[Onyo, Fundisho na Ukumbusho Waliopewa Vijana Wengi Wasiokuwa na Furaha] Siku moja vijana kadhaa wenye akili walikuja kwangu, wakihitaji jambo jingine lenye athari ili wajihifadhi dhidi ya hatari za katika maisha, ujana, na tamaa za roho. Kama nilivyowaambia wale ambao hapo awali walitaka msaada kutoka katika Risale-i Nur, pia niliwaambia vijana hawa: Ujana wenu kwa hakika utakutokeni, na kama hambakii katika wigo wa halali, mtapotea, na badala ya furaha hizi, utakuleteeni majanga na maumivu duniani, kaburini, na Akhera. lakini kama, kwa mafunzo ya Kiislamu, mtatumia neema ya ujana wenu kama shukurani kwa heshima, katika unyoofu na utii, matokeo yake utasalia ukiendelea na utakuwa sababu ya kupata ujana wa milele. Ama kuhusu uhai, kama ni bila ya imani, au kwa sababu ya uasi, imani haiathiri, italeta maumivu, huzuni na masikitiko ya juu, kuliko furaha za mpito na faraja inayoleta. Kwa kuwa, tofauti na Wanyama, mwanaadamu ana akili na fikra, ameunganika na wakati huu uliopo, uliopita na ujao. Anaweza kupata maumivu na furaha katika nyakati hizo. Ilhali, kwa kuwa Wanyama hawafikirii, huzuni inayokuja kutokana na wakati uliopita na hofu na wasiwasi kwa ajili ya mustakabali hauharibu furaha zao za sasa. Na hususani kama furaha ni haramu; basi ni kama asali yenye sumu kwa pamoja. Maana yake, kutokana na mtizamo wa furaha ya maisha, mwanaadamu anaangukia katika kiwango cha kuwa chini kuliko Wanyama. Kwa hakika, maisha ya watu wapotovu na wasio wazingatiaji, na kwa hakika kuwepo kwao, hata dunia yao, ni siku ambamo wao hujikuta humo. Kutokana na mtizamo wa upotovu wao, wakati wote na ulimwengu wa wakati uliopita haupo, umekufa. Hivyo akili zao, zinazowaunganisha wao kwenye wakati uliopita na ijao, huwaletea kiza na weusi. Na kutokana na kukosa kwao imani, mustakabali pia haupo. Zaidi ya hivyo, kwa sababu wana fikra, utenganisho wa milele unaotokana na kutokuwepo huku kunaendelea kuwazalishia giza katika maisha yao. Ilhali, kama imani inayapa uhai maisha, kupitia katika nuru ya imani, huangaza wakati uliopita na ujao na kuwezesha kuwepo. Kama wakati wa sasa, inaleta furaha tukufu za juu na nuru za kuwepo kwa ajili ya roho na moyo -kwa mujibu wa imani. Kuna maelezo juu ya ukweli huu katika ‘Matumaini ya Saba’ katika Ujumbe kwa wazee. Unaweza kurejea huko. Na kwa hivyo, maisha ndivyo yalivyo. Kama unataka furaha ya uhai, uhuishe uhai wako kwa imani, na uupambe kwa matendo ya kidini. Na uuhifadhi kwa kujiepusha na madhambi. Kuhusu ukweli wa kutisha wa kifo, unaooneshwa na vifo kila siku, kila mahali, kwa nyakati zote, nitakuelezeni kwa mifano hai, halikadhalika hayo niliwaambia vijana wengine. Mathalani, vitanzi vimesimamishwa hapa mbele ya macho yenu. Licha ya kuwa ofisi ya bahati nasibu, lakini inagawa tiketi kwa zawadi kubwa za kweli. Sisi tuliopo hapa tuko watu kumi, iwe tunapenda au hapana, tutaitwa hapo; hakuna mbadala. Watatuita, na kwa kuwa wakati huo ni siri, dakika yoyote wanaweza kusema ama: “Njoo uchukue tiketi ya kunyongwa kwako! Panda kwenye kitanzi!” Au: “Tiketi ya kujishindia zawadi za mamilioni ya dola zenye thamani ya dhahabu zimekufikia. Njoo uchukue!” Katika hali ya kuwasubiri waseme hayo, watu wawili ghafla wanatokea mlangoni. Mmoja ni mwanamke aliyevaa mavazi ya kubana, mzuri na mwenye kuhadaa. Mkononi mwake ameshika vitu ambavyo kwa juujuu ni vitamu sana, lakini kwa hakika ni haluwa yenye sumu, ametuletea ili tule. Mwingine ni mtu makini asiyedanganya wala kudanganywa. Anaingia baada ya mwanamke huyo na kusema: “Nimekuleteeni zindiko, fundisho. Mkilisoma, na msipokula haluwa hiyo, mtanusurika mbali na vitanzi. Kwa zindiko hili, mtapata tiketi kwa ajili ya zawadi zisizo na kifani. Angalia, mnaona kwa macho yenu kuwa wanaokula asali wanapanda kwenye vitanzi, na mpaka wakati huo wanapata maumivu makali ya tumbo kutokana na sumu ya haluwa. Na nani atakayepokea tiketi kwa ajili ya zawadi kubwa hajulikani; inaonekana kuwa wao pia watapanda kwenye vitanzi. Lakini kuna mamilioni ya mashahidi wanaoshuhudia kuwa wanaweza kuingia kwenye uwanja wa zawadi kirahisi. Kwa hivyo, angalieni dirishani! Maofisa wa juu kabisa na watu wenye hadhi za juu jambo hili kwa sauti za juu: ‘Kama mnavyoona kwa uhakika kabisa kwa macho yenu hao wanaopanda kwenye vitanzi, kwa hivyo pia muwe na hakika kama mwangaza wa mchana, bila ya shaka au wasiwasi, wanaokuwa na zindiko wanapata tiketi kwa ajili ya zawadi.’” Kwa hivyo, kama mshabaha ulivyo, kwa kuwa furaha potovu za ujana katika uwanja wa haramu, ambazo ni kama asali yenye sumu, hupoteza imani, ambayo ni tiketi kwa ajili ya hazina ya milele na viza ya kuelekea kwenye furaha ya milele, mtu anayejiingiza humo anaishia kwenye mauti, ambayo ni kama vitanzi, na taabu za kaburi ambazo ni kama mlango wa kwenda kwenye kiza cha milele. Na kwa kuwa saa iliyopangwa haijulikani, myongaji wake, hatofautishi kati ya kijana na mzee, wakati wowote anaweza kukata kichwa chako. Kama utaacha matamanio haramu, ambayo ni kama asali yenye sumu, na kupata imani na kutekeleza wajibu wa kidini, ambao ni zindiko la Qur’an, manabii mia moja ishirini na nne elfu (rehema na amani ziwafikie) pamoja na mawalii wasio na idadi na watu wa kweli wamesema kwa kauli moja kuwa mtapata tiketi kwa ajili ya hazina ya furaha ya milele inayokuja kutoka katika bahati nasibu ya ajabu ya majaaliwa ya kibinaadamu. Na wameonesha alama zake. Kifupi: Ujana utaondoka. Na kama utaendelea kubadhiriwa, utaleta majanga mengi sana na maumivu duniani na Akhera. Na kama mnataka kufahamu namna vijana wengi wa aina hiyo wanavyoishia mahospitalini wakiwa na magonjwa yanayotokana na ujana uliotumika vibaya na ubadhirifu, na katika jela au hosteli kwa ajili ya mafukara katika ziada zao, na katika sehemu za starehe kutokana na huzuni zitokanazo na maumivu yao, basi nenda ukaulize mahospitalini, magerezani na makaburini. Kwa hakika, kama utakavyosikia kutoka katika hospitali nyingi minong’ono na kugumia ya wanaougua kutokana na ubadhirifu na ufisadi unaotokana na misukumo ya ujana, ndivyo pia utakavyosikia magerezani miguno ya majuto ya vijana wasio na furaha walioadhibiwa kwa matendo ya haramu hususani yanayotokana na matumizi mabaya ya ujana. Na mtafahamu kuwa adhabu nyingi za kaburi -ambalo ni Ulimwengu wa Kati na Kati ambao ni milango ambayo inaenendelea kufunguliwa na kufungwa kwa wenye kuingia- ni matokeo ya ujana uliotumiwa vibaya, kama inavyoshuhudiwa na watu wa ufunuo wa maisha ya kaburi, na yamethibitishwa na watu wa kweli. Pia, waulize wazee na wagonjwa, ambao ndiyo wengi katika idadi ya watu. Kwa hakika, wengi katika wao watasema kwa huzuni na majuto: “Tambueni! Tumepoteza ujana wetu katika matamanio na njozi; kwa hakika, kwa maumivu. Muwe na tahadhari, msifanye kama tulivyofanya!” Kwa sababu, matokeo ya furaha za haramu za vijana watano kati ya kumi, mtu anapata maumivu kwa miaka mingi ya masikitiko na majuto duniani, adhabu na madhara katika Ulimwengu wa Kati na Kati, na majanga ya jahanamu katika Akhera. Na ingawa mtu wa aina hiyo yupo katika hali ya kusikitisha, yeye kwa vyovyote anastahiki kusikitikiwa. (Kwa wanaoridhika kujiingiza katika matendo haramu anaweza kuwa asisikitikiwe) . Hawastahiki. حَفِظَنَا اللّٰهُ وَإِيَّاكُمْ مِنْ فِتْنَةِ هٰذَا الزَّمَانِ الْمُغْرِيَةِ وَنَجَّانَا مِنْ شُرُورِهَا. آمِينَ
Source text is preserved. When a suitable model is available, translation is displayed separately.
Sözler
The Thirteenth Word
بِاس۟مِهٖ سُب۟حَانَهُ Wale walio jela wana haja kubwa ya faraja ya kweli ya Risale-i Nur. Hususani wale waliopata maumivu ya vipigo vya ujana, wanaopitisha ujana wao, maisha matamu jela; wana haja na Risale-i Nur kama wanavyohitaji mkate. Kwa hakika, ujana unazingatia hisia badala ya sababu, na hisia na utashi ni upofu; hawafikirii athari zake; Wanapendelea wakia moja ya furaha ya papo hapo badala ya tani za furaha za baadaye. Wao huua kwa ajili ya furaha ya dakika moja ili kufurahia ulipizaji kisasi, halafu wanapata maumivu kwa saa elfu themanini ya maumivu ya jela. Na starehe potovu ya saa moja katika masuala ya heshima inaweza kupelekea furaha ya maisha kuteketezwa kabisa kwa kuhofia jela na maadui. Na kuna mifano mingi mingine, hatari nyingi zisizoonekana kwa vijana wenye mikosi kwa sababu ambayo wanabadili maisha yao matamu sana kuwa machungu sana na maisha ya hatari. Fikiria hali kubwa ya kaskazini; imepata umiliki wa tamaa za vijana wake na inatikisa karne hii yote kwa dhoruba zake. Kwani imehalalisha kwa vijana wake mabinti wazuri na wake wa watu walionyooka, na vijana hawa wanatenda kwa kufuata hisia zao tu, ambazo hazioni athari zote. Kwa hakika, kwa kuruhusu wanaume na wanawake kwenda pamoja katika bafu za umma, wanahamasisha ukosefu wa maadili. Na wanachukulia kuwa ni halali kwa wahuni na masikini kupora mali za matajiri. Watu wote wanatetemeka katika kukabili balaa hili. Na kwa hivyo ni lazima sana katika karne hii kwa vijana wote wa Kiislamu kufanya ushujaa, na kujibu mashambulizi haya mawili yanayouma kwa mapanga ya ari kama Matunda ya Imani na Mwongozo kwa Kijana kutoka Risale-i Nur. Vinginevyo vijana wasiobahatika watavunja yote mawili, mustakabali wao duniani, na maisha yao yenye kukubalika, na starehe yao ya Akhera, na maisha yao ya milele, na kuyageuza kuwa adhabu na taabu. Na ubadhirifu wao na ufisadi, wataishia mahospitalini, na kwa kukithirisha maishani mwao, katika magereza. Uzeeni kwao, watalia sana huku wakiwa na majuto mengi. Kama, kwa upande mwingine, watajihifadhi kwa mafunzo ya Qur’an, na kwa ukweli wa Risale-i Nur, watakuwa vijana shujaa kikweli kweli, watu wenye sifa nzuri, waislamu wenye mafanikio, na kwa namna nyingine watawala kwa viumbe hai na wanyama wote. Kwa hakika, kijana anapopitisha saa moja jela kati ya ishirini na nne kila siku katika swala za faradhi, na akajutia makosa yaliyokuwa sababu ya balaa lake, na akajizuia dhidi ya maovu mengine, madhambi, hilo litamnufaisha sana maishani mwake, na mustakabali wake, na nchi yake, na taifa lake, na nduguze, ndivyo pia atanufaika katika ujana wake wa mpito kwa miaka kumi mpaka kumi na mitano ya ujana wa kudumu na mzuri sana. Kwanza kabisa Qur’an ya Ufafanuzi wa Kimiujiza, na maandiko yote yaliyoteremshwa, yametoa bishara hii ya uhakika. Kama kijana wa aina hiyo anashukuru neema nzuri ya ujana kwa wastani na utii, itauzidisha, na kuufanya wa milele, na kuufanya starehe. Vinginevyo utakuwa balaa, na kuwa wenye maumivu, na jinamizi, na kisha utaondoka. Itamsababisha awe kama mzururaji, mwenye kuwakosea ndugu na jamaa zake, nchi na taifa lake. Kama mfungwa amefungwa kwa dhuluma, kwa sharti kuwa anaswali swala tano, kila saa moja italingana na ibada ya siku nzima, na jela itakuwa kama chumba cha mtu anayeishi peke yake. Atahesabiwa miongoni mwa watawa wachamungu wa hapo zamani waliokimbilia mapangoni kwa ajili ya kujiweka katika ibada. Kama ni masikini, mwenye umri mkubwa, na mgonjwa, na anayetaka ukweli wa imani, kwa sharti kuwa anaswali swala tano za faradhi na anatubu, kila saa italingana na saa ishirini za ibada, na jela itakuwa kama nyumba yake ya mapumziko, na kwa sababu ya marafiki zake humo wanaompenda, nafasi ya upendo, mafunzo, na elimu. Huenda akawa mwenye furaha zaidi kukaa jela kuliko kuachiliwa huru, kwa kuwa nje anachanganyikiwa na anapata mashambulizi ya madhambi kutoka kila upande. Anaweza kupata elimu kamili kutoka jela. Siku ya kuachiliwa, haitakuwa kama muuaji, au kuwa na kiu ya ulipizaji kisasi, bali mtu mwenye subira, aliyethibitishwa na majaribu, mwenye tabia njema, na mwenye manufaa kwa taifa lake. Kwa hakika, wafungwa wa Denizli kwa hivyo wamekuwa na maadili mema ajabu baada ya kusoma Risale-i Nur kwa muda mfupi tu ambao baadhi ya waliohusika walisema: “Kusoma Risale-i Nur kwa wiki kumi na tano kuna athari zaidi katika kuwabadili wao kuliko kuwaweka gerezani kwa miaka kumi na mitano.” Kwa kuwa kifo hakifi na saa iliyopangwa haijulikani, kinaweza kuja katika wakati wowote; na kwa kuwa kaburi haliwezi kufungwa, na kikundi baada ya kikundi huingia na kupotea; na kwa kuwa imeoneshwa katika ukweli wa Qur’an kuwa kifo kwa waumini kimebadilika kuwa nyaraka za kuruhusiwa watoke katika ukandamizwaji wa kudumu, ilhali kwa wakorofi na mafisadi ni kupotelea milele katika maangamizi ya milele, na pia ni utenganishwaji usio na kikomo baina yao na wapenzi wao na viumbe wote, lililo na hakika na bila ya shaka yoyote, mtu mwenye bahati sana ni aliye mvumilivu na anashukuru kikamilifu manufaa tangu wakati wake wa jela, na kusoma Risale-i Nur kwa ajili ya kuitumikia Qur’an na imani yake katika njia iliyonyooka. Ewe mtu uliyezoea furaha na starehe! Mimi nina umri wa miaka sabini na tano, na ninajua kwa hakika kutokana na wingi wa uzoefu, shuhuda, na matukio kuwa furaha ya kweli, starehe isiyo na maumivu, isiyo na masikitiko, na furaha ya maisha inaweza tu kupatikana katika imani na katika wigo wa ukweli wa imani. Starehe moja ya kidunia hata hivyo, huleta maumivu mengi. Kama vile kupigwa makofi kumi kwa ajili ya tunda moja la zabibu, huondoa starehe zote za maisha. Enyi watu msiobahatika wanaopata janga ndani ya jela! Kwa kuwa dunia yenu inalia na maisha yenu ni machungu, fanyeni jitihada ili Akhera yenu pia isilie, na maisha yenu ya milele yafurahi na kuwa matamu! Nufaikeni na jela! Kama ambavyo wakati mwingine katika hali iliyoshitadi katika kumkabili adui, uangalizi wa saa moja unaweza kulingana na ibada ya mwaka mmoja, ndivyo pia katika hali iliyoshitadi unayoweza kuwepo, ugumu wa kila saa iliyotumika katika ibada inakuwa yenye kulingana na saa nyingi, hubadili ugumu huo na kuwa rehema.
Kwa Jina Lake, (s.w) Hakuna chochote isipokuwa kinamtukuza Yeye kwa sifa. اَلسَّلَامُ عَلَي۟كُم۟ وَ رَح۟مَةُ اللّٰهِ وَ بَرَكَاتُهُ اَبَدًا دَائِمًا Rafiki zangu gerezani na ndugu zangu katika dini! Ilinitokea kukuelezeni ukweli utakaokuokoeni dhidi ya adhabu ya duniani na Akhera. Ni kama ifuatavyo: Mathalani: Mtu akimuua ndugu wa mtu mwingine au jamaa yake mmojawapo. Mauaji yenye kuleta furaha ya dakika moja ya ulipizaji kisasi yanasababisha mamilioni ya dakika za huzuni moyoni na maumivu makali ya jela. Na hofu ya kisasi kutoka kwa ndugu na jamaa za aliyeuawa, na wasiwasi wa kukabiliana uso kwa uso na adui yake huondoa furaha na starehe zote maishani. Anapata adhabu ya kuwa na hofu na hasira. Kuna utatuzi mmoja tu katika hili, na hilo ni mapatano, ambayo Qur’an inaamuru, na ukweli, usahihi, manufaa, utu, na matakwa ya Uislamu na ujasiri. Kwa hakika, kinachohitajika kweli ni amani, kwa sababu saa imeshapangwa, haibadiliki. Kwa kuwa saa yake iliyopangwa imefika, mtu aliyeuawa asingekaa zaidi katika hali yoyote. Na ama kwa muuaji, ilikuwa njia ya kudura ya Allah kufanyika. Kwa kuwa hakuna mapatano, pande zote mbili zinapata adhabu za hofu na kisasi. Ni kwa sababu ya hili ndipo Uislamu unaamuru kuwa “muumini mmoja asikasirikiane na muumini mwingine kwa zaidiyasikutatu”. Kamamauajihayakuwamatokeo ya mfundo au uadui uliothibitika, na mfanya vurugu ndumila kuwili ameanzisha mfarakano, ni muhimu kufanya amani kwa haraka. Vinginevyo, tatizo hilo dogo linakuwa kubwa, na kuendelea. Kama wanafanya amani, na muuaji anatubu na anamwombea mtu aliyemuua bila ya kukoma, basi pande zote mbili zitapata zaidi na kuwa kama ndugu. Katika nafasi ya ndugu aliyeondoka, atapata ndugu wengi wa kidini. Atakuwa ameondolewa kwa Kudura ya kiungu na kumsamehe adui wake. Na hususani kwa kuwa wanazingatia mafunzo ya Risale-i Nur, amani na ustawi wa mtu mmoja mmoja, na umma, na undugu uliopo katika wigo wa Risale-i Nur unahitaji kuwa waweke pembeni hisia zote ngumu zilipo baina yao. Ilikuwa hivyo katika Gereza la Denizli; wafungwa wote waliokuwa maadui wakawa ndugu kwa mafunzo ya Risale-i Nur. Ilikuwa sababu mojawapo ya kuachiliwa kwetu, na ilisababisha hata ukosefu wa dini na kutomjua mungu kusema kuhusu wafungwa hao: “Mashallah! Barakallah!” na ilikuwa faraja kabisa kwa wafungwa hao. Mimi mwenyewe nimewaona hapa watu mia moja wakipata taabu kwa sababu ya mtu mmoja na kutokutoka kwenda kushughulika kwa pamoja. Ni dhuluma kwao. Muumini wa kiume mwenye ufahamu hatamdhuru kila mmoja katika mamia ya waumini wengine kwa sababu ya kosa dogo au manufaa machache. Kama atafanya kosa na kusababisha madhara, anapaswa atubu upesi.
Kwa Jina Lake, (s.w) Ndugu zangu waaminifu na wafungwa wa zamani! Nimefanya suluhisho imara ambalo, kwa heshima ya upendeleo wa kiungu, nyinyi ni sababu muhimu ya sisi kuingia kwetu hapa. Maana yake, kwa faraja yake na ukweli wa imani, Risale-i Nur ni yenye kukuokoeni dhidi ya huzuni ya balaa la gereza na kutoka katika madhara mengi ya kidunia, na maisha yenu yasipite bila ya manufaa na kukosa kitu kwa masikitiko na huzuni na kupotezwa katika upepo wa udhanifu, na Akhera yenu dhidi ya kulia kama dunia yenu inavyolia sasa; inakupeni kitulizo cha kweli. Kwa kuwa ukweli wa jambo hilo ni huu, kwa kweli lazima muwe ndugu nyinyi kwa nyinyi, kama wafungwa wa Denizli na Wanafunzi wa Risale-i Nur. Mnaweza kuona kuwa wanachunguza mali zenu zote, chakula, mkate, na mchuzi unaokuja kutoka nje ili kisu kisikufikieni miongoni mwenu na msishambuliane. Maaskari magereza wanaokuhudumieni kwa uaminifu hupata taabu sana. Pia, hamtoki nje kwenda kufanya mazoezi kwa pamoja, kama vile mtashambuliana kama wanyama wa mwituni. Na kwa hivyo, marafiki wapya, ambao kwa asili ni wakakamavu na jasiri, kwa ujasiri mkubwa wa kimaadili mnapaswa mliambie kundi hilo kwa wakati huu: “Kama si visu, bali bastola zingegawiwa kwetu, na amri ya kupiga pia, tusingewadhuru marafiki zetu wenye mkosi na waliopata janga hili kama sisi. Kwa mwongozo na kwa amri ya Qur’an, na imani, na undugu wa Kiislamu, na utashi wetu, tumeamua kuwasamehe na kujaribu kutowakashifu, hata kama hapo mwanzo kulikuwa na sababu mia moja za uadui na uhasama wetu.” Hivyo basi, ndivyo mnavyobadili gereza hili liwe nafasi kubwa ya mafunzo.
[Mazungumzo na baadhi ya vijana ambao japo wamezingirwa na vishawishi, hawajapoteza uwezo wao wa kimantiki.] Huku likiwa limevamiwa na anasa za kilaghai na potovu za zama hizi, kundi la vijana lilikuwa likiuliza: “Tutawezaje kuokoa maisha yetu katika Akhera?” na wakatafuta msaada katika Risale-i Nur. Kwa hivyo nikawaambia yafuatayo kwa jina la Risale-i Nur: Kaburi lipo na hakuna wa kulikana. Watake wasitake, kila mmoja lazima ataingia. Licha ya ‘Njia tatu’ zifuatazo, hakuna njia nyingine ya kuliendea: Njia ya Kwanza: Kwa waumini, kaburi ni mlango wa kuingia katika ulimwengu bora zaidi kuliko dunia. Njia ya Pili: Kwa wenye kuamini Akhera, lakini wanaiendea kwa njia ya ubadhirifu na upotovu, ni mlango wa kuingia jela ya kifungo cha upweke, gereza la milele, ambapo watatenganishwa na wapenzi wao wote. Njia ya Tatu: Kwa makafiri na wapotevu wasioamini Akhera, ni mlango wa kuelekea kifo cha milele. Maana yake, ni vitanzi vya kuwanyongea wao na wote wanaowapenda. Kwa kuwa wanadhania hivyo, hivyo ndivyo hasa watakavyokuwa: kama adhabu. Njia hizi mbili za mwisho ziko dhahiri, hazihitaji ushahidi, ni wazi kwa wenye kuona. Kwa kuwa saa iliyoteuliwa ni siri, na kifo kinaweza kuja wakati wowote na kukikata kabisa kichwa cha mmojawapo, na hakibagui kati ya kijana na mzee, na kudumu katika hali ya hofu hiyo na jambo zito mbele yake, mtu asiye na furaha kwa hakika atatafuta njia za kujitoa kutoka katika kifo cha milele, kifungo hicho cha upweke kisichokwisha; njia za kubadili mlango wa kaburi kuwa mlango unaoelekea ulimwengu wa milele, furaha ya milele, na dunia ya nuru. Litakuwa swali kubwa kwake kama dunia. Ukweli wa kifo, basi, unaweza tu kufikiwa kwa njia hizi tatu, na mitume na manabii wanyoofu mia moja na ishirini na nne elfu, waliokuwa na miujiza kama dalili za uthibitisho – wametangaza kuwa njia hizo tatu ni kama zilivyoelezwa hapo juu. Kwa kuegemea katika nuru na maono yao, mawalii milioni mia moja ishirini na nne wamethibitisha na kuweka alama zao katika bishara za kinabii. Na Wanazuoni wengi wamethibitisha kimantiki kwa shuhuda zao dhahiri katika kiwango cha ‘uhakika katika kiwango cha elimu . Wote kwa kauli moja wametangaza kuwa ni uhakika kabisa, kwa kusema: “Njia pekee ya kunusurika na kifo na kifungo cha milele, na kupelekwa kwenye furaha ya milele, ni kwa kumwamini Allah na kumtii.” Kama mtu anazingatia lakini hafuati neno la mjumbe mmoja la kutokufuata njia ya hatari yenye asilimia moja ya hatari ya kuangamia, na akaifuata, wasiwasi alionao wa kuangamia unaweza kumwondolea hata hamu yake ya kula. Hivyo, mamia ya maelfu ya mitume wa kweli na waliothibitishwa wametangaza kuwa kuna uwezekano wa asilimia mia moja kuwa upotovu na uovu unapelekea katika vitanzi vya kaburi, mbele kabisa ya macho, na kifungo cha milele cha upweke, na kuwa kuna uwezekano wa asilimia mia moja kuwa imani na ibada huondoa vitanzi hivyo, hulifunga gereza la upweke, na kubadili kaburi la dhahiri daima na kuwa mlango unaoelekea katika hazina ya milele na kasri la furaha; na wameonesha dalili na alama za hayo. Kama alivyokabiliwa, basi, kwa jambo hili geni, la kutisha, ikiwa mwenye huzuni na - hususani kama yeye ni mwislamu - haamini na kuabudu, Je, ataweza kweli kuondoa maumivu ya huzuni yenye kuletwa na wasiwasi alionao kwa kuwa muda wote anangojea zamu yake ya kuitwa kwenye vitanzi hivyo, mbele kabisa ya macho yake, hata kama amepewa utawala juu ya dunia yote pamoja na furaha zake zote? Ninakuulizeni. Kwa kuwa uzee, maradhi, majanga, na katika pande zote kifo hufungulia maumivu ya kutisha na pia ni ukumbusho, hata kama watu wa upotovu na uovu wanafurahia anasa na furaha mia moja elfu, kwa hakika kabisa wanapata namna ya jahanamu nyoyoni mwao, lakini mzubao mkubwa wa kutokuwa na usikivu huwafanya kwa muda mfupi wasiihisi. Kwa kuwa wanaoamini na kuabudu kaburi, ambalo mara zote liko machoni mwao, ni mlango wa kuelekea kwenye hazina ya milele na furaha ya milele, na kwa kuwa, kwa sababu ya ‘kuponi ya imani’, tiketi kutoka katika bahati nasibu ya milele ya kudura ya Kiungu kwa mamilioni ya mamilioni ya dhahabu na almasi za thamani kubwa zimekuja kwa kila mmoja wao, muda wote wanasubiri neno, “Njooni mchukue tiketi zenu” kwa furaha kubwa ya kweli na ya kiroho. Furaha hii ipo kwa kiasi kwamba, kama inakuwa kitu na mbegu inakuwa mti, itakuwa kama pepo binafsi. Hata hivyo, anayeacha furaha na anasa kubwa kutokana na misukumo ya ujana, na kuchagua namna ya ufisadi na ufasiki, furaha zilizoharamishwa, zinazofanana na asali yenye sumu iliyochafuliwa na maumivu yale mengi, anaangukia katika kiwango kidogo mno kuliko hata mnyama. Zaidi ya hivyo, mtu wa namna hiyo hatakuwa kama Wamagharibi wasioamini, kwani kama watamkanusha Nabii Muhammad (s.a.w), wanaweza kuwatambua manabii wengine. Kama hawamjui Allah, wanaweza kuwa na sifa nzuri ambazo ni njia za makamilifu ya hakika. Lakini mwislamu anajua manabii, na Mwenye kumruzuku, na ukamilifu wote kupitia kwa Muhammad (s.a.w). Kama mmoja wao ataacha maelekezo ya Nabii atakuwa anajitoa nje ya mlolongo wake, hatamtambua nabii yeyote mwingine, wala hatamtambua Allah. Wala hatajua msingi wowote rohoni mwake utakaohifadhi makamilifu yake. Kwa kuwa Muhammad (s.a.w) ni nabii wa mwisho na mtukufu, na dini yake na ulinganiaji ni kwa watu wote, na kwa kuwa yeye ni mbora kuliko wote kwa miujiza yake na dini, na yeye ni mwanaadamu kwa watu wote katika mambo yote kuhusu uhakika, na ameyathibitisha haya katika namna nzuri sana kwa karne kumi na nne, na ni sababu ya fahari ya wanaadamu, mwislamu anayekataa mafundisho muhimu ya Muhammad (s.a.w) na misingi ya dini yake kwa hakika hataweza kupata nuru, wala kupata ukamilifu wowote. Ataanguka kabisa. Na kwa hivyo, enyi wenye hasara waliotawaliwa na anasa za maisha ya dunia, na kuwa na wasiwasi wa mustakabali, pambaneni ili kuuhifadhi na maisha yenu! Kama mnataka anasa, raha, furaha, na wepesi duniani, fanyeni mambo ya halali. Hayo yanatosha kukupeni furaha. Kwa hakika mtakuwa mnafahamu kutoka sehemu nyingine za Risale-i Nur kuwa katika kila furaha iliyo nje ya hilo, na ni haramu, kuna maumivu mengi sana. Kama matukio ya hapo baadaye - mathalani, ya miaka hamsini tangu sasa yangeoneshwa katika sinema kama wanavyoonesha kwa wakati huu matukio yaliyopita, wanaojiingiza katika uovu watalia huku wakiwa wamejaa hofu na maudhi katika mambo ambayo kwa sasa yanawafurahisha. Wale wanaotaka wawe na furaha ya kudumu na ya milele duniani na Akhera wafuate maelekezo ya Muhammad (s.a.w) katika wigo wa imani.
بِاس۟مِهٖ سُب۟حَانَهُ Kwa Jina Lake, (s.w) اَلسَّلَامُ عَلَي۟كُم۟ وَ رَح۟مَةُ اللّٰهِ وَ بَرَكَاتُهُ Ndugu zangu wapendwa na waaminifu! Nitaeleza kitulizo muwafaka katika ‘Nukta’ tatu kwa wenye kupata taabu jela, na kwa wenye kuwasaidia kwa wema na kiimani wanaosimamia chakula chao, kinachowajia kutoka nje. Nukta ya kwanza: Kila siku inayopita katika jela inaweza kuleta mpaka siku kumi za ibada, na, kwa kuangalia matunda yake, inaweza kugeuza saa zile fupi na kuwa saa za kudumu, na adhabu ya miaka mitano au kumi inaweza kuwa njia ya kumwokoa mtu kwa mamilioni ya miaka ya kifungo cha milele. Kwa waumini, hali ya kupata faida hii muhimu na yenye thamani kubwa ni kuswali swala tano za faradhi, kutubu madhambi yaliyokuwa sababu ya kufungwa, na kuwa na shukurani katika subira. Kwa hakika, gereza ni kizuizi cha madhambi mengi: Haiwapi fursa. Nukta ya Pili: kama ambavyo kukoma kwa starehe kunasababisha maumivu, ndivyo pia kukoma kwa maumivu kunavyoleta starehe. Kwa hakika, katika kuifikiria furaha iliyopita, siku za raha, kila mmoja anahisi maumivu ya majuto na shauku, na kusema: “Basi!”, na kukumbuka siku za nyuma za majanga, zisizo za furaha, wanapata namna ya furaha kwa kuwa yameshapita, na anasema: “Sifa njema na shukurani ni kwa Allah, balaa lile limeacha zawadi nyuma yake na limeshaondoka.” Anatoa pumzi ya faraja. Maana yake, maumivu mafupi na ya huzuni huacha nyuma namna ya furaha rohoni, ilhali saa ya furaha huacha maumivu. Kwa kuwa ukweli ni hivyo; na kwa kuwa balaa zilizopita pamoja na maumivu yake hayapo, na siku zijazo za dhiki kwa sasa hazipo, na hakuna maumivu yanayoletwa kutokana na kisichokuwepo, kuendelea kula mkate na kunywa maji leo, mathalani, kwa sababu ya uwezekano wa kusikia njaa na kiu kwa siku kadhaa zijazo, ni upumbavu mkubwa. Na kwa namna hiyo hiyo, kwa sasa kufikiria saa za huzuni zilizopita na zijazo, ambazo kwa sasa hazipo, na kukosa subira, na mtu kusahau makosa yake, kunong’ona kama vile kumlalamikia Allah ni pia upumbavu mkubwa. Kwa kuwa nguvu ya subira haijasambazwa kwenda kushoto na kuume, yaani, katika wakati uliopita na ujao, na imeimarishwa katika kukabili saa ya sasa na siku, kunatosha. Huzuni inaporomoka kutoka kumi hadi moja. Kwa hakika, lakini isiwe malalamiko, upendeleo wa kiungu umeashiria ukweli wa hapo juu kwangu ilhali nikiwa katika siku chache za maumivu ya kimwili na kiroho, maradhi, na majaribu ambayo mfano wake sikuwahi kuyapata kabla maishani mwangu, nilikandamizwa hususani kwa kukata tamaa na huzuni, niliyohisi katika moyo na roho kwa kushindwa kwangu kuihudumia Qur’an na imani kwa Risale-i Nur. Basi nikawa nimeridhika na maradhi ya kuhuzunisha na kifungo cha jela. Kwa kusema: “Ni faida kubwa kwa mwenye mkosi kama mimi anayengojea katika mlango wa kaburi ili kufanya saa moja inayoweza kupitishwa katika upuuzi na kutozingatia saa kumi za ibada”, nikashukuru. Nukta ya Tatu: kuna faida kubwa katika kuwasaidia wafungwa kwa huruma, katika kuwapa mahitaji yao, na katika kutuliza vidonda vyao vya kiroho kwa kuwafariji. Na kuwapa chakula chao kinachokuja kutoka nje ni kama zaka ambayo, ni kwa kiasi hasa cha chakula, imeandikwa katika kitabu cha amali njema kwa hao, wa nje na ndani, wanaofanya haya, pamoja na waangalizi wanaohusika. Na hususani kama mfungwa asiye na furaha ni mzee, mgonjwa, masikini, au mgeni, basi malipo ya zaka hii yanazidi kwa mara nyingi. Hivyo faida hii ya thamani kubwa sharti lake ni kuswali swala tano za faradhi, ili huduma hiyo iwe ni kwa ajili ya Allah. Na hali nyingine ni kuharakisha kuwasaidia kwa ikhlasi, huruma na furaha, na katika namna ya kutowafanya wao kuhisi kuwa wenye kulazimishwa.
Nitadokeza kwa kifupi ukweli mpana sana na mrefu uliotokea moyoni mwangu katika Usiku wa Cheo. Kwa sababu ya uasi mkubwa na udhalimu wa Vita vya Dunia vya mwisho na uharibifu wake usio na huruma, na mamia ya wasio na hatia kutawanyika na kuhiliki kwa sababu ya jeshi moja, na ukataji tamaa mkubwa kwa walioshindwa, na mshituko wa kutisha wa washindi na maumivu yao makali yanayotokana na ukuu wasioweza kuudumisha na uharibifu wasiyoweza kuukarabati, na hali ya mpito na muda mfupi wa maisha ya dunia na hali ya hadaa, na ulevi wa ndoto za ustaarabu kudhihirika kwa wote, na uwezo wa juu katika hali halisi ya binaadamu na dhati yake kujeruhiwa katika hali ya kuenea kote na ya kutisha, na mapenzi ya ndani ya mwanaadamu ya kutaka kuendeleza kuishi na kutokujali na upotovu na kutosikia, hali ya asili isiyokuwa na uhai kupondwapondwa na panga la almasi la Qur’an, na uso mbaya zaidi wa siasa ya dunia kuwa dhahiri, ambao ni kifuniko chenye kusonga koo na kuhadaa kwa kutokujali na upotovu, kwa hakika zaidi na bila kivuli chochote cha shaka, kwa kuwa maisha ya dunia - ambayo hupendwa na wanaadamu - ni mabaya na ya mpito hasa, hali halisi ya mwanaadamu itatafuta uzima wa milele kwa nguvu zake zote, anaoupenda na kuutamani kikweli, kama kulivyo na alama za kutokea huku kwa Kaskazini, Magharibi, na Marekani. Na lililo hakika zaidi pasi na shaka ni kwa kuwa Qur’an yenye Ufafanuzi wa Kimiujiza, ambayo kila karne kwa miaka elfu moja mia tatu na sitini imekuwa na wanafunzi milioni mia tatu hamsini, na kuweka muhuri juu ya kila tangazo lake na kudai kwa uthibitisho wa mamilioni ya wanazuoni wakubwa, wanyoofu, na kila dakika imekuwepo kwa utukufu wake nyoyoni mwa mamilioni ya mahafidhi na imetoa maelekezo kwa wanaadamu kwa ndimi zao, na ambayo katika namna ya kutolingana na kitabu kingine chochote kinafikisha bishara ya uzima wa milele na furaha ya milele kwa mwanaadamu na kuponya vidonda vyao, - kwa kuwa Qur’an imeeleza habari hizi njema za uhakika kuhusu uzima wa milele na furaha kwa maelfu ya msisitizo wake, aya zenye nguvu na zenye kujirudia, na kwa shuhuda imara na hoja zisizo na idadi za wazi, inatoa habari waziwazi na kwa kudokezea mara maelfu ya idadi, kwa kuwa mwanaadamu hapotezi akili yake yote na kiama cha kimwili na kiroho hakilipukii kichwani mwake, makundi makubwa na mataifa makubwa duniani yataitafuta Qur’an yenye Ufafanuzi wa Kimiujiza, na baada ya kupata ukweli wake, wataipokea kwa uhai wao wote na roho, kama kulivyo [kwa sasa] kuna wahubiri katika Sweden, Norway, Finland na Uingereza wakifanya kazi ya kufanya Qur’an ipokelewe, na jamii muhimu ya Marekani inatafuta dini ya kweli. Kwa sababu katika mtizamo wa ukweli huu, Qur’an kwa hali yoyote haina wala haitakuwa na chenye kulingana nayo. Na bila ya shaka hakuna kinachoweza kuchukua nafasi ya muujiza huu mkubwa. Pili: Kwa kuwa Risale-i Nur imetoa huduma kama upanga wa almasi mkononi mwa muujiza huu mkubwa zaidi na kuwashurutisha maadui zake wakaidi kutii, na inafanya kazi kama mpiga mbiu kwenye hazina za Qur’an katika mtindo unaoangaza na kuponya moyo na roho kikamilifu, na hisia, na haina chanzo wala mamlaka mengine ghairi ya Qur’an na ndiyo muujiza wake, inafanya kazi hiyo kikamilifu. Zaidi ya hivyo imewang’oa kikamilifu wakana mungu wakaidi na propaganda zao za kutisha dhidi yake, na kupondaponda kwa risala ya (Asili, Sababu au Athari), ambayo ni ngome isiyoshindika ya upotovu, na kwa mada ya Sita ya (Matunda ya Imani) pamoja na Shuhuda za Kwanza, Pili, Tatu na Nane ambazo zote zimo katika kitabu (Fimbo ya Musa), zimeondoa hali ya kutokujali katika mtindo mzuri zaidi katika uwanja wake mnene, wenye kukaba koo na mpana chini ya vizuizi vikubwa vya sayansi na kuonesha nuru ya umoja wa kiungu. Kwa hakika, kwa kuwa maelekezo ya kidini kwa sasa yameruhusiwa rasmi na ruhusa imetolewa kufungua sehemu binafsi za masomo, ni lazima kwetu na lazima kwa umma kuwa, kadiri iwezekanavyo, Wanafunzi wa Risale-i Nur wanapaswa wafungue Kituo kidogo cha Kusoma Risale-i Nur kila mahali. Ingawa kila mmoja atanufaika na yaliyomo humo, si kila mmoja anaweza kufahamu kila jambo kikamilifu. Lakini kwa kuwa masuala haya ni maelezo ya mambo ya ukweli wa imani, yote ni kujifunza, na kumjua Allah, na huelekezea kwenye kuwepo kwa Allah, na pia ni ibada. Inshallah, Madrasa hizi za Risale-i Nur zitahifadhi katika majuma matano mpaka kumi, matokeo yaleyale ambayo Madrasa zilizotangulia zimeleta katika miaka mitano mpaka kumi - na kwa hivyo, zimekuwa zikifanya kwa miaka ishirini. Pia ni muhimu kwa serikali kutokuingilia Miale hii ya Qur’an, Risale-i Nur, ambayo ni mpiga mbiu wa Qur’an na ni pia ni yenye kufaa kwa njia nyingi katika maisha ya kidunia na kisiasa kwa umma na nchi hii, na kwa ajili ya maisha yake katika Akhera. Badala yake, ifanye kazi ya kuieneza kikamilifu na kukubalika, ili ifute madhambi yake mabaya ya muda uliopita, na kuweka kizuizi kwenye majaribu mengi na vurugu za mustakabali.

