanuni za kiungu zilizopangiliwa ambazo wanazitekeleza maelfu ya wahudumu wenye kuidhihirisha nuru mfano wa umeme. Suala la tatu: Kuundwa kwa miili haraka na mfano wake nayo ni: Kuanzishwa upya kwa miti yote, majani ambayo yanazidi idadi yake mara elfu juu ya idadi ya wanadamu, kwa mkupuo mmoja ndani ya siku chache, ndani ya majira ya machipuo, na kwa namna kamilifu, na kwa umbo lile ambalo lilikuwa katika majira ya machipuo yaliyopita, na hivyo hivyo kupatisha kwa maua yote ya miti na matunda yake, majani yake kwa kasi ya haraka mno, kama ilivyokuwa katika majira ya machipuo yaliyopita, na hivyo hivyo vimbegu na kokwa na mbegu zinazindua na hazidhibitiki wala kuhesabika na ambazo zinatokana na majira hayo ya machipuo, wakati mmoja kwa pamoja na kufunuka kwake na kuhuika kwake, na kadhalika kufufuka kwa mizoga iliyosimama na maumbo makubwa ya miti, na kutii kwake amri kwa haraka, (kufufuka baada ya mauti), na kadhalika kuhuisha katika aina ya wanyama nyeti na makundi yake yasio na idadi kwa ukomo wa umadhubuti na ustadi, na kadhalika kufufuliwa kwa mataifa ya vijidudu, na hasa nzi (anaonekana mbele ya macho yetu na ambaye anatukumbusha kutia udhu na kufanya usafi kwa kule kusafisha mikono yake na macho yake na mbawa zake mfululizo na kutunonea kwenye nyuso zetu), ambapo inavuka idadi ya wanaosambazwa ndani ya mwaka mmoja, idadi ya wanadamu wote kutokea adamu (as). Basi kufufua kidudu hiki kwa kila majira ya machipuo pamoja na vijidudu vingine na kuvihuisha ndani ya siku chache tu, haitoi mfano mmoja tu bali maelfu ya mifano katika kuunda miili ya wanadamu haraka siku ya kiama. Naam, maadamu dunia ni nyumba ya (hekima) na nyumba ya akhera ni nyumba ya (Qudura), basi hakika kuvipatisha vitu duniani imekuwa kwa kiasi fulani cha hatua kidogo kidogo, na kwa muda, kwa mujibu wa hekima ya Kiungu na kwa mujibu wa aghlabu ya majina mazuri mfano (الحَكِيمُ˛ المرتِّبُ˛ المدبِّرُ˛ المربِّي). Ama akhera (Qudura) na (Rehema), vinajionesha zaidi kuliko (hekima), basi hapana haja ya maada na muda wala kungojea, huko vitu vinaundwa kwa punde tu, na kile ambacho Qur’an inakiashiria وَمَا أَمْرُ السَّاعَةِ إِلَّا كَلَمْحِ الْبَصَرِ أَوْ هُوَ أَقْرَبُ ni kwamba kinachoundwa hapa ndani kwa siku moja na mwaka mmoja huko akhera, kinaundwa ndani ya punde tu kama kupepesa jicho, na kama unataka ujue kwamba ujio wa ufufuo, ni jambo la kukatwa shauri halina ubishi, kama ilivyo ujio wa majira ya machipuo yajayo na uhakika wake, tazama kwa makini (Neno la kumi) na (Neno la ishirini na tisa) na kama hutasadiki kama ujio wa majira haya ya machipuo, utakuwa na haki ya kunihesabu hesabu nzito. Suala la nne: Kufa kwa dunia na kusimama kwa kiama na mfano wake: Lau ingegongana sayari moja au kimondo kwa amri ya kiungu, na tufe letu hili la ardhi ambako ndio mji wa ugeni wetu, ingeteketeza mafikio na makazi yetu, - yaani ardhi - kama kasri linavyoteketezwa ambalo limejengwa kwa miaka kumi ndani ya dakika moja. * * *
❀ قَالَ مَنْ يُحْيِي الْعِظَامَ وَهِىَ رَم۪يمٌ ❀ قُلْ يُحْي۪يهَا الَّذ۪ٓي اَنْشَاَهَٓا اَوَّلَ مَرَّةٍ وَهُوَ بِكُلِّ خَلْقٍ عَل۪يمٌ Imekuja kwenye mfano wa tatu katika hakika ya tisa ya neno la kumi kuwa: Mmoja wao akikwambia; Mtu mkubwa wakati ambao anaunda jeshi kubwa mbele ya macho yetu ndani ya siku moja, anaweza kukusanya kundi moja kamili katika askari waliotawanyika kwa mapumziko kwa kupuliza baragumu, na kuwafanya wanajumuika chini ya mpangilio wa kikosi na ukasema: Hapana, Sisadiki hilo, je, jibu lako na kukanusha kwako hakuwi ni wendawazimu na wehu? Kadhalika, yule aliyevipatisha viwiliwili vya wanyama wote, na vyenye uhai vyote kutoka katika hali ya kutokuwepo, miili hiyo kama vikosi vya askari vya viumbe vyenye kushabihiana, na jeshi kubwa na akapangilia vichembe vyake vidogo sana, na uzuri wake na kuviweka katika mahala pake panapofaa, kwa mpangilio kamili na mizani yenye hekima kwa amri (كُنْ فَيَكُونُ) na yeye ambaye anaumba, kwa kila karne moja, bali katika kila majira ya machipuo, mamia ya maelfu ya sampuli ya vyenye uhai na mataifa yake yanayoshabihiana na jeshi, je, huyu Mweza na huyu Mjuzi yawezekana akaulizwa, vipi atakusanya kwa ukelele mmoja kutoka katika baragumu la Israfil, vichembe vidogo mno vyote vya msingi, na sehemu ya asili katika wanajeshi wanaojuana chini ya bendera ya kikosi cha mwili na mpangilio wake? Na je, yawezekana kukanushwa hili kwake? Na je, haiwi kulikanusha ni upumbavu na uwendawazimu? Na vile vile Qur’an tukufu yaweza kutaja katika matendo ya Allah (s.w), ya kidunia ya ajabu na ya kupendeza ili kuandaa akili kupata kusadiki na kuhudhurisha nyoyo kuamini matendo yake ya muujiza ya akhera, na kwamba inasawiri matendo ya kiungu ya ajabu, ambayo yatatokea baadaye, na akhera kwa namna ambayo tunakinai na kutulia kwayo, kwa mifano yake mingi tunayoishuhudia. Mfano: أَوَ لَمْ يَرَ الْإِنْسَانُ أَنَّا خَلَقْنَاهُ مِنْ نُطْفَةٍ فَإِذَا هُوَخَصِيْمٌ مُبِيْنٌ mpaka mwisho wa sura (Yaasini), hapa katika kadhia ya ufufuo, Qur’an tukufu inathibitisha na kuleta hoja mbali mbali juu ya jambo hili, kwa sura saba au nane mbali mbali na sampuli tofauti. Inaleta uumbwaji wa mwanzo kwanza, na kuonesha mbele ya macho kwa kusema: Hakika mnaona mwanzo wa kuumbwa kwenu kutokana na tone, hadi pande la damu, na kutoka katika pande la damu hadi kuwa mnofu, na kutoka katika mnofu hadi kuumbwa kwa mwanaadamu, basi vipi tena mnakanusha kuumbwa kwa mwisho, ambako ni mfano wa kuumbwa huku bali ni rahisi zaidi kuliko kuumbwa huku? Kisha inaashiria kwa: الَّذِي جَعَلَ لَكُمْ مِنَ الشَّجَرِ الْأَخْضَرِ نَارًا kwenye neema hizo, na hisani na kuneemeshwa ambako Al-haq (s.w) amemneemesha mwanaadamu, basi ambaye anaye waneemesha neema kama hizi, hatakuwacheni bure bure, au kwa mchezo tu muingie kaburini na mkalale humo bila kusimama, inasema kwa njia ya alama: Mnaona kuhuishwa na kutiwa kijani miti iliokufa, basi vipi mnakanusha kupewa uhai mifupa inayoshabihiana na kuni na msipimishie na hilo? Na kisha je, inawezekana kushindwa aliyeumba mbingu na ardhi kumuhuisha mwanaadamu na kumfisha na yeye ni tunda la mbingu na ardhi? Na je, yawezekana kwa anayeendesha mambo ya mti na kuuchunga akapuuzia tunda lake na kuwaachia wengine? Na je, mnadhani (mti wa uumbaji) utaachwa kufanyiwa mchezo ambao sehemu zake zote zimefinyangwa kwa hekima, na kwamba atapuuza tunda na matokeo yake? Na kama hivi hakika ambaye atakuhuisheni kwenye ufufuo ni yule ambaye mkononi mwake kuna sukani za mbingu na ardhi, na viumbe vinanyenyekea kwake namna ya askari watiifu wanavyonyenyekea kwa amri yake, na kuwatiisha kwa amri ya (كُنْ فَيَكُونُ) utiisho kamili, na ambaye kwake kuumba majira ya machipuo ni vyepesi na rahisi kama kuumba ua moja, na kupatisha viumbe vyote ni rahisi mbele ya uweza wake, kama kupatisha nzi mmoja. Haulizwi wala hatoulizwa kwa kushindwa mwenye uweza huu (s.w): مَنْ يُحْيِي الْعِظَامَ Kisha kwa ibara فَسُبْحَانَ الَّذِي بِيَدِهِ مَلَكُوتُ كُلِ شَيْئٍ inabainisha kwamba yeye (s.w) mkononi mwake kuna sukani ya kila kitu, na kwake kuna funguo za kila kitu, na anapindua usiku na mchana, masika na kiangazi kwa wepesi wote, kana kwamba ni kurasa za kitabu, na dunia na akhera kwake ni kama nyumba mbili, anafunga nyumba hii na anafungua ile, basi maadamu mambo yako hivyo matokeo ya dalili zote ni: وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ(Na kwake mtarejeshwa), yaani atakuhuisheni kutoka kaburini, na kuwapelekeni kwenye ufufuo, na atatimiza hisabu yake kwenye daftari lake takatifu. Na kama hivi unaona aya hizi zimeandaa akili, na kuhudhurisha nyoyo ili kukubali kadhia ya ufufuo, kwa kule kuonesha mifano ya kutenda kwake hapa duniani. Na kweli Qur’an yaweza kutaja pia matendo ya kiakhera kwa namna inayotia hisia na kuashiria mifano yake ya kidunia, ili kuzuia kupinga na kukanusha, mathalan: بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ ﴿إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ ۞ وَإِذَا النُّجُومُ انْكَدَرَتْ ۞ وَإِذَا الْجِبَالُ سُيِّرَتْ ۞ وَإِذَا الْعِشَارُ عُطِّلَتْ ۞ وَإِذَا الْوُحُوشُ حُشِرَتْ ۞ وَإِذَا الْبِحَارُ سُجِّرَتْ ۞ وَإِذَا النُّفُوسُ زُوِّجَتْ ۞ وَإِذَا الْمَوْءُودَةُ سُئِلَتْ ۞ بِأَيِّ ذَنْبٍ قُتِلَتْ ۞ وَإِذَا الصُّحُفُ نُشِرَتْ ۞ وَإِذَا السَّمَاءُ كُشِطَتْ ۞ وَإِذَا الْجَحِيمُ سُعِّرَتْ ۞ وَإِذَا الْجَنَّةُ أُزْلِفَتْ ۞ عَلِمَتْ نَفْسٌ مَا أَحْضَرَتْ﴾ إِلَى آخِرِ السُّورَةِ بِسْمِ اللهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيْمِ ﴿إِذَا السَّمَاءُ انْفَطَرَتْ ۞ وَإِذَا الْكَوَاكِبُ انْتَثَرَتْ ۞ وَإِذَا الْبِحَارُ فُجِّرَتْ ۞ وَإِذَا الْقُبُورُ بُعْثِرَتْ ۞ عَلِمَتْ نَفْسٌ مَا قَدَّمَتْ وَأَخَّرَتْ...﴾ إِلَى آخِر السُّورَةِ بِسْمِ اللهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيْمِ ﴿إِذَا السَّمَاءُ انْشَقَّتْ ۞ وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ ۞ وَإِذَا الْأَرْضُ مُدَّتْ ۞ وَأَلْقَتْ مَا فِيهَا وَتَخَلَّتْ ۞ وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ...﴾ إِلَى آخِر السُّورَةِ Utaona kwamba sura hizi zinataja mabadiliko makubwa na utendaji mkubwa wa kiungu bwana mlezi wa hali ya juu, kwa mbinu inaufanya moyo mateka na kupigwa na mshangao mkubwa, akili inakuwa finyu mbele yake na kubaki katika kutahayari, lakini mwanaadamu haoni mifano yake katika majira ya mapukutiko, na machipuo ila anakubali kwa wepesi wote kabisa, na ilivyokuwa tafsiri ya sura tatu hizi ni ndefu tutachukua neno moja tu kama kielelezo, kwa mfano: Utaona kwamba sura hizi zinataja mabadiliko makubwa na utendaji mkubwa wa kiungu bwana mlezi wa hali ya juu, kwa mbinu inaufanya moyo mateka na kupigwa na mshangao mkubwa, akili inakuwa finyu mbele yake na kubaki katika kutahayari, lakini mwanaadamu haoni mifano yake katika majira ya mapukutiko, na machipuo ila anakubali kwa wepesi wote kabisa, na ilivyokuwa tafsiri ya sura tatu hizi ni ndefu tutachukua neno moja tu kama kielelezo, kwa mfano: وَإِذَا الصُّحُفُ نُشِرَتْ Aya hii inafidisha kuwa, katika ufufuo zitakunjuliwa amali zote za mja zikiwa zimeandikwa kwenye waraka, na kwa kuwa suala hili lilivyokuwa la ajabu akili haioni njia yake, isipokuwa sura kama inavyoashiria ufufuo wa majira ya machipuo, na kama zilivyo nukta za akhera zina mifano yake na wenzake, basi vivyo hivyo wenza wa kukunjuliwa nyaraka na mifano yake ni wazi dhahiri. Kwani kila tunda, kila jani na kila mti, kila kimoja kina matendo na kazi na wadhifa maalumu, na utumishi na tasbihi, kwa namna ambayo hudhihirishwa na majina mazuri ya Allah (s.w), matendo yote hayo yanaingia pamoja na historia ya uhai wake katika mbegu na kokwa zake zote. Na zote zitadhihiri katika majira mengine ya machipuo, na mahali pengine, yaani; Kama inavyotaja kwa ufasaha mkubwa matendo ya mama zake na mashina yake, kwa sura na umbo la wazi, basi hukunjua vile vile kurasa za matendo yake, kwa kukunjua matawi na kufungua majani na matunda. Naam, ambaye anafanya haya mbele ya macho yetu kwa hekima na hifadhi yote, uendeshaji na malezi ya upole ndiye asemaye: وَإِذَا الصُّحُفُ نُشِرَتْ Na kama hivi basi pima nukta nyinginezo kwa mtindo kama huu, kama una nguvu ya kutoa hukumu kwenye nafsi fanya hivyo. Na kwa ajili ya kukusaidia pia tutataja: إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ pia. Neno (كُوِّرَتْ) ambalo linapatikana katika maneno haya ni kwa maana ya kuviringishwa na kukusanywa, ni mfano maridadi wa wazi zaidi ya kuwa unaashiria mwenza na mfano wake Duniani. Kwanza: Hakika Allah (s.w) amenyanyua pazia za kutokuwepo na athiir (ether) na mbingu, katika umbo la jua linaloangazia dunia kama taa, akilitoa kutoka katika hazina ya rehema yake na kulidhihirisha duniani, na umbo hilo ataliviringisha na vifuniko vyake, wakati dunia hii itakapokwisha na milango yake kufungika. Pili: Hakika jua ni kitenda kazi na kiamuriwa kueneza sehemu za mwanga usiku wa manane, na kufunga katika nyakati za jioni, na hivyo hupokezana usiku na mchana katika eneo la ardhi, na kubeba mizigo yake ikipunguza muamala wake, au mwezi unaweza kuwa kwa kiasi fulani mjumbe wa kuichukua na kuitoa, yaani kama ilivyo mtenda kazi huyu hukusanya mizigo yake, na kufunga madaftari ya kazi zake kwa sababu hizi, hapana budi itakuja siku litakaposamehewa kazi zake, na kuachishwa wadhifa wake, hata kama hakuna sababu za kusamehe na kuondosha, na huenda ukunjufu wa wanayoyashuhudia wanaanga kwenye sura yake ya maeneo mawili madogo sasa yanakunjuka na kukua kidogo kidogo, inarejesha jua kwa kukunjuka huku na kwa amri kutoka kwa Allah (s.w) kile ilichokifunga na kukikunjua kwenye kiini cha ardhi kwa idhini ya Allah (s.w) katika mwanga, na kujiviringisha kwayo. Hapo atasema bwana mlezi mwenye ushindi asiyeshindwa: Hadi hapa, jukumu lako limekwisha na ardhi, na sasa njoo Jahannam ukawachome wale walio kuwa wakikuabudu na wakamdhalilisha mtumishi mtiifu kama wewe, na kumdharau kwa kumtuhumu kufanya hiana na kutokuwa mtekelezaji wa wajibu. Na kwa hivi jua linasoma amri ya Allah (s.w): إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ juu ya sura yake iliyowekwa dimbwi. * * *
Habari kutoka kwa wateule bora mia moja na ishirini na nne elfu, na ni Manabii na Mursaliin juu yao rehema na amani, kama ilivyoeleza hivyo hadithi - kwa maelezo ya ijmai na tawaatur wakitegemea kwa mashahidi wa baadhi yao, na kwa haki ya yakini kwa wengine, juu ya kuwepo kwa maisha ya akhera na kutangaza kwao kwa ijmai kwamba watu watapelekwa huko na kuwa Muumba (s.w) ataleta nyumba ya akhera pasi na shaka, kama alivyoahidi hilo ahadi ya kukata shauri. Na uhakika wa kusadiki mawalii mia moja na ishirini na nne milioni, kwa kashfu (kufunuliwa yaliofichikana) na ushahidi ambao Mitume (as) wameshaeleza, na ushahidi wao juu ya kuwepo kwa akhera kwa elimu ya yakini, ni dalili yenye nguvu na dalili ifaayo juu ya kuwepo kwa akhera. Pia kudhihiri kwa majina yote mazuri ya Muumba wa ulimwengu yanayojidhihirisha katika pande zote ulimwenguni, yanahitajia uwazi kuwepo kwa ulimwengu mwengine wa kudumu milele na kujulisha kwa uwazi kabisa juu ya kuwepo kwa akhera. Na hivyo hivyo uweza wa kiungu na hekima yake visivyo na kikomo, ambazo hazina israf wala mchezo, na ambayo inahuisha jeneza za miti iliokufa na maumbo yake iliyonyooka, huihuisha na hali haihesabiki wala kudhibitika juu ya sura ya ardhi. Kwa kila majira ya machipuo, na kwa kila mwaka kwa amri (كُنْ فَيَكُونُ), na kuijaalia ni alama ya (ufufuo baada ya umauti) na kufufua mia tatu elfu sampuli, katika mataifa ya mimea na umati wa wanyama na kuwatawanya, kwa kufanya hivyo akidhihirisha mamia ya maelfu ya vielelezo vya ufufuo na kukusanywa na dalili za kuwepo kwa akhera. Na hivyo hivyo rehema kunjufu ambayo inadumisha uhai kwa viumbe vinavyohitajia riziki kwa ujumla, na kuyapatia maisha upole kamilifu kwa njia ya ajabu mno, na uangalizi wa kudumu, ambao hudhihirisha aina za mapambo yaliyo mazuri bila idadi, ndani ya muda mfupi sana katika kila majira ya machipuo, hakuna shaka kuwa mawili hayo yanalazimu kuwepo kwa akhera bila ubishi wowote. Na vile vile, huba ya kubaki milele, na shauku ya kudumu na matumaini ya kuishi milele yaliyopandikizwa kimaumbile yasiyotoweka katika maumbile ya mwanaadamu huyu, ambaye ndiye tunda kamili la ulimwengu huu, na kiumbe anayependwa sana kwa Muumba wa ulimwengu, na mwenye mahusiano madhubuti zaidi pamoja na viumbe vyote vya ulimwenguni, hapana shaka inaashiria kwa uwazi kabisa katika kuwepo kwa ulimwengu wa kudumu, baada ya ulimwengu huu wa kutoweka na kuwepo kwa ulimwengu wa akhera, na mji wa furaha ya milele. Basi dalili zote hizi zinathibitisha kwa kukata shauri kabisa hadi kufikia hali ya kulazimu kukubali kuwepo kwa akhera, ni mithili ya uwepo wa uwazi wa kuwepo Dunia Maadamu somo muhimu ambalo Qur’an inatufundisha ni (Imani ya akhera), na somo hili ni imara na madhubuti kwa ngazi hii, na katika imani hiyo kuna nuru angavu, na matarajio makubwa na maliwazo kwa namna ambayo kama ungekusanyika uzee wenye idadi ya mia moja elfu kwa mtu mmoja, nuru hiyo ingemtosha, matarajio hayo, maliwazo hayo yatokanayo na imani hii, kwa ajili hiyo, ni juu yetu sisi wazee kufurahia uzee wetu na kushangilia kwa kusema: الْحَمْدُ لِلَّهِ عَلَى كَمَالِ الْإِيْمَانِ

