Sözler

The Fourteenth Word

Source: risaleinur multilingual dataset, risale.site source · Risale-Nur multilingual research corpus
Risale reading plan
§1

Kofi la ughafilikaji na funzo lenye kuonya وَمَا ال۟حَيٰوةُ الدُّن۟يَٓا اِلَّا مَتَاعُ ال۟غُرُورِ Ewe nafsi yangu maskini iliyozama katika mghafala, inayoona maisha haya kuwa ni matamu, umesahau akhera, na kutafuta dunia tu! Unajua mfano wako? Mbuni! Anamuona mwindaji lakini hawezi kuruka, basi anaweka kichwa chake kwenye mchanga ili mwindaji asimuone. Mwili wake mkubwa unabakia wazi na mwindaji anauona. Lakini macho yake yamefumbwa katika mchanga na hawezi kumwona. Ewe nafsi yangu, zingatia mlinganisho ufuatao, na uuone! Kuuzuilia uoni wa mtu humu duniani unabadili furaha kubwa kuwa maumivu ya kuhuzunisha. Mathalani, kuna watu wawili humu kijijini, yaani, huko Barla. Tisini na tisa kati ya marafiki mia moja wa mtu mmojawapo wamekwenda Istanbul, ambapo wanaishi vizuri. Mmoja tu amebakia hapa, na yeye pia atakwenda huko. Kwa sababu hii, mtu anatamani kwenda Istanbul na kuifikiria; anataka kuungana na marafiki zake. Anapoambiwa kuenda huko, anafurahi sana. Ama kuhusu mtu wa pili, marafiki tisini na tisa wameondoka hapa. Lakini wengine wameangamia na wengine wamewekwa katika mahali ambapo hawawezi kuona wala kuonekana. Anafikiria kuwa wameondoka na kutawanyika katika taabu. Mtu huyu maskini anakuwa na urafiki na mgeni mmoja mahali pa wote hao, na anataka kupata faraja. Kupitia kwake anataka kusahau maumivu yake ya kuhuzunisha ya utengano. Ewe nafsi yangu! Mpendwa sana na Allah (s.a.w) na marafiki zako wote wako nyuma ya kaburi. Mmoja au wawili waliobakia pia wataondoka kwenda huko. Kwa hivyo usiogope mauti, kuwa na wasiwasi kaburini, na kugeuza kichwa chako. Angalia kaburi kwa ujasiri, na sikiliza linachokitaka. Cheka mbele ya uso wa mauti kama mwanaume, na uone yanachokitaka. tahadhari, usiwe mwenye kughafilika, na kufanana na mtu wa pili. Ewe nafsi yangu! Usiseme, “Nyakati zimebadilika, zama hizi ni tofauti, kila mmoja amezama humu duniani na kuabudu maisha haya. Kila mmoja ameleweshwa na jambo la kuhangaikia uchumaji riziki. Kwa kuwa mauti hayabadiliki. Utengano haubadiliki kuwa udaima na hauwi tofauti. Udhaifu na umaskini wa mwanadamu havibadiliki, vinazidi. Safari ya mwanadamu haikatwi, inakuwa ya haraka. Pia, usiseme, “Mimi ni kama mwingine yeyote.” Kwa kuwa kila mmoja anafanya urafiki nawe mpaka kaburini tu, na faraja za kuwa pamoja na kila mmoja mwingine katika majanga haina maana yoyote baada ya kuingia kaburini. Wala usijidhanie kuwa uko huru na kujitegemea, kwani kama utaiangalia nyumba ya wageni ya dunia kwa jicho la busara, utaona kuwa hakuna kabisa kisicho na mpangilio na bila ya lengo? Matukio duniani kama vile matetemeko ya ardhi hayatokei kwa kubahatisha. Madhali unaona kuwa mashati yaliyopangiliwa sana na kudariziwa vizuri, moja juu ya nyingine na moja ndani ya nyingine, ambazo ni nguo za duniani kutoka katika aina mbalimbali za wanyama na mimea, zimepambwa na kurembwa kutoka juu mpaka chini kwa malengo na mifano ya hekima, na unajua kuwa dunia inazunguka na kugeuka kama kurukwa akili kwa Maulawiyya katika mpangilio kamili katika malengo matukufu sana. Basi inakuwaje, kama mkanaji Mungu alivyochapisha, wanachukulia kuwa matukio ya mauti - matukio ya dunia, kama vile tetemeko la ardhi, linalofanana na dunia kujitikisa ili kuondoa uzito wa namna fulani za ughafilikaji isiyouridhia kwa wanadamu, na hususani kutoka kwa waumini, kutokuwa na lengo na kutokea kwa bahati nasibu tu? Inakuwaje kuwa wanaonesha hasara za kuhuzunisha za wote waliopatwa kuwa bila ya fidia na kuondoka burebure tu, na kuwatupia kwenye ukataji tamaa wa kutisha? Wote wanafanya kosa kubwa. Kwa hakika, matukio hayo hutokea kwa amri ya Mwingi wa Hekima na Mwingi wa Rehema, ili kubadili mali ya mpito za waumini kuwa sawa na zaka, na kuifanya ya kudumu. Nayo huwafutia dhambi zao zinazotokana na kukosa shukrani kwa neema. Kama ambavyo itafika siku ambayo dunia hii iliyotiishwa itaona kazi za mwanadamu, ambayo ni mapambo ya uso wake, yaliyotia doa kwa kumshirikisha Allah, na kutokuwa njia ya shukrani, na hilo litawafanya wawe wabaya. Kwa amri ya Muumbaji, itawafutia uso wake wote na kuusafisha. Kwa amri ya Allah, atawatupia Jahanamu wote wanaomshirikisha Allah na atawaambia wenye kumshukuru, “Njooni na muingie Peponi.”

Private reading note

This note stays on this device and is never uploaded to a server.

Up to 1,200 characters